Sikiliza MAELEZO PODCASTS (Podcasts za Kiswahili kutoka Idara ya Habari MAELEZO, Tanzania) kupata taarifa na matukio mbalimbali nchini Tanzania. Idara ya Habari (MAELEZO) ipo chini ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, ikiwa na jukumu la kutoa taarifa kuhusu utekelezaji wa Sera, Mipango na Miradi ya Maendeleo vinavyotekelezwa na Serikali kwa wananchi, kusimamia vyombo vya habari hasa magazeti na machapisho na kuishauri Serikali juu ya sera na sheria za habari.
Tanzania Information Services Department, Habari-MAELEZO
Watanzania kwa ujumla tuanze kupanda miche ya kisasa ya Michikichi kutokana na nchi kutumia gharama kubwa kuagiza mafuta ya mawese yatokanayo na zao hilo kutoka mataifa mengine duniani.
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii inatekeleza mradi wa kukuza utalii kusini mwa Tanzania (REGROW). Mradi wa REGROW ni mkopo kutoka Benki ya Dunia na lengo kuu la mradi huu ni kuboresha maeneo yenye vivutio vya utalii katika ukanda wa kusini mwa Tanzania.Hii ni pamoja na kuboresha usimamizi wa maliasili na kuimarisha fursa za kiuchumi kwa wananchi wanaozunguka hifadhi ili kuongeza mchango wa sekta ya utalii katika maendeleo ya kiuchumi nchini . Serikali inadhamiria mradi huu uwe wa mfano katika kuleta maendeleo kwa kufungua fursa za kiuchumi kwa jamii na taifa kwa ujumla.
Mkutano wa Mkurugenzi wa Idara ya Habari - MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali, Ndg. Gerson Msigwa na Waandishi wa Habari mkoani Singida, Septemba 26, 2021 #Kaziiendelee
Maelezo ya Msemaji Mkuu wa Serikali na Mkurugenzi wa Idara ya Habari MAELEZO juu ya Upotoshaji unaoendelea mitandaoni kuhusu Chanjo ya UVIKO-19
Wimbo huu ni zawadi kwa Hayati Dkt. John Pombe Magufuli, Rais wa Awamu ya Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. JPM alikua baba wa wanyonge, mtetezi wa masikini na mzalendo wa kweli. JPM anaishi na ataishi ndani yetu milele.
Uzalendo ni hali ya mtu kuipenda, kuithamini na kujitoa kwa ajili ya nchi yake. Mzalendo wa kweli daima anaweka maslahi ya nchi mbele na ya kwake binafsi nyuma. Kwa maana hiyo hapo juu, mzalendo ni mtu yeyote mzawa na mwenye kuipenda na kujitoa mhanga na saa nyingine ikibidi kufa kwa ajili ya nchi yake. Uzalendo unabeba dhana nyingi sana ikianzia asili, utamaduni, lugha, siasa, historia, nk. Dhana zote zikifungwa kwenye dhana kuu ya utaifa
Watanzania kwa Ujumla Tuanze Kupanda Miche ya Kisasa ya Michikichi Kutokana na Nchi Kutumia Gharama Kubwa Kuagiza Mafuta ya Mawese Yatokanayo na Zao Hilo Kutoka Mataifa Mengine - Kassim Majaliwa Majaliwa, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
From the high snowy peaks of Mount Kilimanjaro to the palm tree fringed Indian Ocean islands of Zanzibar and Pemba, Tanzania simply has it all. Whether it’s the mega herds of Selous, Ruaha and Katavi; the habituated chimpanzees of Mahale and Gombe Stream; the wildebeest migration of the Serengeti; the giant tuskers of Tarangire; or the whale sharks swimming around Mafia Island, the variety and quality of wildlife safari experiences in Tanzania is unrivalled. Tanzania is unquestionably a remarkable and an incomparable African travel destination.
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni Muungano wa Nchi huru mbili zilizojulikana kama Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya watu wa Zanzibar. Nchi hizi mbili ziliingia kwenye Mkataba wa Muungano mnamo tarehe 22 Aprili, 1964 na kuwa Dola ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuanzia tarehe 26 Aprili, 1964. Muungano huu ni wa serikali mbili, yaani Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (SMT) inayoshughulikia mambo yote ya Muungano kama yalivyoainishwa katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya mwaka 1977 na yasiyo ya Muungano kwa upande wa Tanzania Bara na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) inayoshughulikia mambo yasiyo ya Muungano kwa upande wa Tanzania Zanzibar.Mkataba wa Muungano ulitiwa sahihi na aliyekuwa Rais wa Tanganyika, Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na aliyekuwa Rais wa Zanzibar, Hayati Sheikh Abeid Amani Karume tarehe 22 Aprili, 1964 huko Zanzibar. Mkataba huo ulithibitishwa tarehe 26 Aprili, 1964 na mnamo tarehe 27 Aprili, 1964, viongozi wa nchi zote mbili walikutana katika ukumbi wa Karimjee, Dar es Salaam na kubadilishana hati za Muungano. Sheria za Muungano zilitoa tamko la Jamhuri ya Muungano kwamba:“Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar zitalazimika, baada ya kuungana na siku zote baada ya kuungana, kuunganishwa kuwa Dola ya Jamhuri kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar’ (Ibara ya 4 Sheria za Muungano)Jina hili la “Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar” lilibadilishwa baadae na kuwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kupitia sheria ya Jamhuri ya Muungano, Sheria namba 61 ya mwaka 1964.
Mradi wa Maji wa Ziwa Victoria kutoka Solwa Mkoani Shinyanga hadi Itumba Tabora umegharimu Shilingi Bilioni 605 na unawanufaisha wakazi milioni moja na laki mbili katika vijiji 102 vya Mikoa ya Shinyanga na Tabora na miji ya Nzega, Igunga, Isikizya na mji wa Tabora.Mradi huu umejengwa na miundombinu mipana ikiwemo bomba kubwa kutoka Solwa kwenda Itumba Tabora lenye urefu wa Kilomita 280 lna enye kipenyo cha Sq/m 1000 sawa na Mita 1 linalosukuma maji lita milioni 54 kwa siku.Mradi mzima katika Mkoa wa Tabora una jumla ya matanki 29 huku kubwa zaidi likiwa nje kidogo ya Mji wa Tabora katika eneo la Itumba likiwa na uwezo wa ku- hifadhi maji lita milioni 9.Hii inamaanisha watakaofikiwa na mradi watanufaika kwa asilimia mia moja.