Podcasts about oktoba

  • 32PODCASTS
  • 1,156EPISODES
  • 24mAVG DURATION
  • 2DAILY NEW EPISODES
  • Nov 5, 2025LATEST

POPULARITY

20172018201920202021202220232024


Best podcasts about oktoba

Latest podcast episodes about oktoba

Wimbi la Siasa
Nini hatima ya Tanzania baada ya uchaguzi mkuu uliokumbwa na vurugu ?

Wimbi la Siasa

Play Episode Listen Later Nov 5, 2025 10:16


Machafuko yalikumba uchaguzi mkuu wa Tanzania, uliofanyika Oktoba 29, 2025 na rais Samia Suluhu Hassan kutangazwa mshindi kwa kupata asilimia 97.6 ya kura. Chama kikuu cha upinzani CHADEMA, kimesema ushindi wa Samia ni kichekesho cha demokrasia. Anapaswa kufanya nini ili kuirejesha Tanzania katika utulivu wa kisiasa ? Tunachambua.

Siha Njema
Afueni kwa wanawake wanaokatwa matiti yao kutokana na saratani

Siha Njema

Play Episode Listen Later Nov 2, 2025 9:56


Kila mwezi wa Oktoba, ulimwengu huadhimisha Mwezi wa Uhamasishaji wa Saratani ya Matiti, lengo kuu likiwa kuhamasisha vipimo vya mapema ili kupunguza hatari ya ugonjwa huu na kutafuta msaada wa kifedha kwa ajili ya utafiti kuhusu saratani ya matiti. Inakadiriwa kuwa, wagonjwa wapya zaidi ya milioni 2.3 wa saratani ya matiti hugunduliwa kila mwaka, kulingana na takwimu za Shirika la Afya Duniani. Wengi wa wanawake waliopatwa na saratani hii walilalzimika kukatawa titi moja au yote mawili ili kuokoa maisha yao,  na hivyo kupoteza kiungo muhimu cha mwili.

Habari za UN
31 OKTOBA 2025

Habari za UN

Play Episode Listen Later Oct 31, 2025 9:59


Hii leo jaridani tunaangazia Siku ya Kimataifa ya Majiji, vifo na majeruhi vilivyotokea katika maandamano yanayohusiana na uchaguzi mkuu uliofanyika nchini Tanzania na uwezeshaji wa wanawake nchini huko huko Tanzania.Dunia leo ikiadhimisha Siku ya Kimataifa ya Majiji, majiji ya kisasa pamoja na kukumbatia teknolojia yametakiwa kuhakikisha yanazingatia zaidi watu ili wengine wasiachwe nyuma au kutengwa na maendeleo hayo.Ofisi ya Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Haki za Binadamu imeeleza wasiwasi mkubwa kufuatia vifo na majeruhi vilivyotokea katika maandamano yanayohusiana na uchaguzi mkuu uliofanyika nchini Tanzania tarehe 29 mwezi huu wa Oktoba.Mpango wa “Chaguo Langu, Haki Yangu” nchini Tanzania ni jitihada thabiti zinazolenga kuwawezesha wanawake na wasichana kuishi maisha huru dhidi ya ukatili na vitendo hatarishi. Kwa ufadhili wa Serikali ya Finland, Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu (UNFPA) kwa kushirikiana na Serikali ya Tanzania kupitia Shirika la IPS, linafanya mabadiliko halisi katika jamii.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!

Habari za UN
Kauli ya ofisi ya UN ya Haki za binadamu kufuatia vurugu Tanzania baada ya uchaguzi mkuu

Habari za UN

Play Episode Listen Later Oct 31, 2025 2:42


Ofisi ya Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Haki za Binadamu imeeleza wasiwasi mkubwa kufuatia vifo na majeruhi vilivyotokea katika maandamano yanayohusiana na uchaguzi mkuu uliofanyika nchini Tanzania tarehe 29 mwezi huu wa Oktoba. Selina Jerobon na maelezo zaidi.

Shirin Safe 0500 UTC - Voice of America
Shirin Safe 0500 UTC (30:00) - Oktoba 31, 2025

Shirin Safe 0500 UTC - Voice of America

Play Episode Listen Later Oct 31, 2025 30:00


Kullum da karfe 6 na safe agogon Najeriya da Nijar muna gabatar da labarai da rahotanni da dumi-duminsu, sannan mu na gabatar da wasu shirye-shirye kamar Noma da Lafiya Uwar Jiki.

Alfajiri - Voice of America
Alfajiri - Oktoba 31, 2025

Alfajiri - Voice of America

Play Episode Listen Later Oct 31, 2025 30:00


Matangazo ya nusu saa kuhusu habari za mapema asubuhi pamoja na habari za michezo.

Jioni - Voice of America
Jioni - Oktoba 31, 2025

Jioni - Voice of America

Play Episode Listen Later Oct 31, 2025 59:59


Matangazo ya saa nzima kuhusu habari za kutwa, ikiwa ni pamoja ripoti kutoka kwa waandishi wetu sehemu mbali mbali duniani na kote Afrika Mashariki na Kati, na vile vile vipindi na makala maalum kuhusu afya, wanawake, jamii na maendeleo.

VOA Express - Voice of America
VOA Express - Oktoba 31, 2025

VOA Express - Voice of America

Play Episode Listen Later Oct 31, 2025 29:59


VOA Express ni matangazo mapya yenye mwendo wa kasi yakiangalia habari mpya za mchana na maelezo ya maswala yanayohusu vijana na wanawake. Matangazo haya yanafuatilia habari zilizojitokeza nyakati za mchana na ripoti za kina za habari ambazo hazisikiki sana katika matangazo mengineyo. VOA Express pia inafuatilia kwa karibu sana maswala yanayovuma katika mitandao ya kijamii kama sehemu moja muhimu ya upashanaji habari siku hizi.

Kwa Undani - Voice of America
Kwa Undani - Oktoba 31, 2025

Kwa Undani - Voice of America

Play Episode Listen Later Oct 31, 2025 29:59


Kwa Undani ni matangazo ya dakika 25 yanayochambua habari kwa undani zaidi na kumpa msikilizaji maelezo ya kina kuliko ilivyo kawaida kuhusu tukio au swala lililojitokeza katika habari.

Shirin Hantsi 0700 UTC - Voice of America
Shirin Hantsi 0700 UTC (30:00) - Oktoba 31, 2025

Shirin Hantsi 0700 UTC - Voice of America

Play Episode Listen Later Oct 31, 2025 29:59


Mu kan komo da karfe 8 na safe agogon Najeriya da Nijar domin sake gabatar muku da labarai da hirarraki, da sharhin jaridu kama daga Najeriya zuwa Nijar har Ghana, da kuma ra'ayoyinku.

Habari za UN
30 OKTOBA 2025

Habari za UN

Play Episode Listen Later Oct 30, 2025 11:41


Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina ambayo Bi. Lucy Githinji, mkazi wa jimbo la New Jersey nchini Marekani amezungumza na idhaa hii baada ya matembezi ya hiari kwa ajili ya kuhamasisha jamii kuhusu saratani ya titi, akisema hakika dawa zinafanya kazi.Mratibu wa Umoja wa Mataifa wa Masuala ya Kibinadamu nchini Sudan, Denise Brown amesema ni kweli wamepokea ripoti za mauaji ya baadhi ya wahudumu wa kujitolea huko El Fasher jimboni Darfur wakati huu ambapo mji huo umetwaliwa na wapiganaji wa Vikosi vya Usaidizi wa Haraka, (RSF).Kimbunga Melissa kimepungua nguvu baada ya kutua nchini Jamaica kama kimbunga cha kiwango cha 5, na kuvunja rekodi ya kimbunga chenye nguvu zaidi, kabla ya kuelekea kaskazini mashariki kupita Cuba hadi Bahamas, na kusababisha mafuriko makubwa, uharibifu na kukatika kwa umeme katika maeneo mbalimbali ya Karibea na Amerika ya Kati.Nchini Cameroon, kufuatia mauaji ya raia wakati wa maandamano ya kupinga kutangazwa kwa Paul Biya kuwa mshindi wa kiti cha Urais kwenye uchaguzi uliofanyika Oktoba 12, Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Binadamu imeeleza wasiwasi wake juu ya ripoti za vifo hivyo.Na katika Katika kujifunza lugha ya Kiswahili hii leo,  mtaalam wetu Onni Sigalla, Mhariri mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania, BAKITA. Anafafanua maana za neno "SUMIA."Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!

Shirin Safe 0500 UTC - Voice of America
Shirin Safe 0500 UTC (30:00) - Oktoba 30, 2025

Shirin Safe 0500 UTC - Voice of America

Play Episode Listen Later Oct 30, 2025 29:59


Kullum da karfe 6 na safe agogon Najeriya da Nijar muna gabatar da labarai da rahotanni da dumi-duminsu, sannan mu na gabatar da wasu shirye-shirye kamar Noma da Lafiya Uwar Jiki.

Alfajiri - Voice of America
Alfajiri - Oktoba 30, 2025

Alfajiri - Voice of America

Play Episode Listen Later Oct 30, 2025 29:34


Matangazo ya nusu saa kuhusu habari za mapema asubuhi pamoja na habari za michezo.

Jioni - Voice of America
Jioni - Oktoba 30, 2025

Jioni - Voice of America

Play Episode Listen Later Oct 30, 2025 29:59


Matangazo ya saa nzima kuhusu habari za kutwa, ikiwa ni pamoja ripoti kutoka kwa waandishi wetu sehemu mbali mbali duniani na kote Afrika Mashariki na Kati, na vile vile vipindi na makala maalum kuhusu afya, wanawake, jamii na maendeleo.

Habari za UN
29 OKTOBA 2025

Habari za UN

Play Episode Listen Later Oct 29, 2025 9:53


Leo jaridani tunamulika kimbunga Melissa huko Karibea, uhamishaji wagonjwa kutoka Gaza kwenda nchi za nje kupata huduma za kigeni na hali tete kwa watoto nchini Sudan. Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi.Katibu Mkuu wa Umoja wa MataifaAntonio Guterres ameonesha wasiwasi mkubwa wakati Kimbunga Melissa kikiwa miongoni mwa vimbunga vyenye nguvu zaidi kuwahi kurekodiwa katika Bahari ya Atlantiki kinaendelea kusababisha uharibifu mkubwa katika eneo la Karibea.Kupitia taarifa yake iliyotolewa leo mjini New York Marekani na msemaji wake Katibu Mkuu amesema kimbunga hicho kimeacha athari kubwa nchini Jamaica, Cuba na Bahamas  huku mafuriko makubwa yakiripotiwa pia nchini Haiti na Jamhuri ya Dominika.Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa Duniani, WHO, limeongoza uhamishwaji wa kwanza  wagonjwa kutoka Gaza tangu awamu mpya ya kusitishwa kwa mapigano. Katika muda wa siku mbili, wagonjwa 41 waliokuwa katika hali mbaya pamoja na familia zao 145 wamehamishwa kutoka eneo la mgogoro, huku maelfu zaidi wakiendelea kusubiri matibabu ya dharura. Flora Nducha na taarifa zaidi.Nchini Sudan hususani katika eneo la El Faher kusinimagharibi mwa nchi, hali ya kibinadamu inazidi kuwa mbaya kila siku, huku ghasia, njaa, na vizuizi vya utoaji misaada vikiendelea kuathiri mamilioni ya watu wakiwemo watoto waliokwama katika maeneo ya vita. Anold Kayanda na taarifa zaidi.

Habari za UN
Wagonjwa wanaohitaji tiba zaidi Gaza wasafirishwa kupata tiba zaidi Afrika Kusini na kwingineko

Habari za UN

Play Episode Listen Later Oct 29, 2025 3:24


Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ulimwenguni, WHO, limeongoza uhamishwaji wa wagonjwa kutoka Gaza eneo la Palestina linalokaliwa kimabavu na Israeli, ikiwa ni  mara ya kwanza tangu kuanza kwa awamu mpya ya kusitishwa kwa mapigano kwenye  ukanda huo.Katika muda wa siku mbili, wagonjwa 41 waliokuwa katika hali mbaya pamoja na familia zao 145 wamehamishwa kutoka eneo la mgogoro, kuelekea Afrika Kusini, Uswisi na kwingineko, huku maelfu zaidi wakiendelea kusubiri matibabu ya dharura.Katika hospital iliyojengwa kwa mahema  katika eneo la AL-MAWASI, RAFAH kwenye Ukanda wa Gaza wagonjwa wakihudumiwa kila kona watoto kwa wakubwa Miongoni mwao ni Ibrahim Abu Ashiba, mkurugenzi wa filamu ambaye maisha yake yamebadilika ghafla. Anakumbuka wakati alipojeruhiwa. Anasema, "Nilipigwa risasi mara kadhaa, mara moja kwenye kifua, mara moja kwenye bega, mara mbili mkononi. Risasi hizo mbili zilikata mishipa ya neva ya mkono wangu. Sasa siwezi kushika kamera wala kunyoosha mkono wangu kawaida. Ghafla, maisha yangu yote yalisimama."Safari ya kupona kwa Ibrahim inaanzia Afrika Kusini, ambapo amekubaliwa kwenda kupokea matibabu maalum ambapo anasema "Maisha yangu yote yalikuwa yamesimama baada ya kujeruhiwa hadi waliponipigia simu na kunijulishakwamba nitasafiri kwenda Afrika Kusini kwa matibabu. Ilionekana kama nimezaliwa upya."Mgonjwa mwingine katika hospitali hii ni, Maria Al-Shaer, alijeruhiwa vibaya katika mashambulizi yaliyokuwa yakiendelea Gaza, huku akipoteza ndugu zake. Mama yake, Raghda Ahmed Al Shaer, anaelezea mateso hayo. "Maria amepoteza baba yake na ndugu zake wote. Alijeruhiwa na kuvunjika mguu, mifupa na kupoteza nyama. Anahitaji upasuaji wa kuwekewa viungo bandia. Maisha yake yamegeuka, hawezi kutembea, na hali yake ya kisaikolojia imeathirika sana."Uhamishwaji huu umeratibiwa na Shirikisho la Chama cha Msalaba Mwekundu Palestina, kwa msaada wa WHO. Dkt. Luca Pigozzi, Mratibu wa Timu ya Dharura ya WHO, anafafanua umuhimu wake."Huu ni uhamishaji wa kwanza wa matibabu tangu kusitishwa kwa mapigano Oktoba 10. Tumejizatiti kuongeza uwezo wetu kusaidia na kuratibu uhamishaji kwa ajili ya matibabu, kwa ushirikiano wa karibu na Shirikisho la chama cha Msalaba Mwekundu la Palestina."Raghda anaeleza matumaini kwa ajili ya binti yake wanapohama kwenda Uswisi. "Wametupigia kutuarifu kwamba Maria amekubaliwa kusafiri kwenda Uswisi kwa matibabu. Tumefurahi sana kwamba atatembea tena, na hali yake ya kisaikolojia itaboreka. Atarudi kuwa Maria wa kawaida kama tuliyemjua."WHO inasisitiza kuwa wagonjwa takriban 15,000 bado wanangojea idhini ya kupata matibabu nje ya Gaza na inatoa wito kwa nchi zote kufungua milango yote za dharura kwa ajili ya uokoaji wa wagonjwa.

Shirin Safe 0500 UTC - Voice of America
Shirin Safe 0500 UTC (30:00) - Oktoba 29, 2025

Shirin Safe 0500 UTC - Voice of America

Play Episode Listen Later Oct 29, 2025 29:59


Kullum da karfe 6 na safe agogon Najeriya da Nijar muna gabatar da labarai da rahotanni da dumi-duminsu, sannan mu na gabatar da wasu shirye-shirye kamar Noma da Lafiya Uwar Jiki.

Alfajiri - Voice of America
Alfajiri - Oktoba 29, 2025

Alfajiri - Voice of America

Play Episode Listen Later Oct 29, 2025 29:59


Matangazo ya nusu saa kuhusu habari za mapema asubuhi pamoja na habari za michezo.

Jioni - Voice of America
Jioni - Oktoba 29, 2025

Jioni - Voice of America

Play Episode Listen Later Oct 29, 2025 30:00


Matangazo ya saa nzima kuhusu habari za kutwa, ikiwa ni pamoja ripoti kutoka kwa waandishi wetu sehemu mbali mbali duniani na kote Afrika Mashariki na Kati, na vile vile vipindi na makala maalum kuhusu afya, wanawake, jamii na maendeleo.

Habari za UN
28 OKTOBA 2025

Habari za UN

Play Episode Listen Later Oct 28, 2025 11:02


Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayoangazia mradi wa TANZIE huko Chuo Kikuu Mzumbe, mkoani Morogoro, mashariki mwa Tanzania, unaolenga kusongesha Malengo ya Maendeleo Endelevu SDGs. Pia tunakuletea habari kwa ufupi na uchambuzi wa neno la wiki.Mamilioni ya watu nchini Jamaica na katika ukanda wote wa Karibea wanajiandaa kukabiliana na madhara makubwa ya kimbunga Melissa huku Umoja wa Mataifa na washirika wake wakionya kuhusu tishio kubwa na la haraka la kibinadamu.Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres, ameelezea wasiwasi wake mkubwa kufuatia kuongezeka kwa mapigano ya kijeshi mjini El Fasher, jimbo la Darfur Kaskazini, nchini Sudan. Kupitia taarifa iliyotolewa na Msemaji wake usiku wa tarehe27 Oktoba 2025 kwa saa za New York marekani, Guterres amesema kwa zaidi ya miezi kumi na minane, wakazi wa El Fasher na maeneo ya jirani wamekuwa wakikabiliwa na mateso makubwa huku makundi ya Wanamgambo wa Rapid Support Forces (RSF) yakizingira mji huo.Na hii leo, Ofisi ya Umoja wa Matiafa ya Haki za Binadamu na Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa Usaidizi nchini Afghanistan wamechapisha waraka wa taarifa kuhusu madhara makubwa ya kina za haki za binadamu yaliyotokana na kusitishwa kwa huduma za mawasiliano nchini Afghanistan tarehe 29 Septemba hadi tarehe mosi mwezi huu, — hatua ambayo imezidisha changamoto nyingi ambazo tayari zinawakabili wananchi.Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili leo ukumbi ni wake mlumbi wa Kiswahili Joramu Nkumbi kutoka nchini Tanzania, anafafanua maana ya neno "KIMBIMBI"Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!

Shirin Safe 0500 UTC - Voice of America
Shirin Safe 0500 UTC (30:00) - Oktoba 28, 2025

Shirin Safe 0500 UTC - Voice of America

Play Episode Listen Later Oct 28, 2025 29:59


Kullum da karfe 6 na safe agogon Najeriya da Nijar muna gabatar da labarai da rahotanni da dumi-duminsu, sannan mu na gabatar da wasu shirye-shirye kamar Noma da Lafiya Uwar Jiki.

Alfajiri - Voice of America
Alfajiri - Oktoba 28, 2025

Alfajiri - Voice of America

Play Episode Listen Later Oct 28, 2025 29:59


Matangazo ya nusu saa kuhusu habari za mapema asubuhi pamoja na habari za michezo.

Jioni - Voice of America
Jioni - Oktoba 28, 2025

Jioni - Voice of America

Play Episode Listen Later Oct 28, 2025 29:59


Matangazo ya saa nzima kuhusu habari za kutwa, ikiwa ni pamoja ripoti kutoka kwa waandishi wetu sehemu mbali mbali duniani na kote Afrika Mashariki na Kati, na vile vile vipindi na makala maalum kuhusu afya, wanawake, jamii na maendeleo.

Habari za UN
27 OKTOBA 2025

Habari za UN

Play Episode Listen Later Oct 27, 2025 10:00


Hii leo jaridani tunaangazia machafuko ya muda mrefu nchini Myanmar, hali ya kibinadamu nchini Sudan kufuatia ripoti za vifo vya raia na wimbi la wakimbizi wa ndani, na masuala ya afya nchini Kenya.Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres, ametoa wito kwa dunia na mataifa wanachama wa Jumuiya ya Nchi za Kusini-Mashariki mwa Asia, ASEAN kuchukua hatua za haraka kumaliza machafuko ya muda mrefu nchini Myanmar, akisisitiza kuwa mgogoro huo si tishio kwa watu wa Myanmar pekee bali pia kwa amani na usalama wa kanda nzima ya Asia ya Kusini Mashariki.Ofisi ya Uratibu wa Misaada ya Kibinadamu ya Umoja wa Mataifa (OCHA) imeelezea wasiwasi mkubwa kufuatia ripoti za vifo vya raia na wimbi la wakimbizi wa ndani, kufuatia kuendelea kwa mapigano makali katika mji wa El Fasher, huko Darfur Kaskazini nchini Sudan. Tupate tarifa zaidi kutoka kwa Leah Mushi.Katika kaunti ya Mombasa nchini Kenya, Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) kwa kushirikiana na wa Mastercard Foundation na Serikali ya Kaunti ya Mombasa, imechukua hatua za kukabiliana na mlipuko wa MPOX kwa kutoa huduma muhimu za afya na WASH kwa wagonjwa na waliopona, ikiwa ni pamoja na vifaa vya kujikinga (PPEs), vituo vya kusafisha mikono na ujumbe wa mabadiliko ya tabia za kijamii.Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!

Shirin Safe 0500 UTC - Voice of America
Shirin Safe 0500 UTC (30:00) - Oktoba 27, 2025

Shirin Safe 0500 UTC - Voice of America

Play Episode Listen Later Oct 27, 2025 29:59


Kullum da karfe 6 na safe agogon Najeriya da Nijar muna gabatar da labarai da rahotanni da dumi-duminsu, sannan mu na gabatar da wasu shirye-shirye kamar Noma da Lafiya Uwar Jiki.

Alfajiri - Voice of America
Alfajiri - Oktoba 27, 2025

Alfajiri - Voice of America

Play Episode Listen Later Oct 27, 2025 29:59


Matangazo ya nusu saa kuhusu habari za mapema asubuhi pamoja na habari za michezo.

Jioni - Voice of America
Jioni - Oktoba 27, 2025

Jioni - Voice of America

Play Episode Listen Later Oct 27, 2025 29:59


Matangazo ya saa nzima kuhusu habari za kutwa, ikiwa ni pamoja ripoti kutoka kwa waandishi wetu sehemu mbali mbali duniani na kote Afrika Mashariki na Kati, na vile vile vipindi na makala maalum kuhusu afya, wanawake, jamii na maendeleo.

Shirin Safe 0500 UTC - Voice of America
Shirin Safe 0500 UTC (30:00) - Oktoba 26, 2025

Shirin Safe 0500 UTC - Voice of America

Play Episode Listen Later Oct 26, 2025 29:59


Kullum da karfe 6 na safe agogon Najeriya da Nijar muna gabatar da labarai da rahotanni da dumi-duminsu, sannan mu na gabatar da wasu shirye-shirye kamar Noma da Lafiya Uwar Jiki.

Jioni - Voice of America
Jioni - Oktoba 26, 2025

Jioni - Voice of America

Play Episode Listen Later Oct 26, 2025 29:59


Matangazo ya saa nzima kuhusu habari za kutwa, ikiwa ni pamoja ripoti kutoka kwa waandishi wetu sehemu mbali mbali duniani na kote Afrika Mashariki na Kati, na vile vile vipindi na makala maalum kuhusu afya, wanawake, jamii na maendeleo.

Shirin Safe 0500 UTC - Voice of America
Shirin Safe 0500 UTC (30:00) - Oktoba 25, 2025

Shirin Safe 0500 UTC - Voice of America

Play Episode Listen Later Oct 25, 2025 29:59


Kullum da karfe 6 na safe agogon Najeriya da Nijar muna gabatar da labarai da rahotanni da dumi-duminsu, sannan mu na gabatar da wasu shirye-shirye kamar Noma da Lafiya Uwar Jiki.

Jioni - Voice of America
Jioni - Oktoba 25, 2025

Jioni - Voice of America

Play Episode Listen Later Oct 25, 2025 29:59


Matangazo ya saa nzima kuhusu habari za kutwa, ikiwa ni pamoja ripoti kutoka kwa waandishi wetu sehemu mbali mbali duniani na kote Afrika Mashariki na Kati, na vile vile vipindi na makala maalum kuhusu afya, wanawake, jamii na maendeleo.

Habari za UN
24 OKTOBA 2025

Habari za UN

Play Episode Listen Later Oct 24, 2025 9:56


Hii leo jaridani tunaangazia siku ya Umoja wa Mataifa ikiwa ni miaka 80 tangu kuanzishwa kwake 1945.Leo ni siku ya Umoja wa Mataifa ni miaka 80 tangu kuanzishwa kwake 1945, lakini pia ni kumbukizi ya miaka 80 tangu kuanzishwa kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ambalo lilikuwa ni tukio la kihistoria na la kukumbukwa. Akiwahutubia wajumbe wa Baraza hilo kwa njia ya mtandao katika kikao cha kumbukizi hii, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres ametoa wito wa mageuzi ya dharura na mwamko mpya wa uwajibikaji, akiwakumbusha jukumu lao kuu la kulinda amani ya dunia.Tukiendelea na Siku ya Umoja wa Mataifa, ikitukumbusha kuanzishwa kwake tarehe 24 mwezi Oktoba mwaka 1945. Maudhui ya mwaka huu ni "Miaka 80 ya Umoja wa Mataifa: Kujenga Mustakabali Wetu kwa Pamoja - Ishara ya Matumaini kwa ushirikiano wa Kimataifa." Katika kumulika hili, Sabrina Saidi wa idhaa hii amezungumza na mwakilishi wa vijana pamoja na mmoja wa watumishi wa Umoja wa Mataifa kuhusu maadhimisho ya siku hii, huko jijini Dar es Salaam, nchini Tanzania.Msikilizaji, bila shaka umeyasikia mengi kuhusu Umoja wa Mataifa, lakini Umoja wa Mataifa ni nini hasa? Japo kwa ufupi, Anold Kayanda anakufahamisha akianza na historia.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!

Habari za UN
Siku ya UN ni ukumbusho wa wajibu wetu kuendelea maono ya shirika hilo

Habari za UN

Play Episode Listen Later Oct 24, 2025 2:10


Leo ni Siku ya Umoja wa Mataifa, ikitukumbusha kuanzishwa kwake tarehe 24 mwezi Oktoba mwaka 1945. Maudhui ya mwaka huu ni "Miaka 80 ya Umoja wa Mataifa: Kujenga Mustakabali Wetu kwa Pamoja - Ishara ya Matumaini kwa ushirikiano wa Kimataifa." Katika kumulika hili, Sabrina Saidi wa idhaa hii amezungumza na mwakilishi wa vijana pamoja na mmoja wa watumishi wa Umoja wa Mataifa kuhusu maadhimisho ya siku hii, huko jijini Dar es Salaam, nchini Tanzania. 

Shirin Safe 0500 UTC - Voice of America
Shirin Safe 0500 UTC (30:00) - Oktoba 24, 2025

Shirin Safe 0500 UTC - Voice of America

Play Episode Listen Later Oct 24, 2025 29:59


Kullum da karfe 6 na safe agogon Najeriya da Nijar muna gabatar da labarai da rahotanni da dumi-duminsu, sannan mu na gabatar da wasu shirye-shirye kamar Noma da Lafiya Uwar Jiki.

Alfajiri - Voice of America
Alfajiri - Oktoba 24, 2025

Alfajiri - Voice of America

Play Episode Listen Later Oct 24, 2025 29:59


Matangazo ya nusu saa kuhusu habari za mapema asubuhi pamoja na habari za michezo.

Habari za UN
23 OKTOBA 2025

Habari za UN

Play Episode Listen Later Oct 23, 2025 15:53


Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayoangazia siku ya Umoja wa Mataifa na tutasikia kutoka mashinani wananchi na asasi za kiraia zina yapi ya kusema kuhusu shirika hili kubwa na la kipekee linalounganisha nchi wanachama 193 duniani.Mashirika manne ya Umoja wa Mataifa lile la uhamiaji IOM, la kuhudumia wakimbizi UNHCR, la Kuhudumia watoto UNICEF na la mpango wa chakula duniani WFP leo yametoa wito wa dharura kwa dunia kuchukua hatua mara moja kukabiliana na janga la kibinadamu linaloongezeka nchini Sudan. Zaidi ya watu milioni 30 wanahitaji msaada, nchini humo wakiwemo watoto milioni 15 na wakimbizi karibu milioni moja.Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) jana Oktoba 22 ilisema Israeli lazima itimize majukumu yake kama “anayekalia kimabavu” kwa kuhakikisha kuwa msaada unaweza kupita bila vizuizi na kwa kuheshimu haki za Umoja wa Mataifa na mashirika mengine ya kibinadamu yanayofanya kazi katika Ardhi ya Palestina Iliyokaliwa kwa Mabavu. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres ameelezea maoni hayo ya ICJ kuwa “muhimu sana,” akiongeza kuwa yametolewa wakati ambapo Umoja wa Mataifa unafanya kila juhudi kuongeza kasi ya misaada kuingia Gaza baada ya kusitishwa kwa mapigano.Nchini Kenya, wahudumu wa afya waliokuwa wakisubiri hadi siku 15 kupata malipo sasa wanapokea pesa ndani ya saa 72 pekee, shukrani kwa mfumo mpya wa malipo ya kidijitali uliotolewa na Shirika la Sfya la Umoja wa Mataifa WHO na Wizara ya Afya ya nchi hiyo. Mfumo huu unapeleka fedha moja kwa moja kwenye pochi za simu za wafanyakazi, ukipunguza ucheleweshaji, gharama na kuongeza motisha. Wafanyakazi zaidi ya 120,000 sasa wanafaidika, kuboresha ufanisi wa kampeni za chanjo na juhudi za kudhibiti polio.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!

Shirin Safe 0500 UTC - Voice of America
Shirin Safe 0500 UTC (30:00) - Oktoba 23, 2025

Shirin Safe 0500 UTC - Voice of America

Play Episode Listen Later Oct 23, 2025 30:00


Kullum da karfe 6 na safe agogon Najeriya da Nijar muna gabatar da labarai da rahotanni da dumi-duminsu, sannan mu na gabatar da wasu shirye-shirye kamar Noma da Lafiya Uwar Jiki.

Alfajiri - Voice of America
Alfajiri - Oktoba 23, 2025

Alfajiri - Voice of America

Play Episode Listen Later Oct 23, 2025 30:00


Matangazo ya nusu saa kuhusu habari za mapema asubuhi pamoja na habari za michezo.

Habari za UN
22 OKTOBA 2025

Habari za UN

Play Episode Listen Later Oct 22, 2025 11:18


Hii leo jaridani tunaangazia mifumo ya tahadhari za mapema dhidi ya majanga, elimu kuhusu uraia nchini Sudan kusini, na kilimo endelevu na vijana nchini Rwanda.Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amesema mifumo ya tahadhari za mapema dhidi ya majanga si chaguo tena, bali ni lazima kwa kila mtu duniani, akisisitiza kuwa hatua hizo zinaokoa maisha na mali.Kuanzia furaha ya uhuru hadi maumivu ya kurejea kwa mzozo, safari ya amani ya kudumu Sudan Kusini imekuwa ndefu na bado inaendelea. Licha ya changamoto hizo, matumaini bado ni makubwa miongoni mwa jamii nchini kote kwamba uchaguzi wa amani, huru na wa haki utaleta usalama uliotafutwa kwa muda mrefu pamoja na fursa za maendeleo na ukuaji wa uchumi.Wanawake ni nguzo muhimu katika maendeleo ya kilimo na jamii za vijijini. Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Maendeleo ya Kilimo( IFAD) inahakikisha zaidi ya asilimia 50 ya washiriki wa miradi yake ni wanawake, kwa lengo la kuimarisha usawa wa kijinsia na kupunguza umaskini. Kupitia mafunzo, huduma za kifedha, na upatikanaji wa masoko, wanawake wanawezeshwa kiuchumi na kijamii. Tafiti zinaonesha kuwa kufuta pengo la kijinsia katika kilimo kunaweza kuongeza pato la dunia kwa asilimia 1. Nchini Rwanda, miradi kama R-YES imewezesha wanawake vijana kuanzisha biashara za kilimo na kutoa ajira.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!

Shirin Safe 0500 UTC - Voice of America
Shirin Safe 0500 UTC (30:00) - Oktoba 22, 2025

Shirin Safe 0500 UTC - Voice of America

Play Episode Listen Later Oct 22, 2025 29:59


Kullum da karfe 6 na safe agogon Najeriya da Nijar muna gabatar da labarai da rahotanni da dumi-duminsu, sannan mu na gabatar da wasu shirye-shirye kamar Noma da Lafiya Uwar Jiki.

Alfajiri - Voice of America
Alfajiri - Oktoba 22, 2025

Alfajiri - Voice of America

Play Episode Listen Later Oct 22, 2025 30:00


Matangazo ya nusu saa kuhusu habari za mapema asubuhi pamoja na habari za michezo.

Habari za UN
21 OKTOBA 2025

Habari za UN

Play Episode Listen Later Oct 21, 2025 13:03


Katika Jarida la Habari za Umoja wa Mataifa hii leo Leah Mushi anakuletea-Gaza Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula Duniani WFP lasema usitishaji wa mapigano umeleta afueni kwa wakaazi kwani sasa misaada inaendelea kuwafikia wenye uhitaji-Naibu Mratibu wa Misaada ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa Joyce Msuya amekuwa ziarani Jamhuri ya Afrika ya Kati CAR na kujionea hali halisi ya wakimbizi, wakimbizi wa ndani na msaada wa kibinadamu-Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa leo limesema katika tathimini yake kuwa ukataji wa misitu umepungua duniani kote ingawa bado kuna shinikizo na hatua zaidi zahitajika-Katika mada kwa kina tunakupeleka nchini Tanzania ambako Vyuo Vikuu vinachukua hatua ya kusongesha Malengo ya Maendeleo Endelevu, SDGs hususan lile namba 17 la ubia kupitia umataifishaji. -Na kwenye jifunze Kiswahili unapata ufafanuzi wa methali " “NG'OMBE WA MNYONGE HAZAI" 

Shirin Safe 0500 UTC - Voice of America
Shirin Safe 0500 UTC (30:00) - Oktoba 21, 2025

Shirin Safe 0500 UTC - Voice of America

Play Episode Listen Later Oct 21, 2025 29:59


Kullum da karfe 6 na safe agogon Najeriya da Nijar muna gabatar da labarai da rahotanni da dumi-duminsu, sannan mu na gabatar da wasu shirye-shirye kamar Noma da Lafiya Uwar Jiki.

Alfajiri - Voice of America
Alfajiri - Oktoba 21, 2025

Alfajiri - Voice of America

Play Episode Listen Later Oct 21, 2025 30:00


Matangazo ya nusu saa kuhusu habari za mapema asubuhi pamoja na habari za michezo.

Habari za UN
20 OKTOBA 2025

Habari za UN

Play Episode Listen Later Oct 20, 2025 9:59


Karibu kusikiliza jarida la habari za Umoja wa Mataifa, leo utasikia mengi ikiwemo mkutano wa kujadili kuhusu tahadhari za mapema unaoenda sambamba na miaka 75 tangu kuanzishwa kwa shirika la Umoja wa Mataifa la hali ya hewa WMO. Pia utasikia juhudi za mashirika ya UN kusaidia wananchi huko mashinani na kuboresha maisha yao. UNDP nchini Tanzania na UNMISS huko jimboni Yambui nchini Sudan Kusini. Mtangazaji wako ni Leah Mushi. 

Shirin Safe 0500 UTC - Voice of America
Shirin Safe 0500 UTC (30:00) - Oktoba 20, 2025

Shirin Safe 0500 UTC - Voice of America

Play Episode Listen Later Oct 20, 2025 29:59


Kullum da karfe 6 na safe agogon Najeriya da Nijar muna gabatar da labarai da rahotanni da dumi-duminsu, sannan mu na gabatar da wasu shirye-shirye kamar Noma da Lafiya Uwar Jiki.

Shirin Safe 0500 UTC - Voice of America
Shirin Safe 0500 UTC (30:00) - Oktoba 19, 2025

Shirin Safe 0500 UTC - Voice of America

Play Episode Listen Later Oct 19, 2025 29:59


Kullum da karfe 6 na safe agogon Najeriya da Nijar muna gabatar da labarai da rahotanni da dumi-duminsu, sannan mu na gabatar da wasu shirye-shirye kamar Noma da Lafiya Uwar Jiki.

Habari za UN
17 OKTOBA 2025

Habari za UN

Play Episode Listen Later Oct 17, 2025 10:25


Hii leo jaridani tunaangazia ripoti ya UNDP ya umaskini, mradi wa kusaidia jamii kupambana na athari za mabadiliko ya tabianchi nchini Zambia na juhudi za kuboresha hali ya lishe kwa watoto nchini Kenya.Takribani watu milioni 887 duniani ambao ni maskini wanaishi kwenye maeneo yanayokumbwa moja kwa moja na madhara manne yasababishwayo na mabadiliko ya tabianchi ambayo ni joto kali, mafuriko, ukame na uchafuzi wa hewa, imesema ripoti mpya iliyotolewa leo na shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo, UNDP kwa kushirikiana na wadau. Ripoti inaonesha bayana kuwa hali hiyo inazidi kutwamisha watu hao kwenye hali tete zaidi.Mradi wa kusaidia jamii kupambana na athari za mabadiliko ya tabianchi nchini Zambia mbali na kusaidia wananchi kwenye kilimo pia umewawezesha kiuchumi na kuwaondoa baadhi yao kwenye mstari wa umasikini. Mmoja wa walio utupa mkono umasikini ni Judith Mabeta aliyetoka kuishi nyumba ya udongo mpaka kuwa na nyumba ya kupangisha na sasa ni mama mwenye nyumba.Kupitia  msaada wa fedha kutoka Ufaransa, juhudi za kuboresha hali ya lishe kwa watoto nchini Kenya, hasa kwa jamii zilizo katika mazingira hatarishi zinaendelea ambapo juhudi za hivi karibuni ni kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) kwa kushirikiana na Shirika la Msalaba Mwekundu la Kenya ambao kwa pamoja wameimarisha huduma hizo kwa manusura wa mafuriko Magharibi mwa taifa hilo la Afrika Mashariki. Huduma hizi ni sehemu muhimu ya kuhakikisha watoto na familia wanapata vyakula vyenye virutubishi kwa ustawi wa maisha yao.Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!

Habari za UN
16 OKTOBA 2025

Habari za UN

Play Episode Listen Later Oct 16, 2025 13:01


Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayoangazia siku ya chakula duniani ikienda sambamba na maadhimisho ya miaka 80 ya kuanzishwa shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo, FAO, na utamsikia Mwakilishi wa FAO nchini Tanzania Bi. Nyabenyi Tito Tipo akieleza.Maadhimisho ya siku ya chakula duniani yamefanyika kimataifa leo huko Roma nchini Italia, yakienda sambamba na sikukuu ya miaka 80 tangu kuanzishwa kwa Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na kilimo, FAO. Katika ujumbe wake alioutoa kwa njia ya video Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amesema, “Miaka themanini iliyopita, katika dunia iliyosambaratishwa kwa vita, nchi zilikutana kukabiliana na njaa. Miongo kadhaa tangu wakati huo, dunia imepiga hatua kubwa. Lakini bado majanga yanyoonesha kuwa hatuwezi kubweteka iwapo tunataka kuendeleza mafanikio tuliyopata. Tuna mbinu, ufahamu, rasilimali za kutokomeza njaa, na kupatia kila mtu chakula kizuri na chenye afya. Tunachohitaji ni umoja.Huko Gaza, eneo la Palestina linalokaliwa na Israeli, raia wamerejea kufuatia makubaliano ya sitisho la mapigano lakini wanahaha kujenga upya makazi yao huku wakiwa wamezingirwa na vifusi. Miongoni mwao Ayman Awadallah, amesema “hakuna maji, hakuna miundombinu ya majitaka, hakuna maisha hapa, hakuna chochote.”Na kufuatia kifo cha aliyewahi kuwa Waziri Mkuu wa Kenya Raila Odinga, kilichotokea Jumatano Oktoba 15 nchini India, Umoja wa Mataifa kupitia Katibu Mkuu umetuma salamu za rambirambi na kusema hayati Odinga, alikuwa mtu muhimu katika maendeleo ya kidemokrasia nchini Kenya na  pia mtetezi thabiti wa mageuzi ya kikatiba na utawala jumuishi.Na katika kujifunza Kiswahili hii leo, mtaalam wetu Onni Sigalla, Mhariri mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania, BAKITA anafafanua maana za neno "KIMWA"Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!

Habari za UN
15 OKTOBA 2025

Habari za UN

Play Episode Listen Later Oct 15, 2025 10:47


Hii leo jaridani tunaangazia kiwango cha gesi ya hewa ukaa, yaani carbon dioxide au CO₂, siku ya Kimataifa ya Wanawake wa Vijijini inayotupeleka nchini Kenya kumulika juhudi za wanawake za kumudu mahitaji ya familia zao, na uvuvi na uhalifu katika Ziwa Victoria.Ripoti mpya ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Hali ya Hewa Duniani, WMO, inasema kiwango cha gesi ya hewa ukaa, yaani carbon dioxide au CO₂, kimeongezeka kwa kiwango cha kuvunja rekodi mwaka 2024, na kufikia viwango vipya vya juu zaidi kuwahi kurekodiwa.Kuanzia Oktoba 15 mwaka 2008 dunia imekuwa ikiadhimisha siku ya Kimataifa ya Wanawake wa Vijijini kama fursa ya kutambua mchango mkubwa wa wanawake hawa katika maendeleo ya kijamii, kiuchumi, na kimazingira.Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji IOM kwa kushirikiana na Ofisi ya Marekani ya Masuala ya Kimataifa ya kupambana na Dawa za Kulevya na Utekelezaji wa Sheria (INL), na mamlaka kutoka Kenya, Tanzania na Uganda wanashirikiana kuimarisha uwezo na kukabiliana na uhalifu wa kimataifa unaotekelezwa katika ziwa victoria ambao ukiachwa unaweza kuleta athari kwa zaidi ya watu milioni 40 wanaotegemea ziwa hilo.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!