Jukwaa la Michezo

Follow Jukwaa la Michezo
Share on
Copy link to clipboard

Makala haya yanaangazia maendeleo ya michezo mbalimbali Ulimwenguni na pia huwa haiwaweki kando wanamichezo waliobobea na vilevile kufanya uchanganuzi wa kina wa michezo wakati wa mashindano mbalimbali.

RFI Kiswahili


    • Feb 21, 2026 LATEST EPISODE
    • weekly NEW EPISODES
    • 23m AVG DURATION
    • 230 EPISODES


    Search for episodes from Jukwaa la Michezo with a specific topic:

    Latest episodes from Jukwaa la Michezo

    Gofu: Mkenya Njoroge Kibugu afuzu mchujo wa Magical Kenya Open

    Play Episode Listen Later Feb 21, 2026 23:56


    Mkenya Njoroge Kibugu alifuzu mchujo wa mashindano ya dunia ya gofu ya Magical Kenya Open wakati mnyarwanda Celestin Nsazuwera akiweka historia, uchambuzi wa droo ya michuano ya klabu bingwa Afrika, mashindano ya wanawake ya COSAFA, wakenya wang'ara katika michuano ya fencing ya Afrika, TFF yafungua zabuni ya haki za kamari katika debi la kariakor, Fifa kufadhili ujenzi wa viwanja vya soka huko Palestina na uchambuzi wa michuano ya mchujo ligi ya mabingwa ulaya.

    Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika 2027 zitafanyika Juni-Julai

    Play Episode Listen Later Feb 14, 2026 23:51


    Leo tumeangazia CAF kudhibitisha kuwa AFCON 2027 itaandaliwa Afrika Mashariki licha ya tetesi za kuahirishwa au kuhamishwa, uchambuzi wa raundi ya mwisho ya hatua ya makundi mechi za klabu bingwa, mechi za kufuzu kombe la dunia la wasichana U20, siku ya kwanza ya michuano ya raga ya wachezaji saba kila upande divisheni ya pili ya HSBC, mfumo mpya wa mashindano ya Tour du Rwanda, kiungo wa Ghana Thomas Partey akumbwa na shtaka jipya lakini pia michezo ya Olimpiki msimu wa baridi.

    Yanga yalenga ushindi muhimu kukaribia robo fainali michuano ya klabu bingwa

    Play Episode Listen Later Feb 7, 2026 23:53


    Leo tumeangazia mechi za klabu bingwa Afrika, Yanga itachuana na FAR Rabat nayo Azam ikicheza na Maniema, matukio kuelekea michuano ya gofu ya Magical Kenya Open, mechi za kufuzu kombe la dunia la kina dada chini ya miaka ishirini, rais wa soka DR Congo asimamisha shughuli zote katika uwanja wa Tata Raphael, Rais wa FIFA Infantino asema marufuku dhidi yz Urusi hayajasaidia chochote, mzozo kati ya Ronaldo na Al Nassr waendelea kwa mechi ya pili sasa.

    Uamuzi wa CAF kwenye fainali ya Afcon 2025: Udhibiti wa Haki au Uharibifu?

    Play Episode Listen Later Jan 31, 2026 23:48


    Leo tumeangazia kwa undani hukumu na uamuzi wa Caf kufuatia matukio yaliyoibuka kwenye fainali ya AFCON 2025, Simba inajandaa kwa mechi ya kufa kupona kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika, raundi ya kwanza ya kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika mechi za Futsal yakamilika, msimu wa sita wa Ligi ya Afrika ya basketboli kumalizia nchini Rwanda, Faith Kipyegon ajenga hospitali huko Kenya, TP Mazembe yapata kocha mpya, fainali ya Australian Open, Ligi ya Mabingwa Ulaya yaingia raundi ya mtoano.

    CAF: Michuano ya klabu bingwa Afrika imerejea raundi ya tatu ya makundi

    Play Episode Listen Later Jan 24, 2026 23:49


    Leo kwenye kipindi tumeangazia uchambuzi wa mashindano ya AFCON 2025, vilabu vya Afrika Mashariki vinatafuta tiketi ya mchujo mechi za klabu bingwa, Kinshasa kuandaa Kombe la Mataifa ya Afrika ya Voliboli mwaka huu, wachezaji kadhaa wa ligi ya NBA waonesha nia kuiwakilisha Nigeria kwenye Olimpiki ya 2028, mashindano ya Afrika ya handboli inayoendelea Kigali, Uganda yapata kocha mpya wa basketboli, mfumo mpya wa mashabiki kupata visa mapema kuelekea Kombe la Dunia wafunguliwa rasmi

    AFCON 2025: Senegal, Morocco zatinga fainali. Je, nusu fainali ziliendaje?

    Play Episode Listen Later Jan 17, 2026 23:53


    Leo tumeangazia pakubwa uchambuzi wa matukio na matokeo ya mechi za nusu fainali mechi za Kombe la Mataifa ya Afrika 2025 na mechi ya mshindi wa tatu leo usiku, hotuba ya rais wa CAF Patrice Motsepe kabla ya fainali, Droo ya mashindano ya WAFCON ya kina dada ya mwaka huu, Rwanda kuwa mwenyeji wa michuano ya Afrika ya Handboli, Rwanda na Burkina Faso zafuta kazi makocha wao.

    AFCON 2025: Mbio za kuwania kufuzu kwa nusu fainali zinazidi kupamba moto

    Play Episode Listen Later Jan 10, 2026 23:53


    Leo tutakufahamisha matukio yote kwenye raundi ya 16 bora, uchambuzi wa mechi haswa kuondolewa kwa DRC na Tanzania walivyolakiwa kishujaa nyumbani Dar es Salaam baada ya kutoka Morocco na uchambuzi wa mechi za robo fainali za jana na leo. Morocco na Senegal washajikatia tiketi ya nusu fainali. Algeria dhidi ya Nigeria na Misri dhidi ya Ivory Coast. 

    Uchambuzi wa Mada: Je, AFCON 2025 inatoa msisimko kama mashindano yaliyopita?

    Play Episode Listen Later Jan 4, 2026 24:34


    Leo tunajadili kwa undani kauli ya kocha wa Afrika Kusini, Hugo Broos kuwa michuano ya mwaka huu haina mvuto na msisimko kama Afcon zilizopita. Uchambuzi wa mechi za jana na leo kwenye hatua ya 16 bora - Tanzania vs Morocco, Afrika Kusini vs Cameroon, DRC vs Algeria. Hatua ya serikali ya Gabon kuvunjilia mbali timu ya Gabon huku marais wa Msumbiji na Benin wakitoa ahadi za pesa kwa timu zao. Morocco kuandaa michuano ya Kombe la Dunia la Vilabu 2029 nayo Ethiopia ikiwania kuandaa Afcon ya 2028.

    AFCON 2025: Mtazamo wa hatua ya mtoano, timu 16 zitawania tiketi ya fainali

    Play Episode Listen Later Jan 3, 2026 23:48


    Leo tumeangazia kwa undani matokeo na matukio ya hatua ya makundi iliyokamilika kwenye michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika inayoendelea Morocco, uchambuzi wa hatua ya 16 bora - nani atafuzu robo fainali?, tathmini ya hatua ya serikali ya Gabon kuvunja kabisa timu ya taifa ya Gabon, ahadi za pesa kutoka kwa marais kadhaa Afrika kwa timu zao kuelekea robo fainali, usajili wa Rayon Sport, kwa nini Maresca aliondoka Chelsea?, dereva wa Anthony Joshua afunguliwa mashtaka baada ya ajali Nigeria.

    AFCON 2025: Morocco dhidi ya Comoros kufungua mashindano leo usiku

    Play Episode Listen Later Dec 21, 2025 24:00


    Leo tunaangazia pakubwa kuanza kwa mashindano ya AFCON 2025; tunachambua mechi ya ufunguzi kati ya Morocco na Comoros, mjadala kuhusu mageuzi katika michuano hii, namna timu zilivyotua nchini Morocco kwa kuvalia mavazi ya kitamaduni, Morocco wapo kwenye shinikizo ya kunyakua ubingwa kwa kuwa mwenyeji lakini pia ubashiri wa mechi ya ufunguzi na atakayebeba taji la mwaka huu.

    AFCON 2025: Mashindano kufanyika kila baada ya miaka minne baada ya 2028

    Play Episode Listen Later Dec 20, 2025 23:56


    Usiku mmoja kabla ya kuanza kwa michuano ya Afcon 2025 tunakufahamisha mambo yote unayostahili kujua pamoja na mabadiliko ya michuano hii kuendelea mbele, michezo ya chipukizi ya Afrika yatamatika Angola, Rayon Sports na Simba zapata makocha wapya, mkenya David Munyua aweka historia katika mchezo wa darts duniani, Anthony Joshua amlaza Jake Paul kupitia knockout, droo ya nusu fainali ya kombe la Carabao.

    CAF: Wachezaji gani wameitwa kwa ajili ya michuano ya AFCON 2025?

    Play Episode Listen Later Dec 13, 2025 23:53


    Leo tunachambua vikosi vilivyotajwa na mataifa kuelekea Kombe La Mataifa ya Afrika nchini Morocco, Ligi ya Afrika ya basketboli ya kina dada imeingia hatua ya nusu fainali, michezo ya chipukizi ya Afrika inayoendelea Angola, mabadiliko katika mashindano ya Tour du Rwanda, mechi za kufuzu mashindano ya shule za upili ya CAF, Ben Sulayem achaguliwa kuendelea kuongoza shirikisho la kimataifa la mchezo wa magari, sakata la MoSalah klabuni Liverpool na ziara ya Messi huko India yazua rabsha.

    Droo ya Kombe la Dunia 2026: Fahamu makundi ya michuano hii ya mwakani

    Play Episode Listen Later Dec 6, 2025 23:55


    Tuliyukuandalia leo ni pamoja na timu za Afrika zimepangwa kwenye makundi gani katika Kombe la Dunia la mwaka ujao, nani ataibuka na taji la Formula 1 kesho, Kenya kuandaa mashindano ya dunia ya Taekwondo, michuano ya kufuzu mashindano ya shule za upili barani Afrika, kuanza kwa Ligi ya Afrika ya basketboli ya wanawake, wachezaji wa soka Afrika waanzisha kampeni dhidi ya polio, Onana na Aboubakar watemwa kikosini Cameroon huku nahodha wa Nigeria Troost Ekong akistaafu soka la kimataifa.

    Washikadau wa Fencing Afrika Mashariki waziomba serikali za Afrika kusaidia ukuaji wa mchezo

    Play Episode Listen Later Nov 29, 2025 23:59


    Tuliyokuandalia leo ni pamoja na kilio cha washikadau wa mchezo wa fencing Afrika Mashariki kwa serikali za Afrika kusaidia kukuza mchezo, mashindano ya Tong Il Moo Do yarejea tena nchini Kenya baada ya marufuku ya mwaka mmoja, uchambuzi wa mechi za klabu bingwa Afrika, Sudan Kusini yaanza vyema michuano ya kufuzu Kombe la Dunia la Basketboli 2027, mfaransa Sebastian Ogier akaribia kushinda taji la dunia la tisa, uchambuzi wa mechi za ligi ya mabingwa Ulaya.

    CAF: Achraf Hakimi ashinda tuzo ya mwanasoka bora wa Afrika mwaka 2025

    Play Episode Listen Later Nov 22, 2025 23:54


    Leo tumezingatia tuzo za CAF 2025, AS FAR yaibuka washindi wa kombe la Ligi ya Afrika ya kina dada, kuanza kwa michuano ya klabu bingwa Afrika kwa wanaume huku AS FAR ikinyakua taji la kina dada, matokeo ya mechi za kufuzu AFCON U17 ukanda wa Cecafa, Curacao yakuwa taifa dogo zaidi kuwahi kufuzu Kombe la Dunia huku Marekani ikizindua mfumo maalum wa kutoa visa kwa wanunuaji tiketi.

    KPA (Kenya), APR na REG za Rwanda zafuzu Ligi ya Mpira wa Kikapu Afrika kwa kina dada

    Play Episode Listen Later Nov 15, 2025 23:53


    Tuliyokuandalia leo ni pamoja na kuanza kwa michuano ya raga ya Afrika kwa kina dada wachezaji saba kila upande, michuano ya kufuzu Ligi ya Basketboli Afrika kwa kina dada, ligi ya klabu bingwa Afrika kwa kina dada, mechi za kufuzu Kombe la Dunia mwaka 2026 - Gattuso asema Afrika inafaa kupewa nafasi chache, uchaguzi wa Kamati kuu ya Olimpiki nchini DRC, bingwa wa dunia Beatrice Chebet apokea tuzo ya kitaaluma.

    Miguel Gamondi kuiongoza Taifa Stars kwenye michuano ya AFCON 2025 Morocco

    Play Episode Listen Later Nov 8, 2025 23:57


    Tuliyokuandalia ni pamoja na kocha Gamondi kuteuliwa kuwa kaimu kocha wa Tanzania, Kipchoge akutana na Obama, Tume Huru ya Uchaguzi ya Kamati ya Olimpiki ya Kongo yachapisha orodha ya mwisho ya wagombea, kukosekana kwa Beatrice Chebet na Faith Kipyegon kwenye tuzo za mwanariadha bora wa mwaka, makundi ya michuano ya afrika ya raga kwa kina dada na mechi za kufuzu Ligi ya Afrika ya Basketboli, droo ya michuano ya klabu bingwa Afrika, uchambuzi wa matokeo ya ligi ya mabingwa Ulaya

    Kenya na Tanzania zafuzu michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (WAFCON2026)

    Play Episode Listen Later Nov 1, 2025 23:44


    Tuliyokuandalia leo ni pamoja na Sudan kusherehekea kambi ya kwanza kabisa ya ndondi ya wanawake nchini humo, Nairobi itakuwa mwenyeji wa michuano ya kufuzu ligi ya afrika ya basketboli mwezi huu, Kinshasa itaandaa michuano ya kitaifa ya ndondi ya chipukizi, Tanzania na Kenya zimefuzu michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa kina dada mwaka 2026, Ethiopia itaandaa michuano ya kufuzu AFCON U17, ratiba ya mechi za mchujo kufuzu Kombe la Dunia, Paris Masters, Pogba apata jeraha jipya.

    WAFCON: Michuano ya kufuzu kombe la mataifa ya Afrika ipo raundi ya mwisho

    Play Episode Listen Later Oct 25, 2025 23:51


    Tuliyokuandalia leo ni pamoja na waamuzi watatu nchini Rwanda kusimamishwa kwa muda, Kongamano la nne la Kibiashara la Soka lakamilika nchini Kenya, awamu ya mwisho ya kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika kwa kina dada, tuzo za CAF mwaka huu, mechi za kufuzu hatua ya makundi michuano ya Klabu Bingwa Afrika, mkenya Ruth Chepngetich apigwa marufuku ya miaka mitatu, bingwa wa dunia wa MotoGP Marquez kukosa msimu mzima uliosalia na nusu fainali ya tenisi Vienna Open

    FIFA: Ni mataifa gani ya Afrika ambayo tayari yamefuzu Kombe La Dunia mwaka 2026

    Play Episode Listen Later Oct 11, 2025 24:03


    Tuliyokuandalia leo ni pamoja na tathmini ya timu za Afrika ambazo zimefuzu Kombe la Dunia 2026 na ni nani ambao wana nafasi ya kufuzu kuelekea raundi ya mwisho ya mechi za kufuzu, FIFA yateua wajumbe kutoka CECAFA, Herita Ilunga ndiye mkurugenzi mpya wa FECOFA nchini DRC, kocha wa zamani wa Yanga Nassredine Nabi waachana na Kaizer Chiefs, nyota tajika wa tenisi duniani wabwagwa kwenye mashindano ya Wuhan Open, Rovapera kustaafu mchezo wa kuendesha magari

    Mashindano ya boti za umeme zinafanyika Afrika kwa mara ya kwanza Lagos, Nigeria

    Play Episode Listen Later Oct 4, 2025 23:57


    Tuliyokuandalia leo ni pamoja na Rwanda kuwa taifa la kwanza Afrika kudhamini vilabu vya basketboli Ulaya, nini kinachoendelea klabuni Simba washikadau wanaendelea kuondoka, TP Mazembe yajiondoa katika Chama cha Vilabu vya Soka vya Kongo, Afrika inaandaa kwa mara ya kwanza mashindano ya boti za umeme nchini Nigeria, mwanawe Zidane aitwa kikosini Algeria, FIFA yazindua mpira utakaotumika mwaka ujao kwenye Kombe la Dunia, Hamilton akabiliwa na uchunguzi kuelekea mkondo wa Singapore.

    Waafrika wa kutazama kwenye Mashindano ya Riadha ya Dunia huko Tokyo, Japan

    Play Episode Listen Later Sep 13, 2025 23:51


    Tuliyokuandalia ni pamoja na kuanza kwa mashindano ya riadha ya dunia, michuano ya Cecafa inayoendelea kwa kina dada na wanaume, Simba Day na Yanga Day huko Tanzania, michuano ya basketboli ya Afrika ya wavulana wasiozidi miaka 16, kinachotarajiwa baada ya rabsha katika mechi ya DRC na Senegal

    Morocco ni timu ya kwanza ya Afrika kufuzu Kombe la Dunia la mwaka 2026

    Play Episode Listen Later Sep 6, 2025 24:16


    Tuliyokuandalia leo ni pamoja na uchambuzi wa matokeo ya mechi za kufuzu kombe la dunia la mwaka ujao, mechi za kufuzu mashindano ya vilabu bingwa kwa kina dada ukanda wa CECAFA, mashindano ya CECAFA Kagame Cup, wanariadha watatu wa Uganda kukosa Riadha za Dunia mwezi huu nchini Japan, rais wa Marekani Donald Trump kuhudhuria fainali ya wanaume ya US Open, Luis Suarez apewa adhabu ya mechi sita baada ya kumtemea mate mwanachama wa benchi la ufundi ya klabu ya Seattle Sounders.

    CHAN 2024: Nani atashinda kati ya Morocco na Madagascar ?

    Play Episode Listen Later Aug 30, 2025 20:58


    Morocco na Madagascar zinachuana katika fainali ya mchezo wa CHAN 2024. Hii ni michuano inayowashirikisha wachezaji wanaoshiriki ligi za ndani. Fainali hii inachezwa kwenye uwanja wa Kimataifa wa Kasarani, Agosti 30 2025. Wanamichezo wetu Jason Sagini na Paul Nzioki, wanachambua kutoka uwanjani.

    CHAN 2024: Wenyeji Kenya, Uganda na Tanzania watupwa nje ya mashindano

    Play Episode Listen Later Aug 23, 2025 23:52


    Leo tumekuandalia mengi ikiwemo kubanduliwa kwa Kenya na Tanzania kwenye michuano ya CHAN katika hatua ya robo fainali, michuano ya basketboli ya Afrika ya wanaume imeingia hatua ya nusu fainali, shirikisho la soka nchini Sudan Kusini limetangaza tarehe mpya ya kuanza kwa msimu mpya wa ligi ya wanawake, Wan Bissaka ajumuishwa katika kikosi cha soka cha DRC, Mohammed Salah ashinda tuzo la mchezaji bora wa wachezaji kwa mara nyingine.

    CHAN 2024: Kenya, DRC, Morocco zafukuzia ushindi mechi za mwisho za makundi

    Play Episode Listen Later Aug 16, 2025 21:13


    Leo tumekuandalia uchambuzi wa timu ambazo zimefuzu, gani zimeondolewa na nani wanaweza kufuzu hatua ya mtoano kwenye mashindano ya Chan, michuano ya baskeboli ya wanaume ya Afrika, viongozi wa mashabiki Sudan Kusini waandaa mechi ya kirafiki kuchangisha fedha za kusaidia watu wasiojiweza, rais wa AS Kigali aahidi kuongeza tuzo za ligi iwapo atachaguliwa kuwa rais wa shirikisho, Alcaraz afuzu robo fainali michuano ya Cincinnati Open.

    CHAN 2024: Kenya yafukuzia ushindi dhidi ya Morocco, Tanzania ikihitaji sare tu

    Play Episode Listen Later Aug 9, 2025 23:52


    Leo tumekuandalia uchambuzi, matokeo na matukio ya raundi ya pili ya hatua ya makundi ya michuano ya CHAN pamoja na mechi za leo usiku na kesho mchana, droo ya michuano ya awali ya kufuzu hatua ya makundi mechi za klabu bingwa barani Afrika, uhamisho wa wachezaji Afrika Mashariki huku Kinshasa ikichaguliwa kuandaa mkutano mkuu wa CAF mwezi Oktoba, Thomas Partey kujiunga na Villareal licha ya kesi za ubakaji, 

    CHAN 2024: Tanzania na Kenya zashinda mechi zao za kwanza za makundi

    Play Episode Listen Later Aug 3, 2025 23:54


    Tunaendelea kuangazia michuano ya CHAN ambapo wenyeji Kenya na Tanzania wasajili ushindi mechi zao za kwanza, Sudan Kusini yabanduliwa kwenye hatua ya nusu fainali michuano ya basketboli ya kina dada ya Afrobasket, bondia Patrick Mukala wa DRC ndiye bingwa mpya wa Afrika uzani wa light heavyweight, Hojlund wa Man Utd awekewa dau la pauni milioni 30 kuuzwa, matokeo ya hatua ya tisa ya Tour du France na Formula One mkondo wa Hungarian Grand Prix

    CHAN 2024: Tanzania na Burkina Faso kufungua mashindano ya Chan leo usiku

    Play Episode Listen Later Aug 2, 2025 23:56


    Tumekuandalia mengi leo ikiwemo kuanza kwa mashindano ya CHAN - uchambuzi, matukio na matokeo, michuano ya basketboli ya wanawake yaingia nusu fainali, Gor Mahia yapata benchi mpya la ufundi huku shirikisho la soka nchini Kenya likipata mdhamini mpya wa ligi, tetesi za uhamisho ulaya, matokeo ya hatua ya tatu ya Canada Open, Barcelona yaingia kwenye udhamini wa jewi na taifa la DRC

    CAF: Nigeria na Morocco kuchuana leo kwenye fainali ya WAFCON

    Play Episode Listen Later Jul 26, 2025 23:56


    Leo tumeangazia fainali ya Kombe la Mataifa ya Wanawake kati ya Nigeria na Morocco, maandalizi ya CHAN yapamba moto, kamati ya Olimpiki nchini Kenya yapata viongozi wapya, kurejea kwa soka nchini Sudan licha ya vita, chama cha wachezaji Fifpro kikidai wachezaji wanahofia kulalamikia mrundiko wa mechi kwenye kalenda ya soka, uhamisho wa wachezaji ulaya, Verstappen ashinda mashindano ya mazoezi ya Belgian GP, Tour de France yafikia hatua ya 20 na fainali ya Kombe la EURO kwa wanawake.

    CAF: Nigeria na Morocco zimefuzu nusu fainali ya michuano ya WAFCON 2025

    Play Episode Listen Later Jul 19, 2025 23:57


    Leo tumeangazia hatua ya mtoano ya michuano ya Wafcon, maandalizi ya timu za Afrika Mashariki kuelekea CHAN 2024, mshikilizi wa rekodi ya dunia Chepng'etich asimamishwa kwa muda, Yanga yaendelea kusajili pakubwa, Vipers SC yapata kocha mpya kutoka Ubelgiji, raia wa Cameroon Bryan Mbeumo ajiunga na Man Utd, Ons Jabeur aamua kuchukua pumziko fupi kwenye tenisi, hatua ya 14 ya Tour de France, michuano ya EURO ya wanawake.

    CAF: Kenya yazidisha maandalizi yake kuelekea kuandaa CHAN 2024

    Play Episode Listen Later Jul 12, 2025 23:54


    Leo tumeangazia raundi ya pili ya makundi mechi za WAFCON, maandalizi ya Kenya kuandaa CHAN, riadha za Monaco Diamond League, michuano ya raga bara Afrika, fainali ya Congo Cup, msimamo wa jedwali wa hivi punde wa FIFA, Rwanda yajiandaa michuano ya bara Afrika basketboli kwa wanawake, uhamisho wa wachezaji kutoka Afrika huko Ulaya, fainali ya Kombe la Dunia la Vilabu, fainali za Wimbledon, hatua ya nane ya Tour du France na mechi za mwisho za makundi Kombe la EURO kwa kina dada.

    CAF: Kipute cha Kombe la Mataifa ya Wanawake 2025 yaanza nchini Morocco

    Play Episode Listen Later Jul 5, 2025 24:09


    Leo tumeangazia kuanza kwa mashindano ya kombe la mataifa ya kina dada nchini Morocco, Kenya mashindano ya soka ya ufukweni ukanda wa Cecafa, uchaguzi katika shirikisho wa soka Tanzania na Uganda na uhamisho wa makocha Gamondi na Ibenge katika ligi ya Tanzania, FIFA imeteua viongozi wapya katika kamati ya mpito ya soka nchini DRC, nyota wa Liverpool Diogo Jota na kakake wazikwa, Thomas Partey ashtakiwa na kesi za ubakaji na matokeo ya Kombe la Dunia la Vilabu, Euro ya wanawake na Wimbledon.

    Yanga yashinda ubingwa wa 26 huku CAF ikitoa ratiba rasmi ya michuano ya Chan

    Play Episode Listen Later Jun 28, 2025 23:59


    Tuliyokuandalia leo ni pamoja na Yanga kushinda ubingwa wao wa 26, klabu ya Les Aigle du Congo yashinda ubingwa wa ligi ya DRC, historia zilizowekwa na Faith Kipyegon na Khaman Maluach wiki hii, Aish Manula arejea kikosini Taifa Stars kuelekea Chan, nini sababu ya vilabu vyote vya Afrika kubanduliwa kwenye kombe la dunia la vilabu? Ligi kuu ya Uingereza kuleta mabadiliko mapya mapumzikoni msimu ujao, Pogba,Giroud warejea katika ligi ya Ufaransa huku Lyon ikishushwa kutokana na matatizo ya fedha

    Fainali ya CHAN 2024 kuchezwa Kenya, mechi ya ufunguzi kupigwa Tanzania

    Play Episode Listen Later Jun 21, 2025 24:00


    Tuliyokuandalia leo ni pamoja na CAF kutangaza viwanja vitakavyoandaa michuano ya CHAN, kombe la CECAFA kwa kina dada, DRC yakuwa mshiriki rasmi wa AC Milan, matokeo ya Paris Diamond League na Mauritius 7s. Matokeo ya vilabu vya Afrika kwenye raundi ya kwanza ya Kombe la Dunia la Vilabu huku mshindi wa French Open Carlos Alcaraz akifuzu nusu fainali yake ya saba mwaka huu kwenye tenisi.

    Kipkeino Classic: Lachlan Kennedy aibuka mshindi wa mbio za mita 100

    Play Episode Listen Later May 31, 2025 23:50


    Tuliyokuangalia leo ni pamoja na matokeo ya riadha za Kipkeino Classic, mkutano mkuu wa FKF, tuzo za soka Rwanda, APR yasajili mchezaji Omot kuelekea fainali za BAL, DRC yajiandaa mechi za kirafiki kuelekea WAFCON, uchambuzi wa fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya

    CAF: Simba kuchuana na RS Berkane leo kwenye fainali ya Kombe la Shirikisho

    Play Episode Listen Later May 17, 2025 23:58


    Leo tumekuandalia mengi ikiwemo fainali ya kombe la shirikisho la CAF kati ya Simba na RS Berkane, fainali za Afcon U20, Congo Brazaville yarejeshwa katika soka ya kimataifa, droo kamili ya michuano ya Chan 2024, mkondo wa Nile katika ligi ya basketboli ya Afrika, tuzo za wanasoka bora ligi kuu ya Uingereza.

    BAL: APR ya Rwanda inalenga fainali za Afrika watakaposhiriki mara ya pili

    Play Episode Listen Later May 10, 2025 23:53


    Leo tumeangazia michuano ya Afcon U20 ambayo imeingia hatua ya mtoano, ripoti maalum kuhusu APR inapojiandaa kushiriki BAL kwa mara ya pili, debi za soka nchini Kenya na Tanzania zayumbayumba, promota wa ndondi kutoka Uganda ahamia nchini Kenya, uchambuzi wa fainali za ligi za klabu bingwa Ulaya, mechi ya kwanza ya Evra kwenye ndondi ya kuchanganywa yaahirishwa huko Paris huku Mohammed Salah akishinda tuzo lake la tatu la waandishi wa habari za soka

    AFCON U20: Michuano ya vijana ya soka yang'oa nanga nchini Misri

    Play Episode Listen Later May 3, 2025 23:53


    Hii leo tumeangazia michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika ya vijana chini ya miaka 20 kuanza nchini Misri, mkondo wa mtoano katika msururu wa raga duniani, diamond league mkondo wa pili huko Uchina na Ligi ya Basketboli mkondo wa Sahara ukiendelea, Cecafa yapata rais mpya, nembo ya Visit Rwanda yaendelea kupanuka, bondia wa DRC Martin Bakole kupigana leo usiku, PSG, Man Utd, Spurs na Chelsea zavuna matokeo mazuri kwenye nusu fainali ligi za vilabu bingwa ulaya.

    Riadha: Ni nani atashinda mbio za London Marathon mwaka 2025?

    Play Episode Listen Later Apr 26, 2025 24:06


    Leo tumeangazia michuano ya klabu bingwa kufuzu fainali, riadha za Diamond League, Boston na London Marathon, Cameroon yafuzu Kombe la Dunia la U17, uchaguzi wa kamati ya Olimpiki nchini Kenya watibuka, Gor Mahia yanuia kujenga uwanja wao, uchambuzi wa debi ya El Clasico huku Carlos Alcaraz akijiondoa kwenye mashindano ya Madrid Open.

    Jean-Jacques wa DRC kati ya waamuzi waliochaguliwa kwenye Kombe la Dunia la Vilabu

    Play Episode Listen Later Apr 19, 2025 23:53


    Jumamosi hii tunaangazia nusu fainali ya michuano ya klabu bingwa Afrika, waamuzi kutoka Kenya na DRC miongoni mwa waamuzi kusimamia michuano ya Kombe la Dunia la Vilabu Marekani mwaka huu, fainali wa Afcon U17, kwenye riadha Chepngetich na Jepchirchir wajiondoa kwenye London Marathon, mechi za kufuzu Kombe la Dunia la wasichana chini ya umri wa miaka 17 pamoja uchambuzi wa robo fainali tatanishi kwenye ligi za mabingwa ulaya wiki hii.

    CAF: Simba yatinga nusu fainali michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika

    Play Episode Listen Later Apr 12, 2025 24:00


    Tuliyokuandalia ni pamoja na uchambuzi wa matokeo ya robo fainali mechi za klabu bingwa Afrika, Uganda yalenda kufuzu Kombe la Dunia wasiozidi miaka 17, timu ya taifa ya raga ya kina dada ya Kenya yalenga kurejea katika msururu wa dunia, michuano ya vilabu ya Afrika mchezo wa voliboli, Rwanda yaadhimisha miaka 31 michezoni tangu mauaji ya kimbari, Maluki atangaza nia ya kuwania urais wa Nock, Salah asaini kandarasi mpya Liverpool, Real Madrid itageuza meza dhidi ya Arsenal?

    Raga: Nafasi ya Shujaa 7s kusalia kwenye msururu wa raga duniani ni gani?

    Play Episode Listen Later Apr 5, 2025 23:54


    Leo kwenye kipindi tumeangazia mkondo wa kwanza robo fainali ya michuano ya klabu bingwa barani Afrika, matokeo ya Uganda na Tanzania kwenye michuano ya AFCON U17 huk Morocco, nafasi ya Shujaa 7s ya Kenya kusalia kwenye msururu wa raga duniani, mnyarwanda Celestine Nsanzuwera ashinda michuano ya gofu ya Sunshine Tour Afrika Mashariki, wachezaji watano wa ufaransa wa tenisi wapokea adhabu kwa makosa ya upangaji matokeo, Muller na De Bruyne kuondoka vilabuni mwao mwishoni mwa msimu huu.

    Kenya: Nani atatamba kwenye "Debi ya Mashemeji" AFC Leopards vs Gor Mahia?

    Play Episode Listen Later Mar 29, 2025 23:54


    Miongoni tuliyokuandalia ni pamoja na matokeo ya raga mkondo wa HongKong 7s, sakata la upangaji mchezaji dhidi ya golikipa wa Kenya Patrick Matasi, maandalizi ya debi ya Mashemeji, Misri yapewa haki za kuandaa AFCON U20 huku CAF ikiifungulia uwanja wa Benjamin Mkapa, tuzo nono kwa washindi wa Kombe la Dunia la vilabu, kocha wa Brazil atimuliwa naye Djokovic akikaribia kushinda taji lake la 100.

    Mashindano ya kukimbiza magari, yapamba moto nchini Kenya

    Play Episode Listen Later Mar 22, 2025 23:40


    Mashindano ya dunia ya kukimbiza magari, Safari Rally yanaendelea nchini Kenya. Madereva mbalimbali  kutoka  duniani, wanakutana mjini Naivasha kwa ajili ya kutafuta ubingwa wa mwaka 2025.

    CAF: Motsepe achanguliwa tena kuwa rais kwa muhula wa pili wa miaka minne

    Play Episode Listen Later Mar 15, 2025 23:49


    Tuliyokuandalia Jumamosi hii ni pamoja na uchaguzi wa CAF, uwanja wa Mkapa wafungiwa kwa muda, michuano ya kufuzu dimba la dunia kwa kina dada chini ya umri wa miaka 17, maandalizi ya mashindano ya kuendesha magari ya WRC Safari Rally, uchambuzi wa mechi za klabu bingwa Ulaya hatua ya kumi na sita bora naye Neymar alazimika kuaga kikosi cha Brazil kufuatia jeraha

    Misri, Morocco,Tunisia zang'ara mashindano ya tenisi ya vijana chini ya miaka 14

    Play Episode Listen Later Mar 2, 2025 23:46


    Tuliyokuandalia hii leo ni pâmoja na matokeo ya mashindano ya tenisi ya vijana barani Afrika chini ya miaka 14, kocha mpya wa Kenya ni nani, matokeo ya mechi za kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika kwa kina dada, timu sita kushiriki ligi ya Afrika ya basketboli kwa mara ya kwanza, huku Afrika Kusini ikijiandaa kutuma ombi rasmi la kuandaa mkondo mmoja wa F1 na Jose Mourinho apata afueni baada ya adhabu yake kupunguzwa.

    Simba kukutana na Al Masry kwenye Droo ya robo fainali Kombe la Shirikisho CAF

    Play Episode Listen Later Feb 22, 2025 23:49


    Tuliyokuandalia Jumamosi hii ni pamoja na matokeo kwenye mashindano ya kimataifa ya gofu ya Magical Kenya Open, bondia wa DRC kupambana na muingereza huko Saudi Arabia, maandalizi ya Tour du Rwanda, Droo ya robo fainali michuano ya klabu bingwa Afrika, mechi za kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika kwa kina dada 2026 na basketboli ya 2025, halikadhalika Droo ya 16 bora mechi za klabu bingwa Ulaya na michuano ya raga ya Vancouver 7s.

    Gofu: Wachezaji 150 kutoka mataifa 30 duniani kushiriki Magical Kenya Open 2025

    Play Episode Listen Later Feb 15, 2025 23:54


    Tuliyokuandalia Jumamosi hii ni pamoja na taarifa kuelekea mashindano ya gofu duniani ya Magical Kenya Open 2025, bodi ya Ligi ya soka nchini Tanzania yashusha rungu kwa Pamba Jiji na Ally Kamwe, timu 18 zimehakikisha kushiriki mashindano ya voliboli ya ukanda wa tano nchini Uganda, droo ya michuano ya Afcon U17 na U20, mechi za kufuzu Kombe la Mataifa ya kina dada 2026, Jannik Sinner akubali kufungiwa miezi mitatu, raundi ya mtoano mechi za klabu bingwa Ulaya.

    AFCON 2025: Uganda, Tanzania kundi moja katika mashindano ya mwezi Disemba

    Play Episode Listen Later Feb 1, 2025 23:57


    Hii leo tumeangazia yaliyozungumziwa kwenye mkutano mkuu wa jinsia wa Afrika Mashariki jijini Nairobi, shirikisho la kimataifa la mchezo wa baiskeli yapinga madai kuwa Rwanda itapokonywa haki za kuandaa mashindano ya chipukizi ya dunia mwezi Septemba kufuatia mzozo unaoendelea DRC, uchambuzi wa droo ya AFCON 2025, maandalizi ya CHAN 2024 tarehe mpya zatajwa na uchaguzi wa CAF mwaka huu. Pia tumechabua hatua ya mchujo mechi za Ligi ya Mabingwa Ulaya na tetesi za uhamisho ulaya.

    Ligi kuu ya Tanzania bara imetajwa nafasi ya nne barani Afrika na 57 duniani

    Play Episode Listen Later Jan 25, 2025 23:52


    Jioni hii kwenye makala ya Jukwaa la Michezo tumeangazia Congo kufutiliwa kushiriki mashindano ya CHAN 2024, kufutwa kazi kwa kocha wa Rwanda Torsten Spittler, uwanja mpya wa Talanta jijini Nairobi unaendelea kupiga hatua kwenye ujenzi huku ligi ya Tanzania ikitajwa nafasi ya nne katika orodha ya ligi bora Afrika, Kenya yang'ara mashindano ya chipukizi ya tenisi, msururu wa raga ya dunia mkondo wa tatu, fainali za Australian Open na tetesi za uhamisho ulaya na Afrika.

    Claim Jukwaa la Michezo

    In order to claim this podcast we'll send an email to with a verification link. Simply click the link and you will be able to edit tags, request a refresh, and other features to take control of your podcast page!

    Claim Cancel