Podcasts about serikali

  • 35PODCASTS
  • 710EPISODES
  • 15mAVG DURATION
  • 5WEEKLY NEW EPISODES
  • Sep 16, 2026LATEST

POPULARITY

20192020202120222023202420252026


Best podcasts about serikali

Latest podcast episodes about serikali

Habari RFI-Ki
DRC : Upinzani wapinga mpango wa serikali kubadili katiba

Habari RFI-Ki

Play Episode Listen Later Sep 16, 2026 9:50


Upinzani nchini DRC wapinga mpango wa serikali kurekebisha katiba Shabarikiliza maoni ya mskilizaji .

afrika drc eac serikali katiba
MAELEZO PODCASTS
Tahadhari ya Mvua za El Niño Kuanzia Oktoba, 2026

MAELEZO PODCASTS

Play Episode Listen Later Aug 31, 2026 56:17 Transcription Available


Kufuatia tahadhari iliyotolewa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) juu ya uwepo wa mvua kubwa za El Nino, kupitia Maelezo Podcast ili kupata ufafanuzi tumezungumza na Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dkt. Ladislaus Chang'a ambaye anaeleza kuhusu mvua hizi zinavyotokea na tahadhari za kuchukua.Support the showMsemaji Mkuu wa Serikali

el nino tma dkt serikali oktoba mamlaka
MAELEZO PODCASTS
Aina Tatu za Saratani Zinazoathiri Maisha ya Wengi Nchini.

MAELEZO PODCASTS

Play Episode Listen Later Aug 29, 2026 51:23 Transcription Available


Katika kujenga uelewa kuhusu ugonjwa wa saratani, kupitia Maelezo Podcast tumemualika Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Saratani kutoka Taasisi ya Saratani ya Ocean Road (ORCI), Dkt. Chrispin Kahesa, tumezungumza kuhusu saratani na namna inavyoathiri makundi mbalimbali katika jamii, jitihada za kuzuia na tiba ya saratani.Support the showMsemaji Mkuu wa Serikali

aina tatu maisha katika dkt wengi serikali
SBS Swahili - SBS Swahili
Taarifa ya Habari:Australia yatoa kifurushi cha usaidizi cha dola milioni 5 kwa jamii zilizoathiriwa nchini Nepal

SBS Swahili - SBS Swahili

Play Episode Listen Later Aug 28, 2026 14:52


Serikali ya Australia inaanzisha kifurushi cha usaidizi cha dola milioni 5 kwa jamii zilizoathiriwa nchini Nepal, huku idadi ya Waaustralia waliopotea ikiongezeka hadi 39.

Habari RFI-Ki
DRC : Serikali na waasi wa M23 wakubaliana

Habari RFI-Ki

Play Episode Listen Later Aug 24, 2026 9:54


Serikali ya DRC na waasi wa AFC/M23 wamebaliana kuhusu mpango wa mazungumzo ya amani, hatua inayotoa nafasi ya kutekelezwa kwa mkataba wa amani wa Doha na Washington, ili kumaliza vita mashariki mwa nchi hiyo. Skiza maoni ya mskilizaji.

Habari RFI-Ki
DRC : Serikali na waasi wa M23 wakubaliana

Habari RFI-Ki

Play Episode Listen Later Aug 24, 2026 9:54


Serikali ya DRC na waasi wa AFC/M23 wamebaliana kuhusu mpango wa mazungumzo ya amani, hatua inayotoa nafasi ya kutekelezwa kwa mkataba wa amani wa Doha na Washington, ili kumaliza vita mashariki mwa nchi hiyo. Skiza maoni ya mskilizaji.

MAELEZO PODCASTS
Changamoto ya Afya ya Akili, ni Akina Nani Waathirika Zaidi?

MAELEZO PODCASTS

Play Episode Listen Later Aug 21, 2026 64:45 Transcription Available


Kupitia Maelezo Podcast tunajadili kuhusu afya ya akili kwa kumualika Daktari Veronica Lyimo, Bingwa wa Afya na Magonjwa ya Akili kutoka Taasisi ya Afya ya Akili Tanzania, ambaye anatupitisha kwenye visababishi vya changamoto ya afya ya akili, dalili, utofauti wa ugonjwa wa akili na changamoto ya afya ya akili na namna ya kukabiliana na changamoto hizo.Support the showMsemaji Mkuu wa Serikali

Habari za UN
Licha ya changamoto mijini, Somalia yafanikisha kampeni ya chanjo ya polio

Habari za UN

Play Episode Listen Later Aug 17, 2026 2:43


Zoezi la siku tano la utoaji chanjo dhidi ya polio limekamilika katika mkoa wa Banadir nchini Somalia, likiwafikia watoto zaidi ya 122,000 walio chini ya umri wa miaka mitano. Kampeni hiyo imeendeshwa kwa ushirikiano wa Serikali ya Somalia, mashirika ya Umoja wa Mataifa na wadau wengine. Tupate taarifa zaidi kutoka kwa Flora Nducha.(TAARIFA YA FLORA NDUCHA)Kampeni hiyo imetekelezwa katika wilaya za Daynile, Garasbaley na Kahda, ambako kuna familia nyingi zilizolazimika kuyakimbia makazi yao na ambazo imekuwa vigumu kuwafikia watoto wao katika kampeni zilizopita.Kwa muda wa miezi mitatu, Wizara ya Afya ya Somalia, utawala wa mkoa wa Banadir, Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani WHO, Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto UNICEF na wadau wengine walifanya maandalizi ya kina ili kuwafikia watoto walio hatarini zaidi.Katika utekelezaji wake, timu 178 zilitumwa kutoa chanjo ya matone dhidi ya polio nyumba kwa nyumba, katika vituo maalumu, maeneo ya vituo vya mpito na kupitia timu zinazohamahama.Timu hizo zilitumia takwimu za idadi ya watu, ramani za kijiografia na taarifa kutoka maeneo husika kutambua makazi na watoto ambao hawajapata chanjo.CHANGAMOTO MIJINIKatika taarifa yake kutoka Mogadishu nchini Somalia, WHO imeeleza  kuwa kufikia kila mtoto katika maeneo ya mijini bado ni changamoto.Mkoa wa Banadir unapokea watu wengi wanaokimbia maeneo mengine kutokana na ukosefu wa usalama nchini Somalia. Baadhi yao huishi katika makazi yasiyo rasmi na kuhama mara kwa mara, hali inayofanya iwe vigumu kuwatambua na kuwafuatilia watoto ambao hawajapatiwa chanjo.Licha ya changamoto hizo, watoto 122,067 walipatiwa chanjo, sawa na asilimia 94 ya lengo la awali. Juhudi zinaendelea, watoto waliokosa chanjo watatafutwa na kupatiwa huduma hiyo haraka.Mwakilishi wa WHO nchini Somalia, Dkt. Mohamed Ali Kamil, amesema “Kumfikia kila mtoto kunahitaji uongozi imara wa serikali, ushiriki wa jamii na ushirikiano madhubuti wa wadau wote. Kampeni hii ni fursa muhimu ya kujaribu mbinu inayolenga zaidi mahitaji na kuimarisha uwajibikaji katika utoaji chanjo mijini.”KWA NINI CHANJO YA POLIO?Chanjo hiyo ni muhimu kwa sababu polio inaweza kusababisha ulemavu wa kudumu, lakini pia inaweza kuzuilika kwa chanjo.Somalia imekuwa ikikabiliana na mlipuko wa polio tangu mwaka 2017, hivyo kumfikia kila mtoto ni hatua muhimu katika kuziba pengo la kinga, kukomesha maambukizi na kulinda kizazi kijacho.

somalia polio mogadishu umoja kwa katika afya timu dkt mataifa serikali baadhi shirika wizara kampeni
Habari za UN
FAO yawezesha wanawake na vijana katika sekta ya mwani Zanzibar

Habari za UN

Play Episode Listen Later Aug 17, 2026 2:22


Nchini Tanzania hususan visiwani Zanzibar, Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo, (FAO) tangu mwaka 2019, kwa kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wanaimarisha sekta ya mwani, kwa kuwekeza katika mafunzo yanayolenga kuongeza uzalishaji, tija na kipato. Miongoni mwa walionufaika zaidi ni vikundi vya wanawake, ambavyo vimejengewa uwezo kuhusu mbinu bora za uzalishaji, uanikaji na uhifadhi wa mwani, pamoja na kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya tabianchi. Assumpta Massoi anatuletea taarifa inayomhusu mnufaika mmoja wa mafunzo hayo.(Taarifa ya Assumpta Massoi)Jumla ya vikundi 33 vya wanawake vimewezeshwa kwa chanja bora za kuanikia mwani na maturubai maalum ya kuufunika wakati wa mvua.Aidha, wanawake wamejengewa uwezo kuhusu teknolojia ya kilimo mchanganyiko inayowawezesha kulima mwani sambamba na kufuga majongoo bahari.Teknolojia hii inalenga kuongeza tija, kuboresha matumizi ya rasilimali za bahari na kuwawezesha wanawake kupata vyanzo mbalimbali vya kipato.FAO pia imewawezesha vijana kupitia Zanzibar Technology and Business Incubator (ZTBI), kwa kuwapatia mafunzo kuhusu usindikaji, ubunifu na uongezaji thamani wa bidhaa za mwani. Mafunzo hayo yamejikita pia katika uboreshaji wa ubora, upatikanaji wa ithibati na masoko, huku vijana wakipatiwa vifaa vya kuendeleza uzalishaji na ujasiriamali katika sekta ya mwani.

zanzibar fao umoja sekta katika vijana wanawake mataifa serikali shirika teknolojia miongoni
MAELEZO PODCASTS
Kwanini ni marufuku kutunza kwa kutupa fedha chini?

MAELEZO PODCASTS

Play Episode Listen Later Aug 17, 2026 57:38 Transcription Available


Mazungumzo na Bw. Atufigwege Mwakabalile, Afisa Mwandamizi wa Benki kutoka Benki Kuu Tanzania (BOT) kuhusu sheria ya fedha nchini na marufuku iliyotilewa ya kutotunza fedha kwa kutupa chini.Support the showMsemaji Mkuu wa Serikali

bw chini serikali fedha
SBS Swahili - SBS Swahili
Taarifa ya Habari:Ripoti ya mwisho kuhusu mabadiliko yaliyopendekezwa na Serikali kwa Mpango wa Kitaifa wa Bima ya Ulemavu itawasilishwa Bungeni

SBS Swahili - SBS Swahili

Play Episode Listen Later Aug 14, 2026 15:52


Ripoti ya mwisho kuhusu mabadiliko yaliyopendekezwa na Serikali kwa Mpango wa Kitaifa wa Bima ya Ulemavu itawasilishwa Bungeni leo. Uchunguzi huo ulizinduliwa katika mwezi Mei ili kuchunguza mapendekezo ya Serikali, ya kuokoa karibu dola bilioni 38 kwa kipindi cha miaka minne.

bima habari serikali ripoti
SBS Swahili - SBS Swahili
Makala Leo:Serikali kuwekeza mamilioni katika nyumba za waathiriwa wa unyanyasaji wa majumbani; lakini je, inatosha?

SBS Swahili - SBS Swahili

Play Episode Listen Later Aug 14, 2026 11:36


Mgogoro wa makazi ukiendelea, vurugu za kifamilia na majumbani (DFSV) ndio sababu kuu ya wanawake na watoto kuondoka nyumbani kwao na kukosa makazi.

makala katika lakini serikali nyumba
SBS Swahili - SBS Swahili
Taarifa ya Habari:Serikali yawahakikishia watu kwamba Sensa itakuwa salama

SBS Swahili - SBS Swahili

Play Episode Listen Later Aug 11, 2026 13:24


Serikali inawahakikishia watu kwamba Sensa itakuwa salama, kufuatia visa vya hivi karibuni vya roboti za AI kufanya ujambazi na uvunjaji wa data katika mashirika makubwa.

SBS Swahili - SBS Swahili
Taarifa ya Habari:Wafanya biashara waomba ushirikiano na serikali kabla ifanye mabadiliko katika uhamiaji

SBS Swahili - SBS Swahili

Play Episode Listen Later Aug 10, 2026 6:09


Vikundi vya wafanyabiashara vinaihimiza serikali ya shirikisho kushirikiana nao, katika mashauriano kabla ya mabadiliko yoyote makubwa kutangazwa kuhusu sera ya uhamiaji.

katika habari biashara kabla serikali
Gurudumu la Uchumi
Sehemu ya Pili: Hatifungani ni nini na kwanini inakuhusu

Gurudumu la Uchumi

Play Episode Listen Later Aug 5, 2026 10:03


Mara kadhaa tumesikia serikali zetu zikitangaza kuwa zinauza hati fungani za Serikali za muda mfupi na muda mrefu, yaani Government Bonds na Treasury bill, serikali zikikusanya mabilioni ya fedha kutoka kwa wawekezaji. Sasa je, hatifungani ni nini? Je, mwananchi wa kawaida anaweza kuwekeza?

treasury nini pili sasa eac government bonds sehemu serikali
Gurudumu la Uchumi
Sehemu ya Pili: Hatifungani ni nini na kwanini inakuhusu

Gurudumu la Uchumi

Play Episode Listen Later Aug 5, 2026 10:03


Mara kadhaa tumesikia serikali zetu zikitangaza kuwa zinauza hati fungani za Serikali za muda mfupi na muda mrefu, yaani Government Bonds na Treasury bill, serikali zikikusanya mabilioni ya fedha kutoka kwa wawekezaji. Sasa je, hatifungani ni nini? Je, mwananchi wa kawaida anaweza kuwekeza?

treasury nini pili sasa eac government bonds sehemu serikali
MAELEZO PODCASTS
Sheria ya Kuasili Mtoto (Child Adoption) Tanzania

MAELEZO PODCASTS

Play Episode Listen Later Jul 31, 2026 33:44 Transcription Available


Kupitia MAELEZO PODCASTS leo tunazungumza na Bi. Ludovicka Samare, Afisa Ustawi Mwandamizi kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, anatupitisha kwenye utaratibu na Sheria ya kuasili mtoto (Child Adoption), nchini Tanzania Support the showMsemaji Mkuu wa Serikali

bi tanzania sheria jamii maendeleo serikali child adoption wizara
MAELEZO PODCASTS
Elimu ya Hisa, Hati Fungani, Uwekezaji

MAELEZO PODCASTS

Play Episode Listen Later Jul 24, 2026 45:04 Transcription Available


Mazungumzo na Imani Mhingo, Mtaalamu wa Elimu ya Fedha na Mitaji ya dhamana kutoka Benki ya CRDB kuhusu elimu ya hisa; nani anatakiwa kuwa na hisa? uvumi upi usio wa kweli kuhusu hisa? Angalizo na namna ya kutengeneza faida kwa njia ya umiliki wa hisa.Support the showMsemaji Mkuu wa Serikali

hati hisa elimu serikali fedha
MAELEZO PODCASTS
Tiba ya Upandikizaji wa Uume kwa Wanaume

MAELEZO PODCASTS

Play Episode Listen Later Jul 17, 2026 50:17 Transcription Available


Dkt. Rugakingira kutoka Hospitali ya Benjamin Mkapa, Dodoma anatupitisha kwenye huduma hii iliyojizolea umaarufu ya upandikizaji wa uume kwa wanaume wenye changamoto za uzazi. Amejibu kuhusu nani anaweza kupandikiziwa uume, gharama na matarajio baada ya huduma.Support the showMsemaji Mkuu wa Serikali

tiba dkt serikali
SBS Swahili - SBS Swahili
Taarifa ya Habari:Ombi latolewa kuharamisha matamshi ya chuki dhidi yawa Aboriginal na wakaazi wa Torres Strait

SBS Swahili - SBS Swahili

Play Episode Listen Later Jul 16, 2026 5:20


Kuna wito wa kuharamisha matamshi ya chuki dhidi yawa Aboriginal na watu kutoka Visiwa vya Torres Strait, huku vikao vikiendelea katika uchunguzi wa ubaguzi wa rangi wa Serikali ya Shirikisho huko Darwin.

SBS Swahili - SBS Swahili
Taarifa ya Habari:Vyuo vikuu kukabiliwa na faini kubwa vikishindwa kupambana na ubaguzi wa rangi

SBS Swahili - SBS Swahili

Play Episode Listen Later Jul 14, 2026 13:56


Serikali ya Shirikisho inasema vyuo vikuu vinaweza kukabiliwa na faini ikiwa vitashindwa kupambana na ubaguzi wa rangi chini ya viwango vipya vilivyoanzishwa Jumatatu 13 Julai 2026.

MAELEZO PODCASTS
Ukweli Kuhusu Faida za Vyama vya Ushirika

MAELEZO PODCASTS

Play Episode Listen Later Jul 13, 2026 45:52 Transcription Available


Mazungumzo na Mkurugenzi wa Maendeleo ya Ushirika kutoka Shirikisho la Vyama vya Ushirika Tanzania, Bw. Florian Haule kuhusu ushirika na ukweli wake vile umesaidia kuinua uchumi wa Watanzania tangu zamani hadi sasa.Support the showMsemaji Mkuu wa Serikali

bw maendeleo serikali mkurugenzi
MAELEZO PODCASTS
Fursa kwa Watanzania Kuelekea AFCON 2027

MAELEZO PODCASTS

Play Episode Listen Later Jul 10, 2026 39:07 Transcription Available


Kuelekea Michuano ya AFCON 2027 ambayo Tanzania anatarajiwa kuwa mwenyeji wa michuano hii mikubwa Barani Afrika, tumemualika Bw. Allan Allex, Afisa Michezo Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Michezo, Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, ambaye pia ni Afisa Programu wa Baraza la Michezo la Afrika Kanda ya Nne.Tumezungumza kuhusu fursa zilizopo, zinazoendelea kujitokeza na zinazotarajiwa kujitokeza katika michuano hiyo na namna Mtanzania anaweza kunufaika nazo.Support the showMsemaji Mkuu wa Serikali

tanzania afcon bw sanaa baraza habari nne maendeleo serikali michezo wizara
MAELEZO PODCASTS
Siri ya Tarehe 7 Julai na Historia ya Tanzania Iliyowafanya UNESCO kuichagua kuwa Siku ya Kiswahili Duniani

MAELEZO PODCASTS

Play Episode Listen Later Jul 6, 2026 42:49 Transcription Available


Mazungumzo na Profesa Rehema Erasto., Mhadhiri wa Kiswahili kutoka Idara ya Kiswahili, Chuo Kikuu cha Dodoma kuhusu historia ya siku ya Kiswahili Duniani, nafasi ya lugha za kijamii (makabila), makosa kwenye lugha ya kiswahili na namna ya kusahihisha.Mazungumzo haya yanapatikana pia kupitia chaneli ya Youtube ya Maelezo TV.Support the showMsemaji Mkuu wa Serikali

SBS Swahili - SBS Swahili
Taarifa ya Habari:Serikali ya shirikisho yaongeza gharama ya maombi kwa vitengo kadhaa vya visa za Australia kwa asilimia 25

SBS Swahili - SBS Swahili

Play Episode Listen Later Jul 3, 2026 14:08


Ada ya maombi ya visa ya mwanafunzi imeongezeka tangu Julai 1 kutoka $2,000 hadi $2,500, huku Visa ya Muda ya Uzamili, au visa nambari 485, sasa inagharimu $5,750.

MAELEZO PODCASTS
Kwanini Kongamano la Kiswahili Ufaransa na si kwingine? Majibu ya Msemaji Mkuu wa Serikali

MAELEZO PODCASTS

Play Episode Listen Later Jun 29, 2026 29:35 Transcription Available


Gerson Msigwa, Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo; na Msemaji Mkuu wa Serikali akitoa majibu ya ni kwanini Kongamano la Kiswahili la Pili la Kimataifa limefanyika nchini Ufaransa na si kwingineko.Pia tumezungumzia asili ya makongamano ya kiswahili ya kimataifa, fursa na ushiriki wa wananchi katika makongamano haya.Support the showMsemaji Mkuu wa Serikali

pili sanaa kiswahili habari serikali mkuu ufaransa kimataifa michezo wizara
Habari za UN
23 JUNI 2026

Habari za UN

Play Episode Listen Later Jun 23, 2026


Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayoturejesha hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa ambapo Leah Mushi ameketi chini na Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Nassriya Nassir Ali akieleza safari yake ya uongozi wa nafasi za umma kupitia mkalimani wake wa lugha ya alama Tusajigwa Ernest. Pia tunakuletea Muhtasariw a habari na jifunze Kiswahili.Janga la tabianchi linakaribia kwa kasi zaidi kuliko inavyodhaniwa ameonya leo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres, huku akitoa wito wa hatua saba za haraka kupunguza uzalishaji wa gesi chafuzi na kuachana na matumizi ya mafuta ya kisukuku. Akizungumza mjini London kwenye mkutano wa hatua dhidi ya tabianchi, ametaja hatua hizo kuwa ni pamoja na Serikali zichukue hatua madhubuti za tabianchi, dunia iongeze matumizi ya nishati safi, ilinde jamii zilizo hatarini, ihakikishe ufadhili wa haki kwa nchi zinazoendelea, isimamie kwa uwajibikaji matumizi ya teknolojia ya akili mnemba na kupambana na upotoshaji wa taarifa kuhusu tabianchi. Guterres amesema hatua hizo ni muhimu ili kudhibiti ongezeko la joto duniani na kuzuia madhara makubwa zaidi kwa binadamu na mazingira.Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi, UNHCR, limekaribisha makubaliano mapya kati ya DRC na Rwanda ya kusaidia wakimbizi kurejea nyumbani kwa hiari, usalama na heshima. Katika mkutano uliofanyika Addis Ababa Ethiopia, serikali za nchi hizo mbili zimeahidi kuimarisha ushirikiano kwa msaada wa UNHCR ili kuwezesha urejeaji salama wa wakimbizi.Zaidi ya wagonjwa 1,000 vya Ebola wamethibitishwa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, huku watu 254 wakifariki dunia kwa mujibu wa Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa Duniani WHO likiongeza kuwa wagonjwa 100 wamepona, jambo linaloonesha kuwa huduma ya afya ya haraka inaweza kuokoa maisha.Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili hii leo mtaalam wetu Onni Sigalla, Mhariri mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania, BAKITA anafafanua maana za neno "TANUWINI"Mwenyeji wako ni Feissal Kirwa, karibu!

SBS Swahili - SBS Swahili
Taarifa ya Habari:Mpango wa serikali wa kurekebisha NDIS waiweka pabaya bungeni

SBS Swahili - SBS Swahili

Play Episode Listen Later Jun 23, 2026 14:45


Chama cha Greens kimeita mpango wa serikali wa kurekebisha Mpango wa Kitaifa wa Bima ya Watu Wenye Ulemavu kuwa sheria 'isiyo ya kibinadamu'.

SBS Swahili - SBS Swahili
Yaliyojiri Afrika:Kasi yakuenea kwa ugonjwa wa Ebola kwa lazimisha serikali ya Congo kutoa tahadhari

SBS Swahili - SBS Swahili

Play Episode Listen Later Jun 23, 2026 6:07


Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, imetahadharisha umma kuhusu kuenea kwa kasi kwa ugonjwa wa Ebola.

congo afrika ebola kongo kasi jamhuri serikali ugonjwa kidemokrasia
Habari za UN
UN Women na EU waleta matumaini kwa wanawake waathirika wa ukatili viziwani Zanzibar

Habari za UN

Play Episode Listen Later Jun 19, 2026 2:43


Je, maisha yangekuwaje kama kila manusura wa ukatili wa kijinsia angejua mahali pa kupata msaada kwa wakati? Kisiwani Zanzibar nchini Tanzania Shirika la Umoja wa Mataifa la Masuala ya Wanawake (UN Women), kwa ufadhili wa Muungano wa Ulaya (EU) na kwa ushirikiano na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, linaimarisha upatikanaji wa haki na huduma za msaada kwa manusura wa ukatili wa kijinsia, hususan katika maeneo ya pembezoni. Kupitia mradi wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Wasichana Zanzibar na Kuimarisha Uongozi wa Wanawake, manusura wanapata habari muhimu, ushauri nasaha na msaada wa kisheria wakati wowote. Feissal Kirwa na taarifa zaidi.

european union tanzania zanzibar un women gbv umoja wanawake na eu mataifa serikali shirika
Habari za UN
19 JUNI 2026

Habari za UN

Play Episode Listen Later Jun 19, 2026 9:57


Hii leo jaridani tunaangazia wito wa UN wa kulinda mamilioni wa wakimbizi kote duniani, masuala ya kijinsia Zanzibar nchini Tanzania, na ripoti mpya ya Katibu Mkuu wa UN kuhusu watoto katika maeneo ya machafuko imeonesha hali ya kutisha duniani.Kuelekea maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wakimbizi kesho Juni 20, viongozi wa Umoja wa Mataifa wametoa wito wa kuimarishwa kwa mshikamano na hatua za kimataifa za kuwalinda mamilioni ya watu waliolazimika kuyakimbia makazi yao kote duniani kutokana na vita, vurugu na mateso.Ripoti mpya ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu watoto katika maeneo ya machafuko imeonesha hali ya kutisha duniani. Takribani watoto 24,174 waliuawa, kujeruhiwa, kulazimishwa kujiunga na makundi yenye silaha, kubakwa au kuathiriwa kwa namna nyingine na ukiukwaji mkubwa wa haki katika maeneo yenye mizozo mwaka 2025.Je, maisha yangekuwaje kama kila manusura wa ukatili wa kijinsia angejua mahali pa kupata msaada kwa wakati? Kisiwani Zanzibar nchini Tanzania Shirika la Umoja wa Mataifa la Masuala ya Wanawake (UN Women), kwa ufadhili wa Muungano wa Ulaya (EU) na kwa ushirikiano na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, linaimarisha upatikanaji wa haki na huduma za msaada kwa manusura wa ukatili wa kijinsia, hususan katika maeneo ya pembezoni. Kupitia mradi wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Wasichana Zanzibar na Kuimarisha Uongozi wa Wanawake, manusura wanapata habari muhimu, ushauri nasaha na msaada wa kisheria wakati wowote.Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!

tanzania zanzibar gbv umoja hii siku wanawake mataifa serikali kimataifa ripoti
MAELEZO PODCASTS
Kuelekea Kongamano la Pili la Kiswahili la Kimataifa, Paris - Ufaransa

MAELEZO PODCASTS

Play Episode Listen Later Jun 18, 2026 34:12 Transcription Available


Send us Fan MailSerikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) inatarajia kufanya Kongamano la pili la kimataifa la Kiswahili kati ya Julai 4 - 7, 2026, jijini Paris, Ufaransa.Tumezungumza na Bw. Tito Lulandala, Afisa Utamaduni Mwandamizi, kutoka Idara ya Maendeleo ya Utamaduni, na Mwenyekiti wa Kikosi Kazi cha Maandalizi ya Kongamano la Pili la Kiswahili la Kimataifa kuhusu maendeleo ya Kiswahili, fursa zilizopo, ajenda muhimu kuelekea kongamano la pili la kimataifa la Kiswahili nchini Ufaransa, pamoja na mafanikio ya kongamano la kwanza lililofanyika Havanna, nchini Kuba, mwaka 2024.Support the showMsemaji Mkuu wa Serikali

tanzania kuba bw pili umoja havanna kiswahili julai elimu mataifa jamhuri serikali maendeleo shirika ufaransa kimataifa
Habari za UN
12 JUNI 2026

Habari za UN

Play Episode Listen Later Jun 12, 2026 9:59


Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina. Mkutano wa 19 wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Haki za Watu Wenye Ulemavu CRPD, umehitimishwa jana katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani. Watu wenye ulemavu na wadau mbalimbali wa Serikali na Mashirika yasiyo ya Serikali walikusanyika kutoka kila pembe ya dunia kujadili hatua zilizopigwa katika kipindi cha miaka 20 ya Mkataba wa Kimataifa wa Haki za Watu Wenye Ulemavu, CRPD. Mmoja wa waliohudhuria ni Bwana Kibaya Laibuta ambaye licha ya kupoteza uwezo wa kuona akiwa na umri wa miaka 24 alipokuwa mwanafunzi katika Chuo Kikuu cha Nairobi bado alifanikiwa kusonga mbele akamaliza masomo yake ya sheria na masomo mengine ya ngazi za juu na sasa miaka mingi baadaye ni Jaji katika Mahakama ya Rufaa ya Kenya. Siri yake ya mafaniko ndio hasa anaihamasisha kote duniani na anaiweka wazi katika mazungumzo yafuatayo na Anold Kayanda wa Idhaa hii ya Umoja wa Mataifa ili watu wengine wenye ulemavu wafanikiwe kama yeye. Pia tunakuletea muhtasari wa habari zikiwemo za hatua za kupambana na UKIMWI, maambukizi ya ugonjwa wa Ebola hasa kwa watoto DRC, na ujumbe katika siku ya kimataifa ya kupinga utumikishaji wa watoto.Mwenyeji wako ni Rashid Malekela.

new york kenya siri ebola nairobi drc umoja hii haki afya watoto watu crpd mataifa serikali marekani kimataifa mkutano mashirika chuo kikuu
MAELEZO PODCASTS
Fursa, Ushirikiano kati ya Algeria na Tanzania: Balozi Matinyi

MAELEZO PODCASTS

Play Episode Listen Later Jun 12, 2026 7:19 Transcription Available


Send us Fan MailMheshimiwa Balozi Mobhare Matinyi akizungumza mara baada ya kukabidhi hati zake za utambulisho wa kibalozi kwa Mheshimiwa Abdelmadjid Tebboune, Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Algeria, katika hafla iliyofanyika kwenye Ikulu ya Algiers tarehe 10 Juni, 2026. Balozi Mobhare Matinyi anayeiwakilisha Tanzania nchini Algeria, ametoa wito kwa Watanzania kutumia fursa za ushirikiano mzuri baina ya nchi hizi kufaidika katika nyanja mbalimbali.Support the showMsemaji Mkuu wa Serikali

tanzania algeria algiers rais watu jamhuri serikali kidemokrasia
SBS Swahili - SBS Swahili
Yaliyojiri Afrika: Duale "serikali haita shauriana na raia kuhusu karantini ya Ebola"

SBS Swahili - SBS Swahili

Play Episode Listen Later Jun 5, 2026 7:37


Rais wa Kenya, William Ruto, amesema serikali yake inafanya jambo sahihi kwa kuruhusu Marekani kujenga kituo cha karantini ya Ebola nchini humo.

kenya afrika ebola rais raia duale serikali marekani
SBS Swahili - SBS Swahili
Taarifa ya Habari: Upinzani wa mseto wapanga njama yakuzuia kupitishwa kwa sheria ya kodi ya serikali ndani ya Seneti

SBS Swahili - SBS Swahili

Play Episode Listen Later Jun 5, 2026 13:22


Mabadiliko ya kodi ya serikali ya shirikisho yamepitishwa ndani ya nyumba la Wawakilishi - ila, upinzani wa mseto hauja tupilia mbali uwezekano wa muungano na chama cha Greens kuzuia mabadiliko hayo kupitishwa ndani ya Seneti na kuwa sheria.

SBS Swahili - SBS Swahili
Taarifa ya Habari:Chama cha Nationals chataka uchaguzi uitishwe kuhusu hatma ya mageuzi ya kodi ya serikali

SBS Swahili - SBS Swahili

Play Episode Listen Later May 29, 2026 12:41


Chama cha Nationals kimemtaka Waziri Mkuu Anthony Albanese kuitisha uchaguzi mkuu, kuhusu mabadiliko hasi ya kodi ya vifaa na faida ya mtaji yaliyoainishwa katika bajeti ya shirikisho.

SBS Swahili - SBS Swahili
Taarifa ya Habari:Serikali ya Shirikisho ya tetea jibu lake kwa mlipuko wa Diphtheria

SBS Swahili - SBS Swahili

Play Episode Listen Later May 22, 2026 5:14


Waziri wa Afya Mark Butler ametetea utoaji wa kifurushi cha dola milioni 7 kutoka kwa serikali kusaidia kujibu mlipuko wa ugonjwa wa diphtheria ambayo ni maambukizi makubwa ya bakteria yanayoambukiza sana na huathiri njia zakupumua na inaweza sababisha vidonda kwenye mwili pia.Kiwango cha ukosefu wa ajira nchini Australia kimepanda hadi asilimia 4.5, huku kazi 19,000 zikiaondoka katika uchumi mnamo Aprili. Ofisi ya Takwimu ya Australia inasema ongezeko la ukosefu wa ajira imechangiwa na kupungua kwa ajira ya wanawake, kushuka kwa kwanza katika kitengo hicho tangu Agosti 2025.Shirika la Afya Duniani WHO limesema mlipuko wa Ebola ambao tayari umesababisha vifo vya watu 130 nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo huenda ulianza miezi miwili iliyopita.Bonyeza hapo juu kwa taarifa zaidi.

australia lake ebola kongo diphtheria agosti habari waziri jamhuri aprili serikali shirika
SBS Swahili - SBS Swahili
SBS Examines:Nini inaweza fanywa kusimamisha kupandisha bei ya mafuta kwa njia ya unyonyaji?

SBS Swahili - SBS Swahili

Play Episode Listen Later May 21, 2026 12:47


Serikali ya Australia imeanzisha hatua kadhaa za kusaidia kupunguza shinikizo la usambazaji wa mafuta linalo endelea.Hatua hizo zinajumuisha kupunguzwa kwa muda kwa ushuru wa mafuta, na mamlaka zaidi kwa ACCC kupambana na kupandisha bei kwa njia ya unyonyaji.Bonyeza hapo juu kwa taarifa zaidi

australia nini accc njia hatua serikali
SBS Swahili - SBS Swahili
Yaliyojiri Afrika: Seriklai ya DRC kufungua vituo vitatu vya matibabu ya virusi vya Ebola

SBS Swahili - SBS Swahili

Play Episode Listen Later May 19, 2026 7:20


Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imesema Jumatatu itafungua vituo vitatu vya matibabu, kwa ajili ya watu walioambukizwa virusi vya Ebola katika jimbo la Ituri.

afrika ebola kongo ituri jamhuri serikali virusi kidemokrasia
SBS Swahili - SBS Swahili
Taarifa ya Habari: Ghana kuwaondoa raia wake 300 wanaoishi Afrika Kusini

SBS Swahili - SBS Swahili

Play Episode Listen Later May 14, 2026 6:06


Serikali ya Ghana imetangaza kuwa itawarudisha raia wake 300-wanaoishi nchini Afrika Kusini, kufuatia ongezeko la visa vya wageni kushambuliwa.

SBS Swahili - SBS Swahili
Taarifa ya Habari: Ugavi wa nyumba utakuwa muhimu katika bajeti ya shirikisho ya kesho serikali ya sema

SBS Swahili - SBS Swahili

Play Episode Listen Later May 11, 2026 8:00


Waziri wa Makazi Clare O'Neil, anasema bajeti ya shirikisho itasaidia sana kushughulikia upungufu wa usambazaji wa makazi.

sema katika habari waziri serikali nyumba kesho
Habari za UN
Serikali ya Tanzania inajali usawa na haki kwa watu wote kupata huduma kwa usawa - Profesa Malebo

Habari za UN

Play Episode Listen Later May 6, 2026 2:34


Siku tano zilizopita Jukwaa la Kudumu la Umoja wa Mataifa kuhusu Masuala ya Watu wa Asili (UNPFII) limefunga pazia hapa katika makao ya Umoja wa Mataifa  jijini New York, Marekani  baada ya majadiliano ya takribani wiki mbili ya wadau kutoka nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa kuhusu sera, mafanikio na kukabiliana na changamoto mbalimbali katika kuhudumia wananchi wao ikiwemo jamii za watu wa asili. Kwa upande wa Tanzania, mmoja wa walioshiriki ni Katibu Mtendaji wa Tume ya shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni, UNESCO ya Taifa la Tanzania, Profesa Hamisi Masanja Malebo.Feisal Kirwa wa idhaa hii alifanya mahojiano naye kwanza akitaka kufahamu Tanzania ina mikakati gani ya kuhakikisha watu wa asili wanajumuishwa katika huduma za afya kwa wote?

new york tanzania unesco umoja haki kwa siku watu taifa tume wote elimu mataifa serikali marekani jukwaa
SBS Swahili - SBS Swahili
Taarifa ya Habari: Serikali yakana shutuma kwamba inawalenga wawekezaji wa "mama na baba" katika bajeti mpya

SBS Swahili - SBS Swahili

Play Episode Listen Later May 5, 2026 15:28


Jim Chalmers amepuuza mapendekezo kwamba mabadiliko yanayowezekana kwa matumizi hasi ya vifaa au kodi ya faida ya mtaji yatakuwa ni kuvunja ahadi na wapiga kura.

SBS Swahili - SBS Swahili
Taarifa ya Habari: Upinzani waikosoa Serikali ya Madola kwa kuto fanya yakutosha kuimarisha usalama wa taifa

SBS Swahili - SBS Swahili

Play Episode Listen Later May 1, 2026 13:19


Mbunge wa Upinzani Jonathon Duniam amesema Serikali ya shirikisho lazima iende mbali zaidi ili kuimarisha usalama wa taifa, kufuatia kutolewa kwa ripoti ya muda iliyotolewa na Tume ya Kifalme inayochunguza maswala ya chuki dhidi ya wayahudi na Uwiano wa Kijamii.

Habari za UN
30 APRILI 2026

Habari za UN

Play Episode Listen Later Apr 30, 2026 9:59


Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina ambapo tunamsikia Dkt. Tulia Ackson, Rais wa Muungano wa Mabungeni duniani, (IPU) ambaye hivi karibuni akiwa makao makuu ya UN, Marekani aliongoza kikao kilichokuwa sehemu ya Mkutano wa CSW70. Mara baada ya kikao hicho Assumpta Massoi wa Idhaa hii ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa alizungumza naye masuala kadhaa ikiwemo yale waliyopatia kipaumbele ili kusongesha usawa wa kijinsia duniani.Karibu Dkt. Tulia.Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres hii leo saa 3 asubuhi kwa saa za New York Marekani ameeleza kuwa na wasiwasi mkubwa kuhusu suala la kufungwa kwa mlango bahari wa Hormuz wakati mzozo huko mashariki ya kati ukiingia mwezi wa tatu licha ya kuwepo kwa usitishaji mapigano aliouita kuwa ni dhaifu. Katibu Mkuu ameonya kuwa kadri hali inavyoendelea, ndivyo gharama kwa ubinadamu zinavyoongezeka, akisisitiza kuwa nchi zinazoendelea zitaathirika zaidi kutokana na madeni makubwa na kupotea kwa ajira na kuwataka wahusika wote kurejesha mara moja uhuru wa usafiri kama ilivyoainishwa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kupitia Azimio namba  2817.Ripoti mpya ya pamoja iliyotolewa leo na mashirika ya Umoja wa Mataifa yanayohusika na chakula, kilimo na uchumi yakishirikiana na Tume ya Muungano wa Afrika imeonesha kuna pengo kubwa kati ya ufadhili wa sasa wa umma na binafsi wa kilimo na kiwango cha ufadhili kinachohitajika ili kubadilisha mifumo ya kilimo barani Afrika. Ripoti hiyo pia inathibitisha ongezeko linaloendelea la njaa na ukosefu wa uhakika wa chakula kote barani Afrika, ikisisitiza uharaka wa ufadhili mkubwa na endelevu ili kubadilisha mifumo ya kilimo.Na leo ni siku ya kuadhimisha muziki wa jazz duniani, siku inayotukumbusha nafasi ya muziki wa jazz kama daraja la kuleta amani, umoja na mazungumzo kati ya watu wa tamaduni tofauti. Kupitia midundo yake ya kipekee, jazz imeendelea kuwa chombo muhimu cha elimu na ushirikiano, ikiunganisha jamii duniani kote. Serikali, taasisi za elimu, mashirika ya kiraia na watu binafsi huungana kusherehekea mchango wa jazz katika kujenga jamii jumuishi.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!

ethiopia afrika hormuz rais umoja hii kiswahili tume tulia ipu baraza dkt mataifa aprili serikali marekani mkutano ripoti azimio
Habari za UN
22 APRILI 2026

Habari za UN

Play Episode Listen Later Apr 22, 2026 9:50


Hii leo jaridani tunaangazia sitisho la mapigano katika Mashariki ya kati, kilimo endelevu kinachowakwamua wakimbizi na wenyeji Kakuma nchini Kenya, na mafunzo ya UNDP ya uchimbaji salama wa madini ya ujenzi nchini Tanzania.Umoja wa Mataifa umekaribisha tangazo la Rais wa Marekani Donald Trump la kuongeza muda wa sitisho la mapigano kati ya Marekani na Iran, ukisema hiyo ni hatua muhimu kuelekea kupunguza mvutano kati ya mataifa hayo mawili.Maisha ya wakimbizi katika eneo la Kakuma, kaskazini mwa Kenya, yanaanza kubadilika kwa kasi kupitia miradi ya kilimo na lishe inayowezeshwa na mashirika ya Umoja wa Mataifa likiwemo lile la Mpango wa Chakula Duniani  (WFP) na la Chakula na Kilimo (FAO). Kwa ushirikiano na Serikali ya Kaunti ya Turkana chini ya ufadhili wa  Muungano wa Ulaya (EU) sasa wakimbizi wana uwezo wa kuzalisha chakula chao wenyewe, kuboresha lishe, na kujenga maisha ya kujitegemea.Shirika la Umoja wa Mataifa  la Mpango wa Maendeleo (UNDP), kwa kushirikiana na Tume ya Madini nchini  Tanzania katikati mwa wiki iliyopita yaani Aprili 16 na 17 wamefanya warsha ya mafunzo mkoani Singida katikati mwa nchi. Mafunzo hayo yamelenga kuimarisha ujuzi wa uchimbaji salama, unaozingatia sheria, na wenye faida kwa wanawake na vijana wanaojihusisha na uchimbaji mdogo wa madini ya ujenzi.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!

iran kenya tanzania undp rais wfp maisha umoja hii kwa turkana kakuma tume mataifa aprili serikali marekani mashariki shirika kaunti singida
Habari za UN
Kilimo endelevu charejesha matumaini ya kujitegemea Kakuma, Neema aibuka kutoka utegemezi hadi uzalishaji

Habari za UN

Play Episode Listen Later Apr 22, 2026 3:00


Maisha ya wakimbizi katika eneo la Kakuma, kaskazini mwa Kenya, yanaanza kubadilika kwa kasi kupitia miradi ya kilimo na lishe inayowezeshwa na mashirika ya Umoja wa Mataifa likiwemo lile la Mpango wa Chakula Duniani  (WFP) na la Chakula na Kilimo (FAO). Kwa ushirikiano na Serikali ya Kaunti ya Turkana chini ya ufadhili wa  Muungano wa Ulaya (EU) sasa wakimbizi wana uwezo wa kuzalisha chakula chao wenyewe, kuboresha lishe, na kujenga maisha ya kujitegemea. Feissal Kirwa anasimulia.

Habari za UN
20 APRILI 2026

Habari za UN

Play Episode Listen Later Apr 20, 2026 10:44


Hii leo jaridani tunaangazia yaliyojiri katika Jukwaa la Kudumu la Umoja wa Mataifa kuhusu Watu wa Asili hapa Makao Makuu, mafunzo Kenya ya "Social Media 4 Peace" yaani ya kuondoa habari potofu na deepfakes mtandaoni, na mlo shuleni shuleni nchini Tanzania.Jukwaa la Kudumu la Umoja wa Mataifa kuhusu Watu wa Asili (UNPFII) limefungua pazia leo Aprili 20 ikiwa ni kikao cha ishirini na tano hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York, Marekani likiadhimisha miaka 25 tangu kuanzishwa kwake kama jukwaa la kipekee la kimataifa linalowakutanisha wadau kuhusu Watu wa Asili.  Maudhim aka huu yakimulika kuhakikisha afya ya watu wa jamii za asili ikiwemo kwenye mizozo.Ni dhahiri hivi sasa watu wengi zaidi wanatumia mitandao ya kijamii katika shughuli mbalimbali na pia kupata taarifa, na kwakuzingatia ukweli huo, Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni, UNESCO, likishirikiana na Umoja wa wamiliki vya vyombo vya habari vya mtandaoni (Wanablogu) nchini Kenya, BAKE (inatamkwa ‘BEKI'), limeandaa mafunzo maalum jijini Nairobi yaliyopewa jina la "Social Media 4 Peace" yaani mitandao ya kijamii kwa amani. Karibu Rashid Malekela utujuze zaidi.Elimu imeanza kung'aa tena kwa watoto katika kijiji cha Twabagondozi, ambapo njaa iliyokuwa kikwazo kikubwa cha masomo sasa inapungua kupitia mpango wa lishe na malezi bora unaoungwa mkono na shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto, UNICEF Tanzania kwa ufadhili wa Serikali ya Japan. Kupitia juhudi hizi, watoto kama Magdalena A. Prosper wamepata nafasi ya kurejea darasani, kujifunza na hata kuwa viongozi shuleni.Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!

Habari za UN
Lishe yarejesha matumaini ya elimu Kigoma, Magdalena arejea shuleni na kuwa chanzo cha mabadiliko

Habari za UN

Play Episode Listen Later Apr 20, 2026 3:02


Elimu imeanza kung'aa tena kwa watoto katika kijiji cha Twabagondozi, ambapo njaa iliyokuwa kikwazo kikubwa cha masomo sasa inapungua kupitia mpango wa lishe na malezi bora unaoungwa mkono na shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto, UNICEF Tanzania kwa ufadhili wa Serikali ya Japan. Kupitia juhudi hizi, watoto kama Magdalena A. Prosper wamepata nafasi ya kurejea darasani, kujifunza na hata kuwa viongozi shuleni. Feissal kirwa anasimulia.

japan tanzania umoja kuwa elimu mataifa serikali