POPULARITY
Jaridani leo jaridani tunaangazia hali ya kibinadamu katika ukanda wa Gaza, haki za binadamu nchini Sudan Kusini na ujumbe wa Katibu Mkuu kuhusu siku ya demokrasia duniani.Kamishina Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia wakimbizi wa Kipalestina UNRWA, Philippe Lazzarini, ametoa onyo kali kuwa “hakuna sehemu yoyote iliyo salama Gaza, na hakuna mtu aliye salama”akisema zahma na madhila yametanda kila kona ya eneo hilo linalokaliwa kimabavu na Israel.Leo ni siku ya demokrasia duniani ambapo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres, ameeleza bayana kuwa demokrasia iko hatarini duniani.Nchini Sudan Kusini ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo UNMISS unaendelea kuimarisha mfumo wa mahakama ili kuhakikisha haki inapatikana kwa wote hata maeneo yote ya nchi hiyo.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
Nchini Sudan Kusini ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo UNMISS unaendelea kuimarisha mfumo wa mahakama ili kuhakikisha haki inapatikana kwa wote hata maeneo yote ya nchi hiyo. Leah Mushi na taarifa zaidi
Karibu kusikiliza jarida la habari za Umoja wa Mataifa, hii leo utasikia juhudi zinazofanyika kusaidia wananchi walioathirika na tetemeko la ardhi nchini Afghanistan. Kutoka barani Afrika utasikia juhudi za kulinda raia wa Sudan Kusini wanaoathirika na vita vya wenyewe kwa wenyewe huko jimboni Tambura na kutoka nchini Tanzania utasikia msaada kwa wakimbizi walioko magharibi mwa taifa hilo.
Katika jitihada za kuimarisha amani na usalama katika maeneo yaliyoathiriwa na machafuko ya kikabila nchini Sudan Kusini, Umoja wa Mataifa kupitia Ujumbe wake wa amani nchini humo UNMISS wameendelea kuimarisha ulinzi na kuongeza doria za magari usiku na mchana huko Greater Tambura katika jimbo la Equatoria Magharibi.Sabrina Saidi anaangazia juhudi za UNMISS katika kuhakikisha hali ya usalama inarejea na wananchi waliokimbilia katika kambi za wakimbizi kusakama usalama wanarejea makwao.TAARIFA YA SABRINA SAIDI)NAT...Video ya UNMISS inaanza kwa kumulika doria zinazofanywa na walinda amani wa Umoja wa Mataifa huko katika kaunti ya Greater Tambura katika jimbo la Western Equatoria, kusini-magharibi mwa nchi ya Sudan Kusini karibu na mipaka ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo DRC na Jamuhuri ya Afrika ya Kati.Tangu mwaka 2021, mizozo ya wenyewe kwa wenyewe, umeendelea kugharimu maisha ya watu wengi na kuwalazimu maelfu kuyakimbia makazi yao.Wananchi waliokumbwa na hofu wamekuwa wakijificha vichakani, wengine wakikimbilia nchi jirani, huku wengi wakitafuta hifadhi katika kambi mbalimbali za wakimbizi wa ndani zilizopo maeneo ya karibu.Ili kuwalinda vyema raia UNMISS wameimarisha uwepo wao katika eneo hilo na kuongeza doria za magari usiku na mchana, wakipita katika barabara mbovu zilizotapakaa tope na kuharibiwa na mvua. Walinda amani hao maarufu kama 'Blue Helmets', wamekuwa wakitembelea kambi mbalimbali za wakimbizi wa ndani na kuzungumza na jamii mbalimbali za kikabila zilizopata hifadhi huko.Tereza Martin ni mmoja wa wakimbizi wa ndani aliyepata hifadhi na hapo, anazungumza kwa hofu na simanzi...CUT: Sauti ya Tereza Martin"Hatuelewi chanzo cha mzozo huu. Tumekuwa tukiishi katika kambi hii kwa takribani miaka sita, tukiishi kwa njaa na mateso. Makazi yetu ya muda ni mabovu. Msimu wa mvua umefanya hali kuwa mbaya zaidi, sasa tunalala juu ya maji ya mvua. Hatuwezi kwenda shambani kwa hofu ya kushambuliwa. Tunaomba serikali na wadau kutuangalia kwa jicho la huruma."NAT....Margret Dominic naye ni mkimbizi wa ndani kambini hapo, anasema doria hizi zinampa amani CUT: Sauti ya Margret Dominic-"Hatuwezi kutoka nje ya kambi. Tunaweza kulala kwa sababu wanapiga doria usiku. Kama wasingekuwepo, hatujui kama tungeweza hata kupata usingizi."Emmanuel Dukundane ni Afisa wa Masuala ya Kiraia wa UNMISS, anasema wanajenga kambi mpya katika maeneo ya kimkakati.CUT: Sauti ya Emmanuel DukundaneHili lina maana kubwa sana kwa sababu tuna rasilimali nyingi, na kwa kujiweka katika kambi hiyo mpya, tutaweza kufanya doria zaidi, kufanya mazungumzo zaidi, na kuwezesha mchakato wa upatanisho na amani kwa ujumla."Ingawa UNMISS itaendelea kuisaidia serikali ya Sudan Kusini katika kuwalinda raia wa Greater Tambura, amani ya kweli na upatanisho wa kudumu vinapaswa kukubaliwa na kupatikana kupitia juhudi za jamii husika na viongozi wao wenyewe.
Maelfu ya watu wameyakimbia makazi yao huko Tambura, jimbo la Equatoria Magharibi, tangu ghasia zilipozuka upya mwaka 2021 nchini Sudan Kusini. Hadi leo, wengi wao bado wanaishi kambini bila chakula cha uhakika, huduma za afya wala usalama huku wanawake na watoto wakibeba mzigo mkubwa zaidi wa mateso hayo. Kupitia video ya mpango wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo UNIMSS Flora Nducha anamulika kauli za baadhi ya wanawake waathirika wanaosihi katika kambi ya wakimbizi wa ndani.
Jaridani leo tunaangazia Majaribio ya Nyuklia, na machafuko nchini Sudan Kusini. Makala tunakwenda nchini Nepal na mashinani tunasalia huko huko Sudana Kusini, kulikoni?Dunia ikiadhimisha Siku ya Kimataifa yakupinga Majaribio ya Nyuklia, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres ametoa onyo kali kuhusu kuongezeka kwa hatari za nyuklia kufuatia mvutano wa kisiasa unaondelea duniani na amehimiza kuridhiwa kwa mkataba wa kupiga marufuku majaribio hayo ya kinyuklia.Maelfu ya watu wameyakimbia makazi yao huko Tambura, jimbo la Equatoria Magharibi, tangu ghasia zilipozuka upya mwaka 2021 nchini Sudan Kusini. Hadi leo, wengi wao bado wanaishi kambini bila chakula cha uhakika, huduma za afya wala usalama huku wanawake na watoto wakibeba mzigo mkubwa zaidi wa mateso hayo.Makala tunakwenda nchini Nepal kumulika suala la waume kwenda kusaka ajira nje ya nchi na kuacha wake zao wakihaha kukimu familia zao katika mazingira ambamo wanawake wanakuwa hawana uthabiti wa kiuchumi limeanza kupatiwa muarobaoni.Na katika mashinani fursa ni yake Anna Pita, Msimamizi wa hospitali ya Kator nchini Sudan Kusini akieleza ni kwa jinsi gani mifumo ya nishati ya jua iliyofadhiliwa na shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo, UNDP na wadau wake inabadilisha utoaji wa huduma katika hospitali na vituo vya afya nchini humo.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
Leo tumekuandalia mengi ikiwemo kubanduliwa kwa Kenya na Tanzania kwenye michuano ya CHAN katika hatua ya robo fainali, michuano ya basketboli ya Afrika ya wanaume imeingia hatua ya nusu fainali, shirikisho la soka nchini Sudan Kusini limetangaza tarehe mpya ya kuanza kwa msimu mpya wa ligi ya wanawake, Wan Bissaka ajumuishwa katika kikosi cha soka cha DRC, Mohammed Salah ashinda tuzo la mchezaji bora wa wachezaji kwa mara nyingine.
Leo tumekuandalia uchambuzi wa timu ambazo zimefuzu, gani zimeondolewa na nani wanaweza kufuzu hatua ya mtoano kwenye mashindano ya Chan, michuano ya baskeboli ya wanaume ya Afrika, viongozi wa mashabiki Sudan Kusini waandaa mechi ya kirafiki kuchangisha fedha za kusaidia watu wasiojiweza, rais wa AS Kigali aahidi kuongeza tuzo za ligi iwapo atachaguliwa kuwa rais wa shirikisho, Alcaraz afuzu robo fainali michuano ya Cincinnati Open.
Mahakama ya kuhamahama iliyopelekwa katika eneo la utawala la Greater Pibor, Kaunti ya Pibor jimboni Jonglei Mashariki mwa Sudan Kusini imeleta haki na amani kwa kiasi kikubwa katika eneo hilo. Anold Kayanda anatupasha kwa kina
Jaridani hii leo tunaangazia hakiza binadamu nchini Uganda, na mahakama ya kuhamama kwa ajili ya amani Sudan Kusini. Makala tunaangazia vijana na mpango wa wa kuwa wazazi siku zijazo, na mashinani tunakwenda nchini Kenya kumulika vijana wakulima.Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Binadamu, (OHCHR), imesema kitendo cha kiongozi wa upinzani nchini Uganda Kizza Besigye pamoja na mshirika wake Obeid Lutale kunyimwa dhamana mara kwa mara katika kesi inayowakabili ni jambo linalotia hofu kubwa. Assumpta Massoi na maelezo zaidi.Mahakama ya kuhamahama iliyopelekwa katika eneo la utawala la Greater Pibor, Kaunti ya Pibor jimboni Jonglei Mashariki mwa Sudan Kusini imeleta haki na amani kwa kiasi kikubwa katika eneo hilo.Makala wakati hapo jana dunia iliadhimisha siku ya kimataifa ya vijana duniani, shirika la Umoja wa Mataifa la afya ya uzazi na idadi ya watu UNFPA liliwahoji vijana iwapo wangependa kuwa na watoto hapo baadaye.Na katika mashinani fursa ni yake Emily, mwanachama wa kikundi cha vijana wakulima nchini Kenya wanaolima mbogamboga kupitia mradi uliofanikishwa na shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula WFP wa kilimo cha bustani.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
Miongoni mwa taarifa utakazoziskia ni pamoja na; sintofahamu yaendelea kuhusu kuanza kwa mazungumzo ya moja kwa moja kati ya Kinshasa na Muungano wa Vikosi vya Kidemokrasia vya Ukombozi wa Kongo AFC/M23, Rais wa DRC, Felix Tshisekedi amefanya mabadiliko katika baraza lake la mawaziri na kujumuisha upinzani. Tutakueleza punde zaidi katika uchaguzi wa Tanzania. Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Afrika Magharibi na eneo la Sahel, yasema hali ya usalama katika eneo hilo inasalia kuwa ya wasiwasi mkubwa na kimataifa Rais wa Marekani, Donald Trump, asema huenda hivi karibuni akakutana ana kwa ana na rais wa Urusi, Vladmir Putin, kuzungumzia mzozo wa Ukraine.
Hii leo jaridani tunaangazia hali ya msaada wa kibinadamu katika ukanda wa Gaza, na mlipuko wa kipindupingu nchini Sudan. Makala tunafuatilia ziara ya katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Kazakhstan na mashinani tunamulika unyonyeshaji Sudan Kusini.Simulizi za huzuni, majonzi na kukata tamaa zinaendelea kila uchao huko Ukanda wa Gaza, eneo la Palestina linalokaliwa kimabavu na Israel hasa wakati huu ambapo raia wanaokwenda kusaka chakula wanakumbwa na mashambulizi yanayosababisha vifo. Ijumaa iliyopita Umoja wa Mataifa uliripoti kuwa zaidi ya watu 100 waliuawa na mamia kadhaa walijeruhiwa katika siku mbili pekee Wakisaka chakula.Zaidi ya watoto 640,000 walio na umri wa chini ya miaka mitano wapo hatarini kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu huko Kaskazini mwa Darfur, nchini Sudan.. Katika makala Anold Kayanda anatupeleka Asia ya Kati ambako Umoja wa Mataifa na Kazakhstan wamesaini makubaliano ya Kazakhstan kuwa mwenyeji wa Kituo cha Kikanda cha Umoja wa Mataifa cha Malengo ya Maendeleo Endelevu kwa ajili ya ukanda wa Asia ya Kati na Afghanistan..Na mashinani nawapisha wanafunzi wawili,Wanga pamoja na Kifaya ambao ni wanafunzi katika shule ya Sekondari ya Askofu Abangite iliyopo jimbo la Yambio,kusini Magharibi mwa Sudani Kusini karibu na mpaka wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.Wakizungumza na shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia watoto UNICEF nchini humo wameeleza umuhimu wa maziwa ya mama kwa mtoto.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
Tunaendelea kuangazia michuano ya CHAN ambapo wenyeji Kenya na Tanzania wasajili ushindi mechi zao za kwanza, Sudan Kusini yabanduliwa kwenye hatua ya nusu fainali michuano ya basketboli ya kina dada ya Afrobasket, bondia Patrick Mukala wa DRC ndiye bingwa mpya wa Afrika uzani wa light heavyweight, Hojlund wa Man Utd awekewa dau la pauni milioni 30 kuuzwa, matokeo ya hatua ya tisa ya Tour du France na Formula One mkondo wa Hungarian Grand Prix
Hii leo jaridani Assumpta Massoi anamulika mauaji Ituri, DRC; Haki za binadamu hususan suala la Israeli kukalia Palestina kimabavu; Mifumo ya kuzalisha chakula; Mradi wa umwagiliaji kwa kutumia nishati ya sola huko Bidibidi, Uganda. MONUSCO, ambao ni Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa Kulinda Amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, imelaani vikali shambulio lililoanza usiku wa juzi tarehe 26 hadi jana 27 Julai 2025 huko Komanda eneo la Irumu, takribani kilomita 60 kusini-magharibi mwa Bunia mji mkuu wa jimbo la Ituri, mashariki mwa nchi. Anold Kayanda ameifuatilia taarifa hiyo na anatujuza zaidi.Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa haki za binadamu Volker Türk ameyahimiza mataifa yote ulimwenguni kuchukua hatua za haraka ili Israel ikomeshe uwepo wake kinyume cha sheria katika ardhi ya Palestina inayoikalia kimabavu, na kuhakikisha suluhu ya mataifa mawili inapatikana. Tupate taarifa zaidi kutoka kwa Leah MushiKatika makala Sabrina Said anakupeleka Addis Ababa nchini Ethiopia, kumulika mkutano wa Umoja wa Mataifa wa viongozi kuhusu mifumo ya uzalishaji chakula. Mkutano huu ni wa pili na unafanyika kwa siku tatu, leo ikiwa ni siku ya pili. Mashinani: Mary, Mkimbizi mwenye umri wa miaka 26 kutoka Sudan Kusini anayeishi katika makazi ya wakimbizi ya Bidibidi nchini Uganda. Yeye ni mkulima wa nyanya kutoka kikundi cha wakulima cha Anika ambao ni wanufaika wa mradi wa umwagiliaji wa Sola uliofanikishwa na shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula, WFP.
Jaridani leo tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini Tanzania kumulika SDG17 katika mazungumzo ya Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Benki ya CRDB, Tully Esther Mwambapa na idhaa hii hivi karibuni hapa New York. Pia tunakuletea mutasari wa habari na mashinani.Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa, Volker Türk, leo jijini Geneva Uswisi amekemea amri za hivi karibuni za Israel za kuwahamisha watu Gaza, zilizoambatana na mashambulizi makali katika eneo la kusini-magharibi mwa Deir El Balah na kwamba zimeongeza machungu zaidi kwa mateso ya Wapalestina wenye njaa.Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani, (WFP) limeeleza leo kuwa kutokana na upungufu wa ufadhili, mamilioni ya watu Sudna Kusini wako hatarini kukosa msaada wa chakula. Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa WFP ambaye pia ni Afisa Mkuu wa Uendeshaji, Carl Skau, ambaye hivi karibuni ametembelea Sudan Kusini anasema, "Kote Sudan Kusini, takriban watu milioni 8 wanakabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula, wengi wao wakitegemea msaada kutoka WFP ili kuendelea kuishi.Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Amina J. Mohammed, ametoa wito mzito wa kuchukua hatua za haraka na za kimfumo ili kuongeza kasi ya maendeleo barani Afrika. Ameyasema hayo wakati wa mkutano wa wadau uliofanyika jana Julai 21 katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa, New York, Marekani kujadili matokeo na mapendekezo ya ripoti ya hivi karibuni ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu utekelezaji wa ahadi za maendeleo ya Afrika.Na katika mashinani hii leo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ameweka bayana shuhuda za kuvutia na madhubuti juu ya kwa nini mapinduzi ya nishati mbadala hayaepukiki sasa, pamoja na manufaa yatakayotokana na mabadiliko ya haki kutoka nishati ya kisukuku kuelekea nishati salama. Ushahidi huo madhubuti ni pamoja na makao makuu ya Umoja wa Mataifa kutumia nishati ya sola na Guterres amefika kwenye eneo lenye paneli hizo.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayoturejesha katika mkutano wa 69 wa kamisheni ya hali ya wanawake duniani CSW69 kumsikia Mkurugenzi wa TEN/MET Nasra Kibukila kuhusu jitihada zao za kuhakikisha watoto wote wa Kitanzania wanapata elimu bora, jumuishi na yenye usawa, kwa kushirikiana na Serikali na wadau mbalimbali wa elimu ndani na nje ya nchi.Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa Volker Turk, amesikitishwa sana na mauaji ya jana ya watu wapatao 10, sambamba na uporaji na uharibifu wa mali wakati polisi walipokabiliana na waandamanaji kwenye mji mkuu wa Kenya, Nairobi na katika kaunti nyingine 16.Huko Geneva, Uswisi kumeanza mkutano wa siku 4 kuhusu matumizi ya Akili Mnemba au AI kwa maslahi ya wote ambapo Katibu Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la mawasiliano, ITU, Doreen Bogdan-Martin ameuliza washiriki ni jambo gani wanafanya AI ihudumie ubinadamu.?Na kuelekea kumbukizi yamauaji ya Srebrenica tarehe 11 mwezi huu wa julai, Umoja wa Mataifa unakumbuka mauaji hayo yaliyofanyika wakati wa vita vilivyofuatia baada ya kuvunjika kwa iliyokuwa Yugoslavia. Zaidi ya watu 100,000 huko Bosnia na Herzegovina waliuawa kati ya mwaka 1992 na 1995, wengi wao wakiwa waislamu wa Bosnia. Umoja wa Mataifa unasema mauaji ya Srebrenica ni moja ya vipindi vya kiza zaidi vya vita.Na katika mashinani tunakupeleka katika miji ya mpakani ya Matar na Muon katika eneo la Gambella nchini Ethiopia ambako maelfu ya wakimbizi wamewasili kutoka Jimbo la Upper Nile nchini Sudan Kusini wakikimbia vita na njaa, na sasa wanasubiri usajili na usaidizi kutoka kwa Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula. Nyandow Wie Deng ni mmoja akisimulia yaliyomkumba.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
Mwezi Juni mwaka 2025, Tume ya Ulaya iliorodhesha Kenya miongoni mwa nchi zenye changamoto ya utakatishaji wa fedha, huku Uganda ikipata afueni kwa kuondolewa kwenye orodha hiyo. Hatua hii ina maana kuwa mashirika ya kifedha – ikiwemo benki – zinalazimika kuzingatia kwa makini uhusiano wa kibiashara na miamala yoyote inayohusiana na nchi zilizo kwenye orodha hiyo, na kuchukua hatua kali za udhibiti wa fedha. Nchi nyingine katika orodha hiyo ni pamoja na Sudan Kusini, Tanzania, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Msumbiji, Nigeria, Afrika Kusini, na zingine. Katika Makala haya, Gurudumu la Uchumi, tunachambua hatua hii na athari zake kwa uchumi, lakini pia nini mamlaka katika nchi hizo zinaweza kufanya hili kujiondoa kwenye orodha hiyo.
Mwezi Juni mwaka 2025, Tume ya Ulaya iliorodhesha Kenya miongoni mwa nchi zenye changamoto ya utakatishaji wa fedha, huku Uganda ikipata afueni kwa kuondolewa kwenye orodha hiyo. Hatua hii ina maana kuwa mashirika ya kifedha – ikiwemo benki – zinalazimika kuzingatia kwa makini uhusiano wa kibiashara na miamala yoyote inayohusiana na nchi zilizo kwenye orodha hiyo, na kuchukua hatua kali za udhibiti wa fedha. Nchi nyingine katika orodha hiyo ni pamoja na Sudan Kusini, Tanzania, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Msumbiji, Nigeria, Afrika Kusini, na zingine. Katika Makala haya, Gurudumu la Uchumi, tunachambua hatua hii na athari zake kwa uchumi, lakini pia nini mamlaka katika nchi hizo zinaweza kufanya hili kujiondoa kwenye orodha hiyo.
Hii leo jaridani tunaangazia mashambulizi ya anga yaliyofanywa na Marekani dhidi ya vituo vya nyuklia vya Iran, na juhudi za kurejesha matumaini miongoni mwa jamii zilizotengana kwa migogoro Sudan Kusini. Makala tunakwenda nchini Tanzania na mashinani nchini Kenya.Hali ya taharuki yaendelea kushuhudiwa Mashariki ya Kati kufuatia mashambulizi ya anga yaliyofanywa na Marekani dhidi ya vituo vya nyuklia vya Iran mwishoni mwa wiki. Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki IAEA, Rafael Grossi, leo ametoa wito wa dharura wa shirika hilo kuruhusiwa kufika kwenye maeneo hayo yaliyoharibiwa, ili kutathmini kiwango halisi cha uharibifu.Katika juhudi za kuimarisha mshikamano na kurejesha matumaini miongoni mwa jamii zilizotengana kwa migogoro, ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Sudan Kusini, UNMISS, kwa kushirikiana na shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni, UNESCO, hivi karibuni waliandaa tamasha maalum la muziki katika mji wa Malakal, jimbo la Upper Nile – eneo ambalo kwa miezi ya hivi karibuni limekuwa kitovu cha machafuko.Katika makala Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Mashirika yanayotoa huduma ya msaada wa kisheria nchini Tanzania, TANLAP, Christina Kamili Ruhinda anaeleza wanavyotekeleza mpango wao wa kuhakikisha wanawake wanapata nafasi zaidi kwenye meza za uamuzi nchini Tanzania.Na mashianani fursa ni yake Priscillah Lesurkukwa, Mwanamke mkulima kutoka kaunti kame ya Samburu nchini Kenya ambaye ni mnufaika wa mradi wa Shrika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula WFP, ambao umewapatia wakulima mafunzo ya kutengeneza makinga maji na kuchimba mashimo yenye umbo la nusu mwezi ili kuvuna na kuhifadhi maji kwenye mashamba yao, na sasa mbinu hizo zimebadilisha mazingira kuwa na malisho ya kijani kibichi na miti inayostawi.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
Katika juhudi za kuimarisha mshikamano na kurejesha matumaini miongoni mwa jamii zilizotengana kwa migogoro, ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Sudan Kusini, UNMISS, kwa kushirikiana na shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni, UNESCO, hivi karibuni waliandaa tamasha maalum la muziki katika mji wa Malakal, jimbo la Upper Nile – eneo ambalo kwa miezi ya hivi karibuni limekuwa kitovu cha machafuko. Sharon Jebichii anatupasha zaidi
Katika eneo la Mata, karibu na mpaka wa Ethiopia na Sudan Kusini, ambakomaelfu ya wakimbizi kutoka Sudan Kusini wanapokea msaada wa dharura kupitia juhudi za Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani, WFP. unaolenga kuwalinda baada ya kukimbia mapigano makali nchini mwao. Nyibol Chueny Puok, mama wa watoto 4 ni miongoni mwao. Sharon Jebichi anatupasha zaidi...
Hii leo jaridani tunaangazia siku ya Wakimbizi Duniani, mwaka huu ikibeba maudhui “Mshinamano na wakimbizi”, tukisikia ujumbe wa Umoja wa Mataifa na kazi wanazozifanya kuinua Maisha ya wakimbizi, na pia tunakuletea sauti za wakimbizi kutoka DRC, Burundi, Ethiopia na Sudan Kusini.Leo ni Siku ya Wakimbizi Duniani, mwaka huu ikibeba maudhui “Mshinamano na wakimbizi” na Umoja wa Mataifa umetaka mshikamano huo kwa vitendo wakati idadi ya watu wanaolazimika kufungasha virago na kukimbia makayo yao ikifikia kiwango cha kihistoria.Tukisalia na siku ya wakimbizi duniani tunaelekea eneo la Mata, karibu na mpaka wa Ethiopia na Sudan Kusini, ambakomaelfu ya wakimbizi kutoka Sudan Kusini wanapokea msaada wa dharura kupitia juhudi za Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani, WFP. unaolenga kuwalinda baada ya kukimbia mapigano makali nchini mwao. Nyibol Chueny Puok, mama wa watoto 4 ni miongoni mwao.Katika makala Assumpta Massoi kupitia video ya shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi, UNHCR anakupeleka Kusini-Magharibi mwa Burundi kwenye kituo cha wakimbizi cha Musenyi kumsikia mkimbizi kutoka DRC ambaye ananufaika na kauli mbiu ya siku ya wakimbizi mwaka huu ya Mshikamano na Wakimbizi.Na mashianani tukisalia na siku ya wakimbizi duniani, tutakwenda nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC kumsikia mtoto mkimbizi ambaye alitumikishwa katika vita na waasi wenye silaha.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina na leo ikiwa ni siku ya kimataifa ya kupinga utumikishaji wa watoto ambapo shirika la Umoja wa Mataifa la Kazi duniani, ILO, linasema maudhui ni Maendeleo yako dhahiri, lakini bado kuna mengi ya kufanya: Hebu tuongeze kasi. Tunakupeleka nchini Tanzania kumulika harakati za kuwaepusha watoto kutumikishwa.Watu waliolazimika kukimbia makazi yao kutokana na vita, ukatili na mateso duniani kote imefikia kiwango cha juu kisichovumilika, hasa wakati huu ambapo ufadhili wa misaada ya kibinadamu unapungua kwa kasi. Kwa mujibu wa Ripoti ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia wakimbizi UNHCR iliyotolewa leo kuhusu mwelekeo wa Ulimwengu, kufikia mwisho wa Aprili mwaka huu, kulikuwa na watu milioni 122.1 waliolazimika kuhama kwa nguvu, ikilinganishwa na watu milioni 120 mwaka uliopita katika kipindi kama hicho.Ikiwa leo ni Siku ya Kimataifa ya kupinga ajira kwa watoto, utafiti uliofanywa na mashirika ya Umoja wa Mataifa lile la kazi duniani, ILO na la kuhudumia Watoto UNICEF unaonesha licha ya hatua zilizopigwa, ajira kwa watoto bado inaathiri watoto milioni 138 duniani kote, kati yao milioni 54 wakifanya kazi hatarishi ambazo zinaweza kuhatarisha afya yao, usalama wao au maendeleo yao kwa ujumla.Nchini Sudan Kusini watu wako katika hatari ya njaa katika miezi ijayo, kutokana na kuongezeka kwa mapigano katika jimbo la Upper Nile. Utafiti mpya kutoka katika Mfumo wa Uainishaji wa Viwango vya Uhakika wa Chakula (IPC) unaonesha kudorora kwa hali ya chakula na lishe katika maeneo ya Sudan Kusini yaliyoathiriwa na mapigano katika miezi ya karibuni.Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili hii leo mchambuzi wetu mlumbi wa Kiswahili Joramu Nkumbi kutoka nchini Tanzania, anafafanua maana ya maneno "MBEUZI, MNYWANYWA NA MACHAGU.”Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!
Hii leo jaridani tunaangazia haki za binadamu nchini Ukraine na upatikanaji wa elimu nchini Kenya. Makala tunakupeleka nchini Sudan Kusini, na amashinani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, kulikoni?Tume Huru ya Umoja wa Mataifa ya Uchunguzi kuhusu Ukraine imehitimisha kwamba vikosi vya kijeshi vya Urusi vimetenda uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya ubinadamu, hasa mauaji, kupitia mashambulizi ya ndege zisizo na rubani (drones) yaliyoelekezwa dhidi ya raia.Mradi wa "operesheni rejea shuleni" unaoendeshwa na shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia watoto UNICEF kwa ushirikiano na wizara ya elimu ya Kenya, shirika liliso la kiserikali la Hapag Lloyd na wadau wengine kwa kuzipa fedha familia zisizojiweza kuendesha shughuli za kiuchumi, umerejesha mautumaini ya elimu kwa mamia ya watoto katika Kaunti ya Kwale Pwani ya Kenya ambao waliacha shule sababu ya umasikini. Katika makala ikielekea siku ya walinda amani kesho Mei 29, tunamulika harakati za walinda amani wa Umoja wa Mataifa nchini SUdan Kusini za kulinda raia na mwenyeji wako katika makala hii iliyoandaliwa kupitia video ya ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa Kulinda amani Sudan Kusini, UNMISS ni Sharon Jebichii.Na katika mashinani huku machafuko yakiendelea mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, wafanyakazi wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR wako mashinani mjini Goma na maeneo mengine yaliyoathirika ili kutoa msaada muhimu, ikiwa ni pamoja na kufanikisha nia ya wakimbizi wanaorejea nchini mwao Rwanda. Raab na Ruusi ni baadhi yao.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
Kuelekea siku ya walinda amani Mei 29, tunakwenda nchini Sudan Kusini kumulika walinda amani na ulinzi wa raia. Katika taifa hilo changa zaidi duniani walinda amani wa Umoja wa Mataifa kutoka Mongolia wanaohudumu kwenye Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo (UNMISS) walikuwa msaada mkubwa wakati kijiji cha Abiemnhom kaskazini mwa Sudan Kusini kilipovamiwa. Walinda amani hao walifika haraka kutoka kituo chao cha karibu na kutoa msaada wa kuokoa manusura na miili ya waliouawa. Je nini kilifanyika zaidi Sharon Jebichii anasimulia kwenye makala hii iliyotokana na video ya UNMISS.
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini Tanzania kuangazia siku ya familia iliyokutanisha wadau wakimulika pamoja na mambo mengine nafasi ya vyombo vya habari katika kuimarisha malezi na makuzi ya mtoto.Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu misaada ya dharura OCHA hii leo imesema wakati mpango tata wa Israeli wa kugawa misaada kwenye eneo la Palestina la Gaza linalokaliwa kimabavu na Israeli ukiendelea, Umoja wa Mataifa kwa mara nyingine tena umesihi mamlaka za Israeli kuruhusu ongezeko la kiwango cha misaada ya kufikia walengwa kwenye eneo hilo lililozingirwa ili kuepusha uhaba wa chakula..Kadiri nchi zinavyokumbwa zaidi na majanga ya asili, gharama halisi za majanga ni mara 10 zaidi ya ilivyodhaniwa hapo awali, zikiwa na athari mbaya zaidi katika sekta za afya, makazi, elimu na ajira, imesema Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kupunguza hatari za majanga katika ripoti iliyochapishwa Jumanne.Nchini Namibia, makazi yaliyojengwa na shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu na Afya ya Uzazi, UNFPA kwa ajili ya wajawazito wanaoishi maeneo ya mbali kusubiria ili kujifungua kwa usalama, yamesaidia kupunguza vifo vya wajawazito na watoto wachanga.Na katika mashinani, kupitia video iliyoandaliwa na Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani Sudan Kusini UNMISS, tunakutana na Mary Aban Akon, mkazi wa kijiji cha Hai Matar huko Sudan Kusini. Yeye ni miongoni mwa wakimbizi waliorejea nyumbani baada ya kupatiwa makazi mapya yaliyojengwa kwa msaada wa mashirika ya kibinadamu chini ya mradi uliofadhiliwa na Umoja wa Mataifa na wadau wake.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
Ukosefu wa vyakula na bidhaa zingine muhimu, umelazimisha UNHCR kuomba msaada wa dharura kwa wakimbizi wenye asili ya Sudan Kusini, walio kimbilia DRC.
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayoturejesha hapa makao makuu ambako Idhaa hii Dokta Willis Ochieng kutoka Kenya aliyehudhuria ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika lisilo la kiserikali linalojihusisha na masuala ya kilimo na maendeleo. Pia tunakuletea muhtasari wa habari, na mashinani tunakwenda Ghana.Ukuaji wa maendeleo ya binadamu – yanayopimwa kwa uhuru na ustawi wa watu – umeendelea kuwa wa kasi ndogo tangu mshtuko mkubwa wa janga la COVID-19 lakini kuna matumaini makubwa kwamba Akili Mnemba au AI, ikiwa itatumika kwa njia sahihi, inaweza kuwa chombo chenye nguvu cha kuboresha maisha ya mamilioni ya watu. Hii ni kwa mujibu wa Ripoti ya kila mwaka ya Maendeleo ya Binadamu iliyotolewa leo na Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo duniani, UNDP.Kulengwa kwa hospitali ya Médecins Sans Frontières nchini Sudan Kusini kunaweza kuwa uhalifu wa kivita imeeleza leo Kamisheni ya Umoja wa Mataifa kuhusu Haki za Binadamu Sudan Kusini kufuatia mashambulizi ya angani yaliyotekelezwa dhidi ya hospitali ya Médecins Sans Frontières (MSF) huko Old Fangak, Jimbo la Jonglei mapema majuzi asubuhi ya Jumamosi na kusababisha vifo vya takribani raia saba na kujeruhi wengine. Shambulio hilo lilifanyika baada ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Sudan Kusini (SSPDF) kutoa onyo la kufanya shambulizi iwapo dai lao la kuachiliwa meli zao zilizotekwa halitatekelezwa.Ripoti mpya ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani, WHO, iliyotolewa leo imeonesha jinsi mahali mtu anakozaliwa kulivyo na mchango katika maisha yake. Ripoti inasema, “mahali mtu anakozaliwa huweza kuamua kama ataishi zaidi ya miongo mitatu kuliko mtu mwingine aliyezaliwa katika nchi yenye hali duni za makazi, elimu na fursa za ajira.”Na mashinani leo nampa fursa Dorcas Awortwe, Naibu Mkurugenzi wa Tume ya Maendeleo ya Kanda ya Kati kutoka Ghana, aliyeshiriki kwenye mkutano wa jukwaa la watu wa asili hapa Makao Makuu wiki iliyopita anazungumzia changamoto zinazowakabili watu wa asili katika jamii yake na ombi lake kwa Umoja wa Mataifa.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani WFP nchini Sudan Kusini chini ya ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Korea KOICA wanaendesha mradi wa kusaidia wananchi katika kilimo ili kujenga ustahimilivu na kupambana na utapiamlo. Tupate taarifa zaidi kutoka kwa Evarist Mapesa.
Hii leo jaridani tunaangazia siku ya Kimataifa ya Usalama na Afya Kazini, na juhudi za Umoja wa Mataifa za kusaidia wakulima Sudan Kusini kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi. Makala tunasalia na usalama kazini na mashinani tunakwenda nchini Kenya, kulikoni?Leo ni Siku ya Kimataifa ya Usalama na Afya Kazini mwaka huu ikibeba maudhui “Mapinduzi ya usalama na afya Kazini: Nafasi ya Akili mnemba na teknnolojia ya kidijitali mahala pa kazi” lengo likiwa kudhihirisha nguvu ya AI na teknolojia zinapotumika vyema zinaweza kuleta mabadiliko kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kazi duniani ILO.Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani WFP nchini Sudan Kusini chini ya ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Korea KOICA wanaendesha mradi wa kusaidia wananchi katika kilimo ili kujenga ustahimilivu na kupambana na utapiamlo. Tupate taarifa zaidi kutoka kwa Evarist Mapesa.Makala tunabisha hodi nchini Indonesia, taifa hili la Kusini-Mashariki mwa bara la Asia, kubwa hasa ni kumulika ni kwa vipi sekta ya uvuvi nchini humu inatekeleza kivitendo wito wa shirika la Umoja wa Mataifa la Kazi, ILO kuhusu usalama na afya Kazini. Na katika mashinani fursa ni yake Abdikani Haji Hassan kutoka kambi ya wakimbizi ya Daadab iliyoko katika kaunti ya Garissa nchini Kenya ambaye kupitia Mpango wa Prospects unaoungwa mkono na Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF amejikwamua kimaisha na sasa ana ndoto ya kuenda ng'ambo ili kuendeleza ujuzi wake wa kupiga picha.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
Nchini Sudan Kusini, familia zilizo kwenye hali duni katika eneo la kaskazini mashariki mwa nchi hiyo ziko katika hali tete sana huku mapigano yakizidi kuongezeka na njaa ikikaribia kufikia viwango vya juu kabisa, limeonya leo Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP). Anold Kayanda na maelezo zaidi.
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini Kenya kumulika elimu ya mtoto wa kike kama moja ya nguzo muhimu katika jamii ukizingatia malengo endelevu ya maendeleo ya Umoja wa Mataifa.Pia tunakuletea muhtasari wa habari na sauti za mashinani.Viongozi wa Umoja wa Mataifa leo wamelaani vikali mashambulizi ya anga ya Israel huko Ukanda wa Gaza na kutoa wito kwa kusitisha uhasama mara moja. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ameonesha mshtuko na wasiwasi mkubwa kuhusu mashambulizi hayo akitoa wito kwa pande zote kuheshimu usitishaji mapigano, kurejesha misaada ya kibinadamu bila vikwazo, na kuhakikisha kuachiliwa mara moja na bila masharti kwa mateka waliobaki.Ghasia zinazoendelea katika kaunti za Nasir, Ulang, na Baliet, Jimbo la Upper Nile nchini Sudan Kusini zimeathiri vibaya jamii za eneo hilo na shughuli za kibinadamu, na kusababisha watu takriban 50,000 kukimbia makazi yao tangu mwishoni mwa mwezi Februari amesema Mratibu wa Masuala ya Kibinadamu wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini, Bi. Anita Kiki Gbeho, na kuonesha wasiwasi mkubwa kuhusu hali hiyo, akiwataka wahusika wote kuheshimu raia, wahudumu wa misaada, na miundombinu muhimu.Siku ya 7 ya mkutano wa 69 wa Kamisheni ya Hali ya Wanawake duniani, Tanzania ina tukio la kando kuonesha harakati za kumwinua mwanamke kiuchumi na miongoni mwa wazungumzaji ni Tully Esther Mwambapa, Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Benki ya CRDB nchini Tanzania ambaye ameieleza Idhaa ya Umoja wa Mataifa ujumbe wake kwenye tukio hilo kuhusu walivyosaidia wanawake kuondokana na kikwazo cha kukosa dhamana wanapotaka kujikwamua kiuchumi.Na katika mashinani tunasalia hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa katika mkutano unaoendelea wa 69 wa Kamisheni ya Hali ya Wanawake duniani CSW69, kusikia ujumbe wa mshiriki wa kuwaunga mkono wasichana na wanawake na kutokomeza ndoa za utotoni.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
Wakati mkutano wa 69 wa Kamisheni ya Hali ya wanawake Duniani CSW69 ukiendelea hapa New York Marekani nchini Sudan Kusini wanawake na wasichana wanaendelea kuonja shubiri ya vita, wakibakwa, kuuawa, kukosa elimu na kupitia changamoto nyingine lukuki sababu ya vita. Mmoja wa washiriki wa mkutano wa CSW69 kutoka Sudan Kusini akizungumza na Flora Nducha wa Idhaa hii ya Kiswahili amesema sasa imetosha amekuja na ujumbe mmoja tu, anataka jinamizi la vita lazima likome.
Hii leo jaridani tunaangazia mpango mpya wa UN80, unaolenga kuimarisha kazi na ufanisi wa chombo hicho ambacho mwaka huu kinatimiza miaka 80, na yaliyojiri katika mkutano wa CSW69. Makala na mashinani tunasalia hapa hapa makao makuu, kulikoni?Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, amezindua Mpango mpya wa UN80, unaolenga kuimarisha kazi na ufanisi wa chombo hicho ambacho mwaka huu kinatimiza miaka 80 tangu kuanzishwa kwake huku akisisitiza umuhimu wa mshikamano wa kimataifa..Wakati mkutano wa 69 wa Kamisheni ya Hali ya wanawake Duniani CSW69 ukiendelea hapa New York Marekani nchini Sudan Kusini wanawake na wasichana wanaendelea kuonja shubiri ya vita, wakibakwa, kuuawa, kukosa elimu na kupitia changamoto nyingine lukuki sababu ya vita. Mmoja wa washiriki wa mkutano wa CSW69 kutoka Sudan Kusini akizungumza na Flora Nducha wa Idhaa hii ya Kiswahili amesema sasa imetosha amekuja na ujumbe mmoja tu, anataka jinamizi la vita lazima likome.Makala tukisalia hapa hapa katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa Jijini New York, Marekani ambako Mkutano wa 69 wa Kamisheni ya Hali ya Wanawake Duniani, (CSW69) umeingia siku ya tatu, nimezungumza na Nuria Mshare ambaye amewakilisha taasisi ya Haki Elimu ya nchini Tanzania.Na Katika mashinani fursa ni yake Janet Zebedayo Mbene kutoka Tanzania aliyehududhuria mkutano huu hapa makao makuu, kama mwenyekiti wa shirika lisilo la kiserikali la mtandao wa uwezeshaji wa wanawake Tanzania na angependa kuwashauri wanawake na wasichana wanaopitia changamoto wajikite katika fursa mbalimbali. Kila kitu kina changamoto. Wajitie moyo na waondoe uoga, na kwa kile kidogo walicho nacho wanaweza kujiinua na kuinua jamii kwa ujumla.Mwenyeji wako ni Assumpta, karibu!
Viongozi wa kisiasa wa Sudan Kusini lazima wakabiliane na ukwepaji wa sheria na ufisadi unaochochea ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu, la sivyo watahatarisha mpito wa kisiasa wa nchi hiyo, imesema Tume ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Binadamu Sudan Kusini katika ripoti yake iliyotolewa leo kama anavyoripoti Flora Nducha.
Hii leo jaridani tunaangazia migogoro ambayo yameendelee kwa muda mrefu Sudan Kusini, na ujumbe wa Katibu Mkuu ikielekea kuanza kwa mfungo wa mwezi Mtukufu wa Ramadhani. Makala inatupeleka nchini Kenya, na mashinani nchini Tanzania.Viongozi wa kisiasa wa Sudan Kusini lazima wakabiliane na ukwepaji wa sheria na ufisadi unaochochea ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu, la sivyo watahatarisha mpito wa kisiasa wa nchi hiyo, imesema Tume ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Binadamu Sudan Kusini katika ripoti yake iliyotolewa leo.Kuelekea kuanza kwa mfungo wa mwezi Mtukufu wa Ramadhani mwishoni mwa wiki hii, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres ametuma ujumbe wake wa kutaka kipindi hicho cha takribani siku 30 kitumike kuleta amani na kuongoza kuelekea dunia yenye yenye haki na huruma zaidi..Katika makala Anold Kayanda wa Idhaa hii kutokana na video iliyoandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kazi duniani, anakupeleka nchini Kenya kukutanisha na mkimbizi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC ambaye amenufaika na Mpango wa Utambuzi wa Ujuzi wa Awali kwa hisani ya ILO, serikali ya Kenya na wadau.Na mashinani fursa ni yake Ashura Hamis Sayid kutoka Tanzania ambaye ni Mratibu wa Mpango wa U-report unaoungwa mkono na Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF ili kuwapa vijana uhuru wa kujieleza na kutoa maoni yao juu ya maswala mbalimbali .Ameweza kutufafanulia zaidi madhumuni ya mpango huu na jinsi gani inatumika katika jamii.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
Mashirika ya Umoja wa Mataifa, lile la Kuhudumia Watoto, UNICEF na la Mpango wa Chakula duniani, WFP kwa kushirikiana na mradi wa pamoja wa kimataifa wa mnepo ,au Joint Resilience Project (JRP) nchini Sudan Kusini ,wanatekeleza msaada wa chakula bora na salama bila malipo kwa watoto shuleni ,kwa zaidi ya wanufaika laki tano alfu Hamsini 550,000 ili kuhakikisha ndoto za watoto hao zinatimia. Ni sauti ya watoto wakitembea kuelekea shuleni huku wakiwa wamevibeba vitabu vyao mikononi.Kupitia video iliyoandaliwa na UNICEF, Tieng Maleng, mnufaika wa mradi wa JRP kutoka kijiji cha Pangapdit anaonekana akiwapa watoto wake kiamsha kinywa huku wakiwa wamekaa nje ya boma lao wakiwa wamevalia sare zao tayari kwenda shule. Kwa furaha anaeleza jinsi mradi huu umekuwa wa manufaa kwa familia yake.“Baada ya kupokea msaada wa kifedha, nilitumia fedha kidogo kulipa ada ya shule ya watoto wangu. Nikachukua sehemu kidogo ya fedha hizo kununua viatu vyao, na dawa. Pia nilitumia sehemu nyingine ya msaada huo katika kilimo.”Katika shule ya msingi ya Pangapdit inayoungwa mkono na mradi huu, watoto wanaonekana wakiwa wamesimama kwenye gwaride la shule wakisikiliza maelekezo kutoka kwa walimu wao. Aluel,Mwanawe Tieng Maleng, ambaye ni mwanafunzi katika shule hiyo anasema, “Tunaenda shule kila asubuhi na ndoto yangu ni kufanya kazi na mashirika yanayosaidia watu. Wakati kengele ya shule inapolia, tunakusanyika kwa ajili ya mkutano na baadaye tunaenda darasani.”Kupitia mradi huu,wanafunzi wamepokea vitabu vya kusoma,wamejengewa madarasa mapya, vyoo bora , na mifereji ya kunawa mikono.UNICEF na WFP wanafanya kila wawezalo kuhakikisha kuwa watoto wanatimiza ndoto zao.
Hii leo jaridani tunaangazia miaka mitatu ya vita nchini Ukraine, machafuko nchini DRC na elimu Sudan Kusini. Makala inatupeleka katika ukanda wa Gaza kumulika harakati za chanjo ya polio, na mashinani nchini Kenya kusikia ujumbe kuhusu umuhimu wa lugha mama.Mkutano wa 58 wa Baraza la Umoja wa Mataifa la Haki za Binadamu umeanza leo jijini Geneva, Uswisi ambapo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amezungumzia kiza kilichotanda duniani hivi sasa kutokana na mapigano yanayoendelea sehemu mbalimbali kuanzia Ukraine, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC hadi Ukanda wa Gaza, yakiambatana na ukiukwaji mkubwa wa haki, akitaka kila juhudi zichukuliwe kusaka amani ya kudumu.Huko Gaza Kaskazini, kwenye eneo la wapalestina linalokaliwa na Israeli, wanafamilia zilizofurushwa makwao kutokana na vita kati ya Israeli na wanamgambo wa Hamas wanavumilia msimu wa baridi kali katika makazi ya muda ya mahema yanayopigwa na upepo na mvua usiku na mchana, limesema shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Watoto UNICEF. Nyumba zao zimeharibika na kuacha watoto kuishi katika mazingira mabaya.Katika makala Anold Kayanda wa Idhaa hii anaangazia chanjo inayoendelea katika Ukanda wa Gaza dhidi ya polio chini ya usimamizi wa Wizara ya Afya ya Palestina kwa kusaidiwa na Mashirika ya Umoja wa Mataifa.Na mashinani ikiwa hivi majuzi Dunia iliadhimisha siku ya kimataifa ya lugha mama, tunakwenda Kajiado nchini Kenya kusikia ujumbe kuhusu umuhimu wa lugha mamaMwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina leo inayotupeleka Kenya kufuatilia juhudi za shirika la Umoja wa Mstaifa la mazingira UNEP na serikali ya nchi hiyo za kuichagiza jamii kuhama kutoka kwenye vyombo vya usafiri vinavyotumia mafuta yanayochafua mazingira na kukumbatia magari na vyombo vingine vya usafiri vinavyotumia nishati ya umeme. Pia tunakuletea Muhtasari wa habari na mashinani inayotupeleka nchini Sudan Kusini. Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
Matangazo ya nusu saa kuhusu habari za mapema asubuhi pamoja na habari za michezo.
Mwaka 2024 ukielekea ukingoni, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR nchini Uganda limetoa rai kwa jumuiya ya kimataifa kutolisahau taifa hilo la Afrika Mashariki ambalo ni maskani ya idadi kubwa zaidi ya waomba hifadhi na wakimbizi barani Afrika. Rai hiyo iliyotolewa mwishoni mwa wiki inataka ufadhili wa fedha uongezwe ili liweze kuendelea kukirimu watu hao ambao wengi wanakimbia machafuko. Huyo ni Moulid Hujale afisa wa UNHCR nchini Uganda akitoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kushikamana na Uganda akiwa kwenye makazi makubwa ya wakimbizi ya Kiryandongo Magharibi mwa nchi hiyo. Anasema kuna mambo matatu muhimu ambayo dunia inapaswa kufahamu kuhusu Uganda na wakimbizi.“Mosi Uganda inahifadhi idadi kubwa zaidi ya wakimbizi na waomba hifadhi Afrika ikiwa na zaidi ya watu milioni 1.7 wengi wao wakitoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC na Sudan Kusini.”Zaidi ya hapo ukarimu wa Uganda anasema hauna kipimo“Pili, Uganda ina sera ya kufugua mlango kwa wakimbizi na pia kwa miongo mingi imekuwa ikiwakaribisha watu wanaokimbia machafuko bila kujali utaifa wao. Kitu ambacho ni kikubwa na cha kipekee kuhusu nchi hii ni kwamba wakati wakimbizi wanapowasili hapa hupewa ardhi, mahali pa kuishi na hata kulima mazao kwa ajili ya kujikimu. Wana uhuru wa kutembea na haki ya kuajiriwa. Hawajatengwa lakini wanaishi ndani ya jamii inayowahifadhi. Sera hii ya Uganda inawaruhusu wakimbizi kujumuishwa katika huduma za kitaifa ambapo wanafaidika na elimu na huduma za afya.”Lakini Kutokana na changamoto za fedha Moulid anasema ukarimu huo sasa uko njia panda"Tatu: Ukarimu wa Uganda uko hatarini kwani wakimbizi zaidi wanaingia kutoka nchi jirani. UNHCR, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, liko mashinani kufanya kazi na Serikali ya Uganda kusaidia kutoa msaada wa kuokoa maisha kwa watu hawa. Hata hivyo, rasilimali ni chanche. Tunahitaji msaada wenu ili Uganda iendelee kuwa mfano wa kuigwa kwa dunia nzima.”Kwa nyjibu wa UNHCR licha ya idadi kubwa ya watu na rasilimali kidogo, sera za Uganda zinammanisha kwamba wakimbizi ni sehemu ya maisha ya kijamii na kiuchumi na ongezeko la rasilimali litakidhi haja za waliopo sasa na watakaokuja.
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina na tunaelekea nchini Kenya kuangazia moja ya ukiukwaji Mkubwa wa haki za binadamu dhidi ya wanawake, jinamizi la ukeketaji na jitihada zinazochukuliwa na UNFPA na wadau mbalimbali. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na mashinani inayotupeleka nchini Namibia.Baada ya serikali ya Bashar Al-Assad kupinduliwa na kuibuka kwa taarifa za baadhi ya nchi duniani kuanza kusitisha mchakato wa kushughulikia maombi ya Wasyria waliokuwa wameomba hifadhi kuokoa usalama wa maisha yao pindi hali ilipokuwa tete nchini mwao, Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) linaendelea kutoa wito kwa mataifa yote kufungua milango, kuwapa hifadhi na ulinzi raia wa Syria wanaotafuta usalama. UNHCR imeahidi pia mara tu hali ya Syria itakapokuwa wazi zaidi, itatoa mwongozo kuhusu mahitaji ya ulinzi kwa Wasyria walioko hatarini.Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) limekaribisha mchango wa dola za Marekani milioni 22 kutoka shirika la Korea Kusini la Ushirikiano wa Maendeleo ya Kimataifa (KOICA) ili kuimarisha mnepo kwa tabianchi na uhakika wa chakula kwa wakulima wadogo, wafugaji na makundi yaliyoko pembezoni nchini Kenya, Somalia na Sudan Kusini. Vituo vya utabiri wa hali ya hewa vinatabiri hali ya La Niña mashariki mwa Pembe ya Afrika na uwezekano wa kupunguza mvua katika kipindi hikiNa walinda amani wa kikosi cha 11 cha Tanzania -TANZBATT-11 kinachohudumu kwenye ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, DRC, MONUSCO jimboni Kivu Kaskazini wametunukiwa nishani ya umoja wa mataifa ikiwa ni alama ya kufanya kazi kwa utii,uhodari na uaminifu. Miongoni mwao ni Private Selina Kisemvule.Katika mashinani ikiwa ni siku ya mwisho ya maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia, fursa ni yake Rais Nangolo Mbumba wa Namibia ambaye kupitia ukurasa wa X wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ya Uzazi na Idadi ya Watu, UNFPA anawahimiza wananchi na dunia nzima kwa jumla kusimama kidete ili kutokomeza unyanyasaji wa kijinsia.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
Mazungumzo ya kuunda serikali ya mseto Sudan Kusini, yame kwama baada ya pande husika kuto afikiana kuhusu jinsi wata wagawa mamlaka.
Hii leo jaridani tunaangazia wakimbizi wa ndani nchini Haiti, na mafunzo ya stadi za kujikimu kimaishwa kwa vijana Tambura Sudan Kusini. Makala inatupeleka nchini Uganda na mashinani nchini Kenya, kulikoni?Zaidi ya watu 20,000 wamekimbia makazi yao katika mji mkuu wa Haiti Port-au-Prince katika muda wa siku nne tu, ikiwa ni pamoja na watu wengine zaidi ya 17,000 wanaohifadhiwa katika makazi 15 ya wakimbizi wa ndani, kutokana na kuongezeka kwa ghasia za magenge ya uhalifu ambazo ziumevuruga kabisa minyororo muhimu ya usambazaji wa misaada na kulitenga jiji la Port-au-Prince limesema shirika la Umoja wa Mataifa la uhamiaji IOM.Vijana katika mji wa Tambura ulioko jimbo la Equatoria Magharibi nchini Sudan Kusini wanageuza mafunzo ya ufundi stadi kuwa nguvu ya amani na ustawi, mafunzo ambayo yalifanikishwa na ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo, UNMISS.Katika makala Selina Jerobon kupitia video ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi anakupeleka Uganda kuona harakati za wakimbizi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC kujikwamua kiuchumi baada ya machungu waliyopitia nyumbani kwao.Mashinani tutaelekea nchini Kenya kusikia ni kwa jinsi gani jamii katika maeneo kame wanakabiliana na mabadiliko ya tabianchi.Mwenyeji wako ni Bosco Cosma, karibu!
Vijana katika mji wa Tambura ulioko jimbo la Equatoria Magharibi nchini Sudan Kusini wanageuza mafunzo ya ufundi stadi kuwa nguvu ya amani na ustawi, mafunzo ambayo yalifanikishwa na ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo, UNMISS.Shamrashamra zilitawala wakati vijana 61, wakiwemo wasichana 41 na wavulana 20 walipohitimu mafunzo ya ufundi stadi yenye lengo la kuwaondoa katika umaskini na pia kuwaepusha kutumikishwa katika mzozo unaoendelea nchini humo tangu Desemba 2013.Walifundishwa urembo wa nywele, kutengeneza sabuni, halikadhalika ushoni, mafunzo yaliyofadhiliwa na UNMISS na kutolewa na shirika la kiraia Star Trust Organization, linalohusika na kupunguza ghasia kwenye jamii kwa kuwajegena vijana uwezo.Miongoni mwao ni Suzan James, mama wa watoto wawili aliyejifunza urembo wa nywele na akiwa anamhudumia mteja wakati wa mafunzo anasema.“Ninashukuru mno, kwa sababu nimejifunza mambo mengi ambayo awali sikuyafahamu, lakini sasa ninaweza kufanya. Inanisaidia sana, na ninajivunia na nina furaha. Baada ya hili, nitaenda kufungua sehemu yangu mwenyewe ya urembo wa nywele ili kusaidia jamii.”Huyu ni Justin Alex yeye amejifunza ushoni na akiwa kwenye chereheni yake anasema.. “iwapo nitapekela hii cherehani nyumbani, nitaweza kufanya kazi na kusaidia familia yangu. Kama kijana tusikae nyumbani au tusifanye uhalifu mjini na kusababisha vifo kwa jamii zetu kwa sababu si jambo zuri. Kuanzia sasa tunahitajika kushiriki kwenye shughuli za kusaidia jamii, kama kupeleka hii cherehani nyumbani ili nisaidie jamii yangu.”Wahitimu wamepatiwa vifaa vya kuanzia kufanyie kile walichojifunza. Katika hafla ya utoaji wa vyeti UNMISS iliwakilishwa na afisa wake wa masuala ya ulinzi na ujumuishaji kwenye jamii Ibrahim Tahiru ambaye amesema..“Mradi huu unaweza kuleta amani, lakini pia mradi huu huu unahitaji amani ili uweze kuendelea. Bila amani hivi vitu vitakuwa bure. Kwa sababu wahitimu wanahitaji mazingira yenye amani ili waweze kutumia stadi zao kwa ajili ya kuboresha maisha yao na ya jamii zao. Mradi huu ni ishara ya nia yetu ya kuendelea kushirikiana na Sudan Kusini na kusaidia kufikia amani ya kudumu na kuondokana na umaskini.”Mamlaka za Tambura zina Imani kubwa na mradi huu kama asemavyo Kaimu Kamishna wa Tambura Moses Masisere.“Hakika, Tambura tumekuwa tukililia amani. Kwa hiyo kwa msaada huu tunaamini kuwa mafunzo kwa vijana zaidi kutawasaidia washiriki kwenye harakati za kiuchumi na kupunguza mauaji na uhalifu mwingine Tambura.”
Huko Maban, jimboni Upper Nile, kaskazini mashariki mwa Sudan Kusini, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi ,UNHCR linajenga vifaa vya kuhifadhi maji pamoja na makinga maji ili kuepusha mashamba dhidi ya mafuriko ya msimu yanayokumba eneo hilo mara kwa mara, eneo ambalo ardhi yake ina rutuba kwa ajili ya kilimo cha mazao ya chakula na biashara. Hapa shambani jimboni Upper Nile nchini Sudan Kusini, wakulima wakiwemo wenyeji na wakimbizi wakiwa shambani wakiimba. Awad Usman mwenyeji wa hapa anasema kuimba kunatuliza fikra zangu. Nyimbo hazisaidii kupanda mazao, lakini zinaweza kupunguza msongo wa mawazo.Msongo wa mawazo unatokana na madhara ya mabadiliko ya tabianchi yaletayo mvua kubwa na mafuriko kwenye mashamba yao.Awad anasema nakumbuka mafuriko ya mwaka 2019, yalisomba kila kitu. Ufuta wote ulisombwa. Mtama pekee ulisalia. Tulikaa ndani ya nyumba kwa siku tano, na tulipotoka tulikuta shamba zima limetwama kwenye maji.Alex Noel Kilong, afisa wa UNHCR anasema mafuriko yanaongeza machungu kwa shida ambazo tayari jamii inakumbana nazo. Mafuriko yanazidi kuongezeka na kusoma barabara, mifugo, mashamba na vituo vya afya hivyo anasema..“Tunahitaji kujenga mbinu za kujipatia kipato. Maban ina fursa kubwa sana, udongo una rutuba, tunatakiwa pia kujenga mapipa ya kuhifadhi maji juu ya ardhi, na maji haya yanaweza kutumiwa wakati wa ukame, ili kilimo kiwe shughuli inayoweza kufanyika mwaka mzima. Kwa njia hiyo tutaweza kupunguza njaa. Tutapunguza ukosefu wa uhakika wa chakula miongoni mwa wenyeji na pia kwa wakimbizi.UNHCR pia imepatia wakulima kama Awad mbegu ya ufuta mweupe, ambayo anasema ni bora na hivyo atakavyovuna , kiasi atauza na nyingine atahifadhi kwa matumizi ya kula nyumbani na pia kama mbegu.
Hii leo jaridani tunaangazi ufadhili kwa wakulima huku mkutano wa COP29 ukiendelea Baku, na madhara ya mafuriko kwa wakulima nchini Sudana Kusini tukimulika jinsi Umoja wa Mataifa wanavyohaha kuwasaidia. Makala inatupeleka nchini DRC na mashinani tunasalia huko huko Sudan Kusini, kulikoni?Kuongeza kiwango cha fedha kwenye ufadhili wa miradi ya kukabili na kuhimili tabianchi nchi ikiwa ni moja ya masuala muhimu yanayojadiliwa katika mkutano wa 29 wa nchi wanachama wa mkataba wa mabadiliko ya tabianchi, COP29 huko Baku, Azerbaijan, leo ikiwa ni siku ya pili ya mkutano huo, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema bila kupunguza kwa kiasi kikubwa hewa chafuzi, na kuimarisha miradi ya kuhimili na kukabili mabadiliko ya tabianchi, kila uchumi duniani utakumbwa na madhara makubwa.Huko Maban, jimboni Upper Nile, kaskazini mashariki mwa Sudan Kusini, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR linajenga vifaa vya kuhifadhi maji pamoja na makinga maji ili kuepusha mashamba dhidi ya mafuriko ya msimu yanayokumba eneo hilo mara kwa mara, eneo ambalo ardhi yake ina rutuba kwa ajili ya kilimo cha mazao ya chakula na biashara.Katika Makala George Musubao, mwandishi wetu huko Jimboni Kivu Kaskazini, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC akimulika mkutano ulioandaliwa na watendaji wa Umoja wa Mataifa ya eneo hilo kuangalia jinsi ya kukabiliana na habari potofu na za uongo.Na mashinani tutakuwa Sudan Kusini, ambako shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP linasaidia jamii zilizoathiriwa na mafuriko kupata suluhisho la kudumu.Mwenyeji wako ni Bosco Cosmas, karibu!
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayoangazia uvuvi katika mji wa Kalokol karibu na fuo za Ziwa Turkana Kaskazini mwa Kenya. Pia tunakuletea muhtasari wa habari zikiwemo za mkutano wa WUF12 Cairo Misri, chanjo ya malaria Sudan, siku ya Tsunami, na mashinani.Mkutano wa 12 wa Jukwaa la Miji Duniani, WUF12 umeingia siku ya pili hii leo huko Cairo, Misri, ambako Ming Zing ambaye ni Mkurugenzi wa Miji, Mnepo na Ardhi kutoka Benki ya Dunia amezungumzia umuhimu wa kujumuisha wanawake na vijana katika mipango miji.Sudan imekuwa nchi ya 16 barani Afrika na ya kwanza katika Ukanda wa WHO wa Mashariki na Mediterania kuanzisha chanjo dhidi ya Malaria kwa watoto wasiozidi umri wa miezi 12. Chanjo imeanza kutolewa jana katika majimbo ya Gedaref na Blue Nile ambapo WHO na wadau wamesema mwaka 2025 na 2026 chanjo itapelekwa katika maeneo 129 nchini kote Sudan.Na leo ni siku ya kimataifa ya kuhamasisha umma kuhusu tsunami, ambayo ni mawimbi makubwa ya maji yatokanayo na tetemeko chini ya bahari. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres katika ujumbe wake anasema pamoja na kukumbuka waliopoteza maisha kwa tsunami miaka 20 iliyopita, tunaahidi tena kulinda zaidi ya watu milioni 700 duniani kote walio hatarini kukumbwa na Tsunami.Mashinani tutaelekea Sudan kusini kuangazia harakati za Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa Kulinda Amani nchini humo, UNMISS za kuimarisha ulinzi wa wanawake katika migogoro na majanga.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula duniani, (WFP) leo kwa mara nyingine tena limetahadharisha kwamba bila msaada wa kibinadamu nchini Sudan, mamia ya maelfu wanaweza kufa kwa njaa. Vita vya kikatili nchini Sudan vimesababisha janga kubwa zaidi la njaa duniani, imeandika WFP katika ukurasa wake wa X leo Oktoba 28 na kufafanua zaidi kwamba mtu mmoja kati ya watu wawili nchini humo anatatizika kupata mlo kila siku.WFP inaeleza kuwa njaa imethibitishwa Kaskazini mwa Darfur na mahitaji ya kibinadamu ni makubwa sana.Kabla ya taarifa hii ya leo ya WFP, jana kupitia pia ukurasa wa mtandao wa X, Mkurugenzi Mtendaji wa shirika hilo, Cindy McCain ambaye hivi karibuni alikuwa Sudan mojawapo ya maeneo yenye njaa zaidi duniani, ambapo watu milioni 25 wanakabiliwa na njaa kali ameandika kwamba WFP iko Sudan inatoa msaada wa kuokoa maisha lakini wanahitaji kwa haraka mambo matatu ambayo ni kuwafikia watu ili kuwasaidia, misaada kuweza kupita katika kila kivuko na usaidizi zaidi wa kimataifa kwa Wasudani walio katika mazingira hatarishi.Kwa miaka mingi, Sudan imekuwa ikisumbuka na migogoro. Mgogoro wa hivi karibuni zaidi, ulioanza Aprili mwaka jana 2023, umezua janga baya zaidi duniani la watu kuhama makwao na janga kubwa zaidi la njaa duniani linalosambaa Sudan, Sudan Kusini na Chad.
Wakimbizi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC wanaendelea kukimbilia Uganda kukwepa machafuko nchini mwao, huku rasilimali zikikaribia kikomo. Ameonya Kamishina mkuu wa shirika la Umoja wa Mtaifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR, Filippo Grandi, akiwa ziarani nchini Uganda hivi karibuni kwenye kambi inayohifadhi wakimbizi wa DRC na kutoa wito kwa jamii ya kimataifa kuongeza msaada.Wakimbizi wanaokimbia mzozo nchini DRC wanashuhudia matukio ya kutisha ya mauaji na ubakaji amesema Grandi, alipotembelea kambi ya ......aliyetembelea kambi za wakimbizi, Uganda na kusimuliwa hadithi za uchungu mkubwa“Sijawahi kusikia simulizi za machungu na hofu kama hizi za mauaji, ubakaji wa watoto mbele ya mama zao, wanawake wajawazito kukatwa vipande na makundi yenye silaha, na hofu kutawala maeneo yote ya Mashariki mwa Congo.”Kutokana na hali hii, Grandi anasema amani ndiyo inahitajika zaidi kwa sasa ili kumaliza dhuluma zinazowakumba wakimbizi wa Congo.“Ni wakati sasa jamii ya kimataifa ijitolee kwa dhati kusaidia Congo kutoka kwenye hali hii. Nilifanya kazi kama afisa wa eneo zaidi ya miaka 30 iliyopita Mashariki mwa Congo, na hali haijabadilika kimsingi.”Uganda inahifadhi jumla ya wakimbizi...... wengi wakiwa kutoka DRC, Sudan na Sudan Kusini.