POPULARITY
Katika Jarida la Habari za Umoja wa Mataofa hii leo Anold Kayanda anakuleteaIdadi ya vifo kufuatia mafuriko makubwa Nepal na Cina inaendelea kuongezeka kwa mujibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa sasa Nepal ni 987 na China 16 huku kukiwa na hofu kuhusu wanawake na wasichanaMashariki ya Kati hali Gaza na Ukingo wa Magharibi bado ni tete kuhusu huduma za afya na upatikanaji wa chakula na mahitaji mengine muhimu yamesema Mashirika la Umoja wa Mataifa la WFP na WHOBarani Afrika , Shirika la Umoja wa Mataifa la masuala ya Ukimwi UNAIDS, Shirika la Maendeleo la Kusini mwa Afrika SADC na China wameingia ubia wa kuimarisha teknolojia kwa ajili ya huduma za afyaNa katika mada kwa kina leo tuko Rwanda ambayo yaimarisha ubora wa kofia ngumu ili kuokoa maisha ya watumiaji wa pikipiki au bodaboda
Katika jarida la Habari za Umoja wa Mataifa hii leo Flora Nducha anakuletea-Harakati za kutokomeza Ebola ya virusi vya Bundibugyo huko Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, zinakumbwa na mkwamo kwani wananchi wamesema wanahitaji sio tu matibabu dhidi ya ugonjwa huo, bali pia maji, chakula, matibabu ya malaria, chanjo na huduma za afya uzazi, mama na mtoto.-hirika la Umoja wa Mataifa la Afya duniani, WHO limetoa mwongozo mpya kuhusu ubora wa maji ya kunywa, likizitaka nchi kuimarisha kanuni, ufuatiliaji na usimamizi wa hatari zozote zinazoweza kujitokeza . Licha ya maendeleo yaliyopatikana, watu bilioni 2.1 bado hawana huduma ya maji ya kunywa inayosimamiwa kwa usalama-kingo wa Magharibi eneo la Palestina linalokaliwa kimabavu na Israeli, Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Kibinadamu, OHCHR, imezisihi mamlaka za Israel kusaidia familia za Wapalestina ambazo zimezingirwa na walowezi ndani ya nyumba zao kwa siku kadhaa, huku kampeni ya kuwapokonya ardhi yao ikizidi kushika kasi.-Na katika mada kwa kina leo tunajikita na Akili Mnemba (AI) na kilimo na kilimo biashara Afrika utamsikia Afisa wa FAO Meshack Malo
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina Flora Nducha wa Idhaa hii anazungumza na mmoja wa walioshiriki mkutano wa CSW70, Masidis Scholastica Madowo Mbunge katika Bunge la Kaunti ya Siaya akiwakilisha kata ya South East Alego jimbo la Magharibi mwa Kenya, ili kuangazia kile anachokifanya kwenye Kaunti yake kuhakikisha wanawake wanapata haki hizo.Hii leo katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York Marekani kutafanyika mdahalo wa wagombea wa nafasi ya Katibu Mkuu wa Umoja huo ambapo wagombea wanne wamejitokeza kuwania wawili wanaume na wawili wanawake. Wagombea hao ni Michelle Bachelet kutoka nchini Chile, Rafael Grossi kutoka nchini Argentina, Rebeca Grynspan kutoka Costa Rica, na Macky Sall kutoka nchini Senegal.Wakati huo huo Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, Annalena Baerbock, amesema mchakato wa kumchagua Katibu Mkuu mpya wa Umoja wa Mataifa ni hatua muhimu itakayoamua mwelekeo wa taasisi hiyo na mustakabali wa ushirikiano wa kimataifa. Akizungumza na waandishi wa habari katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York Marekani kabla ya kuanza kwa mdahalo huo wa wazi, Baerbock ameeleza kuwa uchaguzi huo una umuhimu mkubwa duniani kote, ukigusa maisha ya zaidi ya watu bilioni nane, “Uamuzi huu si wa kiutawala tu, bali ni ujumbe kuhusu maadili na mwelekeo wa Umoja wa Mataifa katika kukabiliana na changamoto za dunia ya leo.”Takribani wahamiaji 8,000 waliripotiwa kufariki dunia au kutoweka duniani kote mwaka 2025, na kufanya jumla ya wahamiaji waliopoteza maisha tangu 2014 kufikia zaidi ya watu 82,000, hii imebainishwa katika takwimu mpya zilizotolewa leo na Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji IOM. Takwimu hizo pia zinaonesha athari kubwa kwa familia, ambapo takribani watu 340,000 wameathirika moja kwa moja. IOM imeonya kuwa njia za uhamiaji si salama na zinazidi kuwa hatari.Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili na hii leo Mtaalam wetu Dkt. Mwanahija Ali Juma, Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili, Zanzibar nchini Tanzania, BAKIZA anafafanua maana na matumizi ya neno "UNYUMBA" Mwenyeji wako ni Rashid Malekela, karibu!
Jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini Kenya kusikia ujumbe wa Hanna Wendot Cheptumo Waziri wa Jinsia, Utamaduni na Maslahi ya Watoto wa Jamhuri ya Kenya ambaye alikuwa miongoni mwa washiriki wa CSW70 akieleza ni kwa namna gani Kenya inapiga hatua katika Lengo namba 5 la Usawa wa Kijinsia.Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amelaani vikali mashambulizi makubwa ya anga yaliyofanywa na Israel dhidi ya Lebanon tarehe 8 Aprili, mashambulizi ambayo yamesababisha mamia ya raia kuuawa na kujeruhiwa, wakiwemo watoto, sambamba na kuharibu kwa kiasi kikubwa miundombinu ya kiraia. Taarifa iliyotolewa New York, Marekani na Msemaji wa Umoja wa Mataifa inamnukuu Guterres akionesha wasiwasi mkubwa kuhusu ongezeko la vifo miongoni mwa raia na kutoa pole kwa watu na Serikali ya Lebanon, akiwatakia nafuu ya haraka wale waliojeruhiwa.Katika tukio jingine hii leo, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amezindua Mfuko wa Urejeshaji wa Palestina uliopewa jina la Horizon Fund, akisisitiza umuhimu wa kuchukuliwa kwa hatua za haraka kusaidia wananchi wa Palestina kurejesha maisha yao na kujenga mustakabali bora. Akizungumza kupitia ujumbe wa video wakati wa uzinduzi uliofanyika Ramallah, huko Ukingo wa Magharibi eneo la Palestina linalokaliwa kimabavu na Israel, Guterres amesema mfuko huo ni sehemu muhimu ya ushirikiano kati ya Umoja wa Mataifa na Taifa la Palestina.Wakati mgogoro wa Sudan ukikaribia kutimiza miaka mitatu, zaidi ya wakimbizi milioni moja wa Sudan walioko nchini Chad wanakabiliwa na hatari kubwa ya kupunguzwa kwa msaada muhimu wa kibinadamu. Onyo hilo limetolewa leo na mashirika mawili ya Umoja wa Mataifa ambayo ni lile la kuhudumia wakimbizi (UNHCR) pamoja na la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) wakitanabaisha kuwa huduma za msingi kama chakula, maji, malazi, ulinzi na huduma za afya zitalazimika kupunguzwa zaidi katika miezi ijayo iwapo pengo la ufadhili la dola milioni 428 halitazibwa haraka.Mwenyeji wako ni Rashid Malekela, karibu!
Mvua kubwa imesababisha mafuriko ya ghafla katika sehemu za Sydney usiku kucha wa Alhamisi hadi Ijumaa, wafanyakazi wakujitolea wa S-E-S wakitoa huduma za uokoaji 44 za maji ya haraka.
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina tukimsikia Barbara Batte Guevara, Mkufunzi anayefundisha lugha ya Kiswahili katika Chuo Kikuu cha Havana nchini Cuba. Kwa kushirikiana na Tanzania chuo hicho ambacho mwezi uliopita kimetimiza miaka 298 tangu kuanzishwa kwake, hivi karibuni kimetoa fursa kwa Wacuba kujifunza lugha ya Kiswahili.Anold Kayanda wa Idhaa hii amemtembelea Profesa Barbara Batte katika jiji la Havana nchini Cuba ili kufahamu zaidi kuhusu hatua hii na mafanikio yaliyofikiwa hadi kufikia sasa. Pia tunakuletea habari kwa ufupi kama zifuatazo.Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametoa wito wa kuanzishwa kwa Mfuko wa Kimataifa wa Akili Mnemba au AI wenye thamani ya dola bilioni 3, ili kuhakikisha teknolojia hiyo inawanufaisha watu wote duniani, badala ya kuwa mali ya mataifa machache au kampuni chache zenye nguvu. Akizungumza katika Mkutano wa Kimataifa wa kujadili Athari za AI huko New Delhi nchini India, Guterres amesema mustakabali wa AI unapaswa kujengwa kwa ushirikiano wa kimataifa”.Mashambulizi makali yanayoendelea kufanywa na Israeli dhidi ya maeneo ya Palestina ya Gaza na Ukingo wa Magharibi ambayo inakalia kimabavu yanatia hofu ya uwezekano wa utokomezaji wa kabila, imesema Ripoti mpya ya Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Binadamu (OHCHR), ya kuanzia Novemba 1 2024 hadi Desemba 31 2025. Ripoti inasema mashambulizi ya Israeli yameweka mazingira ambamo kwamo wapalestina kama kundi watashindwa kuendelea kuishi Gaza huku Ajith Sunghay, Mkuu wa Ofisi ya OHCHR Palestina akisema, “ripoti inachambua mwenendo wa mapigano ya jeshi la Israeli, linaloendelea kuua idadi kubwa ya raia, kusababisha njaa, kuwahamisha takribani wakazi wote wa Gaza, tena zaidi ya mara moja — na kuharibu miundombinu iliyosalia ya kiraia ya Gaza.”wanamgambo wa vikosi vya Rapid Support Forces (RSF) nchini Sudan walitekeleza kampeni iliyoratibiwa ya uharibifu dhidi ya jamii zisizo za kiarabu ndani ya mji wa El-Fasher na viunga vyake, kampeni yenye viashiria vya mauaji ya kimbari, imeeleza ripoti mpya iliyotolewa leo na Tume Huru ya Umoja wa Mataifa ya Kuchunguza Ukweli kuhusu Sudan. Ripoti imetaja vitendo hivyo ni pamoja na kuua wanachama wa kundi la kikabila linalolindwa; kusababisha madhara makubwa ya kimwili na kiakili; ambavyo ni vipengele muhimu vya kosa la mauaji ya kimbari chini ya sheria za kimataifa.Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili tunawasikiliza baadhi ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Havana wanaojifunza lughaya Kiswahili. Tuanze na Yibran Nunez Batte.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
Demokrasia na utaratibu wa kimataifa unaozingatia sheria ziko hatarini, kulingana na ripoti ya kila mwaka ya Shirika la haki za binadamu ama Human Rights Watch. Kuna msisitizo mahususi juu ya Marekani na kile ambacho chombo cha kimataifa kinaelezea kama kudorora kwa haki za binadamu, lakini pia kuna tahadhari juu ya Australia. Sera za uhamiaji na kuwekwa kizuizini kwa vijana za Australia zinaorodheshwa kama 'mapungufu makubwa', zikionyeshwa kuwa ni demokrasia pekee ya Magharibi isiyo na sheria ya kitaifa ya haki za binadamu.
Hii leo jaridani tunaangazia mafuriko makubwa yaliyoikumba Msumbiji, ripoti inayomulika kupungua kwa muda mrefu kwa maji ya chini ya ardhi, na mradi unaolenga kuimarisha sekta ya kilimo katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan kwa ajili ya kuwasaidia wakulima.Kufuatia mafuriko makubwa yaliyoikumba Msumbiji kutokana na mvua zinazoendelea, serikali ya nchi hiyo ya kusinimashariki mwa Afrika imetangaza kuwa hadi kufikia sasa imerekodi vifo vya watu 120 na maelfu ya nyumba zimeharibiwa huku kiwango kikubwa cha fecha kikihitajika.Katika muktadha wa kupungua kwa muda mrefu kwa maji ya chini ya ardhi, matumizi kupita kiasi ya rasilimali za maji, uharibifu wa ardhi na udongo, ukataji miti, pamoja na uchafuzi wa mazingira, Chuo Kikuu cha Umoja wa Mataifa UNU leo kimetoa ripoti ikitangaza kuingia kwa “enzi ya kufilisika kwa maji duniani” na kutoa wito kwa viongozi wa dunia kuendana na uhalisia huu mpya kwa kuzingatia ushahidi wa kisayansi.Kwa muongo mmoja kuanzia mwaka wa 2016 hadi mwaka wa 2025, Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo Duniani (FAO) kwa ushirikiano na serikali ya Canada limechangia kwa kiasi kikubwa kuimarisha sekta ya kilimo katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan likilenga kuwasaidia wakulima na vyama vya ushirika kushinda changamoto za muda mrefu za uzalishaji, masoko na mnepo wa maisha.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
Kwa muongo mmoja kuanzia mwaka wa 2016 hadi mwaka wa 2025, Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo Duniani (FAO) kwa ushirikiano na serikali ya Canada limechangia kwa kiasi kikubwa kuimarisha sekta ya kilimo katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan likilenga kuwasaidia wakulima na vyama vya ushirika kushinda changamoto za muda mrefu za uzalishaji, masoko na mnepo wa maisha. Sheilah Jepngetich na taaarifa zaidi.
Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) leo limeonya kuwa bila rasilimali na hatua za haraka, watu walio katika mazingira magumu zaidi Afrika Magharibi na Kati wanakabiliwa na mwaka mwingine mgumu sana wa njaa. Anold Kayanda na taaarifa zaidi.
Katika wiki za hivi karibuni, moto wa nyika umesababisha uharibifu wa nyumba na mali katika maeneo ya pwani ya katikati ya kaskazini ya New South Wales, Geraldton huko Magharibi mwa Australia na mashariki mwa Tasmania. Wataalamu wanaonya kuwa huu ni mwanzo tu wa msimu wa moto na nyinyi ambao mnasafiri kwa ajili ya likizo mnahitaji kuwa na ufahamu na maandalizi mkiwa mbali na nyumbani.
Kwa mtengenezaji wa mvinyo wa Kipalestina kutoka Australia, Sari Kassis, ukweli wa kilimo katika Ukingo wa Magharibi ni hali ya hatari ya kila wakati, kimwili na kiakili. Kwa kuongezeka kwa vurugu za walowezi katika Ukingo wa Magharibi, mavuno ya mwaka huu yameona idadi ya juu zaidi ya mashambulizi ya Waisraeli kwenye mashamba na mali.
Hii leo jaridani tunaangazia ripoti ya UNDP ya umaskini, mradi wa kusaidia jamii kupambana na athari za mabadiliko ya tabianchi nchini Zambia na juhudi za kuboresha hali ya lishe kwa watoto nchini Kenya.Takribani watu milioni 887 duniani ambao ni maskini wanaishi kwenye maeneo yanayokumbwa moja kwa moja na madhara manne yasababishwayo na mabadiliko ya tabianchi ambayo ni joto kali, mafuriko, ukame na uchafuzi wa hewa, imesema ripoti mpya iliyotolewa leo na shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo, UNDP kwa kushirikiana na wadau. Ripoti inaonesha bayana kuwa hali hiyo inazidi kutwamisha watu hao kwenye hali tete zaidi.Mradi wa kusaidia jamii kupambana na athari za mabadiliko ya tabianchi nchini Zambia mbali na kusaidia wananchi kwenye kilimo pia umewawezesha kiuchumi na kuwaondoa baadhi yao kwenye mstari wa umasikini. Mmoja wa walio utupa mkono umasikini ni Judith Mabeta aliyetoka kuishi nyumba ya udongo mpaka kuwa na nyumba ya kupangisha na sasa ni mama mwenye nyumba.Kupitia msaada wa fedha kutoka Ufaransa, juhudi za kuboresha hali ya lishe kwa watoto nchini Kenya, hasa kwa jamii zilizo katika mazingira hatarishi zinaendelea ambapo juhudi za hivi karibuni ni kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) kwa kushirikiana na Shirika la Msalaba Mwekundu la Kenya ambao kwa pamoja wameimarisha huduma hizo kwa manusura wa mafuriko Magharibi mwa taifa hilo la Afrika Mashariki. Huduma hizi ni sehemu muhimu ya kuhakikisha watoto na familia wanapata vyakula vyenye virutubishi kwa ustawi wa maisha yao.Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!
Kupitia msaada wa fedha kutoka Ufaransa, juhudi za kuboresha hali ya lishe kwa watoto nchini Kenya, hasa kwa jamii zilizo katika mazingira hatarishi zinaendelea ambapo juhudi za hivi karibuni ni kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) kwa kushirikiana na Shirika la Msalaba Mwekundu la Kenya ambao kwa pamoja wameimarisha huduma hizo kwa manusura wa mafuriko Magharibi mwa taifa hilo la Afrika Mashariki. Huduma hizi ni sehemu muhimu ya kuhakikisha watoto na familia wanapata vyakula vyenye virutubishi kwa ustawi wa maisha yao. Sheilah Jengetich na taarifa zaidi kupitia video ya UNICEF Kenya.
Leo Agosti 25 ni miaka minane tangu kufurushwa kwa wingi watu wa kabila la Rohingya kutoka katika jimbo la Rakhine nchini Myanmar. Umoja wa Mataifa unatoa wito wa mshikamano wa kimataifa kuwasaidia kwani mateso kwa watu hao yanaendelea kuwa mabaya zaidi kila uchao. Anold Kayanda na taarifa zaidi.Asante AssumptaMyanmar (zamani ikiitwa Burma) ni nchi ya Kusini Mashariki mwa Asia yenye zaidi ya makabila 100, inayopakana na India, Bangladesh, China, Laos na Thailand.Warohingya wanafurushwa na kuteswa kwasababu mbalimbali zikiwemo za kihistoria kwa madai kuwa walitoka Bangladesh ingawa wameishi vizazi na vizazi nchini Myanmar. Pia sababu ya imani yao kwa uislamu miongoni mwa sababu nyingine.Ni miaka minane sasa tangu ufurushwaji mkubwa wa jami hii kutoka jimbo la Rakhine pwani ya Magharibi mwa Myanmar. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres anaonya kuwa Warohingya na raia wengine bado wanakabiliwa na ukiukaji wa haki za binadamu na kufurushwa. Anaeleza wasiwasi wake kuhusu tarifa za kufukuzwa na kupunguzwa kwa nafasi za hifadhi katika ukanda huo, huku wakimbizi walioko Bangladesh wakikabiliana na upungufu mkubwa wa msaada wa chakula, elimu na huduma za afya.Guterres anasisitiza tena wito wake wa kulindwa kwa raia wote kwa mujibu wa sheria za kimataifa na anataka mshikamano mkubwa wa kimataifa. Hata hivyo ana matumaini kuwa Mkutano wa Ngazi ya Juu kuhusu Rohingya utakaofanyika New York mwezi ujao utasaidia kupata suluhu za kudumu.Kwa upande wake, Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa, Volker Türk, anaeleza kuwa jeshi la Myanmar na Jeshi la Rakhine bado wanaendeleza uhalifu mkubwa dhidi ya Rohingya bila kuchukuliwa hatua, kinyume na sheria za kimataifa na maagizo ya Mahakama ya Kimataifa ya Haki na anatoa wito wa kukomesha matendo hayo ili kuvunja mzunguko wa vurugu.
Hii leo jaridani tunaangazia hali ya msaada wa kibinadamu katika ukanda wa Gaza, na mlipuko wa kipindupingu nchini Sudan. Makala tunafuatilia ziara ya katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Kazakhstan na mashinani tunamulika unyonyeshaji Sudan Kusini.Simulizi za huzuni, majonzi na kukata tamaa zinaendelea kila uchao huko Ukanda wa Gaza, eneo la Palestina linalokaliwa kimabavu na Israel hasa wakati huu ambapo raia wanaokwenda kusaka chakula wanakumbwa na mashambulizi yanayosababisha vifo. Ijumaa iliyopita Umoja wa Mataifa uliripoti kuwa zaidi ya watu 100 waliuawa na mamia kadhaa walijeruhiwa katika siku mbili pekee Wakisaka chakula.Zaidi ya watoto 640,000 walio na umri wa chini ya miaka mitano wapo hatarini kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu huko Kaskazini mwa Darfur, nchini Sudan.. Katika makala Anold Kayanda anatupeleka Asia ya Kati ambako Umoja wa Mataifa na Kazakhstan wamesaini makubaliano ya Kazakhstan kuwa mwenyeji wa Kituo cha Kikanda cha Umoja wa Mataifa cha Malengo ya Maendeleo Endelevu kwa ajili ya ukanda wa Asia ya Kati na Afghanistan..Na mashinani nawapisha wanafunzi wawili,Wanga pamoja na Kifaya ambao ni wanafunzi katika shule ya Sekondari ya Askofu Abangite iliyopo jimbo la Yambio,kusini Magharibi mwa Sudani Kusini karibu na mpaka wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.Wakizungumza na shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia watoto UNICEF nchini humo wameeleza umuhimu wa maziwa ya mama kwa mtoto.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa haki za binadamu Volker Türk ameyahimiza mataifa yote ulimwenguni kuchukua hatua za haraka ili Israel ikomeshe uwepo wake kinyume cha sheria katika ardhi ya Palestina inayoikalia kimabavu, na kuhakikisha suluhu ya mataifa mawili inapatikana. Tupate taarifa zaidi kutoka kwa Leah MushiKamishna Turk ameyasema hayo katika tarifa yake aliyoitoa kwa njia ya video kabla ya kuanza kwa mkutano wa ngazi ya juu hapa katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York Marekani unaolenga kujadili Suluhu ya kudumu kwa mgogoro kati ya Israel na Palestina ambao umedumu kwa miongo kadhaa sasa.Turk amesema: “Ninahimiza hatua za haraka za Israel kukomesha uwepo wake kinyume cha sheria katika ardhi ya Palestina inayokaliwa kwa mabavu, na kwa pande zote kufanyia kazi maendeleo yanayoonekana kuelekea suluhu ya Serikali mbili.”Akatoa angalizo kwa zile nchi zitakazo shindwa kuweka shinikizo kwa Israel kukomesha mauaji huko katika Ukanda wa Gaza.“Nchi ambazo zinashindwa kutumia nguvu zao zinaweza kuwa na hatia katika uhalifu wa kimataifa. Kila siku tunaona madhila yasiyoelezeka huko Gaza na Ukingo wa Magharibi kwa hofu na kufadhaika. Kila siku, tunaona uharibifu zaidi, mauaji zaidi, na udhalilishaji zaidi wa Wapalestina.”Mkuu huyo wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa amehitimisha video yake ya dakika 4 na sekunda 7 kwa kusema kuwa dunia itaihukumu mikutano ya aina hii kwa kile inachokifanya kwa vitendo, na kuongeza kuwa ofisi yake iko tayari kusaidia taifa la Palestina katika ujenzi wa nchi yenye msingi wa haki za binadamu na utawala wa sheria, pindi utulivu utakapopatikana.
Jaridani leo tunaangazia msaada wa kibinadamu katika ukanda wa Gaza, na uhakika wa chakula nchini Uganda. Makala tunaangazia mradi wa kulinda mazingira na kazi za kujitolea. Mashinani inamulika utayari wa nchi ya Nigeia kufanikisha Malengo ya Maendeleo Endelevu, SDGs. Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani, WFP, kupitia Apu yake ya kidigitali Gawa Chakula au ShareTheMeal, limeingia ushirikiano na Apu maarufu huko Mashariki ya Kati iitwayo Careem na kuzindua kampeni ya kuchangisha msaada wa dharura kwa watu wanaokumbwa na njaa katika eneo la Gaza na Ukingo wa Magharibi maeneo yanayokaliwa kimabavu na Israeli.Licha ya changamoto za ufadhili, Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) nchini Uganda linasisitiza umuhimu wa usafirishaji katika kutoa msaada wa chakula. Sahir Aslam, Mkuu wa Idara ya Ugavi ya WFP Uganda, akizungumza kutokea huko huko Uganda katika maghala ya shirika hilo anafafanua kila kilomita moja ambayo msaada wa chakula wa WFP unasafiri.Katika makala Assumpta Massoi anatupitisha kwenye kazi ya kujitolea iliyofanyika kuadhimisha siku ya Nelson Mandela Julai 18 hapa Marekani.Na katika mashinani fursa ni yake Esse Oduwan, msichana mwenye umri wa miaka 14 kutoka Nigeria, akihoji utayari wa nchi kufanikisha Malengo ya Maendeleo Endelevu, SDGs baada ya nchi tatu ikiwemo Eswatini na Bangladesh kuwasilisha tathmini za utekelezaji wa Malengo hayo yanayofikia ukomo 2030.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani, WFP, kupitia Apu yake ya kidigitali Gawa Chakula au ShareTheMeal, limeingia ushirikiano na Apu maarufu huko Mashariki ya Kati iitwayo Careem na kuzindua kampeni ya kuchangisha msaada wa dharura kwa watu wanaokumbwa na njaa katika eneo la Gaza na Ukingo wa Magharibi maeneo yanayokaliwa kimabavu na Israeli. Leah Mushi na taarifa zaidi
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini Tanzania kumulika juhudi za kinamama wajawazito na wanao kuambatana wakihudhuria kliniki kwa ajili ya mimbasalama. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na mashinani.Takribani wapalestina 900 wameuawa katika wiki za hivi karibuni huko Ukanda wa Gaza, eneo linalokaliwa kimabavu na Israeli. wakihaha kupokea chakula. Msemaji wa Ofisi ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa Thameen Al-Kheetan amewaeleza waandishi wa habari Geneva, Uswisi kuwa watu 674 kati yao waliuawa wakiwa kwenye maeneo ya Mfuko wa Kiutu wa Gaza, (GHF) unaoendeshwa na Israeli na Marekani.Wakati huo huo Bwana Al-Kheetan amezungumzia mauaji yanayoendelea Ukingo wa Magharibi ikiwemo Yerusalemu Mashariki akisema, “muathirika mdogo zaidi ni Laila Khatib mwenye umri wa miaka miwili. Alipigwa risasi ya kichwa na jeshi la Israeli akiwa nyumbani kwao kijijini Ash-Shuhada.”Na leo ikiwa siku ya kimataifa ya stadi kwa vijana Sangheon Lee, Mkurugenzi wa Ajira na Sera katika Shirika la Umoja wa Mataifa la Ajira amesema …lazima tuhakikishe kuwa vijana wanapata ujuzi ambao ni wa maana, unaoweza kutumika katika mazingira mbalimbali, na unaotambuliwa na waajiri.Na kaika mashinani tunakupeleka jijini Nairobi, Kenya, ambako kupitia video iliyoandaliwa na washirika wetu Radio Domus, tunamsikia Dennis Mabuku, Mkuu wa Idara ya Usalama, Afya, Mazingira na Ubora katika kampuni ya BOC Kenya. Dennis anaeleza jinsi wanavyoichakata hewa ya kawaida na kuisafisha ili kupata hewa safi ya oksijeni kwa ajili ya matumizi ya hospitali na mabaki mengine kwa ajili ya matumizi mengine ya viwandani.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
Hii leo jaridani tunaangazia hali ya wahamiaji na wakimbizi nchini Libya, na wakimbizi wajasiriamali katika makazi ya wakimbizi ya Kakuma nchini Kenya. Makala inatupeleka Jerusalemu Mashariki, na mashinani nchini Chad, kulikoni?Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji, IOM, limeeleza mshtuko mkubwa na wasiwasi wake kufuatia kugunduliwa kwa makaburi mawili nchini Libya walimozikwa wahamiaji kadhaa, baadhi yao wakiwa na majeraha ya risasi.Katika kambi ya wakimbizi ya Kakuma, kutokana na ufadhili wa shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP), kundi la vijana wanajishughulisha na ufugaji wa wadudu nyenje (Crickets) ili kukabiliana na changamoto ya utapiamlo miongoni mwa watoto wachanga.Katika makala Sharon Jebichii anakupeleka Mashariki ya Kati kumulika ziara aliyofanya Mkuu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Misaada ya Dharura, OCHA huko Ukingo wa Magharibi na Gaza ili kujionea hali halisi ya raia.Na mashinani kupitia video ya shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu, UNFPA, nampisha Daralssalam, kutoka Sudan ambaye alikuwa Mhadhiri Chuo Kikuu lakini sasa mkimbizi nchini Chad akieleza changamoto alizopitia na kuomba jamii ya kimataifa isaidie wanawake wa Sudan.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
Huko Mashariki ya Kati Mkuu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Misaada ya Dharura, OCHA Tom Fletcher alifanya ziara ya siku tatu huko Ukingo wa Magharibi na Gaza ili kujionea hali halisi ya raia. Katika Sharon Jebichii amefuatilia ziara yake na kutuandalia makala hii..
Hii leo jaridani tunaangazia magonjwa ya mfumo wa kupumua vikiwemo virusi vya metapneumovirus, na watoto waathirika wa vita Gaza. Makala inatupeleka nchini Mali na mashinani nchini Tanzania, kulikoni?Huku kukiwa na ripoti za kuongezeka kwa maambukizi ya magonjwa ya mfumo wa kupumua vikiwemo virusi vya metapneumovirus (HMPV) wakati huu wa msimu wa baridi nchini China na kuleta hofu ulimwenguni kuhusu uwezekano wa kutokea kwa janga jingine la ugonjwa kama ilivyokuwa Covid-19, mamlaka ya afya nchini humo inasema kiwango na nguvu za ugonjwa huo viko chini ikilinganishwa na wakati kama huu mwaka jana, ameeleza Hans Kluge, Mkurugenzi wa shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ulimwenguni kanda ya Ulaya akisisitiza ulimwengu kupata taarifa sahihi.Baada ya miezi 14 ya vita Gaza maelfu ya watu wakiwemo watoto wamesalia na ulemavu wa maisha kwa kulazimika kukatwa viungo kutokana na kujeruhiwa katika vita inayoendelea kwa miezi 15 akiwemo mtoto wa umri wa miaka 7 Mahmmoud ambaye sasa amepooza baada ya kupigwa risasi mgongoni na anahitaji huduma za haraka za afya ili akatibiwe limesema shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu masuala ya kibinadamu na misaada ya dharura OCHA.Katika makala Assumpta Massoi anakupeleka Magharibi mwa Afrika kusikia jinsi raia wa taifa la Mali walioko ughaibuni wanavyoleta nuru kwa wakulima wa mpunga nchini mwao.Mashinani fursa ni yake Hilda, Mama mwenye umri wa miaka 31 ambaye ni mkimbizi kutoka Burundi anayeishi katika makazi ya wakimbizi nchini Tanzania, anashukuru mfuko wa msaada wa marekani wa kitengo cha Idadi ya watu, wakimbizi na uhamiaji, PRM (Population, Refugees, and Migration Bureau, PRM) kwa huduma za afya ya watoto na kinamama wajawazitito kupitia Shirika la Umoja wa Mataifa ya kughudumia wakimbizi UNHCR.Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!
Matangazo ya nusu saa kuhusu habari za mapema asubuhi pamoja na habari za michezo.
Matangazo ya nusu saa kuhusu habari za mapema asubuhi pamoja na habari za michezo.
Kadri siku zinavyozidi kusonga mbele, hali ya usalama na kibinadamu huko Ukanda wa Gaza inazidi kuzorota huku raia na hata wafanyakazi wa kutoa misaada wakisalia wamepigwa butwaa kwani mashambulizi kutoka Israeli yanaendelea kila uchao. Naanzia ndani ya hospitali ya Kamal Adwan kaskazini mwa Gaza, mtoto aliyejeruhiwa amebebwa akilia kwa uchungu. Kwingineko mgonjwa mwingine anatolewa kwenye gari la wagonjwa! Ni taswira iliyozoeleka sasa Gaza.Louise Wateridge ambaye ni Afisa Mwandamizi wa Masuala ya Dharura katika shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi wa kipalestina, UNRWA akihojiwa na Idhaa ya Umoja wa Mataifa kutoka Gaza Kati amesema hali si hali.Anasema, “mambo kwa kweli yanazidi kuwa mabaya hapa. Kukata tamaa ni kila mahali. Namaanisha, watu unaozungumza nao, na wafanyakazi wenzangu niliozungumza nao hawajui sasa wafanye nini. Hawafahamu waende wapi. Unaweza kusikia nyuma yangu milio ya makombora ikiendelea.”Bi. Wateridge akaendelea kusema kuwa, “kutokuwa na matumaini ndio neno pekee lililosalia Gaza. Unafahamu watu milioni 2.2. Inabidi umkumbushe kila mtu kwamba wamenasa. Hakuna njia ya kutoka nje ya Ukanda wa Gaza na mashambulio ya mabomu yanaendelea mchana kutwa na usiku kucha.”Hali ikiendelea hivyo hii leo huko katikati mwa Gaza, hapo jana jeshi la Israeli lilishambulia na kuharibu kwa kiasi kikubwa ofisi ya UNRWA iliyoko Ukingo wa Magharibi, ofisi ambayo ilikuwa inategemewa zaidi katika kutoa msaada kwa wakimbizi zaidi ya 14,000 wa kipalestina wanaoishi katika kambi ya Nur Shams.UNRWA kupitia mtandao wa X imesema kitendo cha kushambulia ofis iza UN lazima kikome na badala yake zilindwe wakati wote.
Hali Gaza inaendelea kuwa tete wakati ucheleweshwji wa kuhamisha wagonjwa hususan watoto wanaohitaji msaada wa haraka wa huduma za afya imekuwa ni hukumu ya kifo kwao huku maelfu ya watu wakiendelea kukosa mahitaji ya muhimu ya kila siku ikiwemo chakula kama mkate, yameonya leo mashirika ya Umoja wa Mataifa.Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF limeonya kwamba idadi ya watoto wanaohamishwa Gaza kwa ajili ya huduma za dharura za matibabu imeshuka sana hadi kufikia mtoto mmoja kwa siku na kusema kiwango hiki kikiendelea itachukua zaidi ya miaka 7 kuhamisha watoto 2500 wanaohitaji huduma ya dharura ya matibabu.Akizungumza na waandishi wa habari mjini Geneva Uswis msemaji wa UNICEF James Elder amesema “matokeo yake watoto wanakufa Gaza sio tu kutokana na mabomu na risasi na makombora yanayofurusmishwa lakini kwa sababu hata kama miujiza inatokea , hata kama mabomu yanalipuka na nyumba kuporomoka, na vifo kuongezeka watoto wananusurika, lakini kisha wanazuiliwa kuondoka Gaza Kwenda kupokea huduma za afya zitakazookoa maisha yao.”Ameongeza kuwa tangu Januari hadi Mei mwaka huu kwa wastan watoto 296 walihamishwa kwa mwezi kwenda kupata matibabu lakini tangu kufungwa kivuko cha Rafah idadi imeshuka hadi watoto 22 kwa mwezi.Kwa upande wake shirika la Umoja wa Mataifa la msaada kwa wakimbizi wa Kipalestina UNRWA linasema maisha ya kawaida yanazidi kuwa jinamizi kwani kukidhi mahitaji ya msingi kama chakula ni mtihani mkubwa wengi mathalani katika mji wa Deir al-Balah hata mkate ambao ni chakula kikuu kupatikana ni changamoto,Kila mtu katika Ukanga wa Gaza anakabiliwa na hatari ya baa la njaa kutokana na kuendelea kwa mashambulizi ya mabomu, ghasia, kuharibiwa kwa mashamba na wahudumu wa kibinadamu kushindwa kuwafikia wenye uhitaji.Wataalam wa Umoja wa Mataifa wa haki za binadamu nao wamesema wanahofia hali mbaya ya Wapalestina wenye ulemavu ambao wamekwama Gaza, wakionya kwamba watu hao wenye ulemavu wanakabiliwa na hatari za ulinzi ikiwemo kutoepuka kifo na majeraha wakati wa mashambulizi ya vikosi vya Israel na hili ni janga juu ya janga wamesema.Nalo shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu misaada ya kibinadamu na masuala ya dharura OCHA likimulika Ukingo wa Magharibi limesema “Makumi ya jamii zinakabiliwa na ongezeko la mashambulizi na vikwazo vya kufikia ardhi yao wakati wa mavuno ya mizeituni ya mwaka huu. Kati ya matukio yote yanayohusiana na walowezi, matukio 104 yamesababisha hasara au uharibifu mkubwa wa mali tangu kuanza kwa mwezi huu wa Oktoba ”.
Tume hiyo huru imeyasema hayo katika taarifa mpya ya msimamo wa kisheriia iliyotolewa mjini Geneva Uswis kuhusu eneo linalokaliwa la Palestina ikiwemo Jerusalem Mashariki ambayo imeweka wazi maoni ya tume kuhusiana na wajibu wa serikali na jinsi Baraza Kuu na Baraza la Usalama linavyoweza kutambua na kutekeleza mbinu na hatua sahihi zinazohitajika kwa kazi hiyo hadi mwisho wa ukaliwaji huo, na kwa haraka iwezekanavyo.Tume ihiyo imebaini kwamba maoni ya ushauri ya Mahakama ya Kimataifa ya Haki kuhusu matokeo ya Kisheria yanayotokana na sera na desturi za Israel katika eneo linalokaliwa la Palestina ikiwa ni pamoja na Jerusalem Mashariki ni wenye mamlaka na usio na utata kwa kusema kwamba kuendelea kuwepo kwa Israel katika eneo la Palestina linalokaliwa kwa mabavu ni kinyume cha sheria na sheria ya kimataifa.Taarifa hiyo ikitolewa Geneva Gaza kwenyenyewe hali inaendelea kuwa tete, kwa mujibu wa Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la msaada kwa wakimbizi wa Kipalestinna UNRWA Phillipe Lazzarini, kwani shule nyingine ya UNRWA imeshambuliwa leo Jabalia Kaskazini mwa Gaza, watu kadhaa wameripotiwa kuuawa na miongoni mwao Watoto wengi waliokuwa wakipata hifadhi katika jengo hilo.Lazzarini amesema hili ni shambulio la tatu dhidi ya majengo ya UNRWA kwa wiki moja. Na pia wafanyakazi wa shirika hilo wanaendelea kuuawa sasa wameffikia 231 tangu kuanza kwa vita hii Oktoba mwaka jana.Naye msemaji wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Watoto UNICEF James Elder akizungumza na waandishi wa habari mjini Geneva Uswisi hii leo amesema “Gaza ni mfano halisi wa ulimwengu wa kuzimu duniani kwa watoto milioni moja wa eneo hilo. Na hali inazidi kuwa mbaya, siku baada ya siku, tunapoona athari za kutisha za mashambulizi ya anga ya kila siku na operesheni za kijeshi za Israek kwa watoto wa Kipalestina.”Nalo shirika la kuratibu misaada ya kibinadamu OCHA likiangazia Ukingo wa Magharibi limesema “Vikosi vya Israel vimekuwa vikitumia mbinu mbaya za vita katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan, na kuibua wasiwasi mkubwa juu ya matumizi ya nguvu kupita kiasi na kuongeza mahitaji ya kibinadamu ya watu.” Ameelezea wasiwasi kuhusu mashambulizi ya walowezi wa Israel dhidi ya Wapalestina na miti yao ya mizeituni wakati huu wa mavuno ya kila mwaka.
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka Mwanza kaskazini Magharibi mwa Tanzania kupata ufafanuzi wa athari za moshi wa kuni kwa binadamu. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na sauti kutoka mashinani.Miaka 63 tangu kifo cha ajali ya ndege cha Katibu Mkuu wa pili wa Umoja wa Mataifa Dag Hammarskjöld huko Ndola Zambia, bado majibu hayajapatikana ya nini kilisababisha ajali hiyo wakati akielekea kusaka amani kwa iliyokuwa Congo, sasa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi wa kipalestina, UNRWA limesema kampeni ya chanjo eneo la kaskazini mwa Gaza imeendelea leo jumanne licha ya tukio la jana la jeshi la Israeli kuzuia kwa saa nane msafara wa wafanyakazi waliokuwa wanasafiri kwenda kutoa huduma hiyo.Na leo septemba 10, mkutano wa 78 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, UNGA78 unakunja jamvi baada ya mwaka mzima wa mikutano na mijadala, na hivyo kuashiria kuanza kwa mkutano wa 79 ambapo kuanzia tarehe 22 vitaanza vikao vya ngazi ya juu na Mjadala Mkuu wa Baraza Kuu. Rais anayemaliza muda wake ni Balozi Dennis Francis kutoka Trinidad na Tobago na anayempatia kijiti ni Philemon Yang kutoka Cameroon.Katika mashinani, tunamulika mwaka mmoja tangu kimbunga Daniel kipige mji wa Dema mashariki mwa Libya na vitongoji vyake na kuleta mvua kubwa iliyosababisha mafuriko yaliyoua zaidi ya watu 5,000, na kuacha makovu hadi sasa. Maelezo ya Hawa Bu Zqeeba aliyempoteza baba yake katika mafuriko hayo yanakupatia taswira halisi ya makovu.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
Vuta nikuvute ikiendelea Gaza kuhusu ufikishaji, usambazaji na utoaji wa chanjo dhidi ya polio wakati huu ambapo makombora yanaendelea kurindima kutoka jeshi la Israeli, hii leo shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ulimwenguni WHO, limethibitisha kubainika kwa mgonjwa mmoja wa polio, ikiwa ni miaka 25 tangu ugonjwa huo utokomezwe eneo hilo. Assumpta Massoi na maelezo zaidi.(Taarifa ya Assumpta Massoi)Ni kwamba tarehe 20 mwezi uliopita wa Julai, mtoto huyo mwenye umri wa miezi 10 alilazwa katika hospitali ya Al-Aqsa akiwa ana homa kali, anatapika, anahara huku akiwa hana nguvu mwilini, limesema shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi wa kipalestina, UNRWA katika ripoti yake ya 130 kutolewa tangu vita ianze huko Gaza, ikimulika Gaza, Ukingo wa Magharibi na Yerusalem Mashariki.Tarehe 22 Wizara ya Afya kwenye eneo linalokaliwa la Palestina likathibitisha ugonjwa wa polio virusi namba 2 kwa mtoto huyo ambaye hakuwa amepatiwa chanjo kutoka Deir al-Balah huko Gaza. Siku tatu baadaye yaani tarehe 25 Julai mtoto huyo akapooza sehemu ya chini ya mguu wake. Hivi sasa anaendelea na matibabu na hali yake ni nzuri.Uchunguzi uliofanywa na Kituo cha Marekani cha Kudhibiti na Kuzuia magonjwa, CDC ukaunganisha virusi hivyo na aina ya ile iliyobainika kwenye mazingira huko Gaza mwezi Juni mwaka huu.Sasa WHO imethibitisha kuwa ni polio ambapo Mkurugenzi Mkuu wa UNRWA Philippe Lazzarini kupitia mtandao wa X amesema “inasikitisha sana kwamba mtoto huyo amepooza kutokana na Polio. Polio haitotofautisha kati ya watoto wa Palestina na Israeli. Kuchelewecha sitisho la mapigano kwa misingi ya kiutu kutaongeza hatari ya ugonjwa huo kusambaa zaidi kwa watoto.”Awamu mbili za utoaji chanjo zimepangwa kuanza wiki zijazo na UNRWA imesema wataalamu wake wa afya na kupitia kliniki zake tembezi watasaidia usambazaji kwa ushirikiano na WHO na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF.
Matangazo ya nusu saa kuhusu habari za mapema asubuhi pamoja na habari za michezo.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken alijadili mageuzi ya kiutawala na Rais wa Palestina Mahmoud Abbas wakati wa mkutano wao leo Jumatano katika Ukingo wa Magharibi, pamoja na juhudi za kuimarisha misaada ya kibinadamu kwa watu wa Ukanda wa Gaza.
Matangazo ya nusu saa kuhusu habari za mapema asubuhi pamoja na habari za michezo.
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina ambapo leo ninatupeleka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, kama ilivyo sehemu nyingi za Afrika Mashariki nako lugha ya kiswahili inatajwa kuwa chombo chenye nguvu sana kinachoingilia kati ujenzi wa amani na pia katika biashara hasa kwa wakaazi wa mji wa Goma katika jimbo la Kivu Kaskazini mashariki mwa nchi hiyo. Kiswahili ndio lugha ya kwanza nchini DRC yenye idadi kuwa ya wazungumzaji katika mikoa ya Mashariki na Magharibi mwa nchi ambako inatumiwa hata kwenye vyombo vya habari kama Redio na televisheni. Pia tunaangazi ripoti ya UNFPA ya idadi ya watu Duniani. Mashinani tunakupeleka nchini Haiti, kulikoni?Mwenyenji wako ni Leah Mushi, karibu!
Wanachama wa Jumuiya ya DR Congo wanao ishi mjini Sydney, walijumuika katika hafla maalum yaku adhimisha miaka 63 ya uhuru wa nchi yao pendwa.
Hii leo ni Siku ya Kimataifa ya Uelewa Kuhusu Ualbino na kama ilivyo ada ya kila Jumanne tunakuletea mada kwa kina ambapo tutamsikia mwanamuziki Roben X akieleza kuhusu maisha yake ya Ualbino. Pia tunakuletea habari kwa ufupi zikiwemo za DRC, Myanmar na Ukraine. Mashinani tunasalia hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa tukikuletea ujumbe kuhusu ujumuishaji na uajiri wa watu wenye ualbino.Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Watoto UNICEF limesema imeshtushwa na shambulio dhidi ya kambi ya wakimbizi wa ndani lililofanyika jana Jumatatu katika jimbo la Ituri, Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC.Nchini Ukraine Umoja wa Mataifa unashirikisha serikali ya taifa hilo na ya Shirikisho la Urusi ili kuhakikisha upatikanaji wa fursa ya kuwafikia raia wote walioathiriwa na uharibifu mkubwa wa bwawa la Kakhovka.Na mwezi mmoja baada ya kimbunga Mocha kupiga Magharibi mwa Myanmar, mratibu mkazi na wa misaada ya kibinadamu wa umoja wa Mataifa Ramanathan Balakrishnan amesema leo kwamba baraza la uongozi wa jimbo la Rakhine limesitisha fursa ya kufikisha misada ya kibinadamu katika jimbo hilo na hivyo kuathiri usambazaji wa misaada ya kuokoa Maisha katika jamii zilizoathirika.Na katika mashinani leo nampisha Mtaalam Huru wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za watu wenye ualbino.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina aambapo tutasalia hapa makao makuu kusikiliza msimamo wa Tanzania kuhusu Umoja wa Mataifa kufuatia mazungumzo yetu na Mwakilishi mpya wa kudumu wa Tanzania kwenye Umoja wa Mataifa Balozi Hussein Kattanga. Pia tunaluletea habari kwa ufupi zikiwemo za machafuko nchini Sudan, njaa uliokithiri katikati mwa Afrika na ukosefu wa elimu ka wasichana nchini Afghanistan. Mashinani tunakupeleka nchini Malawi, kulikoni?Kamishina Mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Volker Türk, ametoa wito wa kusitishwa uhasama mara moja nchini Sudan akilisihi jeshi la serikali SAF na vikosi vya upinzani Rapid Support Forces RSF kurejea katika meza ya mazungumzo.Kiwango cha kutokuwa na uhakika wa chakula katika nchi za Magharibi na katikati mwa afrika kinaratajiwa kuwa cha juu Zaidi mwaka huu katika kipindi cha miaka 10 huku kikitishia kusambaza njaa katika nchi nyingine za pwani na zile zinazokabiliwa na mizozo kama Burkina Faso na Mali kwa mujibu wa utafiti mpya uliotolewa leo na shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP.Na utafiti mpya uliofanywa na shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa maendeleo UNDP unaonyesha kwamba bila wasichana kuendelea na masomo na wanawake kufanya kazi nchini Afghanistan matarajio ya kujikwamua kiuchumi kwa taifa hilo yatasalia kuwa ndoto.Na katika mashini tutaelekea nchini Malawi kushuhudia furaha ya wenyeji baada ya kupata hakikisho la chakula kufuatia kilimo kinachostahimili mabadiliko ya tabianchi.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, Karibu!
Nchini Tanzania, shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo, FAO kupitia mradi wake FISH4ACP limepokea matokeo ya Utafiti kuhusu Usawa wa Kinjisia katika Masuala ya Uvuvi, moja ya hoja ambayo ikitekelezwa vema itasaidia kufanikisha malengo ya maendeleo endelevu, SDGs hasa la kutokomeza njaa na kuondokana na umaskini.Uzinduzi wa matokeo hayo umefanyika wakati wa kikao cha siku mbili hapa mkoani Kigoma na unatoka na Utafiti kuhusu Usawa wa kijinsia katika mnyororo wa thamani wa mazao ya Uvuvi Ziwa Tanganyika ukishirikisha wadau mbalimbali wakiwemo wavuvi, wachakataji, wasafarishaji, Jeshi la Polisi, serikali na wadau wa maendeleo.Devotha Songorwa wa Redio washirika Kids Time FM nchini Tanzania ndio shuhuda wetu wa uzinduzi huo uliofanyika katika Mkoa wa Kigoma, Magharibi mwa Taifa hilo la Afrika Mashariki amezungumza na Afisa Mtaalamu Mnyororo wa Thamani wa Uvuvi na Ufugaji Viumbe Maji, kutoka FAO nchini Tanzania anayesimamia mikoa ya Katavi, Rukwa na Kigoma nchini Tanzania, Hashim Muumin, ambaye amempatia muhtasari wa matokeo ya utafiti huo kutokana na mradi huo wa miaka mitano unaotekelezwa katika nchi 12 za Afrika ikiwemo Tanzania .“Imeonekana uvuvi ni suala la kiume zaidi kuliko wanawake lakini kwa utafiti tulioufanya tuliona asilimia 78 ya wachakataji ni wanawake na asilimia 99 ya wavuvi ni wanaume na kuna masuala ambayo yanawakwaza kina wanawake na wanaume wavuvi katika kujikwamua kiuchumi,” amesema Afisa huyo.Ameeleza kuwa utafiti huo utasaidia kubaini changamoto zinazokabili masuala ya Jinsia na fursa zake katka Ziwa Tanganyika ili kutoa mwamko kwa wanawake na watu wenye ulemavu kujihusisha na Uvuvi kuinua kipato chao.“Shirika la FAO limeanzisha dawati la jinsia katika Wizara ya Mifugo na Uvuvi ambalo linafanya kazi na sisi kama mradi wa FISH4ACP tunafanya kazi kwa karibu sana kuhakikisha sera, mikakati na sheria za Serikali zinatekelezwa,” amebainisha Hashim.
Hii leo jaridani tunaangazia wasichana waliotekwa nyara katika shule ya bweni huko Chibok Nigeria ambapo mpaka sasa 96 bado wapo utumwani, na matokeo ya mradi wa FISH4ACP nchini Tanzania. Makala tunakupeleka nchini Rwanda na Mashinani nchini Jamhuri ya Congo, Brazaville, kulikoni?Ikiwa ni miaka tisa imepita tangu wasichana 276 kutekwa nyara wakiwa katika shule ya bweni huko Chibok Nigeria ambapo mpaka sasa 96 bado wapo utumwani, Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF limetaka wadau kusaidia katika kuwekeza zaidi katika usalama wa wanafunzi mashuleni kwani bado vitendo vya utekaji vinaendelea nchini humo.Nchini Tanzania, shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo, FAO kupitia mradi wake FISH4ACP limepokea matokeo ya Utafiti kuhusu Usawa wa Kinjisia katika Masuala ya Uvuvi, moja ya hoja ambayo ikitekelezwa vema itasaidia kufanikisha malengo ya maendeleo endelevu, SDGs hasa la kutokomeza njaa na kuondokana na umaskini. Devotha Songorwa wa Redio washirika Kids Time FM nchini Tanzania ndio shuhuda wetu wa uzinduzi huo uliofanyika katika Mkoa wa Kigoma, Magharibi mwa Taifa hilo la Afrika Mashariki.Katika tunasalia hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa kusikiliza simulizi ya manusura wa mauaji ya kimbari dhidi ya watutsi nchini Rwanda mwaka 1994, ikiwa leo Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa lina kumbukizi maalum ya mauaji hayo.Na katika mashini tutaelekea katika mji mkuu wa Jamhuri ya Congo, Brazaville kusikia ushauri kutoka kwa mwanamke ambaye amekuwa akiishi na Virusi vya Ukimwi, VVU kwa miaka 24.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, Karibu!
Katika Jarida la Umoja wa Mataifa hii leo:Angola yatakiwa kubadili sheria ya kuengua watu wenye ulemavu katika kusimamia haki zao.TANBATT 6 wanaohudumu chini ya MINUSCA washiriki huduma ya kutoa matibabu na kukabidhi msaada wa dawa katika zahanati ya WAPO, Berberati, Mambéré-Kadéï.Mradi wa ufumbuzi wa tatizo la maji kwa kutumia teknolojia ya nishati ya jua wahakikisha upatikanaji wa maji safi na salama mkoani Kigoma, Magharibi mwa Tanzania.UNICEF yafadhili mafunzo ya kuwaelimisha walimu nchini Rwanda ili kuwashauri wanafunzi.
Vita ya Ukraine ikiwa inaingia mwaka wake wa pili, wawakilishi mbalimbali wa nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa wametoa maoni yao kufuatia uamuzi kwa njia ya kura uliofanywa na Kikao Maalumu cha dharura cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kupitisha azimio jipya la kutaka amani ya haki na ya kudumu nchini Ukraine na kwamba Urusi bila masharti yoyote iondoe mara moja majeshi yake katika ardhi ya Ukraine. Umaalumu wa kikao hiki cha siku mbili kilichokamilika jana jijini, New York, Marekani ni kwa mujibu wa azimio lilipotishwa mwaka 1950 na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kwamba Baraza hilo linaweza kushughulikia masuala ya kimataiafa yanayohusu amani na usalama pale ambapo Baraza la Usalama linakuwa limeshindwa kufanya hivyo. Kwa msingi huo kutokana na mara kwa mara Urusi kutumia kura ya turufu katika Baraza la Usalama kuzuia uamuzi wa kuibana, ndipo kikao hiki cha Baraza Kuu kikaitishwa kwa siku mbili Jumatano na Alhamis katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York Marekani ili nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa wapige kura kuiambia Urusi iondoke Ukraine.Awali kabla ya azimio kupigiwa kura, Vassily Nebenzia Waziri wa Mambo ya nje wa Urusi aliliambia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kuwa kufanya uamuzi kwa kuangalia tu yaliyotokea Februari 24 mwaka jana 2022 ni jaribio la makusudi la nchi za Magharibi kuficha sababu za kweli za mzozo huo. Hata hivyo matokeo ya kura yakaonesha kuwa walioinga mkono Urusi ni nchi 7 tu, 31 zikionesha kutokuwa upande wowote huku 141 zikiliunga mkono Azimio. Vita ikome, Urusi iondoke Ukraine.Kwa upande wake Waziri wa Mambo ya nje wa Ukraine, Dmytro Kuleba, mara tu baada ya kupitishwa kwa azimio… anasema “nchi yangu imeridhika na matokeo na ujumbe uko wazi; Haijalishi ni nini Urusi inajaribu na jinsi inavyojaribu kudhoofisha utaratibu wa kimataifa, inashindwa kila mara.” Naye Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa aliwasisitizia wajumbe akisema, “uchokozi ni kinyume cha sheria. Kumvamia jirani ni kinyume cha sheria. Kujimegea kipande cha nchi nyingine ni kinyume cha sheria.” Miongoni mwa nchi 32 ambazo zimepiga kura isiyoonesha kama zinaunga mkono azimio au la pamoja na Burundi, Msumbiji, Ethiopia, Congo, Zimbabwe, Afrika Kusini, China, India na Pakistan. Na zile ambazo zimeiunga mkono Urusi kwa kulipinga azimio hilo la kumaliza vita Ukraine ni Belarus, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Korea, Eritrea, Mali, Nicaragua, Urusi yenyewe na Syria.
Katika kuhakikisha wanawavutia wakimbizi wa ndani kurejea makwao, ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini UNMISS, umekarabati na kukabidhi jengo la mahakama pamoja na kujenga jengo jipya la jela huko jimboni Equatorial Magharibi katika kaunti ya Maridi.Nchini Sudan Kusini wananchi waliokuwa wakimbizi wa ndani na sasa wameanza kurejea katika vijiji vyao wanataka kurejea katika mazingira ambayo kuna utawala wa sheria.Sarah Barnet ni kiongozi wa wanawake wa kaunti ya Maridi iliyoko jimboni Equatorial Magharibi, “Tunahitaji kuona haki ikitendeka, hasa kwa wanawake. Kuna kesi nyingi za unyanyasaji wa kijinsia katika jamii yetu, na zinapaswa kushughulikiwa na mahakama. Haki zetu kama wanawake lazima ziheshimiwe.”Kwakutambua hili na kutekeleza jukumu lake la kuhakikisha wanalinda amani na kuimarisha mifumo ya haki nchini Sudan Kusini UNMISS wametekeleza mradi uliogharimu takriban dola 100,000 kwa kukarabati jengo la mahakama ya kaunti ya Maridi na kujenga jengo jipya la jela ili yaweze kutoa huduma ya kuhakikisha sheria zinafuatwa na wale wasiofuata sheria jela mpya iliyojengwa lipo kwa ajili yao.Ibrahim Tahiru ni afisa wa Ulinzi, Mpito na Uunganishaji wa UNMISS na anasema wanachukulia utekelezaji wa miradi hii ya kuleta mabadiliko haraka kuwa ni kichocheo muhimu cha kuwavutia watu wengi zaidi kuweza kurejea makwao kutoka ukimbizini, "Tunaamini kuwa tutaweza kukuza hali ya kudumu ya watu kurejea makwao na kuwaunganisha wakimbizi hawa wa ndani pamoja na waliokimbilia nje ya mipaka ya nchi. Tunataka waweze kujisikia kulindwa na kujua kwamba hawata pokonywa mali zao kiholela. Pia tunataka wajue watalipwa ikiwa, walipokuwa wakikimbia mzozo baadhi ya mali zao zilichukuliwa na watu wengine. Kwa hivyo, taratibu zote hizi kama ujenzi wa mahakama na jela zinategemeana. Tunaamini kuwa mfumo madhubuti wa haki utawasaidia sana watu wanaotafuta haki.”Ujumbe wa Umoja wa Mataifa ya kulinda amani nchini humo, UNMISS haujajitolea tu kuboresha uwezo wa mfumo wa haki nchini Sudan Kusini, bali pia kukuza heshima na kufuata matakwa ya haki za binadamu.Jamii ikiwa imewekewa mazingira bora ya kuwawajibisha wahalifu, ukiukaji wa haki za binadamu unatarajiwa kupungua.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema dunia haiwezi kutatua changamoto kubwa inazokabiliwa nazo hivi sasa kuanzia mabadiliko ya tabianchi, vita ya Ukraine, mdororo wa uchumi na athari zinazoendelea za janga la COVID-19 katikia hali ya sasa ya mgawanyiko na kutokuwa na mshikamano hivyo wakati wa kufumbia macho changamoto hizi umepita na wanaochangia wawajibishwe.Katibu Mkuu Guterres ameyasema hayo mjini Davos Uswis katika hotuba yake kuhusu hali ya dunia kwenye siku ya pili ya jukwaa la uchumi duniani akibainisha kwamba wakati dunia inahitaji ushirikiano zaidi katika masuala ya mabadiliko ya tabianchi , upunguzaji wa mzigo wa madeni na afya uya kimataifa kuna mgawanyiko na changamoto inaongezeka linapokuja suala ya vita ya Ukraine akisema "Hasa uvamizi wa Urusi kwa Ukraine sio tu kwa sababu ya mateso yasiyoelezeka kwa watu wa Ukraine, lakini kwa sababu ya athari zake kubwa za kimataifa kwa bei ya chakula na nishati, kwenye minyororo ya biashara na usambazaji na maswala ya usalama wa nyuklia, kwa misingi hiyo hiyo ya sheria za kimataifa”. Akisisitioza kuhusu suala la mabadiliko ya tabianchi amelaani makampuni makubwa ya mafuta kwa kupuuza sayansi kuhusu mabadiliko ya tabianchi, na kushutumu sekta ya mafuta na gesi kwa kutafuta kupanua zaidi wigo wa uzalishaji licha ya kujua kwamba kwamba mtindo wao wa biashara hauendani na maisha ya binadamu. Amesema"Baadhi ya makampuni makubwa ya mafuta wanadanganya kwa kiasi kikubwa na kama vile ilivyo kwa sekta ya tumbaku, wale wanaohusika kuchochea mabadiliko ya tabianchi lazima wawajibishwe." Pia amezungumzia migawanyiko ikiwemo baina ya Mashariki na Magharibi hasa Marekani na Uchina hususan katika suala la haki za binadamu na usalama wa kikanda na Kaskazini na Kusini ambao amesema hashawishiki kwamba Kaskazini inatambua kiwango cha madhila yanayowakabili watu wa Kusini hasa linapokuja suala la afya kuhusu usawa wa usambazaji wa chanjo. Amehitimisha hotuba yake kwa kutoa wito kwa serikali zote, sekta binafsi na wadau wote kuunda njia za ushirikiano zaidi, ikisisitiza haja ya kuziba pengo la migawanyiko yote kwa kurekebisha na kujenga usawa katika mfumo wa fedha wa kimataifa, Kuchukua hatua za maana dhidi ya mabadiliko ya tabianchi, Kurekebisha muundo wa biashara na mazoea ili kuendeleza malengo ya maendeleo endelevu, kuongoza njia ya kufikia fursa za kiuchumi kwa wanawake, na kufikia lengo la uhakika wa chakula duniani . Hivyo amesisitiza kwamba “Sasakuliko wakati mwingine wowote, ni wakati wa kutengeneza njia za ushirikiano katika dunia yetu lililogawanyika kwani dunia haiwezi kusubiri."
Takriban asilimia 60 ya nchi za kipato cha chini barani Afrika hivi sasa ziko kwenye mzigo wa madeni, shinikizo kubwa au katika hatari ya kuingia kwenye madeni huku mamilioni ya Waafrika wakitumbukia tena kwenye umasikini wakati huu wakiwa kwenye hatari kubwa ya kutokuwa na uhakika wa chakula, imeonya ripoti mpya ya biashara na maendeleo kwa mwaka 2022 iliyotolewa leo na kamati ya Umoja wa Mataifa ya biashara na maendeleo UNCTAD. Flora Nducha na taarifa kamili Kwa mujibu wa ripoti hiyo iliyotolewa mjini Geneva Uswis kiwango cha ukuaji uchumi cha Afrika kimeshuka na mwaka huu wa 2022 kinatarajiwa kukua kwa asilimia 2.7 huku 2023 kikikuwa wa asilimia 2.4 ukiulinganisha na ukuaji wa asilimia 5.1 uliokuwa mwaka 2021. Na matokeo yake watu wengine milioni 58 barani Afrika watalazimia kutumbukia kwenye umasikini uliokithiri mwaka huu na kujiunga na wengine milioni 55 ambao tayari wako kwenye ufukara. Katibu Mkuu wa UNCTAD Rebeca Grynspan amesema”Kuzorota huku kwa uchumi kunasababisha mkwamo wa kufikia agenda ya 2030 ya maendeleo endelevu. Na madeni yanazikabili sekta zote Afrika kuanzia za umma na sekta binafsi.” Mbali ya mzigo wa madeni ripoti hiyo ya UNCTAD inasema zaidi ya asilimia 60 ya nchi za Afrika zinahitaji msaada wa chakula kutoka nje wakati huu njaa ikisambaa haraka kwenye bara hilo. Imeongeza kuwa kudorora huko kwa uchumi kunaleta changamoto zingine lukuki ikiwemo ongezeko kubwa la bei za mafuta na chakula, shinikizo katika sera za fedha kwa nchi zilizoendelea na hatari kubwa ya kutokuwa na uhakika wa chakula katika maeneo mengi ya kanda hiyo. Katika nchi tatu za Africa ambazo uchumi wake ndio unashikilia asilimia 60 ya pato la bara hilo Nigeria, Misri na Afrika Kusini ripoti inasema ukuaji wa uchumi umeshuka ikilinganishwa na mwaka 2021. Kwingineko kwa mujibu wa ripoti " Shirika la fedha duniani IMF na Benki ya Dunia wameingilia kati kwa programu maalum kuzisaidia nchi 16 za kipato cha chini Afrika zilizo na mzigo mkubwa wa madeni na zilizo katika hatari ya mzigo huo ili kupunguza mzingo huo zikiwemo Zambia, Ghana na Tunisia. " Wakati huohuo shirika la chakula na kilimo la Umoja wa Mataifa FAO limekadiria kuwa nchini 33 za Afrika zinahitaji msaada wa chakula toka nje wakati hali ya kutokuwa na uhakika wa chakula ikitarajiwa kuwa mbaya zaidi katika miezi 18 ijayo katika nchi hizo. “Kupanda kwa bei ya mbolea kwa sababu ya vita inayoendelea Ukraine kunatishia kupunguza uzalishakji wa chakula na kuongeza mgogoro wa chakula duniani huku wakulima wadogo wakiwa ndio waathirika zaidi. Hali ni mbaya zaidi hususan Mashariki na Magharibi mwa Afrika kutokana na uzalishaji mdogo wa kilimo , ukame, na migogoro”. Amesema Rebeca Grynspan.
Katika Jarida la habari la Umoja wa Mataifa leo Ijumaa Flora Nducha anakuletea -Katika siku ya kimataifa ya kulinda shule dhidi ya mashambulizi mashirika ya Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF na la elimu sayansi na utamaduni UNESCO yanasema Afrika ya Kati na Magharibi ni nyumbani kwa karibu robo ya watoto wote duniani wasiokwenda shule -Taasisi ya Molteno ya lugha, kusoma na Kuandika kutoka nchini Afrika Kusini imetunukiwa tuzo ya kujua kusoma na kuandika ya mwaka 2022 ijulikanayo kama confucius ambayo hutolewa na shirika la elimu sayansi na utamaduni la Umoja wa Mataifa UNESCO. -Makala yetu leo inatupeleka kuangazia wahamiaji na changamoto wanazopitia kwenda kusala hifazi hasa raia wa Venezuela wanapoikimbia nchi yao kuingia Chile -Mashinani inaturejesha Makao Makuu ya Un kwenye mkutano wa waathirika wa ugaidi na mmoja wao anakumbuka siku ambayo hatoisahau maishani shambulio la ugaidi lilipobisha hodi kwenye sherehe ya harusi yake
Jamii zawatu wenye tamaduni mbali mbali wanao ishi Magharibi Australia, wamepata sehemu mpya yakupokelea huduma, kuchangia taarifa nakuendesha shughuli zao.
Kutokana na athari za mabadiliko ya tabianchi kuleta ukame katika maeneo mbalimbali ya dunia, kusababisha kupungua kwa mvua za masika, baadhi ya wakulima wa wilaya ya Uyui mkoani Tabora, nchini Tanzania wanasema hawajasazwa katika kukumbana na athari za mabadiliko hayo kwani hata mvua za masika walizokuwa wanazitegemea kukuzia mazao yao, zimekuwa za kusuasua. Kwa sababu hiyo wameamua kujikita katika kilimo cha muda mfupi katika bustani ndogondogo ili waweaze kujikumu kimaisha lakini bado wanakumbana na changamoto nyingine ikiwemo kukosa mbegu na pembejeo, na kulazimika kutumia sumu nyingi ambazo ni hatari kwa mazingira na afya. Hamad Rashid wa Redio washirika Tanzania kidstime fm kutoka Mkoa wa Morogoro amesafiri hadi Magharibi mwa Tanzania Kata ya Ibelamilundi Wilaya ya Uyui Mkoa wa Tabora na kuzungumza na wakulima.
Kutokana na athari za mabadiliko ya tabianchi kusababisha ukame katika maeneo mbalimbali ya dunia, kusababisha kupungua kwa mvua za masika, baadhi ya wakulima wa wilaya ya Uyui mkoani Tabora, nchini Tanzania wanasema hawajasazwa katika kukumbana na athari za mabadiliko hayo kwani hata mvua za masika walizokuwa wanazitegemea kukuzia mazao yao, zimekuwa za kusuasua. Kwa sababu hiyo wameamua kujikita katika kilimo cha muda mfupi katika bustani ndogondogo ili waweze kujikumu kimaisha lakini bado wanakumbana na changamoto nyingine ikiwemo kukosa mbegu na pembejeo, na kulazimika kutumia sumu nyingi ambazo ni hatari kwa mazingira na afya. Hamad Rashid wa Redio washirika Tanzania kidstime fm kutoka Mkoa wa Morogoro amesafiri hadi Magharibi mwa Tanzania Kata ya Ibelamilundi Wilaya ya Uyui Mkoa wa Tabora na kuzungumza na wakulima.