Makala ya kila siku yanayompa fursa msikilizaji kutoa maoni yake juu ya habari zilizopewa uzito wa juu kwa siku husika. Msikilizaji hushiriki kwa kutuma ujumbe mfupi pamoja na kupiga simu.
RFI - Radio France Internationale
Juma hili waskilizaji wetu walikuwa na maoni haya kuhusu taarifa zetu
Katika makala haya tunajadili athari ya vita vya ukraine na Urusi na sasa tishio la vita nyingine kati ya India na Pakistan. Je ni shara ya kutokea kwa vita vya pili vya dunia ? ndilo swali tumekuuliza. Skiza baadhi ya maoni ya waskilizaji.
Shaba ya makala haya inalenga news Zealand ambapo serikali inapendekeza marufuku ya matumizi ya mitandao kwa watoto walio na umri wa chini ya miaka 16, lengo likiwa kuwakinga dhidi ya athari za mitandao. Njia gani wazazi wa kiafrika wanaweza kuwalinda watoto na mitandao ya kijamii? Ndilo swali tumeuuliza na haya hapa baadhi ya maoni yako, skiza makala haya.
Leo mada yetu inajikita kwa siku ya kimataifa ya uhuru wa vyombo vya habari, ambapo Umoja wa Mataifa umesema licha ya baadhi ya nchi kupiga hatua katika ulinzi wa wanahabari, hofu ya uhuru wa habari kuendelea kuminywa inaendelea kutanda. Mwaka jana jumla ya wanahabari 82 walipoteza maisha wakitekeleza majukumu yao. Tuambie nchini mwako vyombo vya habari viko huru? Haya hapa baadhi ya maoni yako, skiza makala.
Kwa sasa macho yakiwamulika makadinali 135 watakaochagua papa mpya ndani ya siku chache zijazo, mjadala kuhusu Papa kutoka Afrika ukishamiri.Mchakato wa kumchagua p
Juma lililopita ripoti ambazo hazijathibitishwa rasmi zilieleza kuwa rais wa zamani wa DRC, Joseph Kabila alirejea nchini Mwake kupitia mji wa Goma unaokaliwa na waasi wa M23 wanaosaidiwa na Rwanda. Hata hivyo hatua yake imeifanya serikali ya Kinshasa, kusimamisha shughuli zote za chama chake cha PPRD, ikikituhumu kushurikiana na waasi hao.Unazungumziaje kurejea kwa rais Kabila?Ndilo swali tumekuuliza katika makala haya.Skiza maoni ya mskilizaji.
Katika makala haya shaba yetu inalenga nchini DRC, ambapo Rais mustaafu wa DRC, Joseph Kabila, ametangaza kurejea nchini humo, kutoka nchini Afrika Kusini ambako amekuwa akiishi kwa zaidi ya mwaka moja , ili kuchangia kutafuta suluhu kwa mzozo wa usalama mashariki mwa nchi yake. Unazungumziaje hatua hii ya Kabila? Ndilo swali tulikuuliza, skiza makala haya kuskia maoni ya waskilizaji wetu.
Kwenye makala haya tunajadili, hatua ya rais wa Marekani, Donald Trump kutangaza kuongeza ushuru kwa bidhaa zote zanazoingizwa Marekani, kutoka mataifa ya Kigeni, hatua inayoonekana kutikisa uchumi wa Dunia. Je unahisi hatua ya rais Trump ni sahihi?Ndilo swali tumeuuliza.Skiza makala haya kujua maoni ya waskilizaji.
Shaba yetu kwenye makala haya inalenga hatua ya Serikali ya Kenya, kueeendelea kuwarejesha mamia ya raia wake waliotapeliwa na kusafirishwa hadi nchini Myanmar kwa ahadi ya kupewa ajira. Nchini mwako visa kama hivi vinaripotiwa?Ndilo swali letu, skiza makala haya kuskia baadhi ya maoni ya waskilizaji.
Katika makala haya tunajadili haja ya kuwepo sheria za kudhibiti mitandao ya kijamii kwa baadhi ya mataifa ya Africa Mashariki. Skiza makala haya kuskia mano ya waskilizaji wetu.
Makala haya ni maoni ya waskilizaji kuhusu ripoti maalum ya namna wananchi wanavyopigwa na wafanyabiashara kwenye mizani wanapopimiwa nafaka mbalimbali za chakula, huku gesi ya kupikia pia ikitajwa.
Shaba yetu leo kwenye makala haya inalenga taifa la Qatar ambapo taifa hilo juma hili lilifanikiwa kuwaleta pamoja marais Felix Tshiesekedi wa DRC na mwenzake wa Rwanda Paul Kagme, katika juhudi za kutafuta suluhu kwa mzozo wa mashariki ya DRC. Unafikiri Qatar itafanikiwa kuzima mzozo wa mashariki mwa DRC. Skiza makala haya kujua baadhi ya maoni ya waskilizaji.
Tunajadili hatua ya Kanisa la Anglikana nchini Kenya, kwa mara nyingine limesisitiza marufuku ya kuwazuia wanasiasa kuzungumza kanisani katika juhudi za kuzuia wanasiasa kufanya siasa kanisani. Je unazungumziaje hatua hii ya kanisa Anglikana nchini Kenya? Skiza makala haya kuskia baadhi ya maoni ya waskilizaji wetu.
Katika makala haya tunajadili hatua ya serikali ya Rwanda, kutangaza kusitisha uhusiano wa Kidiplomasia na taifa la Ubelgiji kutokana na kile Rwanda imesema Ubelgiji kuendeleza propaganda kuihusu kutokana na mzozo wa mashariki mwa DRC. Unazungumziaje hatua ya Rwanda Skiza makala haya kuskia baadhi ya maoni ya waskilizaji.
Tunajadili hatua ya bazara la wakikimbizi la Denmark, kuchachapisha ripoti inayoonesha kuwa, watu zaidi ya milioni 6 duniani watakosa mahali pakuishi ifikapo mwishoni mwa mwaka ujao, kutokana na mizozo, mabadiliko ya tabia nchi na kusitishwa kwa misaada toka Marekani. Unazungumziaje hatua hii? ndilo swali tumeuliza, skiza makala haya kufahamu mengi.
Kila Ijumaa rfi Kiswahili inatoa nafasi kwa mskilizaji kuchaniua mada mbalimbali kuhusu taarifa zetu. Juma hili hizi ni haya ni baadhi ya maoni ya waskilizaji wetu
Shaba yetu inalenga nchini DRC, ambapo taifa la Angola limesema linajaribu kufanikisha mazungumzo ya moja kwa moja kati ya rais wa DRC, Felix Tshisekedi na waasi wa M23, ili kutafuta suluhu la mzozo wa mashariki mwa DRC. Je unafiriki Angola itafanikiwa katika hili?Haya hapa baadhi ya maoni yako.
Mkuu wa majeshi nchini Uganda, ambaye pia ni mwana wa rais Yoweri Museveni, Muhoozi Kainerugaba, amedai wanjeshi wa taifa lake wamewasili Sudan Kusini ili kusaidia jeshi la taifa hilo kutatua mzozo ndani ya serikali ya umoja wa kitaifa Tunakuuliza je mzozo wa Sudan Kusini unastahili kutatuliwa kijeshi?Skiza makala haya kuskiza baadhi ya maoni yenu.
Shaba yetu leoinalenga nchini Kenya ambapo Vijana wameanza kuandamana kupinga kile wanadai wanasiasa kutoa kiasi kikubwa cha pesa kwenye maeneo ya kuabudu ili hali wao hawana ajira. Tumekuuliza hatua hii ni sahihi?Haya hapa baadhi ya maoni yako.
Mwishoni mwa juma lililopita rais wa Kenya William Ruto na kiongozi wa upinzani Raila Odinga walitiliana saini mkataba wa ushirikiano wa kisiasa, wanaosema utasaidia kutatua changamoto zinazowakabili raia wa taifa hilo. Unaamini makubaliano ya viongozi hawa ni sahihi?Ndilo swali tumekuuliza na haya hapa maoni yako.
Nchini Gabon, kiongozi wa kijeshi jenerali Brice Oligui Nguema ametangaza kuwa atagombea urais katika uchaguzi wa mwezi ujao, baada ya kutwaa madaraka kupitia mapinduzi ya kijeshi ya 2023.Hili linajiri wakati huu viongozi wengine wa kijeshi kwenye nchi za Burkina Faso, Mali na Niger wakielekea kuchukua mkondo huo.
Leo ni Ijumaa ,,siku ya mada huru kwenye habari rafiki ambapo Tunakupa nafasi ya kuzungumzia suala lolote ambalo limetokea nchini mwako wiki hii au kile ambacho umekisikia kwenye matangazo yetu ya juma hili
Mada ni kuhusu..kauli ya Rais wa Uganda Yoweri Museveni Akiwa katika ziara ya kawaida kuzungumza na raia wake , ameeleza kuguswa na kusikitishwa na hali ya umasikini anayoshuhudia kwenye nchi yake,,,wakati huu tatizo la umasikini linashuhudiwa pia kwenye mataifa mengine ya ukanda.Tulimuuliza mskilizaji anazungumziaje kauli ya Rais Museveni na je viongozi wa ukanda wamefanya vyakutosha kupambana na umasikini?
Karibu kwenye kipindi cha leo ambapo tunaangazia tangazo la Rais wa DRC, Felix Tschsekedi, kuwa ataunda Serikali ya umoja wa kitaifa, hatua inayokuja wakati huu akiwa katika shinikizo kutoka ndani na nje ya nchi yake, kuhusu namna alivyoshughulikia mzozo wa mashariki mwa nchi yake, wakati huu waasi wa M23 wakichukua miji zaidi.
Ikiwa ni siku ya Ijumaa, ni wakati wa mada huru, yaani tunampatia mskilizaji nafasi kuchangia habari kuu ambazo tumekuwa nazo wiki hii hapa RFI Kiswahili au kutueleza jambo ambalo limetokea nchini mwake juma hili. Leo pia msikilizaji ni siku ya lugha mama, ningependa sana nikusalimie kwa lugha yako mama lakini ningependa kusikia kutoka kwako kwanza. Jambo!
Haya ni makala ya Habari Rafiki tukiangazia maoni ya waskilizaji wa RFI Kiswahili kuhusu mada kwamba, Marekani imeanza mazungumzo na Urusi, lengo likiwa kupata mkataba wa kusitisha vita nchini Ukraine. Ukraine ambayo haijashirikishwa kwenye mchakato huo inasema haitakubali mkataba wowote bila kuhusishwa.Tumemuuliza msikilizaji je, Marekani inaweza kumaliza vita vya Ukraine? Na anafikiri ni kwanini Marekani haijaishirikisha Ukraine na mataifa ya Ulaya kwenye harakati hizi?
Wanamgambo wa RSF wanaopigana na jeshi nchini Sudan na washirika wake wakiwemo wanasiasa wapo jijini Nairobi nchini Kenya, wanakojadiliana kuhusu uundwaji wa serikali mbadala wakati huu inapoendelea na vita.Unazungumzia vipi harakati hizi za RSF ?Unafikiri ni kwanini Kenya imewaruhusu wanamgambo hao kukutana katika nchi yake ?
Makala ya leo yanaangazia Kikao cha viongozi wa Afrika, kilichotamatika rasmi mwishoni mwa juma lililopita nchini Ethiopia, mzozo wa DRC na Sudan ukigubika mijadala yao.Hata hivyo vikao hivyo vimekamilika bila suluhu ya mizozo ya nchi zote mbili, ambapo vyongozi waliishia kwa kutoa wito wa kusitisha mapigano. tulimuuliza msikilizaji iwapo anaridhika na matokeo ya kikao hicho na anadhani nini cha zaidi viongozi hawa wangefanya kukomesha mizozo barani Afrika
Mkutano wa kila mwaka wa viongozi wa Afrika umeanza rasmi jijini Addis Ababa, #Ethiopia ambapo maswala muhimu ikiwemo usalama mashariki mwa #DRC, mapinduzi ya kijeshi na vita dhidi ya makundi ya kijihadi yakitarajiwa kugubika mkutano huu.Tulimuuliza mskilizaji natarajia nini kipya kutoka kwa viongozi wa AU? na iwapo anafikiri viongozi wameshindwa kumaliza changamoto za bara hili..
Kwenye kipindi cha leo tunaangazia kauli tata ya Rais Donald #trump, kuhusu mzozo wa #Gaza, safari hii akitishia kuvunjika kwa mkataba wa usitishaji mapigano, ikiwa Hamas haitawaachia mateka wote ifikapo Jumamosi ya wiki hii.Juma lililopita alidai kuwa nchi yake itachukua udhibiti wa Gaza na kuwahamisha Wapalestina.Tulimuuliza mskilizaji anazungumziaje kauli hiyo ya Trump and je huenda zikachochea mzozo zaidi kati ya #Israel na Hamas?
Makala haya yanaangazia hatua ya Serikali ya kenya kusema hakutakuwa na haja ya mahojiano kwa waomba vitambulisho toka katika maeneo ya mpakani, uamuzi ambao umeibua mjadala kuhusu masuala ya usalama.Tulimuuliza msikilizaji anazungumziaje hatua hiyo ya Kenya vile vile nchini mwake hali ikoje
kwenye makala ya leo tunaangazia hatua ya wakuu wa nchi za #SADC na EAC kutaka kusitishwa mapigano maramoja ,na kutaka kuondoka kwa vikosi vya kigeni mashariki mwa #DRC, pamoja na Serikali ya Kinshasa kuzungumza moja kwa moja na waasi wa #M23 ambapo wito huo umepokelewa kwa hisia mseto na raia wa ukanda.
Kila siku ya ijumaa ni mada huru ambapo Tunampa nafasi msikilizaji kujadili suala lolote ambalo limetokea nchini mwake wiki hii au kile ambacho amekisikiliza kwenye habari zetu juma hili.
Wakuu wa nchi za Afrika walikutana juma hili nchini Tanzania ambapo walijadiliana kuhusu changamoto za upatikanaji wa Nishati ya Uhakika katika mataifa hayo.Licha ya rasilimali za bara la Afrika bado hakuna nishati ya uhakika na endelevu? Bonyeza uskilize maoni mbalimbali.
Uamuzi wa Rais wa Marekani #DonaldTrump, kuagiza kusitishwa kwa muda utowaji wa misaada yote ya kigeni umeibua mjadala na sintofahamu hasa kwa nchi za Afrika, ambazo sekta muhimu ikiwemo afya zinategemea msaada wa Marekani.Tulimuuliwa msikilizaji anazungumziaje hatua hii ya Marekani na Nchi za Afrika zifanye nini kuacha kutegemea misaada ya nchi za Kigeni?
Mizozo inayosibu ukanda wa Afrika ya Mashariki inaendelea kuongezeka, ikiwemo Sudan Kusini na sasa DRC. Viongozi wa Afrika wanasisitiza matatizo ya Afrika sharti kutatuliwa kwa suluhu kutoka Afrika. Je hili linawezekana?
Ukanda wa Afrika unazidi kushuhudia ongezeko la migogoro huku viongozi wakisisitiza Afrika ina majibu ya mizozo hiyo
Mapigano kati ya waasi wa M23 na wanajeshi wa serikali ya DRC yanayoendelea na sasa yamefika jimboni Kivu Kusini,Tume ya Umoja wa Mataifa inayoshughulikia masuala ya kibinadamu OCHA ikisema maelfu ya watu wameendelea kukimbia makaazi yao.Kwenye makala haya tumemuuliza msikilizaji nani wa kulaumiwa kuhusu vita hivi vinavyoendelea? na anafikiri ni kwanini imekuwa vigumu kupata suluhu?