Podcasts about mashariki

Province of Kenya

  • 26PODCASTS
  • 460EPISODES
  • 14mAVG DURATION
  • 5WEEKLY NEW EPISODES
  • Jun 2, 2026LATEST
mashariki

POPULARITY

20192020202120222023202420252026


Best podcasts about mashariki

Latest podcast episodes about mashariki

Habari za UN
02 JUNI 2026

Habari za UN

Play Episode Listen Later Jun 2, 2026 10:47


Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini Jamhuri ya Kidokrasia ya Congo DRC katika mji wa Mavivi jimboni kivu kaskazini Mashariki mwa nchi hiyo kusikia ni kwa jinsi gani walinda amani kutoka Tanzania wanaohudumu chini ya MONUSCO. wanavyochangia katika ulinzi wa amani na msaada wa kibinadamu.Umoja wa Mataifa umezitaka nchi zote duniani kuimarisha mifumo ya tahadhari za mapema baada ya kuthibitisha kuanza kwa hali ya El Niño, ukionya kuwa mabadiliko hayo ya joto la Bahari ya Pasifiki yataleta viwango vya juu vya joto kuliko kawaida karibu kila mahali duniani kati ya mwezi Juni mpaka Agosti na kuchochea matukio mabaya zaidi ya hali ya hewa. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Geneva Uswisi Katibu Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Hali ya hewa duniani WMO, Celeste Saulo amesema "Taarifa hizi ni muhimu kwa sababu El Niño ni kichocheo kikubwa cha hali ya hewa duniani na mifumo ya mabadiliko ya tabianchi, bahari yenye joto, huongeza joto na unyevu kwenye mfumo wa hali ya hewa ambao unaweza kutumika kuzidisha hali mbaya ya hewa ikiwa ni pamoja na joto kali, na mvua kubwa.”.'Zinakaribia siku 100 sasa tangu kuanza kwa mzozo wa Mashariki ya Kati ambao athari zake zimesambaa duniani kote kwani umevuruga njia za usafirishaji na umeongeza gharama za usafiri na kuchelewesha utoaji wa huduma muhimu. Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya watoto UNICEF limeeleza kuwa fedha nyingi sasa zinatumika kwenye usafirishaji badala ya kununua vifaa vya kuokoa maisha ya watoto. Gharama za kusafirisha chanjo kwenda baadhi ya nchi barani Afrika zimeongezeka kwa hadi asilimia 70, huku gharama za kusafirisha chakula tiba, na vifaa vya elimu, nazo zikipanda kwa kiwango kikubwa. Shirika hilo linaonya kuwa hali hiyo inalazimisha kufanya maamuzi magumu kuhusu ni watoto gani wapate msaada kwanza". Mlipuko wa ugonjwa wa Ebola uliogundulika nchini Jamhuri ya Kidemokrasia Congo DRC na Uganda mwezi uliopita wa Mei ambapo mpaka sasa watu 49 wamepoteza maisha, 48 nchini DRC na mmoja nchini Uganda. Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la afya ulimwenguni WHO Dkt. Tedros Adhanom Ghebreyesus amezihimiza jumuiya za kimataifa kutoa usaidizi unaohitajika ili kudhibiti mlipuko. Pia amelihimiza nchi kutoweka vikwazo vya usafiri kwa DRC, ili kuhakikisha msaada wa kiafya na kibinadamu unaweza kufikia kiwango kinachohitajika.Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili hii leo mtaalam wetu Onni Sigalla, Mhariri mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania, BAKITA. Anafafanua maana za neno "CHOTORA"Mwenyeji wako ni Rashid Malekela, karibu!

Wimbi la Siasa
Mpango wa DRC kuwakubali wahamiaji waliofukuzwa Marekani kwazua mjadala

Wimbi la Siasa

Play Episode Listen Later May 6, 2026 9:59


Hatua ya serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, kuingia kwenye makubaliano na Marekani ili kuwapokea wahamiaji haramu waliofukuzwa nchini humo, kumezua mjadala mzito katika nchi hiyo inayoendelea kukabiliwa na utovu wa usalama, hasa maeneo ya Mashariki. Kwanini kuna mvutano ?

congo drc felix tshisekedi hatua jamhuri marekani mashariki kidemokrasia
Habari za UN
04 MEI 2026

Habari za UN

Play Episode Listen Later May 4, 2026 9:57


Hii leo jaridani tunaangazia ugonjwa unaotokana na virusi vya hantavirus, njaa na afya kwa raia nchini Somalia, na ujumbe wa mshiriki wa mkutano wa CSW70 Hanna Wendot Cheptumo Waziri wa Jinsia, Utamaduni na Maslahi ya Watoto wa Jamhuri ya Kenya kuhusu ukeketaji.Shirika la Umoja wa Mataifa la afya ulimwenguni WHO kanda ya Afrika linafuatilia kwa karibu na kutoa msaada unaohitajika kufuatia tukio la afya ya umma kuhusu ugonjwa wa Virusi vya Hanta uliothibitishwa kutokea katika meli ya kitalii iliyosafiri katika Bahari ya Atlantic ambapo mpaka sasa watu watatu wamepoteza maisha.Wanawake na watoto waliokimbia ukame na migogoro nchini Somalia wameonya kuwa wanazidi kutumbukia katika janga la kibinadamu la njaa na mateso huku kupungua kwa ufadhili wa misaada ya kibinadamu kukiendelea kuathiri maisha ya watu kote nchini humo. Onyo lao limetolewa wakati mkuu wa masuala ya dharura na misaada ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa, Tom Fletcher, akihitimisha ziara yake katika kambi za wakimbizi na vituo vya afya mjini Mogadishu na Baidoa mwishoni mwa wiki.Ukeketaji bado ni changamoto katika maeneo kadhaa duniani na takwimu za Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani, WHO hadi mwaka jana kulikuwa na zaidi ya wasichana na wanawake zaidi ya milioni 230 walio hai waliokeketwa katika nchi 30 za Afika, Mashariki ya Kati na Asia. Kupitia mahojiano yaliyofanyika kandoni mwa Mkutano wa Kamisheni ya Hali ya Wanawake Duniani, CSW70 jijini New York, Marekani, miezi miwili iliyopita, Hanna Wendot Cheptumo Waziri wa Jinsia, Utamaduni na Maslahi ya Watoto wa Jamhuri ya Kenya anaeleza hatua zinazochukuliwa na nchi yake kupambana na hali hiyo ya ukeketaji.”Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!

new york atlantic kenya afrika somalia mogadishu umoja hii tom fletcher bahari afya hantavirus watoto wanawake jamhuri mataifa onyo marekani virusi mkutano shirika mashariki baidoa
Habari za UN
Kenya tunashirikiana na mataifa jirani kutokomeza ukeketaji_ Hanna Wendot Cheptumo

Habari za UN

Play Episode Listen Later May 4, 2026 3:00


Ukeketaji bado ni changamoto katika maeneo kadhaa duniani na takwimu za Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani, WHO hadi mwaka jana kulikuwa na zaidi ya wasichana na wanawake zaidi ya milioni 230 walio hai waliokeketwa katika nchi 30 za Afika, Mashariki ya Kati na Asia. Kupitia mahojiano yaliyofanyika kandoni mwa Mkutano wa Kamisheni ya Hali ya Wanawake Duniani, CSW70 jijini New York, Marekani, miezi miwili iliyopita, Hanna Wendot Cheptumo Waziri wa Jinsia, Utamaduni na Maslahi ya Watoto wa Jamhuri ya Kenya anaeleza hatua zinazochukuliwa na nchi yake kupambana na hali hiyo ya ukeketaji.

new york kenya fgm umoja watoto jamhuri mataifa marekani shirika mkutano mashariki
Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii
Watu 518 walifariki Tanzania wakati wa vurugu za uchaguzi, mapigano bado yanaendelea DRC

Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii

Play Episode Listen Later Apr 25, 2026 20:11


Taarifa kuu wiki hii ni ripoti ya tume ya uchunguzi nchini Tanzania iliyosema watu 518 walifariki wakati wa ghasia za uchaguzi mkuu wa mwezi Oktoba mwaka uliopita.  Tunaangazia pia taarifa kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ambapo licha makubaliano ya kusitisha vita kati ya waasi wa M23/AFC na serikali ya Kinshasa, kuendelea kushuhudiwa kwa mapigano ya mara kwa mara. Kiongozi wa kanisa katoliki duniani Papa Leo wa 14 alikamilisha ziara ya siku kumi barani Afrika juma hili; na katika mzozo wa Mashariki ya kati, Marekani yaongeza muda wa kusitisha mapigano na Iran, hatua sawa ikichukuliwa kati ya Israeli na Lebanon.

israel iran kenya israelis uganda lebanon congo tanzania afrika burundi drc kinshasa watu wakati jamhuri oktoba marekani kiongozi mashariki uchaguzi kidemokrasia tunaangazia
Changu Chako, Chako Changu
Historia ya vita vya Iran na Israeli huko mashariki ya kati

Changu Chako, Chako Changu

Play Episode Listen Later Apr 25, 2026 20:13


Makala hii imejikita huko mashariki ya kati ambapo tumeangazia kwa undani historia ya nchi ya Iran, na katika utamaduni kabila la wabembe kutoka Fizi mashariki mwa jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, na maeneo mengine ya nchi jirani, wakati katika kipengee cha muziki ni maadhimisho ya miaka kumi tangu alipotoweka mwanamuziki nguli, mfalme wa rumba almaarufu Papa Wemba huko Ivory Coast

Habari za UN
23 APRILI 2026

Habari za UN

Play Episode Listen Later Apr 23, 2026 9:59


Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina ambapo juzi Jumanne na jana Jumatano wagombea wa nafasi ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa walipata fursa kunadi serra zao mbele ya nchi wanachama kwenye Baraza Kuu wakiwemo wawakilishi wa asasi za kiraia walioweza kuwauliza maswali. Miongoni mwa wawakilishi hao ni Irene Kitoti, Mwanzilishi na mkurugenzi wa asasi ya kiraia ya Genesis For Children Organization ya nchini Tanzania aliyezungumza na Flora Nducha wa Idhaa hii ya Kiswahili. Pia tunakuletea muhtasari wa habari kama zifuatazo.Kutokana na mafanikio ya kihistoria kwa afya ya umma ya eneo la Karibe, Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Ulimwenguni, WHO limeipongeza nchi ya Bahamas kwa kuwa taifa la hivi karibuni zaidi katika ukanda huo wa Karibe kuthibitishwa kuwa limekomesha maambukizi ya Virusi Vya UKIMWI, VVU kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto. Mkurugenzi Mkuu wa WHO, Daktari Tedros Adhanom Ghebreyesus, kupitia taarifa ya shirika hilo ameipongeza Bahamas kwa mafanikio haya makubwa, yanayoimarisha miaka ya dhamira ya kisiasa na kujitolea kwa wahudumu wa afya.Ikiwa leo imetimia miaka 15 tangu kuanza maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wasichana katika Teknolojia ya Habari na Mawasilino, TEHAMA au ICT, Katibu Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la Mawasiliano (ITU), Doreen Bogdan-Martin katika ujumbe wake mahususi wa maadhimisho ya mwaka huu amesema, “kwa sasa tunaishi katika kipindi cha mabadiliko makubwa na ya kusisimua zaidi ya kiteknolojia katika historia ya binadamu lakini vilevile kwa sasa fursa zinazohusiana na mabadiliko haya ya kiteknolojia hazimfikii kila mtu kwa usawa”.Mgogoro wa usafirishaji katika Mlango Bahari wa Hormuz uliosababishwa na vita vya Mashariki ya Kati umefichua tishio jipya: upungufu  wa madini ya kimkakati yanayoendesha uchumi duniani kote  na sasa nchi huenda zitaanza kuhaha kuyapata. Katika mkutano na waandishi wa habari leo jijini Geneva Uswisi, Dario Liguti, Mkurugenzi wa Kitengo cha Nishati Endelevu cha Tume ya kiuchumi ya Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Ulaya, UNICE amesema,  “hatua ya kwanza, mbali na ongezeko la bei bila shaka, itakuwa viwanda kupunguza matumizi yake yake ya madini ya kimkakati na hivyo kupunguza uzalishaji… iwe ni paneli za sola, sumaku, betri na kadhalika, katika siku zijazo.”Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili hii leo mtaalam wetu Onni Sigalla, Mhariri mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania, BAKITA. Anafafanua maana za neno "KUPARAMA"Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!

bahamas tanzania ict hormuz umoja hii kiswahili katika siku afya tume taifa baraza habari tehama mataifa aprili shirika kimataifa mashariki teknolojia ikiwa miongoni mkurugenzi doreen bogdan martin
Habari za UN
22 APRILI 2026

Habari za UN

Play Episode Listen Later Apr 22, 2026 9:50


Hii leo jaridani tunaangazia sitisho la mapigano katika Mashariki ya kati, kilimo endelevu kinachowakwamua wakimbizi na wenyeji Kakuma nchini Kenya, na mafunzo ya UNDP ya uchimbaji salama wa madini ya ujenzi nchini Tanzania.Umoja wa Mataifa umekaribisha tangazo la Rais wa Marekani Donald Trump la kuongeza muda wa sitisho la mapigano kati ya Marekani na Iran, ukisema hiyo ni hatua muhimu kuelekea kupunguza mvutano kati ya mataifa hayo mawili.Maisha ya wakimbizi katika eneo la Kakuma, kaskazini mwa Kenya, yanaanza kubadilika kwa kasi kupitia miradi ya kilimo na lishe inayowezeshwa na mashirika ya Umoja wa Mataifa likiwemo lile la Mpango wa Chakula Duniani  (WFP) na la Chakula na Kilimo (FAO). Kwa ushirikiano na Serikali ya Kaunti ya Turkana chini ya ufadhili wa  Muungano wa Ulaya (EU) sasa wakimbizi wana uwezo wa kuzalisha chakula chao wenyewe, kuboresha lishe, na kujenga maisha ya kujitegemea.Shirika la Umoja wa Mataifa  la Mpango wa Maendeleo (UNDP), kwa kushirikiana na Tume ya Madini nchini  Tanzania katikati mwa wiki iliyopita yaani Aprili 16 na 17 wamefanya warsha ya mafunzo mkoani Singida katikati mwa nchi. Mafunzo hayo yamelenga kuimarisha ujuzi wa uchimbaji salama, unaozingatia sheria, na wenye faida kwa wanawake na vijana wanaojihusisha na uchimbaji mdogo wa madini ya ujenzi.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!

iran kenya tanzania undp rais wfp umoja maisha hii kwa turkana kakuma tume mataifa aprili serikali marekani shirika mashariki kaunti singida
Habari za UN
Raia wa Beni DRC: Asante TANZQRF-05 kwa kutushika mkono

Habari za UN

Play Episode Listen Later Apr 17, 2026 2:55


Raia wa Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, waishio mji wa Oicha uliopo Mavivi katika Jimbo la Kivu Kaskazini, wamewashukuru walinda amani kutoka Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wa Kikundi cha Tano Cha Utayari (TANZQRF-05), kinachohudumu chini ya mwamvuli wa Mpango wa Umoja wa Mataifa wa Kulinda amani nchini humo  (MONUSCO) kwa kutoa msaada wa dawa na huduma za kitabibu kwenye Hospitali Kuu ya Rufaa  ya Mji wa Oicha wiki hii. Private Habibu Shaban alikuwa shuhuda wa tukio hilo ungana naye kwa taarifa hii

tanzania jimbo drc beni asante umoja raia congo drc afya monusco jeshi jamhuri mataifa mashariki kidemokrasia wananchi
Habari za UN
17 APRILI 2026

Habari za UN

Play Episode Listen Later Apr 17, 2026 9:59


Hii leo jaridani tunaangazia ripoti ya mauaji wa wanawake na wasichana Gaza, ukatili wa kijinsia na wa kingono unaotumiwa kama silaha ya vita Sudan, na msaada wa dawa na matibabu ya bure nchini DRC yanyoendeshwa na walinda amani wa MONUSCO kutoka Tanzania.Uchambuzi mpya wa utafiti uliotolewa leo Aprili 17 na Shirika la Umoja wa Mataifa la Masuala ya Wanawake, UN Women umeweka wazi kuwa zaidi ya wanawake na wasichana 38,000 wameauawa kati ya mwezi Oktoba mwaka 2023 na Desemba 2025 huko Ukanda wa Gaza, eneo la Palestina linalokaliwa kimabavu na Israel ikiwa ni wastani wa takribani wanawake na wasichana 47 wanaouawa kila siku. Anold Kayanda ameufuatilia utafiti huo na kutuandalia taarifa ifuatayo.Ukatili wa kijinsia na wa kingono unatumiwa kama silaha ya vita nchini Sudan, jambo ambalo limesahaulika huku migogoro ikiendelea katika maeneo mengi mengi kote duniani amesema Tonderai Chikuhwa, Mshauri Mwandamizi wa Sera katika Ofisi ya Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika masuala ya Ukatili wa kijinsia katika Migogoro, katika mahojiano na Khaled Mohamed wa Idhaa ya Kiarabu ya Umoja wa Mataifa.Raia wa Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, waishio mji wa Oicha uliopo Mavivi katika Jimbo la Kivu Kaskazini, wamewashukuru walinda amani kutoka Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wa Kikundi cha Tano Cha Utayari (TANZQRF-05), kinachohudumu chini ya mwamvuli wa Mpango wa Umoja wa Mataifa wa Kulinda amani nchini humo (MONUSCO) kwa kutoa msaada wa dawa na huduma za kitabibu kwenye Hospitali Kuu ya Rufaa ya Mji wa Oicha wiki hii.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!

israel gaza tanzania sudan sera palestina jimbo drc un women umoja raia congo drc hii afya monusco wanawake jeshi jamhuri mataifa aprili oktoba shirika mashariki kidemokrasia desemba wananchi
Habari za UN
16 APRILI 2026

Habari za UN

Play Episode Listen Later Apr 16, 2026 9:59


Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini Uganda ambayo ni moja ya nchi zinazohifadhi wakimbizi wengi zaidi duniani na tutasikia simulizi za wakimbizi kutoka Sudan ambao Uganda iliwapokea na kuwapa makazi katika Makazi ya Wakimbizi ya Kiryandongo yaliyoko magharibi mwa nchi.Wataalamu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa wametaka uchunguzi wa haraka na uwajibikaji wa kimataifa kufuatia madai ya usafirishaji haramu wa wanawake na wasichana yaliyoibuliwa katika “faili za Epstein.” Wamesema madai hayo yanaonyesha mtandao mpana wa unyonyaji wa kingono uliodumu kwa miaka mingi na kuhusisha watu mashuhuri.mashambulizi makali ya anga ya Israel yameendelea kusini mwa Lebanon, yakilenga maeneo karibu na ngome ya Hezbollah ya Bint Jbeil, huku mashambulizi ya roketi kuelekea kaskazini mwa Israel nayo yakiendelea na kuongeza hofu ya kuongezeka kwa mapigano. Katika hatua nyingine, jeshi la Marekani limesema limezuia meli 10 kupita katika Mlango Bahari wa Hormuz, likitekeleza zuio lake lililotangazwa dhidi ya bandari za Iran. Wakati huo huo, mvutano wa kidiplomasia unaongezeka katika Umoja wa Mataifa, ambapo Baraza Kuu linakutana leo kujadili matumizi ya kura ya turufu kufuatia azimio la Baraza la Usalama kuhusu Mashariki ya Kati lililoungwa mkono na wengi lakini kuzuiwa na China na Urusi.Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto, UNICEF, leo limeeleza wasiwasi mkubwa kufuatia ongezeko la watoto waliouawa au kujeruhiwa nchini Ukraine, ambapo watoto 89 wameathirika mwezi Machi 2026 pekee. Kwa mujibu wa takwimu zilizothibitishwa na ripoti ya uangalizi wa haki za binadamu nchini Ukraine, idadi hiyo imeongezeka kwa asilimia 65 ikilinganishwa na mwezi Februari, hali inayoonesha madhara makubwa ya mashambulizi yanayoendelea kwa familia na jamii. Mashambulizi mabaya ya usiku wa tarehe 15 Aprili yalipiga miji kadhaa mikubwa, ikiwemo Dnipro, Kharkiv, Kyiv na Odesa, yakionesha hatari kubwa inayowakabili watoto.Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili, leo mchambuzi wetu ni Dkt. Josephat Gitonga, ambaye ni Mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi nchini Kenya, kwenye Kitivo cha Tafsiri na Ukalimani anafafanua maana ya methali “AWALI KUWA HERI SI AJABU” asMwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!

Habari za UN
Kuvurugika kwa meli kupita mlango bahari wa Hormuz kunazua wasiwasi kuhusu bei za chakula na minyororo ya usambazaji duniani

Habari za UN

Play Episode Listen Later Apr 13, 2026 3:25


Wakati mazungumzo ya kumaliza vita huko Mashariki ya Kati baina ya Marekani na Iran yakigonga mwamba mwishoni mwa wiki, shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo FAO limeonya kuwa kuvurugika kwa meli kupita katika mlango Bahari wa Hormuz kunaleta hatari zinazoongezeka si tu kwenye nishati bali pia katika mifumo ya chakula duniani. Tupate taarifa zaidi kutoka kwa Leah Mushi. 

Habari za UN
13 APRILI 2026

Habari za UN

Play Episode Listen Later Apr 13, 2026 11:37


Hii leo jaridani tunaangazia mlango Bahari wa Hormuz, mafuriko na ukarabati wa miundombinu huko jimbo la Upper Nile nchini Sudan Kusini, na juhudi za FAO nchini Tanzania za kuwapatia mafunzo jamii kuhusu lishe bora.Wakati mazungumzo ya kumaliza vita huko Mashariki ya Kati baina ya Marekani na Iran yakigonga mwamba mwishoni mwa wiki, shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo FAO limeonya kuwa kuvurugika kwa meli kupita katika mlango Bahari wa Hormuz kunaleta hatari zinazoongezeka si tu kwenye nishati bali pia katika mifumo ya chakula duniani.Kufuatia mafuriko makubwa yanayoendelea kuharibu miundombinu na kukwamisha ulinzi wa amani huko  jimbo la Upper Nile nchini Sudan Kusini, ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa Kulinda Amani nchini humo, UNMISS unaendelea kujitahidi kukarabati miundombinu kama njia mojawapo ya kuongeza ustahimilivu na kuchochea amani.Nchini Tanzania, kupitia Mpango wa Pamoja wa Kigoma Awamu ya Pili (KJPII) unaotekelezwa chini ya uongozi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo (FAO), maafisa ugani wa kilimo, wataalamu wa lishe na afya mkoani Kigoma waliungana kuandaa tukio la Siku ya Afya na Lishe Mitaani au SALIMI sambamba na Siku ya Shamba la Mkulima ili kuwapatia wakulima na wanajamii elimu ya vitendo kuhusu uzalishaji na matumizi ya mazao yenye lishe.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!

iran tanzania hormuz fao umoja hii bahari siku afya pamoja wakati mataifa aprili unmiss marekani shirika mashariki sudan kusini
SBS Swahili - SBS Swahili
Makala leo: Maumivu ya madereva katika vituo vya petroli yanaweza endelea kwa muda

SBS Swahili - SBS Swahili

Play Episode Listen Later Apr 10, 2026 8:31


Tangazo la kusitisha mapigano Mashariki ya Kati linaonekana kupunguza maumivu ya madereva katika vituo vya petroli, Iran ikikubali kuruhusu meli kupitia Mlango-Bahari wa Hormuz.

iran muda hormuz makala katika mashariki tangazo endelea
SBS Swahili - SBS Swahili
Taarifa ya Habari:Australia yashinikiza kupanua usitishaji mapigano Mashariki ya Kati ujumuishe Lebanon

SBS Swahili - SBS Swahili

Play Episode Listen Later Apr 9, 2026 5:22


Waziri Mkuu Anthony Albanese ametoa wito kwa Israel kukomesha mashambulizi yake dhidi ya Lebanon, akisema usitishaji wa mapigano katika eneo hilo la Mashariki ya Kati unapaswa kupanuliwa ili kuijumuisha Lebanon.

Habari za UN
07 APRILI 2026

Habari za UN

Play Episode Listen Later Apr 7, 2026 11:03


Jaridani tunakuletea mada kwa kina hii leo ikiwa ni siku ya kimataifa ya Tafakari kuhusu Mauaji ya Kimbari ya 1994 dhidi ya Watutsi nchini Rwanda. Na katika kupata tafakari hiyo Assumpta Massoi wa Idhaa hii amezungumza na Mwakilishi wa Kudumu wa Rwanda kwenye Umoja wa Mataifa Balozi Martin Ngoga. Balozi Ngoga anaanza kwa kuelezea mawanda ya mauaji hayo.Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amezisihi pande zinazo hasimiana katika mgogoro wa Mashariki ya Kati kuacha kushambulia miundombinu kwani ni kinyume cha sheria za Kimataifa. Mkurugenzi wa Huduma za Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa wa mjini Geneva Uswisi Alessandra Vellucci amewaambia waandishi wa habari kuwa “Umoja wa Mataifa ulishtushwa na matamshi yaliyoonekana katika chapisho la mitandao ya kijamii ambayo yalitishia mashambulizi ya Marekani dhidi ya mitambo ya kuzalisha umeme, madaraja na miundombinu mingine, iwapo Iran haitakubali makubaliano. Katibu Mkuu amezitaka pande zote kuzingatia wajibu wao kuhusu mwenendo wa mgogoro huo. Miundombinu ya kiraia, ikiwa ni pamoja na miundombinu ya nishati, haiwezi kushambuliwa, hata kama miundombinu maalum ya kiraia ingekuwa ikitumika kwa lengo la kijeshi. Umefika wakati wa pande husika kukomesha mzozo huu.”Leo ikiwa ni siku ya afya duniani, shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani (WHO) limetoa wito kwa jamii ya kimataifa kuimarisha ushirikiano na kuunga mkono sayansi kama msingi wa kuboresha afya ya binadamu. WHO imesema sayansi inapaswa kuwa msingi wa maamuzi yote ya afya katika ngazi za kitaifa na kimataifa na kutoa wito kwa serikali, taasisi na watu binafsi kuongeza ushirikiano ili kuhakikisha sera na hatua za afya zinazingatia ushahidi wa kisayansi. Kauli mbiu ya siku hii ni “Pamoja kwa Afya, Simama na Sayansi.”Na hii leo dunia inakumbuka mauaji ya Kimbari yaliyotokea nchini Rwanda mwaka 1994 dhidi ya watutsi nchini Rwanda, matukio ya kumbukizi yamefanyika kwenye ofisi za  Umoja wa Mataifa huko Nairobi, Kenya, Geneva nchini Uswisi na hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa kwenye ukumbi wa Baraza Kuu. Matukio yamehudhuriwa na manusura, viongozi wa Umoja wa Mataifa na Rwanda na mashirika ya kiraia ujumbe mkuu ukiwa hatua zichukuliwe kuhakikisha mauaji ya kimbari hayatokei tena.Mwenyeji wako ni Rashid Malekela, karibu!

israel iran kenya rwanda nairobi umoja afya pamoja kauli mataifa aprili marekani kimataifa mashariki mkurugenzi
SBS Swahili - SBS Swahili
Makala leo: Wakristo waadhimisha Pasaka na Jumapili ya Matawi kwa mioyo mizito na furaha

SBS Swahili - SBS Swahili

Play Episode Listen Later Apr 7, 2026 9:36


Waumini wa dini laki kristo walisherehekea Jumapili ya Pasaka, wakiadhimisha tukio hilo wakati vita katika maeneo ya Mashariki ya Kati vikifunika sehemu kubwa ya dunia.

makala pasaka mashariki jumapili
Habari za UN
Ukandamizaji wa uhuru wa kujieleza huko Mashariki ya Kati - Türk

Habari za UN

Play Episode Listen Later Apr 1, 2026 3:14


Tangu kuanza kwa mashambulizi ya Marekani na Israeli dhidi ya Iran, ukandamizaji wa nafasi ya kiraia na uhuru wa kujieleza umeongezeka kwa kiasi kikubwa kwenye eneo la  Mashariki ya Kati, ukiongeza hali ya hofu iliyokuwepo tayari kutokana na migogoro na misukosuko mingi, ameonya hii leo Kamishna Mkuu wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Binadamu, Volker Türk. Assumpta Massoi na maelezo zaidi.

iran israelis opt umoja uhuru haki mataifa marekani huko mashariki
Habari za UN
01 APRILI 2026

Habari za UN

Play Episode Listen Later Apr 1, 2026 9:56


Hii leo jaridani tunaangazia ukandamizaji wa nafasi ya kiraia na uhuru wa kujielez tangu mashambulizi ya Marekani na Israeli dhidi ya Iran, mabomu ya kutegwa ardhini na ujumbe wa watetezi wa haki za wanawake na wasichana kutoka Kenya.Tangu kuanza kwa mashambulizi ya Marekani na Israeli dhidi ya Iran, ukandamizaji wa nafasi ya kiraia na uhuru wa kujieleza umeongezeka kwa kiasi kikubwa kwenye eneo la  Mashariki ya Kati, ukiongeza hali ya hofu iliyokuwepo tayari kutokana na migogoro na misukosuko mingi, ameonya hii leo Kamishna Mkuu wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Binadamu, Volker Türk.Tarehe 4 mwezi Aprili mwaka huu ni siku ya kimataifa ya kuelimisha umma kuhusu mabomu ya kutegwa ardhini ambayo yamekuwa ‘mwiba' kwa wananchi walioko maeneo siyo tu ya vita hivi sasa bali pia yale ambamo mapigano yamemalizika lakini masalia ya mabomu yanaendelea kutesa wananchi. Nchini Sudan mwanamke mmoja anatekeleza kwa vitendo maudhui ya siku hii mwaka huu ambayo ni Wekeza kwenye amani, wekeza kwenye hatua dhidi ya mabomu ya kutegwa ardhini.Kutoka nchini Kenya, kijana aliyeshiriki mkutano wa 70 wa Kamisheni ya Hali ya Wanawake duniani, CSW70 amezungumzia jinsi vikao kama hivyo vimekuwa fursa kwa watetezi wa haki za wanawake na wasichana kuwasilisha changamoto kutoka maeneo yao na kusaka suluhu kwa pamoja na washiriki wenzao.Mwenyeji wako ni Rashid Malekela, karibu!

iran kenya israelis sudan umoja hii haki vijana wanawake mataifa aprili marekani mashariki
Habari za UN
31 MACHI 2026

Habari za UN

Play Episode Listen Later Mar 31, 2026 11:23


Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kia inayotorejesha katika mkutano wa CSW7O amabko Flora Nducha wa Idhaa hili kandoni mwa kikao hicho alipata fursa ya kuzungumza na Onyonge Mengo kijana mpigania haki za wanawake, mtafiti na wakili kutoka Mahakama Kuu ya Kenya  ambaye pia anafanyakazi na shirika la kimataifa la maendeleo la Hivos ili kufahamu kwa kina nini wanachokifanya kusongesha haki za kisheria za wanawake na wasichana.Mzozo wa Mashariki ya Kati ukiwa umeingia siku ya 31 , zaidi ya watu 200,000 wamevuka mpaka wa Lebanon na kuingia Syria tangu mashambulizi baina ya Israeli na Hezbollah yaanze mwishoni mwa mwezi uliopita baada ya Marekani na Israeli kushambulia Iran. Ripoti mpya ya iliyotolewa leo na Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo UNDP, inaonya kuwa idadi kubwa ya watu nchini Iran inaweza kutumbukia kwenye umaskini kadri misukosuko ya kiuchumi inavyozidi kuathiri maisha ya kila siku. Shirika hilo linasema hali hiyo inahatarisha kufuta mafanikio ya maendeleo yaliyopatikana kwa miaka kadhaa, huku Kiwango cha Maendeleo ya Binadamu (HDI) kikitarajiwa kushuka kwa kiasi kikubwa sawa na kupotea kwa zaidi ya mwaka mmoja wa maendeleo.Na Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji IOM, leo limeomba dola milioni 277 kusaidia watu walio hatarini zaidi waliokumbwa na mizozo na ukosefu wa makazi nchini Sudan na nchi jirani kwa mwaka huu wa 2026, wakati mgogoro huo ukikaribia kuingia mwaka wake wa tatu. Mkurugenzi Mkuu wa IOM Amy Pope ameonya kuwa familia zinakabiliwa na “chaguo ngumu lisilowezekana kati ya kubaki bila huduma muhimu au kurejea katika jamii zilizosambaratishwa na vita”. Fedha hizo zitatumika kuimarisha mifumo ya kibinadamu, kupanua njia za misaada, na kuimarisha operesheni za kuvuka mipaka ili kusaidia waathirika kuishi na kujijenga upya.Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili hii leo Dkt. Mwanahija Ali Juma, Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili, Zanzibar nchini Tanzania, BAKIZA anafafanua maana na matumizi ya neno "GIDA."Mwenyeji wako ni Rashid Malekela, karibu!

Habari za UN
30 MACHI 2026

Habari za UN

Play Episode Listen Later Mar 30, 2026 11:29


Hii leo jaridani tunaangazia migogoro yanayoendelea Mashariki ya Kati, ujumbe wa Katibu Mkuu leo dunia ikiadhimisha siku ya Kimataifa ya kutozalisha taka, na kampeni ya upatiaji mifugo dawa za minyoo na  udhibiti wa wadudu waenezao magonjwa Isiolo nchini Kenya.Vita vya Mashariki ya Kati vimeingia mwezi wa pili huku ghasia zikiongezeka katika maeneo kadhaa, ikiwemo Lebanon, Iran na Ghuba. Mlinzi wa amani wa Kikosi cha Mpito cha Umoja wa Mataifa nchini Lebanon UNIFIL ameuawa baada ya kombora kulipuka katika kituo cha Umoja wa Mataifa karibu na Adchit Al Qusayr, huku mwingine akiwa mahtuti hospital.Wakati hii leo dunia ikiadhimisha siku ya Kimataifa ya kutozalisha taka, Umoja wa Mataifa umetoa wito kwa kila mtu kujifunza upya yamna ya kufanya manunuzi ya vitu na mapishi ambayo hayatasababisha umwagaji wa chakula ili kunusuru mifumo ya ikolojia na afya ya binadamu.Nchini Kenya katika kaunti za Isiolo, Garissa, Samburu na Mto Tana, shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo, FAO limeendesha kampeni ya upatiaji mifugo dawa za minyoo na  udhibiti wa wadudu waenezao magonjwa, sambamba na kupatia wananchi fedha taslimu bila masharti kama mojawapo ya kujengea jamii mnepo wakati wa ukame unaosababishwa na mabadiliko ya tabianchi.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!

Habari za UN
UN: Hali inaendelea kuwa mbaya Mashariki ya Kati ikikatili zaidi maisha ya watu

Habari za UN

Play Episode Listen Later Mar 30, 2026 3:14


Vita vya Mashariki ya Kati vimeingia mwezi wa pili huku ghasia zikiongezeka katika maeneo kadhaa, ikiwemo Lebanon, Iran na Ghuba. Mlinzi wa amani wa Kikosi cha Mpito cha Umoja wa Mataifa nchini Lebanon UNIFIL ameuawa baada ya kombora kulipuka katika kituo cha Umoja wa Mataifa karibu na Adchit Al Qusayr, huku mwingine akiwa mahtuti hospitali. Flora Nducha na Taarifa zaidi

Habari za UN
27 MACHI 2026

Habari za UN

Play Episode Listen Later Mar 27, 2026 11:31


Hii leo jaridani mwenyeji wako Flora Nducha anamulika Mashariki ya Kati, mzozo Sudan Kusini unavyoendelea kuleta machungu kwa raia. Ingawa hivyo kuna habari njema ya jinsi FAO inavyoleta nuru kwa wakulima nchini Somalia kwa kukarabati mifereji ya umwagiliaji. Karibu!===========================Vita huko Mashariki ya Kati vinaendelea leo ikiwa ni siku ya 28, mashambulizi yanasababisha hofu, mateso, na kuzidisha mgogoro wa kibinadamu katika eneo lote. Huko Geneva, Uswisi wanadiplomasia katika Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa hii leo wanajadili shambulizi la shule lililotokea Minab, Iran, ambalo limeua zaidi ya watoto 100. Leah Mushi anasimulizi hii ya kusikitisha.Hofu imetanda kwa mara nyingine katika kambi ya wakimbizi ya Makpandu iliyopo Yambio, jimboni Equatoria Magharibi nchini Sudani Kusini, ambapo maelfu ya wakimbizi kutoka Sudan wanakabiliwa na vitisho vipya vya usalama kwa mujibu wa Mpango wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo UNMISS. Rashid Malekela anatupeleka kufahamu maisha ya wakimbizi huo yapoje?Shirika la Umoja wa Mataifa Chakula na Kilimo (FAO) kwa ufadhili wa Muungano wa Ulaya (EU) kupitia mradi wa Maisha Himilivu kwa Mabadiliko ya Tabianchi CLIMB unaolenga kuongeza uzalishaji wa chakula na kuimarisha lishe, limeanza kubadilisha maisha ya wakulima nchini Somalia, hasa katika maeneo ya Kismayo, Marka na Jowhar yaliyokuwa yameathiriwa kwa muda mrefu na ukame na mvua zisizotabirika. Feissal Kirwa anaangazia zaidi.

SBS Swahili - SBS Swahili
Taarifa ya Habari: Vituo na Wasambazaji kupewa faini ya milioni $100 wakiongeza bei ya mafuta kwa njia bandia

SBS Swahili - SBS Swahili

Play Episode Listen Later Mar 27, 2026 14:18


Vituo vya mafuta na wasambazaji watakaopatikana wakiongeza bei kutokana na vita vya Mashariki ya Kati watakabiliwa na adhabu mpya kali.

milioni habari njia mashariki
Habari za UN
26 MACHI 2026

Habari za UN

Play Episode Listen Later Mar 26, 2026 9:59


Hii leo jaridani tunamulika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, (DRC), hali Mashariki ya Kati, Amerika ya Kati, kilimo cha migomba kinachohimili mabadiliko ya tabianchi huko Pemba, Zanzibar nchini Tanzania na katika kujifunza lugha ya Kiswahili ni uchambuzi wa neno, 'Nyapanyapa.'MUHTASARIMabaraza ya Umoja wa Mataifa lile la Usalama na lile la Haki za Binadamu kwa nyakati tofauti yajadili hali ya usalama na haki za binadamu huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.Huko Mashariki ya Kati hali  ya usalama na kibinadamu yazidi kuwa tete Lebanon na Ukanda wa Gaza kutokana na mashambulizi yanayoendelea kila uchao.Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya duniani, WHO azungumzia hali tete ya afya nchini Cuba kutokana na kutokuwepo kwa huduma ya uhakika ya umeme.MADA KWA KINA: Jinsimafunzo ya kilimo cha migomba kinachohimili mabadiliko ya tabianchi yalivyoanza kuonesha matokeo chanya huko Pemba, Zanzibar nchini Tanzania. Mradi ni wa FAO kwa kushirikiana na SMZ.JIFUNZE KISWAHILI- Mchambuzi wetu Onni Sigalla kutoka BAKITA Tanzania anafafanua maana ya neno 'Nyapanyapa.'Karibu na mwenyeji wako ni Assumpta Massoi.

Habari za UN
Meli zilizokuwa zikipita Hormuz zilikuwa 129 kwa siku, sasa ni 2 hadi 7 kwa siku: UNCTAD

Habari za UN

Play Episode Listen Later Mar 25, 2026 3:07


Tangu kuanza kwa vita huko Mashariki ya Kati baada ya Israel na Marekani kuishambulia Iran mnamo tarehe 28 Februari na kisha Iran kujibu mashambulizi, wasiwasi umekuwa ukiongezeka kuhusu kupanda kwa bei za mafuta na bidhaa nyingine. Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo na Biashara UNCTAD linafuatilia kwa karibu hali inayoendelea na kutoa takwimu na uchambuzi ili kuzisaidia serikali na wadau wengine waweze kujipanga na kuratibu vyema mambo yao hususan yanayohusiana na usafiri wa baharini.Katikati ya vita hii inayoendelea Mashariki ya Kati kuna suala la mlango bahari wa Hormuz, hili ni eneo muhimu sana lililopo Iran ambako takriban robo ya mafuta yote duniani, meli zake hupita hapo. Bidhaa nyingine muhimu zinazopita hapo ni gesi asilia na mbolea. Ingawa mlango bahari wa Hormuz haujafungwa rasmi, lakini umewekewa vikwazo vikali, huku kukiwa na mashambulizi mengi ya Iran dhidi ya meli tangu vita vilipozuka siku 26 zilizopita. Akizungumza na Idhaa ya Umoja wa Mataifa, Mkuu wa Kitengo cha Masuala ya Uchumi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo na Biashara UNCTAD Frida Youssef anaanza kwa kutueleza hali ilivyokuwa kabla ya vita.“Kabla tu ya mzozo, tunapoangalia wastani wa idadi ya meli kwa siku zilizokuwa zikipitia Hormuz, ilikuwa karibu meli 129, 130 na katika wiki mbili zilizopita, ilikuwa karibu meli mbili hadi saba kwa siku.”Kwa lugha nyingine upungufu ni takriban asilimia 95. Je ni maeneo gani yameathirika zaidi? “Usafirishaji wa mbolea unaathirika pamoja na bei ya uzalishaji, kwa mfano, mbolea za nitrojeni ambazo hutegemea sana gesi. Kwa hivyo, hii inabadilisha tena kuwa ni athari kwenye kilimo ambayo baadaye itaonekana kwenye kupanda kwa bei ya chakula.” UN News/Daniel DickinsonKufungwa kwa mlangobahari wa Hormuz kunaathiri biashara kwa kiwango cha kimataifa.Akiendea na tathmini yake Mkuu huyo wa Kitengo cha Masuala ya Uchumi wa UNCTAD anasema hivi sasa bei za mafuta zimepanda.“Tumeona bei ya mafuta yanayotumika katika vyombo vya usafiri baharini ikiongezeka maradufu. Hii pia inaathiri gharama ya usafiri, si tu kwasababu bei ya mafuta imepanda bali pia bei, kwa mfano, ya bima. Malipo ya bima ya vita yameongezeka, katika baadhi ya maeneo imeongezeka mara nne.”UNCTAD inaendelea kufuatilia na kutoa taarifa kwa serikali na wadau kwani vita hii inayoendelea inaathari kwa kila mtu lakini nchi zenye uchumi mdogo ndio zitakazo athirika zaidi kwani zinauwezo mdogo zaidi wa kuvumilia mshtuko huu wa kiuchumi na ndio zitakazohisi athari zake kwa nguvu zaidi. “Inaathiri usafiri, inaathiri nishati, inaathiri chakula na pia inaongeza gharama na upatikanaji ni mgumu. Kwa hivyo, haya yote kwa pamoja yanakuwa na athari kwenye uchumi wa umma katika nchi, pamoja na gharama za maisha kwa kaya.” 

israel iran hormuz hadi meli sasa umoja hii kwa unctad siku mataifa kabla maendeleo mkuu marekani shirika mashariki
SBS Swahili - SBS Swahili
Makala leo: Jinsi vita Mashariki ya Kati vina chochea wasiwasi kuhusu usalama wa chakula

SBS Swahili - SBS Swahili

Play Episode Listen Later Mar 24, 2026 12:55


Vita katika maeneo ya Mashariki ya Kati, na kufungwa kwa Mlango-Bahari wa Hormuz, kumesababisha kile ambacho wataalamu wanakielezea kama moja ya migogoro mikubwa zaidi ya nishati katika miongo kadhaa.

hormuz makala jinsi mashariki
Habari za UN
Madhara ya vita vya Israeli/Marekani dhidi ya Iran yazidi kudhihirika

Habari za UN

Play Episode Listen Later Mar 23, 2026 3:15


Mzozo wa Mashariki ya Kati ukiingia wiki ya nne tangu uanze tarehe 28 mwezi uliopita wa Februari, Umoja wa Mataifa leo umeonya kuwa athari mbaya za kibinadamu na uchumi wa kimataifa zinaongezeka wakati mzozo huo ukivuruga kabisa njia muhimu za usambazaji wa bidhaa ndani ya Mashariki ya Kati na kwingineko duniani. Flora Nducha na taarifa zaidi.Asante Assumpta. Kwa mujibu wa mashirika ya Umoja wa Mataifa, mzozo unaoendelea Mashariki ya Kati sasa umevuka mipaka ya eneo hilo, ukiathiri pia Asia na Afrika, hasa katika biashara na usafirishaji.Taarifa ya Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Miradi na Huduma, UNOPS inaonya kuwa mamilioni ya watu wako hatarini kutokana na athari za kibinadamu na kiuchumi. Mkuu wa shirika hilo, Jorge Moreira da Silva, amesema kuvurugika kwa usafirishaji kupitia Mlango Bahari wa Hormuz kumesababisha mshtuko mkubwa wa kiuchumi duniani.Amesema “Nchi zinazoendelea barani Asia na Afrika zina uwezekano mkubwa wa kubeba gharama kubwa zaidi hali inayotishia usalama wa chakula,” na kuongeza kuwa njaa duniani inaweza kuongezeka kwa makumi ya mamilioni ya watu.Pia amesema mgogoro huu unazidisha hali mbaya iliyopo katika nchi kama Sudan, Sudan Kusini, Afghanistan, Yemen, na Somalia, ambapo mifumo ya chakula tayari ni dhaifuAmeonya pia kuwa mashambulizi dhidi ya meli na kuvunjika kwa minyororo ya usambazaji kunazuia upatikanaji wa dawa na misaada, hasa Gaza, huku vita vikienea vinaweza pia kuhatarisha fedha zinazotumwa nyumbani kwa familia, hasa Asia Kusini.Nchini Lebanon, kwa mujibu wa Sirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto UNICEF, zaidi ya watu 1,000 wameuawa na wengine zaidi ya 2,500 kujeruhiwa tangu mapema Machi, wakiwemo wahudumu wa afya, wanahabari na wafanyakazi wa misaada.Watoto wanaendelea kubeba mzigo mkubwa. Naibu Mkurugenzi wa UNICEF, Ted Chaiban, anasema “Watoto wanaouawa au kujeruhiwa ni sawa na darasa moja kila siku.”UNICEF inaonya pia juu ya athari kubwa za kisaikolojia kwa watoto na wahudumu wa misaada.Katika Ukanda wa Gaza, hali inazidi kuwa mbaya. Shirika la Umoja wa Mataifa la Msaada kwa Wakimbizi wa Kipalestna UNRWA,  limesema  mamia ya watu wamepata ulemavu wa kudumu huku huduma za afya na misaada zikizidi kuwa finyu.Wakati huo huo, hofu ya usalama wa nyuklia inaongezeka kufuatia mashambulizi karibu kweny vituo nyeti nchini Iran na Israel. Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Nishati ya Atomic IAEA,  Rafael Grossi, ameonya kuwa: “Hakuna hatua ya kijeshi inayopaswa kuhatarisha usalama wa vituo vya nyuklia.”Ingawa hakuna ongezeko la mionzi lililoripotiwa, Shirika la Umoja wa Mataifa a Afya Duniani WHO,  tayari linaanza maandalizi ya dharura.Mashirika ya Umoja wa Mataifa yanaonya kuwa bila hatua za haraka za kupunguza mzozo, dunia inaweza kukabiliwa na mgogoro mkubwa zaidi wa kibinadamu na kiuchumi.

Habari za UN
23 MACHI 2026

Habari za UN

Play Episode Listen Later Mar 23, 2026 10:59


Katika Jarida la Habari la Umoja wa Mataifa hii leo Assumpta Massoi anakuletea-Mzozo wa Mashariki ya Kati waingia wiki ya nne, vifo vyaongezeka, uchumi wa dunia waathirika, hofu ya nyuklia linaendelea huku Un ikionya kuhusu athari za kouchumi-Kenya yajivunia hatua nzuri katika kuwaondolea wanawake changamoto ya maji, utamsiki Waziri wa Masuala ya wanawake wa Kenya akifafanua hilo-Tarehe 20 Machi iliadhimisjwa Siku ya Furaha Duniani utawasiki baadhi ya wakaazi wa Mwanza Kaskazini-Magharibi mwa Tanzania wakielezea nafasi ya mitandao ya kijamii katika kujenga au kubomoa furaha ya binadamu.

SBS Swahili - SBS Swahili
Makala leo: Waziri Mkuu ateua kikosi kazi chaku kabili maswala yaliyo sababishwa na vita Mashariki ya Kati

SBS Swahili - SBS Swahili

Play Episode Listen Later Mar 20, 2026 8:42


Waziri Mkuu amemteua 'mratibu wa mafuta' kusaidia kushughulikia masuala ya mnyororo wa ugavi yaliyosababishwa na vita katika maeneo ya Mashariki ya Kati.

kazi makala mashariki waziri mkuu
Habari za UN
19 MACHI 2026

Habari za UN

Play Episode Listen Later Mar 19, 2026 10:57


Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina leo baada ya takribani wiki mbili mkutano wa 70 wa CSW70 unakunja jamvi.  Maudhui yalikuwa kuendeleza Haki, Sheria na Kuchagiza Hatua kwa ajili ya wanawake na wasichana, na sasa washiriki wanaeleza Idhaa hii wanachoondoka nacho.Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres leo akizungumza na waandishi wa habari Mjini Brussels Ubelgiji kuhusu kinachoendelea Mashariki ya Kati akiwa a na Rais wa Baraza la Muungano wa Ulaya António Costa, ametoa ujumbe mahsusi kwa wahusika wakuu wa mzozo huo. Amesema “Kwanza kwa Marekani na Israel, ni wakati muafaka kumaliza vita hivi ambavyo viko hatarini kutodhibitiwa kabisa, vikisababisha mateso makubwa kwa raia, na athari zake zinaenea katika uchumi wa dunia kwa kiwango cha kutisha, zikiwa na uwezekano wa kusababisha madhara makubwa zaidi hasa kwa nchi zenye maendeleo duni”Kisha ujumbe wake wa pili ni “Kwa Iran, acheni kushambulia majirani zenu. Hawakuwa sehemu ya mgogoro huu. Baraza la Usalama limelaani mashambulizi haya na kuamuru yasitishwe, pamoja na kuagiza kufunguliwa kwa Mlango Bahari wa Hormuz.”Na kuelekea Siku ya Kimataifa ya Furaha hapo Kesho Machi 20 raia Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, eneo lililoghubikwa na mizozo ya silaha wanaeleza furaha kwao inamaanisha nini.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!

Habari za UN
FAO yaonya kuwa mgogoro wa Mashariki ya Kati watishia mifumo ya chakula duniani

Habari za UN

Play Episode Listen Later Mar 18, 2026 2:36


Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) linaonya kuwa kuongezeka kwa mgogoro katika Ghuba ya Uajemi au Mashariki ya Kati kunahatarisha mifumo ya chakula duniani, likitaja kupanda kwa gharama za nishati, mbolea na uzalishaji wa chakula kama athari kuu. Flora Nducha anafafanua zaidi katika taarifa hii

umoja kuwa shirika mashariki
Habari za UN
18 MACHI 2026

Habari za UN

Play Episode Listen Later Mar 18, 2026 9:58


Hii leo jaridani tunaangazia machafuko na uhakika wa chakula katika mshariki ya kati, na kazi ya walinda amani wa Umoja wa mataifa nchini Sudan Kusini.Mgogoro unaoiendelea Mashariki ya Kati unaendelea kuzorotesha hali ya kibinadamu katika ukanda huo huku watu wakikimbia makazi yao, wasiwasi wa usalama wa nyuklia ukiongezeka, na vitisho vikiongezeka dhidi ya usafiri wa baharini..Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) linaonya kuwa kuongezeka kwa mgogoro katika Ghuba ya Uajemi au Mashariki ya Kati kunahatarisha mifumo ya chakula duniani, likitaja kupanda kwa gharama za nishati, mbolea na uzalishaji wa chakula kama athari kuu.Mji wa Bentiu ulioko Kaskazini mwa Sudan Kusini ni eneo linalokumbwa na mafuriko yanayoharibu makazi na migogoro inayowafanya maelfu ya watu kuishi kwenye kambi za wakimbizi. Katika mazingira haya magumu, Afisa wa Polisi wa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo, UNMISS, Wafaa Assri Sameeh Al-Goussous kutoka nchini Jordan, anafanya kazi ya kujenga uaminifu na uhusiano madhubuti kati ya jamii na vyombo vya dola kupitia doria na mafunzo. Rashid Malekela anatupeleka huko kufahamu maisha ya kila siku ya Afisa Wafaa yakoje.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!

israel iran lebanon umoja machi polisi hii katika mataifa unmiss shirika mashariki ujumbe sudan kusini
Habari za UN
Vita Mashariki ya Kati, wasiwasi watanda kuhusu nyuklia, usafiri baharini na wengi wayakimbia makazi yao

Habari za UN

Play Episode Listen Later Mar 18, 2026 2:33


Mgogoro unaoiendelea Mashariki ya Kati unaendelea kuzorotesha hali ya kibinadamu katika ukanda huo huku watu wakikimbia makazi yao, wasiwasi wa usalama wa nyuklia ukiongezeka, na vitisho vikiongezeka dhidi ya usafiri wa baharini. Anold Kayanda anatueleza kwa kina.

israel iran lebanon wengi mashariki
Habari za UN
17 MACHI 2026

Habari za UN

Play Episode Listen Later Mar 17, 2026 9:59


Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina kutoka hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa kwenye Kikao cha CSW70. Leo Flora Nducha wa Idhaa hii anazungumza na mshiriki Nelly Mbangu Lumbulumbu, mwanasheria na mwanaharakati wa Haki za binadamu kutoka DRC.Nelly ni mwanzilishi na mkurugenzi wa shirika lisilo la kiserikali la “Sauti ya Mama Mukongomani” lililoanzishwa mwaka 2008, anaanza kwa kumueleza kwa nini alinzisha shirika hilo.Mashirika ya Umoja wa Mataifa yanaeleza kuwa idadi ya wakimbizi wa ndani inazidi kuongezeka, mathalan huko Lebanon watu 816,000 sawa na asilimia 14 ya watu wote wamekimbia makazi yao. Na huko Iran watu milioni 3.2 wanakadiriwa kukimbilia maeneo ya Kaskazini mwa taifa hilo na vijijini wakikimbia machafuko. Namba ya dharura ya msaada ya Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Wakimbizi UHCHR inapokea zaidi ya simu 1,000 kwa siku za watu wakiomba msaada.Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP, limeonya kuwa njaa duniani inaweza kufikia viwango vya juu mwaka huu iwapo mzozo wa Mashariki ya Kati utaendelea na bei ya mafuta itabaki kuwa juu. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Geneva Uswisi Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa WFP Carl Skau amesema “Ongezeko la gharama za chakula na mafuta duniani zinaweza kuacha mamilioni ya familia zikiwa nje ya uwezo wa kununua vyakula, hasa katika nchi zinazotegemea uagizaji bidhaa kama vile Afrika, Kusini mwa Jangwa la Sahara na Asia. Kwa hakika, uchambuzi wetu unakadiria kwamba, kama mzozo wa Mashariki ya Kati utaendelea hadi mwezi Juni, watu zaidi ya milioni 45 wanaweza kuingizwa kwenye njaa kali kutokana na bei kuwa juu na hii itaweka rekodi ya juu ya njaa duniani kote. Na haya ni matarajio mabaya.".Hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa hii leo moja ya matukio ya kando ya Mkutano wa 70 wa Kamisheni ya Hali ya Wanawake duniani, CSW70 ni Kushughulikia vikwazo vya haki ya kijinsia kupitia mfumo wa Mahakama ya Mtandao nchini Tanzania kwa lengo la kufanikisha haki kwa wanawake na wasichana. Barke Sehel ambaye ni Jaji wa Mahakama ya Rufani nchini Tanzania anasema mashinani mfumo unatumia simu zisizo janja na akisema mobile app ni apu ya kwenye simu.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!

Habari za UN
16 MACHI 2026

Habari za UN

Play Episode Listen Later Mar 16, 2026 9:59


Hii leo jaridani tunaangazia vita nchini Iran, sauti za vijana katika wiki ya pili ya mkutano wa CSW70, na mafunzo ya vitendo kwa vijana nchini Uganda kuhusu mbinu za kisasa za ufugaji nyuki.Katika siku ya 16 ya vita nchini Iran iliyoanza baada ya Marekani na Israeli kushambulia taifa hilo la Mashariki ya Kati na kisha lenyewe kujibu mashambulizi yanayosambaa hadi ukanda mzima wa eneo hilo, hii leo suala hilo limepatiwa kipaumbele kwenye Baraza la Umoja wa Mataifa la Haki za Binadamu huko Geneva, Uswisi ambapo mtaalamu huru wa Umoja wa Mataifa, Mwenyekiti wa Tume ya Uchunguzi na Mwakilishi wa Iran wametoa maoni yao kuhusu kinachoendelea na nini kifanyike.Sauti za vijana zinaendelea kusikika kwa nguvu katika wiki ya pili ya kikao cha 70 cha Kamisheni ya Hali ya Wanawake duniani kinachofanyika hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York Marekani ambapo wanaharakati, watunga sera na wadau kutoka sehemu mbalimbali za dunia wamekusanyika kujadili namna ya kuendeleza haki , haki za kisheria na fursa kwa wanawake na wasichana.Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) na wadau wake chini ya mpango Kilimo na Msaada wa Masoko (AMS), vijana nchini Uganda wamepata mafunzo ya vitendo kuhusu mbinu za kisasa za ufugaji nyuki. Mafunzo hayo yamewasaidia kukimu mahitaji yao kupitia uzalishaji wa asali.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!

Habari za UN
Raia nchini Iran wanabeba gharama ya vita inayoendelea - Mtaalamu

Habari za UN

Play Episode Listen Later Mar 16, 2026 2:40


Katika siku ya 16 ya vita nchini Iran iliyoanza baada ya Marekani na Israeli kushambulia taifa hilo la Mashariki ya Kati na kisha lenyewe kujibu mashambulizi yanayosambaa hadi ukanda mzima wa eneo hilo, hii leo suala hilo limepatiwa kipaumbele kwenye Baraza la Umoja wa Mataifa la Haki za Binadamu huko Geneva, Uswisi ambapo mtaalamu huru wa Umoja wa Mataifa, Mwenyekiti wa Tume ya Uchunguzi na Mwakilishi wa Iran wametoa maoni yao kuhusu kinachoendelea na nini kifanyike. Assumpta Massoi amefuatilia na kuandaa taarifa ifuatayo.

Habari za UN
Guterres awasili nchini Lebanon na kusisitiza sitisho la mapigano

Habari za UN

Play Episode Listen Later Mar 13, 2026 2:27


Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres, aliyeko ziarani huko Lebanon, ameelezea wasiwasi mkubwa kuhusu mateso yanayowakabili wananchi wa taifa hilo la Mashariki ya Kati lililotumbukizwa kwenye vita isiyowahusu. Flora Nducha na Maelezo kamili.

Habari za UN
13 MACHI 2026

Habari za UN

Play Episode Listen Later Mar 13, 2026 9:59


Hii leo jaridani tunaangazia ujumbe wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres, aliyeko ziarani huko Lebanon, ujumbe wa kijana kutoka Uganda anayehudhuria mkutano wa CSW70, na mradi wa intaneti kwa wanafunzi nchini Kenya.Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres, aliyeko ziarani huko Lebanon, ameelezea wasiwasi mkubwa kuhusu mateso yanayowakabili wananchi wa taifa hilo la Mashariki ya Kati lililotumbukizwa kwenye vita isiyowahusu.Mikutano hii inayokutanisha Umoja wa Mataifa watetezi wa haki za wanawake dunia inawapa ujasiri vijana wa kuona kuwa nao wana uwezo na fursa ya kusaka majawabu katika jamii zao. Ni kauli ya kijana wa kike kutoka nchini Uganda anayeshiriki mkutano wa 70 wa Kamisheni ya Hali ya wanawake Duniani (CSW70 ) unaoendelea hapa katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani.Maelfu ya wanafunzi katika eneo la Kajiado nchini Kenya wameanza kunufaika na mradi wa kusambaza intaneti shuleni uitwao ‘Last Mile Connectivity'. Mradi huu unalenga kuboresha ujuzi wa kidijitali na matokeo ya masomo kwa wanafunzi ili kuwaandaa na maisha ya baadaye, huku shule 1,000 zikitarajiwa kufikiwa.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!

Habari za UN
06 MACHI 2026

Habari za UN

Play Episode Listen Later Mar 6, 2026 11:13


Katika Jarida la Habari Hii leo Kutoka Umoja wa Mataifa Assumpta Massoi anakuletea-Mashirika ya UN yatahadharisha kuongezeka kwa vurugu Mashariki ya Kati.-Mafunzo ya haki ya kumiliki ardhi yanayotolewa na Kituo cha Msaada wa Kisehria kwa Wanawake WLAC yamebadilisha maisha ya familia ikiwemo ya Jovita Provius: WLAC-Mpango wa Jamii Rafiki kwa Mtoto wazinduliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto UNICEF katika Kaunti ya Samburu

iran kenya lebanon tanzania umoja machi samburu wanawake mataifa wlac shirika mashariki kaunti mashirika
SBS Swahili - SBS Swahili
Taarifa ya Habari: DFAT yatuma timu kuwasaidia Waaustralia waliokwama Mashariki ya Kati

SBS Swahili - SBS Swahili

Play Episode Listen Later Mar 5, 2026 5:56


Waziri wa Mambo ya Nje wa Australia Penny Wong amesema dunia ina wasiwasi kuhusu jinsi Iran inavyo jibu mashambulizi ya Marekani na Israel yaliyomuua kiongozi wake, Ayatollah Khamenei na kulenga miundombinu ya nyuklia.

Habari za UN
Iran: Siku ya tano ya mzozo Iran na Mashariki ya Kati watu waendelea kufurumushwa, mashirika ya UN yatoa usaidizi

Habari za UN

Play Episode Listen Later Mar 4, 2026 3:19


iran tano siku watu mashariki mashirika
Habari za UN
04 MACHI 2026

Habari za UN

Play Episode Listen Later Mar 4, 2026 13:06


Miongoni mwa utakayo yasikia hii leo jaridani ni mzozo huko Mashariki ya Kati baada ya Israel na Marekani kuishambulia Iran na kisha Iran kujibu mashambulizi. Sasa nchi jirani nazo zimeathirika ikiwemo Lebanon ambapo sasa UNHCR inatoa msaada kwa wananchi. Zikiwa ni siku chache kabla ya Siku ya wanawake duniani tarehe 08 Machi, leo utasikilia simulizi ya mwanamke aliyekuwa akifanyiwa ukatili na mume wake na msaada aliopokea kutoka WLAC. Katika masuala hayo hayo ya wanawake tutasikia wanawake wa Masrabit wanavyoelimisha wenzao kukataa ukeketaji kupitia mradi wa UNFPA nchini Kenya

Habari za UN
03 MACHI 2026

Habari za UN

Play Episode Listen Later Mar 3, 2026 9:58


Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka huko Mashariki ya Kati ambako Leo ni siku ya nne ya mzozo mabomu yameripotiwa kuendelea kulipuka. Makombora yanarindima katika ukanda huo huku ndege zisizo na rubani au droni zikisababisha maafa sasa katika nchi 12. Pia tunakuletea muhtasari wa habari kama zifuatazo.Mgogoro wa Iran ukiendelea kupamba moto, Umoja wa Mataifa na mashirika yake wanaendelea kufuatilia kwa ukaribu kuhusu hali hiyo tete huku wakiendelea kuhamasisha amani kupitia diplomasia kwani tayari madhara ya moja kwa moja kwa wanadamu yameshaonekana. Mathalani leo Msemaji wa ofisi ya Umoja wa Mataifa wa Haki za Binadamu, OHCHR, Ravina Shamdasani akirejelea  tukio moja baya la kusikitisha ambapo inaripotiwa wasichana kadhaa waliuawa na kujeruhiwa wakati shule yao ya msingi huko Minab, kusini mwa Iran, iliposhambuliwa wakati wa saa za masomo, amesema, “watoto, wasichana wadogo katikati ya siku ya shule, mwanzoni mwa siku ya masomo, wanauawa kwa namna hii, mabegi yao ya shule yakiwa na, unajua, madoa ya damu juu yake.Shirika la Umoja wa Mataifa la Nishati ya Atomiki, IAEA leo limeeleza kwamba kulingana na picha mpya za satelaiti, sasa linaweza kuthibitisha baadhi ya uharibifu wa hivi karibuni kwenye majengo ya milango ya Kiwanda cha Kuchakata Mafuta cha FEP kilichojengewa chini ya ardhi huko Natanz, Iran. Ujumbe wa IAEA umefafanua kuwa hakuna athari zozote za mionzi zinazotegemewa na hakuna athari za ziada zilizobainika kwenye Kiwanda cha FEP chenyewe, ambacho tayari kilikuwa kimeharibiwa vibaya katika mzozo wa mwezi Juni.Leo ni Siku ya Kimataifa ya Wanyamapori mwaka huu kaulimbiu ya siku ikilenga “Mimea ya Dawa na Harufu nzuri inaangazia nafasi muhimu ya mimea hii katika kudumisha afya ya binadamu, urithi wa kitamaduni, na kipato cha jamii za wenyeji. Katika ujumbe wake mahususi kwa ajili ya siku hii, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres akionesha wasiwasi wake kuhusu kutoweka kwa miea asili ya dawa ametoa wito akisema,ninazihimiza nchi zote ziwe watunza bustani wa rasilimali za pamoja za dunia.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!

israel iran iaea dawa umoja natanz machi hii haki katika siku fep ohchr mataifa marekani shirika kimataifa mashariki ujumbe
Habari za UN
IAEA yaonya hatari ya nyuklia kadri mzozo Mashariki ya Kati unavyozidi kupamba moto

Habari za UN

Play Episode Listen Later Mar 2, 2026 2:53


Mwelekeo mpya wa mzozo katika eneo la Mashariki ya Kati ukiwa umeingia siku yake ya tatu leo Jumatatu ukichochewa na mashambulizi ya mabomu dhidi ya Iran yaliyofanywa na Israel na Marekani, mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la nishati ya atomiki, IAEA, Rafael Grossi amehimiza kurejea kwa diplomasia, akitaja “hatari inayoongezeka kwa usalama wa nyuklia” katika eneo hilo. Anold Kayanda na  maelezo zaidi.

Habari za UN
02 MACHI 2026

Habari za UN

Play Episode Listen Later Mar 2, 2026 11:03


Hii leo jaridani tunaangazia hatari inayoongezeka kwa usalama wa nyuklia huku vita vikiendelea kushika kasi nchini Iran, masuala ya afya ya wanawake na watoto nchini Burundi, na maisha ya baadaye ya watoto katika ukanda wa Gaza.Mwelekeo mpya wa mzozo katika eneo la Mashariki ya Kati ukiwa umeingia siku yake ya tatu leo Jumatatu ukichochewa na mashambulizi ya mabomu dhidi ya Iran yaliyofanywa na Israel na Marekani, mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la nishati ya atomiki, IAEA, Rafael Grossi amehimiza kurejea kwa diplomasia, akitaja “hatari inayoongezeka kwa usalama wa nyuklia” katika eneo hilo.Uhaba wa vifaa na maji safi na salama katika kambi ya muda ya wakimbizi ya Busuma iliyoko mashariki mwa Burundi umekuwa changamoto kubwa kwa wanawake wajawazito wanaojifungua kambini hapo, wakati huu ambapo shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu na Afya ya Uzazi, (UNFPA) nchini Burundi linasema katika kipindi cha mwezi mmoja takribani watoto 200 wamezaliwa.Hakuna maisha ya baadaye! Siyaoni maisha ya baadaye kwani sioni wanaoshikamana nasi! Hayo ni sehemu tu ya maoni ya watoto walioko Ukanda wa Gaza, eneo la Palestina linalokaliwa kimabavu na Israeli wakati huu ambapo makombora yanaendelea kurindima, mustakabali wao uko mashakani, na wanachohitaji kama inawezekana ni amani na ujenzi mpya wa makazi ili waweze kurejea katika maisha ya kawaida ndani ya nyumba zao na kuacha kuishi kama wakimbizi katika ardhi yao wenyewe.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!

Capital FM
MTV Shuga Mashariki Cast, Renee Gichuki & Wilson Muchemi on The Fuse

Capital FM

Play Episode Listen Later Feb 18, 2026 19:44


MTV Shuga Mashariki Cast, Renee Gichuki & Wilson Muchemi on The Fuse by Capital FM

Habari za UN
Redio Okapi iliokoa maisha yangu: Mkimbizi Bahati Yohane

Habari za UN

Play Episode Listen Later Feb 13, 2026 3:33


Katika maeneo ya migogoro, redio huwa nguzo ya utulivu. Mathalani Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, Radio Okapi ya Umoja wa Mataifa imekuwa sauti ya kuaminika na kuwasaidia wakimbizi kusaka usalama tangu kuanzishwa kwake mwaka 2002 kama sehemu ya ujumbe wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa nchini humo MONUSCO. Mmoja wa wakimbizi kutoka Mashariki mwa DRC ambaye sasa anaishi kambi ya wakimbizi ya Kyangwali nchini Uganda amemweleza John Kibego kutoka Redio washirika wetu Kazi Njema FM ya mjini Hoima jinsi matangazo ya redio Okapi yalivyonusuru maisha yake wakati wa vita

uganda drc umoja maisha congo drc okapi katika bahati monusco jamhuri mataifa mashariki redio kidemokrasia
Habari za UN
03 JANUARI 2026

Habari za UN

Play Episode Listen Later Feb 3, 2026 12:52


Hii leo jaridani kesho ikiwa ni siku ya kimataifa ya kuelimisha umma kuhusu ugonjwa wa saratani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini Kenya kumulika hatua ambazo ni uzinduzi wa Mpango wa Utekelezaji wa Kitaifa wa kutokomeza saratani ifikapo mwaka 2030.Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa  Duniani, WHO, leo limetoa ombi la dola bilioni moja ili kukabiliana na majanga ya afya mwaka 2026 katika dharura 36 zilizo mbaya zaidi duniani. Ombi hilo linalenga kusaidia huduma za afya zinazookoa maisha katika nchi zilizoathiriwa na migogoro na majanga, zikiwemo Gaza, Sudan, Haiti na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC.Mashariki ya Kati, wakati muda ukiendelea kuyoyoma kwa maelfu ya wagonjwa mahututi huko Gaza, kufunguliwa tena kwa kivuko cha Rafah kunaleta mwanga wa matumaini. Kivuko hicho kilifunguliwa Jumatatu baada ya kufungwa kwa zaidi ya mwaka mmoja, chini ya mpango wa amani unaoungwa mkono na Marekani, na kuruhusu uhamisho wa kwanza wa wagonjwa tangu mwaka 2025.Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia watoto UNICEF leo liimesema linaongeza juhudi zake zamsaada wa msimu wa baridi nchini Ukraine huku watoto na familia wakikabiliwa na kukatika kwa umeme, kukosa vipasha joto na maji kufuatia mashambulizi yanayoendelea dhidi ya miundombinu ya nishati na baridi kali. Tangu Novemba, shirika hilo limesambaza jenereta 106 kote nchini kusaidia huduma za maji na mifumo ya kupasha joto, huku takribani jenereta 150 zaidi zikitarajiwa kuwasili katika wiki zijazo.Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili na hii leo Dkt. Mwanahija Ali Juma, Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili, Zanzibar nchini Tanzania, BAKIZA anafafanua maana na matumizi ya neno "KUNVI"Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!

TED Talks Daily
How to make AI a force for good in climate | Amen Ra Mashariki and Manoush Zomorodi

TED Talks Daily

Play Episode Listen Later Dec 19, 2025 12:39


In a now-famous Go match against a human in 2016, AI made Move 37 — a seemingly nonsensical play that baffled every expert but ultimately won it the match. Amen Ra Mashariki, director of AI at the Bezos Earth Fund, thinks we need AI to make that same kind of creative leap for climate solutions. In conversation with TED Radio Hour host Manoush Zomorodi, he shares a vision for new AI solutions to environmental problems that human experts haven't yet dreamed up. Hosted on Acast. See acast.com/privacy for more information.