Podcasts about mwenyezi

  • 6PODCASTS
  • 14EPISODES
  • 40mAVG DURATION
  • ?INFREQUENT EPISODES
  • Feb 12, 2024LATEST

POPULARITY

20172018201920202021202220232024


Best podcasts about mwenyezi

Latest podcast episodes about mwenyezi

Radio Maria Tanzania
Kwanini Adam na Eva hawakumuomba Mwenyezi Mungu msamaha walipokosea?

Radio Maria Tanzania

Play Episode Listen Later Feb 12, 2024 21:44


Karibu katika kipindi cha Maswali yahusuyo Imani Leo tupo naye  Frateri Daud Fungameza, kutoka Seminari kuu ya Mtakatifu Augustino Peramihio, Jimbo kuu la Songea  swali la msikilizaji linalojibiwa linasema Kwanini Adam na Eva walipomkosea  na kumtii Mwenyezi Mungu kwanini hawakumuomba msamaha au yalikuwa makusudi ya Mungu iliandiko lake litimie? L'articolo Kwanini Adam na Eva hawakumuomba Mwenyezi Mungu msamaha walipokosea? proviene da Radio Maria.

Radio Maria Tanzania
Wafahamu watu gani wanapaswa kupata Baraka za Mwenyezi Mungu?

Radio Maria Tanzania

Play Episode Listen Later Jul 12, 2023 21:12


Ungana na Brigitha Msasalaga katika Kipindi cha Maswali ya Imani, na swali linalojibiwa linahoji  juu ya mtu asiyebatizwa na anashiriki shughuli zote za kikanisa  anapata baraka za Mwenyezi Mungu,  Mwezeshaji Frateri Franco Abel Ubanga,  kutoka Parokia ya Mtakatifu Boniface Shahidi  Madibila- Jimbo  Katoliki la Iringa.

baraka gani mungu watu kipindi ungana maswali mwenyezi
Salama Na
SE7EP36 - SALAMA NA ALLY BEE | KULE NI KULE…

Salama Na

Play Episode Listen Later Feb 16, 2023 64:32


Kwenye jiji la ‘Maraha' hapa nyumbani kwetu Tanzania ambayo kwa miaka ya hivi karibuni sehemu za starehe zimekua tele na kila mmoja ana uwezo wa kula bata zake vizuri tu kulingana na urefu wa mfuko wake basi hakuna ambaye HAJUI jina la DJ huyu mahiri ambaye kwa ubunifu wake ameweza sana kubadilisha kabisa jinsi ambavyo wenzake walomtangulia walikua wanafanya. Yaani Ally alikichukua kitabu cha jinsi ya kutoa burudani kama DJ na kukichanachana na kisha akaanza kuandika cha kwake, ambacho mpaka tunaenda mtamboni kiiila msomaji wake anapeeenda ambayo yameandikwa na ambayo anaendelea kuyaandika. Wakati msimu huu unaanza Ally Bee hakua moja ya majina ambayo yalikua yameandikwa kama mmoja ya watu ambao tungependa kujua story ya maisha yake, kutaka kujua nini kinampa hamasa ya kufanya ambacho anafanya na pengine mambo mengine tele ambayo atakua na uhuru wa ku share na sisi. Ila kuna siku nilikua nyumbani na Rafiki yangu ambaye pia ni mdogo wangu Ndugu Sadam Almando Sanare ambaye nilikua namuuliza maswali kuhusu Dj mwengine kabisa huku nikilalamika kuhusu huyo mtu kwamba pengine kuna jambo haliko sawa kuhusu simulizi zake za baadhi ya mambo maana amekua kama anaongelea sana skuizi, then yeye akaniambia kuhusu Ally Bee (binafsi hupenda kumuita Ally Bee kwasababu wote tunamjua nyuki, na ukali wake lakini asali yake sote ndo kama hivyo, hopefully it will make sense kwake someday

Salama Na
SE7EP24 - SALAMA NA DORIS MOLLEL | HALF WOMAN, HALF AMAZING

Salama Na

Play Episode Listen Later Nov 24, 2022 75:48


Doris Mollel kwa kuanzia tu tuanze na jina lake, ni zuri lenye kukumbukwa ki rahisi, yeye mwenyewe pia ni mrembo na mkarimu, sana. Roho yake ni kama rangi yake, nyeupe na kwa bahati Mimi namfahamu yeye kiasi kwa kupitia rafiki zangu ambao yeye anafanya nao kazi na pia ana mahusiano nao mazuri, sana. Pia namfahamu mume wake ambaye tukianza shindano la kumtafuta nani mkarimu kati yao tunaweza kukamaliza kwa suluhu. Huwa naamini Mwenyezi aliwakutanisha ili kwa pamoja waweze kufanya makubwa kwaajili yao na familia zao na jamii ambayo imewanzunguka ambayo kwa kiasi kikubwa ina uhitaji wa yale ambayo wao wameyaona wanaweza kufanya jambo ili yawe mepesi. Sasa tuanze kwa vipi Doris amekua akifanya ambayo anayafanya sasa ambayo baada ya kufanya kipindi hiki mengi ambayo aliyaongelea kama ya Serikali ya Uganda kumpa tuzo na kumkaribisha nchini mwao ili aweze kushirikiana nao bega kwa bega kwenye suala zima la kuwaokoa watoto wanaozaliwa kabla ya wakati yaani ‘NJITI' na hivi karibuni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia S. Hassan kutoa MILIONI 70 kwaajili ya kuchangia mfuko wake wa Doris Mollel Foundation. Yeye alikua anataka tu kufanya kitu kwaajili ya kuisadia jamii yake, ananiambia wakati analizungumzia hilo huku akitafuta jambo la kufanya ndipo Mama yake alipomfugua macho kwa kumuambia masuala ya watoto njiti, taa iliwaka sasa baada ya Mama yake kumkumbusha kwamba hata yeye alizaliwa kabla ya wakati. Alipoambiwa hivyo hakukua na kurudi nyuma tena baada ya hapo. Ananisimulia vikwazo ambayo aliwahi kupata mwanzo kuanzia nyumbani mpaka kwenye kutafuta hizo pesa ambazo zinasaidia mpaka leo hii, Doris ananihadithia jinsi ambavyo alipata bahati ya kuwa na watu ambao wamemsapoti na wanamsapoti mpaka leo kuanzia nyumbani kwa mume wake. Mtu ambae ndoa yao ilikua changa kuanza kuwa na vikao na watu mbali mbali mpaka usiku wa manane inamtaka mtu muelewa sana kuweza kuamini na kuyaacha mambo yaende. Mumewe alikua huyo mtu. Kwa ambao walimpigia simu mara ya kwanza baada ya kuona anchojaribu kufanya, watu kama Asas wa kule Iringa na wengine ambao wamekua wakijitokeza siku baada ya siku. Anakumbuka na anajua kwamba kutokata tamaa kwasababu ya changamoto kadhaa ndo ambapo kunamfanya awe ni mmoja ya watu wanao heshimika zaidi kwa mchango wake kwenye jamii yetu. Binafsi naamini huu ni mwanzo tu wa mazuri mengi ambayo binti huyu halisi wa ki Tanzania anajaribu kufanya. Sekta ya kulea watoto ambao wamezaliwa kabla ya wakati inahitaji hela nyingi na kwasababu ambazo Mimi na wewe hatuzijui kumekua na vifaa VICHACHE sana vya kuwahifadhi watoto hao mara tu wanapo zaliwa. Doris na Foundation yake amekua akipigana vita hiyo kuhakikisha vifaa vinapatikana sio mjini tu, hata mikoani ili kuokoa maisha ya watoto hawa ambao wengine huishia kwenye debe la taka kwasababu tu walizaliwa kabla ya wakati wao. Yangu matumaini utamuelewa na utapata nafasi ya kumfuatilia na kama utakua na lolote ambalo unaweza kuchangia basi yuko kwenye mitandao ya kijamii maana siku hizi kumpata mtu na kujua ambacho anakifanya imekua rahisi kupitia mitandao hiyo. Mimi najivunia sana yeye na yangu matumaini atafanikiwa sana kwenye sekta hii kama nasi tutaweza kumsaidia pale panapowezekana. Tunahitaji kina Doris tele kwenye jamii yetu maana vya kusaidia viko vingi. Yangu matumaini episode hii itasaidia kukufungua macho kwenye mengi ambayo jamii yetu ina uhitaji. Love, Salama. --- Support this podcast: https://anchor.fm/yahstonetown/support

Salama Na
SE7EP12- #SalamaNaDrTulia| BULYAGA 1976

Salama Na

Play Episode Listen Later Sep 1, 2022 51:16


Tulia Ackson ni jina kubwa kati ya majina makubwa kwenye Serikali ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania na kwa sisi kuweza kulipata jina kubwa na kukubali kuja kuketi kwenye kiti chetu chakavu ilikua ni BARAKA sana. Ila ukiachana na kwamba ni jina kubwa ila yeye ni binadamu, tena wa kawaida tu. Ni Mama, ni mke, ni Dada, ni Binti kwa Mama yake na ni Mbunge kwa wana Mbeya mjini lakini pia ni Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Wadhifa ambao baada ya uchaguzi wa 2020 alirudi bungeni kama Naibu Spika ila baada ya aliyekua Spika kujiuzulu Dr Tulia aliona fursa ya yeye kuvaa viatu hivyo na wabunge nao walimpa kura zao zote za kuridhia Mwana Dada huyu AWAONGOZE. Baada ya uchaguzi wa 2020 na yeye alirudi bungeni kama MBUNGE kamili, si tunakumbuka baada ya 2015 alienda bungeni kama Mbunge wa kuteuliwa ila mwaka 2020 aliamua kwenda kugombea jimbo la Mbeya mjini ambako Gwiji wa Bongo Flava Kaka yangu Joseph Mbilinyi aka Sugu alikua ndo Mbunge wake? Sugu alikaa kule kwa miaka 10 ilikua ni moja ya ngome za wapinzani ambazo walikua wanajivunia nazo, kwa Dr Tulia kuamua kwenda kugombea pale iliwafanya watu wengi watake kufuatilia mchuano huo mkali ambao mwisho wa siku Dr Tulia aliibuka kidedea. Na haya yalikua ni moja ya maswali ambayo nilikua na hamu ya kumuuliza na kwa urefu alinijibu tu vizuri sana. Sasa nchi yetu inaongozwa na Rais mwanamke kwa mara ya KWANZA toka tulipopata uhuru wetu mwaka 1961, na hii haikuja kwa kupangwa ila baada ya kutokea ambalo Mwenyezi alikua ameliandika, na hata hili la kuwa na Spika Mwanamke (ingawa huko nyuma Mama Anne Makinda alishawahi kuwa) nalo halikua limepangwa maana Spika tayari tulikua naye baada ya Uchaguzi wa 2020. So suala la kuwa na Rais mwanamke na Spika mwanamke bila ya shaka linalipa Taifa letu utofauti na HESHIMA flani hivi ambao mataifa mengi yanavutiwa nayo. So kwake yeye nini hasa kimebadilika? Yaani kutoka kuwa Naibu mpaka sasa Spika? Ilikua easy kwake kuichukua nafasi hiyo baada ya kuwepo na nafasi hiyo? Alifikiria mara mbili? Kwa maongezi yetu haya pia nimegundua Dr Tulia alikua hapendi kabisa siasa, yeye aliyapenda zaidi maisha yake ya kuwa Lecturer pale Chuo Kikuu, alipenda zaidi kuandika na kusoma na kujifunza. Alikua akiwaona wana Siasa kama watu flani ambao pengine wanajiona tofauti na watu wengine, pengine wanajiona wa MUHIMU sana. Je na yeye sasa? Akiwa nao kule bungeni wanaishi vipi? Sasa pia kama Kiongozi wa mhimili huo wa NCHI nini zaidi kimebadilika? Nini zaidi kigumu? Maongezi yetu yalianzia nyuma kiasi na mbele pia yakafika, pia humu tumeongelea Tulia Trust na vitu ambavyo inafanya ili kuwafikia wale ambao wana uhitaji. Na sasa amekua naye MWANASIASA, nini kimebadilika? Msemo wa Siasa ni mchezo mchafu, kwake yeye una maana gani? Yangu matumaini uta enjoy na kujifunza jambo kutoka kwa Kiongozi huyu ambaye pia ni Dada yetu. Love, Salama. --- Support this podcast: https://anchor.fm/yahstonetown/support

Radio Maria Tanzania
Je! Mwenyezi Mungu Ana Nafasi Gani Katika Biashara Yako?

Radio Maria Tanzania

Play Episode Listen Later Jun 30, 2022 53:43


Na Padre Richard Matanda Tesha wa Jimbo Katoliki la Moshi.

Habari za UN
Ni lazima wanawake tujiamini – Fundi viatu Jovia Kyomuhendo

Habari za UN

Play Episode Listen Later Dec 7, 2021 3:41


Ubunifu ni moja ya mambo yanayotazamwa kuwa na mchango mkubwa katika kufanikisha Malengo ya Maendeleo Endelevu, SDGs. Nchini Uganda, msichana Jovia Kyomuhendo amepata sifa kwa kuwa kijana mbunifu ambaye amefikia hatua ya kujiajiri kwa kuanzisha kiwanda kidogo cha kushona na pia kutengeneza viatu. Safari yake imekuwaje hadi kufikia kutunukiwa tuzo na Muungano wa Viwanda Vidovidogo nchini Uganda USSIA? Tupate taarifa zaidi kutoka kwa mwandishi wetu wa Uganda, John Kibego. Jovia Kyomuhendo akieleza hisia zake baada kushinda tuzo ya kijana mbunifu mwaka jana anasema, “Eee! Mungu wangu, sikuamini kwamba ndio mimi aliyetuzwa kwa sababu tulikuwa na ushindani mkali uliohusisha wavulana na wasichana ambapo kila mmoja alikuwa anafahamu anachofanya.” Tuzo hiyo iliadaliwa kijiimarisha katika utengenezaji wa vyatu ambapo kwa sasa anajiajiri mjini Kinubi, "lakini kwa nguvu za Mwenyezi mungu, nifanikiwa  kuwa wa pili. Nadhani hii ni kwa sababu nilikuwa najiamini sana kuhusu kile ninacchofanya. Na pia ninachofanya kinachangia kwneye uhifadhi wa mazingira kwani natumia magurudumu kutengeneza viatu hivyo na kuyaondoa katika mazingira.” Wengi hushangaa wanapoona mwanamke akijishughulisha na utengenezaji wa viatu, “kila mtu huwa anasema ‘Eee” hiyo kazi ni ya wanaume lakini motisha ulionayo ndio inakusaidia kuchapa kazi. Je, unapenda kazi hiyo? Ikiwa unaipenda bila shaka unaweza kuifanya.” Mazingira ya nyumbani hayakumruhusu Kyomuhendo kuendelea na elimu hadi elimu ya sekondari ya juu na vyuo. Lakini je, anajuta? “sijuti hata kidogo kwa sababu nimefanikiwa. Unakuta kwamba wengi wa walioendelea hadi kwneye vyuo vikuu hawana kazi lakini kwangu ninachapa kazi. Hata wakati wa COVID-19 nilikuwa nikifanya kazi kwani watu walikuwa wakitembea wakitumia viatu nikitengeneza na kuwashonea viatu vipya.” Ujuzi huu umekuwa nuru kwa Kyomuhendo, kijamii na kiuchumi, “nimepata marafiki wengi sana na mawasiliano muhimu sana  duniani. Mfano ni USSIA ambao kupitia kwao nimepata tuzo. Tuzo ya kijana mbunifu” Kwa upande wa kipato, “kiuchumi ninasema kwamba ninajitegemea. Sitegemei yeyote kwa sababu unakuta kwamba wasichana wengi hupenda kutegemea wengine kuwapatia mahitaji wakati wote, wakisema sisi wanawake ni wa kupewa na anakaa nyumbani lakini mimi ninajitegemea” Kyomuhendo anaelezea kwa nini anapenda kazi yake hii, “kwa sababu nina soko kubwa sana kiasi kwamba kila mtu huvaa viatu. Wanawake, watoto wadogo, vijana na wazee hata babu yangu anavaa viatu. Inamaanisha hili ni soko kubwa sana lilopo” Kwa mantiki hiyo, anatoa mawaidha kw awanawake, “ni kwamba sisi wanawake, ni lazima tujiamini. Kuwa mwanamke haimanishi kwamba hauwezi kufanya lolote. Usikubali kupuuzwa kwa sababu unaona sasa hivi mimi aliye mkode namna hivi ndio anayetengeneza viatu hivi” Katika panda shuka ya maisha, Kyomuhendo amewahi kuwa mwalimu katika shule ya msingi na kuanza kuusomea ili awe mtaalamu lakini, aliaacha kwani alipata pesa za kununua machine alizokuwa anaihitaji ili ajiajiri katika utengenezaji wa viatu.

Ni Salama
Kumwamini Mungu kwa kumfuata Yesu Kristo (Sehemu ya Kwanza)

Ni Salama

Play Episode Listen Later Jul 19, 2019 10:05


KUMWAMINI MUNGU KWA KUMFUATA/KUPITIA KWA YESU KRISTO. Hapa nilitaka uone katika ule mji Yesu alimpata mtu mmoja tu kwa lugha ya sasa tungesema “kwenye safari ya Yesu kuingia gharama ya kuvuka na boti kwenda kule na kufanya huduma alimpata mtu mmoja tu kwenye ule mji, na tofauti yao ilikuwa kwenye akili. Ingawa kwenye lile eneo wengine hawakuwa vichaa, haina maana kwamba akili zao zilikuwa huru hazijashikwa. Huyu Mgerasi kichaa alipofunguliwa alikuwa huru na ikawa rahisi sana kwa yeye kumfuata na kumhubiri Yesu, wenzake wote walimwambia Yesu aondoke kwao, lakini huyo aliyeponywa bado alikuwa ana ujasiri wa kurudi na kumhubiria huyo huyo Yesu waliyemfukuza. Ukisoma Mwanzo 2:7 “BWANA Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi, akampulizia puani pumzi ya uhai; mtu akawa nafsi hai.” Ayubu 32:8 “Lakini imo roho ndani ya mwanadamu, Na pumzi za Mwenyezi huwapa akili.” Kwa hiyo akili iko ndani ya nafsi na ubongo uko ndani ya mwili. Kama katika uumbaji wa mtu, Mungu alitanguliza roho halafu akaleta mwili ndipo akaleta nafsi, kazi mojawapo ya nafsi ni kuwa kiungo, si tu cha mawasiliano kati ya roho na mwili. Lakini ukitaka kufikia roho kirahisi unapita kwenye nafsi, na ukitaka kufikia mwili kirahisi unapitia kwenye nafsi. Roho na mwili lugha zao hazielewani (roho inaenda kwa imani, mwili unaenda kwa milango ya fahamu (kuona, kugusa, kunusa, kuhisi kwa ngozi). Kwa hiyo nafsi imekaa hapo katikati, na akili imekaa hapo katikati. Biblia inajitafsiri yenyewe, ukikuta mstari huu huuelewi, unakuta mahali pengine neno hilo limefafanuliwa.

Ni Salama
Nafsi na mwili viliumbwa vimilikiwe na roho

Ni Salama

Play Episode Listen Later Jul 7, 2019 9:59


NAFSI NA MWILI VILIUMBWA VIMILIKIWE NA ROHO Zaburi 63:1 “Ee MUNGU, Mungu wangu, nitakutafuta mapema, Nafsi yangu inakuonea kiu, Mwili wangu wakuonea shauku, Katika nchi kame na uchovu, isiyo na maji.” Mwandishi anamwambia Mungu, “Mungu wangu nitakutafuta mapema”, anaposema nitakutafuta ni roho ya Daudi inamweleza Mungu ya kwamba nitakutafuta mapema. Roho hiyo hiyo inasema kwa niaba ya nafsi, inasema nafsi yangu inakuonea kiu, lakini pia inasema kwa niaba ya mwili inasema mwili wangu wakuonea shauku. Nilitaka uone ya kwamba hauwezi kusema nafsi yangu kama haijapangiwa imilikiwe na roho na hauwezi kusema mwili wangu kama roho haikupangiwa kumiliki mwili. Ni dhambi iliyokuja na kukorofisha utaratibu wa uumbaji na mwili ukaonekana kama ndio unao tawala kila kitu, lakini Mungu aliweka kwa makusudi kabisa kwamba roho ya mtu ndiyo imiliki nafsi na mwili. AKILI IMO NDANI YA NAFSI Ayubu 32:8 “Lakini imo roho ndani ya mwanadamu, Na pumzi za Mwenyezi huwapa akili.” Unganisha na kile kitabu cha Mwanzo ili uelewe vizuri zaidi: Mwanzo 2:7 “Bwana Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi, akampulizia puani pumzi ya uhai; mtu akawa nafsi hai.” Kwa hiyo kama pumzi iliachilia nafsi ndani ya mtu na pumzi iliachilia akili ndani ya mtu kwa hiyo akili imo ndani ya nafsi. Akili tumeipata kwa msaada wa pumzi ya Mungu na nafsi tumeipata kwa msaada wa pumzi ya Mungu. Wakati nafsi inaingizwa ndani yetu na akili ziliingizwa, na ndiyo maana kama unayo nafsi lazima na akili unazo, hakuna mtu ambaye ameumbwa bila akili, ile kwamba huzitumii haina maana kwamba huna. AKILI SIO UBONGO, LAKINI MUNGU ALIVIUMBA VIFANYE KAZI KWA KUSHIRIKIANA Biblia ya Kiswahili inafundisha vizuri zaidi juu ya akili kuliko Biblia ya Kiingereza. Ukisoma Biblia ya Kiingereza unahitaji kuwa mwangalifu sana kutafuta neno akili kwa sababu limeandikwa kwa tafsiri tofauti tofauti kutegemeana na waliokuwa wakitafsiri na inategemea pia picha nzima ya habari inayozungumzwa. Kwa sababu ubongo kwenye Kiingereza wanasema ni Brain lakini wengine wanasema ni Brains wengine wanasema ni intelligence na wengine wanasema ni mind lakini kwenye Biblia ya Kiswahili wamenyooka na kupata neno nzuri kabisa ambalo ni akili. Ubongo upo kwenye mwili na akili ipo kwenye nafsi. Na ndiyo maana hata ukienda hospitali wataalam watakuambia ubongo ulipo lakini watapata shida sana kukueleza akili zilipo. Mungu aliumba akili na ubongo vifanye kazi pamoja lakini akili imo ndani ya nafsi na ubongo umo ndani ya mwili. Kazi ya ubongo ni kupokea elimu na kazi ya akili ni kuchukua elimu na kuibadilisha kuwa maarifa Ubongo haubadilishagi elimu kuwa maarifa. Na ndiyo maana ukishikwa akili zako hata kama una akili kiasi gani ubongo unaweza kukusaidia ukafaulu darasani lakini huwezi kufaulu kwenye maisha. Kwa sababu maisha hayafaulishwi na ubongo wako bali ufaulishwa na akili yako na nafsi yako. Biblia inasema watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa na sio kwa kukosa ubongo. Na ndiyo maana mtu anaweza kuwa na shahada kadhaa lakini maisha hana. Ile tu kwamba mtu amesoma haina maana kisomo kinampa maisha. Kisomo kinaweza kikakupa cheti, kazi, heshima kwenye jamii lakini hakiwezi kikakupa maisha kwa sababu maisha yalinyang’anywa dhambi ilipoingia maana mwanadamu hakupewa maisha ya kwake alipewa maisha ya Mungu ambayo yanaitwa uzima. Yesu alisema nimekuja ili wawe na uzima kisha wawe nao tele. Huwezi kupata maisha ambayo Mungu aliyakusudia nje ya Yesu. Ubongo unapokea habari/information lakini akili inageuza habari kuwa ufahamu Haisemi ndipo akawafunulia akili zao wapate kusoma maandiko, kusoma hakuna shida, unaweza kusoma Biblia, ukakariri na kuimaliza yote lakini kuielewa akili lazima iingie kazini.

Sampuli Za Jihadi Katika Njia Ya Mwenyezi Mungu
Sampuli Za Jihadi Katika Njia Ya Mwenyezi Mungu

Sampuli Za Jihadi Katika Njia Ya Mwenyezi Mungu

Play Episode Listen Later Mar 1, 2015 51:08


Sampuli Za Jihadi Katika Njia Ya Mwenyezi Mungu

Ubora Wa Kumtaja Mwenyezi Mungu
Ubora Wa Kumtaja Mwenyezi Mungu No 1

Ubora Wa Kumtaja Mwenyezi Mungu

Play Episode Listen Later Feb 18, 2015 51:08


Ubora Wa Kumtaja Mwenyezi Mungu No 1

mungu ubora mwenyezi
Ubora Wa Kumtaja Mwenyezi Mungu
Ubora Wa Kumtaja Mwenyezi Mungu No 2

Ubora Wa Kumtaja Mwenyezi Mungu

Play Episode Listen Later Feb 18, 2015 51:08


Ubora Wa Kumtaja Mwenyezi Mungu No 2

mungu ubora mwenyezi
Ubora Wa Kumtaja Mwenyezi Mungu
Ubora Wa Kumtaja Mwenyezi Mungu No 3

Ubora Wa Kumtaja Mwenyezi Mungu

Play Episode Listen Later Feb 18, 2015 51:08


Ubora Wa Kumtaja Mwenyezi Mungu No 3

mungu ubora mwenyezi
Ubora Wa Kumtaja Mwenyezi Mungu
Ubora Wa Kumtaja Mwenyezi Mungu No 4

Ubora Wa Kumtaja Mwenyezi Mungu

Play Episode Listen Later Feb 18, 2015 51:08


Ubora Wa Kumtaja Mwenyezi Mungu No 4

mungu ubora mwenyezi