POPULARITY
Mkuu wa Majeshi nchini Kenya, Jenerali Jenerali Charles Kahariri na Mkuu wa idara ya ujasusi Noordin Haji, wameonya dhidi ya kampeni inayoendelea kwenye mitandao ya kijamii na mikutano ya hadhara ya –Ruto Must Go- au Ruto lazima aondoke, inatishia hali ya kisiasa nchini Kenya na ni lazima, ikome.Je, jeshi la Kenya linaingilia siasa ? Tunajadili…
Tunajadili hatua ya Kanisa la Anglikana nchini Kenya, kwa mara nyingine limesisitiza marufuku ya kuwazuia wanasiasa kuzungumza kanisani katika juhudi za kuzuia wanasiasa kufanya siasa kanisani. Je unazungumziaje hatua hii ya kanisa Anglikana nchini Kenya? Skiza makala haya kuskia baadhi ya maoni ya waskilizaji wetu.
Tunajadili hatua ya Kanisa la Anglikana nchini Kenya, kwa mara nyingine limesisitiza marufuku ya kuwazuia wanasiasa kuzungumza kanisani katika juhudi za kuzuia wanasiasa kufanya siasa kanisani. Je unazungumziaje hatua hii ya kanisa Anglikana nchini Kenya? Skiza makala haya kuskia baadhi ya maoni ya waskilizaji wetu.
Tunajadili hatua ya bazara la wakikimbizi la Denmark, kuchachapisha ripoti inayoonesha kuwa, watu zaidi ya milioni 6 duniani watakosa mahali pakuishi ifikapo mwishoni mwa mwaka ujao, kutokana na mizozo, mabadiliko ya tabia nchi na kusitishwa kwa misaada toka Marekani. Unazungumziaje hatua hii? ndilo swali tumeuliza, skiza makala haya kufahamu mengi.
Tunajadili hatua ya bazara la wakikimbizi la Denmark, kuchachapisha ripoti inayoonesha kuwa, watu zaidi ya milioni 6 duniani watakosa mahali pakuishi ifikapo mwishoni mwa mwaka ujao, kutokana na mizozo, mabadiliko ya tabia nchi na kusitishwa kwa misaada toka Marekani. Unazungumziaje hatua hii? ndilo swali tumeuliza, skiza makala haya kufahamu mengi.
Wakati huu serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, inapoendelea kukabiliwa na changamoto ya usalama Mashariki mwa nchi hiyo, baada ya waasi wa M23 kuingia katika miji ya Bukavu na Goma, rais Felix Tshisekedi ametangaza mpango wa kuunda serikali ya umoja wa kitaifa kwa kuwashirikisha wanasiasa wa upinzani.Tunajadili iwapo hatua hii itasaidia kutatua mzozo wa mashariki mwa DRC.
Rais wa Marekani Donald Trump, baada ya kurejea madarakani Januari 20, ametangaza hatua ya serikali yake, kusitisha misaada hasa ya kifedha kwa nchi za kigeni, kupitia Shirika la Misaada ya Kimataifa (USAID).Hatua hii inamaanisha nini hasa kwa mataifa ya Afrika ? Tunajadili hili kwa akina na Suba Churchil, rais wa kituo cha taifa cha mashirika ya kiraia akiwa jijini Arusha Tanzania.
Tunajadili visa vya watu kutekwa nyara kuendelea kuripotiwa katika ya mataifa yetu ya Africa hivi karibuni visa kama hivi vikiripoti kwa wingi nchini Kenya, vyombo vya usalama vikituhumiwa kwa utekaji huo. Je nchini mwako kuna visa kama hivyo ? ndio baadhi ya maswali tumeuuliza karibu Haya hapa baadhi ya maoni yako.
Tunajadili visa vya watu kutekwa nyara kuendelea kuripotiwa katika ya mataifa yetu ya Africa hivi karibuni visa kama hivi vikiripoti kwa wingi nchini Kenya, vyombo vya usalama vikituhumiwa kwa utekaji huo. Je nchini mwako kuna visa kama hivyo ? ndio baadhi ya maswali tumeuuliza karibu Haya hapa baadhi ya maoni yako.
Matangazo ya saa nzima kuhusu habari za kutwa, ikiwa ni pamoja ripoti kutoka kwa waandishi wetu sehemu mbali mbali duniani na kote Afrika Mashariki na Kati, na vile vile vipindi na makala maalum kuhusu afya, wanawake, jamii na maendeleo.
Tunajadili ubashiri wako kwa mechi za leo za kuwania ubingwa wa kombe la Afrika, Afcon ambazo zitagarazazwa leo, ikiwa NI nusu fainali DRC ikipiga dhidi ya Ivory Coast nayo Nigeria ikichuana na Afrika Kusini. Nani atatambaa kwenye mechi za leo?Haya hapa baadhi ya maoni yenu?
Tunajadili ubashiri wako kwa mechi za leo za kuwania ubingwa wa kombe la Afrika, Afcon ambazo zitagarazazwa leo, ikiwa NI nusu fainali DRC ikipiga dhidi ya Ivory Coast nayo Nigeria ikichuana na Afrika Kusini. Nani atatambaa kwenye mechi za leo?Haya hapa baadhi ya maoni yenu?
LIVETAK: Tunajadili michuano ya mpira wa miguu AFCON inayoanza Jumamosi nchini Ivory Coast
Tunajadili ziara za Mfalme Charles nchini Kenya na Rais Steinmeier nchini Tanzania na uhusiano kati ya nchi za Afrika Mashariki na watawala wao wa zamani wa kikoloni
Wananchi wa Zimbabwe, wanapiga kura kumchagua rais na wabunge. Rais Emmerson Dambudzo Mnangagwa 80, anapambana na mgombea wake mkuu Nelson Chamisa, 45. Nini hatima ya demokrasia nchini Zimbabwe ? Tunajadili kipimo cha demokrasia katika taifa hilo la Kusini mwa Afrika.
Kwa Undani ni matangazo ya dakika 25 yanayochambua habari kwa undani zaidi na kumpa msikilizaji maelezo ya kina kuliko ilivyo kawaida kuhusu tukio au swala lililojitokeza katika habari.
Kwanini mswada wa fedha unazua gumzo na mjadala nchini Kenya ? Tunajadili hili kwenye Makala ya Wimbi la Siasa
Suluhu ya kudumu kuhusu mzozo wa usalama Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, haijapatikana mpaka sasa. Waasi wa M 23, wameendelea kupambana na wanajeshi wa serikali. Jumuiya ya Kimataifa, inasema suluhu ni ya kisiasa. Je, itawezekana ?Tunajadili hili na wachambuzi, Price Mugasalusha na Edwin Kegolu, kutoka kwenye ukumbi wa Alliance Francais jijini Nairobi.
Didier Deschamps ametangaza kuwa ataendelea kuwa kocha wa timu ya taifa ya soka ya Ufaransa hadi michuano ijayo ya kombe la dunia mwaka 2026. Tunajadili hili na mengine mengi katika Makala ya leo ya Jukwaa la Michezo.
Klabu za soka barani Afrika, zinachuana katika michuano ya kufuzu katika hatua ya makundi kuwania taji la klabu bingwa na Shirikisho barani.Tunajadili hili na mengine mengi.
Mkutano wa wiki hii wa viongozi wa nchi na serikali wanachama wa jumuiya ya maendeleo ya Kusini mwa Afrika SADC imepitisha maazimio kadhaa ambayo wageni wetu wa Livetalk, wakiwa ni pamoja na Wataalam na wachambuzi wa masuala ya kieneo wanayadadisi.
Miongoni mwa yale tuliyokuandalia ni pamoja na Shirikisho la soka barani Afrika CAF, kutangaza kuanza kwa michuano ya Super League, baina ya klabu. Tunajadili hili na mengine mengi.
Siku ya Jumatatu, Juni 13, waasi wa M 23 waliokuwa wanapambana na wanajeshi wa serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, wameuteka mji wa Bunagana, ulio kwenye mpaka na Uganda. DRC inaishtumu Rwanda kwa kuwaunga mkono waasi hao, madai ambayo Kigali inakanusha. Tunajadili.
Shirikisho la soka barani Afrika CAF, limetangaza droo ya michuano ya kufuzu kucheza fainali ya Afrika mwaka 2023 nchini Ivory Coast. Zimbabwe na Kenya ambazo zimefungiwa na FIFA nazo zimejumuishwa. Tunajadili.
Shirikisho la soka barani Afrika, limetangaza droo ya hatua ya robo fainali, kuwania taji la klabu bingwa na Shirikisho barani Afrika.Tunajadili hili na mengine mengi.
Maafisa wa usalama nchini wametekeleza visa vya uhalifu wa kivita na ukiukwaji wa haki wa binadamu dhidi ya Watigray Kaskazini mwa nchi hiyo, kwa mujibu wa ripoti ya pamoja iliyotolewa na Mashirika mawili ya Kimataifa, Amnesty International na Human Rights Watch. Tunajadili hili.
Droo ya michuano ya soka kuwania taji la dunia, imetolewa jijini Doha nchini Qatar. Tunajadili hili na mengine mengi.
Mashirikisho mbalimbali ya michezo, yameifungia Urusi kutoshiriki kwenye mashindano mbalimbali ya kimataifa baada ya kuivamia Ukraine. Tunajadili hili na mengine mengi, Jumamosi hii.
Viongozi wa dini nchini Jamhuri ya Kidemokrasia wameshindwa kuelewana kuhusu ni nani awe Mwenyekiti mpya wa Tume ya Uchaguzi nchini humo CENI kuelekea Uchaguzi Mkuu mwaka 2023. Tunajadili
Tunajadili siku 100 za serikali ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Sama Lukonde.
Michezo ya Olimpiki, iliyocheleweshwa kwa mwaka mmoja kutokana na janga la Covid 19, imeanza rasmi huko jijini Tokyo nchini Japan. Tunajadili nafasi ya mataifa ya Afrika Mashariki na Kati.
Kenya inajiandaa kuwa na Uchaguzi Mkuu mwaka 2022. Vyama vya siasa vimeanza maandalizi kujiweka tayari kwa uchaguzi huo. Lakini je, vyama hivi vimejiandaa vya kutosha ? Tunajadili.
Michuano ya soka kuwania taji la bara Ulaya, imeanza kutifua vumbi. Mashindano ya kuwania taji la French Open katika mchezo wa Tennis, yanafika tamati jijini Paris. Tunajadili, haya na mengine mengi.
Michuano ya mchezo wa soka, hatua ya robo fainali, kuwania taji la klabu bingwa barani Afrika zinachezwa katika mataifa mbalimbali barani Afrika. Tunajadili hili na matukio mengine yanatokea viwanjani wikiendi na wiki hii.
Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ameahidi kukutana na viongozi wa upinzani na kujadiliana nao kuhusu mustakabali wa kisiasa nchini humo baada ya baadhi yao kukimbia nchi na wengine kulalamikia kuminywa kwa misingi ya demokrasia. Je, itakuwaje ? Tunajadili
Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Felix Tshisekedi amesema Kenya imekubali kutuma wanajeshi wake Mashariki mwa nchi hiyo kusaidia katika vita dhidi ya ugaidi, kauli aliyotoa baada ya ziara ya rais wa Kenya Uhuru Kenyatta jijini Kinshasa. Tunajadili.
Bingwa mara mbili wa Michezo ya Olimpiki katika mbio za Mita 800 mwanadada Caster Semenya kutoka Afrika Kusini, anataka kufuzu katika Michezo ya mwaka huu nchini Japan kukimbia mbio za Mita 5,000. Dennis Onyango, kipa wa siku nyingi wa timu ya taifa ya soka ya Uganda, ametangaza kustaafu. Tunajadili haya na mengine mengi.
Utovu wa usalama linasalia suala tata Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Kumekuwa na maandamano ya kutaka jeshi la Umoja wa Mataifa MONUSCO kuondoka nchini humo kwa kushindwa kuwainda raia. Tunajadili
Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, ameagiza kufunguliwa kwa Televisheni za mitandaoni zilizofungiwa. Je, analeta mwamko mpya wa uhuru wa vyombo vya Habari nchini humo ? Tunajadili kwenye Makala ya Wimbi la Siasa.
Klabu ya Simba SC ya Tanzania, na Al Ahly ya Misri, zimefuzu katika hatua ya robof fainali kuwania taji la klabu bingwa barani Afrika. Simba iliishinda AS Vita Club mabao 4-1 lakini Al Ahly ya Misri ilitoka sare ya mabao 2-2 na Al Al-Merrikh ya Sudan. Tunajadili hili na mengine mengi.
Rais mpya wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, amewaahidi raia wake kuwa, hatokuwa na huruma na yeyote atakayehusika na wizi wa fedha za umma. Je, atafanikiwa katika changamoto hii ? Tunajadili.
Timu za taifa za mchezo wa soka za Comoros na Gambia, zimefuzu katika michuano ya bara Afrika, AFCON itakayofanyika mwaka 2022 nchini Cameroon, lakini mataifa mengine kama DRC , Kenya, Tanzania, yakishindwa kufuzu. Tunajadili hili kwa kina.
Patrice Motsepe, ndiye rais mpya wa Shirikisho la soka barani Afrika CAF, anachukua nafasi ya Ahmed Ahmed, baada ya kuidhinishwa na wakuu wa vyama vya soka kutoka mataifa ya bara hilo. Wapenzi wa soka barani Afrika wana matarajio gani ? Tunajadili kwa kina.
Karibui miaka mitatu tangu Ahmad Ahmad kuchaguliwa kuwa rais wa shirikisho la kandanda barani Afrika, CAF, shirikisho hilo linakabiliwa na mshororo wa tuhuma za rushwa na matumizi mabaya ya fedha. Tunajadili katika makala ya Jukwaa la Michezo. Ungana na Fredrick Nwaka akiwa na wachambuzi wa soka Juma Mudimi na Bonface Osano
Rais wa shirikisho la kandanda duniani Fifa Gian Infantino amependekeza fainali za mataifa ya Afrika kuchezw akila baada ya miaka minne badala ya miaka miwili ya sasa. Tunajadili kwa kina katika jukwaa la michezo. Ungana na Fredrick Nwaka akiwa na wachambuzi wa soka Mustapha Mtupa, Samwel John na Bonface Osano
Wananchi wa Msumbiji, wanasubiri matokeo ya Uchaguzi Mkuu baada ya kupiga kura siku ya Jumanne. Ni uchaguzi ambao wachambuzi wa siasa wanasema ni kipimo cha demokrasia na utekelezwaji wa mkataba wa amani uliotiwa saini kati ya waasi wa Renamo na serikali, miezi miwili iliyopita. Tunajadili suala hili.
Venezuela imejikuta katika mzozo wa kisiasa na kiuchumi, kiongozi wa upinzani Juan Guaido amejiapisha kuwa rais, huku kiongozi wa nchi hiyo Nicolas Maduro akitishia kumchukulia hatua kali. Tunajadili hili kwa kina.
DRC imempata rais mpya, Felix Thisekedi. Nchi hiyo ya Afrika ya Kati imeshuhudia ubadilishanaji wa madaraka kwa njia ya amani kwa mara ya kwanza tangu ilipopata uhuru mwaka 1960. Tunajadili hili kwa kina.
Wananchi wa DRC, wanatarajiwa kupiga kura siku ya Jumapili kumchagua rais mpya na viongozi wengine, baada ya zoezi hilo kuahirishwa kwa wiki moja baada ya kuteketea kwa jengo la kuhifadhi vifaa vya kupigia kura jijini Kinshasa. Tunajadili hili, tukiwa na Steven Chondo, mmoja wa maafisa wa kampeni wa mgombea wa chama tawala Emmanuel Shadary, lakini pia Reubens Mikindo , Naibu Katibu Mkuu wa chama kikuu cha upinzani UDPS, ambacho mgombea wake ni Felix Tshisekedi.
Siku 10 kuelekea Uchaguzi Mkuu nchini DRC, mauaji yameripotiwa katika kampeni za siasa hasa katika mikutano ya Martin Fayulu, mgombea vya vyama upinzani lakini pia kuteketea moto kwa jengo la kuhifadhi vifaa vya kupigia kura jijini Kinshasa. Tunajadili hili kwa kina.
Kuelekea Uchaguzi Mkuu nchini DRC, bado kuna mvutano wa matumizi ya mashine za kupigia kura. Wanasiasa wa upinzani na mashirika ya kiraia yanataka zisitumiwe kwa hofu ya wizi wa kura, lakini Tume ya Uchaguzi CENI, inasisitiza kuwa ni sharti zitumiwe. Wajumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, wametoa wito wa kufanyika kwa mazungumzo ili mwafaka kupatikana. Tunajadili hili kwa kina.
Kuna dalili kuwa rais Joseph Kabila wa DRC anapanga kuibadilisha Katiba ili kuwania urais kwa muhula wa tatu. Mabango ya picha ya rais Kabila, yaliyo na maandishi "Huyu ndio mgombea wetu" yameonekana jijini Kinshasa. Hii inamaanisha nini ? Tunajadili.
Tume ya Uchaguzi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo CENI, imepata mitambo ya kieletroniki kuwatambua wapiga kura wakati wa Uchaguzi Mkuu mwezi Desemba. Je, mitambo hii itsaidia Uchaguzi huo kuwa huru na haki ? Tunajadili hili na mbunge wa Francois Rubota kutoka muungano unaomuunga mkono rais Joseph Kabila, Majorite Preidentielle, lakini pia Naibu Katibu Mkuu wa chama Kikuu cha upinzani UDPS Reubens Mikindo.