POPULARITY
Karibu uungane nami Elizabeth Masanja, katika Kipindi cha Maswali yahusuyo Imani Mwezeshaji ni Frateri Jackob Mkandawile kutoka Parokia ya Bikira Maria mpalizwa Mbinguni Jimbo Katoliki Iringa, akijibu swali la Msikilizaji linalosema Je, heshima kwa Bikira Maria ina misingi gani kibiblia?” L'articolo Je, heshima kwa Bikira Maria ina misingi gani kibiblia? proviene da Radio Maria.
Matangazo ya saa nzima kuhusu habari za kutwa, ikiwa ni pamoja ripoti kutoka kwa waandishi wetu sehemu mbali mbali duniani na kote Afrika Mashariki na Kati, na vile vile vipindi na makala maalum kuhusu afya, wanawake, jamii na maendeleo.
Kwa Undani ni matangazo ya dakika 25 yanayochambua habari kwa undani zaidi na kumpa msikilizaji maelezo ya kina kuliko ilivyo kawaida kuhusu tukio au swala lililojitokeza katika habari.
Nchini Tanzania Mpango wa Umoja wa Mataifa wa kushirikisha kampuni kuzingatia será na misingi endelevu na inayojali jamii, au kwa kiingereza UN Global Compact Tanzania umeanza kuona mabadiliko katika kushirikisha kampuni kuzingatia misingi 7 ya kumwezesha mwanamke kwenye sekta ya biashara.Jijini Dar es salaam, mji mkuu wa kibiashara wa Tanzania nashiriki kwenye tukio la Gonga Kengele kwa usawa wa jinsia, mwezi huu wa Machi ambao unamulika masuala ya wanawake. Tukio limeandaliwa na UN Global Compact Tanzania na Mkurugenzi wake Masha Makatta akaeleza sababu. Akimaanisha gonga kengele kwa usawa wa kijinsia katika taifa hili ambalo takwimu za mwaka 2019 kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu, NBS zinaonesha ni asilimia 18 tu ya wataalamu walioajiriwa katika Sayansi na Uhandisi ni wanawake. Bi. Makatta akaelezea walichojumuisha kwenye tukio la mwaka huu kwa lengo la kumjumuisha mwanamke. Na je kulikuwa na mafanikio yoyote? Kwa Women Empowerment Principles anamaanisha Kanuni za Uwezeshaji mwanamka ambazo kwa mujibu wa UN Global Compact ziko 7 na miongoni mwao ni kuendeleza elimu, mafunzo na ueledi kwa wanawake. Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Tanzania Zlatan Milišić, akanieleza hatua ya muda mrefu itakayomuinua zaidi mtoto wa kike, “Umoja wa Mataifa nchini Tanzania una miradi mbalimbali inayoelekea kwenye vipaumbele tofauti vya kazi zetu zinazogusa wanawake. Kuna ambayo ni mahsusi kwa wanawake kwa minajili kwamba hatutaki waachwe nyuma katika maeneo fulani. Lakini mingine ni ya jumla lakini bila shaka inapatia kipaumbele wanawake pale ambako idadi yao ni ndogo.”
Watoto wakieleza Misingi ya imani ya kanisa la Waadventista wa Sabato
Watoto wakieleza Misingi ya imani ya kanisa la Waadventista wa Sabato
Baraka Kizuguto si moja ya majina yajulikanayo miungoni mwa wa Tanzania wengi ambao asilimia kubwa ya wenye simu za mkononi hupendelea zaidi habari za maisha ya watu maarufu na mashuhuri, kutaka kujua wanakula nini, wanaishi wapi, wanalala wapi, wanalala na nani na kadhalika. Na kama wewe ni mmoja wa watu hao na si mpenzi wa mpira basi kumfahamu mgeni wetu wa kwenye kiti chakavu wiki hii itakuwia vigumu. Ila kwa wale watu wa mpira, au wafanyakazi kwenye Vyama vya mpira hapa kwetu na Afrika kwa ujumla au wachezaji au waalimu wa mpira jina na sura yake si ngeni kabisa kwao. Mimi na yeye tulifahamiana hapa mjini miaka kadhaa iliyopita na rafiki yetu mmoja ndo alituunghanisha. Mapenzi yangu kwa mpira wa miguu nayo yalifanya urafiki wetu ukolee zaidi, amekua kiungo kwenye mambo yangu mengi yanayohusiana na kiwanda hiko kwa muda sasa. MSHAURI wangu pia baada ya mimi kupata kibali cha kuweza kuwasisamia wachezaji wa mpira wa miguu duniani. Yeye ni mtu ambaye anawajua wachezaji karibia wote wanaocheza mpira nchi hii na nje, na msaada wake kwangu ni wa kipekee kabisa. Nia na madhumuni ya kusema aje tuongee nae kwenye kipindi chetu ni kwasababu ambazo nimezieleza hapo juu kwenye wasifu wake. Waswahili wanasema ‘kizuri kula na nduguzo' na kwa msaada na elimu ambayo mimi hupata kutoka kwake nikasema kwanini sasa tusimlete mezani na wengine wakamsikia? Ukichukulia suala la ajira mi kipengele kweli kweli kwenye nchi yetu. Baraka yeye ana ajira ambayo kama tukimsikiliza vizuri basi wengi wanaweza kuchagua njia hiyo na wakapata chochote kitu. Sasa NINI ambacho Baraka hufanya? Kwenye episode hii anatuelezea majukumu yake ya muda mwingi kutoka Shirikisho la Mpira wa miguu Tanzania na Shirikisho la Mpira la Africa. Kukiwa na michezo mbali mbali kama ya nchi na nchi, au klabu kwa klabu yeye ndo huwa msimamizi wa kwanza kwenye michezo hiyo. Safari za kila wikiendi haziishi na kaniambia nidhamu na kujifunza kila siku ndo msingi wake, na je ungependa kujua kikubwa zaidi ambacho ni muhimu kuliko hayo yote? Baraka anasema ni kuweza kuheshimu WAKATI. Hiyo ndo siri ya mafanikio yake, na ndo siri ya yeye kuweza kupata kazi zaidi na zaidi na kuheshimika pia. Kama akiwa kapangiwa mechi ya kusimamia tuseme nchini Angola, labda Kuna mechi kati ya Angola na pengine Madagascar au mechi za klabu kutoka nchi hizo, yeye ndo anakua wakwaza kufika kabla ya team na waamuzi. Kazi yake ni kuhakikisha kila anaye husika na mchezo huo anafanya jambo lake kwa wakati unaotakiwa. Ukaguzi wa hoteli watakazokaa wageni wa mchezo, waamuzi, team, jinsi watakavyoenda uwanjani, mikutano ya waandishi wa habari, ulinzi wa waamuzi wa mchezo huo, kuhusu ball boys, jinsi team zitakavyo ingia uwanjani, kuhakikisha mchezo unaanza kwa wakati na kila kitu kwenda sawa sawa. Jinsi ambavyo unafanya kazi yako vizuri ndo jinsi ambavyo Shirikisho linakuamini na ndo ambavyo CV yako inazidi kukua. Kwahiyo mmoja anawezaje kupata nafasi ya kufanya hayo yote? Yeye aliwezaje mpaka akafika huko? Nini challenge ya hizi kazi? Je kuna ambao Shirikisho linawaandaa kwaajili ya kuzifanya kazi hizo pia? Na wako wangapi ambao wanaliwakilisha Taifa kwenye hiyo kazi? Na je vipi kuhusu malipo yake? Ni kitu ambacho mmoja anaweza kusema ndo anataka kukifanya kama kazi? Misingi yake ikoje? Mtu anatakiwa aanzie wapi hasa? Na ni kitu ambacho anaweza kufanya kwa muda gani mpaka afikie huko ambako yeye yupo sasa? Vipi kuhusu FIFA? Huko yeye ana mpango nako? Ki ukweli yalikua mazungumzo mazuri kwangu na kwake na natumai pia yatakua na uzito flani kwako na kama si kwako ambaye ushajichagulia cha kufanya, basi hata kwa mwengine ambaye unamjua na ana interest na mpira ukamuelekeza juu ya hili. Tafadhali enjoy. Love, Salama. --- Support this podcast: https://anchor.fm/yahstonetown/support
Ubaguzi wa rangi na ubaguzi mwingine dhidi ya watoto kwa misingi ya makabila, lugha na dini zao umeenea duniani kote na kuleta athari kwenye mfumo wa haki, usawa na hata uwezo wa kujua kusoma, hayo yapo kwenye ripoti iliyotolewa leo na Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Watoto UNICEF.Taarifa iliyotolewa leo na UNICEF kutoka New York Marekani imeeleza kuwa katika utafiti uliofanywa kwenye nchi 22 za kipato cha chini na cha kati umeonesha jinsi watoto wanavyobaguliwa katika afya, kupata rasilimali zinazotolewa na serikali, na elimu.Mkurugenzi Mtendaji wa UNICEF Catherine Russell amesema ubaguzi wa rangi na kimfumo unawaweka watoto katika hatari ya kunyimwa haki na kutengwa vitendo ambavyo vinaweza kuwa na athari katika Maisha yao yote. Bi. Russell amesema “Hii inatuumiza sisi sote. Kulinda haki za kila mtoto hata awe nani, popote anapotoka ndiyo njia ya uhakika ya kujenga ulimwengu wenye amani zaidi, ustawi na haki kwa kila mtu.”Ripoti hiyo ya utafiti iliyopewa jina la Haki zilizonyimwa: Athari za ubaguzi kwa watoto imeonesha kuwa wale walio katika kundi la kunufaika wameonekana kuwa na uwezekano maradufu wa kuwa na stadi za kimsingi za kusoma. Kwa wastani, wanafunzi walio na umri wa miaka 7 mpaka 14 kutoka kundi lililonufaika zaidi wana uwezekano wa kuwa na ujuzi wa kusoma wa kimsingi zaidi ya mara mbili, kuliko wale wa kundi lisilo na faida zaidi.Ubaguzi na kutengwa kunazidisha umaskini wa vizazi na vizazi na kusababisha watu kuwa na afya duni, lishe isiyo bora, ujauzito katika umri mdogo, mimba nyingi miongoni mwa wasichana barubaru, uwezekano mkubwa wa kufungwa, na viwango vya chini vya ajira na mapato wakiwa watu wazima.Kwa mfano, katika sera za kinidhamu nchini Marekani, watoto Weusi wana uwezekano wa karibu mara nne zaidi wa kusimamishwa shule kuliko watoto wa kizungu, na zaidi ya mara mbili ya uwezekano wa kukamatwa kutokana na makosa mbalimbali shuleni, imeeleza ripoti hiyo.Ripoti pia imeonesha utofauti mkubwa kati ya makabila madogo na jamii za asili.Kwa mfano, nchini Lao, asilimia 59 ya watoto walio na umri wa chini ya miaka 5 kutoka kabila la Wamon-Khmer walio wachache wameandikishwa wakati wa kuzaliwa, wakati wale wa kabila la Lao-Tai waliowengi waliaondikishwa ni asilimia 80. Usajili wa watoto wakati wa kuzaliwa ni muhimu kwakuwa ni sharti la kupata haki za kimsingi kwa taifa.
Ikiwa leo ni maadhimisho ya siku ya Umoja wa Mataifa, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema ni wakati muhimu wa kurejesha tena matumaini na imani katika kile ambacho ubinadamu unaweza kufanikiwa pindi jamii yote ya kimataifa itakapofanya kazi kama kitu kimoja na kwa mshikamano wa kimataifa. Thelma Mwadzaya na taarifa kamili.Siku ya Umoja wa Mataifa huadhimishwa tarehe 24 ya mwezi Oktoba kila mwaka kukumbuka tarehe kama hiyo mwaka 1945 wakati Chata ya kuanzisha Umoja huo ilipoanza kutumika baada ya kutiwa saini na kuridhiwa na nchi waanzilishi 51 zikiwemo tano zenye ujumbe wa kudumu katika Baraza la Usalama ambazo ni China, Ufaransa, Uingereza, Urusi na Marekani.,Katibu Mkuu Guterres katika ujumbe wake wa siku hii anasema Umoja wa Mataifa ni tunda la matumaini. Matumaini na azma baada ya Vita Kuu ya Pili ya Dunia ya kwamba kusonga kutoka mizozo na kuelekea katika ushirikiano wa kimataifa.Guterres amesema “leo hii shirika letu linakumbwa na majaribu kuliko wakati wowote ule. Lakini Umoja wa Mataifa uliundwa kwa ajili ya nyakati kama hizi. Sasa kuliko wakati wowote ule tunahitaji kurejesha tena uhai wa misingi ya Chata ya Umoja wa Mataifa katika pembe zote za dunia.”Misingi mikuu saba ya Umoja wa Mataifa ambao sasa una wanachama 193 ni pamoja na kila nchi mwanachama ni sawa na mwingine na migogoro yote inapaswa kutatuliwa kwa njia ya amani.Katibu Mkuu anasema hilo lifanyike kwa kupatia fursa amani na kwa kumaliza migogoro ambayo inavuruga maisha, mustakabali na maendeleo ya dunia.Halikadhalika kwa kufanya kazi kutokomeza lindi la umaskini, kupunguza ukosefu wa usawa na kunusuru malengo ya maendeleo endelevu, SDGs.Ametaja pia kulinda sayari dunia, ikiwemo kuondokana na uraibu wa matumizi ya nishati kisukuku na kuanza kutekeleza mapinduzi ya nishati jadidifu isiyoharibu mazingira.Hatimaye kuweka mizania ya fursa na uhuru kwa wanawake na wasichana na kuhakiksha haki zao kibinadamu zinazingatiwa.Wakati Chata ya Umoja wa Mataifa ina misingi saba, kwa upande wa malengo yake ni manne ambayo ni kulinda amani na Usalama duniani, kuimarisha uhusiano wa kirafiki baina ya nchi, kufanikisha ushirikiano wa kimataifa katika kutatua matatizo ya kiuchumi, kijamii, kitamaduni au kiutu na kuwa kitovu cha kuweka utangamano wa vitendo vya nchi katika kufanikisha malengo hayo.
KACOU 21: KUCHAGULIWA KABLA YA DUNIA KUWEKA MISINGI by Prophète Kacou Philippe
Mashindano ya michezo ya Olimpiki ya majira ya baridi kali yakianza Ijumaa ya tarehe 4 mwezi huu wa Februari mwaka 2022 huko nchini China, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametaka kila mtu kuzingatia azimio la sitisho la mapigano wakati wa mashindano hayo. Wanamichezo wa kiwango cha juu wakiwa tayari huko jijini Beijing China na viunga vingine ya taifa hilo la bara la Asia kwa ajili ya mashindano hayo ya olimpiki ya majira ya baridi kali, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres anakumbushia makubaliano yaliyopitishwa na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mwezi Desemba mwaka jana ya kusitisha mapigano. Katika ujumbe wake Guterres anasema wanamichezo wanashiriki mashindano hayo kwa misingi ya maelewano, kujituma na bila kuoneana. “Misingi hii inatuvutia sote. Azimio la Olimpiki kuhusu sitisho la mapigano linatoa wito kwa pande zote kusitisha mapigano katika kipindi chote cha mashindano ya olimpiki.” Amesema Guterres. Kwa mujibu wa azimio hilo, nchi zinatakiwa kusiweko na mapigano siku 7 kabla ya kuanza kwa michezo hiyo hadi siku saba baada ya kumalizika kwa mashindano ya olimpiki ya majira ya baridi kwa watu wenye ulemavu, ambayo yatafikia ukomo tarehe 13 mwezi ujao wa Machi. Katibu Mkuu amesema mapigano yakisambaa na mivutano ikiongezeka, ombi la sitisho la mapigano linatoa fursa ya kuamliza tofauti na kusaka njia bora ya amani ya kudumu. “Tunavyohaha kutokomeza janga la COVID-19, hebu na tuungane kwa mustakabali salama zaidi, wenye ustawi na endelevu kwa kila mtu. Natoa wito kwa kila mtu kuzingatia mkataba wa Olimpiki wa sitisho la mapigano wakati wa mashindano ya olimpiki sambamba na yale ya walemavu. Kupitia nguvu ya michezo, na maadili ya Olimpiki, hebu na tujenge utamaduni wa amani.” Ametamatisha Guterres. Azimio hilo lililopatiwa jina Kujenga dunia yenye amani na bora zaidi kupitia michezo na maadili ya Olimpiki, lilipitishwa kwa kauli moja na lilikuwa limewasilishwa na mataifa 173.
Baada ya kutambua kusudi la Mungu maishani mwako ni muhimu kuijua misingi ya kusudi hilo ili uweze kuliishi vilivyo. --- Send in a voice message: https://anchor.fm/bintiwayesu/message
Misingi Imara Ya Ustawi Wa Kweli
Misingi Imara Ya Ustawi Wa Kweli
Misingi Imara Ya Ustawi Wa Kweli
Misingi Imara Ya Ustawi Wa Kweli
Misingi Imara Ya Ustawi Wa Kweli
Misingi Imara Ya Ustawi Wa Kweli
Misingi Imara Ya Ustawi Wa Kweli
MWAKASEGE: MISINGI YA UCHUMI WAKO INAHITAJI KUTENGENEZWA NA DAMU YA YESU website:www.sirizabiblia.com +255 758 708 804 whatssap only --- Send in a voice message: https://anchor.fm/siri-za-biblia/message
Misingi ya ujana Mwema
Misingi ya ujana Mwema
Katika siku ya kimataifa ya kuwakumbuka waathirika wa utumwa na biashata ya utumwa katika bahari ya Atlantiki hii leo Katiku Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema ili kuwaenzi vyema mamilioni ya watu wenye asili ya Afrika waliopitia madhila asiyoelezeka katika utumwa na biashara ya utumwa ni vyema kuyania wazi yaliyowasibu na kuhakikisha yatokomezwa. Katika ujumbe wake wa siku hii Antonio Guterres amesema (SAUTI YA ANTONIO GUTERRES)
Shirika la African Women Unity, huwakilisha wanawake kutoka kanda ya mashariki ya Afrika, wanao ishi mjini Sydney Australia.
Misingi Ya Da’awa Ya Kweli
Misingi Bora Ya Malezi Ya Watoto Katika Uislam 1
Misingi Bora Ya Malezi Ya Watoto Katika Uislam 5
Misingi Bora Ya Malezi Ya Watoto Katika Uislam 4
Misingi Bora Ya Malezi Ya Watoto Katika Uislam 3
Misingi Bora Ya Malezi Ya Watoto Katika Uislam 2