1971 studio album by Herbie Hancock
POPULARITY
Maisha yanarejea katika hali ya kawaida huko Goma baada ya siku kadhaa za mapigano kati ya jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, (FARDC) na waasi wa M23 mashariki mwa. Mwandishi wetu wa habari jimboni Kivu Kaskazini amesema kwamba shughuli zinaanza tena katika mji wa ziwa la Kivu, Goma, wakati M23 imechukua wilaya nyingi za mji mkuu wa Jimbo hili. Alikutana na Muhindo Kibwana muendesha pikipiki akiwa kwenye maegesho yake ya kazi, jina lake limebadilishwa kwa usalama wake.
Hii leo jaridani tunaangazia hali ya usalama Goma DRC, na masuala ya haki za binadamu. Makala na mashinani inaturejesha nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC kufuatilia simulizi za wakimbizi wa ndani.Maisha yanarejea katika hali ya kawaida huko Goma baada ya siku kadhaa za mapigano kati ya jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, (FARDC) na waasi wa M23 mashariki mwa. Mwandishi wetu wa habari jimboni Kivu Kaskazini amesema kwamba shughuli zinaanza tena katika mji wa ziwa la Kivu, Goma, wakati M23 imechukua wilaya nyingi za mji mkuu wa Jimbo hili.Ofisi ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa (OHCHR) imesisitiza haja ya kusonga mbele kuelekea awamu inayofuata ya usitishaji mapigano huko Gaza, kuachiliwa kwa mateka na wafungwa wote waliokamatwa kiholela, kukomesha vita na kujenga upya Gaza, kwa kuheshimu kikamilifu sheria ya kimataifa ya kibinadamu na sheria za kimataifa za haki za binadamu.Makala leo inakukutanisha na Mwamini Sebororo mmoja wa mamilioni ya raia wa Jamhuri ya Kidemkrasia ya Congo DRC waliopoteza makazi yao na kila kitu katika jimbo la Kivu Kaskazini mashariki ya taifa hilo huku mgogoro ukiendelea kufurusha watu zaidi, akiwa kambini Bushagara anasimulia kilichomsibuNa katika mashinani tutarejea nchini Jamhuri wa Kidemokrasia ya Congo DRC kusikia ujumbe wa mkimbizi wa ndani ambaye ni mwathirika wa vita Goma.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
Nyota ya Bensoul katika sanaa ina zidi kung'aa kila kukicha.
Shirika la Umoja wa mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limefanikiwa kumnyanyua msichana Nosizi Dube na kutimiza ndoto yake ya kuepuka ndoa ya utotoni na kupata shahada ya kwanza ya chuo kikuu. Msichana huyo mwenye umri wa miaka 24 ni wa kwanza katika jamii ya Washona wanaoishi mjini Nairobi Kenya kupata elimu katika ngazi hiyo. Mpango wa UNHCR wa kupambana na kutokuwa na utaifa kwa ushirikiano na serikali ya Kenya umekuwa chachu ya mafanikio ya msichana huyo. Mwandishi wetu wa Nairobi Thelma Mwadzaya alimtembelea Nosizi nyumbani kwake ili kupata undani wa safari yake..
Talking to the legendary Eddie Henderson was a dream come true for me. As I tell Eddie in the beginning of this episode, I've been listening to him for all my life: My father played Herbie Hancock's “Mwandishi” albums for me as a kid and when I was 13 I saw Eddie with Herbie's “Gershwin's … Continue reading Eddie Henderson
Leo ikiwa ni siku ya kimataifa ya haki za binadamu tunaelekea Kenya kuangazia moja ya ukiukwaji Mkubwa wa haki za binadamu dhidi ya wanawake, jinamizi la ukeketaji na jitihada zinazochukuliwa na wadau mbalimbali ikiwa ni pamoja na shirika la Umoja wa Mataifa ya idadi ya watu na afya ya uzazi UNFPA kutokomeza janga hilo. Mwandishi wetu wa Nairobi Thelma Mwadzaya amefuatilia kuhusu suala hilo na kwa undani zaidi ungana naye ..
Umoja wa Mataifa unatambua ni kwa kiasi gani habari potofu na habari za uongo kuwa ni mojawapo ya vikwazo vikuu vinavyokabili operesheni zake za kulinda amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC. Hii imesababisha Umoja huo kuhaha kila wakati kuona ni kwa vipi itakabiliana na habari hizo, iwe ni kupitia mafunzo kwa wanahabari, au kusaidia ujenzi wa vyombo vya habari, na hata kuzungumza na wananchi. Hivi karibuni Umoja Wa Mataifa kupitia Idara yake ya Ulinzi wa Amani, kitengo cha uadilifu wa habari, ulituma Tume yake Mashariki mwa DRC kukutana na wakazi ili kujua ni nini Umoja wa Mataifa unapaswa kufanya ili kupambana na habari potofu na za uongo nchini humo. Mwandishi wetu wa Mashariki mwa DRC, hususan jimboni Kivu Kaskazini, George Musubao alishuhudia ziara hiyo na ametuletea makala hii.
Umoja wa Mataifa kupitia shirika lake la Mpango wa Chakula Duniani WFP, ungali unaendelea kuwasaidia wakimbizi wa ndani nchini Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) ili kurejesha tabasamu la waliopoteza makazi yao kutokana na hali ya ukosefu wa usalama nchini humo. Chakula na pesa taslimu zilitolewa kwa wale wanaohitaji jimboni Kivu Kaskazini Mashariki mwa DRC. Mwandishi wetu George Musubao amekutana na Esther Josephine, mama wa watoto 3 aliyekimbia kutoka Kitsanga kwa sababu ya mapigano kati ya jeshi la serekali ya DRC (FARDC) na waasi wa M23, na anatueleza jinsi mama huyu amewezakujikwamua kiuchumi katika makala hii.
Umoja wa Mataifa unaendelea kuunga mkono serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC katika kukabili habari potofu na za uongo hususan huko mashariki mwa nchi ambako vikundi vilivyojihami vinaendelea kushambulia raia na kupambana na jeshi la serikali. Hivi karibuni Umoja wa Mataifa kupitia ujumbe wake wa kulinda amani nchini humo, MONUSCO, umeipatia kituo cha Taifa cha Redio na Televisheni, RTNC huko Beni jimboni Kivu Kaskazini jengo na vifaa vyenye thamani ya takriban dola elfu hamsini za Kimarekani. Hatua hiyo iliwezesha RTNC kuanza tena matangazo yake. Mwandishi wetu wa DRC, George Musubao alifika kituoni hapo kuzungumza na wahusika na wanufaika.
Mbali na usaidizi mkubwa kwa watu waliokimbia makazi yao kutokana na migogoro mashariki mwa DRC, shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) linatoa msaada kupitia miradi iliyo ndani ya mfumo wa kuzuia na kupunguza hatari za unyanyasaji wa kijinsia unaohusishwa na uhakika wa kupata chakula. Takriban wanawake 40 waliokimbia makazi yao wanaoishi katika kambi ya Bulengo jimboni Kivu Kaskazini, mashariki mwa DRC wamenufaika na mafunzo ya kusoma na kuandika tangu mwanzoni mwa mwaka huu wa 2024. Walengwa waliojifunza kusoma na kuandika wanashuhudia kwamba yamebadilisha maisha yao. Mwandishi wetu wa habari mashariki mwa DRC, George Musubao alisafiri kutoka Beni hadi Goma katika kambi ya Bulengo kuzungumza na mmoja wao.
Mwandishi wetu Steven Mumbi amezungumza na kundi la wasani la viongozi generation.
Hii leo jaridani tunaangazia mashambulizi ya kutisha ya kingono nchini Sudan, na mafunzo ya kidijitali. Makala na mashinani tunakupeleka nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, kulikoni?Ujumbe Huru wa Kimataifa wa Umoja wa Mataifa wa kutafuta ukweli nchini Sudan, leo Septemba 6 jijini Geneva, Uswisi, wametoa wito wa kuwekwa vikwazo vya silaha kote nchini Sudan kutokana na kukithiri kwa vitendo vya kikatili kama vile mashambulizi ya kutisha ya kingono.Uhusiano kati ya teknolojia, elimu, na mabadiliko ya tabianchi ni upi? Hili ndilo limekuwa swala kuu katika mkutano wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) uliopewa jina la Wiki ya Kujifunza kwa Kidijitali au Digital Learning Week uliokamilika jana Alhamisi huko Paris Ufaransa. Mkutano huu uliangazia maswala nyeti ya mchango wa teknolojia katika elimu inayolenga maendeleo.Makala tunaelekea DRC ambako George Musubao, Mwandishi wetu wa Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC akizungumza na Mkuu wa kikosi cha kujibu mashambulizi, FIB cha ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini DRC-MONUSCO anayemaliza muda wake mwezi huu baada ya kuhudumu kwa mwaka mmoja Brigedia Jenerali Alfred Matambo. Brigedia Jenerali Matambo anaanza kwa kuzungumzia matokeo ya moja ya operesheni kubwa za kijeshi 15 walizotekeleza dhidi ya makundi yenye silaha likiwemo la CODECO.Na katika mashinani, Daktari Erick Mashimango aliyeko nchini DRC anatueleza kuwa kuenea kwa ugonjwa wa mpox kwa kasi nchini humo ambako kumegharimu maisha ya ziadi ya watu 600 kumewafanya wananchi kuwa tayari kupokea chanjo.Mwenyeji wako ni Assumpta, karibu!
Mkuu wa kikosi cha kujibu mashambulizi, FIB cha ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini DRC-MONUSCO anayemaliza muda wake mwezi huu baada ya kuhudumu kwa mwaka mmoja Brigedia Jenerali Alfred Matambo akizungumza na George Musubao, Mwandishi wetu wa Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, anaeleza matokeo ya moja ya operesheni kubwa za kijeshi 15 walizotekeleza dhidi ya makundi yenye silaha likiwemo la CODECO na kazi za ujumbe huo nchini DRC.
Mwandishi wetu Steven Mumbi amezungumza na msani wa muziki huu wa Baibuda
Makala ya Gurudumu la Uchumi juma hili, inaangazia namna wafanyabiashara wamejipanga katika mwaka 2024, kuhakikisha biashara zao zinashamiri licha ya changamoto za kiuchumi zinazoikabili dunia kwa sasa. Mwandishi wetuj Victor Moturi, kwa niaba ya mtayarishaji wa makala haya, Emmanuel Makundi, amezungumza na wafanyabiashara nchini Kenya, ambao mwaka uliopita, walilalama kupata changamoto za kifedha na hata upandaji wa bidhaa na kukosekana kwa dola.
Makala ya Gurudumu la Uchumi juma hili, inaangazia namna wafanyabiashara wamejipanga katika mwaka 2024, kuhakikisha biashara zao zinashamiri licha ya changamoto za kiuchumi zinazoikabili dunia kwa sasa. Mwandishi wetuj Victor Moturi, kwa niaba ya mtayarishaji wa makala haya, Emmanuel Makundi, amezungumza na wafanyabiashara nchini Kenya, ambao mwaka uliopita, walilalama kupata changamoto za kifedha na hata upandaji wa bidhaa na kukosekana kwa dola.
Makala hii imejadili hatua ya rais wa Somalia, Hassan Sheikh Mohamud kusaini sheria ya kufuta makubaliano kati ya Ethiopia na eneo lililojitenga la Somaliland, hii ikiashiria kutoridhishwa na matumizi ya bandari ya Berbera, uamuzi unaoibua hofu ya kutokea mgogoro baina ya pande hizo mbili.Mwandishi wetu Ruben Lukumbuka ameangazia hili pamoja na mchambuzi wa siasa za kimataifa akiwa Washington Marekani, Abdullahi Boru pamoja na profesa Macharia Munene ni mchambuzi wa siasa, na mtaalamu wa maswala ya kidiplomasia akiwa Jijini Nairobi hapa Kenya
Katika makala wimbi la siasa tunaangazia hisia mseto zinazoenea kwenye eneo la ukanda wa nchi za maziwa makuu, baada ya mwishoni mwa juma lililopita, wakuu wa nchi kutoka Jumuiya ya SADC waliokutana mjini Luanda, Angola, kushindwa kutoa terehe kamili ya vikosi vyake kupelekwa mashariki mwa DRC. Aidha, viongozi wa SADC walikubaliana kumpa muda zaidi rais wa Angola, Joao Lourenco, kuendelea na juhudi za upatanishi kati ya nchi ya DRC na Rwanda. Mwandishi wetu George Ajowi anazungumza na Haji Kaburu akiwa Tanzania na Guershome Kahebe akiwa Marekani..
Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo - DRC, Shirika la Umoja wa Mataifa la kutegua Mabomu ya ardhini (UNMAS) Jumanne Julai 18 mwaka huu wa 2023 lilitegua bomu lenye uzito wa kilo 250 lililogunduliwa wiki iliyopita na wakulima katika eneo la Kididiwe, wilayani Beni. Jimboni Kivu Kaskazini. Wakazi wanaonesha furaha yao kwa Umoja wa Mataifa kwa kutegua bomu hilo linalosababisha vifo. Mwandishi wetu wa nchini DRC, George Musubao amefuatilia na kuandaa makala hii.
Hii leo jaridani tunakuletea kipindi maalum kuelekea siku ya kimataifa ya lugha ya Kiswahili itakayoadhimishwa wiki hii na leo tutakuwa nchini Kenya ambapo mada kuu ya mwaka huu ya Siku ya Kiswahili inampa faraja Wangari Grace, Mwandishi wa vitabu vya kiswahili, msimulizi wa hadithi na msanii kwani amefanikiwa kusimulia hadithi kwa watu walioko kwenye mataifa mbalimbali kupitia majukwaa ya kijamii kama vile Youtube, TikTok, podcast na hata pia kuandika vityabu vya dijitali yaani e-book. Pia tunakuletea habari kwa ufupi zikiwemo za UNICEF, Baraza la haki za binadamu na UNHCR. Mashinani tutaelekea nchini Tanzania, kulikoni? Nchi 12 barani Afrika zinatazamiwa kupokea dozi milioni 18 za chanjo ya kwanza ya malaria katika kipindi cha miaka miwili ijayo imeeleza leo taarifa ya pamoja iliyotolewa na Mashirika ya Umoja wa Mataifa lile la Afya ulimwenguni WHO na lilanoshughulika na watoto UNICEF huku wakishirikiana na Ubia wa chanjo duniani, GAVI.Mtaalamu huru wa Umoja wa Mataifa anayehusika na masuala ya wakimbizi wa ndani Paula Gaviria ameliambia Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa kuwa idadi ya wakimbizi wa ndani inazidi kufurutu ada na huo ni ukweli wa kutisha. Na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi,UNHCR limeeleza kunasikitishwa na ripoti zinazoendelea za raia nchini Sudan, wakiwemo wakimbizi wa ndani na wakimbizi waliokumbwa na mzozo unaoendelea, wamekuwa wahanga wa mauaji ya kiholela wa mapigano na kuzuiwa kutafuta usalama.Na katika mashinani leo tunaelekea katika Wilaya ya Mbozi nchini Tanzania kusikiliza ni kwa jinsi gani wazazi na walezi wanaweza kuweka nyumba zao salama dhidi ya ukatili kupitia malezi bora toka mtoto anapozaliwa hadi anapokuwa kijana barubaru.Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!
Muungano wa mashirika ya kiraia katika eneo la Kalehe jimboni Kivu Kusini, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC wako katika harakati za kuhamasisha wananchi kupanda miti na kuchukua hatua nyingine zitakazosaidia kupambana na mabadiliko ya tabianchi baada ya eneo hilo kukumbwa na mafuriko yaliyosababisha vifo na uharibifu mkubwa mapema mwezi Mei Mwaka huu. Mwandishi wetu wa DRC George Musubao amefika huko na kutuandalia makala ifuatayo. Kwako George.
Hii leo jaridani tunaangazia Migogoro nchini Ukraine na wakimbizi nchini Kenya. Makala tunakupeleka nchini Tanznai na mashinani tunasalia hapa hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa, kulikoni? Mratibu wa masuala ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa nchini Ukraine Matthew Hollingworth amelaani vikali shambulio lililofanywa na Urusi kwenye eneo la Kherson lililoathirika vibaya na mafuriko ya bwawa la Kakhovka, na kukatili maisha ya mfanyakazi wa ukoaji na kujeruhi wengine.Serikali ya Kenya inaendesha mradi wa “shiriki” ambao unawapa fursa wakimbizi wanaosihi katika kambi ya wakimbizi ya Kakuma iliyoko katika kaunti ya Turkana nchini humo kujitegemea kwa kufanya kilimo cha mbogamboga kupitia chama cha ushirika wa wakulima. Serikali hiyo imetenga ekari 21katika kambi ya Kakuma ili kutumika katika mradi huo ambao sio tu unawapa lishe bora wakimbizi, matumaini na kipato lakini pia umekuwa neema kwa jamii za wenyeji. Katika makala Mwandishi wa redio washirika wetu MVIWATA FM ya Tanzania anatupeleka visiwani Zanzibar ambako umezinduliwa mradi wa AliVE awamu ya pili unaolenga kupima stadi za maisha na maadili kwa wanafunzi Watoto wa umri wa miaka 6 hadi 12.Na mashinani leo ikiwa ni siku ya Yoda duniani tunarejea makao makuu ya Umoja wa Mataifa kusikia ujumbe kutoka kwa Katibu Mkuu wa Umoja huo alieleza kwa nini yoga ni muhimu katika maisha ya mwanadamu.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
Taasisi 16 zikiwemo mashirika yasiyo ya kiserikali, asasi za kiraia na vyuo vikuu ambao kwa pamoja ni wanachama wa Mtandao wa Elimu Afrika Mashariki (RELI) wamekutana mjini Morogoro, Tanzania kujengewa uwezo wa namna ya kuimarisha juhudi za kuchochea mabadiliko ya elimu na kuhamasisha ujengaji fikra tunduizi kwa vijana ili kusongesha lengo namba 4 la Malengo ya Umoja wa Mataifa ya Maendeleo Endelevu SDGs. Mafunzo haya yameratibiwa na Shirika lisilo la kiserikali la GESCI (The Global e-Schools and Communities Initiative) kutoka nchini Kenya linalotekeleza mradi wa ADAPT Kenya na Tanzania, Mwandishi wa Habari Hamad Rashid wa Redio washirika wetu MVIWATA FM ya Morogoro Tanzania amefuatilia mafunzo hayo ya siku tatu na kutuandalia makala ifuatayo.
Tangu kuanza kwa hali mbaya ya usalama mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, Shirika la Umoja wa Mataifa wa Kuhudumia Wakimbizi UNHCR limekuwa likifanya kazi ya kuboresha hali ya maisha ya wakimbizi na kwa wakimbizi wa ndani. Ujumbe mkuu wa shirika hilo la UNHCR upo katika ziara ya siku kadhaa katika jimbo la Kivu kaskazini na umekuwa ukibadilishana mawazo na watu waliokimbia makazi yao nchini humo. Moja ya maeneo ambayo Ujumbe huo wa UNHCR umetembelea ni eneo la wakimbizi la Rusayo. Mwandishi wa hii ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa nchini DRC, Byobe Malenga ameandaa makala hii kuhusu ziara hiyo.
Ni takribani wiki moja tangu eneo la Kalehe lililoko jimbo la Kivu Kusini nchini DRC, likumbwe na mafuriko kufuatia kuongezeka kwa kina cha maji katika mito kulikosababishwa na mvua kubwa. Serikali ya DRC na mashirika yasiyo ya kiserikali yametuma wajumbe mbalimbali papo hapo kwenda kufanya uchunguzi ili kutoa misaada ya kibinadamu kwa wahanga. Mwandishi wa Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa nchini DRC George Musubao amezungumza kwa njia ya simu na Yvon Edoumou ambaye ni msemaji wa ofisi ya Umoja wa Mataifa ya uratibu wa misaada ya dharura, OCHA nchini humo ili kufahamu hali inaendeleaje.
Jaridani leo tunakuletea mada kwa kina na leo tunamulika juhudi za kumkwamua mjasiriamali hasa nchini Kenya. Pia tunakuletea habari kwa ufupi zikiwemo ziara za Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Qatar, haki za binadamu na misaada kutoka mashirika nchini Sudan. Katika mashinani na kuelekea siku ya kimataifa ya uhuru wa vyombo vya habari hapo kesho, tunakuletea ujumbe wa Mwandishi wa Habari kutoka Uingereza kuhusu changamoto zinazowakumba waandishi wa habari.Mratibu Mkuu wa Umoja Mataifa kuhusu misaada ya dharura, Martin Griffiths ambaye yuko Kenya kusaka suluhu ya kufikisha misaada ya kiutu nchini Sudan, amemshukuru Rais William Ruto kwa uongozi na usaidizi wake kuona hatua za dharura za kiutu zinachukuliwa ili misaada ifikie nchini Sudan. Ametoa kauli hiyo baada ya Rais Ruto kuongoza mkutano uliohudhuriwa na viongozi waandamizi wa Umoja wa Mataifa wakiwemo Naibu Katibu Mkuu wa UN Amina Mohammed, Mkuu wa UNHCR Filippo Grandi na Bwana Griffiths.Hayo yakiendelea, msemaji wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya uratibu wa misaada ya dharura, OCHA Jens Laerke amezungumza na waandishi wa habari huko Geneva Uswisi hii leo na kusema mashirika ya Umoja wa Mataifa ya usaidizi wa kiutu yanakabiliwa na pengo la dola bilioni 1.5 la kufanikisha operesheni zake Sudan wakati huu mahitaji yanaongezeka kutokana na mapigano yanayoendelea, maelfu ya watu wakifurushwa makwao.Naye msemaji wa shirila la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi duniani, UNHCR mjini Geneva, Uswisi Olga Sarrado Mur amewaambia waandishi wa habari hii leo kwamba shirika hilo litazindua Mpango wa mashirika ya Umoja wa Mataifa wa kuchukua hatua za usaidizi Sudan, wakati huu ambapo takwimu za serikali, wadau na UNHCR zinaonesha zaidi ya watu 800, 000 wamekimbia Sudan na kuelekea Chad, Ethiopia, Sudan Kusini, na kwingineko, ambapo 600,000 ni wasudan na 200,000 ni wasudan kusini na wengineo waliokuwa wanapatiwa hifadhi Sudan.Na katika mashinani na kuelekea siku ya kimataifa ya uhuru wa vyombo vya habari hapo kesho, tunakuletea ujumbe wa Mwandishi wa Habari kutoka Uingereza kuhusu changamoto zinazowakumba waandishi wa habari.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
Leo ni siku ya furaha duniani ambapo Umoja wa Mataifa unasema ni siku ya kutabua umuhimu wa furaha kwa watu wote ulimwenguni kwani ni msingi wa lengo la ubinadamu na pia huchagiza ukuaji wa kiuchumi. Mwandishi wetu wa Beni jimboni Kivu Kaskazini nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC. Wa kwanza kuzungumza mjini Beni ambako vikundi vya waasi vimekuwa vikishabulia raia, ni Vakekya Kaswera mama huyu wa watoto 7 akiwa shambani anasema furaha kwake yeye ni shamba lake analolima mihogo. Shambani anapata sombe au kwa kiswahili kisamvu na pia anapata unga wa muhogo. Hata hivyo anasema “furaha yangu inapotea pale mbuzi wanapokuja na kuharibu mazao yangu. Napenda kazi ya kilimo kwa sababu ndio kazi yangu tangu mdogo na inaniweza kutunza familia. Wazazi walitufundisha kulima na pia walitupeleka shuleni.” Mkazi mwingine Serge Kyamundu kwake yeye furaha ni pale enzi hizo ilikuwa inawezekana kupata starehe mjini Beni. “Kwangu ni furaha ni pale ninaona mji wangu uko katika starehe. Miaka iliyopita katika mji wetu wa Beni muziki ulipigwa ilikuwa furaha hakika. Lakini leo hii wakati usalama umemalizika katika mji wetu furaha kwangu imekwisha.” Ametoa wito kwa watu wengine wa nje na serikali za mbali zisaidie kurejesha usalama ili furaha irejee Beni kwani katika siku ya leo ya furaha“watoto wa Beni hatuna hakika furaha kwani tunakosa usalama katika mji wetu.” Naye Sylvie Mbakania, mkulima amesema “furaha yangu ni kutazama mazingira yakiwa mazuri. Ninapoona mbegu zimechipuka hunipatia furaha.” Hata hivyo hivi sasa furaha yake si kamilifu “kwa sababu ya vita katika nchi yetu. Natoa wito kwa Umoja wa Mataifa kufanya juhudi zaidi kurejesha amani ili kukamilisha furaha yangu kama vile mahali pengine wanasherehekea siku hii.” Tarehe 12 mwezi Julai mwaka 2012, Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa lilipitisha tarehe 20 ya kila mwaka kuwa siku ya furaha duniani kwa kutambua mchango wake furaha na ustawi kama malengo ya kimataifa na matamanio ya kila binadamu.
Hii leo jaridani tunaangazia taarif aya UNICEF kuhusu kipindupindu, na ziara ya Baraza la Usalama DR Congo. Makala tutasalia huko huko DR Congo kushuhudia maadhimisho wa makabidhiano kati ya TANZBATT 9 na TANZBATT 10, na mashinani tukuletea ujumbe kutoka CSW67.Nchi 11 Mashariki na Kusini mwa Afrika zinakabiliwa na hali mbaya ya mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu ambako hadi sasa kumeripotiwa wagonjwa 67,822 na vifo 1, 788 kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF.Ujumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa umewasili nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC , ikiwa ni sehemu ya ziara ya kikazi ya kutathmini hali ya usalama na utekelezaji wa majukumu ya vikosi vya umoja wa mataifa vya kulinda mamani nchini humo MONUSCO. Mwandishi wetu wa Kinshasa Byobe Malenga amefuatilia kuhusu ziara hiyo na kutuandalia taarifa ifuatayo.Makala tunakwenda nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC ambako huko kikosi cha 9 cha Tanzania kwenye ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo MONUSCO kimetamatisha jukumu lake na sasa kimekabidhi majukumu kwa TANZABATT-10 kama anavyoripoti Afisa habari wa kikosi hicho Kapteni Denisia Lihaya.Na mashinani tukuletea ujumbe wa mbunge kutoka Tanzania ambaye anashiriki mkutano wa kamisheni ya hali ya wanawake duniani CSW kikao cha 67 hapa makao makuu wa Umoja wa Mataifa.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC Bintou Keita amesema kwamba mpango wa Umoja wa Mataifa nchini huomo MONUSCO unasisitiza wito wa Antonio Guterres, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwa makundi yenye silaha yanayoendesha operesheni zao DRC kuweka chini silaha zao mara moja pasi na masharti yoyote.Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC Bintou Keita amesema kwamba mpango wa Umoja wa Mataifa nchini humo MONUSCO unasisitiza wito wa Antonio Guterres, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwa makundi yenye silaha yanayoendesha operesheni zao DRC kuweka chini silaha zao mara moja pasi na masharti yoyote. Mwandishi wetu wa Kinshasa BYOBE MALENGA na tarifa zaidi.Bi Bintou Keita, Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu nchini DRC ametoa kauli hio wakati wa mkutano na waandishi wa habari wakati ahitimisha ziara yake mwishoni mwa wiki katika majimbo matatu ya Mashariki mwa nchi amambapo amesema amehuzunishwa sana na hali ya wakimbizi wa ndani,“Nilikuja kuona kwa uhakika athari za kuzorota kwa hali ya usalama katika maisha ya mamia kwa maelfu ya watu walio katika mazingira magumu, wakiwemo wanawake na watoto. Nimetembelea maeneo ya Bushagara na mugwera huko Kivu Kaskazini na KISOGE huko Ituri. Nimekutana na wanawake na wanaume walio katika dhiki lakini ambao bado wana matumaini. Wana nia moja tu ya kurejea kwa amani ili warudi majumbani kwao salama. Haya ni matakwa yetu ya pamoja.” Keita amewataka waasi wa kundi la M23 kuheshimu mkataba wa mwisho wa mkutano mdogo wa kilele uliofanyika mjini Launda nchini Angola ambao unaowataka waasi hao kuondoka na kurejea katika nafasi yao ya awali kwenye Mlima Sabinyo kabla ya Jumanne ya Machi 7 mwaka huu bila masharti kabla ya kutaka mazungumzo yoyote na serikali ya DRC, “Ninakaribisha hatua ya mpatanishi wa Umoja wa Afrika, Rais wa Angola Joao Lourenço, ambayo imefanya Ijumaa kutolewa ahadi ya M23 ya kusitisha mapigano mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kuanzia Jumanne tarehe 7 Machi saa 12 Jioni. Ninatoa wito kwa vuguvugu hili la waasi wa M23 kuheshimu bila masharti au kusita, masharti ya tamko la Luanda la Novemba 23, ambalo linadai wajiondoe katika maeneo yanayokaliwa, kusitishwa kwa mapigano yote, kuwaondoa wapiganaji wao na kurudi katika eneo lao la awali kwenye Mlima Sabino “. Wito huo unakuja wakati waasi wa M23 wakiteka vijiji kadhaa katika maeneo ya Masisi, Rutshuru na Nyiragongo, hali iliyosababisha zaidi ya watu 600,000 kuyahama makazi yao.
Welcome to the latest Courtney Pine Global Podcast Bitesize Edition! A coffee break's worth of cool jazzy vibes to wet your appetite for the full show. Commercial free, and hand-picked by Courtney for a vibrant, and soulful listen! This week: foot-tappin' goodness from the Greyboy Allstars, Peruvian beats from Alex Acuna and Analog fusion from Wasafiri!Please let all your jazz friends know that they can listen for free on Apple podcasts, Google Podcasts, Amazon Music and always at jazz-pod.comVisit our archive here Join the CPG community by following us on Facebook & Instagram Ask us ANYTHING(!) about jazz over on Twitter Watch our FAB & FUN artist features over on Tiktok1 The Greyboy Allstars - Quantico (A Town Called Earth/Knowledge Room Records/Light in the Attic) The Greyboy Allstars—Karl Denson sx Robert Walter keys Elgin Park (aka Mike Andrews gtr Chris Stillwell bs Zak Najor dr One of the longest surviving bands to arise on the fledgling acid jazz and jam scenes in the ‘90s, The Greyboy Allstars stay busy individually, as well. Two of its founding members are on the road this summer with classic rock royalty: Karl Denson is holding down saxophone duties with The Rolling Stones across Europe in what is his seventh year as a touring member of the band, while Robert Walter is currently playing keys with Roger Waters on his “This Is Not A Drill” North American tour. 2 Alex Acuna - Cuncho (Gift LE COQ) Alex Acuna dr Otmaro Ruiz keys Ramón Stagnaro gtr John Peña bs Lorenzo Ferrero sx The incredible journey of Alex Acuña has seen the renowned drummer-percussionist travel from his small rural hometown in Peru to being a first-call session drummer in the country's capital city, Lima, then touring the United States with mambo king Pérez Prado, gigging in Las Vegas with Elvis Presley and ultimately touring internationally with Weather Report, the premiere fusion band of the mid-1970s. An in-demand Los Angeles session musician for decades, he has appeared on nearly 900 studio records and movie soundtracks while also releasing half a dozen albums under his own name.3 Wasafiri - G's Bounce (Klearlight EASTWOOD) Max Gerl bs/comp Kwinton Gray, keys Ethan Ditthardt gtr Marcus Jones dr Nick Rothouse perc Shelley Carrol fl/tnr Matthew Babineaux fl/sx Cole Riddle synth Gerl's an alumni of Berklee College of Music in Boston and Booker T. Washington High School for the Performing Arts in Dallas where Roy Hargove, Norah Jones, and Erykah Badu went to high school. In order to get the right vibe, Wasafiri recorded the album at Klearlight Studio in Dallas, Texas – a spot known for its assortment of vintage analog gear. It would afford them the opportunity to employ some of the original tools that Miles Davis, Joe Zawinul and Chick Corea used some 50 years prior – all recorded through an Auditronics 501 console that had once resided at the famed Wally Heider Studios in San francisco – the same studio where Herbie Hancock recorded Mwandishi, Head Hunters and Sextant in the early 70's. Next week on Courtney Pine Global: original sounds from Jazz Is Dead and inspirational northern lights from Norway! Hit subscribe wherever you're listening so you don't miss it!
Kampeni ya utoaji wa chanjo dhidi ya ugonjwa wa kipindupindu iliyoanza tarehe 25 mwezi huu huko Kivu Kaskazini nchini jamhuri ya Kidemokraia ya Congo, DRC imekunja jamvi jana Jumanne ya tarehe 30 mwezi hu uwa Januari ambapo shirika la Umoja wa Mataifa la afya ulimwenguni WHO lilizindua kampeni hiyo ya chanjo kwa wakimbizi wa ndani katika kambi ya wakimbizi hao ya Kanyaruchinya wilayani nyiragongo katika mji wa Goma jimboni Kivu Kaskazini.Mwandishi wetu wa DRC Byobe Malenga ambaye ameshuhudia uzinduzi huo amesema uliongozwa na Gavana wa jimbo la Kivu Kaskazini Jenerali Ndima Constant, na Mwakilishi wa shirika WHO nchini DRC kwa lengo la kuokoa mamia ya familia hususan za wakimbizi wa ndani ambao tayari makumi kwa makumi wameripotiwa kupata ugonjwa huo na wengine wamefariki dunia.Jean Bruno, ni Mkuu wa Ofisi ya WHO Kivu Kaskazini na anasema ameridhishwa na shauku ya siku ya kwanza na zaidi ya yote amesema,« Tumewalenga watu 364,127 ambao ni wakimbizi wa ndani, pamoja na familia zinazowapokea. Tayari tumepokea dozi 364,150 ambazo zipo na zitatumika. chanjo itafanyika kwa awamu ya dozi moja na tutafanya hivyo kupitia kampeni ya nyumba kwa nyumba kwenye maeneo haya . Tumeridhika na ukweli ni kwamba kumekuwa na dhamira muhimu kwa upande wa serikali kwenye ngazi ya taifa na mkoa, lakini pia tumekuwa na hakikisho kutoka kwa jamii ya watu na wakimbizi wa ndani ambayo imekubali chanjo hiyo ambayo itafanyika kwa wakati».Eneo la Nyiragongo lilipokea idadi kubwa ya watu waliokimbia makazi yao kutokana na mashambulizi yanayofanywa na waaasi wa M23 huku watu 233 elfu waliokimbia makazi yao, zaidi ya 95% yao wamelundikana kwenye makanisa, shule, viwanja vya michezo na maeneo yasio salama kwa afya yao.Gavana wa Kivu Kaskazini, Jenerali Ndima Constant, anakiri kwamba janga la kipindupindu linaathiri sana eneo la Nyiragongo akisema kwamba hadi Jumanne ya Januari 24 wagonjwa 3706 wa kipindupindu walisajiliwa huku kukiwa na vifo 16 na ili kupunguza mlolongo wa maambukizi amewasihi raia kupata chanjo akishukuru WHO kwa msaada wao.« Madhumuni ya kampeni hii ya chanjo ni kulinda idadi ya watu dhidi ya kipindupindu katika jimbo la Kivu Kaskazini na hasa katika maeneo ya watu waliofurushwa ili kupunguza vifo. Mabibi na mabwana, wageni mashuhuri, ili kufunga maoni yangu, ningependa kuwakumbusha kuwa pamoja na chanjo utakayopokea, kufuata hatua za kuzuia maambukizi ni muhimu..”Ametaja njia za kujikunga kuwa ni pamoja na kunawa mikono mara kwa mara kwa maji safi na sabuni au majivu, kunywa maji yaliyotakasishwa tu au yaliyochemshwa. Kupika na kufunika milo yetu, matumizi sahihi ya vyoo huku tukiwa wasafi na kuweka usafi kwenye maeneo yetu ya makazi kila wakati.Waliokimbia makazi yao wanafahamu tishio hilo kwa sababu janga hilo limeathiri zaidi ya 89% ya waliokimbia makazi katika miezi ya hivi karibuni na chanjo inatekelezwa nyumba kwa nyumba.Watu waliohamishwa wanasubiri dozi zao nyumbani. Damaseni Butera ni miongoni mwa watu wa kwanza kupata dozi moja dhidi ya kipindupindu na anashukuru mpango huu wa WHO na anasema, «chanjo ni muhimu sana katika mapambano dhidi ya magonjwa kama kipindupindu, malaria na mengine.Tumejifunza habari kuhusu chanjo hiyo, tumefurahi sana kwa sababu tutakuwa na kinga, asante sana kwa shirika la WHO ambalo lilitufikiria. Asante sana»Kando na hilo, Mweze Shemba, aliyekimbia kutoka kijiji cha Kiwanja, pia alinufaika na chanjo hii. Licha ya njaa,yeye anapendelea kujilinda pamoja na familia yake dhidi ya janga hili akisema, «kilichonifanya nipate chanjo ya leo hapa katika kambi ya wakimbizi ni kwa sababu tunapatwa na magonjwa ya taabu. kama vile kuharana kutapika hasa tunapokunywa maji machafu. Lakini wakati tunapata hii chanjo tunaona kama vile ni kinga kwetu tunashukuru sana »Katika juhudi za kuepusha msongamano wa wagonjwa wa janga hili , WHO ilijenga vitalu 3 kama kitengo cha matibabu ya wagonjwa wa Kipindupindu (UTC) katika eneo la Bushagara na…
Ripoti mpya ya shirika la Umoja wa Mataifa la kazi duniani, ILO imepigia chepuo mipango bunifu ya ufanyaji kazi kama ile iliyoanza kutumika kufuatia mlipuko wa janga la COVID-19 ikisema inaweza kuleta manufaa kwa uchumi, biashara na wafanyakazi.Ikipatiwa jina Mizania kati ya saa kazi na saa za kufurahia maisha duniani kote, ripoti imesema mipango hiyo inaweza kuongeza tija zaidi na mizania ya kazi na maisha yenye afya kwa mtumishi. Ripoti inamulika mambo makuu mawili ambayo ni muda wa kazi ikiwa ni saa za kufanya kazi na mipango ya ufanyaji wa hizo kazi namizania zaidi kati ya ufanyaji kazi au ratiba za kazi na upande wa pili athari ya mambo hayo kwenye utendaji wa biashara husika na jinsi mtumishi anaweza kuweka mizania kati ya kazi na maisha yake. Mipango ya utendaji kazi iliyochambuliwa kwenye ripoti hiyo na athari zake kwenye utendaji kazi na maisha ya mtumishi ni pamoja na kufanya kazi kwa zamu, kufanya kazi kwa saa nyingi mfululizo na kisha mapumziko, halikadhalika kusubiri kuitwa endapo mtumishi atahitajika. Ripoti ina takwimu mpya zaidi saa za kazi kabla na wakati wa janga la COVID-19 ambapo utafiti uliozalisha ripoti hiyo umebaini kuwa idadi kubwa ya watu wanafanya kazi kwa saa nyingi au kidogo ikilinganishwa na muda unaotakiwa kisheria wa saa 8 kwa siku au saa 40 kwa wiki. Zaidi ya theluthi moja ya wafanyakazi walikuwa wanafanya kazi zaidi ya saa 48 kwa wiki, ilhali mfanyakazi 1 kati ya 5 duniani kote anafanya kazi ya kibarua ya chini ya saa 35 kwa wiki. Ripoti inasema wafanyakazi kwenye sekta isiyo rasmi wako katika nafasi ya kufanya kazi kwa muda mrefu au mfupi zaidi. Ripoti imeonesha ushahidi ya kwamba kumpatia mfanyakazi chaguo la jinsi ya kufanya kazi, wapi afanyie kazi na wakati gani afanya kazi kunaweza kuleta tija kwa mtumishi na mwajiri, na kwamba kudhibiti mazingira hayo kunaweza kuongeza gharama ikiwemo watumishi kuacha kazi. Mwandishi kiongozi wa ripoti hiyo Jon Messenger amesema kitendo cha watumishi wengi kuamua kwa hiari kuacha kazi kimeweka mbele hoja ya mizania ya kazi na maisha kwenye masuala ya jamii na soko la ajira baada ya janga la COVID-19. Amesema “iwapo tutatumia baadhi ya kile tulichojifunza kutokana na janga la COVID-19 na kuangalia vyema mpangilio wa saa za kazi na urefu wake, tunaweza kuwa na mazingira ya kazi yenye maslahi kwa pande zote, kuimarisha utendaji wa kampuni na mizania ya kazi na maisha kwa mtumishi.” ILO ina mapendekezo matano ikiwemo kutambua kuwa sheria za saa za kazi na kanuni kuhusu kiwango cha juu cha saa za kazi na likizo ni mafanikio yanayochangia kwa afya na ustawi wa jamii na hivyo visiwekwe hatarini. Ripoti inatanabaisha kuwa saa nyingi za kazi zinasababisha tija kidogo ilhali saa chache za kazi zinachangia tija kubwa. Kisha nchi zitumie uzoefu wao wakati wa kupunguza saa za kazi wakati wa janga la COVID-19 ikiwemo saa za kazi kulingana na mazingira ya mtumishi. Halikadhalika ripoti pia inapendekeza mpango wa mtumishi kufanya kazi kutoka eneo lolote duniani kwani unasaidia kuendeleza ajira ya mtumishi na kujenga mazingira ya mtumishi kujisimamia. Hata hivyo imeonya umakini katika mfumo huu kwa kuweka sera za kuainisha ni wakati gani mtumishi ana haki ya kutofanya kazi wakati wa saa za kazi.
Hii leo katika Habari za UN tunakuletea Habari kwa Ufupi, Mada kwa Kina na Mashinani na zote zikiwa ne mrengo wa mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi unaofanyika huko Sharm el-Sheikh nchini Misri.Habari kwa Ufupi: Ripoti ya UNICEF kuhusu mafuriko kuathiri watoto milioni 27.7 duniani kote; WMO kutaka viongozi wachukue hatua kuhusu namna ya kutumia vema maji kama suluhu ya mabadiliko ya tabianchi; Mwandishi mshirika wetu Joyce Shebe akiwa Sharm el-Sheikh anatupatia kile kilichosemwa na marais wa Tanzania, Malawi na Kenya.Mada kwa kina: Flora Nducha akiwa Kigali nchini Rwanda ametembelea mradi wa vijana Greencare Liimted wakihakikisha wanadhibiti utupaji taka kama njia ya kulinda mazingira.Mashinani: Mwanaharakati kijana Leah Namugerwa kutoka Uganda akiwa huko Sharm el-Sheikh anahoji iwapo viongozi wanataka wakumbukwe kama walikuwa madarakani bila kufanya lolote au vipi?Karibu na mwenyeji wako ni Assumpta Massoi.
Viongozi wa Umoja wa mataifa pamoja na serikali ya Jamhuri ya Kidemoktrais ya Congo, DRC wametoa heshima zao za mwisho kwa walinda amani watano wa kwenye ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo MONUSCO waliokufa wakati wa maandamano na uvamizi wa vituo vya ujumbe huo huko Goma na Butembo jimboni Kivu Kaskazini. Walinda amani hao wanatoka Morocco na India ambapo Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini humo Bintou Keita amesema MONUSCO iko tayari kwa mazungumzo ya amani ili kuendeleza na kudumisha amani nchini humo. Taarifa iliyoandaliwa na Mwandishi wetu wa DRC, Byobe Malenga inaeleza zaidi. Tukio la kuaga walinda amani hao wa Umoja wa Mataifa limefanyika mbele ya Mkuu wa operesheni za ulinzi wa amani za Umoja wa Mataifa Jean-Pierre Lacroix na Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini DRC Bintou Keita. Bwana Lacroix amesema walinda amani hao mashujaa waliokufa wakilinda sio tu Umoja wa Mataifa bali pia raia na kwamba sheria ichukue mkondo wake kuepusha chuki baina ya walinda amani wa UN na raia nchini humo. “Kwa hivyo, ingawa tunasikitishwa na kuwapoteza mashujaa wetu hawa watano waliofariki dunia katika huduma ya kulinda amani, kumbukumbu inatuwajibisha sote kuwa na shukrani. Walitenda kazi kwa ushujaa kutulinda na kulinda watu licha ya maandamano kupita kiasi na hila zilizosababisha tukio hili baya. Haki lazima itolewe kwa wenzetu wote wa Umoja wa Mataifa ambao wamepoteza maisha, lakini bila shaka haki lazima itolewe kwa ndugu na dada zetu wote wa DRC ambao wanaendelea kuteseka na vitisho vya vita." Amesema Jean-Pierre Lacroix Naye Bintou Keita ambaye pia ni Mkuu wa MONUSCO ameelezea mshikamano wake na rambirambi kwa familia zinazoomboleza na kuthibitisha utayari wa ujumbe huo kupokea ukosoaji na uwazi wake wa mazungumzo na pande zote DRC zinazotaka kuwasilisha malalamiko yao kwa amani akisema, “MONUSCO inakabiliwa na wimbi la maandamano na uhasama. Ningependa kuthibitisha uwazi wa Monusco na timu nzima ya Monusco kwa ukosoaji wowote na upatikanaji wake wa kufanya mazungumzo na wale wote wanaotaka kueleza malalamiko yao kwa njia ya amani ili kuchangia MONUSCO kuondoka kwa utaratibu na kuwajibika kwa ujumbe wetu.”
Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC imesihi utulivu miongoni mwa wananchi baada ya maandamano na uvamizi dhidi ya vituo vya ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani MONUSCO kwenye miji ya Goma na Butembo jimboni Kivu Kaskazini, tukio ambalo hata Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametaka mamlaka zichunguze na sheria ichukue mkondo wake. Mwandishi wetu wa DRC Byobe Malenga ana taarifa zaidi. Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC imesihi utulivu miongoni mwa wananchi baada ya maandamano na uvamizi dhidi ya vituo vya ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani MONUSCO kwenye miji ya Goma na Butembo jimboni Kivu Kaskazini, tukio ambalo hata Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametaka mamlaka zichunguze na sheria ichukue mkondo wake. Mwandishi wetu wa DRC Byobe Malenga ana taarifa zaidi.
Kikundi cha tisa cha walinda amani kutoka Tanzania, TANZBATT-9, kinachohudumu chini ya ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, MONUSCO kimeanza kusambaza daftari na vifaa vingine vya shule kwa watoto katika maeneo ya Mavivi huko BENI mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kwa lengo la kuwahimiza wanafunzi hao kuzungumza lugha ya Kiswahili ili wakimaliza shule waweze kuwasiliana na mataifa mengine. Hii imekuja wiki chache tu baada ya kusherehekewa (nimondoa kushereekewa) kwa Siku ya Kiswahili Duniani ambayo iliadhimishwa tarehe 7 mwezi huu Julai. Mwandishi wetu wa DRC Byobe Malenga ametuandalia makala ifuatayo.
In previous episodes, we've talked about what people commonly understand as fusion, which drummer Lenny White, who appeared in episode two of this series, prefers to call jazz-rock. That's the version that starts with Miles Davis's Bitches Brew and Tony Williams' Lifetime and quickly branches out with Mahavishnu Orchestra and Return To Forever and Weather Report and on and on. But as we've continued the discussion, we've expanded the scope of inquiry to include adventurous funk and R&B fusion, which includes everything from P-Funk and Earth, Wind & Fire and the Ohio Players — and wow, do the Ohio Players deserve a place in the fusion conversation that they are very rarely granted — to Donald Byrd and Freddie Hubbard and especially George Duke.Adam Rudolph is a fusion artist in about as broad a sense as you can imagine. He's been a percussionist for close to 50 years, and should be much better known than he is. He's been around since the early '70s and has worked with everyone: Yusef Lateef, Fred Anderson, Don Cherry, Roscoe Mitchell, Pharoah Sanders, Sam Rivers, Wadada Leo Smith, Herbie Hancock, Maulawi, Foday Musa Suso, Hassan Hakmoun, Jon Hassell… he's part of the Bill Laswell company of players, too, so he's on a zillion records through that connection. Plus he leads two main groups of his own, Moving Pictures and the Go! Organic Orchestra, which have made many, many albums and even crossed over with each other a time or two.Adam and I had a really fascinating conversation over the course of two phone calls. The impetus was Symphonic Tone Poem For Brother Yusef, a collaboration between him and reeds player Bennie Maupin that's just been released. Bennie Maupin of course is a legend on his own — he played on Miles Davis's Bitches Brew and On The Corner, he was a member of Marion Brown's group in the 1960s, he was in Mwandishi and the Headhunters with Herbie Hancock, he played with Woody Shaw, and his own album from 1974, The Jewel In The Lotus, is an absolutely brilliant record that blends spiritual jazz with almost New Age ambient music. There's really no other album like it; if you've never heard it, it's a must-hear. So obviously Rudolph and I talk about Maupin, whom he's worked with off and on for decades, but we also talk about Laswell and about Lateef and about the whole idea of world music and fusion-as-creative-mindset that I've been discussing with every artist I've interviewed for the podcast this year. We talk a lot about the philosophy that goes into bringing together musicians from all sorts of traditions, from all over the globe, and finding ways to make their ideas flow together. That's what he does with Go! Organic Orchestra, the membership of which is completely open and the music of which is created through spontaneous conduction. So he was really the ideal person to talk about all this stuff with. I think you'll come away from this episode with a lot to think about. I know I did. And I hope you enjoy listening to it. All the music you'll hear, by the way, comes from Symphonic Tone Poem For Brother Yusef.
Ikiwa leo ni siku ya bahari duniani Umoja wa Mataifa unamchagiza kila mtu kuchukua hatua na kulinda mazingira ya bahari ambayo sio tu ni muajiri mkubwa wa sekta ya uvuvi duniani bali ni mdau mkubwa wa maendeleo ya kiuchumi na kupambana na athari za mabadiliko ya tabianchi. Kwa mujibu wa takwimu za Umoja wa Mataifa duniani kote thamani ya soko la sekta ya bahari na rasilimali zake inakadiriwa kuwa ni dola trilioni 3 kwa mwaka au asilimia 5 ya pato la dunia ndio maana unaichagiza dunia kushikama kuchukua hatua kuilinda bahari kwa maslahi ya kizazi cha sasa na kijacho. Mwandishi wetu wa Kenya Thelma Mwadzaya amekwenda Vanga Pwani ya Kenya katika bahari ya Hindi mpakani na Tanzania kuzungumza na wakazi wa eneo hilo je wanatambua umuhimu wa bahari? na nini wanafanya ili kuilinda, ungana naye katika makala hii.
Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres hivi karibuni akizungumza na Baraza la Usalama alitaka hatua zichukuliwe kukomesha vita alipokuwa akizungumzia namna ambavyo ni vita ni chachu kubwa ya njaa duniani kote. Vita ya hivi karibuni ambayo imeongeza chumvi katika jeraha ni kutokana na uvamizi wa Urusi kwa Ukraine ambao pamoja na madhara mengine kwa ulimwengu, imeathiri uzalishaji na usambazaji wa mafuta ambayo ni bidhaa mtambuka kwa mambo mengi na inapoyumba inayumbisha karibu mihimili yote ya uchumi. Abuu Maahiry Mmelekwa, Mwandishi wa redio washirika wetu Irangi FM ya wilayani Kondoa, mkoani Dodoma katikati mwa Tanzania amemuangazia mmoja wa wafanyabiashara wadogo katika makao makuu ya Tanzania, Dodoma ambaye ni miongoni mwa wanaolamba shubiri ya athari za vita kati ya Urusi na Ukraine ambavyo vimesababisha athari ya kiuchumi kote duniani.
Jaridani Jumatano Mei 18, 2022 na Leah Mushi -Joto laendelea kuongezeka duniani kwa mwaka wa 7 mfululizo: WMO -Mkutano wa kirafiki wakutanisha walinda amani kutoka Tanzania na baadhi ya viongozi viongozi mashariki mwa DRC -Katika makala tunaelekea nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC kuungana na Mwandishi wetu wa huko Byobe Malenga akiangazia matumizi ya mitandao ya kijamii miongoni mwa wakimbizi katika kambi ya Lusenda. -mashinani tutasikia kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani, WFP.
Takribani miaka miwili iliyopita, Umoja wa Mataifa ulizindua mkakati wake na ukapewa jina "iliyothibitishwa" au “Verified initiative” ambao unataka watu kote duniani kutafakari kabla ya kusambaza taarifa au maaudhi kwenye mitandao ya kijamii. Mitandao ya kijamii ni moja ya njia inayotumiwa na jamii sio tu kwa mawasiliano kwa wapendwa wao bali pia kupata taarifa muhimu sehemu mbalimbali na za muhimu katika maisha ya kila siku. Katika Kambi ya Lusenda jimboni Kivu ya kusini mashariki mwa jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, wakimbizi, hususani vijana wamekuwa wakitumia mitandao hiyo kama vile Facebook na WhatsApp lakini wanasema kuwa moja ya changamoto ni kuwa wakati mwingine kunakuwa na habari za uongo zinazozagaa katika mitandao hiyo. Mwandishi wetu wa DRC, Byobe Malenga ametembelea kambi hyio na kuzungumza na baadhi ya vijana kuhusu suala hilo.
Watu zaidi ya milioni 3 wameathirika vibaya na ukame nchini Kenya kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu masuala ya kibinadamu na misaada ya dharura OCHA huku eneo lililoathirika zaidi ni kaunti ya Turkana. Maelfu ya watu wanahaha kupata mlo, Watoto imekuwa changamoto kwenda shule na maji ambayo ni uhai imekuwa bidhaa adimu kupatikana, sasa watu hao wanaililia jumuiya ya kimataifa kunyoosha mkono kunusuru uhai na maisha yao. Mwandishi wetu wa Kenya Thelma Mwadzaya aliambatana na ziara ya mkuu wa OCHA Martin Griffith wiki hii kwenye kaunti hiyo kushuhudia hali halisi. Amezungumza na wakazi wa kaunti hiyo na kuandaa Makala hii.
Jaridani Alhamisi Mei 12, 2022 na Grace Kaneiya HABARI KWA UFUPI Mratibu mkuu wa Umoja wa Mataifa wa masauala ya kibinadamu na misaada ya dharura Martin Griffiths yuko ziarani nchi Kenya kwa lengo la kuitanabaisha jumuiya ya kimataifa janga la kibinadamu lililosababishwa na mabadiliko ya tabianchi katika Pembe ya Afrika, nchini Ethiopia, Somalia na Kenya. Zaidi ya watu milioni 15 hawana uhakika wa chakula kutokana na ukame mkali ambapo Kenya pekee watu milioni 3.5 wanakabiliwa na njaa huku viwango vya utapiamlo vikiongezeka mara mbili. Mwandishi wetu wa Kenya Thelma Mwadzaya amekuwa shuhuda wetu katika ziara hiyo iliyoanzia Lodwar jimbo la Turkana (TAARIFA YA THELMA) ===================== Wagonjwa wa COVID-19 wanaongezeka kwa wiki ya tatu mfululizo Kusini mwa Afrika wakati huu msimu wa baridi unapokaribia kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo na shirika la afya la Umoja wa Mataifa WHO. Shirika hilo linasema wagonjwa 46, 271 wamerekodiwa katika wiki iliyoishia tarehe 8 Mei 2022, ikiashiria ongezeko la asilimia 32% zaidi ya wiki iliyotangulia. Ongezeko hilo limechangiwa zaidi na idadi kubwa ya wagonjwa nchini Afrika Kusini ambapo visa vinavyorekodiwa kila wiki vimeongezeka mara nne katika wiki tatu zilizopita ingawa idadi ya vifo haijaongezeka sana. ================================ Na ikiwa leo ulimwengu unaadhimishwa kwa mara ya kwanza Siku ya Kimataifa ya Afya ya Mimea, IDPH, Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo, FAO, limesema mabadiliko ya tabianchi na shughuli za binadamu zinabadilisha mifumo ikolojia na kuharibu bayonuai huku hali hiyo ikiunda maeneo mapya kwa ajili ya wadudu waharibifu kustawi. Aidha FAO imeeleza kuwa usafiri wa kimataifa na biashara, ambavyo vimeongezeka mara tatu katika muongo uliopita vimechangia kueneza wadudu na magonjwa. Umoja wa Mataifa uliipitisha tarehe 12 Mei kila mwaka kuwa Siku ya Kimataifa ya Afya ya Mimea ili kuongeza uelewa wa kimataifa kuhusu jinsi kulinda afya ya mimea kunaweza kusaidia kutokomeza njaa, kupunguza umaskini, kulinda viumbe hai na mazingira na kukuza maendeleo ya kiuchumi na hivyo wito unatolewa kuchukua hatua za kuilinda mimea. MWISHO WA HABARI KWA UFUPI Katika mada kwa kina tunaangazia msanii wa uchoraji kutoka Tanzania. Kataika kujifunza neno la wiki linafafanuliwa neno mteremezi
Serikali nchini Tanzania imeshauriwa kuboresha Sekretarieti ya mfumo wa uombaji ajira kwa njia ya mtandao maarufu kama Ajira Portal ili uweze kuwatambua watu wenye ulemavu na hivyo kumiza matakwa ya sera ya ajira ambayo ina kipengele mahususi kinacholenga kuwajumuisha watu wenye ulemavu. Ushauri huo umetolewa na Shega Mboya wa Morogoro, Tanzania ambaye pamoja na kuwa na elimu ya juu ya digrii mbili, hajaweza kupata ajira ingawa anaamini pamoja na vigezo vingine ambavyo anaamini anavyo, laiti mfumo wa kidijitali ungeweza kutambua watu wenye ulemavu, ingekuwa rahisi kwake na kwa wengine. Hamad Rashid ni Mwandishi wa Habari wa Redio washirika Tanzania Kids time fm kutoka Morogoro amezungumza na msichana huyo na ameandaa makala ifuatayo.
Episode 73 of the Burning Ambulance podcast features an interview with pianist Cameron Graves.I have a single subject we're going to be exploring through all ten episodes that I'm going to be presenting this season, and that subject is fusion. Fusion means much more, I think, than just the music that most people probably think of when they hear the word. Of course, it immediately brings to mind bands from the 1970s like the Mahavishnu Orchestra, Return to Forever, and Weather Report: groups that were formed by ex-members of Miles Davis's band, playing extremely complex compositions that blurred the lines between progressive rock and jazz, while still leaving room for extended improvisation. But if you think of fusion as a process rather than a style, the discussion gets a lot more interesting. Because then you can pull in the music being made by Yes, King Crimson, Emerson, Lake & Palmer, Santana, etc., all of which gets filed under just plain rock. And you can talk about the music Latin artists like Eddie Palmieri, Ray Barretto, and the Fania All Stars were making at the same time. Or the really adventurous funk and R&B that was being made by Sly and the Family Stone, Parliament, Funkadelic, the Isley Brothers, Earth, Wind & Fire, the Ohio Players, Slave, which then leads you to jazz-funk names like George Duke, Billy Cobham, the Crusaders, Donald Byrd, Freddie Hubbard, Eddie Henderson, and of course Mwandishi and the Headhunters. This is how I prefer to think about fusion. It's not just a specific, narrow slice of music, it's the sound of walls being knocked down across the landscape.So that's the kind of philosophical starting point for all the interviews I'm doing this season, and that's what makes Cameron Graves such a perfect person to talk to. Because he's a guy who crosses all sorts of musical boundaries. He's had a lot of classical music training, as I learned during this conversation, he spent several years studying Indian music, and obviously he's got a deep jazz background starting out as a member of the Young Jazz Giants with Kamasi Washington and the Bruner brothers, Stephen aka Thundercat on bass and his brother Ronald on drums, which evolved into the West Coast Get Down and all the albums that they've made over the last half dozen years or so. But Cameron's also a lifelong metalhead — in fact, he played keyboards and guitar in Wicked Wisdom, the nu-metal band fronted by Jada Pinkett Smith in the early 2000s. So he's not only toured the world with Kamasi Washington and with Stanley Clarke, because he's a member of Clarke's band, too — he also played Ozzfest.And here's an interesting connection: the drummer for Wicked Wisdom was Philip “Fish” Fisher, the drummer for Fishbone. And when you talk about fusion as the kind of big-tent/umbrella sort of conceptual thing that I'm talking about, you have to include them in there. They mixed funk and hard rock and punk and metal and ska and reggae and jazz into one big swirl, particularly on their most ambitious album, 1991's The Reality of My Surroundings. There's all kinds of music on there, from Bad Brains-style hardcore to Last Poets-style abstract jazz poetry. And of course they were the best live band on the planet from the mid '80s to the early '90s.Fishbone were never as big as they deserved to be, but they were absolute heroes in L.A., and they were a huge inspiration to all kinds of open-minded musicians who came up in their wake. Last year, I interviewed Terrace Martin, who's an alto saxophonist affiliated with the West Coast Get Down but is also a hip-hop producer who's worked with Snoop Dogg for years — in fact, he put together a live band for Snoop in about 2010 that included Kamasi Washington, Thundercat, Ryan Porter, who's been on this podcast before, and other people from their circle as well. Anyway, when I talked to Martin, he expressed a lot of love for Fishbone. And he's now a member of Herbie Hancock's band, in addition to being part of R+R=NOW, a group that also includes Robert Glasper and Christian Scott. And Thundercat and his brother, Ronald Bruner Jr., were both members of Suicidal Tendencies, playing straight-up punk and thrash, for years. There are so many connections between jazz and funk and metal, when you look for them, and bands that combine them in various really fascinating ways. It's all fusion, in the broad sense.Another thing that's really interesting, to me anyway, is that there are so many direct connections between the West Coast Get Down guys and the Seventies fusion artists. Like I said, Cameron Graves is in Stanley Clarke's band. Terrace Martin is in Herbie Hancock's band. Ronald Bruner Jr. played with George Duke before Duke died. Thundercat covered a George Duke song on one of his albums, and had Steve Arrington from Slave on his most recent record. It really is like they're the next generation of fusion. And we talk about all this and a lot more in the interview you're about to hear. This was a really fun conversation that went in some very interesting directions, and I hope you enjoy listening to it.Music in this episode:Cameron Graves, “Planetary Prince” (from Planetary Prince)Cameron Graves, “The Life Carriers” (from Seven)Cameron Graves, “Red” (from Live From the Seven Spheres)
Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani, WHO linaeleza kuwa kutokana na uwepo wa ugonjwa wa COVID-19 pamoja na migogoro katika mataifa mbalimbali, kumekuwa na ongezeko la wagonjwa wa kifua kikuu, TB ikilinganishwa na miaka ya nyuma ambapo mapambano ddhidi ya ugonjwa huu yalikuwa yanaendelea vizuri. Kifua Kikuu ni ugonjwa hatari unaohitaji muda mrefu kutibu na unaweza kuwa sugu kwa dawa, lakini vile vile una kinga ambayo ni chanjo.. Thomas Oduor ni mkazi wa Nairobi ambaye aligundulika kuuugua kifua kikuu sugu mwaka 2020 na kutibiwa kwa mwaka mmoja na nusu. Na sasa miezi sita baada ya kukamilisha dozi ya dawa, afya yake inaendelea kuimarika. Mwandishi wetu wa Kenya Thelma Mwadzaya amezungumza naye.
Dr. Eddie Henderson is arguably one of the greatest trumpet players in jazz history. He has a storied career that lasts over 60 years, playing with Herbie Hancock's Mwandishi band, Pharoah Sanders, and Art Blakey among many others. Listen as he shares about personal relationships with Louis Armstrong, Miles Davis, Freddie Hubbard, Lee Morgan, and Woody Shaw, the difference between playing the trumpet and playing music, and what's helped him sustain a long career in the music business. Visit Eddie Henderson on Facebook: https://bit.ly/3ulPlnkVisit John Raymond: www.john-raymond.comMusic: “North” (IU Jazz Studies Faculty) + "Joy Ride" (John Raymond & Real Feels)Interview Edited by Tom PieciakProduced & Edited by John Raymond
Mbali na janga la Janga la Corona au COVID-19 ambalo limeikumba dunia kwa zaidi ya miaka miwili, wananchi wa Uganda waishio karibu na Ziwa Albert kwa miaka hiyo miwili wamekuwa wakikabiliwa na changamoto ya ziada ya mafuriko. Wanawake wanachama wa kikundi cha Kaizo Women's Group (KWG) wilayani Hoima ni moja wapo ya vikundi ambayo mipango yao ilikwamishwa na atahri za mafuriko na ambao sasa wanaomba msaada wa kifedha kutoka serikali katika juhudi zao za kujikwamua kutokana na uharibifu wa maji huku wakikabiliana na janga la COVID-19. Mwandishi wetu wa Uganda, John Kibego amefanya mahojiano na Ongyera Aness afisa wa ujasiriamali katika kikundi hicho.