Podcasts about marekani

  • 32PODCASTS
  • 922EPISODES
  • 16mAVG DURATION
  • 5WEEKLY NEW EPISODES
  • Jul 18, 2026LATEST

POPULARITY

20192020202120222023202420252026


Best podcasts about marekani

Latest podcast episodes about marekani

Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii
Matokeo ya uchaguzi mdogo Ol Kalou Kenya; rais wa DRC aitisha mazungumzo jumuishi

Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii

Play Episode Listen Later Jul 18, 2026 20:13


Miongoni mwa yaliyojiri wiki hii ni wapiga kura na wanahabari walivyoshambuliwa wakati wa  uchaguzi mdogo Ol Kalau na kuzua hofu kuhusu uchaguzi wa 2027 nchini Kenya: wanafunzi wasiopungua 20 kupoteza maisha katika ajali ya barabarani kule Uganda, shambulio la waasi wa ADF huko Mangina mashariki mwa DRC, usalama kuzorota huko Sudan, ziara ya waziri mkuu wa Ufaransa Sebastien Lecornu kule Morocco, Trump aishutumu China kwa kuingilia uchaguzi wa Marekani, na mengine zaidi.-

Habari za UN
16 JULAI 2026

Habari za UN

Play Episode Listen Later Jul 16, 2026 9:56


Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka Ukanda wa Gaza ambako sitisho la mapigano kati ya Israeli na Palestina lililotiwa Saini tarehe 10 mwezi Oktoba mwaka jana wa 2025 limewezesha wakulima wa eneo hilo kurejea mashambani. Pia tunakuletea Muhtasariw a habari.Mashirika mawili ya Umoja Umoja wa Mataifa lile la Uhamiaji, IOM na la Kuhudumia Wakimbizi, UNHCR kupitia taarifa waliyoitoa kwa pamoja jijini Gneva Uswusi na BangKok Thailand, wameeleza wasiwasi mkubwa kufuatia taarifa kwamba boti mbili zilizokuwa zimebeba zaidi ya watu 500 huenda zimezama katika pwani ya Myanmar katika siku za hivi karibuni. Kwa mujibu wa taarifa za awali, boti hizo mbili ziliondoka mwishoni mwa mwezi Juni kutoka Jimbo la Rakhine nchini Myanmar zikiwa zimewabeba zaidi ya abiria wa jamii ya Rohingya, wakiwemo baadhi waliokuwa wametoka katika kambi za wakimbizi za Cox's Bazar nchini Bangladesh.Zaidi ya watoto milioni 23 wengine zaidi ya wale ambao wako tayari kwenye umaskini duniani wanaweza kutumbukia katika umaskini wa kipato ifikapo mwisho wa mwaka huu wa 2025 kutokana na kuendelea kwa mzozo wa Mashariki ya Kati na athari zake kwa biashara ya kimataifa, kwa mujibu wa ripoti mpya iliyotolewa leo na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) jijini New York, Marekani.Na Uganda leo imeanza rasmi kuhesabu siku 42 kuelekea kutangazwa kumalizika kwa mlipuko wa ugonjwa wa Ebola baada ya mgonjwa wa mwisho aliyethibitishwa kuwa na maambukizi kupimwa mara ya pili na kubainika hana virusi hivyo, kisha kuruhusiwa kutoka hospitalini. Hatua hiyo ni mafanikio muhimu katika juhudi za nchi hiyo kudhibiti mlipuko, imesema taarifa iliyotolewa leo na Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Ulimwenguni, WHO ofisi ya Uganda.Mwenyeji wako ni Feissal, karibu!

Habari RFI-Ki
Argentina kuvaana na Uhuspania kwenye fainali

Habari RFI-Ki

Play Episode Listen Later Jul 16, 2026 9:50


Fainali ya kombe la dunia katika mchezo wa soka, itawakutanisha mabingwa watetezi Argentina na Hispania waliowahi kushinda taji hili mwaka 2010. Mechi hiyo itapigwa siku ya Jumapili nchini Marekani. Unatarajia nani ataibuka mshindi katika mechi hiyo na kwanini. Skiza ya mskilizaji

argentina hispania mechi kwenye marekani jumapili
Habari RFI-Ki
Argentina kuvaana na Uhuspania kwenye fainali

Habari RFI-Ki

Play Episode Listen Later Jul 16, 2026 9:50


Fainali ya kombe la dunia katika mchezo wa soka, itawakutanisha mabingwa watetezi Argentina na Hispania waliowahi kushinda taji hili mwaka 2010. Mechi hiyo itapigwa siku ya Jumapili nchini Marekani. Unatarajia nani ataibuka mshindi katika mechi hiyo na kwanini. Skiza ya mskilizaji

argentina hispania mechi kwenye marekani jumapili
Wimbi la Siasa
Kwanini vita vya Marekani na Iran vimeanza tena ?

Wimbi la Siasa

Play Episode Listen Later Jul 15, 2026 10:06


Marekani na Iran zimeanza tena kushambuliana, na kuzua wasiwasi wa kuendelea kwa vita vilivyoanza mwezi Februari 2026. Mashambulizi haya yamelenga kudhibiti eneo la Bahari ya Hormuz, njia muhimu inayotumiwa na meli zinazosafirisha mafuta na gesi kuelekea katika maeneo mbalimbali ya dunia. Kwanini Marekani na Iran zimeanza tena kushamuliana na hii inamanisha nini ?

Habari za UN
14 JULAI 2026

Habari za UN

Play Episode Listen Later Jul 14, 2026 9:58


Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka katika mkutano wa HLPF hapa makao makuu ya UN kumsikia Profesa Peter Wanderi Mwangi ambaye amewakiwakilisha Chuo Kikuu cha Mount Kenya cha nchini Kenya chenye matawi mbalimbali katika Afrika Mashariki katika mkutano wa United Nations Academic Impact (UNAI), Mpango unaosisitiza nafasi muhimu ya taasisi za elimu ya juu katika kuhimiza maendeleo endelevu na kuunga mkono utekelezaji wake. Baada ya ziara yake mjini Bunia, jimboni Ituri nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC ambako ndio kitovu cha mlipuko wa sasa wa Ebola ya virusi vya Bundibugyo, Mkurugenzi Mtendaji wa WHO anayehusika na Programu ya Dharura za Afya, Dkt. Chikwe Ihekweazu, amewambia waandishi wa habari Geneva, Uswisi kwamba mlipuko wa sasa ni moto ambao kinachouchochea kiko katikati, huku ukiendelea kusambaa.Shirika la Umoja wa Mataifa la Masuala ya Bahari (IMO) limesema lina wasiwasi mkubwa kufuatia mashambulizi ya jana usiku yaliyolenga meli kwenye mlango wa bahari wa Hormuz na viunga vyake na kusababisha vifo vya takribani mabaharia wawili na wengine kadhaa wamejeruhiwa. Kupitia taarifa yake iliyotolewa London, Uingereza, IMO imesema inafanya kazi kwa haraka na mamlaka husika ili kubaini mazingira halisi ya tukio hilo.Na uungwaji mkono wa umma kwa wakimbizi unaendelea kuwa imara licha ya kuwepo kwa changamoto na kutokuweko kwa uhakika wa mustakabali duniani, hii ni kwa mujibu wa utafiti wa pamoja uliofanywa na kampuni ya IPSOS na shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi, UNHCR, Utafiti umebaini kuwa asilimia 66 ya washiriki katika nchi 29 wanakubaliana kwamba watu wanaokimbia vita au mateso wanapaswa kuruhusiwa kusaka hifadhi katika nchi nyingine, ikiwa ni punguzo la asilimia moja tu ikilinganishwa na mwaka 2025.Utafiti huu umefanywa ikiwa ni miaka 75 tangu kupitishwa kwa Mkatab awa Kimataifa wa kulinda wakimbizi.Mwenyeji wako ni Feissal Kirwa, karibu!

iran kenya congo ebola hormuz imo sdgs drc ipsos unhcr unai umoja programu hii ituri afya mount kenya julai baada dkt bunia mataifa jamhuri marekani shirika kimataifa afrika mashariki uingereza kidemokrasia chuo kikuu
SBS Swahili - SBS Swahili
Makala Leo:Mashambulizi mapya yashuhudiwa Iran na Marekani zikibishana kuhusu kufunguliwa kwa Hormuz

SBS Swahili - SBS Swahili

Play Episode Listen Later Jul 14, 2026 10:22


Marekani na Iran zimebadilishana wimbi jingine la mashambulizi, huku mapigano yakiongezeka kuhusu Mlango-Bahari wa Hormuz yakisukuma makubaliano ya kidiplomasia ya mwezi uliopita karibu kuvunjika.

Habari za UN
13 JULAI 2026

Habari za UN

Play Episode Listen Later Jul 13, 2026 9:59


Hii leo jaridani tunaangazia malengo ya maendeleo endelevu, uhuru wa usafiri katika maji, na shughuli za Redio Miraya za kutumia redio kujenga amani na kutoa tahadhari za mapema za hali ya hewa nchini Sudan Kusini. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres, ameonya kwamba dunia ipo nyuma katika kutekeleza ahadi zake kuhusu upatikanaji wa maji safi na salama na huduma za kujisafi. Hivyo basi amezitaka serikali, sekta binafsi na jamii kuchukua hatua za haraka kukabiliana na uhaba unaoongezeka wa maji, uchafuzi wa mazingira na shinikizo linalotokana na mabadiliko ya tabianchi.Taarifa iliyotolewa leo na Shirika la Umoja wa Mataifa la Usafiri wa Baharini (IMO) imeeleza kuwa Baraza la shirika hilo lililohitimisha kikao chake cha 137 linasisitiza tena umuhimu wa kulinda haki na uhuru wa usafiri katika maji kwa mujibu wa sheria za kimataifa. Nchini Sudan Kusini, Redio ndiyo chanzo kikuu cha taarifa kwa takribani asilimia 60 ya wananchi wa nchi hiyo changa zaidi barani Afrika. Ndiyo maana kuendelea kwa matangazo ya Radio Miraya ambayo yamedumu kwa miaka ishiriki katika redio hii inayomilikiwa na UNMISS yaani Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa Kulinda Amani Sudan Kusini ni kipaumbele cha juu katika juhudi zake za kuzuia migogoro na kujenga amani.Mwenyeji wako ni Feissal Kirwa, karibu!

iran ant afrika hormuz sdgs guterres umoja hii julai baraza mataifa unmiss marekani shirika redio ujumbe sudan kusini
Habari za UN
IMO yatetea uhuru wa usafiri wa majini, sheria za kimataifa na usalama wa mabaharia

Habari za UN

Play Episode Listen Later Jul 13, 2026 2:33


Taarifa iliyotolewa leo na Shirika la Umoja wa Mataifa la Usafiri wa Baharini (IMO) imeeleza kuwa Baraza la shirika hilo lililohitimisha kikao chake cha 137 linasisitiza tena umuhimu wa kulinda haki na uhuru wa usafiri katika maji kwa mujibu wa sheria za kimataifa. Anold Kayanda ameifuatilia taarifa hiyo. 

iran hormuz umoja uhuru sheria baraza mataifa marekani shirika kimataifa
Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii
Makubaliano kati ya Marekani na Iran kuvunjika, maandamano ya mawakili wa Kenya

Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii

Play Episode Listen Later Jul 11, 2026 20:11


Yaliyojiri wiki hii ni kuvunjika kwa makubaliano kati ya Marekani na Iran, mazishi ya kiongozi wa kiroho wa Iran A.Khamenei, rais wa Tanzania Samia Suluhu kuwaonya wanaharakati dhidi ya kuchochea vurugu-wanasiasa wa upinzani, wanahabari pamoja na wanaharakati, Uganda waishi kwa hofu kutokana na vitisho vya mkuu wa majeshi, wapinzani wa jukwaa la C64 DRC walikutana na rais wa Burundi Evariste Ndayishimiye, na maandamano ya mawakili nchini Kenya

Habari za UN
10 JULAI 2026

Habari za UN

Play Episode Listen Later Jul 10, 2026 9:58


Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina na leo tunakwenda Afrika Mashariki hususan nchini Tanzania katika visiwa vya Zanzibar. Tunamulika jinsi serikali ya Zanzibar kwa ushirikiano na shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo nchini humo, UNDP wanaboresha huduma za utalii kwa kutumia Akili Mnemba au AI. Ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa imeonya kuwa kupunguzwa kwa misaada rasmi ya maendeleo tangu Januari 2025 kumesababisha takribani wanawake na wasichana milioni moja duniani kupoteza huduma muhimu katika nchi zilizoathiriwa na migogoro. Ikitolewa leo Geneva, Uswisi na New York, Marekani na shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia masuala ya wanawake, UN Women, ripoti hiyo iliyopatiwa jina ‘Zaidi ya Kiwango cha Kuvumilika' miongoni mwa changamoto ilizozitaja ni pamoja na kuwa asilimia 84 ya mashirika ya wanawake yameripoti kuongezeka kwa mahitaji ya huduma, lakini takribani asilimia 90 ya mahitaji hayawezi tena kuyakidhi na kwamba mashirika mawili kati ya matano yanatarajia kufungwa ndani ya mwaka mmoja kutokana na ukosefu wa fedha.Huko Sudan, nchi inayoumia kwa vita kwa miaka minne sasa, kumetangazwa mlipuko mpya wa ugonjwa wa kipindupindu hali inayozidisha wasiwasi kuhusu usalama wa jamii zilizo hatarini, hususan katika mji wa El-Obeid uliozingirwa, ambako mashambulizi ya kila siku ya ndege zisizo na rubani yanaendelea kuzuia upatikanaji wa misaada ya kibinadamu. Dkt. Shible Sahbani, Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani (WHO) nchini Sudan akizungumza kwa njia ya video na waandishi wa habari leo mjini Geneva, uswisi amesema, “tumerekodi zaidi ya wagonjwa 1,330 wa kipindupindu, huku watu 114 wakifariki dunia kutokana na ugonjwa huo. Hii inaonesha kiwango cha vifo miongoni mwa wagonjwa wa kipindupindu cha asilimia 13.7, ambacho ni cha juu sana. Na bila shaka, msimu wa mvua unaotarajiwa utaifanya hali kuwa mbaya zaidi.”Na utafiti wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni, UNESCO kuhusu Ufuatiliaji wa Elimu Duniani, umeonesha kuwa misaada ya kimataifa kwa sekta ya elimu imeendelea kupungua na nchi 113 duniani zinatumia fedha nyingi kulipa madeni kuliko pesa wanazoziwekeza kwenye elimu. Matokeo ya utafiti huo yamewekwa wazi leo mbele ya viongozi kutoka nchi mbalimbali wanaohudhuria Mkutano wa Mageuzi ya Elimu TES+4 unaofanyika Paris, Ufaransa ili kufuatilia utekelezaji wa maazimio ya mkutano wa kwanza wa Mageuzi ya Elimu uliofanyika mwaka 2022 na pia ili kusongesha zaidi ufikiaji wa Lengo namba 4 la Maendeleo Endelevu linalohusu Elimu Bora.Mwenyeji wako ni Feissal Kirwa, karibu!

new york ai tanzania sudan unesco zanzibar un women undp zaidi umoja hii afya julai wanawake elimu dkt mataifa maendeleo marekani lengo shirika ufaransa mkutano afrika mashariki ripoti
Habari za UN
08 JULAI 2026

Habari za UN

Play Episode Listen Later Jul 8, 2026 9:58


Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina. Kesho, Julai 9, ni miaka 15 tangu Sudan Kusini ipate uhuru wake kutoka Sudan. Hata hivyo, matumaini ya amani yalitikiswa miaka miwili baadaye, mwezi Desemba 2013, baada ya kuzuka kwa mapigano kati ya serikali na makundi pinzani, hali iliyoendelea kuwaathiri mamilioni ya wananchi hadi leo. Katika juhudi za kurejesha amani, Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo, UNMISS, kwa ushirikiano na serikali ya jimbo la Equatoria Magharibi, umezindua kampeni mpya iitwayo "Tusikilizeni, Chukueni Hatua Sasa" (Hear Us, Act Now), inayolenga kuimarisha maridhiano, mshikamano wa kijamii na kuwahamasisha vijana kushiriki kikamilifu katika ujenzi wa amani. Feissal Kirwa, kupitia video ya UNMISS, amefuatilia uzinduzi wa kampeni hiyo na sasa anatuletea mada hii kwa kina.Pia tunakuletea muhtasari wa habari na jifunze Kiswahili..Ripoti mpya ya hali ya saratani duniani kwa mwaka huu wa 2026 iliyotolewa leo na shirika la Umoja wa Mataifa la Afya duniani (WHO) na shirika lake tanzu la utafiti wa saratani, IARC ikionya kuwa unyanyapaa ni moja ya vikwazo vya kutokomeza saratani wakati huu idadi ya wagonjwa ikikadiriwa kuongezeka maradufu ifikapo 2050, manusura wa saratani ya titi Abigael Hartz mkazi wa Ireland lakini anatokea Nigeria anasimulia alichoshuhudia alipotembelea hospitali moja ya kupima saratani Nigeria.Wiki mbili tangu matetemeko makubwa ya ardhi yapige mji mkuu wa Venezuela, Caracas na viunga vyake, idadi ya waliokufa imeripotiwa kufikia 3,685, majeruhi 16,740 na waliookolewa 6,462, Mkuu wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Msaada wa Dharura, OCHA, Tom Fletcher yuko nchini humo na anasema.. “Hapa ni La Guaira, ambalo kwa hakika ndilo eneo lililokumbwa zaidi na janga hili. Nimekutana na mama mmoja aliyepoteza watoto wake watano waliokuwa kwenye jengo lililo kule. Bado anasubiri kwa matumaini, ingawa matumaini hayo yanazidi kufifia, kwamba huenda watoto wake bado wakapatikana wakiwa hai. Kwa hiyo, tupo hapa katikati ya vifusi na harufu ya miili ya waliopoteza maisha, tukijitahidi kuwafikishia manusura chakula, maji na huduma za matibabu, huku tukiwasaidia kuanza kufikiria namna ya kujenga upya maisha yao. Lakini safari ya kurejea katika hali ya kawaida bado ni ndefu sana.”wakati huu ambapo ripoti za vyombo vya Habari zinaeleza kuwa jeshi la Marekani usiku wa kuamkia leo limekamilisha awamu mpya ya mashambulizi dhidi ya Iran, yakilenga zaidi ya maeneo 80 zikiwemo meli tatu za kibiashara zilizokuwa zinapita Mlango wa Bahari wa Hormuz huko Ghuba ya Uajemi, Katibu Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Masuala ya Bahari, IMO Arsenio Dominguez amelaani mashambulizi hayo mapya akionya kuwa kwa mara nyingine maisha ya mabaharia wasio na hatia yanawekwa hatarini.Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili hii leo mtaalam wetu Onni Sigalla, Mhariri mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania, BAKITA. Anafafanua maana za neno "KICHAKATA MATINI".Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!

Habari za UN
07 JULAI 2026

Habari za UN

Play Episode Listen Later Jul 7, 2026 9:59


Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina leo ikiwa ni siku ya kimataifa ya lugha ya Kiswahili nampisha John Kibego wa redio washirika, Kazi Njema Redio nchini Uganda, kukueleza  kuhusu harakati za kukuza lugha hiyo  barani Afrika wakati huu ambapo UNESCO imeshaitangaza miaka mitano iliyopita kuwa lugha ya kimataifa.John, anamulika mpango wa ujenzi wa makao makuu ya kamisheni ya Kiswhaili ya Mungano wa Afrika. Pia tunakuletea muhtasari wa habari.Ikiwa leo ni  maadhimisho ya tano ya Siku ya Kimataifa ya Lugha ya Kiswahili chini ya Kaulimbiu "Kiswahili kwa Amani, Mshikamano na Diplomasia ya Uchumi wa Dunia" Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Togolani Mavura anafafanua ni kwa namna gani lugha ya Kiswahili inaweza kuyafanikisha hayo.Ugonjwa wa Ebola umeendelea kusambaa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC na idadi ya vifo vya watu imevuka 500 limesema leo Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani, WHO. Mwakilishi wa WHO nchini humo, Dkt. Anne Ancia akizungumza kwa njia ya video kutoka Bunia, mji mkuu wa Jimbo la Ituri mashariki mwa DRC ambako ni kitovu cha mlipuko huu, amewaambia waandishi wa habari mjini Geneva, Uswisi kwamba kufikia tarehe 4 mwezi huu, serikali ya nchi hiyo ilikuwa imerekodi wagonjwa 1,561, vikiwemo vifo 506. Taarifa njema ni kuwa…“Jaribio la kitabibu lilianza tarehe 2 Julai kwa lengo la kubaini tiba madhubuti dhidi ya ugonjwa huo unaosababishwa na virusi vya Bundibugyo.”Na asubuhi hii kwa saa za New York Marekani, kwa mara ya 34 tangu mwaka 1992, Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa limekaa ili kujadili umuhimu wa kumaliza vikwazo vya kiuchumi na kibiashara vilivyowekwa na Marekani dhidi ya Cuba tangu mwaka 1960. Katika barua ya mwaliko ambayo Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Annalena Baerbock amewapelekea wajumbe wa Baraza anasema, “ninayo heshima kukujulisha kwamba nimepokea barua iliyoambatanishwa ya tarehe 16 Juni 2026 kutoka kwa Mhe. Bwana Ernesto Soberón Guzmán, Mwakilishi wa Kudumu wa Cuba katika Umoja wa Mataifa, akiomba kuitishwa kwa kikao cha Baraza Kuu ili kujadili ajenda namba 38 yenye kichwa: “Umuhimu wa kukomeshwa kwa vikwazo vya kiuchumi, kibiashara na kifedha vilivyowekwa na Marekani dhidi ya Cuba.”Mwenyeji wako ni Feissal Kirwa, karibu!

SBS Swahili - SBS Swahili
Uhispania na Ubelgiji za tinga robo fainali wakati Ronaldo aaga Kombe la Dunia

SBS Swahili - SBS Swahili

Play Episode Listen Later Jul 7, 2026 4:51


Uhispania na Ubelgiji zimefuzu kwa robo fainali, wakati ndoto za Kombe la Dunia za wenyeji Marekani na Ureno ya Cristiano Ronaldo ziki gonga miamba.

Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii
DRC yasherehekea miaka 66 ya uhuru, amnesty yalaani vita Sudan, mazishi ya Khamenei huko Iran

Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii

Play Episode Listen Later Jul 4, 2026 20:12


Makala imeangazia maadhimisho ya miaka 66 ya uhuru wa jamahuri ya kidemokrasia ya Congo, kuanzishwa kwa majaribio ya dawa zizonaweza kuwa tiba ya Ebola aina ya Bundibugyo huko DRC, kufungwa kwa kituo cha televisheni cha NTV na Gazeti la Daily Moniter nchini Uganda, shirika la Amnesty International, layatuhumu mataifa ya nje  kwa kuendelea kuchochea mzozo wa Sudan. Polisi nchini Afrika Kusini wazuia maandamano ya ghasia, utawala wa Tehran wakanusha kuomba mazungumzo na Marekani

Habari RFI-Ki
Timu ya DRC ya Leopard yaondolewa na Uingereza kwenye mashindano ya kombe la dunia

Habari RFI-Ki

Play Episode Listen Later Jul 3, 2026 10:04


leopards dunia drc timu kwenye marekani kombe uingereza
Habari RFI-Ki
Timu ya DRC ya Leopard yaondolewa na Uingereza kwenye mashindano ya kombe la dunia

Habari RFI-Ki

Play Episode Listen Later Jul 3, 2026 10:04


leopards dunia drc timu kwenye marekani kombe uingereza
Habari za UN
30 JUNI 2026

Habari za UN

Play Episode Listen Later Jun 30, 2026 9:59


Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayoangazia sekta ya ufugaji wa samaki na viumbe vingine na mimea baharini na kwenye maziwa, sekta ambayo inaendelea kushuhudia ukuaji mkubwa duniani, huku uzalishaji wa samaki ukifikia kiwango cha juu zaidi kuwahi kurekodiwa.Shughuli za uokoaji zinaendelea nchini Venezuela kufuatia athari za matetemeko makubwa ya ardhi yaliyoua maelfu ya watu na kuwaacha maelfu wengine bila makazi. Mashirika ya Umoja wa Mataifa yalipozungumza na waandishi wa habari leo jijini Geneva, Uswisi yametahadharisha kuwa uhaba wa huduma za afya, chakula na makazi unaongeza hatari ya milipuko ya magonjwa. Msemaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani, WHO, Christian Lindmeier amesisitiza wawasi huo akisema “Huduma za afya ziko chini ya shinikizo kubwa sana kwa sasa.”Tathmini mpya ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo, UNDP imeonya kuwa mlipuko wa Ebola katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC unaweza kuwasukuma karibu watu milioni moja zaidi kuingia kwenye umaskini, huku wanawake wakitarajiwa kuathirika zaidi kiuchumi na kiafya. Ripoti hiyo iliyotolewa leo New York Marekani na Kinshasa, DRC pia inaeleza kuwa mlipuko huu wa sasa unaweza kugharimu uchumi wa Afrika hadi dola bilioni 3.6 za Marekani iwapo athari zake zitaenea zaidi.Na, Kuelekea Mdahalo wa kwanza wa Kimataifa Kuhusu Usimamizi wa Akili Mnemba, AI utakaofanyika wiki ijayo jijini Geneva, Uswisi, Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto, UNICEF limezitaka serikali na wadau kuhakikisha haki za watoto zinazingatiwa katika usimamizi wa matumizi ya akili mnemba (AI). Shirika hilo linataka sheria madhubuti za kuzuia unyanyasaji wa watoto unaowezeshwa na AI, mifumo ya AI iliyo salama na yenye uwazi, pamoja na uwekezaji katika utafiti, elimu ya matumizi ya AI.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!

ai venezuela congo afrika ebola unicef drc kinshasa undp umoja hii watoto mataifa jamhuri maendeleo marekani shirika ripoti kidemokrasia mashirika
Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii
Maandamano ya Gen Z Kenya, ziara ya rais Ndayishimiye DRC,vifo Venezuela vyafikia920

Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii

Play Episode Listen Later Jun 27, 2026 20:11


Maandamno ya vijana wa Gen Z kuwakumbuka wenzao waliouawa katika maandamano ya mwaka wa 2024 nchini Kenya, kesi ya aliyekuwa meya wa jiji la Kampala Uganda Erias Lukwago, ziara ya rais wa Burundi pia mwenyekiti wa Umoja wa Afrika, jijini Kinshasa DRC, Evariste Ndayishimiye, yaliyojiri huko Sudan, Nigeria, Tunisia lakini pia mitetemeko miwili ya ardhi huko Venezuela iliyouwa watu zaidi ya 900, na pia kinachoendelea katika mlango bahari wa Hormuz kuhusu mkataba kati ya Irani na Marekani

Habari za UN
IMO yatangaza mpango wa kuwaondoa mabaharia waliokwama Hormuz

Habari za UN

Play Episode Listen Later Jun 24, 2026 3:08


Shirika la Umoja wa Mataifa la Usafiri wa Baharini (IMO) limetangaza mpango wa kuwaondoa zaidi ya mabaharia 11,000 waliokwama katika Mlango Bahari wa Hormuz kufuatia makubaliano ya amani kati ya Iran na Marekani yaliyolenga kurejesha usalama wa usafiri wa baharini katika eneo hilo. Anold Kayanda amefuatilia hatua hiyo. Karibu Anold utufahamishe zaidi. 

iran hormuz umoja mataifa marekani shirika
Habari za UN
24 JUNI 2026

Habari za UN

Play Episode Listen Later Jun 24, 2026 9:55


Hii leo jaridani tunaangazia usalama wa mabaharia katika Mlango Bahari wa Hormuz, ongezeko kubwa la ukatili wa kingono unaohusiana na mzozo nchini Sudan, na ujumbe wa Papa Leo wa Kumi na Nne (Leo XIV), kuhusu ongezeko la njaa duniani.Shirika la Umoja wa Mataifa la Usafiri wa Baharini (IMO) limetangaza mpango wa kuwaondoa zaidi ya mabaharia 11,000 waliokwama katika Mlango Bahari wa Hormuz kufuatia makubaliano ya amani kati ya Iran na Marekani yaliyolenga kurejesha usalama wa usafiri wa baharini katika eneo hilo. Anold Kayanda amefuatilia hatua hiyo.Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Binadamu, OHCHR, imetoa ripoti kuhusu ongezeko kubwa la ukatili wa kingono unaohusiana na mzozo nchini Sudan tangu mapigano yalipoanza zaidi ya miaka mitatu iliyopita. Ofisi hiyo imekumbusha jumuiya ya kimataifa umuhimu wa kuhakikisha haki na uwajibikaji vinapewa kipaumbele wakati juhudi za kusitisha mapigano na kutafuta suluhu ya mzozo huo zikiendelea.Katika kipindi ambacho idadi ya watu wanaokabiliwa na njaa duniani inaendelea kuongezeka kutokana na migogoro, mabadiliko ya tabianchi na changamoto za kiuchumi, kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Leo wa Kumi na Nne (Leo XIV), ametuma ujumbe wa mshikamano kwa kutembelea makao makuu ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani, WFP, mjini Roma nchini Italia wiki hii. Ziara hiyo imeangazia umuhimu wa kuimarisha juhudi za kimataifa katika mapambano dhidi ya njaa.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!

SBS Swahili - SBS Swahili
Taarifa ya Habari: Marekani na Iran zasaini mkataba wa kumaliza vita

SBS Swahili - SBS Swahili

Play Episode Listen Later Jun 19, 2026 14:46


Rais wa Marekani Donald Trump alisaini makubaliano na Iran jana Jumatano ambayo yanaitaka Jamhuri hiyo ya Kiislamu kupunguza kiwango cha akiba yake ya madini ya urani iliyorutubishwa.

iran rais habari jamhuri marekani
SBS Swahili - SBS Swahili
Frank "Kombe hili halitabiriki lakini tuna matumaini makubwa kwa timu za Afrika"

SBS Swahili - SBS Swahili

Play Episode Listen Later Jun 18, 2026 11:08


Mashabiki wa soka wana endelea kupata burudani kupitia Kombe la Dunia la FIFA 2026 linalo andaliwa nchini, Canada, Marekani na Mexico.

Habari za UN
15 JUNI 2026

Habari za UN

Play Episode Listen Later Jun 15, 2026 9:55


Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini Kenya kufuatilia ziara ya kihistoria ya Rais wa Baraza Kuu la UN, Annalena Baerbock, kwenye kituo cha kukusanya, kuchakata  na kurejeleza taka cha Korogocho (Korogocho Material Recovery Facility - MRF) kujionea namna vijana wanavyogeuza taka kuwa fursa ya kiuchumi na silaha ya kutokomeza umasikini na uhalifu mitaani.Kufuatia makubaliano ya sitisho la mapigano la kudumu baina ya Marekani na Iran yaliyotangazwa jana jumapili Juni 14, viongozi wa ngazi za juu wa Umoja wa Mataifa wampongeza kufikiwa kwa makubaliano hayo huku wakihimiza yaheshimiwe na pia kufunguliwe upenyo maalum wa kupitisha misaada ya kibinadamu katika mlango bahari wa Hormuz huko nchini Iran.Kutoka Mashariki ya Kati twende Afrika, ambako mapigano nchini Sudan yanaelezwa kutoonesha dalili yoyote ya kupungua, huku pande zinazohasimiana zikituhumiwa kutumia mbinu za kukamatwa kiholela, mateso na kutoweshwa kwa raia kwa nguvu. Taarifa iliyotolewa leo na Tume Huru ya Umoja wa Mataifa ya Kuchunguza Ukweli kuhusu Sudan imesema vitendo hivyo vinaweza kuhesabiwa kuwa uhalifu dhidi ya ubinadamu.Na leo ni Siku ya siku ya Uelimishaji Kuhusu Ukatili dhidi ya Wazee Duniani ambapo Umoja wa Mataifa umesema hatua zaidi zinahitajika kuwalinda wazee dhidi ya ukatili, huku ukionya kuwa uelimishaji pekee hautoshi na kwamba dunia inapaswa kuimarisha sheria, huduma za afya na mifumo ya kuripoti matukio ya unyanyasaji.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!

SBS Swahili - SBS Swahili
Taarifa ya Habari: Iran yathibitisha vita dhidi ya Marekani na Israel vita isha leo usiku

SBS Swahili - SBS Swahili

Play Episode Listen Later Jun 15, 2026 6:01


Iran imethibitisha kwamba vita kati ya Marekani na Israeli katika nyanja mbalimbali Mashariki ya Kati vita isha usiku wa leo.

israel iran israelis isha habari marekani usiku mashariki
SBS Swahili - SBS Swahili
Ujerumani wafanya unyama, Japan na Uholanzi ziki ng'ang'ania alama moja

SBS Swahili - SBS Swahili

Play Episode Listen Later Jun 15, 2026 4:54


Ujerumani umeanza vyema kampeni yao ya Kombe la Dunia la 2026, ikiwashinda Curaçao inayo shiriki katika michuano hiyo kwa mara ya kwanza kwa mabao 7-1 katika Kundi E katika Uwanja wa Houston, Marekani.

japan cura dunia moja alama ziki marekani kombe ujerumani
Habari za UN
12 JUNI 2026

Habari za UN

Play Episode Listen Later Jun 12, 2026 9:59


Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina. Mkutano wa 19 wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Haki za Watu Wenye Ulemavu CRPD, umehitimishwa jana katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani. Watu wenye ulemavu na wadau mbalimbali wa Serikali na Mashirika yasiyo ya Serikali walikusanyika kutoka kila pembe ya dunia kujadili hatua zilizopigwa katika kipindi cha miaka 20 ya Mkataba wa Kimataifa wa Haki za Watu Wenye Ulemavu, CRPD. Mmoja wa waliohudhuria ni Bwana Kibaya Laibuta ambaye licha ya kupoteza uwezo wa kuona akiwa na umri wa miaka 24 alipokuwa mwanafunzi katika Chuo Kikuu cha Nairobi bado alifanikiwa kusonga mbele akamaliza masomo yake ya sheria na masomo mengine ya ngazi za juu na sasa miaka mingi baadaye ni Jaji katika Mahakama ya Rufaa ya Kenya. Siri yake ya mafaniko ndio hasa anaihamasisha kote duniani na anaiweka wazi katika mazungumzo yafuatayo na Anold Kayanda wa Idhaa hii ya Umoja wa Mataifa ili watu wengine wenye ulemavu wafanikiwe kama yeye. Pia tunakuletea muhtasari wa habari zikiwemo za hatua za kupambana na UKIMWI, maambukizi ya ugonjwa wa Ebola hasa kwa watoto DRC, na ujumbe katika siku ya kimataifa ya kupinga utumikishaji wa watoto.Mwenyeji wako ni Rashid Malekela.

new york kenya siri ebola nairobi drc umoja hii haki afya watoto watu crpd mataifa serikali marekani kimataifa mkutano mashirika chuo kikuu
Habari za UN
11 JUNI 2026

Habari za UN

Play Episode Listen Later Jun 11, 2026 10:43


Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina. Mkutano wa 19 wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Haki za Watu Wenye Ulemavu CRPD, umetamatishwa leo katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani. Idhaa hii imepata fursa ya kuzungumza na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya mkutano huu muhimu, Mtanzania Zuleikha Tambwe. Pia tunakuletea muhtasari wa habari kama zifuatazo..Hatari ya Ebola wakati wa Kombe la Dunia la Soka 2026 ni ndogo na hakuna sababu ya mashabiki kubadili mipango yao ya safari kuelekea Canada, Mexico na Marekani, limesema Shirika la Afya Duniani WHO kombe hilo liking'oa nanga leo. Mkurugenzi wa WHO Kanda ya Ulaya, Hans Henri P. Kluge, amesema hakuna wagonjwa wa Ebola katika nchi hizo wala Ulaya na amesisitiza, “Safirini kama kawaida na furahieni mashindano hayo.” WHO imefafanua kuwa Ebola haisambai kwa njia ya hewa na visa vingi vipo katika maeneo ya mbali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, Annalena Baerbock, amehitimisha ziara  ya siku mbili jijini Nairobi nchini Kenya, ambapo amesisitiza nafasi muhimu ya Umoja wa Mataifa katika kuendeleza maendeleo, amani na ushirikiano barani Afrika. "Kila siku Umoja wa Mataifa na washirika wake huokoa maisha. Bila UN, mamilioni ya watoto wasingepata elimu kupitia UNICEF wala chanjo muhimu kupitia WHOna tusingekuwa na ushirikiano kama huu."Mkutano wa 19 wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Haki za Watu Wenye Ulemavu CRPD, uliokuwa unafanyika hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani umefikia tamati leo. Kaulimbiu ya mwaka huu ni “kuadhimisha miaka 20 ya mkataba huo na kuimarisha utekelezaji wake katika dunia inayobadilika.” Kibaya Laibuta, Jaji wa Mahakama ya Rufani nchini Kenya, ambaye pia ni mlemavu aliyeoona au  kipofu, ameshiriki na anaeleza alivyouona mkutano huu.Mwenyeji wako ni Rashid Malekela, karibu!

Habari za UN
09 JUNI 2026

Habari za UN

Play Episode Listen Later Jun 9, 2026 9:57


Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina. Kesho kutwa Alhamisi ya Juni 11, macho na masikio yanaelekezwa Mexico, Canada na hapa Marekani kwa ajili ya fainali za kombe la dunia kwa mpira wa miguu, au soka al maarufu kabumbu. Ingawa hivyo zama za sasa za mchezo huo maarufu zaidi duniani zinakumbwa na madhara ya  athari za mabadiliko ya tabianchi. Ongezeko la joto kali linavuruga mechi na kuzua wasiwasi kuhusu mustakabali wa mchezo huo. Ni kwa kuzingatia hilo, Sekretarieti ya Mkataba wa Kimataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi, UNFCCC inamulika suala hilo na kutoa mapendekezo ya nini kifanyike kwani hivi sasa madhara ya joto kali kwenye kabumbu ni dhahiri. Feissal Kirwa anamulika hilo kupitia video iliyoandaliwa na UNFCCC.Pia tunakuletea muhtasari wa habari na jifunze Kiswahili.Takriban watoto milioni 138 duniani kote bado wako katika ajira za watoto, wakiwemo watoto milioni 54 wanaofanya kazi hatarishi. Hayo yamo katika ripoti mpya iliyotolewa leo na Shirika la Kazi la Umoja wa Mataifa ILO. Katika ujumbe wakwe kwenye ripoti hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa ILO, Gilbert F. Houngbo, ametoa wito wa kuchukuliwa hatua za haraka ili kubadili hali hii.“Habari njema ni kwamba hadi sasa tuna wagonjwa 19 ambao wamepona, hivyo utambuzi wa mapema na matibabu vinaokoa maisha,”  Huyo ni Mkurugenzi wa Operesheni za Tahadhari na Hatua za Dharura za Afya wa Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa Duniani (WHO), Dkt. Abdirahman Mahamud, akizungumza na waandishi wa habari mjini Geneva leo kwa njia ya video kutoka Bunia katika Jimbo la Ituri, nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, jimbo ambalo linachangia asilimia 94 ya wagonjwa wote wa Ebola.Mkutano wa 19 wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Haki za Watu Wenye Ulemavu CRPD, umeanza leo Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York na utaendelea hadi 11 Juni. Kaulimbiu ya mwaka huu ni “kuadhimisha miaka 20 ya mkataba huo na kuimarisha utekelezaji wake katika dunia inayobadilika.” Washiriki wanajadili namna ya kutokomeza ukandamizaji, ukatili na manyanyaso dhidi ya watu wenye ulemavu, kuimarisha mifumo ya huduma na msaada, pamoja na kuongeza ushiriki na uwakilishi wao katika maisha ya kisiasa na umma.Katika kujifunza lugha ya Kiswahili hii leo Dkt Mwanahija Ali Juma, Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili, Zanzibar nchini Tanzania, BAKIZA anafafanua maana na matumizi ya neno "MKWARUZO."Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!

new york canada mexico fifa tanzania ebola jimbo zanzibar drc ilo kazi unfccc umoja congo drc hayo hii haki kiswahili katika ituri afya baraza habari joto dkt bunia hatua mataifa jamhuri marekani shirika kimataifa mkutano kesho kidemokrasia mkurugenzi alhamisi
SBS Swahili - SBS Swahili
Yaliyojiri Afrika: Duale "serikali haita shauriana na raia kuhusu karantini ya Ebola"

SBS Swahili - SBS Swahili

Play Episode Listen Later Jun 5, 2026 7:37


Rais wa Kenya, William Ruto, amesema serikali yake inafanya jambo sahihi kwa kuruhusu Marekani kujenga kituo cha karantini ya Ebola nchini humo.

kenya afrika ebola rais raia duale serikali marekani
SBS Swahili - SBS Swahili
Taarifa ya Habari:Mahakama ya Kenya yasimamisha kujengwa kituo cha karantini cha Ebola

SBS Swahili - SBS Swahili

Play Episode Listen Later Jun 4, 2026 5:26


Mahakama Kuu ya Kenya Jumanne ilisimamisha kwa wiki tatu zaidi mpango wa kujenga kituo cha karantini ya Ebola, kilichopendekezwa na Marekani.

Habari za UN
03 JUNI 2026

Habari za UN

Play Episode Listen Later Jun 3, 2026 10:33


Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini Tanzania Kaskazini mwa taifa hilo la Afrika Mashariki, ambako Hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro inaendelea kuwa mfano wa jinsi binadamu, wanyamapori na urithi wa kitamaduni vinavyoweza kuishi pamoja huku vikichangia maendeleo ya utalii endelevu na ulinzi wa mazingira. Je nini kinafanyika kuhakikisha uhifadhi, utamaduni, mazingira na utalii vinakutana kwa mustakabali endelevu? Ili kupata majawabu Flora Nducha wa Idhaa hii amezungumza na Kamishna wa Hifadhi ya Ngorongoro, Abdul-Razaq Badru.Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la afya ulimwenguni WHO Dkt. Tedros Adhanom Ghebreyesus ameendelea kusisitiza umuhimu wa ugunduzi wa mapema kwani hatua zikichukuliwa haraka wagonjwa wa Ebola wanapona. Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Geneva Usiswi baada kurejea kutoka ziarani mashariki mwa DRC amesema, Kufikia sasa, watu sita wamepona nchini DRC na wawili nchini Uganda, jambo linaloonesha kuwa watu wanaweza kupona Ebola iwapo watapata huduma za afya na kwenda vituo vya afya mara tu wanapoanza kuonyesha dalili za ugonjwa huo.Kuelekea kuanza kwa michuano ya Kombe la Dunia la FIFA wiki ijayo hapa Marekani na katika nchi jirani, Canada na Mexico, Shirika la Afya la Nchi za Amerika (PAHO) limetoa wito kwa nchi za bara la Amerika kuimarisha ufuatiliaji wa ugonjwa wa surua na Rubella kufuatia  mikusanyiko mikubwa inayotarajiwa na milipuko inayoendelea ya surua na ongezeko la safari za kimataifa vinaweza kuongeza kasi ya kuenea kwa ugonjwa huo. Shirika hilo linazitaka mamlaka za afya kubaini maeneo yaliyo katika hatari kubwa na kuimarisha hatua za kukabiliana haraka ili kuzuia maambukizi zaidi. Na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa asubuhi hii kwa saa za New York, Marekani wanachagua wanachama watano wapya wasio wa kudumu wa Baraza la Usalama kwa muhula kipindi cha miaka miwili kuanzia tarehe 1 Januari 2027 hadi 31 Desemba 2028. Kutoka Barani Afrika mgombea mmoja ni Zimbabwe ambaye hata hivyo anatarajiwa kupita kwani hana mpinzani katika nafasi hiyo. Nchi zitakazochaguliwa zinachukua nafasi za Somalia, Pakistan, Panama, Denmark na Ugiriki, ambazo mihula yao itaisha mwishoni mwa mwaka huu 2026.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!

Habari za UN
19 MEI 2026

Habari za UN

Play Episode Listen Later May 19, 2026 10:29


Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka katika Kaunti ya Kilifi Mombasa Kenya kumsikia Mbunge Martha Koki ambaye kandoni mwa mkutano wa CSW70 uliomalizika mwezi uliopita alizungumza na Idhaa hii kufafanua haki za wanawake za umiliki wa ardhi.Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la afya ulimwenguni WHO nchini Jamhuri ya kidemokrasia Congo DRC Daktari Anne Ancia amewaambia waaandishi wa habari kuwa “Kuna zaidi ya washukiwa 500 na vifo 130 vinavyohisiwa kutokana na ugonjwa wa Ebola, na maabara zimethibitisha watu 30 wanaugua ugonjwa huo.” Mbali ya DRC, wagonjwa wawili wamegundulika huko Kampala Uganda na mwingine raia wa Marekani ambaye amepelekwa nchini Ujerumani kwa matibabu zaidi, wakati huu ambapo WHO bado inakumbwa na sintofahamu kuhusu chanzo cha mlipuko wa sasa wa Ebola DRC.Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo na Biashara UNCTAD, limetoa ripoti ukionesha uchumi wa dunia unakabiliwa na mtihani mpya kutokana na mishtuko ya biashara, chakula na fedha inayosambaa kimataifa. Ripoti hiyo inaonya kuwa licha ya kuanza kwa mwaka kwa matumaini mazuri, hali ya kijiografia, vita na changamoto za masoko sasa zinatishia ukuaji wa uchumi duniani. UNCTAD inaeleza kuwa nchi zinazoendelea ndizo zilizo hatarini zaidi, zikikabiliwa na mtikisiko wa mitaji, mzigo wa madeni na hofu ya uhaba wa chakula. Shirika hilo linashauri mataifa kuchukua hatua za kuimarisha sera za uchumi, biashara na uwekezaji ili kujikinga na madhara ya mishtuko hiyo.Na panya wanazua balaa huko Ukanda wa Gaza eneo la Palestina linalokaliwa kimabavu na Israel. Wananchi wanasema kuwa panya wanaingia kwenye mahema kila siku, wanachafua akiba ya chakula, na kushambulia watoto wadogo nyakati za usiku. Ikumbukwe baada ya vita kusitishwa wananchi walirejea katika maeneo yao lakini kwakuwa nyumba zililipuliwa wengi wanaishi kwenye mahema huku mazingira yakiwa machafu na mifumo ya maji ikiwa haifanyi kazi na hayo ni mazingira mazuri kwa panya kuzaliana.Mwenyeji wako ni Rashid Malekela, karibu!

israel kenya gaza ebola palestina baku drc kuna umoja hii unctad mbali kampala uganda kilifi wanawake mataifa jamhuri maendeleo miji marekani shirika ripoti kaunti ujerumani wananchi
SBS Swahili - SBS Swahili
Australia Yafafanuliwa: Vidokezo vya kupunguza gharama ya petroli |Mafuta Yalengwa

SBS Swahili - SBS Swahili

Play Episode Listen Later May 15, 2026 9:17


Bei za petroli na dizeli nchini Australia zinaendelea kukabiliwa na shinikizo wakati huu ambapo vita kati ya Marekani na Iran vina ingia mwezi wa tatu.Bei za petroli na dizeli nchini Australia zinaendelea kukabiliwa na shinikizo wakati huu ambapo vita kati ya Marekani na Iran vina ingia mwezi wa tatu.

Habari za UN
06 MEI 2026

Habari za UN

Play Episode Listen Later May 6, 2026 9:59


Hii leo jaridani tunaangazia maambukizi wa Hantavirus, juhudi za kutokomeza Adhabu za Viboko shuleni nchini Tanzania, na ujumbe wa Profesa Hamisi Masanja Malebo kuhusu haki za watu wa asili.Imethibitishwa kuwa abiria mwingine aliyekuwa kwenye meli ya kitalii iliyohusishwa na mlipuko wa ugonjwa wa virusi vya Hanta au Hantavirus ameambukizwa ugonjwa huo, ugonjwa ambao tayari umeua watu watatu waliokuwa ndani ya meli na kusababisha tahadhari ya kimataifa iliyoratibiwa na Shirika la Afya Duniani (WHO) la Umoja wa Mataifa.Siku ya Kimataifa ya Kukomesha Adhabu za Viboko huadhimishwa Aprili 30 ya kila mwaka, na mwaka huu katika maadhimisho ya siku hiyo wiki iliyopita, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Watoto, UNICEF, nchini Tanzania kwa kushirikiana na wadau wa haki za binadamu na elimu lilizindua kampeni iitwayo ‘No Collabo' iliyolenga kukomesha adhabu ya viboko kwa mtindo ambao walimu zaidi ya mmoja humchapa mwanafunzi viboko kwa wakati mmoja. Rashid Malekela amezungumza na wazazi mkoani Mwanza Kaskazini Magharibi mwa nchini hiyo kupata maoni yao.Siku tano zilizopita Jukwaa la Kudumu la Umoja wa Mataifa kuhusu Masuala ya Watu wa Asili (UNPFII) limefunga pazia hapa katika makao ya Umoja wa Mataifa  jijini New York, Marekani  baada ya majadiliano ya takribani wiki mbili ya wadau kutoka nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa kuhusu sera, mafanikio na kukabiliana na changamoto mbalimbali katika kuhudumia wananchi wao ikiwemo jamii za watu wa asili. Kwa upande wa Tanzania, mmoja wa walioshiriki ni Katibu Mtendaji wa Tume ya shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni, UNESCO ya Taifa la Tanzania, Profesa Hamisi Masanja Malebo.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!

Habari za UN
Serikali ya Tanzania inajali usawa na haki kwa watu wote kupata huduma kwa usawa - Profesa Malebo

Habari za UN

Play Episode Listen Later May 6, 2026 2:34


Siku tano zilizopita Jukwaa la Kudumu la Umoja wa Mataifa kuhusu Masuala ya Watu wa Asili (UNPFII) limefunga pazia hapa katika makao ya Umoja wa Mataifa  jijini New York, Marekani  baada ya majadiliano ya takribani wiki mbili ya wadau kutoka nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa kuhusu sera, mafanikio na kukabiliana na changamoto mbalimbali katika kuhudumia wananchi wao ikiwemo jamii za watu wa asili. Kwa upande wa Tanzania, mmoja wa walioshiriki ni Katibu Mtendaji wa Tume ya shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni, UNESCO ya Taifa la Tanzania, Profesa Hamisi Masanja Malebo.Feisal Kirwa wa idhaa hii alifanya mahojiano naye kwanza akitaka kufahamu Tanzania ina mikakati gani ya kuhakikisha watu wa asili wanajumuishwa katika huduma za afya kwa wote?

new york tanzania unesco umoja haki kwa siku watu taifa tume wote elimu mataifa serikali marekani jukwaa
Habari za UN
04 MEI 2026

Habari za UN

Play Episode Listen Later May 4, 2026 9:57


Hii leo jaridani tunaangazia ugonjwa unaotokana na virusi vya hantavirus, njaa na afya kwa raia nchini Somalia, na ujumbe wa mshiriki wa mkutano wa CSW70 Hanna Wendot Cheptumo Waziri wa Jinsia, Utamaduni na Maslahi ya Watoto wa Jamhuri ya Kenya kuhusu ukeketaji.Shirika la Umoja wa Mataifa la afya ulimwenguni WHO kanda ya Afrika linafuatilia kwa karibu na kutoa msaada unaohitajika kufuatia tukio la afya ya umma kuhusu ugonjwa wa Virusi vya Hanta uliothibitishwa kutokea katika meli ya kitalii iliyosafiri katika Bahari ya Atlantic ambapo mpaka sasa watu watatu wamepoteza maisha.Wanawake na watoto waliokimbia ukame na migogoro nchini Somalia wameonya kuwa wanazidi kutumbukia katika janga la kibinadamu la njaa na mateso huku kupungua kwa ufadhili wa misaada ya kibinadamu kukiendelea kuathiri maisha ya watu kote nchini humo. Onyo lao limetolewa wakati mkuu wa masuala ya dharura na misaada ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa, Tom Fletcher, akihitimisha ziara yake katika kambi za wakimbizi na vituo vya afya mjini Mogadishu na Baidoa mwishoni mwa wiki.Ukeketaji bado ni changamoto katika maeneo kadhaa duniani na takwimu za Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani, WHO hadi mwaka jana kulikuwa na zaidi ya wasichana na wanawake zaidi ya milioni 230 walio hai waliokeketwa katika nchi 30 za Afika, Mashariki ya Kati na Asia. Kupitia mahojiano yaliyofanyika kandoni mwa Mkutano wa Kamisheni ya Hali ya Wanawake Duniani, CSW70 jijini New York, Marekani, miezi miwili iliyopita, Hanna Wendot Cheptumo Waziri wa Jinsia, Utamaduni na Maslahi ya Watoto wa Jamhuri ya Kenya anaeleza hatua zinazochukuliwa na nchi yake kupambana na hali hiyo ya ukeketaji.”Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!

new york atlantic kenya afrika somalia hantavirus mogadishu umoja hii tom fletcher bahari afya watoto wanawake mataifa jamhuri onyo marekani shirika virusi mkutano mashariki baidoa
Habari za UN
Kenya tunashirikiana na mataifa jirani kutokomeza ukeketaji_ Hanna Wendot Cheptumo

Habari za UN

Play Episode Listen Later May 4, 2026 3:00


Ukeketaji bado ni changamoto katika maeneo kadhaa duniani na takwimu za Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani, WHO hadi mwaka jana kulikuwa na zaidi ya wasichana na wanawake zaidi ya milioni 230 walio hai waliokeketwa katika nchi 30 za Afika, Mashariki ya Kati na Asia. Kupitia mahojiano yaliyofanyika kandoni mwa Mkutano wa Kamisheni ya Hali ya Wanawake Duniani, CSW70 jijini New York, Marekani, miezi miwili iliyopita, Hanna Wendot Cheptumo Waziri wa Jinsia, Utamaduni na Maslahi ya Watoto wa Jamhuri ya Kenya anaeleza hatua zinazochukuliwa na nchi yake kupambana na hali hiyo ya ukeketaji.

new york kenya fgm umoja watoto mataifa jamhuri marekani shirika mkutano mashariki
Habari za UN
30 APRILI 2026

Habari za UN

Play Episode Listen Later Apr 30, 2026 9:59


Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina ambapo tunamsikia Dkt. Tulia Ackson, Rais wa Muungano wa Mabungeni duniani, (IPU) ambaye hivi karibuni akiwa makao makuu ya UN, Marekani aliongoza kikao kilichokuwa sehemu ya Mkutano wa CSW70. Mara baada ya kikao hicho Assumpta Massoi wa Idhaa hii ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa alizungumza naye masuala kadhaa ikiwemo yale waliyopatia kipaumbele ili kusongesha usawa wa kijinsia duniani.Karibu Dkt. Tulia.Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres hii leo saa 3 asubuhi kwa saa za New York Marekani ameeleza kuwa na wasiwasi mkubwa kuhusu suala la kufungwa kwa mlango bahari wa Hormuz wakati mzozo huko mashariki ya kati ukiingia mwezi wa tatu licha ya kuwepo kwa usitishaji mapigano aliouita kuwa ni dhaifu. Katibu Mkuu ameonya kuwa kadri hali inavyoendelea, ndivyo gharama kwa ubinadamu zinavyoongezeka, akisisitiza kuwa nchi zinazoendelea zitaathirika zaidi kutokana na madeni makubwa na kupotea kwa ajira na kuwataka wahusika wote kurejesha mara moja uhuru wa usafiri kama ilivyoainishwa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kupitia Azimio namba  2817.Ripoti mpya ya pamoja iliyotolewa leo na mashirika ya Umoja wa Mataifa yanayohusika na chakula, kilimo na uchumi yakishirikiana na Tume ya Muungano wa Afrika imeonesha kuna pengo kubwa kati ya ufadhili wa sasa wa umma na binafsi wa kilimo na kiwango cha ufadhili kinachohitajika ili kubadilisha mifumo ya kilimo barani Afrika. Ripoti hiyo pia inathibitisha ongezeko linaloendelea la njaa na ukosefu wa uhakika wa chakula kote barani Afrika, ikisisitiza uharaka wa ufadhili mkubwa na endelevu ili kubadilisha mifumo ya kilimo.Na leo ni siku ya kuadhimisha muziki wa jazz duniani, siku inayotukumbusha nafasi ya muziki wa jazz kama daraja la kuleta amani, umoja na mazungumzo kati ya watu wa tamaduni tofauti. Kupitia midundo yake ya kipekee, jazz imeendelea kuwa chombo muhimu cha elimu na ushirikiano, ikiunganisha jamii duniani kote. Serikali, taasisi za elimu, mashirika ya kiraia na watu binafsi huungana kusherehekea mchango wa jazz katika kujenga jamii jumuishi.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!

ethiopia afrika hormuz rais umoja hii kiswahili tume tulia ipu baraza dkt mataifa aprili serikali marekani mkutano ripoti azimio
Habari za UN
Lenga nyota ili ukizikosa uupate mwezi asema Alinda Mashiku, Mhandisi NASA

Habari za UN

Play Episode Listen Later Apr 28, 2026 28:18


Anold Kayanda wa Idhaa hii anazungumza na Dkt. Alinda Mashiku, Mhandisi wa masuala ya anga katika moja ya Vituo vya masuala ya anga za mbali nchini Marekani, NASA. Kwa kuzingatia kuwa Umoja wa Mataifa unapigia chepuo wasichana na wanawake kupata fursa katika sayansi na teknolojia, swali la kwanza la Anold Kayanda kwa Alinda Mashiku ni ameipokeaje hatua ya hivi karibuni ambapo kwa mara ya kwanza mwanamke Christina Cochameshiriki katika timu ya wana-anga waliosafiri na kufanikiwa kuuzunguka mwezi katika eneo mbali zaidi katika anga ya mbali ambako kulikuwa hakujawahi kufikiwa na  wanadamu?

interview nasa umoja kwa asema dkt mwezi mataifa marekani
SBS Swahili - SBS Swahili
Makala leo: Mazungumzo kati ya Marekani na Iran yavunjika tena

SBS Swahili - SBS Swahili

Play Episode Listen Later Apr 28, 2026 11:19


Mazungumzo kati ya Marekani na Iran yamevunjika baada ya Rais wa Marekani Donald Trump, kutangaza Jumapili kwamba anafuta safari ya mjumbe wake kwenda Pakistan.

SBS Swahili - SBS Swahili
Wiki Hii barani Afrika: Somaliland tayari kuipa Marekani rasilimali zake kwa ajili yakutambuliwa kama taifa

SBS Swahili - SBS Swahili

Play Episode Listen Later Apr 24, 2026 7:02


Uongozi wa Somalilanda, uko tayari kuipa marekani haki za kuchimba madini nakuweka kambi zaki jeshi, kwa ajili yakutambuliwa kama nchi huru.

Habari za UN
22 APRILI 2026

Habari za UN

Play Episode Listen Later Apr 22, 2026 9:50


Hii leo jaridani tunaangazia sitisho la mapigano katika Mashariki ya kati, kilimo endelevu kinachowakwamua wakimbizi na wenyeji Kakuma nchini Kenya, na mafunzo ya UNDP ya uchimbaji salama wa madini ya ujenzi nchini Tanzania.Umoja wa Mataifa umekaribisha tangazo la Rais wa Marekani Donald Trump la kuongeza muda wa sitisho la mapigano kati ya Marekani na Iran, ukisema hiyo ni hatua muhimu kuelekea kupunguza mvutano kati ya mataifa hayo mawili.Maisha ya wakimbizi katika eneo la Kakuma, kaskazini mwa Kenya, yanaanza kubadilika kwa kasi kupitia miradi ya kilimo na lishe inayowezeshwa na mashirika ya Umoja wa Mataifa likiwemo lile la Mpango wa Chakula Duniani  (WFP) na la Chakula na Kilimo (FAO). Kwa ushirikiano na Serikali ya Kaunti ya Turkana chini ya ufadhili wa  Muungano wa Ulaya (EU) sasa wakimbizi wana uwezo wa kuzalisha chakula chao wenyewe, kuboresha lishe, na kujenga maisha ya kujitegemea.Shirika la Umoja wa Mataifa  la Mpango wa Maendeleo (UNDP), kwa kushirikiana na Tume ya Madini nchini  Tanzania katikati mwa wiki iliyopita yaani Aprili 16 na 17 wamefanya warsha ya mafunzo mkoani Singida katikati mwa nchi. Mafunzo hayo yamelenga kuimarisha ujuzi wa uchimbaji salama, unaozingatia sheria, na wenye faida kwa wanawake na vijana wanaojihusisha na uchimbaji mdogo wa madini ya ujenzi.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!

iran kenya tanzania undp rais wfp umoja maisha hii kwa turkana kakuma tume mataifa aprili serikali marekani shirika mashariki kaunti singida
Habari za UN
Diplomasia yapewa nafasi, Umoja wa Mataifa wakaribisha kuongezwa kwa sitisho la mapigano kati ya Marekani na Iran

Habari za UN

Play Episode Listen Later Apr 22, 2026 2:28


Umoja wa Mataifa umekaribisha tangazo la Rais wa Marekani Donald Trump la kuongeza muda wa sitisho la mapigano kati ya Marekani na Iran, ukisema hiyo ni hatua muhimu kuelekea kupunguza mvutano kati ya mataifa hayo mawili. Tupate maelezo zaidi kutoka kwa Leah Mushi. 

israel iran rais umoja mataifa marekani
SBS Swahili - SBS Swahili
Taarifa ya Habari:Australia ya omba matokeo ya mazungumzo katika Mlango-Bahari wa Hormuz

SBS Swahili - SBS Swahili

Play Episode Listen Later Apr 21, 2026 13:51


Waziri wa Mambo ya Nje Penny Wong anasema Australia ina omba matokeo ya mazungumzo katika Mlango-Bahari wa Hormuz, baada ya Marekani kushambulia na kukamata meli ya mizigo yenye bendera ya Iran.

Habari za UN
UN yaadhimisha miaka 25 ya Jukwaa linalojikita katika haki za Watu wa Asili mkazo ukiweka zaidi katika changamoto za afya na mabadiliko ya tabianchi

Habari za UN

Play Episode Listen Later Apr 20, 2026 3:06


Jukwaa la Kudumu la Umoja wa Mataifa kuhusu Masuala ya Watu wa Asili (UNPFII) limefungua kikao chake cha ishirini na tano leo Aprili 20 katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York, Marekani likiadhimisha miaka 25 tangu kuanzishwa kwake kama jukwaa la kipekee la kimataifa linalowakutanisha wadau kuhusu Watu wa Asili. Kikao hiki kinafanyika katika muktadha wa changamoto zinazoendelea duniani, zikiwemo afya, migogoro na ukosefu wa usawa. Pia kinakuja wakati ambapo mfumo wa ushirikiano wa kimataifa, ndani ya mfumo wa mipango kama Mpango wa Mageuzi ya Umoja wa Mataifa, UN80 unakabiliwa na mahitaji yanayoongezeka ya ujumuishwaji, uhalali na ufanisi. Anold Kayanda amelifuatilia tukio hilo. 

new york zaidi umoja haki katika asili afya watu miaka mataifa aprili marekani jukwaa
Habari za UN
20 APRILI 2026

Habari za UN

Play Episode Listen Later Apr 20, 2026 10:44


Hii leo jaridani tunaangazia yaliyojiri katika Jukwaa la Kudumu la Umoja wa Mataifa kuhusu Watu wa Asili hapa Makao Makuu, mafunzo Kenya ya "Social Media 4 Peace" yaani ya kuondoa habari potofu na deepfakes mtandaoni, na mlo shuleni shuleni nchini Tanzania.Jukwaa la Kudumu la Umoja wa Mataifa kuhusu Watu wa Asili (UNPFII) limefungua pazia leo Aprili 20 ikiwa ni kikao cha ishirini na tano hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York, Marekani likiadhimisha miaka 25 tangu kuanzishwa kwake kama jukwaa la kipekee la kimataifa linalowakutanisha wadau kuhusu Watu wa Asili.  Maudhim aka huu yakimulika kuhakikisha afya ya watu wa jamii za asili ikiwemo kwenye mizozo.Ni dhahiri hivi sasa watu wengi zaidi wanatumia mitandao ya kijamii katika shughuli mbalimbali na pia kupata taarifa, na kwakuzingatia ukweli huo, Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni, UNESCO, likishirikiana na Umoja wa wamiliki vya vyombo vya habari vya mtandaoni (Wanablogu) nchini Kenya, BAKE (inatamkwa ‘BEKI'), limeandaa mafunzo maalum jijini Nairobi yaliyopewa jina la "Social Media 4 Peace" yaani mitandao ya kijamii kwa amani. Karibu Rashid Malekela utujuze zaidi.Elimu imeanza kung'aa tena kwa watoto katika kijiji cha Twabagondozi, ambapo njaa iliyokuwa kikwazo kikubwa cha masomo sasa inapungua kupitia mpango wa lishe na malezi bora unaoungwa mkono na shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto, UNICEF Tanzania kwa ufadhili wa Serikali ya Japan. Kupitia juhudi hizi, watoto kama Magdalena A. Prosper wamepata nafasi ya kurejea darasani, kujifunza na hata kuwa viongozi shuleni.Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!

Habari za UN
16 APRILI 2026

Habari za UN

Play Episode Listen Later Apr 16, 2026 9:59


Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini Uganda ambayo ni moja ya nchi zinazohifadhi wakimbizi wengi zaidi duniani na tutasikia simulizi za wakimbizi kutoka Sudan ambao Uganda iliwapokea na kuwapa makazi katika Makazi ya Wakimbizi ya Kiryandongo yaliyoko magharibi mwa nchi.Wataalamu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa wametaka uchunguzi wa haraka na uwajibikaji wa kimataifa kufuatia madai ya usafirishaji haramu wa wanawake na wasichana yaliyoibuliwa katika “faili za Epstein.” Wamesema madai hayo yanaonyesha mtandao mpana wa unyonyaji wa kingono uliodumu kwa miaka mingi na kuhusisha watu mashuhuri.mashambulizi makali ya anga ya Israel yameendelea kusini mwa Lebanon, yakilenga maeneo karibu na ngome ya Hezbollah ya Bint Jbeil, huku mashambulizi ya roketi kuelekea kaskazini mwa Israel nayo yakiendelea na kuongeza hofu ya kuongezeka kwa mapigano. Katika hatua nyingine, jeshi la Marekani limesema limezuia meli 10 kupita katika Mlango Bahari wa Hormuz, likitekeleza zuio lake lililotangazwa dhidi ya bandari za Iran. Wakati huo huo, mvutano wa kidiplomasia unaongezeka katika Umoja wa Mataifa, ambapo Baraza Kuu linakutana leo kujadili matumizi ya kura ya turufu kufuatia azimio la Baraza la Usalama kuhusu Mashariki ya Kati lililoungwa mkono na wengi lakini kuzuiwa na China na Urusi.Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto, UNICEF, leo limeeleza wasiwasi mkubwa kufuatia ongezeko la watoto waliouawa au kujeruhiwa nchini Ukraine, ambapo watoto 89 wameathirika mwezi Machi 2026 pekee. Kwa mujibu wa takwimu zilizothibitishwa na ripoti ya uangalizi wa haki za binadamu nchini Ukraine, idadi hiyo imeongezeka kwa asilimia 65 ikilinganishwa na mwezi Februari, hali inayoonesha madhara makubwa ya mashambulizi yanayoendelea kwa familia na jamii. Mashambulizi mabaya ya usiku wa tarehe 15 Aprili yalipiga miji kadhaa mikubwa, ikiwemo Dnipro, Kharkiv, Kyiv na Odesa, yakionesha hatari kubwa inayowakabili watoto.Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili, leo mchambuzi wetu ni Dkt. Josephat Gitonga, ambaye ni Mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi nchini Kenya, kwenye Kitivo cha Tafsiri na Ukalimani anafafanua maana ya methali “AWALI KUWA HERI SI AJABU” asMwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!

Habari za UN
14 APRILI 2026

Habari za UN

Play Episode Listen Later Apr 14, 2026 9:58


Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayomulika Mauaji ya kimbari nchini Rwanda ambapo Waziri wa sheria na ambaye pia ni mwanasheria Mkuu wa nchi hiyo Dkt. Emmanuel Ugirashebuja amezungumza na Idhaa hii na anaeleza siri ya wananchi wa Rwanda kuweza kuishi kwa amani baada ya mauaji hayo.Kama mapigano yataendelea nchini Sudan hadi mwaka 2030, umaskini wa kupindukia unaweza kuongezeka na kuvuka asilimia 60, huku watu wengine milioni 34 wakitumbukia kwenye ufukara, imesema Ripoti ya uchambuzi mpya wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo (UNDP) iliyotolewa leo Sudan na Marekani ikiwa kesho inatimia miaka mitatu kamili tangu kuanza kwa vita.Nayo mashirika ya Umoja wa Mataifa yametoa kauli zao tofauti tofauti kuhusu miaka mitatu ya vita nchini Sudan ambapo lile la kuhudumia watoto UNICEF linasema watoto wanaendelea kulipa gharama ya vita kwani zaidi ya watoto 245 wameuawa au kujeruhiwa nchini humo tangu Januari hadi Machi mwaka huu, huku mashambulizi ya ndege zisizo na rubani au droni yamesababisha takriban asilimia 80 ya majeruhi na vifo hivyo.Mzozo wa Israeli na Lebanon ulioshika kasi baada ya wapiganaji wa Hezbollah kushambulia Israeli kupinga hatua ya Marekani na Israeli kushambulia Iran, hii leo huko Washington DC, hapa Marekani kunafanyika mazungumzo kati ya Israel na Lebanon. Umoja wa Mataifa unasihi pande zote kutumia diplomasia kumaliza uhasama na kusongesha azimio namba 1701 la Baraza la Usalama linalozuia mapigano mpakani mwa mataifa hayo mawili.Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili hii leo mtaalam wetu Onni Sigalla, Mhariri mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania, BAKITA. Anafafanua maana za neno "KUDA"Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!

Habari za UN
13 APRILI 2026

Habari za UN

Play Episode Listen Later Apr 13, 2026 11:37


Hii leo jaridani tunaangazia mlango Bahari wa Hormuz, mafuriko na ukarabati wa miundombinu huko jimbo la Upper Nile nchini Sudan Kusini, na juhudi za FAO nchini Tanzania za kuwapatia mafunzo jamii kuhusu lishe bora.Wakati mazungumzo ya kumaliza vita huko Mashariki ya Kati baina ya Marekani na Iran yakigonga mwamba mwishoni mwa wiki, shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo FAO limeonya kuwa kuvurugika kwa meli kupita katika mlango Bahari wa Hormuz kunaleta hatari zinazoongezeka si tu kwenye nishati bali pia katika mifumo ya chakula duniani.Kufuatia mafuriko makubwa yanayoendelea kuharibu miundombinu na kukwamisha ulinzi wa amani huko  jimbo la Upper Nile nchini Sudan Kusini, ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa Kulinda Amani nchini humo, UNMISS unaendelea kujitahidi kukarabati miundombinu kama njia mojawapo ya kuongeza ustahimilivu na kuchochea amani.Nchini Tanzania, kupitia Mpango wa Pamoja wa Kigoma Awamu ya Pili (KJPII) unaotekelezwa chini ya uongozi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo (FAO), maafisa ugani wa kilimo, wataalamu wa lishe na afya mkoani Kigoma waliungana kuandaa tukio la Siku ya Afya na Lishe Mitaani au SALIMI sambamba na Siku ya Shamba la Mkulima ili kuwapatia wakulima na wanajamii elimu ya vitendo kuhusu uzalishaji na matumizi ya mazao yenye lishe.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!

iran tanzania hormuz fao umoja hii bahari siku afya pamoja wakati mataifa aprili unmiss marekani shirika mashariki sudan kusini