POPULARITY
Leo jaridani kuna Mada kwa Kina inakupeleka Uganda kumulika Siku ya Ziwa duniani hususan Ziwa Albert.Lakini pia kuna Muhtasari ukiwasilishwa na Leah Mushi akiangazia kumalizika kwa mlipuko wa Ebola, Uganda; Kauli ya Katibu Mkuu wa UM kuhusu maambukizi ya Ebola nchini DR Congo na kisha chuki dhidi ya wageni nchini Afrika Kusini.Jifunze Kiswahili leo inabisha hodi nchini Burundi kwa Mwenyekiti wa CHAWARUNDI Karibu na mwenyeji wako ni Assumpta Massoi.
Hii leo jaridani mwenyeji wako ni Feissal Kirwa akikuletea Muhtasari wa Habari na Mada kwa Kina. Kwa ujumla anaangazia masuala ya amani na usalama, usaidizi wa kibinadamu, amani na usalama, haki za binadamu na hali ya hewa.MUHTASARI1. Wimbi jipya la mashambulizi makubwa ya Urusi dhidi ya Ukraine yaliyosababisha vifo vya raia na majeruhi wengi, limelaaniwa vikali na Mratibu wa Masuala ya Kibinadamu wa Umoja wa Mataifa nchini Ukraine, Matthias Schmale, akisisitiza kuwa raia lazima walindwe kwa mujibu wa sheria za kimataifa za kibinadamu.Mashambulizi hayo ya usiku yaliyoanza mwezi huu wa Agosti yamekuja baada ya mwezi Julai kuwa mwezi ulioshuhudia idadi kubwa zaidi ya vifo vya raia nchini Ukraine tangu Aprili mwaka 2022. 2. Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa, kupitia msemaji wake Jeremy Laurence, ameeleza wasiwasi mkubwa kuhusu kuongezeka kwa utekelezaji wa hukumu za kifo nchini Iran. Kwa mujibu wa Ofisi ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa, adhabu ya kifo inaendelea kutumiwa kama njia ya kuwatia hofu wananchi na kukandamiza sauti za wanaopinga serikali.Akizungumza leo jijini Geneva, Uswisi, Jeremy Laurence amesema,“tunazihimiza mamlaka za Iran kusitisha mara moja utekelezaji wa hukumu zote za kifo na kuelekea katika kufuta kabisa adhabu ya kifo.” 3. Utafiti wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) unaonesha kuwa uimarikaji wa mwenendo wa hali ya hewa ya El Niño unatarajiwa kuongeza kwa kiasi kikubwa uhaba wa chakula duniani hadi mwaka 2027. Shirika hilo linaongeza juhudi za kujiandaa na kukabiliana na athari hizo, huku El Niño ikiwa tayari imeanza kuwaathiri watu walio katika maeneo yenye hali ya njaa. MADA KWA KINAKituo kipya cha kutoa huduma kwa walioambukizwa ugonjwa wa Ebola, kinafunguliwa wiki hii huko Bunia, jimboni Ituri, Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, (DRC) ambako ndio kitovu cha mlipuko wa sasa wa Ebola ya virusi vya Bundibuvyo. Kituo hiki kitakuwa kituo kikubwa zaidi nchini humo cha kutibu Ebola. Je nini kinafanyika? Assumpta Massoi anatupitisha kwa kutumia video iliyoandaliwa na Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu misaada ya dharura, OCHA.
Hii leo jaridani mwenyeji wako ni Assumpta Massoi akikuletea Muhtasari wa Habari na Mada kwa Kina. Kwa ujumla anaangazia masuala ya usaidizi wa kibinadamu, amani na usalama pamoja na afya.Muhtasari wa habari:Utapiamlo mkali nchini Afghanistan umefikia viwango vya kutisha, huku majimbo 12 yakirekodi kiwango cha juu zaidi kuwahi kushuhudiwa cha utapiamlo miongoni mwa watoto wakati huu watu milioni 14 wakikabiliwa na njaa kali, imesema WFP.Mjumbe Maalum wa Shirikisho la Kimataifa la Vyama vya Msalaba Mwekundu na Hilali Nyekundu (IFRC) kwa ajili ya Sudan, Derk Segaar, leo amewaeleza waandishi wa habari jijini Geneva Uswisi kwamba wiki iliyopita alisafiri kwa njia ya Barabara nchini Sudan na kwamba ingawa macho ya dunia yameelekezwa zaidi katika maeneo ya Darfur na Kordofan, athari za vita zinaendelea kote nchini Sudan ambayo ni miongoni mwa nchi zinazokabiliwa na migogoro mikubwa zaidi ya kibinadamu duniani, lakini pia ni miongoni mwa migogoro inayopuuzwa zaidi.Na Umoja wa Mataifa na wadau wake wanaendelea kuisaidia Rwanda kujiandaa dhidi ya Ebola. Hatua hizo zinajumuisha ufuatiliaji katika vituo vya afya, jamii na mipakani, huku zaidi ya wahudumu 100 wakipelekwa kwenye vituo vya kuingilia nchini. Pia, wahudumu karibu 400 wanapatiwa mafunzo ya utambuzi wa mapema.Mada kwa kina:Na sasa ni wasaa wa mada kwa kina inayotupeleka nchini Afrika Kusini, ambako dawa mpya ya kujikinga na Virusi Vya Ukimwi, VVU, iitwayo Lenacapavir, imeanza kutolewa kama sehemu ya jitihada dhidi ya maambukizi mapya, hasa miongoni mwa vijana walio katika hatari kubwa zaidi.Kwa mara ya kwanza, mtu anaweza kujikinga na VVU, kwa kudungwa sindano moja tu kila baada ya miezi sita, bila kumeza kidonge kila siku. Lenacapavir imeonesha ufanisi wa zaidi ya asilimia 96 katika kuzuia maambukizi, na sasa imeanza kutolewa katika nchi tisa barani Afrika, ikiwemo Afrika Kusini, nchi yenye idadi kubwa zaidi duniani ya watu wanaoishi na VVU. Kupitia video iliyoandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la kupambana na Ukimwi, UNAIDS, Feissal Kirwa wa Idhaa hii anakusimulia. Kwako Feissal.
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayoturejesha hapa Makao Makuu ya UN kusikia mahojiano maalum na ya kina baina ya Flora Nducha wa Idhaa hii na Mkuu mpya wa ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Dawa na Uhalifu UNODC. Pia tunakuletea Muhtasari wa habari.Kumekuwepo na imani kwamba ugonjwa wa Ebola si halisi, hali iliyowafanya baadhi ya wananchi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, kuzika wapendwa wao waliokufa kwa Ebola bila kufuata hatua za kujikinga dhidi ya maambukizi. Kutafuta suluhu ya changamoto hiyo, Shirika la Afya Duniani WHO kwa kushirikiana na Shirikisho la Kimataifa la chama cha Msalaba Mwekundu na Hilali Nyekundu, IFRC, wamesikiliza maoni ya jamii kuhusu taratibu za mazishi.Takriban nusu ya watoto wote duniani au watoto bilioni 1.1 sasa wanakabiliwa na angalau hatari tatu za mabadiliko ya tabianchi zinazolingana, zikihatarisha afya zao, elimu, na maisha yao, imesema ripoti iliyotolewa leo na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto UNICEF.Na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres, yuko nchini Haiti kwa ziara maalum ya mshikamano ili kujionea hali halisi ya wananchi walioathiriwa na ghasia na ukosefu wa usalama. Akiwa huko, Guterres anakutana na wananchi, kufanya mazungumzo na Waziri Mkuu wa Haiti, na kutathmini juhudi za serikali, Umoja wa Mataifa na jumuiya ya kimataifa za kurejesha utulivu nchini humo.Mwenyeji wako ni Feissal Kirwa, karibu!
Hii leo kwenye Jarida la Habari tuna Muhtasari na Mada kwa Kina.MUHTASARIOngezeko la idadi ya wagonjwa wa Ebola nchini DRCUmuhimu wa kushirikisha jamii kwenye udhibiti wa Ebola Mpango wa Tanzania wa kukabiliana na makazi duniMADA KWA KINAInaangazia uchambuzi wa ripoti ya uanishaji wa upatikanaji wa chakula nchini Tanzania ambapo tumezungumza na Afisa kutoka shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo (FAO) katika taifa hilo la Afrika Mashariki. Hali iko vipi ? na nini kinafanyika kusaidia waliokumbwa na uhaba wa chakula.Msomaji wako leo ni Rashid Malekela
Hii leo jaridani ni:Muhtasari;Mada kwa Kina na Jifunze lugha ya Kiswahili. Jarida leo linawasilishwa na Rashid Maleka kutoka Mwanza nchini Tanzania.Muhtasari wa Jarida:dadi ya vifo kutokana na shambulio dhidi ya hospitali moja huko Darfur, Sudan, Ijumaa iliyopita imeongezeka zaidi,Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi,UNHCR limetoa wito wa msaada wa haraka wa kimataifa ili kuhakikisha urejeaji wa wakimbizi wa Jamhuri ya Kidemokrasia Congo, DRC wanaorejea kutoka Burundi unafanyika katika mazingira ya usalama na utu.Leo katika kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Kifua Kikuu (TB) inayoadhimishwa tarehe 24 mwezi Machi kila mwaka, WHO inazihimiza nchi kuharakisha hatua za kumaliza TB na kupanua upatikanaji wa huduma za kuokoa maisha kwa kutumia ubunifu mpya ikiwemo vipimo vinavyotumia mate.Mada kwa kina: Leah Mushi amezungumza na Naibu Mrajisi wa Mahakama Kuu ya Zanzibar, Tanzania Chausiku Kafuti Kuya kando ya CSW70 iliyokunja jamvi wiki iliyopita hapa New York, Marekani. Jifunze lugha ya Kiswahili: Methali - “ATETEAYE MTUKU NI TANGUKO LA BURE”Karibu!
Jaridani hii leo tuna Muhtasari wa Habari ukiangazia hali ya njaa Sudan, mchango wa Marekani dhidi ya VVU/ Ukimwi na kauli ya UNRWA kufuatia taarifa potofu dhidi ya shirika hilo. Halikadhalika mada kwa kina kutoka AfyaAFRIKA.Maeneo mawili zaidi katika jimbo la Darfur Kaskazini ya Um Baru na Kernoi sasa yameingia katika baa la njaa kufuatia utapiamlo wa kupindukia au unyafuzi kuvuka wiwango vya kutokuwa na uhakika wa chakula.Shirika la Umoja wa mataifa linalohusika na vita dhidi ya ukimwi UNAIDS limekaribisha kwa dhati hatua ya Marekani kutia saini kuwa sheria kifurushi cha matumizi ya kimataifa chenye thamani ya dola bilioni 5.88, kwa ajili ya hatua za kimataifa za kukabiliana na virusi vya ukimwi VVU .Kamishina Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la msaada kwa wakimbizi wa Kipalestina UNRWA Phillippe Lazzarini amesema taarifa potofu dhidi ya UNRWA zinaendelea kulenga shirika hilo katikati ya mgogoro Gaza ikiwemo madai ya hivi karibuni kabisa, yaliyoibuliwa na video ya jeshi la Israel ikionesha mifuko mitupu ya unga karibu na mabomu, ambapo amesema ni taarifa za uongo na hazijadhibitishwa.Katika Mada kwa Kina: Kuelekea siku ya kutokomeza FGM kesho Februari 6, tunazungumza na Catherine Mootian, Muasisi na Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la kiraia la AfyAfrika la huko Narok nchini Kenya. Yeye ni manusura wa FGM aliyeamua kuchukua hatua kuepusha wengine.
Hii leo Jaridani, Anold Kayanda anakupeleka nchini Kenya kusikia usaidizi wa FAO kwenye harakati za kuondokana na njaa katika taifa hilo la Afrika Mashariki kupitia uimarishaji wa sekta ya kilimo. Lakini pia kuna Muhtasari kutoka kwa Leah Mushi akimulika:Baa la Njaa kuthibitishwa huko El Fasher na Kadugli nchini SudanAzimio la Doha lenye lengo la kuimarisha maendeleo ya jamii dunianiKauli ya Joyce Msuya, Naibu Mkuu wa OCHA akiwa huko Doha, Qatar kufuatia kupitishwa kwa azimio hilo.Na kipengele cha Jifunze Kiswahili leo kinaelezea matumizi ya neno Mhanga na Wahanga.Karibu!
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina leo inayotupeleka Kenya kufuatilia juhudi za shirika la Umoja wa Mstaifa la mazingira UNEP na serikali ya nchi hiyo za kuichagiza jamii kuhama kutoka kwenye vyombo vya usafiri vinavyotumia mafuta yanayochafua mazingira na kukumbatia magari na vyombo vingine vya usafiri vinavyotumia nishati ya umeme. Pia tunakuletea Muhtasari wa habari na mashinani inayotupeleka nchini Sudan Kusini. Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
Majadiliano ya tofauti kati ya dini na kiroho. (A discussion of the difference between religion and spirituality.)
Muhtasari wa mafundisho yaliyotolewa hadi sasa katika podikasti. (A summary of the teachings provided so far in the podcast.)
Karibu usikilize Jarida ambapo leo kwenye Muhtasari wa habari utasikia kuhusu - Baraza la usalama ambalo limekutana katika mjadala wa wazi kujadili hali inavyoendeea nchini Afghanistan. -watoto wameanza kurejea shuleni nchini nchini Palestina - Hali nchini Haiti huwenda kuwa mbaya zaidi leo usiku Na katika mada kwa kina tunaenda nchini Tanzania kufuatilia ziara ya mafunzo ya wakulima kutoka mkoani Kigoma kwenda Kagera, ziara iliyoratibiwa na shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo, FAO.
Deutsch – warum nicht? Fungu 3 | Kujifunza Kijerumani | Deutsche Welle
Dr. Thürmann anamfahamisha Andreas mradi wake mpya... Muhtasari wa sarufi: vitendo: 1. vinavyokwenda na mashamirisho na 2. vinavyofuatwa na vihusishi
Deutsch – warum nicht? Fungu 4 | Kujifunza Kijerumani | Deutsche Welle
Hadithi ya Kaizari mwenye ndevu nyekundu... Muhtasari wa sarufi: Vitenzi vya mahusiano (II)
Deutsch – warum nicht? Fungu 4 | Kujifunza Kijerumani | Deutsche Welle
Namna Martin Luther alivyookolewa... Muhtasari wa sarufi: Vitenzi vya mahusiano (III)
Deutsch – warum nicht? Fungu 4 | Kujifunza Kijerumani | Deutsche Welle
Je, Ex anaweza kufanywa aonekane... Muhtasari wa sarufi: Hakuna sarufi mpya
Deutsch – warum nicht? Fungu 2 | Kujifunza Kijerumani | Deutsche Welle
Andreas anapokea simu kutoka mtu anayemjua... Muhtasari wa sarufi: Wakati timilifu (perfect tense) wa vitendo vinavyotenganishwa
Deutsch – warum nicht? Fungu 2 | Kujifunza Kijerumani | Deutsche Welle
Kumtembelea mgonjwa Dr. Thürmann. Muhtasari wa sarufi:Wakati timilifu wa vitendo visivyotenganishwa
Deutsch – warum nicht? Fungu 2 | Kujifunza Kijerumani | Deutsche Welle
Andreas, Dr. Thürmann na Frau Berger wanaandaa safari ya meli... Muhtasari wa sarufi: Vitendo vyenye uhusika wa ‚dative‘ na ‚accusative‘
Deutsch – warum nicht? Fungu 2 | Kujifunza Kijerumani | Deutsche Welle
Ex mara ametoweka... Muhtasari wa sarufi: Hakuna sarufi mpya
Deutsch – warum nicht? Fungu 3 | Kujifunza Kijerumani | Deutsche Welle
Mwimbaji mashuhuri – na wimbo mashuhuri... Muhtasari wa sarufi: Hakuna sarufi mpya
Deutsch – warum nicht? Fungu 1| Kujifunza Kijerumani | Deutsche Welle
Andreas anatafuta tena kisingizio... Muhtasari wa sarufi: Vitendo visivyo kawaida (irregular verbs)
Deutsch – warum nicht? Fungu 3 | Kujifunza Kijerumani | Deutsche Welle
Andreas na Ex wanawazuru watu mashuhuri... Muhtasari wa sarufi: Hakuna sarufi mpya
Deutsch – warum nicht? Fungu 1| Kujifunza Kijerumani | Deutsche Welle
Kualikana chakula kikazi: Frau Berger, Andreas na Ex... Muhtasari wa sarufi: Majina katika uhusika wa moja kwa moja (accusative)
Deutsch – warum nicht? Fungu 3 | Kujifunza Kijerumani | Deutsche Welle
Dr. Thürmann anasimulia hadithi ya jengo mashuhuri... Muhtasari wa sarufi: Mwendesho wa vivumishi vya sifa (II)
Deutsch – warum nicht? Fungu 1| Kujifunza Kijerumani | Deutsche Welle
Andreas anatahayari... Muhtasari wa sarufi: Viwakilishi na kidhihirishi katika uhusika wa moja kwa moja (accusative)
Deutsch – warum nicht? Fungu 1| Kujifunza Kijerumani | Deutsche Welle
Herr Thürmann ana kazi ya kumpatia Andreas – mjini Berlin... Muhtasari wa sarufi: Vitendo vinavyotenganishwa
Deutsch – warum nicht? Fungu 3 | Kujifunza Kijerumani | Deutsche Welle
Kwa nini Ex ameondoka? Dr.Thürmann anajaribu kutoa maelezo... Muhtasari wa sarufi: Marudio ya mtungo wa maneno
Deutsch – warum nicht? Fungu 3 | Kujifunza Kijerumani | Deutsche Welle
Barua kwa wazazi wa Andreas... Muhtasari wa sarufi: Mwendesho (declension) wa vivumishi vya sifa (I)
Deutsch – warum nicht? Fungu 3 | Kujifunza Kijerumani | Deutsche Welle
Andreas anawahoji watu mjini Berlin... Muhtasari wa sarufi: Wakati ujao (future tense)
Deutsch – warum nicht? Fungu 3 | Kujifunza Kijerumani | Deutsche Welle
Andreas anampigia simu Dr.Thürmamm... Muhtasari wa sarufi: Sentensi saidizi zinazotumia dass
Deutsch – warum nicht? Fungu 3 | Kujifunza Kijerumani | Deutsche Welle
Andreas na Ex wanawasili Berlin... Muhtasari wa sarufi: Sentensi saidizi (subordinate clauses)
Deutsch – warum nicht? Fungu 3 | Kujifunza Kijerumani | Deutsche Welle
Andreas na Ex wanafanya safari ndefu... Muhtasari wa sarufi: Viunganishi (conjunctions)
Deutsch – warum nicht? Fungu 3 | Kujifunza Kijerumani | Deutsche Welle
Kurudi kwa mtu umjuaye ... Muhtasari wa sarufi: Vivumishi vya sifa
Deutsch – warum nicht? Fungu 3 | Kujifunza Kijerumani | Deutsche Welle
Mshairi miongoni mwa panya – Frau Berger anasimulia hadithi... Muhtasari wa sarufi: Wakati uliopita wa vitendo visivyo vya kawaida
Deutsch – warum nicht? Fungu 3 | Kujifunza Kijerumani | Deutsche Welle
Mgeni wa hoteli akutana na matatizo... Muhtasari wa sarufi: Marudio ya mtungo wa maneno katika sentensi kuu
Deutsch – warum nicht? Fungu 3 | Kujifunza Kijerumani | Deutsche Welle
Ziara ya mji wa Aachen... Muhtasari wa sarufi: Marudio ya hali ya kuamuru (imperative)
Deutsch – warum nicht? Fungu 3 | Kujifunza Kijerumani | Deutsche Welle
Hakuna habari zozote kutoka kwa Ex... Muhtasari wa sarufi: Wakati timilifu kwa kutumia haben na sein
Deutsch – warum nicht? Fungu 1| Kujifunza Kijerumani | Deutsche Welle
Andreas anaandika barua nyumbani... Muhtasari wa sarufi: Mwendesho wa Vitendo (V)
Deutsch – warum nicht? Fungu 3 | Kujifunza Kijerumani | Deutsche Welle
Hanimuni (honeymoon) mjini Aachen...Muhtasari wa sarufi: Marudio ya majina (nomino) na vijineno
Deutsch – warum nicht? Fungu 3 | Kujifunza Kijerumani | Deutsche Welle
Safari ya kwenda Brussels – na tukio lisilopendeza...Muhtasari wa sarufi: Marudio ya vitendo visivyo vya kawaida (irregular verbs)
Deutsch – warum nicht? Fungu 3 | Kujifunza Kijerumani | Deutsche Welle
Je, umekosa Sehemu ya 1 na 2? Humu wahusika walikuwa...Muhtasari wa sarufi: Marudio ya wakati uliopo (present tense)
Deutsch – warum nicht? Fungu 3 | Kujifunza Kijerumani | Deutsche Welle
Mwimbaji mashuhuri – na wimbo maarufu...Muhtasari wa sarufi: Marudio ya njia za kusikiliza Kijerumani
Aachen. Bwana mmoja mwenye umri wa makamo anaita teksi. Anataka kwenda ‚Hotel Europa‘... Muhtasari wa sarufi: Namna za kuamkiana
Deutsch – warum nicht? Fungu 1| Kujifunza Kijerumani | Deutsche Welle
Andreas, Hanna, Frau Berger – wahusika wanajijulisha... Muhtasari wa sarufi: Mwendesho wa kitendo kisaidizi sein (II)
Deutsch – warum nicht? Fungu 1| Kujifunza Kijerumani | Deutsche Welle
Ex anashangazwa na fikara za Andreas... Muhtasari wa sarufi: Mwendesho wa kitendo (II)
Deutsch – warum nicht? Fungu 1| Kujifunza Kijerumani | Deutsche Welle
Marafiki wa zamani na ripota kijana mwanamke – wageni Hotel Europa... Muhtasari wa sarufi: Maswali yanayotumia woher na kihusishi aus
Deutsch – warum nicht? Fungu 1| Kujifunza Kijerumani | Deutsche Welle
Mgeni mpya anawasili... Muhtasari wa sarufi: Kuuliza swali kwa kiwakilishi cha kuuliza
Deutsch – warum nicht? Fungu 1| Kujifunza Kijerumani | Deutsche Welle
Ex na Andreas wanashangazwa na Dr. Thürmann... Muhtasari wa sarufi Mwendesho wa kitendo (III)