POPULARITY
Akili Mnemba au AI inakuja kwa kasi kubwa sana na kubadilisha mwenendo wa walimu na wanafunzi darasani. Inaleta fursa za kipekee kama kufundisha kwa njia ya kibinafsi na upangaji wa masomo wenye ufanisi zaidi. Lakini pamoja na zana hizi, changamoto zimeibuka: kutegemea sana teknolojia hii, masuala ya kimaadili, na kupungua kwa ujuzi wa kusoma kwa kina. Walimu wanajifunza jinsi ya kuendesha mabadiliko haya, wakiwaonesha wanafunzi jinsi ya kutumia AI kama mshirika wa kufikiri badala ya njia ya mkato ya kuuliza na kunakili. Ubunifu na kufikiri kwa kina vinabaki kuwa ujuzi muhimu zaidi, ambao hakuna teknolojia inayoweza kuchukua nafasi yake. Je, walimu wana mawazo gani? Assumpta Massoi anakupeleka Paris, Ufaransa kusikia mazungumzo ya walimu wawili wakijadili mustakabali wa Akili Mnemba kwenye ufundishaji.
Umoja wa Mataifa unasema kwamba vita mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC imefanya taifa hilo kuwa pahala hatari zaidi duniani kwa watoto kuishi, kutokana na mateso ya kimwili na kisaikolojia wanayoyapitia. Kwa kutambua hilo walinda amani wanawake wa Umoja wa Mataifa kutoka Tanzania wanaohudumu kwenye ujumbe wa UN nchini humo, MONUSCO wamechukua hatua kuona watoto wanaishi kama watoto. Video ya MONUSCO ikianza na walinda amani wakijongea kwa jamii, Kapteni Noella Nyaisanga kiongozi wa kikundi hicho cha wanawake cha kikosi cha 11 cha walinda amani wa Tanzania kwenye MONUSCO, TANZBATT-11 anaeleza jinsi kikundi chao kinavyosogea kwa jamii na hasa watoto ili kutatua changamoto zinazowakabili kutokana na mapigano kati ya jeshi la serikali na waasi kwenye eneo hili la Beni, jimboni Kivu Kaskazini, mashariki mwa DRC. Anafafanua zaidi lengo lao.Lengo ni kujenga uaminifu kwa raia ambao tunawalinda. Kwa hiyo tukaamua kuandaa masomo shuleni, ambayo yataweza kuwaimarisha wao, kuwasaidia tatizo la kuwa wameathirika kisaikolojia.Zavadi Mbambu ni miongoni mwa walimu waliopatiwa mafunzo ya kusaidia watoto walioathiriwa na changamoto lukuki ikiwemo mapigano. Akisema stress, anamaanisha msongo.“Unakuwa na wanafunzi wanaokuwa na msongo wa mawazo kutokana na jambo ambalo wanaishi, na hata mauaji. Kuna wale ambao hata wameua wazazi wao , hata familia yao yote. Na kwa hao wanafunzi wanapoingia shuleni , wanakuwa kama hawako ndani, fikra zao zinakuwa mbali . Lakini kupitia mafunzo nimewaelewa , na tumejua namna gani ya kuishi nao. Na tayari mabadiliko yameanza kuonekana.”Pacifique Kyakimwa, mmoja wa wanafunzi anasimulia mkasa mmoja.“Kuna mwenzetu aliyekuwa na tatizo, yaani tukiwa ndani ya shule, alikuwa anacheka, yaani anatusumbua hadi hatumwelewi mwalimu. Lakini tangu wameanza kufundisha hili somo, wameanza kuelewa . Ameanza kuwa na akili inayotumika vizuri. Mafunzo haya yamefika wakati tunahitaji , na imetusaidia sana.”
Hii leo jaridani tunaangazia machafuko nchini Lebanon, na kesho ikiwa ni Siku ya walimu Dunia tunakupeleka Paris, Ufaranza kutsikia toka UNESCO. Makala tunafuatili ajali ya boti iliyozama katika ziwa Kivu nchini DRC na mashinani tunakupeleka Burundi, kulikoni? Mashirikika ya kibinadamu ya Umoja wa Mataifa leo yameonya kwamba hali ya kibinadamu inazidi kuwa mbaya nchini Lebanon wakati mashambulizi ya anga ya Israel yakiendelea kushika kasi na kuwafungisha virago maelfu ya watu, wengi wakikimbia nchi jirani ya Syria ambako nako si shwari.Washiriki wa hafla ya kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Walimu ililofanyika leo Oktoba 4 katika makao makuu ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) jijini Paris, Ufaransa wamesisitiza wito wa kuthamini mawazo ya walimu katika kuboresha elimu ya ulimwengu.Makala inakupeleka huko Goma, jimboni Kivu Kaskazini, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC ambako janga la kuzama kwa boti ya abiria na mizigo liligubika eneo hilo Alhamisi asubuhi za huko.Na mashinani kupitia video ya WHO Afrika, tunamsikia Dkt. Dieudonné Niyongere akizungumza kuhusu msaada muhimu wa washirika katika kuimarisha juhudi za kukabiliana na mlipuko wa Mpox nchini Burundi.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
Washiriki wa hafla ya kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Walimu ililofanyika leo Oktoba 4 katika makao makuu ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) jijini Paris, Ufaransa wamesisitiza wito wa kuthamini mawazo ya walimu katika kuboresha elimu ya ulimwengu. Kama tunavyofahamu, siku yenyewe ya Kimataifa ya Walimu ni kesho Oktoba 5 kama ilivyo ada ya kila mwaka lakini katika makao makuu ya UNESCO hapa Paris Ufaransa, maadhimisho yamefanyika leo kuelekea mkesha wa siku hii muhimu kwa elimu ya ulimwengu.Miongoni mwa waliozungumza ni Mkurugenzi Msaidizi Mkuu wa Elimu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Bi Stefania Giannini, ambaye ameitumia nafasi hii kusisitiza kauli mbiu ya mwaka huu ambayo ni 'Kutambua sauti za walimu.'Anasema, “walimu ni uti wa mgongo wa mifumo ya elimu na mawakala wakuu wa mabadiliko ya kubuni sera za elimu na kufanikisha SDGs. Tunapaswa kuthamini sauti za walimu; hili ndilo lengo kuu la Siku ya Kimataifa ya Walimu mwaka huu.”Kulingana na takwimu zilizotolewa na UNESCO, dunia inahitaji walimu wa ziada milioni 44 ili kufikia elimu ya msingi na sekondari kwa wote ifikapo mwaka 2030. Ingawa mahitaji ya walimu ni makubwa zaidi katika baadhi ya maeneo, uhaba wa walimu ni wa kimataifa.Walimu wanajiondoa kwenye taaluma hii kwa kiwango mara mbili zaidi ya miaka mitano iliyopita, hasa katika elimu ya sekondari. Hii inatokana na hali zao za kazi, zikiwemo mishahara midogo, mzigo mkubwa wa kazi, na ukosefu wa ushiriki katika maamuzi yanayohusu elimu. Akiiangizia changamoto hii, Mkurugenzi wa Kimataifa wa Elimu na Maendeleo ya Vijana katika Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) Bi. Pia Britto, aliyejiunga katika hafla ya leo kwa njia ya video akiwa Pakistani amesema,"Leo nilikuwa na fursa nzuri ya kuzungumza na walimu wengi, ikiwa ni pamoja na mwalimu Tahseen Bashir hapa Islamabad, ambaye amenieleza baadhi ya changamoto wanazokabiliana nazo ikiwa ni pamoja na kufundisha madarasa mengi, uhaba wa vifaa vya kujifunzia, na changamoto za kutoweza kufundisha namna wanavyodhamiria. Lakini pia amenieleza jinsi alivyofurahi kuona wanafunzi wake wakifaulu. Wakati sauti ya mwalimu inaposikilizwa na wakati sauti za walimu zinapopewa kipaumbele, wanajiona kama wadau katika kuboresha elimu kwa wakati wote, na hatua hizo zinahitajika ili kuleta mabadiliko chanya hasa katika hali ngumu zaidi."Siku hii ya kimataifa ya walimu ni mahususi kwa ajili ya kutambua na kusherehekea mchango muhimu wa walimu ulimwenguni kote katika kutoa elimu bora na kujenga mustakabali wa jamii. Pia, ni fursa ya kuangazia changamoto wanazokabiliana nazo walimu.Kutoka hapa Paris Ufaransa, mimi ni Cecily Kariuki..
Jumamosi ulimwengu unaadhimisha Siku ya Walimu Duniani, tarehe iliyotengwa na Umoja wa Mataifa kwa ajili ya kuwaenzi walimu kote duniani, na kuangazia changamoto wanazopitia na mafaniko wanayojivunia.
Sintofahamu Kenya baada ya vyama viwili vya walimu kutofautiana kuhusu mgomo
VOA EXPRESS
Jinsi serikali inashughulikia mgomo wa walimu wa JSS kunaonesha serikali isiyojali. Mbona tunachezea elimu ya watoto wetu? Mbona suala hili halifanywi kipaumbele?
Sasisoma , 22 Desember 2023
Walimu wa watoto katika ufundishaji
Walimu wa watoto katika ufundishaji
Baadhi ya walimu kutoka mataifa ya Afrika mashariki watoa maoni yao kuhusu siku hii, wakati kauli mbiu ya mwaka huu ikiwa ni 'Uimarishwaji wa elimu unaanzia kwa walimu.'
Mkutano wa Ngazi ya juu wa Umoja wa Mataifa kuhusu marekebisho ya mfumo wa elimu duniani ukianza leo katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa, Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Watoto UNICEF limetoa taarifa inayoeleza idadi ya Watoto wasiojua kusoma imeongezeka ulimwenguni ikilinganishwa na miaka miwili iliyopita.Tupate taarifa zaidi kutoka kwa Assumpta Massoi Jijini New York, Marekani katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa, UNICEF wameweka mfano wa darasa kando mwa bustani ya mawaridi, darasa hili linaitwa “Darasa la Mgogoro wa kujifunza”, lengo ni kufikisha ujumbe wa changamoto ya elimu duniani hivi sasa. Katika kuhakikisha wanafikisha ujumbe wa changamoto ya elimu UNICEF wameweka mfano wa darasa kando mwa bustani ya mawaridi katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa, darasa hili linaitwa “Darasa la Mgogoro wa kujifunza”. Darasa hili limewekwa ubao na madawati lakini theluthi moja ya madawati hayo yametengenezwa kwa mbao na kuwekwa mabegi ya mgongoni ikiwakilisha theluthi moja ya Watoto wenye umri wa miaka 10 wanaokadiriwa kuwa na uwezo wa kusoma na kuelewa ulimwenguni. Kabla ya Janga la COVID-19 miaka miwili iliyopita watoto waliojua kusoma wenye umri wa miaka 10 ulimwenguni walikuwa nusu lakini sasa UNICEF linasema idadi yao ni theluthi moja hii ikiwa sawa na mtoto mmoja kati ya watatu ndio mwenye uwezo wa kusoma na kuelewa hadithi fupi. Katika taarifa yake iliyotolewa jijini New York Marekani Mkurugenzi Mtendaji wa UNICEF Catherine Russell ameeleza sababu za kuporomoka kwa uwezo wa Watoto kujua kusoma ni shule zilifungwa muda mrefu kipindi cha janga la CORONA na kuwaacha mamilioni ya Watoto bila ujuzi wa msingi wa kusoma na kuhesabu, elimu haikuwa bora na kufichua mapungufu mengi ndio maana idadi ya Watoto wasiojua kusoma na kuhesabu imeongezeka kwa kiwango cha kushtusha na kuonya hii ni hatari kwa Maisha ya baadae ya watu wote duniani. Taarifa hiyo imemnukuu Bi Russelle akisema “Mifumo yetu ya elimu ndio mwelekeo wa maisha yetu ya baadae. Tunahitaji kubadili mwelekeo wa sasa au itatubidi kukabiliana na matokeo ya kushindwa kuelimisha kizazi chote. Viwango vya chini vya kujifunza vya leo inamaanisha fursa ndogo kesho.” Wakati viongozi wakikutana katika Mkutano wa marekebisho ya mfumo wa elimu UNICEF imetoa wito kwa serikali kujitolea kuwafikisha Watoto elimu bora kwa kuongeza uwekezaji kwenye elimu, kuweka mazingira salama ya kujifunzia, kuandikisha Watoto wengi shule na kuboresha maslahi ya walimu. Mkuu huyo wa UNICEF amesema hali ya sasa ni mbaya “Shule hazina rasilimali, walimu wanalipwa ujira mdogo, walimu wengine wasio na sifa wanaajiriwa, msongamano wa wanafunzi madarasani, mitaala ya kizamani na vyote hivi vinasababisha Watoto kushindwa kufikia uwezo wa juu wa ufaulu.”
Serikali ya Uganda imesema kwamba sasa ipo tayari kuzungumza na waalimu wa sanaa wanaolalamikia kuongezwa kwa mishahara ya wenzao wa sayansi kwa asilimia 300, lakini ni lazima warejee kazini kwanza.
Wanaharakati wa kutetea haki za vijana wanaitaka tume ya walimu Kenya kutilia maanani kwamba vijana wengi waliohitimu vyuo vikuu hawana kazi wakati ikanza mchakato wa kuwaajiri walimu takriban 15,000
Kwa Undani ni matangazo ya dakika 25 yanayochambua habari kwa undani zaidi na kumpa msikilizaji maelezo ya kina kuliko ilivyo kawaida kuhusu tukio au swala lililojitokeza katika habari.
Kwa Undani ni matangazo ya dakika 25 yanayochambua habari kwa undani zaidi na kumpa msikilizaji maelezo ya kina kuliko ilivyo kawaida kuhusu tukio au swala lililojitokeza katika habari.
Wafanyakazi hao wanasema kwamba dhamani ya fedha imeshuka kiasi cha mishahara yao kutoweza kumudu gharama ya maisha. Hayo yamejiri licha ya ahadi ya mwezi uliopita kutoka kwa serikali kwamba mishahara ingeongezwa maradufu.
Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limesema walimu nchini Honduras wanaathiriwa kwa kiasi kikubwa na ghasia za magenge ya wahalifu na sasa walimu wanatambuliwa kuwa moja ya makundi yenye uwezekano mkubwa wa kulazimika kuyakimbia makazi yao. Mwanzoni mwa kila mwaka mpya wa shule, wakati maeneo mengine duniani walimu na wanafunzi hufurahia shule funguliwa, walimu wa nchini Honduras taifa dogo lililoko Amerika ya Kati, hali huwa ni tofauti kwani huwa na hofu wakikaa kusubiri maagizo tena si kutoka serikalini bali katika magenge ya wahalifu ya namna ya kuendesha mafunzo kama anavyoeleza mwalimu Horacio Montes, “wavulana huja kila tunapoanza mwaka wa shule, na wanawasiliana nami ili kunijulisha miongozo ambayo watatupa kuhusu uendeshaji wa shule katika mwaka.” Maisha ya walimu nayo ni magumu kwani wengine hulazimika kutoa hongo ili waende kazini, huku wakitafuta pesa kila mara wanapovuka mipaka isiyoonekana inayotenganisha maeneo ya magenge kama inavyodhibitishwa na Mwalimu mkuu Miguel Lopez wa shule moja huko Honduras, “Kuna wakati tunaweka maisha yetu rehani, na miili yetu katika hatari ili kuwalinda wavulana na mabinti zetu. Tunaweza kusema kwamba ‘tunabeba mzigo', lakini hatuna ulinzi sisi wenyewe.” Walimu wa kike wako katika hatari zaidi, kwani wanaweza kulengwa kwa unyanyasaji wa kijinsia na kushambuliwa kama anavyoeleza Alba Flores Mwalimu Mkuu msaidia wa shule ya awali, “Tunatafuta njia za ulinzi sisi wenyewe, kwa ajili ya wenzetu, wanafunzi na, wakati mwingine, kwa wazazi. Daima tutakuwa marafiki zao watoto, tunawapenda, na tunafanya kazi kwa ajili yao” Uchunguzi uliofanyika mwaka 2016 wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuwahudumia wakimbizi UNHCR, Shirika linalowakilisha walimu wa shule wa Honduras Comité Docent , pamoja na Shirika lisilo la kiserikali la Save the Children, ulibainisha walimu kuwa miongoni mwa makundi nchini Honduras ambayo huathirika zaidi na kulazimishwa kuyakimbia makazi yao. Walimu wa Honduras wanajikuta kwenye mstari wa mbele wa wakimbizi wa ndani ambapo zaidi ya watu 247,000 wameyakimbia makazi yao. Wadau wa elimu wamekuwa yakifanya kazi pamoja tangu mwaka 2016 kutafuta suluhu za matatizo yaliyokita mizizi ya walimu ili kuwaweka katika kazi zao na jamii zao nyumbani, lakini pale baadhi ya walimu wanapokuwa katika hatari zaidi hupelekwa UNHCR, ambayo inafanya kazi ya kuwahamishia kwenye usalama zaidi ikiwa ni ndani au nje ya Honduras.
Programu ya kufundisha masuala ya haki za binadamu katika shule za watoto wakimbizi wa kipalestina katika ukanda wa Gaza, imesaidia siyo tu wanafunzi kutambua haki zao bali pia walimu ambao wanawafundisha na hivyo kusaidia katika kusongesha amani kwenye eneo ambalo hugubikwa na migogoro. Taarifa iliyoandaliwa na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi wa kipalestina, UNRWA inasomwa hapa studio na Happiness Pallangyo wa Radio washirika Radio Uhai FM ya Tabora Tanzania. Fatma Issa Al Hams mwalimu wa shule ya Rafah, ambayo ni shule ya maandalizi kwa wasichana, anafundisha masomo ya kijamii. Amekuwa akifanya kazi na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi wa kipalestina, UNRWA kwa miaka 33 sasa. Anasema, “mwaka 2017 nilipata mafunzo ufundishaji wa haki za binadamu, mizozo na stahmala. Sasa ni mratibu wa Bunge la shule na kiongozi wa kamati ya shule kuhusu haki za binadamu, mizozo na stahmala.” Programu hii ikiungwa mkono na Marekani imekuwa ikifundishwa na UNRWA kwa miaka 20 sasa ambapo Mwalimu Fatma anasema, “kuwafundisha watoto kuhusu haki za binadamu ni muhimu kwa sababu wanapotambua haki zao wanaheshimu pia haki na wajibu wa watu wengine. Elimu ya haki za binadamu kwa watoto inaimarisha maadili yao ya stahmala, haki za watoto na pia kujiamini.” Na tayari mwalimu Fatma anaona mabadiliko chanya akisema, “imeimarisha kujiamini na pia kujiheshimu wao na kuheshimu wengine. Wanashiriki kikamilifu kwenye mafunzo kwa sababu wanafunzi ndio kito vu cha mchakato mzima wa masomo. Na kwangu mimi kama mwalimu, imenifungua macho kwa sababu kuna mbinu za ufundishaji ambazo awali sikuzitambua kabisa licha ya uzoefu wangu wa muda mrefu wa kufundisha.” Tarehe 19 mwezi Desemba mwaka 2011, Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa lilipitisha azimio kuhusu elimu na mafunzo kuhusu haki za binadamu ambalo linasisitiza umuhimu wa kila mtu kuwa na haki za kufahamu, kutafuta na kupata tarifa kuhusu haki zao za binadamu na haki za aina mbalimbali za uhuru.
Walimu wa shule za umma pamoja na walimu wakuu wame andamana kote jimboni NSW, dhidi ya mishahara midogo pamoja na kazi nyingi.
Shule kadhaa zimeripotiwa kuwatoza wanafunzi wote faini kufuatia visa vya kuteketezwa shule. Mbona kuwabebesha mzigo wanafunzi wote na hali makosa yamefanywa na wachache? Hatua kama hizo zinaashiria kwamba wakuu wa shule bila shaka hawawasikizi wanafunzi!
Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni, UNESCO na wadau wake linasema ufufuaji wa elimu unaofanikiwa unategemea kuongezeka kwa uwekezaji katika ustawi, mafunzo, ukuzaji wa kitaalam na hali ya ufanyaji kazi ya waalimu milioni 71 ulimwenguni ili kurejea katika hali nzuri baada ya kupotea kwa muda wa masomo kutokana na Covid-19. Taarifa ya Lucy Igogo ina maelezo zaidi. Huo ndio ujumbe muhimu wa Siku ya Walimu Duniani, siku inayoadhimishwa kila tarehe 5 mwezi Oktoba, mwaka huu ikiwa na kauli mbiu "Walimu katika kiini cha kupona kwa elimu." Siku hii inatoa wito kwa serikali na jamii ya kimataifa kuzingatia walimu na changamoto zinazoikabili taaluma ya walimu. Katika taarifa ya pamoja, wakuu wa mashirika waandaaji wa maadhimisho ya siku hii ya Walimu Duniani, Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO, Augrey Azoulay, Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la Umoja wa Mataufa la kuhudumia watoto, UNICEF, Henrietha Fore, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la kimataifa la kazi ILO, Guy Ryder na Katibu Mkuu wa shirika la Education International Bwana David Edwards wamesema, “leo tunasherehekea kujitolea kwa kipekee na ujasiri wa walimu wote, uwezo wao wa kubadilika na ubunifu katika hali ngumu sana na isiyo na uhakika. Ndio wahusika wakuu wa juhudi za kufufua elimu ulimwenguni na ni muhimu katika kuharakisha maendeleo kuelekea elimu bora iliyo jumuishi na yenye usawa kwa kila mwanafunzi, katika kila hali.” Viongozi hao wameongeza wakisema, “sasa ni wakati wa kutambua jukumu la kipekee la walimu na kuwawezesha na mafunzo, ukuzaji wa taaluma, msaada na mazingira ya kazi wanayohitaji kupeleka vipaji au talanta zao. Ufufuaji wa elimu utafanikiwa ikiwa utafanywa kwa mkono na walimu, kuwapa sauti na nafasi ya kushiriki katika kufanya uamuzi.” Uvurugwaji elimu uliosababishwa na Covid-19 umeonesha jukumu muhimu la walimu katika kudumisha mwendelezo wa ujifunzaji. Walimu wamekuwa kiini cha kielimu, kuanzia katika kutumia teknolojia kwa ubunifu hadi kutoa msaada wa kijamii na kihisia kwa wanafunzi wao na kufikia wale walio katika hatari zaidi ya kurudi nyuma pia Covid-19 imeziweka wazi changamoto kubwa zinazoikabili taaluma ya ualimu, pamoja na ukosefu wa fursa za maendeleo ya kazi katika ufundishaji mtandaoni na ujifunzaji kwa njia ya masafa, kuongezeka kwa mzigo wa kazi unaohusishwa na madarasa ya zamu mbili. Kwa mujibu wa utafiti wa UNESCO, asilimia 71 ya nchi zimewapa kipaumbele walimu katika chanjo, lakini ni nchi 19 tu ndizo zilizowajumuisha walimu katika chanjo ya kwanza, wakati nchi 59 hazijawapa kipaumbele walimu katika mipango yao ya chanjo.
Njia yakuwa mwalimu nchini Australia kama unavyeti kutoka ng'ambo, mara nyingi huwa ngumu na inawafungia njia maelfu yawalimu watarajiwa kuingia katika mfumo.
This week we are talking about Joycon Drifting, Monster Hunter Generations, Trips to Vegas, and much more This has been a Knowitsgood production and keep it cheesy
This week we have Eric of Walimu.me in house to talk about the latest reveals at this years Games Developers Conference, the new indies to grace the Nintendo Switch, Pan sounds and much more This has been a Knowitsgood production and keep it cheesy
Datooga Biblia (Non-umetiwa chumvi) - Datooga Bible (Non-dramatized)
Walimu wa Sheria swali maswali - Teachers of the Law question questions.
Walimu wa Sheria swali maswali - Teachers of the Law question questions.
Walimu wa Sheria swali maswali - Teachers of the Law question questions.
Walimu wa Sheria swali maswali - Teachers of the Law question questions.
Walimu wa Sheria swali maswali - Teachers of the Law question questions.
Walimu wa Sheria swali maswali - Teachers of the Law question questions.
Kiswahili Biblia (non-umetiwa chumvi) Habari Njema - Kiswahili Habari Njema Bible (non-dramatized)
Walimu wa Sheria swali maswali - Teachers of the Law question questions.
Walimu wa Sheria swali maswali - Teachers of the Law question questions.
Walimu wa Sheria swali maswali - Teachers of the Law question questions.
Walimu wa Sheria swali maswali - Teachers of the Law question questions.