POPULARITY
Misri ipo kwenye njia panda kuhusu utekelezaji wa sheria zake za kudhibiti matumizi ya tumbaku haswa sigara na Shisha. Kwa njia moja sigara inaleta mapato makubwa kwa mfuko wa mapato ya serikali ya Misri ,ni tabia inayoruhusiwa ila kwa upande mwingine inakodolea macho hatari kubwa ya kiafya inayotokana na uvutaji sigara.Unapowasili Cairo jiji kuu la Misri ,ukutana na harufu tamu ya mikate ,keki na bidhaa zingine za ngano za kuokwa,marashi yanayonukia lakini pia kuna harufu ya shisha, aina ya tumbaku ya kisasa zenye ladhaa za kupendeza lakini pia harufu kali zaidi ya sigara.Zipo sheria zinazokataza uvutaji sigara katika sehemu za umma ,shule ,vituo vya afya ila utekelezaji wake bado ni changamoto kubwa.Kuna mpango pia wa treni mwendo kasi ,maarufu Greenline ambapo uvutaji sigara umeharamishwa.Hata hivyo kibarua bado kipo cha kubadilisha mtazamo wa baadhi ya wananchi wanaoamini uvutaji sigara ni starehe ,kitu cha hadhi na unaweza kufanya hivyo popote muradi usikamatwe.Misri pia inabidi kuangalia kwa jicho la pili sheria zake za kutoza ushuru bidhaa za tumbaku iwapo lengo ni kuleta mapato kwa serikali ,kuwafaidi wazalishaji au kwa maslahi ya afya ya wengi.Kwa mujibu wa shirika la afya duniani,WHO, asilimia 20-25% ya watu wazima nchini Misri huvuta sigara.
Misri imepambana kwa karibu miaka 100 kabla kupata cheti cha WHO cha kufaulu kutokomeza Malaria Oktoba 2024 Katika mkakati ambao umetumia Misri kuangamiza Malaria ni udhibiti wa Mbu,ambapo serikali iliwekeza kwenye kupiga dawa kwenye maeneo yanayoweza kuwa makazi ya mbu .Ufuatiliaji na ubainishaji wa haraka umechangia pia pakubwa kuushinda ugonjwa wa Malaria ,mkakati ambao pia jamii ilibidi kushirikishwa.Kitengo cha afya ya umma kimekuwa kikifanya hamasisho kwa wanajamii kukumbatia mbinu za kuzuia mbu kwa kutumia vyandarua na pia kupata matibabu ya haraka mtu anapoonesha dalili za Malaria.
Unhappy about ceasefire, which they see as Indian govt's 'cowardice', extreme right-wing X accounts called foreign secretary 'spineless', 'traitor', even viciously attacking his daughter.
Hii leo tumeangazia michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika ya vijana chini ya miaka 20 kuanza nchini Misri, mkondo wa mtoano katika msururu wa raga duniani, diamond league mkondo wa pili huko Uchina na Ligi ya Basketboli mkondo wa Sahara ukiendelea, Cecafa yapata rais mpya, nembo ya Visit Rwanda yaendelea kupanuka, bondia wa DRC Martin Bakole kupigana leo usiku, PSG, Man Utd, Spurs na Chelsea zavuna matokeo mazuri kwenye nusu fainali ligi za vilabu bingwa ulaya.
Miongoni tuliyokuandalia ni pamoja na matokeo ya raga mkondo wa HongKong 7s, sakata la upangaji mchezaji dhidi ya golikipa wa Kenya Patrick Matasi, maandalizi ya debi ya Mashemeji, Misri yapewa haki za kuandaa AFCON U20 huku CAF ikiifungulia uwanja wa Benjamin Mkapa, tuzo nono kwa washindi wa Kombe la Dunia la vilabu, kocha wa Brazil atimuliwa naye Djokovic akikaribia kushinda taji lake la 100.
Matangazo ya saa nzima kuhusu habari za kutwa, ikiwa ni pamoja ripoti kutoka kwa waandishi wetu sehemu mbali mbali duniani na kote Afrika Mashariki na Kati, na vile vile vipindi na makala maalum kuhusu afya, wanawake, jamii na maendeleo.
Tuliyokuandalia hii leo ni pâmoja na matokeo ya mashindano ya tenisi ya vijana barani Afrika chini ya miaka 14, kocha mpya wa Kenya ni nani, matokeo ya mechi za kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika kwa kina dada, timu sita kushiriki ligi ya Afrika ya basketboli kwa mara ya kwanza, huku Afrika Kusini ikijiandaa kutuma ombi rasmi la kuandaa mkondo mmoja wa F1 na Jose Mourinho apata afueni baada ya adhabu yake kupunguzwa.
Hii leo jaridani tunaangazia juhudi za kukabiliana na mlipuko wa homa ya marburg Tanzania, na elimu kwa wakimbizi katika makazi ya Kakuma nchini Kenya. Makala inatupeleka nchini Lebanon na mashinani inaturejesha Gaza.Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la afya duniani, WHO, Dkt. Tedros Ghebreyesus amesema wanashirikiana na serikali ya Tanzania kudhibiti mlipuko wa homa ya Marbug iliyoripotiwa mkoani Kagera, kaskazini magharibi mwa taifa hilo la Afrika Mashariki.Migogoro, vita na mabadiliko ya tabianchi mara nyingi vimekuwa vikiwapora watoto fursa ya elimu na hata kusambaratisha mustakbali wao na wengi wanajikuta wakiishia kwenye makambi ya wakimbizi linasema shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF. Kwa kulitambua hilo shirika hilo linaendesha miradi mbalimbali ya kuhakikisha watoto waliokosa elimu hata kama wana umri mkubwa wanapewa fursa ya pili kusoma kama ilivyokuwa kwa mkimbizi Philip Lon'golea kutoka Sudan aliyekimbilia Uganda kwanza lakini sasa yuko kwenye kambi ya wakimbizi ya Kakuma nchini Kenya.Katika makala Thelma Mwadzaya anatupeleka Lebanon ambako tarehe 17 mwezi huu wa Januari Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa akiwa ziarani Lebanon alitembelea walinda amani wa Umoja wanaohudumu chini ya ujumbe wa Mpito wa UN nchini Lebanon, UNIFIL, ambao walikumbwa na zahma wakati jeshi la Israeli liliposhambulia kituo chake kinyume na azimio namba 1701 la mwaka 2006, linalozuia mashambulizi kwenye eneo tenganishi kati ya Israeli na Lebanon.Na mashinani tutaelekea Gaza kusikia kauli kutoka kwa mkimbizi wa ndani baada ya kuanza kutekelezwa usitishaji uhasama na kuachiliwa kwa mateka na wafungwa.Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!
Makala haya yanazungumzia jinsi dampo la Taka la Nkumba nchini Uganda limekuwa tishio la kimazingira kwa ziwa victoria ambalo ndilo chanzo kuu cha mto Nile.Baada ya dampo la Kiteezi jijini Uganda kuporomoka Agosti 9 mwaka wa 2024 na kuwauwa watu kadhaa,serikali nchini humo ilitoa amri taka zote kutoka Kampala ielekezwe Nkumba karibu na ziwa ,hatua hiyo ikiongeza uchafuzi zaidi wa mazingira .
Matangazo ya nusu saa kuhusu habari za mapema asubuhi pamoja na habari za michezo.
Mystery writers Angel Misri and Sam Wiebe recommend some heart-pumping holiday reads; Amy Stuart shares what it was like collaborating with a hockey legend on Home and Away; T. Thomason can't get enough of sci-fi books; Richard Van Camp talks about Star Wars toys and gratitude; and Leslie Jamison on evolving while re-reading Good Morning, Midnight on this episode of The Next Chapter.
(0:00) Intro(1:25) Hulia Mubarak Hazrat Musa (AS)(2:22) Hazrat Jibraeel (AS) doodh aur sharab Hazrat Musa (AS) ke samne laye(3:12) Nabi ﷺ ne Hazrat Yunus (AS) ke baare mein kya kaha?(5:38) 10th Muharram ka roza kab sunnat hua?Stories and Teachings of Hazrat Musa (AS)(7:05) Koh-e-Toor par Allah ki tajalli(9:34) Hazrat Musa (AS) qayamat ke din sabse pehle hosh mein kyun aayenge?(11:48) Firauniyon par toofan aur azabLessons from Hazrat Musa (AS) and Hazrat Khizar (AS)(14:14) Hazrat Musa (AS) aur Khizar (AS) ka waqia(15:50) “Main sabse bara aalim hun” kehna kaisa hai?(18:03) Ghairat ki wajah se ghussa aana(20:36) Khadim ki ghalti par maaf karna(22:09) Yusha (AS) ne ghalti ka malba kis par dala?(22:59) Khizar (AS) ka hairan hona Musa (AS) ke salam par(24:02) Takveeni kaamon ki haqeeqatPractical Islamic Guidance(27:20) Darhi rakhne par Imam Shafai ka qoul(31:36) Nizam ki tabdeeli ke liye kya karein?(32:44) Jinn utarne ke liye aamil ke paas jana?(34:00) Mufti sb ka challenge aamilon ko(35:16) Jamiatur Rasheed mein aamilon ke chakkar(36:20) Mufti sb ka hamzad aur aamilIslamic Rulings and Everyday Matters(37:24) Aashurah ka roza nafal?(37:30) Sabz mirch aur doosri sabziyon mein ushar ka hukam?(38:04) Mobile mein game khelne se paisa kamaana?(38:20) Waldain ka imtiyazi salook ghareeb bete ke saath?(39:14) Farz namaz mein imam ko luqma dena?(39:24) Misri ulama darhi kyun nahi rakhte?Hazrat Khizar (AS) and Some Questions(40:18) Hazrat Khizar (AS) zinda hain?(41:18) Mufti sb ke FB page par blue tick kyun nahi?(41:41) Mufti sb ka 1.5 hours Friday bayan sunna?Cleanliness and Pets in Islam(43:10) Kutte ka jhoota najas hai ya pak?(47:04) Kutte ke jhootay bartano ko 7 bar dhona ya 3 bar? + mitti se dhona?(52:53) Kutta palna? Europe mein God ke bajaaye dog?(54:02) Kutta palne ke Islami ehkam?(55:58) Billi ka jhoota najas hai ya pak?(1:02:58) Billi ke jhootay bartano ko 1 bar dhona laazim?Wudu and Masah Guidance(1:04:44) Mozon par masah ke ehkam aur Surah Maaidah ki aayaat Hosted on Acast. See acast.com/privacy for more information.
Can taking a selfie be good for your health? This week on StartUp Health NOW, we explore a revolutionary new approach to health screening with Kavi Misri, CEO & Founder of Hibiscus Health. Misri is a long-time Health Transformer; after his first StartUp Health portfolio company – Rose Health – was acquired, he launched Hibiscus Health and rejoined the StartUp Health Community. Discover how Hibiscus leverages smartphone selfies to analyze facial blood flow and identify potential risks for diabetes and other conditions: Easy, intuitive screenings designed for broad adoption Works with existing smartphone cameras and webcams Unlocking the potential of selfies for health screening Plus, learn about StartUp Health's Cardiometabolic Health Moonshot Community and how it helps innovative companies accelerate growth. This episode is a must-listen for anyone interested in the future of healthcare, preventive medicine, and leveraging technology for better health outcomes. Listen now and see if your selfie can unlock your potential health risks! Are you ready to tell your story? Members of our Health Moonshot Communities are leading startups with breakthrough technology-driven solutions for the world's biggest health challenges. Exposure in StartUp Health Media to our global audience of investors and partners – including our podcast, newsletters, magazine, and YouTube channel – is a benefit of StartUp Health's PRO Membership. To schedule a call and see if you qualify to join and increase brand awareness through our multi-media storytelling efforts, submit our three-minute application. If you're mission-driven, collaborative, and ready to contribute as much as you gain, you might be the perfect fit. Learn more and apply today. Want more content like this? Sign up for StartUp Health Insider™ to get funding insights, news, and special updates delivered to your inbox.
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayoangazia uvuvi katika mji wa Kalokol karibu na fuo za Ziwa Turkana Kaskazini mwa Kenya. Pia tunakuletea muhtasari wa habari zikiwemo za mkutano wa WUF12 Cairo Misri, chanjo ya malaria Sudan, siku ya Tsunami, na mashinani.Mkutano wa 12 wa Jukwaa la Miji Duniani, WUF12 umeingia siku ya pili hii leo huko Cairo, Misri, ambako Ming Zing ambaye ni Mkurugenzi wa Miji, Mnepo na Ardhi kutoka Benki ya Dunia amezungumzia umuhimu wa kujumuisha wanawake na vijana katika mipango miji.Sudan imekuwa nchi ya 16 barani Afrika na ya kwanza katika Ukanda wa WHO wa Mashariki na Mediterania kuanzisha chanjo dhidi ya Malaria kwa watoto wasiozidi umri wa miezi 12. Chanjo imeanza kutolewa jana katika majimbo ya Gedaref na Blue Nile ambapo WHO na wadau wamesema mwaka 2025 na 2026 chanjo itapelekwa katika maeneo 129 nchini kote Sudan.Na leo ni siku ya kimataifa ya kuhamasisha umma kuhusu tsunami, ambayo ni mawimbi makubwa ya maji yatokanayo na tetemeko chini ya bahari. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres katika ujumbe wake anasema pamoja na kukumbuka waliopoteza maisha kwa tsunami miaka 20 iliyopita, tunaahidi tena kulinda zaidi ya watu milioni 700 duniani kote walio hatarini kukumbwa na Tsunami.Mashinani tutaelekea Sudan kusini kuangazia harakati za Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa Kulinda Amani nchini humo, UNMISS za kuimarisha ulinzi wa wanawake katika migogoro na majanga.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini DRC kufuatilia kazi za kituo cha Taifa cha Redio na Televisheni, RTNC huko Beni jimboni Kivu Kaskazini za kakabiliana na habari potofu. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na mashinani.Ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa iliyotolewa leo mjini Cairo, Misri, imebainisha kwamba athari za vita zimerudisha nyuma maendeleo huko Gaza kwa takriban miaka 69. Ripoti hiyo iliyoratibiwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo UNDP na Kamisheni ya Umoja wa Mataifa ya Kiuchumi na Kijamii kwa Asia Magharibi imeonya kwamba bila kuondoa vikwazo vya kiuchumi na kuwekeza katika maendeleo, uchumi wa Palestina unaweza kushindwa kurejesha viwango vya kabla ya vita na kusonga mbele kwa kutegemea misaada ya kibinadamu pekee.Kiongozi wa timu ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani (WHO) ya kupambana na mlipuko wa ugonjwa wa Marburg Dkt. Janet Diaz ameeleza kwamba uongozi thabiti wa serikali ya Rwanda umewezesha kufanya uamuzi wa haraka na kuchukua hatua kuanzisha mwitikio wa sekta mbalimbali dhidi ya mlipuko wa sasa wa ugonjwa huo wa Marburg nchini humo.Na uongozi wa Kikosi cha Muda cha Umoja wa Mataifa nchini Lebanon (UNIFIL) umeendelea kusisitiza kwamba pamoja na changamoto zilizopo, walinda amani wa UNIFIL wanaendelea kufanya kazi kwa karibu na jamii za kusini mwa Lebanon ili kuwezesha utoaji wa misaada ya kibinadamu kwa wenye uhitaji. Hivi karibuni kumekuwa na mashambulizi dhidi ya walinda amani hao wa Umoja wa Mataifa yanayotekelezwa na majeshi ya Israeli.Mashinani kupitia video ya Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu masuala ya Kibinadamu na misaada ya dharura OCHA tunamuangazia mmoja wa watu waliokimbia makazi yao akiwa katika shule ya Al Rimal, akielezea changamoto wanazokutana nazo katika kukabiliana na hali ngumu inayowakabili raia wa Gaza.Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!
Tuliyokuandalia ni pamoja na michuano ya kufuzu AFCON U20 mwaka ujao, namna timu za Afrika zilicheza kwenye wiki ya kwanza ya Kombe la Dunia la kina dada wasiozidi miaka 17, timu ambazo tayari zimefuzu AFCON ya 2025 nchini Morocco na nafasi ya timu za Afrika Mashariki na Kati, AFCON ya ufukweni yaanza leo nchini Misri, droo ya klabu bingwa Afrika kwa kina dada, mashindano ya magari ya Rwanda Mountain Gorilla Rally, kutimuliwa kwa kocha Kavazovich klabuni Vipers na Ligi za ukanda na Ulaya
Ni wiki iliyoshuhudia matukio mengi miongoni ni pamoja na serikali ya Kenya kuendelea na uchunguzi wa mkasa wa moto uliowauwa wanafunzi, maandamano ya maelfu ya wakimbizi kwenye mji wa Goma mashariki mwa DRC wakiomba serikali iwarejeshe makwao na kumaliza vita, kule Senegal rais Bassirou alilivunja Bunge la taifa, na mdahalo wa kwanza wa televisheni kati ya rais wa zamani wa Marekani Donald Trump na makamu wa rais Kamala Harris wanaowania kiti cha urais katika uchaguzi wa Novemba na mengineyo.
Makala hii imeangazia hali ya kibinadamu inavyoendelea kuwa mbaya ndhini Sudan licha ya juhudi za kimataifa zinzoendelea.Nini kifanyike ili kufikia amani ya kudumu ya Sudan? kwa nini serikali imekataa kukaa meza moja na wapiganaji wa RSF? kuangazia hili, Ruben Lukumbuka anazungumza na Lugete Musa Lugete ni mchambuzi wa siasa za Kimataifa akiwa Tanzania, lakini pia Dismas Mokua mchambuzi wa masuala ya kisiasa akiwa Nairobi nchini Kenya
Matukio ya dunia yaliyokithiri vichwa vya habari ni pamoja na virusi vya Mpox kutangazwa kuwa janga la dharura la kiafya huku bara la Afrika likiathiriwa zaidi, Burundi yamwachia mwanahabari aliyehukumiwa kifungo cha miaka 10, tutaangazia siasa za Tanzania baada ya wanasiasa wa upinzani kukamatwa baadaye wakaachiwa, lakini pia hatua za mazungumzo kule Geneva kuhusu amani nchini Sudan. Pia tutaangazia mgomo wa vyombo vya habari nchini Senegal kadhalika tutachambua wito wa Umoja wa Mataifa kutaka Afrika kupewa kiti cha kudumu katika baraza la usalama la umoja huoKule Gaza, kundi la Hamas limekataa masharti 'mpya' ya upatanishi na Israeli na mazungumzo ya kupata mkataba wa kusitisha vita hivyo, kurejelewa tena wiki hii jijini Cairo, Misri.
Joshua Cheptegei ashinda medali ya dhahabu kwenye mbio za mita 10,000 huku Malkia Strikers ikibanduliwa mashindanoni. Morocco na Misri zafuzu nusu fainali huku waafrika kwenye uogeleaji wakifanya vibaya. Pia tutakufahamisha matokeo ya judo, basketboli, kuendesha basikeli na jedwali la medali ambapo Uchina inazidi kuongoza jedwali hilo
This is the fourth episode in a 6-part magazine mini series. Here you'll meet award-winning journalist, author and educator, Angela Misri. You'll hear about Angela's career path in different media spaces: in print, in audio and on the web. You'll hear specific examples related to telling stories in added value ways; the why and the how of telling the same story differently across mediums.You'll also hear about the shifts that Angela's seen in the last 20 years in publishing industry, and what parts of journalism Angela believes are most at risk from AI domination. You'll also hear what Angela believes we'll be talking about in a year's time when it comes to AI and journalism.This episode is part of a guest lecture series in CGCM 720 Magazine Production & Publishing, as well as DG 8111 Digital Publishing in The Creative School at Toronto Metropolitan University.I'm all about interesting projects with interesting people! Let's Connect on the web or via Instagram. :)
Misri yatangaza nia ya kuunga mkono kesi ya Afrika Kusini dhidi ya Israel
Matangazo ya saa nzima kuhusu habari za kutwa, ikiwa ni pamoja ripoti kutoka kwa waandishi wetu sehemu mbali mbali duniani na kote Afrika Mashariki na Kati, na vile vile vipindi na makala maalum kuhusu afya, wanawake, jamii na maendeleo.
Matangazo ya saa nzima kuhusu habari za kutwa, ikiwa ni pamoja ripoti kutoka kwa waandishi wetu sehemu mbali mbali duniani na kote Afrika Mashariki na Kati, na vile vile vipindi na makala maalum kuhusu afya, wanawake, jamii na maendeleo.
Misri yasema haitaruhusu tishio lolote kwa Somalia au usalama wake
Matangazo ya nusu saa kuhusu habari za mapema asubuhi pamoja na habari za michezo.
NBF 218- Dhul Noon Al-Misri- Dr Shadee Elmasry by Safina Society
Wa Australia ambao wamekwama mjini Gaza, wamesema wameshauriwa mara kwa mara waende katika kivukio cha mpaka wa Rafah na Misri, hata hivyo walipofika huko walipata mpaka huo umefungwa.
Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ulimwenguni WHO limesema takriban nusu ya idadi ya watu ulimwenguni hivi sasa wapo hatarini kuungua ugonjwa wa Dengue huku ikikadiriwa kila mwaka watu kati ya milioni 100 mpaka 400 wanapata maambukizi. Dengue ni ugonjwa unaoenezwa na mbu aina ya Aedes. Ugonjwa huo hutokea zaidi katika nchi zenye hali ya hewa ya kitropiki na ya joto. Mkuu wa Kitengo kinachohusika na magonjwa ya Kitropiki yasiyopewa kipaumbele ambaye pia ni mratibu wa mpango wa magonjwa ya Dengue na Arbovirus katika shirika la Afya ulimwenguni WHO Dkt. Raman Velayudhan, akizungumza na waandishi wa habari hii leo jijini Geneva Uswisi amesema ugonjwa huu wa Dengue “Umeongezeka kwa kasi duniani kote katika miongo ya hivi karibuni, huku idadi ya wagonjwa wanaoripotiwa WHO wakiongezeka kutoka nusu milioni mwaka 2000 hadi zaidi ya milioni 4.2 mwaka 2022. Hiyo ni takriban mara 8 zaidi katika miongo miwili.”Ugonjwa wa Dengue, ambao pia huitwa homa ya mfupa, ni maambukizi ya kawaida ya virusi ambayo huenea kutoka kwa mbu hadi kwa binadamu. Watu wengi walio na ugonjwa huu hawana dalili na hupata nafuu baada ya wiki 1 mpaka 2. Hata hivyo Dkt. Velayudhan amesema “Kwa wengine hupata dalili za kawaida ikiwemo homa kali, maumivu ya kichwa, maumivu ya mwili, kichefuchefu na vipele. Iwapo mtu ataugua na kupona na kisha kuugua kwa mara ya pili ana uwezekano mkubwa kupata dalili za dengue kali.”Watu ambao hupata Dengue kali wanahitaji kupatiwa matibabu hospitalini kwani wakichelewa wanaweza kupoteza maisha.Ingawa hakuna matibabu kamili ya ugonjwa huu mpaka sasa , wale wanaogundulika hupatiwa dawa za kupunguza joto na maumivu ya mwili. Watu wanaweza kupunguza hatari ya kupata dengue kwa kuepuka kuumwa na mbu, hasa mchana.Wakati takriban asilimia 70 ya wagonjwa wengi wakiripotiwa kutoka Barani Asia, Ukanda wq Jangwa la Sahara idadi kubwa ya wagonjwa wameripotiwa kutoka nchini Sudan ambapo kulikuwa na wagonjwa 8239 na vifo 45 tangu Julai 2022. Katika wiki za hivi karibuni WHO imepokea ripoti za uwepo wa wagonjwa wa dengue nchini Misri.WHO imezitaka wizara za Afya kuchukua hatua kwani wakati kuna milipuko, dengue inaweza kuchukua rasilimali za thamani kutoka kwenye mfumo wa afya, na kuongeza mzigo zaidi kwa taifa.
Kurejeshwa kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya Uturuki na Misri kunaongeza matumaini ya kumaliza mizozo huko Mashariki ya Kati na Afrika
Hii leo jaridani tunaangazia wanawake na wasichana nchini Sudan na kazi ya walinda amani nchini CAR. Makala tutakupeleka nchini DRC na mashinani nchini Misri, kulikoni?Wanawake na wasichana wanaokimbia machafuko yanayoendelea mjini Kharthoum nchini Sudan wanakabiliwa na changamoto lukuki hususan kwa wajawazito wanaohitaji msaada wa kujifungua, kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu na afya ya uzazi UNFPA ambalo sasa limechukua jukumu la kuhakikisha uzazi salama kwa wanawake hao.Walinda amani wa Umoja wa Mataifa wa kikosi cha 6 kutoka Tanzania (TANBAT 6) wanaohudumu chini ya Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Afrika ya kati, CAR (MONUSCO) wametoa mafunzo ya upishi kwa vikindi vya wanawake wa Kijiji cha Moro kilichoko takribani kilometa 50 kutoka Mji wa Berberati, jimboni Mambere Kadei yalipo makao makuu ya kikosi hicho. Makala tunakupeleka nchini DRC ambapo Muungano wa mashirika ya kiraia katika eneo la Kalehe jimboni Kivu Kusini, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC wako katika harakati za kuhamasisha wananchi kupanda miti na kuchukua hatua nyingine zitakazosaidia kupambana na mabadiliko ya tabianchi baada ya eneo hilo kukumbwa na mafuriko yaliyosababisha vifo na uharibifu mkubwa mapema mwezi Mei Mwaka huu.Katika mashinani na leo tutaelekea nchini Misri ambapo wanawake waliokimbia migogoro nchini Sudan kuelekea nchini humo wanapokea huduma za afya ya akili baada ya kupitia machungu.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
Jaridani hii leo ni mada kwa kina leo tunaelekea nchini DRC kuangazia kikosi cha pili cha walinda amani kutoka Kenya cha kuchukua hatua za haraka KEN QRF 2 kinachohudumu mjini Beni, Jimboni Kivu Kaskazini, Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, (DRC) chini ya Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo, DRC-MONUSCO. Pia tunakuletea habari kwa ufupi zikiwemo za matumaini kwa familia zilizokata tamaa zilizokwama katika kitovu cha mzozo nchini Sudan, msaada wa kibinadamu kwa watoto nchini humo, na wakimbizi wanaohama kwa nchi jirani. Mashinani tutakupeleka nchini Tanzania, kulikoni?Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) leo Jumanne limeeleza kuwa kwa mara ya kwanza tangu mapigano yazuke nchini Sudan tarehe 15 Aprili, wahudumu wa kibinadamu sasa wameweza kufikisha msaada wa chakula kwa familia zilizokata tamaa zilizokwama katika kitovu cha mzozo huo, Khartoum. Tukisalia na taarifa kuhusu hali ya Sudan, hii leo pia Msemaji wa UNICEF James Elder amewaambia waandishi wa habari mjini Geneva kwamba "watoto wengi zaidi nchini Sudan wanahitaji usaidizi wa kuokoa maisha kuliko hapo awali", huku watoto milioni 13.6 wakihitaji msaada wa haraka. Na akifanya kulinganisha idadi hiyo akasema kwamba, "Hii ni zaidi ya idadi ya watu wote wa Sweden, Ureno au Rwanda,"Na Kamishna Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) Filippo Grandi akihitimisha ziara ya siku tatu nchini Misri ametoa wito wa dharura wa msaada kwa watu wanaokimbia Sudan na akazisihi nchi zinazowapokea wakimbizi wa Sudan kuendelea kuacha mipaka yao wazi kwa ajili ya wale wanaotoroka vita.Katika mashinani tunakuletea ujumbe wa Kamishna Suzan Kaganda ambaye anahusika na Utawala na Raslimali watu katika Jeshi la Polisi Tanzania akizungumzia mikakati ya Jeshi la Polisi la Tanzania kushiriki katika shughuli za ulinzi wa amani duniani.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, Karibu!
Jaridani leo tunaangazia machafuko nchini Sudan na ukame uliokithiri katika pembe ya Afrika. Makala tunakupeleka nchini Misri na mashinani nchini DRC, kulikoni? Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan, Volker Perthes, ambaye pia ni Mkuu wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kusimamia kipindi cha mpito SUDAN, UNITAMS amesema bila kujali ni nani anayehusika na janga la kibinadamu nchini Sudan, Umoja wa Mataifa utaendelea kuwasaidia wananchi. Hii leo jijini New York Marekani, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres kwakushirikiana na nchi saba wanachama wa UN wanaendesha tukio la uchangishaji fedha lengo likiwa ni kukusanya dola bilioni 7 kwa ajili ya usaidizi wa kibinadamu kwa nchi zilizopo pembe ya Afrika.Makala tunaelekea Misri, taifa lenye watu milioni 100 hivi sasa, lakini ni asilimia 30 tu ya watu hao yani watu milioni 36.8 ndio wenye akaunti za benki. Katika zama hizo za huduma za fedha kimtandao, mashirika ya mawasiliano ya simu yanaingia ubia na benki ili kupanua wigo wa huduma hizo.Katika mashinani na tukiwa tunaelekea siku ya walinda amani duniani leo tutaelekea nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kusikiliza ni kwa jinsi gani tasnia ya michezo ya kuigiza na vipaji vya wenyeji vimesaidia kuzuia unyanyasaji na ukatili wa kingono unaosababishwa na walinda amani na wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa nchini humo.Mwenyeji wako ni Flora Nducha, Karibu!
Misri, taifa lenye watu milioni 100 hivi sasa, lakini ni asilimia 30 tu ya watu hao yani watu milioni 36.8 ndio wenye akaunti za benki. Katika zama hizo za huduma za fedha kimtandao, mashirika ya mawasiliano ya simu yanaingia ubia na benki ili kupanua wigo wa huduma hizo. Ukosefu wa huduma za fedha kimtandao zinakuwa kikwazo kwani wananchi hupoteza muda mwingi benki kusubiria malipo ambayo wangaliweza kuyapokea kupitia simu za kiganjani au rununu. Shuhuda pande zote mbili hizo ni msichana mmoja mkazi wa Cairo nchini Misri kama anavyosimulia Assumpta Massoi kwenye makala hii iliyoandaliwa na shirika la Umoja wa Mataifa la Mawasiliano duniani, ITU.
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina ambapo tunamulika juhudi za wanawake wa jamii ya kifugaji mkoani Arusha ambao wameamua kujihusisha na ufugaji nyuki. Pia tunakuletea habari kwa ufupi zikiwemo za siku za UN, msaada wa kibinadamu nchini Sudan na ulizi wa amani nchini DRC. Na katika jifunze lugha ya tunakuletea maana ya methali JINO LA PEMBE SI DAWA YA PENGO, karibu!.Hii leo ni siku ya kimataifa ya wanawake katika sekta ya usafirishaji baharini ambapo Katibu Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la usafirishaji baharini, IMO, Kitack Lim ametoa ujumbe ambao pamoja na mambo mengine unatambua mchango wa wafanyakazi hao baharini na nje ya bahari katika kusaidia mpito wa kupunguza utoaji wa hewa ya ukaa, matumizi ya dijitali na mustakabli endelevu wa tasnia hiyo. Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula duniani, WFP limefikishia jumla ya watu 54,000 msaada wa dharura wa chakula kwenye vituo viwili vya mpakani huko Aswan na Misri wakati huu ambapo familia zinazidi kuingia Misri zikikimbia mapigano nchini Sudan.Na huko Bukavu, jimboni Kivu Kusini, nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo unaendesha mafunzo kwa polisi wa DRC juu ya ulinzi wa raia ambacho ni kipaumbele muhimu cha kupatia polisi hao usaidizi muhimu wa kuongeza uelewa wa jukumu hilo kuelekea mpito wa MONUSCO kuondoka nchini humo.Na katikajJifunze Kiswahili Dkt Mwanahija Ali Juma, Katibu Mkuu wa Baraza la Kiswahili, Zanzibar nchini Tanzania, BAKIZA anachambua methali Jino la Pembe si dawa ya pengo.Mwenyeji wako ni Anold Kyanda, Karibu!
Mzozo nchini Sudan ukiingia mwezi wa pili, hii leo Umoja wa Mataifa na wadau wake wamefanyia marekebisho ombi la usaidizi kwa nchi hiyo na sasa linafikia dola bilioni 3 kwa ajili ya kusaidia mamilioni ya watu nchini humo na mamia ya maelfu wengine waliokimbilia nchi jirani kusaka usalama.Uzinduzi wa ombi hilo lililorekebishwa umefanywa kwa pamoja hii leo huko Geneva Uswisi na ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu misaada ya dharura, OCHA na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi duniani, UNHCR. Hivi sasa jumla ya dola bilioni 2.56 zinahitajika kwa mwaka 2023, ikiwa ni nyongeza ya dola milioni 800 kutoka miezi michache iliyopita, ili kusaidia watu milioni 18 hadi mwishoni mwa mwaka huu na hivyo kufanya ombi hili kuwa ombi kubwa zaidi kuwahi kutolewa kwa Sudan. Marekebisho hayo yanazinagatia ongezeko la mahitaji lililochochewa na mapigano yanayoendelea ambapo Mkuu wa ofisi ya OCHA mjini Geneva, Ramesh Rajasingham amewaambia waandishi wa habari kuwa, “mahitaji nchini Sudan ni ya msingi na yamesambaa kama unavyoweza kufikiria kutokana na majanga: kulindwa dhidi ya mapigano, matibabu, chakula, maji, huduma za kujisafi, malazi na huduma dhidi ya kiwewe. Tunapata pia taarifa za ongezeko la ukatili wa kingono na waathirika hawawezi kupata huduma. Watoto wako hatarini zaidi katika janga hili linalozidi kuibuka.” Akifafanua kuhusu ombi la usaidizi kwa wakimbizi waliosaka hifadhi Jamhuri ya Afrika ya Kati, Chad, Misri, Ethiopia, Sudan Kusini na wakimbizi waliorejea nyumbani kutokana na changamoto Sudan, Kamishna Msaidizi wa UNHCR akihusika na operesheni, Raouf Mazour amesema, “hii leo tunatoa ombi la takribani dola milioni 472 ili kukidhi mahitaji ya zaidi ya watu milioni 1 katika kipindi cha miezi 6 ijayo.” Mapigano yalizuka Sudan tarehe 15 mwezi Aprili mwaka huu na hadi sasa mamia ya watu Sudan wameuawa, zaidi ya 5,000 wamejeruhiwa na mamilioni wamejificha majumbani mwao bila uwezo wa kupata huduma muhimu kama vile matibabu. UNHCR na OCHA wanasema leo hii, watu milioni 25 nchini Sudan, zaidi ya nusu ya idadi ya watu Sudan wanahitaji misaada ya kibinadamu na ulinzi.
Takriban watu milioni 2 hadi milioni 2.5 wanatarajiwa kutumbukia kwenye janga la njaa nchini Sudan katika miezi michache ijayo kwa sababu ya vita inayoendelea nchini humo limeonya leo shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP.Kwa mujibu wa taarifa ya shirika hilo iliyotolewa mjini Roma Italia na Port Sudan , hii itafanya hali mbaya ya kutokuwa na uhakika wa chakula Sudan kufikia rekodi ya juu kabisa huku kukiwa na watu milioni 19 ambao ni theluthi mbili ya watu wote nchini humo wakiwa wameathirika.Majimbo yanayotarajiwa kuathirika zaidi ni Darfur Magharibi, Kordofan Magharibi, Blue Nile, Red Sea na Darfur Kaskazini.Shirika hilo la mpango wa chakula linasema bei ya chakula imeongezeka mara dufu nchi nzima na sasa bei ya kikapu kimoja cha chakula kitatazamiwa kupanda kwa asilimia 25 katika miezi mitatu hadi sita ijayo.Kutokana na mapigano yanayoendelea wakulima wengi inasema WFP hawawezi Kwenda mashambani mwao kupanda katika msimu wa mvua kati ya Mei na Julai hali ambayo itapandisha hata zaidi bei za vyakula.Shirika hilo baada ya kusitisha kwa muda operesheni zake sasa imerejea kugawa msaada wa kuokoa Maisha na wiki iliyopita pekee imewafikia watu 35,000, lengo likiwa kuwafikia watu 384,000 walioathirika na mapigano mapya, wakimbizi wa zamani, wakimbizi wa ndani na jamii zinazowahifadhi katika majimbo ya Gedaref, Gezira, Kassala na White NileKatika miezi ijayo WFP pia itaongeza operesheni zake ili kuwasaidia watu milioni 4.9 katika maeneo ambayo usalama unaruhusu, ikiwa ni Pamoja na kuzuia na kutibu utapiamlo kwa Watoto 600,000 wa chini ya umri wa miaka mitano na wanawake wanaonyonyesha.Pia WFP ikishirikiana na wadau wengine likiwemo shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR na la kuhudumia Watoto UNICEF inasaidia nchi jirani ambako watu wanakimbilia kwa msaada wa chakula na maji ikiwemo Chad, Sudan Kusini, Misri na Jamhuri ya Afrika ya Kati CAR.
Hii leo jaridani tunaangazia wanawake na wasichana katika sayansi, na msaada wa binadamu mashariki ya kati kwa waathirika wa tetemeko la ardhi. Makala tunakupeleka nchini Tanzania na mashinani nchini Misri, kulikoni? Uwepo wa idadi kubwa ya wanawake na wasichana katika sekta ya sayansi ni faida kuwa kwa sekta ya sayansi na jamii kwa ujumla amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres akihimiza kuchagiza wanawake na wasicha kuingia zaidi katika sekta hiyo.Mashirika ya Umoja wa Mataifa yanaendelea kupeleka na kusambaza misaada nchini Uturuki au Türkiye na Syria ili kusaidia walioathiriwa na matetemeko makubwa ya ardhi yaliyotokea Jumatatu wiki hii na kujeruhi, kuua maelfu na kuharibu miundombinu. Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) lina lengo la kuwafikia watu nusu milioni katika nchi zote mbili ijapokuwa kuna changamoto za kiusalama katika baadhi ya maeneo.Makala tunakupeleka mkoa wa Njombe, kusini mwa Tanzania ambako huko leo kumefanyika maadhimisho ya siku ya mikunde duniani, ngazi ya kitaifa na John Kibambala wa redio washirika KIDS Time FM amezungumza na wanafunzi wa shule ya msingi Itipingi katika halmashauri ya wilaya ya Njombe, ambao ni wanufaika wa mradi wa kilimo cha bustani na mlo shuleni unaopatia kipaumbele kilimo na mlo wa mazao aina ya mikunde, mradi unaofadhiliwa na shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo FAO nchini humo.Na katika mashinani nampisha Dkt. Menatallah Elserafy kutoka Misri, ambaye ni Profesa msaidizi na mtafiti wa kuzingatia taratibu za ukarabati wa vinasaba au DNA katika Kituo cha Genomics cha Jiji la Sayansi na Teknolojia la Zuwail nchini humo. Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
Huko Sharm-el-Sheikh nchini Misri, kwenye mkutano wa 27 wa nchi wanachama wa Mkataba wa mabadiliko ya tabianchi, COP27, tarehe 17 mwezi huu wa Novemba yalishuhudiwa maandamano ya maelfu ya wawakilishi wa watu wa jamii ya asili, wanawake, wanarahakati wa masuala ya jinsia, vijana, mazingira na haki kwa tabianchi kutoka pande mbalimbali za dunia. Wao waliandamana kwa niaba ya maelfu ya mashirika na mamilioni ya watu na kupitisho azimio lao la umma kuhusu haki kwa tabianchi. Wanapaza sauti je ni sauti zipi? Wanataka nini? Anold Kayanda amefuatilia maandamano hayo na kuandaa Makala haya..
Hii leo jarida linaangazia ripoti iliyotolewa leo na UNICEF kuhusu ubaguzi wa rangi na ubaguzi dhidi ya watoto na pia habari kutoka Garissa, Kenya, makala ya maandamanano ya wanaharakati huko Sharm-el-Sheikh nchini Misri kwenye mkutano wa 27 wa nchi wanachama wa Mkataba wa mabadiliko ya tabianchi, COP27, kisha mashinani nchini Ethiopia.Ubaguzi wa rangi na ubaguzi mwingine dhidi ya watoto kwa misingi ya makabila, lugha na dini zao umeenea duniani kote na kuleta athari kwenye mfumo wa haki, usawa na hata uwezo wa kujua kusoma, hayo yapo kwenye ripoti iliyotolewa leo na Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Watoto UNICEF.Msaada wa kisima cha maji uliofanikishwa na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF katika shule ya Msingi ya Daley kwenye Kijiji cha Daley, Kaunti ya Garissa nchini Kenya, umesaidia sana jamii hasa katika suala la elimu katika eneo hilo la nchi ambalo limekosa mvua ya kutosha kwa misimu mitano mfululizo.Makala tunafuatilia maandamanano ya wanaharakati huko Sharm-el-Sheikh nchini Misri kwenye mkutano wa 27 wa nchi wanachama wa Mkataba wa mabadiliko ya tabianchi, COP27, maandamanayo yaliyofanyika tarehe 17 mwezi huu wa Novemba, kulikoni?Mashinani tunakwenda nchini Ethiopia kuona ni kwa vipi mtoto mmoja kwa kuwa ni wa kike analazimika kutumia muda wake kuteka maji badala ya kwenda shuleni.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
Hii leo jaridani tunaangazia mabadiliko ya tabianchi na athari kwa wakimbizi, ziara ya afisa wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan, Makala tunamulika haki za wenye ualbino Uganda na mashinani tunamulika nafasi ya wananawake kwenye maamuzi.1. Endapo uwekezaji wa haraka hautofanyika katika njia za kupambana na mabadiliko ya tabianchi na kujenga mnepo katika nchi za Sahael , basi kuna hatari ya kuwa na miongo ya vita vya silaha na watu kuendelea kutawanywa vinavyochochewa na ongezeko la joto duniani , uhaba wa rasilimali na kutokuwa na uhakika wa chakula limeonya leo shirika la Umoja wa Mastaifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR kwa kushirikiana na mratibu maalum wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya maendeleo.2. Wakati idadi ya wakimbizi wa ndani nchini Sudan ikizidi kuongezeka ambapo mpaka sasa wamefikia milioni 3.7 na kati yao 200,000 wakiwa wamerekodiwa mwaka huu pekee Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa Volker Türk amefunga safari mpaka nchi huko kwenda kuzungumza na wawakilishi wa wakimbizi, asasi za kiraia na serikali.3. Makala na tunakwenda nchini Uganda ambako huko ndoto ya mtoto mmoja mwenye ualbino ya kutaka kuwa rubani almanusura itumbukie nyongo, lakini harakati za serikali ya Uganda na Umoja wa Mataifa zimeirejesha ndoto hiyo, kulikoni?4. Mashinani wakati mkutano wa nchi wanachama wa Mkataba wa Mabadiliko ya Tabianchi COP27 ukiendelea nchini Misri, Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Amina J. Mohammed anasema wanawake na wasichana ni viongozi muhimu na Madhubuti wa kushughulikia changamoto za mabadiliko ya tabianchi lakini hawathaminiwi na wanapuuzwa.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
Hii leo katika Habari za UN mwenyeji wako akiwa Assumpta Massoi tunamulika ugonjwa wa kisukari barani Afrika, jawabu la nishati salama Malawi, vijana na wito wao huko Sharm el- sHeikh kwenye COP27 na ujumbe wa Balozi mwema wa IFAD Sabrina Dhowre Elba.1. Wakati dunia ikiadhimisha hii leo siku ya kisukari duniani kwa lengo la kuelimisha umma kuhusu ongezeko la mzigo wa ugonjwa huo na mikakati ya kuzuia na kudhibiti tishio lake, bara la Afrika linaonekana kuwa na changamoto kubwa ya ugonjwa huo, kwa mujibu wa takwimu za shirika la Umoja wa Mataifa la afya duniani, WHO. 2. Nchini Malawi, shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa maendeleo duniani, UNDP limewezesha serikali kutumia mito na jua kama vyanzo vya nishati na hivyo kusaidia zaidi ya kaya 3,000 kupata nishati salama na nafuu na sasa hata vipato vyao vimeongezeka halikadhalika kuepusha vifo vya wajawazito.3. Makala: Tunakwenda nchini Misri katika mji wa Sharm el-Sheikh ambako vijana kutoka kila kona ya dunia wamekusanyika kuhudhuria mkutano wa 27 wa nchi wanachama wa mkataba wa mabadiliko ya tabianchi, COP27 na wanataka kuhakikisha kwamba uwepo wao si tu unaonekana bali ujumbe waliopeleka unasikika na hatimaye uweze kufanyiwa kazi.4. Mashinani: Balozi mwema wa Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Maendeleo ya Kilimo IFAD Sabrina Dhowre Elba ametoa wito kwa mataifa tajiri duniani kuhakikisha yanasaidia wakulima wadogo vijijini.
Ule usemi wa vijana ni taifa la kesho, umeonekana kuwa kesho haitaweza kufika na ndio maana vijana kutoka kila pembe ya dunia wamefunga safari kwenda kuhudhuria mkutano wa 27 wa nchi wanachama wa mkataba wa mabadiliko ya tabianchi, COP27 unaofanyika huko nchini Misri. Vijana hao wake kwa waume wamefanya mambo mbalimbali ikiwemo kushiriki katika mikutano ya wakuu wa nchi na serikali, kufanya maandamano nje ya kumbi za mikutano na pia kuendesha mikutano wenyewe kueleza kile wanachotaka kifanyike na tena kwa kuwashirikisha ili dunia kukabiliana na changamoto zinazoletwa na mabadiliko ya tabianchi.Wanasema hawataki tena 'Bla Bla'. Tuungane na Leah Mushi aliyefuatilia na kuandaa makala ifuatayo.
Mkurugenzi wa masuala ya utafiti na matumizi ya hali ya hewa kutoka Mamlaka ya hali ya hewa nchini Tanzania TMA Dr. Ladislaus Chang'a amesema ni vyema wataalamu wa Afrika wakaongeza kasi katika kufanya tafiti na kuzichapisha katika majarida ya kimataifa ili tafiti zao ziweze kutumika katika utungaji wa será za kupambana na athari za mabadiliko ya tabianchi.Dkt. Chang'a ameyasema hayo akiwa Sharm el-Sheikh nchini Misri kunakofanyika mkutano wa 27 wa nchi wanachama wa mkataba wa mabadiliko ya tabianchi, COP27Mkurugenzi huyo ambaye katika Mkutano huo wa COP27 ni mwenyekiti wa kusimamia majadiliano ya kuhusiana na masuala ya sayansi pamoja na uangazi wa hali ya hewa amehojiwa na Joyce Shebe mwandishi wa Clouds FM ambayo ni redio washirika wetu na kusema kwa sasa matukio yanaongezeka kwa ukubwa na wingi.“Maamuzi yoyote yanayofanyika katika kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya tabianchi yanakuwa yanatokana na matokeo ya kisayansi na vile vile yanatokana na uangazi ambapo ni muhimu kwa ajili ya kutambua na kukabiliana na changamoto za hali ya hewa hususan matukio ya hali mbaya ya hewa ambayo yanaendelea kuongezeka kwa idadi na ukubwa.”Je, Afrika inafanya tafiti za kutosha?“Tafiti zinafanyika lakini hazitoshi, na ndio maana tunaendelea kusisitiza watafiti wetu na wataalamu wetu waendelee kuongeza kasi na tija katika kufanya tafiti na hususan katika kuhakikisha kwamba tunachapisha tafiti hizo katika majarida ya kimataifa ambapo ndipo yanapoweza kuzingatiwa katika kutengeneza será za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi kidunia na katika ukanda wa Afrika.”Je kuna umuhimu wa kuzingatia utafiti?“ Umuhimu ni mkubwa kwasababu maamuzi yoyote lazima yatokane na matokeo ya kisayansi ili yaweze kuwa na tija na ufanisi, mathalani kumekuwa na ongezeko la matukio ya hali mbaya ya hewa ambayo yanajumuisha mvua kubwa za muda mfupi ambazo zinaweza kuleta madhara makubwa. Kwahivyo ni vyema jamii na dunia ikajua haya matukio yapo namna gani katika sehemu mbalimbali za dunia, na wakati gani ambapo yanaongezeka zaidi na hicho kiwango kikoje, hii itasaidia tunapopanga mipango mathalani ya kujenga barabara au madaraja basi tuweze kuzingatia ukubwa na ongezeko la matukio ya hali mbaya ya hewa ikiwemo mvua kubwa, upepo mkali na kadhalika.
Karibu katika jarida la Habari za UN hii leo ambalo kwa kiasi kikubwa linamulika harakati za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi na wakati huo huo hatua za kuchukua wakati huu ambapo mabadiliko ya tabianchi yanaathiri jamii mbalimbali duniani.Takriban nusu ya vijana barani Afrika wamesema wanafikiria upya suala la kupata watoto ama la, kutokana na mabadiliko ya tabianchi, kwa mujibu wa ripoti mpya ya matokeo ya kura ya maoni iliyoendeshwa na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF bakwa kuwahoji watu 243,512 duniani kote.Miradi mbalimbali ya kukabiliana na uchafuzi wa mazingira inasaidia kuifanya dunia kuwa sehemu salama. Nchini Haiti Shirika la Benki ya plastiki linaendesha mradi wa kukusanya plastiki ikiwa ni moja ya njia za kuboresha afya ya na pia ni chanzo cha mapato kwa wakusanyaji taka. Makala: Leo tunakwenda nchini Zambia ambako kijana mmoja amegeuza taka za mabaki ya shaba kuwa mtaji wa nishati salama kwa jamii yake isiyo na kipato!Mashinani: Tunabisha hodi Sharm el-Sheikh nchini Misri kunakofanyika mkutano wa Umoja wa Mataifa wa mabadiliko ya tabianchi na nakuunganisha na Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la uhamiaji IOM António Vitorino akiwapa ujumbe maalum washiriki wa mkutano huo
Hii leo katika Habari za UN tunakuletea Habari kwa Ufupi, Mada kwa Kina na Mashinani na zote zikiwa ne mrengo wa mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi unaofanyika huko Sharm el-Sheikh nchini Misri.Habari kwa Ufupi: Ripoti ya UNICEF kuhusu mafuriko kuathiri watoto milioni 27.7 duniani kote; WMO kutaka viongozi wachukue hatua kuhusu namna ya kutumia vema maji kama suluhu ya mabadiliko ya tabianchi; Mwandishi mshirika wetu Joyce Shebe akiwa Sharm el-Sheikh anatupatia kile kilichosemwa na marais wa Tanzania, Malawi na Kenya.Mada kwa kina: Flora Nducha akiwa Kigali nchini Rwanda ametembelea mradi wa vijana Greencare Liimted wakihakikisha wanadhibiti utupaji taka kama njia ya kulinda mazingira.Mashinani: Mwanaharakati kijana Leah Namugerwa kutoka Uganda akiwa huko Sharm el-Sheikh anahoji iwapo viongozi wanataka wakumbukwe kama walikuwa madarakani bila kufanya lolote au vipi?Karibu na mwenyeji wako ni Assumpta Massoi.
Hii leo jaridani mwenyeji wako ni Assumpta Massoi akimulika tabianchi na mazingira kwa kiasi kikubwa kutokana na mkutano wa mabadiliko ya tabianchi unaofanyika Misri.Mkutano wa 27 wa nchi wanachama wa mkataba wa mabadiliko ya tabianchi, COP27 ukiingia siku ya pili hii leo huko Sharm el-Sheikh nchini Misri Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amewakumbusha viongozi wa dunia na wote wanaohudhuria mkutano huo kwamba suluhu ya changamoto ya mabadikio ya tabianchi iko mikononi mwao na wakati wa kuchukua hatua ni sasa kwani hakuna tena muda wa kusubiri.Nchini Gabon, Benki ya Dunia imerejesha matumaini kwa jamii za wavuvi ambao uvuvi ndio tegemeo kuu la kujipatia kipato wakati huu ambapo uvuvi haramu ulianza kuleta shaka, shuku na hofu miongoni mwa jamii lakini sasa hatua za pamoja za uvuvi unaojali mazingira umeleta amani.Makala: tunaelekea nchini Colombia ambako kikundi kinachoongozwa na wanawake wanasayansi cha Blue Indigo kinasaidia katika urejeshaji wa miamba ya matumbawe ili kuokoa mifumo ya ikolojia baharini iliyoharibiwa na mabadiliko ya tabianchi pamoja na shughuli za utalii.Mashinani: Jyotsna Puri, Makamu Rais wa Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Maendeleo ya Kilimo, IFAD akiongoza Idara ya Mkakati na Ufahamu na anatoa wito wa usaidizi kwa wakulima wadogo ambao ndio huathiriwa zaidi na madhara ya mabadiliko ya tabianchi.
Hii leo kwenye Jarida la Umoja wa Mataifa tunakuletea mada kwa kina ikimulika filamu ya chapa tatu iliyotengenezwa na taasisi ya Tai Tanzania kuhusu haki za binadamu yeyote yule wakiwemo watu wenye ualbino, Mtoto Njaro ana uwezo mkubwa wa ubunifu, anakutana na changamoto kwenye jamii yake lakini hakati tamaa, anasonga mbele hadi anaibuka mshindi.Kuna habari kwa ufupi kutoka kwake Flora Nducha akimulika:Kuelekea mkutano wa 27 wa nchi wanachama wa mkataba wa kimataifa wa mabadiliko ya tabianchi, COP27 huko Sharm el Sheikh nchini Misri barani Afrika yaelezwa kuwa athari za mabadiliko ya tabianchi kwa watoto katika kipindi cha kuanzia sasa mpaka mwaka 2050 yatakuwa makubwa. Shirika la afya la Umoja wa Mataifa WHO kanda ya Afrika limesema mazingira wezeshi, uwekezaji na utashi wa kisiasa vinaweza kubadilisha mwelekeo wa changamoto za afya ya uzazi na masuala ya ngono (SRHR) nchini Zimbabwe na Afrika kwa ujumla. Na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR, limesema linatiwa hofu kubwa na kitendo cha serikali ya Malaysia kuendelea kuwarudisha nchini mwao waomba hifadhi kutoka Myanmar hali inayoweka maisha yao hatarini. Na mashinani tunabisha hodi nchini Msumbiji kwa mhamasishaji wa utoaji wa chanjo dhidi ya Polio. Karibu na mwenyeji wako ni Assumpta Massoi.