Podcasts about waziri mkuu

  • 16PODCASTS
  • 121EPISODES
  • 18mAVG DURATION
  • 1EPISODE EVERY OTHER WEEK
  • Sep 26, 2025LATEST

POPULARITY

20172018201920202021202220232024


Best podcasts about waziri mkuu

Latest podcast episodes about waziri mkuu

Habari za UN
26 SEPTEMBA 2025

Habari za UN

Play Episode Listen Later Sep 26, 2025 9:57


Hii leo ni hotuba ya Israeli kwenye mjadala mkuu wa baraza kuu, nini kilitokea? Kijana daktari mwanaharakati kutoka Ghana aishiye Uingereza akiwa UNGA80 na matumaini mapya ya kinga dhidi ya maambukizi ya VVU.Mjadala Mkuu wa Mkutano wa 80 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa ukiwa umeingia katika siku yake ya nne hapa kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani leo Ijumaa, Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu amekuwa wa kwanza kuzungumza akitumia muda wake mwingi kushambulia wanamgambowa kipalestina, Hamas na kutetea kila uamuzi wa Israel. Anold Kayanda ameifuatilia hotuba hiyo kwa kina. Karibu Anold utupe japo kwa muhtasari.Tukisalia hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa, moja ya mikutano ya ngazi ya juu iliyofanyika kando ya mjadala mkuu wa Baraza Kuu, ni ule wa kuadhimisha miaka 30 tangu kuanzishwa kwa program ya Umoja wa Mataifa kuhusu vijana, mkutano ukileta vijana kutoka kona mbali mbali za dunia. Miongoni mwao ni daktari wa tiba na mwanaharakati wa kijamii wa vijana kutoka Uingereza mwenye asili ya  Ghana, Dkt. Khadija Owusu. Amezungumza na Flora Nducha anayetujulisha zaidi katika taarifa hiiKatika hatua kubwa ya kihistoria kwenye mapambano dhidi ya Virusi Vya UKIMWI (VVU) dawa mpya ya kudungwa inayoitwa Lenacapavir  inatarajiwa kupatikana kwa gharama nafuu katika nchi 120 zenye kipato cha chini na kati kuanzia mwaka 2027. Dawa hiyo itauzwa kwa kiasi cha dola 40 pekee ikiwa ni gharama ya vidonge vya kila siku vya kujikinga na VVU ambavyo mhusika atatumia kwa mwaka mzima. Sabrina Saidi ana taarifa zaidi.

Habari za UN
UNGA80:Hotuba ya Netanyahu yakumbana na upinzani, yeye augeuza ukumbi kuwa darasa

Habari za UN

Play Episode Listen Later Sep 26, 2025 3:54


Mjadala Mkuu wa Mkutano wa 80 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa ukiwa umeingia katika siku yake ya nne hapa kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani leo Ijumaa, Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu amekuwa wa kwanza kuzungumza akitumia muda wake mwingi kushambulia wanamgambowa kipalestina, Hamas na kutetea kila uamuzi wa Israel. Anold Kayanda ameifuatilia hotuba hiyo kwa kina. Ilikuwa majira ya saa tatu na dakika chache hivi asubuhi ya leo saa za New York nchini Marekani ambapo Waziri Mkuu wa Isreal Benjamin Netanyahu amepewa fursa ya kuhutubia na ndipo ukumbi wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa ukakosa utulivu. Wajumbe kwa makundi walinyanyuka katika viti vyao na kuondoka huku wakiwaacha maafisa wa Israel wakimpigia makofi kiongozi wao na pia nchi zinazoiunga mkono Israel zikasalia katika viti vyao ikiwemo Marekani.Baadhi ya wajumbe watoka njeKatika eneo la walipotakiwa kukaa wawakilishi wa Palestina kulikuwa wazi, huku katika eneo la Iran ikibakia picha iliyokusanya sura za baadhi ya watu wao waliouawa na mashambulizi ya Israel. Bwana Netanyahu kwa mara nyingine tena ameingia na ubao wenye picha ya ramani ya eneo la Mashariki ya Kati akiutumia kuishambulia Iran na kwa kutumia kalamu akiweka alama ya vema kuonesha namna ambavyo Israel imefanikiwa kupambana na ngome za Irani katika ukanda huo. Katika suti yake, kifuani upande wa kulia, Bwana Netanyahu pia ameweka kibandiko chenye QR Code na akawaambia watu kuwa Israel bado inakumbuka tukio walilofanyiwa na Hamas mwezi Oktoba mwaka juzi na kwamba ikiwa watu wamesahau hilo basi waelekeze simu zao kwenye QR Code hiyo kwenye nguo yake ili iwaoneshe madhara yaliyofanywa na Hamas.Majina ya mateka yakasomwaWaziri Mkuu huyo wa Israel ameyasoma majina ya mateka ambao bado wako mikononi mwa Hamas katika eneo la Ukanda wa Gaza na pia akaueleza mkutano kuwa amesambaza vipaza sauti au spika katika eneo lote la Gaza ili anapoongea leo, azungumze moja kwa moja na mateka huko walikofichwa. Na hapo akabadilisha lugha na kuongea kwa kihebrania akiwaahidi kuwa atawakomboa. Vilevile amedokeza kuwa kwa namna ya kiintelijensia Israel imefanya simu leo ziweze kusambaza hotuba katika ukanda wa Gaza na hivyo akautumia muda huo kupeleka ujumbe mkali kwa Hamas kuwa ataendelea kuwadhibiti. Bwana Netanyahu pia  ameingia ukumbini na vibao viwili vyenye maswali na majibu ya kuchagua japokuwa jibu sahihi kwa mujibu wake na waliojibu kuwa ni All the Above, yaani majibu yote ni sahihi. Maswali yote yalikuwa yakiwatuhumu Iran, Hamas, Al Caeda, Hezbollah na Houthi kuwa pia wanaitakia kifo Marekani na wameua watu wengi Ulaya. Huenda hotuba hii ya Netanyahu ikaingia katika orodha ya hotuba tano ndefu zaidi baada ya ile ya Rais wa Marekani Donald Trump wa Marekani, Ya Mahmoud Abbass wa Palestina na Félix-Antoine Tshisekedi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC ambao wote hao walitumia zaidi ya dakika arobaini licha ya muda wa hotuba uliopangwa kuwa angalau dakika 15.

SBS Swahili - SBS Swahili
Taarifa ya Habari 23 Septemba 2025

SBS Swahili - SBS Swahili

Play Episode Listen Later Sep 23, 2025 17:02


Waziri Mkuu amesema ombi la utaifa wa Palestina ni fursa ya amani, katika hotuba yake kuhusu soluhu ya nchi mbili, alipo hudhuria kikao cha Umoja wa Mataifa hii leo Jumanne 23 Septemba 2025.

palestina umoja habari mataifa septemba waziri mkuu
SBS Swahili - SBS Swahili
Taarifa ya Habari 12 Septemba 2025

SBS Swahili - SBS Swahili

Play Episode Listen Later Sep 12, 2025 15:33


Waziri Mkuu amesifu msaada wa wanachama wa kongamano la Visiwa vya Pasifiki, Australia inapo saka uenyeji wa kongamano la mazingira la Umoja wa Mataifa la, COP-31.

Habari za UN
10 SEPTEMBA 2025

Habari za UN

Play Episode Listen Later Sep 10, 2025 10:18


Leo jaridani Assumpta Massoi anamulika kauli ya OHCHR kufuatia maandamano yanayoendelea Nepal; Utipwatipwa 'wapiku' utapiamlo na harakati za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi huko Karamoja nchini Uganda,Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Haki za Binadamu ameonesha wasiwasi mkubwa kufuatia ghasia zinazoendelea na kushika kasi nchini Nepal, huko barani Asia, ambako maandamano dhidi ya ufisadi na marufuku ya mitandao ya kijamii yamesababisha vifo vya watu wengi pamoja na majeruhi. Flora Nducha amefuatilia taarifa hiyo na anatupasha zaidi.Kwa mara ya kwanza idadi ya watoto na vijana wa umri wa kwenda shule wenye unene wa kupindukiaau utipwatipwa imezidi idadi ya watoto wenye utapiamlo duniani ikiathiri watoto milioni 188 sawa na mtoto 1 kati ya kila watoto 10 imesema leo ripoti iliyotolewa leo na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF. Tuungane na Leah Mushi kusikia zaidi kuhusu ripoti hiyo, karibu LeahKaramoja, eneo la kaskazini mashariki mwa Uganda, linakabiliwa na changamoto kubwa za tabianchi kama vile ukame wa mara kwa mara na milipuko ya magonjwa ya mimea na mifugo, hali inayotishia uhakika wa chakula. Kupitia mradi wa PROACT, mashirika ya Umoja wa Mataifa lile la  Chakula na Kilimo Duniani (FAO), na Mpango wa chakula Duniani (WFP) pamoja na Ofisi ya Waziri Mkuu wa Uganda kwa ufadhili wa Muungano wa Ulaya, EU, wameshirikiana katika kuimarisha mifumo ya kushughulikia mabadiliko ya kiikolojia na kijamii. Anold Kayanda na maelezo zaidi.

Habari za UN
Harakati za UN na serikali ya Uganda kukabili tabianchi huko Karamoja

Habari za UN

Play Episode Listen Later Sep 10, 2025 2:55


Karamoja, eneo la kaskazini mashariki mwa Uganda, linakabiliwa na changamoto kubwa za tabianchi kama vile ukame wa mara kwa mara na milipuko ya magonjwa ya mimea na mifugo, hali inayotishia uhakika wa chakula. Kupitia mradi wa PROACT, mashirika ya Umoja wa Mataifa lile la  Chakula na Kilimo Duniani (FAO), na Mpango wa chakula Duniani (WFP) pamoja na Ofisi ya Waziri Mkuu wa Uganda kwa ufadhili wa Muungano wa Ulaya, EU, wameshirikiana katika kuimarisha mifumo ya kushughulikia mabadiliko ya kiikolojia na kijamii. Anold Kayanda na maelezo zaidi.(Taarifa ya Anold Kayanda) Video iliyoandaliwa na FAO inaanza ikionesha wana jamii katika eneo la Karamoja wanavyojihusisha na shughuli mbalimbali za kijamii ikiwemo kilimo na ufugaji licha ya changamoto za tabianchi.  Dustan Balaba Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu Uganda anaeleza kuhusu mradi huu mpya akisema,"Wadau wameweza kuhakikisha kwamba kuna maendeleo ya haraka katika upatikanaji wa taarifa na tunatumia maendeleo ya kiteknolojia kwa manufaa yetu. Tumejiandaa vyema kutabiri matukio mengi ya tabianchi.”Mpango huu unalenga kutumia mifumo ya tahadhari ya mapema na hatua za kabla ya majanga ili kukuza uwezo wa jamii za Karamoja kukabiliana na majanga, pamoja na kushirikisha wadau mbalimbali kwa ushirikiano.Lokong Robert, Kaimu Afisa wa Kilimo wa Wilaya Kaabong anaeleza akisema, "Tunachagua kaya hizo. Baada ya kuchagua tunapewa maelezo juu ya madhumuni ya kuwachagua. viongozi wa meneo, maafisa wa ugani, na washauri wa ujenzi wa uwezo waliajiriwa na FAO huenda kukusanya taarifa katika kata."Naye Stella Nagujja, mtaalamu wa usimamizi wa hatari za tabianchi WFP Uganda anasema "mshikamano kati ya mamlaka zetu tofauti ulitufanya tufikiri kuwa itakuwa kimkakati kushirikiana na FAO ili kuokoa maisha na kuwafikia jamii zilizo katika mazingira magumu."Lakini kiini cha mradi huu kipo katika sauti za watu waliopokea huduma na kunufaika moja kwa moja. Kuanzia Moroto hadi Nabilatuk, jamii si wapokeaji tu wa msaada, bali ni washiriki  kamilifu katika kujenga uwezo wao wa kujitegemea.Jolly Aisu, afisa kilimo wilaya ya Nakapiripirit, anasema ,  “tunapanga ziara za mashambani ili kutusaidia kutambua na kuchambua ugonjwa au mdudu gani ameshambulia mimea ya mkulima. Kisha kutoka hapo tunawaelekeza cha kufanya kutumia taarifa kutoka katika mifumo ya tahadhari ya mapema na mipango iliyo wazi.”Hata hivyo, pamoja na maendeleo haya, changamoto bado zipo. Rasilimali chache na hali ya ukosefu wa usalama miongoni mwa jamii vinaweza kuhatarisha mafanikio ya mradi huu.Lukeng  Emmanuel, Mkulima wa Kaabong anatamatisha kwa kusema, "Tunashindwa hata kununua dawa ya kunyunyizia kwa sababu kile kidogo tunachokipata hapa tunatumia kwa chakula, karo ya shule, na matibabu. Tunaliacha shamba lipambane kivyake hadi tutakapopata pesa kidogo ya kununua dawa ndipo tunanyunyizia."

SBS Swahili - SBS Swahili
Taarifa ya Habari 5 Agosti 2025

SBS Swahili - SBS Swahili

Play Episode Listen Later Aug 5, 2025 12:17


Waziri wa mambo ya nje Penny Wong ame muhamasisha Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu, asikize wito wakisitisha vita mara moja Gaza.

SBS Swahili - SBS Swahili
Taarifa ya Habari 22 Julai 2025

SBS Swahili - SBS Swahili

Play Episode Listen Later Jul 22, 2025 14:15


Waziri Msaidizi wa Waziri Mkuu amesema serikali iko tayari kuwafanyia kazi wa Australia, katika kikao cha kwanza cha bunge la shirikisho hii leo.

SBS Swahili - SBS Swahili
Taarifa ya Habari 27 Juni 2025

SBS Swahili - SBS Swahili

Play Episode Listen Later Jun 27, 2025 15:19


Waziri Mkuu wa Anthony Albanese ametetea msimamo wa serikali kwa matumizi ya ulinzi, nakutupilia mbali wito kutoka utawala wa Trump kuongeza matumizi hadi asilimia 3.5 ya pato la taifa.

Wimbi la Siasa
Sudan yampata Waziri Mkuu, vita vikiendelea kupamba moto

Wimbi la Siasa

Play Episode Listen Later Jun 4, 2025 10:26


Uongozi wa kijeshi nchini Sudan mwishoni mwa mwezi Mei, ulimteua mwanasiasa  na mwanadiplomasia mkongwe Kamil Idris, kuwa Waziri Mkuu mpya wakati huu vita vikiendelea kati ya jeshi na wanamgambo wa RSF. Tangu kuanza kwa vita Aprili 2023, watu zaidi ya 20,000 wamepoteza maisha, huku wengine Milioni 15 wakikimbia makaazi yao, wakiwemo zaidi ya Milioni nne ambao wamekimbilia katika nchi jirani kwa mujibu wa takwimu za Umoja wa Mataifa. Nini hatima ya Sudan ?

SBS Swahili - SBS Swahili
Taarifa ya Habari 6 Mei 2025

SBS Swahili - SBS Swahili

Play Episode Listen Later May 6, 2025 16:29


Anthony Albanese ata anza muhula wake wa pili kama Waziri Mkuu akiwa na serikali ya wengi, baada ya ushindi mkubwa wa chama cha Labor, chama chake kilishinda viti 86 bungeni.

SBS Swahili - SBS Swahili
Taarifa ya Habari 11 Aprili 2025

SBS Swahili - SBS Swahili

Play Episode Listen Later Apr 11, 2025 11:25


Waziri Mkuu amekabiliana na maswali kuhusu uwezekano wa mkataba wa manowari ya Australia na Marekani pamoja na Uingereza, kufuatia utoaji wa ushuru wa Marekani ambao ume tikisa dunia nzima.

australia habari aprili marekani uingereza waziri mkuu
SBS Swahili - SBS Swahili
Taarifa ya Habari 17 Machi 2025

SBS Swahili - SBS Swahili

Play Episode Listen Later Mar 18, 2025 6:16


Waziri Mkuu na kiongozi wa zamani wa chama cha Liberals Malcolm Turnbull, amesema hadhani Australia inastahili endelea mbele na ushirikiano wa AUKUS, ametoa maoni hayo wakati wasiwasi una ongezeka iwapo mkataba huo uta tekelezwa chini ya muhula wa pili wa uongozi wa Trump.

SBS Swahili - SBS Swahili
Taarifa ya Habari 25 Februari 2025

SBS Swahili - SBS Swahili

Play Episode Listen Later Feb 25, 2025 20:14


Waziri Mkuu amesema serikali ya shirikisho inapitia bajeti "mstari kwa mstari" kupata jinsi yakuwekeza ahadi yake ya Medicare.

medicare habari waziri mkuu
Wimbi la Siasa
Mahamoud Ali Youssouf ashinda Uenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika

Wimbi la Siasa

Play Episode Listen Later Feb 19, 2025 9:35


Waziri wa Mambo ya nje wa Djibouti Mahmoud Ali Youssouf alichaguliwa na wakuu wa mataifa ya Afrika Februari 15 2025, kuwa Mwenyekiti mpya wa Tume ya Umoja wa Afrika na kumshinda mwanasiasa mkongwe na aliyekuwa Waziri Mkuu wa Kenya Raila Odinga. Tunachambua ushindi wake na kazi kubwa inayomsubiri

Jioni - Voice of America
Russia ni tishio kubwa kwa usalama wa EU, asema waziri mkuu wa Italy - Desemba 22, 2024

Jioni - Voice of America

Play Episode Listen Later Dec 22, 2024 29:59


Habari za UN
Mjumbe wa UN aendelea na ziara ya kukutana na wadau nchini Syria

Habari za UN

Play Episode Listen Later Dec 16, 2024 1:31


Mjumbe Maalum wa Umoja wa Mataifa kwa Syria Geir O. Pedersen bado yuko nchini Syria alikowasili jana Jumapili  ikiwa ni wiki moja baada ya wapiganaji wa Hayʼat Tahrir al-Sham (HTS) walioko kwenye orodha ya vikundi vya kigaidi kutwaa mji mkuu Damascus na kusababisha Rais Bashar Al-Assad kukimbia nchi. Ikiwa ni sehemu ya juhudi za Umoja wa Mataifa kuhakikisha mabadiliko ya utawala nchini Syria yanafanyika kwa amani na kuisaidia Syria kutokuingia kwenye mgogoro zaidi, Bwana Pederson aliyewasili jana Damascus  hadi sasa ameshakutana na Kamanda wa Utawala Mpya Ahmed al-Sharaa na Waziri Mkuu wa Serikali ya Muda Mohammed al-Bashir.Taarifa iliyotolewa leo na Ofisi yake inasema Pederson ameeleza muhtasari wa matokeo ya Mkutano wa Kimataifa wa Aqaba kuhusu Syria uliofanyika tarehe 14 ya mwezi huu wa Desemba akisisitiza haja ya kuwepo kwa mpito wa kisiasa unaoaminika na unaoongozwa na kumilikiwa na Wasyria wenyewe kama kanuni za azimio 2254 la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa (2015) zilivyopendekeza. Aidha Mjumbe huyo maalum amesisitiza azma ya Umoja wa Mataifa ya kutoa usaidizi wa kina kwa watu wa Syria.Taarifa imedokeza kuwa Bwana Pedersen ana shughuli nyingi zilizopangwa siku zijazo katika harakati za kusaka suluhu ya amani nchini Syria.

Alfajiri - Voice of America
Waziri Mkuu wa Mali asimamishwa kazi baada ya kukosoa serikali kwa kuchelewesha uchaguzi wa kidemokrasia. - Desemba 05, 2024

Alfajiri - Voice of America

Play Episode Listen Later Dec 5, 2024 29:59


Matangazo ya nusu saa kuhusu habari za mapema asubuhi pamoja na habari za michezo.

mali kazi baada serikali uchaguzi desemba kidemokrasia waziri mkuu
SBS Swahili - SBS Swahili
Taarifa ya Habari 29 Novemba 2024

SBS Swahili - SBS Swahili

Play Episode Listen Later Nov 29, 2024 18:08


Waziri Mkuu amekataa kuweka wazi jinsi mamlaka yaku wafurusha watu katika nchi ya tatu yata tumiwa.

habari novemba waziri mkuu
Habari za UN
21 NOVEMBA 2024

Habari za UN

Play Episode Listen Later Nov 21, 2024 9:59


Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini Kenya kushuhudia jinsi mpango wa Usimamizi wa Ardhi uliopatiwa wa "kusaidia jamii kufikia Ajenda 2030” ambao FAO imetekeleza kwa kaunti kadhaa. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na uchambuzi wa neno.Hague kwenye mahakama ya kimataifa ya uhalifu inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa ICC ambayo leo imetoa kibali cha kukamatwa Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu, Waziri wa zamani wa ulinzi Yoav Galant  na kiongozi wa kundi la kipalestina la Hamas Mohamed Diab Ibrahim al-Masri alimaarufu kama  kwa makosa ya uhalifu dhidi ya ubinadamu na uhaifu wa vita ulitendeka wakati wa vita inayoendelea baina ya Israel na Hamas.Mjini  Baku nchini Azerbaijan mkutano wa 29 wa mkataba wa nchi wanachanama wa Umoja wa Mataifa kuhusu mabadiliko ya tabainchi COP29 unaelekea ukingoni  na leo ukijikita na masuala ya kijinsia na mabadiliko ya tabianchi. Miongoni mwa waliozungumzia changamoto ya tabianchi kwa wanawake ni  Jemimah Njuki, mkuu wa kitengo cha uwezeshaji wa kiuchumi katika shirika la Umoja wa Mataifa la masuala ya wanawake UN Women.“Raia  wanaoshtakiwa katika mahakama za kijeshi nchini Uganda hukosa dhamana sawa ya mchakato wa kisheria kama wale wanaoshtakiwa katika mahakama za kiraia,” amesema Volker Türk, Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Haki za Binadamu hii leo kufuatia tukio la kutekwa kwa mwanasiasa wa upinzani nchini Uganda Kiiza Besigye akiwa nchini Kenya.Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili na hii leo Dkt. Mwanahija Ali Juma, Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili, Zanzibar nchini Tanzania, BAKIZA anafafanua maana ya neno MHARABU”.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu! 

Alfajiri - Voice of America
Waziri Mkuu wa India Narendra Modi afanya ziara ya kwanza nchini Nigeria. - Novemba 18, 2024

Alfajiri - Voice of America

Play Episode Listen Later Nov 18, 2024 29:59


Matangazo ya nusu saa kuhusu habari za mapema asubuhi pamoja na habari za michezo.

Habari za UN
01 OKTOBA 2024

Habari za UN

Play Episode Listen Later Oct 1, 2024 11:00


Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina ikiwa Mjadala mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa UNGA79, umekunja jamvi jana Jumatatu, tunaangazia sehemu ya pili ya mahojiano na mmoja wa washiriki wa mjadala huo waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa. Pia tunakuletea muhtasari wa habari, na sauti za mashinani, kulikoni?Baada ya siku 6 za viongozi wa nchi 193 wanachama wa Umoja wa Mataifa kutoa hotuba kuhusu masuala muhimu yanayogusa dunia hivi sasa, wakizingatia maudhui ya kutomwacha nyuma mtu yeyote, hatimaye Mjadala mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa umekunja jamvi Jumatatu ya Septemba 30 jijini New York, Marekani.Hii leo shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ulimwenguni, WHO limesema kufuatia tangazo la serikali ya Rwanda juu ya mlipuko wa ugonjwa wa homa ya virusi vya marburg tarehe 27 mwezi uliopita, hadi sasa watu 8 wamefariki dunia kati ya 26 waliothibitishwa kuugua ugonjwa huo, mara ya kwanza kuripotiwa Rwanda. Rwanda inashirikiana na wadau ikiwemo WHO kudhibiti kusambaa kwa virusi vya ugonjwa huo ambao hadi sasa hauna chanjo wala tiba. Asilimia 70 ya wagonjwa ni wahudumu wa afya kutoka vituo viwili vya afya kwenye mji mkuu Kigali.Na baada ya jeshi la Israeli hapo jana kujulisha Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa Mpito nchini Lebanon, UNIFIL juu ya nia yake ya kuanza mashambulizi ya ardhini dhidi ya wapiganaji wa Hezbollah nchini humo, hii leo ujumbe huo umesema licha ya hatari inayoendelea ya mashambulizi, walinda amani wamejipanga. UNIFIL imesema mara kwa mara wanabadili mwenendo na operesheni zao na tayari wana mipango ya kutekeleza iwapo itahitajika kufanya hivyo. IDF na Hezbollah wamekuwa wanashambuliana kusini mwa Lebanon.Mashinani leo ikiwa ni siku ya Kimataifa ya Wazee Duniani tunakupeleka nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC kusikia ujumbe kutoka kwa mmoja ya wazee, ana maoni gani?Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!

Habari za UN
Sehemu ya 2 ya mahojiano na Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa - Viuavijiumbe maradhi/Tabianchi

Habari za UN

Play Episode Listen Later Oct 1, 2024 6:25


Mjadala mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa UNGA79, umekunja jamvi jana Jumatatu ambapo viongozi wa Dunia walikusanyika hapa New York kwenye Umoja wa Mataifa na kujikita na mada kadha wa kadha, katika sehemu hii ya pili ya mahojiano na mmoja wa washiriki wa mjadala huo waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa -Majaliwa. Flora Nducha ameangazia mbili kati ya mada kuu 4 zilizopewa uzito, Ambayo ni usugu wa dawa na changamoto ya mabadiliko ya tabianchi.

Jioni - Voice of America
Waziri Mkuu wa Israel amepa nchi yake itatoa majibu ya “kiwango kikubwa” kufatia shambulizi la kombora katikati mwa Israel. - Septemba 16, 2024

Jioni - Voice of America

Play Episode Listen Later Sep 16, 2024 29:59


Matangazo ya saa nzima kuhusu habari za kutwa, ikiwa ni pamoja ripoti kutoka kwa waandishi wetu sehemu mbali mbali duniani na kote Afrika Mashariki na Kati, na vile vile vipindi na makala maalum kuhusu afya, wanawake, jamii na maendeleo.

Jioni - Voice of America
Mfalme wa Jordan ateuwa kaimu waziri Mkuu baada ya kuvunjwa kwa serikali. - Septemba 15, 2024

Jioni - Voice of America

Play Episode Listen Later Sep 15, 2024 29:59


Matangazo ya saa nzima kuhusu habari za kutwa, ikiwa ni pamoja ripoti kutoka kwa waandishi wetu sehemu mbali mbali duniani na kote Afrika Mashariki na Kati, na vile vile vipindi na makala maalum kuhusu afya, wanawake, jamii na maendeleo.

Jioni - Voice of America
Waziri Mkuu wa zamani wa Kenya Raila Odinga yupo kwenye kinyang'anyiro cha kuwania nafasi ya uenyekiti wa tume ya Umoja wa Afrika - Agosti 27, 2024

Jioni - Voice of America

Play Episode Listen Later Aug 27, 2024 29:59


Matangazo ya saa nzima kuhusu habari za kutwa, ikiwa ni pamoja ripoti kutoka kwa waandishi wetu sehemu mbali mbali duniani na kote Afrika Mashariki na Kati, na vile vile vipindi na makala maalum kuhusu afya, wanawake, jamii na maendeleo.

Alfajiri - Voice of America
Rais Biden na Waziri Mkuu Netanyahu wafanya mazungumzo - Agosti 22, 2024

Alfajiri - Voice of America

Play Episode Listen Later Aug 22, 2024 30:00


Matangazo ya nusu saa kuhusu habari za mapema asubuhi pamoja na habari za michezo.

Jioni - Voice of America
Maelfu ya waandamanji wakusanyika nje ya jengo la bunge la Marekani kabla ya waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu, kulihutubia. - Agosti 07, 2024

Jioni - Voice of America

Play Episode Listen Later Aug 7, 2024 29:59


Matangazo ya saa nzima kuhusu habari za kutwa, ikiwa ni pamoja ripoti kutoka kwa waandishi wetu sehemu mbali mbali duniani na kote Afrika Mashariki na Kati, na vile vile vipindi na makala maalum kuhusu afya, wanawake, jamii na maendeleo.

Jioni - Voice of America
Waziri Mkuu wa Uingereza Keir Starmer anaapa kuweka vikwazo vya uhalifu kuhusu ghasia za mrengo wa kulia zilizozuka nchini mwake. - Agosti 05, 2024

Jioni - Voice of America

Play Episode Listen Later Aug 5, 2024 29:59


Matangazo ya saa nzima kuhusu habari za kutwa, ikiwa ni pamoja ripoti kutoka kwa waandishi wetu sehemu mbali mbali duniani na kote Afrika Mashariki na Kati, na vile vile vipindi na makala maalum kuhusu afya, wanawake, jamii na maendeleo.

keir starmer agosti afrika mashariki uingereza waziri mkuu uhalifu
SBS Swahili - SBS Swahili
Taarifa ya Habari 2 Agosti 2024

SBS Swahili - SBS Swahili

Play Episode Listen Later Aug 2, 2024 16:25


Waziri Mkuu amesema maoni ya watu wanao ishi na ulemavu yanasikizwa, kufuatia ukosoaji ulio ibuka kufuatia jibu la serikali kwa tume yakifalme kwa ulemavu.

agosti habari waziri mkuu
Jioni - Voice of America
Maelfu ya waandamanaji wakusanyika nje ya jengo la bunge la Marekani kabla ya Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu kulihutubia. - Julai 24, 2024

Jioni - Voice of America

Play Episode Listen Later Jul 24, 2024 29:59


Matangazo ya saa nzima kuhusu habari za kutwa, ikiwa ni pamoja ripoti kutoka kwa waandishi wetu sehemu mbali mbali duniani na kote Afrika Mashariki na Kati, na vile vile vipindi na makala maalum kuhusu afya, wanawake, jamii na maendeleo.

Jioni - Voice of America
Waziri Mkuu wa Uingereza Keir Starmer anasema serikali yake haitatekeleza sera za mtangulizi wake kuwahamisha waomba hifadhi kwenda Rwanda - Julai 06, 2024

Jioni - Voice of America

Play Episode Listen Later Jul 6, 2024 29:59


Matangazo ya saa nzima kuhusu habari za kutwa, ikiwa ni pamoja ripoti kutoka kwa waandishi wetu sehemu mbali mbali duniani na kote Afrika Mashariki na Kati, na vile vile vipindi na makala maalum kuhusu afya, wanawake, jamii na maendeleo.

SBS Swahili - SBS Swahili
Viongozi wadini, Waziri Mkuu waomba uwepo wa heshima na maelewano katika jamii

SBS Swahili - SBS Swahili

Play Episode Listen Later Apr 26, 2024 10:32


Viongozi kutoka jumuiya za wayahudi, waislamu na wakristo mjini Sydney wame kemea kwa pamoja vurugu na maneno yakugawanya ambayo yame ibuka kufuatia matukio mawili ya shambulizi ya visu mjini Sydney.

SBS Swahili - SBS Swahili
Taarifa ya Habari 23 Aprili 2024

SBS Swahili - SBS Swahili

Play Episode Listen Later Apr 23, 2024 18:03


Waziri Mkuu amewasifu wanajeshi wa Australia walio kuwa sehemu ya historia ya jeshi, katika eneo la Kokoda Track anapo jiandaa kutembea katika nyayo zamagwiji.

SBS Swahili - SBS Swahili
Taarifa ya Habari 19 Aprili 2024

SBS Swahili - SBS Swahili

Play Episode Listen Later Apr 19, 2024 15:34


Waziri Mkuu ame sisitiza umuhimu wa mshikamano wakijamii nchini Australia, kufuatia uchunguzi kwa shambulizi lakigaidi la kudungwa kisu ndani ya kanisa wiki hii.

Alfajiri - Voice of America
Rais mpya wa Senegal Faye amteua mshirika wake Ousmane Sonko kama waziri mkuu - Aprili 03, 2024

Alfajiri - Voice of America

Play Episode Listen Later Apr 3, 2024 29:59


Alfajiri - Voice of America
Makazi ya waziri mkuu wa Libya yashambuliwa kwa guruneti - Aprili 01, 2024

Alfajiri - Voice of America

Play Episode Listen Later Apr 1, 2024 30:00


libya aprili waziri mkuu
Jioni - Voice of America
Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed yupo Kenya kwa ziara ya kiserikali inayolenga kuimarisha ushirikiano baina ya nchi ya Ethiopia na Kenya - Machi 13, 2024

Jioni - Voice of America

Play Episode Listen Later Mar 13, 2024 29:59


Matangazo ya saa nzima kuhusu habari za kutwa, ikiwa ni pamoja ripoti kutoka kwa waandishi wetu sehemu mbali mbali duniani na kote Afrika Mashariki na Kati, na vile vile vipindi na makala maalum kuhusu afya, wanawake, jamii na maendeleo.

Jioni - Voice of America
Waziri mkuu mstaafu wa Tanzania, Edward Lowassa azikwa - Februari 17, 2024

Jioni - Voice of America

Play Episode Listen Later Feb 17, 2024 29:59


Matangazo ya saa nzima kuhusu habari za kutwa, ikiwa ni pamoja ripoti kutoka kwa waandishi wetu sehemu mbali mbali duniani na kote Afrika Mashariki na Kati, na vile vile vipindi na makala maalum kuhusu afya, wanawake, jamii na maendeleo.

SBS Swahili - SBS Swahili
Taarifa ya Habari 8 Februari 2024

SBS Swahili - SBS Swahili

Play Episode Listen Later Feb 9, 2024 6:39


Waziri Mkuu wa Papua New Guinea James Marape, ame hotubia bunge la Australia.

australia habari waziri mkuu
SBS Swahili - SBS Swahili
Taarifa ya Habari 6 Februari 2024

SBS Swahili - SBS Swahili

Play Episode Listen Later Feb 6, 2024 21:08


Waziri Mkuu amekosoa upinzani kwa kufeli kuwa na msimamo kwa pendekezo lake la awamu ya tatu ya makato ya kodi, wakati vikao vya bunge la shirikisho vina anza tena.

habari waziri mkuu
SBS Swahili - SBS Swahili
Taarifa ya Habari 24 Novemba 2023

SBS Swahili - SBS Swahili

Play Episode Listen Later Nov 24, 2023 19:32


Waziri Mkuu amesisitiza kuwa serikali yake inafanya iwezavyo kupunguza mfumuko wa bei, na kiongozi wa benki kuu ana amini inaendelea kutokea ndani.

habari novemba waziri mkuu
Alfajiri - Voice of America
DRC kuhamisha ubalozi wake wa Israeli kutoka Tel Aviv hadi Jerusalem - Septemba 22, 2023

Alfajiri - Voice of America

Play Episode Listen Later Sep 22, 2023 29:59


Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo itahamisha ubalozi wake wa Israeli hadi Jerusalem kutoka Tel Aviv, Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu alisema Ijumaa.

SBS Swahili - SBS Swahili
Taarifa ya Habari 21 2023

SBS Swahili - SBS Swahili

Play Episode Listen Later May 21, 2023 18:48


Upinzani wa shirikisho waukosoa mpango wa Waziri Mkuu, kufanya ziara China kabla ya vikwazo vyote vya kibiashara kuondolewa dhidi ya Australia.

SBS Swahili - SBS Swahili
Taarifa ya Habari 16 Mei 2023

SBS Swahili - SBS Swahili

Play Episode Listen Later May 16, 2023 18:30


Waziri Mkuu ametupilia mbali madai kuwa sera yamakazi ya serikali, ita andikwa tena katika kongamano lakitaifa la chama cha Labor.

labor habari waziri mkuu
SBS Swahili - SBS Swahili
Taarifa ya Habari 7 Machi 2023

SBS Swahili - SBS Swahili

Play Episode Listen Later Mar 7, 2023 18:14


Waziri Mkuu akataa kutenga gesi kwenye matumizi ya nishati, ili muswada wake uungwe mkono na chama cha Greens bungeni.

SBS Swahili - SBS Swahili
Taarifa ya Habari 5 Machi 2023

SBS Swahili - SBS Swahili

Play Episode Listen Later Mar 5, 2023 14:14


Waziri Mkuu aikosoa serikali ya NSW katika kampeni ya uchaguzi jimboni humo.

nsw machi habari waziri mkuu
Habari za UN
18 JANUARI 2023

Habari za UN

Play Episode Listen Later Jan 18, 2023 0:11


Hii leo jaridani tunakupeleka Davos Uswisi kusikiliza hotuba ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa na pia kuangazia tuzo ya mwaka 2023 iitwayo Crystal Award. Makala na mashinani tunasalía huko huko, kulikoni?Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema dunia haiwezi kutatua changamoto kubwa inazokabiliwa nazo hivi sasa kuanzia mabadiliko ya tabianchi, vita ya Ukraine, mdororo wa uchumi na athari zinazoendelea za janga la COVID-19 katikia hali ya sasa ya mgawanyiko na kutokuwa na mshikamano hivyo wakati wa kufumbia macho changamoto hizi umepita na wanaochangia wawajibishwe.Mabalozi wawili wa shirika la Umoja wa Mataifa la maendeleo ya kilimo duniani, IFAD, Sabrina Dhowre Elba na mumewe Idris Elba wamepatiwa tuzo ya mwaka 2023 iitwayo Crystal Award kutokana na uongozi wao wa kupaza sauti kwa niaba ya mamilioni ya wakulima wadogo maskini duniani kote ambao hufanya kazi kila siku kuzalisha theluthi moja ya chakula chote duniani.Makala tunakwenda huko Fez, kuangazia mkutano wa tisa wa Jukwaa la Umoja wa Mataifa la Muungano wa Ustaarabu, UNAOC.Na katika mashinani tunasalia huko nchini Uswisi ambapo tutamsikia Waziri Mkuu wa Finland. Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!

SBS Swahili - SBS Swahili
Taarifa ya Habari 22 Novemba 2022

SBS Swahili - SBS Swahili

Play Episode Listen Later Nov 22, 2022 17:56


Waziri Mkuu na kiongozi wa New South Wales wametembelea mji wa Eugowra ambao uliathiriwa kwa mafuriko, kutangaza utoaji wa ruzuki ya ziada.

Habari za UN
26 SEPTEMBA 2022

Habari za UN

Play Episode Listen Later Sep 26, 2022 12:51


Hii leo kwenye Habari za UN Flora Nducha anaanza na Sudan Kusini ambako wataalamu wa Umoja wa Mataifa wa haki za binadamu nchini humo wanataka jamii ya kimataifa itupie jicho la umakini mkataba wa amani wa mwaka 2018 ili uweze kutekelezwa kwa umakini, kwani hivi sasa kuna shaka na shuku ya utekelezaji wake kikamilifu. Kisha ni nchini Tanzania ambako shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo, FAO limezindua mradi wa thamani ya zaidi ya dola milioni 9 ili kuimarisha usalama wa mazao. Makala ni kijana mkimbizi kutoka Sudan Kusini ambaye sasa anaishi Canada. Mashinani tunamulika mjadala mkuu wa mkutano wa 77 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kwa ujumbe wa Waziri Mkuu wa Samoa kuhusu athari za mabadiliko ya tabianchi hasa kwa nchi za visiwa vidogo. Karibu!