Makala ya kila siku yanayompa fursa msikilizaji kutoa maoni yake juu ya habari zilizopewa uzito wa juu kwa siku husika. Msikilizaji hushiriki kwa kutuma ujumbe mfupi pamoja na kupiga simu.
Je umoja wa mataifa umesalia kimya ukiukaji wa haki ukiendelea? Skiza makala haya kuskia hisia za waskilizaji wetu.
Kila mwaka tarehe 8 Septemba ulimwengu husherehekea maendeleo katika ujuzi wa kusoma na kuandika katika ngazi ya kimataifa, kikanda na kitaifa. Mwaka huu imekuwa ni fursa ya kutafakari kwa kina kuhusu maana ya kusoma na kuandika katika enzi hii ya kidijitali.
Tunazungumzia hatua ya Kenya na Uganda kukubaliana rasmi kuondoa vizuizi vyote vya kibiashara, vikiwemo vizuizi vya ushuru na visivyo vya ushuru, ili kuwezesha mtiririko huru wa bidhaa, huduma, na watu kati ya mataifa hayo mawili
Kampeni za uchaguzi mkuu wa Tanzania utakaofanyika tarehe 29 Oktoba zimeanza. Chama kikuu cha upinzani Chadema hakipo kwenye kampeni hizi, kufuatia msimamo wake wa kutaka mageuzi kwenye mfumo wa uchaguzi. Wasikilizaji wetu wanazungumzia aje kampeni hii na raia wa Tanzania wanatarajia sera gani kutoka kwa viongozi mbalimbali?
Michuano ya CHAN imemalizika rasmi mwishoni mwa juma, nchini Kenya, Morocco wakitawazwa mabingwa na Madagascar wakimaliza wa pili. Kuisha kwa michuano hii ni mwanzo wa maandalizi ya michuano ya AFCON itakayofanyika tena kwenye nchi za Kenya, Uganda na Tanzania mwaka 2027. Tumemuuliza msikilizaji wetu iwapo amefurahia michuano ya mwaka huu? Timu ipi ilikuwa bora kwake na kipi kifanyike kuelekea mashindano ya AFCON 2027.
Timu za Kenya Uganda na Tanzania zimeaga mchuano katika hatua ya robo fainali
Michuano ya CHAN inaendelea kuchezwa je umeridhishwa na michezo hiyo hadi kufikia sasa Skiza maoni ya mskilizaji.
Nchini Tanzania, nchi hiyo imebuni sheria kuwafungia nje wafanyakazi kutoka mataifa ya nje. Waskilizaji wetu walikuwa na haya ya kusema Skiza makala
Rais wa Kenya William Ruto, yupo kwenye shinikizo kubwa za kuwataja hadharani wabunge na Maseneta, aliodai wanapokea rushwa kutoka kwa Mawaziri na Magavana, asasi za kiraia zinasema hiyo ndio njia pekee ya kuwaaminisha wananchi kuwa, kiongozi huyo ana nia ya kupambana na ufisadi nchini humo.
Baada ya mkutano kati ya rais Donald Trump na rais Volodymyr zelensky na viongozi wa nchi za ulaya jijini Washington siku ya Jumatatu tarehe18 08 2025, Marekani sasa inajaribu kuwakutanisha rais Vladimir Putin na Zelensky ili kupata mwafaka wa mzozo wa Ukraine.
Mapema mwezi Agosti 2025 wabunge walipitisha sheria mpya itakayowaruhusu wasichana wa miaka 15 kupata huduma za uzazi wa mpango bila ruhusa ya wazazi, kwa lengo la kukabili mimba za utotoni. Awali sheria ya nchi hiyo ilikuwa inaruhusu wanawake wa miaka 18 pekee kupata huduma hizo.
Zelensky kuandamana na viongozi wa nchi za Ulaya kukutana na rais Donald Trump kujadili namna ya kumaliza uvamizi wa Urusi nchini Ukraine.
Mada ya leo ni kuhuus michuano ya CHAN inapoendelea kushika kasi kwenye nchi za Kenya, Uganda na Tanzania, nchini Kenya baadhi ya mashabiki wamekuwa wakitumia nguvu kuingia uwanjani bila ya tiketi, hatua ambayo shirikisho la soka la Afrika CAF, limelazimika kupunguza idadi ya mashabiki kuingia uwanjani kwa sababu za kiusalama.,,tumemuuliza nini kifanyike kudhibiti usalama wa mashabiki na viwanja? na Kwenye nchi yako wakati wa mechi kubwa hali huwaje?
Leo ni siku ya mada huru. Tunampa nafasi mskilizaji kuchangia suala lolote ambalo limejiri nchini mwake wiki hii,na pia anaweza kuzungumzia kile ambacho amekisikia katika matangazo yetu ya juma hili.
mada ya leo ni kuhusu Nchini Tanzania ambapo baadhi ya wanasiasa wa CCM ambao hawakufaulu katika uteuzi wa chama, wameanza kuhamia vyama vingine ili kugombea viti mbalimbali kwenye uchaguzi wa oktoba mwaka huu.Hali hii imekuwa ikishuhudiwa pia katika mataifa mbalimbali barani Afrika. Tunamuuliza msikilizaji anaizungumziaje hatua hii ya hama hama kisiasa,na hali hii inashuhudiwa nchini mwake,,
Wawakilishi kutoka kote duniani wanakutana, wako Geneva, kujadili hatua za mwisho za kukabiliana na matumizi ya bidhaa za plastiki ambazo zimeendelea kuharibu mazingira.Tumemuuliza msikilizani ni njia zipi mbadala zitumike badala ya bidhaa za plastiki na anafikiri ni kwa nini nchi hazitaki kuachana na matumizi ya mifuko ya Plastiki.
Al Shabab imezidisha mashambulizi yake na kuiteka miji zaidi wakati vikosi vya umoja wa Afrika vikitarajiwa kuondoka
Rais wa Eritrea Isaias Afwerki ameionya Ethiopia dhidi ya kuzuka tena kwa mzozo kwa kulazimisha kutumia eneo lake ya Bahari.
Nchini Zimbabwe wataalam wanasema wagonjwa wa Malaria wanaongezeka kwa kasi tangu Marekani kupitia shirika lake la USAID kukatisha misaada yake kwa nchi hiyo na bara la Afrika
Kila Ijumaa rfi kiswahili inakupa nafasi ya kuchangia mada yoyote ile kwenye makala haya. Skiza maoni ya waskilizaji.
Maandamano nchini Kenya na mataifa mengine ya Afrika yamekumbwa na mauaji na uporaji huku mali za watu zikiharibiwa. Je, unafikiri ni sahihi kwa waandamanaji kupora na kuharibu mali za watu? Nini vyombo vya usalama vinapaswa kufanya kuzuia uharibifu? Haya hapa baadhi ya maoni yako.
Katika makala haya tujadili hatua ya mahakama ya juu zaidi nchini Kenya, kuagiza kwamba mtoto aliyezaliwa nje ya ndoa kwenye dini ya kiislamu ana haki ya kumiliki mali ya babake kama watoto wengine waliozailiwa ndani ya ndoa, hatua inayoenda kinyume kabisa na tamaduni za dini hiyo. Unazungumziaje uamuzi huu wa mahakama nchini Kenya ? Haya hapa baadhi ya maoni yako.
Kaika makala haya tunajadili hatua ya bunge nchini Ufaransa kupiga kura na kupitisha mswada wa kurudishwa nchini Ivory Coast ngoma maalum inayozungumza iliyochukuliwa katika nchi hiyo ya Afrika kutoka kabila la Ebrie wakati wa ukoloni mwaka 1916. Je umefika wakati kwa koloni za zamani za Bara la Afrika kurejesha vyombo walivyopora ? Ndilo swali tumekuuliza . Haya hapa maoni yako.
Siku ya kiswahili duniani, ambayo imekuwa ikiadhimishwa tangu mwaka 2022. Maadhimisho ya mwaka huu imefanyika jijini Kigali nchini Rwanda, ambako mamia ya wataalam na wapenzi wa Kiswahili wamekutana kwa siku mbili kujadiliana kuhusu nafasi na umuhimu wa lugha ya Kiswahili kwa raia wa nchi zote za Jumuiya. Kauli mbiu ni kusherehekea lugha ya Umoja, utambulisho na mchango wake kwa dunia.RFI kiswahili imeshirikiana na taasisi ya mafunzo ya biashara na ufundi stadi, NIBS ya jijini Nairobi, kuandaa makala maalum ya Habari RAFIKI na mwandishi wetu Ruben Lukumbuka ameongoza makala hii
Wanatuhumiwa kwa mauaji, ugaidi, ubakaji na makosa mengine. Wanaharakati wa haki za binadamu, wanasema, wanawake 14 walibakwa wakati wa maandamano hayo.
Umoja wa Afrika umekaribisha makubaliano yaliyotiwa saini mwishoni mwa juma lililopita kati ya Rwanda na DRC, hatua ambayo itashuhudia unyang'anyaji wa silaha na kuondolewa kwa mamluki wa kigeni mashariki mwa Congo.
Bunge la Uingereza hivi majuzi liliidhinisha mswada wa huduma ya kusaidiwa kufa
Waandamanaji wakabiliana na polisi siku nzima wakati ya maandamano ya kuwakumbuka watu waliopoteza maisha wakati wa maandamano ya mwaka jana ya Gen Z
Rais wa Zambia Hakainde Hichilema ameendelea kusisitiza kufanya mazishi ya kitaifa kwa mtagulizi wake Edgar Lungu Licha ya mzozo uliopo baina yake na familia juu ya utekelezwaji ya matakwa ya marehemu ya kukataa kufanyiwa mazishi ya kitaifa.Tunakuuliza maoni yako kuhusu mzozo huo.
Kila siku ya Ijumaa, hapa RFI Kiswahili, tunampa mskilizaji wetu nafasi kuzungumzia habari kuu ambazo tumekuwa nazo wiki hii au kutueleza jambo lolote ambalo limetokea nchini mwake. Wiki hii maoni mseto yameangazia, miongoni mwa taarifa zingine, tangazo kwamba Rwanda itatia saini makubaliano na DRC tarehe 27 Juni, kumaliza mapigano mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, lakini pia mashambulio baina ya Israeli na Iran.
Rais wa Burundi Evariste #Ndayishimiye ametoa wito kwa upinzani kushiriki katika mazungumzo na chama chake CNDD-FDD baada ya uchaguzi wa wiki iliyopita ambao ulikumbwa na upinzani mkubwa kwa ukosefu wa uwazi. Hata hivyo upinzani haujaonyesha nia ya kushiriki mazungumzo hayo. Tunakuuliza, ni sahihi upinzani kujiunga na serikali ? skiza makala haya kuskia maoni ya mskilizaji.
Juni 12, ni Siku ya Kimataifa ya Kupinga Ajira kwa Watoto. Inakadriwa, takriban watoto milioni 200 kote duniani wanatumikishwa badala ya kuwa shuleni. Tunakuuliza, serikali yako inafanya vya kutosha kukomesha utumwa wa watoto? Unamfahamu mtoto anayefanyishwa kazi?
Makala haya yanaangazia afya ya akili, ikizingatiwa kuwa Juni ni Mwezi wa Uhamasishaji wa Afya ya Akili ya Wanaume. Unafikiri ni kwanini wanaume wanashindwa kutafuta ushauri wa afya ya akili? Unadhani afya ya akili ya mwanaume inasahaulika? Skiliza makala ya leo usikie maoni kutoka kwa waskilizaji wetu.
Leo shaba yetu inalenga nchi ya Rwanda ambapo nchi hiyo imetangaza kujiondoa kwenye Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika ya Kati, na kuituhumu jirani wake DRC, kwa kutumia baadhi ya wanachama kuendeleza ajenda zake zinazokandamiza Rwanda. Skiza makala hay kuskia maoni ya mskilizaji wetu.
Kila Ijumaa rfi Kiswahili inakupa nafasi ya kuchangia mada yoyote iwe kila uliskia kwenye habari zetu au kile kinachoendelea hapo ulipo. Skiza maoni ya mskilizaji.
Leo shaba yetu inalenga taifa la Uganda ambapo rais Yoweri #Museveni pamoja na mkewe wameomba raia wa nchi hiyo msamaha kwa mabaya yote ambayo serikali yao imetekeleza kwa miaka 39. Je, unafikiri kauli ya Rais Museveni na Mama Janet kuomba msamaha ni ya kweli au ni ya kisiasa?Skiza maoni ya mskilizaji wetu.