Podcasts about kiswahili

Bantu language spoken mainly in East Africa

  • 155PODCASTS
  • 1,013EPISODES
  • 18mAVG DURATION
  • 5WEEKLY NEW EPISODES
  • Sep 11, 2025LATEST
kiswahili

POPULARITY

20172018201920202021202220232024


Best podcasts about kiswahili

Show all podcasts related to kiswahili

Latest podcast episodes about kiswahili

Habari za UN
11 SEPTEMBA 2025

Habari za UN

Play Episode Listen Later Sep 11, 2025 9:59


Katika Jarida la Habari za Umoja wa Mataifa leo Flora Nducha anakuletea-Utapiamlo kwa watoto katika Ukanda wa Gaza eneo la Palestina linalokaliwa kimabavu na Israel umefikia kiwango cha kutisha, huku takwimu mpya zikionesha ongezeko kubwa mwezi Agosti kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa-Umoja wa Mataifa umeanzisha mradi mpya wa miaka mitatu wenye lengo la kusaidia nchi za Afrika Mashariki kukabiliana na matumizi ya kigaidi ya vilipuzi. Kupitia mradi huu, Kenya, Somalia na Uganda zitasaidiwa-Hali nchini Haiti inaendelea kuzorota, sehemu kubwa ya nchi inadhibitiwa na magenge yenye silaha, nusu ya idadi ya watu wanakabiliwa na upungufu wa chakula, na idadi ya watu waliofurushwa  imefikia kiwango ambacho hakijawahi kushuhudiwa amesema Tom Fletshe mkuu wa OCHA-Mada kwa kina inatupeleka Uganda watumiaji wa Ziwa Albert wafunguka kuhusu changamoto za uvuvi haramu na faida za ziwa hilo-Na katika jifunze KIswahili leo mtaalam wetu Dkt Mwanahija Ali Juma, Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili, Zanzibar nchini Tanzania, BAKIZA anafafanua maana ya neno "UKWASI!

Habari za UN
09 SEPTEMBA 2025

Habari za UN

Play Episode Listen Later Sep 9, 2025 9:58


-Katika Jarida la Habari la Umoja wa Mataifa hii leo Flora Nducha anakuletea UNGA79yafikia tamati hii leo na kupisha UNGA80  chini ya uongozi wa Rais mpya Annalena Baerbock-Ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa iliyozinduliwa leo imesema matumizi ya kijeshi duniani yalifikia dola trilioni 2.7 mwaka 2024, yakiwa yameongezeka kwa zaidi ya asilimia 9 kutoka mwaka 2023-Mratibu wa Misaada ya Dharura wa Umoja wa Mataifa Tom Fletcher ametangaza leo  dola milioni 1 za kimarekani kutoka  Mfuko wa Dharura wa Umoja wa Mataifa CERF ili kudhibiti mlipuko wa kipindupindu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC. -Mada kwa kina inatupeka Pemba Kaskazini kisiwani Zanzibar nchini Tanzania kuangazia mradi wa FAo wa ZJP unavobadili maisha ya wakulima wa ndiziNa katika jifunze Kiswahili utamsikia mlumbi Jorum Nkumbi kutoka Tanzania akifafanua maana ya neno LISANI

Habari za UN
Wanavyosema wadau kuhusu Siku ya kujua kusoma na kuandika katika zama za kidijitali

Habari za UN

Play Episode Listen Later Sep 8, 2025 2:31


Ikiwa leo tarehe 8 Septemba ni siku ya Kimataifa ya kujua kusoma na kuandika ambapo Umoja wa Mataifa ulianzisha siku hii ili kuwakumbusha watunga sera, walimu, wadau wa elimu, na jamii juu ya umuhimu wa ujuzi wa kusoma na kuandika katika kujenga jamii yenye elimu, haki, amani na endelevu,  Sabrina Saidi wa Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa anaiangazia kauli mbiu ya mwaka huu  "Kukuza ujuzi wa kusoma na kuandika katika zama za kidijitali" akiwashirikisha baadhi ya wadau wa elimu nchini Tanzania.Amezungumza na baadhi ya wadau kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino, SAUT kilichoko jijini Mwanza, kaskazini-magharibi mwa Tanzania.Dismas Nziku ni mwalimu wa masomo ya Biashara na Ujasiriamali  anazungumza kuhusu ni kwa jinsi gani ufundishaji wa zama hizi za kidijitali unavyochochea na kukuza ujuzi wa kusoma na kuandika. "Kwenye dunia ya sasa ujuzi wa kusoma na kuandika kidijitali ni msingi mkubwa kwa mwanafunzi, na miongoni mwa juzi hizi muhimu ni kama vile kujua kutumia vifaa vya kidijitali kama kompyuta, simu janja kwa ajili ya kujisomea na kutafuta maarifa, lakini pia kama mwalimu ninawafundisha wanafunzi kwa njia ya vitendo,kuandaa maswali ya utafiti kwa kutumia internet,kufanya kazi na kufanya kazi ya kikundi mitandaoni."Kuhusu umuhimu wa siku hii kwake na inachangia vipi katika kukuza uelewa wa umuhimu wa kusoma na kuandika shuleni na katika jamii Mwalimu Nziku amesema, "Siku ya Kimataifa ya kujua kusoma na kuandika ni kumbusho muhimu kwamba elimu ni haki ya msingi, na ni msingi wa maendeleo kwa kila mmoja kujua kusoma na kuandika hasa hasa kidijitali, inanipa hamasa kama mwalimu kuendelea kuwajengea wanafunzi ujuzi wa kusoma na kuandika si kwa ajili ya mitihani tu, bali kwa maisha yao ya kila siku."Didas Karoli ni mwanafunzi katika chuo hicho cha SAUT akisoma shahada ya kwanza ya Mawasiliano kwa Umma, ameeleza kuhusu siku hii na jinsi maendeleo ya kidijitali yanavyochagiza katika kujifunza kwake akisema "Zana za kidijitali zimebadilisha sana upeo wangu katika suala la kujifunza,kutokana na zamani nilikuwa nategemea vitabu lakini hivi sasa natumia tu smartphone au kompyuta na kutengeneza notisi zangu mwenyewe za kujifunzia.Siku ya hii ya kujua kusoma na kuandika ni siku ambayo ni muhimu inafanya watu waweze kujua umuhimu wa kusoma na kuandika."

Habari za UN
Jifunze KIswahili: Maana ya methali "MASIKINI HANA MIIKO"

Habari za UN

Play Episode Listen Later Sep 4, 2025 0:43


Leo katika jifinze Kiswahili mchambuzi wetu ni Dkt. Josephat Gitonga,  ambaye ni Mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi nchini Kenya,  kwenye kitivo cha Tafsiri na Ukalimani anafafanua maana ya methali "MASIKINI HANA MIIKO"

Habari za UN
02 SEPTEMBA 2025

Habari za UN

Play Episode Listen Later Sep 2, 2025 10:53


Jaridani leo tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini Tanzania kufuatilia mradi wa FAO Mjini Morogoro, uliokutanisha viongozi wa Serikali kutoka katika Taasisi zinazojihusisha na udhibiti na usalama wa chakula. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na jifunze Kiswahili.zaidi ya watu bilioni moja duniani wanaishi na changamoto za afya ya akili kama vile msongo wa mawazo na mfadhaiko, kwa mujibu wa takwimu mpya zilizotolewa leo na Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa Duniani WHO. Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo Dkt. Tedros Adhanom Ghebreyesus amesema nchi wanachama zinapaswa kushughulikia tatizo hilo kwa “Kuwekeza katika afya ya akili, kwani kuwekeza kwa watu, jamii na uchumi ni uwekezaji ambao hakuna nchi inayoweza kuupuuzia.”Umoja wa Mataifa umetuma salamu za rambirambi na pole kwa wananchi wa sudan kufuatia maporomoko ya udongo yaliyosababishwa na mvua mkubwa iliyonyesha kwa siku kadhaa ambayo imesababisha maafa katika kijiji cha Tarsin huko Jebel Marra nchini Sudan mwishoni mwa wiki.Nchini Afghanistan ambako idadi ya vifo inaendelea kuongezeka kufuatia tetemeko la ardhi lililotokea juzi jumapili, wafanyakazi wa misaada ya Kibinadamu wa Umoja wa Mataifa wanafanya kila juhudi kuhakikisha wanafikisha misaada kwa waathirika. Akizungumza na waandishi wa habari kutokea Kabul Afghanistan Indrika Ratwatte ambaye ni mwakilishi wa UN nchini humo amesema “Sio rahisi kufika maeneo yaliyoathirika kitu ambacho kinawafanya majeruhi waendelee kufungiwa.” Ametaja juhudi za haraka zinazofanyika ni pamoja na kuzika miili ya waathirika na kufukia mifugo ili kuzuia magonjwa ya milipuko ambayo yanaweza kusambaa kwa haraka.”.Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili hii leo, mtaalam wetu Onni Sigalla, Mhariri mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania, BAKITA. Anafafanua tofauti ya "URAIBU NA HITARI”.Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!

Habari za UN
Jifunze Kiswahili: Tofauti ya maneno "URAIBU NA HITARI”.

Habari za UN

Play Episode Listen Later Sep 2, 2025 1:03


Katika kujifunza lugha ya Kiswahili hii leo,  mtaalam wetu Onni Sigalla, Mhariri mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania, BAKITA. Anafafanua tofauti ya "URAIBU NA HITARI”.

Habari za UN
28 AGOSTI 2025

Habari za UN

Play Episode Listen Later Aug 28, 2025 9:59


Jaridani leo tunakuletea mada kwa kina, wiki ya Maji ikifikia tamati leo Agosti 28 na maudhui yakiwa Maji kwa ajili ya Hatua kwa Tabianchi, tunabisha hodi kaunti ya Kajiado nchini Kenya kumsikia mtendaji kwenye mradi wa maji wa Kerarapon Water Association  ambalo ni shirika la kijamii linalohusika na maji na mazingira huko kaunti ya Kajiado nchini Kenya. Mengine ni kama yafuatayo.Ukraine ambapo leo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres ameungama na mashirika mengine ya Umoja wa Mataifa kulaani vikali mashambulizi ya makombora na ndege zisizo na rubani droni yaliyofanywa na Urusi usiku kucha kuamkila dhidi ya miji ya Ukraine na kusababisha vifo na majeruhi kwa raia, wakiwemo watoto, na pia kuharibu majengo ya kidiplomasia jijini Kyiv. Amesisitiza kuwa mashambulizi dhidi ya raia na miundombinu yao yanakiuka sheria za kimataifa za kibinadamu, akitaka yakome mara moja na kurudia wito wake wa kusitisha mapigano ili kuelekea amani ya kudumu itakayoheshimu uhuru wa watu, uhuru wa kitaifa na mipaka ya Ukraine kama inavyotambuliwa kimataifa.Kuhusu Mashariki ya Kati Katibu Mkuu António Guterres akizungumza na waandishi wa Habari hii leo kwenye Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa      ameonya kuwa operesheni za kijeshi mjini Gaza zitakuwa na zahma kubwa na amesisitiza “hili lazima likome.” Amesema njaa si tishio tena bali janga la sasa, huku raia, wahudumu wa afya na waandishi wa habari wakiuawa  wakati “macho ya dunia yakitazama.” Guterres ameikumbusha Israel wajibu wake wa kisheria kulinda raia na kuruhusu msaada wa kibinadamu bila vikwazo akisema “Hakuna visingizio tena. Hakuna vizuizi tena. Hakuna uongo tena,”  akitoa wito wa usitishaji mapigano haraka na kuachiliwa kwa mateka wote.Kikosi cha 11 cha Tanzania TANZBATT 11 kinachohudumu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC chini ya mpango wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani MONUSCO kimetoa msaada wa magodoro kwa raia walioathirika na machafuko ya karibuni katika kijiji Oicha  jimboni Kivu Kaskazini. Miongoni mwao ni Bi Masika Jistine na Mzee Bahati Paluku ambao hawakusita kuonesha furaha yao.Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili na hii leo Dkt Mwanahija Ali Juma, Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili, Zanzibar nchini Tanzania, BAKIZA anafafanua maana ya neno "MKWIJI!.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!

Habari za UN
Jifunze Kiswahili: Maana ya neno "MKWIJI!.

Habari za UN

Play Episode Listen Later Aug 28, 2025 1:01


Katika kujifunza lugha ya Kiswahili na hii leo Dkt. Mwanahija Ali Juma, Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili, Zanzibar nchini Tanzania, BAKIZA anafafanua maana ya neno "MKWIJI! 

Morning Majlis
The Perfect Way to Learn a New Language (21/08/25)

Morning Majlis

Play Episode Listen Later Aug 21, 2025 17:32


Want to develop your linguistic skills? Dr Bilal Al-Omar, Senior Lecturer of Arabic at The Africa Institute, explains this exciting programme on offer that can allow you to learn Arabic, Kiswahili, Hausa, and Amharic, within just 12 weeks. This affordable programme offers a modernised way of teaching, that can be accessible online as well. #AfricanLanguages #LanguageLearning #LearnArabic #LearnHausa #LearnKiswahili #LearnAmharic #Sharjah #TheAfricaInstitute Listen to #Pulse95Radio in the UAE by tuning in on your radio (95.00 FM) or online on our website: www.pulse95radio.com ************************ Follow us on Social. www.facebook.com/pulse95radio www.twitter.com/pulse95radio

Habari za UN
Ukatili wa kijinsia katika mizozo

Habari za UN

Play Episode Listen Later Aug 20, 2025 3:20


Msikilizaji wa Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa leo tunakuletea makala yenye kugusa maisha ya maelfu ya watu kote duniani, ukatili wa kingono katika maeneo yenye mizozo. Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa tarehe 19 Agosti limekutana jijini New York Marekani kujadili hali hii inayozidi kuongezeka, na kushuhudia jinsi waathirika wanavyobaki bila msaada wa kutosha kutokana na ukosefu wa rasilimali.Ripoti ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa iliyowasilishwa na Mwakilishi wake imeonesha ongezeko kubwa la kesi za ukatili wa kingono, jambo linaloibua maswali makubwa kuhusu uwajibikaji na huduma kwa manusura. Leah Mushi ametuandalia makala ifuatayo ikieleza hayo kwa kina.

Habari za UN
Jifunze Kiswahili: Maana ya neno “MAHAZAMU”

Habari za UN

Play Episode Listen Later Aug 14, 2025 1:09


Katika kujifunza lugha ya Kiswahili hii leo, fursa ni yake mtaalam wetu Onni Sigalla, Mhariri mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania, BAKITA. Anafafanua maana ya neno “MAHAZAMU”. 

Kiswahili, Lugha Ya Afrika
AI, AGI na ASI zinamaanisha nini?

Kiswahili, Lugha Ya Afrika

Play Episode Listen Later Aug 9, 2025 8:22


Katika makala haya ya kipekee, tunafichua siri kuhusu Akili Bandia—kuanzia AI ya kawaida, hadi AGI (Artificial General Intelligence), na hatimaye ASI (Artificial Super Intelligence)!Tunakufafanulia kwa Kiswahili sanifu na kwa lugha rahisi:✅ AI ni nini na kwa nini iko kila mahali sasa?✅ AGI inatishia kazi zako—ina uwezo sawa na binadamu!✅ ASI ni hatua ya hatari sana—inaweza kuwa mwisho au mwanzo mpya kwa wanadamu.✅ Faida na hasara za kila hatua ya maendeleo ya akili unde.✅ Hatua za kuchukua ili kulinda jamii kutokana na madhara ya AI.

Habari za UN
07 AGOSTI 2025

Habari za UN

Play Episode Listen Later Aug 7, 2025 10:51


Jaridani leo tunaangazia mada kwa kina inayokupeleka katika Hospitali hiyo kusikia wanavyolitekeleza suala la unyonyeshaji hasa kuwaelimisha akina mama wenye hofu ya kunyonyesha kutokana na changamoto zao nyingine za kiafya. Mengine ni kama yafuatayo.Ushahidi unaonesha kuwa unyanyasaji bado ni jambo la kawaida katika huduma kwa wajawazito na watoto wachanga, limesema shirika la Umoja wa Mataifa la Afya duniani, (WHO) hii leo. Mathalani katika nchi nne, utafiti umebaini kuwa zaidi ya asilimia 40 ya wajawazito walikumbana      na kauli chafu wakati wa kujifungua ili hali zaidi ya asilimia 60 walifanyiwa uchunguzi sehemu zao za siri bila idhini yao.Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa nchi zisizo na bandari za baharini, LLDCs ukiendelea huko Awaza, Turkmenistan, shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo, UNDP limetaka kubadilika kwa fikra ya kwamba nchi hizo kama vile Rwanda na Uganda zina mkwamo wa kibiashara na maendeleo. Mwakilishi wa UNDP nchini Ethiopia Dkt. Samuel Doe akizindua mpango mpya wa kuonesha faida za nchi hizo kwa muunganiko wao kwa njia ya ardhi amesema…. hii leo LLDCs zinatumia vema uwepo wao kimkakati, katikati ya Afrika  na muunganiko wa kikanda kuwa vitovu muhimu vya kuunganisha nchi kiuchumi , biashara na ubunifu. Wataalamu wa Umoja wa Mataifa wa haki za binadamu leo wamesema ili kuzuia vifo zaidi na mateso kutokana na njaa huko Gaza, Israel inapaswa kurejesha mara moja ruhusa kwa mashirika ya Umoja wa Mataifa ya kibinadamu kuingia bila vikwazo vyovyote eneo la Palestina inalokalia kimabavu.Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili, leo mchambuzi wetu ni Dkt. Josephat Gitonga,  ambaye ni Mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi nchini Kenya, kwenye kitivo cha Tafsiri na Ukalimani anafafanua maana ya methali "SAMAKI WOTE HUNUKA, WALIMSHUKU KAMBALE."Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!

Habari za UN
Jifunze Kiswahili: Maana ya methali "SAMAKI WOTE HUNUKA, WALIMSHUKU KAMBALE."

Habari za UN

Play Episode Listen Later Aug 7, 2025 1:16


Katika kujifunza lugha ya Kiswahili, leo mchambuzi wetu ni Dkt. Josephat Gitonga,  ambaye ni Mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi nchini Kenya, kwenye kitivo cha Tafsiri na Ukalimani anafafanua maana ya methali "SAMAKI WOTE HUNUKA, WALIMSHUKU KAMBALE." 

Habari za UN
31 JULAI 2025

Habari za UN

Play Episode Listen Later Jul 31, 2025 9:56


Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayoturesha katika Jukwaa la Vijana la Baraza la Umoja wa Mataifa la Masuala ya Kiuchumi na Kijamii (ECOSOC) lilifanyika katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani mwezi Aprili mwaka huu wa 2025, ambapo Idhaa hii ilizungumza na Kapwani Kavenuke, kutoka Tanzania kuhusu ujumuishwaji wa vijana katika será za maendeleo.Nchini Somalia ziara ya siku nne ya Naibu Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji IOM Ugochi Daniels imeonesha namna taifa hilo lilivyoathirika vibaya na mabadiliko ya tabianchi hali inayofanya baadhi ya watu kukimbilia maeneo yenye rasilimali chache na hivyo kujikuta wakigombania rasilimali hizo.Huko Gaza mashariki ya kati, eneo la Wapalestina linalokaliwa kimabavu na Israel bado hali si hali kwani njaa ni Kali. Wakati malori ya misaada yakiendelea kuingiza chakula, mafuta na vifaa vya matibabu, mfanyakazi mmoja wa Umoja wa Mataifa anasimulia kumuona baba mmoja wa makamo akiwa amepiga magoti chini akiokota kwa mikono yake na kuweka kwenye fulana yake dengu zilizokuwa zimeanguka kutoka kwenye moja ya malori yanayoingiza chakula Gaza, hii ndio hali halisi. Umoja wa Mataifa umelaani shambulio lililotekelezwa hii leo na majeshi ya Urusi katika mji mkuu wa Ukraine, Kyiv na kusababisha vifo vya watu kadhaa akiwemo mtoto mwenye umri  wa miaka sita huku watu wengine kadhaa wakijeruhiwa..Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili. Onni Sigalla, Mhariri Mwandamizi kutoka Baraza la Kiswahili Tanzania, BAKITA anafafanua maana ya neno MTAGARUKI.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!

Habari za UN
Jifunze Kiswahili: Maana ya neno MTAGARUKI

Habari za UN

Play Episode Listen Later Jul 31, 2025 0:55


Katika kujifunza lugha ya Kiswahili. Onni Sigalla, Mhariri Mwandamizi kutoka Baraza la Kiswahili Tanzania, BAKITA anafafanua maana ya neno MTAGARUKI.

Habari za UN
24 JULAI 2025

Habari za UN

Play Episode Listen Later Jul 24, 2025 12:16


Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayomulika utapiamlo kwa watoto na madhila yasiyo fikirika  kwa wananchi wa kawaida huko Mashariki ya Kati, Ukanda wa Gaza eneo la Palestina linalokaliwa kimabavu na Israeli. Pata pia muhtasari wa habari na jifunze Kiswahili.Ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa imeweka bayana jinsi mitandao ya kihalifu duniani inavyoingiza kwenye masoko dawa za binadamu zenye viwango vya juu vya kemikali za sumu ambazo zimesababisha vifo na kuathiri afya ya wagonjwa wengi hasa watoto kwenye nchi za kipato cha chini.Tunasalia na afya ambapo hii leo WHO imethibitisha kwamba Timor-Leste imetokomeza ugonjwa wa malaria, hatua ya kipekee kwa nchi ambayo ilipatia kipaumbele malaria na kuanzisha juhudi za kitaifa na zilizoratibiwa mara tu baada ya kupata uhuru wake mwaka 2002. Mkuu wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Binadamu Volker Türk, amesema maoni ya ushauri yaliyotolewa na Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) kuhusu wajibu wa Mataifa kuhusiana na mabadiliko ya tabianchi ni ushindi mkubwa kwa wote wanaopigania kulinda hali salama ya tabianchi na sayari kwa ajili ya binadamu wote. Halikadhalika ni uthibitisho usio na shaka kuhusu madhara mapana ya mabadiliko ya tabianchi na wajibu mkubwa wa Mataifa, chini ya sheria za haki za binadamu na zaidi ya hapo, kuchukua hatua za haraka ili kuzuia uharibifu.Na katika kujifunza Kiswahili, leo mchambuzi wetu ni Dkt. Josephat Gitonga, kutoka Kenya ambaye ni mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi kwenye kitivo cha tafsiri na ukalimani anatufafanulia maana ya methali "UKIONA KIVULI CHA MTU MFUPI KIMEANZA KUREFUKA JUA KUMEKUCHA AU NI MACHWEO."Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!

Habari za UN
Methali: "Ukiona kivuli cha mtu mfupi kimeanza kurefuka jua kumekucha au ni machweo"

Habari za UN

Play Episode Listen Later Jul 24, 2025 1:09


Katika kujifunza lugha ya Kiswahili, leo mchambuzi wetu ni Dkt. Josephat Gitonga, kutoka Kenya ambaye ni mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi kwenye kitivo cha tafsiri na ukalimani anatufafanulia maana ya methali "UKIONA KIVULI CHA MTU MFUPI KIMEANZA KUREFUKA JUA KUMEKUCHA AU NI MACHWEO."

Habari za UN
17 JULAI 2025

Habari za UN

Play Episode Listen Later Jul 17, 2025 11:05


Jaridani leo tunakuletea mada kwa kina inayoangazia Afrika Mashariki Fest ya nchini Uganda kwa kushirikiana na serikali ya Tanzania na Uganda inayotumia  kampeni yake ya “Twende Zetu Butiama” ili kuyatumimiza malengo hayo.Hii leo shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Ulimwenguni, WHO katika eneo la Palestina linalokaliwa kimabavu na Israeli limeongoza uhamishaji wa wagonjwa 35, wengi wao watoto kwenda Jordan, kwa ajili ya matibabu zaidi kutokana na huduma za afya kuvurugwa Gaza. WHO inasema zaidi ya watu 10,000 Gaza wanahitaji kuhamishiwa nchi nyingine kwa ajili ya matibabu.Harakati za kusaka amani ya kudumua nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC zinazidi kushamiri ambapo hatua za hivi karibuni ni kutoka Muungano wa Afrika, (AU) zikiongozwa na marais wa zamani, Sahle Work Zewde wa Ethiopia, na Catherine Samba-Panza wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, (CAR).kuelekea mkutano wa 30 wa nchi wanachama wa Mkataba wa mabadiliko ya tabianchi, COP30 huko Brazil baadaye mwaka huu, huko Nairobi, nchini Kenya bara la Afrika linajipanga kuhakikisha mkutano huo unakuwa na tija. Dkt. Richard Muyungi, Mwenyekiti wa Kamati ya Wataalamu na mabalozi wanaoshughulikia masuala ya tabianchi barani Afrika, anasema wanachokitaka.Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili hii leo Dkt. Mwanahija Ali Juma, Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili, Zanzibar nchini Tanzania, BAKIZA anafafanua maana ya neno "KIKWANYUKWANYU!.Mwenyeji wako ni Leah Moshi, karibu!

Habari za UN
Jifunze Kiswahili: maana ya neno "KIKWANYUKWANYU"

Habari za UN

Play Episode Listen Later Jul 17, 2025 0:43


Katika kujifunza lugha ya Kiswahili hii leo Dkt. Mwanahija Ali Juma, Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili, Zanzibar nchini Tanzania, BAKIZA anafafanua maana ya neno "KIKWANYUKWANYU!.

Habari za UN
16 JULAI 2025

Habari za UN

Play Episode Listen Later Jul 16, 2025 10:59


Hii leo jaridani tunaangazia wakazi wa Gaza walioko eneo la Palestina linalokaliwa kimabavu na Israeli; na ujumbe wa Uganda wa hatua zake katika kulitekeleza lengo namba 5 la Usawa wa Kijinsia. Makala tunasalia hapa makao makuu na mashinani tunakwenda Tanzania, kulinkoni?Amri mpya za kuhama zinazotolewa na jeshi la Israeli kwa wakazi wa Gaza walioko eneo la Palestina linalokaliwa kimabavu na Israeli zinazidi kuhatarisha maisha ya makumi ya maelfu ya watu ambao wameshahama mara kadhaa, wakiwemo wagonjwa wanaotakiwa kupata huduma za kusafisha damu mwilini kila wiki.Jukwaa la Kisiasa la Ngazi ya Juu la Umoja wa Mataifa kuhusu Maendeleo Endelevu, HLPF, la mwaka huu wa 2025 linaendelea hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani. Wadau mbalimbali zikiwemo nchi zinazohudhuria zinabadilishana uzoefu, changamoto na mafaniko katika kutekeleza Malengo ya Umoja wa Mataifa ya Mendeleo Endelevu, SDGs. Uganda imeeleza hatua zake katika kulitekeleza lengo namba 5 la Usawa wa Kijinsia.Makala tunasalia hapa New York, Marekani, ambako Sharon Jebichii wa idhaa hii ya Kiswahili amezungumza na kijana kutoka Tanzania anayeshiriki mafunzo kwa vitendo kwenye Idara ya hapa Umoja wa Mataifa ya Masuala ya Kiuchumi na Kijamii, UNDESA. Anasimulia safari yake ya mafunzo kwa vitendo, changamoto, mafanikio na ushauri kwa vijana wengine wanaotamani kufuata nyayo zake.Na katika mashinani Edtrudith Lukanga Mkurugenzi wa Mradi wa Usimamizi wa Mazingira na Maendeleo kwenye Ziwa Victoria, EMEDO. Akishiriki kwenye mkutano hapa New York, MArekani wa kusongesha majawabu bunifu yenye ushahidi ili kuzuia watu kuzama majini, ametaja moja ya majawabu hayo ambayo ni Programu ya Shule ya Usalama kwenye maji huko Tanzania.Mwenyeji wako ni Leah Moshi, karibu!

Habari za UN
Jifunze Kiswahili: maana ya maneno "CHARAKAMU na BARAKALA"

Habari za UN

Play Episode Listen Later Jul 10, 2025 0:50


Katika kujifunza lugha ya Kiswahili hii leo mchambuzi wetu mlumbi wa Kiswahili Joramu Nkumbi kutoka nchini Tanzania, anafafanua maana ya maneno "CHARAKAMU na BARAKALA

Habari za UN
10 JULAI 2025

Habari za UN

Play Episode Listen Later Jul 10, 2025 10:36


Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini Tanzania kushuhudia mafunzo ya ukufunzi kwa wanadhimu wa Umoja wa Mataifa. Pia tunakuletea muhtasari wa habari zikiwemo za mkataba wa amani DRC na Rwanda, UKIMWI, na maadhimisho ya Siku ya kimataifa ya Kiswahili, na uchambuzi wa neno.Wajumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wamekaribisha mkataba wa amani kati ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC na Rwanda uliotiwa saini tarehe 27 mwezi uliopita wa Juni, huku wakishukuru Marekani, Qatar na Muungano wa Afrika kwa juhudi za usuluhishi.Ukata uliosababishwa na wahisani kukata au kupunguza ghafla na kwa kiasi kikubwa ufadhili kwenye miradi ya kupambana na UKIMWI umekuwa na madhara kwa nchi zilizoathiriwa vibaya na ugonjwa huo, imesema ripoti mpya ya shirika la Umoja wa Mataifa la kukabiliana na Ukimwi, UNAIDS.Leo kwenye Ofisi za Umoja wa Mataifa jijini Nairobi, Kenya kumefanyika maadhimisho ya siku ya kimataifa ya lugha ya Kiswahili ambapo wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Juu ya Mangu wametuma ujumbe wao wa umuhimu wa lugha hiyo kupitia ngonjera.Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili na hii leo mchambuzi wetu mlumbi wa Kiswahili Joramu Nkumbi kutoka nchini Tanzania, anafafanua maana ya maneno "CHARAKAMU na BARAKALA!Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!

Habari za UN
07 JULY 2025

Habari za UN

Play Episode Listen Later Jul 7, 2025 10:00


Hii leo jaridani tunaangazia mafuriko katika Jimbo la Texas, Marekani, na shairi linaloenzi siku ya Kiswahili Duniani. Makala inamulika haki za watu wenye ulemavu hususani wanawake, na mashinani tunakwenda Osaka nchini Japani kunakofanyika maonesho au EXPO2025, kulikoni?Umoja wa Mataifa umeonesha mshikamano mkubwa na watu wa Jimbo la Texas, Marekani serikali kufuatia mafuriko makubwa yaliyotokea Ijumaa na kusababisha vifo hasa vya watoto na uharibifu mwingine mkubwa.Kuelekea siku ya Kiswahili duniani hapo Julai 7 mwaka huu ikibeba maudhui “Kiswahili: zama zilizopita, sasa na zijazo” kwa lengo la kutathimini ukuaji na mabadiliko katika ligha hiyo adhimu leo tunakupeka Nairobi Kenya kwenye mpango wa kujitolea wa Umoja wa Mataifa UNV apmbapo mmoja wa wafanyakazi wa mpango huo mghani wa mashairi Jescah Muyia ameamua kuienzi lugha hiyo kwa shairi murua.Makala inaturejesha Zanzibar Tanzania katika sehemu ya mwisho ya mahojiano baina Flora Nducha wa Idhaa hii na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Bi. Abeida Rashid Abdallah kuhusu ujumuishwaji wa watu wenye ulemavu ungana nao.Na katika mashinani, kuanzia Aprili 13 hadi Oktoba 2025 huko Osaka nchini Japani kunafanyika maonesho au EXPO2025 ikileta nchi na mashirika ya Umoja wa Mataifa maudhui yakiwa Kuumba Jamii za siku zijazo kwa maisha yetu. Banda la Umoja wa Mataifa limedadavua maudhui hayo na kuwa kujikita kwenye Kuungana kwa Mustakabali Bora washiriki wakionesha masuala tofauti tofauti ikiwemo onesho la picha likisimamiwa na mpiga picha kutoka Ufaransa. Mhusika anafafanua.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!

Habari za UN
Kiswahili kitukuzwe shairi - Jescah Muyia UNV

Habari za UN

Play Episode Listen Later Jul 7, 2025 1:48


Kuelekea siku ya Kiswahili duniani hapo Julai 7 mwaka huu ikibeba maudhui “Kiswahili: zama zilizopita, sasa na zijazo” kwa lengo la kutathimini ukuaji na mabadiliko katika ligha hiyo adhimu leo tunakupeka Nairobi Kenya kwenye mpango wa kujitolea wa Umoja wa Mataifa UNV apmbapo mmoja wa wafanyakazi wa mpango huo mghani wa mashairi Jescah Muyia ameamua kuienzi lugha hiyo kwa shairi murua.

Habari za UN
Jifunze Kiswahili: Maana ya neno KUTOHOA

Habari za UN

Play Episode Listen Later Jul 3, 2025 1:16


Katika kujifunza lugha ya Kiswahili leo mchabuzi wetu Onni Sigalla, Mhariri Mwandamizi kutoka Baraza la Kiswahili la Taifa, BAKITA nchini Tanzania, anachambua neno KUTOHOA.

Habari za UN
03 JULAI 2025

Habari za UN

Play Episode Listen Later Jul 3, 2025 9:58


Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayokupeleka nchini Uganda katika Mbuga ya Wanyama inayofahamika kwa jina Murchison Falls National Park kuangazia namna washiriki wa Kongamano la kimataifa la lugha ya Kiswahili lililofanyika mapema mwaka huu jijini Kampala walivyofurahia mazigira asili nchini Uganda na namna yanavyounufaisha ulimwengu.Mkutano wa 4 wa ufadhili kwa maendeleo umemalizika leo huko Sevilla, Hispania ambapo mashirika ya kiraia yametaka utekelezaji kwa vitendo kwa yale yaliyomo katika nyaraka iliyopitishwa iliyopatiwa jina Makubaliano ya Sevilla.Mmoja wa wawakilishi wa mashirika ya kiraia, Paula Sevilla amesema kinachohitajika ni uongozi kutoka nchi tajiri ambako ndiko zilizko kampuni kubwa zinazokwepa kodi.Ripoti mpya iliyotolewa leo na shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo, FAO kuhusu vijana na mifumo ya uzalishaij chakula na kilimo inaonesha kuwa karibu asilimia 85 ya vijana duniani wanaishi katika nchi za kipato cha chini na cha kati, ambako mifumo hiyo ni muhimu kwa ajira na maisha yao. Ripoti inasema kuwajumuisha vyema vijana katika mifumo hiyo kunaweza kuleta mchango wa hadi trilioni moja ya dola kwa uchumi wa dunia..Na mwezi uliopita wa Juni umeshuhudia ongezeko kubwa la familia za raia wa Afghanistan zikirejeshwa nyumbani kutoka Iran, tofauti na awali ambapo waliokuwa wakirejeshwa walikuwa ni wanaume peke yao.Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili leo mchabuzi wetu Onni Sigalla, Mhariri Mwandamizi kutoka Baraza la Kiswahili la Taifa, BAKITA nchini Tanzania, anachambua neno KUTOHOA.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!

Bring It On! – WFHB
Bring It On! – June 30, 2025: World Kiswahili Language Day – July 7

Bring It On! – WFHB

Play Episode Listen Later Jun 30, 2025 59:00


In today’s edition of Bring It On!, hosts Clarence Boone and Liz Mitchell spend the hour with Dr. Alwiya Saleh Omar and Dr. Ng’uono Okelo to discuss World Kiswahili Language Day. Both Dr. Omar and Dr. Ng'uono are affiliated with the African Studies Program and the National African Language Resource Center at Indiana University’s Hamilton …

Habari za UN
26 JUNI 2025

Habari za UN

Play Episode Listen Later Jun 26, 2025 10:13


Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini Tanzania, ambako mshikamano na wakimbizi unatekelezwa kwa vitendo na mashirika ya Umoja Mataifa likiwemo lile la Chakula na Kilimo (FAO) na la kuhudumia wakimbizi, UNHCR kupitia Programu wa Pamoja ya Kigoma (KJP).Katika siku ya kimataifa ya kupambana na dawa za kulevya na usafirishaji haramu, ripoti mpya ya dunia ya Dawa za Kulevya mwaka 2025 iliyotolewa leo imeonya kuwa kutokuwepo kwa utulivu duniani kunachochea ongezeko la matumizi ya dawa za kulevya na uhalifu wa kupangwa. Kwa mujibu wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Dawa na Uhalifu UNODC, watu milioni 316 walitumia mihadarati mwaka 2023. Mkurugenzi Mtendaji wa UNODC, Ghada Waly, amesema "Makundi haramu yanatumia migogoro kama fursa tunahitaji ushirikiano na uwekezaji kulinda jamii zetu.”Leo ni kumbukizi ya uzinduzi wa Chata ya Umoja wa Mataifa miaka 80 iliyopita mjini San Francisco, hatua iliyoweka msingi wa kuundwa kwa Umoja wa Mataifa mnamo Oktoba 24, 1945. Katibu Mkuu António Guterres anasema Umoja wa Mataifa bado unaakisi matumaini yaliyozaliwa kutoka kwenye majivu ya vita naye mwanahistoria Stephen Schlesinger akizungumza na UN News ameakumbusha kuwa “Chata hii ilikuwa kilio cha wanadamu wakitafuta amani, suluhu za mazungumzo, na maisha bora duniani.”Asilimia 93 ya kaya Gaza hazina uhakika wa maji safi kutokana na ukosefu wa mafuta unaopelekea mifumo ya maji kukaribia kusambaratika yameonya mashirika ya Kibinadamu ya Umoja wa Mataifa leo yakiongeza kuwa familia zinakumbwa na njaa kali, wakila mlo mmoja kwa siku huku watu wazima wakikosa kula ili kuwasaidia watoto na wazee.Na leo katika kujifunza lugha ya Kiswahili mchambuzi wetu mlumbi wa Kiswahili Joramu Nkumbi kutoka nchini Tanzania, anafafanua maana ya neno "AFRITI KIJITI”Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!

Habari za UN
Jifunze Kiswahili: Maana ya neno AFRITI KIJITI

Habari za UN

Play Episode Listen Later Jun 26, 2025 0:36


Katika kujifunza lugha ya Kiswahili mchambuzi wetu mlumbi wa Kiswahili Joramu Nkumbi kutoka nchini Tanzania, anafafanua maana ya neno "AFRITI KIJITI.”

Habari za UN
19 JUNI 2025

Habari za UN

Play Episode Listen Later Jun 19, 2025 10:44


Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina, ikiwa kesho tarehe 20 mwezi Juni ni siku ya kimataifa ya wakimbizi maudhui yakiwa Mshikamano na Wakimbizi, tunakupeleka kwenye kambi ya wakimbizi ya Kakuma iliyoko kaunti ya Turkana, kaskazini-magharibi mwa Kenya.Uwekezaji wa moja kwa moja kutoka nje FDI umeshuka kwa mwaka wa pili mfululizo, ukihatarisha mustakabali wa maendeleo katika nchi zinazoendelea, kwa mujibu wa wa ripoti iliyotolewa leo na kamati ya Umoja wa Mataifa ya biashara na maendeleo UNCTAD. ikionya kuwa pengo la mitaji linaongezeka huku sekta muhimu kama nishati safi na miundombinu zikikosa ufadhili wa muda mrefu.Katika siku ya kimataifa ya kutokomeza ukatili wa kingono kwenye mizozo, Umoja wa Mataifa umetoa onyo kuwa ukatili wa kingono unazidi kutumika kama silaha ya vita huku wanawake na wasichana wakiathirika zaidi. Kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu na afya ya uzazi UNFPA "Huu si uharibifu wa bahati mbaya  ni uhalifu wa kivita. Na waathirika lazima wawe kiini cha amani, haki, na urejeshwaji wa maisha."Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa  Duniani (WHO) leo limezindua mwongozo wake wa kwanza wa kimataifa wa kudhibiti ugonjwa wa seli mundu (sickle cell) wakati wa ujauzito, ukilenga kupunguza hatari za maisha kwa mama na mtoto. WHO inasema wanawake wenye ugonjwa huu wana hatari hadi mara 11 zaidi ya kufariki dunia wakati wa ujauzito. Hivyo huduma bora za afya zinaweza kuokoa maisha, lakini visa vya seli mundu vinaongezeka duniani, huku Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara ikichangia asilimia 80.Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili hii leo Dkt Mwanahija Ali Juma, Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili, Zanzibar nchini Tanzania, BAKIZA anafafanua maana ya neno "KIHORO!.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!

Habari za UN
Jifunze Kiswahili: Maana ya neno KIHORO

Habari za UN

Play Episode Listen Later Jun 19, 2025 0:40


Katika kujifunza lugha ya Kiswahili hii leo Dkt. Mwanahija Ali Juma, Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili, Zanzibar nchini Tanzania, BAKIZA anafafanua maana ya neno "KIHORO!"

Habari za UN
12 JUNI 2025

Habari za UN

Play Episode Listen Later Jun 12, 2025 9:58


Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina na leo ikiwa ni siku ya kimataifa ya kupinga utumikishaji wa watoto ambapo shirika la Umoja wa Mataifa la Kazi duniani, ILO, linasema maudhui ni Maendeleo yako dhahiri, lakini bado kuna mengi ya kufanya: Hebu tuongeze kasi. Tunakupeleka nchini Tanzania kumulika harakati za kuwaepusha watoto kutumikishwa.Watu waliolazimika kukimbia makazi yao kutokana na vita, ukatili na mateso duniani kote imefikia kiwango cha juu kisichovumilika, hasa wakati huu ambapo ufadhili wa misaada ya kibinadamu unapungua kwa kasi. Kwa mujibu wa Ripoti ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia wakimbizi UNHCR iliyotolewa leo kuhusu mwelekeo wa Ulimwengu, kufikia mwisho wa Aprili mwaka huu, kulikuwa na watu milioni 122.1 waliolazimika kuhama kwa nguvu, ikilinganishwa na watu milioni 120 mwaka uliopita katika kipindi kama hicho.Ikiwa leo ni Siku ya Kimataifa ya kupinga ajira kwa watoto, utafiti uliofanywa na mashirika ya Umoja wa Mataifa lile la kazi duniani, ILO na la kuhudumia Watoto UNICEF unaonesha licha ya hatua zilizopigwa, ajira kwa watoto bado inaathiri watoto milioni 138 duniani kote, kati yao milioni 54 wakifanya kazi hatarishi ambazo zinaweza kuhatarisha afya yao, usalama wao au maendeleo yao kwa ujumla.Nchini Sudan Kusini watu wako katika hatari ya njaa katika miezi ijayo, kutokana na kuongezeka kwa mapigano katika jimbo la Upper Nile. Utafiti mpya kutoka katika Mfumo wa Uainishaji wa Viwango vya Uhakika wa Chakula (IPC) unaonesha kudorora kwa hali ya chakula na lishe katika maeneo ya Sudan Kusini yaliyoathiriwa na mapigano katika miezi ya karibuni.Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili hii leo mchambuzi wetu mlumbi wa Kiswahili Joramu Nkumbi kutoka nchini Tanzania, anafafanua maana ya maneno "MBEUZI, MNYWANYWA NA MACHAGU.”Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!

Habari za UN
Jifunze Kiswahili: Maana ya maneno "MBEUZI, MNYWANYWA NA MACHAGU.”

Habari za UN

Play Episode Listen Later Jun 12, 2025 0:54


Katika kujifunza lugha ya Kiswahili hii leo mchambuzi wetu mlumbi wa Kiswahili Joramu Nkumbi kutoka nchini Tanzania, anafafanua maana ya maneno "MBEUZI, MNYWANYWA NA MACHAGU.”

Habari za UN
11 JUNI 2025

Habari za UN

Play Episode Listen Later Jun 11, 2025 9:59


Hii leo jaridani tunaangazia ajali mbayá ya meli katika pwani ya Djibouti lililokuwa linabeba wahamiaji wengi. Pia tunasalia hapa makao makuu ambapo Kikao cha 18 cha Nchi Wanachama wa Mkataba wa Haki za Watu wenye Ulemavu COSP18. Mashinani tutakwenda nchini DRC.Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji, (IOM) kwa ushirikiano wa karibu na mamlaka za Djibouti, linaongeza juhudi zake za kibinadamu kufuatia tukio la kusikitisha lililotokea pwani ya Djibouti ambapo takriban wahamiaji wanane walikufa maji na wengine 22 hawajulikani walipo.Katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Kikao cha 18 cha Nchi Wanachama wa Mkataba wa Haki za Watu wenye Ulemavu COSP18, kinaendelea na mwaka huu, mada kuu ni kuongeza uelewa wa haki na mchango wa watu wenye ulemavu katika maendeleo ya kijamii. Miongoni mwa washiriki ni ya kijana kutoka Louisiana, hapa  Marekani.Makala tutasalia hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa New York Marekani ambapo Kikao cha 18 cha Nchi Wanachama wa Mkataba wa Haki za Watu wenye Ulemavu COSP18, kinaendelea na tutamsikiliza mmoja wa washiriki wa mkutano huu Bongani Simphiwe Makama kutoka Ufalme wa Eswatini ambaye amepata nafasi ya kuzungumza na idhaa ya Kiswahili.Na katika mashinani fursa ni yake fursa ni yake Byamungu Rukera, Mwakilishi wa watu waliokimbia makazi yao huko Sake, Kivu Kaskazini nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC akipazia sauti wakimbizi wenzake kwa wafanyakazi wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu na misaada ya dharura OCHA ambao wanawagawia chakula licha ya uhaba wa msaada huo.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!

Habari za UN
Akili Mnemba (AI) au teknolojia inaweza kuwasaidia watu wenye ulemavu – Bongani Simphiwe Makama

Habari za UN

Play Episode Listen Later Jun 11, 2025 3:49


Kikao cha 18 cha Nchi Wanachama wa Mkataba wa Haki za Watu Wenye Ulemavu – COSP18 – kinaendelea hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani ikiangazia juhudi za kimataifa za kuhakikisha usawa na ujumuishaji kwa watu wenye ulemavu. Miongoni mwa washiriki ni Bongani Simphiwe Makama mwakilishi wa watu wenye ulemavu kutoka Ufalme wa Eswatini, ambaye amepata nafasi ya kuzungumza na Idhaa ya Kiswahili kuhusu uzoefu wake, yale aliyojifunza, na changamoto zinazowakabili watu wenye ulemavu nchini kwake. Sharon Jebichii na Makala zaidi.

Habari za UN
Jifunze Kiswahili: maana ya neno KIHEREHERE

Habari za UN

Play Episode Listen Later Jun 5, 2025 0:45


Katika kujifunza lugha ya Kiswahili na hii leo Dkt. Mwanahija Ali Juma, Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili, Zanzibar nchini Tanzania, BAKIZA anafafanua maana ya neno KIHEREHERE.

Habari za UN
05 JUNI 2025

Habari za UN

Play Episode Listen Later Jun 5, 2025 11:03


Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina ambayo leo ikiwa ni siku ya mazingira duniani mwaka ikibeba maudhui “Tokomeza taka za Plastiki,” tunakwenda Tanzania kumsikia Clara Makenya, Mkua wa UNEP nchini humo na afisa mawasiliano wa shirika hilo kwa ajili ya Namibia akizungumza kuhusu changamoto ya taka za plastiki Tanzania na nini kifanyike kuzitokomeza.Naanzia hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa New York, Marekani ambapo leo kumefanyika tukio maalum la kukumbuka na kuenzi watumishi 168 wa Umoja wa Mataifa waliopoteza maisha wakitekeleza majukumu yao ya ulinzi wa amani, haki, na usaidizi, Mishumaa iliwashwa na kisha walitajwa majina yao mmoja baada ya mwingine akiwemo Nats.. mlinda amani wa UN kutoka Tanzania. Wanafamilia walipokea tuzo maalum za kutambua mchango wao.Leo ikiwa ni siku ya kimataifa ya mazingira, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres ametaka hatua za dharura kutokomeza janga la uchafuzi utokanao na taka za plastiki, akilitaja kama “janga” linaloikaba dunia na kutishia afya ya binadamu, mifumo ya ikolojia, na hali ya hewa. Guterres amesema, kadri plastiki zinavyovunjika na kuwa vipande vidogo vidogo zinaingia kila mahali: kuanziaubongo wa binadamu hadi maziwa ya mama.Huko nchini Tanzania hii leo kwenye Chuo Kikuu Mzumbe mjini Morogoro, kumefanyika kongamano kumulika uhaba wa maji na sera bora zinazoweza kufanikisha upatikanaji wa huduma hiyo, kongamano lililoandaliwa kwa pamoja na shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo, UNDP na Muungano wa Ulaya. Dkt. Saida Fundi Mhadhiri Mwandamizi kutoka Chuo Kikuu Mzumbe anasema.Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili na hii leo Dkt. Mwanahija Ali Juma, Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili, Zanzibar nchini Tanzania, BAKIZA anafafanua maana ya neno "KIHEREHERE!.Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!

Habari za UN
29 MEI 2025

Habari za UN

Play Episode Listen Later May 29, 2025 9:58


Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayoangazia Walinda Amani wa Umoja wa Mataifa ikitupeleka nchini DRC, Sierra Leone na Ghana. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na maana ya neno "MISHEMISHE.”Leo ni Siku ya Kimataifa ya Walinda Amani ambayo mwaka huu inajikita na maudhui ya “mustakabali wa ulinzi wa amani.”Katika ujumbe wake wa siku hii Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema walinda amani wa Umoja wa Matafa wako katika changamoto kubwa “Leo hii, walinda amani wanakabiliwa na hali zinazozidi kuwa ngumu katika dunia inayozidi kuwa na changamoto, ikiwemo uugawanyika na kutofautiana kwa mitazamo duniani kunazidi kuongezeka, operesheni za ulinzi wa amani zinakabiliwa, hatari zaidi kutokana na wingi wa vitisho kama vile ugaidi na walinda amani kulengwa kwa makusudi kupitia taarifa potofu zenye madhara makubwa na changamoto zinazovuka mipaka kuanzia janga la mabadiliko ya tabianchi hadi uhalifu wa kimataifa.Kikosi cha 11 cha Tanzania kinachohudumu chini ya mpango wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo MONUSCO kimeungana na walinda amani wengine kuadhimisha Siku ya Walinda Amani Duniani. Maadhimisho hayo yamefanyika Mavivi, yakiongozwa na Brigedia Jenerali Diamond Meshack Madie, Mnadhimu Mkuu wa Vikosi vya MONUSCO.Shirika la Umja wa Mataifa la Mazingira UNEP limezindua mpango mpya wa dola milioni 15 kusaidia uwekezaji endelevu katika Bonde la Kongo – moja ya mifumo muhimu zaidi ya ikolojia duniani. Mpango huu unalenga kufungua fursa za biashara rafiki kwa mazingira kwa wajasiriamali wadogo na wa kati katika sekta za kijani. Msitu wa mvua wa Bonde la Kongo ni moja ya vyanzo vikubwa vya kaboni duniani na ni makazi ya watu zaidi ya milioni 75, wakiwemo jamii za asili.Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili mtaalam wetu leo ni Onni Sigalla, Mhariri Mwandamizi  Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania, BAKITA anafafanua maana ya neno "MISHEMISHE.”Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!

Habari za UN
Jifunze Kiswahili: Maana ya neno "MISHEMISHE.”

Habari za UN

Play Episode Listen Later May 29, 2025 0:38


Katika kujifunza lugha ya Kiswahili mtaalam wetu leo ni Onni Sigalla, Mhariri Mwandamizi  Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania, BAKITA anafafanua maana ya neno "MISHEMISHE.”

Habari za UN
23 MEI 2025

Habari za UN

Play Episode Listen Later May 23, 2025 9:56


Hii leo jaridani tunaangazia haki za kibinadamu za raia nchini Uganda, na simulizi ya mkimbizi nchini Mexico ambaye alikimbia machafuko nchini mwake Haiti. Makala tunakwenda nchini Kenya na mashinani nchini Ethiopia, kulikoni?Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa , Volker Türk, leo Ijumaa mjini Geneva, Uswisi kupitia msemaji wake ameelezea wasiwasi wake kuhusu kupitishwa kwa muswada uliopendekezwa na Bunge la Uganda unaoruhusu raia kuhukumiwa katika mahakama za kijeshi.Wakati raia wa Haiti Giovanni Rotschild alipowasili Mexico mwaka 2022 baada ya safari ndefu isiyo na uhakika kutoka nchi mwake kulikosheheni ghasia, hakufahamu mtu yeyote wala hakuzungumza kabisa lugha ya kispanyola. Lakinialipata msaada kumwezesha kujenga upya maisha na kupata jamii mpya.Makala tukielekea siku ya kandanda, kabumbu au mpira wa miguu duniani itakayoadhimishwa Jumapili wiki hii Mei 25 ikibeba maudhui nguvu ya kdandanda katika kuleta mabadiliko tuabisha hodi Nairobi Kenya ambapo leo Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Global Youth Forum linalounganisha vijana Kenya kwa lengo la kutokomeza umasikini na kuishi maisha bora kupitia michezo mbalimbali ikiwemo kandanda akizungumza na Idhaa hii ya Kiswahili anaeleza umuhimu wa kandanda katika ajenda ya Umoja wa Mataifa ya maendeleo endelevu.Na katika mashinani, fursa ni yake Hola msichana mwenye umri wa miaka 15 kutoka wilaya ya Sire nchini  Ethiopia ambaye  kutokana na mafunzo ya stadi za maisha ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto UNICEF yanayoungwa mkono na asasi ya kupinga ndoa za utotoni ya GPChild Marriage ameweza kuepuka ndoa za utotoni na sasa anatumia mafunzo hayo kutahadharisha na kulinda wenzake.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!

Habari za UN
Vijana Kenya watumia mpira wa miguu kutokomeza umasikini na kuishi maisha bora - Peter Omondi

Habari za UN

Play Episode Listen Later May 23, 2025 3:06


Katika kuelekea siku ya kandanda, kabumbu au mpira wa miguu duniani itakayoadhimishwa Jumapili wiki hii Mei 25 ikibeba maudhui nguvu ya kdandanda katika kuleta mabadiliko tuabisha hodi Nairobi Kenya ambapo leo Peter Omondi, Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Global Youth Forum linalounganisha vijana Kenya kwa lengo la kutokomeza umasikini na kuishi maisha bora kupitia michezo mbalimbali ikiwemo kandanda akizungumza na Idhaa hii ya Kiswahili anaeleza umuhimu wa kandanda katika ajenda ya Umoja wa Mataifa ya maendeleo endelevu. Anaanza kwa kujitambusha.

Habari za UN
22 MEI 2025

Habari za UN

Play Episode Listen Later May 22, 2025 9:59


Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini kumsikia mgeni wetu Prof. Wallah Bin Wallah, mwandishi mashuhuri wa vitabu vya Kiswahili kutoka Kenya ambaye anamulika umuhimu wa vitabu katika kukuza lugha ya Kiswahili. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na uchambuzi wa neno.Kwa mara ya kwanza tangu mwezi Februari, msaada wa kuokoa maisha umefika Gaza. Baada ya wiki 11 za kizuizi kutoka kwa mamlaka za Israeli, malori 198 yaliyobeba chakula, dawa na unga wa ngano yameingia leo kupitia mpaka wa Kerem Shalom kwa mujibu wa mashirika ya kibinadamu ya Umoja wa Mataifa.Mratibu mkuu wa misaada wa Umoja wa Mataifa, Tom Fletcher, ameiitaja hatua hiyo kuwa ya muhimu sana, huku malori 90 yakipakuliwa usiku kwa ajili ya kusambazwa haraka.Mwaka 2024, vita havikuishia kwenye uwanja wa mapambano pekee      vilivunja nyumba, masoko na shule. Kuanzia Gaza hadi Ukraine, Sudan hadi Myanmar na zaidi ya raia 36,000 walipoteza maisha yao katika mizozo 14 ya kivita kulimgana na ripoti ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres kwa Baraza la Usalama hii leo linalojadili ulinzi wa raia katika mizozo ya silaha.Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili hii leo Dkt Mwanahija Ali Juma, Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili, Zanzibar nchini Tanzania, BAKIZA anafafanua maana ya neno "DAHARI”Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!

Habari za UN
Jifunze Kiswahili: Maana ya neno "DAHARI"

Habari za UN

Play Episode Listen Later May 22, 2025 0:36


Katika kujifunza lugha ya Kiswahili hii leo Dkt. Mwanahija Ali Juma, Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili, Zanzibar nchini Tanzania, BAKIZA anafafanua maana ya neno "DAHARI."

Habari za UN
15 MEI 2025

Habari za UN

Play Episode Listen Later May 15, 2025 9:59


Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayoturejesha katika mkutano wa CSW68 kumsikia Christina Kamili Ruhinda, Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Mashirika yanayotoa huduma ya msaada wa kisheria nchini Tanzania, TANLAP. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na uchambuzi wa neno la wiki.Wakati dunia ikiadhimisha miaka 77 tangu Nakba ambapo zaidi ya wapalestina 700,000 walifurushwa kutoka vijiji na miji yao mwaka 1948, shirika la Umoja wa Mataifa la msaada kwa Wakimbizi wa Kipalestina UNRWA limetoa onyo kali kuhusu sura mpya ya mateso na ufurushwaji wa lazima uonaoendele Gaza.Akiwa na wasiwasi kutokana na ripoti za kuaminika kwamba wakimbizi wa Rohingya kutoka Myanmar walilazimishwa kushuka kutoka kwenye meli ya jeshi la wanamaji la India na kutoswa katika bahari ya Andaman wiki iliyopita, Mtaalamu wa UN wa Haki za Binadamu kuhusu wakimbizi wa Myanmar, ameanzisha uchunguzi kuhusu kitendo hicho alichoeleza kuwa ni cha kushangaza na kisichokubalika.Na baada ya muda mrefu kuonekana kama mchangiaji mkubwa wa utoaji wa hewa chafuzi duniani, sekta ya usafirishaji majini sasa iko mstari wa mbele katika kuonesha ushirikiano wa kipekee wa kimataifa wa kupunguza hewa hizo zitolewazo na meli za usafirishaji majini.Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili mtaalam wetu ni Onni Sigalla, Mhariri Mwandamizi Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania, BAKITA anafafanua maana ya neno "KIANGO".Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!

Habari za UN
Jifunze Kiswahili: Maana ya neno "KIANGO."

Habari za UN

Play Episode Listen Later May 15, 2025 0:52


Katika kujifunza lugha ya Kiswahili mtaalam wetu ni Onni Sigalla, Mhariri Mwandamizi Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania, BAKITA anafafanua maana ya neno "KIANGO."

Habari za UN
Kutimiza azimio la watu wa jamii za asili ni jukumu la mataifa yote duniani - Adam Ole Mwarabu

Habari za UN

Play Episode Listen Later May 8, 2025 6:48


Jukwaa la Umoja wa Mataifa kuhusu watu wa jamii za asili limekunja jamvi mwishoni mwa wiki iliyopita hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa na kandoni mwa jukwaa hilo Flora Nducha wa Idhaa hii ya Kiswahili alipata fursa ya kuzungumza na mmoja wa washiriki kiongozi wa kijamii kutoka Jamii ya wafugaji ya Wamaasai mkoani Morogoro Mashariki mwa Tanzania Adam Kulet Ole Mwarabu, wamejadili mengi lakini Ole Mwarabu anaanza kwa kukumbusha alichokibeba kwenye jukwaa la mwaka jana kinavyotekelezwa nchini mwake.

Habari za UN
08 MEI 2025

Habari za UN

Play Episode Listen Later May 8, 2025 11:12


Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa ambayo Flora Nducha wa Idhaa hii ya Kiswahili alipata fursa ya kuzungumza na kiongozi wa kijamii kutoka Jamii ya wafugaji ya Wamaasai mkoani Morogoro nchini Mashariki mwa Tanzania Adam Kulet Ole Mwarabu.Wiki kumi baada ya kuanza kwa mzingiro kamili wa Israel dhidi ya wakazi wa Gaza, zaidi ya robo tatu ya kaya katika eneo la Palestina kuna uhaba mkubwa wa huduma ya maji, huku hali ya usafi ikizidi kuwa mbaya, yameonya leo mashirika ya misaada ya Umoja wa Mataifa huku wasiwasi ukiongezeka kuhusu athari za "uhaba huo wa maji kwa kuzingatia kuwa msimu wa joto unakaribia.”Ripoti kutoka Sudan zikidai kwamba juzi jumatano kulikuwa na jaribio la mashambulizi mapya ya ndege zisizo na rubani dhidi ya kitovu muhimu cha misaada nchini humo juzi, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres kupitia tamko alilolitoa jana jioni kwa saa za New York, Marekani, ameongeza nguvu yake katika kutoa wito unaozidi kuwa wa muhimu kuhamasisha kuanzishwa kwa mazungumzo ya amani ya kweli.Kufuatia kuendelea kwa mvutano wa majirani, India na Pakistani, Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, Philemon Yang, ametoa wito wa kuzitaka nchi hizo mbili kuchukua tahadhari na kuepuka hatua zinazoweza kuongeza mzozo. Balozi Yang anasisitiza mazungumzo ya amani na kufuata sheria za kimataifa ndiyo njia pekee ya kusuluhisha migogoro.”Na katika jifunze Kiswahili leo Dkt. Mwanahija Ali Juma, Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili Zanzibar nchini Tanzania, BAKIZA anafafanua maana ya neno "DALALI”Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!

Habari za UN
Jifunze Kiswahili: Maana ya neno "DALALI”

Habari za UN

Play Episode Listen Later May 8, 2025 0:45


Katika kujifunza lugha ya Kiswahili leo Dkt. Mwanahija Ali Juma, Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili Zanzibar nchini Tanzania, BAKIZA anafafanua maana ya neno "DALALI”

Habari za UN
Maoni kutoka washiriki kutoka maeneo mbalimbali waliohudhuria mkutano wa jamii za asili UNPFII

Habari za UN

Play Episode Listen Later Apr 30, 2025 3:24


Hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa, mkutano wa 24 wa Jukwaa la Kudumu la Watu wa jamii za asili (UNPFII) linaendelea kujadili utekelezaji wa Azimio la Umoja wa Mataifa kuhusu haki za watu wa asili na kubaini mbinu bora za kushughulikia changamoto zinazowakabili, ukileta pamoja washiriki kutoka maeneo mbalimbali kote duniani. Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa walipata fursa ya kuzungumza na baadhi yao.