Uchumi na Biashara

Follow Uchumi na Biashara
Share on
Copy link to clipboard

Inahusu masuala ya ujasiriamali, biashara ndogo ndogo, ushauri kuhusu uwekezaji na shughuli nyinginezo za kiuchumi.

Standard Media


    • Dec 11, 2022 LATEST EPISODE
    • every other week NEW EPISODES
    • 12m AVG DURATION
    • 59 EPISODES


    Search for episodes from Uchumi na Biashara with a specific topic:

    Latest episodes from Uchumi na Biashara

    Mbona Magari ya Umeme? | Uchumi na Biashara Podcast

    Play Episode Listen Later Dec 11, 2022 14:35


    Baadhi ya kampuni za uagizaji na uuzaji wa magari nchini zimebadili mwelekeo na sasa zinajitosa katika uagizaji wa magari yanayotumia umeme. Kampuni ya hivi punde kufanya hivyo ni ya BasiGo na ya kwanza kuagiza mabasi 15 ya umeme ambayo yalitengenezwa na Kampuni ya BYD Automotive iliyo nchini Uchina. Mabasi haya tayari yamewasili nchini kupitia Bandari ya Mombasa na yanatarajiwa kutoa huduma za uchukuzi jijini Nairobi. Lakini je, mbona wafanyabiashara waanze kufuata muelekeo wa uagizaji wa magari ya umeme? Robert Menza amewahoji baadhi ya washikadau katika sekta hiyo

    Kuvuma kwa Utalii Krisimasi na Mwaka Mpya | Uchumi na Biashara Podcast

    Play Episode Listen Later Nov 25, 2022 21:59


    Huku msimu wa Krimasi na Mwaka Mpya ukikaribia Sekta ya Utalii inategemea sana msimu huu kuimarika kutokana na watalii wa mataifa ya kigeni wanaolenga kuzuru maeneo mbalimbali ya kitalii nchini. Mojawapo ya maeneo hayo ni eneo la Pwani hususani Kaunti ya Mombasa. Je, wafanyabiashara hasa wa hoteli za kitalii wamejiandaa vipi msimu huu? Robert Menza amezungumza na Josephat Iha ambaye ni Meneja wa Mauzo katika Mkahawa wa Massai Beach.

    Serikali saidia, biashara zetu zazorota | Uchumi na Biashara Podcast

    Play Episode Listen Later Oct 29, 2022 14:46


    Licha ya serkali kuahidi kushughulikia changamoto za wafanyabiashara wadogo wadogo, bado mahangaiko yanashuhudiwa mwezi mmoja baada ya Kenya Kwanza kuchukua hatamu za uongozi. Wengi wa wafanyabiashara hao wanalalamikia kuongezwa kwa bei ya mafuta, na kusababisha hasara katika sekta ya matatu. Charles Macharia, mhudumu wa teksi na Jimmy Mwangi, mhudumu wa matatu wanatishia kugura biashara hii. Mwanahabari wetu Edwin Mbugua amefanya mazungumzo na baadhi ya wafanyabiashara hao katika Kaunti ya Nyeri.

    Nyumba za Bei Nafuu | Uchumi na Biashara Podcast

    Play Episode Listen Later Oct 25, 2022 18:04


    Washikadau mbalimbali wanaunga mkono mpango wa ujenzi wa nyumba kwa bei nafuu unaoendelezwa na serikali, mfano mradi wa Buxton Point katika Kaunti ya Mombasa unaoendelezwa na mfanyabiashara, Suleiman Shahbal na Serikali ya Kaunti ya Mombasa. Robert Menza amezungumza na Martin Kariuki, anayesimamia uuzaji wa nyumba hizo.

    Uzalishaji wa mayai | Uchumi na Biashara Podcast

    Play Episode Listen Later Oct 24, 2022 10:14


    Licha ya Shirika la Afya Dunia, WHO kushauri kuwa binadamu anafaa kula mayai 180 kwa mwaka, imebainika kwamba taifa la Kenya halijaafikia kiasi hicho takwimu zikionesha kuwa mayai 36 tu huliwa kwa wastani kulinganishwa na mataifa mengine mfano taifa jirani la Uganda na Afrika Mashariki. Hali hii imesababishwa na Wakenya kuzalisha mayai kwa wingi kwa minajili ya kufanya biashara ikilinganishwa na Uganda ambapo huzalishwa vijijini. Mwanahabari wetu Martin Ndiema amesema na wafanyabiashara wa mayai kubaini jinsi uzalishaji na ulaji huathiri biashara yao.

    GMO na hofu kuhusu bei masokoni | Uchumi na Biashara Podcast

    Play Episode Listen Later Oct 11, 2022 8:33


    Katika Makala Uchumi na Biashara Podcast, mwanahabari wetu wa Kaunti ya Trans Nzoia, Martin Ndiema amesema na wakulima ili kubaini ikiwa wameridhia kupanda mimea iliyoboreshwa kwa njia ya kijenetiki yaani GMO. Wapo ambao wamekumbatia na wengine kuirai serikali kuutafakari upya kuhusu uamuzi huo wa Baraza la Mawaziri wa kupitisha GMO. Aidha, amesema na mtaalamu wa mimea akizamia ubora wa mazao ya mimea ya GMO, soko la kimataifa na usalama wa chakula kwa matumizi ya binadamu.

    Sarafu ya pamoja na boda huru Barani Afrika

    Play Episode Listen Later Sep 20, 2022 8:15


    Leo kwenye Makala Uchumi na Biashara mwanahabari wetu wa Kaunti ya Trans Nzoia, Martin Ndiema anaangazia juhudi zinazowekwa na viongozi wa matabaka mbalimbali Barani Afrika kufanikisha kuwapo kwa sarafu moja inayopendekezwa kuitwa AFRO. Aidha amezamia suala la kuafikia boda huru kustawisha uchumi wa bara hili.

    Uchumi na Biashara Podcast; Kenya haina deni la shilingi trilioni 8.47, asema Jimmy Wanjigi

    Play Episode Listen Later Jul 29, 2022 6:30


    Mfanyabiashara Jimmy Wanjigi sasa anapinga kwamba taifa lina deni la shilingi trilioni 8.47 jinsi ilivyochapishwa na Benki Kuu-CBK. Kulingana na Wanjigi, deni ni chini ya trilioni 3. Pia amedai fedha za mikopo ya ndani kwa ndani-domestic debts hazikutumika katika miradi ya serikali badala yake kuibwa.

    Uchumi na Biashara Podcast: Bei ya unga - hatupunguzi ng'o!

    Play Episode Listen Later Jul 21, 2022 4:18


    Wasaga-nafaka mjini Kitale, Kaunti ya Trans Nzoia wanasema hawatakubali kuuza unga wa pakiti ya kilo 2 kwa shilingi 100 hadi serikali itakapowafidia. Mmoja wao kwa jina Robert Wanyonyi anasema kufikia sasa hakuna mikakati iliyowekwa kuhusu jinsi watakavyofidiwa na serikali. Anasema mkutano wa Jumatano katika Ikulu ulihudhuriwa na wachache, wengi wao wakiachwa nje. Hata hivyo, amekiri kwamba wateja wamekosa kununua unga wakishinikiza kuuziwa kwa shilingi 100. Katika mahojiano na Martin Ndiema, Wanyonyi anasema huenda wasaga-nafaka wakatapa hasara iwapo hawatafidiwa. Wakenya nao wanaipongeza serikali kwa kupunguza bei ya unga wa mahindi.

    Uchumi na Biashara Podcast; Wabunge ni wasaliti-deni kila siku

    Play Episode Listen Later Jul 1, 2022 14:29


    Wakenya wameendelea kulalamikia kupanda kwa gharama ya maisha, serikali nayo ikizidisha deni hadi trilioni 10 sasa. Aidha, wabunge na maseneta wamelaumiwa kwa kupitisha pendekezo la kuongeza deni la taifa kutoka shilingi trilioni 9, hadi 10 hali inayochangia kupanda kwa bei za bidhaa. Mike Ekutan ametangamana na Wakenya mjini Lodwar, Kaunti ya Turkana.

    Uchumi na Biashara Podcast; Bidhaa ghali, pigo kwa uuzaji chakula

    Play Episode Listen Later Jun 23, 2022 21:57


    Bi. Mwansa, mwanamke mwenye umri wa miaka 70 amekuwa akijihusisha na upishi wa vyakula mbalimbali ambavyo huviuza kwa wateja kila siku, biashara ambayo ameifanya kwa zaidi ya miaka arubaini sasa. Biashara hii aliitegemea sana kuyakidhi mahitaji yake pamoja na wanawe kukiwamo kugharimia karo ya ya wanawe. Mwanamke huyu ambaye ni mkazi wa Majengo, Mvita katika Kaunti ya Mombasa anajihuisha na upishi wa chapati na maharagwe ya nazi. Vyakula vingine ambavyo pia Bi. Mwansa hupika ni mikate ya sinia na mitai. Kupanda kwa gharama ya bidhaa za upishi ukiwamo ya unga wa ngano, mafuta ya kupikia miongoni mwa bidhaa nyingine ambapo huzitumia kwa upishi kumemwathiri sana. Mwanahabari wetu wa Mombasa Robert Menza amezungumza naye katika Uchumi na Biashara Podcast

    Uchumi na Biashara Pocast: Gharama ya maisha; bidhaa bei ghali

    Play Episode Listen Later Jun 17, 2022 11:16


    Wakenya wanaendelea kulalamikia ongezeko la bei za bidhaa ya kimsingi na kupanda kwa gharama ya maisha. Wengi wameamua kupunguza matumizi ya fedha kukiwamo kutembea badala ya kutumia magari au bodaboda na kula chakula mara moja kwa siku. Martin Ndiema amesema na Wakenya mjini Kitale.

    Madharau kazini yanavunja moyo

    Play Episode Listen Later May 13, 2022 9:03


    Vincent Oduor akumbuka jinsi alivyoathiriwa na ghasia za baada ya uchaguzi, kazi yake ya ushonaji kutumia cherahani ikiathirika pakubwa. Anakumbukwa jinsi mashine za ushonaji zilivyoibwa wakati wa ghasia hizo. Kwa sasa kazi yake inanawiri na anapata faida

    Uchumi umeimarika kwa asilimia 7.5, nani amefaidika?

    Play Episode Listen Later May 6, 2022 3:52


    Uchumi wa Kenya uliimarika mwaka wa 2021 baada ya kuathirika kufuatia Janga la Korona mwaka wa 2020. Kwa mujibu wa ripoti ya Taasisi ya Takwimu, KNBS uchumi ulikua kwa asilimia 7.5, kiwango hiki kikitajwa kuwa cha juu zaidi baada ya kipindi cha miaka kumi na mmoja. Aidha, nafasi 923,100 za kazi zilibuniwa katika mwaka huo wa 2021, wageni waliokuja nchini wakiongezeka hadi 871,300. Esther Kirong ametupambia makala haya.

    Kiwango cha chini cha nyongeza ya mshahara: Uhuru

    Play Episode Listen Later May 2, 2022 7:44


    Je, tangazo la Rais Kenyatta kuhusu asimilia 12 ya nyongeza ya mshahara wa chini kwa wafanyakazi, linamaanisha nini? Na je, ni wafanyakazi gani hasa watakanufaika kutokana na agizo hili ambalo limetakiwa kutekelezwa kuanzi mwezi huu? Jinsi anavyoarifu Victor Mulama, ni wafanyakazi wa viwango vya chini pekee ndio watakaoathirika, na licha ya hayo nyongeza ya mshahara itatozwa kodi.

    Uchumi na Biashara Podcast: Makazi bora; ushirikiano mwema na serikali

    Play Episode Listen Later Mar 31, 2022 14:54


    Serikali ikijizatiti kufanikisha mpango wa ujenzi wa nyumba za bei nafuu kwa Wakenya, Kampuni ya ABC Homes vilevile imeweka mikakati kuhakikisha mpango huo unafaulu. Mhandisi Eveline Muringa ambaye ni Meneja wa Mradi wa ujenzi wa nyumba hizo anasema kwamba lengo lao hasa ni kuhakikisha Wakenya wengi wanamiliki nyumba kwa gharama ya chini. Robert Menza amezungumza naye.

    Wanabodaboda wakerwa na polisi wanaoitisha hongo

    Play Episode Listen Later Mar 19, 2022 7:37


    Leo katika kitengo hiki tunaandazia mahangaiko ya waendeshaji pikipiki kufuatia msako katika harakati za kuinadhifisha sekta ya bodaboda. Msako huo ambao hata hivyo ulisitishwa kuruhusu mazungumzo, umesababisha madhara wahudumu hao wanaokiri ndoa zao zinayumba, wake zao wakiwatoroka kwa kutokuwa na fedha. Mwanahabari wetu wa Kaunti ya Trans Nzoia , Martin Ndiema ametangamana na baadhi yao na kufanya mahojiano nao.

    Uchumi na Biashara Podcast; Bei ghali ya mbolea na pembejeo nyinginezo

    Play Episode Listen Later Mar 19, 2022 11:23


    Wakenya kwenye maeneo yanayoendeshwa kilimo msimu huu wanalalamikia kupanda kwa bei ya mbolea kwa zaidi ya asilimia hamsini, huku mbolea gunia moja ya kilo hamsini ikiuzwa kwa shilingi elfu sita na hata elfu saba mia saba katika baadhi ya maduka. Wakulima wanadai kuwa bei ya mbolea ni ya juu sana ikilinganishwa na bei ya mahindi gunia moja la kilo tisini hivyo kupandisha maradufu gharama ya uzalishaji. Aidha, kuna wale ambao tayari wanasema kuwa hawataweza kupanda mahindi msimu huu kutokana na kupanda kwa gharama ya uzalishaji. Tumezungumza na mkulima Samuel Lelei Karuma.

    Uchumi na Biashara Podcast; Kilio cha wanabodaboda kwa Rais Kenyatta

    Play Episode Listen Later Mar 12, 2022 10:17


    Wahudumu wa bodaboda wamewalaumu polisi kwa kuwahangaisha wakitekeleza agizo la Rais kunadhifisha sekta hiyo. Kulingana Wycliffe Nyanamba, Mwenyekiti wa Wanabodaboda hapa jijini Nairobi, polisi wanawahangaisha hadi kwenye makazi yao wakiendesha msako huo wengine wakiwapunja pesa. Hata hivyo, Nyanamba amewalaumu baadhi ya wahudumu hao kwa kukiuka sheria za trafiki. Msako huu unafuatia kisa ambapo wanabodaboda wa Forest Road walimvamia na kumdhulumu kimapenzi mwanamke mmoja. Kauli yake inajiri wakati ambapo oparesheni hiyo imesitishwa kwa muda kupisha mazungumzo.

    Uchumi na Biashara Podcast: Korona yaathiri biashara ya magari

    Play Episode Listen Later Mar 12, 2022 17:15


    Patrick Wachira, mfanyabiashara wa kuyauza magari anasema amefanya biashara hiyo kwa zaidi ya miaka sita ila korona ilimsababishia hasara ya mamilioni ya fedha. Kwa mujibu wa Wachira, biashara ya magari ni bahati nasibu kwani huwezi kujua idadi ya magari utakayouza kwa mwezi au wiki. Aidha, Wachiri amesema Wakenya hawajakumbatia magari ya umeme kikamilifu. Robert Menza amezungumza naye.

    Uchumi na Biashara Podcast; Biashara ufuoni, mapato tosha kwa vijana

    Play Episode Listen Later Mar 3, 2022 12:15


    Biashara za ufuoni katika Kaunti ya Kilifi zimesadia vijana wengi kujimudu kimaisha na kuacha uraibu wa mihadarati. Gibson Kombe ni baharia na mwanzilishi wa fuo moja maarufu[vidazini beach, Kilifi ambaye amefungua biashara mbalimbali katika fuo hiyo na pia kuwaajiri vijana wengi na kuwawezesha kuanza kujimudu kimaisha kwa zaidi ya miaka kumi sasa. Mwanahabari wetu Marion Kithi anatupambia sehemu hii.

    Uchumi na Biashara Podcast: Wauza-bidhaa katika hafla za kisiasa

    Play Episode Listen Later Feb 17, 2022 14:31


    Wanasiasa wakiendeleza mikutano katika kaunti mbalimbali nchini, ni afueni kwa wafanyabiashara ambao biashara zao zilikuwa zimeathirika kutokana na Covid-19. Wengi wa wafanyabiashara hunufaika pakubwa na mikutano ya kisiasa kwa kuuza bidhaa zao katika majukwaa hayo. Katika Kaunti ya Pokot Magharibi, wanasiasa wameendelea kuziinua biashara kwa kuwanunulia wafuasi wao bidhaa mbalimbali. Moses Kiraese amefanya mazungumzo na wafanyabiashara mjini Kapenguria

    Uchumi na Biashara Podcast; Mapato ya ushonaji nguo yashinda mshahara wa Dubai

    Play Episode Listen Later Feb 3, 2022 10:21


    Mama Esther anavyotambulika na wateja wake ,ni mama wa watoto watano na amekuwa akifanya kazi ya cherehani kwa miaka minane. Kazi hii inampa mapato tosha kwani amewasomesha nduguze na kumjengea mamaye nyumba. Hata hivyo, janga la korona limetikisa biashara yake kwani wateja wamepungua. Mwanahabari wetu Marion Kithi amemtembelea na kuzungumza naye kuhusu biashara yake.

    Uchumi na Biashara Podcast; Korona ilinipokonya ajira, sasa nauza mboga Nyamira

    Play Episode Listen Later Jan 27, 2022 14:12


    Chris Agata, ana shahada katika Taaluma ya Uhasibu. Licha ya kukamilisha masomo na kuhitimu, Agata ni mfanyabiashara wa mboga, anazotoa shambani mwake. Alifutwa kazi kutokana na janga la korona, hivyo kumlazimu kuzamia biashara ili kujikimu maishani. Anasema biashara yake inaendelea kukua, hivyo amekumbatia mfumo wa kujiajiri. Agata amezungumza na mwanahabari wetu, William Omasire.

    Uchumi na Biashara Podcast; Usidharau Mutura, inanipa mapato tosha

    Play Episode Listen Later Jan 20, 2022 7:21


    Mutura ni mojawapo ya kitoweo kinachopendwa na wengi, mutura huuzwa nyakati za jioni jioni, wateja wakisema utamu wake ni giza, vumbi na kutojua unakula nyama ya nini hasa. Mutura ni mchanganyiko wa vipande vipande vya nyama, wenyewe huita sausage ya watu wa kawaida. Caleb Kimtai, mfanyabiashara mjini Makutano Kaunti ya Pokot Magharibi amezungumza na mwanahabari wetu Moses Kiraese na anakiri kuwa japo baadhi hudharau mutura, anajua siri ni nini kwani kupitia mutura, anakimu familia yake na pia ametekeleza miradi mbalimbali nyumbani kwao

    Uchumi na Biashara Podcast: Utalii Pwani wanoga Krisimasi na Mwaka Mpya

    Play Episode Listen Later Dec 23, 2021 17:14


    Licha ya athari za janga la korona, sekta ya utalii inazidi kunawiri msimu huu wa Krisimasi na Mwaka Mpya kulinganishwa na mwaka jana. Ilivyo sasa hoteli nyingi zimeandikisha takriban asimilia tisini ya wageni. Asilimia kubwa ni watalii wa humu nchini. Maeneo mengine pia ya kitalii yamenakili idadi ya juu ya wageni ambao wameyazuru na wengine ambao pia wananuia kuyazuru. Mwanahabari wetu, Robert Menza amezungumza na Mwenyekiti wa Chama cha Kitaifa cha Sekta ya Watalii wa humu nchini, Dkt. Tuqa Jirmo.

    Uchumi na Biashara Podcast; Biashara ya maji imeninunulia ploti na nyumba

    Play Episode Listen Later Dec 16, 2021 14:09


    Maji ni uhai, ni hitaji la kila mtu. Hapa jijini Nairobi, kuna wakati watu hawana maji katika nyumba zao, na ndipo Justus Ambani sawa na wengine wengi, hujihusisha na kazi ya kuuza maji kutumia mkokoteni. Ambani anayeendesha shughuli hii katika mitaa ya Fedha na Tassia Embakasi Mashariki, anasema kupitia biashara hii amenunua kipande cha ardhi vilevile nyumba. Esther Kirong' amemhoji katika makala ya leo ambapo anasema aliacha kazi ya kuajiriwa kisha kujiajiri. Ameweza kuwaajiri wengine wakiwamo vijana.

    Uchumi na Biashara Podcast: Krismasi ya taabu; bidhaa ghali, maisha magumu

    Play Episode Listen Later Dec 9, 2021 7:56


    Msimu wa Krismasi na mwaka mpya kwa kawaida huwa wenye shamrashamra. Watu wengi hununua vyakula, wengine nao husafiri kwenda kusherehekea pamoja na jamaa, ndugu na marafiki. Lakini msimu huu, huenda mambo yakawa tofauti kulinganishwa na miaka ya awali kutokana na kupanda kwa bei za bidhaa za msingi. Mwanahabari wetu, Martin Ndiema amezungumza na baadhi ya Wakenya kuhusu kupanda kwa bei za bidhaa na jinsi wanavyopanga kusherehekea msimu huu.

    Uchumi na Biashara Podcast; Biashara ya ndizi mbichi

    Play Episode Listen Later Dec 1, 2021 12:11


    Ndizi ni zao la biashara. Katika Kaunti za Kisii na Nyamira, karibu kila familia ina ndizi kwa ajili ya chakula na biashara. Kijijini Konate Nyamira, William Mose Gesora anajihusisha na biashara ya ndizi mbichi. Gesora anasema biashara hii imemsaidia si kupata mahitaji ya kimsingi tu bali hata kuwalipia wanawe karo. Gesora ambaye ana shamba ekari mbili la ndizi amezungumza na mwanahabari wetu William Omasire na anasema biashara yakupasa uwe wa kwanza kuwajibika ili kutojilaumu.

    Uchumi na Biashara Podcast; Kipato cha pombe ya mnazi, ila polisi wanasumbua

    Play Episode Listen Later Nov 24, 2021 9:21


    Pombe ya mnazi ni kinywaji cha kiasili kinachopendwa sana na ni maarufu zaidi kwenye maeneo ya Pwani na baadhi ya wenyeji wamekuwa wakitegemea pombe hiyo kibiashara. Jackline Kenga, mmoja wa wafanyabiashara wa pombe ya mnazi anasema licha ya kwamba biashara hiyo inamsaidia, anahangaishwa na polisi wanaoendesha oparesheni kila uchao. Hata hivyo, anasema kamwe hataasi biashara yenyewe kwani anapata mapato ya kutosha. Marioni Kithi amezungumza naye.

    Uchumi na Biashara Podcast; Nguo za Kimijikenda

    Play Episode Listen Later Nov 18, 2021 20:01


    Edna Dhababu mwenye umri wa miaka 27, mkazi wa Rabai katika Kaunti ya Kilifi ni mfanyabiashara anyejihusisha na uuzaji wa mavazi ya utamaduni wa Jamii ya Mijikenda. Si hilo tu, Dhahabu pia hukodisha mavazi hayo kwa wateja ambao huwa na hafla mbalimbali zikiwamo za ukumbusho wa kuzaliwa na harusi. Mwanahabari wetu Robert Menza ametangamana naye na kufanya mahojiano ya moja kwa moja.

    Uchumi na Biashara Podcast; Kuondolewa kwa Kafyu afueni katika biashara

    Play Episode Listen Later Nov 11, 2021 8:52


    Mwenyekiti wa Wafanyabiashara Wadogo-wadogo katika Soko la Kakamega, Harey Magero anasema kwamba tangu kuondolewa kwa marufuku ya kuwa nje, sekta ya biashara inazidi kunawiri. Magero amekiri kwamba sekta hiyo ilikuwa imeathirika pakubwa kutokana na janga la korona. Benard Lusigi amefanya mahojiano naye.

    Uchumi na Biashara Podcast; Uuzaji wa Samaki, kipato tosha

    Play Episode Listen Later Nov 4, 2021 28:05


    Nelson Babu ana taaluma ya uhasibu. Alifutwa kazi wakati korona iliporipotiwa nchini. Hata hivyo hakukata tamaa; amezamia biashara ya samaki mtaani Pipeline, Nairobi. Biashara yake licha ya kuanza ikiwa ndogo, amefanikiwa kufungua tawi jingine mtaani Umoja na anatazamia kufungua matawi zaidi, mbali na kuwapa vijana ajira. Esther Kirong' amezungumza naye

    Uchumi na Biashara Podcast: Mitumba imeniwezesha kununua mashamba

    Play Episode Listen Later Oct 28, 2021 7:27


    Peter Mureithi maarufu Boiyoo anauza long'i za mitumba mjini Kapenguria, Pokot Magharibi. Boiyoo ameuza nguo hizi kwa zaidi ya miaka thelathini. Anasema kazi hii imemsaidia kununua vipande kadhaa vya ardhi. Katika mazungumzo na mwanahabari wetu Moses Kiraese, anaelezea matumaini ya kufurahia matunda ya biashara yake hata atakapostaafu.

    Uchumi na Biashara Podcast; Biashara ya mitumba

    Play Episode Listen Later Oct 22, 2021 9:21


    Katika podcast hii tunaangazia panda-shuka za wafanyabiashara wa nguo za mitumba wakati huu wa janga la korona. Mmoja wa wafanyabiashara hao mjini Kitale kwa jina Andrew Chongo anayeuza suti za mitumba anasema kupigwa marufuku kwa uagizaji wa baadhi hizo kulisambaratisha biashara zao na hata wengine kulazimika kubadili biashara ili kuzikimu familia zao. Chogo anasema amri ya Rais Kenyatta ya kuondoa kafyu itastawisha uchumi wa taifa hili ikizingatiwa kwamba sasa wanaweza kusafiri ama kuagiza nguo kutoka mataifa mengine. Hata hivyo Chogo analipendekezea serikali kufufua na kuanzisha viwanda vya pamba na kuwawezesha wakulima kupanda mmea huo na kuwafuga kondoo aina ya merino ili kutoa ajira kwa vijana na kuwapiga jeki wakulima kiuchumi. Mwanahabari wetu wa Trans Nzoia, Martin Ndiema amemhoji mfanyabiasha huyo.

    Uchumi na Biashara Podcast; Biashara ya ngozi yaathirika Turkana

    Play Episode Listen Later Oct 14, 2021 22:22


    Wafanyabiashara wa ngozi katika Kaunti ya Turkana wanakadiria hasara kutokana na ukosefu wa karo baada ya soko na bei ya ngozi kusambaratika. Wakizungumza na mwanahabari wetu wa Turkana, Mike Ekutan wafanyabiashara hao wanalazimika kutupa ngozi za ng'ombe, kondoo na mbuzi kwa kukosa thamani. Hata hivyo, wanaowachinja punda wanapata faida kwani ngozi yake hununuliwa na kupelekwa Uchina.

    Uchumi na Biashara Podcast; COVI-19, pigo kwa sekta ya hoteli

    Play Episode Listen Later Oct 7, 2021 8:53


    Athari za virusi vya korona zinazidi kushuhudiwa katika sekta mbalimbali hasa zinazotegemewa na Wakenya, huku baadhi ya sekta hizo zikikadiria hasara kubwa au mapato ya chini ikilinganishwa na hapo awali. Mwanahabari wetu wa Kunti ya Taita Taveta, Rajab Kafuta amezuru baadhi ya hoteli za kitalii katika Mbuga ya Wanyamapori ya Tsavo, na kufanya mahojiano na Willie Mwadilo ambaye ni Meneja wa Hoteli za Taita Hills. Mwadilo ameweka wazi jinsi hali ilivyokuwa kabla ya taifa hili kukumbwa na korona na hali ilivyo kwa sasa ikizingatiwa maagizo yaliyowekwa na Wizara ya Afya kudhibiti virusi hivyo. Kuu linalojitokeza katika mahojiano haya ni kwamba sekta hiyo ingali inakadiria hasara ya mamilioni ya fedha na kuna haja ya masharti kulegezwa ili kuikwamua.

    Uchumi na Biashara Podcast; Bei za mafuta, pigo kwa sekta ya matatu

    Play Episode Listen Later Oct 1, 2021 19:54


    Anthony Ndirangu, Mwenyekiti wa Chama cha Ushirika cha Uchukuzi wa Umma la NYENA SACCO anaeleza masaibu wanayopitia kufuatia kupanda kwa bei za mafuta. Ndirangu anasema shirika hilo limekuwa likiandikisha hasara kubwa hasa baada ya mafuta kuongezwa bei licha ya kuwa limekuwa likipata hasara kutokana na athari za korona. Kwa mujibu wa Ndirangu, serikali inazidi kuikandamiza sekta ya uchukuzi. Mwanahabari wetu, John Mbuthia amezungumza naye ambapo anasimulia yanayowasibu kutokana na kupanda kwa bei za mafuta.

    Uchumi na Biashara Podcast: Mtumba Man; sarakasi za kuwavutia wateja

    Play Episode Listen Later Sep 22, 2021 11:21


    Steve Opondo, maarufu Mtumba Man kutoka Kaunti ya Kisumu ni mfanyabiashara aliyejipatia umaarufu kutokana na sarakasi zake wakati wa kuuza nguo za mitumba. Anasema aliamua kubuni njia ya kuwavutia wateja wake ambao wengi ni akina dada. Mtumba Man sasa ni jina kubwa; amepewa kandarasi ya miaka mitano katika duka la nguo la Devine Collections hapa jijini Nairobi. Maishani, anatazamia kuwa mfanyabiashara mkubwa. Mtumba Man amezungumza na mwanahabari wetu, Esther Kirong' katika podcast hii.

    Uchumi na Biashara Podcast: Kuuza Nyama; Maneno Matamu kwa Wateja

    Play Episode Listen Later Sep 16, 2021 22:28


    Moses Wafula, muuza-nyama mjini Kapenguria katika Kaunti ya Pokot Magharibi anasema biashara yake inanawiri kutokana na mazungumzo mazuri na wateja wake. Wafula anasema hoteli, shule na hata hospitali ni wateja wake wakuu. Hofu yake kuu ni kuharibika kwa nyama kwa kukosa friji. Pia anasema nyama ya ng'ombe wa gredi huharibika haraka kulinganishwa na wale wa kiasili. Wafula amezungumza na mwanahabari wetu Moses Kiraese katika podcast hii.

    UCHUMI NA BIASHARA PODCAST; Biashara ya mipakani; nchi na nchi

    Play Episode Listen Later Sep 5, 2021 20:29


    Kwa mujibu wa Mwanauchumi Ken Gichinga, usalama wa wafanyabiashara, uhusiano na mataifa mengine hasa mipakani iwapo soko linafunguliwa mpakani, usafi wa eneo, sheria za ulipaji kodi na zile za kudhibiti uingizaji wa bidhaa nchini ni mambo muhimu ya kuzingatiwa. Anasema Wakenya wamechangia kuzorota kwa uchumi kwani wengi huagiza bidhaa kwa bei rahisi kutoka mataifa jirani. Pia anapendekeza kubuniwa kwa sheria za kudhibiti uagizaji wa bidhaa zinazochangia kuharibika kwa soko la bidhaa za humu nchini. Mwanahabari wetu, Esther Kirong' amefanya mahojiano naye.​

    UCHUMI NA BIASHARA PODCAST; Ukopaji; nizingatie nini kabla kukopa?

    Play Episode Listen Later Aug 10, 2021 14:11


    Zipo sheria ambazo sharti zifuatwe kabla ya kuchukua mkopo katika taasisi zozote za fedha. Hata hivyo, programu-tumizi yaani Apps za kutoa mikopo mitandaoni zimechangia katika utepetevu miongoni mwa Wakenya ambao wengi huchukua mikopo bila kufuata sheria. Aidha, madai kwamba Naibu wa Rais, William Ruto aliipigia simu benki moja na mwekezaji wa Uturuki, Harrun Aydin akapewa mkopo wa shilingi bilioni 15 ni kinyume na sheria kwani mikopo haitolewi kwa kupiga simu. Mwanauchumi ambaye pia ni mshauri wa kifedha, Charles Karissa anasema yeyote hata awe wa ngazi gani ni sharti awe na mwamana, guarantor hivyo kupiga simu tu hakutoshi. Karissa amezungumza na mwanahabari wetu Esther Kirong'.

    UCHUMI NA BIASHARA PODCAST; Kodi ya Thamani ya Ziada (VAT), mzigo kwa mwananchi

    Play Episode Listen Later Jul 23, 2021 13:22


    Hatua ya Rais Uhuru Kenyatta kutia saini Mswada wa Fedha wa 2021 inazidi kuwakandamiza wananchi ambao wanalazimika kugharimia ada mpya ya asilimia 16. Aidha, wanawalaumu wabunge kwa kusalia kimya. Wanasema hali hii imechangia talaka katika familia, wanawake wakikosa kabisa kuelewa kuhusu kodi hiyo ya thamani. Pia wameghadhabishwa na jinsi serikali inavyopandisha bei ya mafuta huku ikishindwa kuchimba bidhaa hiyo katika eneo la Lokichar, Kaunti ya Turkana. Mwanahabari wetu Mike Ekutan amefanya mahojiano na wafanyabiashara, wahudumu wa bodaboda vilevile wasomi mjini Lodwar.

    UCHUMI NA BIASHARA PODCAST; Umuhimu wa wanawake katika ukuaji wa uchumi

    Play Episode Listen Later Jul 12, 2021 22:08


    Mkurugenzi wa Idara ya Baishara katika Benki ya Absa, Susan Situma amesema ili uchumi wa taifa uimarike, ni sharti wanawake wajumuishwe. Amekariri kwamba kuna haja ya serikali kuwashirikisha wajasiriamali wanawake ili pato la taifa likue. Kwa mujibu wa Situma, Benki ya Absa imezindua akaunti ya Absa She Account inayolenga kuhakikisha wafanyabiashara wadogo wadogo hususan wanawake wanapata fursa ya kuwekeza na kuomba mikopo hadi shilingi milioni kumi. Aidha, amewasihi wanawake na Wakenya kwa jumla kuchukua bima ya maisha ili kusaidika wanaposhindwa kulipia mikopo ya benki. Amesema wakati huu wa korona, wateja wengi wa Absa waliokuwa wamechukua mikopo walilipiwa na bima mbalimbali hasa baada ya biashara zao kuathirika. Situma amezungumza na mwanahabari wetu Esther Kirong' na anasema kando na Absa kuwawezesha wafanyabiasha, vilevile inawapa ushauri nasaha jinsi watakavyotumia fedha za mikopo vilevile kuwekeza.

    UCHUMI NA BIASHARA PODCAST; Mfumo wa mixed economy ni bora, sio 'bottom-up'

    Play Episode Listen Later Jul 4, 2021 14:56


    Mwanauchumi, Ken Gichinga anataja mifumo mbalimbali ya kuimarisha uchumi, akisema mfumo mzuri zaidi ni ule wa mchanganyiko yaani mixed economy model hasa ikizingatiwa taifa la Kenya linakua kiuchumi. Aidha, Gichinga anasema mfumo wa kuwainua wananchi wenye tabaka la chini kiuchumi; bottom - up economy ni bora iwapo siasa za nchi zitaimarishwa. Vilevile anaangazia mfumo wa trickle down economy ili kuhakikisha sekta ya kibiashara inakwamuliwa. Pia, Gichinga anasema Rais wa Marekani, Joe Biden sawa na Naibu wa Rais, William Ruto wanashabikia mfuko wa bottoms-up-economy. Gichinga amezungumza na mwanahabari wetu, Esther Kirong'​.

    UCHUMI NA BIASHARA PODCAST; Bandari ya Lamu, kitega-uchumi kwa Wapwani

    Play Episode Listen Later Jul 1, 2021 17:55


    Afisa wa Mamlaka ya Bandari ya Lamu, KPA Haji Mwasomo anasema bandari hiyo imechangia ukuaji wa uchumi kwa asilimia kubwa kwenye eneo zima la Pwani. Haji anasema mradi huo wa Lapset umeimarisha uhusiano wa kibiashara kati ya Kenya na mataifa mengine. Anasema serikali inajenga mabomba ya mafuta kutoka Lamu hadi Sudan Kusini hivyo kuimarisha biashara hata zaidi. Mwanahabari wetu wa Mombasa, Robert Menza amefanya mazungumzo na Haji kujua hali halisi ya bandari hiyo ya Lamu.

    UCHUMI NA BIASHARA PODCAST: KRA yapiga mnada magari na bidhaa nyingine Mombasa

    Play Episode Listen Later Jun 25, 2021 15:45


    Mamlaka ya Ukusanyaji Kodi, KRA jijini Mombasa imenadi magari na bidhaa nyingine ambazo hazikulipiwa ushuru na walioziagiza. Aidha, baadhi walishindwa kuwasilisha stakabadhi zinazofaa za uagizaji. Lengo la mnada huo ni kupunguza msongamano katika Bandari ya Mombasa. Shughuli hiyo iliipa KRA kati ya shilingi milioni 150-200. Mwanahabari wetu Robert Menza amezungumza na Wakenya waliofika bandarini humo kununua bidhaa hasa magari.

    UCHUMI NA BIASHARA PODCAST; Bajeti ya 2021/ 2022 ni mzigo kwa Mkenya

    Play Episode Listen Later Jun 15, 2021 16:21


    Bajeti ya shilingi trilioni 3.6 ni nzuri kwa mwonekano wa nje ila Wakenya watabebeshwa mzigo mkubwa zaidi wa kodi, amesema mwanauchumi Ken Gichinga. Aidha, anasema serikali ya Rais Uhuru Kenyatta imefeli kwani miradi inayotengewa fedha za mkopo inazidi kukwama. Vilevile anasema kuongezwa kwa matozo ya kodi kwa bidhaa mbalimbali ni pigo kwa mwananchi. Kulingana na Gichinga, matozo hayo hayatasaidia iwapo serikali itaendeleza hulka za kukopa. Anaishauri serikali kuweka mikakati ya kukabili wizi na utumiaji mbaya wa fedha za umma.​

    Uchumi na Biashara Podcast; App ya kuagiza bidhaa - Khetias

    Play Episode Listen Later Jun 10, 2021 12:53


    Dukakuu la Khetias limezindua App kwa jina CashBackApp ili kuimarisha huduma za mitandaoni kwa wateja wake. App hiyo itawawezesha wateja kuagiza bidhaa na kulipia kupitia mtandaoni. Pia inalenga kupunguza foleni ndefu vilevile msongamano wa watu wakati taifa linapokumbwa na janga la korona. Martin Ndiema amezungumza na Oscar Shivoga, mvumbuzi wa App hiyo.

    UCHUMI NA BIASHARA PODCAST: Hasara tele katika sekta ya matatu, kipindi cha Korona - Simon Kimutai

    Play Episode Listen Later Jun 5, 2021 14:05


    Mwenyekiti wa Muungano na Wamiliki wa Matatu Nchini, Simon Kimutai anasema sekta ya matatu imeathirika pakubwa kutokana na janga la korona. Aidha, ameiomba serikali kupunguza matozo ya kodi ili kuikwamua sekta hiyo kiuchumi. Kimutai amekariri kwamba Wakenya wanaotegemea uchukuzi wa umma wanakodolea macho janga kubwa zaidi kwani huenda sekta hiyo ikasambaratika katika siku zijazo. Amezungumza na Esther Kirong katika makala haya.

    UCHUMI NA BIASHARA PODCAST: Biashara ya mahindi - changamoto na faida zake

    Play Episode Listen Later May 26, 2021 9:50


    Biashara ya mahindi mwaka huu ni ngumu kulinganishwa na miaka iliyopita kutokana na bei duni. Aidha, Bodi ya Nafaka na Mazao, NCPB inafanya biashara na mawakala wanaowanyanyasa wakulima. Martin Ndiema amezungumza na Joseph Lamai, mkulima wa mahindi na mkazi wa Kaunti ya Trans Nzoia kuhusu suala hili.

    Claim Uchumi na Biashara

    In order to claim this podcast we'll send an email to with a verification link. Simply click the link and you will be able to edit tags, request a refresh, and other features to take control of your podcast page!

    Claim Cancel