Changu Chako, Chako Changu

Follow Changu Chako, Chako Changu
Share on
Copy link to clipboard

Changu Chako, Chako Changu ni makala inayozungumzia masuala ya historia, utamaduni, muziki na lugha ya Kifaransa Afrika Mashariki na Kati na duniani. Makala haya yatakuhabarisha pia kuhusu Jumuiya ya Kimataifa ya Watu Wanaotumia lugha ya Kifaransa kwenye Mawasiliano (L'OIF) na jinsi gani kujifunza n…

Rfi - Ruben Kakule Lukumbuka


    • Jun 1, 2025 LATEST EPISODE
    • every other week NEW EPISODES
    • 20m AVG DURATION
    • 202 EPISODES


    Search for episodes from Changu Chako, Chako Changu with a specific topic:

    Latest episodes from Changu Chako, Chako Changu

    Fuatilia hapa toleo la 78 la tamasha la filamu maharufu duniani Festival de Cannes

    Play Episode Listen Later Jun 1, 2025 20:09


    Shukran sana kwake maulana kutukutanisha tena jumapili ya leo, ambapo nakuletea historia na namna tamasha la filamu maharugu duniani lijulikanalo kama Festival de cannes ambalo hufanyika mwezi Mei ya kila mwaka, kwenye Palais du festival  huko Cannes. Kwenye le parler francophone nitakujuza ratiba ya shughuli mbalimbali kwenye vituo vya Alliance Francaise za ukanda na kwenye Muziki nitakuletea mwanamuziki Ali Kiba,

    Historia kuhusu uteuzi wa papa Leo wa XIV, miaka 44 yangu kifo cha Bob Marley

    Play Episode Listen Later May 10, 2025 20:15


    Makala ya changu chako chako changu inaangazia kuhusu uteuzi wa kiongozi wa kanisa katoliki duniani, ambapo RFI Kiswahili imezungumza na askofu Sebastian Muyengo wa dayosisi ya Uvira mkoani Kivu kaskazini mashariki mwa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, na katika utamaduni kabila la wabembe huko Fizi nchini DRC na katika muziki maadhimisho ya miaka 44 tangu kifo cha muasisi wa miondoko ya regae Bob Marley

    Historia ya uhuru wa wanahabari na changamoto za usambazaji wa habari za uongo

    Play Episode Listen Later May 4, 2025 20:04


    Karibu mpenzi msikilizaji wa RFI Kiswahili katika Makala Changu Chako Chako Changu maalum kabisa kuhusu historia ya siku ya kimataifa ya uhuru wa wanahabari ambayo huadhimishwa kila Mei 3. Ambapo maadhimoisho haya yanakuja wakati dunia ikikabiliana na changamoto za usamabazaji wa habari za uongo kwa kutumia akili bandia. Mimi ni Ali Bilali Karibu.

    Historia ya muungano wa Tanganiyika na Zanzibar na msanii wa Burundi Tomson the Voice

    Play Episode Listen Later Apr 27, 2025 20:09


    Karibu kuungana nami katika makala changu chako chako changu leo jumapili ambapo nakuletea Historia ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Kwenye le parler francophone nitakujuza ratiba ya shughuli za kitamaduni Alliance francaise ya Nairobi, na kwenye Muziki nitakuletea mwanamuziki Thomson the voice kutoka nchini Burundi, mimi ni Ali Bilali, bienvenue ama Karibu.

    Changu Chako Chako Changu mahakama ya jadi kutoka kabila la Wameru sehemu ya kwanza

    Play Episode Listen Later Apr 13, 2025 20:02


    Kwenye makala haya utapata kufahamu mahakama hii ya Jadi nchini Kenya kutoka Kabila la Wameru ambayo inakubalika na serikali katika utatuzi wa mizozo mbalimbali kutoka jamii ya wameru. Utapa pia kufahamu historia ya msanii kutoka nchini Ufaransa Hiro le Coq.

    Historia ya Jumuiya ya nchi zinazo zungumza lugha ya Kifaransa, Francophonie

    Play Episode Listen Later Mar 27, 2025 19:58


    Ni Jumapili nyingine tunakutana tena katika Makala haya Changu Chako Chako Chako Changu, Makala ambayo hukuletea Historia ya mambo mbalimbali, Utamaduni le parler francophone na Muziki, ambapo leo nakuletea historia ya siku ya kimataifa ya nchi zinazozungumza lugha ya Kifaransa, ama Organisation internationale de la francophonie. Nitakuletea pia ratiba za shughuli za kitamaduni kupitia vituo vya utamaduni wa Ufaransa vya Ukanda, na kwenye Muziki nitakuletea mwanamuziki Frederic Francois. Kumbuka pia kutufollow kwenye mitandao ya kijamii kwa kubonyeza hapa 

    Historia ya siku ya wanawake duniani machi 8 kila mwaka

    Play Episode Listen Later Mar 25, 2025 19:59


    Katika Makala haya mtangazji wa ko Ali Bilali anakuletea Historia ya siku ya wanawake duniani ambayo husherehekewa kila ifikapo machi 8 ya kila mwaka

    Historia ya mkutano wa Berlin sehemu ya pili March 2 2025

    Play Episode Listen Later Mar 25, 2025 19:58


    Makala haya, mtangazaji wako anakuletea sehemu ya pili ya historia ya mkutano wa Berlin

    Historia ya mkutano wa Berlin sehemu ya kwanza Feb 23 2025

    Play Episode Listen Later Mar 25, 2025 30:09


    Makala haya yanazungumzia historia ya mkutano wa Berlin

    Historia ya maisha ya Cassypool hadi kuwa Chawa wa marais

    Play Episode Listen Later Feb 11, 2025 19:59


    Katika Makala haya, mtangazaji wako Ali Bilali anazungumza na Cassypool mwanamitandao na muhamasishaji kutoka nchini Kenya, ambae amejizolea umaharufu kupitia kile alichokiita tasnia ya uchawa, ambapo anaeleza kuwa chawa wa rais wa Kenya William Ruto na sasa ni chawa wa rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan. Kumbuka pia kutufollow kwa instagram @billy_bilali

    kenya historia hadi marais sanaa maisha kuwa muziki kenya william ruto katika makala tanzania samia suluhu hassan ali bilali
    Historia ya kabila la Wakalejin,Sanaa ya Kuigiza ya African Twist Pamoja na Historia yake Yemi Alade

    Play Episode Listen Later Jan 26, 2025 19:55


    Makala ya Changu Chako ,chako Changu hii leo yanaangazia  historia na tamaduni za kabila la Wakalenjin kutokea Kenya.Kisha kwenye kipengele cha Leorparle Francophone tutangaazia  maonyesho kuhusu mabadiliko yaliyofanyika kwenye muziki kuanzia miaka ya 1960  alafu kwenye kipengele chetu ya mwisho cha Muziki tutamuangazia mwanamuziki Yemi Alade.

    Waskilizaji wa RFI kiswahili watakiana heri ya mwaka mpya kupitia Makala Changu Chako

    Play Episode Listen Later Jan 16, 2025 20:02


    Katika Makala haya ya kwanza kabisa ya mwaka 2025, mtangazaji wako asiependa makuu Ali Bilali anakupa fursa ya kuwatakia heri ya mwaka mpya ndugu jamaa na marafiki.

    Makala ya mwisho katika mwaka 2024, salamu wa wasikilizaji na msanii Isifiwe Kibangula

    Play Episode Listen Later Dec 29, 2024 20:03


    Heri ya mwaka mpya msikilizaji wa RFI Kiswahili popte pale ulipo. Ali Bilali mtangazaji wako asiependa makuu ninakukaribisha katika makala haya ya mwishgo kabisa changu chako chako changu katika mwaka 2024. Leo nakukumbusha mada kadhaa zilizo zungumziwa mwaka 2024, lakini pia ninapokea salam zako za mwaka mpya wa 2024, na kwenye Muziki nitakuletea mwanamuziki isifiwe Kibangula kutoka hko Sweeden ambae ametangawa kubadili muziki wake.Karibu na kwa mara nyingine tena kheri ya mwaka mpya.

    Historia ya kabila la Wamasai ,Sanaa ya Uchoraji na Historia ya Muziki wake Burna Boy

    Play Episode Listen Later Dec 22, 2024 20:04


    Makala ya changu chako ,chako changu,hii leo utaskia historia ya kabila la wamasai wanaopatikana AFrika hasaa kenya na Tanzania,kisha kwenye kipengele cha pili utaskia maonyesho ya Sanaa ya uchoraji yanayoendelea katika ukumbi wa Alliance Francaise na mwisho kabisaa katika kipengele cha muziki makala haya yataangazia  historia yake mwanamuziki kwa jina Burna Boy kutokea  Nigeria .

    Historia ya Kenya kupata Uhuru pamoja na Maonyesho ya Sanaa ya Uchoraji Alliance Francaise Nairobi

    Play Episode Listen Later Dec 15, 2024 19:53


    Makala haya yataangazia Historia ya nchi ya Kenya na jinsi ilivyopata Uhuru,kwenye kipengele cha pili utaskia safari ya vijana wanaofanya sanaa ya Uchoraji kutoka shirika lisilo la kiserikali la Uweza Art Gallery na mwisho kabisa kwenye kipengele cha historia ya mwanamuziki utaskia historia yake Juma Jux kutokea Tanzania.

    Teknolojia yabadilisha muziki ,Ujio wake Msanii Sean Paul nchini Kenya

    Play Episode Listen Later Dec 8, 2024 19:49


    Tutaangazia historia ya muziki wa Afrika, tukiangalia mabadiliko makubwa yaliyotokea kabla na baada ya kuibuka kwa teknolojia. Muziki wa Afrika ni sehemu muhimu ya utamaduni wetu, na umetumika kwa karne nyingi kama njia ya kuwasiliana, kusherehekea, na kuponya.

    Hatuwa za mwisho za maandalizi ya tamasha la watu wa kabila la bashi la desemba 6

    Play Episode Listen Later Dec 1, 2024 20:03


    Uhusiano baina ya lugha na utamaduni, mila na mirathi ya jamii kwa jumla huenda ukafahamika angalau kwa wepesi, iwapo tutazingatia mambo kadhaa ikiwemo lugha na matumizi yake, tabia, utu, utamaduni, mila,mitindo na mengineo. Watu wa kabila la washi mashariki mwa DRC wameandaa tamasha la kutambulisha utamaduni wao, ambalo ni msimu wa pili na limepangwa kufanyika desemba 6 hadi 8 huko Bukavu. Katika makala haya mtangazaji wako Ali Bilali anakuletea sehemu hii ya tatu na ya mwisho ya maandilizi ya makala haya. unaweza kusikiliza sehemu ya kwanza kubonyeza hapa (sehemu ya kwanza) Lakini pia sehemu ya pili kwa kubonyeza hapa (Sehemu ya pili) Asante kwa kuendelea kuwa muaminifu kwa radio yako na kwa mtangazaji wako asiependa makuu unaweza kumfollow kwa kubonyeza hapa Billy Bilali

    Sehemu ya pili ya makala kuhuus tamasha la watu wa kabila la washi Nov 24 2024

    Play Episode Listen Later Nov 23, 2024 19:56


    Makala haya Ali Bilali anazungumza na msanii Oliver wa nyimbo za asili ya washi wahavu mashariki mwa DRC kuelekea tamasha la Bushi ama Festival de Bushi.

    Maandalizi ya Tamasha la watu wa Kabila la Washi kutoka Bukavu sehemu ya kwanza.

    Play Episode Listen Later Nov 18, 2024 20:01


    Shindano la filamu kwa kutumia simu ya Mkononi na msanii kutoka Mombasa Rojo Mo

    Play Episode Listen Later Nov 9, 2024 19:58


    Karibu katika makala changu chako chako changu Jumapili yaleo ambapo tutakijita zaidi kwenye matokeo ya shindano la kutengeneza filamu kwa kutumia simu ya mkononi liliooandaliwa na Alliance Francaise ya Nairobi nchini Kenya na kwenye Muziki tutakuwa naye msanii kutoka Mombasa Rojo Mo. Mimi ni Ali Bilali Bienvenue ama Karibu, restons ensemble mwanzo hadi tamati, yaani tubaki pamoja mwanzo hadi mwisho.

    Alliance Francaise ya Nairobi inavyoikuza sanaa ya uigizaji jukwaani sehemu ya kwanza.

    Play Episode Listen Later Nov 4, 2024 19:55


    Katika Makala haya Ali Bilali amejielekeza Alliance Francaise ya Nairobi ambayo imeandaa Onyesho la Kwanza la tamthilia ya ‘Mgonjwa Mwitu', utayarishaji wao wa kila mwaka wa maigizo yaliyotolewa na tamthilia za waandishi mashuhuri wa Ufaransa. Kwa maadhimisho ya miaka 75, chaguo ni 'Le Malade Imaginaire' na Molière. Hii ni comedy ya mwisho kuandikwa na Molière. Ingawa ilionyeshwa kwa mara ya kwanza mnamo 1673, kichekesho hiki cha kejeli, mojawapo ya bora zaidi za Moliere, hakijapoteza mvuto wake wa dhati na wa ulimwengu wote.Kumbuka pia kumfollow mtangazaji wako @billy_bilali kwenye mitandao ya kijamii @billy_bilali

    Fahamu hapa kuhusu liliokuwa soko la watumwa nchini DRC Oct 20 2024

    Play Episode Listen Later Nov 4, 2024 20:09


    Karibu katika Makala Changu Chako Chako Changu, ambapo Ali Bilali mtangazaji wako asiependa makuu ameungana na Denise Maheho kutoka Lubumbashi kuzungumzia kuhusu iliokuwa barabara ya watumwa zama za ukoloni.Kumbuka pia kutuachia comment na kumfollow mtangazaji wako asiependa makuu @billy_Bilali kwenye mitandao yake ya kijamii Instagram na facebook.

    Utamaduni wa ndoa kulingana na kabila la Wameru sehemu ya pili Oct 13 2024

    Play Episode Listen Later Oct 13, 2024 20:11


    Ali Bilali ndio jina langu tunakutana tena Jumapili hii katika makala Changu Chako Chako Changu ambapo nakuletea sehemu ya pili ya Makala kuhusu Utamaduni w andoa kulingana na kabila la Wameru, kwenye le parler francophone nitakupa ratiba ya shughuli kwenye vituo vya Alliance Francaise ya Nairobi na Dar es salaam. Na kwenye Muziki tutamaliza na kibao Pambe chake Christian Bella kutoka huko nchini Tanzania, Karibu ama Bienvenue.

    Utamaduni wa watu wa Kabila la Wameru kutoka nchini Kenya

    Play Episode Listen Later Oct 6, 2024 19:47


    Makala haya mtangazaji wako Ali Bilali anazungumzia kuhusu utamaduni wa watu wa kabila la Wameru kutoka nchini Kenya, wapo pia nchini Tanzania.

    Utamaduni wa ndoa kabila la wamakonde na wahangaza kutoka nchini Tanzania sehemu ya 2

    Play Episode Listen Later Sep 29, 2024 20:11


    karibu, Jumapili nyingine kuwa nami katika Makala Changu Chako Chako Changu Makala ambayo hukuletea Historia na utamaduni wa mambo mbalimbali, le Parler francophone na Muziki. Wiki iliopita nilikuletea Utamaduni wa ndoa kutoka makabila ya Wamakonde na wahangaza, ambapo leo nakuletea sehemu ya pili. Na kwenye le parler francophone nitakuletea ratiba za shughuli za kitamaduni kutoka Alliance francaise ya Nairobi na Dar es salaam, Tutamaliza na Wimbo wa Ibrah kutokz Tanzania

    Utamaduni wa watu wa makabila ya wahangaza na wamakonde kutoka nchini Tanzania

    Play Episode Listen Later Sep 22, 2024 20:04


    Katika makala haya, mtangazaji wako Ali Bilali amezungumza na Amua Rushita kutoka Mkoa wa Mtwara pamoja na Hillary Alexanda Ruhundwa kutoka Mkoa wa Ngara nchini Tanzania kuzungumzia utamaduni wa ndoa kulingana na makabila hayo mawili. Kumbuka pia nawe unaweza kushiriki moja kwa moja studio au kwa njia ya simu. Wasiliana na mtangazaji wako asiependa makuu kufahamu zaidi.

    Toleo la 11 la Bourse Ghislaine Dupont na Claude Verlon kutolewa huko Benin

    Play Episode Listen Later Aug 26, 2024 19:49


    RFI inaandaa toleo la kumi na moja la Bourse Ghislaine Dupont na Claude Verlon, kwa heshima kwa waandishi wake wawili waliouawa kaskazini mwa Mali  Novemba 2, 2013. Bourse hii, ambayo huwafunza waandishi wa habari vijana kumi wa redio na mafundi vijana kumi wa kuripoti kila mwaka, iko wazi. kwa wagombea kutoka nchi zote za Afrika zinazozungumza Kifaransa. Mafunzo hayo yatafanyika Cotonou. Maombi yamefunguliwa hadi Jumapili Agosti 25 saa sita usiku saa za Paris.

    Changu Chako Chako Changu: Utamaduni wa mahari kwa baadhi ya makabila brani Afrika

    Play Episode Listen Later Aug 26, 2024 19:47


    Makala haya yanaangazia kuhusu gharama ya sherehe za harusi katika karne hii, hususan ukusanyaji wa michango kwa ajili ya kufanaikisha sherehe.

    Changu chako chako changu Tasnia ya ulimbwende sehemu ya pili

    Play Episode Listen Later Aug 13, 2024 20:01


    Karibu katika makala changu chako chako changu, makala ambayo hukuletea historia ya mambo mbalimbali utamaduni, le parler francophone na Muziki, ambapo leo nakuletea sehemu ya pili ya makala kuhusu Ulimbwende au Model,

    Changu Chako Chako Changu tasnia ya ulimbwende sehemu ya kwanza Agost 04 2024

    Play Episode Listen Later Aug 4, 2024 20:00


    Karibu katika makala changu chako chako changu, makala ambayo hukuletea mambo mbalimbali ya utamaduni, le parler francophone na Muziki, ambapo leo nakuletea sanaa ya Ulimbwende au Model, na kwenye la parler francophone nitakuletea shughuli zinazoendelea kwenye vituo vya Alliance francaise za ukanda kipindi hiki cha michuano ya Olympiki, mimi ni Ali Bilali Bienvenue.

    Historia ya kabila la Wabukusu pamoja na sanaa ya muziki kutokea kwa Bendi ya An Noor

    Play Episode Listen Later Jul 21, 2024 20:34


    Karibu kwenye makala ya  changu  chako ,chako  changu juma hili ukiwa nami Florence Kiwuwa. Na kwenye kipengele cha historia hii leo tutaangazia historia ya kabila la Waluhya wanaofahamika kama wabukusu kisha kwenye kipengele chetu cha pili cha LeParle Francophone tutaangazia maonyesho ya Taarab yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Alliance France kisha tutamalizia na mwanamuziki wa Kenya almarufu kama Freshely Mwamburi.

    Matumizi ya lugha ya kiswahili katika enzi ya Kijiditali

    Play Episode Listen Later Jul 16, 2024 20:14


    Kiswahili kinazungumzwa na zaidi ya watu milioni 200 afrika mashariki na kwenye makala haya ya changu chako,chako changu ,Florence Kiwuwa amefanya majadiliano na wanafunzi katika chuo kikuu cha Multmedia ili kujua kuhusu mchango wa lugha hii katika kuendeleza utamaduni na utengamano na vilevile katika kipengele cha muziki amemuangazia mwanamuziki wa Tanzania Harmonize.

    Changu Chako Chako Changu maalum kuhusu maadhimisho ya miaka 14 ya RFI Kiswahili

    Play Episode Listen Later Jul 7, 2024 19:56


    Karibu katika Makala Changu Chako Chako Changu jumapili ya leo ambapo nakulrtea Makala maalum kuhusu maadhimisho ya kumbukumbu ya miaka 14 tangu Ple RFI Kiswahili ilipoanza kupeperusha matangazo yake mubashara kutoka nchini Tanzania ambapo ilikuwa idhaa ya kwanza ya Kimataifa kutangaza ikiwa Afrika mashariki. Na kwenye Muziki nitakuletea Burudani ya Muziki wa Idd Aziz Kiswahili kitukuzwe wakati huu tukielekea kuadhimisha siku ya Kiswahili duniani. Mimi naitwa Ali Bilali, Bienvenue ama Karibu.  Kumbuka pia kumfollow mtangazaji wako Ali Bilali kwa kubonyeza hapa @billy_bilali

    Changu Chako Chako Changu, maadhimisho ya miaka 64 ya uhuru wa DRC

    Play Episode Listen Later Jul 6, 2024 20:00


    Makala haya Ali Bilali anazungumzia kuhsu maadhimisho ya miaka 64 ya Uhuru wa DRC.

    drc sanaa uhuru makala miaka maadhimisho ali bilali
    CHANGU CHAKO CHAKO CHANGU HISTORIA NA UTAMADUNI WA WATU WA KABILA LA WANUBI

    Play Episode Listen Later Jun 16, 2024 20:02


    Eid Mubaraka kwako mskilizaji wa RFI Kiswahili popopte pale ulipo ausubuhi hii. Karibu kuungana nami katika Makala haya Changu Chako Chako Changu. Leo nakuletea Historia ya watu wa Kabila la Wanubi, na kwenye Muziki nakupeleka  nchini Burundi ambapo nazungumza na msanii wa kizazi kipya, Keypeacvaldiny. mimi ni Ali Bilali mtangazaji wako asiependa makuu Karibu ama bienvenue. Jina lake halisi ni Nzeyimana touré hamissi, anatumia jina la kisanii a @keypeac_valdyn amezaliwa April 8 mwaka 2002 jijini Bujumbura inchini burundiAlianza muziki mwaka 2017, ila sababu ya harakati za masomo na familia alilazimika kuachana kabisa na muziki na kujikita zaidi na masomo. Baada ya kumaliza shule mwaka 2023 akaamuwa kurejea kwenye tasnia ya Muziki ambapo amekuja na EP yake iliowekwa hewani tangu April 15 mwaka 2024. EP yake hiyo ina nyimbo 3 ambazo ni:Track n°1.carolinaTrack n°2.sorryTrack n°3.mmmhna songs hizo zote zipo kwenye platforms zake zote anapatikana kwa jina la @keypeac valdynyupo kwenye platforms  zifwatazo kama : apple music, spotify, boomplay, youtube, rhapsody, deezer, amazon mp3, google play, shazam, tidal, tiktok, instagram, x ,  threads, na zingine.Unaweza kumfollow mtangazaji wako Ali Bilali kwa kubonyeza hapa https://www.instagram.com/billy_bilali/

    Historia ya madaraka Day nchini Kenya na ziara ya Mistachampagne studio za RFI Kiswahili

    Play Episode Listen Later Jun 4, 2024 20:04


    Karibu katika makala ya leo changu chako chako changu ambapo leo nakuletea historia ya siku ya madaraka ambayo huadhimishwa kila Juni Mosi nchini Kenya. Na kwenye le parler francophone kama kawaida nakuletea ratiba ya shughuli za kitamaduni Alliance francaise za ukanda. Na Kwenye Muziki nitakuwa naye Mr Champagne msanii kutoka nchini Burundi ambaye yupo nchini Kenya kwa ajili ya kutangaza wimbo wake mpya Niko tu. Mimi ni Ali Bilali bienvenue ama karibu. Kumbuka pia kumfollow mtangazaji wako kwenye mitandao ya kijamii @billy_bilali 

    Historia na utamaduni wa kabila la wanyakyusa sehemu ya pili

    Play Episode Listen Later May 30, 2024 20:05


     Karibu katika Makala haya changu chako chako changu, jumapili ya leo ambapo nakuletea awamu ya pili ya makala kuhusu historia na utamaduni wa watu wa kabila la Wanyakyusa, na kwenye Muziki nakupa muendelezo wa mazungumzo na wasanii Kidum Kibidon na EstherNish. Mimi ni Ali Bilali. Bienvenue.

    Historia na Utamaduni wa wanyakyusa na muziki wa Kidum pamoja na Esther Nish

    Play Episode Listen Later May 19, 2024 20:03


    Furaha ilioje kukutana nawe Jumapili ya leo katika Makala Changu chako Chako Changu, ambayo hukuletea historia ya mambo mbalimbali utamaduni le parler francophpone na Muziki ambapo leo nakuletea sehemu ya kwanza ya makala kuhusu historia ya Wanyakyusa, na kwenye Miuziki nitakuletea mwanamuziki Esthernish pamoja ni Kidum. Mimi ni Ali Bilali bienvenue. Ama Karibu. Kumbuka pia kutufollow kwa Instagram @billy 

    Sehemu ya makala kuhusu utamaduni wa waluo na waluhya hasa kwenye maswala ya ndoa

    Play Episode Listen Later May 16, 2024 20:03


    Karibu katika Makala haya changu chako chzako changu Jumapili ya leo ambapo nakuletea sehemu ya pili ya makala kuhusu tamaduni za wa Luhya na wa luo nchini Kenya ambapo sasa tutaangazia kuhusu tamadunbi za ndoa, na kwenye le parler francophone nakuletea ratiba ya shughuli za kitamaduni Alliance francaise ya Nairobi na kwenye muziki nitakuletea mwanamuziki Mbosso kutoka nchini Tanzania. Mimi ni Ali Bilali Karibu.

    Utamaduni wa watu wa kabila la Waluo na Waluhya kutoka nchini Kenya

    Play Episode Listen Later May 5, 2024 20:00


    Maoni ya washiriki katika kongamano la idhaa za kiswahili duniani sehemu ya mwisho

    Play Episode Listen Later Apr 21, 2024 20:02


    Ni jumapili nyingine tunakutana tena katika Makala haya Changu Chako Chako Changu, Makala ambayo hukuletea Historia ya mambo mbalimbali, utamaduni, le parler francophone na Muziki, na leo tunahitimisha mlolongo wa Makala kuhusu kongamano la idhaa za kiswahili duniani lililofanyika huko Mbeya, na kwenye le parler francophone nakuletea ratiba ya shughuli za kitamaduni kutoka Alliance Francaise ya Arusha na Nairobi, na kwenye Muziki nitakuletea mwanamuziki King Kaka kutoka nchini Kenya.

    Sehemu ya tatu ya Makala kuhusu kongamano la nne la idhaa za Kiswahili duniani

    Play Episode Listen Later Apr 14, 2024 20:00


    Ni Jumapili nyingine tunakutana katika Makala Changu Chako Chako Changu, Makala ambayo hukuletea Historia ya mambo mbalimbali, Utamaduni, le parler francophone na Muziki, leo ninakuletea mazungumzo kuhusu ubidhaishaji wa lugha ya kiswahili, ikiwa ni kauli mbiu ya kongamano la nne za idhaa za Kiswahili Duniani lililofanyika mkoani Mbeya Mwezi Machi. Na kwenye le parler francophone nitakuletea mradi wa Creation Afrika unaonadaliwa na Allliance francaise ya Nairobi

    Kongamano la idhaa za kiswahili duniani, umuhimu wa kujifunza lugha ya Kiswahili

    Play Episode Listen Later Apr 9, 2024 19:57


    Makala haya mtangazaji wako Ali Bilali amezungumza na Msimamizi wa kituo cha radio China Kimataifa ambaye ni raia wa China kufahamu zaidi kwanini alivutiwa na swala la kujifunza lugha ya kiswahili, ni katika muktada wa kongamano la idhaa za kiswahili duniani lililofanyika Mbeya nchini Tanzania. Kwenye Muziki utasikiliza wimbo wa mwanamuziki Lupman mwenye asili ya Burundi anaefanya kazi yake huko Sweeden. https://www.youtube.com/watch%3Fv%3DdsIZZ0MmadE

    Kongamano la nne la idhaa za kiswahili duniani "Tasnia ya habari na ubidhaishaji Kiswahili duniani"

    Play Episode Listen Later Mar 31, 2024 20:00


    Karibu kuungana nami katika Makala haya Changu Chako Chako Changu, Makala ambyo hukuletea Historia ya mambo mbalimbali, utamaduni, le parler francophone na Muziki, ambapo leo nakuletea sehemu ya kwanza ya mazungumzo kuhusu Kongomano la nne la idhaa za Kiswahili duniani. Kwenye le Parler francophone nitakueleza ratiba ya shughuli za kitamaduni Alliance francaise ya Nairobi na Dar es salaam. Na kwenye Muziki nitakuletea mwanamuziki Idd Aziz kutoka nchini Kenya.

    Maadhimisho ya siku ya kimataifa ya lugha ya kifaransa sehemu ya pili

    Play Episode Listen Later Mar 25, 2024 19:45


    Makala haya yameandaliwa na Florence Kiwuwa kwa ushirikiano na Ruben Lukumbuka.

    Maadhimisho ya siku ya kimataifa ya lugha ya kifaransa

    Play Episode Listen Later Mar 20, 2024 20:22


    Makala maalum ya changu chako chako changu inafanyika hapa Mombasa pwani ya Kenya katika luktadha wa maadhimisho ya siku ya kimataifa ya lugha ya kifaransa, inayofahamika Kama La Francophonie, ambapo Taasisi inayofundisha watu lugha hii na tamaduni za Ufaransa, Alliance Francaise ya Mombasa, imeandaa maadhimisho haya maalum kwa kuenzi namna ambavyo Francophonie inavyotia fora nchini DRC. Ungana na mwandishi wetu Reuben Lukumbuka moja kwa moja akiwa Alliance francaise ya Mombasa

    Historia ya siku ya kimataifa ya wanawake duniani na namna ilivyosherehekewa mwaka huu wa 2024

    Play Episode Listen Later Mar 9, 2024 20:00


    Maandalizi ya siku ya wanawake duniani ya March 08

    Play Episode Listen Later Mar 9, 2024 19:47


    Makala haya mtangazaji wako Ali Bilali amezungumza na mwanaharakati Florence Kiwuwa ambae pia ni mtangazaji wa RFI Kiswahili kuhusu maandalizi ya siku ya kimataifa ya wanawake duniani.

    Umuhimu wa kujifunza lugha mama na changamoto zake katika maisha ya kila siku

    Play Episode Listen Later Feb 25, 2024 20:03


    Makala haya mtangazaji wako Ali Bilali anazungumzia kuhusu umuhimu wa kujifunza lugha Mama, wakati huu shirika la Umoja wa Mataifa la Sayansi na Utamaduni Unesco likiwa na wasiwasi wa kutokewa kwa zaidi ya lugha mama zaidi ya 3000.

    Historia ya kombe la mataifa bingwa barani Afrika CAN sehemu ya pili

    Play Episode Listen Later Feb 24, 2024 19:58


    Makala haya ni sehemu ya pili ya historia ya michuano ya mataifa bingwa barani Afrika CAN.

    Historia ya michuano ya kombe la mataifa ya Afrika CAN sehemu ya kwanza

    Play Episode Listen Later Feb 15, 2024 19:55


    Karibu kuungana naye Ali Bilali katika Makala ya leo Changu chako chako changu, ambapo anakuletea historia ya kombe la mataifa ya afrika na atiba ya shughuli kutoka Alliance francaise za ukanda na kwenye muziki atakuletea historia fupi ya mwanamuziki rapa kutoka nchini Kenya King Kaka. Kumbuka pia kumfolow kwa instagram @billy_bilali

    Claim Changu Chako, Chako Changu

    In order to claim this podcast we'll send an email to with a verification link. Simply click the link and you will be able to edit tags, request a refresh, and other features to take control of your podcast page!

    Claim Cancel