Podcasts about desemba

  • 20PODCASTS
  • 630EPISODES
  • 22mAVG DURATION
  • 5WEEKLY NEW EPISODES
  • Dec 18, 2025LATEST

POPULARITY

20172018201920202021202220232024

Best podcasts about desemba

Latest podcast episodes about desemba

Habari za UN
18 DESEMBA 2025

Habari za UN

Play Episode Listen Later Dec 18, 2025 10:38

Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina ya vijana wanaotafuta fursa za mafunzo kwa vitendo. Umoja wa Mataifa ni moja ya mashirika ya kimataifa yanayotoa fursa hii kwa vijana kutoka duniani kote kuja hapa Makao Makuu jijini New York Marekani au hata katika nchi husika.Ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa iliyotolewa leo imefichua mauaji ya kutisha, ubakaji na matumizi ya njaa kama silaha ya vita katika kambi ya Zamzam, Darfur, Sudan. Kwa mujibu wa ofisi ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa OHCHR, raia wasiopungua 1,013 waliuawa katika mashambulizi ya siku tatu ya wanamgambo wa RSF mwezi Aprili, huku zaidi ya watu 400,000 wakilazimika kukimbia makazi yao.Leo, katika maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wahamiaji, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amemulika mchango mkubwa wa mamilioni ya wahamiaji duniani, wakati uhamiaji ukiendelea kuwa mgumu zaidi kutokana na migogoro, majanga yanayohusiana na tabianchi na shinikizo za kiuchumi. Ameeleza kuwepo kwa viwango vya juu zaidi vya watu waliolazimika kuhama makazi yao na idadi kubwa zaidi kuwahi kushuhudiwa ya vifo vya wahamiaji wakiwa safarini, huku akisisitiza kuwa uhamiaji salama na unaosimamiwa vyema unaweza kuchochea ukuaji wa uchumi, ubunifu na maendeleo katika nchi za asili na zinazopokea wahamiaji. Guterres amesema, “Uhamiaji unapokuwa salama na unasimamiwa vyema, si janga la kuogopa, bali ni nguvu kubwa ya kuleta mema.”.Na Ama K. Babebrese Balozi mwema wa kitaifa wa shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji IOM mwenye asili ya Ghana ambaye sasa ni muhamiaji nchini Uingereza, katika siku hii ya uhamiaji ametoa ujumbe maalum akisema "Napenda kumtia moyo kila mtu kwamba tunaweza kuwa tofauti, hadithi zetu za uhamiaji ni tofauti tumetoka kwenye mazingira tofauti lakini kitu cha muhimu ni kwamba kama jamii sisi ni kitu kimoja. Uhamiaji ndio hadithi yangu”.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!

Habari za UN
17 DESEMBA 2025

Habari za UN

Play Episode Listen Later Dec 17, 2025 11:14

Hii leo jaridani tunaangazia tiba asili, machafuko katika jimbo la Kivu Kusini nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC na ubakaji unaotumika kama silaha ya vita nchini humo humo.Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa Duniani WHO, linaweka mkazo mpya wa kisayansi katika tiba asili au mitishamba, wakati mawaziri, wanasayansi na viongozi wa jamii za asili kutoka zaidi ya nchi 100 wakikutana mjini New Delhi India kuanzia leo kuangazia mchango wa tiba za asili.Kuongezeka kwa machafuko katika jimbo la Kivu Kusini nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC kumesababisha watu wengi kuyahama makazi yao ndani na kumbilia kusaka hofadhi nchi Jirani ya Burundi. Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya wakimbizi limeeleza mpaka sasa karibu wakimbizi 64,000 tayari wamewasili Burundi, na idadi ikitarajiwa kuongezeka.Ubakaji unaotumika kama silaha ya vita huacha majeraha yasiyofutika ya mwili,  akili na ya roho. Katika ushuhuda huu wenye nguvu, manusura mmoja kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC ambaye sasa anaishi kama mkimbizi nchini Burundi, anasimulia safari yake ya maumivu baada ya kunusurika ukatili wa kingono uliomsababishia majeraha makubwa ya mwili, ikiwemo fistula, pamoja na makovu ya kina ya kihisia.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!

Habari za UN
16 DESEMBA 2025

Habari za UN

Play Episode Listen Later Dec 16, 2025 11:45

Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini Kenya kwake Afisa Habari wa UN Stella Vuzo ambaye kandoni mwa mkutano wa UNEA-7 uliokunja jamvi mwishoni mwa wiki, alizungumza na Frida Amani, Mchechemuzi wa UNEP wa masuala ya mazingira.Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani, WHO, linasema aina mpya ya virusi vya mafua inaenea kwa kasi duniani, ikiwa imeripotiwa katika zaidi ya nchi 30. WHO wanasema licha ya aina hiyo kutosababisha ugonjwa mkali zaidi wa mafua, chanjo bado ni kinga bora zaidi dhidi ya madhara makubwa na kulazwa hospitalini na inawahimiza wananchi, hasa makundi yaliyo hatarini, kupata chanjo mapema huku ikionya kuwa msimu huu wa likizo unaweza kuongeza maambukizi ya magonjwa ya njia ya hewa.Tuelekee Bujumbura Burundi ambapo maelfu ya wakimbizi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia Congo wamepatiwa hifadhi baada ya kukimbia machafuko nchini mwao. Innocent Chubaka kutoka shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR aliyeko katika kambi ya muda ya Mugara katika jimbo la Rumonge nchini Burundi anasema “tumepokea idadi kubwa ya wakimbizi wa Congo ambao wamefika kupitia njia ya ziwa wakiwa na mitumbwi kuu kuu.Na kwa mara nyingine tena Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa Volker Türk amezisihi pande zote katika mzozo nchini Sudan na Mataifa yenye ushawishi kuhakikisha mapigano yanasitishwa mara moja na kuzuia ukatili. Turk amelaani vikali mauaji ya raia zaidi ya watu 104 pia mauaji ya walinda amani sita wa Umoja wa Mataifa katika mashambulizi ya ndege zisizo na rubani kwenye kambi ya Umoja wa Mataifa huko Kaduguli, Kordofan Kusini, mnamo Desemba 13.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!

Habari za UN
15 DESEMBA 2025

Habari za UN

Play Episode Listen Later Dec 15, 2025 9:59

Hii leo jaridani tunaangazia kilichojiri katika Mkutano wa COSP11 kuhusu ufisadi mjini Doha Qatar, haki za kibinadamu na vijana nchini Kenya, afya ya akili ikimulika upweke na jinsi unavyoweza kuepukana nayo.Mkutano mkubwa zaidi duniani wa kupambana na rushwa au ufisadi umeanza leo Desemba 15 mjini Doha nchini Qatar kwa wito wa kutumia teknolojia zinazoibuka katika mapambano dhidi ya rushwa na kushughulikia uhusiano wake na uhalifu wa kupangwa na makosa mengine ya kifedha.Haki ni msingi wa Kila siku, hiyo ndio ilikuwa kaulimbiu ya siku ya Haki za binadamu mwaka huu iliyoadhimishwa wiki iliyopita. Lakini kila uchao haki za binadamu zinaendelea kukiukwa kuanzia nyumbani hadi kwenye mtandao. Kwa kutambua umuhimu wa kushirikisha vijana katika kupambana na ukiukwaji wa haki hasa mtandaoni, Ofisi ya Umoja wa Maataifa ya Haki za Binadamu (OHCHR) jijini Nairobi Kenya umewakusanya vijana kujadiliana nao na kuwapa mafunzo ya kumakinika hasa mtandaoni.Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya duniani WHO linaendelea na mfululizo wa programu ya kuiunganisha jamii au Social Connection ikiwa na lengo la kusaidia watu kutojitenga na kujihisi wapweke, mmoja kati ya walionufaika wa programu hiyo ni Roz, binti mwenye umri wa miaka 21 raia wa India, aliyehisi upweke mkubwa wakati baba yake alipokuwa akipambana na ulevi.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!

Habari za UN
Mkutano wa kupambana na rushwa waanza kwa wito wa kutumia Akili Mnemba (AI)

Habari za UN

Play Episode Listen Later Dec 15, 2025 2:13

Mkutano mkubwa zaidi duniani wa kupambana na rushwa au ufisadi umeanza leo Desemba 15 mjini Doha nchini Qatar kwa wito wa kutumia teknolojia zinazoibuka katika mapambano dhidi ya rushwa na kushughulikia uhusiano wake na uhalifu wa kupangwa na makosa mengine ya kifedha. Selina Jerobon na maelezo zaidi.

Alfajiri - Voice of America
Alfajiri - Desemba 15, 2025

Alfajiri - Voice of America

Play Episode Listen Later Dec 15, 2025 29:59

Matangazo ya nusu saa kuhusu habari za mapema asubuhi pamoja na habari za michezo.

desemba
Jioni - Voice of America
Jioni - Desemba 15, 2025

Jioni - Voice of America

Play Episode Listen Later Dec 15, 2025 30:00

Matangazo ya saa nzima kuhusu habari za kutwa, ikiwa ni pamoja ripoti kutoka kwa waandishi wetu sehemu mbali mbali duniani na kote Afrika Mashariki na Kati, na vile vile vipindi na makala maalum kuhusu afya, wanawake, jamii na maendeleo.

Kwa Undani - Voice of America
Kwa Undani - Desemba 15, 2025

Kwa Undani - Voice of America

Play Episode Listen Later Dec 15, 2025 29:59

Kwa Undani ni matangazo ya dakika 25 yanayochambua habari kwa undani zaidi na kumpa msikilizaji maelezo ya kina kuliko ilivyo kawaida kuhusu tukio au swala lililojitokeza katika habari.

desemba
VOA Express - Voice of America
VOA Express - Desemba 15, 2025

VOA Express - Voice of America

Play Episode Listen Later Dec 15, 2025 29:59

VOA Express ni matangazo mapya yenye mwendo wa kasi yakiangalia habari mpya za mchana na maelezo ya maswala yanayohusu vijana na wanawake. Matangazo haya yanafuatilia habari zilizojitokeza nyakati za mchana na ripoti za kina za habari ambazo hazisikiki sana katika matangazo mengineyo. VOA Express pia inafuatilia kwa karibu sana maswala yanayovuma katika mitandao ya kijamii kama sehemu moja muhimu ya upashanaji habari siku hizi.

express desemba
Jioni - Voice of America
Jioni - Desemba 14, 2025

Jioni - Voice of America

Play Episode Listen Later Dec 14, 2025 29:59

Matangazo ya saa nzima kuhusu habari za kutwa, ikiwa ni pamoja ripoti kutoka kwa waandishi wetu sehemu mbali mbali duniani na kote Afrika Mashariki na Kati, na vile vile vipindi na makala maalum kuhusu afya, wanawake, jamii na maendeleo.

Changu Chako, Chako Changu
Kumbukumbu ya Makala za mwaka 2025 sehemu ya kwanza Desemba 14 2025

Changu Chako, Chako Changu

Play Episode Listen Later Dec 14, 2025 20:06

Katika Makala haya mtagazaji wako Ali Bilali anakukumbusha baadhi ya makala zilizoruka hewani katika mwaka 2025 ikiwa ni sehemu ya kwanza.

kwanza makala mwaka muziki sehemu desemba katika makala ali bilali
Jioni - Voice of America
Jioni - Desemba 13, 2025

Jioni - Voice of America

Play Episode Listen Later Dec 13, 2025 29:59

Matangazo ya saa nzima kuhusu habari za kutwa, ikiwa ni pamoja ripoti kutoka kwa waandishi wetu sehemu mbali mbali duniani na kote Afrika Mashariki na Kati, na vile vile vipindi na makala maalum kuhusu afya, wanawake, jamii na maendeleo.

Habari za UN
12 DESEMBA 2025

Habari za UN

Play Episode Listen Later Dec 12, 2025 12:23

Hii leo jaridani tunaangazia machafuko nchini Sudan, mkutano unaomulika hatua za tabianchi barani Afrika UNEA7, na juhudi za vijana nchini Kenya za kujikwamua kiuchumi kupitia kilimo endelevu.Nchini Sudan, barani Afrika, wasiwasi mkubwa unaendelea kuhusu makumi ya maelfu ya watu wanaoaminika kuwa bado wamenaswa mjini El Fasher katika eneo la Darfur,magharibi mwa nchi lakini mashirika ya misaada ya Umoja wa Mataifa yanaamini kwamba huenda yakaruhusiwa kufika katika mji huo uliogubikwa na mapigano.Leo Dunia inapoadhimisha miaka kumi tangu Mkataba wa Paris wa mabadiliko ya Tabianchi kupitishwa, wataalamu wa masuala ya tabianchi barani Afrika wanasema maadhimisho haya ni wakati wa kupima hatua zilizofikiwa lakini pia kukabili pengo linalopanuka kati ya sera na utekelezaji wa hatua za tabianchi.Kutoka mashambani hadi kwenye majukwaa ya kidijitali, vijana wa kaunti ya Kirinyaga nchini Kenya wanaongoza enzi mpya ya kilimo kinachoendana na mabadiliko ya tabianchi. Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya Watoto UNICEF limeunga mradi wa vijana uitwao Empowering Kenyan Youth in Agribusiness and Nutrition (EKYAN) kuwawezesha vijana kwa mafunzo ya vitendo na zana muhimu ili kukuza biashara zao za kilimo, kuimarisha mifumo ya chakula ya ndani, na kujenga jamii zinazohimili mabadiliko ya tabianchi.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!

Alfajiri - Voice of America
Alfajiri - Desemba 12, 2025

Alfajiri - Voice of America

Play Episode Listen Later Dec 12, 2025 30:00

Matangazo ya nusu saa kuhusu habari za mapema asubuhi pamoja na habari za michezo.

desemba
Jioni - Voice of America
Jioni - Desemba 12, 2025

Jioni - Voice of America

Play Episode Listen Later Dec 12, 2025 59:59

Matangazo ya saa nzima kuhusu habari za kutwa, ikiwa ni pamoja ripoti kutoka kwa waandishi wetu sehemu mbali mbali duniani na kote Afrika Mashariki na Kati, na vile vile vipindi na makala maalum kuhusu afya, wanawake, jamii na maendeleo.

VOA Express - Voice of America
VOA Express - Desemba 12, 2025

VOA Express - Voice of America

Play Episode Listen Later Dec 12, 2025 30:00

VOA Express ni matangazo mapya yenye mwendo wa kasi yakiangalia habari mpya za mchana na maelezo ya maswala yanayohusu vijana na wanawake. Matangazo haya yanafuatilia habari zilizojitokeza nyakati za mchana na ripoti za kina za habari ambazo hazisikiki sana katika matangazo mengineyo. VOA Express pia inafuatilia kwa karibu sana maswala yanayovuma katika mitandao ya kijamii kama sehemu moja muhimu ya upashanaji habari siku hizi.

express desemba
Kwa Undani - Voice of America
Kwa Undani - Desemba 12, 2025

Kwa Undani - Voice of America

Play Episode Listen Later Dec 12, 2025 29:59

Kwa Undani ni matangazo ya dakika 25 yanayochambua habari kwa undani zaidi na kumpa msikilizaji maelezo ya kina kuliko ilivyo kawaida kuhusu tukio au swala lililojitokeza katika habari.

desemba
Habari za UN
11 DESEMBA 2025

Habari za UN

Play Episode Listen Later Dec 11, 2025 11:30

Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini Sudan Kusini kufuatilia mradi wa kilimo cha mpunga ulivyoleta ustawi kwa jamii ya katikati mwa Sudan unaofanikishwa kwa msaada wa mafunzo wa walinda amani wa UN kutoka Korea Kusini wanaohudumu katika UNMISS kupitia wanasayansi na wakulima wa eneo la Bor katika. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na ufafanuzi wa methali.Mapigano makali mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo yamesababisha vifo vya zaidi ya raia 70, kuwafurusha watu zaidi ya 200,000, na kusitisha msaada wa chakula kwa maelfu. Umoja wa Mataifa unasema hali katika Kivu Kusini imezorota kwa kasi, huku msaada wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula WFP ukisimama na shule zaidi ya 30 zikigeuzwa makazi ya dharura. Katika taarifa yake, Naibu Msemaji wa Umoja wa Mataifa, Farhan Haq, amesema hali imefikia kiwango cha hatari, akionya: “Familia zinazoishi kwa njaa sasa zinagawana chakula chao cha mwisho na watu waliokimbia makazi. Hii ni dharura inayovuka mipaka.” UN inazitaka pande zote kusitisha mapigano mara moja na kuruhusu misaada kufika kwa walio hatarini.Mkutano wa kikao cha 7 wa Baraza La Mazingira la Umoja wa Mataifa UNE-7 unaeelekea ukingoni jijini Nairobi Kenya na miongoni mwa washiriki ni kijana mwanaharakati wa mazingira kutoka asasi ya Umoja wa Mataifa YUNA nchini Tanzania Ally MwamzoraNa leo Umoja wa Mataifa unaadhimisha Siku ya Kimataifa ya Milima, ukisisitiza umuhimu wa milima kama “kitovu cha maji ya dunia.”  Kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo FAO, takriban asilimia 70 ya maji safi ya Dunia yamehifadhiwa kama theluji au barafu, yakitoa mito inayosambaza maji ya kunywa, kilimo, viwanda, na umeme wa maji na takriban watu bilioni mbili, ikiwa ni pamoja na jamii nyingi za asili, wanategemea maji ya milima kwa mahitaji yao ya kila siku, maisha, na tamaduni zao. Wataalamu wanasisitiza kuwa kulinda mazingira ya milima ni muhimu ili kuhakikisha upatikanaji wa maji kwa vizazi vijavyo.Katika kujifunza lugha Kiswahili, leo mchambuzi wetu ni Dkt. Josephat Gitonga, ambaye ni Mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi nchini Kenya,  kwenye kitivo cha Tafsiri na Ukalimani anafafanua maana ya methali "“MWENDAWAZIMU HAPEWI UPANGA"Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!

Alfajiri - Voice of America
Alfajiri - Desemba 11, 2025

Alfajiri - Voice of America

Play Episode Listen Later Dec 11, 2025 29:59

Matangazo ya nusu saa kuhusu habari za mapema asubuhi pamoja na habari za michezo.

desemba
Jioni - Voice of America
Jioni - Desemba 11, 2025

Jioni - Voice of America

Play Episode Listen Later Dec 11, 2025 29:59

Matangazo ya saa nzima kuhusu habari za kutwa, ikiwa ni pamoja ripoti kutoka kwa waandishi wetu sehemu mbali mbali duniani na kote Afrika Mashariki na Kati, na vile vile vipindi na makala maalum kuhusu afya, wanawake, jamii na maendeleo.

VOA Express - Voice of America
VOA Express - Desemba 11, 2025

VOA Express - Voice of America

Play Episode Listen Later Dec 11, 2025 30:00

VOA Express ni matangazo mapya yenye mwendo wa kasi yakiangalia habari mpya za mchana na maelezo ya maswala yanayohusu vijana na wanawake. Matangazo haya yanafuatilia habari zilizojitokeza nyakati za mchana na ripoti za kina za habari ambazo hazisikiki sana katika matangazo mengineyo. VOA Express pia inafuatilia kwa karibu sana maswala yanayovuma katika mitandao ya kijamii kama sehemu moja muhimu ya upashanaji habari siku hizi.

express desemba
Kwa Undani - Voice of America
Kwa Undani - Desemba 11, 2025

Kwa Undani - Voice of America

Play Episode Listen Later Dec 11, 2025 29:59

Kwa Undani ni matangazo ya dakika 25 yanayochambua habari kwa undani zaidi na kumpa msikilizaji maelezo ya kina kuliko ilivyo kawaida kuhusu tukio au swala lililojitokeza katika habari.

desemba
Habari za UN
10 DESEMBA 2025

Habari za UN

Play Episode Listen Later Dec 10, 2025 12:12

Hii leo jaridani tunaangaziz siku ya Haki za Binadamu tukikuletea ujumbe wa Volker Türk, Safari ya manusura wa usafirishaji haramu wa binadamu, na vikosi vya 4 na 5 vya ulinzi wa amani kutoka Tanzania nchini DRC.Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa, Volker Türk, ametumia Siku ya Haki za Binadamu hii leo kutoa onyo kali akisema ulinzi wa haki za binadamu uko mashakani wakati migogoro na ukandamizaji vinaongezeka kwa kasi isiyo na mfano.Kwa manusura wengi wa usafirishaji haramu wa binadamu, msaada hukatika mapema mno. Kutokana na rasilimali chache na mifumo isiyotoa huduma za muda mrefu, wengi hutolewa kwenye mfumo bila kupata usaidizi wa kutosha wa kisaikolojia au utambuzi unaozidi simulizi zao. Malaika Oringo, mama, mwanaharakati, na manusura wa usafirishaji  haramu wa binadamu ameamua kubadilisha hali hiyo. Kama mwanzilishi wa shirika la Footprint to Freedom, linaloongozwa na manusura na linalolenga kuwawezesha na kuwarejesha katika jamii waathiriwa wa usafirishaji haramu wa binadamu, anatetea kuhakikisha sauti za manusura zinakuwa kiini cha utungaji wa sera na hatua za serikali duniani.Kikosi cha 4 cha ulinzi wa amani kutoka Tanzania kinachohudumu chini ya mwamvuli wa FIB MONUSCO, kimehitimisha rasmi jukumu lake la ulinzi wa amani nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya kongo DRC kwa gwaride maalumu la makabidhiano lililofanywa na Tanzqrf ya 4 pamoja na Tanzqrf ya 5 katika makao makuu ya kikosi hico mjini Beni Mavivi katika jimbo la kivu kaskazini.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!

Alfajiri - Voice of America
Alfajiri - Desemba 10, 2025

Alfajiri - Voice of America

Play Episode Listen Later Dec 10, 2025 29:59

Matangazo ya nusu saa kuhusu habari za mapema asubuhi pamoja na habari za michezo.

desemba
Jioni - Voice of America
Jioni - Desemba 10, 2025

Jioni - Voice of America

Play Episode Listen Later Dec 10, 2025 29:59

Matangazo ya saa nzima kuhusu habari za kutwa, ikiwa ni pamoja ripoti kutoka kwa waandishi wetu sehemu mbali mbali duniani na kote Afrika Mashariki na Kati, na vile vile vipindi na makala maalum kuhusu afya, wanawake, jamii na maendeleo.

VOA Express - Voice of America
VOA Express - Desemba 10, 2025

VOA Express - Voice of America

Play Episode Listen Later Dec 10, 2025 29:59

VOA Express ni matangazo mapya yenye mwendo wa kasi yakiangalia habari mpya za mchana na maelezo ya maswala yanayohusu vijana na wanawake. Matangazo haya yanafuatilia habari zilizojitokeza nyakati za mchana na ripoti za kina za habari ambazo hazisikiki sana katika matangazo mengineyo. VOA Express pia inafuatilia kwa karibu sana maswala yanayovuma katika mitandao ya kijamii kama sehemu moja muhimu ya upashanaji habari siku hizi.

express desemba
Kwa Undani - Voice of America
Kwa Undani - Desemba 10, 2025

Kwa Undani - Voice of America

Play Episode Listen Later Dec 10, 2025 30:00

Kwa Undani ni matangazo ya dakika 25 yanayochambua habari kwa undani zaidi na kumpa msikilizaji maelezo ya kina kuliko ilivyo kawaida kuhusu tukio au swala lililojitokeza katika habari.

desemba
Habari za UN
09 DESEMBA 2025

Habari za UN

Play Episode Listen Later Dec 9, 2025 9:59

Hii leo jaridani tunakuletea ufafanuzi wa umuhimu wa maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Haki za binadamu kutoka kwa Seifu Magango Msemaji wa Ofisi ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa ambaye anaanza kwa kuzungumzia azimio la tamko hilo la haki za binadamu.Utafiti uliofanywa na Tume ya Ulaya kwakushirikiana na shirika la Umoja wa Mataifa linalaoshughulikia masuala ya wanawake UN Women umebaini kuwa wanawake saba kati ya kumi wakiwemo watetezi wa haki za binadamu, wanaharakati na waandishi wa habari wanakumbana na ukatili mtandaoni.Meneja Mawasiliano wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulika na masuala ya watoto UNICEF Tess Ingram yupo ziarani Ukanda wa Gaza huko Mashariki ya kati ambapo hii leo amezungumza na waandishi wa habari jijini Geneva Uswisi na kuwaeleza aliyoshuhudia huko ikiwemo wajawazito walio na utapiamlo kujifungua watoto wenye uzito mdogo au kuzaliwa kabla ya wakati, ambao wengine wanakufa katika vyumba vya wagonjwa mahututi      au wengine hupona lakini watoto hao hukabiliwa na utapimlo au matatizo mengine ya kiafya.Kamati ya Umoja wa Mataifa ya Kutokomeza Ubaguzi wa Rangi CERD, leo imetoa onyo kali kwa Sudan, ikieleza wasiwasi mkubwa kuhusu ongezeko la matumizi ya lugha ya kudhalilisha, kauli za chuki na ukiukaji Mkubwa wa haki za binadamu unaochochewa na misingi ya kikabila. Kamati imesem Mashambulizi haswa dhidi ya jamii za Fur, Masalit na Zaghawa, yanadaiwa kufanywa na Kikosi cha Msaada wa Haraka RSF na makundi washirika katika maeneo ya El Fasher, Darfur Kaskazini.Katika kujifunza lugha ya Kiswahili hii leo, mtaalam wetu Onni Sigalla, Mhariri mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania, BAKITA. Anafafanua maana za neno "PEKUPEKU"Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!

Alfajiri - Voice of America
Alfajiri - Desemba 09, 2025

Alfajiri - Voice of America

Play Episode Listen Later Dec 9, 2025 29:59

Matangazo ya nusu saa kuhusu habari za mapema asubuhi pamoja na habari za michezo.

desemba
Jioni - Voice of America
Jioni - Desemba 09, 2025

Jioni - Voice of America

Play Episode Listen Later Dec 9, 2025 29:59

Matangazo ya saa nzima kuhusu habari za kutwa, ikiwa ni pamoja ripoti kutoka kwa waandishi wetu sehemu mbali mbali duniani na kote Afrika Mashariki na Kati, na vile vile vipindi na makala maalum kuhusu afya, wanawake, jamii na maendeleo.

Habari za UN
08 DESEMBA 2025

Habari za UN

Play Episode Listen Later Dec 8, 2025 9:40

Leo katika Jarida la UNMlipuko wa kipindupindu wa mwaka huu nchini DRC ni mbaya zaidi katika kipindi cha miaka 25.Wananchi wanaojitolea wanavyosaidia wananchi wenzao nchini Sudan.Janga la kibinadamu Sudan haliwezi tena kupuuzwa, wakati ni sasa kulishughulikia.

sudan drc janga desemba wananchi
Alfajiri - Voice of America
Alfajiri - Desemba 08, 2025

Alfajiri - Voice of America

Play Episode Listen Later Dec 8, 2025 29:59

Matangazo ya nusu saa kuhusu habari za mapema asubuhi pamoja na habari za michezo.

desemba
Jioni - Voice of America
Jioni - Desemba 08, 2025

Jioni - Voice of America

Play Episode Listen Later Dec 8, 2025 29:59

Matangazo ya saa nzima kuhusu habari za kutwa, ikiwa ni pamoja ripoti kutoka kwa waandishi wetu sehemu mbali mbali duniani na kote Afrika Mashariki na Kati, na vile vile vipindi na makala maalum kuhusu afya, wanawake, jamii na maendeleo.

Jioni - Voice of America
Jioni - Desemba 07, 2025

Jioni - Voice of America

Play Episode Listen Later Dec 7, 2025 29:59

Matangazo ya saa nzima kuhusu habari za kutwa, ikiwa ni pamoja ripoti kutoka kwa waandishi wetu sehemu mbali mbali duniani na kote Afrika Mashariki na Kati, na vile vile vipindi na makala maalum kuhusu afya, wanawake, jamii na maendeleo.

Jioni - Voice of America
Jioni - Desemba 06, 2025

Jioni - Voice of America

Play Episode Listen Later Dec 6, 2025 29:59

Matangazo ya saa nzima kuhusu habari za kutwa, ikiwa ni pamoja ripoti kutoka kwa waandishi wetu sehemu mbali mbali duniani na kote Afrika Mashariki na Kati, na vile vile vipindi na makala maalum kuhusu afya, wanawake, jamii na maendeleo.

Habari za UN
UN: Mchango wa watu wanaojitolea ni muhimili wa mabadiliko

Habari za UN

Play Episode Listen Later Dec 5, 2025 3:03

Katika dunia inayohitaji mshikamano ili kufikia maendeleo, mchango wa watu wanaojitolea umeendelea kuwa nguvu muhimu ya kuleta mabadiliko chanya kwenye jamii kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa. Kila mwaka tarehe 5 mwezi Desemba, dunia huadhimisha Siku ya Kimataifa ya Wanaojitolea, mwaka huu ikiwa imebeba maudhui“Kila Mchango Una Umuhimu.”  Maadhimisho ya mwaka huu pia yanazindua rasmi Mwaka wa Kimataifa wa Wanaojitolea kwa Maendeleo Endelevu 2026. Kutoka Dar es Salaam, Tanzania Sabrina Saidi amezungumza na kijana  ambaye anajitolea katika Asasi ya Vijana ya Umoja wa Mataifa Tanzania YUNA Je kasema nini?.

Habari za UN
05 DESEMBA 2025

Habari za UN

Play Episode Listen Later Dec 5, 2025 11:07

Hii leo jaridani tunaangazia masuala ya haki za binadamu na maandamano ya amani nchini Tanzania, siku ya kujitolea tukikuletea ujumbe wa mfanyakazi wa kujitolea, na elimu jumuishi kwa ajili ya watu wenye ulemavu nchini Ethiopia.Wakati Tanzania ikijiandaa kwa maandamano makubwa yaliyopangwa kufanyika tarehe 9 Desemba siku ya maadhimisho ya Uhuru, Ofisi ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa OHCHR imetoa tahadhari na wito kwa serikali ya taifa hilo la Afrika Mashariki. Seif Magango ni msemaji wa ofisi ya Haki za binadamu ametufafanulia kuhusu tamko lao.Katika dunia inayohitaji mshikamano ili kufikia maendeleo, mchango wa watu wanaojitolea umeendelea kuwa nguvu muhimu ya kuleta mabadiliko chanya kwenye jamii kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa. Kila mwaka tarehe 5 mwezi Desemba, dunia huadhimisha Siku ya Kimataifa ya Wanaojitolea, mwaka huu ikiwa imebeba maudhui “Kila Mchango Una Umuhimu.”  Maadhimisho ya mwaka huu pia yanazindua rasmi Mwaka wa Kimataifa wa Wanaojitolea kwa Maendeleo Endelevu 2026.Katika eneo la Tigray kaskazini mwa Ethiopia, jitihada za kuimarisha makuzi na elimu kwa watoto wenye ulemavu zinaendelea kuleta matumaini mapya, kupitia programu inayoungwa mkono na Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu na Masuala ya Dharura OCHA, na Mfuko wa Dharura wa Umoja wa Mataifa, CERF. Je nini kinafanyika?Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!

Habari za UN
OHCHR yaitahadharishaTanzania kufuatia maandamano yaliyopangwa kufanyika tarehe 9 Desemba

Habari za UN

Play Episode Listen Later Dec 5, 2025 3:43

Wakati Tanzania ikijiandaa kwa maandamano makubwa yaliyopangwa kufanyika tarehe 9 Desemba siku ya maadhimisho ya Uhuru, Ofisi ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa OHCHR imetoa tahadhari na wito kwa serikali ya taifa hilo la Afrika Mashariki. Seif Magango ni msemaji wa ofisi ya Haki za binadamu ametufafanulia kuhusu tamko lao.

Alfajiri - Voice of America
Alfajiri - Desemba 05, 2025

Alfajiri - Voice of America

Play Episode Listen Later Dec 5, 2025 30:00

Matangazo ya nusu saa kuhusu habari za mapema asubuhi pamoja na habari za michezo.

desemba
Jioni - Voice of America
Jioni - Desemba 05, 2025

Jioni - Voice of America

Play Episode Listen Later Dec 5, 2025 59:59

Matangazo ya saa nzima kuhusu habari za kutwa, ikiwa ni pamoja ripoti kutoka kwa waandishi wetu sehemu mbali mbali duniani na kote Afrika Mashariki na Kati, na vile vile vipindi na makala maalum kuhusu afya, wanawake, jamii na maendeleo.

Habari za UN
04 DESEMBA 2025

Habari za UN

Play Episode Listen Later Dec 4, 2025 12:02

Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini Kenya kwa mwanariadha na mchchemuzi wa masuala ya wanawake, akieleza hatua zinazochukuliwa kutokomeza dhulma wa kijinsia. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na jifunze lugha ya Kiswahili.Huku mapigano yakizidi kushika kasi katika eneo la Kordofan nchini Sudan, Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa, Volker Türk, ameonya hii leo kuhusu hatari ya mashambulizi mapya dhidi ya raia, baada ya kuripotiwa vifo zaidi ya watu 269 kutokana na mashambulizi ya angani, mabomu na mauaji ya kiholela tangu mwishoni mwa mwezi Oktoba. Ofisi yake imeeleza kupokea taarifa za ulipizaji kisasi, utekaji, ukatili wa kingono na ulazimishaji wa watoto kujiunga na makundi ya kivita, huku miji kama Kadugli, Dilling na El Obeid ikikabiliwa na njaa, kuzingirwa na kukwama kwa misaada ya kibinadamu.Malaria, ugonjwa ambao takriban asilimia 95 ya vifo vinavyoripotiwa duniani ni kutoka nchi za Afrika tena kwa watoto walio na umri wa chini ya miaka 5. Ulionekana kuweza kudhibitiwa lakini sasa Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la Afya duniani WHO, Dkt. Tedros Ghebreyesus, anasema unaelekea kubaya kutokana na kuongezeka kwa usugu wa dawa, hali inayotishia kuyafuta mafanikio yaliyookoa maisha ya watu milioni moja mwaka 2024 kupitia chanjo na vyandarua vipya vyenye dawa ya kukabiliana na mbu waenezao Malaria.Na tuhitimishie nchini Msumbiji ambako Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji IOM Amy Pope amefanya ziara ya siku tatu na kujionea athari zilizoletwa na Mafuriko, vimbunga na kuzorota kwa usalama huko Kaskazini mwa nchi hiyo hali iliyosababisha zaidi ya 100,000 wameyakimbia makazi yao, na zaidi ya 600,000 wakihitaji msaada.Katika kujifunza lugha ya Kiswahili leo ukumbi ni wake mlumbi wa lugha ya Kiswahili Joramu Nkumbi kutoka nchini Tanzania, anafafanua maana za maneno "MADHALI"Mwenyeji wako ni Sabrina Moshi, karibu!

Alfajiri - Voice of America
Alfajiri - Desemba 04, 2025

Alfajiri - Voice of America

Play Episode Listen Later Dec 4, 2025 30:00

Matangazo ya nusu saa kuhusu habari za mapema asubuhi pamoja na habari za michezo.

desemba
Jioni - Voice of America
Jioni - Desemba 04, 2025

Jioni - Voice of America

Play Episode Listen Later Dec 4, 2025 29:59

Matangazo ya saa nzima kuhusu habari za kutwa, ikiwa ni pamoja ripoti kutoka kwa waandishi wetu sehemu mbali mbali duniani na kote Afrika Mashariki na Kati, na vile vile vipindi na makala maalum kuhusu afya, wanawake, jamii na maendeleo.

Habari za UN
03 FEBRUARY 2025

Habari za UN

Play Episode Listen Later Dec 3, 2025 11:55

Hii leo jaridani tunaangazia ujumbe wa Katibu Mkuu kuhusu siku ya Kimataifa ya Watu wenye Ulemavu, simulizi ya Mwalimu mwenye ulemavu wa kuona na huduma za afya ya uzazi kwa wasichana vigori nchini Kenya.Umoja wa Mataifa leo Desemba 3 unaadhimisha Siku ya Kimataifa ya Watu wenye Ulemavu kwa ujumbe mzito kutoka kwa Katibu Mkuu António Guterres ujumbe unaotaka jamii ziwe si tu zinazoweza kufikiwa na watuwenye ulemavu, bali pia zenye ujumuishi wa kweli.Ili kuyajadili baadhi ya masuala aliyoyagusia Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, basi Diana Katabarwa wa redio washirika wetu Uhai FM amezungumza na Mwalimu mwenye ulemavu wa kuona, Bahati Sanga, Katibu wa Chama Cha Wasioona, Mkoa wa Tabora.Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu na Afya ya Uzazi UNFPA kupitia ufadhili kutoka kwa asasi ya Adolescent Sexual and #ReproductiveHealth Development Impact Bond, limewezesha wasichana nchini Kenya kupata huduma za uzazi wa mpango bila malipo, taarifa muhimu, na kufanya maamuzi sahihi na hivyo kulinda afya zao na kuboresha mustakabali wao.Mwenyeji wako ni Sabrina Moshi, karibu!

Habari za UN
Guterres: Kunapokuwa na ujumuishwaji wa kweli kila mtu ananufaika katika jamii

Habari za UN

Play Episode Listen Later Dec 3, 2025 2:53

Umoja wa Mataifa leo Desemba 3 unaadhimisha Siku ya Kimataifa ya Watu wenye Ulemavu kwa ujumbe mzito kutoka kwa Katibu Mkuu António Guterres ujumbe unaotaka jamii ziwe si tu zinazoweza kufikiwa na watuwenye ulemavu, bali pia zenye ujumuishi wa kweli. Flora Nducha na taarifa zaidi

Alfajiri - Voice of America
Alfajiri - Desemba 03, 2025

Alfajiri - Voice of America

Play Episode Listen Later Dec 3, 2025 30:00

Matangazo ya nusu saa kuhusu habari za mapema asubuhi pamoja na habari za michezo.

desemba
Habari za UN
02 DESEMBA 2025

Habari za UN

Play Episode Listen Later Dec 2, 2025 12:39

Hii leo jaridani tukiendelea kukupa taarifa mbalimbali kuhusu siku 16 za kuhamasisha umma kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake, leo tunaelekea Mjini Hoima Magharibi mwa Uganda kusikia hisia za wanawake kuhusu ukatili dhidi ya wanawake mtandaoni.Watu takribani 100,000 wamekimbia makazi yao kaskazini mwa Msumbiji ndani ya wiki mbili, huku Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia wakimbizi UNHCR likionya kuwa mashambulizi yanaongezeka na kuyakumba hata maeneo yaliyokuwa salama. Mwakilishi wa UNHCR, Xavier Creach, amesema mgogoro “unazidi kuzorota kwa kasi ya kutisha” huku familia zikikimbia usiku gizani wakati watu wenye silaha wakivamia vijiji vyao. UNHCR inasema linahitaji dola milioni 38.2 kukidhi mahitaji yanayoongezeka.Kaskazini mwa Asia, dhoruba za kitropiki na mvua zisizo za kawaida zimesababisha vifo vya mamia na watu wengi kukimbia makazi yao, imesema WMO. Clare Nullis, msemaji wa shirika hilo, alisema Indonesia, Ufilipino, Sri Lanka, Thailand na Vietnam ndizo zimeathirika zaidi. “Tunahitaji kuzingatia kuwa Asia iko hatarini sana kutokana na mafuriko,” amesema Nullis, akibainisha kuwa dhoruba karibu na Ekweta ni nadra na jamii hazina uzoefu wa kukabiliana nazo. Indonesia pekee, watu 604 wamefariki, 464 hawajulikani walipo, na 2,600 wamejeruhiwa, huku zaidi ya milioni 1.5 wakiathirika na 570,000 wakikimbia makazi yao.Wakati dunia ikiadhimisha Siku ya Kimataifa ya Kukomesha Utumwa leo Desemba      2 Shirika la Umoja wa Mataifa la Kazi Duniani ILO limeonya kuhusu kuongezeka kwa utumwa wa kisasa wa binadamu, likionesha kuwa watu milioni 10 zaidi walikuwa wakiishi katika kazi za kulazimisha au ndoa za shuruti mwaka 2021 ikilinganishwa na mwaka 2016. Makadirio haya mapya yanaweka idadi ya walioathirika duniani kote kuwa watu milioni 50 huku wanawake na watoto wakiendelea kuwa wenye hatari kubwa zaidi.Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili, leo mchambuzi wetu ni Dkt. Josephat Gitonga, ambaye ni Mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi nchini Kenya, kwenye kitivo cha Tafsiri na Ukalimani anafafanua maana ya methali "KOTI LA BABU HALIKOSI CHAWA".Mwenyeji wako ni Sabrina Moshi, karibu!

Alfajiri - Voice of America
Alfajiri - Desemba 02, 2025

Alfajiri - Voice of America

Play Episode Listen Later Dec 2, 2025 30:00

Matangazo ya nusu saa kuhusu habari za mapema asubuhi pamoja na habari za michezo.

desemba
Habari za UN
01 DESEMBA 2025

Habari za UN

Play Episode Listen Later Dec 1, 2025 11:33

Hii leo jaridani tunaangazia ujumbe wa Umoja wa Mataifa katika Siku ya UKIMWI Duniani, simulizi wa mwathirika wa ugonjwa huu amabye aliolewa na umri wa miaka 15, na juhudi za UNICEF Wajir nchini Kenya za kuhakikisha ujumuishwaji wa watoto wenye ulemavu darasani.Leo ni Siku ya UKIMWI Duniani na mwaka huu inaadhimishwa kwa onyo kali kuhusu janga hilo pamoja na wito wa kuchukua hatua. Ikibeba kaulimbiu “Kukabili misukosuko, kubadili mwelekeo wa hatua za UKIMWI,” Umoja wa Mataifa unasema dunia ipo katika kipindi cha uamuzi muhimu katika vita dhidi ya VVU.Pooja aliolewa akiwa na umri wa miaka 15, baadaye akiwa mdogo bado akagundua kuwa ana Virusi Vya Ukimwi, VVU, na leo ni Mratibu wa Kitaifa wa Vijana chini ya Muungano wa Kitaifa wa Watu wanaoishi na VVU nchini India (NCPI+), akifanya kazi moja kwa moja na zaidi ya vijana 1,800 kote India. Katika mahojiano yaliyofanywa na Anshu Sharma wa Idhaa ya Kihindi ya Umoja wa Mataifa, Pooja anasimulia safari yake, nafasi ya jamii na familia, na ujumbe wake kwa watu wanaoishi na VVU. Anaposema ART anazungumzia dawa za kufubaza virusi, sawa na ARV lakini katika mkusanyiko wa dawa nyingi kwa pamoja.Katika Kaunti ya Wajir Kaskazini Mashariki mwa Kenya, Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Watoto UNICEF kwa kushirikiana na Taasisi ya Elimu Maalum ya Kenya KISE wameanzisha mpango maalum wa kuwasaidia watoto wenye ulemavu kupata tathmini za kitabibu na kielimu. Mpango huu umeleta matumaini mapya kwa familia nyingi ambazo hapo awali zilikuwa na ugumu wa kupata huduma hizo.Mwenyeji wako ni Sabrina Moshi, karibu!

Alfajiri - Voice of America
Alfajiri - Desemba 01, 2025

Alfajiri - Voice of America

Play Episode Listen Later Dec 1, 2025 29:59

Matangazo ya nusu saa kuhusu habari za mapema asubuhi pamoja na habari za michezo.

desemba