POPULARITY
Jaridani leo jaridani tunakuletea mad akwa kina inayoangazia mjadala Mkuu wa mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na ufafanuzi wa neno la wiki.Tume ya Uchunguzi ya Umoja wa Mataifa imesema Israel imetekeleza mauaji ya kimbari Gaza. Ripoti ya tume hiyo hiyo iliyotolewa leo mjini Geneva pia inamtaja Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu na maafisa wengine wakuu wa Israel kwa kuchochea vitendo hivyo. Israel imepinga vikali, na kuuita ripoti hiyo kuwa ni “kashfa.” Taarifa hii imetolewa huku mashambulizi makali ya anga yakiendelea usiku kucha mjini Gaza bila dalili za kukoma.Hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa, shirika hilo limekamilisha makadirio mapya ya bajeti ya mwaka 2026, yakionesha kupunguzwa kwa zaidi ya dola milioni 500. Hatua hiyo ni sehemu ya mpango wa mageuzi ya UN80, unaolenga kuongeza ufanisi wakati Umoja wa Mataifa ukiadhimisha miaka 80. Bajeti mpya inapendekeza kupunguzwa kwa rasilimali kwa zaidi ya asilimia 15 na nafasi za kazi kwa karibu asilimia 19 ikilinganishwa na mwaka 2025.Huko Nairobi, Kenya leo imezindua maabara ya kisasa ya polio iliyoidhinishwa na Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa Duniani WHO katika Taasisi ya Utafiti wa Tiba ya Kenya, KEMRI. Kituo hicho, kilichofadhiliwa na WHO na wakfu wa Gates, kimeelezwa kuwa nyenzo muhimu katika kugundua mapema na kukabiliana na virusi vya polio pamoja na magonjwa mengine yenye uwezekano wa kusambaa, si tu nchini Kenya bali pia katika kanda nzima ya Afrika.Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili hii leo, mtaalam wetu Onni Sigalla, Mhariri mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania, BAKITA, anafafanua maana za neno "MJOLI"Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
Kaunti ya Kirinyaga, iliyoko katikati mwa nchi ya Kenya kaskazini mwa mji mkuu wa nchi hiyo, Nairobi, inashuhudia mageuzi mapya katika sekta ya kilimo kupitia mradi wa kuwahusisha vijana katika kilimo na lishe unaojulikana kama EKYAN. Mradi huu unatekelezwa kwa ushirikiano kati ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto UNICEF, na wadau nchini humo. Karibu Sabrina Saidi utupe taarifa zaidi.....(TAARIFA YA SABRINA SAIDI)Mradi wa EKYAN ni mfano wa ujasiriamali wa kilimo unaoongozwa na vijana, ukiwa na lengo la kutengeneza fursa za ajira, kuwanufaisha na kubadilisha maisha ya vijana walioko vijijini, kupitia mbinu bora za kilimo na lishe, ukitekelezwa kwa ushirikiano kati ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto UNICEF, serikali ya kaunti ya Kirinyaga na shirika linalotoa mafunzo, elimu ya biashara ndogo ndogo na uwezeshaji barani Afrika KUZA Biashara.Felista Nyakio Mutungi kijana mkulima wa kaunti ya Kirinyaga, ni mmoja wa wanufaika wa mafunzo kupitia mradi huo. Na hapa anasema....CUT 2- Sauti ya Felista Nyakio Mutungi“Kabla ya kuanza kilimo, nilikuwa nauza barabarani viazi vya kukaanga au chipsi, na mihogo, pamoja na nafaka. Haikuwa vizuri sana, lakini ndiyo nafasi pekee niliyokuwa nayo wakati huo. Kupitia serikali ya kaunti ya Kirinyaga, tulisajiliwa kama vijana wanaopenda kilimo na tukapata mafunzo kupitia KUZA na UNICEF. Sasa mimi ni mkulima na mjasiriamali.”Felista anasema awali alikuwa akilima robo ekari ya mpunga na kuvuna magunia manne hadi matano pekee. Lakini baada ya mradi wa EKYAN, kwa robo ekari hiyo hiyo sasa anapata hadi magunia saba. Aidha, shamba lake limepanuka hadi ekari nne katika eneo la 'mradi wa umwagiliaji wa Bura.Felista hakutaka kuwa mchoyo wa manufaa aliyopata, hivyo ameamua kueneza ujuzi wa kilimo cha kibiashara kwa kuwafundisha baadhi ya wakulima wengine mbinu na maarifa ya kilimo hiki.CUT- Sauti ya Felista Nyakio Mutungi“Sasa si tu kwamba nalima, bali pia nawafundisha wakulima wengine kuongeza thamani katika mazao yao. Wanapata ujuzi wa kufanya biashara kupitia kilimo. Na kwa kweli tunawashukuru wahisani na UNICEF kwa kutuwezesha. Bila mpango huu, nisingekuwa hapa nilipo leo.”Kwa upande wake mtaalamu wa ubunifu wa UNICEF nchini Kenya Lilian Njoro, anaeleza kwa nini mradi huo ni muhimu kwa vijana.CUT- Sauti ya Lilian Njoro."Ni asilimia 10 pekee ya vijana wanaojihusisha na sekta ya kilimo. Kwa hivyo, kupitia mradi wa EKYAN, tulitaka kuona jinsi ya kuwahusisha vijana wengi zaidi katika kilimo na kuwavutia ili waweze kuanza kupata maisha yenye utulivu na ajira bora kupitia sekta hii.”Njoro anasisitiza kuwa teknolojia mpya zinafungua njia kwa kilimo cha kisasa tofauti na enzi za wazazi na mababu zao.Namna kilimo kinavyofanyika nyakati hizi ni tofauti na zamani,hii ni kwa sababu ya uwepo wa teknolojia bunifu, majukwaa ya kidijitali, na fursa nyingi.Kwa sasa, mradi wa EKYAN umeendelea kuwajengea vijana ujuzi, kuwapatia nafasi ya ajira, na kubadilisha mtazamo wao kuhusu kilimo, kutoka shughuli ya kizamani hadi kuwa biashara yenye faida.Link: https://youtu.be/hv17nk-2l5kTAGS:UNICEF Kenya/Kilimo/Biashara na ujasiriamali
Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani WHO limefanya mabadiliko muhimu katika orodha yake ya dawa muhimu duniani au Essential Medicines List – EML na orodha ya dawa muhimu kwa watoto (EMLc) ikijumuisha dawa za kisasa za saratani, kisukari, unene uliopitiliza na magonjwa mengine sugu.Orodha za WHO za dawa muhimu ni nyenzo za mwongozo zinazotumiwa na zaidi ya nchi 150 kupanga ununuzi, bima za afya na upatikanaji wa dawa. Kwa lugha rahisi, dawa zinazoorodheshwa hapa huwa na nafasi kubwa zaidi ya kununuliwa na kutolewa kwa wagonjwa kupitia huduma za umma kwani wanachama wa WHO wanaziweka dawa hizi kama kipaumbele cha kiafya kwa mamilioni ya watu duniani.WHO wakati wakitangaza orodha hiyo mpya waliweka bayana kuwa dawa hizi mpya si za majaribio, bali ni zile ambazo zimethibitishwa kitabibu kuwa zinaokoa maisha, kupunguza madhara ya magonjwa na kuboresha maisha ya wagonjwa.Nini maana yake?Kuongezwa kwa dawa hizi ni hatua ya mbele katika safari ya kuhakikisha afya bora kwa wote. Inamaanisha wagonjwa zaidi wa saratani, kisukari na magonjwa mengine sugu wanaweza kuwa na matumaini ya maisha marefu na bora. Pia ni wito kwa mataifa kuchukua hatua ili kuhakikisha upatikanaji wa dawa unakuwa wa haki na usawa, bila kumwacha mtu yeyote nyuma.Changamoto ya bei na usawa wa kiafyaChangamoto kubwa sasa ni bei kubwa ya dawa hizi mpya, ambazo zinaweza kufanya wagonjwa wengi kushindwa kuzipata.WHO inapendekeza mikakati ya kupunguza gharama na kuhakikisha dawa hizi zinapatikana kwenye ngazi ya huduma za msingi za afya.Deusdedit Mubangizi, Mkurugenzi wa Sera na Viwango vya Dawa WHO, anasema “Sehemu kubwa ya matumizi ya nje ya mfuko wa magonjwa yasiyoambukiza yanaelekezwa kwenye dawa, ikiwa ni pamoja na zile zinazoainishwa kama muhimu na ambazo kimsingi, zinapaswa kupatikana kwabei rahisi kwa kila mtu. Ili kufikia upatikanaji sawa wa dawa muhimu kunahitajika mwitikio madhubuti wa mfumo wa afya unaoungwa mkono na dhamira dhabiti ya kisiasa, ushirikiano wa sekta nyingi na programu zinazozingatia watu ambazo hazimwachi mtu nyuma.”Kwa maneno mengine, dawa hizi haziwezi kuwa za matajiri pekee lazima mifumo ya afya, serikali na sekta binafsi zishirikiane kuhakikisha kila mtu anayehitaji anapata dawa kwa gharama nafuu.© UNOCHA/Ali Haj SuleimanDaktari akimpatia matibabu mgonjwa wa Saratani huko nchini SyriaSaratani, kisukari na unene uliopitiliza ni changamotoSaratani na kisukari ni miongoni mwa magonjwa yanayosababisha vifo na ulemavu kwa mamilioni ya watu duniani kila mwaka. Kwa mfano, saratani pekee inaua karibu watu milioni 10 kila mwaka.Kuongeza dawa mpya za saratani kama pembrolizumab na atezolizumab, ambazo zinasaidia kinga ya mwili kushambulia chembe chembe za saratani, kunaleta matumaini mapya hasa kwa wagonjwa katika nchi zenye rasilimali chache.Kwa upande mwingine, dawa za kundi la GLP-1 receptor agonists kama semaglutide na tirzepatide zimeingizwa kwenye orodha ili kusaidia wagonjwa wa kisukari cha aina ya pili wanaoishi pia na unene uliopitiliza au matatizo ya moyo na figo. Dawa hizi husaidia kudhibiti sukari, kupunguza hatari ya magonjwa ya moyo na figo, na pia kusaidia kupunguza uzito.
Wakati mabilioni ya watu wakiendelea kuvuta hewa chafu inayosababisha zaidi ya vifo vya mapema milioni 4.5 kila mwaka, wataalamu wa hali ya hewa wa Umoja wa Mataifa leo Ijumaa (5 Septemba) wamebainisha madhara ya chembe ndogo ndogo za moshi kutoka katika moto wa nyika ambazo husafiri umbali mrefu duniani kote. Philip Mwihava na maelezo zaidi.(Taarifa ya Mwihava)“Ubora wa hewa hauheshimu mipaka,” anasema Lorenzo Labrador, Afisa wa Kisayansi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Hali ya Hewa Duniani (WMO). Anaendelea kueleza kwamba, “moshi na uchafuzi unaotokana na moto wa nyika katika msimu huu wa kihistoria katika Rasi ya Iberia tayari umepatikana Ulaya Magharibi, kwa hiyo athari zake hazibaki tu kwenye Rasi ya Iberia, bali zinaweza kusambaa kote barani Ulaya.”Akiwasilisha taarifa ya WMO kuhusu Hewa Safi na Tabianchi, ambayo inakusanya data kutoka vyanzo mbalimbali vya kimataifa, leo jijini Geneva, Uswisi Bwana Labrador ametangaza mwendelezo wa mwenendo wa kuzorota kwa ubora wa hewa duniani.Ameonyesha ramani ya dunia ya mwaka 2024 iliyoonesha alama za chembechembe ndogo zinazojulikana kama “PM 2.5” kutokana na moto wa nyika, zikionekana kwa alama nyekundu kwenye maeneo ya Chile, Brazil na Ecuador, pamoja na Canada, Afrika ya Kati na Siberia. Takwimu hizo zinathibitisha mwenendo wa kuendelea kwa kuzorota kwa ubora wa hewa duniani kama ilivyoonekana katika miaka iliyopita.Kwa upande wa habari njema, mwanasayansi huyo wa WMO amesisitiza kupungua kwa uzalishaji wa hewa chafuzi katika baadhi ya maeneo ya dunia.(Sauti ya Labrador) - sauti ya kiume“Tunaona mwenendo wa kuzorota kwa ubora wa hewa hasa kwa kuhusiana na PM 2.5, na pia tunaona kupungua kwa uzalishaji wa hewa chafuzi katika maeneo fulani ya dunia, hasa mashariki mwa China na Ulaya, mwaka baada ya mwaka.”Mfano mzuri uliotolewa katika taarifa ya leo mashariki mwa China, katika miji kama Shanghai, ambako kumepigwa hatua katika kuboresha ubora wa hewa kwa kufungua bustani zaidi na kupanda miti mingi. Na ingawa bado kuna msongamano mkubwa wa magari, mengi sasa ni ya umeme.Hata hivyo WMO inasema licha ya mafanikio hayo, miji michache tu duniani ina viwango vya ubora wa hewa chini ya vile vinavyopendekezwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani (WHO). Hii inamaanisha kuwa, licha ya maboresho ya karibuni, ubora wa hewa bado ni changamoto kubwa kwa afya ya umma.Umoja wa Mataifa unaongoza juhudi za kupambana na uchafuzi wa hewa majumbani ambao ni mojawapo ya vitisho vikubwa zaidi kwa afya ya umma duniani na hasa ni hatari kwa watoto.
Katika Jarida la Habari la Umoja wa Mataifa leo Flora Nducha anakuletea-Shirika la Umoja wa Mataifa la makazi duniani UN-HABITAT lataka wakusanyaji na wachakataji wa taka watambuliwe kwani ni uti wa mgongo wa kuhakikisha mazingira safi na salama mijini-Katibu MKuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ameipongeza Papua New Guinea kwa kuwa kisima cha kuvuna hewa ukaa na kuzitaka nchi za G-20 kuwajibika katika kudhibiti mabadiliko ya tabianchi-Nchini Mali, Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa, Volker Türk, ameonya juu ya kuzorota zaidi kwa hali ya haki za binadamu. -Na leo katika jifunze Kiswahili Je wafahamu maana ya methali "MASIKINI HANA MIIKO"? basi msikilize mtaalam wetu Dkt. Josephat Gitonga, ambaye ni Mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi nchini Kenya, kwenye kitivo cha Tafsiri na Ukalimani
Juhudi kubwa za msaada kwa waathirika wa tetemeko la ardhi lililoipiga Afghanstan mwishoni mwa wiki, zimeendelea leo huku watoa misaada wakikabiliwa hali ngumu ya kuwafikia wanaohitaji msaada kutokana na Barabara kuzibwa na kukatika kwa mawasiliano. Anold Kayanda na taarifa zaidi.(Taarifa ya Anold Kayanda)Taarifa mpya kutoka kwa timu za tathmini za Umoja wa Mataifa zilizofanikiwa kuwafikia waathirika katika wilaya ya milimani ya Ghazi Abad jana Jumanne kwa njia ya miguu, zimeweka wazi umuhimu wa kuendeleza tena kwa haraka msaada wa kibinadamu.Salam Al-Jabani kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) mjini Kabul anasema, “jambo la dharura ni kuwatoa watu chini ya vifusi na Watu wanasema wanachohitaji kwa haraka ni msaada wa kuwazika waliofariki dunia na kuwatoa waliofunikwa.”UNICEF inasema watoa misaada wake walilazimika kutembea kwa saa mbili ili kuwafikia watu na bado kuna vijiji ambavyo ili kuvifikia unahitaji kutumia saa sita hadi saba na hata helikopta hazijafanikiwa kufika huko.Mkurugenzi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani, WFP ambao walikuwa wa kwanza kupeleka msaada kwenye eneo la tukio, Bwana John Aylieff, akiwa mjini Kabul amesema, “WFP inaweza tu kumudu kuwalisha waathirika wa tetemeko la ardhi kwa wiki chache zijazo kabla ya ufadhili kuisha.”Kwa upande wake, Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) linapeleka msaada muhimu wa dharura kutoka maghala yake yaliyopo Kabul, ikiwemo mahema, blanketi na taa za sola. Pia maelfu ya wanajamii wa eneo hilo wameelekea eneo lililoathirika kusaidia juhudi za uokoaji, wakiwa na maji na chakula.
Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR kwa kushirikiana na Baraza la Wakimbizi la Norway NRC wanahakikisha wakimbizi wanaoishi katika kambi za wakimbizi za mkoani Kigoma Magharibi mwa Tanzania ikiwemo kambi ya nyarugusu wanapata huduma muhimu za maji na usafi kupitia ushirikiano wa viongozi wa wakimbizi. Huduma hizo zimekuwa changamoto kubwa katika kambi za wakimbizi zikichangiwa na ukata wa ufadhili. Flora Nducha na taarifa zaidi (TAARIFA YA FLORA NDUCHA)Vita vya wenyewe kwa wenyewe vilipoibuka Burundi mwaka 2015, na baadaye mapigano kuighubika upya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, maelfu ya watu walikimbia na kuvuka mpaka kuingia Tanzania. Leo, wengi wao wanaishi katika kambi za wakimbizi mkoani Kigoma kama vile Mtendeli, Nduta, na Nyarugusu.Lakini maisha kambini hayajakuwa rahisi. Kwa ufadhili mdogo, familia zinapata shida kupata huduma za msingi kama maji safi, makazi, na elimu.Hapo ndipo Shirika la UNHCR, na Baraza la Wakimbizi la Norway NRC, wanapoingia. Tangu mwaka 2016, wamekuwa wakitoa huduma muhimu ikiwemo kufunga mifumo ya maji, kujenga vyoo, na kusambaza sabuni na mahitaji mengine ya usafi.Miongoni mwa wanaofanya mabadiliko kupitia msaada huo ni Ahunga Msama, mkimbizi mwenye umri wa miaka 55 kutoka DR Congo, ambaye ni afisa msimamizii wa huduma za maji, usafi, kujisafi na usafi wa mazingiira WASH katika kambi ya Nyarugusu.(AHUNGA CLIP 1)“Ninasaidia jamii yetu ya kambi ya Nyarugusu ili wawe wanapata maji safi na salama”Ahunga anasema jamii yake iliteseka sana iliteseka sana kwa magonjwa yanayosababishwa na maji machafu ndio maana aliamua kuchukua hatua kulinda afya zao. Kila siku ahakikisha watu wanapata maji safi na huduma za usafi salama.Akiwa pamoja na wakimbizi wenzake, Ahunga anapita nyumba kwa nyumba kufundisha familia jinsi ya kuzuia magonjwa kupitia usafi kwani anaamini elimu ni ufunguo(AHUNGA CLIP 2)“Tunasaidia kuelimisha jamii yetu ili wawe wasafi. Wawe na vyoo, wawe na mabafu, wawe na vichanja na wawe na mashimo ya takataka.”Watu wakielewa, wanaweza kujilinda.Anasema watu wakieelewa ni rahisi kujilinda na juhudi zake zinaokoa maisha na kuhamasisha wengine, zikionyesha kwamba hata katika mazingira magumu, wakimbizi wanaweza kuongoza mabadiliko katika jamii zao na anasema hilo ni la muhimu sana kwani(AHUNGA CLIP 3)“Tunasaidia jamii yetu ili wajilinde na magonjwa ya milipuko”Kwa msaada wa UNHCR na Baraza la Wakimbizi la Norway, maelfu ya wakimbizi katika kambi za wakimbizi za Kigoma sasa wana maji salama, usafi wa mazingira ni bora, na wana matumaini mapya ya maisha.
Jaridani leo tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini Tanzania kufuatilia mradi wa FAO Mjini Morogoro, uliokutanisha viongozi wa Serikali kutoka katika Taasisi zinazojihusisha na udhibiti na usalama wa chakula. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na jifunze Kiswahili.zaidi ya watu bilioni moja duniani wanaishi na changamoto za afya ya akili kama vile msongo wa mawazo na mfadhaiko, kwa mujibu wa takwimu mpya zilizotolewa leo na Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa Duniani WHO. Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo Dkt. Tedros Adhanom Ghebreyesus amesema nchi wanachama zinapaswa kushughulikia tatizo hilo kwa “Kuwekeza katika afya ya akili, kwani kuwekeza kwa watu, jamii na uchumi ni uwekezaji ambao hakuna nchi inayoweza kuupuuzia.”Umoja wa Mataifa umetuma salamu za rambirambi na pole kwa wananchi wa sudan kufuatia maporomoko ya udongo yaliyosababishwa na mvua mkubwa iliyonyesha kwa siku kadhaa ambayo imesababisha maafa katika kijiji cha Tarsin huko Jebel Marra nchini Sudan mwishoni mwa wiki.Nchini Afghanistan ambako idadi ya vifo inaendelea kuongezeka kufuatia tetemeko la ardhi lililotokea juzi jumapili, wafanyakazi wa misaada ya Kibinadamu wa Umoja wa Mataifa wanafanya kila juhudi kuhakikisha wanafikisha misaada kwa waathirika. Akizungumza na waandishi wa habari kutokea Kabul Afghanistan Indrika Ratwatte ambaye ni mwakilishi wa UN nchini humo amesema “Sio rahisi kufika maeneo yaliyoathirika kitu ambacho kinawafanya majeruhi waendelee kufungiwa.” Ametaja juhudi za haraka zinazofanyika ni pamoja na kuzika miili ya waathirika na kufukia mifugo ili kuzuia magonjwa ya milipuko ambayo yanaweza kusambaa kwa haraka.”.Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili hii leo, mtaalam wetu Onni Sigalla, Mhariri mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania, BAKITA. Anafafanua tofauti ya "URAIBU NA HITARI”.Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!
Shirika la UNHCR limesema viongozi wa Rwanda na Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo wamekubali kuwarejesha wakimbizi walio toroka makwao mashariki mwa DRC.
Katika Jarida la Habari la Umoja wa Mataifa hii leo Flora Nducha anakulatea-Ripoti mpya kwa jina Maendeleo katika Maji ya Kunywa na Kujisafi Majumbani iliyozinduliwa leo na mashirika ya Umoja wa Mataifa imeonesha kwamba, licha ya hatua kupigwa, mtu 1 kati ya 4 duniani bado hana upatikanaji wa maji salama ya kunywa. -Ofisi ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa, OHCHR imetoa wito kwa mamlaka za Misri kukomesha mfumo wa “mzunguko” unaofanya wakosoaji wa Serikali kuzuiliwa kiholela na kwa muda mrefu, hata baada ya kumaliza vifungo vyao. - Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi,UNHCR leo limepongeza Serikali ya Kifalme ya Thailand kwa kupitisha azimio litakalowapa wakimbizi wa muda mrefu kutoka Myanmar haki ya kufanya kazi nchini Thailand.-Katika mada kwa kina tunamulika uzinduzi wa shule ya kwanza ya Akili Mnemba iliyoanzishwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la masuala ya wanawake UN Women huko ukanda wa Asia na Pasifiki-Na mashinani utamsikia Ibrahim Al-Najjar mkimbizi huko Ukanda wa Gaza, eneo la Palestina linalokaliwa kimabavu na Israeli akielezea hali tete ya ajira hivi sasa tangu vita ianze Oktoba 7, 2023.
Baada ya miaka miwili ya vita katika Ukanda wa Gaza eneo la Palestina linalokaliwa kimabavu na Israel Ijumaa tarehe 22 Agosti Umoja wa Mataifa ukatangaza jambo baya zaidi, ripoti ya njaa duniani IPC ikathibitisha wananchi wa Gaza rasmi wana kabiliwa na baa la njaa.Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP ni moja kati ya mashirika ya Umoja wa Mataifa ambayo pamoja na hali ya vita yamekuwa yakitoa msaada wa chakula huko Gaza na wameeleza kwamba baa la njaa lazima likomeshwe kwa gharama yoyote ile. Kusitishwa kwa mapigano mara moja na kukomesha mzozo ni muhimu ili kuruhusu misaada kuweza kuingizwa Gaza ili kuokoa maisha. Makala hii Leah Mushi anamuangazia mmoja wa watoto wanaokabiliwa na njaa
Machafuko yanayoendelea Kaskazini Mashariki mwa Burkina Faso yamefurusha maelfu ya watu, kukatili maisha na kuwalazimisha wengi kuwa wakimbizi ndani ya nchi yao. Miongoni mwa simulizi za kugusa ni ya Fadima Bandé mama aliyelazimika kufungasha virago kunusuru maisha yake na wanawe wawili lakini akaishia kupoteza mmoja, je ilikuwaje? kupitia video ya Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF Flora Nducha anasimulia zaidi.Katika kambi ya wakimbizi wa ndani ya Dori Mashariki mwa Burkina Faso, sasa ni maskani ya Fadima, maisha hapa ni magumu na hana tena njia ya kujipatia kipato. Kila uchao analazimika kupambana kuhakikisha watoto wake wanapata angalau mahitaji ya msingi, anakumbuka safari ya uchugu kutoka Kijiji kwake Sohlan hadi hapaWakati tunakimbia mmoja wa binti zangu mapacha aliugua baada ya kunyeshewa na mvua kubwa na kupata mafua makali, wakati tayari alikuwa anaumwa utapiamlo. Tulimkimbiza hospitai mjini Sebba lakini akafariki dunia.”Baada ya kupata hifadhi kambini Dori Fadima akajaliwa mapacha wengine wawili ambao sasa wana umri wa miezi tisa na kwa bahati mbaya wote wana utapiamlo kutokana na changamoto ya chakula.“Hapa Dori tumebarikiwa watoto mapacha lakini wametukuta hatua makazi, hatuna chochote na tuna njaa na kibaya zaidi sikuwa hata na maziwa ya kutosha kuwanyonyesha”Watoto wa Fadima wamekuwa wakiishi kwa msaada wa kibinadamu unaotolewa na mashirika mbalimbali ikiwemo UNICEF ambayo sasa inasema hali yao inaweza kuwa mbaya zaidi kutokana na kupunguzwa kwa bajeti ya kimataifa misaada wanayoitoa na hivyo kuhatarisha maisha na mustakabali wa watoto wake. Fadima anasema“Unapotawanywa na machafuko huwezi kufanya kazi, unakuwa kama mtu asiye na ajira na hapo ndio madhila yanapokuwa makubwa zaidi, lakini bado hapa ni bora kuliko ningesalia kijijini kwetu.”Kwa mujibu wa UNICEF Burkina Faso ni moja ya migogoro ya kibinadamu iliyopuuzwa zaidi duniani. Ingawa UNICEF iko hapa kusaidia, lakini inasema msaada zaidi unahitajika haraka.
Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani, WHO, licha ya mazingira magumu linaendelea na juhudi za kuokoa uhai wa kila binadamu katika eneo la Ukanda wa Gaza linalokaliwa kimabavu na Israel. Wakati huo huo linatoa wito kwa mataifa mengine kufuata mfano wa Umoja wa Falme za kiarabu, UAE ambao juzi Jumatano wamewapokea baadhi ya wagonjwa mahututi na majeruhi waliobahatika kuhamishwa Gaza ili kupata huduma za kiafya wanazozihitaji. Anold Kayanda anaeleza anawaangazia baadhi yao.
Jaridani leo tunaangazia baa la njaa katika ukanda na huduma za afya katika ukanda wa Gaza. Makala tunafuatilia harakati dhidi ya ugaidi ukimulika ripoti ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, na mashinani tunaangazia simulizi za wakimbizi kupitia vyombo vya habari.Zaidi ya nusu milioni ya watu huko Gaza wameripotiwa kukumbwa na baa la njaa, hali ambayo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres ameielezea kuwa “janga lililosababishwa na mwanadamu, shutuma ya kimaadili na kushindwa kwa ubinadamu.Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani, WHO, licha ya mazingira magumu linaendelea na juhudi za kuokoa uhai wa kila binadamu katika eneo la Ukanda wa Gaza linalokaliwa kimabavu na Israel. Wakati huo huo linatoa wito kwa mataifa mengine kufuata mfano wa Umoja wa Falme za kiarabu, UAE ambao juzi Jumatano wamewapokea baadhi ya wagonjwa mahututi na majeruhi waliobahatika kuhamishwa Gaza ili kupata huduma za kiafya wanazozihitaji.Katika makala Assumpta Massoi anamulika Mkutano wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa uliofanyika wiki hii hapa makao makuu ya Umoja wa mataifa kuangazia harakati dhidi ya ugaidi ukimulika ripoti ya Katibu Mkuu wa Umoja huo kuhusu kikundi cha kigaidi cha ISIL kijulikanacho pia kama Da'esh.Na katika mashinani fursa ni yake Abraham Mwani mwandishi wa habari za wakimbizi kutoka Radio Pacis miongoni mwa wananufaika wa mafunzo ya UNESCO ya kuwezesha vyombo vya habari kusimulia vyema habari za wakimbizi.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
Jaridani leo tunaangazia amani na usalama nchini Ukraine, na ajira kwa vijana katika sekta ya biashara ya kilimo vijijini. Makala tunaangaazia wahudumu wa kibinadamu Gaza, na mashinani tunamulika afya kwa wanawake wajawazito nchini Tanzani.Mashambulizi ya ndege zisizo na rubani za Urusi nchini Ukraine yaliyofanyika usiku kucha, ikiwemo katika miji ya Kharkiv na Zaporizhzhia, yameripotiwa kuua watu 10 wakiwemo watoto watatu, kwa mujibu wa taarifa ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto UNICEF iliyotolewa leo.Mashirika mawili ya Umoja wa Mataifa, lile la ajira, ILO na mfuko wa Maendeleo ya Kilimo, IFAD yanatekeleza mradi wa ProAgro YOUTH unaolenga kuongeza ajira kwa vijana katika sekta ya biashara ya kilimo vijijini.Makala Umoja wa Mataifa umetenga siku maalum ya kuwashukuru watoa huduma za misaada ya kibinadamu na siku hiyo ni Agosti 19 kila mwaka. Takwimu za Shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu misaada ya kibinadamu zinaeleza kuwa mwaka huu wa 2025, watu milioni 305.1 kutoka nchi 72 wanahitaji usaidizi wa kibinadamu ambao utagharibu dola bilioni 47.4. Takwimu hizi zinaonesha umuhimu na uhitaji wa watoa huduma wa kibinadamu.Na katika mashinani nampisha Mchanga Omari Kombo kutoka Pemba Zanzibar ambaye ni mnufaika wa mpango mpya wa afya ya uzazi unaofadhiliwa na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watotot UNICEF na wadau wake umewasaidia wanawake wajawazito kama kuondokana na upungufu wa damu na kujifungua watoto wenye afya njema.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
Umoja wa Mataifa umetenga siku maalum ya kuwashukuru watoa huduma za misaada ya kibinadamu na siku hiyo ni Agosti 19 kila mwaka. Takwimu za Shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu misaada ya kibinadamu zinaeleza kuwa mwaka huu wa 2025, watu milioni 305.1 kutoka nchi 72 wanahitaji usaidizi wa kibinadamu ambao utagharibu dola bilioni 47.4. Takwimu hizi zinaonesha umuhimu na uhitaji wa watoa huduma wa kibinadamu.Kuelekeza maadhimisho hayo hapo kesho Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masual ya Watoto UNICEF limetengeneza makala inayoangazia watoa huduma wa misaada ya kibinadamu huko Ukanda wa Gaza, eneo la palestina linalokaliwa kimabavu na Israel. Leah Mushi anatujuza kilichopo katika makala hiyo.
Mashambulizi ya ndege zisizo na rubani za Urusi nchini Ukraine yaliyofanyika usiku kucha, ikiwemo katika miji ya Kharkiv na Zaporizhzhia, yameripotiwa kuua watu 10 wakiwemo watoto watatu, kwa mujibu wa taarifa ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto UNICEF iliyotolewa leo. Flora Nducha na taarifa zaidi
Jaridani leo tunaangazia mkataba wa Kimataifa wenye nguvu kisheria kuhusu uchafuzi wa plastiki, na vidokezo vya malezi salama ya watoto. Makala tunakwenda nchini Tanzania na mashinani nchini Chad, kulikoni?Siku 10 za mkutano wa Kamati ya Kimataifa ya Majadiliano (INC) ya kuandaa Mkataba wa Kimataifa wenye nguvu kisheria kuhusu uchafuzi wa plastiki, ikiwemo katika mazingira ya bahari, zimemalizika huko Geneva, Uswisi bila muafaka kwenye nyaraka tarajiwa, ambapo mkutano umeahirishwa hadi tarehe itakayotangazwa baadaye.Kuwa mzazi si rahisi kila wakati, lakini usaidizi unaofaa unaweza kuleta mabadiliko ndio maana Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya watoto UNICEF limekuwa likiendesha mafunzo kwa wazazi juu ya namna bora za kulea watoto. Alinune Nsemwa ambaye ni mtaalamu wa masuala ya malezi, makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto kutoka UNICEF nchini Tanzania ameeleza vidokezo vitatu muhimu vya kuwalea watoto ambavyo vinaweza kuleta utofauti mkubwa.Makala ninakukutanisha na Sawiche Wamunza Mtaalamu wa Mawasiliano ya Kimkakati wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo, UNDP nchini Tanzania ambaye baada ya mafunzo ya siku tatu ya uchumi rejeleshi katika mkoa wa Mtwara, Kusini-Mashariki mwa Tanzania alizungumza na Godlove Makunge Muasisi na Mkurugenzi wa kampuni ya kuzoa taka na usafi wa mazingira, iitwayo Shikamana Investment. Bwana Makunge anaanza kwa kuelezea mtazamo wa jamii kwake baada ya kuamua kuanza kuzoa taka.Na katika Radwa Ahmed, Mkimbizi kutoka Sudan ambaye alianza kwa kuoka mikate kwa ajili ya familia yake, na kwa ufadhili wa shirika la Umoja wakimbizi Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR, ameweza kuigeuza talanta yake kuwa biashara ya kuuza mikate na kuajiri wakimbizi wenzake.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
Kuwa mzazi si rahisi kila wakati, lakini usaidizi unaofaa unaweza kuleta mabadiliko ndio maana Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya watoto UNICEF limekuwa likiendesha mafunzo kwa wazazi juu ya namna bora za kulea watoto. Alinune Nsemwa ambaye ni mtaalamu wa masuala ya malezi, makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto kutoka UNICEF nchini Tanzania ameeleza vidokezo vitatu muhimu vya kuwalea watoto ambavyo vinaweza kuleta utofauti mkubwa.
Makala inamulika mnufaika wa Jamii Biashara ambalo ni jukwaa la mtandaoni la masoko lililobuniwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kazi duniani, (ILO) na Chama cha Wafanyabiashara na Viwanda Kenya, (KNCCI). Jukwaa hili limefungua fursa kwa wakimbizi wanaoshughulika na biashara ndogo ndogo ili kujikimu maisha katika kambi ya wakimbizi ya Kakuma nchini Kenya. Assumpta Massoi ndiye mwenyeji wako kupitia video ya ILO.
Moja ya changamoto kubwa wanazokutana nazo wakimbizi pale wanapokaa nchi waliyopatiwa uhifadhi kwa muda mrefu ni kukosa nyaraka muhimu za utambulisho. Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya wakimbizi UNHCR limekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha wanapata suluhu ya changamoto hii.
Jaridani leo tunaangazia waandishi wa habari waliouawa katika ukanda wa Gaza, na wakimbizi wa Burundi huko Tanzania. Makala inamulika maendeleo na ustawi kwa wakimbizi Kakuma nchini Kenya na mashinani inatupeleka katika kaunti ya Tana River nchini humo, kulikoni?Kufuatia kuuawa kwa waandishi sita wa habari huko Gaza, viongozi wa mashirika mbalimbali ya Umoja wa Mataifa wamekosoa vikali shambulio hilo lililotekelezwa na majeshi ya Israel usiku wa kuamkia leo.Moja ya changamoto kubwa wanazokutana nazo wakimbizi pale wanapokaa nchi waliyopatiwa uhifadhi kwa muda mrefu ni kukosa nyaraka muhimu za utambulisho. Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya wakimbizi UNHCR limekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha wanapata suluhu ya changamoto hii. Makala inamulika mnufaika wa Jamii Biashara ambalo ni jukwaa la mtandaoni la masoko lililobuniwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kazi duniani, (ILO) na Chama cha Wafanyabiashara na Viwanda Kenya, (KNCCI). Jukwaa hili limefungua fursa kwa wakimbizi wanaoshughulika na biashara ndogo ndogo ili kujikimu maisha katika kambi ya wakimbizi ya Kakuma nchini Kenya. Assumpta Massoi ndiye mwenyeji wako kupitia video ya ILO.Na katika mashinani fursa ni yake Mariam Kazungu kutoka Kaunti ya Tana River nchini Kenya, ambaye anasema Watoto wake wamenufaika kupitia mradi wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF wa utoaji wa chanjo dhidi ya homa ya tumbo na ugonjwa wa surua.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
Bado dunia ikiendelea kuadhimisha Wiki ya Unyonyeshaji mtoto maziwa ya mama, Kelvin Keitany wa Radio Washirika, Domus Radio iliyoko huko Kajiado, eneo linalokabiliwa na madhara ya mabadiliko ya tabianchi, kama vile ukame, anamulika ni kwa jinsi gani madhara hayo yanakwamisha unyonyeshaji wa mtoto maziwa ya mama. Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya duniani, WHO limetoa mwongozo mtoto anyonyeshwe maziwa ya mama miezi sita ya mwanzo ya uhai bila kitu chochote, Je hali iko vipi Kajiado. Kelvin Keitany na maelezo zaidi.
Jaridani hii leo tunaangazia suala la afya katika ukand wa Gaza, na wito wito wa Umoja wa Mataifa wa kutaka kuachiliwa huru kwa mateka wa Israeli huko Gaza. Makala tunakwenda nchini Kenya na mashinani nchini Tanzania, kulikoni?Ikiwa ni siku 668 tangu Hamas ambao ni wanamgambo wa kipalestina wateke waisraeli 250 baada ya kushambulia taifa hilo la Mashariki ya Kati, vuta nikuvute ilikuwa bayana kwenye Baraza la Usalama baada ya kikao cha dharura kuitishwa na Israeli kufuatia kuchapishwa kwa picha za mateka wawili walio hoi bin taaban.Leo tuna habari njema kutoka Gaza, eneo la palestina linalokaliwa kwa mabavu na Israel huko Mashariki ya Kati, Shirika la Umoja wa Mataifa la afya ulimwenguni WHO kwa kushirikiana na Umoja wa falme za Kiarabu UAE wamefanikiwa kuingiza dawa, vifaa tiba na damu salama kwa ajili ya matibabu ya wanagaza ambao wanaendelea kuteseka na madhila ya vita. Makala inakupeleka nchini Kenya, hususan kaunti ya Kajiado. Bado dunia ikiendelea kuadhimisha Wiki ya Unyonyeshaji mtoto maziwa ya mama, Kelvin Keitany wa Radio Washirika, Domus Radio iliyoko huko Kajiado, eneo linalokabiliwa na madhara ya mabadiliko ya tabianchi, kama vile ukame, anamulika ni kwa jinsi gani madhara hayo yanakwamisha unyonyeshaji wa mtoto maziwa ya mama. Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya duniani, WHO limetoa mwongozo mtoto anyonyeshwe maziwa ya mama miezi sita ya mwanzo ya uhai bila kitu chochote, Je hali iko vipi Kajiado.Na mashinani fursa ni yake Dkt. Beatrice mwilike, Mkunga Bingwa na Rais wa Chama cha wakunga Tanzania (TAMA) ambaye kupitia mradi unaolenga uzazi salama kwa watoto milioni 10 ifikapo 2030 lililozinduliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ya Uzazi na Idadi ya Watu, UNFPA kwa kusaidiana na serikali ya Denmark, anasema wakunga wanatumia appu na njia za kisasa zinazowapa taarifa sahihi.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
Leo tuna habari njema kutoka Gaza, eneo la palestina linalokaliwa kwa mabavu na Israel huko Mashariki ya Kati, Shirika la Umoja wa Mataifa la afya ulimwenguni WHO kwa kushirikiana na Umoja wa falme za Kiarabu UAE wamefanikiwa kuingiza dawa, vifaa tiba na damu salama kwa ajili ya matibabu ya wanagaza ambao wanaendelea kuteseka na madhila ya vita. Leah Mushi na taarifa zaidi.
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina ambayo inamulika unyonyeshaji mtoto maziwa ya mama, uwekezaji kwenye mustakabali yao, kauli mbiu ya Wiki ya unyonyeshaji duniani iliyoanza tarehe Mosi mwezi huu wa Agosti na itakunja jamvi tarehe 7.Mashirika ya Umoja wa Mataifa lile la Wanawake, UN Women na la watoto, UNICEF yamewaeleza waandishi wa habari jijini Geneva Uswisi kuwa hali ya njaa Sudan inazidi kuwa kali zaidi. Salvator Nkurunziza, Mwakilishi wa UN Women Sudan amesema kwamba UN Women inashauri zipewe kipaumbele kaya zinazoongozwa na wanawake, pamoja na makundi kama wanawake wajawazito, wanaonyonyesha, na wasichana balehe katika kila aina ya msaada wa chakula.Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres leo katika ufunguzi wa Mkutano kuhusu nchi zisizo na Bahari LLDC3 unaofanyika Awaza, Turkmenistan amewasihi viongozi kufikiria upya maendeleo kwa mataifa yasiyo na bahari akisema, “leo tunakusanyika hapa kuthibitisha ukweli kwamba jiografia haipaswi kamwe kuamua hatima ya nchi.” Tukirejea Geneva, Uswisi unakofanyika mkutano utakaweka mwelekeo wa jinsi ya kukabiliana na uchafuzi unaotokana na plastiki duniani, Inger Andersen, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Mazingira Duniani, UNEP, ameonya kwamba, “uchafuzi wa plastiki tayari upo katika mazingira, baharini, na hata katika miili yetu. Tukizidi kuendelea kwa mwelekeo huu, dunia yote itazama katika uchafuzi wa plastiki.”Na mashinani leo tuko katika shoroba za makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani ambapo wageni hutoka kila pembe ya Dunia kutembelea jengo hili la kihistoria. Mwalimu Maria Rulands ni mmoja wao.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
Mnamo mwezi April mwaka huu Shirika la Fedha la Kimataifa IMF lilitoa makadirio na mtazamano wa uchumi wa dunia ambapo lilieleza pamoja na mambo mengine kuongezeka kwa vikwazo vya biashara kunasababisha kushuka kwa kasi kwa ukuaji wa uchumi wa dunia mwelekeo ambao ulielezwa kuathiri nchi nyingi duniani.Tarehe 29 Julai IMF ikatoa ripoti mpya, ambapo tathmini mpya ya mwelekeo wa uchumi wa Dunia kwa mwaka 2025 na 2026 ikionesha matumaini tofauti na hali ilivyoonesha miezi mitatu mitatu iliyopita. Leah Mushi amefuatilia ripoti hiyo nakutuandalia makala hii akieleza kwa kina.
Tanzania, kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani (WHO), iko mbioni kuzindua mpango wa “Beat the Heat” yaani “Lishinde Joto”, mpango wenye lengo la kukabiliana na joto kali na hatari za kimazingira katika sehemu za kazi na kwenye matukio makubwa ya kijamii. Anold Kayanda anafafanua zaidi taarifa iliyochapishwa leo na WHO jijini Dar es Salaam, Tanzania.
Hii leo jaridani tunaangazia hatua za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi nchini Tanzania, na biashara ndogondogo kwa wananchi wa Rwanda. Makala tunakupeleka nchini Kenya ma Mashinani tunakwenda Geneva Uswisi, kulikoni?Tanzania, kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani (WHO), iko mbioni kuzindua mpango wa “Beat the Heat” yaani “Lishinde Joto”, mpango wenye lengo la kukabiliana na joto kali na hatari za kimazingira katika sehemu za kazi na kwenye matukio makubwa ya kijamii. Anold Kayanda anafafanua zaidi taarifa iliyochapishwa leo na WHO jijini Dar es Salaam, Tanzania.Katika kijiji kimoja nchini Rwanda, ndoto ya muda mrefu ya Chantal Uwizeyimana imegeuka kuwa njia ya kujikwamua kiuchumi. Kupitia mradi wa STARLIT unaotekelezwa na Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Maendeleo ya Kilimo – IFAD, wakulima wadogo kama Chantal wamepata mafunzo, pembejeo na maarifa ya kubadili kilimo kuwa chanzo cha mapato ya uhakika. Sasa si tu kwamba mavuno yameongezeka, bali pia maisha yamebadilika kwa namna isiyotarajiwa. Makala inakupeleka Kenya kwake Kevin Keitany wa Radio washirika Radio Domus akimulika siku ya kimataifa ya urafiki inayoadhimishwa leo Julai 30, ikimulika urafiki katika ngazi ya mtu mmoja mmoja, baina ya watu zaidi ya mmoja, jamii, tamaduni na hata mataifa na mchango wake katika amani na utulivu duniani. Kelvin anamulika urafiki kati ya watu wawili.Na katika mashinani tuelekee jijini Geneva, Uswisi ambako unafanyika Mkutano wa Sita wa Spika wa Mabunge Duniani kumsikia Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani akitoa wito kwa viongozi wenzake kuutetea Umoja wa Mataifa.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
Hii leo jaridani tunaangazia hali ya kibinadamu Gaza, na Siku ya Kimataifa ya Wanawake na Wasichana wa Asili ya Afrika. Makala inatupeleka nchini Tanzania na mashinani tunakwenda nchini Uganda, kulikoni?Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres, ameonya kuwa mateso yanayoendelea katika Ukanda wa Gaza, eneo la Palestina linalokaliwa kimabavu na Israeli, ni zaidi ya janga la kibinadamu – ni janga la maadili linalopasua dhamira ya jumuiya ya kimataifa.Leo, tarehe 25 Julai, ni Siku ya Kimataifa ya Wanawake na Wasichana wa Asili ya Afrika, ikiwa na kaulimbiu ya mwaka huu: “Kuinuka Pamoja: Wanawake na Wasichana wa Asili ya Afrika Wakiongoza kwa Nguvu.” Idhaa ya Umoja wa Mataifa imefanya mahojiano na Patricia Da Silva, Mratibu wa Kimataifa wa Timu ya Hakuna Kumwacha Yeyote Nyuma katika shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ya Uzazi na Idadi ya Watu, UNFPA na akafafanua kidogo siku hii inabeba nini hasa. Makala inatupeleka Pemba, visiwani Zanzibar nchini Tanzania, ambapo mpango mpya wa afya ya mama unawasaidia wanawake wajawazito kukabiliana na upungufu wa damu na kujifungua watoto wenye afya. Kupitia Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, kwa ushirikiano na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF na kwa msaada wa kifedha kutoka Wakfu wa Gates, zaidi ya wanawake 16,000 sasa wanapata huduma bora kupitia Virutubisho vya Madini Mbalimbali (MMS) na huduma zilizoboreshwa za kliniki za wajawazito. Assumpta Massoi amefuatilia mradi huo kupitia video ya UNICEF TAnzania.Na katika Arinda Angella, kiongozi wa wanafunzi kutoka Mbarara, Uganda akieleza jinsi ushiriki wake katika mafunzo haya ya uongozi ambayo yameendeshwa kwa ushirikiano wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo UNDP na Kituo cha Mafunzo cha Julius Nyerere unavyompa mwanga mpya kuhusu nafasi ya vijana na wanawake katika kufanikisha Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs).Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
Mradi unaoendeshwa kwa ushirikiano kati ya serikali ya Ethiopia, Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP), ubalozi wa China wa kutumia nishati jadidifu ya jua kwa umwagiliaji, umeleta matumaini mapya kwa jamii za wakulima katika mkoa wa Sidama, kusini mwa Ethiopia. Sharon Jebichii na taarifa zaidi.
Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) nchini Nigeria limesema litalazimika kusitisha msaada wake wa dharura wa chakula na lishe kwa watu milioni 1.3 kaskazini-mashariki mwa nchini hiyo ifikapo mwishoni mwa mwezi huu kutokana na ukata. Anold Kayanda na maelezo zaidi.
Hii leo jaridani tunaangazia msaada wa kibinadamu nchini Nigeria, na mradi wa nishati ya sola ya kusaidia wakulima nchini Ethiopia. Makala inakupeleka nchini Afrika Kusini na mashinani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC.Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) nchini Nigeria limesema litalazimika kusitisha msaada wake wa dharura wa chakula na lishe kwa watu milioni 1.3 kaskazini-mashariki mwa nchini hiyo ifikapo mwishoni mwa mwezi huu kutokana na ukata.Mradi unaoendeshwa kwa ushirikiano kati ya serikali ya Ethiopia, Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP), ubalozi wa China wa kutumia nishati jadidifu ya jua kwa umwagiliaji, umeleta matumaini mapya kwa jamii za wakulima katika mkoa wa Sidama, kusini mwa Ethiopia. Katika makalaShirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya watoto UNICEF kwakushirikiana na wakfu wa LEGO wametengeneza video yenye kuonesha familia nne na jinsi zinavyopambana na malezi ya Watoto wakiwa ni wazazi kwa mara ya kwanza. Leah Mushi ametazama video hiyo ya takriban dakika 30 na hapa anakuleta simulizi ya familia kutoka nchini Afrika Kusini.Na katika mashinani Noella Bagula, Mwanachama wa Alleluyah Safe Space ambaye ni mama mkimbizi wa ndani kutoka Goma nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, ambako wanawake na wasichana wanapitia ukatili wa kijinsia katika migogoro. Bi Bagula anasema yeye sasa anajua jinsi ya kujilinda katika hali hatari kufuatia mafunzo yanayoendeshwa na shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu na Afya uzazi, (UNFPA) katika maeneo salama yaliyotengwa kwa ajili yao.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya watoto UNICEF kwakushirikiana na wakfu wa LEGO wametengeneza video yenye kuonesha familia nne na jinsi zinavyopambana na malezi ya Watoto wakiwa ni wazazi kwa mara ya kwanza. Leah Mushi ametazama video hiyo ya takriban dakika 30 na hapa anakuleta simulizi ya familia kutoka nchini Afrika Kusini.
Jaridani leo tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini Tanzania kumulika SDG17 katika mazungumzo ya Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Benki ya CRDB, Tully Esther Mwambapa na idhaa hii hivi karibuni hapa New York. Pia tunakuletea mutasari wa habari na mashinani.Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa, Volker Türk, leo jijini Geneva Uswisi amekemea amri za hivi karibuni za Israel za kuwahamisha watu Gaza, zilizoambatana na mashambulizi makali katika eneo la kusini-magharibi mwa Deir El Balah na kwamba zimeongeza machungu zaidi kwa mateso ya Wapalestina wenye njaa.Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani, (WFP) limeeleza leo kuwa kutokana na upungufu wa ufadhili, mamilioni ya watu Sudna Kusini wako hatarini kukosa msaada wa chakula. Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa WFP ambaye pia ni Afisa Mkuu wa Uendeshaji, Carl Skau, ambaye hivi karibuni ametembelea Sudan Kusini anasema, "Kote Sudan Kusini, takriban watu milioni 8 wanakabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula, wengi wao wakitegemea msaada kutoka WFP ili kuendelea kuishi.Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Amina J. Mohammed, ametoa wito mzito wa kuchukua hatua za haraka na za kimfumo ili kuongeza kasi ya maendeleo barani Afrika. Ameyasema hayo wakati wa mkutano wa wadau uliofanyika jana Julai 21 katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa, New York, Marekani kujadili matokeo na mapendekezo ya ripoti ya hivi karibuni ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu utekelezaji wa ahadi za maendeleo ya Afrika.Na katika mashinani hii leo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ameweka bayana shuhuda za kuvutia na madhubuti juu ya kwa nini mapinduzi ya nishati mbadala hayaepukiki sasa, pamoja na manufaa yatakayotokana na mabadiliko ya haki kutoka nishati ya kisukuku kuelekea nishati salama. Ushahidi huo madhubuti ni pamoja na makao makuu ya Umoja wa Mataifa kutumia nishati ya sola na Guterres amefika kwenye eneo lenye paneli hizo.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani, WFP, kupitia Apu yake ya kidigitali Gawa Chakula au ShareTheMeal, limeingia ushirikiano na Apu maarufu huko Mashariki ya Kati iitwayo Careem na kuzindua kampeni ya kuchangisha msaada wa dharura kwa watu wanaokumbwa na njaa katika eneo la Gaza na Ukingo wa Magharibi maeneo yanayokaliwa kimabavu na Israeli. Leah Mushi na taarifa zaidi
Jaridani leo tunaangazia msaada wa kibinadamu katika ukanda wa Gaza, na uhakika wa chakula nchini Uganda. Makala tunaangazia mradi wa kulinda mazingira na kazi za kujitolea. Mashinani inamulika utayari wa nchi ya Nigeia kufanikisha Malengo ya Maendeleo Endelevu, SDGs. Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani, WFP, kupitia Apu yake ya kidigitali Gawa Chakula au ShareTheMeal, limeingia ushirikiano na Apu maarufu huko Mashariki ya Kati iitwayo Careem na kuzindua kampeni ya kuchangisha msaada wa dharura kwa watu wanaokumbwa na njaa katika eneo la Gaza na Ukingo wa Magharibi maeneo yanayokaliwa kimabavu na Israeli.Licha ya changamoto za ufadhili, Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) nchini Uganda linasisitiza umuhimu wa usafirishaji katika kutoa msaada wa chakula. Sahir Aslam, Mkuu wa Idara ya Ugavi ya WFP Uganda, akizungumza kutokea huko huko Uganda katika maghala ya shirika hilo anafafanua kila kilomita moja ambayo msaada wa chakula wa WFP unasafiri.Katika makala Assumpta Massoi anatupitisha kwenye kazi ya kujitolea iliyofanyika kuadhimisha siku ya Nelson Mandela Julai 18 hapa Marekani.Na katika mashinani fursa ni yake Esse Oduwan, msichana mwenye umri wa miaka 14 kutoka Nigeria, akihoji utayari wa nchi kufanikisha Malengo ya Maendeleo Endelevu, SDGs baada ya nchi tatu ikiwemo Eswatini na Bangladesh kuwasilisha tathmini za utekelezaji wa Malengo hayo yanayofikia ukomo 2030.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
Licha ya changamoto za ufadhili, Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) nchini Uganda linasisitiza umuhimu wa usafirishaji katika kutoa msaada wa chakula. Sahir Aslam, Mkuu wa Idara ya Ugavi ya WFP Uganda, akizungumza kutokea huko huko Uganda katika maghala ya shirika hilo anafafanua kila kilomita moja ambayo msaada wa chakula wa WFP unasafiri.
Huko Manispaa ya Caluquembe jimboni Hiula, Kusini Magharibi mwa Angola, Shirika la Afya Duniani (WHO), kwa kushirikiana na mamlaka za mitaa, limeongeza juhudi za ushirikishwaji wa jamii na afua za afya ya umma, ili kukabiliana na mlipuko wa kipindupindu unaoendelea nchini humo. Lengo kuu likiwa ni kuongeza uelewa kuhusu kipindupindu kupitia mikutano ya jamii, jumbe za afya ya umma, na ujenzi wa miundombinu muhimu kama vile vyoo na vituo vya kupata maji safi ya kunywa ndani ya manispaa. Sabrina Saidi amefuatilia na kueleza zaidi katika makala hii.
Jaridani leo naangazia hafla ya Siku ya Kimataifa ya Nelson Mandela katika makao makuu ya Umoja wa mataifa na ujumbe wa washindi wa Tozo ya Mandela. Makala tunakwenda nchini Angola na mashinani nchini Kenya, kulikoni?Umoja wa Mataifa leo katika makao yake makuu jijini New York, Marekani, umeadhimisha Siku ya Kimataifa ya Nelson Mandela kwa heshima ya maisha na urithi wa shujaa wa mapambano dhidi ya ubaguzi wa rangi, nchini Afrika Kusini, Nelson Rolihlahla Mandela, al maarufu Madiba. Assumpta Massoi amefuatilia na kutuandalia taarifa ifuatayo.Mapema kabla ya kushiriki hafla hii ya utoaji wa tuzo katika siku hii ya kimataifa ya Nelson Mandela hapa New York, Kennedy Odede alizungumza na Zipporah Musau wa Umoja wa Mataifa.Katika makala Sabrina Saidi anatupeleka huko Manispaa ya Caluquembe jimboni Hiula, Kusini Magharibi mwa Angola, Shirika la Afya Duniani (WHO), kwa kushirikiana na mamlaka za mitaa, limeongeza juhudi za ushirikishwaji wa jamii na afua za afya ya umma, ili kukabiliana na mlipuko wa kipindupindu unaoendelea nchini humo. Lengo kuu likiwa ni kuongeza uelewa kuhusu kipindupindu kupitia mikutano ya jamii, jumbe za afya ya umma, na ujenzi wa miundombinu muhimu kama vile vyoo na vituo vya kupata maji safi ya kunywa ndani ya manispaa.Na katika mashinani fursa ni yake Purity Christine, mwanzilishi mwenza wa kampuni ya ShopOkoa, jukwaa la kifedha linalowawezesha wajasiriamali wadogo na wa kati kujiunga na mfumo wa kijamii wa akiba na mikopo nchini Kenya, anasimulia safari yao kupitia Programu ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP ya timbuktoo Fintech, ambapo wamejifunza jinsi ya kuboresha jukwaa lao na kuweka malengo makubwa ya kufikia maelfu ya wafanyabiashara barani Afrika.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini Tanzania kumulika juhudi za kinamama wajawazito na wanao kuambatana wakihudhuria kliniki kwa ajili ya mimbasalama. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na mashinani.Takribani wapalestina 900 wameuawa katika wiki za hivi karibuni huko Ukanda wa Gaza, eneo linalokaliwa kimabavu na Israeli. wakihaha kupokea chakula. Msemaji wa Ofisi ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa Thameen Al-Kheetan amewaeleza waandishi wa habari Geneva, Uswisi kuwa watu 674 kati yao waliuawa wakiwa kwenye maeneo ya Mfuko wa Kiutu wa Gaza, (GHF) unaoendeshwa na Israeli na Marekani.Wakati huo huo Bwana Al-Kheetan amezungumzia mauaji yanayoendelea Ukingo wa Magharibi ikiwemo Yerusalemu Mashariki akisema, “muathirika mdogo zaidi ni Laila Khatib mwenye umri wa miaka miwili. Alipigwa risasi ya kichwa na jeshi la Israeli akiwa nyumbani kwao kijijini Ash-Shuhada.”Na leo ikiwa siku ya kimataifa ya stadi kwa vijana Sangheon Lee, Mkurugenzi wa Ajira na Sera katika Shirika la Umoja wa Mataifa la Ajira amesema …lazima tuhakikishe kuwa vijana wanapata ujuzi ambao ni wa maana, unaoweza kutumika katika mazingira mbalimbali, na unaotambuliwa na waajiri.Na kaika mashinani tunakupeleka jijini Nairobi, Kenya, ambako kupitia video iliyoandaliwa na washirika wetu Radio Domus, tunamsikia Dennis Mabuku, Mkuu wa Idara ya Usalama, Afya, Mazingira na Ubora katika kampuni ya BOC Kenya. Dennis anaeleza jinsi wanavyoichakata hewa ya kawaida na kuisafisha ili kupata hewa safi ya oksijeni kwa ajili ya matumizi ya hospitali na mabaki mengine kwa ajili ya matumizi mengine ya viwandani.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani (WHO) leo Julai 11 limetangaza kwamba limeidhinisha Burundi kuwa imefanikiwa kuondoa ugonjwa wa macho unaofahamika kama trakoma au vikope kama tatizo la kiafya la umma, na kuifanya kuwa nchi ya nane katika Kanda ya Afrika ya WHO kufikia mafanikio haya muhimu. Anold Kayanda anafafanua zaidi kuhusu taarifa hii.
Hii leo jaridani tunaangazia masuala ya afya nchini Burundi, na elimu ya upatanishi kwa jamii Ituri nchini DRC. Makala tunakupeleka nchini Kenya kumulika kilimo kichopatia riziki jamii na mashinani tunasalia hapa makao makuu kusikia ujumbe kuhusu haki za wasichana.Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani (WHO) leo Julai 11 limetangaza kwamba limeidhinisha Burundi kuwa imefanikiwa kuoandoa ugonjwa wa macho unaofahamika kama trakoma au vikope kama tatizo la kiafya la umma, na kuifanya kuwa nchi ya nane katika Kanda ya Afrika ya WHO kufikia mafanikio haya muhimu.Huko Djugu, jimboni Ituri, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, wanawake wapatanishi waliopatiwa mafunzo na ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo, MONUSCO, wamewezesha kurejea kwa mazungumzo baina ya jamii za Ezekere na Mandro ambazo kwa miaka kadhaa zilikuwa zinazozana.Katika makala Sharon Jebichii anatupeleka Kaunti ya Tana River huko Kenya kumulika juhudi za Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo (UNDP) kwa kushirikiana na Mamlaka ya Kitaifa ya Kusimamia Ukame (NDMA) na Serikali za Kaunti katika kilimo, ambayo imeleta mabadiliko na matumaini kwa jamii za wakulima.Na kaika mashinani leo ikiwa siku ya idadi ya watu duniani, nampisha Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu na AFya ya Uzazi, Dkt. Natalia Kanem akizungumzia umuhimu wa takwimu katika kuboresha maisha ya wakazi wa dunia!Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
Katika maeneo kame ya Kenya, mvua moja ikikosa kunyesha, inaweza kuleta njaa, umaskini na kukosa matumaini. Lakini badala ya kukata tamaa, jamii za wakulima katika kaunti za Tana River sasa zinatoa simulizi kwa ujasiri na mabadiliko. Kupitia msaada kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP) kwa kushirikiana na Mamlaka ya Kitaifa ya Kusimamia Ukame (NDMA) na Serikali za Kaunti, wakulima wanatumia teknolojia rafiki kama umwagiliaji wa maji kwa nishati ya jua, kilimo cha kisasa na ushirika wa kijamii kuinua maisha yao. Sharon Jebichii na maelezo zaidi.
Hii leo jaridani tunaangazia ziara ya Katibu Mkuu wa UN Amina J. Mohammed akiwa barani Afrika; na Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Viongozi kuhusu Upashanaji wa Taarifa duniani. Makala tunakwenda nchini Burundi na mashinanitunasalia hapa makao makuu, kulikoni?Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Amina J. Mohammed akiwa ziarani barani Afrika ambapo juzi tarehe 7 aliingia nchini Gambia, kwa njia ya mtandao wa X ameonesha namna ziara yake ilivyokuwa ya mafanikio kwa kukutana na viongozi na wadau mbalimbali nchini humo katika harakati za kufanikisha Malengo ya Umoja wa Mataifa ya Maendeleo Endelevu.Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Viongozi kuhusu Upashanaji wa Taarifa duniani, (WSIS) ukiingia siku ya 3 hii leo huko Geneva, Uswisi, washiriki wanapazia sauti umuhimu wa kila mtu kokote pale aliko afikiwe na teknolojia inayomwezesha kupokea taarifa kwa urahisi, usahihi na kwa haraka.Katika makala shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu (UNFPA), kwa kushirikiana na serikali ya Burundi, limekuwa mstari wa mbele katika kuwasaidia vijana wakimbizi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), walioko kwenye kambi ya Musenyi, mkoani Rutana huko Burundi. Kupitia michezo, tamaduni, na shughuli za elimu ya afya ya uzazi, vijana hawa wamepata matumaini mapya na fursa ya kujenga maisha yao upya. Mradi huu unaangazia umuhimu wa kuwekeza kwa vijana walioko katika mazingira magumu ili kuwasaidia kufikia ndoto zao.Na katika mashinani fursa ni yake Dkt. Natalia Kanem, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu na afya ya uzazi UNFPA ambaye katika mahojiano maalum na Idhaa ya Umoja wa Mataifa amesisitiza kuwa kila msichana anahitaji huduma muhimu za afya uzazi ili waweze kuendelea na elimu, akitaja mfano wa kazi zao nchini Kenya.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu (UNFPA), kwa kushirikiana na serikali ya Burundi, limekuwa mstari wa mbele katika kuwasaidia vijana wakimbizi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), walioko kwenye kambi ya Musenyi, mkoani Rutana huko Burundi. Kupitia michezo, tamaduni, na shughuli za elimu ya afya ya uzazi, vijana hawa wamepata matumaini mapya na fursa ya kujenga maisha yao upya. Mradi huu unaangazia umuhimu wa kuwekeza kwa vijana walioko katika mazingira magumu ili kuwasaidia kufikia ndoto zao.
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayoturejesha katika mkutano wa 69 wa kamisheni ya hali ya wanawake duniani CSW69 kumsikia Mkurugenzi wa TEN/MET Nasra Kibukila kuhusu jitihada zao za kuhakikisha watoto wote wa Kitanzania wanapata elimu bora, jumuishi na yenye usawa, kwa kushirikiana na Serikali na wadau mbalimbali wa elimu ndani na nje ya nchi.Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa Volker Turk, amesikitishwa sana na mauaji ya jana ya watu wapatao 10, sambamba na uporaji na uharibifu wa mali wakati polisi walipokabiliana na waandamanaji kwenye mji mkuu wa Kenya, Nairobi na katika kaunti nyingine 16.Huko Geneva, Uswisi kumeanza mkutano wa siku 4 kuhusu matumizi ya Akili Mnemba au AI kwa maslahi ya wote ambapo Katibu Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la mawasiliano, ITU, Doreen Bogdan-Martin ameuliza washiriki ni jambo gani wanafanya AI ihudumie ubinadamu.?Na kuelekea kumbukizi yamauaji ya Srebrenica tarehe 11 mwezi huu wa julai, Umoja wa Mataifa unakumbuka mauaji hayo yaliyofanyika wakati wa vita vilivyofuatia baada ya kuvunjika kwa iliyokuwa Yugoslavia. Zaidi ya watu 100,000 huko Bosnia na Herzegovina waliuawa kati ya mwaka 1992 na 1995, wengi wao wakiwa waislamu wa Bosnia. Umoja wa Mataifa unasema mauaji ya Srebrenica ni moja ya vipindi vya kiza zaidi vya vita.Na katika mashinani tunakupeleka katika miji ya mpakani ya Matar na Muon katika eneo la Gambella nchini Ethiopia ambako maelfu ya wakimbizi wamewasili kutoka Jimbo la Upper Nile nchini Sudan Kusini wakikimbia vita na njaa, na sasa wanasubiri usajili na usaidizi kutoka kwa Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula. Nyandow Wie Deng ni mmoja akisimulia yaliyomkumba.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
Hii leo jaridani tunaangazia wahamiaji na njia bunifu ya kuwawezesha kujikimu kimaisha, na malezi bora ya watoto nchini Tanzania. Makala tunasalia huko huko Tanzania kumulika uwekezaji na ufadhili wa miradi ya maendeleo, na mashinani tunakwenda nchini Kenya.Katika Mkutano wa 4 wa Kimataifa wa Ufadhili wa Maendeleo (FFD4) unaoendelea jijini Seville, Hispania, Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji (IOM) limetoa wito wa kuimarisha uwekezaji wa kibunifu katika uhamiaji wa watu ili kuchochea ukuaji wa uchumi na kusaidia kuziba pengo la kila mwaka la dola trilioni 4 za ufadhili wa maendeleo.Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF limekuwa likihimiza umuhimu wa malezi na makuzi chanya kwa watoto kama njia mojawapo ya kulinda haki kuu nne za msingi za mtoto ambazo ni kuishi, kuendelezwa, kushirikishwa na kulindwa..Katika makala mkutano wa 4 wa Ufadhili wa Maendeleo (FFD4) ukikunja jamvi leo huko Sevilla Hispania, juhudi za kuhakikisha nchi zinajitegemea kifedha kupitia vyanzo jumuishi na vya ubunifu zimezidi kupewa kipaumbele. Katika hafla ya kufungua mafunzo ya Muongozo wa Upatikanaji wa Fedha kwa Mamlaka za Serikali za Mitaa, au Intergrated Local Financing Framework (ILFF) yaliyofanyika katika Manispaa ya Morogoro kaskazini-mashariki mwa Tanzania hivi majuzi , Umoja wa Mataifa kupitia shirika lake la Mpango wa Maendeleo nchini humo, UNDP umetoa mafunzo ya namna halmashauri zinaweza kuandaa mikakati madhubuti ya kuhimiza maendeleo ya ndani kupitia ushirikiano kati ya sekta binafsi, mashirika ya kiraia, benki na jamii.Na mashinani, vijana na wahudumu wa afya katika kaunti ya Kajiado nchini Kenya, wameshikamana kuhamasisha umma kuhusu hedhi salama. Kupitia video iliyoandaliwa na washirika wetu Radio Domua, mmoja wa vijana anaelezea umuhimmu wa hedhi salama kama njia ya kutokomeza unyanyapaa dhidi ya wanawake na wasichana.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF limekuwa likihimiza umuhimu wa malezi na makuzi chanya kwa watoto kama njia mojawapo ya kulinda haki kuu nne za msingi za mtoto ambazo ni kuishi, kuendelezwa, kushirikishwa na kulindwa.
Katika Mkutano wa nne wa kimataifa wa Ufadhili wa Maendeleo (FFD4) unaoendelea jijini Seville, Hispania, Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji (IOM) limetoa wito wa kuimarisha uwekezaji wa kibunifu katika uhamiaji wa watu ili kuchochea ukuaji wa uchumi na kusaidia kuziba pengo la kila mwaka la dola trilioni 4 za ufadhili wa maendeleo. Anold Kayanda anaeleza zaidi.