Podcasts about nchi

  • 50PODCASTS
  • 458EPISODES
  • 15mAVG DURATION
  • 5WEEKLY NEW EPISODES
  • Sep 10, 2025LATEST

POPULARITY

20172018201920202021202220232024


Best podcasts about nchi

Latest podcast episodes about nchi

Habari za UN
Kwa mara ya kwanza watoto wenye utipwatipwa duniani ni wengi kuliko wenye utapiamlo

Habari za UN

Play Episode Listen Later Sep 10, 2025 2:59


Kwa mara ya kwanza idadi ya watoto na vijana wa umri wa kwenda shule wenye unene wa kupindukiaau utipwatipwa imezidi idadi ya watoto wenye utapiamlo duniani ikiathiri watoto milioni 188 sawa na mtoto 1 kati ya kila watoto 10 imesema leo ripoti iliyotolewa leo na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF. Tuungane na Leah Mushi kusikia zaidi kuhusu ripoti hiyo, karibu LeahRipoti hii mpya ya UNICEF iitwayo “Faida kwenye vyakula: Jinsi Mazingira ya Chakula yanavyowaangusha watoto” imechambua takwimu kutoka nchi zaidi ya 190 na kubaini kwamba kiwango cha watoto wenye utapiamlo kimepungua tangu mwaka 2000, lakini wale wenye unene wa kupindukia kimeongezeka mara tatu.Kwa sasa, utipwatipwa umeenea katika kila eneo la dunia isipokuwa Afrika eneo la Kusini mwa Jangwa la Sahara na Asia Kusini. Nchi za visiwa vidogo vya Pasifiki ndizo zinaongoza kwa kuwa na viwango vya juu zaidi, ikiwemo Niue yenye asilimia 38 ya watoto wenye umri wa miaka 5 hadi 19 wakiwa na unene wa kupindukia.Nini kimesababisha?UNICEF inasema mabadiliko ya mifumo ya lishe kutoka vyakula vya asili hadi vyakula vya kutengenezwa kwa haraka na vya bei nafuu lakini vyenye sukari, mafuta na chumvi nyingi ndiyo chanzo kikuu cha ongezeko hili.Pia inatahadharisha kuwa matangazo ya kidijitali ya vinywaji vyenye sukari na vyakula vya viwandani yanawafikia vijana wengi, hata katika nchi zenye migogoro.Mkurugenzi Mtendaji wa UNICEF, Catherine Russell, amesema utipwatipwa ni changamoto kubwa  ya kiafya kwa watoto kwa sababu huongeza hatari ya kupata kisukari, shinikizo la damu na magonjwa ya moyo katika maisha ya baadaye.Russell amesema “Tunapozungumza kuhusu utapiamlo, hatuzungumzii tu kuhusu watoto wenye uzito mdogo, utipwatipwa ni changamoto kubwa inayoendelea kuongezeka ambayo inaweza kuathiri afya na maendeleo ya watoto. Vyakula vya viwandani vinazidi kuongezeka na kuchukua nafasi ya matunda, mboga mboga na protini katika wakati ambao lishe ina jukumu muhimu katika ukuaji wa watoto, ukuaji wa utambuzi na afya ya akili.”Nini kifanyike?Ili kukabiliana na hali hii, UNICEF inazitaka serikali kuchukua hatua madhubuti ikiwemo kupiga marufuku uuzaji wa vyakula visivyo na lishe shuleni, kudhibiti matangazo ya vyakula vyenye sukari na mafuta, na kuweka sera za kusaidia familia kupata chakula bora na chenye lishe.Kwa mujibu wa UNICEF, bila hatua za haraka, gharama za kiafya na kiuchumi zitakazotokana na tatizo la utipwatipwa wa utotoni zinatarajiwa kupindukia dola trilioni 4 kila mwaka ifikapo mwaka 2035.Zipo juhudi za kupambana na hali hiyo ambazo zimeanza kuchukuliwa na baadhi ya nchi, mfano mzuri ni Mexico ambayo hivi karibuni imepiga marufuku uuzaji wa vyakula vilivyosindikwa na vile vyenye chumvi, sukari na mafuta mengi katika  maeneo ya shule za umma.

Habari RFI-Ki
Raia wa nchi za Afrika wapendekeza watu wazima kupewa fursa ya kusoma na kuandika

Habari RFI-Ki

Play Episode Listen Later Sep 10, 2025 9:59


Kila mwaka tarehe 8 Septemba ulimwengu husherehekea maendeleo katika ujuzi wa kusoma na kuandika katika ngazi ya kimataifa, kikanda na kitaifa. Mwaka huu imekuwa ni fursa ya kutafakari kwa kina kuhusu maana ya kusoma na kuandika katika enzi hii ya kidijitali.

Habari RFI-Ki
CHAN 2025: Nchi gani ilipendeza wasikilizaji wetu na maandalizi yalikuwa aje?

Habari RFI-Ki

Play Episode Listen Later Sep 4, 2025 9:58


Michuano ya CHAN imemalizika rasmi mwishoni mwa juma, nchini Kenya, Morocco wakitawazwa mabingwa na Madagascar wakimaliza wa pili.   Kuisha kwa michuano hii ni mwanzo wa maandalizi ya michuano ya AFCON itakayofanyika tena kwenye nchi za Kenya, Uganda na Tanzania mwaka 2027. Tumemuuliza msikilizaji wetu iwapo amefurahia michuano ya mwaka huu? Timu ipi ilikuwa bora kwake na kipi kifanyike kuelekea mashindano ya AFCON 2027.

Habari RFI-Ki
CHAN 2025: Nchi gani ilipendeza wasikilizaji wetu na maandalizi yalikuwa aje?

Habari RFI-Ki

Play Episode Listen Later Sep 4, 2025 9:58


Michuano ya CHAN imemalizika rasmi mwishoni mwa juma, nchini Kenya, Morocco wakitawazwa mabingwa na Madagascar wakimaliza wa pili.   Kuisha kwa michuano hii ni mwanzo wa maandalizi ya michuano ya AFCON itakayofanyika tena kwenye nchi za Kenya, Uganda na Tanzania mwaka 2027. Tumemuuliza msikilizaji wetu iwapo amefurahia michuano ya mwaka huu? Timu ipi ilikuwa bora kwake na kipi kifanyike kuelekea mashindano ya AFCON 2027.

Siha Njema
Utengano wa familia unaweza kuleta shinikizo la damu au kisukari

Siha Njema

Play Episode Listen Later Sep 2, 2025 10:04


Wanadamu ni viumbe ambao hukamilika wanapokuwa kwenye jamii ambapo wanaweza kuelezea hisia zao,kujihisi wanathaminiwa na wana mchango kwa wengine. Mambo  hayo yanapokosa,inaweza kuwa chanzo cha matatizo ya kiafya.Na hii ni hali ambao hukuwa nao wakimbizi ambao wametenganishwa na wapendwa wao. Katika kambi ya Kakuma iliyoko kaunti ya Turkana,kaskazini mwa Nchi ya Wakenya,tulizungumza na wakimbizi ambao walilazimika kutengana na wapendwa wao kwa sababu ya migogoro ya kifamilia,ukoo na hata vita. Ingawa wamepata makao katika kambi ya wakimbizi bado maisha yao hayajakamilika . Wengi wameishi kwenye hali ya upweke,huzuni na kiwewe  na kupata matatizo ya kiafya yakiwemo matatizo ya afya ya akili. Aidha kuna wale ambao wamepatwa na maradhi kama shinikizo la damu ,kisukari,ukosefu wa usingizi na chanzo ni matatizo ambayo wamekumbana nao katika kambi,ugumu wa maisha bila watu walio karibu nawe ambao unaweza kuzungumza nao na kuliwazana. Kamati ya kimataifa ya msalaba mwekundu,ICRC pamoja na shirika la msalaba mwekundu nchini ,KRC,katika kujaribu kukabili hali hiyo ,zinatekeleza mpango wa kujaribu kurejesha mawasiliano na uhusiano wa familia za wakimbizi. Kwa kuwatafuta namna ambao wakimbizi hao wanaweza kuwasiliana kupitia ujumbe wa kuandikiwa au  kwa njia ya simu,mashirika hayo wanasema wamefanikiwa kuwarejeshea tabasamu wachache wenye bahati na wanaendelea kuwasaka wanafamilia zaidi kila mwaka. Matunda ya mpango huo yameonekana miongoni mwa wakimbizi wanaozungumza na jamaa zao na pia kwa wahudumu wa kujitolea wanaotangamana karibu kila siku na wakimbizi hao kwenye kambi.

Habari RFI-Ki
Je timu za nchi wenyeji wa CHAN zimefanyaje kwenye mchuoano wa CHAN 2024?

Habari RFI-Ki

Play Episode Listen Later Aug 26, 2025 10:04


Timu za Kenya Uganda na Tanzania zimeaga mchuano katika hatua ya robo fainali

Habari RFI-Ki
Je timu za nchi wenyeji wa CHAN zimefanyaje kwenye mchuoano wa CHAN 2024?

Habari RFI-Ki

Play Episode Listen Later Aug 26, 2025 10:04


Timu za Kenya Uganda na Tanzania zimeaga mchuano katika hatua ya robo fainali

Nyumba ya Sanaa
Wanamuziki mjini Goma walazimika kufanyia muziki katika nchi jirani

Nyumba ya Sanaa

Play Episode Listen Later Aug 2, 2025 20:06


Mji wa Goma mashariki ya DRC unakabiliwa na changamoto baada ya waasi wa M23 kuuchukua mji huo sasa wanamuziki wanalazimika kwenda nchi jirani kufanya Muziki. Tumezungumza naye msani Sisco laga. 

Habari za UN
Türk ataka Israeli ishinikizwe iondoke maeneo inayokalia ya wapalestina

Habari za UN

Play Episode Listen Later Jul 28, 2025 1:54


Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa haki za binadamu Volker Türk ameyahimiza mataifa yote ulimwenguni kuchukua hatua za haraka ili Israel ikomeshe uwepo wake kinyume cha sheria katika ardhi ya Palestina inayoikalia kimabavu, na kuhakikisha suluhu ya mataifa mawili inapatikana. Tupate taarifa zaidi kutoka kwa Leah MushiKamishna Turk ameyasema hayo katika tarifa yake aliyoitoa kwa njia ya video kabla ya kuanza kwa mkutano wa ngazi ya juu hapa katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York Marekani unaolenga kujadili Suluhu ya kudumu kwa mgogoro kati ya Israel na Palestina ambao umedumu kwa miongo kadhaa sasa.Turk amesema: “Ninahimiza hatua za haraka za Israel kukomesha uwepo wake kinyume cha sheria katika ardhi ya Palestina inayokaliwa kwa mabavu, na kwa pande zote kufanyia kazi maendeleo yanayoonekana kuelekea suluhu ya Serikali mbili.”Akatoa angalizo kwa zile nchi zitakazo shindwa kuweka shinikizo kwa Israel kukomesha mauaji huko katika Ukanda wa Gaza.“Nchi ambazo zinashindwa kutumia nguvu zao zinaweza kuwa na hatia katika uhalifu wa kimataifa. Kila siku tunaona madhila yasiyoelezeka huko Gaza na Ukingo wa Magharibi kwa hofu na kufadhaika. Kila siku, tunaona uharibifu zaidi, mauaji zaidi, na udhalilishaji zaidi wa Wapalestina.”Mkuu huyo wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa amehitimisha video yake ya dakika 4 na sekunda 7 kwa kusema kuwa dunia itaihukumu mikutano ya aina hii kwa kile inachokifanya kwa vitendo, na kuongeza kuwa ofisi yake iko tayari kusaidia taifa la Palestina katika ujenzi wa nchi yenye msingi wa haki za binadamu na utawala wa sheria, pindi utulivu utakapopatikana.

Wimbi la Siasa
Je, mkataba kati ya DRC na Rwanda utaleta amani ya kudumu ?

Wimbi la Siasa

Play Episode Listen Later Jul 2, 2025 10:19


Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Rwanda, walitia saini mkataba wa amani, chini ya uangalizi wa Marekani, Juni Juni 27 2025, jijini Washington DC, unaolenga kurejesha amani ya kudumu Mashariki mwa DRC. Nchi hizo mbili zimekubaliana kushirikiana kuyaondoa makundi yenye silaha. Mkataba huu umepokelewa vipi nchini DRC ?

Siha Njema
Je ni muda wa nchi za Afrika kujadili huduma ya kusaidiwa kufa ?

Siha Njema

Play Episode Listen Later Jul 2, 2025 10:12


Hivi majuzi bunge la Uingereza limepitisha mswada wa kuhalalisha huduma ya kusaidiwa mtu kufa Huduma hii itatekelezwa katika hospitali chini ya usimamizi wa wahudumu wa afya ,kwa watu wazima wanaougua magonjwa yasiyopona . Watalaam wa afya wanasisitiza kuwa hatua hiyo sharti mgonjwa kuridhia bila  kushinikizwa .

Gurudumu la Uchumi
Nchi zinazoendelea kulemewa na madeni: Je, Dunia itasikia kilio chao?

Gurudumu la Uchumi

Play Episode Listen Later Jul 2, 2025 9:52


Hivi Leo tunaangazia suala nyeti linalogusa maisha ya mamilioni ya watu katika nchi zinazoendelea hususani za bara la Afrika, kama vile kwenye mzigo wa madeni unaozidi kuwa mzito. Tunajiuliza Nini hasa kiko hatarini? suluhisho gani linapendekezwa? Kujadili hili tunazungumza na Ali Mkimo, mchambuzi wa masuala ya uchumi na biashara akiwa Tanzania.

Gurudumu la Uchumi
Nchi zinazoendelea kulemewa na madeni: Je, Dunia itasikia kilio chao?

Gurudumu la Uchumi

Play Episode Listen Later Jul 2, 2025 9:52


Hivi Leo tunaangazia suala nyeti linalogusa maisha ya mamilioni ya watu katika nchi zinazoendelea hususani za bara la Afrika, kama vile kwenye mzigo wa madeni unaozidi kuwa mzito. Tunajiuliza Nini hasa kiko hatarini? suluhisho gani linapendekezwa? Kujadili hili tunazungumza na Ali Mkimo, mchambuzi wa masuala ya uchumi na biashara akiwa Tanzania.

Gurudumu la Uchumi
Utakatishaji Fedha: Kenya yawekwa kwenye orodha ya nchi zilizo na changamoto, Uganda ikiondolewa.

Gurudumu la Uchumi

Play Episode Listen Later Jun 26, 2025 10:00


Mwezi Juni mwaka 2025, Tume ya Ulaya iliorodhesha Kenya miongoni mwa nchi zenye changamoto ya utakatishaji wa fedha, huku Uganda ikipata afueni kwa kuondolewa kwenye orodha hiyo. Hatua hii ina maana kuwa mashirika ya kifedha – ikiwemo benki – zinalazimika kuzingatia kwa makini uhusiano wa kibiashara na miamala yoyote inayohusiana na nchi zilizo kwenye orodha hiyo, na kuchukua hatua kali za udhibiti wa fedha. Nchi nyingine katika orodha hiyo ni pamoja na Sudan Kusini, Tanzania, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Msumbiji, Nigeria, Afrika Kusini, na zingine. Katika Makala haya, Gurudumu la Uchumi, tunachambua hatua hii na athari zake kwa uchumi, lakini pia nini mamlaka katika nchi hizo zinaweza kufanya hili kujiondoa kwenye orodha hiyo.

Gurudumu la Uchumi
Utakatishaji Fedha: Kenya yawekwa kwenye orodha ya nchi zilizo na changamoto, Uganda ikiondolewa.

Gurudumu la Uchumi

Play Episode Listen Later Jun 26, 2025 10:00


Mwezi Juni mwaka 2025, Tume ya Ulaya iliorodhesha Kenya miongoni mwa nchi zenye changamoto ya utakatishaji wa fedha, huku Uganda ikipata afueni kwa kuondolewa kwenye orodha hiyo. Hatua hii ina maana kuwa mashirika ya kifedha – ikiwemo benki – zinalazimika kuzingatia kwa makini uhusiano wa kibiashara na miamala yoyote inayohusiana na nchi zilizo kwenye orodha hiyo, na kuchukua hatua kali za udhibiti wa fedha. Nchi nyingine katika orodha hiyo ni pamoja na Sudan Kusini, Tanzania, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Msumbiji, Nigeria, Afrika Kusini, na zingine. Katika Makala haya, Gurudumu la Uchumi, tunachambua hatua hii na athari zake kwa uchumi, lakini pia nini mamlaka katika nchi hizo zinaweza kufanya hili kujiondoa kwenye orodha hiyo.

Habari za UN
FAO/WFP: Nchi 13 katika ongezeko la njaa, 5 kati ya hizo wanakabiliwa na njaa kali zaidi

Habari za UN

Play Episode Listen Later Jun 16, 2025 1:56


Ripoti mpya ya pamoja ya Umoja wa Mataifa inaonya kuwa watu katika nchi 5 kati ya nchi 13 zenye njaa kali duniani wako kwenye hatari kubwa ya kukumbwa na njaa kali, vifo na maafa ikiwa msaada wa kibinadamu hautatolewa haraka na juhudi za kimataifa hazitaelekezwa kukomesha migogoro, kupunguza ufurushwaji na kuongeza msaada wa haraka kwa kiwango kikubwa. Anold Kayanda na taarifa zaidi.

Gurudumu la Uchumi
Mabadiliko ya tabia nchi na matumizi ya teknolojia kwenye kilimo

Gurudumu la Uchumi

Play Episode Listen Later Jun 11, 2025 9:49


Wiki hii katika makala ya Gurudumu la Uchumi, tunajadili namna teknolojia inaweza kutumika katika kukifanya kilimo kuwa cha kisasa. Tumezungumza na Mhandisi Octavian Lasway, mtaalamu wa masuala ya mabadiliko ya tabia nchi na umwagiliaji.

Gurudumu la Uchumi
Mabadiliko ya tabia nchi na matumizi ya teknolojia kwenye kilimo

Gurudumu la Uchumi

Play Episode Listen Later Jun 11, 2025 9:49


Wiki hii katika makala ya Gurudumu la Uchumi, tunajadili namna teknolojia inaweza kutumika katika kukifanya kilimo kuwa cha kisasa. Tumezungumza na Mhandisi Octavian Lasway, mtaalamu wa masuala ya mabadiliko ya tabia nchi na umwagiliaji.

Wimbi la Siasa
Trump azuia raia wa nchi 12 kuzuru Marekani

Wimbi la Siasa

Play Episode Listen Later Jun 11, 2025 10:10


Rais wa Marekani Donald Trump ameagiza raia wa nchi 12 hasa kutoka Afrika kutozuru nchi hiyo. Agizo hilo lilianza kutekelezwa Juni 9, 2025. Trump anasema amechukua hatua hii kwa sababu za kiusalama. Wakati hayo yakijiri, maandamano yamekuwa yakishuhudiwa katika mji wa Los Angeles, kupinga sera ya Trump ya kuwasaka na kuwafukuza nchini humo, wageni wanaoishi bila vibali. Tunachambua kwa kina.

Habari RFI-Ki
Rwanda yajiondoa ndani ya muungano wa mataifa ya Africa ya Kati

Habari RFI-Ki

Play Episode Listen Later Jun 9, 2025 9:54


Leo shaba yetu inalenga nchi ya Rwanda ambapo nchi hiyo imetangaza kujiondoa kwenye Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika ya Kati, na kuituhumu jirani wake DRC, kwa kutumia baadhi ya wanachama kuendeleza ajenda zake zinazokandamiza Rwanda. Skiza makala hay kuskia maoni ya mskilizaji wetu.

Habari RFI-Ki
Rwanda yajiondoa ndani ya muungano wa mataifa ya Africa ya Kati

Habari RFI-Ki

Play Episode Listen Later Jun 9, 2025 9:54


Leo shaba yetu inalenga nchi ya Rwanda ambapo nchi hiyo imetangaza kujiondoa kwenye Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika ya Kati, na kuituhumu jirani wake DRC, kwa kutumia baadhi ya wanachama kuendeleza ajenda zake zinazokandamiza Rwanda. Skiza makala hay kuskia maoni ya mskilizaji wetu.

Habari RFI-Ki
Kauli ya rais wa Tanzania Samia Suluhu kuwazuia wanaharakati wa nchi zingine

Habari RFI-Ki

Play Episode Listen Later May 20, 2025 9:27


Leo tunaangazia ,hatua ya  Tanzania kuwazuia  Mawakili, wanaharakati wa haki za binadamu kutoka nchini Kenya, akiwemo Jaji Mkuu mstaafu Willy Mutunga  waliokwenda kusikiliza kesi ya uhaini inayomkabili kiongozi mkuu wa upinzani Tundu Lissu. Rais Samia Suluhu Hassan, amesema serikali yake haitaruhusu wanaharakati wa kigeni kuingia nchini Tanzania na kuingilia masuala ya ndani ya nchi yake.

Habari RFI-Ki
Kauli ya rais wa Tanzania Samia Suluhu kuwazuia wanaharakati wa nchi zingine

Habari RFI-Ki

Play Episode Listen Later May 20, 2025 9:27


Leo tunaangazia ,hatua ya  Tanzania kuwazuia  Mawakili, wanaharakati wa haki za binadamu kutoka nchini Kenya, akiwemo Jaji Mkuu mstaafu Willy Mutunga  waliokwenda kusikiliza kesi ya uhaini inayomkabili kiongozi mkuu wa upinzani Tundu Lissu. Rais Samia Suluhu Hassan, amesema serikali yake haitaruhusu wanaharakati wa kigeni kuingia nchini Tanzania na kuingilia masuala ya ndani ya nchi yake.

Wimbi la Siasa
Rwanda na DRC zawasilisha mapendekezo kuhusu mkataba wa amani

Wimbi la Siasa

Play Episode Listen Later May 7, 2025 10:23


Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, zimewasilisha mapendekezo ya rasimu ya mkataba wa amani kwa Marekani, kujaribu kutafuta mzozo wa Mashariki mwa DRC. Nchi hizo mbili zinatarajiwa kutia saini mkataba wa kudumu mwezi Juni, jijini Washington. Harakati hizi, zitazaa matunda ?

Habari za UN
Ripoti kuhusu Mpox yazitaja nchi 11 za Afrika, Ulaya, China na Amerika nao wamo

Habari za UN

Play Episode Listen Later Apr 30, 2025 2:03


Maambukizi ya ugonjwa wa mpox kutokana na aina ya virusi vya monkeypox clade Ib /ˈmʌŋ.ki.pɑks kleɪd one bee/ (MPXV) yanaendelea kuripotiwa hasa barani Afrika, ambapo mataifa kumi na moja yameripoti maambukizi ya ndani ya jamii katika kipindi cha wiki sita zilizopita. Hiyo kwa mujibu wa ripoti 51 ya Shrika la Umoja wa Mataifa la Afya Ulimwenguni, WHO kuhusu hali ya mlipuko wa mpox katika nchi mbalimbali duniani. Anold Kayanda amefuatilia ripoti hiyo na anatufafanulia kwa ufupi. 

Gurudumu la Uchumi
Vita ya Biashara: Athari kwa Biashara na Uwekezaji kwa nchi za ukanda

Gurudumu la Uchumi

Play Episode Listen Later Apr 30, 2025 10:06


Mizozo ya kibiashara kati ya nchi wanachama wa jumuiya za kikanda kama zile zilizoko SADC na EAC, ina athari endelevu kwa uchumi, biashara na jamii kiujumla.Mfano hivi karibuni Tanzania iliingia katika mvutano na nchi za Malawi na Afrika Kusini, zote zikiwa ni wanachama wa SADC, aidha wakati fulani Tanzania, Kenya na Uganda zilishawahi kuvutana.Ali Mkimo mchambuzi wa masuala ya uchumi na biashara anadadavua hili kwa kina kwenye makala ya wiki hii.

Gurudumu la Uchumi
Vita ya Biashara: Athari kwa Biashara na Uwekezaji kwa nchi za ukanda

Gurudumu la Uchumi

Play Episode Listen Later Apr 30, 2025 10:06


Mizozo ya kibiashara kati ya nchi wanachama wa jumuiya za kikanda kama zile zilizoko SADC na EAC, ina athari endelevu kwa uchumi, biashara na jamii kiujumla.Mfano hivi karibuni Tanzania iliingia katika mvutano na nchi za Malawi na Afrika Kusini, zote zikiwa ni wanachama wa SADC, aidha wakati fulani Tanzania, Kenya na Uganda zilishawahi kuvutana.Ali Mkimo mchambuzi wa masuala ya uchumi na biashara anadadavua hili kwa kina kwenye makala ya wiki hii.

That’s Debatable!
Journalism in the Dock

That’s Debatable!

Play Episode Listen Later Apr 29, 2025 40:26


According to College of Policing guidance, Non-Crime Hate Incidents (NCHIs) help forces build an intelligence picture of community tensions and understand where they need to allocate resources for prevention. Indeed, during a House of Lords debate in November 2024, Lord Hanson, the Home Office minister, told peers: “It is vital that the police monitor non-crime hate incidents when proportionate and necessary to do so to help prevent serious crimes”. However, the Telegraph reports that freedom of information requests submitted to police by Harry Miller, the founder of Fair Cop, revealed that many of the biggest forces, including the Met, Greater Manchester and West Midlands do not actually analyse the NCHI data they collect. Meanwhile, the Conservatives are tabling an amendment to the Crime and Policing Bill to abolish non-crime hate incidents. FSU members can use our Campaigns tool to write to their MPs to urge them to vote for this amendment. In our next item, we discuss the barring of Renaud Camus, a French philosopher, from entering the UK due to his controversial views on immigration. Lord Young is quoted in the Telegraph, “We've reached out to him to see if he'd like any help in appealing this decision, and he said yes. So I anticipate that we are going to be getting an immigration lawyer on the case”. He adds, “I don't think that the common good is endangered by inviting people to set out their contentious views in the public square, particularly not someone as distinguished as Mr Camus”. We end with a brief discussion on a new FSU briefing paper written by Trevor Kavanagh and entitled, “Journalism in the Dock, Sir Keir Starmer's Baseless Prosecution of Tabloid Journalists as Director of Public Prosecutions”. The video of Monday's FSU event, “Lifeblood of Democracy”, where we discussed the issues raised within the paper and Operation Elveden, will soon be available on our website. ‘That's Debatable!'  is edited by Jason Clift.

Mazingira Leo, Dunia Yako Kesho
Cha kutarajiwa katika ahadi mpya za nchi za kukabili mabadiliko ya tabianchi

Mazingira Leo, Dunia Yako Kesho

Play Episode Listen Later Apr 23, 2025 10:10


Ripoti ya umoja wa mataifa inaonesha dunia ipo nyuma sana katika kudhibiti ongezeko la joto chini ya nyuzi joto 1.5.

Alfajiri - Voice of America
Viongozi wa Ulaya wakubaliana kuongeza ufadhili kwa Ukraine na kwa ulinzi wa nchi zao - Machi 07, 2025

Alfajiri - Voice of America

Play Episode Listen Later Mar 7, 2025 29:59


SBS Swahili - SBS Swahili
Wangeci "katika hii nchi wanathamini sana watu wenye ujuzi wa kazi za mikono"

SBS Swahili - SBS Swahili

Play Episode Listen Later Feb 28, 2025 7:43


Wangeci Kones alikuja Australia akiwa na matumaini yakutumia shahada yake ya masoko, katika kazi sawia na alivyo kuwa akifanya nchini Kenya.

SBS Swahili - SBS Swahili
Uchomaji wakitamaduni: kutumia moto kulinda dhidi ya moto na kufufua Nchi

SBS Swahili - SBS Swahili

Play Episode Listen Later Feb 18, 2025 15:34


Kuishi katika mazingira yenye moto kama Australia, wengi wetu hupata ugumu waku ona moto kama kitu kingine zaidi yakuwa tisho.

Habari za UN
Kenya tumepiga hatua kuhakikisha maendeleo ya ustawi wa jamii: Mary Wambui Munene

Habari za UN

Play Episode Listen Later Feb 14, 2025 4:58


Kikao cha 63 cha Baraza la Kiuchumi na Kijamii la Umoja wa Mataifa ECOSOC kuhusu maendeleo ya ujamii kinakunja jamvi hii leo jijini New York Marekani baada ya majadiliano ya juma zima kuhusu maendeleo ya ustawi wa jamii, hatua zinazochukuliwa nan chi katika kufanikisha hilo na kuchagiza mshikamano wa kimataifa kutimiza lengo. Nchi mbalimbali zimetuma wakilishi kuanzia katika ngazi ya serikali, taasisi, mashirika yasiyo ya kiserikali na asasi za kiraia. Flora Nducha wa Idhaa hii amepata fursa kuzungumza na Mary Wambui Munene, mmoja wa washiriki kutokana Kenya. Ungana nao katika Makala hii

SBS Swahili - SBS Swahili
Taarifa ya Habari 6 Februari 2025

SBS Swahili - SBS Swahili

Play Episode Listen Later Feb 6, 2025 7:01


Nchi zaki Arabu, Umoja wa Mataifa na washirika wakaribu wa Marekani wamekosoa pendekezo la Donald Trump kuchukua ukanda wa Gaza, naku tawanya wa Palestina kuwa hatua hiyo ita yumbisha kanda hiyo na kudhoufisha juhudi zakupata suluhu ya nchi mbili.

Alfajiri - Voice of America
Trump apendekeza Wapalestina wahamishwe kutoka Gaza na wapelekwe katika nchi jirani za Kiarabu - Februari 05, 2025

Alfajiri - Voice of America

Play Episode Listen Later Feb 5, 2025 30:00


Alfajiri - Voice of America
Zaidi ya mamluki 280 kutoka nchi za Ulaya washikwa mateka na M23 na kupelekwa Rwanda - Januari 30, 2025

Alfajiri - Voice of America

Play Episode Listen Later Jan 30, 2025 29:59


Matangazo ya nusu saa kuhusu habari za mapema asubuhi pamoja na habari za michezo.

Alfajiri - Voice of America
Maelfu ya wakazi wa Niger, Mali na Burkina Faso waunga mkono uamuzi wa nchi zao kujiondoa kwenye ECOWAS. - Januari 29, 2025

Alfajiri - Voice of America

Play Episode Listen Later Jan 29, 2025 30:00


Matangazo ya nusu saa kuhusu habari za mapema asubuhi pamoja na habari za michezo.

SBS Swahili - SBS Swahili
Jaguar "Tunaomba nchi jirani zisaidie kutafuta amani na usalama DRC"

SBS Swahili - SBS Swahili

Play Episode Listen Later Jan 28, 2025 10:51


Milipuko ya mizinga imeitikisa Goma Jumatatu, saa chache baada ya wanajeshi wa Rwanda na wapiganaji kundi la waasi la M23 kuingia mjini humo.

Habari za UN
UN yaahidi kusaidia Wasyria kuiboresha nchi yao

Habari za UN

Play Episode Listen Later Dec 9, 2024 1:49


Kufuatia jana Wananchi wa Syria kutwaa madaraka kutoka kwa uongozi uliowatawala kwa mabavu kwa zaidi ya miongo mitano, viongozi wa Umoja wa Mataifa wameendelea kutoa wito wa kuhakikisha mabadiliko haya yanakuwa fursa ya mustakabali bora kwa kuzingatia haki za binadamu, uhuru na haki kisheria. Taarifa iliyoandaliwa na Anold Kayanda inaeleza zaidi.

Habari za UN
Miaka 15 ya Mkataba wa Kampala kuhusu wakimbizi wa ndani au IDPs, wito watolewa kwa nchi kuidhinisha na kutekeleza

Habari za UN

Play Episode Listen Later Dec 6, 2024 2:06


Katika kuadhimisha miaka 15 tangu kupitishwa kwa Mkataba wa Kampala wa Ulinzi na Usaidizi wa Wakimbizi wa Ndani barani Afrika chini Muungano wa Afrika, Kamishna Mkuu Msaidizi wa Ulinzi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi UNHCR, Ruven Menikdiwela na Mjumbe Maalumu wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu za Wakimbizi wa ndani Paula Gaviria Betancur wametoa kauli ya pamoja ya kupongeza Muungano wa Afrika kwa maono haya ya mbali na pia kuzisihi nchi zote barani Afrika kuutekeleza mkataba huo muhimu. Selina Jerobon na maelezo zaidi.

SBS Swahili - SBS Swahili
Mh JP Mwirigi "ili nchi ipate heshima yake, kuna miundombinu lazima ijenge"

SBS Swahili - SBS Swahili

Play Episode Listen Later Dec 3, 2024 13:23


Maamuzi ya utoaji wa kandarasi ya ukarabati ya baadhi ya miundombinu, yame iweka serikali ya Kenya chini ya shinikizo kubwa hivi karibuni.

So what you're saying is...
BBC Verify Bias + Labour's Authoritarian Crack Down: Respect Orders To Non - Crime Hate Incidents

So what you're saying is...

Play Episode Listen Later Dec 1, 2024 42:07


Labour's Authoritarian Crack Down: Respect Orders to Non-Crime Hate Incidents + BBC Verify Bias On today's #NCFNewspeak, NCF Director Peter Whittle, Senior Fellows Rafe Heydel-Mankoo and Dr. Philip Kiszely and Amy Gallagher of Stand Up To Woke discuss: * BBC Verify bias exposed: Who will verify BBC Verify? * Labour's new Respect Orders: What are they and should we be worried? * The bizarre list of Non-Crime Hate Incidents. 65 people a day have a NCHI recorded against them.

Habari za UN
Kuna mkwamo kwenye mkutano wa COP29 huku mapendekezo mapya yakitaka nchi tajiri kuzilipa masikini dola bilioni 250 kwa mwaka

Habari za UN

Play Episode Listen Later Nov 22, 2024 2:07


Majadiliano ya mkutano wa 29 wa nchi wanachama wa mkataba wa Umoja wa Mataifa wa mabadiliko ya tabianchi COP29 yamekumbwa na mkwamo huko Baku Azerbaijana muafaka haujapatikana. Majadiliano hayo yaliyotarajiwa kukunja jamvi leo sasa yanaendelea kwa kuwekwa mezani mapendekezo mapya kuhusu ufadhili wa mabadiliko ya tabianchi hasa kwa matifa yanayoendelea. Hakika vuta nikuvute bado inaendelea hata sasa washiriki wako mezani kwakikuna vichwa na kujadili mapendekezo mapya. Mkwamo huo umetokana na kushindwa kuafikiana katika masuala kadhaa kubwa likiwa ufadhili wa  mabadiliko ya tabianchi na hususasn kuhusu ni kiasi gani cha fedha nchi zinazoendelea zinapaswa kupokea kila mwaka hadi ifikapo mwaka 2030 na wapi fedha hizo za ufadhili zitatoka.Nchi zinazoendelea zinataka kulipwa dola trilioni 1.3 kwa mwaka lakini hilo halijaafikiwa na mapendekezo mapya yaliyowasilishwa na raia wa mkataba huo wa UNFCCC yanaonyesha tofauti kubwa na safari ndefu ya kufikia muafaka.Kwa mujibu wa mapendekezo hayo mapya yaliyowasilishwa leo mezani na Rais wa COP29 Mukhtar Babayev yanataka nchi zinazoendelea kupokea dola bilioni 250 kwa mwaka hadi kufikia mwaka 2035 kwa ajili ya kuchukua hatua didi ya mabadiliko ya tabianchi.Na maesema “Fedha hizi zitatoka katika vyanzo mbalimbali ikiwemo sekta za umma na za binafsi, na kitaifa na kimataiifa ikiwemo vyanzo mbadala”.Wakati pia COP29 ikitoa wito wa kufikia lengo la ufadhili wa dola trilioni 1.3 ifikapo mwaka 2035 pia imezikaribisha nchi zinazoendelea kutoa michango ya ziada.Kiwango kilichopendekezwa cha ufadhili kinatarajiwa kuzusha vuta ni kuvute katika majadiliano hayo kwa siku nzima ya leo huenda hadi kesho ingawa mkutano huo unahisi ahuweni kwamba kuna kiwango kilichowasilishwa na unataka hitimisho la mkutano haraka iwezekanavyo. Je nchi zinazoendelea zitapokea vipi pendekezo hili jawabu bado halijulikani. Wapenzi wa UN News Kiswahili endeleeni kufuatilia kwenye kurasa zetu kufahamu hatma ya mkutano huo.

Coffee House Shots
Making sense of non-crime hate incidents

Coffee House Shots

Play Episode Listen Later Nov 15, 2024 11:51


The government has announced a review into how to properly police non-crime hate incidents (NCHIs). This follows the experience of Allison Pearson who, on Remembrance Day morning, was doorstepped by Essex Police demanding an interview about a long-forgotten tweet. Reports of NCHIs have dramatically increased in the last year, with 13,200 recorded in the 12 months to June (around 36 a day). What qualifies as an NCHI and how can the police be expected to enforce them? Is this police overreach or a necessary measure to tackle the rise in instances of anti-Semitism and Islamophobia? Oscar Edmondson speaks to James Heale and Danny Shaw, former adviser to Yvette Cooper. Produced by Oscar Edmondson. 

Alfajiri - Voice of America
Zaidi ya vijana 500 kutoka nchi tofauti wakutana Arusha, Tanzania kuzungumzia umuhimu wa kumiliki ardhi. - Novemba 05, 2024

Alfajiri - Voice of America

Play Episode Listen Later Nov 5, 2024 29:59


Matangazo ya nusu saa kuhusu habari za mapema asubuhi pamoja na habari za michezo.

SBS Swahili - SBS Swahili
Prof Chacha"nchi za Afrika zinastahili tambua jumuiya yaki mataifa hai ongelei tena maswala yao"

SBS Swahili - SBS Swahili

Play Episode Listen Later Oct 25, 2024 7:43


Nchi kadhaa barani Afrika zina endelea kukabiliana na vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Habari za UN
Nchi zote pamoja na mashirika ya kimataifa ikiwemo UN yanawajibika kukomesha ukaliwaji wa Palestina

Habari za UN

Play Episode Listen Later Oct 18, 2024 2:03


Tume hiyo huru imeyasema hayo katika taarifa mpya ya msimamo wa kisheriia iliyotolewa mjini Geneva Uswis kuhusu eneo linalokaliwa la Palestina ikiwemo Jerusalem Mashariki ambayo imeweka wazi maoni ya tume kuhusiana na wajibu wa serikali na jinsi Baraza Kuu na Baraza la Usalama linavyoweza kutambua na kutekeleza mbinu na hatua sahihi zinazohitajika kwa kazi hiyo hadi mwisho wa ukaliwaji huo, na kwa haraka iwezekanavyo.Tume ihiyo imebaini kwamba maoni ya ushauri ya Mahakama ya Kimataifa ya Haki kuhusu matokeo ya Kisheria yanayotokana na sera na desturi za Israel katika eneo linalokaliwa la Palestina ikiwa ni pamoja na Jerusalem Mashariki ni wenye mamlaka na usio na utata kwa kusema kwamba kuendelea kuwepo kwa Israel katika eneo la Palestina linalokaliwa kwa mabavu ni kinyume cha sheria na sheria ya kimataifa.Taarifa hiyo ikitolewa Geneva Gaza kwenyenyewe hali inaendelea kuwa tete, kwa mujibu wa Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la msaada kwa wakimbizi wa Kipalestinna UNRWA Phillipe Lazzarini, kwani shule nyingine ya UNRWA imeshambuliwa leo Jabalia Kaskazini mwa Gaza, watu kadhaa wameripotiwa kuuawa na miongoni mwao Watoto wengi waliokuwa wakipata hifadhi katika jengo hilo.Lazzarini amesema hili ni shambulio la tatu dhidi ya majengo ya UNRWA kwa wiki moja. Na pia wafanyakazi wa shirika hilo wanaendelea kuuawa sasa wameffikia 231 tangu kuanza kwa vita hii Oktoba mwaka jana.Naye msemaji wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Watoto UNICEF James Elder akizungumza na waandishi wa habari mjini Geneva Uswisi hii leo amesema “Gaza ni mfano halisi wa ulimwengu wa kuzimu duniani kwa watoto milioni moja wa eneo hilo. Na hali inazidi kuwa mbaya, siku baada ya siku, tunapoona athari za kutisha za mashambulizi ya anga ya kila siku na operesheni za kijeshi za Israek kwa watoto wa Kipalestina.”Nalo shirika la kuratibu misaada ya kibinadamu OCHA likiangazia Ukingo wa Magharibi limesema “Vikosi vya Israel vimekuwa vikitumia mbinu mbaya za vita katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan, na kuibua wasiwasi mkubwa juu ya matumizi ya nguvu kupita kiasi na kuongeza mahitaji ya kibinadamu ya watu.” Ameelezea wasiwasi kuhusu mashambulizi ya walowezi wa Israel dhidi ya Wapalestina na miti yao ya mizeituni wakati huu wa mavuno ya kila mwaka.

Alfajiri - Voice of America
Watoto milioni 10 katika nchi nne za Afrika Magharibi na Afrika ya Kati waendi shule kutokana na mafuriko makubwa yaliyokumba kanda hiyo - Oktoba 16, 2024

Alfajiri - Voice of America

Play Episode Listen Later Oct 16, 2024 29:59


SBS Swahili - SBS Swahili
Prof Chacha "mtu ambaye amekuwa katika hali ya uchochore hawezi mkashifu anaye msaidia"

SBS Swahili - SBS Swahili

Play Episode Listen Later Oct 11, 2024 7:45


Nchi kadhaa barani Afrika zina endelea kuongeza ushirikiano na China, ambayo kwa upande wayo ina toa zawadi mbali mbali kwa nchi hizo.

Habari za UN
Guterres: Ili kutokuwa na ghasia duniani nchi zibadilishe ahadi kuwa uhalisia

Habari za UN

Play Episode Listen Later Oct 2, 2024 2:12


Ikiwa leo ni Siku ya Kimataifa ya Kutotumia vurugu, Katibu Mkuu wa Umoja Mataifa António Guterres amezitaka nchi kubadilisha kuwa ukweli ahadi za kuleta amani duniani walizojiwekea katika Mkutano wa Zama zijazo uliokamilika hivi majuzi hapa katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani.Ni kupitia kwenye ujumbe wake mahususi kwa ajili ya kuadhimisha Siku hii ya kimataifa ya kutotumia vurugu ambayo huadhimishwa kila tarehe pili ya mwezi Oktoba tarehe ya kuzaliwa Mahatma Gandhi, kiongozi wa vuguvugu la uhuru wa India na mwanzilishi wa falsafa na mkakati wa kutotumia vurugu kama njia ya kufanikisha mabadiliko katika jamii, Bwana Guterres amekumbushia namna ambavyo siku chache zilizopita katika Mkutano wa Zama Zijazo nchi zilikuja pamoja ili kuweka msingi wa umoja mpya wa ushirikiano wa kimataifa, ulio na nyenzo za kusaidia amani katika ulimwengu unaobadilika.Kiongozi huyo wa Umoja wa Mataifa anataja kwamba moja ya ahadi walizojiwekea viongozi wa ulimwengu ni kuangalia upya sababu za msingi za migogoro kuanzia kwa ukosefu wa usawa hadi umaskini na mgawanyiko na kwa hivyo sasa “tunahitaji nchi kubadilisha ahadi hizo kuwa uhalisia.” Akasisitiza.Bwana Guterres anaeleza kwamba siku hii ya kimataifa ya kutotumia vurugu inathibitisha tena maadili ambayo Mahatma Gandhi alijitolea maisha yake yaani usawa, heshima, amani na haki.Gandhi aliamini kutotumia vurugu ndio nguvu kuu zaidi inayopatikana kwa wanadamu yenye nguvu zaidi kuliko silaha yoyote. Na hivyo Guterres akazitaka nchi kwa pamoja, zijenge taasisi za kuunga mkono dira hiyo adhimu.