Gurudumu la Uchumi

Follow Gurudumu la Uchumi
Share on
Copy link to clipboard

Fahamu masuala kadha wa kadha kuhusu uchumi kama vile, namna ya kupambana na umaskini, mfumuko wa bei, kushamiri kwa matumizi ya dola na athari za kuyumba kwa uchumi wa dunia kwa nchi za Afrika. Mada hizi zinafanyiwa utafiti wa kina na zinazungumzwa kwa lugha rahisi inayoeleweka ili kukufanya uelew…

RFI


    • Sep 30, 2026 LATEST EPISODE
    • every other week NEW EPISODES
    • 9m AVG DURATION
    • 179 EPISODES


    More podcasts from RFI

    Search for episodes from Gurudumu la Uchumi with a specific topic:

    Latest episodes from Gurudumu la Uchumi

    Kiwanda cha kusafisha mafuta Lamu: mwanzo wa mapinduzi ya nishati Afrika Mashariki?

    Play Episode Listen Later Sep 30, 2026 10:04


    Kenya inaagiza karibu mahitaji yake yote ya bidhaa za Petroli kutoka nje, hii ikiwa na maana kuwa bei na upatikanaji wa mafuta katika nchi hii, na kwa kiasi kikubwa katika ukanda unaweza kuathiriwa na mambo yanayotokea katika masoko ya kimataifa, hata hivyo habari njema ni kuwa bilionea wa Afrika Aliko Dangote anajenga kiwanda cha kusafisha mafuta huko Lamu. Kwanini hatua hii ni muhimu? Tufuatilie

    Hormuz na Bab el-Mandeb: Njia za baharini zinazotikisa uchumi wa dunia.

    Play Episode Listen Later Sep 23, 2026 10:04


    Msikilizaji hebu fikiria mafuta unayoweka kwenye gari lako, bidhaa zinazofika kwenye maduka yetu kutoka Asia, mbolea inayotumika kwenye kilimo, au hata gharama ya kusafirisha kahawa na chai kutoka Afrika kwenda masoko ya nje, kwa namna moja au nyingine, sehemu ya uchumi huu inategemea bahari na kufungwa kwa njia ya Hormuz na sasa ile ya Bab el-Mandeb kunauweka uchumi wa dunia hatarini. Ungana nami kwenye makala ya wiki hii kufahamu zaidi.

    Maisha mapya: Jinsi akina mama vijana wanavyobadilisha ujuzi kuwa fursa

    Play Episode Listen Later Sep 9, 2026 10:05


    Nchini Kenya, suala la mimba za utotoni ni changamoto. Kwa mujibu wa ofisi ya Takwimu ya taofa nchini Kenya kupitia utafiti wa mwaka 2022 asilimia 15 ya wasichana wenye umri wa miaka 15 hadi 19 walikuwa wamewahi kupata ujauzito. Katika makala ya Gurudumu la Uchumi wiki hii, tunaangazia namna akina mama hawa wanavyogeuza ujuzi, juhudi na fursa za kiuchumi kuwa njia ya kujitegemea na kuwajengea watoto wao maisha yenye matumaini zaidi.

    Umeme unaweza kuwa injini ya ukuaji wa uchumi Afrika Mashariki?

    Play Episode Listen Later Aug 26, 2026 10:04


    Wikendi iliyopita, Tanzania ilizundua rasmi Mradi wa Umeme wa Maji wa bwawa la Julius Nyerere, lenye uwezo wa kuzalisha megawati 2,115. Mradi huu, uliogharimu takribani shilingi trilioni 7.45 za Tanzania sawa na karibu dola za Marekani bilioni 2.9, unaongeza kwa kiasi kikubwa uwezo wa Tanzania kuzalisha umeme. Katika Makala ya Gurudumu la uchumi wiki hii, tunajiuluza Je, megawati hizi zitageuka kuwa uzalishaji, ajira, biashara na ukuaji wa uchumi?

    Goma: Wanawake wapambana na umaskini licha ya changamoto za usalama.

    Play Episode Listen Later Aug 19, 2026 10:03


    Msikilizaji katika mazingira ambayo migogoro na changamoto za kiuchumi zimeathiri maisha ya kila siku ya wananchi, wanawake wengi wamekuwa wakitafuta njia mbadala za kujipatia kipato na kuendesha familia zao.Hali hii inashuhudiwa katika mji wa Goma, mashariki mwa DRC, ambako baadhi ya wanawake wamegeukia ufugaji wa kuku kama njia ya kujikimu, hasa baada ya shughuli za baadhi ya taasisi za kifedha kutatizika katika maeneo yanayodhibitiwa na waasi wa AFC-M23.

    Je, Nchi Inaweza Kuendelea Bila Dira ya Maendeleo?

    Play Episode Listen Later Aug 12, 2026 10:01


    Msikilizaji taifa linaweza kuishi siku moja baada ya nyingine bila kujua linaelekea wapi. Lakini taifa linalotaka kujenga uchumi imara, ajira bora na maisha bora kwa wananchi wake, linahitaji zaidi ya mipango ya leo, kwa kifupî linahitaji dira. Kwenye makala ya wiki hii tunaangazia dira ya taifa ni nini.

    Sehemu ya Pili: Hatifungani ni nini na kwanini inakuhusu

    Play Episode Listen Later Aug 5, 2026 10:03


    Mara kadhaa tumesikia serikali zetu zikitangaza kuwa zinauza hati fungani za Serikali za muda mfupi na muda mrefu, yaani Government Bonds na Treasury bill, serikali zikikusanya mabilioni ya fedha kutoka kwa wawekezaji. Sasa je, hatifungani ni nini? Je, mwananchi wa kawaida anaweza kuwekeza?

    Hatifungani za serikali na hazina: Kwa nini zinahusu kila mwananchi?

    Play Episode Listen Later Jul 29, 2026 10:01


    Mara kadhaa tumesikia serikali zetu zikitangaza kuwa zinauza hati fungani za Serikali za muda mfupi na muda mrefu, yaani Government Bonds na Treasury bill, serikali zikikusanya mabilioni ya fedha kutoka kwa wawekezaji. Sasa je, hatifungani ni nini? Je, mwananchi wa kawaida anaweza kuwekeza?

    Migogoro ya kimataifa inavyoathiri uchumi wa wananchi Afrika

    Play Episode Listen Later Jul 22, 2026 10:03


    Katika Makala haya hivi leo tunajadili uhusiano kati ya siasa za kimataifa na uchumi wa wananchi wa Afrika, mara yingi tunasikia taarifa za vita, migogoro ya kisiasa au mivutano kati ya mataifa makubwa kama Urusi na Ukraine, Mashariki ya Kati, au migogoro inayovuruga usafirishaji wa bidhaa duniani. Kuzungumzia hili, hivi leo nimemualika Safari Fungo, mtaalamu wa masuala ya uchumi, utangamano wa kikanda na biashara za kimataifa akiwa Dar es Salaam, Tanzania.

    Sarafu za kidijitali ‘Cryptocurrency' uwekezaji wa kisasa wenye fursa na hatari

    Play Episode Listen Later Jul 15, 2026 9:41


    Katika miaka ya hivi karibuni, sarafu za kidijitali maarufu kama cryptocurrency zimezidi kuvutia watu wengi duniani. Wapo waliopata faida kubwa, lakini pia wapo waliopoteza fedha nyingi kutokana na kushuka kwa thamani ya sarafu hizo. Leo katika Makala ya Gurudumu la Uchumi, tunajiuliza: Je, sarafu za kidijitali ‘cryptocurrency' ni uwekezaji wa kweli, au ni uwekezaji wenye hatari kubwa ambao watu wanapaswa kuuchukulia kwa tahadhari?

    Kodi na Maendeleo: Je, tunapata thamani ya kodi tunazolipa?

    Play Episode Listen Later Jul 8, 2026 9:56


    Katika makala ya Gurudumu la Uchumi hivi leo, tunajadili nafasi ya kodi katika maendeleo ya uchumi, umuhimu wa kulipa kodi, na jinsi serikali na wananchi wanavyoweza kushirikiana kujenga uchumi imara na wenye manufaa kwa wote.

    Je, kukopa kunasaidia ukuaji wa uchumi au kunaleta hatari za siku zijazo?

    Play Episode Listen Later Jun 24, 2026 10:04


    Msikilizaji nchi nyingi za Afrika Mashariki zimeendelea kukopa ili kufadhili maendeleo, na huku wadau wengine wakisema mikopo ni muhimu kwa ukuaji wa uchumi, Wengine wanaonya kuwa madeni yanapoongezeka kupita kiasi, serikali hulazimika kutumia fedha nyingi kulipa madeni hayo badala ya kuboresha huduma muhimu kama vile afya, elimu na ajira. Katika Makala ya Gurumu la Uchumi hivi leo, tunauliza: Je, deni la taifa ni daraja la maendeleo au ni mzigo unaoweza kuathiri uchumi wa Afrika?

    Kutoka taslimu hadi kidijitali: Namna simu zinavyobadili mfumo wa malipo Afrika

    Play Episode Listen Later Jun 10, 2026 10:03


    Ufanyaji biashara na utumaji wa fedha kwa njia ya simu za kiganjani barani Afrika unakua kwa kasi, pochi za simu zimerekodi takriban asilimia 19 ya uingiaji wa pesa kwenye eneo la Kusini mwa Jangwa la Sahara, huku wastani wa gharama ya utumaji pesa ukishuka hadi karibu asilimia 3.54 hii ni kwa mujibu wa benki ya dunia. Kwanye Makala ya Gurudumu la uchumi wiki hii, tunaangazia matumizi ya telknolojia za malipo ya mtandaoni hasa kupitia simu, jina langu ni Emmanuel Makundi, Karibu.

    Sekta ya maua Kenya yatikiswa na gharama na kuyumba kwa masoko ya kimataifa

    Play Episode Listen Later Jun 4, 2026 9:55


    Msikilizaji Sekta ya maua nchini Kenya, ambayo kwa muda mrefu imekuwa miongoni mwa nguzo muhimu za uchumi na chanzo kikuu cha mapato ya fedha za kigeni, ikiingizia nchi zaidi ya dola bilioni moja za Marekani kila mwaka, sasa inakabiliwa na changamoto zinazotia wasiwasi kuhusu mustakabali wake.

    Umuhimu wa bara la Afrika kufanya biashara za ndani

    Play Episode Listen Later Jun 3, 2026 10:01


    Katika makala ya wiki hii, tunajadili ni kwanini nchi za Afrika zinapaswa kuongeza kasi ya ufanyaji wa biashara za wenyewe kwa wenyewe kukuza utangamano wa kikanda.

    Mkutano wa 'Africa Forward' una maana gani kwa mustakabali wa Afrika

    Play Episode Listen Later May 6, 2026 9:57


    Tarehe 11 na 12 ya wiki ijayo, Jiji la Nairobi, Kenya litakuwa mwenyeji wa mkutano wa kwanza wa kihistoria wa ‘Africa Forward' kati ya Ufaransa na Afrika, mkutano ambao unafanyika kwenye nchi inazungumza Kingereza, ambapo viongozi wa Afrika, wafanyabiashara na wabunifu vijana kutoka Afrika na Ufaransa watakongamana kwa siku mbili. Kwenye Makala ya Gurudumu la Uchumi hivi leo tunaangazia uhusiano mpya kati ya Ufaransa na Afrika, wachambuzi wetu ni Ali Mkimo na Hamduni Marcel.

    Akili unde na mustakabali wa uchumi wa Afrika: Fursa mpya kwa vijana wabunifu

    Play Episode Listen Later Apr 22, 2026 10:01


    Katika kipindi ambacho Afrika inaendelea kukabiliana na changamoto za kiuchumi na kijamii, teknolojia ya Akili Unde (AI) inaibuka kama nyenzo muhimu ya kuleta mabadiliko. Kutoka kilimo hadi afya, na kutoka elimu hadi utawala bora, ubunifu wa kidijitali unaanza kubadilisha namna matatizo ya muda mrefu yanavyotatuliwa.Katika makala hii, tunazungumza na Kevin Obote kijana mbunifu wa teknolojia ambaye anatumia AI kuunda suluhisho zinazolenga mazingira halisi ya Afrika.

    Kwa nini vikwazo vya usafirishaji ni kizuizi kikubwa cha biashara Afrika Mashariki

    Play Episode Listen Later Apr 1, 2026 9:59


    Kupitia ripoti iliyozinduliwa juma hili na shirikisho la wazalishaji nchini Kenya, inaonyesha kuwa kusafirisha bidhaa katika njia muhimu za biashara za Afrika bado ni ghali na haitabiriki, ambapo wakati mwingine hugharimu hadi dola 7,000 za Marekani kwa kontena moja kati ya Nairobi na Lusaka. Kwenye Makala ya Gurudumu la Uchumi juma hili, tumezungumza na Tobias Alando, mkurugenzi mtendaji wa shirikisho la wamiliki wa viwanda nchini Kenya.

    Uwazi kwenye ubinafsishaji wa mashirika ya uma ni muhimu kwa maendeleo

    Play Episode Listen Later Mar 11, 2026 10:03


    Msikilizaji Katika miaka ya hivi karibuni, nchi nyingi za Afrika Mashariki zimekuwa zikifanya mageuzi makubwa ya kiuchumi. Mojawapo ya mageuzi hayo ni ubinafsishaji wa mashirika ya umma. Leo tunajiuliza, Je, ubinafsishaji ni kweli unasaidia uchumi kukua, au serikali inapaswa kubaki na umiliki wa mashirika muhimu?

    Vita ya Iran: Afrika imejipangaje kukabiliana na athari za kiuchumi

    Play Episode Listen Later Mar 4, 2026 10:03


    Msikilizaji mara zote mgogoro wa mashariki ya kati, umekuwa na athari hasi za kiuchumi na biashara duniani, Swali kubwa tunajiuliza hivi leo ni Je, Afrika iko salama kiasi gani? Vita hivi vitaathiri vipi uchumi wa dunia — na gharama za maisha kwa mwananchi wa kawaida barani Afrika?

    Ushirikishwaji wa wanawake katika sekta za kiuchumi chanzo cha ukuaji wa uchumi

    Play Episode Listen Later Feb 25, 2026 10:01


    Benki ya Dunia inasema hata katika nchi zenye sheria za kisasa kuhusu usawa kazini, nchi hizo zimeshindwa kuzitekeleza, hadi sasa hakuna nchi iliyofikia kiwango cha juu cha usawa kazini, n ani asilimia kidogo tu ya wanawake wanaishi kwenye nchi zenye angalau sheria bora, huku mataifa 70 ikiwemo Misri, Madagascra na Somalia zikipiga hatua katika kuboresha mazingira ya usawa kati yam waka 2023 na 2025. 

    Ushirikiano wa kikanda hatarini: Nakisi ya bajeti yaibua maswali mapya

    Play Episode Listen Later Feb 18, 2026 9:47


    Juma hili tunajadili kuhusu mustakabali wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, hasa wakati huu kukiwa na taarifa kuwa inakabiliwa na mgogoro wa kifedha. Taarifa zinaonesha kuwa Jumuiya hiyo inakabiliwa na upungufu wa bajeti unaofikia karibu dola za marekani milioni 89, pengo ambalo huenda likatatiza shughuli za Jumuiya hiyo, jambo ambalo limemfanya rais wa Kenya William Ruto ambaye ni mwenyekiti wa jumuiya kwa sasa, kuitisha mkutano wa dharura wa wakuu wan chi mwezi ujao.

    kenya juma eac afrika mashariki maswali kenya william ruto
    Dubai: Viongozi wa dunia waangazia mageuzi ya sera, ubunifu na mifumo mipya ya utawala

    Play Episode Listen Later Feb 5, 2026 9:59


    Mkutano wa siku tatu wa Serikali za Dunia mwaka 2026 huko Dubai umesisitiza kuhusu udhibiti wa Akili Mnemba, AI, mageuzi ya kidijitali, uchumi endelevu na thabiti duniani.  Viongozi mbalimbali wametoa wito wa kuwepo ushirikiano thabiti wa kimataifa na mifumo mipya ya utawala inayoweza kutazamia changamoto za siku zijazo lakini pia kushughulikia masuala ya pamoja kama vile mabadiliko ya hali ya hewa, usalama wa mtandao na ukosefu wa usawa wa kiuchumi. Ni mkutano ulioandaliwa kutoka Februari 3-5, 2026. #WorldGovernmentsSummit

    Ushindani wa mataifa makubwa na mustakabali wa uchumi wa Dunia

    Play Episode Listen Later Jan 21, 2026 10:01


    Msikilizaji mataifa makubwa kama Marekani, China, Urusi na Ulaya yanaendelea kushindana kiuchumi, kuanzia kwenye biashara, teknolojia, nishati na rasilimali. Lakini je, ushindani wao unaathiri vipi uchumi wa dunia? Leo kwenye Makala ya Gurudumu la Uchumi tunajadili, “Athari za Kiuchumi kwa Dunia Zitokanazo na Ushindani wa Maslahi ya Kiuchumi kati ya Mataifa Makubwa.”

    Kenya Kuwa Singapore ya Afrika: Ndoto au Uhalisia?

    Play Episode Listen Later Jan 14, 2026 9:55


    Msikilizaji Rais wa Kenya, William Ruto, ameendelea kusisitiza azma ya kuifanya nchi yake kuwa Singapore ya Afrika, suala ambalo limeibua mjadala mkali nchini humo baadhi wakisema ni suala ambalo halitawezekana chini ya utawala wake na wengine wakiona ni jambo linalowezekana. Kwenye makala yetu leo tunajiuliza, je, Kenya inaelekea huko? Ndoto hii inawezekana au ni siasa?

    Kutoka Ufugaji wa Mifugo hadi Samaki: Mabadiliko ya Kiuchumi Kajiado

    Play Episode Listen Later Jan 7, 2026 9:58


    Msikilizaji jamii ya Wamaasai kwa muda mrefu imekuwa ikitegemea ufugaji wa mifugo kama chanzo kikuu cha riziki na chakula, hata hivyo, mabadiliko ya tabianchi yaliyoambatana na ukame wa mara kwa mara yamilazimisha jamii hii kutafuta mbinu mbadala za kujipatia kipato, mojawapo ni ufugaji wa samaki.

    Sherehe za mwisho wa mwaka zisikuache bila pesa, fahamu mbinu za kudhibiti matumizi yako.

    Play Episode Listen Later Dec 24, 2025 10:00


    Tunapofika mwisho wa mwaka, jamii huingia katika kipindi cha sikukuu kama krismasi na mwaka mpya, ni wakati wa furaha, sherehe na kukutana na familia, lakini pia ni kipindi ambacho matumizi ya fedha huongezeka, watu wengi hujikuta wakitumia zaidi ya uwezo wao na mipango kusimama, tunajadili namna gani unaweza kuwa na nidhamu ya matumizi ya mwisho wa mwaka iwe kwa muajiriwa, mjasiriamali au mfanyabiashara.

    Ripoti ya Oxfam-Kenya: Uchumi unakua, lakini Wakenya wengi ni masikini, kwa nini?

    Play Episode Listen Later Dec 3, 2025 9:58


    Msikilizaji juma lililopita shirika la kimataifa la kupambana na umasikini, OXFAM nchini Kenya, ilichapisha ripoti inayoonesha kuongezeka kwa pengo la usawa. Kwa mujibu wa shirika hilo, pengo la walionacho na wasio nacho linaendelea kuongezeka ambapo matajiri 125 wa Kenya kwa sasa wana utajiri wa zaidi ya watu milioni 42 raia wa Kenya. Tunajiuliza, kwa nini ukuaji wa uchumi hauwahusu watu wengi?

    Mapinduzi ya Elimu Bondo: Jinsi Teknolojia Inavyowawezesha Wasichana Kuandika Kesho Yao

    Play Episode Listen Later Nov 26, 2025 10:04


    Katika maeneo mengi nchini, hasa magharibi mwa Kenya, wasichana wengi wanaojikuta wakisuasua katika mitihani ya sekondari huishia kwenye ndoa za mapema na mimba za utotoni—mazingira yanayozima ndoto zao kabla hata hazijachanua. Lakini safari hii, upepo wa mabadiliko umeanza kuvuma. Serikali za majimbo, kwa ushirikiano na Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD), zimeanzisha mpango wa mafunzo ya kitaaluma yanaotumia teknolojia ya kisasa, Lengo likiwa ni moja tu, kuwainua wasichana hawa.

    Mandale: Kinywaji Cha Asili Kinachowainua Wanawake wa Goma

    Play Episode Listen Later Nov 19, 2025 10:01


    Msikilizaji katika uhalisia mgumu wa maisha ya wakazi wa Goma, hususan baada ya mji huo kuangukia mikononi mwa waasi wa AFC/M23, imeibuka hadithi ya kipekee ya uvumilivu na ubunifu wa wanawake. Kati ya changamoto za ukosefu wa ajira na kuyumba kwa uchumi wa familia, wanawake kwenye mji huo wamegeukia ujuzi wa jadi wa kutengenezaji wa kinywaji cha asili kinachoitwa Mandale.

    Nini hatma ya Afrika baada ya kumalizika kwa mkataba wa kibiashara na Marekani ‘AGOA'

    Play Episode Listen Later Oct 1, 2025 10:04


    Mkataba wa kibiashara kati ya Afrika na Marekani maarufu kama AGOA umefika tamati, ni mkataba uliokuwa unatoa fursa kwa nchi za Afrika kufikia soko la Marekani bila vikwazo vya kiushuru, bara hili likitengeneza faida ya mabilioni ya dola kupitia mkataba huu, hata hivyo kukoma kwake tayari kunashuhudiwa athari yalke kwenye baadhi ya nchi, kuanzia katika viwanda vya nguo nchini Kenya hadi kwa wasafirishaji huko Ghana, maisha ya watu walioajiriwa kupitia mkataba huu yako mashakani.

    Vijana na ujasiriamali Afrika Mashariki: Nini kifanyike kuwawezesha?

    Play Episode Listen Later Sep 24, 2025 10:02


    Msikilizaji katika nchi zote za Afrika Mashariki, kuna wimbi jipya la matamanio kuhusu hali ya biashara, vijana, wakiongozwa na ubunifu na ustahimilivu! Wakigeuza harakati zao kuwa biashara zinazostawi, kubadili changamoto kuwa fursa na ndoto kuwa ukweli. Tutazungumza na Andrew Lukuwi, yeye ni mjasiriamali kijana akiwa nchini Tanzania, pamoja na Dr Onesmo Kyauke mchambuzi wa masuala ya uchumi na siasa akiwa Tanzania.

    Mzunguko haramu wa Fedha: Kizuizi kisichoonekana kwa ustawi wa Afrika

    Play Episode Listen Later Sep 3, 2025 10:00


    Kulingana na ripoti ya umoja wa Afrika, bara hilo linapoteza takribani dola za Marekani bilioni 88 kila mwaka kupitia njia zisizo halali kama ukwepaji kodi, utakatishaji fedha, utoroshaji wa mali na mitaji na udanganyifu kwenye biashara. Kwenye Makala ya Gurudumu la Uchumi, tunajiuliza, Kwanini hali hii inaendelea licha ya uwepo wa sheria kali? Nani anafaidika? na nini kifanyike kuzuia upotevu huu mkubwa wa rasilimali fedha? Tutakuwa na wataalamu Walter Nguma na Dr Ponsian Ntui.

    Kuwekeza katika Uchumi wa Bluu: Mkakati wa uhakika au Kamari hatari?

    Play Episode Listen Later Aug 27, 2025 10:03


    Leo hii tunatupia jicho uchumi wa bluu, eneo la kiuchumi linalotajwa kama suluhisho jipya la maendeleo endelevu, kukuza ajira na ubunifu, hata hivyo chini ya uso wa maji, maswali magumu yanajitokeza: Je, tunawekeza kimkakati kwa kuzingatia pia jamii zinazozunguka maeneo haya? Tutazungumza na Dr Ponsian Ntui mhadhiri kutoka chuo kikuu cha Mtakatifu Agustino cha jijini mwanza nchini Tanzania, maarufu kama SAUT.

    Huduma jumuishi za kifedha kidijitali, Afrika iko wapi?

    Play Episode Listen Later Aug 13, 2025 10:07


    Katika makala ya Gurudumu la Uchumi, tunazungumzia mabadiliko makubwa ya kiuchumi kuhusu namna malipo ya kidijitali yanavyochochea huduma jumuishi za kifedha, ukuaji wa uchumi, na mageuzi ya kidijitali kwenye nchi za Afrika. Wageni wetu leo ni Ali Mkimo mchambuzi na mtaalamu wa masuala ya uchumi akiwa Tanzania, pamoja na Lucy Nshuti Mbabazi, mkurugenzi wa taasisi ya Better Than Cash Alliance iliyochini ya shirika la maendeleo la umoja wa mataifa UNDP.

    Vijana wamepata elimu lakini hawana ajira: Changamoto ya ujuzi Afrika Mashariki

    Play Episode Listen Later Aug 6, 2025 9:59


    Kenya, Uganda, Tanzania, Rwanda, na kwingineko, ukosefu wa ajira kwa vijana umesalia kuwa wa kiwango cha juu, wakati huu maelfu ya vijana wakihitimu vyuo vikuu kila mwaka.    Bado tuko na Ali Mkimo, mtaalamu na mchambuzi wa masuala ya uchumi na biashara akiwa Tanzania, pamoja na Kamala Dickson kutoka asasi ya Agenda Participation Initiative ya nchini Tanzania.

    Bomu linalosubiri kulipuka: Kwanini vijana wa Afrika Mashariki hawana ajira licha ya kuwa na shahada

    Play Episode Listen Later Jul 30, 2025 9:51


    Msikilizaji leo tunalijadili swali ambalo linaathiri mamilioni ya vijana katika ukanda wa Afrika Mashariki, pamoja na wageni tutajiuliza, Je, mfumo wa elimu unawaandaa vijana kupata ajira ambazo hazipo tena? Au tunakosa fursa katika sekta zinazoibukia kama vile teknolojia na uchumi bunifu? Tutakuwa na Ali Mkimo, mtaalamu na mchambuzi wa masuala ya uchumi na biashara akiwa Tanzania, pamoja na Kamala Dickson kutoka asasi ya Agenda Participation Initiative ya nchini Tanzania.

    Sehemu ya II: Mfumo mbovu au mafanikio, matajiri 4 Afrika kumiliki nusu ya mali za raia wa bara hilo

    Play Episode Listen Later Jul 23, 2025 9:55


    Bar ala Afrika ni tajiri kwa rasilimali, vipaji na uwezo, hata hivyo, mamilioni ya raia wake bado wamenasa katika lindi la umaskini, huku wachache wakilimbikiza mali zisizomithilika, Je, hii inasema nini kuhusu sera, vipaumbele na mustakabali wa bara la Afrika? Hivi leo kwenye Makala ya Gurudumu la Uchumi, tutajadili tumefikaje hapa, ina maana gani kwa maendeleo na nini kinapaswa kubadilika kujenga uchumi wa haki na shirikishi?

    Sehemu ya I: Mfumo mbovu au mafanikio, matajiri 4 Afrika kumiliki nusu ya mali za raia wa bara hilo

    Play Episode Listen Later Jul 16, 2025 10:04


    Katika bara lenye watu zaidi ya bilioni 1.4, ni watu wanne tu wanaomiliki utajiri zaidi ya nusu ya watu wote. Kulingana na ripoti mpya ya Oxfam, ukosefu huu wa usawa unaostua sio tu takwimu - ni ishara ya wazi ya ukosefu wa haki za kiuchumi uliokita mizizi, mifumo iliyovunjika na kukosekana kwa fursa. Kujadili haya yote nimewaalika Johnson Denge mtaalamu wa uchumi akiwa Nairobi na Apronius Mbilinyi yeye ni mtaalamu wa masuala ya Kodi akiwa Tanzania.

    Kutoka jembe hadi kutumia ndege nyuki (drone): Mapinduzi ya Kilimo Afrika Mashariki

    Play Episode Listen Later Jul 9, 2025 10:04


    Mwezi mmoja uliopita nilipata bahati ya kuzungumza na Octavian Lasway, mhandisi wa maji na umwagiliaji, lakini pia yeye kijana ambaye anatumia teknolojia kuwasaidia wakulima wa nchi za Afrika Mashariki, kufanya kilimo biashara, kupata masoko na kuongeza thamani ya mazao yao. Huu hapa muendelezo wa mahojiano yetu.

    Nchi zinazoendelea kulemewa na madeni: Je, Dunia itasikia kilio chao?

    Play Episode Listen Later Jul 2, 2025 9:52


    Hivi Leo tunaangazia suala nyeti linalogusa maisha ya mamilioni ya watu katika nchi zinazoendelea hususani za bara la Afrika, kama vile kwenye mzigo wa madeni unaozidi kuwa mzito. Tunajiuliza Nini hasa kiko hatarini? suluhisho gani linapendekezwa? Kujadili hili tunazungumza na Ali Mkimo, mchambuzi wa masuala ya uchumi na biashara akiwa Tanzania.

    Utakatishaji Fedha: Kenya yawekwa kwenye orodha ya nchi zilizo na changamoto, Uganda ikiondolewa.

    Play Episode Listen Later Jun 26, 2025 10:00


    Mwezi Juni mwaka 2025, Tume ya Ulaya iliorodhesha Kenya miongoni mwa nchi zenye changamoto ya utakatishaji wa fedha, huku Uganda ikipata afueni kwa kuondolewa kwenye orodha hiyo. Hatua hii ina maana kuwa mashirika ya kifedha – ikiwemo benki – zinalazimika kuzingatia kwa makini uhusiano wa kibiashara na miamala yoyote inayohusiana na nchi zilizo kwenye orodha hiyo, na kuchukua hatua kali za udhibiti wa fedha. Nchi nyingine katika orodha hiyo ni pamoja na Sudan Kusini, Tanzania, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Msumbiji, Nigeria, Afrika Kusini, na zingine. Katika Makala haya, Gurudumu la Uchumi, tunachambua hatua hii na athari zake kwa uchumi, lakini pia nini mamlaka katika nchi hizo zinaweza kufanya hili kujiondoa kwenye orodha hiyo.

    Claim Gurudumu la Uchumi

    In order to claim this podcast we'll send an email to with a verification link. Simply click the link and you will be able to edit tags, request a refresh, and other features to take control of your podcast page!

    Claim Cancel