POPULARITY
Katika juhudi za kuimarisha ubunifu na ushindani wa kilimo biashara barani Afrika, Kenya kwa kushirikiana na Ufaransa zimeanzisha mpango wa mafunzo ya matumizi ya teknolojia kwa wakulima wanawake, yakiangazia Akili Mnemba (AI) kuongeza thamani ya mazao, mpango umefikia zaidi ya vikundi na mashirika 1200 ya wanawake wakulima na kuwawezesha kutumia teknolojia za kisasa kuongeza ubora, usindikaji na masoko.
Katika juhudi za kuimarisha ubunifu na ushindani wa kilimo biashara barani Afrika, Kenya kwa kushirikiana na Ufaransa zimeanzisha mpango wa mafunzo ya matumizi ya teknolojia kwa wakulima wanawake, yakiangazia Akili Mnemba (AI) kuongeza thamani ya mazao, mpango umefikia zaidi ya vikundi na mashirika 1200 ya wanawake wakulima na kuwawezesha kutumia teknolojia za kisasa kuongeza ubora, usindikaji na masoko.
Miongoni mwa matukio makubwa ya juma hili ni pamoja na ziara ya rais wa Uganda Yoweri Museveni, iliyotangulizwa na ziara ya wajumbe wa Umoja wa Afrika, nchini Sudan Kusini baada ya makamu wa rais wa nchini hiyo kukamatwa na kuzuiwa nyumbani kwake, kule DRC waasi wa M23 wanaoungwa mkono na Rwanda waripotiwa kujiondoa katika mji wa Walikale mokowani Kivu kaskazini mashariki mwa DRC, tunaangazia Kenya, Uganda, nchi za Afrika mashariki na magharibi pia kwengineko duniani
Ni Jumapili nyingine tunakutana tena katika Makala haya Changu Chako Chako Chako Changu, Makala ambayo hukuletea Historia ya mambo mbalimbali, Utamaduni le parler francophone na Muziki, ambapo leo nakuletea historia ya siku ya kimataifa ya nchi zinazozungumza lugha ya Kifaransa, ama Organisation internationale de la francophonie. Nitakuletea pia ratiba za shughuli za kitamaduni kupitia vituo vya utamaduni wa Ufaransa vya Ukanda, na kwenye Muziki nitakuletea mwanamuziki Frederic Francois. Kumbuka pia kutufollow kwenye mitandao ya kijamii kwa kubonyeza hapa
Msikilizaji juma moja lililopita, mtandao wa wafanyabishara na makampuni ya Ufaransa hapa nchini Kenya, walikutana na wenzao wa Kenya kuangalia namna bora zaidi ya kushirikiana hasa katika masuala ya teknolojia. Kwa mujibu wa takwimu zilizoko hali ya biashara za mtandaoni kikanda inaendelea kuimarika, huku matarajio ya matumizi ya akili mnemba yakionekana kuleta mageuzi makubwa katika sekta hiyo. Victor Moturi alizungumza na Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia wa Kenya, William Kabogo.
Msikilizaji juma moja lililopita, mtandao wa wafanyabishara na makampuni ya Ufaransa hapa nchini Kenya, walikutana na wenzao wa Kenya kuangalia namna bora zaidi ya kushirikiana hasa katika masuala ya teknolojia. Kwa mujibu wa takwimu zilizoko hali ya biashara za mtandaoni kikanda inaendelea kuimarika, huku matarajio ya matumizi ya akili mnemba yakionekana kuleta mageuzi makubwa katika sekta hiyo. Victor Moturi alizungumza na Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia wa Kenya, William Kabogo.
Rais wa Kenya William Ruto na aliyekuwa kiongozi wa upinzani Raila Odinga wameungana kisiasa rasmi, hali ya mzozo wa mashariki mwa DRC Kuchukua sura mpya, vikwazo vya kiuchumi kuikumba nchi ya Rwanda kufuatia uungwaji mkono wake kwa kundi la waasi la M23, Kiongozi wa kijeshi wa Gabon jenerali Oligui Nguema kuwania urais mwezi ujao, mzozo wa kibiashara kati ya Marekani nchi mataifa kadhaa, lakini pia mzozo wa Ukraine na Urusi.
Matangazo ya saa nzima kuhusu habari za kutwa, ikiwa ni pamoja ripoti kutoka kwa waandishi wetu sehemu mbali mbali duniani na kote Afrika Mashariki na Kati, na vile vile vipindi na makala maalum kuhusu afya, wanawake, jamii na maendeleo.
Kwa sehemu kubwa makala ya mtazamo wako imeangazia kuhusu hali ya mashariki mwa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo na mkutano wa pamoja kati ya jumuia ya Afrika mashariki EAC na jumuia ya Nchi za kusini mwa Afrika SADC kutafuta suluhu ya kudumu ya mzozo wa mashariki mwa DRC, huko Gabon upinzani umemtaka kiongozi wa mpito kuweka wazi msimamo wake kuhusu ushiriki wake katika uchaguzi mkuu, na hatua ya rais wa Marekani Donald Trump kukata ufadhili kwa shirika la misaada USAID pia Marekani kudhibiti eneo la Gaza
Akili Mnemba au AI inakuja kwa kasi kubwa sana na kubadilisha mwenendo wa walimu na wanafunzi darasani. Inaleta fursa za kipekee kama kufundisha kwa njia ya kibinafsi na upangaji wa masomo wenye ufanisi zaidi. Lakini pamoja na zana hizi, changamoto zimeibuka: kutegemea sana teknolojia hii, masuala ya kimaadili, na kupungua kwa ujuzi wa kusoma kwa kina. Walimu wanajifunza jinsi ya kuendesha mabadiliko haya, wakiwaonesha wanafunzi jinsi ya kutumia AI kama mshirika wa kufikiri badala ya njia ya mkato ya kuuliza na kunakili. Ubunifu na kufikiri kwa kina vinabaki kuwa ujuzi muhimu zaidi, ambao hakuna teknolojia inayoweza kuchukua nafasi yake. Je, walimu wana mawazo gani? Assumpta Massoi anakupeleka Paris, Ufaransa kusikia mazungumzo ya walimu wawili wakijadili mustakabali wa Akili Mnemba kwenye ufundishaji.
Hii leo jaridani tunaangazia machafuko nchini DRC, na katika elimu tunamsikia msichana wa Afghanistan ambaye ni mnufaika wa ufadhili wa Umoja wa Mataifa. Makala inatupeleka nchini Oaris kumulika matumizi ya AI katika elimu na mashinani tunakwenda nchini Sudan.Mashirika ya Umoja wa Mataifa hii leo yameonya kwamba kuongezeka kwa uhasama kwenye viunga vya mji wa Goma mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) kunakohusisha kundi lisilo la kiserikali linalojihami kwa silaha, M23 kumesababisha watu wengi zaidi kuhama katika eneo hilo lenye utajiri wa madini, huku kukiwa na hofu kwamba mji mkuu wa eneo hilo Goma unaweza kuangukia mikononi mwa wapiganaji hao.Tukiwa bado katika siku ya Elimu duniani kutana na Suhaila msichana mkimbizi kutoka Afghanistan ambaye kupitia mpango wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR wa kuwahamishia wakimbizi katika nchi ya tatu aliwasili Jamhuri ya Kyrgyzstan ambako sio tu alipata maskani ya kudumu na wazazi wake bali pia matumaini na elimu iliyompa ari ya kurejesha matunda yake nyumbani alikotoka.Makala leo ikiwa ni siku ya elimu duniani Assumpta Massoi anakukutanisha na walimu wawili huko Paris nchini Ufaransa wakijadili mustakabali wa Akili Mnemba au AI kwenye ufundishaji darasani. Mahojiano hayo yameandaliwa na shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na UTamaduni, UNESCO.Na katika mashinani Nour Abdallah, Mkimbizi wa ndani katika eneo la Zamzam nchini Sudan kupitia video ya Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula Duniani WFP, anasema janga la njaa limelazimisha jamii kula chakula cha mifugo huku wakiwa na matumaini kwani chakula cha msaada kinaendelea kuwasilishwa kwenye maeneo yaliyoathiriwa na vita.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
Makala hii imeangazia mapigano eneo la mashariki mwa DRC, mvutano wa kisiasa nchini Kenya pamoja na hali ya Sudan, kauli ya rais wa Ufaransa Emmanuel Macron kwamba mataifa ya Afrika hayana shukrani katika kuyataka majeshi ya Ufaransa kuondoka kwenye ardhi zao na mazishi ya aliyekuwa rais wa 39 wa Marekani Jimmy Carter wiki hii
Popote pale ulipo nikukaribishe katika Makala ya jukwaa la michezo ndani ya FRI Kiswahili.Leo tumekuandalia Makala spesheli ambayo inaangazia kushuka pakubwa kwa viwango vya mchezo wa masumbwi nchini Kenya, Makala ambayo tunayapeperusha wiki kadhaa tu baada ya kukamilika kwa michezo ya Olimpiki Jijini Paris nchini Ufaransa. Kwa mara ya kwanza katika, historia ya kenya, hakuna bondia hata mmoja aliyewakilisha taifa katika michezo ya olimpiki jijini Paris. Hatua hii ilizua ngumzo kwa wadau wa mchezo huo.Lakini, Iweje mchezo uliokuwa ukisifika na kuiletea Kenya hadhi katika miaka ya nyuma imedidimia kiasi hiki? Je, ni usimamizi mbaya ama ni ukosefu wa ligi dhabiti au ni kukosa wadhamini wa kuwekeza katika mchezo hili kuiletea fahari inayostahili. Je, Kuna uhasama kati ya wadau ama wasimamizi wameingiwa na kiburi na kujisahau na kuwasahau mabondia?Mwenzangu George Ajowi amezungumza na Mabondia wa zamani, marefa, makocha, mapromota, wanahabari na vile vile wadau wengeni katika sekta hii na kuzungumza nao kuhusiana na matatizo ya ndondi na suhulu ya kufufua mchezo huu katika siku za usoni.
Makala hii imeangazia namna ambavyo nchi zetu zilivyoukaribisha mwaka wa 2025 kwa shamrashamra za kila aina huku wakisema kwaheri kwa mwaka 2024 ulioshuhudia michezo mikubwa zaidi ulimwenguni ya Olimpiki, vita ya Ukraine na kule Gaza, usalama mashariki mwa DRC, Sudan pamoja na kurejea madarakani kwa aliyekuwa rais wa Marekani, Donald Trump.
Matangazo ya nusu saa kuhusu habari za mapema asubuhi pamoja na habari za michezo.
Makala imeangazia namna ambavyo polisi nchini Kenya walivyotawanya maandamano ya wanaharakati waliopinga ukatili dhidi ya wanawake na mauaji nchini humo. Rais wa DRC Felix Tshisekedi alilihutubia taifa mbele y amabunge yote mawili, na kuonyesha kwamba Rwanda inatatiza usalama wa mashariki, siasa za Tanzania, Sudani, na Francois Bayrou ateuliwa kuwa waziri mkuu mpya wa Ufaransa pia hali nchini Israeli.
Habari kuu wiki hii ni pamoja na mkutano kati ya rais wa Marekani anayejiandaa kuondoka madarakani Joe Biden na viongozi wa Afrika huko Lobito Angola, mazungumzo ya amani ya Sudan Kusini kuanza tena baada ya miezi minne, maafisa 20 wa Kenya waliopelekwa Haiti wajiuzulu, rais wa DRC Felix Tshisekedi kukutana na rais wa Rwanda Paul Kagame desemba 15, yaliyojiri Sudan uchaguzi nchini Ghana, na wabunge wa Ufaransa walivyoiangusha serikali ya Michel Barnier lakini pia kanisa kubwa la Notre Dame lafunguliwa jijini Paris Ufaransa, Israel yaendeleza mashambulizi Gaza
Miongoni mwa yale utakayoyasikia kwenye habari ni pamoja na Rais wa DRC, Felix Tschisekedi, kuwataka raia wa nchi yake kuunga mkono mabadiliko ya katiba, , Chama tawala cha CCM nchini Tanzania chaongoza kwa asilimia 99 ya kura.Zaidi ya watu 100 hawajulikani walipo baada ya ajali ya maporomoko ya Udongo nchini Uganda,pia Tutaangazia ziara yake Rais wa Nigeria, Bola Tinubu, nchini Ufaransa, Raia wa Namibia wapiga kura, kisha kimataifa tutaangazia mkutano wa Mawaziri wa mambo ya nje kutoka muungano wa G7,uliofanyika mjini Roma Italia.
Donald Trump achaguliwa kuwa rais wa 47 wa Marekani, Ziara ya rais wa Kenya William Ruto huko Addis Ababa Ethiopia, na Sudan Kusini, na Raila Odinga kuzindua azma yake ya kuwania uenyekiti wa tume ya Umoja wa Afrika, kuelekea uchaguzi huo utakaofanyika Februari mwaka 2025. Mapigano makali kati ya waasi wa M23 na wazalendo mashariki mwa DRC, Umoja wa Mataifa wasema uamuzi wa kuahirishwa uchaguzi nchini Sudani Kusini haukubaliki, Duma Boko atawazwa rasmi kama rais mpya wa Botswana, Uhusiano wa Urusi na Marekani baada ya Trump kushinda uchaguzi
Karibu katika Makala Changu Chako Chako Changu, ambapo Ali Bilali mtangazaji wako asiependa makuu ameungana na Denise Maheho kutoka Lubumbashi kuzungumzia kuhusu iliokuwa barabara ya watumwa zama za ukoloni.Kumbuka pia kutuachia comment na kumfollow mtangazaji wako asiependa makuu @billy_Bilali kwenye mitandao yake ya kijamii Instagram na facebook.
Katika Makala haya Ali Bilali amejielekeza Alliance Francaise ya Nairobi ambayo imeandaa Onyesho la Kwanza la tamthilia ya ‘Mgonjwa Mwitu', utayarishaji wao wa kila mwaka wa maigizo yaliyotolewa na tamthilia za waandishi mashuhuri wa Ufaransa. Kwa maadhimisho ya miaka 75, chaguo ni 'Le Malade Imaginaire' na Molière. Hii ni comedy ya mwisho kuandikwa na Molière. Ingawa ilionyeshwa kwa mara ya kwanza mnamo 1673, kichekesho hiki cha kejeli, mojawapo ya bora zaidi za Moliere, hakijapoteza mvuto wake wa dhati na wa ulimwengu wote.Kumbuka pia kumfollow mtangazaji wako @billy_bilali kwenye mitandao ya kijamii @billy_bilali
Matangazo ya nusu saa kuhusu habari za mapema asubuhi pamoja na habari za michezo.
Washiriki wa hafla ya kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Walimu ililofanyika leo Oktoba 4 katika makao makuu ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) jijini Paris, Ufaransa wamesisitiza wito wa kuthamini mawazo ya walimu katika kuboresha elimu ya ulimwengu. Kama tunavyofahamu, siku yenyewe ya Kimataifa ya Walimu ni kesho Oktoba 5 kama ilivyo ada ya kila mwaka lakini katika makao makuu ya UNESCO hapa Paris Ufaransa, maadhimisho yamefanyika leo kuelekea mkesha wa siku hii muhimu kwa elimu ya ulimwengu.Miongoni mwa waliozungumza ni Mkurugenzi Msaidizi Mkuu wa Elimu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Bi Stefania Giannini, ambaye ameitumia nafasi hii kusisitiza kauli mbiu ya mwaka huu ambayo ni 'Kutambua sauti za walimu.'Anasema, “walimu ni uti wa mgongo wa mifumo ya elimu na mawakala wakuu wa mabadiliko ya kubuni sera za elimu na kufanikisha SDGs. Tunapaswa kuthamini sauti za walimu; hili ndilo lengo kuu la Siku ya Kimataifa ya Walimu mwaka huu.”Kulingana na takwimu zilizotolewa na UNESCO, dunia inahitaji walimu wa ziada milioni 44 ili kufikia elimu ya msingi na sekondari kwa wote ifikapo mwaka 2030. Ingawa mahitaji ya walimu ni makubwa zaidi katika baadhi ya maeneo, uhaba wa walimu ni wa kimataifa.Walimu wanajiondoa kwenye taaluma hii kwa kiwango mara mbili zaidi ya miaka mitano iliyopita, hasa katika elimu ya sekondari. Hii inatokana na hali zao za kazi, zikiwemo mishahara midogo, mzigo mkubwa wa kazi, na ukosefu wa ushiriki katika maamuzi yanayohusu elimu. Akiiangizia changamoto hii, Mkurugenzi wa Kimataifa wa Elimu na Maendeleo ya Vijana katika Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) Bi. Pia Britto, aliyejiunga katika hafla ya leo kwa njia ya video akiwa Pakistani amesema,"Leo nilikuwa na fursa nzuri ya kuzungumza na walimu wengi, ikiwa ni pamoja na mwalimu Tahseen Bashir hapa Islamabad, ambaye amenieleza baadhi ya changamoto wanazokabiliana nazo ikiwa ni pamoja na kufundisha madarasa mengi, uhaba wa vifaa vya kujifunzia, na changamoto za kutoweza kufundisha namna wanavyodhamiria. Lakini pia amenieleza jinsi alivyofurahi kuona wanafunzi wake wakifaulu. Wakati sauti ya mwalimu inaposikilizwa na wakati sauti za walimu zinapopewa kipaumbele, wanajiona kama wadau katika kuboresha elimu kwa wakati wote, na hatua hizo zinahitajika ili kuleta mabadiliko chanya hasa katika hali ngumu zaidi."Siku hii ya kimataifa ya walimu ni mahususi kwa ajili ya kutambua na kusherehekea mchango muhimu wa walimu ulimwenguni kote katika kutoa elimu bora na kujenga mustakabali wa jamii. Pia, ni fursa ya kuangazia changamoto wanazokabiliana nazo walimu.Kutoka hapa Paris Ufaransa, mimi ni Cecily Kariuki..
Hii leo jaridani tunaangazia machafuko nchini Lebanon, na kesho ikiwa ni Siku ya walimu Dunia tunakupeleka Paris, Ufaranza kutsikia toka UNESCO. Makala tunafuatili ajali ya boti iliyozama katika ziwa Kivu nchini DRC na mashinani tunakupeleka Burundi, kulikoni? Mashirikika ya kibinadamu ya Umoja wa Mataifa leo yameonya kwamba hali ya kibinadamu inazidi kuwa mbaya nchini Lebanon wakati mashambulizi ya anga ya Israel yakiendelea kushika kasi na kuwafungisha virago maelfu ya watu, wengi wakikimbia nchi jirani ya Syria ambako nako si shwari.Washiriki wa hafla ya kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Walimu ililofanyika leo Oktoba 4 katika makao makuu ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) jijini Paris, Ufaransa wamesisitiza wito wa kuthamini mawazo ya walimu katika kuboresha elimu ya ulimwengu.Makala inakupeleka huko Goma, jimboni Kivu Kaskazini, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC ambako janga la kuzama kwa boti ya abiria na mizigo liligubika eneo hilo Alhamisi asubuhi za huko.Na mashinani kupitia video ya WHO Afrika, tunamsikia Dkt. Dieudonné Niyongere akizungumza kuhusu msaada muhimu wa washirika katika kuimarisha juhudi za kukabiliana na mlipuko wa Mpox nchini Burundi.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
Mwanasiasa wa upinzani kule Tanzania Tundu Lisu kuishitaki serikali na kampuni ya mawasiliano TIGO kwa jaribio la kumuua, rais wa Kenya William Ruto alisema polisi 2500 watapelekwa Haiti, wakati rais wa DRC Félix Tshisekedi atoa wito kwa jumuia ya kimataifa kuiwekea vikwazo Rwanda kwa kuivamia nchi yake na kushirikiana na waasi wa M23, hali nchini Sudan, siasa za Senegal na maeneo mengine ya Afrika magharibi, mashambulio ya jeshi la Israeli dhidi ya ngome za Hezbollah nchini Lebanon na mengineyo.
Makala hii imeangazia kauli ya rais wa Tanzania kwa mabalozi wanaowakilisha nchi zao ilivyozua gumzo katika uga wa kimataifa, msamaha wa mahakama kwa afisa mkuu wa polisi Kenya, ziara ya mjumbe wake katibu mkuu wa umoja wa mataifa anayehusika na masuala ya kibinadamu ulinzi wa amani Jean Pierre Lacroix huko DRC, UN kughadhabishwa na kuahirishwa uchaguzi wa sudan Kusini, jeshi Ia Israeli lashambulia Hezbollah kwa kulipua vifaa vyao vya mawasiliano na kwengineko duniani.
Makala hii imeangazia mkutano wa tisa kati ya China na Afrika huko Beijing, wafungwa zaidi ya 100 waliuawa katika gereza la makala nchini DRC, Kenya na mkasa wa moto ulivyowaua wanafunzi Kaunti ya Nyeri, uchaguzi kufanyika nchini Tunisia, na nchini Ufaransa Michel Barnier aliteuliwa kuwa waziri Mkuu, miezi miwili baada ya mvutano wa kisiasa nchini Ufaransa, na mambo mengine kwengineko duniani.
Huko Paris, Ufaransa kumekamilika mkutano wa wiki moja ulioandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) ukipatiwa jina Wiki ya Kujifunza Masuala ya Kidijitali au Digital Learning Week ambapo hoja ya Akili Mnemba kudhibiti habari potofu na za uongo imepatiwa kipaumbele.Mkutano huo ulimulika mchango wa teknolojia ya kidijitali katika elimu inayolenga maendeleo badala ya kuyadumaza. Mathalani ni kwa jinsi gani mifumo ya kidijitali inaweza kukabiliana na taarifa potofu kuhusu mabadiliko ya tabianchi.Simon Wanda, Afisa Programu kutoka shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni amefafanua nafasi ya teknolojia kwenye kukabili taarifa hizo.“Mifumo hii inaweza kuchambua na kutathmini yale yanayowekwa kwenye matandao na kutambua taarifa za uongo au za kupotosha.”Mmoja wa washiriki wa mkutano huo ni Doris Mwikali, Mwanasheria na mtetezi wa elimu kutoka Kenya. Tukamuuliza maoni yake kuhusu nafasi ya teknolojia za kidijitali kwa vijana."Ninafahamu kwamba kuna mazungumzo yanaendelea kuhusu jinsi kampuni za mitandao ya kijamii zinavyopambana na habari potofu na za uongo. Lakini nadhani kuna zana mpya za akili mnemba zinazotumika na baadhi ya kampuni, kuhakiki taarifa kwenye mitandao ya kijamii. Ingawa haitakuwa na mchango mkubwa ikilinganishwa na kampuni za mitandao ya kijamii kuchukua jukumu la kudhibiti habari potofu kwenye majukwaa yao, Bado kuna jukumu kubwa kwa akili mnemba katika uhakiki wa taarifa kwenye mitandao ya kijamii, na hiyo imefanywa na mashirika mengi yasiyo ya kiserikali."Nikarejea kwa Bwana Wanda na kumuuliza maoni yake kuhusu maendeleo ya akili mnemba au AI na ujumuishaji wa sauti kutoka pande zote wakati wa kusongesha AI.“Zipo jamii nyingi zetu za kiafrika kama wamaasai wa Kenya na Tanzania, ambao kwa muda mrefu wamekuwa na elimu ya asili kuhusu kuhifadhi mazingira na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, ambayo ni elimu inayofaa kutopuuzwa katika makuzi haya ya teknolojia. Hivyo, hili ni suala la kuhoji sana hasa tunapozingatia kwamba maendeleo katika teknolojia yasiegemee eneo moja la elimu tu, ambayo ni elimu ya magharibi, na kupuuza elimu ya kiasili, ambayo ni tunu.”
Hii leo jaridani mwenyeji wako ni Cecily Kariuki akikupatia yaliyojiri kutoka huko Paris, Ufaransa. Anamulika usalama wa walinda amani wa Umoja wa Mataifa huko DRC; Mradi wa WFP Tanzania kwa vijana wakulima; makala ni ziara ya Naibu Katibu Mkuu wa UN Sudan na mashinani ni afya Tanzania.Afya ya mlinda amani wa Umoja wa Mataifa aliyejeruhiwa katika shambulizi lilitekelezwa na kundi la waasi, CODECO juzi Agosti 28 huko Bali, kaskazini mashariki mwa Djugu jimboni Ituri, Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) inaendelea vizuri, amesema msemaji wa Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani. Taarifa ya Anold Kayanda inaeleza zaidi.Mradi wa Vijana Kilimo Biashara (VKB), unaotekelezwa na shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula duniani (WFP) nchini Tanzania, unawapatia vijana wakulima wadogo ujuzi na rasilimali zinazohitajika, ili kuboresha uzalishaji wa chakula na kujenga uchumi endelevu wakati huu ambao madhara ya El niño [EL NINYO] yanayosabisha ukame na mafuriko yamekuwa dhahiri. Bosco Cosmas na maelezo zaidi.Makala, Evarist Mapesa anatupeleka Sudan kusikia ziara ya ujumbe mzito wa Umoja wa Mataifa nchini humo ukiongozwa na Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Amina J. Mohammed. Mashinani, tunakwenda nchini Tanzania ambako nampisha Daktari bingwa wa ugonjwa wa saratani ya shingo ya kizazi, akihimiza wananchi wa taifa hilo la Afrika Mashariki kusaka huduma dhidi ya ugonjwa huo.
Matangazo haya yanafuatilia habari zilizojitokeza nyakati za mchana na maswala yanayovuma katika mitandao ya kijamii kama sehemu moja muhimu ya upashanaji habari siku hizi.
Kila mmoja achukue hatua kuondokana na vikwazo vya ujumuishaji watu wenye ulemavu - GuterresUmoja wa Mataifa uko tayari kufanya kazi na Kamati ya Kimataifa ya Michezo ya Olimpiki ya Watu wenye Ulemavu (Paralympic) ili kufikia maono ya jamii shirikishi, jumuishi na endelevu, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametoa wito michuano ya Paralympic iking'oa leo jijini Paris, Ufaransa. Anold Kayanda na maelezo zaidi.(Taarifa ya Anold Kayanda)Bwana Guterres aliyeko ziarani nchini Timor Leste, barani Asia, ametuma ujumbe kwa Mkutano wa Kimataifa wa Ujumuishaji watu wenye Ulemavu unaofanyika katika makao makuu ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) jijini Paris Ufaransa ambako michezo ya Olimpiki ya watu wenye ulemavu, Paralimpiki 2024 imeanza kutimua vumbi leo.Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anaamini Michezo ya Olimpiki ya Watu wenye Ulemavu inahimiza kila mtu, kuanzia kwa serikali, mamlaka za mitaa na watoa uamuzi kila mahali, kuchukua hatua ili kuondokana na vikwazo vya ushirikishwaji kamili na wa maana wa watu wenye ulemavu na Umoja wa Mataifa unaahidi kushiriki kikamilifu kutimiza lengo hilo.Aidha katika mkutano huu wa ngazi za juu, UNESCO imeitumia nafasi hiyo kuzindua Kijitabu na mfululizo wa video za mafunzo kuhusu Usawa wa Ulemavu katika Vyombo vya Habari. Kitabu hicho cha mwongozo kina masomo yanayolenga kuwapa wataalamu wa vyombo vya habari maarifa na zana wanazohitaji ili kuhakikisha mashirika yao yanakuwa jumuishi kwa kuwazingatia watu wenye ulemavu.Moja ya vivutio vikubwa katika paralimpiki za mwaka huu zitakazofanyika hadi tarehe 8 ya mwezi ujao Septemba ni timu ya wakimbizi wanane waliopelekwa na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR.
VOA Express pia inafuatilia kwa karibu sana maswala yanayovuma katika mitandao ya kijamii kama sehemu moja muhimu ya upashanaji habari siku hizi.
Matukio ya dunia yaliyokithiri vichwa vya habari ni pamoja na virusi vya Mpox kutangazwa kuwa janga la dharura la kiafya huku bara la Afrika likiathiriwa zaidi, Burundi yamwachia mwanahabari aliyehukumiwa kifungo cha miaka 10, tutaangazia siasa za Tanzania baada ya wanasiasa wa upinzani kukamatwa baadaye wakaachiwa, lakini pia hatua za mazungumzo kule Geneva kuhusu amani nchini Sudan. Pia tutaangazia mgomo wa vyombo vya habari nchini Senegal kadhalika tutachambua wito wa Umoja wa Mataifa kutaka Afrika kupewa kiti cha kudumu katika baraza la usalama la umoja huoKule Gaza, kundi la Hamas limekataa masharti 'mpya' ya upatanishi na Israeli na mazungumzo ya kupata mkataba wa kusitisha vita hivyo, kurejelewa tena wiki hii jijini Cairo, Misri.
VOA Express pia inafuatilia kwa karibu sana maswala yanayovuma katika mitandao ya kijamii kama sehemu moja muhimu ya upashanaji habari siku hizi.
Tuliyokuandalia ni pamoja na uchambuzi wa matokeo ya Olimpiki na mjadala kuhusu wanariadha wanaotarajiwa kung'ara kwenye Olimpiki wiki ijayo riadha zitakapoanza pamoja na matokeo ya Toyota Cup Yanga ikiilaza Kaizer Chiefs huku George Russel akishinda mkondo wa Belgian GP kwenye mashindano ya langalanga.
Makala imeangazia hafla ya ufunguzi wa michezo ya Olimpiki ya Paris siku ya Ijumaa ya wiki hii, huku miundombinu ya treni za umeme ikishambuliwa, rais William Ruto atangaza baraza la mawaziri akiwajumuisha wanasiasa wanne wa upinzani, kesi dhidi ya kiongozi wa muungano wa waasi Corneille Nangaa jijini Kinshasa nchini DRC, Maandamano na kukamatwa kwa vijana kule Uganda, siasa za Afrika Magharibi, na Kaskazini,Joe Biden ajijiondoa katika ki nyang'anyiro cha uchauguzi huku Kamala Harris akiteuliwa kuwa mgombea wa chama cha Demokratic nchini Marekani.
Matangazo ya saa nzima kuhusu habari za kutwa, ikiwa ni pamoja ripoti kutoka kwa waandishi wetu sehemu mbali mbali duniani na kote Afrika Mashariki na Kati, na vile vile vipindi na makala maalum kuhusu afya, wanawake, jamii na maendeleo.
VOA Express ni matangazo mapya yenye mwendo wa kasi yakiangalia habari mpya za mchana na maelezo ya maswala yanayohusu vijana na wanawake.
Makala hii imeangazia hatua ya rais wa Kenya William Ruto ya kuwateua mawaziri wapya baada ya mashinikizo, nchi yake ikishuhudia maandamano ya vijana, Kukamatwa kwa mshukiwa wa mauaji ya watu ambao miili yao ilikutwa jalalani Kware jijini Nairobi akiri kuwaua wanawake 42, rais wa Rwanda Paul Kagame ashinda uchaguzi kwa kishindo, Waasi wa M23 na jeshi la congo FARDC wakubali kusimamisha vita baada ya Marekani kutangaza kuongeza muda wa siku 15 kuruhusu misaada ya kibinadamu...na mengineyo..kwengineko duniani ambako watu wamestushwa ulimwenguni kuhusu hitilafu iliyojitokeza kiteknolojia..-
Nchini Ufaransa licha ya mrengo wa kushoto kuibuka na ushindi kwenye awamu ya kwanza ya uchaguzi wa wabunge, duru ya pili ilikuwa kitendawili kwao baada ya vyama vya mrengo wa ksuhoto kushirikiana na kuzuia vyama vya mrengo wa kulia kupata ushindi. Benson Wakoli anaangazia mbinu alaizotumia rais Emmanuel Macron kuvizuia vyama vya mrengo wa kulia kuibuka na ushindi.Kumsaidia kuangazia hili anaye mchambuzi wa siasa za kimataifa Mali Ali , ambaye yupo Pari Ufaransa, pamoja na Lugete Mussa Lugete akiwa nchini Tanzania eneo la Mwanza.
Makala ya yaliyojiri wiki hii imeangazia hatua ya rais wa Kenya William Ruto kulivunja baraza lake la mawaziri, huku inspekta mkuu wa polisi Japhet Koome akubali kujiuzulu, raia nchini Rwanda wajiandaa kushiriki uchaguzi mkuu wa rais na wabunge nchini Rwanda jumatatu ya julai 15, pia hali ya mapigan yashuhudiwa nchini DRC licha ya wito wa Marekani wa kusitishwa mapigano kwa sababu za kibinadamu.Hali iliyojiri kwenye nchi za Afrika magharibi na kaskazini, Ufaransa, na Marekani.
Tuliyokuandalia ni pamoja na droo ya hatua ya awali kwenye michuano ya klabu bingwa Afrika msimu ujao, matokeo ya Monaco Diamond League, Team Kenya yaanza kuwasili Ufaransa tayari kwa Olimpiki, matokeo ya CECAFA Kagame Cup na tetes iza uhamisho pamoja na uchambuzi wa fainali ya EURO, Copa America na fainali za tenisi kwenye Wimbledon.
Matangazo ya saa nzima kuhusu habari za kutwa, ikiwa ni pamoja ripoti kutoka kwa waandishi wetu sehemu mbali mbali duniani na kote Afrika Mashariki na Kati, na vile vile vipindi na makala maalum kuhusu afya, wanawake, jamii na maendeleo.
Juma hili Ali Bilali yupo kwenye usukani kukuletea Makala Muziki Ijumaa.
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina ambayo inatupeleka Kenya kuangazia awamu ya pili ya mradi wa PLEAD unaoendesha na ofisi ya Umoja wa Mataifa ya dawa na uhalifu UNODC nchini Kenya. Pia tunakuletea habari kwa ufupi zikiwemo za msaada kwa wakulima nchini Ukraine, ripoti ya UNICEF kuhusu watoto katika hatari kubwa ya athari za janga la tabianchi na hafla ya ufunguzi wa Mkutano wa Mkataba Mpya wa Ufadhili wa Kimataifa Paris. Katika kujifunza lugha ya Kiswahili tunabisha hodi kwenye Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania BAKITA kufafanuliwa maana ya neno"TATABISI", salía hapo hapo!Zaidi ya watoto bilioni moja wako katika hatari kubwa ya athari za janga la tabianchi, kwa mujibu wa ripoti mpya kuhusu Hatari za Tabianchi kwa Watoto iliyofanywa na Muungano wa Mpango wa Haki za Mazingira za Watoto (CERI) ambao unahisisha Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF, Plan International na Save the Children. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres hii leo mjini Paris, Ufaransa kupitia hotuba yake kwenye hafla ya ufunguzi wa Mkutano wa Mkataba Mpya wa Ufadhili wa Kimataifa amerelea ombi lake la mageuzi makubwa ya muundo wa fedha wa kimataifa na kuwasilisha mapendekezo yake ikiwa ni pamoja na kichocheo cha Malengo ya Maendeleo Endelevu, (SDG) ili kusaidia nchi zinazoendelea na zinazoibukia kiuchumi ili kuurudisha ulimwengu kwenye mstari wa kufikia Malengo ya Maendeleo Endelevu. Mashirika mawili ya Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo (FAO) na la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) wamezindua mpango wa pamoja kwa ushirikiano na shirika la FSD (Fondation Suisse de Déminage) kusaidia wakulima wadogo na familia za vijijini zilizoathiriwa zaidi na vita huko nchini Ukraine.Na leo katika jifunze Kiswahili tunafafanuliwa maana ya neno "TATABISI" na mtaalam wetu Onni Sigalla, Mhariri mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania, BAKITA.Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!
Ujumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa umewasili nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC , ikiwa ni sehemu ya ziara ya kikazi ya kutathmini hali ya usalama na utekelezaji wa majukumu ya vikosi vya umoja wa mataifa vya kulinda mamani nchini humo MONUSCO. Mara tu baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa jijini Kinshasa, bwana Nicolas de Rivière, Balozi wa kudumu wa Ufaransa kwenye Umoja wa Mataifa amesisitiza kuwa makundi yenye silaha, vyovyote vile yalivyo, lazima yasitishe operesheni zao ili kushiriki katika mchakato wa amani, “Ni wakati muhimu wakuchukua hatua na kwamba vikundi vyote vyenye silaha, kwa hali yao lazima visitishe shughuli zao na washiriki katika mchakato wa kisiasa. Naomba makundi ya kigeni yajiondoe na makundi yanayoungwa mkono na mataifa ya kigeni pia yajiondoe ili hatimaye amani irejee katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo”.Ujumbe huo umekuja nchini DRC wakati kukitarajiwa kuwa na uchaguzi mkuu wa raisi pamoja na wabunge mwezi decembe mwaka huu huku bwana Michel Xavier Biang Balozi wa Gabon kwenye Umoja wa Mataifa akisisitiza lazima uchaguzi huo uwe wa haki, wa uwazi na salama, “ Tuko katika mwaka ambao utakuwa mwaka wa uchaguzi, ujumbe wetu ni wakuhimiza wanasiasa wa pande zote kushiriki katika mchakato wa uchaguzi ambao ni wa uwazi, na wa kuaminika kwa mujibu wa Katiba ya DRC na sheria ya uchaguzi. Tuko hapa kuunga mkono hatua ya MONUSCO na kukumbusha kwamba MONUSCO ni sehemu ya fursa ya suluhu”.Wajumbe hao watakutana na watu kutoka tabaka mbali mbali ikiwemo mashirika ya kiraia na Rais wa DRC Félix Tshisekedi jijini Kinshasa na baadae watakwenda mjini Goma jimboni Kivu Kaskazini, ambako mapigano yamezidi kurindima kwa miezi kadhaa sasa kati ya jeshi la serikali na kundi la wanamkambo wa M23.
Jaridani leo tunakuletea mada kwa kina ambapo leo tunabisha hodi kaunti ya Makueni Kenya kuangazia mchango na faida za mikunde kwa mazingira, wakulima na jamii. Pia tunakuletea habari kwa ufupi zikiwemo afya ya uzazi, intaneti, na msaada wa kibinadamu mashariki ya katiKatika kujifunza Lugha ya Kiswahili tunakwenda Baraza la Kiswahili Tanzania BAKITA kuchambua neno MBWANDA.Kila baada ya dakika 2 mwanamke mwanamke mmoja anafariki dunia kutokana na ujauzito au wakati wa kujifungua duniani kote, imesema leo ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa ikifichua vikwazo vya kutisha dhidi ya afya ya wanawake katika miaka ya karibuni wakati huu ambapo vifo vya wajawazito vimeongezeka au bado viwango vyake vimepungua katika takribani maeneo yote duniani.Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Umoja wa MAtaifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni, UNESCO Audrey Azoulay amefungua mkutano wa kimataifa kuhusu Intaneti kwa ajili ya Kuaminiana huko Paris, Ufaransa na kusema kuzidi kuyoyoma kwa mpaka kati ya ukweli na uongo na kukataliwa kwa taarifa za ukweli za kisayansi, hakukuanzia kwenye mitandao ya kijamii bali kukosekana kwa kanuni za udhibiti na usimamizi na ndio maana uongo unashamirishwa kuliko ukweli.Na nchini Syria, hii leo shirika la Umoja wa Mataifa la afya ulimwenguni, WHO limesafirisha kutoka Gazientep nchini Uturuki, shehena ya tani 34.5 ya vifaa vya matibabu kuingia kaskazini-magharibi mwa Syria kupitia vituo vya mpaka vya Bab Al-Hawa na Bab Al-Salama vikiwa na zaidi ya thamani ya dola milioni 353 ili kuimarisha huduma katika vituo vya afya ambavyo sasa vimezidiwa uwezo kufuatia tetemeko la ardhi lililokumba taifa hilo zaidi ya wiki mbili zilizopita.Na katika Lugha ya Kiswahili na leo Onni Sigalla, Mhariri Mwandamizi kutoka Baraza la Kiswahili la Taifa Tanzania, BAKITA anafafanua neno MBWANDA.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
Zahir Ally Zorro ni mkongwe wa muziki wa dansi na kwa habari ambazo nimepata ni kwamba enzi zake alikua wa moooto sana tena kwenye kila nyanja, kuimba, kuandika, kupiga gitaa na mpaka uvaaji, alikua handsome boy sana na ulimbo kwa kina Dada enzi hizo. Utashi na ucheshi na u sharp wake ndo ambao ulikua unamfanya asimame PEKEE kwenye kadamnasi ya wanamuziki wengi wa kipindi hiko. Naomba nikukumbushe pia kwamba enzi hizo zilikua pia si za kuzichukulia poa kabisa, maana ushindani wa bendi na vipaji binafsi ulikua wa hali ya juu sana, na yeye kama yeye alikua moja ya wale WAKALI wa kipindi hiko. Kama muajiriwa wa Jeshi Mzee Zahir alikua shujaa wa aina yake enzi hizo za ujana wake, kama askari alikua akijituma na ndo maana hakua na cheo cha kinyonge, na kama muandishi na muimbaji na mpiga gitaa pia alikua na nafasi yake ya kipekee. Ukimuangalia hata rangi yake imekaa ki chotara na kwenye mazungumzo haya ana nikumbushia jinsi ambavyo Baba na Mama yake walikutana na ambavyo yeye alizaliwa. Interest yangu zaidi ilikua jinsi ambavyo yeye kama Baba ameweza kuwakuza watoto wake wawili ambao nao wamekuja kuwa wanamuziki wazuri tu tena, Marehemu Maunda Zorro ambaye alifariki mapema mwaka huu (Mwenyezi Mungu amsamehe makosa yake na Amrehemu) na Kaka yake Banana Zorro. Wakati wa kuanza Banana ndo alionekana kuwa angekua super star zaidi ila Maunda nae alipoikamata reli yake kila mtu alimfahamu vizuri. Malezi yao baada ya Marehemu Mama yao nae kutangulia mbele ya haki wakiwa bado wadogo naamini ilikua mtihani mkubwa kwa Mzee Zorro. Ila kwa Rehema za Mwenyezi Mungu Mzee huyo aliweza na ameweza kuhakikisha watoto wake wanakaa kwenye mstari ulio nyooka na kufanya mziki mzuri na kwa heshima na taadhima. Kwenye maisha yangu ya kazi hii nimeshawahi kukutana na Mzee Zorro ila hatukuwahi kufanya maongezi kama haya ingawa nyuma ya ubongo wangu siku zote nilikua nataka kufanya hivyo, na wakati mwengine nilikua nawaza hata ingekua viti VITATU upande ule yaani Baba na watoto wake wawili, kisha nikaona tutakosa kinaga ubaga nyingi, yaani hatutawafaidi sana kama tukiamua kufanya hivyo maana kati ya watatu hao kila mmoja ana story zake ambazo anafaa kupatiwa wasaa wake. Kwa bahati mbaya Maunda alitangulia mbele ya haki na wakati kwa upande wetu ulifika kwa sisi kutaka kukaa chini na Mzee Zorro ili tuyajue yake na kutaka kujifunza kutoka kwake. Mimi na Director wangu wa episode hii tulikua na wakati mgumu kiasi maana pengine tulitaka zaidi ya ambacho tuliweza kupata na hilo Mimi na Alex (Director wangu) tumekubaliana kwamba imetokana na kuondoka kwa Maunda, tunaamini toka Maunda amefariki Mzee Zorro hajarudi katika hali yake ya kawaida, na inaeleweka maana yule hakua tu Binti yake, alikua ni rafiki yake wa karibi saaaana pia. Mzee Zahir alikua analala na Maunda na Banana chumba kimoja mpaka siku chachu tu kabla ya Maunda kukua, na hiyo ilikuja baada ya Banana kumuambia Mzee wake kwamba pengine sasa umefika muda wa wao kulala tofauti. Ananiambia katika episode hii kwamba yeye waala hakua anaona tatizo lolote juu ya hilo maana wenyewe walikua wanaishi tu kwa upendo na maelewano ila baada sasa ya Banana kusema ndo hata yeye alipoona ni kweli muda wa kupeana faragha kwa kila mmoja kuwa na sehemu yake ulikua ushafika. Kwa mtu ambaye walikua wanaonana karibu kila siku na kuongea sana hata baada ya Maunda kuhamia kwa mtu wake ukaribu wao bado ulikua wa karibu sana. Mimi namuombea Mzee Zahir Ally Zorro wepesi katika kipindi hiki kigumu ambacho anapitia na In Shaa Allah arudi katika hali yake ya zamani ya ucheshi na bashasha tele na kwa hii ambayo tumeweza kufanya naye itakupa ufahamu wa kiasi wa legend huyu ambaye pia ni mjuzi wa mambo mengi ya historia na muziki wa jana na wa leo hapa ulimwenguni, ukitaka kuongea na Mzee Zorro hukusu culture ya Mexico, mabadiliko ya tabia nchi, timu ya Taifa ya Ufaransa, mapenzi ya Tabu Ley na Mbilia Bel yote atakua na la kukuambia. Special special human being. Tafadhali enjoy. Love, Salama. --- Support this podcast: https://anchor.fm/yahstonetown/support