Podcasts about kutana

  • 12PODCASTS
  • 69EPISODES
  • 10mAVG DURATION
  • 1MONTHLY NEW EPISODE
  • Apr 9, 2025LATEST

POPULARITY

20172018201920202021202220232024


Best podcasts about kutana

Latest podcast episodes about kutana

Habari za UN
UNICEF na wadau Kenya waelekea kufanikisha ndoto ya Sharlyne kuwa mwandishi wa habari

Habari za UN

Play Episode Listen Later Apr 9, 2025 4:24


Kutana na Shalyne Kaputa, mtoto wa kike mwenye umri wa miaka 16 kutoka kaunti ya Turkana, Kaskazini-Magharibi mwa Kenya. Tofauti na shangazi yake, ambaye hakuweza kuendelea na elimu  yake kutokana na kukosa karo, yeye anasoma elimu ya sekondari sasa ili aweze kutimiza ndoto yake ya kuwa mwandishi wa habari. Yote yanawezekana kutokana na mradi wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF kwa msaada wa shirika la Norway la Maendeleo NORAD na wadau wengine. Je ni usaidizi gani wanapatiwa? Ungana na Assumpta Massoi.

Habari za UN
Umri wa kuoa au kuolewa Côte d'Ivoire ni kuanzia miaka 18 - Francine

Habari za UN

Play Episode Listen Later Mar 14, 2025 4:40


Kutana na Francine Aka Epse Akaanghui  Rais wa Chama cha wanasheria wanawake nchini Côte d'Ivoire huko Afrika Magharibi. Yeye anashiriki mkutano wa 69 wa Hali ya Wanawake duniani, CSW69 akisema taifa lake lina mengi ya kujivunia wakati huu wa kuadhimisha miaka 30 tangu kupitishwa kwa Azimio la Beijing na Jukwaa la Utekelezaji. Francine amezungumza na Assumpta Massoi katika makala hii.

Habari za UN
Kutana na Celestin Mbaruku mkimbizi mnufaika wa Mpango wa Utambuzi wa Ujuzi wa Awali nchini Kenya

Habari za UN

Play Episode Listen Later Feb 28, 2025 3:25


Kama mkimbizi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, Celestin Mbaruku hakuwa na fursa ya ajira rasmi hadi alipothibitishwa ujuzi wake kupitia mpango wa Serikali ya Kenya wa Utambuzi wa Ujuzi wa Awali, uliotengenezwa kwa ushirikiano na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kazi duniani, ILO.Kupitia ILO Celestin Mbaruku ni mnufaika wa ufadhili wa PROSPECTS, ushirikiano wa kimataifa unaojumuisha mashirika kadhaa ya Umoja wa Mataifa ukilenga kuboresha upatikanaji wa elimu, ulinzi wa jamii, na ajira yenye hadhi kwa jamii zinazowakaribisha wakimbizi na watu waliolazimika kuhama makazi yao.Kimakosa, Celestin Mbaruku akiwa nchini mwake DRC alidhaniwa kuwa muasi, akafungwa lakini akamudu kutoroka hadi Kenya.Kabla ya masaibu haya, huko DRC alikuwa Mwalimu anayesimamia nidhamu katika shule alikokuwa anafanya kazi ya lakini kwa kuwa vyeti vyake vilipotea, hata alipovuka kuingia Kenya, hakuwa na uthibitisho wa kiwango cha elimu yake licha ya kuwa ana diploma ya mbinu za ufundishaji.Na hapo ndipo ikabidi achomoe kibindoni ujuzi wake mwingine. Ujuzi binafsi, ufundi wa kushona nguo.Celestin sasa anafundisha wanawake wadogo shughuli za kushona nguo.Hatimaye mwaka jana, 2024, kupitia mpango wa Serikali ya Kenya wa Utambuzi wa Ujuzi wa Awali (RPL), uliotengenezwa kwa ushirikiano na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kazi duniani, ILO utaalamu wake wa kushona nguo ambao haukuwa na cheti, ukathibitishwa rasmi na akapata cheti, hali ambayo imemfungulia milango ya kuomba ajira rasmi.

Habari za UN
Tumetembea wiki mbili kufika kambini Bushagara lakini bado hapa si nyumbani - Mwamini

Habari za UN

Play Episode Listen Later Feb 5, 2025 3:33


Kutana na Mwamini Sebororo mmoja wa mamilioni ya raia wa Jamhuri ya Kidemkrasia ya Congo DRC waliopoteza makazi yao na kila kitu katika jimbo la Kivu Kaskazini mashariki ya taifa hilo huku mgogoro ukiendelea kufurusha watu zaidi. Kuendelea kuzorota kwa hali ya kibinadamu imekuwa mtihani mkubwa kwa wakimbizi wa ndani na jamii zinazowahifadhi. Kupitia video ya shirika la umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR Flora Nducha anafafanua zaidi katika Makala hii.

Habari za UN
Tumechoka na vita tunachotaka ni amani turejee nyumbani: Masimango Mango

Habari za UN

Play Episode Listen Later Jan 31, 2025 1:41


Kutana na mkimbizi Masimango Mango kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, ambaye kwa sasa anaishi kwenye makazi ya wakimbizi wa ndani ya Lushagara Goma jimboni Kivu Kaskazini  Mashariki mwa DRC, anasema kwa hakika vita imemchosha na anacholilia ni amani ili arejee nyumbani na familiia yake. Flora Nducha na taarifa zaidi.

mango drc goma congo drc jamhuri nyumbani mashariki kidemokrasia kutana
Habari za UN
31 JANUARI 2025

Habari za UN

Play Episode Listen Later Jan 31, 2025 9:58


Hii leo jaridani tunaangazia hali ya usalama nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na tutakuletea simulizi ya wakimbizi wa ndani nchini humo. Makala inatupeleka nchini Senegal na mashinani nchini Afghanistan, kulikoni?Mashirika ya Umoja wa Mataifa yameendelea kutoa wito wa kurejeshwa kwa amani mashariki mwa Jamhuri ya Kidemkrasia ya Congo (DRC) kwani hali inazidi kuwa tete na kuuzidi uwezo wa mashirika hayo kusaidia..Kutana na mkimbizi Masimango Mango kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, ambaye kwa sasa anaishi kwenye makazi ya wakimbizi wa ndani ya Lushagara Goma jimboni Kivu Kaskazini Mashariki mwa DRC, anasema kwa hakika vita imemchosha na anacholilia ni amani ili arejee nyumbani na familiia yake.Makala tunakwenda Senegal, magharibi mwa AFrika ambako nishati ya umeme imeleta mabadiliko makubwa kwenye kijiji ambacho awali kiligubikwa na kiza nyakati za usiku.Na katika Zulaikha kutoka Afghanistan ambaye ana matumaini katika msimu huu wa baridi kutokana na msaada wa fedha kutoka Shirika la Marekani la Misaada ya kimaendeleo USAID na lile la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda karibu!  

Habari za UN
Wasichana wakipewa fursa hakuna mchezo utakaowashinda: Saido Noor

Habari za UN

Play Episode Listen Later Dec 20, 2024 3:31


Kutana na Saido Omar Noor, binti mwenye umri wa miaka 25 mkimbizi kutoka Somalia anayeishi Kakuma kambi kubwa zaidi ya wakimbizi nchini Kenya. Kupitia video ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR anasema katika jamii yake ni yeye mwanamke pekee wa Kisomali anayecheza mpira kwa kikapu au basketball. Flora Nducha na taarifa zaidi..

Habari za UN
11 DESEMBA 2024

Habari za UN

Play Episode Listen Later Dec 11, 2024 9:59


Hii leo jaridani tunaangazia ripoti ya WHO inayohusu malaria, na juhudi za UNICEF na wadau wake nchini Rwanda za kusaidia watoto waliozaliwa na ulemavu kuweza kutembea. Makala tunakupeleka nchini Yemen na mashinani nchini Tanzania, kulikoni?Takwimu mpya zilizotolewa leo na ripoti ya shirika la Umoja wa Mataifa la afya duniani WHO, zinaonyesha kuwa ingawa takriban wagonjwa bilioni 2.2 wa malaria na vifo milioni 12.7 vya ugonjwa huo vimeepukwa tangu mwaka 2000 bado ugonjwa huo unaendelea kuwa tishio kubwa la kimataifa la afya hususan katika Kanda ya Afrika ya WHO na hivyo juhudi zaidi zahitajika kuutokomeza.Nchini Rwanda Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto UNICEF kwa msaada wa UNICEF Uswisi na Liechtenstein wamesaidia tiba kwa njia ya mazoezi kuponya watoto wenye ulemavu wa viungo. Selina Jerobon anasimulia akiangazia mtoto mmoja, Joshua.Katika makala Assumpta Massoi anakupeleka Yemen kusikia yaliyojiri baada ya ndoto za vijana kuelekea Saudi Arabia kuishia Yemen.Na mashinani mashinani hivi majuzi dunia iliadhimisha siku ya watu wenye ulemavu duniani ikiangazia uthabiti, ujumuishaji na fursa sawa kwa wote. Kutana na Dorice Mkiva, Mtaalamu wa usimamizi wa maarifa wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF Tanzania ambaye alipoteza uwezo wake wa kutembea akiwa na umri mdogo na sasa anatumia sauti yake kutetea haki za watoto.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!  

Nyumba ya Sanaa
Muziki wa asili kutoka nchini Tanzania

Nyumba ya Sanaa

Play Episode Listen Later Nov 23, 2024 20:12


Sanaa ya Muziki wa asili ni miongoni mwa sanaa zinazokua kwa kasi nchini Tanzania, Kutana na kundi la Sanaa lililowika katika majukwaa ya kimataifa wakiwa na bendi ya kipekee katika makala ya Nyumba ya Sanaa.

Nyumba ya Sanaa
Muziki wa Taarab na chid boy mpiga kinanda wa bendi ya nakshi nakshi

Nyumba ya Sanaa

Play Episode Listen Later Mar 16, 2024 20:07


Muziki wa Taarab unashehenezwa na mirindimo ya vyombo kwa kisasa sambamba na Kinanda , Kutana na Chid Boy Mpiga kinanda wa Bendi ya Nakshi Nakshi na Mmiliki wa Bendi hiyo.

Rugendo@ ttb.twr.org/Gikuyu-kikuyu
Jesu Kutana na Kuringa Ciama na Gutuma Arutwo Ake

Rugendo@ ttb.twr.org/Gikuyu-kikuyu

Play Episode Listen Later Dec 1, 2023 23:12


jesu kutana
Habari za UN
Kutana na Timu ya Taifa ya Kandanda ya Wanawake ya Afghanistan - Wakimbizi katika Michezo

Habari za UN

Play Episode Listen Later Jul 26, 2023 0:04


“Tunajaribu kuleta michezo na nguvu zake katika mazingira magumu sana ya watu wasiojiweza. Mchezo ni mzuri kwa kuwapa watu matumaini ya siku zijazo.” Anasema Filippo Grandi, Kamishna Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi (UNHCR) akirejelea Timu ya mpira wa miguu ya wanawake wakimbizi wanaoishi nchini Australia baada ya kuokoa maisha yao yaliyokuwa hatarini nchini mwao Afghanistan. Anold Kayanda anasimulia zaidi. 

Nyumba ya Sanaa
Msanii chipukizi Hussein Rashid azungumzia safari yake nchini Tanzania

Nyumba ya Sanaa

Play Episode Listen Later Jun 17, 2023 20:04


Mkoa wa Kigoma ,magharibi mwa Tanzania mwambao mwa ziwa Tanganyika ni miongoni mwa mikoa iliyotoa wasanii wakubwa nchini akiwemo Ali Kiba, sasa vijana Chipukizi wanaibuka kufanya sanaa hiyo. Kutana na Hussein Rashid Msanii chipukizi katika Makala ya Nyumba ya Sanaa.

Radio Maria Tanzania
Je nini ukifanye unapo kutana na Mchumba mara ya kwanza.

Radio Maria Tanzania

Play Episode Listen Later May 26, 2023 57:59


Ungana na Mtangazaji Martin Joseph katika Kipindi cha Pro-Life  na mada inayozungumziwa ni Muendelezo mwa mada ya Uchumba, wawezeshaji ni Grace Shayo, Afisa kutoka Pro-Life pamoja Whittness Lihepa, Kutoka Pro-Life.

The AllCreation Podcast
Called to Care: Africa Exchange (2023)

The AllCreation Podcast

Play Episode Listen Later May 5, 2023 88:57


Our first Called to CARE session for 2023 begins like a dinner conversation among friends. In this podcast, AfricaExchange.org co-founders and co-directors, Sam and Melody Harrell, share how their Baptist American-African lives led them to become global leaders in “integrated” sustainable development... “I am blown a-Way.” (Rev. Jimi Calhoun, co-host, legendary musician, author and pastor)Sam and Melody are saving lives and ending poverty with education and holistic, community care. Now celebrating their 25th year, AfricaExchange (AE) has built 14 “integrated child development” preschools in Kenya's most-isolated / least-resourced regions. AE's projects are providing and fostering nutrition, clean water, education, sanitation and infrastructure, jobs, job training, Creation care and restoration, and more, on an ongoing basis in these places to help these children and their communities defeat poverty. Meet. Notice. Exchange. Serve. AfricaExchange's model is rooted in the best of Christianity's and Africa's worldviews. As the children of Baptist missionaries in Africa, Sam and Melody's foundational insight is that CARING FOR OTHERS means: listening, noticing, and being empathetic before acting. AfricaExchange helps communities build upward-spiraling personal and collective assets which benefit the whole community and their local biosphere. AE is exemplar in their work. This podcast is worth multiple listenings for those interested in “learning the lessons that will propel us forward.” (Sam Harrell)#############About our guests • Melody Harrell, spiritual director, AfricaExchange.org • Sam Harrell, executive director, AfricaExchange.org • Rev. Jimi Calhoun, pastor, BridgingAustin.org, author/musician, JimiCalhoun.com • Rev. Julaine Calhoun, pastor, BridgingAustin.org • Chris Searles, director, BioIntegrity.net, exec. editor, AllCreation.org About this seriesIn this time of polarizations and extremes we seem to be going to our Media for answers, and yet our Media is not designed or intended to give us answers. Media is a business (not a healer). Looking honestly at today's shared social challenges, all indicators indicate it is Care through kinship, attention, gentleness, safety, honesty, support, process, nurturing, love, detail, nutrition, structure, generosity, time, etc. — that humans today need most to overcome our current complex, human-made crises. What can More CARE do for modern people? Our guests are asked to share about the effectiveness of greater care for all in the living Creation through greater empathy, mutuality, relationship, conversation, listening, hearing, seeing, connecting, processing, balancing, healing, and nurturing of ourselves, each other, Earth's biodiversity, and “the environment.” #############REFERENCESR.D. Laing#############PROGRAMI. 0:00 WELCOMEII. 2:00 INTRODUCTIONS III. 6:30 INVOCATION, Melody Harrell • “I love the concept of being called to care. It feels like an invitation and it feels like something I already have tools and capacity-for." • RD Lang reading.12:00 Sam, Real-life story  • “We were building an integrated child development center on the side of a mountain in Northwest Kenya…”18:30 Rev. Calhoun  • “…Now I go out of my way to make sure they know I'm aware of them and they matter and they count.”IV. 23:00 METHODOLOGY24:30 Values • S- “Melody and I are the product of missionary parents” • M- “God had already been there… He or She didn't have to be brought from America” • S- “The example of Jesus (is) our motivating factor, but that does not mean you come into an empty slate. People already have an experience of God”30:30 Kutana • “KUTANA means to meet and exchange profound mutuality... so that we can love according to the way that love should be”  • “You won't discover what a need is, unless you have dialogue and interaction… And that takes time and context and interaction and mutuality." • Melody, “The beautiful practice of story-telling takes time and being close and the space for that to happen.”39:30 Services • “We started with street children in Nairobi.”  • “I discovered there were a ton of children who didn't have their needs met in the rural areas" • Their Integrated model: listen to the community, address food, water, health, school/center construction in participatory way.  • CHANGE FOR CHILDREN (program): Clean water, Nutrition, Immunity, Malaria prevention, Deworming ($1 per child), Teacher training, Help community maintain school48:30 Connections • Sam, “The incarnation is Kutana. It's not God from afar, it's God coming close. It's conversation and hands and flesh. Our model is Jesus”  • Rev. Calhoun, "What's happening globally does have an affect on you” • S, African philosophy is based on this one thing, UBUNTU, “I am because we are.” “I don't have an existence on my own, I need others.”  • S, UJAAMA: “Without each other the whole thing collapses.” • Rev. Julian Calhoun, “I think it's important to remind us that we do need each other."V. 58:00 CARE AS IDENTITY • 58:45 Melody, “A very natural response to our upbringing in that place, our love for the place and for the people, and our calling as people of Faith to love and care for others”  • 1:02:00 Sam, “We came about it naturally, we had good examples in our parents... and liminal spaces and events have led me to be conformed after the way of Christ, for the good of humanity… • “If we can be active in trying to engage the world, but also introspective enough to actually see what it is that we're doing and listen for direction, then some wonderful things can happen. That's all I'm looking for” • 1:06:30 Rev. Jimi Calhoun, “I want to address the missionary aspect — Julaine and I have led and received teams that come to paint buildings, pass out tracks, etc. — some kind of doing and very little being. What I'm hearing tonight, and what the importance of what I understand AfricaExchange to be, is the latter. They're asking people to come and take part and BE with the people. I can unequivocally say that's the most important thing we can do as Westerners”  • 1:11:15 Melody, “The work we do is made possible by incredible partners...and I can almost see God making these connections where maybe some resources can cross our borders” • 1:12:45 Sam, “We have a lot of volunteers, amazing people who teach us every day.” TREES FOR LIFE (program) • “In some of our work we try to help communities protect their environment, without trees and sufficient soil erosion protectant when their floods come it wipes them out • “Every four-year-old plants 3 trees a year, and their parents get paid $1 if that tree survives a year… from that comes clean water and soil health and all the rest of it, so, Trees for Life is integrated into our whole.NATURE AS TEACHER • “Whenever Nature teaches me something I take it as from God.” • Intermittent disturbanceON MIGRATION • “”No one leaves home, unless home is the mouth of a shark.” It's not like people are trying to come and take your stuff. People can't live where they are. Why don't we go and see what's happening to cause this? • “I gotta care for my neighbor and that's basic to our Faith. Love of God, love of self, and love of neighbor are inextricable, and if we're following the path of Jesus - boy, we better be caring for our neighbor.”VI. 1:19:15 CLOSING THOUGHTS  • 1:20:30 Melody, “Most of the good, the real, deep, good work, goes on under the radar.”  • 1:22:45 Sam, “I've come to realize, through the help of many wise-people, we really are operating on the basis of a myth of disconnection… A non-dual way of living, one that is about how things are unified in God, is my inspiration.” • “What we're trying to help people who are marginalized have a voice so they can be part of the conversation, so we realize that we're all in this together.” • 1:25:30 Rev. Calhoun, “To keep us mindful of our place in all of this: in my view, it's something we have to give thought-to. It won't come naturally. It won't come from a book. You have to sit around and think who am I, where am I, why am I… why are we? And then reach the conclusion, what part do I have to play? And the answer is, you do have a part of play. Everyone has a part to play.”1:26:30 Chris Searles, Thank you everybody! #################################Thanks for listening. Produced, etc. by Chris Searles.Presented by AllCreation.org and BioIntegrity.net. Visit AllCreation.org/Care for more content. 

Habari za UN
Najivunia ufadhili wa MONUSCO umeniwezesha kuwasaidia wenzangu:Jafari DRC

Habari za UN

Play Episode Listen Later Sep 2, 2022 3:17


Kutana na Alex Jafari kutoka Goma mji mkuu wa jimbo la Kivu Kaskazini nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, mtaalamu huyu wa kutengeneza simu DRC ambaye kwa msaada wa mpango wa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo MONUSCO aliweza kupatia mafunzo au formation[FORMASSION]  kwa lugha ya kifaransa, vijana wa kike na wa kiume, wakiwemo waliotumikishwa vitani , mafunzo ambayo sio tu yaliwaepusha kujihusisha na vita na kuzurura mitaani bali yamebadili maisha yao. Assumpta Massoi alifika kitongoji cha Majengo jimboni humo  kuzungumza na Alex Safari   

Habari za UN
Lugha ya Kiswahili imenipa ajira Umoja wa Mataifa

Habari za UN

Play Episode Listen Later Jul 14, 2022 2:31


Kutana na Priscilla Lecomte, mtaalamu wa mawasiliano wa UN-CBi, mpango unaoratibiwa na Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu misaada ya dharura, OCHA na shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa maendeleo duniani, UNDP kushirikisha sekta binafsi katika kujiandaa kukabliana na majanga na hata kurejea katika hali nzuri baada ya majanga. Bi. Lacomte ni mzaliwa na raia wa Ufaransa ambaye anaamini lugha zina mchango mkubwa katika kufanikisha malengo ya maendeleo endelevu akitolea mfano lugha aanayoipenda, Kiswahili ambayo alianza kujifunza akiwa kwao Ufaransa kabla ya kubobea aliposafri na kuishi Afrika Mashariki na baadaye kupata kazi katika Umoja wa Mataifa ambako alitumia na anaendelea kutumia Kiswahili katika kazi zake.

Habari za UN
Wakimbizi wakipewa fursa wana mchango katika jamii

Habari za UN

Play Episode Listen Later Jun 20, 2022 2:34


Kutana na wakimbizi Bahati Hategekimana kutoka Rwanda, Micheline Muhima kutoka Uganda na Agnes Mude kutoka Sudan Kusini ambao wote walikuwa wakiishi kwenye kambi ya wakimbizi ya Kakuma nchini Kenya, lakini sasa kupitia mradi wa majaribio wa kuthamini mchango wa wakimbizi EMPP, unaoendeshwa na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR, mjini Pictou na serikali ya Canada watatu hao si wakimbizi tena bali ni wafanyakazi wa huduma ya jamii kwenye kituo cha Glen Haven Manor kilichopo jimboni Nova Scotia nchini Canada.  Bahati, mmoja kati ya wasichana hao watatu waliobahatika kuchukuliwa na kuajiriwa kama wafanyakazi wa kudumu wa  huduma kwenye kituo cha kuhudumia wazee jimboni Nova Scotia baada ya kufaulu usaili wakiwa kambini Kakuma , anasema anahisi fursa hiyo aliyopata si hisani bali amestahili kwani ameifanyia kazi na anajivunia.  Jimbo la Nova Scotia nchini Canada mfano wa kuigwa Jamii ya mjini Pictou jimboni Nova Scotia kwa muda mrefu inakumbatia na kukirimu wakaimbizi ikiwapa malazi na chakula lakini sasa inaenda mbali zaidi kwa kubaini ujuzi wa wakimbizi na kuwapatia ajira ikishirikiana na serikali, UNHCR na wadau wengine kupitia mradi wa majaribio wa EMPP.  Sarah Wiseman Mkurugenzi Mtendaji wa zamani wa mji wa Pictou anasema “Tulichokifanya kwa waajiri wa eneo hili ni kuwafahamisha kwamba kuna kundi lingine la waajiriwa wenye ujuzi ambalo wanaweza kuliangaliawatu hao wana ujuzi, uzoefu na eimu wanayohitaji lakini wamejikuta ni wakimbizi”.  Lengo la mradi huo ni kubaini wakimbizi wenye ujuzi na kuwaunganisha na waajiri ambao wanawafanyia usahili popote walipo na kuwapa ajira inayowasafirisha hadi Canada kufanya kazi.  Maisha mapya Canada kutoka ukimbizi Kakuma Baada ya kuwasili Nova Scotia Bahati, Micheline na Agnes walipewa nyumba na wameanza maisha mapya. Micheline Muhima aliwasili na mwanae mdogo mwenye umri wa miaka miwili na ana matumaini makubwa” Najua mustakabali utakuwa bora, kwa familia yangu na watoto wangu na kwangu mimi kwani nataka kuwa na ujuzi fulani wa kazi.”  Agnes Mude anasema maisha yake yamebadilika tangu alipofika Canada na anashindwa kuficha furaha yake “Mahali hapa ni pazuri sana, na watu ninaofanya nao kazi ni wakarimu sana hali inayonifanya kuhisi ninakubalika.”  Wakimbizi wote hawa watatu wa zamani wanaishukuru sana UNHCR lakini zaidi wanasema wanaamini kwamba jamii zikiwakumbatia wakimbizi basi wakimbizi nao wanarejesha fadhila.   

Habari za UN
Mfinyanzi Nduwimana: Merankabandi imenikomboa mimi na familia yangu

Habari za UN

Play Episode Listen Later May 9, 2022 2:46


Kutana na mfinyanzi Nduwimana Cornalie kutoka nchini Burundi ambaye maisha yake yalikuwa duni, akishindwa kukidhi mahitaji ya msingi ya familia ikiwani pamoja na kuweka mlo mezani na hata kupeleka wanawe shule, lakini sasa asante kwa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF lililoanzisha mrandi wa Merankabandi wa kusaidia familia duni kwa ufadhili wa Benki ya Dunia, maisha yake na ya jamii yake yamebadiliaka. Flora Nducha na maelezo zaidi. Mfinyanzi Nduwimana Cornalie anayeishi katika eneo la Butaganzwa jimbo la Ruyigi Nchini Burundi akisema kabla ya kujiunga na mradi wa Merankabandi maisha yake na familia yake yalikuwa ya dhidi sana, “kama mfinyanzi niliishi kwa kutegemea ufinyanzi wa asili ambapo vyungu na mitundi niliyofinyanga haikunisaidia chochote. Maisha yalikuwa magumu , tulipata fedha kidogo sana”  Lakini kama wasemavyo wahenga Mungu si Athumani Nduwimana akapata Habari za mradi wa Merankabandi na kuamua kujiunga nao, mradi ambao hadi sasa unasaidia kaya 56,090 zisizojiweza nchini Burundi,  hii inamaanisha karibu watoto 280,000 pia wanafaidika , na Nduwimana na familia yake wakiwa miongoni mwao.  Mnufaika mwingine ni Nimfasha Consolate pambaye alikuwa mkimbizi kwa muda mrefu lakini sasa amerejea Butaganzwa h na anafanya biashara ya kupika na kuuza mandazi anasema….”Kupokea fedha bila mafunzo haisaidii sana lakini kupitia mradi huu tumejifunza jinsi ya kuzitumia vyema fedha hizo na hiyo imetusaidia kupata faida ya fedha tulizopewa. Ninachukua mkopo na naweza kuulipa bila matatizo. Na leo hii tunajivunia kwamba tuna mradi unaotuletea pesa, tuna chakula na tunamudu kujikimu kimaisha.”  Kwa Nduwimana ambaye kupitia mradi huu ameyapa kisogo matatizo yake, na kumudu kupeleka watoto wake shuleni hana kingine isipokuwa shukrani kwa UNICEF na Benki ya Dunia, “tunashukuru kwa mradi wa Merankabandi tumejifunza njia za kisasa za kufinyanga vyungu. Tunatengeneza vyungu vya maua, vyungu hivyo ambavyo awali tulikuwa tunauza Faranga za Burundi 100 au 200, sasa kwa faida kubwa tunaviuza kwa Faranga 5,000 na 10,000”  Mradi huo ambao ulizinduliwa kwa mara ya kwanza mwaka 2017, uko katika nchi nzima na lengo lake kuu ni kutumika kama ulinzi wa hifadhi ya jamii kwa familia zisizojiweza kwa kuwawezesha kwa miradi mbalimbali ikiwa ni pamoja na biashara za ujasiriamali, kilimo, na hata ufugaji wa mbuzi, ng'ombe na kuku.       

Habari za UN
Mgeni njoo mwenyeji apone ndio hali wakulima Lodwar baada ya ujio wa WFP na FAO

Habari za UN

Play Episode Listen Later Apr 21, 2022 2:36


Kutana na Agnes mkulima kutoka wilaya ya Lodwar kaunti ya Turkana jimbo la Rift Valley nchini Kenya. Mabadiliko ya tabianchi yanayolikumba eneo la Afrika Mashariki kwa kiasi kikubwa yamemuathiri sana yeye na jamii yake, lakini sasa asante kwa mradi wa pamoja wa mashirika ya Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP na la chakula na kilimo FAO wa kuwasaidia wakulima wadogo kujenga mfereji wa maji kwa ajili ya umwagiliaji na kununua mazao yao, maisha ya Agnes na jamii yake yamebadilika.

Nyumba ya Sanaa
Sanaa ya muziki ushairi inavyotia fora nchini Tanzania

Nyumba ya Sanaa

Play Episode Listen Later Jan 15, 2022 20:09


Sanaa ya muziki ushairi ni sanaa nyingine iliyosheheni tenzi za mafu,bo.zilizobeba ujumbe sambamba na matumizi ya nahau na Methali za lugha adhimu ya kiswahili. Kutana na Mrisho Mpoto almaarufu Mjomba katika makala ya Nyumba ya Sanaa na mwandishi wetu Steven Mumbi.

Habari za UN
Zama za kale si kama za sasa mtoto Angela abaini kutoka kwa nyanya yake Muthoni:UNICEF

Habari za UN

Play Episode Listen Later Nov 23, 2021 2:46


Kutana na Angela Andia mshindi wa mwaka 2021 wa mradi wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF uitwao “wisdom project” au mradi wa busara ambao unashirikisha watoto wa umri wa kati ya miaka 9-14 kila mwaka wakishindana katika kuandaa Habari zinazohusu haki za mtoto nchini Kenya.   Mamia ya watoto wanaharakati wa haki za mtoto waliwasilisha kazi zao za sauti, video, na hata makala zisizozidi dakika mbili na nusu, na mwishoni mwa wiki siku ya mtoto duniani  tarehe 20 Novemba Angela ndiye aliyetangazwa kuwa mshindi wa shindano la mwaka huu baada ya kuwasilisha video anayomuhoji nyanya yake Joyce Muthoni kuhusu masuala mbalimbali akilinganisha enzi za nyanya yake na kizazi cha sasa ikiwemo elimu, michezo, na hata ujumbe ambao angezweza kuwapatia kizazi kichanga kama Angela. Hebu wasikilize katika mahojiano yao  

Habari za UN
Mafunzo ya WFP yamsaidia mkulima kulima mazao mengi na kutafuta wateja kidigitali na kujiongezea kipato zaidi

Habari za UN

Play Episode Listen Later Nov 18, 2021 2:25


Kutana na mkulima Mainner mwenye umri wa miaka 44 , ni mama wa watoto wanne na miongoni mwa wakulima wadogo wadogo 150,000 wanaosaidiwa na shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP kupitia mradi wa kuboresha maisha ya wakulima na kuwajengea mneno, mradi ambao kwake na familia yake umekuwa neema kubwa. Taarifa ya Flora Nducha na taarifa zaidi  Nattss….  Katika eneo la Monze jimbo la Kusini nchini Zambia Mainner na familia yake wapo kwenye shambani kuchambua karanga moja ya mazao ambayo wakulima wadogowadogo wa eneo hili wanalima mengine yakiwa ni mahindi, maharagwe na njugu.  Kabla ya kuingia katika mradi wa WFP wa kuwajengea uwezo na mnepo wakulima, Maina alikuwa akihaha kuweka mlo mezani unaotosheleza familia yake na alishindwa kulipa karo za shule, kwani alikuwa akilima zao moja tu la mahindi ambalo kwa sababu ya ukame mavuno yake yalikuwa haba na alikosa cha kuuza.  Lakini sasa kupitia msaada wa WFP na mafunzo ya kulima mazao tofauti analima mazao matatu, anaweza kutafuta masoko kupitia teknolojia ya simu za kiganjani na pia anapata taarifa kuhusu hali ya hewa na jinsi ya kukabiliana nayo  hali ambayo imeboresha kiwango cha mavuno, lishe ya familia yake na kumuinua kiuchumi.  Nattss…  “Kwa kutumia teknolojia ya simu za mkononi kupitia mafunzo ya WFP naweza kupiga picha mazao niliyonayo na kutangaza na hivyo  kupata masoko ya kuuza idadi kubwa ya mazao”  WFP imemsaidia Mainner kuwa mkulima mchuuzi wa jumla kwani anahifadhi mazao yake katika ghala alilopewa na WFP ili kuepusha upotevu wa chakula na anayauza wakati soko limeimarika na fedha anazopata zinamsaidia kukimu mahitaji yote ya familia ikiwa ni pamoja na kulipia watoto wake shule. Baada ya mafiunzo ya WFP ameweza pia kuwasaidia wakulima wenzie na amekuwa balozi wa soko la kidijitali la wakulima wa eneo lake ambalo linawawezesha kuuza mazao yao mtandaoni. Na kutokana na mfanikio makubwa aliyoyapata mwaka 2018 Mainner alipatiwa Medali tuzo inayotolewa na WFP kwa  mkulima bora.  Sasa anachosema ni asante kwa WFP kwani mradi wake na mafunzo umekuwa neema kubwa kwake na familia yake. 

Habari za UN
Mkimbizi wa DRC aeleza alivyojikombia kiuchumi

Habari za UN

Play Episode Listen Later Oct 26, 2021 2:09


Kutana na mkimbizi Felicitee Anibati kutoka Jamhuri ya Kidemkrasia ya Congo ambaye kwa sasa anaishi katika kambi ya wakimbizi ya Makpandu nchini Sudan Kusini , ni mama, mkulima na mjasiriamali mwenye mafanikio ambaye sasa anatumia mafanikio yake kuwasaidia wanawake wenzie ili kufika alipo yeye. Flora Nducha anasimulia zaidi (TAARIFA YA FLORA NDUCHA) Felicitee akiwa kambini Makpandu nchini Sudfan Kusini ambako anasema aliwasili mwaka 2018 kama mkimbizi na alipenda sana kilimo, mwaka jana alianza kulima mahindi na akafanikiwa kuvuna gunia 9 ambapo aliuza magunia 4 na yaliyosalia yalimfaa kwa chakula na familia yake. Baada ya kupitia madhila mengi ya vita Felicitee amebwaga moyo wake hapa kambini na faida aliyoipata baada ya kuuza mavuno yake akaamua kuanzisha biashara ya ujasiriamali ya ufundi cherahani unaomfaa yeye na wanawake wenzie “Nilinunua pia cherahani na nimejenga pia nyumba tatu kwa kutumia fedha ninazopata. Na hela kidogo iliyosalia nikaanzisha kikundi cha wanawake ambao sasa tunashona pamoja. Tunanunua vitambaa na kushona nguo ambazo tunaziuza.” Hakuishia hapo akiba inayopatikana Felicitee anaitumia kuwasaidia wanawake wengi zaidi kupitia bekari ya kuoka na kupika vitu mbalimbali yakiwemo maandazi na hatua hiyo anasema   Felicitee anaishukuru sana jamii inayomuhifadhi yeye na wakimbizi wengine kwani anasema bila upendo na ushirikiano wao asingeweza kuwa alipo, lakini pia analishukuru shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR ambalo linahakikisha wakimbizi wanapata fursa popote walipo.

Nyumba ya Sanaa
Nyumba ya Sanaa - Uandishi wa vitabu nchini Tanzania

Nyumba ya Sanaa

Play Episode Listen Later Oct 23, 2021 20:12


Umahiri katika Sanaa ya Utunzi wa Vitabu, inabebwa na Maudhui yalimo ndani ya kitabu inawaje Jina la kitabu ndio husadifu yaliyomo katika kurasa za kitabu hicho. Kutana na Ismaily Him Mtunzi wa Vitabu Tanzania, Mtunzi wa Vitabu Usasa Usasambu, Wakilia Wanacheka majina ya Vitabu yanayovutia.

Habari za UN
Ng'ombe mmoja huko Burundi akomboa familia iliyokuwa taabani

Habari za UN

Play Episode Listen Later Oct 21, 2021 1:58


Mtamba mmoja wa ng'ombe anaweza kuonekana si chochote kitu kwa wafugaji wabobezi lakini kwa Beatrice Nibogora na familia yake nchini Burundi, mtamba huyo akipatiwa jina Maza amegeuka lulu na ufunguo wa maisha yenye matumaini na kutimiza methali ya wahenga ya kwamba baadhi ya dhiki ni faraja. Hii ni baada ya mradi wa Benki ya Dunia na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF kubisha hodi kunusuru kaya maskini. Anold Kayanda anafafanua zaidi. (Taarifa ya Anold Kayanda) Kutana na Beatrice Nibogora.. mama huyu anaishi na familia yake ambayo ni mumewe Sylvestre na mwanae Chanique kwenye umri wa miaka 3, katika vilima vya Rwimbogo nchini Burundi. Kutana pia na Maza! Maza siyo tu kwamba ni mtamba mzuri wa kupendeza, usidanganyike! Maza ni mtamba ambaye amebadilisha maisha ya familia hii. Kabla ya ujio wa Maza, Beatrice maisha yalikuwa ya tabu. Licha ya kilimo shambani, mlo wao ulikuwa ni mmoja kwa siku. Siku moja, mradi wa Merankabandi unaofadhiliwa na Benki ya Dunia na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto duniani, UNICEF nchini Burundi, ukabisha hodi nyumbani kwake kumuokoa yeye na familia  yake. Katika kipindi cha miaka mitatu, mradi umepatia kaya maskini 56,000 ikiwemo ya Beatrice migao 15 ya dola 20 sawa na jumla ya dola 300, pamoja na mafunzo ya malezi ya watoto, afya ya mama na mtoto na usimamizi wa fedha, Kupitia simu yake ya kiganjani, Beatrice alipokea fedha hizo za kujikimu. Kwa kiasi hicho kidogo cha fedha, alinunua nguruwe na kuku huku akidunduliza fedha. Siku moja, alifanikiwa kumnunua Maza. Maza akazaa ndama na akaanza kuwapatia  lita 2 na nusu za maziwa kila siku. Beatrice pamoja na kumpatia mwanae Chanique maziwa ya kunywa, pia anatengeneza jibini. Samadi kutoka kwa Maza ikawa mbolea shambani na rutuba ikaongezeka sambamba na mavuno. Njaa imetoweka kwenye familia hii, na ameweza pia kuajiri kijana Jean-Marie anayemsaidia kukata majani ya ng'ombe. Maza amegeuza maisha kuwa rahisi na shuku za awali zimetoweka na nuru imeonekana.

Habari za UN
Mkulima wa maharage nchini Rwanda aeleza mafanikio anayopata

Habari za UN

Play Episode Listen Later Aug 25, 2021 2:04


Kutana na mkulima Immaculée kutoka Rwanda ambaye anajivunia sio tu kupata kipato kujikimu kimaisha kutokana na mahindi na maharage anayolima bali pia jinsi mazao yake yanavyosaidia kuwa neema kwa mamia ya watoto kupitia mlo shuleni. Flora Nducha anasimulia zaidi  (TAARIFA YA FLORA NDUCHA)  Immaculée mkulima mdogo wa maharage na mahindi nchini Rwanda akisema anahisi Faraja kubwa kutambua kwamba mazao ya jasho lake yanawafilia mamia ya Watoto katika program ya shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP ya kuwapatia mlo Watoto mashuleni ikiwemo katika jamii yake.  “Kinachonihamasisha zaidi ni kujua kwamba WFP inanunua nincahozalisha na kusambaza mashuleni ambako watoto kutoka katika jamii yetu wanapata mlo shuleni”  Kama mkulima mdogo aliyejikita na kilimo cha maharage yenye madini chuma kwa wingi anakabiliwa changamoto lukuki lakini mwaka 2018 chama cha ushirika anachokiuzia mazao yake kikaanza kupata msaada kutoka WFP hasa kwa kununua maharage hayo kwa ajili ya program yake ya mlo shuleni nchini Rwanda ambayo lengo lake kuwa ni kuhakikisha Watoto wanapata lishe na kuendelea kusoma lakini pia wakulima wanaozalisha lishe hiyo wanafaidika kiuchumi  “Inachokifanya WFP ni kuunganisha chama chetu cha ushirika na masoko kwa mfano katika msimu uliopita wa mavuno chama chetu cha ushirika kiliuza zaidi ya tani 30 za mahindi na tani 60 za maharage kwa sababu WFP ilitusaidia.”  Immaculee anasema faida anayoipata imemuhamasisha kuwa mkulima stadi na kuzalisha zaidi sio tu kwa ajili ya biashara lakini pia kwa kuhakikisha mlo kwenye familia yake kwani WFP zaidi ya kununua mazao yao inatoa mafunzo, pembejeo na mbegu kwa wakulima.  Na sasa anawachagiza wanawake wenzie kutobweteka kuingia katika kilimo kwani jembe halimtupi mkulima.   

Habari za UN
Ujuzi wa kufuma waisaidia familia kiuchumi

Habari za UN

Play Episode Listen Later Aug 17, 2021 2:19


Kutana na mkimbizi Fidaa kutoka Syria ambaye pamoja na mfamilia yake walifungasha virago miaka minane iliyopita wakikimbia mapigano na kupata hifadhi Libya. Sasa changamoto za janga la corona au COVID-19 zimemlazimisha kurejea mapenzi ya zamani ya ufumaji ili kupata mkate wa kila siku wa familia yake.  (TAARIFA YA FLORA NDUCHA)  …..Nikiwa Syria  Fidaa akiwa katika maskani yake mapya ukimbizini Libya anakumbuka kwamba kufuma kwake haikuwa kwa ajili ya kumudu maisha bali kwa ajili ya mapenzi kwani yeye na familia yake walijitosheleza kwa kila hali  Syria wanamiliki nyumba na kuishia maisha yaraha.  Lakini sasa mama huyo mwenye umri wa miaka 42 hana jinsi bali kugeuza mapenzi ya ufumaji kuwa chanzo cha kipato ili kukimu mahitaji ya familia yake. Na anafuma na kuuza vitu mbalimbali kama anavyoeleza “Ninafuma magauni kwa ajili ya wasichana kwa kutumia uzi wa sweta, nafuma mablanketi, soksi, kofia, vibanio vya nywele na kitu kingine chochote kitakachoniingizia kipato.”  Walipowasili Libya mumewe aiywaye Hani ndiye aliyekuwa akiendesha familia kwani aliweza kufanya kazi mbalimbali za mikono ili kumtunza mkewe na watoto wao wawili wa kike Ghazali na Mariam, lakini janga la corona au COVID-19 lilipozuka kitumbua kikaingia mchanga, kupata kazi ikawa tabu na afya yake ikaanza kuzorota ndipo Fidaa aipoamua kuvaa viatu vya mumewe kuinusuru familia yao. Hani anasema “Alipoanza kufanyakazi ya ufumaji aliziba pengo la fedha tulilokuwanalo. Wakati tulipohitaji sahani nyumbani aliuza gauni na badala ya sahani moja alinunua tatu. Na alipouza kitu kingine alinunua sufuria za kupikia.”  Wakimbizi kama Fidaa na Hani ni sehemu tu ya mamilioni ya wakimbizi wa Syria wanaohaha ukimbizini kwa miaka 10 sasa tangu mzozo kuzuka nchini mwao, na wengi wao wako Lebanon, Uturuki, Jordan, Libya na wengine kwa mamilioni wakisalia wakimbizi wa ndani nchini Syria.  

Men. Men. Men. - The Podcast -
Ep 40 - My Time in Prison

Men. Men. Men. - The Podcast -

Play Episode Listen Later Aug 12, 2021 68:26


Kutana na Tito Magoti, mwanasheria kijana kutoka Tanzania. Mwaka 2019, alijikuta gerezani ambapo alikaa kwa zaidi ya mwaka mmoja. Sasa Tito ametoka, anaendelea na maisha yake. Unahitaji nini ili uweze ku “survive” maisha ya gerezani? Watu wako wanaokuzunguka inabidi wafanye nini ili waweze endelea kukutia moyo? Nini kilichompa Tito nguvu na moyo wa kuishi gerezani na kumfanya asikate tamaa ya maisha? Baada ya kutoka gerezani, jamii imempokeaje Tito? Yupo tayari kuishi maisha ya mtu anayeangaliwa sana na jamii kila anapokwenda? Gerezani kumembadilisha vipi Tito? Na zaidi ya yote, vipi kuhusu afya ya akili magerezani? Maswali ni mengi sana kutoka kwa Michael Baruti pamoja na Mwanasaikolojia Nadia Ahmed, karibu usikilize maongezi haya.

Habari za UN
Dereva mwanamke wa malori ya masafa marefu aeleza nini kifanyike kuongeza madereva wanawake

Habari za UN

Play Episode Listen Later Jul 8, 2021 2:03


Kutana na Maissata Cisse al maaruf Mama Afrika, huyu ni dereva pekee wa malori ya safari ndefu katika ukanda wa Afrika Magharibi akiendesha malori ya mizigo katika nchi za Benin, Burkina Faso, Guinea, Côte d'Ivoire baadhi ya nyinginezo akisema kuwa uboreshaji wa miundombinu ya barabara na tararibu za forodha katika ukanda huo vimekuwa jawabu mujarabu wa kazi yake hiyo aliyoifanya kwa miaka 30 sasa. 

Nyumba ya Sanaa
Nyumba ya Sanaa - Sanaa ya uchoraji Tanzania - Nasma Mzee

Nyumba ya Sanaa

Play Episode Listen Later Jun 24, 2021 20:04


Kutana na msichana wa mwaka wa tatu Chuo kikuu cha Dar es salaam,Nasma  Mzee  akichukua Shahada ya Kwanza ya Sanaa na Ubunifu aliyechagua kuwa Mchoraji ili kuwasilisha Maudhui ya Sanaa aliyosomea.   Ungana na Steven Mumbi katika Makala ya Nyumba ya Sanaa akizungumza na Nasma Mzee.

Habari za UN
Kufanya kazi ya kujitolea ni kukumbatia jamii

Habari za UN

Play Episode Listen Later Jun 23, 2021 2:36


Kutana na mfanyakazi wa kujitolea wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini Jason William Gbambi ambaye ni afisa uhamasishaji wa timu ya maadili na nidhamu ya mpango wa Umoja wa Mataifa nchini humo UNMISS. Anasema kufanya kazi ya kujitolea ni kukumbatia jamii na kutambua mahitaji yao na hasa amani ambayo ni adumu nchini humo. 

Nyumba ya Sanaa
Nyumba ya Sanaa - Sanaa ya utunzi wa mashairi nchini Tanzania

Nyumba ya Sanaa

Play Episode Listen Later Jun 12, 2021 20:03


Kutana na Mshairi Zawadi Mengele aliyejikuta akifanya Sanaa ya Ushairi baada ya kumzawadia Mama yake shairi lililo amsha hisia ya Malezi. Ungana na mwandishi wetu Steven Mumbi  katika makala ya Nyumba ya Sanaa akizungumza na mshairi huyo akianisha namna anavyopokelewa Tanzania.

mama tanzania sanaa nyumba ungana kutana steven mumbi
Habari za UN
Lazima tutokomeze ukeketaji : Mwanaharakati Ifra Ahmed

Habari za UN

Play Episode Listen Later Jun 10, 2021 2:49


Kutana na mkimbizi kutoka Somalia, muathirika wa ukeketaji ambaye hakuacha athari za jinamizi hilo kusambaratisha ndoto zake za kuhakikisha hatopumzika hadi pale mangariba wote watakapobwaga manyanga na kuacha ukatili huo nchini Somalia na kwingineko duniani. Kulikoni Flora Nducha anasimulia zaidi  (TAARIFA YA FLORA NDUCHA)    Jina langu ni Ifrah Ahmed Dublin nchini Ireland maskani  ya kudumu ya Ifra mkimbizi wa zamani aliyegeuka kuwa mwanaharakati wa kupinga ukeketaji na sasa anajivunia kuwa raia wa taifa hilo la barani Ulaya. 

Habari za UN
Mkimbizi Marie-Reine: Programu ya rafiki imenipa ujasiri niliohitaji kuanza maisha mapya Ubelgiji

Habari za UN

Play Episode Listen Later May 18, 2021 2:23


Kutana na mkimbizi Marie-Reine kutoka Jamhuri ya Afrika ya Kati CAR, ambaye sasa amepata hifadhi na anaishi Namur nchini Ubeligiji.

Habari za UN
Mkimbizi Donatien: Nchi yako ni kama mama na kujitenga nayo ni mtihani

Habari za UN

Play Episode Listen Later May 5, 2021 2:19


Kutana na Donatien, mkimbizi wa Burundi aliyeishi Rwanda kwa muda wa miaka 4 na sasa amerejea nyumbani na familia yake kupitia mpango wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR wa kurejesha nyumbani wakimbizi kwa hiyari. Donatien anaeleza ni kwa nini yeye mkewe na wanawe wawili wamekata shauri la kurudi nyumbani.  Leah Mushi na taarifa zaidi.

Habari za UN
Mkimbizi Fidel: Je unawezaje kuanza upya maisha ukiwa umepoteza kila kitu

Habari za UN

Play Episode Listen Later Apr 28, 2021 2:13


Kutana na mkimbizi Fidel kutoka Jamhuri ya Afrika ya Kati CAR ambaye hivi sasa anaishi kwenye kambi ya wakimbizi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC. Fidel alipoteza kila kitu ikiwa ni pamoja na mwanaye wa kiume machafuko yaliposhika kasi CAR na ikamlazimu kufungasha virago na kukimbia, sasa anajaribu kujenga upya maisha yake ukimbizini. Flora Nducha na maelezo zaidi. Katika kambi ya wakimbizi Mashariki mwa DRC, Fidel anajaribu kufanya kila awezalo kufungua ukurasa mpya wa maisha yake ukimbizini.  

Habari za UN
Alaa, mkimbizi ambaye ni mfano wa nguvu katika hali ya changamoto za maisha

Habari za UN

Play Episode Listen Later Apr 22, 2021 2:10


Kutana na Alaa, mkimbizi kutoka Syria ambaye amemudu kuwahamasisha wanawake wenzake kutoka Syria na wenyeji wake Lebanon kutumia michezo na mazoezi ya mwili ili kujenga  kujiamini na pia kujenga  jamii hata wakati wa janga la COVID-19. Anold Kayanda anaeleza zaidi kuhusu mwanamke huyu.

NMU PODCAST
MY KISARAWE EXPERIENCE (WITH ANTIDIUS MARTINE)

NMU PODCAST

Play Episode Listen Later Apr 14, 2021 21:36


Karibu tena kwenye episode nyingine ya NMU PODCAST, Kutana na mwanzirishi wa NMU PODCAST Mr Antidius martine) Kila Mwanadamu kuna vitu anapenda katika maisha, wapo wanaopenda mziki, Movies , Mpira na mengine mengi, kwa Ujumla yote hayo tunayaweka kwanye kipengere cha lifestyle, Wengi wanasema namna ya kuishi au staili au mtindo wa maisha, jambo ambalo utofautiana kuringana na mtu husika kwenye maisha yake. Kwenye Episode hii kutana na ANTIDIUS MARTINE ambaye kwa upnde wake anapenda sana kuangalia mazingira (adventure), kudurusu vitu vipya na kujifunza , kwenye episide hii ameshare nasi EXPERIENCE YAKE JUU YA SAFARI ALIYOIFANYA KWENDA SEHEMU MOJA WILAYA YA KISARAWE inayoitwa PUGU KAZIMZUMBWI. Kupitia episode hii utaweza kujua mambo mengi ambayo yanapatikana Wlaya ya KISARAWE sehemu ya Ifadhi ya misitu lakini pia sehemu ya UTARII ambayo ata yeye alikuwa suprised saana kuikuta KISARAWE. Miasha yana maajabu sana na katika maajabu hayo, maajabu mengine yanaweza kuliletea faida Nchi Husika, Nini sasa kinachopatikana Kisarawe kama maajabu? ........ Ungana na Mr Antidius Martine kwenye episode hii, MY KISARAWE EXPERIENCE upate kuyajua mengi yapatikanayo KISARAWE PUGU KAZI MZUMBWI NATURE RESERVE.

music movies martine nini karibu wengi ungana miasha steka kutana
Habari za UN
Msakata kabumbu mwenye asili ya Afrika atangazwa kuwa balozi mwema wa UNHCR

Habari za UN

Play Episode Listen Later Mar 24, 2021 2:09


Kutana na balozi mwema mpya wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR, si mwingine bali ni mwana kaandanda nyota Alphonzo Davies, anayesakata gozi kwenye timu ya FC Bayern Munich ya Ujerumani lakini pia ni mchezaji wa timu ya taifa ya Canada. Ametangazwa leo kufuatia mchango wake mkubwa kwa wakimbizi. Jason Nyakundi anatupasha zaidi (TAARIFA YA JASON NYAKUNDI) Nattss…. 

Habari za UN
Ingawa COVID-19 imesababishwa nikatwe miguu yangu, katu sitoacha kufuata ndoto yangu-

Habari za UN

Play Episode Listen Later Feb 25, 2021 2:28


Kutana na binti kutoka Uganda, Christine Joyce ambaye anasema asilani hatolisahau janga la corona au COVID-19 ambalo mbali ya kumnyima masomo wakati wa sheria za kusalia majumbani limechangia kumwacha na kilema cha maisha. Hata hivyo amesema hatokata tamaa ya kutimiza ndoto yake ya kuendelea na masomo na hatimaye siku moja kuwa daktari.Jason Nyakundi na maelezo zaidi.

Habari za UN
Mkulima aibuka na mbinu za kuepusha wanyamapori kuvamia mashamba yao

Habari za UN

Play Episode Listen Later Feb 9, 2021 2:21


Kutana na mkulima kutoka Zimbabwe ambaye kupitia miradi ya shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo FAO anajaribu kwa kila njia kuhakikisha mfumo wa kilimo unaboreka lakini pia wakulima wa jamii yake  wanalinda mazingira na kuishi kwa amani na wanyamapori. Jason Nyakundi na maelezo zaidi.

Habari za UN
Mhamiaji asimulia mazingira ya Libya yalivyokuwa tete hadi akarejea nyumbani Sudan.

Habari za UN

Play Episode Listen Later Jan 6, 2021 2:22


Kutana na muhamiaji Mohamed Ahmed Bushara aliyekwenda kusaka maisha Libya miaka mitano iliyopita lakini hali ngumu, ubaguzi , machafuko na kuwekwa rumande vilimkatisha tamaa ya kukimbiza ndoto hiyo na akakata shauri kurejea nyumbani Sudan kushika ustaaranu mwingine kwa msaada wa shirika la Umoja wa Mataifa la uhamiaji IOM na Muungano wa Ulaya. 

Habari za UN
Ukosefu wa utaifa wamwacha mama wa watoto wanne katika mazingira ya shida juu ya shida

Habari za UN

Play Episode Listen Later Dec 15, 2020 2:21


Kutana na Mpho Modise, mama wa watoto wanne ambaye licha ya kuishi nchini Afrika Kusini hana uhakika wa utaifa wake na hivyo anashindwa kupata huduma za msingi kama vile afya na hofu yake kubwa ni kwamba shida inayomkabili yeye ya kukosa utaifa inaweza kuhamia kwa watoto wake labda apate utaifa wa Afrika Kusini.

Habari za UN
Sergio Chekaloff ameishi bila utaifa kwa takriban miongo 7, kulikoni?

Habari za UN

Play Episode Listen Later Dec 9, 2020 2:07


Kutana na Sergio Chekaloff ambaye kwa zaidi ya miongo saba anaishi bila utaifa baada ya nchi tatu alizodhani kuwa ni asili yake ambazo ni Ujerumani, Urusi na Armenia zote kukataa kumtambua na  sasa kwa msaada wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR anaishi Ibiza nchini Hispania baada ya kupewa hadhi ya kutokuwa na utaifa. Kulikoni?

Habari za UN
Mwanaharakati wa hisibati, kulikoni?

Habari za UN

Play Episode Listen Later Dec 2, 2020 2:21


Dunia inakuwa mahali bora pa kuishi ikiwa kila mtu atachangia katika kutaka hali hiyo itokee. Kutana na Yusuf Adamu Ibrahim, mwanaharakati mchanga wa hisabati kutoka jimbo la Bauchi, Nigeria ambaye anabadilisha maisha ya watoto wa shule katika jamii yake kwa kuwasaidia kuboresha ujuzi wao wa hesabu. Yusuf ni hamasa kwa wengi, na ni kijana mdogo wa umri wa miaka 18 mpenda mabadiliko.

Habari za UN
Mwanaharakati wa haki za wanawake aanzisha mahala salama kambini Cox's Bazaar

Habari za UN

Play Episode Listen Later Nov 25, 2020 2:52


Kutana na mwanamke mwanasheria na mwanaharakati wa haki za wanawake Razia Sultana ambaye ameanzisha mahala salama kwenye kambi ya Cox’s Bazaar nchini Bangladesh kwa ajili ya kuwapa msaada wa kisaikolojia wanawake wakimbizi wa Rohingya kutoka Myanmar waliopitia ukatilia wa kijinsia au GBV.

Habari za UN
Kijana Richard anatumia ulemavu wake kuelimisa jamii kuhusu umuhimu wa chanjo dhidi ya polio

Habari za UN

Play Episode Listen Later Nov 24, 2020 1:49


Kutana na Richard Elaka mkazi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC ambaye ni manusura wa ugonjwa wa polio. Yeye anatumia hali yake ulemavu kutokana na Polio kuelimisha jamii umuhimu wa kupatia watoto wao chanjo dhidi ya ugonjwa huo usio na tiba lakini una kinga.

ROAD TO SUCCESS
SPEAKERS CONFERENCE 2020 (Kongamano la wajasiriamali na wazungumzaji)

ROAD TO SUCCESS

Play Episode Listen Later Nov 19, 2020 0:57


Kama wewe ni mjasiriamali au mzungumzaji basi hutakiwi kukosa hii. Kutana na Eric Shigongo, Anthony Luvanda, Aunt Sadaka, Rodrick Nabe na wengine wengi. Jifunze kwa waliofanikiwa.

Habari za UN
Ari ya mwalimu Taneka ya kufundisha ni mfano wa kuigwa

Habari za UN

Play Episode Listen Later Nov 16, 2020 2:06


Kutana na mwalimu Taneka MacKoy Phipps kutoka Kingston Jamaica, ambaye anasema ualimu kwake ni zaidi ya kazi ya kulipwa ujira au wajibu bali ni wito. Kwa sababu ya janga la corona au COVID-19 shule zimefungwa Jamaica na maelfu ya wanafunzi hasa kutoka jamii masikini wanakosa masomo, hivyo akaamua kuja na mkakati wa kufungua darasa kwenye kuta mtaani kuhakikisha kila mtoto hata akiwa masikini anapata fursa ya kusoma wakati huu.

Habari za UN
Wasichana tusigande!- Getrude

Habari za UN

Play Episode Listen Later Nov 13, 2020 3:22


Kutana na msichana mtanzania Getrude Mligo, mwanaharakati kijana wa masuala ya kijinsia ambaye mazingira chanya ya makuzi yake yamemjenga na kuweza kuchukua hatua ya kusaidia watoto wengine wa kike na wasichana kujitambua.

getrude kutana
Men. Men. Men. - The Podcast -
Ep - 25 - How Trauma Affected My Speech

Men. Men. Men. - The Podcast -

Play Episode Listen Later Nov 6, 2020 66:44


Ally Abdallah, alimpoteza baba yake akiwa na umri wa miaka mitano. Baada ya hapo, maisha yake hayakua sawa tena. Ally alipata kigugumizi jambo ambalo lilimpelekea kua na ukuaji tofauti na watoto wengi wa umri wake. Akiwa shule ilimlazimu kuficha kua ana kigugumizi, akiwa nyumbani watu walikua wakimshurutisha kua ajitahidi kuongea vizuri. Unadhani kuishi hivi ni rahisi? Kutana na Ally Abdallah, a comedian ambae anaamini kile anachosema ni muhimu zaidi ya jinsi anavyokisema, Kigugumizi hakijamrudisha nyuma wala kumzuia kuishi ndoto zake.

Habari za UN
COVID-19 imetupatia fursa ya kufahamu mengi-barubaru Iran

Habari za UN

Play Episode Listen Later Oct 28, 2020 2:19


Kutana na mapacha wawili barubaru kutoka nchini Iran, wanasema janga la corona au COVID-19 limewafunza mengi, kuanzia kusomea nyumbani, kukabiliana na upweke na msongo wa mawazo na hata kupika na  majukumu mengine ya nyumbani. 

Habari za UN
Yoga yawa mkombozi kwa mkimbizi kambini Kakuma

Habari za UN

Play Episode Listen Later Oct 12, 2020 2:03


Msongo wa mawazo, kiwewe na matatizo mengine ya akili ni moja ya changamoto zinazowapata wakimbizi kutokana na mazingira wanamoishi au maisha waliyopitia. Kutana na Rita Brown, mkimbizi kutoka Uganda ambaye anatumia nguvu ya mazoezi ya viungo aina ya Yoga kuleta ustawi na uponyaji kwa wakimbizi walioko katika kambi ya wakimbizi ya Kakuma nchini Kenya.

Habari za UN
Fiona Beine: Changamoto kwangu ni fursa ya kujifunza:Fiona Beine

Habari za UN

Play Episode Listen Later Oct 1, 2020 2:15


Kutana na Fiona Beine mmoja wa wanawake wanaotoa mchango mkubwa katika operesheni za ulinzi wa amani za Umoja wa Mataifa. Hivi sasa yeye ni naibu mshauri wa masuala ya usalama kwenye kwenye idara ya usalama ya mpango wa Umoja wa Mataifa nchini Iraq UNAMI.  Fiona Bine ni raia wa Uganda akiwa katika eneo lake la kazi mjini Baghdad nchini Iraq anasema yeye ni mtu anayependa kukabili changamoto kwa sababu zinampa mafunzo katika maisha yake. 

Habari za UN
Chiwele: Nilianzisha PsychHealth kuziba pengo la huduma za afya ya akili Zambia.

Habari za UN

Play Episode Listen Later Sep 28, 2020 1:48


Kutana na Kayumba Chiwele mwanaharakati wa masuala ya afya ya akili nchini Zambia na pia mshindi wa tuzo ya Benki ya Dunia ya malengo ya maendeleo endelevu SDGs katika kanda ya Mashariki na Kusini mwa Afrika iliyotolewa mwishoni mwa wiki. Yeye na shirika alilolianzisha la PsychHealth wanapigia upatu upatikanaji wa huduma za afya ya akili hasa wakati huu wa janga la corona au CIVID-19.

Habari za UN
Kuwa mkimbizi bila kazi Lebanon ni mtihani mkubwa: Mkimbizi Ibrahim

Habari za UN

Play Episode Listen Later Aug 27, 2020 2:32


Kutana na mkimbizi Khalili Ibrahim kutoka Syria ambaye ajali na athari za janga la corona au COVID-19 ilimlazimisha kumwachisha binti yake shule ili afanye kazi taarifa zaidi na Jason Nyakundi Mjini Beiruti nchini Lebanon mkimbizi Khalil Ibrahim kutoka Syria akiwa ndani ya hema lake na familia yake kwenye makazi ya wakimbizi ya Tripoli. Miongoni mwa wanafamilia hao ni binti yake Nahid mwenye umri wa miaka 12. 

Habari za UN
Ni wajibu wangu kuwasaidia na kuwalinda watoto hata wakati wa COVID-19: Sreyoun

Habari za UN

Play Episode Listen Later Aug 24, 2020 2:12


Kutana na mtaalam wa huduma za kijamii za watoto nchini Cambodia Tim Sreyoun ambaye anasema licha ya janga la corona au COVID-19 ni wajibu wake kuhakikisha watoto wanahudumiwa na kulindwa dhidi ya ukatili kwani ni zahma aliyoipitia maishani mwake. Mjini Battambang nchini Cambodia huyo ni Tim Sreyoun mtaalam wa ustawi wa jamii ambaye kazi yake kubwa ni kuwalinda watoto dhidi ya ukatili na anafanya kazi na idara ya serikali ya ustawi wa jamii jimboni hapo.  

Msasaonline
FAIDA ZA KUTUMIA MITANDAONI YA KIJAMII ILI KUTANGAZA BIASHARA YAKO.

Msasaonline

Play Episode Listen Later Jul 21, 2020 3:25


1. Inachangia kufahamika zaidi kwa biashara yako. Mitandao ya kijamii ni moja ya njia za kutangaza biashara yako kwa gharama nafuu zaidi na inauhakika wa kuwafikia wateja wengi zaidi, kwani asilimia kubwa ya watu wengi sasa hivi wanatumia muda mwingi sana katika mitandao ya kijamii hivyo kutangaza biashara yako kutakuongezea idadi ya wateja na watu wenye ufahamu wa kutosha kuhusu biashara yako kwa ujumla. 2. Inapanua wigo wa kupata wateja wapya tofauti na wale wanaokuzunguka. Kutumia mitandao ya kijamii kwa ajili ya kutangaza biashara yako kuna kuongezea wigo wa wateja wapya ambao ni vigumu kufahamu kuhusu biashara yako kwani wako mbali na eneo la biashara husika lakini Mitandaoni ya kijamii inakupatia nafasi ya watu wote watakao Kutana na tangazo la biashara yako kuifahamu na kushawishika kutumia bidhaa zako na hivyo kugeuka wateja wa biashara yako. 3. Inajenga uhusiano wa karibu na wateja wako. Kupitia ukaribu unaojengeka baina ya biashara yako na wateja wako hii inasaidia kuweka ukaribu wa kusikiliza maoni, shida na kutafuta ufumbuzi kiurahisi wa kero za wateja wako kwani kwa urahisi kabisa wanaweza kuwasilisha maoni yao kupitia akaunti za biashara yako za mitandao ya kijamii. 4. Inaongeza imani na uaminifu wa watu kwenye biashara yako. Moja ya malengo ya kila biashara ni kutengeneza wateja waaminifu na wakudumu wa bidhaa za biashara hiyo, hivyo Mitandaoni ya kijamii kupitia ukaribu unaojengeka baina ya biashara na wateja wake na urahisi wa taarifa za biashara yako kumfikia mteja inapeleka kutengeneza wateja waaminifu na wakudumu wa biashara yako. 5. Inasaidia kupunguza gharama za uendeshaji wa biashara yako. Biashara nyingi hutumia fedha nyingi kwaajili ya kujitangaza na hili huonekana pale ambapo njia zinazotumika kutangaza biashara husika zinakuwa ni ghali sana na hivyo kuongeza gharama za uendeshaji wa biashara husika. Kupitia matumizi ya mitandao ya kijamii kama njia ya kujitangaza inapunguza gharama hizo na kujitangaza na kupelekea kupunguza gharama za uendeshaji wa biashara na kuipatia nafasi nzuri ya kifedha zaidi. 6. Inaongeza ufahamu wa kutosha dhidi ya soko husika na wateja wako. Kupitia ukaribu unaojengeka wateja wako katika mitandao ya kijamii na kujibu comments za wateja wako katika mitandao ya kijamii hii inapelekea biashara husika kupata taarifa za kutosha za soko husika na kuipa nafasi biashara kuwa na taarifa za kutosha za wateja wake na hii inasaidia biashara Kufanya maamuzi na kuweka mikakati inayohitajika kwa wakati husika na soko husika. Hizo ni baadhi ya faida za kuitumia mitandao ya kijamii kuitangaza biashara yako na kama bado haujaanza kutumia mitandao ya kijamii ni vyema ukaanza sasa kwani unapitwa na mengi ambayo biashara yako ingenufaika kwa kutumia mitandao ya kijamii. Asilimia 90 ya wataalamu wa masoko wanakiri kuwa Mitandaoni ya kijamii ina nguvu sana katika kutangaza biashara na imekuwa ikionyesha matokeo chanya katika biashara zao.baadhi ya mitandao ya kijamii inayotumika sana katika matangazo ya biashara ni kama Facebook, Instagram, Twitter, Blogs, YouTube, LinkedIn,nk.

Habari za UN
Mradi wa UNICEF Liberia wadhihirisha uwezo wa barubaru katika kubadili maisha yao

Habari za UN

Play Episode Listen Later Jul 6, 2020 1:33


Nchini Liberia, mradi wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF wa kuboresha maisha ya wasichana barubaru umekuwa na mchango mkubwa katika kushirikisha kundi hilo kwenye harakati za kuinua jamii zao na wakati huo huo kurejea shuleni. Ahimidiwe Olotu na maelzo zaidi. Kutana na Hawa Wanita Page (Pegh) mratibu wa mradi wa UNICEF kuhus barubaru nchini Liberia.

Habari za UN
India, mradi wa IFAD wawanawirisha wanawake wa vijijini

Habari za UN

Play Episode Listen Later Jul 2, 2020 2:38


Kutana na wanawake wa Tejaswini nchini India,  ikimaanisha kwamba ni wanawake walionawiri na kuwezeshwa. Kupitia mradi wa kuwapa mafunzo wa mfuko wa kimataifa wa maendeleo ya kilimo IFAD wameweza kujitegemea, kusaidia familia zao , kusaidia na kushamiri. Taarifa inasomwa na Jason Nyakundi. Katika jimbo la Marastra nchini India wanawake hawa walionawiri au Tejaswini ni sehemu ya wanawake milioni moja wa India walio katika program ya uwezeshaji wanawake vijijini inayofadhiliwa na IFAD.

Habari za UN
Ingawa mimi ni mkimbizi lakini Kakuma ni nyumbani:Nhial Deng

Habari za UN

Play Episode Listen Later Jun 19, 2020 2:28


Kutana na Nhial Deng mkimbizi kutoka Sudan Kusini anayeishi katika moja ya kambi kubwa ya wakimbizi ya Kakuka nchini Kenya. Leo anatueleza jinsi siku yake inavyokua na anavyojilinda na janga la COVID-19. Ambatana na Jason Nyakundi akisimulia zaidi

covid-19 kenya deng kakuma lakini nyumbani sudan kusini kutana ambatana
Habari za UN
Kutana na Sajenti Desta anayesifika kwa kutengeneza magari ya UNMISS, Sudan Kusini

Habari za UN

Play Episode Listen Later May 28, 2020 2:44


Wanawake wanaohudumu katika shughuli mbalimbali za Umoja wa Mataifa kote duniani wanaendelea kujizolea umaarufu kutokana na uchapakazi wao. Mmoja wao ni Almaz Kabtimer Desta, Sajenti anayefanya kazi katika Mpango wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini UNIMISS akihudumu kama fundi makenika. John Kibego na maelezo zaidi.

AWR - Shan - Voice of Hope - lik tái ရွမ္း

Shan knowledges.healthy life14.Shan modern song end of this earth.I surrender all.Brightly Beams our father mercy.

shan new brain cc2 kutana
Unreached of the Day
Pray for the Kutana in India

Unreached of the Day

Play Episode Listen Later Mar 11, 2020 1:01


People Group Summary: https://joshuaproject.net/people_groups/17345 Listen to the "Gateway to the Unreached" with Greg Kelley, produced by the Alliance for the Unreached: https://alliancefortheunreached.org/podcast/

Nyumba ya Sanaa
Nyumba ya Sanaa - Ushairi umesaidia kukuza Fasihi

Nyumba ya Sanaa

Play Episode Listen Later Dec 14, 2019 20:34


Umuhimu wa Ushairi katika kukuza fasihi,Kutana na Steven Mumbi katika Mkala ya Nyumba ya sanaa.

sanaa umuhimu nyumba kutana steven mumbi
Nyumba ya Sanaa
Nyumba ya Sanaa - Kutana na Mchoraji wa Vibonzo 'Muhidin Msamba'

Nyumba ya Sanaa

Play Episode Listen Later Aug 26, 2019 20:05


Ungana na Steven Mumbi akizungumza na Mchoraji wa Vibonzo Muhidini Msamba kuhusu safari yake ya sanaa na Mapokeo ya sanaa hiyo kwa Ujumla.

sanaa nyumba ungana kutana steven mumbi
Nyumba ya Sanaa
Nyumba ya Sanaa - Hali ya Muziki na Wanamuziki wa Tanzania

Nyumba ya Sanaa

Play Episode Listen Later May 16, 2019 19:57


Kutana na Imelda Munyaga Mwalimu wa Sanaa za aina mbalimbali. Katika Makala haya anazungumza na Steven Mumbi kuhusu Sanaa ya Muziki na Uigizaji.

tanzania sanaa muziki nyumba katika makala kutana steven mumbi
Swahili Talk Radio Podcast
Hamisa VS Diamond

Swahili Talk Radio Podcast

Play Episode Listen Later Sep 27, 2018 6:53


Kutana na mtangazaji wa Sahilitalk Podcast, Rehema nkalami akikuchamulia interview ya hamisa Mobeto...... Hamisa asema kasha zaa na Diamond ham hitaji tena.

diamond rehema kutana