POPULARITY
Watu wengi wanapokaribia kufunga ndoa,hujukumika kufanya vipimo vya virusi vya HIV .Wengi hufanya kipimo hicho si kwa sababu wanajua umuhimu wake bali ni kwa sababu ya ulazima kabla kufunga harusi haswa za Kikristo. Hata hivyo watalaam wa afya wanasema kuna vipimo tele ambavyo ni muhimu pia na vinahitajika kufanywa kabla ndoa. Mwanasaikolojia Naomi Ngugi anasema kando na kipimo cha HIV,kuna kipimo cha Rhesus Factor ambayo kama mtu na mwenzake hana ufahamu ,wanaweza kupata shida ya kuharibika mimba. Kuna pia kipimo cha Genotype kubaini uwepo wa ugonjwa kama Selimundu ,Hepatitis B, Hepatitis C au homa ya ini,vipimo vya Magonjwa sugu, Magonjwa ya akili na Vipimo vya uzazi kubaini ubora wa mbegu za kiume na matatizo ya mirija kuziba upande wa wanawake. Vipimo hivyo vinaweza kugharimu ndoa iwapo wanandoa hawataweka wazi.
Kwa mara ya kwanza idadi ya watoto na vijana wa umri wa kwenda shule wenye unene wa kupindukiaau utipwatipwa imezidi idadi ya watoto wenye utapiamlo duniani ikiathiri watoto milioni 188 sawa na mtoto 1 kati ya kila watoto 10 imesema leo ripoti iliyotolewa leo na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF. Tuungane na Leah Mushi kusikia zaidi kuhusu ripoti hiyo, karibu LeahRipoti hii mpya ya UNICEF iitwayo “Faida kwenye vyakula: Jinsi Mazingira ya Chakula yanavyowaangusha watoto” imechambua takwimu kutoka nchi zaidi ya 190 na kubaini kwamba kiwango cha watoto wenye utapiamlo kimepungua tangu mwaka 2000, lakini wale wenye unene wa kupindukia kimeongezeka mara tatu.Kwa sasa, utipwatipwa umeenea katika kila eneo la dunia isipokuwa Afrika eneo la Kusini mwa Jangwa la Sahara na Asia Kusini. Nchi za visiwa vidogo vya Pasifiki ndizo zinaongoza kwa kuwa na viwango vya juu zaidi, ikiwemo Niue yenye asilimia 38 ya watoto wenye umri wa miaka 5 hadi 19 wakiwa na unene wa kupindukia.Nini kimesababisha?UNICEF inasema mabadiliko ya mifumo ya lishe kutoka vyakula vya asili hadi vyakula vya kutengenezwa kwa haraka na vya bei nafuu lakini vyenye sukari, mafuta na chumvi nyingi ndiyo chanzo kikuu cha ongezeko hili.Pia inatahadharisha kuwa matangazo ya kidijitali ya vinywaji vyenye sukari na vyakula vya viwandani yanawafikia vijana wengi, hata katika nchi zenye migogoro.Mkurugenzi Mtendaji wa UNICEF, Catherine Russell, amesema utipwatipwa ni changamoto kubwa ya kiafya kwa watoto kwa sababu huongeza hatari ya kupata kisukari, shinikizo la damu na magonjwa ya moyo katika maisha ya baadaye.Russell amesema “Tunapozungumza kuhusu utapiamlo, hatuzungumzii tu kuhusu watoto wenye uzito mdogo, utipwatipwa ni changamoto kubwa inayoendelea kuongezeka ambayo inaweza kuathiri afya na maendeleo ya watoto. Vyakula vya viwandani vinazidi kuongezeka na kuchukua nafasi ya matunda, mboga mboga na protini katika wakati ambao lishe ina jukumu muhimu katika ukuaji wa watoto, ukuaji wa utambuzi na afya ya akili.”Nini kifanyike?Ili kukabiliana na hali hii, UNICEF inazitaka serikali kuchukua hatua madhubuti ikiwemo kupiga marufuku uuzaji wa vyakula visivyo na lishe shuleni, kudhibiti matangazo ya vyakula vyenye sukari na mafuta, na kuweka sera za kusaidia familia kupata chakula bora na chenye lishe.Kwa mujibu wa UNICEF, bila hatua za haraka, gharama za kiafya na kiuchumi zitakazotokana na tatizo la utipwatipwa wa utotoni zinatarajiwa kupindukia dola trilioni 4 kila mwaka ifikapo mwaka 2035.Zipo juhudi za kupambana na hali hiyo ambazo zimeanza kuchukuliwa na baadhi ya nchi, mfano mzuri ni Mexico ambayo hivi karibuni imepiga marufuku uuzaji wa vyakula vilivyosindikwa na vile vyenye chumvi, sukari na mafuta mengi katika maeneo ya shule za umma.
Wanadamu ni viumbe ambao hukamilika wanapokuwa kwenye jamii ambapo wanaweza kuelezea hisia zao,kujihisi wanathaminiwa na wana mchango kwa wengine. Mambo hayo yanapokosa,inaweza kuwa chanzo cha matatizo ya kiafya.Na hii ni hali ambao hukuwa nao wakimbizi ambao wametenganishwa na wapendwa wao. Katika kambi ya Kakuma iliyoko kaunti ya Turkana,kaskazini mwa Nchi ya Wakenya,tulizungumza na wakimbizi ambao walilazimika kutengana na wapendwa wao kwa sababu ya migogoro ya kifamilia,ukoo na hata vita. Ingawa wamepata makao katika kambi ya wakimbizi bado maisha yao hayajakamilika . Wengi wameishi kwenye hali ya upweke,huzuni na kiwewe na kupata matatizo ya kiafya yakiwemo matatizo ya afya ya akili. Aidha kuna wale ambao wamepatwa na maradhi kama shinikizo la damu ,kisukari,ukosefu wa usingizi na chanzo ni matatizo ambayo wamekumbana nao katika kambi,ugumu wa maisha bila watu walio karibu nawe ambao unaweza kuzungumza nao na kuliwazana. Kamati ya kimataifa ya msalaba mwekundu,ICRC pamoja na shirika la msalaba mwekundu nchini ,KRC,katika kujaribu kukabili hali hiyo ,zinatekeleza mpango wa kujaribu kurejesha mawasiliano na uhusiano wa familia za wakimbizi. Kwa kuwatafuta namna ambao wakimbizi hao wanaweza kuwasiliana kupitia ujumbe wa kuandikiwa au kwa njia ya simu,mashirika hayo wanasema wamefanikiwa kuwarejeshea tabasamu wachache wenye bahati na wanaendelea kuwasaka wanafamilia zaidi kila mwaka. Matunda ya mpango huo yameonekana miongoni mwa wakimbizi wanaozungumza na jamaa zao na pia kwa wahudumu wa kujitolea wanaotangamana karibu kila siku na wakimbizi hao kwenye kambi.
Mashambulizi ya ndege zisizo na rubani za Urusi nchini Ukraine yaliyofanyika usiku kucha, ikiwemo katika miji ya Kharkiv na Zaporizhzhia, yameripotiwa kuua watu 10 wakiwemo watoto watatu, kwa mujibu wa taarifa ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto UNICEF iliyotolewa leo. Flora Nducha na taarifa zaidi
Katika mahojiano haya, Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Mashirika yanayotoa huduma ya msaada wa kisheria nchini Tanzania, TANLAP, Christina Kamili Ruhinda alipozungumza na Anold Kayanda wa Idhaa hii kandoni mwa Mkutano wa Kamisheni ya hali ya wanawake duniani CSW69 uliofanyika mapema mwaka huu hapa New York, Marekani, anaeleza wanavyotekeleza mpango wao wa kuhakikisha wanawake wanapata nafasi zaidi kwenye meza za uamuzi nchini Tanzania.
Misri ipo kwenye njia panda kuhusu utekelezaji wa sheria zake za kudhibiti matumizi ya tumbaku haswa sigara na Shisha. Kwa njia moja sigara inaleta mapato makubwa kwa mfuko wa mapato ya serikali ya Misri ,ni tabia inayoruhusiwa ila kwa upande mwingine inakodolea macho hatari kubwa ya kiafya inayotokana na uvutaji sigara.Unapowasili Cairo jiji kuu la Misri ,ukutana na harufu tamu ya mikate ,keki na bidhaa zingine za ngano za kuokwa,marashi yanayonukia lakini pia kuna harufu ya shisha, aina ya tumbaku ya kisasa zenye ladhaa za kupendeza lakini pia harufu kali zaidi ya sigara.Zipo sheria zinazokataza uvutaji sigara katika sehemu za umma ,shule ,vituo vya afya ila utekelezaji wake bado ni changamoto kubwa.Kuna mpango pia wa treni mwendo kasi ,maarufu Greenline ambapo uvutaji sigara umeharamishwa.Hata hivyo kibarua bado kipo cha kubadilisha mtazamo wa baadhi ya wananchi wanaoamini uvutaji sigara ni starehe ,kitu cha hadhi na unaweza kufanya hivyo popote muradi usikamatwe.Misri pia inabidi kuangalia kwa jicho la pili sheria zake za kutoza ushuru bidhaa za tumbaku iwapo lengo ni kuleta mapato kwa serikali ,kuwafaidi wazalishaji au kwa maslahi ya afya ya wengi.Kwa mujibu wa shirika la afya duniani,WHO, asilimia 20-25% ya watu wazima nchini Misri huvuta sigara.
Zaidi ya watu 63,000 sasa wamewasili Burundi wakikimbia machafuko nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR na wengi wao wanaishi katika hali ngumu ndani ya uwanja wa michezo wa Rugombo jimboni Cibitoke (CHIBITOKE) huku wakisubiri kuhamishiwa kwenye kambi rasmi za wakimbizi. Flora Nducha amefuatilia safari ya mmoja wa wakimbizi hao, kwako Flora.
Vijana Kenya waeleza juu ya utafiti ulioonyesha matamanio ya wengi kusoma nje ya nchi
VOA Express ni matangazo mapya yenye mwendo wa kasi yakiangalia habari mpya za mchana na maelezo ya maswala yanayohusu vijana na wanawake.
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini DRC katika kambi ya wakimbizi wa ndani ya Bulengo kushuhudia jinsi Umoja wa Mataifa unavyowasaidia wanawake waathrika wa ukatili wa kingoni kuweza kujitegemea na kumudu mahitaji ya familia zao.Kwa mujibu wa takwimu zilizothibitishwa na Ofisi ya Haki za Kibinadamu ya Umoja wa Mataifa, takriban watu 5,601 waliuawa nchini Haiti mwaka 2024 kutokana na ghasia za magenge, likiwa ni ongezeko la zaidi ya mauaji 1,000 ya mwaka 2023. Katika moja ya matukio mabaya zaidi na ya kushtua mwaka jana, takriban watu 207 waliuawa mapema Desemba kwenye mauaji yaliyoratibiwa na kiongozi wa genge lenye nguvu la Wharf Jérémie katika eneo la Cité Soleil huko Port-au-Prince. Wengi wa waliouawa walikuwa wazee walioshutumiwa kusababisha kifo cha mtoto wa kiongozi huyo kwa njia ya uchawi.Leo, Umoja wa Mataifa na Serikali ya Lebanon wametoa ombi la nyongeza ya dola milioni 371.4 za kimarekani, zikilenga kutoa msaada wa kuokoa maisha ya walioathiriwa na mzozo wa hivi karibuni na janga la kibinadamu linaloendelea nchini humo.Na Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa Volker Türk leo ameeleza kusikitishwa sana na ongezeko kubwa la watu walionyongwa nchini Iran mwaka jana. Takriban watu 901 wameripotiwa kunyongwa katika mwaka 2024, arobaini wakiwa wamenyongwa katika wiki moja tu ya mwezi Desemba.Mashinani kupitia video ya Shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu na afya ya uzazi, UNFPA tunamsikia Zubaida AbouBaker, mama mkimbizi wa ndani katika kambi ya Tawila iliyoko Darfur Kaskazini nchini Sudan akisimulia machungu yaliyomkumba kufuatia migogoro inayoendelea nchini humo.Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!
Mkutano wa 29 wa Umoja wa Mataifa wa mkataba wa mabadiliko ya tabianchi COP29 ukianza wiki ya piili mjini Baku Azerbaijan leo, wito umetolewa kwa wanawake amba oni waathirika wakubwa wa janga la mabadiliko ya tabianchi kutopewa kisogo. Anne Cheruto Tek ambaye amebeba bendera ya wanawake waathitika wa mabadiliko ya tabianchi kutoka Afrika ameiambia UN News anachokifanya COP29..“Sana sana kufuatilia haya madhara ya mabadiliko ya tabianchi hasa kwa wanawake na vijana barani Afrika. Sana sana utakuwa wanawake ndio wanaoshughulikia masuala ya maji, masuala ya kuni, masuala ya chakula , lakini mara nyingi kukiwa na janga la mabadiliko ya tabianchi kama ukame, mafuriko, wanawake ndio wanaangamia zaidi, kwa sababu wanawke ndio wanakuwa na jukumu la kuendesha nyumba na hivyo hawana nafasi ya kutafuta fedhha ambaz zinaweza kuwasaidia wakati wa majanga hayo.”Na kutokana na hayo anasema wanawake hukabiliwa na changamoto kubwa“Wengi hupata magonjwa , wengi huathhirika sana wakati wa majanga ikiwemo vifo, ukosefu wa fedha na pia ukatili wa kijinsia wakati wa shida za mabadiliko ya tabianchi.”Na nini ombi lake katika mkutano huo?Kuhakikisha kuwa hizi changamoto zinaangaziwa hasa kwa masuala ya fedha, kuhakikisha kuwa fedha zinawafikia wanawake vijijini , kuhakikisha kuwa wanaweza kuelewa masuala ya mabadiliko ya tabianchi na pia waweze kuelezea hadithi zao jinsi wanavyoathirika na tunaomba hii COP kuangazia haya majanga hasa kwa wanawake, wasichana na watu wasiojiweza kama wenye ulemavu.”
Hii leo jaridani tunamulika kupelekwa kwa chanjo dhidi ya polio huko Gaza; mkimbizi wa Burundi aliyerejea nyumbani kutoka Tanzania ainuliwa kiuchumi; makala ni mkimbizi wa Sudan aliyeko ugenini naye awezeshwa kijasiriamali na mashinani tunabisha hodi nchini Rwanda kumulika usawa wa kijinsia kwenye michezo.Hatimaye shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF linapeleka Gaza huko Mashairki ya Kati dozi milioni 1.2 za chanjo dhidi ya ugonjwa wa polio aina ya 2, wakati huu ambapo ugonjwa huo hatari umethibitishwa kuweko eneo hilo. Anold Kayanda na maelezo zaidi.Kwa wakimbizi, kurejea nyumbani ni jambo moja na kuanza upya ni jambo lingine. Wengi wao hawana chaguo lingine isipokuwa kuanza maisha yao upya. Mkoani Makamba, nchini Burundi, Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) kwa kushirikiana na Shirika la Ushirikiano wa Kimataifa la Korea (KOICA) wanawawezesha waliorejea nyumbani kujijenga upya na kwa tija. Miongoni mwao ni Emelyne Kabura kama anavyosimulia Bosco CosmasKatika makala Evarist Mapesa anatuletea simulizi ya mkimbizi wa Sudan ambaye sasa anaishi Sudan Kusini. Baada ya kupitia madhila lukuki amewezeshwa na mashirika ya Umoja wa Mataifa na sasa anajishughulisha na ujasiriamali.Na sasa ni mashinani Christelle Umuhoza, Mkurugenzi wa Programu wa Rwanda katika shirika la Shooting Touch, kupitia video ya shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni UNESCO nchini humo, anaeleza umuhimu wa michezo katika kuondoa vikwazo vya kijinsia.
Kwa wakimbizi, kurudi nyumbani ni jambo moja na kuanza upya ni jambo lingine. Wengi wao hawana chaguo lingine isipokuwa kuanza maisha yao upya. Mkoani Makamba, nchini Burundi, Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) kwa kushirikiana na Shirika la Ushirikiano wa Kimataifa la Korea (KOICA) wanawawezesha wakimbizi kujenga upya na kuanza maisha yenye tija. Mmoja wa wakimbizi hao ni KABURA Emelyne, ambaye sasa anamiliki nyumba na ni mfanyabiashara. Bosco Cosmas anatupa habari kamili…Tangu mwaka 2017, takriban wakimbizi 250,000 wa Burundi wamepewa msaada wa kurejea nyumbani kutoka nchi jirani ya Tanzania. Wengi kama Emelyne hawakuwa na chaguo jingine ila kuanza maisha upya. Lakini kwa ufadhili wa (UNHCR) kwa ushirikiano na (KOICA) sasa wanaishi kwa tija.Emelyne anasema, “nilifurahi sana kuvuka mpaka wa Manyovu na kurejea nchini mwangu Burundi. Ninapoona maendeleo mapya na miji inayostawi, najihisi nimeridhika. Nilikimbilia Tanzania mwaka 2015 na nikarejea mwaka 2021.”Sasa Emelyne ameanza kujishughulisha na kilimo na kuuza mihogo, kutengeneza mafuta ya mawese, na kufuga sungura kwa ajili ya nyama na mbolea. “Najisikia furaha ninapowalisha sungura wangu kwa sababu wananiwezesha kupata mbolea. Nashukuru kwamba kupitia mauzo ya sungura nilikodi kipande cha ardhi kwa ajili ya kulima na nikapata fedha za kuanzisha biashara yangu ya mihogo na mafuta ya mawese.”Msaada kutoka Shirika la Ushirikiano wa Kimataifa la Korea (KOICA) unawawezesha waliorejea kujenga upya na kuanza maisha mapya. Kwa mujibu wa Emelyne, "UNHCR walitukaribisha na kutusaidia. Kwa msaada wa kifedha tuliopewa, tulinunua ardhi hii, tukatengeneza matofali na kujenga kuta za nyumba yetu. Kisha tukapokea mabati, nguzo, madirisha, na milango ili kukamilisha nyumba. Kama ningalikuwa bado kwenye kambi, nisingeweza kupiga hatua kubwa kiasi hiki.”
Hadithi halisi za wahanga wa mauaji ya 1994 nchini Rwanda, zime zinduliwa katika jumba la sanaa mjini.
Trump aahidi akichaguliwa atarejesha marufuku ya kusafiri kwa baadhi ya nchi zenye waislamu wengi
Wakenya wanao ishi Australia watajumuika katika jiji la Dandenong jimboni Victoria, kuhudhuria hafla la shirika la Taunet Nelel.
Mgomo wa madaktari umetimiza sasa siku 35, naam majuma matano. Hakuna mwafaka wowote wa aina yoyote, na mwananchi anayetegemea huduma za afya katika hospitali za umma ndiye anaumia. Nani atamjali raia huyu?
Kuna ongezeko la magonjwa ya figo na ini kwa mujibu wa shirika la afya duniani WHO inabashiri kuwa ongezeko hilo litakuwa juu zaidi kufikia mwaka 2030 ,hali hii ikichangiwa na hali ya maisha haswa ya raia katika nchi zinazoendeleaUgonjwa wa ini maarufu Hepatitis pia ni tishio kubwa haswa kwa raia wa Afrika ambayo inachangia asilimia 63 ya visa vya HepatatisNchini Sudan watoto wengi haswa walio chini ya umri wa miaka mitano wanazidi kupoteza maisha kutokana na utapiamlo unaohusishwa na ukosefu msaada wa kibinadaam wakati huu vita vikiendelea kurindima
Jeshi la polisi la New South Wales lime anza uchunguzi kwa shambulizi la kisu, lililo wauwa watu sita ndani ya soko kubwa katika vitongoji vya mashariki ya Sydney.
Roberta Steuder ist Zen-Nonne, diplomierte psychologische Beraterin und systematische Aufsteller-Coach. Sie ist Co-Leiterin im Zen-Zentrum Scheunenberg in Wengi bei Büren. Zusammen mit ihrem Mann leitet sie verschiedene Kurse und Ausbildungen, darunter die einjährige Ausbildung «Ganzheitliche Kommunikation». Sie praktiziert Zen seit 1997 und ordinierte 2018 zur Nonne. Im Gespräch erzählt sie, was Religion in der Kindheit für sie bedeutete, wie sie eine Ausbildung machte und eine Familie gründete. Wie sie in einer Treuhandfirma Karriere machte und als Chief Financial Officer, HR-Verantwortliche und Berufsbildnerin tätig war. Ihre Begegnung mit Zen lenkte ihr Leben schliesslich in eine neue Richtung. Roberta blickt aber nicht nur auf ihren Weg zurück, sondern gibt im Gespräch auch ganz praktische Tipps und Hinweise. Sie erläutert, wie man mit Gedanken oder schwierigen Emotionen in der Meditation umgehen kann und wie unterschiedliche Persönlichkeitstypen verschiedene Herangehensweisen brauchen. Anhand des Aufbau des Kurses «Ganzheitliche Kommunikation» gehen wir durch die vier Felder Körper, Emotionen, Geist und Objekte im Geist. Wir sprechen über Projektionen und Projektionsmuster, über das Thema Geld und auch über die Erleuchtung. Wie in der Zen-Tradition üblich, merkt man, wie sehr Roberta im Leben steht und in die Welt wirkt. Mehr zu Roberta findest du auf ihrer Website: www.zencom.ch Inhalt 00:00:00.000 Intro 00:01:48.442 Biografie 00:02:41.642 Religion in der Kindheit 00:07:36.345 Berufswahl und Karriere 00:10:46.955 Warum Zen? 00:14:13.892 Wie funktioniert Zen und in welcher Tradition stehst du? 00:15:53.849 Umgang mit Gedanken in der Meditation 00:22:34.571 Herangehensweisen für verschiedene Persönlichkeitstypen 00:24:18.446 Reaktionen des Umfelds 00:27:00.793 Entscheid, zu ordinieren 00:29:46.104 Bedeutung der Ordination 00:33:25.019 Aufgabe des Treuhandberufs 00:34:56.072 Beschreibung des Zen Zentrums Scheunenberg 00:36:18.883 Kurs «Ganzheitliche Kommunikation» 00:41:13.471 Beschreibung Jahrestraining: Körper 00:47:50.080 Zweite Grundlage der Achtsamkeit: Emotionen 00:54:32.344 Dritter Bereich: Geist 00:56:25.806 Projektionen und Projektionsmuster 01:00:50.815 Objekte des Geistes: Vergänglichkeit, Unzulänglichkeit, Ich-Losigkeit 01:04:25.845 Thema Geld 01:07:23.885 Ziel des Kurses 01:09:25.720 Stellenwert der Erleuchtung 01:12:09.716 Wie sich Robertas Praxis verändert hat 01:14:20.250 Integration ins Leben 01:17:02.491 Umgang mit der Feinfühligkeit 01:19:06.724 Infos zu Robertas Angebot
Serikali ya Tanzania yatoa sababu za upungufu wa sukari, umeme na sarafu ya dola, lakini wachambuzi na wananchi wengi hawajaridhishwa.
Today I'm joined by Federico Wengi, who is a Partner at SquareOne VC. In this conversation, Federico sheds light on the conversations he's had with many companies who consider making the pivot from a closed-source business strategy to an open-source strategy. Federico explains why it's so uncommon for businesses to make that pivot, and lays out the challenges businesses face when they consider taking on such a change. Federico also gives a great example of a company that did successfully complete the pivot to open source, and the choices they made that led to their success. Federico and I discuss why this is one pivot you can't take back, and also why it won't solve all your problems. Despite all that, Federico shares his optimism for the value of open source and the importance of at least considering this strategy when you need to make a change. Highlights:Intro (00:00)I introduce Federico, who is a Partner at SquareOne (00:59)Federico describes his role at SquareOne and the areas of investment they focus on (01:28)What Federico typically sees when companies move from closed source to open source (04:42)How important conversations come up about business strategy and open source versus closed source (07:40)Why many companies end up not pursuing an open-source strategy (11:17)Federico tells the story of a company he worked with that made the leap from closed source to open source (15:03)The most critical things businesses have to do in order to utilize an open-source strategy (16:23)What decisions led to success in the company Federico helped shift from closed source to open source (18:09)The psychological challenges leaders face when considering making a pivot to open source (23:54)Federico shares the advice he would give to a founder who's considering an open-source strategy (26:40)How you can connect with Federico (31:40)Links:FedericoLinkedIn: https://www.linkedin.com/in/federicowengi/Twitter: https://twitter.com/federicowengiCompany: https://squareone.vc/
Viongozi wa jumuiya ya Kokwet wali wa andalia wanachama wao hafla maalum, ambako walichangia vyakula, walifanya maonesho ya mitindo nakumaliza sherehe kwa miziki ya asili yao.
Matangazo ya nusu saa kuhusu habari za mapema asubuhi pamoja na habari za michezo.
Ni kawaida kwa wahamiaji na watu walio wasili Australia kama wakimbizi, kujiunga na vikundi vya jumuiya za asili yao.
Wanachama wa Jumuiya ya DR Congo wanao ishi mjini Sydney, walijumuika katika hafla maalum yaku adhimisha miaka 63 ya uhuru wa nchi yao pendwa.
Matangazo ya nusu saa kuhusu habari za mapema asubuhi pamoja na habari za michezo.
Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji (IOM) linaongeza juhudi za msaada wa kibinadamu kwenye mipaka ya Colombia, Costa Rica na Panama ili kusaidia wahamiaji wanaovuka kuelekea eneo la kaskazini mwa Amerika hasa kupitia msitu hatari wa Darien unaounganisha Amerika kusini na kaskazini. Kwa miaka mingi, jimbo la Darien nchini Panama limekuwa kituo cha kawaida cha kupita kwa wahamiaji wanaotoka kusini mwa Amerika kuelekea kaskazini. Takwimu za hivi karibuni za mwaka huu 2023 zinazidi kwa kiasi kikubwa idadi ya juu ya mwaka 2022, wakati watu 258,000 walivuka mwaka mzima. Kwa mujibu wa Mradi wa Wahamiaji Wasiofahamika waliko, wahamiaji wengi hawana vifaa vya kutosha vinavyofaa kwa safari ya siku mbili hadi kumi na karibu wahamiaji 137 walifariki dunia au kutoweka mwaka jana 2022. Luz Santo ni Afisa Mratibu wa IOM akiwa tu punde amewapokea wahamiaji waliovuka mto Chucunaque anasema, “Katika kituo hiki, tunapokea takriban watu 700 hadi 1,000 kila siku, na tunawapa taarifa za msingi kuhusu huduma zinazopatikana kwa ajili yao katika kituo cha mapokezi cha uhamiaji cha Lajas Blancas, na pia taarifa kuhusu njia." Wakati wa safari ndefu msituni, watoto na familia hukabiliwa na aina nyingi za unyanyasaji, ikiwa ni pamoja na unyanyasaji wa kijinsia, unyonyaji, pamoja na ukosefu wa maji salama na chakula, mashambulizi ya wanyama mwitu, na mito inayofurika. Robo tatu ya watu wamejeruhiwa wakiwa safarini, na theluthi moja wamekumbana na aina fulani ya kutendewa vibaya au unyanyasaji, hasa wakati wa kuvuka msitu huo wa Darien, IOM inaeleza. © UNICEF/Eduard SerraMiongoni mwa wahamiaji wapya waliowasili ni Luisa Maria Laya, mama raia wa Venezuela anayesafiri na watoto wake wawili na mumewe. Waliuza kila kitu walichokuwa nacho ili kumudu chakula na sehemu ya njia yako kutoka Venezuela walikuwa wanatumia usafiri wa kuomba msaada njiani. Matumaini yao ni kujiunga na familia ambayo tayari inaishi Marekani, “Tulipoanza safari yetu msituni, ilikuwa ngumu kwa sababu mimi, mume wangu na watoto wangu hatukuwa tumeizoea. Ilikuwa ngumu, kali, na hatari kwa maisha yetu. Namshukuru Mungu tumefika salama. Muhimu ni kwamba tulifika hai kwa sababu watu wengi huko wanadhani ni mchezo. Si mchezo, kinachoendelea si mchezo kujitosa kwenye msitu huo. Ni kitu hatari, hatari. Unahatarisha maisha ya watoto wako na yako mwenyewe.” Wahamiaji wa zaidi ya mataifa 40 wamevuka eneo la Darién mwaka huu. IOM inaeleza kwamba watu hao wanatoka katika mataifa ya Amerika, Asia na Afrika, kama vile Venezuela, Haiti, Ecuador, China, India, Afghanistan, Cameroon, na Somalia. Wengi wao wanatoka Venezuela lakini pia kumekuwa na ongezeko la idadi ya wahamiaji wa Haiti, Ecuador, na Wachina.
Maelfu ya watu wamevuka na kuingia Sudan Kusini wakikimbia mzozo unaoendelea nchini Sudan. Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) liko linawasaidia wanaowasili lakini mzigo huu wa ziada unaweka shinikizo katika shughuli za shirika hilo ambazo tayari ziko katika hali mbaya ya ufadhili.Video iliyoandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) inatupeleka katika Kaunti ya Renk iliyoko kaskazinimashariki mwa nchi ya Sudan Kusini inakopakana na Sudan. Hapa ni kila mtu anajaribu kukumbatia kile alichofanikiwa kutoroka nacho akikwepa mabaya ambayo yangemkumba ikiwa angesalia Sudan ambako tangu tarehe 15 mwezi jana Aprili kunafukuta mapigano makali. Wanaobahatika wanabebwa na magari ya Umoja wa Mataifa, wengine punda na wengine wametembea mwendo mrefu kufika hapa. Kwa mujibu wa WFP, zaidi ya watu 30,000 hadi sasa wamevuka mpaka kutoka Sudan na kuingia Sudan Kusini. Wengi wao ni waliorejea kwani walikimbia madhila hapa Sudan Kusini lakini nako ugenini Sudan kumechafuka, wamerejea. Naimat Khamis, ni mmoja wa waliorejea anasema, "Tulilazimika kuja hapa kwa sababu ya mapigano ya Khartoum…tulilazimika kukimbia haraka iwezekanavyo kwa sababu ya vita…ilikuwa safari ngumu…tunataka kubaki na jamaa zetu hapa kwa sababu tumeteseka sana.” Hassan Abdallaziz, kijana mwenye umri wa miaka 17 huyu yeye ni raia wa Sudan kwa hiyo kwa Sudan Kusini yuko ukimbizi anasema, “Hali ya nchi ilinilazimu kuja hapa. Hakuna kitu kizuri kilichobaki nchini, hakuna kazi, ni machafuko. Mtu yeyote anaweza kupora mali yako, ni kama msitu." WFP tayari inawasaidia waliowasili na wanaowasili ikiwa ni pamoja na kuwapa chakula, kuwapima watoto, wajawazito na wanaonyonyesha, lakini mzigo huu wa ziada unaongeza chumvi kwenye kidonda. Mary-Ellen McGroarty ni Mkurugenzi wa WFP nchini Sudan Kusini akiwa mjini Juba anasema, "Mgogoro huu umekuja katika wakati mbaya zaidi. Unajua nchini Sudan Kusini tunaingia katika msimu wa muambo na msimu wa mvua. Tayari tuna watu milioni 7.4 wanaohitaji msaada wa chakula. Hatuwezi kuwafikia wote kwa sababu ya changamoto za rasilimali. Tumelazimika kupunguza programu zetu kwa sababu ya vikwazo vikali vya ufadhili. Na sasa tena tunalazimika kuweka vipaumbele upya kati ya watu wenye njaa, hawa wapya wanaowasili, ambao wako hatarini sana.”
Watoto milioni 10 nchini Burkina Faso, Mali na Niger wana uhitaji mkubwa wa misaada ya kibinadamu, idadi ambayo ni maradufu ikilinganishwa na mwaka 2020, limesema shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Watoto duniani, UNICEF hii leo, chanzo kikiwa ni mizozo inayoshamiri kila uchao na kwamba Watoto wengine million 4 nchi Jirani wako hatarini Zaidi kwani mapigano kati ya makundi yaliyojihami na majeshi ya serikali yanavuka mipaka.Tuko Benin na sauti ni ya Abasse, Dahani, mtoto mkimbizi mwenye umri wa miaka 8 kutoka Burkina Faso anasema tulikuja hapa Tanguieta Benin kwa mguu. Tulikimbia nyumbani kwa sababu tulifukuzwa.Abasse anawakilisha mamilioni ya watoto wanaokimbia makwao ukanda wa Sahel kwani Mkurugenzi wa UNICEF kanda ya Afrika Magharibi na Kati Marie – Pierre Poirier anasema “watoto wanazidi kukumbwa kwenye mapigano kama waathirika wa mapigano au walengwa kutoka vikundi vilivyojihami ambavyo si vya kiserikali.”Afisa huyo anatolea mfano Burkina Faso akisema watoto waliothibitishwa kuuawa katika miezi tisa ya mwanzo yam waka 2022 walikuwa mara tatu zaidi kuliko mwaka 2021.Wengi wa watoto hao walikufa kutokanana majerara ya risasi, vijiji vyao kushambuliwa au kulipuka kwa vilipuzi vya kutengeneza au masalia ya mabomu yatumikayo vitani. Bi. Poirier amesema mwaka 2022 ulikuwa wa kikatili Zaidi kwa Watoto Sahel ya Kati na hivyo pande zote kwenye mzozo lazima zikomeshe mashambulizi kwa Watoto, shule zao, vituo vya afya na makazi yao.UNICEF inasema mapigano yanazidi kuwa ya kikatili ambapo baadhi ya vikundi vilivyojihami vinaendesha operesheni zao katika maeneo ya Mali, Burkina Faso na Niger ambako wanatumia mbinu kama vile kuweka vizuizi mijini na vijijini na hata kuharibu mitandao yam aji.Kama hiyo haitoshi, UNICEF inasema kutokana na mashabulizi hayo zaidi ya watu 20,000 kwenye maeneo ya mpaka baina ya Burkina Faso, Mali na Niger watakuwa na kiwango cha kutisha cha ukosefu wa chakula ifikapo mwezi Juni mwaka huu.Vikundi vilivyojihami ambavyo vinapinga elimu inayotolewa na serikali vinatia moto majengo ya shule na kupora mali, vinaweka vitisho, vinateka nyara au kuua walimu.Zaidi ya shule 8,300 zimefungwa katika shule zote kwa sababu zilishambuliwa moja kwa moja na walimu kukimbia au kwa sababu wazazi walikimbia au wanahofia kupeleka watoto wao shuleni.Sasa Abasse na familia yake wako Benin na akiwa darasani akiandika anasema “kwa kuwa sasa naenda shuleni, nimepata marafiki. Napenda kifaransa, nazungumza kidogo. Na mwalimu wangu ni mzuri.”UNICEF inasema janga la Sahel ya Kati bado halijapata ufadhili wa kutosha kuweza kufanikisha operesheni zake kwani mwaka 2022 ilipokea theluthi moja tu ya dol amilioni 391 na kwamba mwaka huu imeomba dola milioni 473 kufanikisha operesheni za kiutu Sahel ya Kati na nchi Jirani. TAGS: Usaidizi wa kibinadamuAdditional: Usaidizi wa kibinadamuNews: Sahel ya KatiRegion: AfrikaUN/Tags: UNICEF
Jamii ya mikunde! Wengi wanaitambua zaidi kama ni kunde zenyewe, na maharagwe lakini ni zaidi ya hiyo. Kuna choroko, mbaazi, dengu, njegere na kadha wa kadha ambapo kutokana na umuhimu wake katika lishe ya binadamu, kurutubisha udongo na pia kuhimili mabadiliko ya tabianchi, ndio maana Umoja wa Mataifa unapigia chepuo.Mathalani nchini Tanzania, shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo, FAO linafadhili mradi wa AgriConnect ambao pamoja na mambo mengine unapatia wananchi, wake kwa waume stadi za mapishi sahihi ya jamii ya mikunde.Hivi karibuni wakati wa siku ya mikunde duniani tarehe 10 mwezi huu wa Februari, FAO ilishindanisha washiriki wa mradi huo kufahamu ni nani bingwa zaidi wa mapishi ya mikunde kwa kutambua kuwa Tanzania ni mmoja wa wazalishaji wakubwa wa mikunde lakini ulaji wake bado unachangamoto. Sasa makala hii inamulika harakati za kuchagiza ulaji wa mikunde pamoja na majani yake na mwenyeji wetu ni John Kabambala wa redio washirika Kids Time FM ya Morogoro, Tanzania. Kwako John!
Mkuu wa kanda ya nchi za kiarabu katika shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya watu duniani, na afya ya uzazi, UNFP Leila Baker amesema pamoja na shirika hilo kuhitaji fedha ili kuweza kuwahudumia wanawake na wasichana waliathiriwa na matetemeko nchini Turkiye na Syria lakini kila sehemu anapopita nchini Syria wanawake hutoa ombi moja tu nalo ni kuhitaji amani.Ni Leila Baker huyo, mkuu wa UNFPA katika kanda ya nchi za kiarabu katika mahojiano maalum na Idhaa ya Umoja wa Mataifa akieleza kwa siku nzima amekuwa katika mji wa Aleppo nchini Syria akizunguka kutembelea kliniki zilizoanzishwa na shirika hilo linalohusika na afya ya uzazi na kuzungumza na kila anayehusika katika kukabiliana na dharura iliyoletwa na matetemeko ya ardhi.Bi. Baker anasema ni vigumu sana kwake kueleza kwa sentensi moja au kuchora taswira ya madhila waliyomo wananchi wa Syria kwani madhara si katika miundombinu pekee bali pia kimwili kwani watu hawa kwa takriban muongo mmoja wamekuwa wakihaha kutokana na nchi hiyo kuwa na mizozo na vita.“Kuna majengo ambayo yameanguka, mtaa mzima umebomolewa, lakini kubwa zaidi ni muunganiko wa uchovu mwingi wa watu hawa ambao wamekuwa wakipigania uwepo wao, na sasa wanahisi kwamba wakati huo huo wanaanza kurudi katika matumaini wakiona mwanga mwisho wa handani ukiangaza kuwapa matumaini, janga la asili linatokea. Tetemeko hili kubwa la ardhi limevunja matumaini yao, kama jinsi majengo yalivyobomoka wakati wa tetemeko lenyewe.”Lakini wanawake na wasichana aliokutana nao ni nini hasa wanataka?“Nitakuambia kile hasa nilichowauliza wanawake kila mahali nilipoenda. Nikawaambia, kama ningeweza kuiambia jumuiya ya kimataifa jambo moja, ungeniomba niwaambie nini? Na bila kukosea, katika kila kundi la wanawake, hata awe mtu binafsi au kikundi, ujumbe wao ulikuwa sawa. Imetosha. Tumechoka, na tunachotaka ni upatanisho. Tunataka amani. Na tunatumaini katika wakati huu wa giza nene, itakuwa wakati ambapo mioyo na akili za kila mtu ziko wazi kuwa kuna uwezekano wa amani.”Wengi wa wakimbizi wa ndani nchini Syria ni wanawake na wasichana hivyo hata kabla ya tetemeko la ardhi kulikuwa na mipango kadhaa iliyokuwa ikisimamiwa na UNFPA kwa kushirikiana na wadau wengine ili kusaidia utoaji wa huduma za afya ya uzazi na kukabiliana na unyanyasaji wakijinsia. Na sasa shirika hilo limelazimika kupanua wigo wa huduma zao kwani watu wengi kwa sasa wameweka kuweka makazi ya muda, katika misikiti, shule na bustani ambazo UNFPA imeeleza maeneo hayana vifaa kwa ajili ya wakazi wa kibinadamu kwani wanakosa maji, hawana usafi mzuri wa mazingira, umeme, na nchi hiyo kwas asa ipo katika msimu wa baridi.Nikutokana na hali hiyo ndio maana Bi.Baker amesema UNFPA imetoa ombi la usaidizi ambapo “kwa Uturuki, ni milioni 19.7. Na kwa Syria ni zaidi ya milioni 24.”Mbali na fedha hizo kutumika kwa ajili ya wanawake na wasichana ya nchi hizo mbili lakini pia zitatumika kwa ajili ya wafanyakazi wa UNFPA.“Tutaimarisha watu wetu na uratibu wetu wa kutoa misaada mashinani kwa sababu tuna wajibu wa kuwatunza watoa huduma wetu pia. Naomba usisahau kwamba hawa ni watu ambao, wao wenyewe wamepatwa na kiwewe, na bado wanafanya kazi bila kuchoka usiku kucha. Tuna wafanyakazi ambao wamelala kwenye magari yao kwa siku nane, wakizunguka tu kutoka sehemu moja hadi nyingine baada ya kumaliza kazi na pia kujitolea muda wao. Tunaimani kuwa hiyo itakuwa hatua inayofuata ya kile tunachotowa.”Mkuu huyo wa UNFPA katika kanda ya nchi za kiarabu alihitimisha mahojiano yake kwa kueleza pamoja changamoto lakini pia kuna habari njema na zakutia moyo ikiwemo wakina mama kuweza kuunganishwa na watoto pamoja na wajukuu zao ambao walipoteana baada ya kutokea kwa tetemeko.
Uwepo wa idadi kubwa ya wanawake na wasichana katika sekta ya sayansi ni faida kuwa kwa sekta ya sayansi na jamii kwa ujumla amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres akihimiza kuchagiza wanawake na wasicha kuingia zaidi katika sekta hiyo.Antonio Guterres katika ujumbe wake wa siku ya kimataifa ya wanawake na wasichana katika sayansi ambayo huadhimishwa kila mwaka Februari 11 amesima siku hii ni ya kutanabaisha hesabu rahisi kabisa kwamba “Wanawake na wasichana zaidi katika sayansi ni sawa na sayansi bora. Wanawake na wasichana huleta utofauti katika utafiti, kupanua wigo wa kundi la wataalamu wa sayansi, na kutoa mitazamo mipya kwa sayansi na teknolojia, ikinufaisha kila mtu.”Ujumbe wake umeendelea kueleza kuwa kuna ushahidi unaoongezeka kwamba upendeleo wa kijinsia katika sayansi unasababisha matokeo mabaya zaidi, kuanzia kwenye majaribio ya dawa za ambayo huchukulia mwili wa mwanamke kama wa hali isiyo ya kawaida, kutafuta kanuni zinazoendeleza upendeleo na ubaguzi. Hata hivyo Guterres ameongeza kuwa katika maeneo mengi sana duniani, upatikanaji wa elimu kwa wanawake na wasichana ni mdogo au unakataliwa kabisa.Wanawake wanapotazamia maendeleo katika taaluma za kisayansi, ukosefu wa usawa na ubaguzi unaendelea kuzuia uwezo wao. Kana kwamba hiyo haitoshi ameongeza kuwa “Wanawake ni chini ya theluthi moja ya wafanyikazi katika sekta ya sayansi, teknolojia, uhandisi, na hesabu na kidogo zaidi katika nyanja za kisasa. Mtaalamu mmoja tu kati ya watano wanaofanya kazi kwenye akili bandia ni mwanamke. Ni lazima na tunaweza kufanya juhudi zaidi kuchagiza wanasayansi wanawake na wasichana kupitia ufadhili, mafunzo kwa vitendo na program za mafunzo ambazo zinatoa jukwaa la kufanikiwa.” Katibu Mkuu amehitimisha ujumbe wake akisema kupitia mfumo maalum, vivutio vya kuwafanya wabaki, na programu za ushauri ambazo huwasaidia wanawake kushinda vikwazo vilivyopo na kujenga taaluma vitasaidia sana. Na muhimu zaidi, ameongeza ni kwa kuzsisitiza haki za wanawake na kuvunja mila potofu, upendeleo, na vizuizi vya kimuundo. Na wito wake ni kwamba “Sote tunaweza kufanya sehemu yetu kuibua talanta kubwa sana ya ulimwengu ambayo haijatumiwa tukianza na kujaza madarasa, maabara na vyumba vya bodi na wanasayansi wanawake.”
Kwenye episode hii nimeeleza kwa kina namna ya kuandika ujumbe wa kuomba msaada kwa mtu mwenye followers wengi. Yawezekana ni programmer au mtu mwenye uzoefu kwenye eneo fulani.
APGCITV Anchor.fm from Lancaster Pennsylvania state in America
News RadioPublic APGCITV-USA --- Support this podcast: https://podcasters.spotify.com/pod/show/apostolicpowerofgod/support
Nchini Sudan Kusini mapigano ya kikabila kwenye jimbo la Upper Nile nchini humo yamesababisha vifo, ukimbizi wa ndani halikadhalika madhila zaidi kwa watoto ambao mustakabali wao unazidi kuwa mashakani huku nao wazee wakishuhudia machungu katika taifa hilo changa zaidi duniani.Nats.. Hospitalini Kodok jimboni Upper Nile nchini Sudan Kusini! Taswira kutoka video ya ujumbe wa Umoja wa Mataifa ya kulinda amani nchini humo, UNMISS, ni watoto walio na majeraha! Ya miguu, mgongoni! Wamekata tamaa!! Nyamer Oyac, mwenye umri wa miaka 60 ni mkimbizi wa ndani akiwa na watoto hawa anasema, “tulikimbia kutoka kijiji cha Aburoc na tukaja hapa Kodok. Tulipitia machungu sana kukimbia na kujificha kwenye vichaka, kuvuka mito na mafuriko kwa sababu tulikuwa tunashambuliwa, tunakimbizwa na kupigwa risasi. Tulipovuka mtu, tulikanyaga watoto mamia ya watoto .Kwa bahati mbaya wengi wao walizama na kufa maji. Niliweza kunusuru hawa hapa waliojeruhiwa kwa sababu hakuna mtu anawalea.” Katika hospitali hii ya kiraia ya Kodok, madaktari na wauguzi wanahaha kuhudumia wagonjwa ambao idadi yao inaongezeka kila uchao. Vifaa ikiwamo dawa ni vichache licha ya msaada kutoka mashirika ya Msalaba Mwekundu, na shirika la Umoja wa Mataifa la afya ulimwenguni, WHO. Wagonjwa mahututi wanapelekwa Malakal na Juba. Dkt Emmanuel William Gordon wa hapa Kodok anafafanua akisema, “idadi ya majeruhi tuliopokea, hasa waliojeruhiwa kwa risasi ni 20. Wengi wao wanajificha kwenye madimbwi ya maji kwa zaidi ya siku 10 wakiwa na majeraha ya kuungua au risasi. Hatuna idadi kamili kwani wagonjwa ni wengi. Kwa mujibu wa tuliowapokea, wengi bado wamejificha na hivyo tunatarajia wagonjwa wengi siku zijazo.” Kwa sasa misaada ya chakula imeanza kuwasili ikiwemo kutoka shirika la World Vision, lakini hofu ya wengi ni usalama na viongozi wao wanatoa wito wa kupatikana kwa amani ili waweze kurejea kwenye makazi yao.
Shirika la GLAPD limekuwa likitoa huduma kwa jamii zawatu kutoka ukanda wa Afrika Mashariki na Kati, zinazo ishi nchini AUstralia kwa zaidi ya miaka sita.
Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limesema limesikitishwa na kuongezeka kwa mapigano katika jimbo la Upper Nile nchini Sudan Kusini ambayo umesababisha takriban watu 20,000 kuyahama makazi yao tangu mwezi Agosti, baadhi yao wakilazimika kukimbia hadi mara nne ili kuokoa maisha yao huku mzozo huo ukiendelea. Kwa mujibu wa taarifa ya UNHCR iliyotolewa leo mjini Geneva Uswis na Juba Sudan takriban watu 3,000 tayari wamekimbilia nchi jirani ya Sudan, na hivyo kuzidisha mzozo wa wakimbizi wa Sudan Kusini, ambao ndio mkubwa zaidi barani Afrika. Mapigano yalizuka katika kijiji cha Tonga huko Upper Nile tarehe 15 Agosti 2022. Ghasia zimeenea zaidi katika jimbo la Upper Nile, sehemu za kaskazini za Jonglei na majimbo ya Unity na machafuko yanasambaa sasa katika kaunti ya Fashoda ya Upper Nile na kutishia mji wa Kodok. Mwakilishi wa UNHRC nchini Sudan Kusini Arafat Jamal amesema “Taharuki inaongezeka na watu zaidi wanakimbia wakati machafuko yakishika kasi. Raia wanashambuliwa katika mgogoro huu usio na huruma lazima tuhakikishe ulinzi wao.” Ameongeza kuwa wanawake, watoto na makundi mengine yaliyo katika hatari kubwa ndio idadi kubwa ya waliotawanywa na baadhi ya wazee na watu wenye ulemavu wameshindwa kukimbia na kulazimika kujificha porini na kando yam to Nile wakati wa mashambulizi. Kwa raia wanaokimbia UNHCR inasema ni “Dhahiri wameathirika na wameripoti mauaji, majeruhi, ukatili wa kijinsia, watu kutekwa, uporaji, unyang'anyi na uchopaji wa mali huku wengi wakisema wamepoteza nyumba zao na kutengana na familia zao.” Wakati huohuo jumuioya ya kibinadamu nchini Sudan Kusini imelaani vilaki kuendelea kwa machafuko hayo na kaimu mratibu wa masuala ya kibinadamu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu masuala ya kibinadamu na misaada yad harira OCHA Peter Van der Auweraert akisistiza kwamba "Jumuiya ya kibinadamu nchini Sudan Kusini inasikitishwa na ghasia zinazoendelea ambazo zina athari mbaya kwa uwezo wa watu kuishi na maisha ya wanawake wa kawaida, wanaume na watoto na wale walio hatarini ambao tayari wameathiriwa na hali mbaya ya kibinadamu nchini humo ndio wanaoteseka zaidi.” Hivi sasa UNHCr na wadau wanaongeza juhudi za msaada wa kibinadamu na kuwafikia hata walio maeneo ya vijijini zaidi. “Watu milioni 6.8 Sudan Kusini wanahitaji haraka msaada wa kuokoa maisha kutokana na changamoto mchanganyiko ikiwemo vita, mafuriko, kutokuwepo uhakika wa chakula na kuyumba kwa uchumi.” Na ombi la UNHCR la usaidiazi kwa taifa hilo mwaka 2022 la dola milioni 214.8 hadi kufikia Novemba mwaka huu lilikuwa limefadhiliwa kwa asilimia 46 pekee.
Wakati dunia ikiadhimisha hii leo siku ya kisukari duniani kwa lengo la kuelimisha umma kuhusu ongezeko la mzigo wa ugonjwa huo na mikakati ya kuzuia na kudhibiti tishio lake, bara la Afrika linaonekana kuwa na changamoto kubwa ya ugonjwa huo, kwa mujibu wa takwimu za shirika la Umoja wa Mataifa la afya duniani, WHO. Flora Nducha na taarifa zaidiTakwimu zilizotolewa leo na WHO kanda ya Afrika zinaonyesha kiwango cha changamoto ya ugonjwa wa kisukari Afrika ni kubwa ambapo watu wazima milioni 24 hivi sasa wanaishi na ugonjwa wa kisukari na idadi inatarajiwa kuongezeka kwa asilimia 129 hadi kufikia watu million 55 ifikapo mwaka 2045. Kupitia ujumbe ake wa siku hii Dkt. Matshidiso Moeti mkurugenzi wa WHO Kanda ya Afrika amesema “Mwaka janga ugonjwa wa kisukari ulikatili maisha ya watu 416,000 barani Afrika na ugonjwa huo unatarajiwa kuwa miongoni mwa vyanzo vikuu vya vifo Afrika ifikapo mwaka 2030. La msingi zaidi ni kwamba kisukari ndio ugonjwaa pekee usio wa kuambukiza ambao hatari yake ya vifo vya mapema inaongezeka badala ya kupungua.” Mkuu huyo wa WHO Afrika ameendelea kusema kwamba “Sababu kuu hatari zinazochangia ongezeko la ugonjwa huo Afrika ni pamoja na historia ya familia, ongezeko la umri na sababu zingine maarufu kama uzito wa kupindukia na utipwatipwa, maisha ya kukaa bila mazoezi, lishe isiyofaa, uvutaji wa sigara na unywaji pombe kupita kiasi. Kwa bahati mbaya, sababu hizi za hatari zinazoweza kubadilishwa zinaongezeka katika nchi zote katika Kanda ya Afrika ya WHO.” Dkt. Moeti amesema “Na changamoto kubwa katika juhudi za kukabiliana na ugonjwa huo ni ukweli kwamba zaidi yam to 1 kati ya kila watu wawili barani Afrika anayeishi na kisukari hajawahi kupimwa na hivyo kuongeza fursa za nyenzo za upimaji na dawa kama insulin,ni moja ya maeneo yanayopaswa kufanyiwa kazi haraka.” WHO imeonya kwamba ukiachwa bila kudhibitiwa, na bila usimamizi na mabadiliko ya mwenendo wa maisha, ugonjwa wa kisukari unaweza kusababisha matatizo mengine mengi. Matatizo hayo ni pamoja na mshtuko wa moyo, kiharusi, figo kushindwa kufanyakazi, kukatwa kwa viongo vya mwili kama miguu, ulemavu wa kutoona, upofu, na uharibifu wa mishipa. Limeendelea kusema shirika hilo kuwa watu walio na ugonjwa wa kisukari pia wako katika hatari kubwa ya kupata dalili kali za COVID-19. Dkt. Moeti amesisitiza kuwa “Leo, tunapoadhimisha siku ya kisukari duniani, ninataka kuchukua fursa hii kutoa wito kwa serikali za nchi wanachama kuweka kipaumbele katika uwekezaji wa bidhaa muhimu, kama vile dawa za insulini, macshine za kuangalia kiwango cha sukaru glucometer na sindano zinazotumika kupimia au strips. Hii ni muhimu ili kuhakikisha fursa sawa kwa kila mtu anayeishi na ugonjwa wa kisukari, bila kujali ni wapi aliko katika bara hili.” Pia amezihimiza serikali za Afrika kupitisha na kubinafsisha malengo ya kimataifa ya ugonjwa wa kisukari, kama sehemu ya mapendekezo ya kuimarisha na kufuatilia hatua za ugonjwa wa kisukari ndani ya programu zao za kitaifa za NCD. Siku ya kisukari duniani huadhimishwa kila mwaka Novemba 14 na maudhui yam waka huu kama yalivyokuwa yam waka jana na yatakavyokuwa mwakani ni “Fursa ya huduma za kisukari” yakisisitiza umuhimu wa kuzuia na juhudi za hatua dhidi ya kisukari.
Lengo la vijana wengi wanao cheza mpira wa miguu nchini Australia, nikuwa wachezaji wakulipwa na hata kushiriki katika michuano yakimataifa.
Kila mtu ana story yake kwenye maisha na haijalishi ni wakati mgumu kiasi gani unapitia kwenye maisha yako tambua kila mtu anapitia magumu yake. Lucas Malembo ni mwanzilishi wa "Malembo Farm" inayojishughulisha na maswala yote ya kilimo, Malembo ana amini kua kilimo kinaweza kutengeneza ajira kwa vijana wengi na vile vile kuikuza nchi yetu ki uchumi. Wengi tumemzoea Lucas Malembo akiongelea kilimo mara kwa mara ila kwenye episode hii amegusia mambo aliyopitia kwenye maisha yake kupelekea kuzaliwa kwa "Malembo Farm". Ni matumaini yangu utafurahia mahojiano haya na kujifunza mambo mengi
Mzozo unaozingira swala la ni nani kiongozi halisi wa walio wengi katika bunge la Kenya, umemlazimu Spika wa bunge hilo Moses Wetangula kumteua Naibu Spika Gladys Boss kwa muda mfupi, kusimamia kamati ya kuratibu shughuli za bunge ili kusitisha usambaratishaji wa shughuli za taasisi hiyo.
Wengi wao hata hivyo wanasema kwamba wanahitaji kuwezeshwa katika kujifunza lugha za wenyeji , pamoja na kusaidiwa kwenye program kama za uangalizi wa watoto, wakati wakitafuta ajira.
Evarist Mapunda ni moja wa makocha wangu wa maisha haya ninayoishi sasa hivi, ananifahamu toka nikiwa na miaka 17 mpaka sasa hivi ingawa hapa katikati baada ya ‘kuwa mkubwa' nilipoteana nae kwenye mahangaiko ya kujitafuta na kutafuta maisha. Ila Mimi na yeye tunajua kila mmoja wetu ni mtu wa aina gani na anamaanisha NINI kwa mwengine. Ukiwauliza watoto na wakubwa wengi wa Upanga watakuambia nini yeye pia anamaanisha kwenye maisha yao, lazima atakua na simulizi kuhusu mwalimu huyu hodari wa basketball na maisha, kama hadithi hiyo itakua haimhusu yeye directly badi itakua inamhusu Ndugu yake au mtoto wake au hata rafiki yake, na kama itakua hana hao wote basi hata ya kusikia atakua nayo. Coach Evarist ni mmoja ya watu ambao wamesaidia kwa kiasi kikubwa mno vijana wa miaka ya 2000 kuwa na HESHIMA ya maisha, Heshima ya kazi na miili yao, kama umepita kwenye mikono yake basi utakua unajua hilo. Na kama ule usemi wa Kiswahili unaosema ‘majuto ni mjukuu' basi ndo faida za yale alotufundisha sisi tunayaona. Tunayaona baada ya kukua maana wakati anatufundisha heshima ya muda na drills ngumu za basketball tulikua tunaona anatuonea sana sana. Binafsi nilikua naona hivyo, nilikua naona kama hanipendi maana kila mara yuko kwenye shingo yangu kuniambia lipi sijafanya vizuri. Sasa hivi nikikaa na kujiuliza kipi hasa kilinifanya nihame Pazi na kwenda kucheza basketball yangu Don Bosco ukiachana na kwamba rafiki zangu wengi walikua kule sasa ndo jibu linakuja kwamba Coach Evarist naye alichangia kwa kiasi kikubwa mimi kuamua hilo. Alikua kijana, mwenye kuujua mchezo na Don Bosco Queens ilikua ni moja ya team BORA zaidi za wasichana kuwahi kutokea miaka hiyo. Wengi wao nilikua aidha nimesoma nao Makongo au nimeenda nao Umiseta mara kadhaa kwahiyo maamuzi yangu hayakua ya kuwaza sana ingawa Pazi ndo ilikua nyumbani kwetu na itaendelea kuwa hivyo. Coach Evarist pia ashawahi kukutana na mitihani kadhaa mikubwa katika maisha yake, ingawa wa yeye kupata ajali mbaya ya gari mwanzoni mwa miaka ya 2000 itaendelea kusimama kuwa mtihani mkubwa zaidi ambao amewahi kukabiliana nao, ukiachana na fainali tele ambazo yeye kama mchezaji au kocha ambazo zilikua dhidi ya timu ngumu na akawahi kushinda, huu ulikua wa aina tofauti sana. Alikua peke yake usiku wa manane wakati anaenda zake nyumbani baada ya kumaliza majukumu yake aliyojiongezea ya basketball ndo mtihani huo ulipomkuta, Coach Evarist anakumbuka idadi ya watu ambao walimzunguka na kumpiga vibaya baada ya ajali hiyo. Mungu pekee ndo anajua alimuokoa okoa vipi katika lile na kwenye operesheni zake zaidi ya kumi na tano ambazo amezifanya mpaka sasa hivi zinamfanya aishi na kwanini haya yote yametokea. Coach Evarist ni muaminifu na mwingi wa imani, mpaka leo hii anaendelea kuishi maisha yake kama hakuna ambalo limemtokea na kubadilisha maisha na muonekano wake kwa maisha yake yote. Yule ambaye anakua na moyo kama ambao Coach Evarist anao pekee ndiye anayeweza kuishi kama ambavyo yeye anaishi. Ndo maana yeye ni wa kipekee sana. Yangu matumaini maongezi yetu juu ya heshima na mustakabali wa mpira wetu wa kikapu na heshima juu ya mambo kadhaa yatakuvutia na kukufunza kitu. Yangu matumaini pia uta enjoy. Love, Salama. --- Support this podcast: https://anchor.fm/yahstonetown/support
Damian Soul ni Superstar na siku ambayo sote tutakubaliana na hiyo statement basi tutaanza kufaidi matunda ya kipaji chake kwa uzuri sana, ila mpaka siku hiyo ifike ni wachache tu ambao wanamuelewa kwa upana huo ndio ambao wataendelea kufaidi kipaji chake kwa nafasi yao. Wale watu wa makampunj mbali mbali kwa mfano CocaCola ambao wanakua na events zao za ndani kwaajili ya watu wao na waalikwa wawili watatu huwa wanamfaidi sana kijana huyu hodari wa ki Tanzania. Na Damian kwa ukali wake akipata nafasi kama hiyo huwa hafanyi makosa hata kidogo, huhakikisha anapeleka mziki wote kwao ili wakati mwengine wanapokua na event basi jina lake liwe la kwanza kwenye list ya waburudishaji wao. Mzaliwa wa Dar es Salaam, mtoto wa Sinza kabisa, Damian amezaliwa kwenye familia ya kishua kabisa, jinsi ambavyo unaona anavaa ki nadhifu vile ukiachana na hereni zake, hivyo ndivyo Marehemu Mzee wake alivyokua ananyuka, nadhifu kabisa. Koti imenyooka na ilivaliwa inakaa hasa mahala pake, kiatu inang'aa vizuri baada ya kuipiga kiwi mwenyewe, Damian anakumbuka unadhifu huo na ki uhakika ameurithi na kuuendeleza. Shule kwake ilikua ni kitu tu ambacho ilibidi akifanye kwasababu pengine kila mtu au mtoto kwa matakwa ya wazazi ilibidi afanye hivyo na ili aweze kutoka pale alipokua ilibidi afunge mabegi yake mpaka Kampala nchini Uganda, kama utakumbuka vizuri kuna miaka ya kati ya 2000 hapo ilikua kama ‘fashion' kwa watoto wa ki Tanzania kwenda kusoma kule, kwa khadithi nyingi nilizo zisikia wengi wao walikua sio waingiaji sana class na badala yake maisha ya ku party na kujitafuta na kujielewa ndo yalikua ki hivyo zaidi. Haikua tofauti pia kwa Damian Soul, Ila yeye sio kwenye ku party ila kwenye kujitafuta na kujua kwamba muziki ndo kitu alitaka kufanya kwa maisha yake yote. Anakumbuka mti ambao alikua anakaa chini yake na ‘kulicharaza' sana gitaa na kila aliyekua anapita pale habari alikua nayo. Upekee wake wa kuanzia sauti mpaka style yake ya mavazi ndo unaomtofautisha yeye na wengine, ukimuona tu utajua kama ni Star maana jinsi ambavyo anajibeba ni tofauti na watu wengine. Hii pia inasababisha watu kujiuliza maswali kuhusu maisha yake na vitu apendavyo kama mtoto wa kiume. Yeye kwa mujibu wa maongezi haya na mengine ambayo mimi na yeye tushawahi kuwa nayo hayamsumbui kabisa. Anajiheshimu na kujielewa na pia anajua mipaka iko wapi. Na pengine kama binadamu tunatakiwa kuwaacha watu wawe wao, especially kwasababu hayo ni maisha yao, na kwa heshima na taadhima wanajua jinsi ya kujibeba kama binadamu na zaidi kama mTanzania. Anakumbuka jinsi ambavyo alikua Sinza hasa baada ya Baba yake kutangulia mbele ya haki, anasema mtaani palikua pa moto sana kwa kugumbikwa na wimbi la vijana kujihusisha na vitendo vya kihuni na wizi na kujikita kwenye matumizi mazito ya madawa ya kulevya. Anasema yeye alifanikiwa kukimbilia kanisani wakati anasubiria mambo yake mengine ya shule yakae sawa. Kanisani ambako alijifunza mambo ya muziki ikiwa pamoja na kujifunza kupiga instruments, ukiachana na sauti yake ya kipekee, Damian pia ni mpiga gitaa mzuri sana na muandishi hodari pia wa ngoma zake. Mimi ni mmoja wa mashabiki wake na binafsi nilichukua nafasi hii ili tukae chini na tuyajenge kama familia na watu wengine pia wapate nafasi ya kumskiliza na kumuelewa vizuri. Wengi wamekua wakimhukumu kwasababu tu ya muonekano wake na kama Dada na rafiki niliona kuna umuhimu wa sisi kupata nafasi ya kukaa chini na kumfahamu kinaga ubaga. Kama binadamu wote tulivyo, kila mmoja wetu ana mitihani yake ambayo anapitia, mengine mpaka leo inaendelea na mengine ilikua tunafaulu na mengine kufeli, ila kupitia huko ndo ambako kumetufanya tuwe bora na wapya na kujifunza ni jinsi gani mmoja anaweza kutengeneza maisha yake na akawa mfano bora kwa familia na jamii ambayo imemzunguka. Kama mtoto kwa Mama yake na kioo cha jamii, Damian yuko humble sana na wala hana papara kwenye kuhakikisha anafika pale ambapo anapaona kuna kitu cha yeye kuweza kukaa. Mpaka sasa hayuko pabaya hata kidogo --- Support this podcast: https://anchor.fm/yahstonetown/support
Ikiwa leo dunia inaadhimisha siku ya kimataifa ya kuelimisha jamii kuhusu watu wenye ualbino, Umoja wa Mataifa umetoa rai kwa nchi zote duniani kuwajumuisha watu wenye ualbino katika mijadala na mipango inayoathiri haki zao za kibinadamu, ili kuhakikisha wanafurahia usawa na ulinzi unaotolewa kwao katika sheria na viwango vya kimataifa. Kauli mbiu ya maadhimisho hayo kwa mwaka huu inasema ”Tuungane pamoja kufanya sauti zetu zisikike” ikihamasisha haja ya kufanya kazi pamoja na kujenga ushirikiano ili kukabiliana na changamoto za haki za binadamu zinazowakabili watu wenye ualbino. Mtaalam Huru wa Umoja wa Mataifa kuhusu ualbino Muluka-Anne Miti-Drummond amesema kupitia taarifa yake aliyotoa leo mjini Geneva Uswisi kuwa sehemu za kufanya maamuzi kuanzia ngazi za kimataifa, kitaifa , kijamii na hata katika sekta binafsi kumekosa uwakilishi wa watu wenye ualibino na hivyo wanashindwa kushiriki katika mijadala ya kufanya maamuzi na hali hiyo inaweza kusababisha ukiukwaji wa haki zao za kibinadamu. Amesema, “ni ubaguzi wa kimuundo na ukosefu wa usawa wa kihistoria. Hakuwezi kuwa na usawa bila kujumuishwa kwa sauti za walio hatarini zaidi. Ikiwa hatutajumuisha watu wenye ualbino katika majadiliano na maamuzi, tunaendeleza ubaguzi wa kimuundo na ukosefu wa usawa wa kihistoria.” Hata hivyo ametoa pongezi akisema, "Tunasherehekea watu wenye ualbino leo kwa sababu tumeona ujasiri wenu na bidii. Tumeona ongezeko la idadi ya watetezi na wapiganaji wa haki za binadamu wenye ualbino, wengi wao ambao wameanzisha mashirika ya kirai wakati waliona haja ya uwepo wa watu wa kuleta mabadiliko. Wengi wenu mmefanya kazi bila kuchoka kukabiliana na mizizi ya unyanyapaa na mauji ya watu wenye ualbino ikiwemo kukabiliana na dhana potofu hatari kupitia kampeni za kuelimisha kwa kuchagiza ufikiaji wa huduma za afya na raslimali na kuhakikisha ujumuishaji katika shule na maeneo ya kazi ili kuongeza nafasi za watu wenye ualbino kupata mbinu za kujipatia kipato endelevu." Maadhimisho ya siku ya kimataifa ya kuelimisha jamii kuhusu watu wenye ualbino mwaka huu pia yanasherehekea kazi zilizofanywa na vikundi vya wenye ualbino katika kupaza sauti zao nakuhamasisha kuendeleza mshikamano wakati wakiendelea kupambana kuhakikisha sauti zao zinasikika.