Podcasts about julai

  • 68PODCASTS
  • 1,270EPISODES
  • 25mAVG DURATION
  • 1DAILY NEW EPISODE
  • Aug 1, 2025LATEST
julai

POPULARITY

20172018201920202021202220232024

Categories



Best podcasts about julai

Show all podcasts related to julai

Latest podcast episodes about julai

Habari za UN
01 AGOSTI 2025

Habari za UN

Play Episode Listen Later Aug 1, 2025 10:49


Hii leo jaridani tunaangazia hali ya wakimbizi wa ndani katika ukanda wa Gaza, na mkutano wa Sita wa Maspika wa Mabunge Duniani uliofanyika jijini Geneva, Uswisi. Makala tunamulika mtazamo mpya wa uchumi wa Dunia kwa mwaka 2025 na 2026, na mashinani tunakwenda nchini Somalia, kulikoni.Harakati za kila uchao kwa raia wa Gaza huko eneo la Palestina linalokaliwa kimabavu na Israeli za kukimbilia chakula huku mashambulizi yakiendelea zimeendelea kusababisha vifo na majeruhi ambapo majeruhi wa hivi karibuni aliyetajwa ni Sahar, mtoto mwenye umri wa miaka 14 aliyepata ulemavu akikimbilia kupokea msaada wa chakula.Mkutano wa Sita wa Maspika wa Mabunge Duniani uliofanyika jijini Geneva, Uswisi, jana Julai 31 umefika tamati baada ya siku tatu za mijadala ambazo zimezaa Azimio la kihistoria linalotoa wito wa "ushirikiano wa kimataifa ulio thabiti na wenye ufanisi zaidi" ili kuendeleza amani, haki, na ustawi. Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani, (IPU), Tulia Ackson kupitia hotuba ya kufunga mkutano huo uliondaliwa kwa ushirikiano wa IPU na Umoja wa Mataifa akadokeza kilichomo katika azimio hilo. Katika makala Leah Mushi anatuletea habari njema kutoka shirika la fedha la kimataifa IMF kuhusu mtazamo mpya wa uchumi wa Dunia kwa mwaka 2025 na 2026.Na mashinani tutakupeleka nchini Ethiopia, kumulika harakati za kujikwamua kiuchumi katikati ya janga la ukame.Mwenyeji wako ni Assumpta, karibu!

Habari za UN
Maspika wa Mabunge wapitisha azimio la kihistoria Geneva, Uswisi

Habari za UN

Play Episode Listen Later Aug 1, 2025 2:22


Mkutano wa Sita wa Maspika wa Mabunge Duniani uliofanyika jijini Geneva, Uswisi, jana Julai 31 umefika tamati baada ya siku tatu za mijadala ambazo zimezaa Azimio la kihistoria linalotoa wito wa "ushirikiano wa kimataifa ulio thabiti na wenye ufanisi zaidi" ili kuendeleza amani, haki, na ustawi. Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani, (IPU), Tulia Ackson kupitia hotuba ya kufunga mkutano huo uliondaliwa kwa ushirikiano wa IPU na Umoja wa Mataifa akadokeza kilichomo katika azimio hilo.

SBS Swahili - SBS Swahili
Taarifa ya Habari 31 Julai 2025

SBS Swahili - SBS Swahili

Play Episode Listen Later Aug 1, 2025 5:56


Wanafunzi milioni tatu nchini Australia wata punguziwa deni zao za elimu, hii ni baada ya muswada wa Labor ulio tazamiwa sana kupitishwa bungeni hii leo.

Habari za UN
31 JULAI 2025

Habari za UN

Play Episode Listen Later Jul 31, 2025 9:56


Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayoturesha katika Jukwaa la Vijana la Baraza la Umoja wa Mataifa la Masuala ya Kiuchumi na Kijamii (ECOSOC) lilifanyika katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani mwezi Aprili mwaka huu wa 2025, ambapo Idhaa hii ilizungumza na Kapwani Kavenuke, kutoka Tanzania kuhusu ujumuishwaji wa vijana katika será za maendeleo.Nchini Somalia ziara ya siku nne ya Naibu Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji IOM Ugochi Daniels imeonesha namna taifa hilo lilivyoathirika vibaya na mabadiliko ya tabianchi hali inayofanya baadhi ya watu kukimbilia maeneo yenye rasilimali chache na hivyo kujikuta wakigombania rasilimali hizo.Huko Gaza mashariki ya kati, eneo la Wapalestina linalokaliwa kimabavu na Israel bado hali si hali kwani njaa ni Kali. Wakati malori ya misaada yakiendelea kuingiza chakula, mafuta na vifaa vya matibabu, mfanyakazi mmoja wa Umoja wa Mataifa anasimulia kumuona baba mmoja wa makamo akiwa amepiga magoti chini akiokota kwa mikono yake na kuweka kwenye fulana yake dengu zilizokuwa zimeanguka kutoka kwenye moja ya malori yanayoingiza chakula Gaza, hii ndio hali halisi. Umoja wa Mataifa umelaani shambulio lililotekelezwa hii leo na majeshi ya Urusi katika mji mkuu wa Ukraine, Kyiv na kusababisha vifo vya watu kadhaa akiwemo mtoto mwenye umri  wa miaka sita huku watu wengine kadhaa wakijeruhiwa..Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili. Onni Sigalla, Mhariri Mwandamizi kutoka Baraza la Kiswahili Tanzania, BAKITA anafafanua maana ya neno MTAGARUKI.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!

Alfajiri - Voice of America
Alfajiri - Julai 31, 2025

Alfajiri - Voice of America

Play Episode Listen Later Jul 31, 2025 29:59


Matangazo ya nusu saa kuhusu habari za mapema asubuhi pamoja na habari za michezo.

Jioni - Voice of America
Jioni - Julai 31, 2025

Jioni - Voice of America

Play Episode Listen Later Jul 31, 2025 29:59


Matangazo ya saa nzima kuhusu habari za kutwa, ikiwa ni pamoja ripoti kutoka kwa waandishi wetu sehemu mbali mbali duniani na kote Afrika Mashariki na Kati, na vile vile vipindi na makala maalum kuhusu afya, wanawake, jamii na maendeleo.

Habari za UN
30 JULAI 2025

Habari za UN

Play Episode Listen Later Jul 30, 2025 9:58


Hii leo jaridani tunaangazia hatua za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi nchini Tanzania, na biashara ndogondogo kwa wananchi wa Rwanda. Makala tunakupeleka nchini Kenya ma Mashinani tunakwenda Geneva Uswisi, kulikoni?Tanzania, kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani (WHO), iko mbioni kuzindua mpango wa “Beat the Heat” yaani “Lishinde Joto”, mpango wenye lengo la kukabiliana na joto kali na hatari za kimazingira katika sehemu za kazi na kwenye matukio makubwa ya kijamii. Anold Kayanda anafafanua zaidi taarifa iliyochapishwa leo na WHO jijini Dar es Salaam, Tanzania.Katika kijiji kimoja nchini Rwanda, ndoto ya muda mrefu ya Chantal Uwizeyimana imegeuka kuwa njia ya kujikwamua kiuchumi. Kupitia mradi wa STARLIT unaotekelezwa na Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Maendeleo ya Kilimo – IFAD, wakulima wadogo kama Chantal wamepata mafunzo, pembejeo na maarifa ya kubadili kilimo kuwa chanzo cha mapato ya uhakika. Sasa si tu kwamba mavuno yameongezeka, bali pia maisha yamebadilika kwa namna isiyotarajiwa. Makala inakupeleka Kenya kwake Kevin Keitany wa Radio washirika Radio Domus akimulika siku ya kimataifa ya urafiki inayoadhimishwa leo Julai 30, ikimulika urafiki katika ngazi ya mtu mmoja mmoja, baina ya watu zaidi ya mmoja, jamii, tamaduni na hata mataifa na mchango wake katika amani na utulivu duniani. Kelvin anamulika urafiki kati ya watu wawili.Na katika mashinani tuelekee jijini Geneva, Uswisi ambako unafanyika Mkutano wa Sita wa Spika wa Mabunge Duniani kumsikia Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani akitoa wito kwa viongozi wenzake kuutetea Umoja wa Mataifa.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!

Habari za UN
Siku ya kimataifa ya urafiki, je wewe wapenda kuwa na rafiki wa aina gani?

Habari za UN

Play Episode Listen Later Jul 30, 2025 3:05


Umoja wa Mataifa kwa kutambua nafasi ya urafiki katika kujenga amani, utulivu na kusongesha maendeleo kuanzia ngazi ya mtu mmoja mmoja hadi ngazi ya mataifa, mwaka 2011 kupitia Baraza lake Kuu, ulitenga Julai 30 kuwa siku ya urafiki duniani.  Umoja wa Mataifa unasema katika wakati ambapo kelele za mgawanyiko zinazidi kuwa kubwa — zikiendeshwa na vita, migogoro, ukosefu wa usawa, na hofu — urafiki unaonekana kuwa wa kishujaa kutokana na unyenyekevu wake. Urafiki huanza na kitu cha utulivu zaidi: mazungumzo, wakati wa pamoja, utayari wa kuonana si kama wageni bali kama wasafiri wenza katika safari ya utu. Je huko Kenya, mkazi mmoja wa Kaunti ya Kajiado, urafiki kwake ni nini? Kelvin Keitany wa Redio washirika Radio Domus amefunga safari na kutuandalia makala hii.

Alfajiri - Voice of America
Alfajiri - Julai 30, 2025

Alfajiri - Voice of America

Play Episode Listen Later Jul 30, 2025 30:00


Matangazo ya nusu saa kuhusu habari za mapema asubuhi pamoja na habari za michezo.

Jioni - Voice of America
Jioni - Julai 30, 2025

Jioni - Voice of America

Play Episode Listen Later Jul 30, 2025 30:00


Matangazo ya saa nzima kuhusu habari za kutwa, ikiwa ni pamoja ripoti kutoka kwa waandishi wetu sehemu mbali mbali duniani na kote Afrika Mashariki na Kati, na vile vile vipindi na makala maalum kuhusu afya, wanawake, jamii na maendeleo.

Habari za UN
29 JULAI 2025

Habari za UN

Play Episode Listen Later Jul 29, 2025 11:42


Hii leo jaridani utasikia muhtasari wa habari utakaoangazia hali ya uhaba wa chakula Gaza, mkutano wa maspika wa bunge duniani na mkutano wa tabianchi na afya. Katika jarida pia utasikia mada kwa kina inayoangazia siku ya kimataifa ya marafiki duniani ambayo ilipitishwa na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mwaka 2011 ikiadhimishwa kila mwaka tarehe 30 Julai. Vijana kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino nchini Tanzania - SAUT wanajadili umuhimu wa siku hii.

SBS Swahili - SBS Swahili
Taarifa ya Habari 29 Julai 2025

SBS Swahili - SBS Swahili

Play Episode Listen Later Jul 29, 2025 16:04


Waziri Mkuu Anthony Albanese amesema anaendeleza juhudi zakupunguza shinikizo za gharama ya maisha, akimulika mpango wakupunguza bei za madawa.

Alfajiri - Voice of America
Alfajiri - Julai 29, 2025

Alfajiri - Voice of America

Play Episode Listen Later Jul 29, 2025 30:00


Matangazo ya nusu saa kuhusu habari za mapema asubuhi pamoja na habari za michezo.

Jioni - Voice of America
Jioni - Julai 29, 2025

Jioni - Voice of America

Play Episode Listen Later Jul 29, 2025 29:59


Matangazo ya saa nzima kuhusu habari za kutwa, ikiwa ni pamoja ripoti kutoka kwa waandishi wetu sehemu mbali mbali duniani na kote Afrika Mashariki na Kati, na vile vile vipindi na makala maalum kuhusu afya, wanawake, jamii na maendeleo.

Habari za UN
Mauaji ya raia Komanda, Ituri, MONUSCO yalaani waasi wa ADF

Habari za UN

Play Episode Listen Later Jul 28, 2025 1:47


 MONUSCO, ambao ni Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa Kulinda Amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, imelaani vikali shambulio lililoanza usiku wa juzi tarehe 26 hadi jana 27 Julai 2025 huko Komanda eneo la Irumu, takribani kilomita 60 kusini-magharibi mwa Bunia mji mkuu wa jimbo la Ituri, mashariki mwa nchi. Anold Kayanda ameifuatilia taarifa hiyo na anatujuza zaidi.Taarifa iliyotolewa na MONUSCO jijini katika mji mkuu wa DRC, Kinshasa imeeleza kwamba kwa mujibu wa taarifa za uhakika, shambulio hilo lililofanywa na wapiganaji wa kundi la waasi wa Allied Democratic Forces (ADF) limesababisha vifo vya raia wasiopungua 43 (wanawake 19, wanaume 15 na watoto 9).Inaripotiwa kuwa waathirika wengi waliuawa kwa kutumia silaha za jadi wakiwa ndani ya nyumba ya ibada. Watu kadhaa walitekwa nyara. Nyumba na maduka pia yalichomwa moto, jambo ambalo limezidisha zaidi hali mbaya ya mazingira ya kibinadamu ambayo tayari ni ya kutisha katika jimbo hilo.Naibu Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwa Masuala ya Ulinzi na Operesheni ambaye pia ndiye Kaimu Mkuu wa MONUSCO, Vivian van de Perre, amenukuliwa akisema, “mashambulizi haya ya kulenga raia wasio na hatia, hasa ndani ya nyumba za ibada, ni ya kushtusha na ni kinyume kabisa na viwango vyote vya haki za binadamu na sheria ya kimataifa ya kibinadamu. MONUSCO itaendelea kushirikiana kwa karibu na mamlaka za DRC ili kuwalinda raia kwa mujibu wa mamlaka yake.”Kwa kushirikiana na mamlaka za eneo, MONUSCO imetoa msaada kwa hatua za awali, ikiwemo kuratibu shughuli za maziko na kutoa huduma za matibabu kwa majeruhi. Wakati huohuo, MONUSCO imeongeza juhudi za kiusalama ndani na nje ya eneo la Komanda kwa kuongeza idadi ya doria katika eneo hilo.MONUSCO imeweka wazi kuwa inasalia na dhamira thabiti ya kushirikiana na mamlaka za DRC na jamii za wenyeji kusaidia kuzuia mashambulizi mengine, kuwalinda raia, kupunguza mvutano, na kuchangia katika kuimarisha utulivu katika maeneo yaliyoathiriwa na machafuko ya kivita.Ujumbe huo wa Umoja wa Mataifa umeeleza masikitiko na ghadhabu kubwa juu ya vitendo hivi vya kikatili, ambavyo ni ukiukaji mkubwa wa sheria ya kimataifa ya kibinadamu na haki za binadamu. Ujumbe huu unatoa rambirambi zake za dhati kwa familia na jamii zilizoathirika na unasisitiza mshikamano wake na wakazi wa maeneo hayo. MONUSCO pia inazitaka mamlaka za DRC kufanya uchunguzi wa kina kuhusu mauaji haya na kuwafikisha wahusika mbele ya sheria.Aidha, MONUSCO imeurudia wito wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwa makundi yote ya waasi kutoka nchi za nje kuweka silaha chini bila masharti na kurejea katika nchi zao za asili.

Habari za UN
28 JULAI 2025

Habari za UN

Play Episode Listen Later Jul 28, 2025 9:58


Hii leo jaridani Assumpta Massoi anamulika mauaji Ituri, DRC; Haki za binadamu hususan suala la Israeli kukalia Palestina kimabavu; Mifumo ya kuzalisha chakula; Mradi wa umwagiliaji kwa kutumia nishati ya sola huko Bidibidi, Uganda. MONUSCO, ambao ni Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa Kulinda Amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, imelaani vikali shambulio lililoanza usiku wa juzi tarehe 26 hadi jana 27 Julai 2025 huko Komanda eneo la Irumu, takribani kilomita 60 kusini-magharibi mwa Bunia mji mkuu wa jimbo la Ituri, mashariki mwa nchi. Anold Kayanda ameifuatilia taarifa hiyo na anatujuza zaidi.Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa haki za binadamu Volker Türk ameyahimiza mataifa yote ulimwenguni kuchukua hatua za haraka ili Israel ikomeshe uwepo wake kinyume cha sheria katika ardhi ya Palestina inayoikalia kimabavu, na kuhakikisha suluhu ya mataifa mawili inapatikana. Tupate taarifa zaidi kutoka kwa Leah MushiKatika makala Sabrina Said anakupeleka Addis Ababa nchini Ethiopia, kumulika mkutano wa Umoja wa Mataifa wa viongozi kuhusu mifumo ya uzalishaji chakula. Mkutano huu ni wa pili na unafanyika kwa siku tatu, leo ikiwa ni siku ya pili. Mashinani:  Mary, Mkimbizi mwenye umri wa miaka 26 kutoka Sudan Kusini anayeishi katika makazi ya wakimbizi ya Bidibidi nchini Uganda. Yeye ni mkulima wa nyanya kutoka kikundi cha wakulima cha Anika ambao ni wanufaika wa mradi wa umwagiliaji wa Sola uliofanikishwa na shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula, WFP.

Alfajiri - Voice of America
Alfajiri - Julai 28, 2025

Alfajiri - Voice of America

Play Episode Listen Later Jul 28, 2025 29:59


Matangazo ya nusu saa kuhusu habari za mapema asubuhi pamoja na habari za michezo.

Jioni - Voice of America
Jioni - Julai 28, 2025

Jioni - Voice of America

Play Episode Listen Later Jul 28, 2025 29:59


Matangazo ya saa nzima kuhusu habari za kutwa, ikiwa ni pamoja ripoti kutoka kwa waandishi wetu sehemu mbali mbali duniani na kote Afrika Mashariki na Kati, na vile vile vipindi na makala maalum kuhusu afya, wanawake, jamii na maendeleo.

Jioni - Voice of America
Jioni - Julai 27, 2025

Jioni - Voice of America

Play Episode Listen Later Jul 27, 2025 29:59


Matangazo ya saa nzima kuhusu habari za kutwa, ikiwa ni pamoja ripoti kutoka kwa waandishi wetu sehemu mbali mbali duniani na kote Afrika Mashariki na Kati, na vile vile vipindi na makala maalum kuhusu afya, wanawake, jamii na maendeleo.

Jioni - Voice of America
Jioni - Julai 26, 2025

Jioni - Voice of America

Play Episode Listen Later Jul 26, 2025 29:59


Matangazo ya saa nzima kuhusu habari za kutwa, ikiwa ni pamoja ripoti kutoka kwa waandishi wetu sehemu mbali mbali duniani na kote Afrika Mashariki na Kati, na vile vile vipindi na makala maalum kuhusu afya, wanawake, jamii na maendeleo.

Habari za UN
25 JULAI 2025

Habari za UN

Play Episode Listen Later Jul 25, 2025 11:03


Hii leo jaridani tunaangazia hali ya kibinadamu Gaza, na Siku ya Kimataifa ya Wanawake na Wasichana wa Asili ya Afrika. Makala inatupeleka nchini Tanzania na mashinani tunakwenda nchini Uganda, kulikoni?Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres, ameonya kuwa mateso yanayoendelea katika Ukanda wa Gaza, eneo la Palestina linalokaliwa kimabavu na Israeli, ni zaidi ya janga la kibinadamu – ni janga la maadili linalopasua dhamira ya jumuiya ya kimataifa.Leo, tarehe 25 Julai, ni Siku ya Kimataifa ya Wanawake na Wasichana wa Asili ya Afrika, ikiwa na kaulimbiu ya mwaka huu: “Kuinuka Pamoja: Wanawake na Wasichana wa Asili ya Afrika Wakiongoza kwa Nguvu.” Idhaa ya Umoja wa Mataifa  imefanya mahojiano na Patricia Da Silva, Mratibu wa Kimataifa wa Timu ya Hakuna Kumwacha Yeyote Nyuma katika shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ya Uzazi na Idadi ya Watu, UNFPA na akafafanua kidogo siku hii inabeba nini hasa. Makala inatupeleka Pemba, visiwani Zanzibar nchini Tanzania, ambapo mpango mpya wa afya ya mama unawasaidia wanawake wajawazito kukabiliana na upungufu wa damu na kujifungua watoto wenye afya. Kupitia Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, kwa ushirikiano na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF na kwa msaada wa kifedha kutoka Wakfu wa Gates, zaidi ya wanawake 16,000 sasa wanapata huduma bora kupitia Virutubisho vya Madini Mbalimbali (MMS) na huduma zilizoboreshwa za kliniki za wajawazito. Assumpta Massoi amefuatilia mradi huo kupitia video ya UNICEF TAnzania.Na katika Arinda Angella, kiongozi wa wanafunzi kutoka Mbarara, Uganda akieleza jinsi ushiriki wake katika mafunzo haya ya uongozi ambayo yameendeshwa kwa ushirikiano wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo UNDP na Kituo cha Mafunzo cha Julius Nyerere unavyompa mwanga mpya kuhusu nafasi ya vijana na wanawake katika kufanikisha Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs).Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!

Habari za UN
Kuinuka Pamoja: Wanawake na Wasichana wa Asili ya Afrika Wakiongoza kwa Nguvu

Habari za UN

Play Episode Listen Later Jul 25, 2025 2:22


Leo, tarehe 25 Julai, ni Siku ya Kimataifa ya Wanawake na Wasichana wa Asili ya Afrika, ikiwa na kaulimbiu ya mwaka huu: “Kuinuka Pamoja: Wanawake na Wasichana wa Asili ya Afrika Wakiongoza kwa Nguvu.” Idhaa ya Umoja wa Mataifa  imefanya mahojiano na Patricia Da Silva, Mratibu wa Kimataifa wa Timu ya Hakuna Kumwacha Yeyote Nyuma katika shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ya Uzazi na Idadi ya Watu, UNFPA na akafafanua kidogo siku hii inabeba nini hasa.

SBS Swahili - SBS Swahili
Taarifa ya Habari 25 Julai 2025

SBS Swahili - SBS Swahili

Play Episode Listen Later Jul 25, 2025 15:40


Australia imefanya makubaliano makubwa na Marekani katika jaribio lakupewa msamaha wa ushuru, kwa kuondoa Marufuku kwa nyama ya Marekani. Hadi sasa, marufuku hiyo ilitumiwa kwa nyama ya ng'ombe walio toka katika nchi za tatu, au ambao asili yao haijulikani.

Alfajiri - Voice of America
Alfajiri - Julai 25, 2025

Alfajiri - Voice of America

Play Episode Listen Later Jul 25, 2025 29:59


Matangazo ya nusu saa kuhusu habari za mapema asubuhi pamoja na habari za michezo.

Jioni - Voice of America
Jioni - Julai 25, 2025

Jioni - Voice of America

Play Episode Listen Later Jul 25, 2025 59:52


Matangazo ya saa nzima kuhusu habari za kutwa, ikiwa ni pamoja ripoti kutoka kwa waandishi wetu sehemu mbali mbali duniani na kote Afrika Mashariki na Kati, na vile vile vipindi na makala maalum kuhusu afya, wanawake, jamii na maendeleo.

Habari za UN
24 JULAI 2025

Habari za UN

Play Episode Listen Later Jul 24, 2025 12:16


Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayomulika utapiamlo kwa watoto na madhila yasiyo fikirika  kwa wananchi wa kawaida huko Mashariki ya Kati, Ukanda wa Gaza eneo la Palestina linalokaliwa kimabavu na Israeli. Pata pia muhtasari wa habari na jifunze Kiswahili.Ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa imeweka bayana jinsi mitandao ya kihalifu duniani inavyoingiza kwenye masoko dawa za binadamu zenye viwango vya juu vya kemikali za sumu ambazo zimesababisha vifo na kuathiri afya ya wagonjwa wengi hasa watoto kwenye nchi za kipato cha chini.Tunasalia na afya ambapo hii leo WHO imethibitisha kwamba Timor-Leste imetokomeza ugonjwa wa malaria, hatua ya kipekee kwa nchi ambayo ilipatia kipaumbele malaria na kuanzisha juhudi za kitaifa na zilizoratibiwa mara tu baada ya kupata uhuru wake mwaka 2002. Mkuu wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Binadamu Volker Türk, amesema maoni ya ushauri yaliyotolewa na Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) kuhusu wajibu wa Mataifa kuhusiana na mabadiliko ya tabianchi ni ushindi mkubwa kwa wote wanaopigania kulinda hali salama ya tabianchi na sayari kwa ajili ya binadamu wote. Halikadhalika ni uthibitisho usio na shaka kuhusu madhara mapana ya mabadiliko ya tabianchi na wajibu mkubwa wa Mataifa, chini ya sheria za haki za binadamu na zaidi ya hapo, kuchukua hatua za haraka ili kuzuia uharibifu.Na katika kujifunza Kiswahili, leo mchambuzi wetu ni Dkt. Josephat Gitonga, kutoka Kenya ambaye ni mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi kwenye kitivo cha tafsiri na ukalimani anatufafanulia maana ya methali "UKIONA KIVULI CHA MTU MFUPI KIMEANZA KUREFUKA JUA KUMEKUCHA AU NI MACHWEO."Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!

SBS Swahili - SBS Swahili
Taarifa ya Habari 24 Julai 2025

SBS Swahili - SBS Swahili

Play Episode Listen Later Jul 24, 2025 6:37


Australia imefanya makubaliano makubwa na Marekani katika jaribio lakupewa msamaha wa ushuru, kwa kuondoa Marufuku kwa nyama ya Marekani. Hadi sasa, marufuku hiyo ilitumiwa kwa nyama ya ng'ombe walio toka katika nchi za tatu, au ambao asili yao haijulikani.

Alfajiri - Voice of America
Alfajiri - Julai 24, 2025

Alfajiri - Voice of America

Play Episode Listen Later Jul 24, 2025 29:59


Matangazo ya nusu saa kuhusu habari za mapema asubuhi pamoja na habari za michezo.

Jioni - Voice of America
Jioni - Julai 24, 2025

Jioni - Voice of America

Play Episode Listen Later Jul 24, 2025 29:59


Matangazo ya saa nzima kuhusu habari za kutwa, ikiwa ni pamoja ripoti kutoka kwa waandishi wetu sehemu mbali mbali duniani na kote Afrika Mashariki na Kati, na vile vile vipindi na makala maalum kuhusu afya, wanawake, jamii na maendeleo.

Habari za UN
23 JULAI 2025

Habari za UN

Play Episode Listen Later Jul 23, 2025 9:58


Hii leo jaridani tunaangazia msaada wa kibinadamu nchini Nigeria, na mradi wa nishati ya sola ya kusaidia wakulima nchini Ethiopia. Makala inakupeleka nchini Afrika Kusini na mashinani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC.Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) nchini Nigeria limesema litalazimika kusitisha msaada wake wa dharura wa chakula na lishe kwa watu milioni 1.3 kaskazini-mashariki mwa nchini hiyo ifikapo mwishoni mwa mwezi huu kutokana na ukata.Mradi unaoendeshwa kwa ushirikiano kati ya serikali ya Ethiopia, Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP), ubalozi wa China wa kutumia nishati jadidifu ya jua kwa umwagiliaji, umeleta matumaini mapya kwa jamii za wakulima katika mkoa wa Sidama, kusini mwa Ethiopia. Katika makalaShirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya watoto UNICEF kwakushirikiana na wakfu wa LEGO wametengeneza video yenye kuonesha familia nne na jinsi zinavyopambana na malezi ya Watoto wakiwa ni wazazi kwa mara ya kwanza. Leah Mushi ametazama video hiyo ya takriban dakika 30 na hapa anakuleta simulizi ya familia kutoka nchini Afrika Kusini.Na katika mashinani Noella Bagula, Mwanachama wa Alleluyah Safe Space ambaye ni mama mkimbizi wa ndani kutoka Goma nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, ambako wanawake na wasichana wanapitia ukatili wa kijinsia katika migogoro. Bi Bagula anasema yeye sasa anajua jinsi ya kujilinda katika hali hatari kufuatia mafunzo yanayoendeshwa na shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu na Afya uzazi, (UNFPA) katika maeneo salama yaliyotengwa kwa ajili yao.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!

Alfajiri - Voice of America
Alfajiri - Julai 23, 2025

Alfajiri - Voice of America

Play Episode Listen Later Jul 23, 2025 29:59


Matangazo ya nusu saa kuhusu habari za mapema asubuhi pamoja na habari za michezo.

Jioni - Voice of America
Jioni - Julai 23, 2025

Jioni - Voice of America

Play Episode Listen Later Jul 23, 2025 29:59


Matangazo ya saa nzima kuhusu habari za kutwa, ikiwa ni pamoja ripoti kutoka kwa waandishi wetu sehemu mbali mbali duniani na kote Afrika Mashariki na Kati, na vile vile vipindi na makala maalum kuhusu afya, wanawake, jamii na maendeleo.

Habari za UN
22 JULAI 2025

Habari za UN

Play Episode Listen Later Jul 22, 2025 10:53


Jaridani leo tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini Tanzania kumulika SDG17 katika mazungumzo ya Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Benki ya CRDB, Tully Esther Mwambapa na idhaa hii hivi karibuni hapa New York.  Pia tunakuletea mutasari wa habari na mashinani.Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa, Volker Türk, leo jijini Geneva Uswisi amekemea amri za hivi karibuni za Israel za kuwahamisha watu Gaza, zilizoambatana na mashambulizi makali katika eneo la kusini-magharibi mwa Deir El Balah na kwamba zimeongeza machungu zaidi kwa mateso ya Wapalestina wenye njaa.Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani, (WFP) limeeleza leo kuwa kutokana na upungufu wa ufadhili, mamilioni ya watu Sudna Kusini wako hatarini kukosa msaada wa chakula. Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa WFP ambaye pia ni Afisa Mkuu wa Uendeshaji, Carl Skau, ambaye hivi karibuni ametembelea Sudan Kusini anasema, "Kote Sudan Kusini, takriban watu milioni 8 wanakabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula, wengi wao wakitegemea msaada kutoka WFP ili kuendelea kuishi.Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Amina J. Mohammed, ametoa wito mzito wa kuchukua hatua za haraka na za kimfumo ili kuongeza kasi ya maendeleo barani Afrika. Ameyasema hayo wakati wa mkutano wa wadau uliofanyika jana Julai 21 katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa, New York, Marekani kujadili matokeo na mapendekezo ya ripoti ya hivi karibuni ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu utekelezaji wa ahadi za maendeleo ya Afrika.Na katika mashinani hii leo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ameweka bayana shuhuda za kuvutia na madhubuti juu ya kwa nini mapinduzi ya nishati mbadala hayaepukiki sasa, pamoja na manufaa yatakayotokana na mabadiliko ya haki kutoka nishati ya kisukuku kuelekea nishati salama. Ushahidi huo madhubuti ni pamoja na makao makuu ya Umoja wa Mataifa kutumia nishati ya sola na Guterres amefika kwenye eneo lenye paneli hizo.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!

SBS Swahili - SBS Swahili
Taarifa ya Habari 22 Julai 2025

SBS Swahili - SBS Swahili

Play Episode Listen Later Jul 22, 2025 14:15


Waziri Msaidizi wa Waziri Mkuu amesema serikali iko tayari kuwafanyia kazi wa Australia, katika kikao cha kwanza cha bunge la shirikisho hii leo.

Alfajiri - Voice of America
Alfajiri - Julai 22, 2025

Alfajiri - Voice of America

Play Episode Listen Later Jul 22, 2025 29:59


Matangazo ya nusu saa kuhusu habari za mapema asubuhi pamoja na habari za michezo.

Habari za UN
Wavuta matoroli, wavaa glovu kutekeleza dakika 67 za kujitolea kwa heshima ya Mandela

Habari za UN

Play Episode Listen Later Jul 21, 2025 3:42


Kujitolea kwa jamii ni jambo ambalo Umoja wa Mataifa na wadau wanalipatia kipaumbele kama njia ya kusaidia kufanikisha Malengo ya Maendeleo Endelevu, SDGs. Ijumaa iliyopita, ofisi ya Masuala ya Kimataifa ya Meya wa jiji la New York, nchini Marekani kwa kushirikiana na Idara ya Mawasiliano ya Kimataifa ya Umoja wa Mataifa pamoja na Ubalozi wa kudumu wa Afrika Kusini kwenye Umoja wa Mataifa, Wakfu wa Kisiwa cha Gavana, Wakfu wa Nelson Mandela na Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa walitekeleza mradi wa kujitolea kwenye kisiwa hicho kama sehemu ya maadhimisho ya siku ya Mandela duniani tarehe 18 Julai mwaka huu wa 2025. Mradi ulilenga kulinda mazingira, je ni kwa vipi? Assumpta Massoi alikuwa shuhuda wetu.

Habari za UN
21 JULAI 2025

Habari za UN

Play Episode Listen Later Jul 21, 2025 9:35


Jaridani leo tunaangazia msaada wa kibinadamu katika ukanda wa Gaza, na uhakika wa chakula  nchini Uganda. Makala tunaangazia mradi wa kulinda mazingira na kazi za kujitolea. Mashinani inamulika utayari wa nchi ya Nigeia kufanikisha Malengo ya Maendeleo Endelevu, SDGs. Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani, WFP, kupitia Apu yake ya kidigitali Gawa Chakula au ShareTheMeal, limeingia ushirikiano na Apu maarufu huko Mashariki ya Kati iitwayo Careem na kuzindua kampeni ya kuchangisha msaada wa dharura kwa watu wanaokumbwa na njaa katika eneo la Gaza na Ukingo wa Magharibi maeneo yanayokaliwa kimabavu na Israeli.Licha ya changamoto za ufadhili, Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) nchini Uganda linasisitiza umuhimu wa usafirishaji katika kutoa msaada wa chakula. Sahir Aslam, Mkuu wa Idara ya Ugavi ya WFP Uganda, akizungumza kutokea huko huko Uganda katika maghala ya shirika hilo anafafanua kila kilomita moja ambayo msaada wa chakula wa WFP unasafiri.Katika makala Assumpta Massoi anatupitisha kwenye kazi ya kujitolea iliyofanyika kuadhimisha siku ya Nelson Mandela Julai 18 hapa Marekani.Na katika mashinani fursa ni yake Esse Oduwan, msichana mwenye umri wa miaka 14 kutoka Nigeria, akihoji utayari wa nchi kufanikisha Malengo ya Maendeleo Endelevu, SDGs baada ya nchi tatu ikiwemo Eswatini na Bangladesh kuwasilisha tathmini za utekelezaji wa Malengo hayo yanayofikia ukomo 2030.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!

Alfajiri - Voice of America
Alfajiri - Julai 21, 2025

Alfajiri - Voice of America

Play Episode Listen Later Jul 21, 2025 29:59


Matangazo ya nusu saa kuhusu habari za mapema asubuhi pamoja na habari za michezo.

Habari za UN
18 JULAI 2025

Habari za UN

Play Episode Listen Later Jul 18, 2025 9:57


Jaridani leo naangazia hafla ya Siku ya Kimataifa ya Nelson Mandela katika makao makuu ya Umoja wa mataifa na ujumbe wa washindi wa Tozo ya Mandela. Makala tunakwenda nchini Angola na mashinani nchini Kenya, kulikoni?Umoja wa Mataifa leo katika makao yake makuu jijini New York, Marekani, umeadhimisha Siku ya Kimataifa ya Nelson Mandela kwa heshima ya maisha na urithi wa shujaa wa mapambano dhidi ya ubaguzi wa rangi, nchini Afrika Kusini, Nelson Rolihlahla Mandela, al maarufu Madiba. Assumpta Massoi amefuatilia na kutuandalia taarifa ifuatayo.Mapema kabla ya kushiriki hafla hii ya utoaji wa tuzo katika siku hii ya kimataifa ya Nelson Mandela hapa New York, Kennedy Odede alizungumza na Zipporah Musau wa Umoja wa Mataifa.Katika makala Sabrina Saidi anatupeleka huko Manispaa ya Caluquembe jimboni Hiula, Kusini Magharibi mwa Angola, Shirika la Afya Duniani (WHO), kwa kushirikiana na mamlaka za mitaa, limeongeza juhudi za ushirikishwaji wa jamii na afua za afya ya umma, ili kukabiliana na mlipuko wa kipindupindu unaoendelea nchini humo. Lengo kuu likiwa ni kuongeza uelewa kuhusu kipindupindu kupitia mikutano ya jamii, jumbe za afya ya umma, na ujenzi wa miundombinu muhimu kama vile vyoo na vituo vya kupata maji safi ya kunywa ndani ya manispaa.Na katika mashinani fursa ni yake Purity Christine, mwanzilishi mwenza wa kampuni ya ShopOkoa, jukwaa la kifedha linalowawezesha wajasiriamali wadogo na wa kati kujiunga na mfumo wa kijamii wa akiba na mikopo nchini Kenya, anasimulia safari yao kupitia Programu ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP ya timbuktoo Fintech, ambapo wamejifunza jinsi ya kuboresha jukwaa lao na kuweka malengo makubwa ya kufikia maelfu ya wafanyabiashara barani Afrika.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!

Alfajiri - Voice of America
Alfajiri - Julai 18, 2025

Alfajiri - Voice of America

Play Episode Listen Later Jul 18, 2025 30:00


Matangazo ya nusu saa kuhusu habari za mapema asubuhi pamoja na habari za michezo.

Habari za UN
17 JULAI 2025

Habari za UN

Play Episode Listen Later Jul 17, 2025 11:05


Jaridani leo tunakuletea mada kwa kina inayoangazia Afrika Mashariki Fest ya nchini Uganda kwa kushirikiana na serikali ya Tanzania na Uganda inayotumia  kampeni yake ya “Twende Zetu Butiama” ili kuyatumimiza malengo hayo.Hii leo shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Ulimwenguni, WHO katika eneo la Palestina linalokaliwa kimabavu na Israeli limeongoza uhamishaji wa wagonjwa 35, wengi wao watoto kwenda Jordan, kwa ajili ya matibabu zaidi kutokana na huduma za afya kuvurugwa Gaza. WHO inasema zaidi ya watu 10,000 Gaza wanahitaji kuhamishiwa nchi nyingine kwa ajili ya matibabu.Harakati za kusaka amani ya kudumua nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC zinazidi kushamiri ambapo hatua za hivi karibuni ni kutoka Muungano wa Afrika, (AU) zikiongozwa na marais wa zamani, Sahle Work Zewde wa Ethiopia, na Catherine Samba-Panza wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, (CAR).kuelekea mkutano wa 30 wa nchi wanachama wa Mkataba wa mabadiliko ya tabianchi, COP30 huko Brazil baadaye mwaka huu, huko Nairobi, nchini Kenya bara la Afrika linajipanga kuhakikisha mkutano huo unakuwa na tija. Dkt. Richard Muyungi, Mwenyekiti wa Kamati ya Wataalamu na mabalozi wanaoshughulikia masuala ya tabianchi barani Afrika, anasema wanachokitaka.Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili hii leo Dkt. Mwanahija Ali Juma, Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili, Zanzibar nchini Tanzania, BAKIZA anafafanua maana ya neno "KIKWANYUKWANYU!.Mwenyeji wako ni Leah Moshi, karibu!

Alfajiri - Voice of America
Alfajiri - Julai 17, 2025

Alfajiri - Voice of America

Play Episode Listen Later Jul 17, 2025 29:59


Matangazo ya nusu saa kuhusu habari za mapema asubuhi pamoja na habari za michezo.

Habari za UN
16 JULAI 2025

Habari za UN

Play Episode Listen Later Jul 16, 2025 10:59


Hii leo jaridani tunaangazia wakazi wa Gaza walioko eneo la Palestina linalokaliwa kimabavu na Israeli; na ujumbe wa Uganda wa hatua zake katika kulitekeleza lengo namba 5 la Usawa wa Kijinsia. Makala tunasalia hapa makao makuu na mashinani tunakwenda Tanzania, kulinkoni?Amri mpya za kuhama zinazotolewa na jeshi la Israeli kwa wakazi wa Gaza walioko eneo la Palestina linalokaliwa kimabavu na Israeli zinazidi kuhatarisha maisha ya makumi ya maelfu ya watu ambao wameshahama mara kadhaa, wakiwemo wagonjwa wanaotakiwa kupata huduma za kusafisha damu mwilini kila wiki.Jukwaa la Kisiasa la Ngazi ya Juu la Umoja wa Mataifa kuhusu Maendeleo Endelevu, HLPF, la mwaka huu wa 2025 linaendelea hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani. Wadau mbalimbali zikiwemo nchi zinazohudhuria zinabadilishana uzoefu, changamoto na mafaniko katika kutekeleza Malengo ya Umoja wa Mataifa ya Mendeleo Endelevu, SDGs. Uganda imeeleza hatua zake katika kulitekeleza lengo namba 5 la Usawa wa Kijinsia.Makala tunasalia hapa New York, Marekani, ambako Sharon Jebichii wa idhaa hii ya Kiswahili amezungumza na kijana kutoka Tanzania anayeshiriki mafunzo kwa vitendo kwenye Idara ya hapa Umoja wa Mataifa ya Masuala ya Kiuchumi na Kijamii, UNDESA. Anasimulia safari yake ya mafunzo kwa vitendo, changamoto, mafanikio na ushauri kwa vijana wengine wanaotamani kufuata nyayo zake.Na katika mashinani Edtrudith Lukanga Mkurugenzi wa Mradi wa Usimamizi wa Mazingira na Maendeleo kwenye Ziwa Victoria, EMEDO. Akishiriki kwenye mkutano hapa New York, MArekani wa kusongesha majawabu bunifu yenye ushahidi ili kuzuia watu kuzama majini, ametaja moja ya majawabu hayo ambayo ni Programu ya Shule ya Usalama kwenye maji huko Tanzania.Mwenyeji wako ni Leah Moshi, karibu!

Habari za UN
15 JULAI 2025

Habari za UN

Play Episode Listen Later Jul 15, 2025 10:57


Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini Tanzania kumulika juhudi za kinamama wajawazito na wanao kuambatana wakihudhuria kliniki kwa ajili ya mimbasalama. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na mashinani.Takribani wapalestina 900 wameuawa katika wiki za hivi karibuni huko Ukanda wa Gaza, eneo linalokaliwa kimabavu na Israeli. wakihaha kupokea chakula. Msemaji wa Ofisi ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa Thameen Al-Kheetan amewaeleza waandishi wa habari Geneva, Uswisi kuwa watu 674 kati yao waliuawa wakiwa kwenye maeneo ya Mfuko wa Kiutu wa Gaza, (GHF) unaoendeshwa na Israeli na Marekani.Wakati huo huo Bwana Al-Kheetan amezungumzia mauaji yanayoendelea Ukingo wa Magharibi ikiwemo Yerusalemu Mashariki akisema, “muathirika mdogo zaidi ni Laila Khatib mwenye umri wa miaka miwili. Alipigwa risasi ya kichwa na jeshi la Israeli akiwa nyumbani kwao kijijini Ash-Shuhada.”Na leo ikiwa siku ya kimataifa ya stadi kwa vijana Sangheon Lee, Mkurugenzi wa Ajira na Sera katika Shirika la Umoja wa Mataifa la Ajira amesema …lazima tuhakikishe kuwa vijana wanapata ujuzi ambao ni wa maana, unaoweza kutumika katika mazingira mbalimbali, na unaotambuliwa na waajiri.Na kaika mashinani tunakupeleka jijini Nairobi, Kenya, ambako kupitia video iliyoandaliwa na washirika wetu Radio Domus, tunamsikia Dennis Mabuku, Mkuu wa Idara ya Usalama, Afya, Mazingira na Ubora katika kampuni ya BOC Kenya. Dennis anaeleza jinsi wanavyoichakata hewa ya kawaida na kuisafisha ili kupata  hewa safi ya oksijeni kwa ajili ya matumizi ya hospitali na mabaki mengine kwa ajili ya matumizi mengine ya viwandani.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!

Habari za UN
14 JULAI 2025

Habari za UN

Play Episode Listen Later Jul 14, 2025 9:51


Hii leo jaridani tunaangazia masuala ya malengo ya maendeleo endelevu, na mradi wa uvuvi unaosaidia kupunguza migogoro Ituri DRC. Makala tunakupeleka nchini Tanzania na mashinani nchini Kenya, kulikoni?Jukwaa la Kisiasa la Ngazi ya Juu la Maendeleo Endelevu, HLPF la mwaka huu wa 2025 limeanza leo hapa katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani ambapo wadau kutoka katika nyanja mbalimbali duniani wanakutana kujadili namna ya kuharakisha utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu, SDGs.Kutoka msituni kupigana upande wa waasi hadi kuingia ziwani na kuwa mtaalamu wa ufugaji wa samaki, ndio simulizi tunayopata kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, simulizi ya matumaini kwa mustakabali wa jamii iliyogubikwa na vita kila uchao.Katika makala tunakupeleka mkoani Mwanza, kaskazini-magharibi mwa Tanzania ambako kuelekea siku ya kimataifa ya vijana na stadi hapo kesho Julai 15, Sabrina Said anazungumza na mmoja wa vijana  anayetumia majukwaa ya kidijitali kutoa elimu ya      uelimishaji rika.Na kaika mashinani leo fursa ni yake Imam Ustaadhi Matano Bin Salim kutoka Kaunti ya Mombasa nchini Kenya, ambaye amewezesha shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF kufika kwenye kituo cha mafunzo ya dini kupatia watoto chanjo. Akisema typhoid ni homa ya tumbo, na measles ni ugonjwa wa surua.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!

Habari za UN
Uwezeshwaji wa vijana mkoani Mwanza Tanzania

Habari za UN

Play Episode Listen Later Jul 14, 2025 3:18


Katika makala tunakupeleka mkoani Mwanza, kaskazini-magharibi mwa Tanzania ambako kuelekea siku ya kimataifa ya vijana na stadi hapo kesho Julai 15, Sabrina Said anazungumza na mmoja wa vijana  anayetumia majukwaa ya kidijitali kutoa elimu ya  uelimishaji rika. 

Habari za UN
Trakoma au Vikope si tatizo tena la kiafya la umma nchini Burundi

Habari za UN

Play Episode Listen Later Jul 11, 2025 1:54


Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani (WHO) leo Julai 11 limetangaza kwamba limeidhinisha Burundi kuwa imefanikiwa kuondoa ugonjwa wa macho unaofahamika kama trakoma au vikope kama tatizo la kiafya la umma, na kuifanya kuwa nchi ya nane katika Kanda ya Afrika ya WHO kufikia mafanikio haya muhimu. Anold Kayanda anafafanua zaidi kuhusu taarifa hii.

Habari za UN
11 JULAI 2025

Habari za UN

Play Episode Listen Later Jul 11, 2025 9:59


Hii leo jaridani tunaangazia masuala ya afya nchini Burundi, na elimu ya upatanishi kwa jamii Ituri nchini DRC. Makala tunakupeleka nchini Kenya kumulika kilimo kichopatia riziki jamii na mashinani tunasalia hapa makao makuu kusikia ujumbe kuhusu haki za wasichana.Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani (WHO) leo Julai 11 limetangaza kwamba limeidhinisha Burundi kuwa imefanikiwa kuoandoa ugonjwa wa macho unaofahamika kama trakoma au vikope kama tatizo la kiafya la umma, na kuifanya kuwa nchi ya nane katika Kanda ya Afrika ya WHO kufikia mafanikio haya muhimu.Huko Djugu, jimboni Ituri, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, wanawake wapatanishi waliopatiwa mafunzo na ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo, MONUSCO, wamewezesha kurejea kwa mazungumzo baina ya jamii za Ezekere na Mandro ambazo kwa miaka kadhaa zilikuwa zinazozana.Katika makala Sharon Jebichii anatupeleka  Kaunti ya Tana River huko Kenya kumulika juhudi za Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo (UNDP) kwa kushirikiana na Mamlaka ya Kitaifa ya Kusimamia Ukame (NDMA) na Serikali za Kaunti katika kilimo, ambayo imeleta mabadiliko na matumaini kwa jamii za wakulima.Na kaika mashinani leo ikiwa siku ya idadi ya watu duniani, nampisha Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu na AFya ya Uzazi, Dkt. Natalia Kanem akizungumzia umuhimu wa takwimu katika kuboresha maisha ya wakazi wa dunia!Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!

Habari za UN
10 JULAI 2025

Habari za UN

Play Episode Listen Later Jul 10, 2025 10:36


Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini Tanzania kushuhudia mafunzo ya ukufunzi kwa wanadhimu wa Umoja wa Mataifa. Pia tunakuletea muhtasari wa habari zikiwemo za mkataba wa amani DRC na Rwanda, UKIMWI, na maadhimisho ya Siku ya kimataifa ya Kiswahili, na uchambuzi wa neno.Wajumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wamekaribisha mkataba wa amani kati ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC na Rwanda uliotiwa saini tarehe 27 mwezi uliopita wa Juni, huku wakishukuru Marekani, Qatar na Muungano wa Afrika kwa juhudi za usuluhishi.Ukata uliosababishwa na wahisani kukata au kupunguza ghafla na kwa kiasi kikubwa ufadhili kwenye miradi ya kupambana na UKIMWI umekuwa na madhara kwa nchi zilizoathiriwa vibaya na ugonjwa huo, imesema ripoti mpya ya shirika la Umoja wa Mataifa la kukabiliana na Ukimwi, UNAIDS.Leo kwenye Ofisi za Umoja wa Mataifa jijini Nairobi, Kenya kumefanyika maadhimisho ya siku ya kimataifa ya lugha ya Kiswahili ambapo wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Juu ya Mangu wametuma ujumbe wao wa umuhimu wa lugha hiyo kupitia ngonjera.Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili na hii leo mchambuzi wetu mlumbi wa Kiswahili Joramu Nkumbi kutoka nchini Tanzania, anafafanua maana ya maneno "CHARAKAMU na BARAKALA!Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!

Habari za UN
09 JULAI 2025

Habari za UN

Play Episode Listen Later Jul 9, 2025 9:59


Hii leo jaridani tunaangazia ziara ya Katibu Mkuu wa UN Amina J. Mohammed akiwa barani Afrika; na Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Viongozi kuhusu Upashanaji wa Taarifa duniani. Makala tunakwenda nchini Burundi na mashinanitunasalia hapa makao makuu, kulikoni?Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Amina J. Mohammed akiwa ziarani barani Afrika ambapo juzi tarehe 7 aliingia nchini Gambia, kwa njia ya mtandao wa X ameonesha namna ziara yake ilivyokuwa ya mafanikio kwa kukutana na viongozi na wadau mbalimbali nchini humo katika harakati za kufanikisha Malengo ya Umoja wa Mataifa ya Maendeleo Endelevu.Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Viongozi kuhusu Upashanaji wa Taarifa duniani, (WSIS) ukiingia siku ya 3 hii leo huko Geneva, Uswisi, washiriki wanapazia sauti umuhimu wa kila mtu kokote pale aliko afikiwe na teknolojia inayomwezesha kupokea taarifa kwa urahisi, usahihi na kwa haraka.Katika makala shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu (UNFPA), kwa kushirikiana na serikali ya Burundi, limekuwa mstari wa mbele katika kuwasaidia vijana wakimbizi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), walioko kwenye kambi ya Musenyi, mkoani Rutana huko Burundi. Kupitia michezo, tamaduni, na shughuli za elimu ya afya ya uzazi, vijana hawa wamepata matumaini mapya na fursa ya kujenga maisha yao upya. Mradi huu unaangazia umuhimu wa kuwekeza kwa vijana walioko katika mazingira magumu ili kuwasaidia kufikia ndoto zao.Na katika mashinani fursa ni yake Dkt. Natalia Kanem, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu na afya ya uzazi UNFPA ambaye katika mahojiano maalum na Idhaa ya Umoja wa Mataifa amesisitiza kuwa kila msichana anahitaji huduma muhimu za afya uzazi ili waweze kuendelea na elimu, akitaja mfano wa kazi zao nchini Kenya.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!