Podcasts about maendeleo

  • 32PODCASTS
  • 221EPISODES
  • 15mAVG DURATION
  • 5WEEKLY NEW EPISODES
  • May 9, 2025LATEST

POPULARITY

20172018201920202021202220232024


Best podcasts about maendeleo

Latest podcast episodes about maendeleo

Habari za UN
Chokoleti itengenezwayo Uganda yavuka mpaka na mabara -UNCTAD

Habari za UN

Play Episode Listen Later May 9, 2025 3:55


Kutoka kakao ghafi huko Bundibugyo, magharibi mwa Uganda hadi Kampala mji mkuu wa kibiashara wa taifa hilo la Afrika Mashariki ndiko kunapatikana kiwanda cha kutengeneza chokoleti cha Equator kinachomilikiwa na Barbara Gonget na mume wake Gustav. Awali wazo la biashara hii lilionekana kutokuwa na mashiko. Ingawa hivyo baada ya ITC, ambacho ni Kituo cha Kimataifa ha Biashara kilicho chini ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Biashara na Maendeleo, UNCTAD pamoja na wadau wao kuweka usaidizi wao, hali imebadilika na sasa biashara inavuka sio tu mipaka bali mabara. Wawili hao Kwa kuchanganya mbinu za hali ya juu, zinazojali jamii, na ufundi wa kitaalamu, wanabadili taswira ya uzalishaji wa chokoleti nchini humo.Je wamefanya nini? Assumpta Massoi anafafanua zaidi kwenye makala hii iliyofanikishwa na ITC.

Habari za UN
06 MEI 2025

Habari za UN

Play Episode Listen Later May 6, 2025 12:03


Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayoturejesha hapa makao makuu ambako Idhaa hii Dokta Willis Ochieng kutoka Kenya aliyehudhuria ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika lisilo la kiserikali linalojihusisha na masuala ya kilimo na maendeleo. Pia tunakuletea muhtasari wa habari, na mashinani tunakwenda Ghana.Ukuaji wa maendeleo ya binadamu – yanayopimwa kwa uhuru na ustawi wa watu – umeendelea kuwa wa kasi ndogo tangu mshtuko mkubwa wa janga la COVID-19 lakini kuna matumaini makubwa kwamba Akili Mnemba au AI, ikiwa itatumika kwa njia sahihi, inaweza kuwa chombo chenye nguvu cha kuboresha maisha ya mamilioni ya watu. Hii ni kwa mujibu wa Ripoti ya kila mwaka ya Maendeleo ya Binadamu iliyotolewa leo na Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo duniani, UNDP.Kulengwa kwa hospitali ya Médecins Sans Frontières nchini Sudan Kusini kunaweza kuwa uhalifu wa kivita imeeleza leo Kamisheni ya Umoja wa Mataifa kuhusu Haki za Binadamu Sudan Kusini kufuatia mashambulizi ya angani yaliyotekelezwa dhidi ya hospitali ya Médecins Sans Frontières (MSF) huko Old Fangak, Jimbo la Jonglei mapema majuzi asubuhi ya Jumamosi na kusababisha vifo vya takribani raia saba na kujeruhi wengine. Shambulio hilo lilifanyika baada ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Sudan Kusini (SSPDF) kutoa onyo la kufanya shambulizi iwapo dai lao la kuachiliwa meli zao zilizotekwa halitatekelezwa.Ripoti mpya ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani, WHO, iliyotolewa leo imeonesha jinsi mahali mtu anakozaliwa kulivyo na mchango katika maisha yake. Ripoti inasema, “mahali mtu anakozaliwa huweza kuamua kama ataishi zaidi ya miongo mitatu kuliko mtu mwingine aliyezaliwa katika nchi yenye hali duni za makazi, elimu na fursa za ajira.”Na mashinani leo nampa fursa Dorcas Awortwe, Naibu Mkurugenzi wa Tume ya Maendeleo ya Kanda ya Kati kutoka Ghana, aliyeshiriki kwenye mkutano wa jukwaa la watu wa asili hapa Makao Makuu wiki iliyopita anazungumzia changamoto zinazowakabili watu wa asili katika jamii yake na ombi lake kwa Umoja wa Mataifa.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!

Habari za UN
WFP yasaidia wananchi Sudan Kusini kupambana na mabadiliko ya tabianchi

Habari za UN

Play Episode Listen Later Apr 28, 2025 1:46


Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani WFP nchini Sudan Kusini chini ya ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Korea KOICA wanaendesha mradi wa kusaidia wananchi katika kilimo ili kujenga ustahimilivu na kupambana na utapiamlo. Tupate taarifa zaidi kutoka kwa Evarist Mapesa.

umoja mataifa maendeleo shirika wananchi sudan kusini
Habari za UN
28 APRILI 2025

Habari za UN

Play Episode Listen Later Apr 28, 2025 10:39


Hii leo jaridani tunaangazia siku ya Kimataifa ya Usalama na Afya Kazini, na juhudi za Umoja wa Mataifa za kusaidia wakulima Sudan Kusini kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi. Makala tunasalia na usalama kazini na mashinani tunakwenda nchini Kenya, kulikoni?Leo ni Siku ya Kimataifa ya Usalama na Afya Kazini mwaka huu ikibeba maudhui “Mapinduzi ya usalama na afya Kazini: Nafasi ya Akili mnemba na teknnolojia ya kidijitali mahala pa kazi” lengo likiwa kudhihirisha nguvu ya AI na teknolojia zinapotumika vyema zinaweza kuleta mabadiliko kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kazi duniani ILO.Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani WFP nchini Sudan Kusini chini ya ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Korea KOICA wanaendesha mradi wa kusaidia wananchi katika kilimo ili kujenga ustahimilivu na kupambana na utapiamlo. Tupate taarifa zaidi kutoka kwa Evarist Mapesa.Makala tunabisha hodi nchini Indonesia, taifa hili la Kusini-Mashariki mwa bara la Asia, kubwa hasa ni kumulika ni kwa vipi sekta ya uvuvi nchini humu inatekeleza kivitendo wito wa shirika la Umoja wa Mataifa la Kazi, ILO kuhusu usalama na afya Kazini.  Na katika mashinani fursa ni yake Abdikani Haji Hassan kutoka kambi ya wakimbizi ya Daadab iliyoko katika kaunti ya Garissa nchini Kenya ambaye  kupitia Mpango wa Prospects unaoungwa mkono na Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF amejikwamua kimaisha na sasa ana ndoto ya kuenda ng'ambo ili kuendeleza ujuzi wake wa kupiga picha.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!  

Habari za UN
Chata ya Umoja wa Mataifa inasongesha amani, maendeleo, urafiki na haki za binadamu - Balozi Yabesh Monari

Habari za UN

Play Episode Listen Later Apr 24, 2025 6:42


Tarehe 25 mwezi Aprili kila mwaka ni siku ya kimataifa ya wajumbe wanaowakilisha nchi zao kwenye Umoja wa Mataifa. Tarehe hiyo mwaka 1945 ndio ulianza mkutano huko San Francisco, Marekani wa wajumbe 850 kutoka nchi 50 waliopitisha Chata ya Umoja wa Mataifa ikilenga kusongesha amani, maendeleo, urafiki na haki za binadamu. Kama unavyofahamu Umoja wa Mataifa sasa umekua na idadi ya wanachama ni 193 na kila moja hupeleka wawakilishi kufanikisha utekelezaij wa malengo ya Umoja huo. Lengo la siku ni kuwatambua kwani wao ndio wamepewa jukumu la kufanikisha chata hiyo. Je wajumbe hao hufanya nini? Assumpta Massoi amezungumza na Balozi Yabesh Monari wa Kenya kwenye mada hii kwa kina.

Habari za UN
Vijana tuna jukumu muhimu katika maendeleo ya jamii zetu tuchangamkie fursa: Winfred Njiru

Habari za UN

Play Episode Listen Later Apr 11, 2025 3:26


Umoja wa Mataifa unaendelea kuchagiza vijana kujitokeza na kushiriki katika kusongesha ajenda ya maendeleo endelevu katika jamii zao na ndio maana wiki iliyopita majadiliano ya viongozi wastaafu kuhusu maendeleo endelevu ya Club De Madrid yaliyofanyika Nairobi Kenya yalitoa fursa kwa vijana kupaza sauti zao kuhusu jinsi wataavyochangia kufanikisha malengo hayo.  Winfred Njiru mwanafunzi wa chuo kikuu fani ya uhakiki au quantity surveyor alizungumza na Stella Vuzo kutoka kitengo cha habari cha Umoja wa Mataifa UNIS Nairobi na kumueleza matahali Kenya vijana wanapaswa kufanya nini ili kuchangia katika maendeleo.

Habari za UN
Dayspring Foundation nchini Tanzania yatekeleza kivitendo dhana ya UN ya michezo kwa maendeleo

Habari za UN

Play Episode Listen Later Apr 7, 2025 4:04


Siku ya kimataifa ya Michezo kwa ajili ya Maendeleo na Amani imeadhimishwa tarehe 6 mwezi huu wa Aprili maudhui yakiwa Ujumuishaji wa kijamii, hususan makundi ya pembezoni. Umoja wa Mataifa kupitia wavuti wake unasema kuwa siku hii inatambuliwa kutokana na nafasi ya michezo katika kuleta mabadiliko chanya, kuondoa vikwazo na kuvuka mipaka. Na usuli wa maudhui ya mwaka huu ni kwamba fikra potofu kwenye jamii zimesababisha baadhi ya watu kutokana na jinsia yao, umri, au rangi wanashindwa kushiriki kwenye michezo ambayo kwa njia moja au nyingine hutokomeza umaskini kwa kuwezesha washiriki kujipatia kipato. Nchini Tanzania shirika la kiraia la Dayspring Foundation limetambua nafasi ya michezo na limeanza kuchukua hatua. Assumpta Massoi wa Idhaa hii amezungumza na Muasisi na Mkurugenzi Mtendaji wa shirika hilo, Rosemary Mwaipopo ambaye anaanza kwa kuelezea ni kwa nini waliamua kujikita katika kusaka vipaji.

Mazingira Leo, Dunia Yako Kesho
Juhudi zinazofanywa na wadau kufadhili wakulima wadogo barani Afrika

Mazingira Leo, Dunia Yako Kesho

Play Episode Listen Later Mar 28, 2025 10:12


Wakulima wadogo wanachangia kwa zaidi ya asilimia 70 uzalishaji wa chakula barani Afrika, hii ni kwa mujibu wa Benki ya Maendeleo barani, Afdb, wakati uo huo, lengo nambari mbili  ya maendeleo endelevu ikinuia kumaliza njaa na kuihakikishia dunia usalama wa chakula kufikia mwaka wa 2030

Habari za UN
20 MACHI 2025

Habari za UN

Play Episode Listen Later Mar 20, 2025 12:27


Hii leo jaridani katika mada kwa kina tunajikita katika mkutano CSW69 ambao umebakiza siku moja tu, kesho Machi 21 unakunja jamvi, na tunamsikia Dkt. Dorothy Gwajima, Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia Tanzania, Waziri Riziki Pembe kutoka Zanzibar na Profesa Smile Dzisi, Mkugenzi wa Shirika la “I believe Global” kutoka Ghana.Kamishna Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi, UNHCR Filippo Grandi amesema kukata ufadhili kwa mashirika yanayotoa huduma za kibinadamu kunasababisha janga la uwajibikaji. Kupitia taarifa iliyotolewa leo Geneva, Uswisi na UNHCR, Bwana Grandi amesema kukata ufadhili kunaweka hatarini maisha ya mamilioni ya watu na madhara yake kwa watu wanaokimbia majanga, yatakuwa makubwa zaidi na yataonekana wazi ikiwemo wanawake na watoto wa kike kukosa huduma zitokanazo na kubakwa.Leo ni siku ya furaha duniani maudhui yakimulika umuhimu wa watu kusaidiana na kujaliana katika masuala mbalimbali ikiwemo chakula. Ripoti mpya ya wadau wa UN iliyozinduliwa leo imeonesha kuwa nchi yenye furaha zaidi duniani ni Finland na ya mwisho kabisa ni Afghanistani. Katika 10 bora zenye furaha hakuna hata moja ya Afrika, ilihali kwenye 10 za mwisho nchi za Afrika ni 7 ambazo ni Lesotho, Comoro, Botswana, Zimbabwe, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, Malawi na Sierra Leone.Mkutano wa 69 wa Kamisheni ya Hali ya Wanawake duniani, CSW69 ukikaribia ukingoni hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa tumemuuliza mshiriki Wakili Rosemary Mwaipopo kutoka Tanzania mkutano umekidhi kiu yake ya kusongesha usawa wa kijinsia?Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili hii leo mchambuzi wetu mlumbi wa Kiswahili Joramu Nkumbi kutoka nchini Tanzania, anafafanua maana ya maneno “Ashiraf, Janabi, gayagaya, kiti cha marimba na kiti cha msaji”Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!  

Habari za UN
17 MACHI 2025

Habari za UN

Play Episode Listen Later Mar 17, 2025 11:28


Hii leo jaridani tunaangazia madeni katika nchi zenye mapato ya chini na ujumbe wa washiriki wa 69 wa Kamisheni ya Hali ya Wanawake duniani CSW69 hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa.Mkutano wa 14 wa Kimataifa wa Usimamizi wa madeni umeanza rasmi hii leo huko Geneva Uswisi ambapo kubwa linalojadiliwa ni namna ya kuhakikisha wakati serikali zikipambana kulipa madeni hazidumazi maendeleo.Akijibu swali la kwa nini pamoja na ongezeko na idadi ya wanawake katika ngazi za uamuzi nchini Tanzania lakini bado kuna changamoto zinazoukabili usawa wa kijinsia, Dkt. Dorothy Gwajima, Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu anayehudhuria mkutano wa 69 wa Kamisheni ya Hali ya Wanawake, CSW69 jijini New York, Marekani kupitia mahojiano maalumu na Anold Kayanda wa Idhaa hii ya Umoja wa Mataifa, anaeleza kuwa      mabadiliko chanya katika jamii hayaji kwa kutumia mabavu.Makala pia inatubakisha hapa Umoja wa Mataifa kwenye mkutano wa 69 wa Kamisheni ya Hali ya Wanawake duniani CSW69. Ili kufanikisha lengo la usawa wa kijinsia Umoja wa Mataifa unasisitiza ushiriki wa wanaume katika mchakato hasa kwa kuzingatia kuwa mfumo dume miaka nenda miaka rudi umekuwa kikwazo cha kufikia lengo hilo, Flora Nducha amebahatika kuzungumza na mmoja wa wanaume wanaoshiriki mkutano huo kusikia maoni yake.Na katika mashinani baadhi ya washiriki wa mkutano wa CSW69 wakizungumza na idhaa hii kandoni mwa mkutano huo, wametoa wito wa mshikamano na msichana na mwanamke yeyote anayepitia changamoto kote duniani hususani wale wanaorejea shuleni baada ya kusitisha masomo kutokana na ujauzito kabla ya wakati. Mshiriki wa kwanza ni Nasra Kibukila anayewakilisha Mtandao wa Elimu Tanzania, TEN/Met.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!  

Habari za UN
Mabadiliko chanya katika jamii yanakuja kwa kueleweshana - Dkt. Gwajima

Habari za UN

Play Episode Listen Later Mar 17, 2025 2:05


Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu Waziri, Dkt. Dorothy Gwajima,  ni mmoja wa wanaohudhuria mkutano wa 69 wa Kamisheni ya Hali ya Wanawake, CSW69 hapa katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani. Anold Kayanda wa Idhaa hii amekutana naye na miongoni mwa mambo mengi amemuuliza ni kwa nini pamoja na ongezeko na idadi ya wanawake katika ngazi za uamuzi nchini Tanzania lakini bado kuna changamoto nyingi zinazoukabili usawa wa kijinsia nchini humo?

Habari za UN
14 MACHI 2025

Habari za UN

Play Episode Listen Later Mar 14, 2025 9:59


Hii leo jaridani tunaangazia ziara ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres huko Bangladesh, na yaliyojiri hapa makao makuu katika mkutano wa CSW69. Makala na mashinani tunasalia hapa hapa makao makuu, kulikoni?Akiwa ziarani katika kambi kubwa zaidi ya wakimbizi duniani, Cox's Bazar, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres leo Machi 14 ameonya kuhusu hali mbaya ya kibinadamu inayowakabili zaidi ya wakimbizi milioni moja wa Rohingya nchini Bangladesh.Hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa, mkutano wa Kamisheni ya Hali ya wanawake Duniani CSW69 unaendelea kujadili mafanikio yaliyopatikana na nini kifanyike zaidi kutimiza lengo la miaka 30 iliyopita la azimio la Beijing. Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Mkutano huo wa mwaka 1995 yuko kwenye mkutano huu CSW69 Flora Nducha wa Idhaa alipata fursa ya kuuliza nini tathimini yake ya utekelezaji wa azimio la Beijing na kinachohitajika zaidi kutimiza lengo la azimio hilo.Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia Kongo DRC hii leo Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo MONUSCO umekabidhi magari sita kwa gavana wa kijeshi wa jimbo la Kivu Kaskazini ili kuwezesha shughuli za polisi katika kuimarisha ulinzi na usalama.Makala tunasalia hapa hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa lakini kwanza ni makala ambapo Assumpta Massoi anazungumza na mshiriki wa CSW69 kutoka Cote D'Ivoire.Na katika mashinani Felicite Djoukouo Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Wadau wa Maendeleo nchini Cameroon ambaye anashiriki mkutano wa CSW69 hapa Umoja wa Mataifa anaelezea matarajio yake ya mkutano huu utakaomalizika tarehe 21 mwezi huu wa Machi.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!  

Radio Maria Tanzania
Fahamu ujumbe wa siku ya Wanawake duniani 2025.

Radio Maria Tanzania

Play Episode Listen Later Mar 4, 2025 25:29


Karibu uungane nami Agatha Kisimba katika kipindi maalaumu cha Jinsia na Maendeleo, ikiwa ni kuelekea siku ya wanawake duniani inayoadhimishwa kila mwaka March 08, Mwaka huu 2025 ikiwa na kauli mbiu ya Wanawake na Wasichana tuimarishe haki, usawa na uwezeshaji. L'articolo Fahamu ujumbe wa siku ya Wanawake duniani 2025. proviene da Radio Maria.

Radio Maria Tanzania
Je, wafahamu kwanini kuna watoto wa Mitaani?

Radio Maria Tanzania

Play Episode Listen Later Feb 20, 2025 45:31


Karibu uungane nami Martin Joseph, katika kipindi cha Elimu Jamii Mwezeshaji ni Bi. Blandina Sekela, Afisa Ustawi wa Jamii Wizara ya Maendeleo na Makundi Maalumu,  Dawati la Haki za Watot0 Kisheria  mada Watoto wanaoishi na wanao fanya kazi Mtaani. L'articolo Je, wafahamu kwanini kuna watoto wa Mitaani? proviene da Radio Maria.

Radio Maria Tanzania
Fahamu umuhimu wa kushiriki kupinga ukatili wa Kijinsia Mtandaoni.

Radio Maria Tanzania

Play Episode Listen Later Feb 18, 2025 24:35


Karibu uungane nami Elizabeth Masnja, katika kipindi cha Jinsia na Maendeleo, Mada ya leo Madhara Ukatilili wa Kijinsia Mtandaoni. L'articolo Fahamu umuhimu wa kushiriki kupinga ukatili wa Kijinsia Mtandaoni. proviene da Radio Maria.

Habari za UN
Kenya tumepiga hatua kuhakikisha maendeleo ya ustawi wa jamii: Mary Wambui Munene

Habari za UN

Play Episode Listen Later Feb 14, 2025 4:58


Kikao cha 63 cha Baraza la Kiuchumi na Kijamii la Umoja wa Mataifa ECOSOC kuhusu maendeleo ya ujamii kinakunja jamvi hii leo jijini New York Marekani baada ya majadiliano ya juma zima kuhusu maendeleo ya ustawi wa jamii, hatua zinazochukuliwa nan chi katika kufanikisha hilo na kuchagiza mshikamano wa kimataifa kutimiza lengo. Nchi mbalimbali zimetuma wakilishi kuanzia katika ngazi ya serikali, taasisi, mashirika yasiyo ya kiserikali na asasi za kiraia. Flora Nducha wa Idhaa hii amepata fursa kuzungumza na Mary Wambui Munene, mmoja wa washiriki kutokana Kenya. Ungana nao katika Makala hii

Gurudumu la Uchumi
Migogoro inavyotatiza ukuaji wa uchumi, maendeleo na utawala bora Afrika

Gurudumu la Uchumi

Play Episode Listen Later Feb 12, 2025 9:43


Hujambo msikilizaji wa RFI Kiswahili popote pale unapotegea sikio matangazo yetu, makala ni Gurudumu la Uchumi na leo hii tunazungumzia kuhusu athari za kiuchumi kutokana na mizozo kwenye nchi za Afrika.Tutazungumza na Hamduni Marcel, mchambuzi wa siasa za kimataifa akiwa Tanzania na Ali Mkimo, mchambuzi wa masuala ya uchumi akiwa Tanzania.

Gurudumu la Uchumi
Migogoro inavyotatiza ukuaji wa uchumi, maendeleo na utawala bora Afrika

Gurudumu la Uchumi

Play Episode Listen Later Feb 12, 2025 9:59


Hujambo msikilizaji wa RFI Kiswahili popote pale unapotegea sikio matangazo yetu, makala ni Gurudumu la Uchumi na leo hii tunazungumzia kuhusu athari za kiuchumi kutokana na mizozo kwenye nchi za Afrika.Tutazungumza na Hamduni Marcel, mchambuzi wa siasa za kimataifa akiwa Tanzania na Ali Mkimo, mchambuzi wa masuala ya uchumi akiwa Tanzania.

Radio Maria Tanzania
Zifahamu mbinu za kuwalea Watotoa katika tabia njema

Radio Maria Tanzania

Play Episode Listen Later Feb 5, 2025 21:45


Karibu uungane nami Elizabeth Masanja, katika kipindi cha Jinsia na Maendeleo  mada,  juu ya ukosefu wa Maadili kwa Watoto, Je ni malezi dhaifu kwa Wazazi? L'articolo Zifahamu mbinu za kuwalea Watotoa katika tabia njema proviene da Radio Maria.

Habari za UN
29 JANUARI 2025

Habari za UN

Play Episode Listen Later Jan 29, 2025 9:59


Hii leo jaridani tuanaangazia masuala ya ufadhili wa huduma za afya, na kilimo cha cacao nchini Liberia. Makala inatupeleka nchini DRC na mashinani nchini Kenya, kulikoni?Baada ya Serikali ya Marekani kutoa tangazo jipya sasa kwamba itaendelea kufadhili huduma zinazolenga vita dhidi ya Virusi vya Ukimwi (VVU), shirika la Umoja wa Mataifa la kukabiliana na VVU na Ukimwi (UNAIDS) limeeleza kuupokea uamuzi huo kwa furaha na kuuita wa kuokoa maisha.Kilimo bora cha kakao huko Liberia kimemwondolea uchovu na kukosa kulala, mkazi wa kaunti ya Nimba, kaskazini mashariki mwa Liberia, baada ya mradi wa mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Maendeleo ya Kilimo, IFAD nchini humo kumwezesha sio tu kugeukia kilimo, bali pia kuajiri vijana wengine na hivyo kufanikisha lengo la Umoja wa Mataifa la kuondokana na umaskini.Makala inatupeleka kwenye msitu wa bonde la mto Congo nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC wa pili kwa ukubwa duniani unaofyonza kiasi kikubwa cha hewa ukaa, ambako mradi wa Umoja wa Mataifa wa kulinda bayoanuwai na kupambana na umasikini UNREDD unaleta nuru kwa jamii na mazingira.Na mashinani fursa ni yake fursa ni yake Esther Wangoi Mbugua, Mama mfugaji nyuki kutoka Kaunti ya Kajiado nchini Kenya ambaye alizungumza na washirika wetu Redio Domus akieleza kuwa ameweza kujipatia kipato na kumudu mahitaji ya familia yake kupitia mradi wa ufugajji nyuki.Mwenyeji wako niAnold Kayanda karibu!  

Habari za UN
Kutoka dereva wa teksi hadi mkulima wa kakao: IFAD Liberia

Habari za UN

Play Episode Listen Later Jan 29, 2025 1:51


Kilimo bora cha kakao huko Liberia kimemwondolea uchovu na kukosa kulala, mkazi wa kaunti ya Nimba, kaskazini mashariki mwa Liberia, baada ya mradi wa mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Maendeleo ya Kilimo, IFAD nchini humo kumwezesha sio tu kugeukia kilimo, bali pia kuajiri vijana wengine na hivyo kufanikisha lengo la Umoja wa Mataifa la kuondokana na umaskini. Assumpta Massoi anasimulia zaidi.

VOA Express - Voice of America
Vijana huko mashariki mwa DRC wanaelezea hali ya mapigano katika eneo na namna inavyoathiri shughuli zao za kila siku za kuleta maendeleo. - Januari 28, 2025

VOA Express - Voice of America

Play Episode Listen Later Jan 28, 2025 29:58


VOA Express pia inafuatilia kwa karibu sana maswala yanayovuma katika mitandao ya kijamii kama sehemu moja muhimu ya upashanaji habari siku hizi.

Habari za UN
Hali tete ikiendelea Goma DRC, MONUSCO/SAMIDRC wadhibiti uwanja wa ndege

Habari za UN

Play Episode Listen Later Jan 27, 2025 2:19


Hali ya usalama kwenye mji mkuu wa jimbo la Kivu Kaskazini, Goma, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, ikiendelea kuwa tete, ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani, nchini humo, MONUSCO pamoja na SAMIDRC ambao ni ujumbe wa kulinda amani kutoka Jumuiya ya Maendeleo ya nchi za Kusini mwa Afrika, SADC wanadhibiti uwanja wa ndege wa Goma. Ripoti ya Selina Jerobon inafafanua zaidi.

Habari za UN
27 JANUARI 2025

Habari za UN

Play Episode Listen Later Jan 27, 2025 9:59


Hii leo jaridani tunaangazia machafuko nchini DRC yanosababishwa na kundi la waasi la M23 mjini Goma. Makala tunakupeleka nchini Tanzania na mashinani ikiwa leo ni siku ya kimataifa ya kukumbuka waathiriwa wa mauaji ya halaiki tutasikia ujumbe wa Umoja wa Mataifa.Hali ya usalama kwenye mji mkuu wa jimbo la Kivu Kaskazini, Goma, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, ikiendelea kuwa tete, ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani, nchini humo, MONUSCO pamoja na SAMIDRC ambao ni ujumbe wa kulinda amani kutoka Jumuiya ya Maendeleo ya nchi za Kusini mwa Afrika, SADC wanadhibiti uwanja wa ndege wa Goma.Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, MONUSCO kwa kushirikiana na polisi wa kitaifa wa nchi hiyo  PNC wameongeza doria katika kambi ya wakimbizi wa ndani ya Bushagara jimboni Kivu Kaskazini kufuatia ongezeko la vitisho na mashambulizi ya kundi la wapiganaji wa M23.Katika makala Anold Kayanda anatupeleka nchini Tanzania ambako katika kuhamasisha elimu iliyo salama inayolenga kumlea na kumfundisha mtoto kwa njia chanya zisizoumiza, Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto, (UNICEF) linamuangazia Mwalimu Magesa Stanslaus ambaye ambaye amebadilika kutoka katika matumizi ya viboko na sasa anatumia motisha tofauti kuwarekebisha wanafunzi wake.Na mashinani fursa ni yake Miguel Ángel Moratinos, Mwakilishi wa Ngazi ya Juu wa Muungano wa Ustaarabu Umoja wa Mataifa UNAOC akitoa ujumbe kuhusu mauaji ya halaiki na sheria za kimataifa za haki za binadamu.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!  

Habari za UN
Asante IFAD kwa kutuwezesha watu wenye ulemavu Liberia

Habari za UN

Play Episode Listen Later Jan 22, 2025 1:57


Nchini Liberia, mradi unaotekelezwa na Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Maendeleo ya Kilimo, IFAD umejengea uwezo watu wenye ulemavu wa kuona na kuwawezesha kuongeza vipato na vile vile uhakika wa kupata chakula. Simulizi ya Sabrina Moshi wa redio washirika SAUT FM mkoani Mwanza nchini Tanzania, inaelezea zaidi.Tuko kaunti ya Lofa, kaskazini kabisa mwa Liberia, magharibi mwa Afrika, tunakutana na Hawa Kamara, yeye ni mlemavu wa kutoona. Yeye pamoja na wenzake wa chama cha watu wenye ulemavu wa kutoona hapa Lofa, wanathibitisha kuwa unapoamua kufanya kitu, hakuna kinachokuzuia.Kupitia mradi wa Mabadiliko ya kilimo kwa wakulima wadogo na uchechemuzi wa kilimo biashara au STAR-P, mavuno ya mpunga kwenye shamba la kikundi hicho, yameongezeka kwa asilimia 300.Hawa anasema, “Mwanzoni hatukuwa na kitu kabisa. Tulihangaika sana kulima mpunga. Lakini baada ya IFAD kutufikia katika maisha yetu na kutusaidia, mambo yalianza kubadilika. Walitupatia pembejeo na mbegu za ubora wa juu kuanzisha mashamba. Tulitumia mbegu hizo kupanda kwenye mashamba yetu Bakadu.”Awali walilima ekari 1.2 tu, lakini baada ya kupatiwa vifaa vya kisasa vya kilimo wameweza kulima hadi ekari 4.3.Mavuno ya mpunga yameongezeka. Wanasagisha mashine, kiasi cham chele wanauza na ziada ni kwa ajili ya matumizi ya nyumbani.Hawa akiwa kwenye shamba lake la mpunga anasema,“Kabla ya STAR-P nilijihisi nimepotea na mpweke. Lakini sasa ninaweza kulima mwenyewe shambani, na ninaweza kujihudumia mimi na pia familia yangu. Zamani niliacha shule. Lakini baada ya kuanza mradi huu, nimerejea shuleni na ninataka kuwa mhasibu mkubwa duniani.”

Habari za UN
Msichana Bangladesh: Sikufahamu ufundi bomba ni nini, sasa ILO imeniwezesha

Habari za UN

Play Episode Listen Later Jan 8, 2025 1:40


Nchini Bangladesh, mradi wa kuimarisha stadi na kufungua fursa za kiuchumi, ISEC miongoni mwa wanawake na vijana, umewezesha wasichana kuvunja mwiko na kuingia kwenye tasnia ambazo zimezoeleka kuwa ni za wanaume, mathalani ufundi bomba. Mradi huo unaolenga wanufaika 24,000 wenye umri kati ya miaka 18 na 35 unatekelezwa na shirika la Umoja wa Mataifa la Kazi duniani, ILO kwa kushirikiana na serikali ya Bangladesh.Video ya ILO hapa Cox's Bazaar inamleta kwako mmoja wa wanufaika hao ambaye hata hivyo jina lake halikutajwa, akiwa ameshikilia vifaa vya ufundi bomba anasema, awali sikufahamu kuhusu hii kozi hadi nilipofahamu kupitia Idara ya Maendeleo ya Vijana. Hii ni mara ya kwanza fursa hii imetufikia katika shule ya sekondari ya juu ya Moheshkhali. Tunajifunza stadi badala ya kupoteza muda nyumbani itanisaidia maisha yangu ya baadaye.Nikihitimu masomo naungana na kaka kwenye duka lakeAnakiri kuwa kabla ya kushiriki mafunzo haya hakuwa anafahamu kabisa ufundi bomba ni kitu gani. Lakini sasa amejifunza kuhusu vifaa mbalimbali ikiwemo msumeno wa mabomba, spana na kadhalika.ILOMradi wa kuimarisha stadi na kufungua fursa za kiuchumi, ISEC miongoni mwa wanawake na vijana, umewezesha wasichana Cox's Bazaar nchini Bangladesh.Na ndoto yake ni kwamba nikihitimu masomo nitakwenda kuungana na kaka yangu kwenye duka lake linalounza vifaa vya ujenzi. Nataka niwe mjasiriamali kama yeye, nijitegemee na nisaidie familia yangu. Siku hizi kwenye nyingi zilizoendelea na hata hapa Bangladesh wasichana wanafanya aina zote za kazi.Wanaweza kufanya kazi ngumu kama wanaume, nami nataka kuwa hivyo.Video ya ILO inamalizika mnufaika huyu amekamilisha kufunga bomba na sasa maji yanatoka, na mkufunzi anatumia maji hayo kunawa mikono.Malengo namba 4, 5, na 8 ya SDGs yanatekelezwaMradi huu ulizinduliwa mwezi Septemba mwaka 2023 ukifadhiliwa na…

Habari za UN
Raia wa Mali walioko ughaibuni waonesha mfano bora wa kuwekeza nyumbani

Habari za UN

Play Episode Listen Later Jan 6, 2025 3:32


Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Maendeleo ya Kilimo, IFAD kwa kushirikiana na wadau na kupitia msaada wa Muungano wa Ulaya unasaidia raia wa Mali wanaoishi ughaibuni kuwekeza kwa ufanisi nyumbani Mali.Wamefanya hivyo kwa kuwasaidia kuanzisha Ciwara Capital, kampuni ya uwekezaji inayomilikiwa na raia wa Mali na sasa wanasaidia wakulima wa mpunga nchini Mali kuimarisha na kuongeza uzalishaji wa mpunga, ikiwemo eneo la Mopti ambalo limekuwa likikabiliwa na ukosefu wa usalama na hivyo wakulima kugubikwa na umaskini.Mfumo huu unadhihirisha kuwa badala ya waafrika kutuma dola bilioni 55 kila mwaka nyumbani kusaidia familia, fedha hizo zinaweza kuwekezwa kwenye miradi endelevu. Je ni kwa vipi, Assumpta Massoi anafafanua kwenye makala hii iliyoandaliwa na IFAD.

Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii
Mwaka mpya wa 2025 na matarajio ya ulimwengu kuhusu usalama amani na maendeleo

Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii

Play Episode Listen Later Jan 4, 2025 20:16


Makala hii imeangazia namna ambavyo nchi zetu zilivyoukaribisha mwaka wa 2025 kwa shamrashamra za kila aina huku wakisema kwaheri kwa mwaka 2024 ulioshuhudia michezo mikubwa zaidi ulimwenguni ya Olimpiki, vita ya Ukraine na kule Gaza, usalama mashariki mwa DRC, Sudan pamoja na kurejea madarakani kwa aliyekuwa rais wa Marekani, Donald Trump.

Habari za UN
Papua New Guinea: Tuhuma za uchawi dhidi ya wanawake zapatiwa  ‘muarobaini'

Habari za UN

Play Episode Listen Later Jan 3, 2025 2:08


Kila mwaka, mamia ya wanawake nchini Papua New Guinea, taifa la visiwani katika bahari ya Pasifiki, hushutumiwa kimakosa kuwa ni wachawi. Matokeo yake hukumbwa na ukatili miongoni mwa wanajamii. Hata hivyo Umoja wa Mataifa kupitia shirika lake la Mpango wa Maendeleo duniani, UNDP nchini humo, limechukua hatua.Kiongozi mkubwa wa Kijiji chetu alifariki dunia, na tulipoenda kwenye maziko, ambapo kila mtu alisema sisi ni wachawi na tulikula moyo wake. Ni kauli ya Annabele, jina lake halisi limehifadhiwa kwa ajili ya usalama wake akielezea tuhuma zilizowakabili kwenye jamii yao ya jimbo la Enga nchini Papua New Guinea, hadi kushambuliwa kwa nondo za moto na nyumba zao kuteketezwa kwa moto. Video ya UNDP inamnukuu akisema kuwa walikuwa 9, ambapo wanne walifariki dunia na watano akiwemo Annabele, walinusurika, “kesho yake asubuhi Askofu na wenzake walifika, halikadhalika jeshi na polisi, na ndio walituokoa.” Askofu huyo Justine Soongie Dayosisi ya Wabag jimboni Enga anasema walipowachukua waliambiwa wahakikishe hawarudi kijijini, “sababu kubwa ya mtu kutuhumiwa ni jamii kukosa uelewa kuhusu chanzo cha kifo. Watu wengi hawafahamu kuwa mtu anaweza kufa kutokana na kiharusi. Watu wetu wa Enga watauliza ni nani amesababisha?” Annabelle baada ya kuokolewa alipelekwa hospitali na kupatiwa matibabu ambayo hata hivyo bado ana kovu na maumivu. Kisha walipelekwa nyumba salama zinazoendeshwa na Kanisa Katoliki kwa ufadhili wa UNDP, ambako waliishi kwa miezi takribani mitano wakipatiwa mavazi, malazi na chakula. Askofu Justine Soongie anasema,“baada ya miezi kadhaa hospitalini, tunarudi kwa familia na jamii na kuzungumza nao mara kadhaa. Tunawaelimisha kuwa ni kosa kumtuhumu mtu uchawi, kuna sheria, na hana pahala pengine pa kwenda, hivyo atarudi.” Jamii ilieleweshwa na Annabelle kwenye video anaonekana tayari yuko kijijini na sasa analima shamba na hata anasema hata mazao anayolima akivuna, anapika na wanajamii wanakula pamoja naye. 

Jioni - Voice of America
Serikali ya kenya inasema imepata ufadhili wa shilingi bilioni 12 kutoka Benki ya maendeleo ya Afrika kuwezesha usambazaji wa umeme. - Desemba 24, 2024

Jioni - Voice of America

Play Episode Listen Later Dec 24, 2024 29:59


Matangazo ya saa nzima kuhusu habari za kutwa, ikiwa ni pamoja ripoti kutoka kwa waandishi wetu sehemu mbali mbali duniani na kote Afrika Mashariki na Kati, na vile vile vipindi na makala maalum kuhusu afya, wanawake, jamii na maendeleo.

Habari za UN
Mradi wa kilimo cha umwagiliaji warejesha matumaini kwa wakulima wa Masvingo, Zimbabwe

Habari za UN

Play Episode Listen Later Dec 23, 2024 3:09


Hivi karibuni mkutano wa Umoja wa Mataifa wa kuzuia kuenea kwa jangwa, ulikunja jamvi huko Riyadh, Saudi Arabia ambapo Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Maendeleo ya Kilimo, IFAD ulitumia fursa hiyo kuelezea harakati zake za kusaidia wakulima barani Afrika walioathiriwa vibaya na kuenea kwa jangwa. Miongoni mwa mataifa hayo ni Zimbabwe ambako IFAD imeshaanza kuchukua hatua na kuleta nuru kwa wakulima kama anavyosimulia Assumpta Massoi kwenye makala hii.

Habari za UN
10 DESEMBA 2024

Habari za UN

Play Episode Listen Later Dec 10, 2024 9:58


Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina na tunaelekea nchini Kenya kuangazia moja ya ukiukwaji Mkubwa wa haki za binadamu dhidi ya wanawake, jinamizi la ukeketaji na jitihada zinazochukuliwa na UNFPA na wadau mbalimbali. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na mashinani inayotupeleka nchini Namibia.Baada ya serikali ya Bashar Al-Assad kupinduliwa na kuibuka kwa taarifa za baadhi ya nchi duniani kuanza kusitisha mchakato wa kushughulikia maombi ya Wasyria waliokuwa wameomba hifadhi kuokoa usalama wa maisha yao pindi hali ilipokuwa tete nchini mwao, Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) linaendelea kutoa wito kwa mataifa yote kufungua milango, kuwapa hifadhi na ulinzi raia wa Syria wanaotafuta usalama. UNHCR imeahidi pia mara tu hali ya Syria itakapokuwa wazi zaidi, itatoa mwongozo kuhusu mahitaji ya ulinzi kwa Wasyria walioko hatarini.Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) limekaribisha mchango wa dola za Marekani milioni 22 kutoka shirika la Korea Kusini la Ushirikiano wa Maendeleo ya Kimataifa (KOICA) ili kuimarisha mnepo kwa tabianchi na uhakika wa chakula kwa wakulima wadogo, wafugaji na makundi yaliyoko pembezoni nchini Kenya, Somalia na Sudan Kusini. Vituo vya utabiri wa hali ya hewa vinatabiri hali ya La Niña mashariki mwa Pembe ya Afrika na uwezekano wa kupunguza mvua katika kipindi hikiNa walinda amani wa kikosi cha 11 cha Tanzania -TANZBATT-11 kinachohudumu kwenye ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, DRC, MONUSCO jimboni Kivu Kaskazini wametunukiwa nishani ya umoja wa mataifa ikiwa ni alama ya kufanya kazi  kwa utii,uhodari na uaminifu. Miongoni mwao ni Private Selina Kisemvule.Katika mashinani ikiwa ni siku ya mwisho ya maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia, fursa ni yake Rais Nangolo Mbumba wa Namibia ambaye kupitia ukurasa wa X wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ya Uzazi na Idadi ya Watu, UNFPA anawahimiza wananchi na dunia nzima kwa jumla kusimama kidete ili  kutokomeza unyanyasaji wa kijinsia.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!

Habari za UN
André Bifuko - Najivunia kupatia wengine ujuzi wangu kwa ajili ya amani na maendeleo

Habari za UN

Play Episode Listen Later Dec 6, 2024 1:57


Dunia ikiwa imeadhimisha siku ya kimataifa ya kujitolea kwa ajili ya amani na maendeleo, tunakupeleka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC ambako mmoja wa wafanyakazi wa kujiolea wa Umoja wa Mataifa anaelezea uzoefu wake na ni kwa nini anajivunia kufanya kazi hiyo. Assumpta Massoi na maelezo zaidi.

VOA Express - Voice of America
Vijana wa Afrika mashariki wanaeleza namna wanavyotumia rasilimali ya udongo katika kuleta maendeleo kwa jamii wanazoishi. - Desemba 05, 2024

VOA Express - Voice of America

Play Episode Listen Later Dec 5, 2024 29:59


VOA Express pia inafuatilia kwa karibu sana maswala yanayovuma katika mitandao ya kijamii kama sehemu moja muhimu ya upashanaji habari siku hizi.

Habari za UN
04 DESEMBA 2024

Habari za UN

Play Episode Listen Later Dec 4, 2024 9:58


Hii leo jaridani tunaangazia uzinduzi wa ombi la ufadhili wa mahitaji ya Kibinadamu (GHO), na umuhimu wa lugha mama katika kukuza haki za binadamu. Makala tunasalia hapa makao makuu ya umoja wa mataifa na mashinani tunakupeleka nchini Senegal, kulikoni?Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu (OCHA) ikizindua Ripoti ya Kimataifa ya mahitaji ya Kibinadamu (GHO) kwa mwaka ujao wa 2025 imetangaza ombi la ufadhili kwani takriban watu milioni 305 duniani kote watahitaji msaada wa kibinadamu katika mwaka ujao.Haki si haki iwapo inatolewa kwa lugha ambayo haileweki kwa wahusika, wamejulishwa washiriki wa mkutano wa pili wa wanazuoni unaofanyika hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa New York, Marekani na pia mtandaoni ukimulika Madaraka, Haki na Binadamu: Utawala wa Sheria na mabadiliko Afrika.Makala tunasalia hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa ambapo mkutano wa mwaka 2024 wa Taaluma kuhusu Afrika leo katika leo umeingia siku ya pili hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani. Mkutano huo ulioandaliwa na Ofisi ya mshauri maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu Afrika UNOSAA ni wa siku tatu na umebeba maudhui "Nguvu, Haki, na watu” kwa ajili ya mabadiliko ya Afrika.Na mashinani fursa ni yake Antar sarr, Kijana mkulima wa mbogamboga kutoka Senegal ambaye ni mmoja wa wanufaika wa mradi wa Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Maendeleo ya kilimo, IFAD unaowawezesha vijana nchini humo kwa kilimo na biashara ndogondogo ili kuondokana na fikra za kwenda Ulaya kusaka Maisha bora na ajira, akisema mradi huo imempatia matumaini.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!  

Habari za UN
02 DESEMBA 2024

Habari za UN

Play Episode Listen Later Dec 2, 2024 10:42


Hii leo jaridani tunaangazia mashauriano huko Busan kuhusu matumizi ya plastiki, na ripoti ya UNODC kuhusu UKIMWI na kudhibiti dawa za kulevya katika magereza. Makala inaturejesha Havana Cuba na mashinani inatupeleka nchini Kenya, kulikoni?Vuta nikuvute kwenye mashauriano huko Busan, Korea Kusini kuhusu mkataba wenye nguvu za kisheria dhidi ya uchafuzi utokanao na matumizi ya plastiki na kulinda mazingira ya baharini imefikia ukingoni kwa mkutano kuahirishwa na wawakilishi wa nchi zilizokuwa zinashiriki kuridhia rasimu mpya yenye ibara 32 itakayojadiliwa mwakani.Wakati jana Desemba Mosi Ulimwengu ukiadhimisha Siku ya Kimataifa ya UKIMWI kwa kuhamasisha haki za binadamu ili kufanikisha vita dhidi ya ugonjwa huu hatari, Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya ya Kudhibiti Dawa za Kulevya na Uhalifu (UNODC) inajivunia miaka 25 ya kujiunga na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kukabiliana na UKIMWI (UNAIDS) katika kushughulikia janga la Virusi Vya UKIMWI (VVU) miongoni mwa watu wanaotumia dawa za kulevya na miaka 20 ya kazi ya kupambana na UKIMWI magerezani.Makala leo inamulika jinsi bidhaa za kitamaduni zinavyotumika kukuza na kuendeleza mila na desturi za Kiswahili mkoani Tanga Kaskazini mwa Tanzania. Je ni bidhaa zipi hizo na zinatumika vipi? Tuungane na Flora Nducha aliyeyabaini hayo hivi karibuni alipokuwa Havana Cuba kwenye kongamano la kimataifa la Kiswahili.Na mashinani tunasikiliza manufaa ya ufadhili wa Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Maendeleo ya kilimo, IFAD kwa wakulima kutoka kwake Sharon Kirui kutoka Kaunti ya Nakuru nchini Kenya ambaye ni mnufaika wa vocha za kielektroniki za ununuzi kutoka kwa IFAD na ameweza kupanua biashara yake ya kilimo.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!  

Habari za UN
29 NOVEMBA 2024

Habari za UN

Play Episode Listen Later Nov 29, 2024 9:59


Hii leo jaridani Assumpta Massoi anamulika adha zinazokumba raia kwenye eneo la Palestina linalokaliwa na Israeli; hakari za kukabili UKIMWI Afrika Kusini; IFAD ilivyonusuru vijana na safari za kwenda Ulaya zinazohatarisha maisha yao; Mkimbizi wa ndani Gaza anayezungumzia harakati za kusaka mkate ili kulisha familia yake.Mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa katika ofisi ya eneo la Palestina linalokaliwa na Israeli, Ajith Sungay amesema miezi 13 ya vita imeufanya Ukanda wa Gaza kuwa kama jehanamu, kwani kuna uharibifu usio na kifani, njaa isiyoelezeka magonjwa na kuendelea kwa mashambulizi ya mabomu yanayotawanya raia kila uchao. Flora Nducha na taarifa zaidi.Kuelekea ya Siku ya Kimataifa ya UKIMWI itakayoadhimishwa Jumapili hii, ripoti ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Kukabiliana na UKIMWI (UNAIDS) iliyotolewa juzi Jumatano imeeleza kuwa dunia inaweza kufikia lengo lililokubaliwa la kukomesha UKIMWI kama tishio la afya ya umma ifikapo mwaka 2030 lakini kwa sharti kwamba viongozi ni lazima walinde haki za binadamu za kila mtu anayeishi na Virusi Vya UKIMWI, VVU au aliyeko hatarini kuambukizwa. Anold Kayanda ameangazia mfano mzuri wa Afrika Kusini unaofahamika kama “Takuwani Riime”.Mkala inayokupeleka nchini Senegal kusikia jinsi mradi wa mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Maendeleo ya Kilimo IFAD umewezesha vijana kuondokana na mawazo ya kuweka rehani maisha yao wakisaka maisha bora Ulaya. Mwenyeji wako ni Bosco Cosmas.Mashinani fursa ni yake nampisha Abu Muhammad, mkimbizi wa ndani huko Deir Al Balah, Ukanda wa Gaza akielezea umuhimu wa mgao wa mikate kutoka shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula, WFP, kwa wakimbizi hao wakati huu ambapo vita inaendelea eneo hilo.

Habari za UN
Mradi wa IFAD wasaidia vijana Senegal kusalia nchini mwao, kulikoni?

Habari za UN

Play Episode Listen Later Nov 29, 2024 4:07


Mradi wa uitwao Agri-Jeunes uliozinduliwa na Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Maendeleo ya kilimo, IFAD ili kusaidia raia wa Senegal kuondokana na umaskini, na janga la njaa, umewapatia vijana wa kiume na wa kike matumaini ya kusalia nchini mwao badala ya kuhamia ughaibuni. Mradi huu umewasaidia vijana hao kwa mafunzo ya kilimo, ufugaji kuku, uvuvi na stadi za kuendesha biashara ndogondogo.Katika miezi mitano ya kwanza ya mwaka 2024, makumi ya maelfu ya watu waligeukia wasafirishaji haramu wa binadamu kwa njia ya bahari ya Atlantiki kuelekea visiwa vya Kanari, lakini zaidi ya watu 5000 wamekufa wakijaribu kufika huko. Haya yote yakisababishwa na ukosefu wa ajira na kipato duni. Kupitia video iliyoandaliwa na IFAD, Bosco Cosmas amefuatilia Maisha ya vijana hao, na kutuandalia makala hii

Habari za UN
Namayombo Mgonela: Utamaduni wa Kiswahili umeniinua kiuchumi

Habari za UN

Play Episode Listen Later Nov 26, 2024 6:16


Lengo namba 5 la Maendeleo ya Maendeleo Endelevu, SDGs, ya Umoja wa Mataifa ni usawa wa kijinsia ambao ni pamoja na kuwawezesha wanawake kiuchumi kwa kuwapatia fursa. Akiwa Havana Cuba hivi karibuni kwenye kongamano la kimataifa la Kiswahili Flora Nducha wa Idhaa hii ya Kiswahili, alikutana na kuzungumza na Namayombo Nyanzala Mgonela, mwanamke mjasiriamali kutoka visiwa vilivyoko Karibea St. Kitts na Nevis ambaye anatumia fursa ya utamaduni wake mchanganyiko wa asili ya Visiwa hivyo na wa Kiswahili kujikwamua kiuchumi kupitia ubunifu wa mitindo na shughuli za mama lishe katika jitihada za kutimiza lengo hilo. Kwa kina zaidi tuungane na Flora Nducha. 

Radio Maria Tanzania
Fahamu taaluma ya tafsiri na maendeleo yake duniani.

Radio Maria Tanzania

Play Episode Listen Later Nov 14, 2024 51:55


Karibu uungane nami Martin Joseph katika kipindi cha Elimu Jamii, Mwezeshaji ni Kusanja Emmanuel Kusanja, Msanifu Lugha kutoka Baraza la Kiswahili Tanzania (BAKITA), leo anatufundisha juu ya taaluma ya tafsiri na maendeleo duniani. L'articolo Fahamu taaluma ya tafsiri na maendeleo yake duniani. proviene da Radio Maria.

Radio Maria Tanzania
Watanzani wahimizwa kusherekea miaka 63 ya Uhuru wa Taifa kwa kupanda Mlima Kilimanjaro.

Radio Maria Tanzania

Play Episode Listen Later Nov 13, 2024 49:18


Karibu uungane nami Martin Joseph katika kipindi cha Elimu ya Jamii Wawezeshaji Mapinduzi Boniface Mdesa Mkuu wa Kitengo cha Utalii Hifadhi ya Taifa Kilimanjaro na Daniel Mweta kutoka Kitengo cha Maendeleo na Biashara (TANAPA)  mada ni juu Twenzetu kileleni katika Mlima wa Kilimanjaro . L'articolo Watanzani wahimizwa kusherekea miaka 63 ya Uhuru wa Taifa kwa kupanda Mlima Kilimanjaro. proviene da Radio Maria.

Radio Maria Tanzania
Fahamu kwanini Wanawake Washiriki katika Uongozi.

Radio Maria Tanzania

Play Episode Listen Later Nov 5, 2024 24:33


Ungana nami Agatha Kisimba katika kipindi cha Jinsia na Maendeleo, Kutoka Studio za Radio Maria Tanzania ambapo leo nipo  na Wadau  wa Masuala ya Kijinsia Bi. Tabu Ally, Bi.Anna Sangai na Bwana Deogratius Temba mchambuzi, mwezeshaji na mtafiti wa masuala ya Kijinsia akielezea Ukweli kuhusu Wanawake na Uongozi. L'articolo Fahamu kwanini Wanawake Washiriki katika Uongozi. proviene da Radio Maria.

Habari za UN
Mwelekeo ni kutengeneza kaukau za ndizi zenye ladha ya kitunguu na nazi

Habari za UN

Play Episode Listen Later Oct 30, 2024 3:37


Uwekezaji rahisi kabisa kwa familia ya Didiki huko nchini India umekuwa na manufaa kwa kaya zaidi ya 20. Zao la ndizi ambalo awali hawakuweza kuongeza thamani ipasavyo lilikuwa na manufaa kidogo kiuchumi. Somo la biashara likamfungua fikra Didiki hadi kupata msaada kutoka Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Maendeleo ya kilimo IFAD kwa ushirikiano na serikali ya India. Msaada umepanua biashara, vijana wamepata ajira, familia zimeongeza kipato na sasa mpango ni kufikia kaya zaidi ya 60,000. Ni kwa vipi? Ungan ana Assumpta Massoi kwenye makala hii.

Habari za UN
Maadhimisho ya kimataifa ya siku ya chakula duniani yaangazia haki ya chakula salama chenye lishe na cha bei nafuu

Habari za UN

Play Episode Listen Later Oct 16, 2024 1:47


Washiriki wa Sherehe za kimataifa za mwaka huu wa 2024 za kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Chakula zilizofanyika leo katika makao makuu ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo (FAO) jijini Roma Italia wamesisitiza haja ya upatikanaji wa vyakula mbalimbali vya kutosha, vyenye lishe, bei nafuu na salama.Ni maadhimisho ambayo yamewaleta wadau wa kilimo na chakula kutoka kote duniani lakini  yanakuja huku kukiwa na mvutano na mizozo ya kimataifa na majanga ya tabianchi ambayo ni miongoni mwa mambo yanayochangia changamoto ya mamia ya mamilioni ya watu duniani kote kukabiliwa na njaa na mabilioni ya watu kushindwa kumudu chakula bora, FAO inaeleza katika taarifa iliyochapishwa katika ukurasa wake wa wavuti.Katika hotuba yake ya ufunguzi Mkurugenzi Mkuu wa FAO, QU Dongyu, amesema mifumo ya kilimo cha chakula inabidi "kusaidia wakulima wadogo, wakulima wa ngazi ya familia na wafanyabiashara wadogo katika mnyororo wa thamani ambao katika nchi nyingi ni wa msingi katika kufanya vyakula vyenye lishe, vya aina mbalimbali vipatikane kwa wote, na kuhifadhi tamaduni za jadi za chakula.” Ujumbe huo wa mkuu wa FAO unafanana na ujumbe wa Papa Francis ambaye amesisitiza wafanya uamuzi wa kisiasa na kiuchumi katika ngazi ya kimataifa lazima wasikilize matakwa ya wale walio chini kabisa katika mnyororo wa chakula.Kwa upande wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres kupitia video amesema, "kuna kitu hakiko sawa katika ulimwengu ambao njaa na utapiamlo ni ukweli wa maisha kwa mabilioni ya watoto, wanawake na wanaume." Akasema ulimwengu usio na njaa unawezekana, lakini "mifumo ya chakula inahitaji mabadiliko makubwa," ili kuwa na ufanisi zaidi, ujumuishi, mnepo na endelevu.Gérardine Mukeshimana, Makamu wa Rais wa Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo (IFAD) ametoa wito wa "uwekezaji wa haraka, wa pamoja na thabiti kwa wakulima maskini wa vijijini kutambua kwa ngazi ya chini kabisa haki yao ya msingi ya chakula chenye lishe." Akabainisha kuwa wakulima wadogo wanazalisha karibu nusu ya chakula cha dunia, ingawa pia wanakabiliwa na njaa na umaskini.Mfalme Letsie III wa Lesotho, ambaye ni Balozi Mwema Maalum wa FAO katika upande wa lishe anaeleza anavyoiunga mkono FAO kwa “kujaribu kuwa mtetezi mwaminifu na mwenye kujitolea katika masuala ya lishe, katika masuala ya uhakika wa chakula.” Anasema, “na mara kwa mara, mimi hutembelea sehemu nyingine za bara la Afrika nikivaa kofia yangu ya FAO, hasa kuhimiza serikali na viongozi kama bara kuwekeza zaidi katika masuala ya lishe na masuala ya uhakika wa chakula.”. 

Habari za UN
UNESCO: Tunapaswa kuthamini sauti za walimu kote duniani

Habari za UN

Play Episode Listen Later Oct 4, 2024 2:58


Washiriki wa hafla ya kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Walimu ililofanyika leo Oktoba 4 katika makao makuu ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) jijini Paris, Ufaransa  wamesisitiza wito wa kuthamini mawazo ya walimu katika kuboresha elimu ya ulimwengu. Kama tunavyofahamu, siku yenyewe ya Kimataifa ya Walimu ni kesho Oktoba 5 kama ilivyo ada ya kila mwaka lakini katika makao makuu ya UNESCO hapa Paris Ufaransa, maadhimisho yamefanyika leo kuelekea mkesha wa siku hii muhimu kwa elimu ya ulimwengu.Miongoni mwa waliozungumza ni Mkurugenzi Msaidizi Mkuu wa Elimu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Bi Stefania Giannini, ambaye ameitumia nafasi hii kusisitiza kauli mbiu ya mwaka huu ambayo ni 'Kutambua sauti za walimu.'Anasema, “walimu ni uti wa mgongo wa mifumo ya elimu na mawakala wakuu wa mabadiliko ya kubuni sera za elimu na kufanikisha SDGs. Tunapaswa kuthamini sauti za walimu; hili ndilo lengo kuu la Siku ya Kimataifa ya Walimu mwaka huu.”Kulingana na takwimu zilizotolewa na UNESCO, dunia inahitaji walimu wa ziada milioni 44 ili kufikia elimu ya msingi na sekondari kwa wote ifikapo mwaka 2030. Ingawa mahitaji ya walimu ni makubwa zaidi katika baadhi ya maeneo, uhaba wa walimu ni wa kimataifa.Walimu wanajiondoa kwenye taaluma hii kwa kiwango mara mbili zaidi ya miaka mitano iliyopita, hasa katika elimu ya sekondari. Hii inatokana na hali zao za kazi, zikiwemo mishahara midogo, mzigo mkubwa wa kazi, na ukosefu wa ushiriki katika maamuzi yanayohusu elimu. Akiiangizia changamoto hii, Mkurugenzi wa Kimataifa wa Elimu na Maendeleo ya Vijana katika Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) Bi. Pia Britto, aliyejiunga katika hafla ya leo kwa njia ya video akiwa Pakistani amesema,"Leo nilikuwa na fursa nzuri ya kuzungumza na walimu wengi, ikiwa ni pamoja na mwalimu Tahseen Bashir hapa Islamabad, ambaye amenieleza baadhi ya changamoto wanazokabiliana nazo ikiwa ni pamoja na kufundisha madarasa mengi, uhaba wa vifaa vya kujifunzia, na changamoto za kutoweza kufundisha namna wanavyodhamiria. Lakini pia amenieleza jinsi alivyofurahi kuona wanafunzi wake wakifaulu. Wakati sauti ya mwalimu inaposikilizwa na wakati sauti za walimu zinapopewa kipaumbele, wanajiona kama wadau katika kuboresha elimu kwa wakati wote, na hatua hizo zinahitajika ili kuleta mabadiliko chanya hasa katika hali ngumu zaidi."Siku hii ya kimataifa ya walimu ni mahususi kwa ajili ya kutambua na kusherehekea mchango muhimu wa walimu ulimwenguni kote katika kutoa elimu bora na kujenga mustakabali wa jamii. Pia, ni fursa ya kuangazia changamoto wanazokabiliana nazo walimu.Kutoka hapa Paris Ufaransa, mimi ni Cecily Kariuki..

Habari za UN
UNMISS: Wananchi wa kaunti ya Nasir watakiwa kuepuka mapigano ili wapelekewe maendeleo

Habari za UN

Play Episode Listen Later Sep 9, 2024 1:56


Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Sudan Kusini (UNMISS) umewaeleza wananchi wa Kaunti ya Nasir au Keich Kon iliyoko jimboni Upper Nile nchini Sudan Kusini kuwa ili waweze kurejeshewa huduma za misaada ya kibinadamu ni vyema wakafikia makubaliano ya kusitisha mapigano. UNMISS pamoja na wadau wengine wa misaada ya kibinadamu walifikia uamuzi wa kusitisha huduma zao katika kaunti ya Nasir kutokana nae eneo hilo kutofikika na pia ukosefu wa usalama uliosababishwa na mapigano ya mara kwa mara baina ya wanajamii wa kuanti hiyo, na pia mapigano na kaunti za jirani.Hata hivyo mwanzoni mwa mwezi huu wa Septemba kilifanyika kikao kilichowaleta pamoja wadau na wananchi baada ya kupatikana uongozi mpya wa kaunti hiyo ambapo katika kikao hicho, wadau wa misaada ya kibinadamu ikiwemo Umoja wa Mataifa waliombwa kurejesha operesheni zao hususan UNMISS, Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula duniani (WFP) na wadau wa Sekta ya afya.Paul Ebikwo ni afisa wa masuala ya kiraia wa UNMISS na akawaeleza anaelewa wasiwasi wao.“Wasiwasi wenu ni wa halali, ni wa kweli, tunaelewa. Lakini mkiongeza mizozo ndani yake, mnafanya mambo kuwa mabaya zaidi, kwa hivyo hebu tufanye maamuzi ya kuachana, na kuweka kando migogoro na sote tufikirie jinsi ya kutatua maswala haya.”Bwana Ebikwo aliongeza kuwa suluhu zote za kuzuia ghasia lazima ziongozwe na wanajamii wenyewe huku akitoa wito kwa makundi ya vijana wanaotumia silaha kujiepusha na mapigano na kutafuta amani.Majadiliano yalihitimishwa kwa wote kukubaliana kuwa na dhamira ya pamoja ya kutafuta njia za kuleta jamii hususani vijana pamoja kwa ajili ya upatanisho na ujenzi wa amani ili kusaidia kurejesha utulivu na kuwezesha jamii katika kaunti ya Nasir kupata ahueni na maendeleo baada ya kuteseka kwa muda mrefu.

sudan hata wfp umoja sekta lakini mataifa maendeleo unmiss shirika ujumbe kaunti wananchi septemba sudan kusini
Habari za UN
Kemia na ujasiriamali vinavyoambatana katika Chuo Kikuu cha Kenyatta

Habari za UN

Play Episode Listen Later Sep 4, 2024 4:39


Je umeshawahi kujiuliza ni kwa vipi wataalamu wa kemia wanahusiana na ujasiriamali? Kama ndivyo, basi vivyo hivyo kwa Assumpta Massoi akiwa Manama, nchini Bahrain akishiriki Jukwaa la Nne la Uwekezaji kwa Wajasiriamali, WEIF2024 lililoandaliwa na shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Viwanda, UNIDO, Ofisi ya Uendelezaji wa Biashara, ITPO nchini humo, alikutana na Profesa Ruth Wanjau, Mtafiti na Mshauri wa Masuala ya STEM yaani Sayansi, Teknolojia, Uhandisi na Hisabati katika Chuo Kikuu cha Kenyatta nchini Kenya. Alimuuliza maswali kadhaa ikiwemo ushiriki wake kwenye jukwaa hilo na nini anafanya kusongesha ujasiriamali.

Habari za UN
JIFUNZE KISWAHILI: TAFSIRI YA NENO LINK

Habari za UN

Play Episode Listen Later Aug 30, 2024 0:58


Maendeleo ya teknolojia hasa kwenye mitandao ya kijamii yamesababisha kushamiri kwa matumizi ya neno la kiingereza link. Baadhi  ya watu wanalitohoa lakini Idhaa ya  Umoja wa Mataifa imemuuliza Mhadhiri Mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa Tanzania, BAKITA ni nini tafsiri sahihi ya neno link kwa lugha ya kiswahili.

Jioni - Voice of America
Kenya yapokea zaidi ya shilingi bilioni 27 kutoka EU, na Benki ya maendeleo ya Ufaransa kwa ajili ya usambazaji wa umeme vijijini. - Mei 28, 2024

Jioni - Voice of America

Play Episode Listen Later May 28, 2024 29:59


Matangazo ya saa nzima kuhusu habari za kutwa, ikiwa ni pamoja ripoti kutoka kwa waandishi wetu sehemu mbali mbali duniani na kote Afrika Mashariki na Kati, na vile vile vipindi na makala maalum kuhusu afya, wanawake, jamii na maendeleo.