POPULARITY
Steven Mumbi anaangazia sanaa ya uchongaji jijini Dar es Salaam nchini Tanzania.
Steven Mumbi amezungumza naye msani Real Jofu kuhusu muziki wa Bongo Fleva.
Lumole Matovolwa ni Miongoni mwa waigazi wa filamu ya kwanza ya Kibiashara nchini Tanzania ya Girl Friend amezungumza na Steven Mumbi katika Makala ya Nyumba ya Sanaa.
Muziki wa asili hubeba ujumbe unaoakisi Utamaduni wa Jamii ,kwa Tanzania Muziki wa Singeli unatajwa kuakisi Utamaduni wa Kitanzania, Ungana na Steven Mumbi katika Makala ya Nyumba ya Sanaa akizungumza na Mwanamuziki wa Muziki wa Singeli Hemed Kiduku.
Safari ya Muziki wa kizazi kipya inaanzia mbali,sasa vijana wanalazimika kusafiri kutoka Mikoani kuja jijini Dar es salaam ili kufaulu kisanaa, Eddy Music ni msanii wa Muziki anazungumza na Steven Mumbi katika Makala haya.
Mara baada ya kutoka Jela Msanii Real Jofu anasema amejifunza kuwa mvumilivu ili kufikia malengo,Ungana na Steven Mumbi kaktika Makala ya Nyumba ya Sanaa akizungumza na Msanii huyo.
Samir Kassim Rashid maarufu Samir Kinyulinyuli ni Msanii wa Sanaa ya Muziki aliyelazimika kukimbilia Dar es salaam akitokea Morogoro ili kufanikiwa kisanaa, Ungana na Steven Mumbi katika Makala ya Nyumba ya Sanaa ya Jumahili.
Sanaa ya Muziki Nyanda za Juu kusini mwa Tanzania, ni sanaa inayokua kwa kasi vijana wanawekeza kulifikia soko la Muziki Afrika Mashariki, B2K ni Msanii anayekonga Nyoyo za Wasichana zaidi kutokana na Tungo zake, Ungana na Steven Mumbi katika Makala ya Nyumba ya Sanaa akizungumza na B2K kutoka Njombe.
Uchoraji ni Ajira ,Wasanii wa sanaa hii Zanzibar wananeemeka na kazi zao, Ungana na Steven Mumbi akizungumza na Obedience na Muki kutoka Zanzibar.
Wachoraji visiwani Zanzibar walia na gharama za kupata maeneo ya kunadi kazi zao za Sanaa hiyo, Ungana na Steven Mumbi katika Makala ya Nyumba ya Sanaa akizungumza na Mchoraji maarufu visiwani humo Jamal.
Taarab Asilia ni Miongoni mwa Miziki ya kale zaidi katika Mwambao mwa Bahari ya Hindi, Zanzibar Taarab Hertage Ensemble ni miongoni mwa Makundi ya Muziki huo kutoka Visiwani Zanzibar, Ungana na Steven Mumbi katika Makala ya Nyumba ya Sanaa.
Wanamuziki wa Muziki wa asili wamebadili vionjo vya asili wakijumuisha na vionjo vya Kisasa ili kuupaisha Muziki Kimataifa, Steven Mumbi amezungumza na Leo Mkanyia Mwanamuziki wa Muziki wa Asili kutoka Tanzania
Wasanii wa Muziki wa kizazi kipya wanaochipukia nchini Tanzania walalama kutakwa Kimapenzi wa Watayarishaji wa Muziki, Ungana na Steven Mumbi katika Makala ya Nyumba ya Sanaa akiwa na Zainisha Nokolage maarufu Zainisha.
Steven Mumbi amezungumza na Lyala Sebastian Mchongaji wa Sanaa za Vinyago.
Wabunifu wa Sanaa ya Uchongaji Vinyago wamewekeza katika kung'amua fursa ya biashara kwa Mataifa ya Afrika Mashariki ili kujikwamua na vipato Duni, Steven Mumbi amezungumza na Mintanga Ramadhani Msanii wa Sanaa za Uchongaji Vinyago kutoka nchini Tanzania.
Sanaa ya ushairi inawavutia zaidi watu wanaotamani kujua utamu na upekee wa lugha adhimu ya Kiswahili, Chuo kikuu cha Dar es salaam kimewatambua na kuwapa fursa vijana waliosomea fani ya sanaa, kubobea katika kughani Mashairi. Ungana na Steven Mumbi katika Makala ya Nyumba ya Sanaa akizungumza na Msanii Michael James maarufu Michael.
Mwandishi wetu Steven Mumbi amezungumza na kundi la wasani la viongozi generation.
Muziki wa kizazi kipya umewawezesha vijana nchini Tanzania kujikwamua kimaisha kwa kujipatia kipato kupitia Sanaa hiyo,Katika Makala haya Steven Mumbi anazungumza na Hussein Mussa Shundi Maarufu Rucky.
Msanii wa Bongo Fleva, Baraka the Prince anauona muziki ni maisha, jambo linalomfanya afikirie zaidi namna mashabiki wake wataishi na kazi zake, Ungana na Steven Mumbi katika Makala ya Nyumba ya Sanaa akizungumza na Msanii huyo.
The Mafiki ni kundi la Muziki lililovuma kwa vionjo vya Muziki wa sasa, sasa wamekuja upya mara baada ya kusambaratika, Ungana na Steven Mumbi akizungumza na wasanii wa kundi hilo.
Mapinduzi ya Muziki wa Taarab yanajidhihirisha katika tenzi za wasanii wa Muziki huu kutoka tungo za Majigambo na sasa tungo za kuburudisha, Ungana na Steven Mumbi katika Makala ya Nyumba ya Sanaa akizungumza na Jike la Chui.
Zumbukuku ni miongoni mwa nyimbo zilizofanya vizuri katika muziki wa taarab, hii inashehenezwa na sauti ya kipekee ya kiume inayosikika katika muziki huo, Ally Star ndie aliyeimba wimbo huo; Ungana na Steven Mumbi katika makala ya Nyumba ya Sanaa akizungumza na Ally Star kuhusu namna nyimbo hizo zilivyotia fora.
Nyota Tiger ni mzaliwa wa jijini Mwanza nchini Tanzania alilazimika kusafiri mpaka maeneo ya kusini mwa Afrika kukwepa adha za wazazi kumnyima fursa ya kufanya muziki. Ungana na Steven Mumbi katika Makala ya Nyumba ya Sanaa.
Muziki wa Singeli ni Miongoni mwa Muziki unaokua kwa kasi nchini Tanzania na nchi za Afrika,Wasanii wa Muziki huo wanapambana kuukuza Kimataifa, Man Fongo ni Miongoni mwa Wasanii Pendwa wa Muziki huo,Ungana na Steven Mumbi anazungumza na Msanii huyo.
Katika Makala ya Wiki hii, Steven Mumbi amezungumza naye Jilema Ng'wana Shija msani wa muziki wa asili kutoka nchini Tanzania.
Karibu katika makala ya Nyumba ya sanaa nami Steven Mumbi, hii leo Msanii Tourna Boy wa kizazi kipya kutoka mjini Goma mashariki mwa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo akielezea kuhusu juhudi za vijana wasanii kuchangia katika juhudi za kurejesha amani ya mashariki mwa nchi hiyo, katika mazungumzo na mwenzangu Ruben Lukumbuka alipotembelea eneo la Goma mwanzoni mwa mwezi mei mwaka huu 2024
Asha Jumbe maarufu White Maria ni Muigizaji aliyejizolea umaarufu akiwa na umri wa Miaka nane tu, sasa ni mtu Mzima aja kivingine kufanya sanaa ya Fimalu za kiswahili,Ungana na Steven Mumbi katika Makala ya Nyumba ya Sanaa akizungumzia safari yake ya Uigizaji.
Sanaa ya Muziki imenihitaji kuliko nilivyo ihitaji, ni kauli yake Steven Ibrahim maarufu Eddy Music alipozungumza na Steven Mumbi katika Makala ya Nyumba ya Sanaa.
Mwandishi wetu Steven Mumbi amezungumza na msani wa muziki huu wa Baibuda
Steven Mumbi amefanya mahojiano na Rahama Machupa msanii wa nyimbo za taarab nchini Tanzania.
Muziki wa Reggae ni miongoni mwa Miziki iliyopata mashiko mapema zaidi ukilinganisha na aina nyingine ya Muziki nchini Tanzania, Innocent Galinoma akiishi nchini Marekani ni miongoni mwa wasanii wa Mwanzo wa Muziki huo nchini Tanzania, Steven Mumbi amezungumza naye katika Makala haya.
Ambwene Mwasongwe ni Muimbaji wa Nyimbo za Injili kutoka nchini Tanzania, aliyejizolea umaarufu kutokana na nyimbo zilizojaa simulizi za Maisha na kubadili mitizamo kuhusu Maisha, Ungana na Steven Mumbi anazungumza na Muimbaji huyo.
Miongoni ma wanamuziki wa muziki wa dansi waliofanikiwa kwenda barani Ulaya ni pamoja na Fresh Jumbe, baada ya kufanya sanaa hiyo kwa miaka mingi nchini Japan sasa amerejea Tanzania, Ungana na Steven Mumbi katika makala ya nyumba ya sanaa akizungumza na msanii huyo.
Diamond Platinumz ni miongoni mwa wasanii wa Tanzania walimvutia kufanya sanaa hiyo, Ungana na Steven Mumbi katika Makala ya Nyumba ya Sanaa
Muziki wa Dansi unachukua sura mpya baada ya Vijana waofanya muziki wa aina nyingine kugeukia muziki huu, Steven Mumbi amezungumza naye Fredrick Fulmeradius
Wazazi chanzo cha Wasichana kutofanya Muziki Tanzania, Steven Mumbi anazungumza na Zulfa Mohamed maarufu Xoul
Anasema wizi wa kazi za sanaa unawarudisha nyuma wasanii na hivyo kuathiri kazi zao.Ungana na Steven Mumbi katika makala ya nyumba ya sanaa akizungumza na msanii huyo.
Wasanii wa Muziki wa Singeli wafurahia kupewa Msaada na Serikali ya Ufaransa ili kuinua kazi zao kimataifa, Ungana na Steven Mumbi akiangazia namna fedha hizo zitakavyowasaidia kubadili Sanaa zao.
Tommy Thomas Msanii wa HIP HOP anasema Muziki wake unapenya kutokana na aina ya Mashairi anayotunga, Steven Mumbi amezungumza naye katika Makala haya ya Nyumba ya Sanaa.
Muziki wa Reggae ni Sanaa iliyofifia nchini Tanzania, miongoni mwa sababu zinazotajwa ni pamoja na kudorora kwa matamasha ya muziki huo, Steven Mumbi anazungumza na Paul Mihambo mwanamuziki wa Reggae nchini humo.
Abby love na Addo Six, vijana wanaofanya Sanaa ya Muziki wa Bongo Fleva kutoka Dar es salaam wakizungumza na Steven Mumbi katika Makala ya Nyumba ya Sanaa.
Faraja Habakuki Group ni kundi la muziki wa Injili kutoka mkowa wa Kivu Kusini eneo la mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ambako vijana wadogo wameanza kujitokeza na kufanya sanaa ya muziki wa Injili, kuepukana na umasikini lakini pia hofu ya mapigano ya mara kwa mara katika eneo hilo. Ungana na Steven Mumbi akizungumza na Kundi hilo.
Lwiza Mbutu ni Muimbaji Pekee wa Muziki wa Dansi nchini Tanzania aliyedumu na Bendi ya African Stars maarufu 'twanga pepeta' Pekee tangu kuasisiwa kwa Bendi hiyo mwaka 1998, nini siri, Steven Mumbi amezungumza na Lwiza Mbutu Makala ya Nyumba ya Sanaa .
Muziki wa Hip Hop kwa wanawake si jambo zoeleka katika sanaa ya muziki nchini Tanzania, kutana na msanii TK NENDEZE akizungumza na mwandishi wetu Steven Mumbi katika makala ya Nyumba ya Sanaa wiki hii.
Steve RNB ni msanii wa muziki wa kizazi kipyamakitamba na kibao Jambo Jambo kipi kilisukuma kufanya sanaa hii ya Muziki, Ungana na Steven Mumbi katika Makala ya Nyumba ya Sanaa akizungumza na msanii huyo.
Pokea Vanillah Music ni miongoni mwa watunzi wa nyimbo na sasa kageukia uimbaji wa muziki wa kizazi kipya, kibao " Unanisitiri " ni miongoni mwa vibao pendwa. Kukipata kibao hiki kwa undani zaidi, ungana na mwandishi wetu Steven Mumbi katika Makala ya Nyumba ya Sanaa akizungumza na Vanillah.
Makala ya Nyumba ya Sanaa ya juma hili, inamwangazia msanii Steven Charles almaarufu Samertz ni mtayarishaji wa muziki wa kizazi kipya kutoka nchini Tanzania, sasa amegeukia uimbaji wa muziki huo, Je nini kimetokea kiasi cha kuanza kuimba? ungana na Steven Mumbi akizungumza na Msanii huyo katika Makala ya Nyumba ya Sanaa.
Mabadiliko ya Sanaa ya uimbaji yamewafikia waimbaji wa nyimbo za Injili, sasa wanafanya Sanaa hiyo kwa kuendana na hali ya mabadiliko ya kiteknolojia kwenye sanaa ya muziki wa kisasa. Ungana na Steven Mumbi katika Makala ya Nyumba ya Sanaa akizungumza na muimbaji wa nyimbo za Injili Goodluck Gozbert.
Uchoraji ni Sanaa ya Urithi, kutoka Mji Mkongwe visiwani Zanzibar urithi wa sanaa hiyo umetamalaki, Ungana na Steven Mumbi katika Makala ya Nyumba ya Sanaa akiangazia sanaa hiyo.
Muziki ni sanaa inachipuka kwa kasi eneo la mashariki mwa DRC, wasanii wanafanya sanaa inakubalika miongoni mwa jamii inayosikiliza lugha adhimu ya Kiswahili, Ogisha Matale ni msanii wa kizazi kipya kutoka mji wa Goma,mkoani Kivu kaskazini mashariki mwa nchi hiyo akielezea changamoto wanazokabiliana nazo wasanii katika kipindi hiki eneo lao likichukuliwa kuwa kitovu cha usalama mdogo. Ungana na Steven Mumbi katika Makala ya Nyumba ya Sanaa.