POPULARITY
Nchini Tanzania, maneno maridhiano na Katiba mpya, yameendelea kutawala vinywa vya wanasiasa na wananchi wa taifa hilo baada ya uchaguzi mkuu uliokumbwa na vurugu wa Oktoba mwaka 2025. Hivi karibuni, rais Samia Suluhu Hassan alikutana nna viongozi wa vyama vya siasa na kutangaza mpango wa maridhiano na mchakato wa katiba mpya. Je, haya yanawezekana bila ushiriki wa chama cha upinzani CHADEMA, ambacho kiongozi wake Tundu Lissu, amezuiwa jela kwa sababu ya kesi ya uhaini ?
Kinara wa upinzani nchini Uganda azirai akiwa mahakamani, mahakama ya katiba nchini DRC ilisema kwamba sheria iliyopendekezwa kuhusu kuandaa kura ya maoni katika nchi hiyo ni ya kikatiba, seneta wa Nairobi Edwin Sifuna autikisa mwamba wa siasa nchini Kenya kuelekea uchaguzi wa 2027, siasa za Tanzania, Sudan, na Morocco ambako wahamiaji waliamua kuogelea kuvuka kwenda ulaya, uhispania, Washington ilisema mkataba wa kujisalimisha kwa Hamas kule Israeli umepatikana.
Shambulio la ADF laua zaidi ya 20 mashariki mwa DRC, ziara ya waziri mkuu Judith Suminwa huko Ituri, gavana wa zamani wa migori akutwa na hatia ya mauaji, huku rais Ruto akionya kuhusu matumizi ya wahuni kwenye mikutano ya kisiasa, siasa za Tanzania, Sudan na rais wa zamani wa Senegal Macky Sall, kuwasilisha maono yake mbele ya baraza la Umoja wa Mataifa, katibu mkuu wa UN Antonio Guteress atoa wito kwa pande zinazohusika katika mzozo wa mashariki ya kati kutafuta suluhu kupitia diplomasia.
Kume kuwa mgwanyiko kati ya kambi yamakanisa katika Jamuhuri yakidemokrasia ya Kongo, kutakana na swala lakubadilisha katiba.
Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, kumeundwa miungano miwili ya kisiasa. Kundi la kwanza linaitwa "C4" linalounga mkono mabadiliko ya katiba, chini ya rais Felix Tshisekedi. Nao vigogo wa upinzani wakiongozwa na Martin Fayulu, Moïse Katumbi na wengine, wao wameunda C64" vuguvugu linalopinga marekebisho yoyote na kuilinda katiba ya sasa. Nini hatima ya makundi haya ? Tunachambua.
Wawakilishi wa serikali ya DR Congo na kundi la M23 wanajiandaa kukutana nchini Uswizi kwa awamu nyingine ya mazungumzo.
Mjadala wa kuibadilisha katiba nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, umepamba moto. Wanasiasa wanaoegemea upande wa rais Felix Tshisekedi na chama chake cha UDPS wanaunga mkono mchakato wa katiba kubadilishwa. Upinzani wakiongozwa na naibu Spika wa Bunge la Seneti aliyejiuzulu Modeste Bahati Lukwebo, unapinga. Ni wakati mwafaka wa kuibadilisha katiba ya DRC ?
Tunajadili kinachoendelea nchini DRC, ambapo mjadala kuhusu mapendekezo ya kufanyia katiba marekebisho, ikiwemo muhula wa urais, unazidi kuibua hisia mseto, baadhi ya raia wakionekana kuunga mkono na baadhi kupinga. Unazungumziaje mjadala huu nchini DRC? Skiza maoni ya mskilizaji.
Tunajadili kinachoendelea nchini DRC, ambapo mjadala kuhusu mapendekezo ya kufanyia katiba marekebisho, ikiwemo muhula wa urais, unazidi kuibua hisia mseto, baadhi ya raia wakionekana kuunga mkono na baadhi kupinga. Unazungumziaje mjadala huu nchini DRC? Skiza maoni ya mskilizaji.
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayomulika Mkataba wa Kimataifa wa kulinda viumbe hai wa baharini kwenye Bahari Kuu na ujumbe wa Mzee Ali Haji, Naibu Katibu Mkuu anayehusika na Katiba na Sheria katika Ofisi ya Rais, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar nchini Tanzania kuhus umuhimu wa mkataba huu.Kesi inaendelea katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki, ICJ mjini The Hague, kuhusu madai kwamba Myanmar ilitekeleza mauaji ya kimbari dhidi ya watu wa Rohingya. Mawakili wa Gambia wameiambia mahakama hiyo kuwa jeshi la Myanmar lilichochea ghasia kupitia kauli za chuki, likiwaita Warohingya “mbwa Waislamu”kabla ya mashambulizi ya mwaka 2017.Baada ya zaidi ya siku 1,000 za mzozo, Sudan inakabiliwa na mgogoro mkubwa zaidi wa njaa na uhamaji wa watu duniani. Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani WFP, leo linaonya kuwa operesheni zake za kuokoa maisha ziko hatarini kutokana na uhaba mkubwa wa ufadhili.Mamilioni ya raia wa Uganda leo walipiga kura katika uchaguzi mkuu wa Rais, wabunge na serikali za mitaa huku Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi UNHCR likisisitiza umuhimu wa wakimbizi zaidi ya milioni moja nchini humo kubaki bila kuegemea upande wowote wa kisiasa. Shirika hilo limeonya kuwa kushiriki katika siasa kunaweza kuwakosesha wakimbizi usalama, kupelekea mateso kutoka nchi zao za asili, au kuathiri ulinzi na hali yao ya hifadhi nchini Uganda.Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili na leo Dkt. Mwanahija Ali Juma, Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili, Zanzibar nchini Tanzania, BAKIZA anafafanua maana na ya neno "MLOWIMA"Mwenyeji wako ni Rashid Malekela, karibu!
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayoangazia simulizi za waahirika wa Kimbunga Melissaikiwa ni wiki ya pili sasa baada ya kupiga magharibi mwa Jamaica, na kuacha zahma kubwa kwa wakaazi. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na jifunze Kiswahili.Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres akieleza kuwa na wasiwasi mkubwa kutokana na ripoti za ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu na mauaji ya halaiki mjini El Fasher, pamoja na kuongezeka kwa mapigano katika maeneo ya Kordofan nchini Sudan. Guterres amesema “Mtiririko wa silaha na wapiganaji kutoka nje lazima ukatwe. Misaada ya kibinadamu lazima iweze kuwafikia haraka raia wanaohitaji, na mapigano lazima yakome,”.Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa Jumatano limemchagua Phoebe Okowa kutoka Kenya kuwa Jaji wa Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ), baada ya duruu nne za upigaji kura. Upigaji kura huo ulifanyika kwa wakati mmoja na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, lakini kwa utaratibu tofauti, kama inavyotakiwa na Katiba ya Mahakama hiyo ya Haki. Bi. Okowa amechaguliwa kwa wingi wa kura ambapo alipata kura 8 katika Baraza la Usalama na kura 106 katika Baraza Kuu.Kumekuwa na ongezeko la uraibu wa nikotini na bidhaa nyingine zinazozalishwa kwa kutumia tumbaku duniani hususani miongoni mwa vijana na tena wengi hivi sasa wanatumia sigara za kielektroniki, limesema shirika la Umoja wa Mataifa la Afya duniani WHO. Tarehe 17 mpaka 21 Novemba utafanyika mkutano mkubwa kujadili namna serikali, mashirika ya kimataifa na asasi za kiraia zitakavyoweza kusaidia kupambana na janga la tumbaku duniani, linalosababisha vifo zaidi ya milioni saba kila mwaka.Katika kujifunza lugha ya Kiswahili hii leo, mtaalam wetu Onni Sigalla, Mhariri mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania, BAKITA. Anafafanua maana za neno "KASIMU"Mwenyeji wako ni Sabrina Said Moshi, karibu!
Baada ya zaidi ya miaka mitatu ya mazungumzo ya kina, hatimaye leo Geneva, Uswisi, Nchi Wanachama wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani (WHO) zimekamilisha rasimu ya makubaliano ambayo itawasilishwa katika Mkutano wa Afya Duniani mwezi Mei mwaka huu wa 2025. Pendekezo hili linakusudia kuimarisha ushirikiano wa kimataifa katika kuzuia, kujiandaa na kukabiliana na vitisho vya majanga ya kiafya yajayo. Anold Kayanda amefuatilia anatujulisha zaidi. "Leo mataifa ya dunia yameandika historia mjini Geneva," amesema Dkt. Tedros Ghebreyesus, Mkurugenzi Mkuu wa WHO na kuongeza kwamba, "kwa kufikia makubaliano kuhusu Mkataba wa Majanga ya kiafya, siyo tu wameweka msingi wa makubaliano ya kizazi hiki yanayolenga kuifanya dunia kuwa salama zaidi, bali pia wameonesha kuwa ushirikiano wa kimataifa bado uko hai, na kwamba hata katika dunia iliyogawanyika, mataifa bado yanaweza kushirikiana kutafuta mwafaka na mwitikio wa pamoja dhidi ya vitisho vya pamoja.” Mwezi Desemba mwaka 2021, wakati janga la COVID-19 likiwa limepamba moto, Nchi Wanachama wa WHO ziliunda Mamlaka ya Majadiliano ya Kiserikali ili kuandaa na kujadiliana kuhusu mkataba, makubaliano au nyenzo nyingine ya kimataifa, chini ya Katiba ya WHO, kwa ajili ya kuimarisha uzuiaji, maandalizi na hatua dhidi ya majanga ya kiafya. Mapendekezo katika rasimu iliyotayarishwa ni pamoja na: kuchukua hatua madhubuti za kuzuia majanga ya kiafya kwa kutumia mbinu ya Afya Moja; kujenga uwezo wa utafiti na maendeleo katika maeneo mbalimbali duniani; kuwezesha uhamishaji wa teknolojia na maarifa, ujuzi na utaalamu unaohusiana na uzalishaji wa bidhaa za afya zinazohusiana na majanga ya kiafya; kuchukua hatua madhubuti za kuimarisha maandalizi, utayari na uimara wa mifumo ya afya; na kuanzisha mtandao wa kimataifa wa mnyororo wa usambazaji na vifaa. Pendekezo hilo linathibitisha mamlaka ya nchi kushughulikia masuala ya afya ya umma ndani ya mipaka yao bila kuingiliwa.
Wakenya wana endelea kukabiliana na uongozi mpya wa mseto kati ya serikali ya Kenya Kwanza na chama kikuu cha upinzani cha Orange Democratic Movement (ODM).
Matangazo ya nusu saa kuhusu habari za mapema asubuhi pamoja na habari za michezo.
Matangazo ya saa nzima kuhusu habari za kutwa, ikiwa ni pamoja ripoti kutoka kwa waandishi wetu sehemu mbali mbali duniani na kote Afrika Mashariki na Kati, na vile vile vipindi na makala maalum kuhusu afya, wanawake, jamii na maendeleo.
Heri ya mwaka mpya wa mwaka 2025. Nchi ya Msumbiji bado ipo kwenye mvutano mkali wa kisiasa, baada ya uchaguzi wa mwezi Oktoba mwaka 2024.Hali imeendelea kuwa mbaya baada ya Baraza la Katiba, kuthibitisha ushindi wa Daniel Chapo kutoka chama tawala FRELIMO, kuwa mshindi wa uchaguzi wa urais huku kiongozi wa upinzani Venancio Mondlane, akiendelea kudai aliibiwa kura.Watu zaidi ya 260 wamepoteza maisha, wengi wao wakipigwa risasi na polisi kwa mujibu wa mashirika ya kutetea haki za binadamu.
Matangazo ya saa nzima kuhusu habari za kutwa, ikiwa ni pamoja ripoti kutoka kwa waandishi wetu sehemu mbali mbali duniani na kote Afrika Mashariki na Kati, na vile vile vipindi na makala maalum kuhusu afya, wanawake, jamii na maendeleo.
Kwa Undani ni matangazo ya dakika 25 yanayochambua habari kwa undani zaidi na kumpa msikilizaji maelezo ya kina kuliko ilivyo kawaida kuhusu tukio au swala lililojitokeza katika habari.
Haki si haki iwapo inatolewa kwa lugha ambayo haileweki kwa wahusika, wamejulishwa washiriki wa mkutano wa pili wa wanazuoni unaofanyika hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa New York, Marekani na pia mtandaoni ukimulika Madaraka, Haki na Binadamu: Utawala wa Sheria na mabadiliko Afrika. Anold Kayanda na maelezo zaidi.
Miongoni mwa yale utakayoyasikia kwenye habari ni pamoja na Rais wa DRC, Felix Tschisekedi, kuwataka raia wa nchi yake kuunga mkono mabadiliko ya katiba, , Chama tawala cha CCM nchini Tanzania chaongoza kwa asilimia 99 ya kura.Zaidi ya watu 100 hawajulikani walipo baada ya ajali ya maporomoko ya Udongo nchini Uganda,pia Tutaangazia ziara yake Rais wa Nigeria, Bola Tinubu, nchini Ufaransa, Raia wa Namibia wapiga kura, kisha kimataifa tutaangazia mkutano wa Mawaziri wa mambo ya nje kutoka muungano wa G7,uliofanyika mjini Roma Italia.
Bunge la DRC limepokea barua ya kukagua muda wa muhula wa rais na mageuzi ya mahakama ya Kongo.
Matangazo ya nusu saa kuhusu habari za mapema asubuhi pamoja na habari za michezo.
Katika kipindi hiki cha "The Friendly Troll," msimulizi Calvin Mulindwa anachunguza kwa kina haki za picha nchini Kenya, akiangazia msingi wao wa kisheria na athari zake katika dunia halisi. Kipindi hiki kinachambua maana ya haki za picha, pamoja na haki ya kudhibiti matumizi ya sura ya mtu katika maeneo ya umma na biashara. Calvin anajadili sheria muhimu kama vile Sheria ya Ulinzi wa Data ya Kenya ya 2019 na Ibara ya 31 ya Katiba, akielezea jukumu lao katika kulinda faragha binafsi. Kupitia kesi muhimu kama vile Wangechi Waweru Mwende dhidi ya Tecno Mobile Limited na Jessica Clarise Wanjiru dhidi ya Davinci Aesthetics, kipindi hiki kinaonyesha jinsi mahakama zilivyoshughulikia ukiukwaji wa haki hizi, ikisisitiza umuhimu wa ridhaa wazi na matumizi halali ya picha binafsi. Majadiliano pia yanatoa ushauri wa vitendo kwa watu binafsi na wadhibiti na wasindikaji wa data juu ya kuheshimu na kulinda haki za picha katika mazingira ya kidijitali na biashara.Malalamiko Yaliyoorodheshwa:Phyllis Nyaboke dhidi ya Grola Tech Limited T/A Lion Cash - Ukiukaji wa kutopata ridhaa ya moja kwa moja.Brian Wainaina na Gathoni Mattai dhidi ya Deltech Capital Kenya Limited T/A Mykes - Kushindwa kutoa taarifa inayofaa kuhusu matumizi ya data, ikisababisha uvunjaji wa faragha.Edith Andeso dhidi ya Shule za Olerai Limited - Masuala kuhusu usimamizi wa ridhaa endelevu kwa madhumuni ya masoko.Christine Wairimu Muturi dhidi ya Shule ya Roma Uthiru - Mahitaji ya ridhaa wazi ya wazazi kwa usindikaji wa data za watoto wadogo.Sheria Zilizonukuliwa: Ibara ya 31. Katiba ya Kenya Sheria ya Ulinzi wa Data ya 2019. Uamuzi wa Mahakama ya Kenya: Wangechi Waweru Mwende dhidi ya Tecno Mobile Limited [2020]Image Rights - Release Form Information Pack Music:Intro/Outro – https://pixabay.com/music/id-102694/
Matangazo ya saa nzima kuhusu habari za kutwa, ikiwa ni pamoja ripoti kutoka kwa waandishi wetu sehemu mbali mbali duniani na kote Afrika Mashariki na Kati, na vile vile vipindi na makala maalum kuhusu afya, wanawake, jamii na maendeleo.
Matangazo ya saa nzima kuhusu habari za kutwa, ikiwa ni pamoja ripoti kutoka kwa waandishi wetu sehemu mbali mbali duniani na kote Afrika Mashariki na Kati, na vile vile vipindi na makala maalum kuhusu afya, wanawake, jamii na maendeleo.
Matangazo ya saa nzima kuhusu habari za kutwa, ikiwa ni pamoja ripoti kutoka kwa waandishi wetu sehemu mbali mbali duniani na kote Afrika Mashariki na Kati, na vile vile vipindi na makala maalum kuhusu afya, wanawake, jamii na maendeleo.
Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ambaye pia ni Mkuu wa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini (UNMISS), Nicholas Haysom ametahadharisha kwamba muda unazidi kuyoyoma kuelekea Sudan Kusini kufanya uchaguzi mkuu unaotarajiwa mwezi Desemba mwaka ujao wa 2024 lakini bado masuala muhimu ya kuufanya uchaguzi huo uende kama ulivyopangwa bila kuchelewa hayajakamilika."Ikiwa imesalia miezi 17 tu kwenye ratiba ya kuelekea uchaguzi wa mwaka 2024, narudia kile nilichokisema katika mkutano wa awali na waandishi wa habari, kwamba mwaka 2023 ni mwaka wa 'kutengeneza au kuvunja'," amesema Bwana Haysom mapema leo Agosti pili alipozungumza na vyombo vya Habari mjini Juba ambao ni mji mkuu wa nchi hiyo changa zaidi duniani. Ghasia miongoni mwa jamii za Sudan Kusini zinaendelea kuongezeka pamoja na shinikizo la kuongezeka kwa ufinyu wa rasilimali huku maelfu ya watu wakiendelea kuingia nchini humo wakikimbia mapigano katika nchi jirani ya Sudan. Kwa mujibu wa Bwana Haysom, miongoni mwa hatua muhimu ambazo inabidi zichukuliwe ni pamoja na hitaji la kuunda upya vyombo vitatu muhimu, ambavyo ni, Tume ya Kitaifa ya Marekebisho ya Katiba, Tume ya Kitaifa ya Uchaguzi, na Baraza la Vyama vya Kisiasa; kukamilisha mipango ya mpito ya usalama; kuendeleza mchakato wa kudumu wa kutengeneza katiba; na kuunda nafasi za kiraia na kisiasa ambapo kila raia ana uhuru wa kujadili na kujihusisha na uchaguzi wa kisiasa na kikatiba bila woga. "Kufanya uchaguzi tu hakutoshi - uaminifu, uwazi na ushirikishwaji wa mchakato ndio unaoleta uhalali. Hii ni pamoja na kwamba vyama vya siasa lazima viweze kujiandikisha na kufanya kampeni kwa uhuru; asasi ya kiraia kwa ajili ya elimu ya uraia na kuwa waangalizi wa mchakato. Inajumuisha vyombo vya habari vinavyoweza kuripoti kuhusu mchakato huo na kutoa nafasi kwa sauti na maoni mbalimbali kwa wapiga kura kufanya uamuzi sahihi,” amesema Mwakilishi huyo wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini. Aidha Bwana Haysom amesisitiza kuwa UNMISS itaendelea kuiunga mkono Sudan Kusini katika michakato ya uchaguzi na uundaji wa katiba kwa kushirikiana na wadau wa kikanda kama vile Muungano wa Afrika (AU) na mamlaka ya pamoja ya kitaifa kwa ajili ya maendeleo kwenye eneo la Pembe ya Afrika (IGAD).
Mungu ametupatia utaratibu wa kufuata katika maisha
Mungu anatupatia muongozo yake kupitia maandiko matakatifu
Jaridani hii leo tunaangazia ni mada kwa kina na nakupeleka mwambao wa Ziwa Tanganyika nchini Tanzania, hususan mkoani Rukwa ambako huko utasikia harakati za Umoja wa Mataifa za kujumuisha wanawake kwenye uvuvi. Pia tunakuletea habari kwa ufupi zikiwemo za Nishati jadidifu, mabadiliko ya tabianchi na afya. Katika mashinani tunakupeleka nchini Sudan Kusini kusikia ni kwa jinsi gani vijana wanachangia katika mchakato wa utengenezaji wa katiba ukielekea uchaguzi mkuu nchini humo.Ripoti mpya iliyozinduliwa leo kuhusu hatua zilizopigwa katika ufikiaji wa lengo namba 7 la maendeleo endelevu SDGs ifikapo mwaka 20230 lihusulo nishati, inasema pengo la nishati duniani bado linaendelea kwani watu milioni 675 hawana umeme, huku watu wengine bilioni 2.3 wanategemea nishati za kupikia ambazo ni hatari kwa afya zao na mazingira. Umoja wa Mataifa umezindua mradi wa miaka miatatu wa kuimarisha mnepo wa jamii dhidi ya mabadiliko ya tabianchi mkoani Kigoma nchini Tanzania ambako mamia kwa maelfu ya wakimbizi wanahifadhiwa.Na kuelekea siku ya usalama wa chakula duniani hapo kesho Juni 7 mashirika ya Umoja wa Mataifa lile la afya duniani WHO na la mpango wa chakula duniani WFP kwa kushirikiana na sekretarieti ya Codex Alimentarius wamesema kila siku takriban watu milioni 1.6 duniani kote wanaugua kutokana na kula chakula kisicho salama.Na katika mashinani Elizabeth Acu, Mwanaharakati wa vijana ambaye pia ni mwanauchumi nchini Sudan Kusini, anaeleza jukumu la vijana katika uundaji na uimarishaji wa katiba, na pia changamoto zinazoikumba nchi hiyo huku mchakato wa uchaguzi mkuu unapokaribia.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, Karibu!
Tamko la Umoja wa Mataifa la Haki za Binadamu mwaka huu linatimiza miaka 75 tangu kupitishwa kwake. Katika kutathmini utekelezaji wake, tunachambua ibara kwa ibara kuona iwapo kuna mafanikio, halikadhalika changamoto. Na kwa mantiki hiyo leotunamulika Ibara ya Tatu ya Tamko hilo inayosema Kila mtu ana haki ya kuishi, haki ya kuwa huru na kulindwa . Na mchambuzi wetu ni Getrude Dyabene Afisa Mwandamizi wa Dawati la Jinsia kutoka Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu nchini Tanzania, LHRC akihojiwa na Assumpta Massoi wa Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa, jijini New York, Marekani. Bi. Dyabene anaanza kwa kuelezea jinsi Katiba ya Tanzania inatambua haki ya kuishi.
Në runë 84 ke nyïïr juïc arëtic ake cë jääl në thukuul yic Bor ku jɔl ya ɣän kɔ̈k në Junub keke ye biäk ë kɔc la abɛ̈c cë të cennë rïnythii lɔ thïn. Në cɛ̈nhdenic, ke kɔc juïc ke keek atɔ̈ keke cë ka juïc bë lɔ guum. Amol Amuɔ̈m ee ya raan töŋë keek ku wuɔk cë bë jam në akölkölden ke tɔ̈ në Canada.
Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Sudan Kusini (UNMISS) umefanya warsha za majadiliano katika mji wa Torit na Magwi mashariki mwa mji mkuu Juba jimboni Equatorial Mashariki ili kujadili kuhusu utungaji katiba na michakato ya uchaguzi.Sudan Kusini kwa sasa inatayarisha katiba yake ya kudumu ambayo si tu ni muhimu bali pia ni sharti la kufanya uchaguzi mkuu wa nchi hiyo uliopangwa kufanyika mwakani, 2024. Makundi mbalimbali ya kijamii yaliyoshiriki katika majadiliano haya yaliyoratibiwa na UNMISS ni pamoja na wanawake, vijana, waliorejea kutoka ukimbizini, wakimbizi wa ndani, na viongozi wa kimila. Jessica Kalmas, mkimbizi aliyerejea ambaye sasa ni Msemaji wa Umoja wa Vijana, Equatoria Mashariki anasema, “Kunapaswa kuwa na uzingatiaji wanaorejea. Pia, suala la ukatili wa majumbani na kijinsia likomeshwe. Hili pia lijumuishwe kwenye katiba ya kudumu.”Masuala ambayo washiriki wameyapa uzito katika majadiliano yao ni nafasi sawa kwa wanawake katika maisha ya umma, kuhakikisha wasichana wote wana haki ya kupata elimu, na kukomesha desturi ya ndoa za kulazimishwa au za utotoni. Angel Omex, Mwanafunzi ni Chuo Kikuu cha Kikatoliki cha Sudan Kusini anaeleza, “Nimehudhuria huu mchakato wa kutengeneza katiba, na nina furaha kuwa sehemu yake. Na, kulingana na maoni yangu binafsi nadhani kinachopaswa kujumuishwa katika mchakato wa kutengeneza katiba ya kudumu ni suala la asilimia 35 ya jinsia. Wanawake wanatakiwa kupewa asilimia 35. Haifai kuwa kusema tu bali inapaswa kutekelezwa. Na sio tu kwamba wanaorejea kutoka ukimbizini ni muhimu sana, lakini pia wanapaswa kurejeshwa katika jamii na kusajiliwa.”Kwa pamoja, waliohudhuria walifikia mapendekezo kuhusiana na katiba ya kudumu na uchaguzi unaofuata, ikiwa ni pamoja na ushiriki wenye nguvu Zaidi wa vijana. UNMISS inashirikiana na mamlaka za serikali na Mashirika ya Umoja wa Mataifa, Fedha na Mipango ili kuandaa warsha kama hizo kote Sudan Kusini.
Mungu ametupatia muongozo wake kupitia maandiko matakatifu yote tunayopaswa kufuata
Katika kipindi cha leo, Mwenyekiti wa jukwaa la katiba Tanzania, Mwalimu Deus Kibamba Pamoja na Wakili Msomi Paul Kisabo wanaendelea kutuelimisha juu ya ibara mbalimbali za katiba hii, katika sura ya kwanza, na mpangilio mzima wa sura hii. Wazungumzaji wetu wanatuelezea juu ya umuhimu wa sura hii na changamoto zilizopo, kwenye sura hii ya kwanza na mapungufu yaliyopo kwenye sura hii na mapendekezo yao juu ya sura hii. Kama unapenda tunachokifanya, tuwezeshe kupitia Lipa Namba TigoPesa - 8212862 Subscribe kwenye chaneli yetu: https://www.youtube.com/@UCtr2I2XphLapB71XkxxrU4A Sikiliza Podcast yetu kupitia: Apple Podcast link: https://apple.co/3ZwLmSA Spotify: http://bit.ly/40v0UYd Google Podcast Link: http://bit.ly/3zm0irZ Audiomack Link: https://audiomack.com/sheriapoa Youtube Link: https://www.youtube.com/@sheriapoa#SheriaPoa #SheriaPoaPodcast #katiba #katibampya #sheria #sheriazaTanzania #tanzania #podcast #podcasts #podcastshow #podcasttanzania --- Send in a voice message: https://podcasters.spotify.com/pod/show/sheriapoa/message
Kwenye Kipindi cha leo tupo na Mawakili Wasomi, Deogratius Bwire pamoja na Nuru Maro wakitupitisha katika Sura ya Pili ya Katikba ya Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania, hususani kwenye Muundo wa Serikali ya kwa mujibu wa katiba hii na madaraka ya Rais. Mawakili wasomi wanatuelezea kwa kina, muundo wa serikali hii na changamoto zilizopo kwenye muundo huu wa serikali na mapendekezo yao ya nini kifanyike kwenye mchakato wa katiba mpya ili kuboresha muundo huu na madaraka ya Rais kwa ujumla. Kama unapenda tunachokifanya, tuwezeshe kupitia Lipa Namba TigoPesa - 8212862 Subscribe kwenye chaneli yetu: / @uctr2i2xphlapb71... Sikiliza Podcast yetu kupitia: Apple Podcast link: https://apple.co/3ZwLmSA Spotify: http://bit.ly/40v0UYd Google Podcast Link: http://bit.ly/3zm0irZ Audiomack Link: https://audiomack.com/sheriapoa Youtube Link: / @sheriapoa #SheriaPoa #SheriaPoaPodcast #katiba #katibampya #sheria --- Send in a voice message: https://podcasters.spotify.com/pod/show/sheriapoa/message
Katika kipindi cha leo, Mwenyekiti wa jukwaa la katiba Tanzania, Mwalimu Deus Kibamba Pamoja na Wakili Msomi Paul Kisabo wanaendelea kutuelimisha juu ya ibara mbalimbali za katiba hii, katika sura ya kwanza, na mpangilio mzima wa sura hii. Wazungumzaji wetu wanatuelezea juu ya umuhimu wa sura hii na changamoto zilizopo, kwenye sura hii ya kwanza na mapungufu yaliyopo kwenye sura hii na mapendekezo yao juu ya sura hii. Kama unapenda tunachokifanya, tuwezeshe kupitia Lipa Namba TigoPesa - 8212862 Subscribe kwenye chaneli yetu: https://www.youtube.com/@UCtr2I2XphLapB71XkxxrU4A --- Send in a voice message: https://podcasters.spotify.com/pod/show/sheriapoa/message
Katika kipindi cha leo, Mwenyekiti wa jukwaa la katiba Tanzania, Mwalimu Deus Kibamba Pamoja na Wakili Msomi Paul Kisabo wanaendelea kutuelimisha juu ya ibara mbalimbali za katiba hii, katika sura ya kwanza, na mpangilio mzima wa sura hii. Wazungumzaji wetu wanatuelezea juu ya umuhimu wa sura hii na changamoto zilizopo, kwenye sura hii ya kwanza na mapungufu yaliyopo kwenye sura hii na mapendekezo yao juu ya sura hii. Kama unapenda tunachokifanya, tuwezeshe kupitia Lipa Namba TigoPesa - 8212862 Subscribe kwenye chaneli yetu: / @uctr2i2xphlapb71... Sikiliza Podcast yetu kupitia: Apple Podcast link: https://apple.co/3ZwLmSA Spotify: http://bit.ly/40v0UYd Google Podcast Link: http://bit.ly/3zm0irZ Audiomack Link: https://audiomack.com/sheriapoa Youtube Link: / @sheriapoa #SheriaPoa #SheriaPoaPodcast #katiba #katibampya --- Send in a voice message: https://podcasters.spotify.com/pod/show/sheriapoa/message
Katika kipindi cha leo, tupo na Mwenyekiti na Muanzilishi wa Jukwaa la Katiba Tanzania Mwl. Deus Kibamba akitupitisha katika historia ya Katiba Ya Mwaka 1977, kutoka kupata uhuru wa Tanganyika mpaka leo. Kama unapenda tunachokifanya, tuwezeshe kupitia Lipa Namba TigoPesa - 8212862 Subscribe kwenye chaneli yetu: https://www.youtube.com/@sheriapoa Sikiliza Podcast yetu kupitia: Apple Podcast link: https://apple.co/3ZwLmSA Spotify: http://bit.ly/40v0UYd Google Podcast Link: http://bit.ly/3zm0irZ Audiomack Link: https://audiomack.com/sheriapoa Youtube Link: https://www.youtube.com/@sheriapoa --- Send in a voice message: https://podcasters.spotify.com/pod/show/sheriapoa/message
Katika kipindi cha leo, tupo na Mwenyekiti na Muanzilishi wa Jukwaa la Katiba Tanzania Mwl. Deus Kibamba akitupitisha katika historia ya Katiba Ya Mwaka 1977, kutoka kupata uhuru wa Tanganyika mpaka leo. Kama unapenda tunachokifanya, tuwezeshe kupitia Lipa Namba TigoPesa - 8212862 Subscribe kwenye chaneli yetu: https://www.youtube.com/@sheriapoa Sikiliza Podcast yetu kupitia: Apple Podcast link: https://apple.co/3ZwLmSA Spotify: http://bit.ly/40v0UYd Google Podcast Link: http://bit.ly/3zm0irZ Audiomack Link: https://audiomack.com/sheriapoa Youtube Link: https://www.youtube.com/@sheriapoa --- Send in a voice message: https://podcasters.spotify.com/pod/show/sheriapoa/message
Ujumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa umewasili nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC , ikiwa ni sehemu ya ziara ya kikazi ya kutathmini hali ya usalama na utekelezaji wa majukumu ya vikosi vya umoja wa mataifa vya kulinda mamani nchini humo MONUSCO. Mara tu baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa jijini Kinshasa, bwana Nicolas de Rivière, Balozi wa kudumu wa Ufaransa kwenye Umoja wa Mataifa amesisitiza kuwa makundi yenye silaha, vyovyote vile yalivyo, lazima yasitishe operesheni zao ili kushiriki katika mchakato wa amani, “Ni wakati muhimu wakuchukua hatua na kwamba vikundi vyote vyenye silaha, kwa hali yao lazima visitishe shughuli zao na washiriki katika mchakato wa kisiasa. Naomba makundi ya kigeni yajiondoe na makundi yanayoungwa mkono na mataifa ya kigeni pia yajiondoe ili hatimaye amani irejee katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo”.Ujumbe huo umekuja nchini DRC wakati kukitarajiwa kuwa na uchaguzi mkuu wa raisi pamoja na wabunge mwezi decembe mwaka huu huku bwana Michel Xavier Biang Balozi wa Gabon kwenye Umoja wa Mataifa akisisitiza lazima uchaguzi huo uwe wa haki, wa uwazi na salama, “ Tuko katika mwaka ambao utakuwa mwaka wa uchaguzi, ujumbe wetu ni wakuhimiza wanasiasa wa pande zote kushiriki katika mchakato wa uchaguzi ambao ni wa uwazi, na wa kuaminika kwa mujibu wa Katiba ya DRC na sheria ya uchaguzi. Tuko hapa kuunga mkono hatua ya MONUSCO na kukumbusha kwamba MONUSCO ni sehemu ya fursa ya suluhu”.Wajumbe hao watakutana na watu kutoka tabaka mbali mbali ikiwemo mashirika ya kiraia na Rais wa DRC Félix Tshisekedi jijini Kinshasa na baadae watakwenda mjini Goma jimboni Kivu Kaskazini, ambako mapigano yamezidi kurindima kwa miezi kadhaa sasa kati ya jeshi la serikali na kundi la wanamkambo wa M23.
Mungu ametupatia Muongozo wa kufuata kama katiba yake
Mtaalamu wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za watu wa jamii ya asili amepongeza uamuzi wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu wa kuagiza serikali ya Kenya illipe fidia watu wa jamii ya asili ya Ogiek nchini humo kwa machungu na ubaguzi waliokumbana nao nchini humo. Kupitia taarifa iliyotolewa leo mjini Geneva Uswisi na ofisi ya Umoja wa Mataifa ya haki za binadamu, mtaalamu huyo Francisco Cali Tzay, amesema uamuzi huo wa mwezi Mei mwaka huu unafuatia hatua ya mahakama hiyo kubaini kuwa serikali ya Kenya ilikiuka haki ya kuishi, kumiliki mali, maliasili, maendeleo, dini na utamaduni wa jamii ya Ogiek, kwa mujibu wa Katiba ya Mahakam ya Afrika ya Haki za binadamu. Bwana Tzay amesema uamuzi huo pamoja na malipo ya fidia ni hatua nyingine muhimu katika kutambuliwa na kulindwa kwa haki ya ardhi ya mababu za watu wa jamii ya ogiek kwenye msitu wa Mau nchini Kenya. Mahakama imeitaka serikali ya Kenya illipe fidia ya takribani dola 489,000 kwa kupotea kwa maliasili ya jamii hiyo na zaidi ya dola 844,000 kwa machungu waliyopitia kutokana na ubaguzi na kunyimwa haki ya maendeleo, utamaduni wao na dini yao. Mahakama pia imetaka serikali ya Kenya ichukue hatua muhimu za kisheria, kiutawala au hatua zozote zile kutambua, kuheshimu na kulinda za waogiek iwe kwenye maendeleo, au uwekezaji wowote kwenye ardhi yao na wapatiwe haki ya kushirikishwa katika miradi yoyote itakayofanyika kwenye eneo lao. Katika kesi hiyo, mtaalamu huyu wa Umoja wa Mataifa naye pia alitoa Ushahidi wa kitaalamu. Bwana Tzay amesema anapongeza sana uamuzi wa mahakama huku akisema unapeleka ujumbe mzito kwa ulinzi wa ardhi na haki za kitamaduni za waogiek nchini Kenya na watu wote wa jamii ya asili barani Afrika na kwingine kote duniani huku akitaka serikali ya Kenya itekeleze uamuzi huo.
Leo ni siku 100 tangu kuanza kwa uvamizi wa Urusi nchini Ukraine ulioanza tarehe 24 Februari mwaka huu. Mashirika ya Umoja wa Mataifa na wadau wake wanasema katika hizi siku 100 tu, uvamizi huu ambao ni ukiukaji wa Katiba ya Umoja wa Mataifa, umewaweka watu wa Ukraine katika hali ya kutisha.