POPULARITY
Jukwaa la Umoja wa Mataifa kuhusu watu wa jamii za asili limekunja jamvi mwishoni mwa wiki iliyopita hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa na kandoni mwa jukwaa hilo Flora Nducha wa Idhaa hii ya Kiswahili alipata fursa ya kuzungumza na mmoja wa washiriki kiongozi wa kijamii kutoka Jamii ya wafugaji ya Wamaasai mkoani Morogoro Mashariki mwa Tanzania Adam Kulet Ole Mwarabu, wamejadili mengi lakini Ole Mwarabu anaanza kwa kukumbusha alichokibeba kwenye jukwaa la mwaka jana kinavyotekelezwa nchini mwake.
Hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa, mkutano wa 24 wa Jukwaa la Kudumu la Watu wa jamii za asili (UNPFII) linaendelea kujadili utekelezaji wa Azimio la Umoja wa Mataifa kuhusu haki za watu wa asili na kubaini mbinu bora za kushughulikia changamoto zinazowakabili, ukileta pamoja washiriki kutoka maeneo mbalimbali kote duniani. Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa walipata fursa ya kuzungumza na baadhi yao.
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka katika mkoa wa Mwanza kaskazini magharibi mwa Tanzania ambapo vijana wameshika hatamu kuboresha mustakabali wao. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na mashinani tunasalia hapa makao makuu.Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa Kudumisha Amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, MONUSCO, umeikaribisha kusainiwa kwa “Azimio la Kanuni” tarehe 25 Aprili 2025 mjini Washington, D.C chini ya usimamizi wa Wizara ya mambo ya nje ya Marekani, kati ya serikali za DRC na Rwanda kwa lengo la kulinda rai ana kutekeleza azimio la Baraza la Usalama namba 2773 (2025).Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Shirika la Umoja wa Mataifa la msaada kwa wakimbizi wa Kipalestina UNRWA, Juliette Touma, akizungumza na waandishi wa habri mjini Geneva kwa njia ya video kutoka mji mkuu wa Jordan, Amman, wakati kuzingirwa kwa Ukanda wa Gaza kukikaribia kuingia mwezi wa pili amesema “Mzingiro wa Gaza ni muuaji wa kimya muuaji wa watoto, wazee, na watu walioko katika mazingira magumu zaidi. Mzingiro huu unamaanisha kwamba familia nzima, watu saba au wanane wanalazimika kushirikiana kopo moja la maharagwe au njegere”.Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo, FAO limezitaka nchi za Kaskazini Magharibi mwa Afrika kuongeza ufuatiliaji na kuchukua hatua za mapema kudhibiti makundi ya nzige wa jangwani. Hii ni baada ya nzige wakubwa na makundi madogo kutoka ukanda wa Sahel kuhamia maeneo ya kusini mwa Sahara, hasa katikati ya Algeria, magharibi mwa Libya, na kusini mwa Tunisia tangu Februari hadi Machi mwaka huu.Na katika mashinani fursa ni yake Maruping Onkemetse Mkurugenzi na Mwanzilishi wa Kituo cha Msaada wa Familia, shirika linaloongozwa na wanawake wa asili katika Wilaya ya Gantsi, kijiji cha Chobokwane nchini Botswana anayeshiriki mkutano unaoendelea hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa wa Jukwaa la Watu wa Asili akizungumzia alichojifunza hadi sasa.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
Hii leo jaridani tunaangazia wakimbizi wa DRC waliokimbilia Burundi, na ujumbe wa Siku ya Kimataifa ya Hakibunifu. Makala inatupeleka nchini Kenya kuangazia ugonjwa wa malaria na mashinani tunasalia hapa makao makuu katika mkutano wa Jukwaa la watu wa asili.Mazingira ya maisha kwa wakimbizi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC waliongia Burundi na kupelekwa katika kambi ya wakimbizi ya Musenyi si endelevu na yanatishia mustakabali wao. Msemaji wa shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi, UNHCR Ayaki Ito, amesema hayo leo huko Geneva, Uswisi wakati akizungumza na waandishi wa Habari kuhusu hali ya wakimbizi hao wanaoendelea kumiminika nchini Burundi.Kesho Aprili 26 ni Siku ya Kimataifa ya Hakibunifu - Siku ambayo ni fursa kwa ulimwengu kukumbushwa umuhimu wa haki kwa watu wanaobuni mambo mbalimbali duniani. Ili kufahamu zaidi kuhusu Hakibunifu tumezungumza na mtaalamu wa Sheria za Sanaa na Hakimiliki, Wakili Joshua Msambila wa nchini Tanzania, kwanza anaeleza kilichomsukuma yeye kujikita katika eneo hili la sheria.”Makala hii leo ikiwa ni siku ya Malaria duniani tunaelekea Kenya kwa mwandishi wetu Thelma Mwadzaya akiangazia juhudi zinazofanyika kupitia chanjo ili kupambana na malaria ugonjwa mbao Shirika la afya la Umoja wa Mataifa WHO linasema mwaka 2023 pekee ulikatili maisha ya watu 597,000 na na asilimia 95 ya vifo hivyo vilitokea barani Afrika, na sasa linataka juhudi mara dufu zifanyike ili kuutokomeza.Na katika mashinanin fursa ni yake Kulet Adam Ole Mwarabu kiongozi wa jamii ya kimaasai kutoka Tanzania anayeshiriki katika mkutano wa Jukwaa la watu wa asili kutoka hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa na anatoa wito wa maendelo, amani na utunzaji wa ardhi na mazingira kwa jamii ya asili na dunia nzima kwa jumla.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
Hii leo jaridani tunaangazia hali ya kibinadamu katika ukanda wa Gaza, na harakati za utekelezaji wa Azimio la Umoja wa Mataifa kuhusu haki za watu wa asili. Makala tunasalia hapa hapa makao makuu na mashinani tunakwenda nchini Burundi, kulikoni?Hali si hali huko Ukanda wa Gaza eneo la Palestina linalokaliwa na Israeli ambako wakimbizi wa ndani wanakabiliwa na hatari za kiafya ambako panya na wadudu kama vile viroboto na nzi wamesambaa kutokana na mlundikano wa taka na ukosefu wa huduma muhimu kama vile maji safi na salama.Hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa, mkutano wa 24 wa Jukwaa la Kudumu la Watu wa jamii za asili (UNPFII) linaendelea kujadili utekelezaji wa Azimio la Umoja wa Mataifa kuhusu haki za watu wa asili na kubaini mbinu bora za kushughulikia changamoto zinazowakabili. Miongoni mwa shiriki wa jukwaa hilo nimwakilishii wa Shirika la Ereto Solidarity Funds ambaye amepata fursa ya kuzungumza na Sharon Jebichii wa Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa.Makala ikiwa leo ni Siku ya Kimataifa ya Kitabu na Haki Miliki ambapo kila mwaka tarehe kama ya leo siku hii huadhimishwa ili kutambua nguvu ya vitabu kama daraja kati ya vizazi na vizazi na tamaduni mbalimbali. Anold Kayanda wa Idhaa hii amezungumza na mwandishi maarufu wa vitabu vya elimu, Uchumi na uhamiaji, Ernest Makulilo mkazi wa Marekani katika jimbo la Missouri.Na mashinani kupitia video iliyoandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo, FAO fursa ni yake Meena Poudel kutoka nchini Nepal, Kusini mwa Asia ambaye ni Katibu wa kikundi cha wanawake watumiaji wa msitu ambacho kinabadilisha takataka za misitu kuwa mbolea rafiki kwa mazingira huku pia wakijipatia kipato."Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!
Mkutano wa 24 wa Jukwaa la Kudumu la Watu wa jamii za asili (UNPFII) hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa linaendelea kujadili utekelezaji wa Azimio la Umoja wa Mataifa kuhusu haki za watu wa asili na kubaini mbinu bora za kushughulikia changamoto zinazowakabili. Miongoni mwa shiriki wa jukwaa hilo nimwakilishii wa Shirika la Ereto Solidarity Funds ambaye amepata fursa ya kuzungumza na Sharon Jebichii wa Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa. Anaanza kwa kujitambulisha
Jukwaa la Vijana la Baraza la Umoja wa Mataifa la Masuala ya Kiuchumi na Kijamii (ECOSOC) linafanyika katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York Marekani ambapo limeanza tarehe 15 Aprili na linatarajiwa kukamilika tarehe 17 Aprili 2025. Vijana kutoka nchi mbalimbali pamoja na wadau wengine wa masuala ya maendeleo na Uchumi wanakuja pamoja kujadili changamoto mbalimbali na namna bora ya kupatia ufumbuzi katika kuubadilisha ulimwengu kuwa mahali penye usawa zaidi na endelevu chini ya mwongozo wa Ajenda ya mwaka 2030 na Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs). Miongoni mwa wanaohudhuria jukwaa hilo ni Kapwani Kavenuke kutoka nchini Tanzania ambaye amefanyiwa mahojiano na Leah Mushi na hapa anaanza kwa kueleza umuhimu wa mikutano huo.
Hii leo jaridani Assumpta Massoi anamulika masuala ya afya hususan harakati za kukabiliana na majanga yajayo ya afya; wakimbizi huko Zambia ambako sera jumuishi zimewajengea uwezo; Jukwaa la vijana na mchango wa sanaa kwenye usawa na utengamano. Baada ya zaidi ya miaka mitatu ya mazungumzo ya kina, hatimaye leo huko mjini Geneva, Uswisi, nchi wanachama wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani (WHO) zimekamilisha rasimu ya makubaliano ambayo itawasilishwa katika Mkutano wa Afya Duniani mwezi ujao wa Mei. Pendekezo hili linakusudia kuimarisha ushirikiano wa kimataifa katika kuzuia, kujiandaa na kukabiliana na vitisho vya majanga ya kiafya yajayo. Anold Kayanda amefuatilia anatujulisha zaidi.Zambia inaendelea kuwahifadhi zaidi ya wakimbizi 106,000, wengi wao wakiwa kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, Burundi, pamoja na wakimbizi wa zamani kutoka Rwanda na Angola. Limesema shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi UNHCR, likiongeza kwamba kwa kuzingatia sera jumuishi ya Zambia, taifa hilo linakuza mshikamano na wakimbizi na kuwawezesha kujitegemea kupitia makazi maalum na ushirikiano na jamii za wenyeji. Flora Nducha na taarifa zaidi.Jukwaa la Vijana la Baraza la Umoja wa Mataifa la Masuala ya Kiuchumi na Kijamii (ECOSOC) limeanza jana hapa katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa na litamalizika kesho tarehe 17 Aprili. Vijana kutoka nchi mbalimbali wamehudhuria jukwaa hilo akiwemo Kapwani Kavenuke kutoka nchini Tanzania ambaye amehojiwa na Leah Mushi wa Idhaa hii. Kapwani anaanza kwa kueleza umuhimu wa mikutano hii.Gislain Kalwira, Muandaaji wa tamasha la Musika na Kipaji nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC linalofanyika kila mwaka kuleta pamoja wasanii wa kike na wa kiume wa fani mbalimbali, kwa kutambua kuwa jana dunia imeadhimisha siku ya sanaa duniani. Kalwira kupitia video iliyochapishwa na ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini DRC, MONUSCO, anafafanua mantiki ya tamasha hilo na kujenga usawa kijinsia.
Karibu kusikiliza jarida la Umoja wa Mataifa ambapo hii leo tunamulika Kongamano la Kimataifa la Kiswahili linalofanyika mjini Kampala Uganda likiwaleta pamoja wadau kutoka kila kona ya Afrika na kwingineko kujadili mikakati ya kukuza lugha hiyo adhimu ya Kiswahili. Utasikiliza muhtasari wa habari ukiangazia miaka miwili tangu kuanza kwa vita vya sasa vya Sudan, UNHCR, yatoa wito kwamba mwitiko mkubwa wa kibinadamu ulioratibiwa vema ni muhimu ili kuzuia mateso zaidi na vifo kwa wananchi wa DRC, na Jukwaa la Vijana la Baraza la Umoja wa Mataifa la Masuala ya Kiuchumi na Kijamii (ECOSOC) limeanza leo tarehe 15 hadi tarehe 17 katika Makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani.
Kutana na Francine Aka Epse Akaanghui Rais wa Chama cha wanasheria wanawake nchini Côte d'Ivoire huko Afrika Magharibi. Yeye anashiriki mkutano wa 69 wa Hali ya Wanawake duniani, CSW69 akisema taifa lake lina mengi ya kujivunia wakati huu wa kuadhimisha miaka 30 tangu kupitishwa kwa Azimio la Beijing na Jukwaa la Utekelezaji. Francine amezungumza na Assumpta Massoi katika makala hii.
Jukwaa la waandishi lamulika habari zilizotamba wiki hii
Jioni hii kwenye makala ya Jukwaa la Michezo tumeangazia Congo kufutiliwa kushiriki mashindano ya CHAN 2024, kufutwa kazi kwa kocha wa Rwanda Torsten Spittler, uwanja mpya wa Talanta jijini Nairobi unaendelea kupiga hatua kwenye ujenzi huku ligi ya Tanzania ikitajwa nafasi ya nne katika orodha ya ligi bora Afrika, Kenya yang'ara mashindano ya chipukizi ya tenisi, msururu wa raga ya dunia mkondo wa tatu, fainali za Australian Open na tetesi za uhamisho ulaya na Afrika.
Viongozi wa kimataifa wa masuala ya kisiasa na biashara wanaokutana Davos Uswisi kwa ajili ya jukwaa la kiuchumi duniani WEF, leo wamekabiliwa na ukweli mchungu kutoka kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres, akilaani ukosefu wa ushirikiano wa kimataifa katika dunia inayokosa mwelekeo, ikikabiliwa na hatari mbili kubwa ambazo ni mabadiliko ya tabianchi na akili mnemba au AI isiyodhibitiwa. Flora Nducha na taarifa zaidiAkizungumza katika Jukwaa hilo la kila mwaka la Kiuchumi Duniani Katibu Mkuu amewaonya viongozi wa dunia na wakuu wa biashara kuhusu vitisho viwili vinavyoongezeka kwa ubinadamu mabadiliko ya tabianchi na akili mnemba au AI isiodhibitiwa amesema “Kunapokuja suala la tishio la kimataifa nyuklia sio tishio pekee. Leo hii tunakabiliwa na matishio mawili makubwa ambayo yanahitaji kupewa uziti Mkubwa wa kimataifa na hatua kwa sababu yanatishia kubadili kabisa maisha tunayoyajua, janga la mabadiliko ya tabianchi na upanuzi wa kasi wa wigo wa akili mnemba.”Akikosoa ukosefu wa ushirikiano katika kukabiliana na changamoto hizi kubwa, Guterres ametoa wito wa kuchukua hatua za pamoja haraka ili kushughulikia dunia aliyoiita dunia inayokosa mwelekeo “Hebu tukabili ukweli , leo hii watu wengi wanapoitazama dunia hawaoni ushirikiano mkubwa wala maarifa ya kutosha . Licha yah atua zilizopigwa uwekezaji katika nishati jadidifu , teknolojia na masuala ya kiafya ni dunia na matatizo yetu mengi yanazidi kuwa mbaya”Kuhusu mabadiliko ya tabianchi, Guterres amelinganisha uraibu wa dunia kwa nishati ya mafuta na mnyama wa Frankenstein, akisisitiza madhara yake makubwa.Amebainisha kuwa baadhi ya bandari kuu za mafuta duniani ziko hatarini kutokana na viwango vya bahari kuongezeka, jambo linalosababishwa na uchomaji wa makaa ya mawe, mafuta, na gesi asilia.Katibu Mkuu amekemea viwanda na taasisi za kifedha zinazosuasua kwenye ahadi zao za tabianchi, akisema hii ni kukosa maono na usaliti wa sayansi na watumiaji wanaotafuta uendelevu.Akizungumzia hatari na fursa za AI, Guterres ameelezea kama upanga wa makali mawili. Ingawa inatoa matumaini katika kubadilisha sekta za afya, kilimo, na elimu, ameonya kuhusu hatari kubwa ikiwa haitadhibitiwa.Amesema AI isiyodhibitiwa inaweza kuvuruga uchumi, kudhoofisha imani kwa taasisi, na kuongeza ukosefu wa usawa.Guterres amehitimisha kwa kutoa wito wa mshikamano wa kimataifa katika kukabiliana na changamoto hizi muhimu akisema “kubadili mwelekeo wa taasisi kunahitaji kubadili fikra kwa sababu tunakabiliwa na changamoto kubwa zinazoweza kuiangamiza dunia na sishawishiki kwamba viongozi wanalielewa hili.”Amesisitiza umuhimu wa kurekebisha mifumo ya utawala wa kimataifa ili kukabiliana ipasavyo na migogoro ya kisasa, akionya kuwa utashi wa kisiasa ni muhimu lakini bado haupo katika kiwango cha kutosha.Ujumbe wake ni bayana kwamba sasa ni wakati wa kuchukua hatua za pamoja na za haraka.
Matangazo ya nusu saa kuhusu habari za mapema asubuhi pamoja na habari za michezo.
Leo kwenye makala ya kwanza kabisa ya Jukwaa la Michezo mwaka 2025, tumeangazia raundi ya nne hatua ya makundi mechi za Ligi ya vilabu bingwa Afrika. Mwanariadha mkenya Beatrice Chebet avunja rekodi yake ya dunia huku raia wa Eritrea mwendesha baiskeli Biniam Girmay akishinda tuzo la Afrika wakati uo huo mashindano ya magari ya Dakar Rally na Kombe la Mapinduzi yaking'oa nanga. Lakini pia tutatupia jicho tetesi za uhamisho ulaya na michuano ya tenisi ya Brisbane Open inayoendelea.
Hii leo jaridani tunaangazia masuala ya afya na lishe katika nchi zinazokumbana na ukame. Makala tunakwenda Ureno na mashinani nchini Sudan, kulikoni?Mkurugenzi mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani WHO, amesema amestushwa na kusikitishwa na kifo cha aliyetarajiwa kushika wadhifa wa mkurugenzi mkuu wa WHO Kanda ya Afrika Dkt. Faustine Engelbert Ndungulile kutoka nchini Tanzania.Awamu ya pili ya mradi wa kuboresha lishe, SUN II nchini Zambia umewezesha wakulima kupanda mazao yanayohimili ukame na vile vile kukabiliana na viwavi jeshi kwa kutumia mbinu za asili, mradi uliotekelezwa na shirika la Umoja la kuhudumia watoto, UNICEF ili wakulima wasikumbwe na njaa wakati huu ambapo ukame umetikisa nchi za kusini mwa Afrika.Jukwaa la 10 la Umoja wa Mataifa la Ustaarabu limekunja jamvi leo huko Cascais, Ureno ambako sambamba na jukwaa hilo, pia vijana kutoka makundi 150 duniani walikusanyika katika jukwaa lao wakiwemo watengeneza filamu chipukizi ambao kupitia filamu wanaeleza mambo kadha ya ulimwengu kama uhamiaji, ujumuishaji, kupambana na ubaguzi na mengine mengi. Miongoni mwa vijana hao ni Dativa Mahanyu na Mariam Mintanga kutoka Tanzania. Kwanza tumsikilize Mariam Mintanga akieleza alivyojisikia kuhudhuria mkutano huu kisha tutamsikia Dativa Mahanyu akieleza kuhusu filamu ya Fid ya ambayo kupitia taasisi ya Tai Tanzania imepata tuzo ya PLURAL+.Na mashinani fursa ni yake Shaza Ahmed, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la wanawake Nada El Azha linalotoa msaada kwa waathirika wa unyanyasaji wa kijinsia nchini Sudana akitoa wito kwa viongozi wa kimataifa wa kutokomeza ukatili wa kijinsia.Mwenyeji wako ni Bosco Cosmas, karibu!
Jukwaa la 10 la Umoja wa Mataifa la Ustaarabu limekunja jamvi leo huko Cascais, Ureno ambako sambamba na jukwaa hilo, pia vijana kutoka makundi 150 duniani walikusanyika katika Jukwaa lao. Katika vijana hao walikuwemo watengeneza filamu chipukizi ambao kupitia filamu wanaeleza mambo kadha ya ulimwengu kama uhamiaji, ujumuishaji, kupambana na ubaguzi na mengine mengi. Miongoni mwa vijana hao waliohudhuria ni Dativa Mahanyu na Mariam Mintanga kutoka Tanzania. Kwanza tumsikilize Mariam Mintanga akieleza alivyojisikia kuhudhuria mkutano huu kisha tutamsikia Dativa Mahanyu akieleza kuhusu filamu ya Fid ya ambayo kupitia taasisi ya Tai Tanzania imepata tuzo ya PLURAL+
Hii leo jaridani tunakletea mada kwa kina ambayo tunamskia mwanamke mjasiriamali kutoka visiwa vya Karibea St. Kitts na Neves akitumia fursa ya utamaduni wake mchanganyiko wa asili ya Visiwa hivyo na wa Kiswahili kujikwamua kiuchumi kupitia ubunifu wa mitindo na shughuli za mama lishe. Pia tunakuletea muhtasari wa habari zikiwemo za mgogoro Lebanon, Afya ya kinywa, na Ujumbe wa Katibu Mkuu kutoka Portugal akihutubia Jukwaa la 10 la Umoja wa Mataifa la Muungano wa Ustaarabu, (UNAOC). Mashinani tunakupeleka katika ukanda wa Gaza kumsikia muathirika wa vita ya Israel.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
Leo ikiwa ni siku ya kimataifa ya kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake, Je wajua kwamba wanawake na wasichana 140 walifariki dunia kila siku duniani kote mwaka 2023 wakiwa mikononi mwa wapenzi wao au ndugu wa karibu, ikimaanisha kuwa mwanmake mmoja anauawa katika kila dakika 10. Na zaidi ya yote bara la Afrika linaongoza? Maudhui ya siku hii yanasema “Hakuna kisingizio” cha ukatili dhidi ya wanawake lama alioushuhudia Ester manusura kutoka Uganda, ambaye kwa miaka mingi amekuwa akifanyiwa ukatili na mpenzi wake anaema “Nilikuwa na umri wa miaka 15 aliponioa naye alikuwa na miaka 28wakati mwingine alikuwa akinivua nguo zote na kunilazimisha kukaa kwenye varandana nilikuwa nikichelewa kurudi ananitandika nje nyumba kila mtu kushuhudia Nilikuwa katika hali mbaya ya uchungu Mkubwa na kuvuja damu.”maadhimisho ya mwaka huu yanaambatana na ripoti iliyotolewa leo jijini New York, Marekani na mashirika ya Umoja wa Mataifa likiwemo lile la masuala ya wanawake, UN Women na Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kudhibiti Dawa za kulevya na Uhalifu, (UNODC), inaangazia mwanga wa janga la mauaji ya wanawake na kutoa wito kwa hatua za dharura ili kukabili janga hilo.Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres katika ujumbe wake wa siku hii inayoadhimishwa tarehe 25 mwezi Novemba kila mwaka, ikiashiria pia kuanza kwa siku 16 za kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake, zikiwa na kilele chake tarehe 10 mwezi Desemba, siku ya Haki za Binadamu duniani amesema “Janga la ukatili dhidi ya wanawake na wasichana linaaibisha ubindamu, dunia lazima iitikie wito huu. Tunahitaji hatua za dharura kwa ajili ya haki na uwajibikaji, na kusaidia uchechemuzi.”Mkurugenzi mtendaji wa UN Women Sima Bahous amesisitiza kuwa “Ukatili dhidi ya wanawake na wasichana si kwamba hauepukiki, unaweza kuzuilika. Tunahitaji sheria thabiti, ukusanyaji bora wa takwimu, uwajibikaji zaidi wa serikali, utamaduni wa kutovumilia, na kuongezeka kwa ufadhili kwa mashirika ya kupigania haki za wanawake na taasisi. Tunapokaribia kuadhimisha miaka 30 ya Azimio la Beijing na Jukwaa la Utekelezaji mwaka 2025, ni wakati wa viongozi wa dunia kuungana na kuchukua hatua kwa haraka, kujitolea na kuelekeza rasilimali zinazohitajika kumaliza mgogoro huu mara moja na kwa wote”Mauaji ya wanawake yanavuka mipaka, hali ya kiuchumi na kijamii, utamaduni. Hata hivyo kiwango au ukubwa wake unatofautiana.Kwa mujibu wa ripoti hiyo, bara la Afrika lilivunja rekodi ya kuwa na viwango vya juu vya wanawake kuuawa na wapenzi wao au mwanafamilia. Wanawake 21,700 waliuawa Afrika mwaka huo wa 2023, ikifuatiwa na bara la Amerika na kisha Oshenia.Mashirika ya UN Women na…
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayoangazia uvuvi katika mji wa Kalokol karibu na fuo za Ziwa Turkana Kaskazini mwa Kenya. Pia tunakuletea muhtasari wa habari zikiwemo za mkutano wa WUF12 Cairo Misri, chanjo ya malaria Sudan, siku ya Tsunami, na mashinani.Mkutano wa 12 wa Jukwaa la Miji Duniani, WUF12 umeingia siku ya pili hii leo huko Cairo, Misri, ambako Ming Zing ambaye ni Mkurugenzi wa Miji, Mnepo na Ardhi kutoka Benki ya Dunia amezungumzia umuhimu wa kujumuisha wanawake na vijana katika mipango miji.Sudan imekuwa nchi ya 16 barani Afrika na ya kwanza katika Ukanda wa WHO wa Mashariki na Mediterania kuanzisha chanjo dhidi ya Malaria kwa watoto wasiozidi umri wa miezi 12. Chanjo imeanza kutolewa jana katika majimbo ya Gedaref na Blue Nile ambapo WHO na wadau wamesema mwaka 2025 na 2026 chanjo itapelekwa katika maeneo 129 nchini kote Sudan.Na leo ni siku ya kimataifa ya kuhamasisha umma kuhusu tsunami, ambayo ni mawimbi makubwa ya maji yatokanayo na tetemeko chini ya bahari. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres katika ujumbe wake anasema pamoja na kukumbuka waliopoteza maisha kwa tsunami miaka 20 iliyopita, tunaahidi tena kulinda zaidi ya watu milioni 700 duniani kote walio hatarini kukumbwa na Tsunami.Mashinani tutaelekea Sudan kusini kuangazia harakati za Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa Kulinda Amani nchini humo, UNMISS za kuimarisha ulinzi wa wanawake katika migogoro na majanga.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
Karibu ufuatilie kipindi cha Jukwaa la Vijana ambapo katika kipindi hiki tunajadili mada kuhusu “utengenezaji wa Nishati mbadala. L'articolo Je unafahamu jinsi ya kutengeneza nishati mbadala ya kupikia? proviene da Radio Maria.
Mkutano wa siku tatu unaolenga kuendeleza bara la Afrika kupitia ukuaji endelevu wa miji umeanza leo jijini Addis Ababa, Ethiopia kwa ushirikiano wa Muungano wa Afrika, shirika la Umoja wa Mataifa la Makazi Duniani, UN Habitat na Serikali ya Ethiopia. Anold Kayanda ameifuatilia siku ya kwanza ya mkutano huu wa siku tatu na hii ni taarifa yake.(Taarifa ya Anold)Ni mkutano ambao unawapa jukwaa wadau wakuu kutoka kote barani Afrika kuendeleza malengo ya Ajenda ya mwaka 2063 inayosema Afrika Tunayoitaka.Jukwaa hili litachunguza jukumu muhimu la ukuaji wa miji katika kufikia malengo ya Ajenda 2063 na kuunda mustakabali wa miji ya Afrika kwa kuweka mikakati ya kujenga miji ambayo ni endelevu kwa mazingira, inayojumuisha jamii, na inayostahimili uchumi.(Nats)Huyo ni Mkurugenzi wa Kitengo cha Ushirikiano wa Kikanda na Biashara cha Kamisheni ya Umoja wa Mataifa ya Uchumi kwa ajili ya Afrika (ECA), Dkt. Stephen Karingi akihutubia mkutano huo anaeleza kuwa ukuaji wa miji wa haraka barani Afrika umekuja na changamoto kama miundombinu duni, kukosekana kwa usawa wa kijamaa na kiuchumi na changamoto za tabianchi na akatumia nafasi hiyo kutoa ahadi kuwa Kamisheni ya Umoja wa Mataifa ya Uchumi kwa ajili ya Afrika (ECA) iko tayari kushirika katika kuzitatua changamoto hizo kwa kuchukua hatua mbalimbali ikiwemo kuweka Sera fanisi za Uchumi mkuu na ufadhili kwa ajili ya maendeleo.Mkutano huu utahusisha shughuli mbalimbali ikiwemo mijadala, matukio ya kandoni mwa mkutano na maonesho.Tags: UN-Habitat, Afrika, Africa Urban Forum, Ajenda 2063
Je umeshawahi kujiuliza ni kwa vipi wataalamu wa kemia wanahusiana na ujasiriamali? Kama ndivyo, basi vivyo hivyo kwa Assumpta Massoi akiwa Manama, nchini Bahrain akishiriki Jukwaa la Nne la Uwekezaji kwa Wajasiriamali, WEIF2024 lililoandaliwa na shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Viwanda, UNIDO, Ofisi ya Uendelezaji wa Biashara, ITPO nchini humo, alikutana na Profesa Ruth Wanjau, Mtafiti na Mshauri wa Masuala ya STEM yaani Sayansi, Teknolojia, Uhandisi na Hisabati katika Chuo Kikuu cha Kenyatta nchini Kenya. Alimuuliza maswali kadhaa ikiwemo ushiriki wake kwenye jukwaa hilo na nini anafanya kusongesha ujasiriamali.
A man believed to be in his early 30s, Gideon Nanpark has been found dead at Jukwa at Western in the Wassa Amenfi East District. Brother of the deceased Evans Yennukwa says his brother from Accra Amassan went to Jukwaa in the Western Region to visit a friend who introduced him to Galamsey.
Wana jumuiya wa Afrika wanao ishi mjini Sydney wamepata sababu yakufanya mtoko, ambao unajumuisha kila mwanachama wa familia.
Hii leo jaridani mwenyeji wako ni Leah Mushi akimulika mkutano wa mifumo ya chakula ulioanza leo Roma, Italia; Kauli ya mshiriki kutoka Tanzania kwenye mkutano uliomalizika hivi karibuni hapa makao makuu ya UN; Makala anabisha hodi Rwanda ilhali mashinani anakupeleka Tunisia.1. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amezungumza kwenye mkutano wa viongozi kuhusu Mifumo ya Upatikanaji wa Chakula huko Roma, Italia hii leo akisema bado inastaajabisha kuwa katika dunia yenye utajiri bado kuna watu hawana chakula au wanakufa njaa, huku akipendekeza mambo makuu matatu ya kuzingatia ili kurekebisha mifumo hiyo.2. Mwanaisha Ulenge ambaye ni Mbunge katika Bunge la Tanzania na pia Mjumbe wa Bunge la Dunia IPU, mmoja wa walioshiriki Jukwaa la Umoja wa Mataifa la Ngazi ya juu la kisiasa kuhusu Malengo ya Maendeleo Endelevu, SDGs, lililokamilika wiki iliyopita akihojiwa na Anold Kayanda wa Idhaa hii ya Umoja wa Mataifa hapa jijini New York, Marekani ametoa wito kwa wanawake ulimwenguni kote kwamba wao pia wanapaswa kuwa na mchango katika kuleta usawa wa kijinsia kwanza kwa wao wenyewe kutojiwekea mipaka.3. Makala: Leo inatupeleka mjini Kigali Rwanda ambako mwishoni mwa wiki umekamilika mkutano wa kimataifa wa Women Deliver 2023 (WD2023) au wanawake wanatekeleza. Mkutano ulijikita na suala la ujumuishwaji ili kusongesha usawa endelevu wa kijinsia. Ulihudhuriwa na washiriki zaidi ya 200,000 mtandaoni na ana kwa ana, miongoni mwao ni Martha Wanza kutoka Kenya, anayefanyakazi na shirika la Jumuiya ya wanawake vijana Wakristo nchini humo YWCA.4. Mashinani: Jinsi mkopo na mafunzo kutoka mfuko wa Umoja wa Mataifa wa maendeleo ya kilimo, IFAD umemuinua kiuchumi Hayet Aouida nchini Tunisia.
Jukwaa la Umoja wa Mataifa la ngazi ya juu la kisiasa kuhusu malengo ya maendeleo endelevu HLPF limekunja jamvi mwishoni mwa wiki iliyopita kwenye Makao makuu ya Umoja wa Mataifa New York Marekani baada ya siku 10 za tathimini ya utekelezaji wa malengo hayo au SDGs. Mhandisi Mwanaisha Ulenge ambaye ni Mbunge katika Bunge la Tanzania na pia Mjumbe wa Bunge la Dunia IPU, mmoja wa walioshiriki Jukwaa hilo la Umoja wa Mataifa la Ngazi ya juu la kisiasa kuhusu SDGs, akihojiwa na Anold Kayanda wa Idhaa hii ya Umoja wa Mataifa hapa jijini New York, Marekani ametoa wito kwa wanawake ulimwenguni kote kwamba wao pia wanapaswa kuwa na mchango katika kuleta usawa wa kijinsia kwanza kwa wao wenyewe kutojiwekea mipaka. Lakini kwanza Mwanaisha Ulenge anaanza kwa kueleza ushiriki wa wabunge katika jukwaa hili la HLPF akisema, “Kikao hiki ambacho tumeshiriki hapa katika Umoja wa Mataifa (New York, Marekani) ni kikao ambacho kinaangazia namna ambavyo Bunge la Tanzania limeweza kuisimamia serikali katika utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu, SDGs. Ndilo lilikuwa lengo kubwa kama Bunge kuangalia ni namna gani ambavyo serikali imeweza kutekeleza. Kwa hiyo serikali pia wameleta watu wao wamewasilisha lakini na Bunge sisi tumewasilisha namna ambavyo tumeisimamia serikali katika kutekeleza Malengo ya Maendeleo Endelevu ya Dunia.” Na kwa kuwa yeye ni mbunge mwanamke na wakati huo huo bado kuna changamoto kwa wanawake kuzifikia nafasi hizo za kushiriki katika ngazi za maamuzi, Mhandisi Mwanaisha Ulenge ana ujumbe kwa wasichana na wanawake kote ulimwenguni kuhusu mchango wao kufanikisha kuondoa pengo la usawa wa kijinsia. “Hakika usawa wa jinsia ni sehemu ya yale Malengo 17 ya Maendeleo Endelevu.” Anasema Mwanaisha akiongeza, “Kwa hiyo mimi niwaambie wanawake kwamba tuna uwezo sawa wa kuweza kuhudumu na kuweza kufanya makubwa kama jinsia nyingine. Mahali popote pale mwanamke ukiweka dhamira ya dhati kabisa katika kulifanya jambo kwa dhamira kubwa na pana inawezekana. Anahitimisha kwa kusema, “Tusijiwekee mipaka na wala tusiwe na woga.”
Jukwaa la Umoja wa Mataifa la ngazi ya juu la kisiasa kuhusu malengo ya maendeleo endelevu HLPF limekunja jamvi jana hapa Makao makuu ya Umoja wa Mataifa New York Marekani baada ya siku 10 za tathimini ya utekelezaji wa malengo hayo au SDGs. Waakilishi wa nchi na serikali, wanazuoni, mashirika ya Umoja wa Mataifa, wanaharakati na vijana ni miongoni mwa waliohudhuria. Kenya haikubaki nyuma katika jukwaa hilo. Susan Auma Mang'eni katibu mkuu wa wizara ya ushirika na biashara ndogondogo wa Kenya alibeba bendera yataifa hilo miongoni mwa waliowasilisha tarifa katika mkutano wa vijana kandoni mwa jukwaa hilo amenieleza kuwa moja ya changamoto kubwa ya utekelezaji wa malengo hayo hasa kwa nchi zinazoendelea kama Kenya ni ufadhili ulioahidiwa na mataifa tajiri ya G20 ambao bado haujatolewa kwa nchi zinazoendelea, “Zikitusaidia sasa tutaweza kuweka mikakati ambayo inatakikana ili tuweze kupunguza hali ngumu ya Maisha na kando ya hapo katika kuangalia masuala ya mabadiliko ya tabianchi tumejitoa ndio maana kuanzia tarehe 4 hadi tarehe 6 mwezi ujao tutakuwa na kongamano kubwa sana la Afrika la kuweza kuangazia mambo ya hatua dhidi ya mabadiliko ya tabianchi tukijiandaa kwenye kwenye kongamano la COP28.”Susan amekiri kwamba changamoto za hali ngumu ya maisha zinazochangiwa na sababu lukuki ikiwemo mabadiliko ya tabia nchi, na vita inayoendelea baina ya Urusi na Ukraine hususa kwa Kenya zimechochea hali ya uchumi hasa mifukoni mwa watu kuwa mbayá zaidi wengi wakishindwa kumudu Maisha ya kila siku na kuzusha maandamano, hata hivyo amesema serikali imesikia kilio chao na inajitahidi kuleta afueni amewasihi Wakenya kuwa na subirá, “Ningependa kuwaambia Wakenya kwamba serikali ina mikakati tulieni, tufanye bidii , tupange pamoja hali itakuwa nzuri, tukiendelea kwenda kufanya maandamano ambayo ni maharibifu katika hiyo hali watu wanapoteza maisha, watu wanaumia hata askari pia wanaumia tuanendelea kufanya hii hali iwe hata ghali kiasi. Ugali hauko barabarani, ugali uko mashambani kwetu , ugali uko kwenye bidii yetu ya biashara ndogondogo. Niwaomba Wakenya kwamba msikubali kupelekwa barabarani bila msimamo kwa sababu hizo changamoto sio za Kenya peke yake.”Mapema wiki hii ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa ilitoa tarifa ikisema inatiwa hofu na maandamano yanayoendelea Kenya baada ya watu 23 kuuawa katika maandamano hayo huku ikivisihi vyombo vya ulinzi na usalama kutotumia nguvu kupita kiasi dhidi ya waandamanaji kwani kuandamana ni haki yao ya msingi ya kiraia.
Hii leo jaridani tunaangazia Afya na malengo ya maendeleo endelevu. Makala tunakupeleka nchini DRC na mashinani nchini Rwanda, kulikoni? Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ulimwenguni WHO limesema takriban nusu ya idadi ya watu ulimwenguni hivi sasa wapo hatarini kuungua ugonjwa wa Dengue huku ikikadiriwa kila mwaka watu kati ya milioni 100 mpaka 400 wanapata maambukizi..Jukwaa la Umoja wa Mataifa la ngazi ya juu la kisiasa kuhusu malengo ya maendeleo endelevu HLPF limekunja jamvi jana hapa Makao makuu ya Umoja wa Mataifa New York Marekani baada ya siku 10 za tathimini ya utekelezaji wa malengo hayo au SDGs. Waakilishi wa nchi na serikali, wanazuoni, mashirika ya Umoja wa Mataifa, wanaharakati na vijana ni miongoni mwa waliohudhuria. Kenya haikubaki nyuma katika jukwaa hilo.Makala inatupeleka nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo - DRC, ambapo Shirika la Umoja wa Mataifa la kutegua Mabomu ya ardhini (UNMAS) Jumanne Julai 18 mwaka huu wa 2023 lilitegua bomu lenye uzito wa kilo 250 lililogunduliwa wiki iliyopita na wakulima katika eneo la Kididiwe, wilayani Beni. Jimboni Kivu Kaskazini. Wakazi wanaonesha furaha yao kwa Umoja wa Mataifa kwa kutegua bomu hilo linalosababisha vifo. .Mashinani tutaelekea nchini Rwanda kusikia ni kwa jinsi gani programu ya remedial ambayo imewafikia watoto zaidi ya 10,000 katika shule 200 na vituo 10 vya vijana imeboresha masomo kwa wanafunzi.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina ambapo Jukwaa la ngazi ya juu la kisiasa kuhusu malengo ya maendeleo endelevu lijulikanalo kama HLPF linafikia tamati hii leo hapa katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York-Marekani. Wawakilishi wa nchi na serikali, wanasayansi, wanazuoni, mashirika ya umoja wa Mataifa, asasi mbalimbali na vijana wamekutana kuanzia tarehe 10 Julai kujadili hatua za kuchukua ili kuhakikisha malengo hayo muhimu ya maendeleo yanatimizwa ifikapo mwaka 2030. Leah Mushi ameketi chini na Gavana wa Kauti ya Kakamega Fernandes Baraza pamoja na Mbunge wa Likuyani Innocent Mugabe wote kutoka nchini Kenya kuzungumza nini wanaondoka nacho baada ya Siku 10 za mkutano huu. Pia tunakuletea habari kwa ufupi zikiwemo ajenda ya Katibu Mkuu, ubaguzi nchini Libya, Mafuta katika meli nchini Yemen. Katika kujifunza lugha ya Kiswahili nakupeleka kwake Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili la Zanzibar, BAKIZA upate uchambuzi wa neno NAZAA. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres kupitia mfululizo wa mapendekezo yake yanayojulikana kama “Ajenda Yetu ya Pamoja” ambayo yanaonesha maono yake kwa miongo ijayo, hii leo akiwa amejikita na Ajenda Mpya ya Amani, ametoa mapendekezo kadhaa na hatua miongoni mwake ikiwa ni kuondoa silaha za nyuklia; kuboresha mbinu ya shughuli za amani na kushughulikia uhusiano kati ya tabianchi, amani na usalama.Wataalamu wa Umoja wa Mataifa leo wameelezea wasiwasi wao kuhusu sera ya kibaguzi iliyotangazwa na Serikali ya Umoja wa Kitaifa ya Libya (GNU) mwezi Aprili mwaka huu 2023 ambayo inazuia haki za wanawake na wasichana kusafiri nje ya nchi bila msimamizi wa kiume au Mahram. Wataalamu hao wamesema, "Siyo tu sera hii ni ya kibaguzi, lakini pia inazuia uhuru wa kutembea ikiwa ni pamoja na wanafunzi wanaoondoka nchini kwenda kusoma nje ya nchi," na kwamba wanawake na wasichana wanaokataa kujaza au kuwasilisha fomu wanazuiwa kuondoka nchini Libya.Na Shirika la Umoja wa Mataifa la UNDP limetangaza kwamba tayari Meli inayofahamika kwa jina Nautica au Yemen, tayari imeifikia meli nyingine ya FSO Safer katika katika ufukwe wa Yemen tayari kuanza kupakua mapipa milioni 1.14 ya mafuta ghafi ambayo kutokana na hali mbaya ya usalama katika ukanda huo yamekwama katika FSO Safer na yanatishia usalama kwani yanaweza kuvuja au kulipuka.Katika kujifunza lugha ya Kiswahili Dkt. Mwanahija Ally Juma, Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili la Zanzibar, BAKIZA anatufafanualia maana ya neno “NAZAA.”Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!
Jukwaa la ngazi ya juu la kisiasa kuhusu malengo ya maendeleo endelevu lijulikanalo kama HLPF linafikia tamati hii leo hapa katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York-Marekani. Wawakilishi wa nchi na serikali, wanasayansi, wanazuoni, mashirika ya umoja wa Mataifa, asasi mbalimbali na vijana wamekutana kuanzia tarehe 10 Julai kujadili hatua za kuchukua ili kuhakikisha malengo hayo muhimu ya maendeleo yanatimizwa ifikapo mwaka 2030. Leah Mushi ameketi chini na Gavana wa Kauti ya Kakamega Fernandes Baraza pamoja na Mbunge wa Likuyani Innocent Mugabe wote kutoka nchini Kenya kuzungumza nini wanaondoka nacho baada ya Siku 10 za mkutano huu.
Jukwaa la ngazi ya juu la kisiasa la Umoja wa Mataifa kuhusu malengo ya maendeleo endelevu HLPF, linaendelea hapa Makao Makuu jijini New York Marekani likitathimini utekelezaji wa malengo hayo yaliyosaliza chini ya miaka 7, kabla ya kufikia ukomo hapo mwaka 2030. Mbali ya tathimini ya utekelezaji wake jukwaa hilo limetoa fursa kwa nchi 39 zilizojitolea kuwasilisha ripoti za kitaifa za utekelezaji wa malengo hayo. Tanzania ni miongoni mwa nchi hizo na iliwasilisha ripoti yake jana Jumanne. Reynald Maeda, Mkurugenzi wa asasi ya Umoja wa Mataifa Tanzania, UNA ni miongoni mwa waliochangia katika ripoti hiyo kwa sasa yuko hapa New York akishiriki jukwaa hilo lakini kabla hajaondoka Tanzania alizungumza na Stella Vuzo wa kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa UNIC Dar es salaam akianza kwa kumueleza mchango wa asasi hiyo katika ripoti iliyowasilishwa.
Hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa New York, Jukwaa la ngazi ya juu la kisiasa la Umoja wa Mataifa kuhusu malengo ya maendeleo endelevu kwa kifupi HLPF linakaribia kufikia ukingoni na leo Mjumbe Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu vijana aliitisha kikao cha kando kuzungumza na vijana kuhusu tathmini yao ya utekelezaji wa Mkakati wa Umoja wa Mataifa kuhusu vijana katika kufanikisha malengo ya maendeleo endelevu, SDGs. Miongoni mwa walioshiriki ni Gibson Kawago, mmoja wa viongozi vijana wa kusongesha SDGs. Nimezungumza naye kufahamu mambo kadhaa ikiwemo alichowasilisha kwenye mkutano huu.
Hii leo jaridani machafuko nchini DRC na mjadala kuhusu malaengo ya maendeleo endelevu unaoendelea hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa. Makala tunasalia hapa hapa makao makuu na mashinani tunakupeleka nchini Tanzania, kulikoni? Hali ya kusikitisha inajitokeza Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, ambapo ghasia zilizozuka upya kati ya makundi yasiyo ya kiserikali yenye silaha na vikosi vya serikali zimerejea katika majimbo ya Kivu Kaskazini, Kivu Kusini na Ituri zikiambatana na ukatili mkubwa dhidi ya wanawake na wasichana na kutawanya maelfu ya watu , limeonya leo shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR.Malengo ya maendeleo endelevu SDGs yanahimiza kuwa wakati wa utekelezaji wake hakuna mtu anapaswa kuachwa nyuma. Makala tunasalia hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa ambapo Jukwaa la ngazi ya juu la kisiasa kuhusu malengo ya maendeleo endelevu HLPF limeingia siku yake ya 5. Tunaendelea kuzungumza na washiriki wa Jukwaa hili na leo ni zamu ya Lawrence Oluwaseun Adeniyi ambaye ni afisa wa Jumuiya ya Kimataifa ya Wachechemuzi wa Amani Ulimwenguni anayehusika na Malengo ya Maendeleo Endelevu.Na katika mashinani tuatelekea Arusha nchini Tanzania kusikia ujumbe wa mhudumu wa afya ambaye anatembea boma kwa boma mashinani kutoa huduma za chanjo.Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!
Lawrence Oluwaseun Adeniyi, raia wa Nigeria anayefanya shughuli zake Houston Marekani amewakilisha taasisi hii ya International Association of World Peace Advocates (IAWPA) inayojitambulisha kwa kazi kuu mbili ambazo ni Utetezi wa Amani na Kuhakikisha Maendeleo Endelevu. Je analoondoka nalo kwenye Jukwaa hili ni lipi? Karibu!
Jukwaa la ngazi ya juu la kisiasa kuhusu malengo ya maendeleo endelevu lijulikanalo kama HLPF limeingia siku yake ya nne hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York-Marekani. Wawakilishi wa nchi na serikali, wanasayansi, wanazuoni, mashirika ya umoja wa Mataifa, asasi mbalimbali na vijana wanakutana kujadili hatua za kuchukua ili kuhakikisha malengo hayo muhimu ya maendeleo yanatimizwa ifikapo mwaka 2030. Mmoja wa wanaoshiriki ni Job Nyangenye Omanga, raia wa Kenya anayeishi Texas-Marekani akijishughulisha na sekta ya afya hapa Marekani na nyumbani Kenya. Mwenzangu Anold Kayanda amezungumza naye na kwanza Omanga anaanza kueleza ujumbe aliokuja nao kwenye Jukwaa hili.
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina ambapo Jukwaa la ngazi ya juu la kisiasa kuhusu malengo ya maendeleo endelevu lijulikanalo kama HLPF limeingia siku yake ya nne hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York-Marekani. Wawakilishi wa nchi na serikali, wanasayansi, wanazuoni, mashirika ya umoja wa Mataifa, asasi mbalimbali na vijana wanakutana kujadili hatua za kuchukua ili kuhakikisha malengo hayo muhimu ya maendeleo yanatimizwa ifikapo mwaka 2030. Pia tunakuletea habari kwa ufupi zikiwemo migogoro nchini Sudan, ripoti ya UNAIDS na msaada wa kibinadamu nchini Zimbabwe. Katika kijifunza Kiswahili tunataungana na mtaalam wetu Onni Sigalla kutoka BAKITA Tanzania. Miili ya takriban watu 87 ya kabila la Masalit na wengine wanaodaiwa kuuawa mwezi uliopita na vikosi vya msaada wa haraka RSF na washirika wao huko Darfur Magharibi nchini Sudan, imezikwa kwenye kaburi la pamoja huko El-Geneina kwa amri ya vikosi hivyo kulingana na taarifa za kuaminika ambazo Ofisi ya Haki za Kibinadamu ya Umoja wa Mataifa imezipata.Ripoti mpya iliyotolewa leo na shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya UKIMWI UNAIDS imeeleza kuna njia ya wazi kabisa ya kumaliza UKIMWI ulimwenguni ifikapo mwaka 2030 na njia hiyo inaweza kusaidia kujiandaa na majanga mengine makubwa yasiyo tazamiwa na hivyo kuwezesha ufikiaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu. Na shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP, limekaribisha mchango wa dola milioni 2 uliotolewa na shirika la Marekani la msaada wa kimataifa USAID ili kusaidia wananchi wa miji mitatu nchini Zimbabwe.Katika kujifunza Kiswahili leo mtaalam wetu Onni Sigalla, Mhariri mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania, BAKITA akieleza maana ya neno “UKUMBIZAJI”.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
Jukwaa la ngazi ya juu la kisiasa kuhusu malengo ya maendeleo endelevu HLPF linaendelea hapa kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa ambapo wawakilishi wa nchi na serikali, wanasayansi, wanazuoni, mashirika ya umoja wa Mataifa asasi mbalimbali na vijana wanashiriki kukuna vichwa kujadili nini cha kufanyua kuhakikisha malengo hayo muhimu ya maendeleo yanatimizwa ifikpo mwaka 2030 na nini kifanyike kuzisaidia nchi zinazosuasua. Miongoni mwa washiriki ni kijana Omesa Mukaya kutoka Kenya ambaye mwezi Mei mwaka huu amehitimu shahada ya kwanza ya masuala ya sayansi ya mazingira na será katika chuo kikuu cha Clark Jimboni Massachussets hapa Marekani, amemweleza Flora Nducha wa Idhaa hii kilichomleta katika jukwaa hili.
Jukwaa la ngazi ya juu la kisiasa kuhusu ,malengo ya maendeleo endelevu lijulikanalo kama HLPF limeanza leo kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa hapa New York Marekani chini ya mwamvuli wa baraza la kiuchumi na kijamii ECOSOC.Jukwaa hilo ambalo litakunja jamvi 20 Julai mwaka huu limebeba maudhui "Kuharakisha kujikwamua kutokana na janga la ugonjwa wa virusi vya corona au COVID-19 na utekelezaji kamili wa ajenda ya 2030 ya maendeleo endelevu katika ngazi zote".Mbali ya viongozi wa ngazi ya juu katikia jukwaa hilo kutakuwa na siku tatu za majadiliano katika ngazi ya mawaziri.Kwa mujibu wa ECOSOC jukwaa hilo “litajumuisha mapitio ya mada ya malengo ya maendeleo endelevu namba 6 kuhusu maji safi na usafi wa mazingira, namba 7 kuhusu nishati nafuu na safi, namba 9 linalohusu viwanda, uvumbuzi na miundombinu, namba 11 linalohusu miji na jamii endelevu, na namba 17 linalohusu ubia kwa ajili ya malengo.”Pia jukwaa hili ltashughulikia changamoto maalum zinazokabili nchi zilizo katika hali maalum. Zaidi ya hapo litathimini vipimo vya kikanda na vya ndani ya nchi kuhusu kujikwamua kutoka kwaenye janga la COVID-19 na hali kuhusu malengo ya maendeleo endelevu SDGs. Na kisha litaunga mkono mapitio ya muda wa kati wa malengo ya SDGs na maandalizi ya mkutano wa mwa ka huu 2023 wa SDG mutaotarajiwa kufanyika Septemba.Leo katika siku ya kwanza ya jukwaa hilo mada kuu zitakazopewa kipaumbele ni “kushinda majanga, kuleta mabadiliko kwa aajili ya SDGs, na kutomwacha mtu yeyote nyuma, Kufadhili hatua zetu za kukabiliana na majanga na kuwekeza katika SDGs.”Nchi 39 zikiwemo Tanzania, Rwanda na Zambia zitafanya mapitio ya kitaifa ya hiari (VNRs) ya utekelezaji wao wa ajenda ya 2030 ya malengo ya maendeleo endelevu katika katika jukwaa hilo la HLPF 2023.Miongoni mwa wazungumzaji wa leo katika jukwaa hilo ni wasaidizi wa Katibu Mkuu Li Junhua, Qu Dongyu ambaye ni mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo FAO, Guy Ryder ambaye ni msaidizi wa Katibu Mkuu kuhusu masuala ya sera, Mami Mizutori msaidizi wa Katibu Mkuu na mkuu wa ofisi ya Umoja wa Msataifa ya upunguzaji wa hatari ya majanga UNDDR, na Filippo Grandi ambaye ni Kamisha mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR.
Hii leo jaridani tunaangazia Jukwaa la ngazi ya juu la kisiasa kuhusu malengo ya maendeleo endelevu na walinda amani nchini DRC. Makala tuankupeleka nchini Kenya na mashinani nchini Chad, kulikoni? Jukwaa la ngazi ya juu la kisiasa kuhusu malengo ya maendeleo endelevu lijulikanalo kama HLPF limeanza leo kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa hapa New York Marekani chini ya mwamvuli wa baraza la kiuchumi na kijamii ECOSOC.Ili kudhibiti unyanyasaji wa kingono ambao wakati mwingine unafanywa na baadhi ya walinda amani wa Umoja wa Mataifa, huko jimboni Ituri katika mji wa Bunia nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo – MONUSCO wanatumia ubunifu wa sanaa za maigizo ya jukwaani kuelimisha umma. Katika Makala Mkurugenzi Mkaazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Umoja wa Mataifa la afya ya uzazi na idadi ya watu UNFPA nchini Kenya Anders Tomsen, ameeleza shirika hilo linatekeleza ipasavyo tamko la Umoja wa Mataifa la haki za binadamu ambalo mwaka huu linafikisha miaka 75 hususan ibara ya Tano ambayo inasema Haki ya mtu ya kwamba asitumbukizwe kwenye vitendo vya mateso, ukatili, au adhabu dhalili.Mashinani tutaelekea Chad ambapo Maelfu ya wananchi wa Chad wanarejea nyumbani wakikimbia mzozo unaoendelea nchini SudanMwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
Hii leo jaridani tanaangazia Jukwaa la Umoja wa Mataifa la misitu linaloendelea hapa makao makuu, vita dhidi ya ukimwi Moldova. Makala tunakupeleka nchini Uganda na Mashinani nchini Rwanda, kulikoni?Jukwaa la 18 la Umoja wa Mataifa la misitu limeanza leo kwenye makao Makuu ya Umoja huo mjini New York Marekani likiwaleta pamoja wadau mbalimbali wakiwemo nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa, mfumo wa Umoja wa Mataifa, mashirika ya kimataifa na kikanda na wadau wa misitu ili kujadili thamani ya rasilimali hiyo muhimu kwa binadamu na mazingira.Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na vita dhidi ya ukimwi UNAIDS limesema ili kuhakikisha ukimwi unatokomezwa ifikapo mwaka 2030 basi kila mtu anapaswa kujumuishwa katika vita hiyo ikiwemo wafungwa na wanaotumia mihadarati, kwani mifumo mingi ya magereza inajitahidi kukabiliana na msongamano, rasilimali duni, ufikiaji mdogo wa huduma za afya na huduma zingine za msingi, vurugu na matumizi ya dawa za kulevya.Makala inatupeleka Uganda kumulika juhudi zinazofanywa na shirika la umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF kupambana na malaria.Mashinani tutaeleke nchini Rwanda kumsikia mkimbizi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC ambaye sasa ana matumaini baada ya kupokea msaada wa kibinadamu.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, Karibu!
Jukwaa la 18 la Umoja wa Mataifa la misitu limeanza leo kwenye makao Makuu ya Umoja huo mjini New York Marekani likiwaleta pamoja wadau mbalimbali wakiwemo nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa, mfumo wa Umoja wa Mataifa, mashirika ya kimataifa na kikanda na wadau wa misitu ili kujadili thamani ya rasilimali hiyo muhimu kwa binadamu na mazingiraKwa mujibu wa shirika la chakula na kilimo la Umoja wa Mataifa FAO misitu ni chanzo kikubwa cha nishati, chakula na malisho, na hutoa riziki kwa mamilioni ya watu, ikiwa ni pamoja na wengi ambao ni maskini zaidi duniani.Watu bilioni 2.4 duniani bado wanatumia nishati inayotokana na kuni kupikia. Lakini misitu pia husaidia kupunguza mabadiliko ya tabianchi na kuboresha rutuba ya udongo, hewa na maji.Shirika hilo linasema ikisimamiwa kwa uendelevu, misitu pia ni chanzo cha malighafi inayoweza kurejelewa, na hivyo kutoa mchango muhimu katika mzunguko wa ujenzi wa uchumi.Jukwaa hili lililoandaliwa na idara ya masuala ya kiuchumi na kijamii ya Umoja wa Mataidfa DESA linataka kila mtu duniani afahamu mambo matano muhimu kuhusu misitu ambayo ni mosi misitu inachukua asilimia 31 ya eneo la dunia,ina asilimia 80 ya bayoanuai ya dunia na inahifadhi hewa ukaa kiasi kikubwa zaidi ya kilichopo hewani.Pili, misitu inasaidia ustawi na maisha ya viumbe duniani, kwani watu zaidi ya bilioni 1.6 wanategemea mistu ili kuishi, kuendesha Maisha yao, ajira na kipato na Afrika takriban watu bilioni 2 na kaya theluthi mbili bado wanategemea misitu kwa kuni kama nishati ya kupikiaTatu misitu yenye afya inasaidia afya ya watu kwani misitu na miti inatoa hewa safi na maji na maji ni Uhai bila kujali mtu anakoishi.Nne misitu inaendelea kuwa hatarini kila mwaka dunia inapoteza ekati milioni 10 za misitu sababu ya uktaji haramu wa magogo, moto wa nyika, uchafuzi wa mazingira, magonjwa, wadudu na athari za mabadiliko ya tabianchi.Na tano kurejesha misitu ni ufunguo wa kuwa na mustakbali endelevu na kurejesha ardhi iliyomomonyoka kutasaidia kufikia malengo ya maendeleo endelevu hasa ya kuongeza eneo la mistu duniani kwa asilimia 3 ifikapo mwaka 2030.Kongamano hilo la siku 5 litakunja jamvi Ijumaa Mei 12
Jaridani leo ripoti ya utalii wa milima na jamii ya watu wa asili wa Inuit. Makala tunakuletea tunasalia hapa Makao Makuu na mashinani tunakupeleka Kisiwa cha Jamhuri ya Kiribati, kulikoni?Ripoti mpya iliyotolewa leo na mashirika ya Umoja wa Mataifa na wadau imeeleza bayana jinsi utalii kwenye maeneo ya milimani unaweza kuwa na manufaa sio tu kwa baiyonuwai bali pia kwa jamii zinazoishi kwenye maeneo hayo.Jamii ya Inuit ya watu wa asili wa Eskimo ni miongoni mwa jamii za walio wachache sana kutoka jimbo la Inuvik nchini Canada.Katika Makala Flora Nducha anazungumza na Kijana Mtanzania Gibson Kawago aliyeko hapa katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa akihudhuria Jukwaa la Vijana la Baraza la Umoja wa Mataifa la Kiuchumi na Kijamii (ECOSOC) la mwaka 2023.Na mashinani mashinani na tutaelekea katika Kisiwa cha Jamhuri ya Kiribati kilichoko Oceania katika Bahari ya Pasifiki ya Kati kusikia ujumbe kuhusu umuhimu wa chanjo.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
Tayari tangu jana Aprili 25, Jukwaa la Vijana la Baraza la Umoja wa Mataifa la Kiuchumi na Kijamii (ECOSOC) la mwaka 2023 limeng'oa nanga ambapo maelfu ya viongozi vijana kutoka duniani kote wanakusanyika katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York kujadili pamoja na mambo mengine, masuala yanayolenga kuharakisha kujikwamua kutoka janga la COVID-19 na utekelezaji kamili wa Ajenda ya 2030 ya Malengo ya Maendeleo Endelevu. Jukwaa la Vijana ndilo jukwaa kuu la vijana kuchangia mijadala ya sera katika Umoja wa Mataifa, ambapo wanaweza kutoa maoni yao, wasiwasi wao, na kuzingatia suluhu zao za kibunifu ili kukabiliana na changamoto zinazokabili ulimwengu.Mmoja wa vijana wanaohudhuria Jukwaa hili ni Gibson Kawago anayechakata betri chakavu za kompyuta na kuzirejesha katika matumizi mengine ya uzalishaji nishati. Flora Nducha wa Idhaa hii ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa amezungumza na kijana huyu. .
Jukwaa la Umoja wa Mataifa la ufadhili kwa ajili ya maendeleo 2023 FfD linaendelea kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa katika jaribio la kubadilisha mfumo wa fedha wa kimataifa na kurejesha ajenda ya maendeleo endelevu ya 2030 katika mstari unaotakiwa ikiwa imesalia chini ya miaka saba kufikia ukomo.Nchi, hususan zinazoendelea zinahaha kuhakikisha zinatimiza malengo yake kwa kila hali na miongoni mwao ni Kenya ambapo Susan Auma Mang'eni Katibu Mkuu wa Idara ya Ukuzaji wa Biashara Ndogondogo iliyo ndani ya Wizara Mpya ya Ushirika na Ukuzaji wa Biashara Ndogondogo au Ujasiriamali nchini humo anahudhuria kongamano hilo na amemweleza Flora Nducha wa Idhaa hii ya Kiswahili amekuja na ujumbe maalum kutoka Kenya.“Kwanza nimekuja hapa ili kuwasilisha ujumbe wetu wa Kenya hasa tunavyoona ufadhili wa maendeleo, kwa sababu lile janga la COVID-19 limedhihirisha bayana kwamba hakuna sehemu yoyote hapa duniani ambayo haina faida ya mambo ya uchumi, hakuna binadamu yeyote ambaye hana uzuri wake, hana thamani ya kiuchumi. Na limeonyesha ya kwamba wakati ule ambao tulikuwa katika zile hekaheka tukijaribu kujiuliza ni jinsi gani tutakabvyoliangamiza hili janga la COVID tulijiuliza maswali lakini hatukuwa na majibu , sasa ilibidi ya kwamba kila sehemu duniani kila nchi ianze kujifikiria kuona ya kwamba ni lipi sisi tunaweza fanya kuangamiza COVID-19. Na tunaona ya kwamba kuna nchi nyingi sana katikia hii dunia ambazo ziliweza kushinda haya madhara ya COVID -19 na sasa hivi imeonesha ya kwamba kama dunia sasa lazima tuanze kujiuliza ni jinsi gani sasa tutakavyoweza kukuza uchumi wetu, ili tuweze kuboresha Maisha ya wananchi wetu ili hapo baadaye litakapotokea tena janga kama hili tusife sana kama jinsi tulivyopoteza wananchi wetu.”Akaenda mbali zaidi na kusema rasilimali watu ipo wanachohitaji sasa na wanachokiomba kwenye mkutano huu ni ufadhili ili kufikia malengo ya maendeleo na ukuzaji uchumi wao.“Tunaweza kusema kwamba majibu mengi yako katika urithi wetu kama nchi na hasa sisi hapo Kenya tunatambua ya kwamba urithi wetu uko katika wananchi wetu, kwa watu wetu ambao wana bidii, wana ndoto nzuri na wameonesha kwamba wao wanaweza kufanya lolote ili kuendelea kimaisha. Na tumeona kwamba ukienda popote pale utaona rasilimali ipo, na hii rasilimali utaitambua kupitia utamaduni wetu, jinsi ambayo tunaishi na jinsi ambavyo tunashirikiana na wengine kwa vyakula vyetu, kwa kilimo chetu , kwa bidii yetu, ndio inaonesha kuwa hiyi ndio rasilimali yetu.”
Hii leo jaridani tunaangazia ripoti ya UNFPA na ujasiriamali. Makala tunaelekea nchini Sudan Kusini na mashinaninchini Kenya, kulikoni?Hii leo shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ya Uzazi na Idadi ya Watu duniani UNFPA limetoa ripoti mpya ambayo imeshauri kuwa badala ya kuuliza jinsi watu wanavyozaliana, viongozi duniani wanapaswa kuuliza kama watu hasa wanawake, wanaweza kujiamulia wao na kwa uhuru kuhusu uzazi, swali ambalo jibu lake, mara nyingi sana, ni hapana.Jukwaa la Umoja wa Mataifa la ufadhili kwa ajili ya maendeleo 2023 FfD linaendelea kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa katika jaribio la kubadilisha mfumo wa fecha wa kimataifa na kurejesha ajenda ya maendeleo endelevu ya 2030 katika msitari unaotakiwa ikiwa imesalia miaka chini ya sabakifikia ukomo.tuelekee nchini Sudan Kusini ambako kumefanyika tamasha la utamaduni kwa amani lililondaliwa na Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo UNMISS kwakushirikiana na serikali ya jimbo la Kaskazini la Bahr El Ghazal.Na katika mashini tutaelekea tutaelekea nchini Kenya kupat aujumbe kuhusu lugha ya Kiswahili.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, Karibu!
Hii leo jaridani tunasalia hapa makao makuu kukuletea yaliyojiri kwenye Jukwaa la kudumu la watu wa asili, na pia kukupeleka nchini DRC kumulika faida ya mradi unaofadhiliwa na Benki ya Dunia wa kupanda miti aina ya migunga. Makala tunaangazia SDG 17 na Mashinani tunakupeleka nchini Tanzania, kulikoni?Hii leo katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York Marekani Jukwaa la kudumu la watu wa asili limeanza rasmi ambapo katika ufunguzi wa jukwaa hilo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema pamoja na majukumu muhimu ya jamii za asili hususan katika kulinda mazingira na mbinu nyingine mbadala za maisha, watu hawa wanazidi kuwa masikini na kuzitaka nchi zote duniani zihakikishe zinawasaidia kuondokana na umasikini.Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, mradi unaofadhiliwa na Benki ya Dunia wa kupanda miti aina ya migunga imeondoa tishio la ukataji miti holela kwenye msitu wa bonde la mto Congo, ambao ni wa pili kwa ukubwa duniani katika kufyonza hewa ya ukaa na sasa wananchi wananufaika sio tu kwa kupata mkaa bali pia hata watu wa jamii ya asili wanaweza kupata kitoweo porini.Katika makala Mwanamuziki Chioma Ogbonna (tamka Obona) “Cill” au Cillsoul wa Nigeria ambaye ni Mchechemuzi wa Kampeni ya Umoja wa Mataifa ya kusongesha Malengo ya Maendeleo Endelevu, SDGs na anaeleza anavyoutumia kipaji chake kusongesha malengo hayo 17.Na katika mashini tutaelekea nchini Tanzania kusikiliza jinsi ambavyo hakikisho la maji safi na salama limeboresha elimu shuleni.Mwenyeji wako ni Flora Nducha, Karibu!
Hii leo jaridani tunakupeleka Davos Uswisi kusikiliza hotuba ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa na pia kuangazia tuzo ya mwaka 2023 iitwayo Crystal Award. Makala na mashinani tunasalía huko huko, kulikoni?Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema dunia haiwezi kutatua changamoto kubwa inazokabiliwa nazo hivi sasa kuanzia mabadiliko ya tabianchi, vita ya Ukraine, mdororo wa uchumi na athari zinazoendelea za janga la COVID-19 katikia hali ya sasa ya mgawanyiko na kutokuwa na mshikamano hivyo wakati wa kufumbia macho changamoto hizi umepita na wanaochangia wawajibishwe.Mabalozi wawili wa shirika la Umoja wa Mataifa la maendeleo ya kilimo duniani, IFAD, Sabrina Dhowre Elba na mumewe Idris Elba wamepatiwa tuzo ya mwaka 2023 iitwayo Crystal Award kutokana na uongozi wao wa kupaza sauti kwa niaba ya mamilioni ya wakulima wadogo maskini duniani kote ambao hufanya kazi kila siku kuzalisha theluthi moja ya chakula chote duniani.Makala tunakwenda huko Fez, kuangazia mkutano wa tisa wa Jukwaa la Umoja wa Mataifa la Muungano wa Ustaarabu, UNAOC.Na katika mashinani tunasalia huko nchini Uswisi ambapo tutamsikia Waziri Mkuu wa Finland. Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
Mabalozi wawili wa shirika la Umoja wa Mataifa la maendeleo ya kilimo duniani, IFAD, Sabrina Dhowre Elba na mumewe Idris Elba wamepatiwa tuzo ya mwaka 2023 iitwayo Crystal Award kutokana na uongozi wao wa kupaza sauti kwa niaba ya mamilioni ya wakulima wadogo maskini duniani kote ambao hufanya kazi kila siku kuzalisha theluthi moja ya chakula chote duniani.Makofi katika ukumbi wakati Idris na mkewe Sabrina wakipokea tuzo hiyo kwenye hafla iliyofanyika mjini Davos, nchini Uswisi kunakofanyika ya Jukwaa la uchumi duniani, WEF, Tuzo hii ya WEF hupatiwa wasanii na viongozi wa kitamaduni ambao mchango wao muhimu kwa jamii umeleta mabadiliko chanya katika kuboresha hali ya dunia. Tangu kuteuliwa kuwa mabalozi wema, Sabrina na Idris wamekuwa wachechemuzi wakubwa wa uwekezaji kwenye maendeleo ya kilimo na vijiji hasa Afrika ambako majanga na mizozo vimeacha wakulima taabani. Pamoja na mikutano na viongozi na taasisi mbalimbali, walitembelea miradi inayofadhiliwa na IFAD, mathalani Sierra Leone, Zambia na Kenya na kushuhudia changamoto za wakulima na kile wanachohitaji. Idris anasema, “Masikini wa dunia hii hawatafuti misaada bali wanataka uwekezaji. Uwekezaji kwa watu, mazingira, ugunduzi na ubia. Tukiweza kupata fedha zaidi, masoko, rasilimali, teknolojia, ufahamu na watu, tunaweza kuwa na mustakabali tofauti.” Sabrina akatoa tathmini ya alichoona na kinachopaswa kufaniyka akisema “Mara nyingi kwa wakulima wadogo, janga moja, au msimu mmoja wa mafuriko au ukame au kutokuvuna msimu mmoja kunawalazimu kuuza rasilimali zao ili waweze kujilisha. Jamii za vijijini zimesheheni vijana wenye vipaji, masoko na uwezo. Tumejionea wenyewe. Si kwamba wanaweza tu kujilisha wenyewe, bali wanaweza na wasaidiwe ili walishe dunia.”
Umoja wa Mataifa unasema robo tatu ya migogoro mikuu ya ulimwengu ina uhusiano na masuala ya kitamaduni na kwa hivyo kuziba pengo kati ya tamaduni ni jambo la haraka na la lazima kwa ajili ya amani, utulivu na maendeleo. Makaburi ya Kiyahudi huko Fez, Morocco ni ushuhuda wa utamaduni tofauti kuishi pamoja kwa amani.Wakiwa katika safari ya kikazi huko Fez, kuangazia Mkutano wa tisa wa Jukwaa la Umoja wa Mataifa la Muungano wa Ustaarabu, UNAOC, May Yacoub na Alban Mendes De Leon kutoka Timu ya Mawasiliano ya Umoja wa Mataifa walikutana na Johanna Devico Ohana, mzaliwa wa Fez, ambaye anatunza makaburi haya yenye umri wa miaka 200, akiheshimu jina la marehemu babake ambaye mwenyewe alikuwa msimamizi wa utunzaji wa makabuli haya hadi alipoaga dunia miezi michache iliyopita. Anold Kayanda anasimulia makala hii kwa lugha ya Kiswahili.