Nyumba ya Sanaa ni Makala ya Utamaduni ambayo inatoa fursa kwa wasanii na wadau wa sanaa kuwasilisha maoni yao kwa ajili ya maendeleo ya kweli ya Afrika na dunia kwa ujumla, tukiwa na lengo la kudumisha na kuendeleza tamaduni nzuri katika mwingiliano wa tamaduni uliopo, tukizingatia maisha ya kis…
Mwandishi Steven Mumbi anaangazia muziki wa dansi na ule wa kizazi kipya nchini Tanzania.
Sanaa ya muziki ni dawa inayofariji na kusaidia kutuma ujumbe wa amani kwa jamii amesema msanii wa miondoko mchanganyiko Gloire Tsongo almaarufu sweet Brown fresh Leader mjini Beni katika mkowa wa Kivu kaskazini mashariki mwa jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, katika mazungumzo maalum na mwandishi wa habari wa RFI Kiswahili Ruben Lukumbuka alipotembelea eneo hilo mwezi february mwaka huu
Sanaa ya Ufumaji ni sanaa ya Mikono inayotumia uzi kufuma Mavazi ya aina mbalimbali, kutana na Farida na Esther wasanii wanaofanya saa hizo walipozungumza na Steven mumbi katika Makala ya Nyumba ya Sanaa.
Samir Kassim Rashid maarufu Samir Kinyulinyuli ni Msanii wa Sanaa ya Muziki aliyelazimika kukimbilia Dar es salaam akitokea Morogoro ili kufanikiwa kisanaa, Ungana na Steven Mumbi katika Makala ya Nyumba ya Sanaa ya Jumahili.
Makala ya nyumba ya sanaa inaangazia utengenezaji wa filamu, mabadiliko ya ubunifu wa filamu unaoendana na teknolojia ya kisasa. Mbali na utovu wa usalama eneo la Beni mashariki mwa jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, vijana pia wamekuwa wakijitahidi katika kufanikisha namna ya kuwapa burudani ya filamu
Nyumba ya sanaa juma hili imekutana na wasanii wa mjini Beni mkoani Kivu kaskazini mashariki mwa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo ambao wamekuwa wakihimiza amani katika nyimbo zao, sanaa ya muziki ikikaribishwa kwa kiasi kikubwa na watu kutoka rika zote nchini na nje ya nchi. Mwenzangu Ruben Lukumbuka hivi karibuni alikutana na msanii wa Beni mashariki mwa DRC Mukombozi Mabenze almaarufu Tata Charles akielezea historia yake na sanaa ya muziki na hali ya eneo hilo
Sanaa ya Muziki Nyanda za Juu kusini mwa Tanzania, ni sanaa inayokua kwa kasi vijana wanawekeza kulifikia soko la Muziki Afrika Mashariki, B2K ni Msanii anayekonga Nyoyo za Wasichana zaidi kutokana na Tungo zake, Ungana na Steven Mumbi katika Makala ya Nyumba ya Sanaa akizungumza na B2K kutoka Njombe.
Uchoraji ni Ajira ,Wasanii wa sanaa hii Zanzibar wananeemeka na kazi zao, Ungana na Steven Mumbi akizungumza na Obedience na Muki kutoka Zanzibar.
Muziki wa kizazi kipya Zanzibar umedorora ukilinganisha na hali ilivyo Tanzania Bara
Wachoraji visiwani Zanzibar walia na gharama za kupata maeneo ya kunadi kazi zao za Sanaa hiyo, Ungana na Steven Mumbi katika Makala ya Nyumba ya Sanaa akizungumza na Mchoraji maarufu visiwani humo Jamal.
Taarab Asilia ni Miongoni mwa Miziki ya kale zaidi katika Mwambao mwa Bahari ya Hindi, Zanzibar Taarab Hertage Ensemble ni miongoni mwa Makundi ya Muziki huo kutoka Visiwani Zanzibar, Ungana na Steven Mumbi katika Makala ya Nyumba ya Sanaa.
Wasanii wa Muziki Afrika na Duniani kote wanakutana visiwani Zanzibar kufurahia uzuri na Upekee wa Muziki, wageni mbalimbali hukusanyika kushuhudia Tamasha la Sauti za Busara kila ifikao mwezi Februari.
Wanamuziki wa Muziki wa asili wamebadili vionjo vya asili wakijumuisha na vionjo vya Kisasa ili kuupaisha Muziki Kimataifa, Steven Mumbi amezungumza na Leo Mkanyia Mwanamuziki wa Muziki wa Asili kutoka Tanzania
Wasanii wa Muziki wa kizazi kipya wanaochipukia nchini Tanzania walalama kutakwa Kimapenzi wa Watayarishaji wa Muziki, Ungana na Steven Mumbi katika Makala ya Nyumba ya Sanaa akiwa na Zainisha Nokolage maarufu Zainisha.
Sanaa ya Muziki wa asili ni miongoni mwa sanaa zinazokua kwa kasi nchini Tanzania, Kutana na kundi la Sanaa lililowika katika majukwaa ya kimataifa wakiwa na bendi ya kipekee katika makala ya Nyumba ya Sanaa.
Steven Mumbi amezungumza na Lyala Sebastian Mchongaji wa Sanaa za Vinyago.
Wabunifu wa Sanaa ya Uchongaji Vinyago wamewekeza katika kung'amua fursa ya biashara kwa Mataifa ya Afrika Mashariki ili kujikwamua na vipato Duni, Steven Mumbi amezungumza na Mintanga Ramadhani Msanii wa Sanaa za Uchongaji Vinyago kutoka nchini Tanzania.
Muziki wa HIP HOP nchini Tanzania umefifia kutokana na ugumu wa kufanya Muziki huo,Msanii PMawenge anasimulia hatua za kuchukua kuurejesha sokoni katika Makala ya Nyumba ya Sanaa.
Sanaa ya ushairi inawavutia zaidi watu wanaotamani kujua utamu na upekee wa lugha adhimu ya Kiswahili, Chuo kikuu cha Dar es salaam kimewatambua na kuwapa fursa vijana waliosomea fani ya sanaa, kubobea katika kughani Mashairi. Ungana na Steven Mumbi katika Makala ya Nyumba ya Sanaa akizungumza na Msanii Michael James maarufu Michael.
Mwandishi wetu Steven Mumbi amezungumza na kundi la wasani la viongozi generation.
Muziki wa kizazi kipya umewawezesha vijana nchini Tanzania kujikwamua kimaisha kwa kujipatia kipato kupitia Sanaa hiyo,Katika Makala haya Steven Mumbi anazungumza na Hussein Mussa Shundi Maarufu Rucky.
Msanii wa Bongo Fleva, Baraka the Prince anauona muziki ni maisha, jambo linalomfanya afikirie zaidi namna mashabiki wake wataishi na kazi zake, Ungana na Steven Mumbi katika Makala ya Nyumba ya Sanaa akizungumza na Msanii huyo.
The Mafiki ni kundi la Muziki lililovuma kwa vionjo vya Muziki wa sasa, sasa wamekuja upya mara baada ya kusambaratika, Ungana na Steven Mumbi akizungumza na wasanii wa kundi hilo.
Mapinduzi ya Muziki wa Taarab yanajidhihirisha katika tenzi za wasanii wa Muziki huu kutoka tungo za Majigambo na sasa tungo za kuburudisha, Ungana na Steven Mumbi katika Makala ya Nyumba ya Sanaa akizungumza na Jike la Chui.
Zumbukuku ni miongoni mwa nyimbo zilizofanya vizuri katika muziki wa taarab, hii inashehenezwa na sauti ya kipekee ya kiume inayosikika katika muziki huo, Ally Star ndie aliyeimba wimbo huo; Ungana na Steven Mumbi katika makala ya Nyumba ya Sanaa akizungumza na Ally Star kuhusu namna nyimbo hizo zilivyotia fora.
Makala ya nyumba ya sanaa wiki hii imepiga kambi mjini Goma huko mashariki mwa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo ambako mwanzoni mwa mwezi mei mwandishi wetu Ruben Lukumbuka alikutana na msanii Ogisha Matale ambapo katika shughuli zake zake amekuwa akijaribu kuhimiza amani nchini, hususan eneo lake lenye kushuhudia mapigano ya mara kwa mara.
Nyota Tiger ni mzaliwa wa jijini Mwanza nchini Tanzania alilazimika kusafiri mpaka maeneo ya kusini mwa Afrika kukwepa adha za wazazi kumnyima fursa ya kufanya muziki. Ungana na Steven Mumbi katika Makala ya Nyumba ya Sanaa.
Katika makala ya nyumba ya sanaa wiki hii mwandishi wetu Ruben Lukumbuka ambaye hivi karibuni alitembelea mashariki mwa DRC ambako alikutana na Olivier wabahavu, msanii maarufu sana kufuatia nyimbo zake anazoimba katika lugha ya kihavu na kishi huko Kivu kusini na kaskazini, amezungumzia mchango wa sanaa ya muziki wa kiasili katika usuluhishi wa migogoro ya kivita mashariki mwa DR Congo.
Muziki wa Singeli ni Miongoni mwa Muziki unaokua kwa kasi nchini Tanzania na nchi za Afrika,Wasanii wa Muziki huo wanapambana kuukuza Kimataifa, Man Fongo ni Miongoni mwa Wasanii Pendwa wa Muziki huo,Ungana na Steven Mumbi anazungumza na Msanii huyo.
Katika Makala ya Wiki hii, Steven Mumbi amezungumza naye Jilema Ng'wana Shija msani wa muziki wa asili kutoka nchini Tanzania.
Karibu katika makala ya Nyumba ya sanaa nami Steven Mumbi, hii leo Msanii Tourna Boy wa kizazi kipya kutoka mjini Goma mashariki mwa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo akielezea kuhusu juhudi za vijana wasanii kuchangia katika juhudi za kurejesha amani ya mashariki mwa nchi hiyo, katika mazungumzo na mwenzangu Ruben Lukumbuka alipotembelea eneo la Goma mwanzoni mwa mwezi mei mwaka huu 2024
Kwenye Makala ya wiki hii Stephen Mumbi anazungumza na msani Abdul Sykes kutoka Mbagala Tanzania.
Makala ya Nyumba ya sanaa wiki hii inamuangazia msanii wa muziki wa regae Mack El Sambo ambaye kwa zaidi ya miaka ishirini amekuwa akihimiza amani katika eneo la mashariki mwa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, hususan kwenye mji wa Goma katika mkowa wa Kivu Kaskazini. Ungana na mwandishi wetu Ruben Lukumbuka ambaye hivi karibuni alitembelea mji wa Goma na kukutana na mwanamziki huyu..
Katika Nyumba ya sanaa wiki hii Steaven Mumbi akishirikiana na Ruben Lukumbuka ambaye wiki iliyopita alitembelea mji wa Goma ulioko mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ambako alikutana na mbunifu wa sanaa mbalimbali ikiwemo ubunifu wa kutengeneza viatu bwana Christian Bazika anayetengeneza bidhaa za ngozi mashariki mwa nchi hiyo.
Asha Jumbe maarufu White Maria ni Muigizaji aliyejizolea umaarufu akiwa na umri wa Miaka nane tu, sasa ni mtu Mzima aja kivingine kufanya sanaa ya Fimalu za kiswahili,Ungana na Steven Mumbi katika Makala ya Nyumba ya Sanaa akizungumzia safari yake ya Uigizaji.
Sanaa ya Muziki imenihitaji kuliko nilivyo ihitaji, ni kauli yake Steven Ibrahim maarufu Eddy Music alipozungumza na Steven Mumbi katika Makala ya Nyumba ya Sanaa.
Msani huyo amesema kuwa alitunga vibao kama bora kushukuru kutokana na changamoto za kimaisha alizokuwa anakabiliwa nazo kipindi fulani katika maisha yake.
Mwandishi wetu Steven Mumbi amezungumza na msani wa muziki huu wa Baibuda
Makala haya hukuletea historia ya sanaa na wasani barani Afrika.