Kwenye makala ya Afrika ya Mashariki unahabarika na kuelimika juu ya changamoto za maisha ya wananchi wa Afrika Mashariki na eneo zima la maziwa makuu. Usipitwe na Makala ya Afrika ya Mashariki kwani unapata nafasi ya kutoa mawazo yako na kusikiliza wataalamu mbalimbali watakaokuwezesha kubadili fi…
Rfi - Victor Melkizedeck Abuso
Tunaangazia juu ya kituo cha wagonjwa wa ukoma na vikongwe kilichoko Kolandoto, mkoani Shinyanga, Tanzania. RFI imefika kituo cha Kolandoto ambapo kituo hicho kilichojengwa mwaka 1914 maalumu kwa wagonjwa wa Ukoma, leo hii kituo hicho kimegeuka kimbilio la vikongwe wanaotuhumiwa kwa uchawi ili wasiuawe na jamii inayowazunguka.
Leo tunaangazia juu ya changamoto za usalama barabarani nchini Tanzania. Kwa namna ya pekee utawasikia wadau mbalimbali wa vyombo vya moto huko mkoani kagera wakiangazia changamoto walizonazo ikiwezo ukosefu wa mafunzo ya utambuzi wa alama za barabarani lakini pia kutojua sheria za barabarani kwa madereva na abiria.
Leo tunaangazia juu ya mapambano dhidi ya biashara, unyonywaji na usafirishaji binadamu kwenye ukanda wa afrika ya mashariki. Kwa mjibu wa mtaalamu wetu Bi. Winnie Mtevu kutoka Nairobi Kenya, vitendo hivo viovu dhidi ya binadamu vinafanywa ndani na hata nje ya mipaka ya nchi husika, ikiwa ni kinyume kabisa na haki za binadamu.
Leo tunaangazia sehemu ya pili na ya mwisho ya baadhi ya makala zilizoletwa kwako mwaka uliopita wa 2021. Baadhi yake ni pamoja na utengenezaji wa nishati mbadala nchini Tanzania, uhusiano baina ya Burundi na Rwanda, wanafunzi kuagizwa kuni shule za msingi Tanzania, pia pendekezo la kuundaa mkoa mpya wa Chato nchini Tanzania.
Tunaangazia sehemu tu ya baadhi ya makala zilizoletwa kwako mwaka huu wa 2021. Baadhi yake ni pamoja na uhusiano baina ya jamii ya wakimbizi na wenyeji Tanzania, Uhusiano baina ya wenyeji na raia wa Burundi na Tanzania, wasomi wa Afrika ya Mashariki kusaka ajira nje ya nchi zao, pamoja na Rushwa nchini Burundi.
Leo tunaangazia juu ya tatizo la mimba kwa watoto wa kike nchini Tanzania hususan nyakati hizi wanafunzi wawapo likizo. Baadhi ya wadau wakiwemo wazazi na viongozi wa kiroho wanaangaziatatizo hilo lilalotatiza ndoto za mtoto wa kike nchini Tanzania.
Leo tunaangazia juu ya changamoto zinazowakumba waendesha vyombo vya moto nchini Tanzania. Kwa namna ya pekee tutajikita kuongea na wadau wa magari na pikipiki huko mkoani Kagera nchini Tanzania akiangazia kuwa baadhi ya changamoto ni pamoja na ukosefu wa mafunzo ya sheria zabarabarani. Waendesha vyombo vya motona baadhi ya abiria wanaeleza uhitaji mkubwa wa elimu juu ya alama za barabarani
Julian Rubavu anaangazia siasa za Burundi hususan taarifa za kupotea na kukamatwa wafuasi wa vyama vya upinzani kikilengwa zaidi chama cha CNL kinachoongozwa na Agathon Rwassa.
Tunaangazia juu ya uhifadhi na utunzaji mazingira nchini Tanzania. Kwa namna ya pekee, RFI imetembelea kiwanda cha kutengeneza mkaa mbadala tofauti na uchomaji miti. Shirika lisilo la kiserikali ya REDESO (relief for development society) ndio linajishughulisha na upatikanaji wa nishati mbadala kwa ajili ya kuhudumia wakimbizi wasio jiweza kambini Nyarugusu, mkoani Kigoma,
Kwenya makala haya mwandishi wetu, Juliani Rubavu, anaangazia uhusiano baina ya raia wa Tanzania wanaoishi kwenye mpaka wa Manyovu wilayani Buhigwe mkoani Kigoma, na jirani zao wa tarafa ya Mabanda mkoani Makamba, nchini Burundi. Wenyeji wa pande zote wanaeleza kuwa uhusiano wao ni mzuri na wanashirikiana kwa kila jambo. __________________________
Leo tunaangazia umuhimu wa Michezo kwa Mwanafunzi kwa Afya ya mwili na akili. Kwenye kipindi hiki utawasikia baadhi ya wadau wakiwakilishaa makundi mbali mbali ya watoto, walezi, wazazi, na wataalamu nchini Tanzania wakiangazia umhimu wa michezo.
Leo tunaangazia kuhusu uhuru wa kujieleza na kutoa maoni pamoja na athari za sheria ya mitandao nchini Tanzania. Kwa miaka ya hivi karibuni nchini Tanzania kumekuwepo na minong'ono ya hapa na pale ndani ya jamii kuhusu misingi ya kidemokrasia, uhuru wa kikatiba, na sheria za mitandao.
Tunaangazia juu ya changamoto za ujasiriamali kwenye vikundi vya walemavu nchini Tanzania. Kwa namna ya pekee tutawasikia baadhi ya walemavu na wadau wengine wanaohusika kuhakikisha mlemavu anajiwezesha kiuchumi huko mjini Bukoba, mkoani Kagera, Magharibi mwa Tanzania.
Juhudi za vijana wa ukanda wa Afrika ya Mashariki na kati ambapo licha ya changamoto za hapa na pale kiuchumi na kijamii, lakini kwa namna ya pekee baadhi ya vijana wa ukanda huu wanajibidisha kuhakikisha wanajiajiri au kuajiriwa huku wakitaja nidhamu na uaminifu kwenye jamii inayowazunguka ndio siri ya mafanikio yao.
Leo tunaangazia juu ya Uhusiano baina ya Burundi na Rwanda. Kwa zaidi ya miaka mitano sasa hali ya uhusiano baina ya nchi hizo mbili umezorota. Baadhi ya sababu zilizotajwa na kila upande, Rwanda inataja Burundi kuhifadhi baadhi ya wahusika wa uhalifu wa kibinadamu waliokimbilia Kongo, na kwa upande mwingine Burndi inataja kwanda kuhifadhi walifanya jaribio la mapinduzi mwaka 2015.
Leo tunaangazia juu ya hatua ya serikali ya Burundi kusimamisha baadhi ya viongozi na maafisa waandamizi wa serikali iliyoko madarakani wengi wao wakiwa watumishi wa ikulu. Serikali ya Burundi ilifahamisha kwamba waliosimamishwa kazi akiwemo aliyewahi kuwa msemaji wa serikali Willy Nyamitwe na wengine, wamesimamishwa kupisha uchunguzi kwa tuhuma za kuchelewa kazini.
Leo tunaangazia juu ya Kinywaji haramu cha ‘Gongo' nchiniTanzania na ‘Chang'aa' nchini Kenya. Baadhi ya wanywaji wa pande zote walioongea na RFI wanaomba serikali za nchi zao kuhalalisha kinywaji hicho cha Gondo ambapo kwa Kenya wao huiita Chang'aa, na kwa upande wa Tanzania huiita Gongo au Supu ya Mawe au Machozi ya Simba na kadhalika.
Leo tunaangazia juu ya Maadili ya Viongozi wa Umma nchini Tanzania. Tutakuwa na baadhi ya wachambuzi ambao ni Ndugu Mjungu akiwa Karagwe mkoani Kagera, pamoja na Dokta. Peter Bujari mchambuzi wa kisiasa, kiuchumi na mshauri wa sera akiwa jijini Dar es Salaam.
Tunaangazia juu ya hatua ya Serikali ya Burundi kupitia upya mikataba ya madini lengo ikiwa ni madini ya nchi hiyo kunufaisha pande zote yaani Burundi na muwekezaji. KWa mjibu wa serikali ya Burundi, kwa sasa taifa hilo linanufaika na pato la madini aslimia 10% -15% na Burundi ingependa kiwango zaidi.
Leo tunaangazia juu ya utamaduni wa kuandika na kusoma vitabu nchini Tanzania. RFI imefika jijini Dar es Salaam kukutana na waandishi wa vitabu Bw. Yerick Nyerere pamoja na Dr. Cyrilo Christopher ambao wamejitahidi saana kuandika vitabu na kuhamasisha usomaji vitabu nchini Tanzania.
Leo tunaangazia juu ya changamoto ya ajira kwa Vijana wa nchi za Afrika ya Mashariki, na leo tunaungana na baadhi ya vijana wa Kenya na Tanzania. Baadhi ya vijana hao wanabainisha kuwa juhudi na bidii ndio njia muafaka ya vijana kufikia ndoto zao. Vijana wanashauri vijana wenzao kutumia elimu na vipaji ili kujiinua kiuchumi.
Leo tunaangazia juu ya changamoto ya Vijana na wataalamu wa nchi za Afrika ya Mashariki wanaofikiria kupata fursa zaidi za ajira na kipato nje ya nchi zao na bara la Afrika.
Tunaangazia juu ya Mkoa wa Kigoma, nchini Tanzania. Mkoa wa Kigoma uko magharibi mwa Tanzania, kwenye mwambao wa ziwa Tanganyika, ambapo Tanzania inapakana nan chi za Burundi, Jamhuri yakidemokrasia ya Congo, na Zambia.
Tunaangazia juu ya vipaji kwa vijana nchini Tanzania. RFI imefika tarafani Rulenge, Wilayani Ngara, mkoani Kagera magharibi mwa Tanzania na kuongea na baadhi tu ya vijana walioamua kuunda kukindi cha ‘JM Group' kuendeleza vipaji vyao, na shughuli zao za vipaji kuwa ajiri, kuwaimarisha kiafya na kudumisha mila na tamaduni.
Sekta ya elimu nchini Tanzania, inashuhudia changamoto hasa wilayani Ngara, mkoani Kagera magharibi, ikibainika kwamba walimu wanawalazimisha wanafunzi wachote maji na kuchanja kuni wakati wa muda wa masomo. Juliani Rubavu anazamia hili kwenye makala haya.
Leo tunaangazia changamoto za utunzaji mazingira nchini Tanzania, tukijikita huko mkoani Kigoma magharibi mwa nchi hiyo. Kama baadhi ya wadau wa mazingira walioko wilayani Kibondo watakavyobainisha, kwasasa mazingira yanaharibiwa kwa kiwango kikubwa na kupelekea wadau kuweka wazi kilio chao.
Leo tunaangazia juu ya mapendekezo ya kamati ya ushauri ya mkoa wa Geita, kuunda mkoa mpya wa Chato, nchini Tanzania. Geita imependekeza mkoa mpya wa Chato uundwe na baadhi ya wilaya za mikoa ya Geita, Kagera, Kigoma na Shinyanga.
Leo tunaangazia juu ya mahusiano baina ya Jamii ya Watanzania na wakimbizi wa kutokea nchi za Kongo na Burundi walioko kwenye kambi ya Nyarugusu iliyoko kwenye tarafa ya Makele, wilayani Kasulu, mkoani Kigoma, magharibi mwa Tanzania.
Leo tunaangazia juu ya uhaba na bei ghali kwa mafuta ya kula nchini Tanzania. Kwa mjibu wa serikali ya Tanzania kupitia wizara ya viwanda na biashara, viwanda vya Tanzania vinazalisha kiwango kidogo cha mafuta ya kula, hali inayopelekea wafanyabiashara kuagiza mafuta nje ya nchi.
Tunaangazia juu ya mfuko wa kusaidia watu wasiojiweza kiuchumi nchini ujulukanao kama TASAF nchini Tanzania. Kumekuwepo na manung’uniko ya hapa na pale kuhusu wanufaikaji ambapo baadhi ya malalamiko yanataja baadhi ya watu au hata viongozi wanaojiorodheshakama wasiojiweza ili wafaidi mfuko huo.
Wakulima wa zao la chai katika mkowa wa Kagera, nchini Tanzania, wameshindwa kuzalisha zao hilo kutoka na changamoto nyingi, ikiwemo kukosa kupata pembejeo za zao hilo. Wengi wakiachana na ukulima wa zao hilo. Juliani Rubavu ametuandalia makala kuhusiana na changamoto za wakulima hao.
Leo tunaangazia juu ya nia ya serikali ya Tanzania kuhamasisha wakimbizi wa Burundi kurejea kwao kwa hiari baada ya kuingia nchini humo mwaka 2015 kufuatia mzozo wa kisiasa.
Wiki hii tunaangazia kuhusu utamaduni, mila na desturi kwa wenyeji wa Visiwa vya Zanzibar. Ungana nasi upate mengi zaidi.
Leo tunaangazia juu ya Mchezo wa Mpira wa Gonga huko Unguja, Zanzibar. Kwa mjibu wa wenyeji niliokuta wakicheza mpira wa Gonga pale Kizingo Beach, Unguja, wameeleza kuwa mpira wa Gonga una asili yake kwenye visiwa vya Brazil, Amerika ya Kusini.
Leo tunaangazia mchezo wa mpira wa ufukweni huko nchini Burundi. Mchezo huu sio maarufu sana kwa baadhi ya watu ukilinganisha na mpira wa miguu au mpira wa kikapu. Huko Burundi mpira wa ufukweni umeanza miaka 13 iliyopita.
Leo tunaangazia changomoto za usafiri wa majini katika Ziwa Victoria nchini Tanzania. Utawasikia abiria wakizungumizia hili.
Leo tunaangazia juu ya fursa na ajira kwa vijana nchini Tanzania. Utawasikia vijana wa huko wilayani Rorya mkoani Mara kaskazini-magharibi mwa Tanzania jirani kabisa na mpaka wa Kenya. Kama utakavosikia kwenye mazungumzo yetu, vijana hao wanabainisha ni jinsi gani wameamua kubuni jinsi ya kujipatia kipato kwa njia ya burudani.
Julian Rubavu anaangazia juu ya uhaba wa dagaa wapatikana katika ziwaTanganyika hukoKigoma, Tanzania. Wenyeji wanasema kuwa dagaa wa Kigomani watamu saana, lakini pia gharama za kuwavua dagaa hao ni kubwa sanaambapo mvuvi anatumia zaidi ya shilingi laki moja na elfu ishirini(120,000). Wenyeji wanasema kuwa sababu nyingine ni zana duni zauvuvi.
Katika makala haya mwanahabari Juliani Rubavu amezuru mwambao wa ziwa Tanyingika, katika kijiji na Ujiji, na kutangamana na wenyeji ambapo ameangazia kwa kina shughuli zao za kila siku.
Katika makala ya juma hili ya Afrika Mashariki, mawanahabari wetu Juliani Rubavu anaangazia hutua ya mataifa ya Afrika mashariki kuwashauri wataalamu wao kutoondoka katika mataifa hayo kutafuta kipato katika mataifa mengine kwa lengo la kuchangia kuimarika kwa uchumi katika mataifa yao.
Leo tunaangazia makubaliano ya viongozi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki waliokutana hivi karibuni jijini Dar es salaam nchini Tanzania na kuidhinisha rasmi Elimu ya juu ya pamoja ndani ya nchi wanachama. Hii inamaanisha nini ? Karibu sana.
Makala ya kwanza kabisa mwaka huu wa 2017 tunaanzia nchini Ugandaambapo tutaangazia vitendo viovu vya ulaji nyama ya binadamu. Kusini mwa Uganda kwenye wilaya za Rakai, Kyotera na nyinginezo watuwanakamatwa, wanachinjwa na kuliwa nyama na binadamu wenzao.
Makala haya ya Afrika ya Mashariki inaangazia juu ya hofu kwa familia zenye watu wenye ulemavu wa ngozi na jamii inayowazunguka magharibi mwa Tanzania.
Makala haya ya Afrika ya Mashariki inaangazia juu ya changamoto za kiuchumi na maendeleo kwenye ukanda wa afrika ya mashariki. Katika makala haya watasikika baadhi ya raia wa Tanzania waishio maeneo ya mpakani, na pia mahojiano na waziri wa Tanzania kwenye jumuiya ya afrika ya mashariki Dr Harrison Mwakyembe akiangazia baadhi ya changamoto kwenye miradi ya kikanda inayoshirikisha jumuiya ya afrika ya mashariki.
Makala haya ya Afrika ya Mashariki yanaangazia juu ya changamoto za mauaji ya walemavu wa ngozi (Albino), ambayo yamekithiri katika kanda ya ziwa Magharibi mwa Tanzania.
Makala hii ya Afrika ya Mashariki inaangazia juu ya umuhimu wa elimu kwa waumini wa dini ya kiislamu katika ukanda wa Afrika ya mashariki.
Makala hii ya Afrika ya Mashariki inaangazia sehemu ya pili kuhusu maendeleo ya kijamii katika kijiji cha Kogelo, kaunti ya Siaya magharibi mwa Kenya, alipozaliwa baba yake Barack Obama , rais wa Marekani. Utamsikia bibi Sarah Onyango Obama, mama mzazi wa baba wa rais wa Marekani Barack Obama, anazungumziaje kuhusu chimbuko la kiongozi huyo wa Marekani.
Katika makala ya Afrika ya Mashariki, tunaangazia juu ya maendeleo ya kijamii katika kijiji cha Kogelo, Kaunti ya Siaya, magharibi mwa Kenya, alipozaliwa baba yake rais wa Marekani Barack Obama.
Makala ya Afrika Mashariki inaangazia juu ya changamoto kwenye sekta ya elimu nchini Tanzania, ambapo baadhi ya shule nyingi za serikali ngazi ya kata zimegeuzwa na kuitwa “ Yeboyebo”, na kwa upande mwingine makala haya yanagusia shule binafsi zenye hadhi za kimataifa.
Makala ya Afrika ya Mashariki inaangazia juu ya changamoto za kiusalaama na elimu kwa walemavu wa ngozi (albino) waishio mikoa ya kanda ya ziwa magharibi mwa Tanzania.
Juma hili, Tanzania imeadhimisha miaka 15 tangu kuaga dunia kwa Mwanzilishi wa taifa lao Mwalimu Julius Kambarage Nyerere mwaka 1999. Ni kiongozi ambaye anakumbukwa ndani ya nje ya Tanzania kama anavyobaini Mwandishi wetu Julian Rubavu.