Makala yanayochambua masuala na matukio mbalimbali yaliyotokea kwenye jamii kwa wiki nzima kwa kina, yanatoa fursa kwa msikilizaji kueleza hisia na mtazamo wake juu ya masuala yanayoendelea kutokea iwe ni katika uga wa uchumi na siasa duniani kote.
RFI - Radio France Internationale
Miongoni mwa taarifa utakazoziskia ni pamoja na; Bunge la seneti nchini DRC lapiga kura ya kumuondolea kinga rais mtaafu Joseph kabila, Wanaharakati wa kutetea haki za binadamu na Mawakili mashuhuri kutoka nchini Kenya, wafukuzwa nchini Tanzania. Kwingineko, Mamlaka nchini Libya zagundua miili 58 iliohifadhiwa kwa muda katika chumba cha kuhifadhi maiti na Waziri mkuu wa Israeli, Benjamin Netanyahu awatuhumu viongozi wa Ufaransa, Uingereza na Canada kwa kuwapa nguvu kundi la Hamas.
Makala haya yanaangazia taarifa mbalimbali ikiwemo, Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki nchini DRC wamtaka Rais Felix Tshisekedi kuwaamini viongozi wa dini kusaidia kuleta amani na utulivu Mashariki mwa nchi hiyo na pia serikali ya Uganda yawasilisha mswada tata bungeni kuruhusu kesi za kiraia kupelekwa kwenye Mahakama ya kijeshi. Taarifa zingine ambazo utaziskia ni uongozi wa kijeshi nchini Mali wasitisha sheria kuhusu vyama vya siasa nchini humo na Mazungumzo ya ana kwa ana kati ya wajumbe wa Ukraine na Urusi yamefanyika wiki hii nchini Uturuki kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2022.
Makala haya yanaangazia taarifa mbalimbali ikiwemo, Mmarekani Robert Francis Prevost, achaguliwa kuongoza kanisa katoliki duniani, akichukua jina la Papa Leo wa kumi na nne. Chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania, Chadema, chatumbukia katika sintofahamu zaidi kufuatia baadhi ya waliokuwa wajumbe wa kamati kuu ya chama, kutangaza kujiondoa kwenye chama hicho. Tarifa zingine utakazoskia, silaha za China zilizoagizwa na taifa la Falme za Kiarabu zimepatikana zikitumika na wapiganaji wa RSF nchini Sudan, na nchi jirani za India na Pakistan zashambiliana kwa silaha nzito na kuzua wasiwasi mkubwa katika maeneo ya mipakani.
Makala hii imeamgazia kuuawa kwa mbunge wa Kasipul Charles Ong'ondo Were, kwa kupigwa risasi na watu waliokuwa kwa pikipiki katika barabara ya Ngong Jijini Nairobi, jumatano, kukamatwa kwa mlinzi wake kiongozi wa chama cha upinzani cha NUP nchini Uganda, nao wawakilishi wa DRC na Rwanda wanaokutana Washington Marekani kusaini mkataba kuelekea makubaliano ya amani ya mashariki mwa DRC, siasa za Tanzania na kushambuliwa kwa kasisi wa kikatoliki na matukio kadhaa ya juma hili kutokea duniani
Makala ya yaliyojiri wiki hii imeangazia mazishi ya kiongozi wa kanisa katoliki duniani Papa Francis, DRC na Rwanda zatia saini makubaliano kuhusu njia ya kupatikana amani ya mashariki mwa Congo, siasa za Tanzania kuelekea uchaguzi wa oktoba, ziara ya rais wa Kenya William Ruto huko China, hali ya vita ya Sudan, vita ya Ukraine na huko Gaza Israeli, ni miongoni mwa Habari kuu za dunia zilizojiri kwa juma hili.
Vita ya sudan Kuingia katika mwaka wa tatu wiki hii, Kenya yatangaza marufuku ya biashara ya figo baada ya ufichuzi, rais wa zamani wa DRC arejea nchini aliwasili mjini Goma huku Marekani ikiitaka nchi ya Rwanda kuondoa wanajeshi wake mashariki mwa nchi hiyo, tumeangazia siasa za Tanzania kuelekea uchaguzi wa Oktoba, kule Sahel na wito wa rais wa Ghana wiki hii akiwataka viongozi wa nchi hizo kuungana pamoja na pia mkutano wa Paris kuhusu hatima ya vita ya Ukraine
Matukio ya wiki: kukamatwa kwa mwenyekiti wa chama cha upinzani cha Chadema nchini Tanzania, Tundu Lisu, maadhimisho ya miaka 31 ya mauaji ya kimbari ya nchini Rwanda mwaka 1994, mafuriko jijini Kinshasa huko DRC, hali ya sudan Kusini kutokana na kukamatwa na kuzuiwa nyumbani kwa makamu wa kwanza wa rais Riek Machar, uchaguzi wa Gabon, na pia mzozo wa kibiashara kati ya Marekani na mataifa mengine ulimwenguni ni miongoni mwa Habari kuu za dunia zilizojiri kwa juma hili.
Miongoni mwa matukio makubwa ya juma hili ni pamoja na ziara ya rais wa Uganda Yoweri Museveni, iliyotangulizwa na ziara ya wajumbe wa Umoja wa Afrika, nchini Sudan Kusini baada ya makamu wa rais wa nchini hiyo kukamatwa na kuzuiwa nyumbani kwake, kule DRC waasi wa M23 wanaoungwa mkono na Rwanda waripotiwa kujiondoa katika mji wa Walikale mokowani Kivu kaskazini mashariki mwa DRC, tunaangazia Kenya, Uganda, nchi za Afrika mashariki na magharibi pia kwengineko duniani
Ni juma ambalo limeshuhudia kukamatwa kwa makamu wa kwanza wa rais wa sudan Kusini Riek Machar na kuzuiwa nyumbani kwake, rais wa Burundi Evariste Ndayishimiye wiki hii aliishutumu Rwanda kwa kupanga kuishambulia nchi yake, waasi wa M23 kukutana na Kiongozi wa Qatar kule Doha,afisa wa polisi ya Kenya kule Haiti kutoweka, utawala wa kijeshi kule Niger kuzindua kipindi cha mpito cha miaka mitano, pia mashambulio ya Israeli kule Lebanon na mkutano wa Ulaya kuhusu Ukraine
Yaliyomo ni pamoja na Mkutano wa ana kwa ana kati ya rais wa DRC Felix Tshisekedi na mwenzake wa Rwanda Paul Kagame mjini Doha Qatar, mapigano kule Sudan Kusini kati ya wanajeshi wa serikali na wapiganaji wa white Army waliotiifu kwa makamu wa kwanza wa rais Riek Machar, Niger kujivua uanachama wa franchophonie, mashambulio ya Israeli kule Gaza, sintofahamu ya sitisho la mapigano kwa muda mfupi kati ya Urusi na Ukraine ni miongoni mwa habari kuu za dunia zilizojiri kwa juma hili.
Mazungumzo ya ana kwa ana kati ya DRC na waasi wa M23 wanaosaidiwa na Rwanda kuanza jumanne ya Marchi 18, SADC kusitisha operesheni zake mashariki mwa DRC, mapigano kule Sudan Kusini kati ya wanajeshi wa serikali na wapiganaji waliotiifu kwa makamu wa kwanza wa rais Riek Machar, juhudi za kikanda kuyahamasisha mataifa ya Mali, Burkina faso na Niger kurejea tena kama wanachama wa ECOWAS, na sitisho la mapigano kwa muda mfupi kati ya Urusi na Ukraine, ni miongoni mwa yaliyojiri wiki hii
Rais wa Kenya William Ruto na aliyekuwa kiongozi wa upinzani Raila Odinga wameungana kisiasa rasmi, hali ya mzozo wa mashariki mwa DRC Kuchukua sura mpya, vikwazo vya kiuchumi kuikumba nchi ya Rwanda kufuatia uungwaji mkono wake kwa kundi la waasi la M23, Kiongozi wa kijeshi wa Gabon jenerali Oligui Nguema kuwania urais mwezi ujao, mzozo wa kibiashara kati ya Marekani nchi mataifa kadhaa, lakini pia mzozo wa Ukraine na Urusi.
Wiki hii kwenye habari za ulimwengu tunaangalia majibizano makali kati ya rais wa Marekani Donald Trump na mwenzake wa Ukraine Volodymyr Zelensky katika Ikulu ya White House, pia tunaangalia mikakati inayowekwa kumaliza mgogoro wa DRC huku Rwanda ikisema haitishwi kutengwa na ulimwengu, Somalia na Ethiopia zarejesha uhusiano wa kidiplomasia, mkutano wa G20 ukikamilika kule Afrika Kusini bila mwafaka kufikiwa.
Habari za wiki hii ni pamoja na hali kule nchini Mashariki mwa DRC, utata wa kidplomasia uanozingira Kenya na Sudan, tutaangazia pia kesi ya kiongozi wa upinzani nchini Uganda Kizza Besigye, lakini tutaangalia kipindi cha mpito nchini Niger. Tumedadisi pia hali kufikia sasa ya vita vya kule Gaza na misimamo ya viongozi mbalimbali wa ulimwengu.
Makala hii imeangazia mkutano wa viongozi wa Afrika mjini Addis Ababa Ethiopia ambapo wamemchagua kiongozi wa tume ya Umoja wa Afrika AU kati ya wagombea watatu, lakini pia mapigano yanayoendelea kati ya waasi wa M23 wanaoungwa mkono na Rwanda dhidi ya jeshi la serikali FARDC na ambao sasa wameudhibiti mji wa Bukavu huko Kivu kusini mashariki mwa DRC, mapigano ya nchini Sudan, siasa za Uganda na pia kwenye nchi za Afrika Magharibi. Lakini pia zoezi la ubadirishanaji wa mateka huko Gaza
Kwa sehemu kubwa makala ya mtazamo wako imeangazia kuhusu hali ya mashariki mwa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo na mkutano wa pamoja kati ya jumuia ya Afrika mashariki EAC na jumuia ya Nchi za kusini mwa Afrika SADC kutafuta suluhu ya kudumu ya mzozo wa mashariki mwa DRC, huko Gabon upinzani umemtaka kiongozi wa mpito kuweka wazi msimamo wake kuhusu ushiriki wake katika uchaguzi mkuu, na hatua ya rais wa Marekani Donald Trump kukata ufadhili kwa shirika la misaada USAID pia Marekani kudhibiti eneo la Gaza
Makala ya yaliyojiri wiki hii kwa sehemu kubwa imejikita katika kudadavua hali yausalama wa mashariki mwa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo ambako tangu mwanzo wa juma hili kulishuhudiwa mapigano makali kati ya jeshi la Nchi hiyo na waasi wa M23 wanaosaidiwa na Rwanda kwenye mji wa Goma, lakini pia siasa za mataifa ya Kenya, Uganda, Tanzania na maeneo mengine duniani
Kuapishwa kwa Donald Trump kama rais wa 47 wa Marekani, Mkutano wa kimataifa kuhusu uchumi huko Davos, Hali ya kibinadamu kuendelea kuzorota mashariki mwa DRC, Tundu Lissu ateuliwa kuwa mwenyekiti mpya wa chama cha Upinzani cha Chadema kule Tanzania, tutaangazia Sisa za Kenya, Sudan na maeneo Ya Afrika magharibi pia kwengineko duniani.
Miongoni mwa yale tumekuandalia wiki hii ni pamoja na kuapishwa kwa Rais Mteule wa Marekani Donald Trump, mapigano yanyoendelea kuripotiwa mashariki ya DRC, makubaliano ya kusitishwa kwa vita kati ya Hamas na Israeli.
Makala hii imeangazia mapigano eneo la mashariki mwa DRC, mvutano wa kisiasa nchini Kenya pamoja na hali ya Sudan, kauli ya rais wa Ufaransa Emmanuel Macron kwamba mataifa ya Afrika hayana shukrani katika kuyataka majeshi ya Ufaransa kuondoka kwenye ardhi zao na mazishi ya aliyekuwa rais wa 39 wa Marekani Jimmy Carter wiki hii
Makala hii imeangazia namna ambavyo nchi zetu zilivyoukaribisha mwaka wa 2025 kwa shamrashamra za kila aina huku wakisema kwaheri kwa mwaka 2024 ulioshuhudia michezo mikubwa zaidi ulimwenguni ya Olimpiki, vita ya Ukraine na kule Gaza, usalama mashariki mwa DRC, Sudan pamoja na kurejea madarakani kwa aliyekuwa rais wa Marekani, Donald Trump.
Makala imeangazia namna ambavyo polisi nchini Kenya walivyotawanya maandamano ya wanaharakati waliopinga ukatili dhidi ya wanawake na mauaji nchini humo. Rais wa DRC Felix Tshisekedi alilihutubia taifa mbele y amabunge yote mawili, na kuonyesha kwamba Rwanda inatatiza usalama wa mashariki, siasa za Tanzania, Sudani, na Francois Bayrou ateuliwa kuwa waziri mkuu mpya wa Ufaransa pia hali nchini Israeli.
Habari kuu wiki hii ni pamoja na mkutano kati ya rais wa Marekani anayejiandaa kuondoka madarakani Joe Biden na viongozi wa Afrika huko Lobito Angola, mazungumzo ya amani ya Sudan Kusini kuanza tena baada ya miezi minne, maafisa 20 wa Kenya waliopelekwa Haiti wajiuzulu, rais wa DRC Felix Tshisekedi kukutana na rais wa Rwanda Paul Kagame desemba 15, yaliyojiri Sudan uchaguzi nchini Ghana, na wabunge wa Ufaransa walivyoiangusha serikali ya Michel Barnier lakini pia kanisa kubwa la Notre Dame lafunguliwa jijini Paris Ufaransa, Israel yaendeleza mashambulizi Gaza
Miongoni mwa yale utakayoyasikia kwenye habari ni pamoja na Rais wa DRC, Felix Tschisekedi, kuwataka raia wa nchi yake kuunga mkono mabadiliko ya katiba, , Chama tawala cha CCM nchini Tanzania chaongoza kwa asilimia 99 ya kura.Zaidi ya watu 100 hawajulikani walipo baada ya ajali ya maporomoko ya Udongo nchini Uganda,pia Tutaangazia ziara yake Rais wa Nigeria, Bola Tinubu, nchini Ufaransa, Raia wa Namibia wapiga kura, kisha kimataifa tutaangazia mkutano wa Mawaziri wa mambo ya nje kutoka muungano wa G7,uliofanyika mjini Roma Italia.
Maaskofu wa kanisa katoliki nchini Kenya wameukosoa utawala wa Ruto, wataka kukomeshwa, utekaji nyara na ukiukaji wa haki za binadamu, wapinzani nchini DRC wajitokeza kupinga mpango wa kubadilisha katiba, Rwanda yafanikiwa katika mapambano yake dhidi ya ugoinjwa wa Murbag, kura ya maoni kuhusu katiba mpya kufanyika jumamosi nchini Gabon,Kamati maalum ya Umoja wa Mataifa yaunga mkono ripoti kwamba Israel inatekeleza mauaji ya kimbari jijini Gaza
Donald Trump achaguliwa kuwa rais wa 47 wa Marekani, Ziara ya rais wa Kenya William Ruto huko Addis Ababa Ethiopia, na Sudan Kusini, na Raila Odinga kuzindua azma yake ya kuwania uenyekiti wa tume ya Umoja wa Afrika, kuelekea uchaguzi huo utakaofanyika Februari mwaka 2025. Mapigano makali kati ya waasi wa M23 na wazalendo mashariki mwa DRC, Umoja wa Mataifa wasema uamuzi wa kuahirishwa uchaguzi nchini Sudani Kusini haukubaliki, Duma Boko atawazwa rasmi kama rais mpya wa Botswana, Uhusiano wa Urusi na Marekani baada ya Trump kushinda uchaguzi
Kuapishwa kwa makamu mpya wa rais wa Kenya Profesa Kithure Kindiki, ziara ya rais wa DRC Félix Tshisekedi Kampala Uganda huku mapigano kati ya waasi wa M23 na wazalendo yakiripotiwa mashariki mwa nchi yake, mkutano wa Comesa watamatika Jijini Bujumbura Burundi, Umoja wa mataifa wasema hali ya kibinadamu nchini Sudan yatia wasiwasi, upinzani washinda uchaguzi mkuu Botswana, kampeni za lala salama Marekani, lakini pia kauli ya Korea Kaskazini kuwa itasimama na Urusi hadi ushindi wake huko Ukraine.
Kauli ya rais wa DRC kuhusu marekebisho ya katiba yazua hisia mseto, kesi ya naibu wa Rais wa Kenya aliyeenguliwa madarakani Rigathi Gachagua yaendelea, umoja wa Ulaya kuendeleza shinikizo ilizoiwekea Burundi mwaka 2015 hadi mwaka 2025. Ziara ya mkuu wa UNHCR Fillipo Grandi nchini Uganda, mgombea wa chama tawala kule Msumbiji awa mshindi wa uchaguzi mkuu, uchaguzi mkuu wa Marekani na mengineyo.
Kuondolewa madarakani kwa naibu wa rais wa Kenya Rigathi Gachagua na uteuzi wa profesa Kithure Kindiki, serikali ya Kinshasa yakaribisha makubaliano yaliyoafikiwa kati ya mawaziri wa mambo ya nje wa DRC na Rwanda kuhusu suala kulitokomeza kundi la FDLR na Rwanda kusema iko tayari kuwaondoa wanajeshi kwenye ardhi ya Congo, maandamano ya upinzani kule Msumbiji baada ya uchaguzi mkuu, kuuawa kwa kiongozi wa Hamas Yahya Sunwar, uchaguzi mkuu wa Marekani na mengineyo.
Wabunge 281 walipiga kura ya ndio kumwondoa naibu wa Rais wa Kenya Rigathi Gachagua madarakani, mazishi ya watu waliokufamaji katika ajali ya Meli huko Goma DRC, ziara ya mkurugenzi wa kituo cha kuzuia na kudhibiti magonjwa barani Afrika, Dr Jean Kaseya, nchini Rwanda kutathmini mikakati ya kupambana na mlipuko wa MPOX pamoja na marburg, mafuriko makubwa nchini Mali, mashambulio ya jeshi la Israeli dhidi ya ngome za Hezbollah nchini Lebanon, mchakato wa uchaguzi mkuu kule Marekani. Ungana na Ruben Lukumbuka kusikiliza zaidi
Makala imeangazia mchakato wa kumwondoa madarakani naibu wa rais wa Kenya Rigathi Gachagua, makumi ya watu wafamaji katika ajali ya boti huko Goma mashariki mwa DRC, hali nchini Rwanda na ugonjwa wa murburg, Uganda na Sudan, siasa za Nigeria na maeneo mengine ya Afrika magharibi, mashambulio ya jeshi la Israeli dhidi ya ngome za Hezbollah nchini Lebanon na yale ya Hezbollah nchini Israeli na mambo mengine.
Mwanasiasa wa upinzani kule Tanzania Tundu Lisu kuishitaki serikali na kampuni ya mawasiliano TIGO kwa jaribio la kumuua, rais wa Kenya William Ruto alisema polisi 2500 watapelekwa Haiti, wakati rais wa DRC Félix Tshisekedi atoa wito kwa jumuia ya kimataifa kuiwekea vikwazo Rwanda kwa kuivamia nchi yake na kushirikiana na waasi wa M23, hali nchini Sudan, siasa za Senegal na maeneo mengine ya Afrika magharibi, mashambulio ya jeshi la Israeli dhidi ya ngome za Hezbollah nchini Lebanon na mengineyo.
Makala hii imeangazia kauli ya rais wa Tanzania kwa mabalozi wanaowakilisha nchi zao ilivyozua gumzo katika uga wa kimataifa, msamaha wa mahakama kwa afisa mkuu wa polisi Kenya, ziara ya mjumbe wake katibu mkuu wa umoja wa mataifa anayehusika na masuala ya kibinadamu ulinzi wa amani Jean Pierre Lacroix huko DRC, UN kughadhabishwa na kuahirishwa uchaguzi wa sudan Kusini, jeshi Ia Israeli lashambulia Hezbollah kwa kulipua vifaa vyao vya mawasiliano na kwengineko duniani.
Ni wiki iliyoshuhudia matukio mengi miongoni ni pamoja na serikali ya Kenya kuendelea na uchunguzi wa mkasa wa moto uliowauwa wanafunzi, maandamano ya maelfu ya wakimbizi kwenye mji wa Goma mashariki mwa DRC wakiomba serikali iwarejeshe makwao na kumaliza vita, kule Senegal rais Bassirou alilivunja Bunge la taifa, na mdahalo wa kwanza wa televisheni kati ya rais wa zamani wa Marekani Donald Trump na makamu wa rais Kamala Harris wanaowania kiti cha urais katika uchaguzi wa Novemba na mengineyo.
Makala hii imeangazia mkutano wa tisa kati ya China na Afrika huko Beijing, wafungwa zaidi ya 100 waliuawa katika gereza la makala nchini DRC, Kenya na mkasa wa moto ulivyowaua wanafunzi Kaunti ya Nyeri, uchaguzi kufanyika nchini Tunisia, na nchini Ufaransa Michel Barnier aliteuliwa kuwa waziri Mkuu, miezi miwili baada ya mvutano wa kisiasa nchini Ufaransa, na mambo mengine kwengineko duniani.
Uzinduzi wa kampeni ya aliyekuwa waziri mkuu wa Kenya Raila Odinga, anayegombea unyekiti wa tume ya Umoja wa Afrika, kongamano la 74 la WHO mjini Brazzaville, nchini Congo, DRC na Kampeni inayoitwa ICC Haki kwa DRC, hali ya usalama kuendelea kuzorota nchini Sudan, shambulio la kigaidi Burkina Faso laua zaidi ya watu 300, hali nchini Israeli, na mchakato wa uchaguzi wa Marekani mwezi Novemba
Tumeangazia katika makala ya wiki hii ni pamoja na ugonjwa wa Mpox ulitangazwa kuwa dharura ya kimataifa, DRC ikiathirika zaidi, nchini Kenya Raila Odinga kutojihusisha tena na siasa, jeshi la Uganda lilivamia na kuharibu kambi ya kundi la waasi la LRA huko Sudan pande hasimu zasusia mkutano wa Geneva, nchini Marekani, makamu wa rais Kamala Harris akubali uteuzi wa chama chake cha Democratic kuwa mgombea wa nafasi ya urais, na mengineyo
Matukio ya dunia yaliyokithiri vichwa vya habari ni pamoja na virusi vya Mpox kutangazwa kuwa janga la dharura la kiafya huku bara la Afrika likiathiriwa zaidi, Burundi yamwachia mwanahabari aliyehukumiwa kifungo cha miaka 10, tutaangazia siasa za Tanzania baada ya wanasiasa wa upinzani kukamatwa baadaye wakaachiwa, lakini pia hatua za mazungumzo kule Geneva kuhusu amani nchini Sudan. Pia tutaangazia mgomo wa vyombo vya habari nchini Senegal kadhalika tutachambua wito wa Umoja wa Mataifa kutaka Afrika kupewa kiti cha kudumu katika baraza la usalama la umoja huoKule Gaza, kundi la Hamas limekataa masharti 'mpya' ya upatanishi na Israeli na mazungumzo ya kupata mkataba wa kusitisha vita hivyo, kurejelewa tena wiki hii jijini Cairo, Misri.
Makala ya Juma hili imeangazia hukumu iliyotolewa dhidi ya kiongozi wa chama cha waasi wa M23/AFC mashariki mwa DRC Corneille Nangaa, Rais wa Kenya aapisha baraza jipya la mawaziri miongoni mwao wanasiasa wa upinzani, mapigano ya nchini Sudan, maandamano nchini Nigeria na uongozi mpya wa mpito nchini Bangladesh baada ya kutoroka kwa waziri mkuu pia tumengazia yaliyojiri kwengineko duniani.
Makala hii imeangazia kuuawa kwa kiongozi wa kundi la Hamas, Ismail Haniyeh nchini Iran, mazishi yake yalifanyika Doha, Urusi, mataifa ya Magharibi wabadilishana wafungwa, waziri mkuu wa DRC Judith Suminwa aongoza kumbukumbu ya mauaji ya halaiki ya wakongo maarufu, Genocost, yaliyojiri nchini Kenya, na mgomo wa wafanyabiashara wa Uganda, hukumu dhidi ya dikteta wa zamani wa nchini Guinea na kwengineko duniani.
Makala imeangazia hafla ya ufunguzi wa michezo ya Olimpiki ya Paris siku ya Ijumaa ya wiki hii, huku miundombinu ya treni za umeme ikishambuliwa, rais William Ruto atangaza baraza la mawaziri akiwajumuisha wanasiasa wanne wa upinzani, kesi dhidi ya kiongozi wa muungano wa waasi Corneille Nangaa jijini Kinshasa nchini DRC, Maandamano na kukamatwa kwa vijana kule Uganda, siasa za Afrika Magharibi, na Kaskazini,Joe Biden ajijiondoa katika ki nyang'anyiro cha uchauguzi huku Kamala Harris akiteuliwa kuwa mgombea wa chama cha Demokratic nchini Marekani.
Makala hii imeangazia hatua ya rais wa Kenya William Ruto ya kuwateua mawaziri wapya baada ya mashinikizo, nchi yake ikishuhudia maandamano ya vijana, Kukamatwa kwa mshukiwa wa mauaji ya watu ambao miili yao ilikutwa jalalani Kware jijini Nairobi akiri kuwaua wanawake 42, rais wa Rwanda Paul Kagame ashinda uchaguzi kwa kishindo, Waasi wa M23 na jeshi la congo FARDC wakubali kusimamisha vita baada ya Marekani kutangaza kuongeza muda wa siku 15 kuruhusu misaada ya kibinadamu...na mengineyo..kwengineko duniani ambako watu wamestushwa ulimwenguni kuhusu hitilafu iliyojitokeza kiteknolojia..-
Makala ya yaliyojiri wiki hii imeangazia hatua ya rais wa Kenya William Ruto kulivunja baraza lake la mawaziri, huku inspekta mkuu wa polisi Japhet Koome akubali kujiuzulu, raia nchini Rwanda wajiandaa kushiriki uchaguzi mkuu wa rais na wabunge nchini Rwanda jumatatu ya julai 15, pia hali ya mapigan yashuhudiwa nchini DRC licha ya wito wa Marekani wa kusitishwa mapigano kwa sababu za kibinadamu.Hali iliyojiri kwenye nchi za Afrika magharibi na kaskazini, Ufaransa, na Marekani.
Miongoni mwa yale utakayosikia katika makala ya wiki hii ni pamoja na hatua ya Rais wa Kenya William Ruto kuzungumza na wapiga kura kwa njia ya mtandao wa X, wanajeshi waliotoroka adui DRC kuhukumiwa na vilevile mkutano wa nchi za Sahel zinazoongozwa na wanajeshi.
Makala hii imeangazia maandamano nchini Kenya huku rais Ruto akisema hatasaini mswada wa fedha wa 2024 uliokuwa umeidhinishwa na wabunge walio wengi, waasi wa M23 huko DRC walifanikiwa kuuteka mji wa kimkakati wa Kanyabayonga wilayani Lubero mashariki mwa DRC, mgomo wa wafanyabiashara nchini Tanzania, na nini hatima yake, siasa za Afrika kusini lakini pia mdahalo kati ya rais wa zamani wa Marekani Donald Trump na Joe Biden kuelekea uchaguzi wa mwaka huu, yaliyojiri nchini Ufaransa na kwengineko Duniani.