POPULARITY
Send us Fan MailWaziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda, akiwasilisha makadirio ya bajeti ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2026/2027, Mei 4, 2026, bungeni, jijini Dodoma.Support the showIdara ya Habari MAELEZO
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kia inayotorejesha katika mkutano wa CSW7O amabko Flora Nducha wa Idhaa hili kandoni mwa kikao hicho alipata fursa ya kuzungumza na Onyonge Mengo kijana mpigania haki za wanawake, mtafiti na wakili kutoka Mahakama Kuu ya Kenya ambaye pia anafanyakazi na shirika la kimataifa la maendeleo la Hivos ili kufahamu kwa kina nini wanachokifanya kusongesha haki za kisheria za wanawake na wasichana.Mzozo wa Mashariki ya Kati ukiwa umeingia siku ya 31 , zaidi ya watu 200,000 wamevuka mpaka wa Lebanon na kuingia Syria tangu mashambulizi baina ya Israeli na Hezbollah yaanze mwishoni mwa mwezi uliopita baada ya Marekani na Israeli kushambulia Iran. Ripoti mpya ya iliyotolewa leo na Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo UNDP, inaonya kuwa idadi kubwa ya watu nchini Iran inaweza kutumbukia kwenye umaskini kadri misukosuko ya kiuchumi inavyozidi kuathiri maisha ya kila siku. Shirika hilo linasema hali hiyo inahatarisha kufuta mafanikio ya maendeleo yaliyopatikana kwa miaka kadhaa, huku Kiwango cha Maendeleo ya Binadamu (HDI) kikitarajiwa kushuka kwa kiasi kikubwa sawa na kupotea kwa zaidi ya mwaka mmoja wa maendeleo.Na Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji IOM, leo limeomba dola milioni 277 kusaidia watu walio hatarini zaidi waliokumbwa na mizozo na ukosefu wa makazi nchini Sudan na nchi jirani kwa mwaka huu wa 2026, wakati mgogoro huo ukikaribia kuingia mwaka wake wa tatu. Mkurugenzi Mkuu wa IOM Amy Pope ameonya kuwa familia zinakabiliwa na “chaguo ngumu lisilowezekana kati ya kubaki bila huduma muhimu au kurejea katika jamii zilizosambaratishwa na vita”. Fedha hizo zitatumika kuimarisha mifumo ya kibinadamu, kupanua njia za misaada, na kuimarisha operesheni za kuvuka mipaka ili kusaidia waathirika kuishi na kujijenga upya.Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili hii leo Dkt. Mwanahija Ali Juma, Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili, Zanzibar nchini Tanzania, BAKIZA anafafanua maana na matumizi ya neno "GIDA."Mwenyeji wako ni Rashid Malekela, karibu!
Leo imetimia siku 1000 tangu kuzuka kwa vita nchini Sudan, vita vinavyohusisha Jeshi la Sudan SAF na Kikosi cha Wanamgambo wa Sudan cha Msaada wa Haraka RSF. Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji IOM limesema mtu mmoja kati ya watatu nchini humo ni mkimbizi ndani ya nchi yake au amekimbilia nje ya nchi huku Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF likieleza mzozo huo ambao umeendelea kusababisha janga kubwa la kibinadamu unawatesa zaidi wanawake na watoto kwani wanabeba mzigo mkubwa wa madhara ya vita. Tuungane na Rashid Malekela kwa taarifa zaidi
Kulingana na ripoti ya umoja wa Afrika, bara hilo linapoteza takribani dola za Marekani bilioni 88 kila mwaka kupitia njia zisizo halali kama ukwepaji kodi, utakatishaji fedha, utoroshaji wa mali na mitaji na udanganyifu kwenye biashara. Kwenye Makala ya Gurudumu la Uchumi, tunajiuliza, Kwanini hali hii inaendelea licha ya uwepo wa sheria kali? Nani anafaidika? na nini kifanyike kuzuia upotevu huu mkubwa wa rasilimali fedha? Tutakuwa na wataalamu Walter Nguma na Dr Ponsian Ntui.
Kulingana na ripoti ya umoja wa Afrika, bara hilo linapoteza takribani dola za Marekani bilioni 88 kila mwaka kupitia njia zisizo halali kama ukwepaji kodi, utakatishaji fedha, utoroshaji wa mali na mitaji na udanganyifu kwenye biashara. Kwenye Makala ya Gurudumu la Uchumi, tunajiuliza, Kwanini hali hii inaendelea licha ya uwepo wa sheria kali? Nani anafaidika? na nini kifanyike kuzuia upotevu huu mkubwa wa rasilimali fedha? Tutakuwa na wataalamu Walter Nguma na Dr Ponsian Ntui.
Mnamo mwezi April mwaka huu Shirika la Fedha la Kimataifa IMF lilitoa makadirio na mtazamano wa uchumi wa dunia ambapo lilieleza pamoja na mambo mengine kuongezeka kwa vikwazo vya biashara kunasababisha kushuka kwa kasi kwa ukuaji wa uchumi wa dunia mwelekeo ambao ulielezwa kuathiri nchi nyingi duniani.Tarehe 29 Julai IMF ikatoa ripoti mpya, ambapo tathmini mpya ya mwelekeo wa uchumi wa Dunia kwa mwaka 2025 na 2026 ikionesha matumaini tofauti na hali ilivyoonesha miezi mitatu mitatu iliyopita. Leah Mushi amefuatilia ripoti hiyo nakutuandalia makala hii akieleza kwa kina.
Hii leo jaridani tunaangazia wahamiaji na njia bunifu ya kuwawezesha kujikimu kimaisha, na malezi bora ya watoto nchini Tanzania. Makala tunasalia huko huko Tanzania kumulika uwekezaji na ufadhili wa miradi ya maendeleo, na mashinani tunakwenda nchini Kenya.Katika Mkutano wa 4 wa Kimataifa wa Ufadhili wa Maendeleo (FFD4) unaoendelea jijini Seville, Hispania, Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji (IOM) limetoa wito wa kuimarisha uwekezaji wa kibunifu katika uhamiaji wa watu ili kuchochea ukuaji wa uchumi na kusaidia kuziba pengo la kila mwaka la dola trilioni 4 za ufadhili wa maendeleo.Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF limekuwa likihimiza umuhimu wa malezi na makuzi chanya kwa watoto kama njia mojawapo ya kulinda haki kuu nne za msingi za mtoto ambazo ni kuishi, kuendelezwa, kushirikishwa na kulindwa..Katika makala mkutano wa 4 wa Ufadhili wa Maendeleo (FFD4) ukikunja jamvi leo huko Sevilla Hispania, juhudi za kuhakikisha nchi zinajitegemea kifedha kupitia vyanzo jumuishi na vya ubunifu zimezidi kupewa kipaumbele. Katika hafla ya kufungua mafunzo ya Muongozo wa Upatikanaji wa Fedha kwa Mamlaka za Serikali za Mitaa, au Intergrated Local Financing Framework (ILFF) yaliyofanyika katika Manispaa ya Morogoro kaskazini-mashariki mwa Tanzania hivi majuzi , Umoja wa Mataifa kupitia shirika lake la Mpango wa Maendeleo nchini humo, UNDP umetoa mafunzo ya namna halmashauri zinaweza kuandaa mikakati madhubuti ya kuhimiza maendeleo ya ndani kupitia ushirikiano kati ya sekta binafsi, mashirika ya kiraia, benki na jamii.Na mashinani, vijana na wahudumu wa afya katika kaunti ya Kajiado nchini Kenya, wameshikamana kuhamasisha umma kuhusu hedhi salama. Kupitia video iliyoandaliwa na washirika wetu Radio Domua, mmoja wa vijana anaelezea umuhimmu wa hedhi salama kama njia ya kutokomeza unyanyapaa dhidi ya wanawake na wasichana.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
Mkutano wa 4 wa Ufadhili wa Maendeleo (FFD4) ukiendelea huko Sevilla Hispania, juhudi za kuhakikisha nchi zinajitegemea kifedha kupitia vyanzo jumuishi na vya ubunifu zimezidi kupewa kipaumbele. Katika hafla ya kufungua mafunzo ya Muongozo wa Upatikanaji wa Fedha kwa Mamlaka za Serikali za Mitaa, au Intergrated Local Financing Framework (ILFF) yaliyofanyika katika Manispaa ya Morogoro kaskazini-mashariki mwa Tanzania hivi majuzi , Umoja wa Mataifa kupitia shirika lake la Mpango wa Maendeleo nchini humo, UNDP umetoa mafunzo ya namna halmashauri zinaweza kuandaa mikakati madhubuti ya kuhimiza maendeleo ya ndani kupitia ushirikiano kati ya sekta binafsi, mashirika ya kiraia, benki na jamii. Lengo ni kuendelea kuunga mkono serikali na wadau mbalimbali barani Afrika katika kutafuta mbinu mbadala za kufadhili maendeleo.Sharon Jebichii na maelezon zaidi.
Mwezi Juni mwaka 2025, Tume ya Ulaya iliorodhesha Kenya miongoni mwa nchi zenye changamoto ya utakatishaji wa fedha, huku Uganda ikipata afueni kwa kuondolewa kwenye orodha hiyo. Hatua hii ina maana kuwa mashirika ya kifedha – ikiwemo benki – zinalazimika kuzingatia kwa makini uhusiano wa kibiashara na miamala yoyote inayohusiana na nchi zilizo kwenye orodha hiyo, na kuchukua hatua kali za udhibiti wa fedha. Nchi nyingine katika orodha hiyo ni pamoja na Sudan Kusini, Tanzania, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Msumbiji, Nigeria, Afrika Kusini, na zingine. Katika Makala haya, Gurudumu la Uchumi, tunachambua hatua hii na athari zake kwa uchumi, lakini pia nini mamlaka katika nchi hizo zinaweza kufanya hili kujiondoa kwenye orodha hiyo.
Mwezi Juni mwaka 2025, Tume ya Ulaya iliorodhesha Kenya miongoni mwa nchi zenye changamoto ya utakatishaji wa fedha, huku Uganda ikipata afueni kwa kuondolewa kwenye orodha hiyo. Hatua hii ina maana kuwa mashirika ya kifedha – ikiwemo benki – zinalazimika kuzingatia kwa makini uhusiano wa kibiashara na miamala yoyote inayohusiana na nchi zilizo kwenye orodha hiyo, na kuchukua hatua kali za udhibiti wa fedha. Nchi nyingine katika orodha hiyo ni pamoja na Sudan Kusini, Tanzania, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Msumbiji, Nigeria, Afrika Kusini, na zingine. Katika Makala haya, Gurudumu la Uchumi, tunachambua hatua hii na athari zake kwa uchumi, lakini pia nini mamlaka katika nchi hizo zinaweza kufanya hili kujiondoa kwenye orodha hiyo.
Alhamisi ya Juni 12, nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa pamoja kupitia Mawaziri wa Fedha, waliwasilisha Bajeti ya mwaka wa fedha ya mwaka 2025/26. Waziri wa fedha John Mbadi aliwasilisha Bajeti ya Shilingi za nchi hiyo Trilioni 4.2. Bajeti ya Tanzania kwa mwaka huu wa fedha ni Shilingi za nchi hiyo Trilioni 56.49 huku Bajeti ya Uganda ikiwa ni Shilingi za nchi hiyo Trilioni 72.3. Lakini bajeti hii ina maana gani kwa raia wa nchi hizo na je bajeti hizi zinatoa taswira halisi ya mikakati yao nchi hizo kujitegemea na pia kukua? Skiliza makala haya upate ufahamu zaidi tukizungumza pia na David Otieno, mtafiti wa masuala ya bajeti kutoka shirika la Amnesty International.
Alhamisi ya Juni 12, nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa pamoja kupitia Mawaziri wa Fedha, waliwasilisha Bajeti ya mwaka wa fedha ya mwaka 2025/26. Waziri wa fedha John Mbadi aliwasilisha Bajeti ya Shilingi za nchi hiyo Trilioni 4.2. Bajeti ya Tanzania kwa mwaka huu wa fedha ni Shilingi za nchi hiyo Trilioni 56.49 huku Bajeti ya Uganda ikiwa ni Shilingi za nchi hiyo Trilioni 72.3. Lakini bajeti hii ina maana gani kwa raia wa nchi hizo na je bajeti hizi zinatoa taswira halisi ya mikakati yao nchi hizo kujitegemea na pia kukua? Skiliza makala haya upate ufahamu zaidi tukizungumza pia na David Otieno, mtafiti wa masuala ya bajeti kutoka shirika la Amnesty International.
Hii leo jaridani tunaangazia ujumbe wa Katibu Mkuu Guterres, wa siku ya kimataifa ya kupambana na kauli za chuki na mradi wa lishe bora kwa watoto huko Kilifi Kenya. Makala tunakwenda nchini Rwanda na mashinani nchini Ghana, kulikoni?Leo Juni 18 ni siku ya kimataifa ya kupambana na kauli za chuki ambapo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres ametumia ujumbe wake kwa siku hii kutoa onyo kuhusu hatari zinazoongezeka za chuki mtandaoni, hasa zikichochewa na akili mnemba au (AI) na na majukwaa ya kidijitali.Katika Kaunti ya Kilifi, iliyoko pwani ya Kenya barani Afrika, Mpango wa Kuboresha Lishe kwa kupatia jamii Fedha na Elimu ya Afya (NICHE) unasaidia kuwaelimisha wazazi kuhusu umuhimu wa baba na mama kulea watoto wao kwa pamoja, mradi unaotekelezwa na shirika la Umoja wa MAtaifa la kuhudumia watoto, UNICEF.Katika makala shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo FAO, kwa kushirikiana na Serikali ya Rwanda, linaendelea kujenga uwezo wa kitaifa katika kuhimiza matumizi ya mbinu rafiki kwa mazingira katika kilimo pamoja na usimamizi salama wa viuatilifu. Hili linafanyika kupitia utekelezaji wa awamu ya tatu ya mradi wa ACP MEAs 3 unaofadhiliwa na Muungano wa Ulaya EU. Mpango huu unalenga kuwawezesha wakulima wadogo kuhamia kwenye mifumo ya kilimo endelevu kimazingira na kuwajengea uwezo wa utekelezaji wa mikataba ya kimataifa ya mazingira.Na katika mashinani leo ikiwa ni siku ya kimataifa Sayansi ya Mapishi au Gastronomia, fursa ni yake Mpishi Mkuu mashuhuri Fatmata Binta kutoka Sierra Leone, ambaye kupitia video ya shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo, FAO, ya kipindi kiitwacho Mazungumzo ya Jikoni , anapazia sauti matumizi ya vyakula vya kiasili kama njia ya kuepuka kusahaulika kwa vyakula vya kiasili ili hatimaye kuweko na lishe endelevu.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
Katika Kaunti ya Kilifi, iliyoko pwani ya Kenya barani Afrika, Mpango wa Kuboresha Lishe kwa kupatia jamii Fedha na Elimu ya Afya (NICHE) unasaidia kuwaelimisha wazazi kuhusu umuhimu wa baba na mama kulea watoto wao kwa pamoja, mradi unaotekelezwa na shirika la Umoja wa MAtaifa la kuhudumia watoto, UNICEF. Assumpta Massoi anamulika moja ya familia zilizonufaika.
S1405. Kanuni 5 Zinazofungua Milango ya Fedha Katika Ufalme wa Mungu
S1404. Kanuni 5 Zinazofungua Milango ya Fedha Katika Ufalme wa Mungu
Kanuni 5 Zinazofungua Milango ya Fedha Katika Ufalme wa Mungu
Kanuni 5 Zinazofungua Milango ya Fedha Katika Ufalme wa Mungu
Kanuni 5 Zinazofungua Milango ya Fedha Katika Ufalme wa Mungu
Kanuni 5 Zinazofungua Milango ya Fedha Katika Ufalme wa Mungu.mp3
Zambia inaendelea kuwahifadhi zaidi ya wakimbizi 106,000, wengi wao wakiwa kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, Burundi, pamoja na wakimbizi wa zamani kutoka Rwanda na Angola, kwa mujibu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi UNHCR, ambalo limesema kwa kuzingatia sera yake jumuishi, nchi hiyo inakuza mshikamano na wakimbizi na kuwawezesha kujitegemea kupitia makazi maalum na ushirikiano na jamii za wenyeji. Flora Nducha na taarifa zaidi Shirika hilo la wakimbizi limesema katika makazi kama Mayukwayukwa na Maheba ambayo ni moja ya kambi kubwa zaidi ya wakimbizi nchini Zambia familia za wakimbizi zilizolazimika kukimbia makwao zinajumuishwa ili ziweze kujikimu na kuishi kwa utangamano na wenyeji wanaowahifadhi. Moulid Hujale, ni afisa habari msaidizi wa UNHCR anasema “Selikali ya Zambia inajumuisha wakimbizi katika huduma za kitaifa kama vile elimu na hata programu za msaada wa kilimo ili kuongeza uzalishaji” Amebainisha kuwa kwa kufanya hivyo Zambia imeonesha mshikamano wa dhati kwa jamii hizo za wakimbizi kwa kuhakikisha kuwa wanapata fursa ya kujenga upya maisha yao, kujikwamua kiuchumi na kuishi kwa heshima.Hata hivyo, UNHCR inasema nchi hiyo ya Kusini mwa Afrika pamoja na ukarimu wake bado inakumbwa na athari za ukame mkali uliotishia uhakika wa chakula na kuyumbisha uchumi na katika hatua za kukabiliana na hali hiyo, Moulid ansema “UNHCR inashirikiana na serikali ya Zambia kuunganisha makazi ya wakimbizi kwenye gridi ya taifa ya umeme. Tunajua muundo huu wa ujumuishwaji na maisha endelevu vinagharimu fedha, Lakini hiki ndicho hasa wakimbizi wanachokihitaji, hivyo tunahitaji msaada wako ili kufanikisha hili”. Licha ya mafanikio yaliyopatikana hadi sasa Zambia katika kuwakirimu wakimbizi, UNHCR imeonya kuwa uhaba wa fedha inaokabiliwa nao unatishia kuathiri mafanikio hayo na hasa utoaji wa huduma muhimu kwa familia hizo zilizolazimika kufungasha virago na kusaka usalama Zambia. Sasa limetoa ombi la msaada wa haraka wa kimataifa ili kuendelea kufanikisha huduma za kuokoa maisha zinazohitajika sana na wakimbizi hao.
Nguvu ya Agano jipya Katika Fedha na Uchumi
Nguvu ya Agano jipya Katika Fedha na Uchumi
Nguvu ya Agano jipya Katika Fedha na Uchumi
Kwenye kikao cha 58 cha Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa kinachoendellea mjini Geneva Uswisi, Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa M ataifa, Volker Türk , amezungumzia hali ya kuzorota na kutoeleweka inayohusu haki za binadamu duniani kote akielezea wasiwasi mkubwa kuhusu kudhoofika kwa makubaliano ya kimataifa kuhusu haki za binadamu,na kuonya kwamba ushawishi wa viongozi wa kiimla, matajiri wakubwa, na viongozi wa kimabavu unatishia kuvuruga maendeleo ya miongo kadhaa. Anold Kakayanda na taarifa kamili.Asante Flora katika taarifa yake Türk amesisitiza umuhimu wa kuhifadhi haki za binadamu na utawala wa sheria ili kuzuia kurudiwa kwa ukatili wa zamani.Moja ya masuala ya dharura yaliyotiliwa mkazo na Türk ni mgogoro wa kibinadamu unhaoendelea huko Gaza. Amelaani uharibifu uliosababishwa na hatua za kijeshi za Israeli dhidi ya mashambulizi ya Oktoba 7, 2023 yaliyofanywa na Hamas na makundi mengine ya wapiganaji wa Kipalestina.Türk amesisitiza haja ya kudumisha usitishaji mapiganona kutoa wito wa mchakato wa amani unaozingatia haki za binadamu, ikiwa ni pamoja na haki ya kujitawala na uwajibikaji. Ametaka kuachiliwa kwa mateka, kukomeshwa kwa vizuizi vya kiholela, na kuanza tena kwa msaada wa kibinadamu mara moja ndani ya Gaza.Kuhujsu mgogoro unaoendelea nchini Ukraine amersema bado ni suala la kutia wasiwasi, huku raia wakiishi kwa hofu ya mara kwa mara kutokana na mashambulizi yasiyokoma.Türk amekemea vikali vikwazo vya Shirikisho la Urusi juu ya haki za msingi katika maeneo yanayokaliwa kwa mabavu na kuelezea masikitiko yake kuhusu ripoti za mauaji ya kiholela na mateso ya kimfumo ya wafungwa wa vita wa Kiukraine.Almeihimiza jumuiya ya kimataifa kufanya kazi kuelekea amani endelevu inayoheshimu haki na matarajio ya watu wa Ukraine.Türk pia ameelekeza mawazo kwenye maeneo mengine yenye migogoro, ikiwa ni pamoja na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, Myanmar, Haiti, na Sudan.Alielezea jinsi watawala wa kiimla, wanasiasa wahubiri wa chuki, na walanguzi wanavyotumia machafuko kwa faida zao binafsi.Amesema Athari za migogoro huenea zaidi ya mstari wa mbele, zikiathiri minyororo ya usambazaji duniani na nafasi za kidijitali.Ametoa wito kwa watu binafsi kutambua jukumu lao la pamoja kwa kufanya maamuzi ya kimaadili ya ununuzi, kushiriki kisiasa, na kuunga mkono uwajibikaji kwa ukiukwaji wa haki za binadamu.Hata hivyo amesema demokrasia zilizoimarika haziko salama dhidi ya kudorora kwa haki za binadamu. Türk ameelezea wasiwasi mkubwa kuhusu mwelekeo nchini Marekani, ambako maendeleo kuhusu usawa wa kijinsia na sera za kupinga ubaguzi yanarudi nyuma.Pia amekosoa Shirikisho la Urusi kwa ukandamizaji wake wa jamii za kiraia na vyombo vya habari huru, ambapo wapinzani wanakabiliwa na unyanyasaji, kukamatwa, au kufurushwa.Kudhoofika kwa haki za binadamu katika mataifa yenye nguvu, Türk alionya kwamba kunaweka mfano hatari kwa ulimwengu mzima, akisisitiza hitaji la dharura la mshikamano wa kimataifa na uwajibikaji kuhusu haki za binadamu.
Majadiliano ya mkutano wa 29 wa nchi wanachama wa mkataba wa Umoja wa Mataifa wa mabadiliko ya tabianchi COP29 yamekumbwa na mkwamo huko Baku Azerbaijana muafaka haujapatikana. Majadiliano hayo yaliyotarajiwa kukunja jamvi leo sasa yanaendelea kwa kuwekwa mezani mapendekezo mapya kuhusu ufadhili wa mabadiliko ya tabianchi hasa kwa matifa yanayoendelea. Hakika vuta nikuvute bado inaendelea hata sasa washiriki wako mezani kwakikuna vichwa na kujadili mapendekezo mapya. Mkwamo huo umetokana na kushindwa kuafikiana katika masuala kadhaa kubwa likiwa ufadhili wa mabadiliko ya tabianchi na hususasn kuhusu ni kiasi gani cha fedha nchi zinazoendelea zinapaswa kupokea kila mwaka hadi ifikapo mwaka 2030 na wapi fedha hizo za ufadhili zitatoka.Nchi zinazoendelea zinataka kulipwa dola trilioni 1.3 kwa mwaka lakini hilo halijaafikiwa na mapendekezo mapya yaliyowasilishwa na raia wa mkataba huo wa UNFCCC yanaonyesha tofauti kubwa na safari ndefu ya kufikia muafaka.Kwa mujibu wa mapendekezo hayo mapya yaliyowasilishwa leo mezani na Rais wa COP29 Mukhtar Babayev yanataka nchi zinazoendelea kupokea dola bilioni 250 kwa mwaka hadi kufikia mwaka 2035 kwa ajili ya kuchukua hatua didi ya mabadiliko ya tabianchi.Na maesema “Fedha hizi zitatoka katika vyanzo mbalimbali ikiwemo sekta za umma na za binafsi, na kitaifa na kimataiifa ikiwemo vyanzo mbadala”.Wakati pia COP29 ikitoa wito wa kufikia lengo la ufadhili wa dola trilioni 1.3 ifikapo mwaka 2035 pia imezikaribisha nchi zinazoendelea kutoa michango ya ziada.Kiwango kilichopendekezwa cha ufadhili kinatarajiwa kuzusha vuta ni kuvute katika majadiliano hayo kwa siku nzima ya leo huenda hadi kesho ingawa mkutano huo unahisi ahuweni kwamba kuna kiwango kilichowasilishwa na unataka hitimisho la mkutano haraka iwezekanavyo. Je nchi zinazoendelea zitapokea vipi pendekezo hili jawabu bado halijulikani. Wapenzi wa UN News Kiswahili endeleeni kufuatilia kwenye kurasa zetu kufahamu hatma ya mkutano huo.
Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa mabadiliko ya tabianchi COP29 leo ukiingia siku ya nne mjini Baku Azerbaijan vijana kutoka Afrika wataka ufadhili uongezwe kutoka mataifa makubwa hususan yanayochangia zaidi hewa ukaa ili kudhibiti athari za mabadiliko ya tabianchi kwa mataifa yanayoendelea ambapomiongoni mwa waathirika wakubwa ni vijana. Asante Bosco na mmoja wa washiriki hao ni Patricial Kombo Mumbua kutoka Kenya akiwasilisha matakwa ya vijana katika mkutano huo, na akizungumza na UN News kuhusu ujumbe wake kwa COP29 amesema“Kwangu kama kiongozi wa vijana jambo la kwanza ni kuweza kupata zile fedha au kuzikusanya ili ziweze kusaidia mataifa ambayo yanapambana na kukabiliwa na changamoto ya mabadiliko ya tabianchi . Pili ni kuhakikisha kuwa viongozi kutoka mataifa ambayo yanazalisha zaidi hewa ukaa yanawajibika ili kuyafanya matifa ambayo yanaendelea kuweza kujilinda , kunufaika , kujiinua dhidi ya janga hilo na pia kujenga mnepo dhidi ya mabadiliko ya tabianchi katika jamii zao.”Na nini anachokitarajia katika mkutano huo wa COP29?“Ni kuweza kuona kuwa hili kongamano litaweza kuhamasisha upatikanaji wa hizo hela kwa mataifa ambayo yanakabiliwa na hizi changamoto za mabadiliko ya tabianchi, Na pia wakati ambapo mataifa yanaendelea kurekebisha michango yao ya kitaifa ya mabadiliko ya tabianchi au NDCs, waweze kuleta michango ambayo inaaambatana na zile changamoto ambazo mataifa yao yanazidi kuathiirika nazo za mabadiliko ya tabianchi.”Mbali ya masuala ya ufadhil mada zingine zinazotamalaki kwenye mijadala ya leo COP29 ni masuala ya nishani safi , mifumo ya tahadhari za mapemba na athari za mabadiliko ya tabianchi kwa matifa ya visiwa vidogo vinavyoendelea.
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka huko Havana Cuba kwenye Kongamano la kimataifa la Kiswahili kusikia kutoka kwa waziziri Zanzibar kuhusu faida za kiplomasia na kiuchumi. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na ujumbe kuhusu Kiswahili.Fedha kwa ajili ya mipango ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, ni jambo lililopatiwa kipaumbele katika ripoti mpya ya leo ya shirika la Umoja wa Mataifa la Mazingira, UNEP wakati huu ambapo kiwango cha joto kinazidi kuongezeka kila uchao na kuleta zahma duniani kote.Shirika la Umoja wa Mataifa la afya ulimwenguni, WHO linasema hii leo watoto 6 wa kipalestina, wamesafirishwa kutoka Gaza kwenye Romania kwa matibabu mahsusi ; watatu wakiwa wanaugua saratani, wawili magonjwa ya damu na mmoja majeraha. Wameambatana na jumla ya waangalizi 15.Na huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo, MONUSCO umezindua mfumo wa uthibitishaji, kama sehemu ya mchakato wa Luanda wenye lengo la kufuatilia makubaliano ya sitisho la mapigano kati ya Rwanda na DRC yaliyoanza kutekelezwa tarehe 4 mwezi Agosti mwaka huu mashariki mwa taifa hilo la Maziwa Makuu.Katika kujifunza lugha ya Kiswahili tunasalia huko huko Havana Cuba, kwenye kongamano la Kiswahili la Kimataifa ambako Dkt. Kisembo Ronex Tendo mshiriki kutoka taasisi ya vijana ya Afrika Mashriki Fest Uganda anaeleza cha kufanya kusongesha Kiswahili nchini Uganda.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
Matangazo ya saa nzima kuhusu habari za kutwa, ikiwa ni pamoja ripoti kutoka kwa waandishi wetu sehemu mbali mbali duniani na kote Afrika Mashariki na Kati, na vile vile vipindi na makala maalum kuhusu afya, wanawake, jamii na maendeleo.
Limiya Daud mwenye umri wa miaka 30 ni mmoja wa wakimbizi wa Sudan aliyekimbilia nchini Sudan Kusini kusaka hifadhi baada ya machafuko kuibuka nchini mwake. Kutokana na wingi wa wakimbizi wanaoingia katika nchi zilizo jirani na Sudan baadhi yao wamekuwa wakihamishwa na kupelekwa katika kambi za wakimbizi ambazo zilishaanzishwa hapo awali ili waweze kupata huduma zote muhimu.Tuungane na Evarist Mapesa akituletea simulizi ya Limiya Daud na watoto wake ambao baada ya kukimbilia nchini Sudan Kusini kusaka hifadhi alihamishiwa katika kambi ya Maban iliyoko huko Renk na msaada wa fedha alioupata kutoka mashirika ya Umoja wa Mataifa umemuwezesha kufungua genge.
Mahakama ya juu Kenya yasimamisha uamuzi wa mahakama ya chini kuhusu sheria ya fedha ya mwaka 2023
Matangazo ya nusu saa kuhusu habari za mapema asubuhi pamoja na habari za michezo.
Maandano yaendelea Kenya licha ya Rais Ruto kukataa kutia saini mswada wa fedha wa 2024
Taasisi kadhaa za Jumuiya ya Afrika Mashariki, zimejipata katika hali ngumu baada ya bajeti zao kuathirika sana.
Afisi ya Wizara ya Fedha ya Marekani inayohusika na Udhibiti wa Mali za Kigeni (OFAC), Jumatatu imeyawekea vikwazo mashirika 16 na watu binafsi, ambao inasema wanahusika katika mtandao mpana wa biashara unaozunguka Pembe ya Afrika, Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) na Cyprus.
Waziri wa Fedha akaribisha uamuzi wa benki ya hifadhi wakuto ongeza kiwango cha riba.
Misri, taifa lenye watu milioni 100 hivi sasa, lakini ni asilimia 30 tu ya watu hao yani watu milioni 36.8 ndio wenye akaunti za benki. Katika zama hizo za huduma za fedha kimtandao, mashirika ya mawasiliano ya simu yanaingia ubia na benki ili kupanua wigo wa huduma hizo. Ukosefu wa huduma za fedha kimtandao zinakuwa kikwazo kwani wananchi hupoteza muda mwingi benki kusubiria malipo ambayo wangaliweza kuyapokea kupitia simu za kiganjani au rununu. Shuhuda pande zote mbili hizo ni msichana mmoja mkazi wa Cairo nchini Misri kama anavyosimulia Assumpta Massoi kwenye makala hii iliyoandaliwa na shirika la Umoja wa Mataifa la Mawasiliano duniani, ITU.
Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) linasema hadi kufikia mwisho wa mwaka huu 2023 linahitaji dola za Marekani milioni 60 ili kutoa msaada wa chakula cha kuokoa maisha nchini Myanmar kwa watu milioni 2.1 walioathiriwa na majanga mengi na magumu kikiwemo kimbunga Mocha.Kwa mujibu wa WFP, kimbunga Mocha, dhoruba kali zaidi kuwahi kutokea katika Ghuba ya Bengal katika kipindi cha muongo mmoja, kimesababisha maafa kwa mamilioni ya watu walio tayari kwenye wakati mgumu, hasa nchini Myanmar. Kimbunga Mocha kimeacha uharibifu katika Jimbo la Rakhine kaskazini mwa Myanmar ambapo kaya katika vitongoji vingi na maeneo ya watu waliohama katika maeneo ya mabondeni wamepoteza akiba kubwa ya chakula na na vyanzo vingine vya kipato. Miundo muhimu kama hospitali na shule vimeharibiwa hasa katika mji mkuu wa jimbo la Rakhine, Sittwe. Mawasiliano na njia za umeme katika eneo hili la Myanmar zimevurugwa. Stephen Anderson ni Mkurugenzi wa WFP nchini Myanmar anaeleza wanachokifanya, "WFP tayari imeanza usambazaji wa haraka wa chakula kwa watu wenye mahitaji makubwa huko Rakhine na Magwe na iataongeza zaidi katika siku zijazo. Tunatumai kuwafikia angalau watu 800,0000 ambao wanachukuliwa kuwa wenye uhitaji mkubwa zaidi. Timu zetu ziko kwenye eneo kufanya kazi mchana na usiku kufanya lolote wawezalo ili kuongeza msaada ili kuwafikia wale wote wanaohitaji popote walipo.” Wakati wa mchana Mei 14 kimbunga kikali kilipiga Mynmar karibu na mpaka wa Bangladesh kwa upepo unaokadiriwa kuwa na kasi ya karibu kilomita 280 kwa saa na hivyo kukifanya kuwa moja ya vimbunga vikali zaidi kuwahi kutokea katika kipindi cha miaka kumi iliyopita kwenye ukanda huo.
Takribani watoto 573,000 wenye umri wa chini ya miaka mitano nchini Malawi wako hatarini kukumbwa na utapiamlo, limesema shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Watoto duniani, UNICEF huku likisema linahitaji dola milioni 87.7 kukidhi mahitaji ya watu milioni 6.5 wakiwemo watoto milioni 3.3 nchini humo, ikiwa ni ombi jipya la fedha lililotolewa leo.Assumpta Massoi na taarifa kwa kina.UNICEF kupitia taarifa yake iliyotolewa jijiini Lilongwe Malawi hii leo, inasema maendeleo yaliyopatikana hivi karibuni ya kukabili utapiamlo yanayoyoma kutokana na uhaba mkubwa wa chakula ukigubikwa na matukio ya mara kwa mara ya madhara ya mabadiliko ya tabianchi, milipuko ya magonjwa yanayozuilika, ukosefu wa utulivu wa kiuchumi na ukosefu mkubwa wa ufadhili kwenye sekta za kijamii.Taarifa hiyo inasema Malawi bado inazingirwa na kiza kinene cha athari mbaya za kimbunga Fredy kilichokumba taifa hilo mwezi Machi na kuacha hadi leo hii watu 659,000 wakimbizi wa ndani wakiwemo watoto.Halikadhalika mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu bado unaendelea na tayari umesababisha vifo vya watu 1,759.UNICEF/Thoko ChikondiDalitso Dines mwenye umri wa miaka 14 in mwanafunzi wa darasa la 8 na manusura wa kimbunga Freddy. Hapa yuko darasani kwenye shule ya msingi ya Chumani huko Mulanje kusini mwa Malawi akijisomea. Hii ni tarehe 23 Machi 2023.Mwakilishi wa UNICEF nchini Malawi Gianfranco Rotigliano anasema watoto nchini Malawi wanakabiliwa na mlolongo wa majanga. Ukosefu wa uhakika wa kupata chakula ukichochewa na janga la mabadiliko ya tabianchi, mlipuko wa magonjwa na kutwama kwa uchumi duniani, vyote vinatishia maisha ya mamilioni ya watoto.Amerejelea ombi la Hatua za Kiutu kwa Watoto, HAC lililozinduliwa leo na UNICEF likionesha ongezeko la matukio ya utapiamlo miongoni mwa watoto katika kipindi cha miaka mitano iliyopita ambapo mwaka 2023 pekee watoto 62,000 wenye umri wa kati ya miezi 6 hadi miaka 5 wako hatarini kukumbwa na unyafuzi au udumavu.Ni kwa mantiki hiyo UNICEF imeongeza ombi lake kwa usaidizi Malawi kutoka zaidi ya dola milioni 52 hadi dola milioni 87 ili kukidhi mahitaji ya watu milioni 6.5 wakiwemo watoto milioni 3.3.Fedha hizo zitatumika kununua mahitaji ya vyakula vilivyo tayari kuliwa ili kutibu unyafuzi, kupata huduma za maji safi na salama, huduma za kujisafi, afya, lishe, elimu, ulinzi dhidi ya watoto na miradi ya fedha taslimu.Bwana Rotigliano amesema bila usaidizi wa kifedha, kaya maskini na za Watoto walio hatarini watasalia bila huduma za msingi na zaidi ya yote amesema pamoja na misaada hiyo ni lazima kujengea mnepo ili kupunguza madhara makubwa ya milipuko na dharura za kiutu.
Mzozo nchini Sudan ukiingia mwezi wa pili, hii leo Umoja wa Mataifa na wadau wake wamefanyia marekebisho ombi la usaidizi kwa nchi hiyo na sasa linafikia dola bilioni 3 kwa ajili ya kusaidia mamilioni ya watu nchini humo na mamia ya maelfu wengine waliokimbilia nchi jirani kusaka usalama.Uzinduzi wa ombi hilo lililorekebishwa umefanywa kwa pamoja hii leo huko Geneva Uswisi na ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu misaada ya dharura, OCHA na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi duniani, UNHCR. Hivi sasa jumla ya dola bilioni 2.56 zinahitajika kwa mwaka 2023, ikiwa ni nyongeza ya dola milioni 800 kutoka miezi michache iliyopita, ili kusaidia watu milioni 18 hadi mwishoni mwa mwaka huu na hivyo kufanya ombi hili kuwa ombi kubwa zaidi kuwahi kutolewa kwa Sudan. Marekebisho hayo yanazinagatia ongezeko la mahitaji lililochochewa na mapigano yanayoendelea ambapo Mkuu wa ofisi ya OCHA mjini Geneva, Ramesh Rajasingham amewaambia waandishi wa habari kuwa, “mahitaji nchini Sudan ni ya msingi na yamesambaa kama unavyoweza kufikiria kutokana na majanga: kulindwa dhidi ya mapigano, matibabu, chakula, maji, huduma za kujisafi, malazi na huduma dhidi ya kiwewe. Tunapata pia taarifa za ongezeko la ukatili wa kingono na waathirika hawawezi kupata huduma. Watoto wako hatarini zaidi katika janga hili linalozidi kuibuka.” Akifafanua kuhusu ombi la usaidizi kwa wakimbizi waliosaka hifadhi Jamhuri ya Afrika ya Kati, Chad, Misri, Ethiopia, Sudan Kusini na wakimbizi waliorejea nyumbani kutokana na changamoto Sudan, Kamishna Msaidizi wa UNHCR akihusika na operesheni, Raouf Mazour amesema, “hii leo tunatoa ombi la takribani dola milioni 472 ili kukidhi mahitaji ya zaidi ya watu milioni 1 katika kipindi cha miezi 6 ijayo.” Mapigano yalizuka Sudan tarehe 15 mwezi Aprili mwaka huu na hadi sasa mamia ya watu Sudan wameuawa, zaidi ya 5,000 wamejeruhiwa na mamilioni wamejificha majumbani mwao bila uwezo wa kupata huduma muhimu kama vile matibabu. UNHCR na OCHA wanasema leo hii, watu milioni 25 nchini Sudan, zaidi ya nusu ya idadi ya watu Sudan wanahitaji misaada ya kibinadamu na ulinzi.
Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Sudan Kusini (UNMISS) umefanya warsha za majadiliano katika mji wa Torit na Magwi mashariki mwa mji mkuu Juba jimboni Equatorial Mashariki ili kujadili kuhusu utungaji katiba na michakato ya uchaguzi.Sudan Kusini kwa sasa inatayarisha katiba yake ya kudumu ambayo si tu ni muhimu bali pia ni sharti la kufanya uchaguzi mkuu wa nchi hiyo uliopangwa kufanyika mwakani, 2024. Makundi mbalimbali ya kijamii yaliyoshiriki katika majadiliano haya yaliyoratibiwa na UNMISS ni pamoja na wanawake, vijana, waliorejea kutoka ukimbizini, wakimbizi wa ndani, na viongozi wa kimila. Jessica Kalmas, mkimbizi aliyerejea ambaye sasa ni Msemaji wa Umoja wa Vijana, Equatoria Mashariki anasema, “Kunapaswa kuwa na uzingatiaji wanaorejea. Pia, suala la ukatili wa majumbani na kijinsia likomeshwe. Hili pia lijumuishwe kwenye katiba ya kudumu.”Masuala ambayo washiriki wameyapa uzito katika majadiliano yao ni nafasi sawa kwa wanawake katika maisha ya umma, kuhakikisha wasichana wote wana haki ya kupata elimu, na kukomesha desturi ya ndoa za kulazimishwa au za utotoni. Angel Omex, Mwanafunzi ni Chuo Kikuu cha Kikatoliki cha Sudan Kusini anaeleza, “Nimehudhuria huu mchakato wa kutengeneza katiba, na nina furaha kuwa sehemu yake. Na, kulingana na maoni yangu binafsi nadhani kinachopaswa kujumuishwa katika mchakato wa kutengeneza katiba ya kudumu ni suala la asilimia 35 ya jinsia. Wanawake wanatakiwa kupewa asilimia 35. Haifai kuwa kusema tu bali inapaswa kutekelezwa. Na sio tu kwamba wanaorejea kutoka ukimbizini ni muhimu sana, lakini pia wanapaswa kurejeshwa katika jamii na kusajiliwa.”Kwa pamoja, waliohudhuria walifikia mapendekezo kuhusiana na katiba ya kudumu na uchaguzi unaofuata, ikiwa ni pamoja na ushiriki wenye nguvu Zaidi wa vijana. UNMISS inashirikiana na mamlaka za serikali na Mashirika ya Umoja wa Mataifa, Fedha na Mipango ili kuandaa warsha kama hizo kote Sudan Kusini.
Te comparto los links de las noticias de las que hablo: La cuenta de ahorro de la Apple Card ya está disponible iOS 17 permitirá instalar apps sin pasar por la App Store #hashtag inventor Chris Messina has signed off of Twitter. Canada's CBC is the latest major news org to step away from Twitter. Twitter etiquetará los tweets que promuevan el discurso de odio Elon Musk claims to be working on ‘TruthGPT' — a ‘maximum truth-seeking AI' Who needs a Starship launch when you can pre-order a Starship torch? Esta sería la fecha de lanzamiento del Pixel Fold, el primer móvil plegable de Google McDonald's lanza una campaña protagonizada por el Hamburglar Esta es Fedha, una presentadora de noticias muy popular que, en realidad, no existe Google va a revolucionar su buscador: esto es lo que se avecina impulsado por IA Europa inaugura su herramienta para abrir las cajas negras de los algoritmos en Internet Netflix abre una boutique erótica para promocionar su nueva serie 'Obsession' Noticias de tecnología, noticias de Marketing y Noticias de YouTube Sígueme en @popinteractivo Visita mi página web: ricardomiranda.es
*) North Korea leader calls for expansion of war deterrence capabilities North Korean leader Kim Jong-un has called for expanding the country's war deterrence capabilities to counter what it called "frantic" aggression by the United States and South Korea. Kim's call on Tuesday comes as Pyongyang has opened the year with a flurry of weapons tests. These tests included nuclear-capable underwater drones and the launch of two intercontinental ballistic missiles. North Korea last year declared itself an "irreversible" nuclear power, effectively ending the possibility of denuclearisation talks. *) Turkish, Russian, Syrian, Iranian FMs likely to meet in May in Moscow A meeting between foreign ministers of Türkiye, Russia, Iran, and Syria is likely to be held in early May in Moscow. Turkish Foreign Minister Mevlut Cavusoglu said this in an interview on Monday. He said the aim of these talks is to revive the political process, lasting stability and peace, fight against terrorism, and guarantee Syria's border and territorial integrity. *) Five killed, at least 6 injured in Kentucky shooting attack Five people were killed and at least six others hospitalised following a shooting targeting a bank on Monday in downtown Louisville, in the US state of Kentucky. A short while after confirming the attack, police said the shooter was dead, without giving further details. It was unclear whether the death toll of five people included the shooter. The incident triggered a massive police deployment outside the Old National Bank building. *) China completes Taiwan war games aimed at 'sealing off' island China says it has "successfully completed" three days of war games around Taiwan. The three-day show of force saw it simulate targeted strikes and practise a blockade of the self-ruled island. Chinese ally Russia defended the drills, with a Kremlin spokesperson saying Beijing had a "sovereign right" to respond to what Moscow called "provocative acts". Beijing's exercises were a response to Taiwan President Tsai Ing-wen's meeting with US House Speaker Kevin McCarthy last week. *) News anchor generated with AI appears in Kuwait A Kuwaiti media outlet has unveiled a virtual news presenter generated using artificial intelligence with plans for it to read online bulletins. "Fedha" appeared on the Twitter account of the Kuwait News website on Saturday as an image of a woman, her light-coloured hair uncovered, wearing a black jacket and white T-shirt. The site is affiliated with the Kuwait Times, founded in 1961 as the Gulf region's first English-language daily.
Nchini Nepal mradi wa BRIDGE unaotekelezwa na shirika la Umoja wa Mataifa la kazi duniani, ILO umewezesha familia moja ya kimaskini kuondokana na sio tu kutumikishwa kwenye ajira za kitumwa bali pia kuepusha baba wa familia kuondokana na kwenda nchi za nje kusaka vibarua.Tuko wilaya ya Bajura magharibi mwa Nepal barani Asia, tunakutana na Shanti Devi Lohar, mama wa familia mwenye umri wa miaka 50. Akifungua redio kujiburudisha akiwa anauza mboga mboga na maboga huku akikumbuka maisha yalivyokuwa awali.Shanti anasema mume wangu amekwenda India kusaka kibarua kutokana na hali mbaya ya kifedha ya familia yetu. Peke yangu nyumbani ilikuwa vigumu kupata kazi. Fedha ilikuwa changamoto kwani hatukuwa na ardhi.Punde anapata mteja na anauza boga moja kwa dola tatu. Msingi wa biashara hii ni nini?Shanti anasema “nilibaini kuwa kituo cha rasilimali watu kilikuwa kinaanzisha mafunzo ya kilimo cha mboga mboga nje ya msimu husika wa mazao hayo kwa wafanyakazi waliokuwa wanatumikishwa. Nilijiunga ili nipate mafunzo ya kilimo na niwe mfanyabiashara ninayejitegemea.”Mafunzo yalifanyika na kisha Shanti alimweleza mumewe ambaye alimtumia mtaji wa dola 343 wa kuanzisha kilimo biashara cha mboga mboga. ILO na mdau wake waliwapatia makaratasi ya nailoni ya kuezekea bustani hizo, madumu ya kumwagilia pamoja na mbegu.Faida ni dhahiri na anasema kwa kuuza viazi faida ni kati ya dola 86 hadi 129 kwa mwaka. Mapato kutokana na kuuza nyanya ni kati ya dola 258 hadi 300.”Ingawa watoto wake wa kiume wanasoma bweni na gharama ni dola 429 kwa mwaka, Shanti hana tena hofu kwani anapata fedha hizo kupitia kilimo biashara na binti zake wawili wanasoma shahada ya kwanza. Na zaidi ya yote anachofurahia Shanti ni kwamba mumewe hatokwenda tena nje ya Nepal kusaka kibarua.
Nchini Malawi,shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto duniani, UNICEF kwa msaada kutoka kwa wadau wake wa maendeleo linatekeleza mradi wa kupatia fedha jamii au MSCTP kwa ajili ya kupunguza umaskini, kukabili utapiamlo halikadhalika kuondokana na utoro shuleni utokanao na wazazi kushindwa kulipa karo. Nats…Video ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto duniani, UNICEF inaanza kwa kuonesha wanawake kwa wanaume wakiwa wamepanga foleni huku wameshikilia nyaraka tayari kupokea mgao wa fedha kwa mwezi kupitia mradi huo wa mgao wa fedha taslim kunusuru kaya maskini.Mary Wale mnufaika kutoka wilaya ya Balaka mkoa wa Kusini wa Malawi anasema, "Niko hapa kunufaika na mradi wa mgao wa fedha za kijamii. Nilikuwa maskini sana, sikuwa na chakula, sikuweza kupeleka watoto wangu shuleni, hata sikuwa na mavazi. Sasa nina furaha sana. Kwa fedha hizo nitatununua mahindi, nitakarabati nyumba yangu kwa kuwa iko kwenye hali mbayá. Nitanunua kuku wa kufuga ili wanisaidie siku za usoni.”Pamoja na kugawa fedha taslimu, mradi huu ulioanza kutekelezwa nchini Malawi mwaka 2006, umeanzisha vikundi vya kuweka na kukopa ambako wanachama wana uwezo wa kukopa fedha na kurejesha.Elube Ositini yeye ameanza kunufaika na mradi huu tangu mwaka 2014 na anasema,“ Kwa miaka yote hii nimeweza kujenga nyumba, kununua mifugo, kupeleka watoto shuleni. Na katika miaka minne ijayo nataka niongeze ng'ombe wafikie 10, niwapeleka watoto wangu hadi shule ya sekondari. Nina furaha sana kwa sababu nilicho nacho sasa sikutarajia kuwa navyo maishani.”Kwa Richard Kakoti ambaye naye yuko kwenye foleni kupata mgao, mradi huu ni mkombozi sana kwao kwani njaa iliwapiga na sasa wana ahueni kubwa akisema “Nimepokea Kwacha za kimalawi elfu 36. Hii ni mara yangu ya kwanza kupokea mgao huu wa fedha. Fedha hizi zitanisaidia mimi kama mkuu wa kaya kununua mahindi, maharagwe na mafuta ya kupikia kwa ajili ya familia yangu.”Kwacha Elfu 36 ni sawa na dola dola 35. UNICEF inasema mradi huo pamoja na kusaidia kukabili njaa, unasaidia pia kujenga mnepo kwa kaya wakati huu ambao mtikisiko wa kiuchumi unaleta changamoto kwenye jamii.
Watu wenye ualbino wamekuwa wakikumbwa na changamoto lukuki ikiwemo za kijamii, kiafya na kiuchumi hali inayofanya mustakabali wao kuwa na mashaka na hata wakati mwingine wanakuwa na wasiwasi kuhusu ndoto zao . Lakini kwa mtoto Elizabeth Ayebare ambaye ndoto yake ilikuwa almanusura itumbukie shimoni, mambo sasa ni shwari kwani sheria ilifuata mkondo wake na waliokuwa wanataka kupeperusha ndoto yake wakachukuliwa hatua ya kumlipa fidia na sasa anaendelea na masomo yake kama kawaida. Nini kilifanyika? Simulizi nzima anayo Anold Kayanda katika Makala hii iliyoandaliwa na ofisi ya Umoja wa Mataifa ya haki za binadamu.
Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani, WFP linasema iwapo halitapokea fedha za nyongeza, litalazimika kusitisha msaada muhimu wa kibinadamu kwa wakazi milioni moja wa jimbo la Cabo Delgado nchini Msumbiji ifikapo kilele cha msimu wa njaa mwezi Februari mwakani kutokana na ukata unaokabili. Leah Mushi na taarifa zaidi.Antonella D'Aprile ambaye ni Mkurugenzi Mkazi wa WFP nchini Msumbiji amewaambia waandishi wa habari mjini Geneva, Uswisi hii leo ya kwamba Cabo Delgado ni jimbo la Msumbiji lisilo na uhakika wa chakula na uhakika wa chakula unadorora kila uchao, huku takribani watu milioni 1.15 jimboni humo wakiwa kwenye janga au udharura wa njaa, huku takwimu mpya zaidi zikionesha hali inaweza kuwa mbaya zaidi.Ghasia zimeshamiri miezi ya karibuni, mashambulizi karibu na Pemba, mji mkuu wa Cabo Delgado pamoja na jimbo Jirani la Nampula, yamelazimu watu wengi zaidi kukimbia vijiji vyao, idadi ya wakimbizi wa ndani imeongezeka mara nne na kufikia milioni moja katika miaka miwili iliyopita.Licha ya ghasia hizo, Bi. D'Aprile amesema WFP imeendelea kusambaza misaada ya dharura, vyakula vyenye lishe kwa wajawazito na watoto, pamoja na miradi ya kujengea mnepo jamii zilizo hatarini, wakiwemo watu 44,000 kupata ardhi yao huko Cabo DelgadoHalikadhalika WFP inaendesha shirika la huduma za ndege la Umoja wa Matiafa, UNHAS ambalo ndilo pekee linalosafirisha wahudumu wa kibinadamu kuelekea maeneo yasiyofikika kwa barabara.Mkuu huyo wa WFP nchini Msumbiji amesema katika maeneo ya ndani kabisa, UNHAS ndio huduma pekee ya anga kwa wahudumu wa misaada na kwamba “mwezi Desemba mwaka 2020, kufuatia kushamiri kwa mapigano na janga la COVID-19, WFP ilifungua njia ya anga ya kuunganisha maeneo ya kaskazini mwa Msumbiji yasiyofikika. Huduma hii ya anga imesafirisha zaidi ya watumishi wa kibinadamu 10,000, na kilo 70,000 za misaada ya kibinadamu sambamba na huduma 330 za kiusalama.”Amesema kutokana na ukata huduma zote hizo zinaweza kusitishwa iwapo hawatopata dola milioni 51.Amesisitiza kuwa wakati wanatoa ombi la usaidizi huo, wataendelea kujitahidi kusambaza huduma kwa mak undi yaliyo hatarini zaidi kama wenye utapiamlo uliokithiri, wajawazito na wanawake wanaonyonyesha watoto, lakini kuna baadhi ambao itabidi washindwe kuwahudumua labda kupatikane fedha za ziada.
Janga la COVID 19 lilipotangazwa mwaka 2019 lilizua taharuki kila kona ya dunia lakini changamoto zilizoletwa na janga hilo zilikuwa fursa kwa vijana nchini Zimbabwe ambao walikuja na wazo la shule mtandaoni na Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa maendeleo duniani, UNDP likawapatia fedha ili watekeleze wazo na kuwanufaisha wanafunzi wa shule za msingi na sekondari. Tuungane na Evarist Mapesa wa Radio Washirika SAUT FM ya Mwanza Tanzania kwa ufafanuzi zaidi.Ni Kudakwashe Mlambo, mwazilishi wa Kampuni ya Digital kiota, kampuni ambayo miongoni mwa kazi zake wana jukwaa liitwalo cheza na ujifunze ambayo anasema“Kimsingi ni jukwaa, la kujifunza mtandaoni ambalo lina maudhui ya video yaliyorekodiwa awali na yanafuata muongozi wa mtaala wa Zimbabwe kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari.” Anasema katika jukwaa hilo wana walimu ambao wanarekodi masomo na pembeni ya video ya mwalimu kunakuwa na picha au michoro inayoonesha kile mwalimu anachofundisha ili kujenga uelewa zaidi.Mlambo anasema wazo la jukwaa hili alilipata akiwa chuoni wakati wakijadiliana na wenzake lakini hakuwa na uwezo wakifedha wala kiufundi wa kulitekeleza kwa wakati huo lakini baada ya kusikia tangazo la UNDP kuwa wanatafuta mawazo mapya katika kipindi cha COVID19 ndio wakaona wazo lao litasaidia mamilioni ya wanafunzi ambao walikuwa majumbani na kuamua kuliwasilisha ambapo waliibuka nafasi ya pili.“Fedha tulizoshinda katika mashindano ya Youth connekt tulinunulia vifaa, tuna camera, taa, sehemu ya kuwekea vipindi vyote tunavyozalisha na pia kompyuta tunazozitumia katika uzalishaji wa vipindi. “Vijana hao hawana utaalamu wa kuendesha biashara UNDP imehakikisha wanapata mafunzo hayo pia“Pia tumepata mafunzo ya kina ya ujasiriamali na tumejifunza kuhusu masoko na kuendesha biashara kwasababu wengi wetu ni wajasiriamali kwa mara ya kwanza kwahiyo tunajifunza sana kadri tunavyoendelea kufanya kazi, madarasa ya kujifunza tunayoshiriki yamekuwa na manufaa sana kwetu.”Mbali na jukaa hilo la cheza na jifunze au kwa kiingereza Playandlearn wameweza kutumia elimu ya ujasiriamali waliyopata katika kuanzisha biashara ya kupiga picha na video na kujipatia kipato cha Zaida kwakutumia vifaa vilevile walivyonunua kwa fedha walizopatiwa na UNDP.