Podcasts about novemba

  • 28PODCASTS
  • 721EPISODES
  • 22mAVG DURATION
  • 5WEEKLY NEW EPISODES
  • Nov 28, 2025LATEST

POPULARITY

20172018201920202021202220232024


Best podcasts about novemba

Latest podcast episodes about novemba

Habari za UN
Katibu Mkuu wa UN ameitaka Guinea-Bissau kurejesha utawala wa kikatiba mara moja

Habari za UN

Play Episode Listen Later Nov 28, 2025 2:14


Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres, amelaani vikali mapinduzi yanayoendelea nchini Guinea-Bissau akitaka “urejeshwaji wa haraka na usio na masharti wa utawala wa kikatiba” baada ya wanajeshi kutwaa madaraka kufuatia uchaguzi mkuu wa uliofanyika tarehe 23 Novemba. Selina Jerobon na maelezo zaidi. 

Habari za UN
28 NOVEMBA 2025

Habari za UN

Play Episode Listen Later Nov 28, 2025 10:59


Hii leo jaridani tunaangazia hali ya amani na usalama nchini Guinea-Bissau, utapiamlo nchini Sudan na juhudi za UNICEF za kuwawezesha vijana ili waweze kujikwamua kimaisha nchini Tanzania.Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres, amelaani vikali mapinduzi yanayoendelea nchini Guinea-Bissau akitaka “urejeshwaji wa haraka na usio na masharti wa utawala wa kikatiba” baada ya wanajeshi kutwaa madaraka kufuatia uchaguzi mkuu wa uliofanyika tarehe 23 Novemba.Zaidi ya miaka miwili na nusu ya vita nchini Sudan imewaacha watu milioni 21 karibu nusu ya watu wote wa nchi hiyo wakikabili njaa kali, huku maeneo mawili yakithibitishwa kukumbwa na baa la njaa. Mapigano yamepungua kwa sasa katika baadhi ya sehemu za Khartoum, na masoko yanaanza kufunguliwa tena., Lakini Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani WFP linaonya kuwa hali bado ni tete.Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto (UNICEF)  kupitia programu yake ya stadi za maisha na mafunzo ya biashara iitwayo Ujana Salama, inayofadhiliwa na mfuko wa maendeleo ya jamii nchini humo TASAF kwa msaada wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS) imewezesha kikundi cha vijana nchini humo kujitegemea. Mmoja wa vijana wanufaika wa programu hiyo ameweza kujenga mustakabali ambao awali aliouna kama ndoto kupitia masomo ya ushoniMwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!

Alfajiri - Voice of America
Alfajiri - Novemba 28, 2025

Alfajiri - Voice of America

Play Episode Listen Later Nov 28, 2025 29:59


Matangazo ya nusu saa kuhusu habari za mapema asubuhi pamoja na habari za michezo.

Alfajiri - Voice of America
Alfajiri - Novemba 27, 2025

Alfajiri - Voice of America

Play Episode Listen Later Nov 27, 2025 29:59


Matangazo ya nusu saa kuhusu habari za mapema asubuhi pamoja na habari za michezo.

Habari za UN
26 NOVEMBA 2025

Habari za UN

Play Episode Listen Later Nov 26, 2025 9:59


Hii leo jaridani tunaangazia usafirir endelevu, udhalilishaji wa mtandaoni tukikuletea ujumbe kutoka Uganda, na ufugaji endelevu unaowawezesha wafugaji katika maeneo kame ya Isiolo na Garissa nchini Kenya.Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres, ameadhimisha Siku ya Kimataifa ya Usafiri Endelevu Duniani kwa kuonya kwamba mifumo ya usafiri duniani ambayo ni muhimu kwa uchumi na maisha ya kila siku inayochochea dunia kuelekea janga la tabianchi na kwa hivyo siku hii inatukumbusha kwamba njia ya kuelekea mustakabali bora inategemea mifumo safi na yenye uendelevu wa usafiri.Siku 16 za uhamasishaji kupinga ukatili dhidi ya wanawake zikiendelea leo tunakupeka mjini Hoima Magharibi mwa Uganda kusiki maoni kutoka kwa wa mji huo kuhusu ukatili mtandaoni yakienda sanjari na kauliimbiu ya kampeni ya ya mwaka huu isemayo “Ukatili wa mtandaoni ni ukatili halisi na hakuna visingizo kwa ukatili mtandaoni”.Katika maeneo yaliyoghubikwa na athari za mabadiliko ya tabianchi kaskazini mwa Kenya, wafugaji wamekuwa wakikumbwa na changamoto kubwa kwani ukame na mafuriko, vinatishia sio tu mali zao bali pia maisha yao. Lakini kupitia mradi wa bima ya mifugo unaoendeshwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula  duniani WFP, kwa ushirikiano na asasi ya Zoetis na kampuni ya ZEP-RE, jamii zinaanza kupata ahuweni na matumaini mapya.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!

Alfajiri - Voice of America
Alfajiri - Novemba 26, 2025

Alfajiri - Voice of America

Play Episode Listen Later Nov 26, 2025 29:59


Matangazo ya nusu saa kuhusu habari za mapema asubuhi pamoja na habari za michezo.

Habari za UN
25 NOVEMBA 2025

Habari za UN

Play Episode Listen Later Nov 25, 2025 12:23


Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, na leo zinaanza siku 16 za uanaharakati kuelimisha umma kuhusu janga la ukatili wa kijinsia, tunamsikia  mmoja wa waathirika wa ukatili wa kingono.Katika kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametoa onyo kali kuhusu ongezeko la ukatili mtandaoni dhidi ya wanawake na wasichana.Ripoti mpya iliyotolewa leo na Shirika la Umoja wa Mataifa la Masuala ya wanawake UN Women na Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya dawa na uhalifu UNODC inaonya kwamba mwaka 2024, wanawake na wasichana 50,000 waliuawa na wapenzi au jamaa sawa na mwanamke mmoja kila dakika 10.Ripoti mpya ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Biashara na Maendeleo (UNCTAD) inaonya kwamba uchumi wa Eneo la Palestina Linalokaliwa kwa Mabavu na Israel umerudi nyuma miaka 22 kwa muda usiozidi miaka miwili kwani umeingia katika hali mbaya zaidi ya mdororo kuwahi kurekodiwa, huku miongo ya maendeleo ikifutwa na operesheni za kijeshi zilizodumu kwa muda mrefu pamoja na vizuizi vya muda mrefu.Katika kujifunza lugha Kiswahili hii leo,  mtaalam wetu Onni Sigalla, Mhariri mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania, BAKITA. Anafafanua maana za neno "MADUYUNI"Mwenyeji wako ni Sabrina Said, karibu!

Alfajiri - Voice of America
Alfajiri - Novemba 25, 2025

Alfajiri - Voice of America

Play Episode Listen Later Nov 25, 2025 29:59


Matangazo ya nusu saa kuhusu habari za mapema asubuhi pamoja na habari za michezo.

Habari za UN
24 NOVEMBA 2025

Habari za UN

Play Episode Listen Later Nov 24, 2025 11:32


Hii leo jaridani tunaangazia hali ya maendeleo na mabadiliko ya tabianchi barani Afrika, mashindano ya mpira wa miguu yanayofahamiaka kama Hope Championship kwa watu waliokatwa viungo katika Gaza na ukatili wa kijinsia.Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres leo ametoa ujumbe mzito kwenye Mkutano wa Muungano wa Afrika AU na Muungano wa Ulaya EU, unaofanyika mjini Luanda, Angola akionya kuwa dunia “inabadilika kwa kiwango cha kutisha,” huku janga la tabianchi, ukosefu wa usawa na mvutano wa kimataifa vikichochea misukosuko mipya duniani.Tukielekea katika siku ya kimataifa ya kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake hapo kesho Novemba 25 leo tunakupeleka Kenya kwake Geradline Ndayisenga, raia kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, (DRC) ambaye sasa anaishi ukimbizini kwenye eneo la Kitengela, Kaunti ya Kajiado nchini humo, anasema kama si usaidizi wa ushauri wa nasaha alioupata kutoka shirika la kiraia la Forum for Women Development, Democracy and Justice, FODDAJ nchini humo, basi hajui maisha yake  yangalikuwa vipi.Mashindano ya mpira wa miguu yanayofahamiaka kama Hope Championship kwa watu waliokatwa viungo katika Ukanda wa Gaza yamemalizika majuzi baada ya siku nne mfululizo za michuano. Mashindano haya yanaandaliwa na Chama cha Soka cha Watu Waliokatwa Viungo cha Palestina kama sehemu ya juhudi za kuwasaidia majeruhi na kuthibitisha ushiriki wao endelevu katika shughuli rasmi za michezo.Mwenyeji wako ni Sabrina Said, karibu!

Habari za UN
Ushauri nasaha wamwezesha mkimbizi nchini Kenya kurejea maisha ya kawaida

Habari za UN

Play Episode Listen Later Nov 24, 2025 2:44


Tukielekea katika siku ya kimataifa ya kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake hapo kesho Novemba 25 leo tunakupeleka Kenya kwake Geradline Ndayisenga, raia kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, (DRC) ambaye sasa anaishi ukimbizini kwenye eneo la Kitengela, Kaunti ya Kajiado nchini humo, anasema kama si usaidizi wa ushauri wa nasaha alioupata kutoka shirika la kiraia la Forum for Women Development, Democracy and Justice, FODDAJ nchini humo, basi hajui maisha yake  yangalikuwa vipi. Je ilikuwaje? Tuungane na Sheilah Jepngetich kwa simulizi zaidi.

Alfajiri - Voice of America
Alfajiri - Novemba 24, 2025

Alfajiri - Voice of America

Play Episode Listen Later Nov 24, 2025 30:00


Matangazo ya nusu saa kuhusu habari za mapema asubuhi pamoja na habari za michezo.

Habari za UN
MONUSCO imelaani vikali mashambulizi ya ADF Lubero nchini DRC yalioua raia 89

Habari za UN

Play Episode Listen Later Nov 21, 2025 2:56


Mpango wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC ujulikanao kama MONUSCO, leo umelaani vikali mashambulizi makubwa yaliyofanywa na kundi lenye silaha la Allied Democratic Forces ADF kati ya tarehe 13 na 19 Novemba 2025 katika baadhi ya maeneo ya Lubero, jimboni Kivu Kaskazini na kukatili maisha ya raia wengi. Flora Nducha na maelezo zaidi

Habari za UN
21 NOVEMBA 2025

Habari za UN

Play Episode Listen Later Nov 21, 2025 12:02


Hii leo jaridani tunaangazia machafuko nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, mbinu bunifu za kilimo cha kakao nchini Peru, na mradi wa miundombinu wa kupunguza athari ya mafuriko na kugeuza maji ziada kuwa rasilimali muhimu kwa jamii nchini Rwanda.Mpango wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC ujulikanao kama MONUSCO, leo umelaani vikali mashambulizi makubwa yaliyofanywa na kundi lenye silaha la Allied Democratic Forces ADF kati ya tarehe 13 na 19 Novemba 2025 katika baadhi ya maeneo ya Lubero, jimboni Kivu Kaskazini na kukatili maisha ya raia wengi.Katika msitu wa Amazon upande wa nchi ya Peru, jamii za watu wa asilizimeonesha namna mbinu bunifu za kilimo zinaweza kuongeza uzalishaji na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi. Yote haya yanakuja wakati dunia ikiendelea kujadili mustakabali wa hatua za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi katika mkutano wa Umoja wa Mataifa COP30 unaoendelea huko Belém, Brazil.Mwezi Mei 2023, Rwanda nchi iliyozungukwa na milima ilikumbwa na mafuriko makubwa yaliyosababisha maporomoko ya ardhi na kusababisha maji kutoka katika milima ya volkano, yakiambatana na mawe mazito kuharibu mashamba, makazi na barabara. Baada ya mafuriko hayo ili kupunguza athari za majanga kama hayo, kwa wakati mwingine Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo (FAO) nchini Rwanda, kwa ufadhili wa Serikali ya Japan, linatekeleza mradi wa Kukabiliana na Majanga Yanayohusiana na Maji katika wilaya za Rutsiro na Burera. Lengo ni kupunguza Athari na kugeuza maji ziada kuwa rasilimali muhimu kwa jamii.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!

SBS Swahili - SBS Swahili
Yaliyojiri Afrika 11 Novemba

SBS Swahili - SBS Swahili

Play Episode Listen Later Nov 21, 2025 6:41


Jason Nyakundi anatujuza yaliyojiri Afrika

SBS Swahili - SBS Swahili
Yaliyojiri Afrika 14 Novemba

SBS Swahili - SBS Swahili

Play Episode Listen Later Nov 21, 2025 6:34


Jason Nyakundi anatujuza yaliyojiri Afrika

SBS Swahili - SBS Swahili
Yaliyojiri Afrika 21 Novemba

SBS Swahili - SBS Swahili

Play Episode Listen Later Nov 21, 2025 8:50


Jason Nyakundi anatujuza yaliyojiri Afrika

SBS Swahili - SBS Swahili
Taarifa ya habari tarehe 21 Novemba

SBS Swahili - SBS Swahili

Play Episode Listen Later Nov 21, 2025 11:08


Elekea kwenye tovuti yetu katika sbs.com.au/swahili kwa habari na taarifa zaidi.

SBS Swahili - SBS Swahili
Yaliyojiri Afrika 18 Novemba

SBS Swahili - SBS Swahili

Play Episode Listen Later Nov 21, 2025 8:44


Jason Nyakundi anatujuza yaliyojiri Afrika

SBS Swahili - SBS Swahili
Taarifa ya habari tarehe 18 Novemba

SBS Swahili - SBS Swahili

Play Episode Listen Later Nov 21, 2025 10:31


Elekea kwenye tovuti yetu katika sbs.com.au/swahili kwa habari na taarifa zaidi.

SBS Swahili - SBS Swahili
Yaliyojiri Afrika 7 novemba

SBS Swahili - SBS Swahili

Play Episode Listen Later Nov 21, 2025 7:09


Jason Nyakundi anatujuza yanayojiri Afrika.

SBS Swahili - SBS Swahili
Taarifa ya habari tarehe 14 Novemba

SBS Swahili - SBS Swahili

Play Episode Listen Later Nov 21, 2025 10:21


Elekea kwenye tovuti yetu katika sbs.com.au/swahili kwa habari na taarifa zaidi.

SBS Swahili - SBS Swahili
Taarifa ya habari tarehe 11 Novemba

SBS Swahili - SBS Swahili

Play Episode Listen Later Nov 21, 2025 12:58


Elekea kwenye tovuti yetu katika sbs.com.au/swahili kwa habari na taarifa zaidi.

Alfajiri - Voice of America
Alfajiri - Novemba 21, 2025

Alfajiri - Voice of America

Play Episode Listen Later Nov 21, 2025 29:59


Matangazo ya nusu saa kuhusu habari za mapema asubuhi pamoja na habari za michezo.

Habari za UN
20 NOVEMBA 2025

Habari za UN

Play Episode Listen Later Nov 20, 2025 10:45


Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka katika Kaunti ya Kajiado iliyoko Kusini na Kusini magharibi mwa jiji la Nairobi nchini Kenya kumulika upatikanaji wa huduma za choo na hasa choo safi na salama ambazo bado ni kizungumkuti kote dunianini.Katibu Mkuu wa Umoja wa, António Guterres,akizungumza na waandishi wa habari hii leo ametoa onyo kali COP30 huko Belém, Brazil, akisisitiza dharura ya hatua dhidi ya mabadiliko ya tabianchi. Amesema “Jamii zilizo mstari wa mbele zinaangalia zikiesabu nyumba zao zilizozamishwa na mafuriko mavuno yaliyoshindikana, vyanzo vya maisha vilivyopotea na kuuliza kwa kiasi gani zaidi wateseke . Wamesikia visingizio vya kutosha, sasa wanatakahatua”.Leo ni Siku ya mtoto Duniani, mwaka huu ikibeba kaulimbiu “Sikilizeni watoto, simameni kwa ajili ya haki za kila mtoto, kila siku.” Ripoti mpya ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto UNICEF iliyotolewa leo ya Hali ya Watoto Duniani 2025 sanjari na maadhimisho haya  inaonya kwamba zaidi ya watoto milioni 417, sawa na mtoto 1 kati ya 5 katika nchi za kipato cha chini na cha kati, wanakabiliwa na ukosefu mkubwa wa mahitaji muhimu angalau katika maeneo mawili ya msingi ya maisha.Mkutano wa wanaharakati vijana wavumbuzi kutoka kila pembe ya dunia umeaanza leo mjini Geneva Uswisi ukibeba mafda kuu “Kutoka Hashtag hadi Hatua”, ukisherehekea vijana wanaobadilisha maisha ya jamii zao kupitia zana za kidijitali na majukwaa ya mtandaoni. Mwaka huu, washindi wa uvumbuzi huo wanatoka nchi mbalimbali, ikiwemo Côte d'Ivoire, India, Lebanon, Japan, na Brazil, wakitambuliwa kwa kazi zao zenye athari kubwa chanya. Waandaaji wa Jukwaa hilo amba oni Umoja wa Mataifa wanasema tukio hili lina lengo la kuhamasisha vijana wengi zaidi kubadilisha ushiriki wao wa mtandaoni kuwa hatua halisi zinazoboresha jamii, kuthibitisha kuwa uanaharakati wa kidijitali unaweza kuleta mabadiliko ya kweli.Na katka kujifunza lugha ya Kiswahili leo ukumbi ni wake mlumbi wa lugha ya Kiswahili Joramu Nkumbi kutoka nchini Tanzania, anafafanua maana za maneno "MTAWALIA.”Mwenyeji wako ni Sabrina Said, karibu!

Alfajiri - Voice of America
Alfajiri - Novemba 20, 2025

Alfajiri - Voice of America

Play Episode Listen Later Nov 20, 2025 29:59


Matangazo ya nusu saa kuhusu habari za mapema asubuhi pamoja na habari za michezo.

Habari za UN
19 NOVEMBA 2025

Habari za UN

Play Episode Listen Later Nov 19, 2025 10:44


Hii leo jaridani tunaangazia ujumbe katika siku ya Choo Duniani, simulizi za wakinamama wakimbizi wa ndani nchini Sudan, na usugu dhidi ya Viua-Vijasumu (AMR).Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa Duniani WHO leo linaadhimisha Siku ya Choo Duniani kwa onyo kali kwamba janga la usafi wa mazingira duniani linagharimu maisha kila siku, na mabadiliko ya tabianchi yanaliweka katika hatari kubwa zaidi huku mamilioni ya watu wakiishi bila huduma muhimu ya choo.Wakinamama wakimbizi wa ndani nchini Sudan wameziomba jumuiya za kimataifa kuwasaidia kuhakikisha vita inaisha nchini mwao ili waweze kuishi kwa amani kwani madhila waliyopitia ni mengi na yanahuzunisha.Usugu dhidi ya Viua-Vijasumu (AMR)unaelezwa kama janga la kimyakimya linalotishia kurudisha nyuma mafanikio ya miongo kadhaa katika tiba na afya. Tunapoadhimisha Wiki ya Kimataifa ya kuelimisha umma kuhusu usugu dhidi ya Viua-Vijasumu au antibiotics, Mkurugenzi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani, WHO Kanda ya Afrika, Profesa Mohamed Janabi, ametahadharisha akisema dawa ambazo hapo awali ziliokoa maisha sasa hazifanyi kazi kama ilivyokuwa na hivyo inabidi kuchukua hatua za pamoja na haraka.Mwenyeji wako ni Sabrina Moshi, karibu!

Alfajiri - Voice of America
Alfajiri - Novemba 19, 2025

Alfajiri - Voice of America

Play Episode Listen Later Nov 19, 2025 29:59


Matangazo ya nusu saa kuhusu habari za mapema asubuhi pamoja na habari za michezo.

Habari za UN
18 NOVEMBA 2025

Habari za UN

Play Episode Listen Later Nov 18, 2025 11:32


Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini Brazil kwenye mkutano wa COP30, ambako Dkt. Richard Muyungi, Mjumbe maalumu kwenye masuala ya mabadiliko ya tabianchi na mazingira kutoka nchini Tanzania anaeleza ni nini bara la Afrika linahitaji.Umoja wa Mataifa umekaribisha kupitishwa kwa Azimio namba 2803 la Baraza la Usalama kuhusu Gaza hapo jana, ukilitaja kuwa hatua muhimu katika kuimarisha usitishaji mapigano. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres, anazitaka pande zote kuheshimu kikamilifu makubaliano hayo na kutafsiri kasi ya kidiplomasia kuwa hatua za dharura na za wazi kwa watu walioko katika eneo hilo. Katika taarifa iliyotolewa na Msemaji wa Guterres, Stéphane Dujarric, amesema Umoja wa Mataifa umejizatiti kuongeza misaada ya kibinadamu na kuunga mkono jitihada zinazoelekezwa katika hatua inayofuata ya usitishaji mapigano.Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), hali ya kibinadamu katika majimbo ya Kivu Kaskazini na Kusini bado ni tete. Mkurugenzi wa Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu, Kanda ya Afrika Patrick Youssef  ambaye amerejea hivi karibuni kutoka DRC amewaleza waandishi wa habari jijini Geneva, Uswisi kwamba raia wa DRC wanaendelea kubeba mzigo mzito wa mapigano, hata wakati shughuli chache za kibiashara zikiendelea kurejea Goma. Ametoa tahadhari kuwa mgogoro huo unakabiliwa na upungufu mkubwa wa ufadhili, ukatili wa kingono unaongezeka, na zaidi ya asilimia 70 ya watu waliojeruhiwa kwa silaha mwaka huu ni raia.Kuanzia leo tarehe 18 inaanza Wiki ya Kimataifa ya Kuelimisha Umma kuhusu Usugu wa Vijiumbemaradhi dhidi ya dawa. Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani, WHO, linaonya kuwa usugu wa vimelea yaani hali ambapo bakteria, virusi na vijidudu vingine havidhuriki tena kwa dawa tayari unatishia mifumo ya afya, uchumi na uhakika wa chakula. Kwa kaulimbiu “Chukua Hatua Sasa: Linda Leo Yetu, Linda Mustakabali Wetu,” WHO inatoa wito kwa serikali, wahudumu wa afya, wakulima, wadau wa mazingira na umma kuchukua hatua madhubuti kutekeleza ahadi za kisiasa ili kupunguza kuenea kwa maambukizi sugu ya dawa.Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili hii leo Dkt. Mwanahija Ali Juma, Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili, Zanzibar nchini Tanzania, BAKIZA anafafanua maana na matumizi ya neno "UPUNGUFU"Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!

Alfajiri - Voice of America
Alfajiri - Novemba 18, 2025

Alfajiri - Voice of America

Play Episode Listen Later Nov 18, 2025 29:59


Matangazo ya nusu saa kuhusu habari za mapema asubuhi pamoja na habari za michezo.

Habari za UN
17 NOVEMBA 2025

Habari za UN

Play Episode Listen Later Nov 17, 2025 11:02


Hii leo jaridani tunaangazia kesi za mauaji ya kimbari nchini Rwanda, ukatili wa kijinsia na zoezi la mahakama tembezi nchini Sudan Kusini.Mfumo wa kimataifa wa kushughulikia mabaki ya kesi za mauaji ya kimbari (IRMCT) umeamua kuwa mtuhumiwa wa mauaji ya kimbari, Félicien Kabuga, hana uwezo wa kiafya kusafiri kwenda Rwanda, uamuzi unaositisha mpango wa awali wa kumhamisha kwenda nchini Rwanda ili kuachiwa kwa muda kutokana na hali yake ya kiafya kuwa tete.Dunia inajiandaa kuadhimisha Siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia kuanzia tarehe 25 mwezi huu wa Novemba hadi tarehe 10 Disemba, kampeni inayolenga kuongeza uelewa na kutoa wito wa kuzuia na kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na wasichana duniani kote. Na katika kuelekea maadhimisho hayo, Sabrina Saidi ameandaa taarifa kutokea huko nchini Ethiopia, akiangazia simulizi ya mwanamke ambaye ameamua kuvunja mzunguko wa mila zenye madhara kwa jamii yake.Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Sudani Kusini UNMISS wakishirikiana na wizara ya haki na masuala ya katiba nchini humo wanaendeleza zoezi la mahakama tembezi nchini humo, mradi ambao unafadhiliwa na Ubalozi wa Norway ili  kuhakikisha wananchi hususan wale walio na kesi mahakama wanapata haki.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!

Habari za UN
Simulizi ya Askalech kutoka Ethiopia - Ukatili wa kijinsia

Habari za UN

Play Episode Listen Later Nov 17, 2025 3:06


Dunia inajiandaa kuadhimisha Siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia kuanzia tarehe 25 mwezi huu wa Novemba hadi tarehe 10 Disemba, kampeni inayolenga kuongeza uelewa na kutoa wito wa kuzuia na kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na wasichana duniani kote. Na katika kuelekea maadhimisho hayo, Sabrina Saidi ameandaa taarifa kutokea huko nchini Ethiopia, akiangazia simulizi ya mwanamke ambaye ameamua kuvunja mzunguko wa mila zenye madhara kwa jamii yake.

Alfajiri - Voice of America
Alfajiri - Novemba 17, 2025

Alfajiri - Voice of America

Play Episode Listen Later Nov 17, 2025 30:00


Matangazo ya nusu saa kuhusu habari za mapema asubuhi pamoja na habari za michezo.

Jioni - Voice of America
Jioni - Novemba 15, 2025

Jioni - Voice of America

Play Episode Listen Later Nov 15, 2025 29:59


Matangazo ya saa nzima kuhusu habari za kutwa, ikiwa ni pamoja ripoti kutoka kwa waandishi wetu sehemu mbali mbali duniani na kote Afrika Mashariki na Kati, na vile vile vipindi na makala maalum kuhusu afya, wanawake, jamii na maendeleo.

Habari za UN
14 NOVEMBA 2025

Habari za UN

Play Episode Listen Later Nov 14, 2025 11:36


Hii leo jaridani tunaangazia ugonjwa wa kisukari, chanjo ya polio katika ukanda wa Gaza na janga la mabadiliko ya tabianchi na athari zake kwa wakimbizi.Tarehe 14 Novemba kila mwaka dunia huadhimisha Siku ya Kisukari na mwaka huu kauli mbiu ni “Kisukari katika hatua mbalimbali za maisha.” Je wafahamu ugonjwa huu unampata mtu gani na unawezaje kujikinga usiugue? Leah Mushi anatujuza zaidi.Mashirika ya Umoja wa Mataifa WHO, UNICEF na UNRWA wameanzisha kampeni ya pamoja ya Uchanjaji watoto waliokosa huduma muhimu za kuokoa maisha kutokana na miaka miwili ya machafuko katika Ukanda wa Gaza umeanza kutekelezwa na mashirika matatu ya Umoja wa Mataifa, lile la afya duniani, la kuhudumia watoto UNICEF na la kusaidia wakimbizi wa Kipalestina, UNRWA.Wiki ya kwanza ya Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi, COP30, unaofanyika Belém Brazil, ikielekea ukingoni, viongozi wa dunia na wanaharakati wanakutana kujadili jinsi ya kushughulikia moja ya changamoto kubwa za wakati huu, ‘janga la mabadiliko ya tabianchi,” Na athari zake kwa wakimbizi hazikupewa kisogo. Flora Nducha anafafanua zaidi katika taarifa hii.Mwenyeji wako ni Sabrina Said Moshi, karibu!

Habari za UN
Je wajua nini kinasababisha ugonjwa wa kisukari na ujikinge vipi?

Habari za UN

Play Episode Listen Later Nov 14, 2025 2:54


Tarehe 14 Novemba kila mwaka dunia huadhimisha Siku ya Kisukari na mwaka huu kauli mbiu ni “Kisukari katika hatua mbalimbali za maisha.” Je wafahamu ugonjwa huu unampata mtu gani na unawezaje kujikinga usiugue? Leah Mushi anatujuza zaidi.

Alfajiri - Voice of America
Alfajiri - Novemba 14, 2025

Alfajiri - Voice of America

Play Episode Listen Later Nov 14, 2025 30:00


Matangazo ya nusu saa kuhusu habari za mapema asubuhi pamoja na habari za michezo.

Jioni - Voice of America
Jioni - Novemba 14, 2025

Jioni - Voice of America

Play Episode Listen Later Nov 14, 2025 59:52


Matangazo ya saa nzima kuhusu habari za kutwa, ikiwa ni pamoja ripoti kutoka kwa waandishi wetu sehemu mbali mbali duniani na kote Afrika Mashariki na Kati, na vile vile vipindi na makala maalum kuhusu afya, wanawake, jamii na maendeleo.

Habari za UN
13 NOVEMBA 2025

Habari za UN

Play Episode Listen Later Nov 13, 2025 10:40


Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayoangazia simulizi za waahirika wa Kimbunga Melissaikiwa ni wiki ya pili sasa baada ya kupiga magharibi mwa Jamaica, na kuacha zahma kubwa kwa wakaazi. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na jifunze Kiswahili.Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres akieleza kuwa na wasiwasi mkubwa kutokana na ripoti za ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu na mauaji ya halaiki mjini El Fasher, pamoja na kuongezeka kwa mapigano katika maeneo ya Kordofan nchini Sudan. Guterres amesema “Mtiririko wa silaha na wapiganaji kutoka nje lazima ukatwe. Misaada ya kibinadamu lazima iweze kuwafikia haraka raia wanaohitaji, na mapigano lazima yakome,”.Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa Jumatano limemchagua Phoebe Okowa kutoka Kenya kuwa Jaji wa Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ), baada ya duruu nne za upigaji kura. Upigaji kura huo ulifanyika kwa wakati mmoja na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, lakini kwa utaratibu tofauti, kama inavyotakiwa na Katiba ya Mahakama hiyo ya Haki. Bi. Okowa amechaguliwa kwa wingi wa kura ambapo alipata kura 8 katika Baraza la Usalama na kura 106 katika Baraza Kuu.Kumekuwa na ongezeko la uraibu wa nikotini na bidhaa nyingine zinazozalishwa kwa kutumia tumbaku duniani hususani miongoni mwa vijana na tena wengi hivi sasa wanatumia sigara za kielektroniki, limesema shirika la Umoja wa Mataifa la Afya duniani WHO. Tarehe 17 mpaka 21 Novemba utafanyika mkutano mkubwa kujadili namna serikali, mashirika ya kimataifa na asasi za kiraia zitakavyoweza kusaidia kupambana na janga la tumbaku duniani, linalosababisha vifo zaidi ya milioni saba kila mwaka.Katika kujifunza lugha ya Kiswahili hii leo, mtaalam wetu Onni Sigalla, Mhariri mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania, BAKITA. Anafafanua maana za neno "KASIMU"Mwenyeji wako ni Sabrina Said Moshi, karibu!

Alfajiri - Voice of America
Alfajiri - Novemba 13, 2025

Alfajiri - Voice of America

Play Episode Listen Later Nov 13, 2025 29:59


Matangazo ya nusu saa kuhusu habari za mapema asubuhi pamoja na habari za michezo.

Habari za UN
12 NOVEMBA 2025

Habari za UN

Play Episode Listen Later Nov 12, 2025 11:27


Hii leo jaridani tunaangazia ripoti ya FAO ya uhaba wa chakula, Mwanaharakati kijana kutoka Kenya katika mkutano wa pili wa WSSD Doha, na mradi wa Mifereji ya Maji wa Jiji la Kampala (Kampala Capital City Drainage Master Plan) inayosaidia kupunguza mafuriko Uganda.Ripoti mpya ya pamoja kutoka mashirika mawili ya Umoja wa Mataifa lile la Chakula na Kilimo Duniani (FAO) na la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) inaonya kwamba uhaba mkubwa wa chakula unazidi kuongezeka katika maeneo 16 yenye njaa duniani, hali inayoweza kusababisha mamilioni zaidi ya watu kukumbwa na njaa kali au hatari ya kufikia kiwango cha baa la njaa.Mkutano wa Pili wa Dunia wa Maendeleo ya Kijamii umefunga pazia mjini Doha, Qatar, mwishoni mwa wiki hii, ukiwaleta pamoja viongozi wa dunia, mashirika ya kiraia na vijana wakitoka na wito wa pamoja dhidi ya umasikini, ukosefu wa usawa na kutengwa kijamii. Kutoka Kenya, mwanaharakati kijana amesema mkutano huo umekuwa wa kuhamasisha akitoa wito wa hatua za haraka.Kituo cha utafiti wa kusaka Suluhu kuhusu mafuriko kinachoendeshwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo (UNDP) nchini Uganda kimetumia maarifa ya pamoja kukabiliana na changamoto za mafuriko katika eneo la Makerere Kavule, makazi yasiyo rasmi yaliyo pembezoni mwa mji wa Kampala, mji mkuu wa Uganda. Kituo hicho kimeunganisha juhudi za jamii, maarifa asilia, na teknolojia ya kisasa kubuni mfumo wa mifereji ya maji unaoendana na Mpango Mkuu wa Mifereji ya Maji wa Jiji la Kampala (Kampala Capital City Drainage Master Plan). Mfumo huu unalenga kupunguza mafuriko si tu katika jamii hiyo, bali pia katika eneo la katikati ya jiji.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!

Alfajiri - Voice of America
Alfajiri - Novemba 12, 2025

Alfajiri - Voice of America

Play Episode Listen Later Nov 12, 2025 29:56


Matangazo ya nusu saa kuhusu habari za mapema asubuhi pamoja na habari za michezo.

Habari za UN
11 NOVEMBA 2025

Habari za UN

Play Episode Listen Later Nov 11, 2025 12:07


Alfajiri - Voice of America
Alfajiri - Novemba 11, 2025

Alfajiri - Voice of America

Play Episode Listen Later Nov 11, 2025 30:00


Matangazo ya nusu saa kuhusu habari za mapema asubuhi pamoja na habari za michezo.

Habari za UN
10 NOVEMBA 2025

Habari za UN

Play Episode Listen Later Nov 10, 2025 10:00


Alfajiri - Voice of America
Alfajiri - Novemba 10, 2025

Alfajiri - Voice of America

Play Episode Listen Later Nov 10, 2025 30:00


Matangazo ya nusu saa kuhusu habari za mapema asubuhi pamoja na habari za michezo.

Habari za UN
07 NOVEMBA 2025

Habari za UN

Play Episode Listen Later Nov 7, 2025 9:55


Jarida hii leo tunamulika harakati za kuzuia  mauaji ya kimbari El Fasher, Sudan, hakuna dalili za kumalizika kwa janga la njaa mashariki mwa DRC na furaha kwa watoto waliopatiwa mabegi ya kwenda shule huko Tigray, Ethiopia.Unapokabiliana na ukatili na mauaji ya kimbari ni vema kuhakikisha wanaotekeleza wanafahamu kuwa wanafuatiliwa na kutazamwa ili hatua stahiki ziweze kuchukuliwa dhidi yao, amesema Chaloka Beyani Mshauri Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu kuzuia mauaji ya kimbari.Mgogoro katika mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) unaendelea kuwa mbaya huku mapigano yakizidi, na kusababisha makumi ya maelfu ya watu kukimbia makazi yao na kuzidisha njaa kali, Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) limeeleza leo.Nchini Ethiopia, Kaskazini Magharibi mwa jimbo la Tigray watoto wamefurahia kupatiwa vifaa kwa ajili ya kurejea upya shuleni baada ya vita ya muda mrefu, shukrani kwa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF. Tupate taarifa zaidi kutoka kwa Leah Mushi.

Habari za UN
06 NOVEMBA 2025

Habari za UN

Play Episode Listen Later Nov 6, 2025 9:59


Habari za UN
05 NOVEMBA 2025

Habari za UN

Play Episode Listen Later Nov 5, 2025 11:27


Katika jarida la habari za Umoja wa Mataifa hii leo utasikia kuhusu wito wa mataifa yote kuwekeza kwenye mifumo ya tahadhari za mapema ikiwa leo dunia inaadhimisha Siku ya kimataifa ya kuelimisha umma kuhusu Tsunami. Utasikia pia ziara ya Rais wa Baraza kuu la Umoja wa Mataifa nchini Qatar ambapo amewatembelea wakimbizi wa kipalestina walioko nchini humo. Kutoka nchini Kenya utasikia juhudi za taasisi ya FODDAJ kusaidia jamii nchini Kenya kupambana na ukatili wa kijinsia. 

Habari za UN
04 NOVEMBA 2025

Habari za UN

Play Episode Listen Later Nov 4, 2025 11:34


Hii leo Jaridani, Anold Kayanda anakupeleka nchini Kenya kusikia usaidizi wa FAO kwenye harakati za kuondokana na njaa katika taifa hilo la Afrika Mashariki kupitia uimarishaji wa sekta ya kilimo. Lakini pia kuna Muhtasari kutoka kwa Leah Mushi akimulika:Baa la Njaa kuthibitishwa huko El Fasher na Kadugli nchini SudanAzimio la Doha lenye lengo la kuimarisha maendeleo ya jamii dunianiKauli ya Joyce Msuya, Naibu Mkuu wa OCHA akiwa huko Doha, Qatar kufuatia kupitishwa kwa azimio hilo.Na kipengele cha Jifunze Kiswahili leo kinaelezea matumizi ya neno Mhanga na Wahanga.Karibu!

Habari za UN
03 NOVEMBA 2025

Habari za UN

Play Episode Listen Later Nov 3, 2025 9:50


Hii leo jaridani tunaangazia hali ya haki za binadamu nchini Sudan, Mpango wa Ufadhili Wajasiriamali Wanawake, (We-Fi) nchini Tanzania, na kilimo ni moja ya sekta muhimu za kiuchumi nchini Nigeria.Ofisi ya Mwendesha Mashtaka wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) imetoa tamko juu ya wasiwasi mkubwa kufuatia ripoti mpya kutoka El-Fasher, jimboni Darfur Kaskazini, nchini Sudan, zikieleza kuwepo kwa mauaji ya halaiki, ubakaji, na uhalifu mwingine unaodaiwa kufanywa wakati wa mashambulizi ya Vikosi vya Usaidizi wa Haraka (RSF).Mpango wa Ufadhili Wajasiriamali Wanawake, (We-Fi) unaofadhiliwa na Benki ya Dunia na wadu umewezesha biashara kukwamuka nchini Tanzania baada ya janga la COVID-19, hatua ambayo imeinua pia jamii nzima na si wajasiriamali wanawake peke yao. Simulizi hii ya Assumpta Massoi inamulika mjasiriamali mwanamke Haika Lawere anayemiliki hoteli ya Mbezi Garden jijini Dar Es Salaam ambako ni jiji kuu la biashara la taifa hilo la Afrika.Kilimo ni moja ya sekta muhimu za kiuchumi nchini Nigeria, kikiajiri zaidi ya theluthi moja ya watu wote nchini humo. Lakini hali ya hewa isiyotabirika imefanya kilimo kuwa shughuli yenye mashaka makubwa — ukame, mafuriko na mvua zisizo na mpangilio zimekuwa tishio kubwa kwa wakulima, ambapo kilio chao kimesikiwa na Benki ya Dunia iliyokuja na suluhisho kwa kuanzisha mradi wa kilimo cha umwagiliaji.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!