POPULARITY
Hii leo tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini Kenya, katika Kijiji cha Embulbul kilichoko Kaunti ya Kajiado, ambako Shirika lisilo la kiserikali la Tulivu Safe Haven, lililoanzishwa kwa kushirikiana na wadau wakiwemo mashirika ya Umoja wa Mataifa, linatekeleza hatua mbalimbali za kuwasaidia wanawake. Hii ni pamoja na kuwaokoa na kuwahifadhi manusura wa ukatili wa kijinsia kwa kuwapatia makazi salama, ushauri nasaha, msaada wa kisheria na uwezeshaji wa kiuchumi, sambamba na kuwarejesha shuleni wasichana walionusurika. Je, nini kinafanyika? Kupitia video iliyoandaliwa na Redio washirika wetu Domus, Feissal Kirwa amefuatilia simulizi za manusura na kutuandalia makala hii. Pia tunakuletea muhtasari wa habari.Maabara tembezi ya kupima virusi vya Ebola imewekwa katika mji wa mpakani wa Kasenyi ulioko kati ya Uganda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC ambako kuna hatari kubwa ya kushamiri kwa mlipuko wa Ebola kutokana na harakati nyingi za safari. Dkt. Olga Ntumba kutoka WHO ambayo inafadhili maabara hiyo inayotoa majibu ndani ya saa moja, amesema “virusi haviheshimu mipaka. Maabara hii ina mchango muhimu kubaini mapema wagonjwa, kuimarisha ufuatiliaji wa ugonjwa, kubadilishana taarifa na juhudi za mwitikio kwenye ukanda mzima.”Mioto ya nyika ikiendelea kutikisa maeneo ya kaskazini mwa dunia shirika la Umoja wa Matiafa la Afya duniani, WHO limekumbusha kuwa moshi utokanao na mioto hiyo ya nyika huvuka taifa, kanda na hata mabara na kuwa na madhara kwa watu hata wanaoishi mbali na moto wenyewe. Hivyo limetangaza mambo tisa ya kuzingatiwa ikiwemo kusikiliza taarifa za mamlaka kama vile viwango vya uchafuzi wa hewa, kuvaa barakoa na kusalia ndani ya nyumba na kufunga madirisha iwapo hujashauriwa kuhama.Na wiki ya kimataifa ya unyonyeshaji watoto maziwa ya mama ikianza kesho Agosti Mosi, Umoja wa Mataifa kupitia mashirika yake, lile la afya, (WHO) na la kuhudumia watoto, (UNICEF) umetaka nchi kuimarisha mifumo ya afya ili iweze kupatia akina mama na watoto wachanga msaada wa kufanikisha unyonyeshaji bora ambao ni msingi wa ukuaji bora wa mtoto na afya ya mama anayenyonyesha. Halikadhalika utekelezaji wa kanuni ya kimataifa kuhusu matangazo ya bidhaa za mbadala wa maziwa ya mama.Mwenyeji wako ni Anold Kyanda, karibu!
Part 5 of 5: On the 22nd of December 2025, Republican appointed federal Judge Roger Benitez (Cuban ethnicity) struck down the Democrat mandated lying to parents in the K-12 school system. We covered it beginning in late December 2025 and in a second episode in late January 2026. The third episode was 17 March 2026 and the last one before this one, the 4th episode, was 8 April 2026. Unusual behavior or conduct of a student at school isn't grounds for a violation of Constitutional rights, Benitez held in Mirabelli v. Olson (Filed 22 Dec 2025), available here : https://cdn.prod.website-files.com/63d954d4e4ad424df7819d46/6949e11ea6bae817c8eaf637_Dkt%20%20307_MSJ%20Order.pdf Part 5. We cover from page 38 through to the end today. This episode concludes with a Chaplain's corner prayer time thanking the Lord for Roger Benitez and asking for wisdom for the future. The Chaplain's corner includes a reading from Psalm 15 NIV and Streams in the Desert 2 Feb (Cowman Publications Lost Feliz Station Lost Angeles Calif). The Republican Professor is a pro-anti-tax-funded-abuse-of-parents podcast. The Republican Professor is produced and hosted by Dr. Lucas J. Mather, Ph.D.
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina. Huko DRC madini ya kimkakati mashariki mwa nchi yamekuwa kichocheo cha mizozo. Mgeni wetu leo pamoja na mambo mengine anaangazia jinsi vita imezuia wao kuendelea na uchimbaji madini. Yeye anaishi Goma, lakini Salama Machaano, wa redio washirika wetu, Adventista World Radio, Tumaini Mkuu iliyoko Bukavu, jimboni Kivu Kusini alifnga safari hadi Goma kuzungumza naye.Pia tunakuletea muhtasari wa habari.Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa leo limekuwa na mjadala wa wazi wa ngazi ya juu kuhusu “Utawala wa rasilimali za asili: Msingi wa amani, usalama na ustawi” chini ya kipengele cha ajenda ya “Kudumisha amani na usalama wa kimataifa.” Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres akihutubia kikao hicho ameeleza vipaumbele vinne kuwa ni kuhakikisha manufaa ya haki yanapatikana kutokana na rasilimali za asili, kuimarisha uwazi na ushirikiano ili kukabiliana na biashara haramu, kukuza utatuzi wa amani wa migogoro inayohusiana na rasilimali, na kuzingatia masuala ya mabadiliko ya tabianchi katika kuzuia migogoro na kujenga amani.Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto, UNICEF, limetoa wito wa kulindwa kwa raia na kuruhusiwa kwa misaada ya kibinadamu kuwafikia wenye uhitaji nchini Sudan baada ya shambulio lililotekelezwa juzi tarehe 20 Julai kwa kutumia ndege zisizo na rubani likilenga soko la Ar Rahad katika jimbo la Kordofan Kaskazini na kusababisha vifo vya watoto wawili na kuwajeruhi wengine sita.Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji (IOM) limeeleza kusikitishwa sana na taarifa kwamba makumi ya wahamiaji wamefariki dunia au hawajulikani walipo kufuatia kuzama kwa meli katika pwani ya Mauritania, ambapo tarehe 18 Julai manusura 38 waliokolewa na Walinzi wa Pwani wa Mauritania karibu na mji wa Nouadhibou walipokuwa wakijaribu bahati yao kuelekea nchini Hispania. IOM kupitia Mkurugenzi wake wa Kanda ya Afrika Magharibi na Kati, Sylvia Ekra, imesema watu wanaendelea kuhatarisha maisha yao kwa sababu zinazowasukuma kuondoka katika nchi zao bado zipo.Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili, na mchambuzi wetu ni Dkt. Josephat Gitonga, ambaye ni Mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi, kwenye kitivo cha Tafsiri na Ukalimani anafafanua maana ya methali “MAJI HAYAPOZI MOYO ILA YAKIWA BARIDI.”Mwenyeji wako ni Feissal Kirwa, karibu!
Katika kujifunza lugha ya Kiswahili, na mchambuzi wetu ni Dkt. Josephat Gitonga, ambaye ni Mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi, kwenye kitivo cha Tafsiri na Ukalimani anafafanua maana ya methali “MAJI HAYAPOZI MOYO ILA YAKIWA BARIDI.”
Dkt. Rugakingira kutoka Hospitali ya Benjamin Mkapa, Dodoma anatupitisha kwenye huduma hii iliyojizolea umaarufu ya upandikizaji wa uume kwa wanaume wenye changamoto za uzazi. Amejibu kuhusu nani anaweza kupandikiziwa uume, gharama na matarajio baada ya huduma.Support the showMsemaji Mkuu wa Serikali
Сотый выпуск DevOps Kitchen Talks! Мы на YouTube шесть лет, и вот он, сотый выпуск. А в гости пришёл Денис Астахов, автор канала ADV-IT, у которого в конце июля свой юбилей: десять лет каналу. Получился кухонный разговор авторов двух образовательных каналов, разговор обо всём и ни о чём. Про технику сегодня почти ничего, зато про ремесло, мотивацию и жизнь. О ЧЁМ ВЫПУСК • Как Денис начал канал в 2016-м: пять уроков Python за раз, вдохновение от thenewboston, работа в Intel. • «Знаменитая кухня» DKT: провальные студии и почему запись переехала домой. • Почему самый популярный ролик за 10 лет не про DevOps, а про SSD-диски. • Мотивация и выгорание за десять лет ведения канала. • Честно про монетизацию: падение роста в 10 раз и сколько реально приносит канал на 140к подписчиков. • AI в обучении и найме: можно ли выучить DevOps через нейросеть и не отупеть от копипаста. • Стоит ли сейчас заводить технический YouTube и что для этого нужно. ГОСТЬ Денис Астахов, автор канала ADV-IT (AWS, DevOps, Terraform, Kubernetes, облака). AWS Hero. 10 лет на YouTube. ADV-IT: https://www.youtube.com/@ADV-IT 100 ВЫПУСКОВ Это наш юбилейный сотый выпуск. Скоро проведём праздничный стрим, следите за анонсами в Telegram. ССЫЛКИ
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka katika mkutano wa HLPF hapa makao makuu ya UN kumsikia Profesa Peter Wanderi Mwangi ambaye amewakiwakilisha Chuo Kikuu cha Mount Kenya cha nchini Kenya chenye matawi mbalimbali katika Afrika Mashariki katika mkutano wa United Nations Academic Impact (UNAI), Mpango unaosisitiza nafasi muhimu ya taasisi za elimu ya juu katika kuhimiza maendeleo endelevu na kuunga mkono utekelezaji wake. Baada ya ziara yake mjini Bunia, jimboni Ituri nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC ambako ndio kitovu cha mlipuko wa sasa wa Ebola ya virusi vya Bundibugyo, Mkurugenzi Mtendaji wa WHO anayehusika na Programu ya Dharura za Afya, Dkt. Chikwe Ihekweazu, amewambia waandishi wa habari Geneva, Uswisi kwamba mlipuko wa sasa ni moto ambao kinachouchochea kiko katikati, huku ukiendelea kusambaa.Shirika la Umoja wa Mataifa la Masuala ya Bahari (IMO) limesema lina wasiwasi mkubwa kufuatia mashambulizi ya jana usiku yaliyolenga meli kwenye mlango wa bahari wa Hormuz na viunga vyake na kusababisha vifo vya takribani mabaharia wawili na wengine kadhaa wamejeruhiwa. Kupitia taarifa yake iliyotolewa London, Uingereza, IMO imesema inafanya kazi kwa haraka na mamlaka husika ili kubaini mazingira halisi ya tukio hilo.Na uungwaji mkono wa umma kwa wakimbizi unaendelea kuwa imara licha ya kuwepo kwa changamoto na kutokuweko kwa uhakika wa mustakabali duniani, hii ni kwa mujibu wa utafiti wa pamoja uliofanywa na kampuni ya IPSOS na shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi, UNHCR, Utafiti umebaini kuwa asilimia 66 ya washiriki katika nchi 29 wanakubaliana kwamba watu wanaokimbia vita au mateso wanapaswa kuruhusiwa kusaka hifadhi katika nchi nyingine, ikiwa ni punguzo la asilimia moja tu ikilinganishwa na mwaka 2025.Utafiti huu umefanywa ikiwa ni miaka 75 tangu kupitishwa kwa Mkatab awa Kimataifa wa kulinda wakimbizi.Mwenyeji wako ni Feissal Kirwa, karibu!
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina na leo tunakwenda Afrika Mashariki hususan nchini Tanzania katika visiwa vya Zanzibar. Tunamulika jinsi serikali ya Zanzibar kwa ushirikiano na shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo nchini humo, UNDP wanaboresha huduma za utalii kwa kutumia Akili Mnemba au AI. Ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa imeonya kuwa kupunguzwa kwa misaada rasmi ya maendeleo tangu Januari 2025 kumesababisha takribani wanawake na wasichana milioni moja duniani kupoteza huduma muhimu katika nchi zilizoathiriwa na migogoro. Ikitolewa leo Geneva, Uswisi na New York, Marekani na shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia masuala ya wanawake, UN Women, ripoti hiyo iliyopatiwa jina ‘Zaidi ya Kiwango cha Kuvumilika' miongoni mwa changamoto ilizozitaja ni pamoja na kuwa asilimia 84 ya mashirika ya wanawake yameripoti kuongezeka kwa mahitaji ya huduma, lakini takribani asilimia 90 ya mahitaji hayawezi tena kuyakidhi na kwamba mashirika mawili kati ya matano yanatarajia kufungwa ndani ya mwaka mmoja kutokana na ukosefu wa fedha.Huko Sudan, nchi inayoumia kwa vita kwa miaka minne sasa, kumetangazwa mlipuko mpya wa ugonjwa wa kipindupindu hali inayozidisha wasiwasi kuhusu usalama wa jamii zilizo hatarini, hususan katika mji wa El-Obeid uliozingirwa, ambako mashambulizi ya kila siku ya ndege zisizo na rubani yanaendelea kuzuia upatikanaji wa misaada ya kibinadamu. Dkt. Shible Sahbani, Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani (WHO) nchini Sudan akizungumza kwa njia ya video na waandishi wa habari leo mjini Geneva, uswisi amesema, “tumerekodi zaidi ya wagonjwa 1,330 wa kipindupindu, huku watu 114 wakifariki dunia kutokana na ugonjwa huo. Hii inaonesha kiwango cha vifo miongoni mwa wagonjwa wa kipindupindu cha asilimia 13.7, ambacho ni cha juu sana. Na bila shaka, msimu wa mvua unaotarajiwa utaifanya hali kuwa mbaya zaidi.”Na utafiti wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni, UNESCO kuhusu Ufuatiliaji wa Elimu Duniani, umeonesha kuwa misaada ya kimataifa kwa sekta ya elimu imeendelea kupungua na nchi 113 duniani zinatumia fedha nyingi kulipa madeni kuliko pesa wanazoziwekeza kwenye elimu. Matokeo ya utafiti huo yamewekwa wazi leo mbele ya viongozi kutoka nchi mbalimbali wanaohudhuria Mkutano wa Mageuzi ya Elimu TES+4 unaofanyika Paris, Ufaransa ili kufuatilia utekelezaji wa maazimio ya mkutano wa kwanza wa Mageuzi ya Elimu uliofanyika mwaka 2022 na pia ili kusongesha zaidi ufikiaji wa Lengo namba 4 la Maendeleo Endelevu linalohusu Elimu Bora.Mwenyeji wako ni Feissal Kirwa, karibu!
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina leo ikiwa ni siku ya kimataifa ya lugha ya Kiswahili nampisha John Kibego wa redio washirika, Kazi Njema Redio nchini Uganda, kukueleza kuhusu harakati za kukuza lugha hiyo barani Afrika wakati huu ambapo UNESCO imeshaitangaza miaka mitano iliyopita kuwa lugha ya kimataifa.John, anamulika mpango wa ujenzi wa makao makuu ya kamisheni ya Kiswhaili ya Mungano wa Afrika. Pia tunakuletea muhtasari wa habari.Ikiwa leo ni maadhimisho ya tano ya Siku ya Kimataifa ya Lugha ya Kiswahili chini ya Kaulimbiu "Kiswahili kwa Amani, Mshikamano na Diplomasia ya Uchumi wa Dunia" Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Togolani Mavura anafafanua ni kwa namna gani lugha ya Kiswahili inaweza kuyafanikisha hayo.Ugonjwa wa Ebola umeendelea kusambaa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC na idadi ya vifo vya watu imevuka 500 limesema leo Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani, WHO. Mwakilishi wa WHO nchini humo, Dkt. Anne Ancia akizungumza kwa njia ya video kutoka Bunia, mji mkuu wa Jimbo la Ituri mashariki mwa DRC ambako ni kitovu cha mlipuko huu, amewaambia waandishi wa habari mjini Geneva, Uswisi kwamba kufikia tarehe 4 mwezi huu, serikali ya nchi hiyo ilikuwa imerekodi wagonjwa 1,561, vikiwemo vifo 506. Taarifa njema ni kuwa…“Jaribio la kitabibu lilianza tarehe 2 Julai kwa lengo la kubaini tiba madhubuti dhidi ya ugonjwa huo unaosababishwa na virusi vya Bundibugyo.”Na asubuhi hii kwa saa za New York Marekani, kwa mara ya 34 tangu mwaka 1992, Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa limekaa ili kujadili umuhimu wa kumaliza vikwazo vya kiuchumi na kibiashara vilivyowekwa na Marekani dhidi ya Cuba tangu mwaka 1960. Katika barua ya mwaliko ambayo Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Annalena Baerbock amewapelekea wajumbe wa Baraza anasema, “ninayo heshima kukujulisha kwamba nimepokea barua iliyoambatanishwa ya tarehe 16 Juni 2026 kutoka kwa Mhe. Bwana Ernesto Soberón Guzmán, Mwakilishi wa Kudumu wa Cuba katika Umoja wa Mataifa, akiomba kuitishwa kwa kikao cha Baraza Kuu ili kujadili ajenda namba 38 yenye kichwa: “Umuhimu wa kukomeshwa kwa vikwazo vya kiuchumi, kibiashara na kifedha vilivyowekwa na Marekani dhidi ya Cuba.”Mwenyeji wako ni Feissal Kirwa, karibu!
Katika kujifunza lugha ya Kiswahili na hii leo Dkt. Mwanahija Ali Juma, Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili, Zanzibar nchini Tanzania, BAKIZA anafafanua maana ya neno "MKUNGURU."
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayokupeleka mjini Caracas nchini Venezuela, mshikamano na raia wa nchi hiyo wadhihirika wakati huu wakiwa kwenye majonzi baada ya matetemeko ya ardhi kukumba wananchi. Pia tunakuletea muhtasari wa habari kama zifuatazo.Nchini Venezuela Mashirika ya Umoja wa Mataifa yanaendelea kutoa msaada kufuatia matetemeko mawili ya ardhi yaliyolikumba taifa hilo wiki iliyopita. Mathalani, Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani, WFP, limeripoti leo kwamba tayari limetoa zaidi ya tani elfu tatu za chakula, kiasi kinachotosha kusaidia familia zaidi ya elfu kumi kwa kipindi cha miezi miwili.”Huko mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia Congo DRC, raia wameelezea haki zao zinazokiukwa ikiwemo kuzuiwa kupatiwa misaada ukatili wa kingono na mauaji. Maelezo hayo yamo kwenye ripoti iliyotolewa leo na Tume Huru ya Umoja wa Mataifa inayochunguza hali ya haki za binadamu katika majimbo ya Kivu Kaskazini na Kivu Kusini, ikiwa ni ripoti yao ya kwanza mbele ya Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa mjini Geneva, Uswisi?”.Na, michuano ya Fainali ya Kombe la Dunia la Mpira wa Miguu inaendelea huku dunia ikishuhudia ongezeko la joto kali. Katika juhudi za kulinda wachezaji, wafanyakazi na mashabiki dhidi ya athari za joto, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya duniani WHO, Dkt. Tedros Adhanom Ghebreyesus amesema “WHO tunashirikiana na FIFA na nchi zinazoandaa michuano hiyo katika kampeni iitwayo Beat the Heat inayolenga kuweka mipango ya utekelezaji, kutoa elimu kwa wananchi, kuanzisha mifumo ya tahadhari za mapema, kuboresha upatikanaji wa maji salama ya kunywa, pamoja na kuweka maeneo ya kujipooza.”Mwenyeji wako ni Rashid Malekela, karibu!
Katika kujifunza lugha ya Kiswahili, tunasalia huko huko Nairobi Kenya kwani leo mchambuzi wetu ni Dkt. Josephat Gitonga, ambaye ni Mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi, kwenye kitivo cha Tafsiri na Ukalimani anafafanua maana ya methali “Lengelenge lako si jipu langu”.
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayokupeleka jijini Nairobi nchini Kenya ambako kunafanyika Mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu Usimamizi wa Matumizi ya Intaneti, IGF, mahususi kwa bara la Afrika pekee, AfIGF. Stella Vuzo, Afisa Habari wa UNIS Nairobi, Kenya amezungumza na mmoja wa vijana washiriki na kukuletea maoni yake.Idadi ya waliokufa kwenye matetemeko mawili makubwa ya ardhi yaliyokumba Venezuela wiki hii ikiongezeka na kufikia 235, afisa wa shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji IOM nchini humo Luis Segovia akizungumza kutoka mji mkuu Caracas baada kusambaza vifaa vya dharura kwa familia amesema, “leo, IOM itaendelea kufanya kazi kwa karibu na mamlaka husika pamoja na washirika wa kibinadamu ili kuhakikisha msaada unawafikia kwa wakati wale wanaouhitaji zaidi.”Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, waambata wa wagonjwa au watu waliokufa kwa Ebola wakishindwa kusalia kwenye karantini ili kudhibiti kusambaa kwa ugonjwa huo, David Stevenson, Mwakilishi Mkazi wa shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula WFP kupitia ukurasa wa X amesema ni muhimu kuongeza usaidizi wa shirika hilo ili liweze kutoa mgao zaidi kwa wahitaji waliko, akitoa mfano wa swali alilosema rahisi lakini chungu kutoka kwa mkimbizi wa ndani Jack aliyefiwa na mwanae kwa Ebola na mkewe yuko karantini, na sasa analea watoto 13 kwa msaada wa mgao wa chakula kutoka WFP. “Kwa watoto wote hawa, mgao huu wa chakula wa mwezi mmoja utadumu kwa wiki mbili tu. Na baada ya hapo, nitawalishaje ilhali sina njia yoyote ya kufanya hivyo?”.Ripoti ya mwaka huu wa 2026 kuhusu dawa za kulevya na uhalifu imeonya kuhusu ongezeko la dawa mpya za kutengenezwa maabara huku maendeleo ya teknolojia yakiwezesha wasafirishaji kukwepa kubainika. Mkurugenzi Mtendaji wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kudhibiti Dawa za Kulevya na Uhalifu, (UNODC) Monica Juma, amesema dunia inashuhudia ongezeko ambalo halijawahi kutokea la aina mpya za dawa za kulevya, huku baadhi zikiwa na nguvu na hatari zaidi kuliko zilizokuwepo awali.Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili, tunasalia huko huko Nairobi Kenya kwani leo mchambuzi wetu ni Dkt. Josephat Gitonga, ambaye ni Mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi, kwenye kitivo cha Tafsiri na Ukalimani anafafanua maana ya methali “Lengelenge lako si jipu langu”.Mwenyeji wako ni Feissal Kirwa, karibu!
Katika kujifunza lugha ya Kiswahili, leo mchambuzi wetu ni Dkt. Josephat Gitonga, ambaye ni Mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi nchini Kenya kwenye kitivo cha Tafsiri na Ukalimani anafafanua maana ya methali “Lililo lujani ni la lusu”.
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina. Kesho kutwa Alhamisi ya Juni 11, macho na masikio yanaelekezwa Mexico, Canada na hapa Marekani kwa ajili ya fainali za kombe la dunia kwa mpira wa miguu, au soka al maarufu kabumbu. Ingawa hivyo zama za sasa za mchezo huo maarufu zaidi duniani zinakumbwa na madhara ya athari za mabadiliko ya tabianchi. Ongezeko la joto kali linavuruga mechi na kuzua wasiwasi kuhusu mustakabali wa mchezo huo. Ni kwa kuzingatia hilo, Sekretarieti ya Mkataba wa Kimataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi, UNFCCC inamulika suala hilo na kutoa mapendekezo ya nini kifanyike kwani hivi sasa madhara ya joto kali kwenye kabumbu ni dhahiri. Feissal Kirwa anamulika hilo kupitia video iliyoandaliwa na UNFCCC.Pia tunakuletea muhtasari wa habari na jifunze Kiswahili.Takriban watoto milioni 138 duniani kote bado wako katika ajira za watoto, wakiwemo watoto milioni 54 wanaofanya kazi hatarishi. Hayo yamo katika ripoti mpya iliyotolewa leo na Shirika la Kazi la Umoja wa Mataifa ILO. Katika ujumbe wakwe kwenye ripoti hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa ILO, Gilbert F. Houngbo, ametoa wito wa kuchukuliwa hatua za haraka ili kubadili hali hii.“Habari njema ni kwamba hadi sasa tuna wagonjwa 19 ambao wamepona, hivyo utambuzi wa mapema na matibabu vinaokoa maisha,” Huyo ni Mkurugenzi wa Operesheni za Tahadhari na Hatua za Dharura za Afya wa Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa Duniani (WHO), Dkt. Abdirahman Mahamud, akizungumza na waandishi wa habari mjini Geneva leo kwa njia ya video kutoka Bunia katika Jimbo la Ituri, nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, jimbo ambalo linachangia asilimia 94 ya wagonjwa wote wa Ebola.Mkutano wa 19 wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Haki za Watu Wenye Ulemavu CRPD, umeanza leo Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York na utaendelea hadi 11 Juni. Kaulimbiu ya mwaka huu ni “kuadhimisha miaka 20 ya mkataba huo na kuimarisha utekelezaji wake katika dunia inayobadilika.” Washiriki wanajadili namna ya kutokomeza ukandamizaji, ukatili na manyanyaso dhidi ya watu wenye ulemavu, kuimarisha mifumo ya huduma na msaada, pamoja na kuongeza ushiriki na uwakilishi wao katika maisha ya kisiasa na umma.Katika kujifunza lugha ya Kiswahili hii leo Dkt Mwanahija Ali Juma, Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili, Zanzibar nchini Tanzania, BAKIZA anafafanua maana na matumizi ya neno "MKWARUZO."Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
Katika kujifunza lugha ya Kiswahili hii leo Dkt. Mwanahija Ali Juma, Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili, Zanzibar nchini Tanzania, BAKIZA anafafanua maana na matumizi ya neno "MKWARUZO."
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inatupeleka nchini nchini Rwanda. Kufuatia changamoto zinazoongezeka kutokana na mabadiliko ya tabianchi, kupanda kwa gharama za mbolea na ushindani wa masoko ya kikanda, Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo FAO linashirikiana na nchi ya Rwanda kutekeleza mkakati mpya wa kuimarisha sekta ya chai lengo likiwa ni kuboresha zao hilo na kuinua pato la mkulima.Mlinda amani wa Umoja wa Mataifa anayehudumu nchini Lebanon amefariki dunia na wengine wawili wamejeruhiwa mapema leo Alhamisi baada ya makombora ya mizinga kulenga eneo lao la kazi karibu na Marjayoun kusini mashariki mwa nchi hiyo, imesema taarifa ya Kikosi cha Mpito cha Umoja wa Mataifa nchini Lebanon UNIFIL. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anatarajiwa kutoa taarifa kuhusu tukio hilo muda wowote kuanzia sasa.Shirika la Umja wa Mataifa la afya Duniani, WHO, limesema chakula kisicho salama kinaendelea kuwa tishio kubwa kwa afya ya umma duniani, kikisababisha takribani wagonjwa milioni 866 na vifo milioni 1.5 kila mwaka, huku watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano wakiwa katika hatari kubwa zaidi. Kwa mujibu wa ripoti mpya watoto hao wadogo, ambao ni asilimia 9 tu ya idadi ya watu duniani, wanachangia karibu theluthi moja ya magonjwa yote yanayosababishwa na chakula.Leo ni siku ya watoto wasio na hatia waathirika wa ukatili duniani, maadhimisho haya yanakuja wakati ambapo ripoti ya Mwaka ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Watoto na Migogoro ya Silaha inaonesha kwamba ukatili dhidi ya watoto katika migogoro ya silaha ulifikia viwango visivyo vya kawaida mwaka 2024, huku kukiwa na ongezeko la asilimia 25 la ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu ikilinganishwa na mwaka uliopita.Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili, leo mchambuzi wetu ni Dkt. Josephat Gitonga, ambaye ni Mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi nchini Kenya, kwenye kitivo cha Tafsiri na Ukalimani anafafanua maana ya methali “La kiliwacho kisicholiwa ni sumu”."Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!
Katika kujifunza lugha ya Kiswahili, leo mchambuzi wetu ni Dkt. Josephat Gitonga, ambaye ni Mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi nchini Kenya, kwenye kitivo cha Tafsiri na Ukalimani anafafanua maana ya methali “La kiliwacho kisicholiwa ni sumu”
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina maalumu ambapo tunamwangazia mmoja wa maafisa waandamizi wa Umoja wa Mataifa, Joyce Msuya. Mwisho wa wiki hii, Joyce, raia wa Tanzania ambaye pia amewahi kuhudumu katika Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo, UNEP na pia Benki ya Dunia anahitimisha utumishi wake katika Umoja wa Mataifa akiwa Msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika masuala ya kibinadamu na pia Naibu wa Mkuu wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Misaada ya Kibinadamu (OCHA). Katika mazungumzo haya na Anold Kayanda wa Idhaa hii, Joyce Msuya anaanza kwa kuitafari miaka minne aliyohudumu katika nafasi hii.Jamhuri ya Kidemokrasia Congo DRC inakumbwa na ugonjwa wa Ebola ambapo Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya duniani WHO, Dkt. Tedros Adhanom Ghebreyesus amefika huko na anaeleza sababu. ‘Nimefika hapa kuzieleza jamii za Ituri, Kivu Kaskazini na Kivu kusini kuwa hawako pekeyao, na kwamba tupo hapa kuwaunga mkono, na tunaelewa machungu yao, lakini pia tunafahamu wana nguvu na yote yanayohitajika kukomesha hili. Ninatumia fursa hii kuziomba jumuiya za kimataifa kuongeza usaidizi wao ili wahudumu wa afya waweze kupata vifaa tiba na vya kujilinda na maambukizi.'Kupigwa marufuku watoto kutumia mitandao ya kijamii, si suluhisho la mara moja kwa suala mtambuka lenye sura nyingi, ndio maana hii leo Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa Volker Türk ametaka hatua kali zichukuliwe na kila nchi, pamoja na makampuni ya teknolojia, ili kufanya mitandao ya kijamii kuwa salama zaidi kwa watoto, akisisitiza udhibiti, usimamizi na uwajibikaji unaofaa. Kamishna Türk amesema "Kuimarisha ulinzi wa watoto mtandaoni ni kipaumbele cha dharura ambacho tunahitaji kuhakikisha sio tu kwamba kinafanyika, bali pia kinafanyika ipasavyo,".Na ukatili wa kingono kwenye maeneo yenye migogoro ulifurutu ada mwaka 2025, hii inamanisha kuna ongezeko kubwa la ukatili wa kingono huku wanawake na wasichana ndio idadi kubwa ya waliokumbwa na madhila hayo yaliyohusisha pia waathirika hao kuuawa baada ya kubakwa. Haya yamebainika kwenye ripoti ya ukatili wa kijinsia unaohusiana na migogoro iliyotolewa na Umoja wa Mataifa leo ambayo pia imeonya kuwa kuongezeka kwa matumizi ya kijeshi duniani na kupungua kwa bajeti za misaada ya kibinadamu kulidhoofisha uwezo wa serikali na taasisi kuzuia na kuchunguza ukatili huo wa kingono. Ripoti hiyo imetoa wito wa kuchukuliwa hatua madhubuti zaidi za kimataifa pamoja na kuhakikisha upatikanaji endelevu wa fedha ili kulinda raia, na kuwasaidia manusura wa ukatili wa kingono unaohusiana na migogoro.Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayomulika nchi zinazochangia vikosi vya kulinda amani vya Umoja wa Mataifa, ikiwa ni pamoja na Taifa la Tanzania na Balozi Togolani Idriss Mavura mara baada ya kuwasilisha hati zake za utambulisho kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amezungumza na Flora Nducha kuhusu suala hili muhimu.“Nataka niwe mkweli; hii ni moja ya changamoto zetu kubwa zaidi. Hatuwezi kufanya kazi hii kama wale wanaojaribu kusaidia wanazuiwa kufanya hivyo, au kuwekwa katika hatari.” Ni sehemu ya barua ya Dkt. Tedros Ghebreyesus, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ulimwenguni, WHO, aliyowaandikia wananchi wa Jamhuri ya Kidemorkasia ya Congo, DRC wakati huu vikwazo kama vile mapigano jimboni Ituri, yanakwamisha harakati za kudhibiti mlipuko wa 17 wa Ebola nchini humo.Vikwazo vingine vya kudhibiti Ebola nchini DRC ni mila. Maki Baraka mkazi wa Beni jimboni Kivu Kaskazini ambako Ebola imeripotiwa mji jirani wa Butembo ana wito.Na Joyce Msuya, Naibu Mkuu wa Ofisi ya UN inayoratibu misaada ya dharura, OCHA anatamatisha jukumu lake baada ya kuhudumu kwa miaka minne. Anold Kayanda amemuuliza anachokumbuka zaidi.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
Send us Fan MailRais wa Rwanda, Mhe. Paul Kagame, amefanya ziara ya siku moja nchini Tanzania, akizungumza na mwenyeji wake, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kuhusu ushirikiano na kukuza uchumi wa pande zote, Mei 3, 2026.Viongozi hawa walikubaliana kuendelea kukuza biashara na uwekezaji kwa kuondoa vikwazo vya kikodi, ili kunufaika na masoko ya kikanda ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na Eneo Huru la Biashara la Afrika (AfCFTA).Support the showIdara ya Habari MAELEZO
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka katika nchi za Afrika Mashariki ambazo zimezindua Siku ya Ziwa Victoria ambayo maadhimisho yake kwa mara ya kwanza yamefanyika tarehe 21 mwezi huu wa Mei huko Mwanza, kaskazini-magharibi mwa Tanzania. Lengo pamoja na mambo mengine ni kuimarisha vivutio vya utalii. Uzinduzi huu ulitanguliwa na jukwaa la wadau wa Bonde la Ziwa hilo lililohudhuriwa na wadau mbalimbali akiwemo Amon Manyama, Mkurugenzi wa Miradi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo, UNDP, nchini Tanzania. Rashid Malekela wa Idhaa hii alituwakilisha na amezungumza naye.Pia tunakuletea muhtasari wa habari na ufafanuzi wa neno kama neno "PEKEPEKE."Mfuko wa dharura wa Umoja wa Mataifa UNCERF umetoa dola milioni 60 kusaidia muitikio wa kupambana na ugonjwa wa Ebola nchini Jamhuri ya Kidemokrasia Congo DRC. Tayari vifaa tiba vimewasilishwa nchini humo na sasa Shirika la Umoja wa Mataifa la afya ulimwenguni WHO na wadau wengine wanaendelea na usaidizi ikiwemo kuweka vituo vya kuimarisha hatua za kuzuia maambukizi na kuhakikisha utunzaji salama wa wagonjwa..Mwakilishi wa mpya wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa Balozi Togolani Mavura amewasilisha rasmi nyaraka zake kwa katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres jijini New York Marekani na kueleza yale aliyokuja nayo.shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji IOM limesema fedha zinazotumwa nyumbani na watu waishio ughaibuni au diaspora sasa zimezidi kiwango cha fedha za misaada rasmi ya maendeleo na uwekezaji wa moja kwa moja kutoka nje. IOM imeeleza pia namna diaspora walivyo na msaada mkubwa wakati wa majanga kwa kutuma fedha haraka, huduma na usaidizi kupitia mitandao ya kuaminika katika nchi mbalimbali ikiwemo Somalia, Haiti, Ufilipino na Ukraine.Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili, hii leo Dkt. Mwanahija Ali Juma, Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili, Zanzibar nchini Tanzania, BAKIZA anafafanua maana na matumizi ya neno "PEKEPEKE."Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
Katika kujifunza lugha ya Kiswahili, hii leo Dkt. Mwanahija Ali Juma, Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili, Zanzibar nchini Tanzania, BAKIZA anafafanua maana na matumizi ya neno "PEKEPEKE."
Send us Fan MailRais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, akihutubia Kongamano la Biashara baina ya Tanzania na Kenya (Tanzania & Kenya Business Forum 2026), tarehe 04 Mei, 2026, JNICC, jijini Dar es Salaam ambapo kongamano hili lilihudhuriwa pia na Rais wa Jamhuri ya Kenya, Mhe. Dkt. William Samoei Ruto.Support the showIdara ya Habari MAELEZO
Katika kujifunza lugha ya Kiswahili, leo mchambuzi wetu ni Dkt. Josephat Gitonga, ambaye ni Mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi nchini Kenya, kwenye kitivo cha Tafsiri na Ukalimani anafafanua maana ya methali “Kware hutetemekea majanini.”
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina ambayo inamulika harakati za kudhibiti mlipuko wa Ebola zinaendelea huko DRC na Uganda. Maafisa wa WHO walipozungumza na waandishi wa habari huko Geneva, Uswisi walitoa ufafanuzi wa masuala kadhaa ikiwemo chanjo na nini cha kufanya ili jamii iwe kitovu cha udhibiti wa maambukizi.Hadi sasa Tani 30 za vifaa vya dharura vya kukabiliana na Ebola zimewasili Bunia, mashariki mwa DRC, ndani ya siku nne kwa msaada wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa MONUSCO. Vifaa hivyo ni pamoja na dawa, vifaa vya maabara, PPE na mahema ya kuhudumia wagonjwa. Wakati huo huo MONUSCO inaendelea kuelimisha wananchi kuhusu njia za kujikinga, huku WHO ikisema zaidi ya watu 600 wanashukiwa kuwa na Ebola na vifo 139 vinavyohusishwa na ugonjwa huo vimeripotiwa tangu mlipuko huo kuanza.Tukisalia na Ebola, Ili vifaa vya Ebola vifike kwa wakati, wako mashujaa nyuma ya pazia wanaohakikisha kila mzigo unasafiri salama. Miongoni mwao ni Milton Oloo, mwenye miaka 30 ya uzoefu wa kupakia mizigo JKIA nchini Kenya, ambaye sasa yuko mstari wa mbele kusaidia safari za ndege za Umoja wa Mataifa, UNHAS. “Tunachokifanya hapa leo ni kuhakikisha kwamba mizigo inayoelekea Congo DRC imepangwa vizuri na kupakiwa ipasavyo ili isiharibike. Pia naona fahari na Maisha ya watu yanayookolewa nafurahi”.Na jukwaa la 13 la miji dunini WUF13 linaelekea ukingoni Baku Azerbaijan likijadili changamoto ya makazi duniani, Rehema Kishoa kutoka Tanzania Mkurugenzi Msaidizi wa Uzingatiaji wa Mipango ya Matumizi ya Ardhi kutoka Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya ardhi anasema wao wamechukua hatua kukabili changamoto hiyo.Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili, leo mchambuzi wetu ni Dkt. Josephat Gitonga, ambaye ni Mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi nchini Kenya, kwenye kitivo cha Tafsiri na Ukalimani anafafanua maana ya methali “Kware hutetemekea majanini.”Mwenyeji wako ni Rashid Malekela, karibu!
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini Tanzania kwa Chama cha Wanawake Majaji, (TAWJA) ambacho kimetambua pengo la upatikanaji wa haki hususan kwa wanawake na wasichana na tunasikia hatua zinazochukuliwa kuziba pengo hilo kutoka kwa mwenyekiti wake, Barke Sehel ambaye ni Jaji wa Mahakama ya Rufaa. Pia tunakuletea mhtasari wa habari kama zifuatazo..Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la afya ulimwenguni WHO Dkt. Tedros Adhanom Ghebreyesus ametangazwa kwa mara nyingine kugundulika kwa virusi vya ugonjwa wa Ebola nchini Jamhuri ya Kidemokrasia Congo DRC katika jimbo la Ituri lililoko kaskazini mashariki mwa nchi hiyo. Hii ni mara ya 17 kwa mlipuko wa Ebola kutokea DRC tangu kugunduliwa kwa mara ya kwanza mwaka 1976. Wagonjwa 13 vimethibitishwa na taasisi ya utafiti wa tiba ya INRB mjini Kinshasa. Dkt. Tedros amesema tayari wametuma wataalamu, vifaa tiba na ameruhusu kutolewa kwa dola laki tano kusaidia kudhibiti mlipuko huo na kuwahudumia wagonjwa.Hali ya kibinadamu nchini Somalia inazidi kuwa mbaya kuliko ilivyotarajiwa hapo awali. Akuzungumza na waandishi wa habari mjini Geneva Uswisi afisa mkuu wa misaada wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia George Conway amesema “Hivi sasa Takriban watu milioni sita nchini Somalia amba ni sawa na mtu mmoja kati ya sita anakabiliwa na njaa ikimaanisha kuwa anaruka muda wa kula chakula, au anaenda siku kadhaa bila chakula cha kutosha. Watoto ndio wanaolipa gharama kubwa zaidi. Karibu watoto milioni mbili wana utapiamlo mkali, ikimaanisha kuwa wana utapiamlo mbaya na dhaifu kimwili, na hivyo kuwaweka katika hatari kubwa ya kuugua au kufa.”.Na leo ni siku ya Kimataifa ya Familia, Umoja wa Mataifa unasema maadhimisho ya mwaka huu yanaangazia jinsi umaskini, ukosefu wa huduma muhimu na msaada mdogo wa malezi vinavyoathiri familia na kudhoofisha maendeleo bora ya watoto. Maadhimisho ya mwaka huu yanaweka mkazo maalum kwenye hatua jumuishi za ulinzi wa kijamii kama vile ruzuku za watoto, likizo za uzazi zenye malipo, huduma nafuu za malezi ya watoto na elimu ya awali kwa watoto wadogo.Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!
Katika kujifunza lugha ya Kiswahili hii leo Dkt. Mwanahija Ali Juma, Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili, Zanzibar nchini Tanzania, BAKIZA anafafanua maana ya neno "MKUNGUNI."
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini Kenya kumsikia kijana ambaye baada ya kukosa ajira, alichagua kujiajiri kwa kuuza miwa na juisi yake, hatua iliyomwezesha kujipatia kipato na kupambana na umaskini. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na jifunze KiswahiliShirika la Afya la Umoja wa Mataifa Duniani WHO limesema abiria na wahudumu waliokumbwa na mlipuko wa hantavirus katika meli ya utalii iliyokuwa Bahari ya Atlantiki huenda waliambukizwa virusi hivyo kabla ya kupanda meli hiyo, ingawa maambukizi miongoni mwa watu ndani ya meli hayawezi kuondolewa kabisa licha ya kuwa ni nadra. Watu saba kati ya abiria na wahudumu 147 wameugua huku wengine wakifariki dunia.Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa Duniani WHO, linaadhimisha Siku ya Kimataifa ya Usafi wa Mikono hii leo 2026 chini ya kauli mbiu “Hatua Zinazookoa Maisha,” kikisisitiza haja ya kuimarisha uzuiaji wa maambukizi katika vituo vya afya. WHO inaonya kuwa maambukizi yanayotokana na huduma za afya bado ni tishio la kila siku katika hospitali na kliniki, yakichangia usugu wa dawa za viua vijasumu au antibiotiki, ongezeko la gharama, pamoja na vifo vinavyoweza kuzuilika.Leo Mei 5 ni Siku ya Kimataifa ya Wakunga, huku Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu na Afya ya Uzazi, UNFPA, likisema wakunga ni wadau muhimu katika huduma za afya ya uzazi duniani kote. Shirika hilo linasema dunia inahitaji wakunga milioni moja zaidi ili kuboresha huduma za afya na kuokoa maisha ya wanawake na watoto wachanga. Kwa mujibu wa UNFPA, wakunga wanahakikisha ujauzito na kujifungua salama, huku pia wakisaidia kupunguza mimba zisizotarajiwa, maambukizi ya VVU kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto na upasuaji usio wa lazima wakati wa kujifungua.”Katika kujifunza lugha ya Kiswahili, leo mchambuzi wetu ni Dkt. Josephat Gitonga, ambaye ni Mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi nchini Kenya, kwenye kitivo cha Tafsiri na Ukalimani anafafanua maana ya methali “Kwendako mema hurudi mema."Mwenyeji wako ni Rashid Malekela, karibu!
Katika kujifunza lugha ya Kiswahili, leo mchambuzi wetu ni Dkt. Josephat Gitonga, ambaye ni Mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi nchini Kenya, kwenye kitivo cha Tafsiri na Ukalimani anafafanua maana ya methali “Kwendako mema hurudi mema."
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina ambapo tunamsikia Dkt. Tulia Ackson, Rais wa Muungano wa Mabungeni duniani, (IPU) ambaye hivi karibuni akiwa makao makuu ya UN, Marekani aliongoza kikao kilichokuwa sehemu ya Mkutano wa CSW70. Mara baada ya kikao hicho Assumpta Massoi wa Idhaa hii ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa alizungumza naye masuala kadhaa ikiwemo yale waliyopatia kipaumbele ili kusongesha usawa wa kijinsia duniani.Karibu Dkt. Tulia.Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres hii leo saa 3 asubuhi kwa saa za New York Marekani ameeleza kuwa na wasiwasi mkubwa kuhusu suala la kufungwa kwa mlango bahari wa Hormuz wakati mzozo huko mashariki ya kati ukiingia mwezi wa tatu licha ya kuwepo kwa usitishaji mapigano aliouita kuwa ni dhaifu. Katibu Mkuu ameonya kuwa kadri hali inavyoendelea, ndivyo gharama kwa ubinadamu zinavyoongezeka, akisisitiza kuwa nchi zinazoendelea zitaathirika zaidi kutokana na madeni makubwa na kupotea kwa ajira na kuwataka wahusika wote kurejesha mara moja uhuru wa usafiri kama ilivyoainishwa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kupitia Azimio namba 2817.Ripoti mpya ya pamoja iliyotolewa leo na mashirika ya Umoja wa Mataifa yanayohusika na chakula, kilimo na uchumi yakishirikiana na Tume ya Muungano wa Afrika imeonesha kuna pengo kubwa kati ya ufadhili wa sasa wa umma na binafsi wa kilimo na kiwango cha ufadhili kinachohitajika ili kubadilisha mifumo ya kilimo barani Afrika. Ripoti hiyo pia inathibitisha ongezeko linaloendelea la njaa na ukosefu wa uhakika wa chakula kote barani Afrika, ikisisitiza uharaka wa ufadhili mkubwa na endelevu ili kubadilisha mifumo ya kilimo.Na leo ni siku ya kuadhimisha muziki wa jazz duniani, siku inayotukumbusha nafasi ya muziki wa jazz kama daraja la kuleta amani, umoja na mazungumzo kati ya watu wa tamaduni tofauti. Kupitia midundo yake ya kipekee, jazz imeendelea kuwa chombo muhimu cha elimu na ushirikiano, ikiunganisha jamii duniani kote. Serikali, taasisi za elimu, mashirika ya kiraia na watu binafsi huungana kusherehekea mchango wa jazz katika kujenga jamii jumuishi.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
Anold Kayanda wa Idhaa hii anazungumza na Dkt. Alinda Mashiku, Mhandisi wa masuala ya anga katika moja ya Vituo vya masuala ya anga za mbali nchini Marekani, NASA. Kwa kuzingatia kuwa Umoja wa Mataifa unapigia chepuo wasichana na wanawake kupata fursa katika sayansi na teknolojia, swali la kwanza la Anold Kayanda kwa Alinda Mashiku ni ameipokeaje hatua ya hivi karibuni ambapo kwa mara ya kwanza mwanamke Christina Cochameshiriki katika timu ya wana-anga waliosafiri na kufanikiwa kuuzunguka mwezi katika eneo mbali zaidi katika anga ya mbali ambako kulikuwa hakujawahi kufikiwa na wanadamu?
Pata ufahamu sahihi kuhusu chanzo, dalili, matibabu pamoja na kinga ya ugonjwa wa Seli Mundu (Sickle Cell) na Dkt. Catherine Mhando wa Hospitali ya Benjamin Mkapa, Dodoma.Support the showIdara ya Habari MAELEZO
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina Flora Nducha wa Idhaa hii anazungumza na mmoja wa walioshiriki mkutano wa CSW70, Masidis Scholastica Madowo Mbunge katika Bunge la Kaunti ya Siaya akiwakilisha kata ya South East Alego jimbo la Magharibi mwa Kenya, ili kuangazia kile anachokifanya kwenye Kaunti yake kuhakikisha wanawake wanapata haki hizo.Hii leo katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York Marekani kutafanyika mdahalo wa wagombea wa nafasi ya Katibu Mkuu wa Umoja huo ambapo wagombea wanne wamejitokeza kuwania wawili wanaume na wawili wanawake. Wagombea hao ni Michelle Bachelet kutoka nchini Chile, Rafael Grossi kutoka nchini Argentina, Rebeca Grynspan kutoka Costa Rica, na Macky Sall kutoka nchini Senegal.Wakati huo huo Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, Annalena Baerbock, amesema mchakato wa kumchagua Katibu Mkuu mpya wa Umoja wa Mataifa ni hatua muhimu itakayoamua mwelekeo wa taasisi hiyo na mustakabali wa ushirikiano wa kimataifa. Akizungumza na waandishi wa habari katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York Marekani kabla ya kuanza kwa mdahalo huo wa wazi, Baerbock ameeleza kuwa uchaguzi huo una umuhimu mkubwa duniani kote, ukigusa maisha ya zaidi ya watu bilioni nane, “Uamuzi huu si wa kiutawala tu, bali ni ujumbe kuhusu maadili na mwelekeo wa Umoja wa Mataifa katika kukabiliana na changamoto za dunia ya leo.”Takribani wahamiaji 8,000 waliripotiwa kufariki dunia au kutoweka duniani kote mwaka 2025, na kufanya jumla ya wahamiaji waliopoteza maisha tangu 2014 kufikia zaidi ya watu 82,000, hii imebainishwa katika takwimu mpya zilizotolewa leo na Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji IOM. Takwimu hizo pia zinaonesha athari kubwa kwa familia, ambapo takribani watu 340,000 wameathirika moja kwa moja. IOM imeonya kuwa njia za uhamiaji si salama na zinazidi kuwa hatari.Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili na hii leo Mtaalam wetu Dkt. Mwanahija Ali Juma, Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili, Zanzibar nchini Tanzania, BAKIZA anafafanua maana na matumizi ya neno "UNYUMBA" Mwenyeji wako ni Rashid Malekela, karibu!
Katika kujifunza lugha ya Kiswahili na hii leo Mtaalam wetu Dkt. Mwanahija Ali Juma, Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili, Zanzibar nchini Tanzania, BAKIZA anafafanua maana na matumizi ya neno "UNYUMBA"
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini Uganda ambayo ni moja ya nchi zinazohifadhi wakimbizi wengi zaidi duniani na tutasikia simulizi za wakimbizi kutoka Sudan ambao Uganda iliwapokea na kuwapa makazi katika Makazi ya Wakimbizi ya Kiryandongo yaliyoko magharibi mwa nchi.Wataalamu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa wametaka uchunguzi wa haraka na uwajibikaji wa kimataifa kufuatia madai ya usafirishaji haramu wa wanawake na wasichana yaliyoibuliwa katika “faili za Epstein.” Wamesema madai hayo yanaonyesha mtandao mpana wa unyonyaji wa kingono uliodumu kwa miaka mingi na kuhusisha watu mashuhuri.mashambulizi makali ya anga ya Israel yameendelea kusini mwa Lebanon, yakilenga maeneo karibu na ngome ya Hezbollah ya Bint Jbeil, huku mashambulizi ya roketi kuelekea kaskazini mwa Israel nayo yakiendelea na kuongeza hofu ya kuongezeka kwa mapigano. Katika hatua nyingine, jeshi la Marekani limesema limezuia meli 10 kupita katika Mlango Bahari wa Hormuz, likitekeleza zuio lake lililotangazwa dhidi ya bandari za Iran. Wakati huo huo, mvutano wa kidiplomasia unaongezeka katika Umoja wa Mataifa, ambapo Baraza Kuu linakutana leo kujadili matumizi ya kura ya turufu kufuatia azimio la Baraza la Usalama kuhusu Mashariki ya Kati lililoungwa mkono na wengi lakini kuzuiwa na China na Urusi.Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto, UNICEF, leo limeeleza wasiwasi mkubwa kufuatia ongezeko la watoto waliouawa au kujeruhiwa nchini Ukraine, ambapo watoto 89 wameathirika mwezi Machi 2026 pekee. Kwa mujibu wa takwimu zilizothibitishwa na ripoti ya uangalizi wa haki za binadamu nchini Ukraine, idadi hiyo imeongezeka kwa asilimia 65 ikilinganishwa na mwezi Februari, hali inayoonesha madhara makubwa ya mashambulizi yanayoendelea kwa familia na jamii. Mashambulizi mabaya ya usiku wa tarehe 15 Aprili yalipiga miji kadhaa mikubwa, ikiwemo Dnipro, Kharkiv, Kyiv na Odesa, yakionesha hatari kubwa inayowakabili watoto.Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili, leo mchambuzi wetu ni Dkt. Josephat Gitonga, ambaye ni Mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi nchini Kenya, kwenye Kitivo cha Tafsiri na Ukalimani anafafanua maana ya methali “AWALI KUWA HERI SI AJABU” asMwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
Katika kujifunza lugha ya Kiswahili, leo mchambuzi wetu ni Dkt. Josephat Gitonga, ambaye ni Mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi nchini Kenya, kwenye Kitivo cha Tafsiri na Ukalimani anafafanua maana ya methali “AWALI KUWA HERI SI AJABU”
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayomulika Mauaji ya kimbari nchini Rwanda ambapo Waziri wa sheria na ambaye pia ni mwanasheria Mkuu wa nchi hiyo Dkt. Emmanuel Ugirashebuja amezungumza na Idhaa hii na anaeleza siri ya wananchi wa Rwanda kuweza kuishi kwa amani baada ya mauaji hayo.Kama mapigano yataendelea nchini Sudan hadi mwaka 2030, umaskini wa kupindukia unaweza kuongezeka na kuvuka asilimia 60, huku watu wengine milioni 34 wakitumbukia kwenye ufukara, imesema Ripoti ya uchambuzi mpya wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo (UNDP) iliyotolewa leo Sudan na Marekani ikiwa kesho inatimia miaka mitatu kamili tangu kuanza kwa vita.Nayo mashirika ya Umoja wa Mataifa yametoa kauli zao tofauti tofauti kuhusu miaka mitatu ya vita nchini Sudan ambapo lile la kuhudumia watoto UNICEF linasema watoto wanaendelea kulipa gharama ya vita kwani zaidi ya watoto 245 wameuawa au kujeruhiwa nchini humo tangu Januari hadi Machi mwaka huu, huku mashambulizi ya ndege zisizo na rubani au droni yamesababisha takriban asilimia 80 ya majeruhi na vifo hivyo.Mzozo wa Israeli na Lebanon ulioshika kasi baada ya wapiganaji wa Hezbollah kushambulia Israeli kupinga hatua ya Marekani na Israeli kushambulia Iran, hii leo huko Washington DC, hapa Marekani kunafanyika mazungumzo kati ya Israel na Lebanon. Umoja wa Mataifa unasihi pande zote kutumia diplomasia kumaliza uhasama na kusongesha azimio namba 1701 la Baraza la Usalama linalozuia mapigano mpakani mwa mataifa hayo mawili.Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili hii leo mtaalam wetu Onni Sigalla, Mhariri mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania, BAKITA. Anafafanua maana za neno "KUDA"Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
Part 4: On the 22nd of December 2025, Republican appointed federal Judge Roger Benitez (Cuban ethnicity) struck down the Democrat mandated lying to parents in the K-12 school system. We covered it beginning in late December 2025 and in a second episode in late January 2026. The third episode, the last one before this one, was 17 March 2026. Unusual behavior or conduct of a student at school isn't grounds for a violation of Constitutional rights, Benitez held in Mirabelli v. Olson (Filed 22 Dec 2025), available here : https://cdn.prod.website-files.com/63d954d4e4ad424df7819d46/6949e11ea6bae817c8eaf637_Dkt%20%20307_MSJ%20Order.pdf Part 4. We cover from Part B on page 30 through to page 38 up to but not including letter C. We'll continue from there next time. This episode includes a Chaplain's corner prayer time thanking the Lord for Roger Benitez and asking for wisdom for the future. The Chaplain's corner includes a reading from Psalm 57 and Streams in the Desert 28 Jan (Cowman Publications Lost Feliz Station Lost Angeles Calif). The Republican Professor is a pro-anti-tax-funded-abuse-of-parents podcast. The Republican Professor is produced and hosted by Dr. Lucas J. Mather, Ph.D.
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini Tanzania kupata ujumbe wa Zahra Salehe, Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la ICCAO linaloshughulika na masuala ya vijana amabye kwa kuwa mwaka huu 2026 ameshiriki tena katika mkutano wa CSW70 anatueleza ni kwa kiasi gani wameweza kulitekeleza malengo ya mikutano haya katika nchini humo.Vita Mashariki ya Kati vilivyoanzishwa na Marekani na Israeli dhidi ya Iran vikiingia mwezi wa pili, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres leo hapa makao makuu ya UN jijini New York, Marekani amezungumza na waandishi wa habari akisisitiza sio tu vita hivyo vikome bali pia anaendeleza diplomasia za kusaka suluhu. Guterres amesema, Ninamtuma Mjumbe wangu Maalum Jean Arnault. Lengo ni kuunga mkono jitihada za kikanda. Lazima tupate njia ya amani ya kutoka katika hali hii. Ujumbe wangu uko wazi. Kwa Marekani na Israeli, ni wakati muafaka kusitisha vita vinavyosababisha mateso makubwa ya kibinadamu na tayari vinaanzisha athari mbaya za kiuchumi. Kwa Iran, isitishe kushambulia majirani zake.. Ripoti mpya ya Kamisheni ya Umoja wa Mataifa kwa Uchumi wa Afrika, (ECA) imependekeza umuhimu wa kuimarisha mifumo ya usimamizi wa deni la umma barani Afrika, ikionya kwamba uendelevu hautegemei tu kiwango cha kukopa bali pia ubora wa taasisi, mifumo ya kisheria, na uwazi. Ikitolewa leo huko Addis Ababa, Ethiopia, ripoti hiyo inataja udhaifu kama vile uwezo mdogo wa kufanya uchambuzi wa hatari, na ushawishi wa mashinikizo ya kisiasa katika maamuzi ya kukopa ikisema kuwa kuboresha usimamizi ni jambo muhimu ili kuhakikisha kuwa deni la umma linachangia ukuaji wa uchumi endelevu badala ya kuwa chanzo cha kuyumba kifedha.Wakati dunia hii leo ikiadhimisha Siku ya Uelewa wa Usonji, familia katika Ukanda wa Gaza, eneo la Palestina linalokaliwa kimabavu na Israeli, zinakabiliwa na changamoto zinazoongezeka katika kuwahudumia watoto usonji katikati ya mzozo unaoendelea na hali mbaya ya kibinadamu. Katika kitongoji cha Sheikh Radwan kaskazini mwa Jiji la Gaza, Layan Abu Qousa mwenye umri wa miaka 16, ambaye ana usonji, anaishi na familia yake katika magofu ya nyumba yao. Familia yake inasema hali ngumu ya maisha imeongeza changamoto zinazohusiana na hali yake, huku ukosefu wa utulivu na mkwamo wa kupata huduma za kitaalamu ukiendelea kudhoofisha ustawi wake.Na katika jifunze Kiswahili, leo mchambuzi wetu ni Dkt. Josephat Gitonga, ambaye ni Mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi nchini Kenya, kwenye Kitivo cha Tafsiri na Ukalimani anafafanua maana ya methali “ATANGULIAYE KUFIKA HUCHAGUA PA KUKAA”Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
Katika jifunze Kiswahili, leo mchambuzi wetu ni Dkt. Josephat Gitonga, ambaye ni Mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi nchini Kenya, kwenye Kitivo cha Tafsiri na Ukalimani anafafanua maana ya methali “ATANGULIAYE KUFIKA HUCHAGUA PA KUKAA”
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kia inayotorejesha katika mkutano wa CSW7O amabko Flora Nducha wa Idhaa hili kandoni mwa kikao hicho alipata fursa ya kuzungumza na Onyonge Mengo kijana mpigania haki za wanawake, mtafiti na wakili kutoka Mahakama Kuu ya Kenya ambaye pia anafanyakazi na shirika la kimataifa la maendeleo la Hivos ili kufahamu kwa kina nini wanachokifanya kusongesha haki za kisheria za wanawake na wasichana.Mzozo wa Mashariki ya Kati ukiwa umeingia siku ya 31 , zaidi ya watu 200,000 wamevuka mpaka wa Lebanon na kuingia Syria tangu mashambulizi baina ya Israeli na Hezbollah yaanze mwishoni mwa mwezi uliopita baada ya Marekani na Israeli kushambulia Iran. Ripoti mpya ya iliyotolewa leo na Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo UNDP, inaonya kuwa idadi kubwa ya watu nchini Iran inaweza kutumbukia kwenye umaskini kadri misukosuko ya kiuchumi inavyozidi kuathiri maisha ya kila siku. Shirika hilo linasema hali hiyo inahatarisha kufuta mafanikio ya maendeleo yaliyopatikana kwa miaka kadhaa, huku Kiwango cha Maendeleo ya Binadamu (HDI) kikitarajiwa kushuka kwa kiasi kikubwa sawa na kupotea kwa zaidi ya mwaka mmoja wa maendeleo.Na Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji IOM, leo limeomba dola milioni 277 kusaidia watu walio hatarini zaidi waliokumbwa na mizozo na ukosefu wa makazi nchini Sudan na nchi jirani kwa mwaka huu wa 2026, wakati mgogoro huo ukikaribia kuingia mwaka wake wa tatu. Mkurugenzi Mkuu wa IOM Amy Pope ameonya kuwa familia zinakabiliwa na “chaguo ngumu lisilowezekana kati ya kubaki bila huduma muhimu au kurejea katika jamii zilizosambaratishwa na vita”. Fedha hizo zitatumika kuimarisha mifumo ya kibinadamu, kupanua njia za misaada, na kuimarisha operesheni za kuvuka mipaka ili kusaidia waathirika kuishi na kujijenga upya.Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili hii leo Dkt. Mwanahija Ali Juma, Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili, Zanzibar nchini Tanzania, BAKIZA anafafanua maana na matumizi ya neno "GIDA."Mwenyeji wako ni Rashid Malekela, karibu!
Katika kujifunza lugha ya Kiswahili hii leo Dkt. Mwanahija Ali Juma, Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili, Zanzibar nchini Tanzania, BAKIZA anafafanua maana na matumizi ya neno "GIDA."
Hii leo katika kujifunza lugha ya Kiswahili, leo mchambuzi wetu Dkt. Josephat Gitonga, ambaye ni Mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi nchini Kenya, kwenye kitivo cha Tafsiri na Ukalimani anafafanua maana ya methali “Ateteaye mtuku ni tanguko la bure."Dkt. Gitonga anasema, "Mtuku ni mtu asiyefaa au asiyeweza kutegemeeka. Methali hii ina maana kwamba mtu asiyetegemeeka kamwe katika jamii na ambaye hana utu, kumtetea ni kujidhalilisha wewe mwenyewe. Ni kazi bure isiyo na faida. Ukimtetea apate labda cheo au kazi fulani utajilaumu mwenyewe kwani hatawajibika hata kamwe. Inatuelimisha kwamba iwapo utakuwa radhi kumtetea mtuku basi kuwa tayari kuhusishwa naye. Tetea walio wema si waovu."
Part 3: On the 22nd of December 2025, Republican appointed federal Judge Roger Benitez (Cuban ethnicity) struck down the Democrat mandated lying to parents in the K-12 school system. We covered it beginning in late December 2025 and in a second episode in late January 2026 Unusual behavior or conduct of a student at school isn't grounds for a violation of Constitutional rights, Benitez held in Mirabelli v. Olson (Filed 22 Dec 2025), available here : https://cdn.prod.website-files.com/63d954d4e4ad424df7819d46/6949e11ea6bae817c8eaf637_Dkt%20%20307_MSJ%20Order.pdf Part 3. We cover from page 18 at line 24 through to Part B on page 30. We'll continue from there next time. This episode includes a Chaplain's corner prayer time thanking the Lord for Roger Benitez and asking for wisdom for the future. The Republican Professor is a pro-anti-tax-funded-abuse-of-parents podcast. The Republican Professor is produced and hosted by Dr. Lucas J. Mather, Ph.D.
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini Tanzania ambako UNHCR inasema ufadhili endelevu na wa uhakika unahitajka ili kuendeleza ulinzi wa wakimbizi na kusaidia urejeaji na ujumuishaji wa raia wanaorudi nchini Burundi. Pia tunakuletea jifunze Kiswahili.Ushirikiano wa kimataifa kupitia mikataba ya kimataifa ya kudhibiti dawa umesaidia watu duniani kote, imesema hii leo Bodi ya Kimataifa ya kudhibiti dawa za kulevya, INCB wakati ikizindua ripoti ya mwaka 2025 kuhusu hali yad awa za kulevya duniani.Wataalamu wa Umoja wa Mataifa wa haki za binadamu wamelaani vikali ukatili unaodaiwa kufanywa na kundi la waasi la M23 nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, dhidi ya watetezi wa haki za binadamu katika majimbo ya Kivu Kaskazini na Kivu Kusini mashariki mwa taifa hilo la Maziwa Makuu.Na leo ikiwa ni siku ya tatu ya Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) huko The Hague Uholanzi kuthibitisha iwapo kuna ushahidi wa kutosha wa kumfikisha mahakamani Rais wa zamani wa Ufilipino Rodrigo Duterte kwa madai ya uhalifu dhidi ya ubinadamu unaohusianana kile kilichoitwa “vita dhidi ya dawa za kulevya” nchini mwake, wakili upande wa utetezi, Nicholas Kaufmann amesema hakuna uhusiano uliothibitishwa kati ya hotuba zake za “kipekee, zenye kauli kali” na mauaji anayotuhumiwa kuyafanya.Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili leo mchambuzi wetu ni Dkt. Josephat Gitonga, ambaye ni Mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi nchini Kenya, kwenye kitivo cha Tafsiri na Ukalimani anafafanua maana ya methali “ANUIAYE KUKUTUKANA HAKOSI MATANGO”Mwenyeji wako ni Rashid Malekela, karibu!
Katika kujifunza lugha ya Kiswahili leo mchambuzi wetu ni Dkt. Josephat Gitonga, ambaye ni Mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi nchini Kenya, kwenye kitivo cha Tafsiri na Ukalimani anafafanua maana ya methali “ANUIAYE KUKUTUKANA HAKOSI MATANGO”
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina kesho Ijumaa tarehe 13 Februari ikiwa ni ni siku ya Redio Duniani mwaka huu ikijikita katika Redio na Akili tunakupeleka mashariki mwa DRC, kwa George Musubao kutoka Televishen na Radio washirika Canal Victoire Du People Kasindi.Leo tarehe 12 Februari ni siku ya Kimataifa ya Kuzuia Itikadi Kali Zinazochochea Ugaidi, ikiwa ni maadhimisho ya nne tangu kuanzishwa kwake na mwaka huu kauli mbiu inasema “Kuzuia ugaidi wa kikatili katika enzi ya teknolojia mpya na zinazoibuka”. Ugaidi na itikadi kali vinaendelea kuwa tishio kubwa kwa amani na usalama wa dunia, huku vikigusa watu wa rika, dini na tamaduni mbalimbali na ndio maana Umoja wa Mataifa unasema ingawa teknolojia kama akili mnemba au AI, mitandao ya kijamii na majukwaa ya kidijitali inaweza kusaidia juhudi za kuzuia misimamo mikali, pia inatumiwa na magaidi kueneza chuki, upotoshaji na kuhamasisha vurugu ndio maana shirika hilo linahimiza ushirikiano wa kimataifa, matumizi ya teknolojia kwa uwajibikaji na suluhisho shirikishi zinazoheshimu haki za binadamu ili kuzuia kuenea kwa itikadi kali.Barani Ulaya ambapo Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa, Volker Türk, ametoa tamko kali akilaani mashambulizi ya mfululizo yanayofanywa na nchi ya Urusi dhidi ya mifumo ya nishati nchini Ukraine. Taarifa iliyotolewa leo kutoka Geneva, Uswisi, imeeleza kuwa mashambulizi hayo yanawanyima raia mahitaji muhimu ikiwemo mifumo ya kupasha joto, maji, na umeme katikati ya msimu wa baridi kali uliopitiliza.Kuelekea kuanza kwa mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani hapo wiki ijayo, katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametuma ujumbe akisema kuwa “Katika zama hizi ngumu na za mgawanyiko, hebu tuitikie wito wa stahmala wa Ramadhani. Kuziba pengo la mgawanyiko. Kufikisha msaada na matumaini kwa wale wanaoumini. Na kulinda haki na utu wa kila mtu…..Hebu Mwezi huu Mtukufu ututie hamasa ya kufanya kazi pamoja ili kujenga dunia yenye amani zaidi, ukarimu na haki kwa watu wote. Ramadhani njema.”Na Katika kujifunza lugha ya Kiswahili na hii leo Dkt. Mwanahija Ali Juma, Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili, Zanzibar nchini Tanzania, BAKIZA anafafanua maana ya neno "UNGUKA"Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
Katika kujifunza lugha ya Kiswahili na hii leo Dkt. Mwanahija Ali Juma, Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili, Zanzibar nchini Tanzania, BAKIZA anafafanua maana ya neno "UNGUKA"
Hii leo jaridani Anold Kayanda wa Idhaa hii amezungumza na Wakili Amon Mpanju, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum kutoka Tanzania aliyehudhuria Mkutano wa Kamisheni ya Maendeleo ya Kijamii (CSocD64).Mashirika ya kibinadamu ya Umoja wa Mataifa leo yametoa onyo kali kuhusu hali mbaya ya kibinadamu inayowakumba watoto nchini Sudan. Mashirika hayo lile la kuhudumia watoto UNICEF, la afya WHO na Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Binadamu wamenasema ghasia zisizoisha, njaa na magonjwa vinawasababisha watoto kupoteza Maisha na kudhoofika, huku mashambulizi dhidi ya vituo vya afya na vikwazo vya upatikanaji wa misaada vikizorotesha juhudi za kuwaokoa. Akizungumza na waandishi wa habari mjini Geneva, msemaji wa UNICEF, Ricardo Pires, amesema “Katika baadhi ya maeneo ya jimbo la Darfur Kaskazini, zaidi ya nusu ya watoto wote wanakabiliwa na utapiamlo mkali, si makadirio, si mfano, imethibitishwa.”.Kikosi cha 12 cha Ulinzi wa Amani kutoka Tanzania TANZBAT 12 kinachohusumu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Condo DRC chini ya mpango wa Umoja wa Mataifa nchini humo MONUSCO kimeendelea kudumisha uhusiano wa kijamii na wakazi wa mji wa Beni Mashariki mwa DRC, kwa kutoa msaada wa vifaa vya elimu kwa wanafunzi katika shule ya msingi Ngite iliyopo eneo la Mavivi. Mkuu wa shule hiyo Neema Nyamwaka amewashukuru walinada amani hao kutoka Tanzania kwa kujali sekta ya elimu.Leo ni siku ya mikunde duniani Shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo FAO likisistiza umuhimu kwa chakula hicho kwa lishe na mazingira. Huko Kigoma Tanzania FAO kupitia mpango wa Pamoja wa KJP imekuwa ikitoa mafunzo kwa wakulima kuhusu umuhimu wa mazao ya jamii ya mikunde huyu ni mmoja wa wanufaika wa mafunzo hayo.Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili, leo mchambuzi wetu ni Dkt. Josephat Gitonga, ambaye ni Mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi nchini Kenya, kwenye kitivo cha Tafsiri na Ukalimani anafafanua maana ya methali “Atokeapo mtoto wa fuko mshike japo wawinda fuko.”Mwenyeji wako ni Rashid Malekela, karibu!