Podcasts about uingereza

  • 23PODCASTS
  • 158EPISODES
  • 19mAVG DURATION
  • 1MONTHLY NEW EPISODE
  • Jun 20, 2025LATEST

POPULARITY

20172018201920202021202220232024


Best podcasts about uingereza

Latest podcast episodes about uingereza

SBS Swahili - SBS Swahili
Taarifa ya Habari 19 Juni 2025

SBS Swahili - SBS Swahili

Play Episode Listen Later Jun 20, 2025 5:30


Ulaya imechukua nafasi yaku fanya mashauriano na Iran, mawaziri wa mambo ya nje wa Uingereza, Ujerumain na Ufaransa wanazungumza na mshirika wao kutoka Iran.

Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii
Kabila aondolewa kinga ya kushtakiwa na Seneti ya DRC, Lissu arejeshwa mahakamani Tanzania

Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii

Play Episode Listen Later May 29, 2025 20:03


Miongoni mwa taarifa utakazoziskia ni pamoja na; Bunge la seneti nchini DRC lapiga kura ya kumuondolea kinga rais mtaafu Joseph kabila, Wanaharakati wa kutetea haki za binadamu na Mawakili mashuhuri kutoka nchini Kenya, wafukuzwa nchini Tanzania. Kwingineko, Mamlaka nchini Libya zagundua miili 58 iliohifadhiwa kwa muda katika chumba cha kuhifadhi maiti na Waziri mkuu wa Israeli, Benjamin Netanyahu awatuhumu viongozi wa Ufaransa, Uingereza na Canada kwa kuwapa nguvu kundi la Hamas.

Jukwaa la Michezo
CAF: Simba kuchuana na RS Berkane leo kwenye fainali ya Kombe la Shirikisho

Jukwaa la Michezo

Play Episode Listen Later May 17, 2025 23:58


Leo tumekuandalia mengi ikiwemo fainali ya kombe la shirikisho la CAF kati ya Simba na RS Berkane, fainali za Afcon U20, Congo Brazaville yarejeshwa katika soka ya kimataifa, droo kamili ya michuano ya Chan 2024, mkondo wa Nile katika ligi ya basketboli ya Afrika, tuzo za wanasoka bora ligi kuu ya Uingereza.

SBS Swahili - SBS Swahili
Taarifa ya Habari 11 Aprili 2025

SBS Swahili - SBS Swahili

Play Episode Listen Later Apr 11, 2025 11:25


Waziri Mkuu amekabiliana na maswali kuhusu uwezekano wa mkataba wa manowari ya Australia na Marekani pamoja na Uingereza, kufuatia utoaji wa ushuru wa Marekani ambao ume tikisa dunia nzima.

australia habari aprili marekani uingereza waziri mkuu
SBS Swahili - SBS Swahili
Taarifa ya Habari 28 Februari 2025

SBS Swahili - SBS Swahili

Play Episode Listen Later Feb 28, 2025 16:26


Wanasiasa wakuu wa Australia wamesema hatma ya mkataba wenye thamana yama bilioni ya dola na Marekani ume hakikishwa, baada ya Rais Donald Trump kuonekana nikama amesahau jina la mkataba huo wa nchi tatu zinazo jumuisha Uingereza.

Habari za UN
UNICEF Burundi: Mradi wa UNICEF wa kuunganisha taarifa na kusajili watoto wanufaisha jamii

Habari za UN

Play Episode Listen Later Jan 8, 2025 3:29


Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF linaisaidia serikali ya Burundi katika kuunganisha taarifa za watu katika mifumo inayosomana ya kiraia na ya huduma ya afya. Euphrasie Butoyi mama akiwa amembeba mtoto wake mchanga, amekuja katika ofisi za msajili za eneo la Busoni jimboni Kirundo kaskazini mwa Burundi, anasema,“kabla ilikuwa vigumu kumwandikisha mtoto. Umbali ulikuwa mrefu. Tulikuwa tunalazimika kulipia tiketi ya safari kwa ajili yetu na mashahidi. Tulikuwa tunaweza kwenda kule hata mara mbili bila kupata cheti cha kuzaliwa.” Damien Ndayisenga ni msajili wa kijamii anathibitisha hilo kwa kusema, “ukweli kabla ya hatua hii, ofisi ya usajili wa raia ya Busoni ilikuwa imezidiwa na idadi kubwa ya watu wanaokuja kusajili watoto wao ili kupata vyeti vya kuzaliwa. Lakini huduma hii imerahisisha.” Hakika mradi huu umekuwa mkombozi kama anavyoendelea kueleza Euphrasie Butoyi. Anaposema faranga elfu 10 fedha ya Burundi hiyo ni takribani dola nne za kimarekani, “leo tofauti ni kuwa kituo cha afya kiko karibu na sisi kwa hiyo si lazima tena kulipa nauli kwa ajili ya mashahidi. Sasa ni rahisi kwetu kusajili watoto wetu baada tu ya kuzaliwa. Hata mume wangu hajui kama niko naandikisha hapa wakati huu. Anadhani nitapata tu chanjo ya mtoto lakini nitakapomuonesha cheti cha kuzaliwa cha mtoto wetu, atafurahi sana. Hatalazimika tena kwenye ofisi za serikali na kulipa faranga za Burundi 10,000 kwa ajili ya usafiri. Ni faida kwetu.” UNICEF pia inasaidia katika kuandikisha watoto ambao walichelewa kusajiliwa katika umri mdogo na hiyo imesaidia sana watoto walio katika mazingira magumu kupata huduma za msingi za kijamii ambazo hapo awali walikuwa nazikosa kwa kuwa hawana utambulisho wowote unaotambuliwa kiserikali. Katika mkoa wa Bugabira jimboni Kirundo kaskazini mwa Burundi, tunakutana na Jean Baptiste Mutaniyonka baba wa mtoto mwanafunzi Karerwa Olivier anaeleza changamoto walizokuwa wanakumbana nazo hapo awali kabla ya huduma ya usajili kuletwa karibu. “Mara ya kwanza nilipoenda kwenye ofisi za mkoa kusajili ilikuwa imefungwa kwa sababu ya sikukuu. Mara ya pili, mashahidi walitutaka kuwapatia faranga za Burundi elfu kumi nila mmoja. Sikuwa na fedha hiyo kwa hiyo ilibidi tuahirishe hiyo miadi ili tutafute pesa.” Mzazi huyu ili kuonesha namna cheti cha kuzaliwa kilivyo na umuhimu mkubwa katika maisha ya mtoto nchini Burundi anasema, “bila cheti cha kuzaliwa mtoto hana haki ya kupata kupata huduma ya bure katika hospitali. Tulikuwa tunaondoka bila bila kupata matibabu. Na katika hali kama hiyo tuligeukia katika tiba za asili au katika maduka ya dawa. Ilikuwa hivyo hivyo katika shule. Watoto wangu walikuwa wanarejeshwa nyumbani kwa kukosa cheti cha kuzaliwa.” Huyo ni Olivier Karerwa mwenyewe, mtoto wa Jean Mutaniyonka. Olivier amesajiliwa kupitia mradi huu wa UNICEF na anasema anataka kuwa mwalimu atakapohitimu masomo yake. Anne Rwasa ni bibi anazungumzia ilivyo rahisi sasa kumuhudumia mjukuu wake akisema, lakini leo mtoto  awe na homa au kuumwa tumbo tunakimbia katika kituo cha afya ambako anapata huduma ya bure ya afya.” Mradi huu wa UNICEF Burundi wa kuunganisha taarifa za watoto za serikali ili ziweze kusomeka pia katika taasisi nyingine kama vile vituo vya afya umepata  pia usaidizi kutoka kwa kamati ya UNICEF ya Uingereza.  

Jukwaa la Michezo
CAF: Niger, Sudan na Zambia zafuzu mashindano ya soka ya CHAN 2024

Jukwaa la Michezo

Play Episode Listen Later Dec 28, 2024 23:53


Ikiwa Jumamosi ya mwisho ya mwaka 2024, tunakuuliza ni tukio gani au mashindano gani ya kispoti yalikufurahisha zaidi mwaka huu? Pamoja na hayo; tumeangazia kifo cha mchezaji nguli wa voliboli nchini Kenya Janet Wanja, Uganda yaibuka mabingwa wa CECAFA michuano ya kufuzu AFCON U17, raundi ya mwisho ya kufuzu michuano ya CHAN 2024, uchambuzi wa raundi ya 18 ya mechi za Ligi Kuu ya Soka nchini Uingereza. 

SBS Swahili - SBS Swahili
Taarifa ya Habari 17 Disemba 2024

SBS Swahili - SBS Swahili

Play Episode Listen Later Dec 17, 2024 20:29


Mawaziri wa kigeni na ulinzi wa Uingereza na Australia wamefanya mkutano wao wa kila mwaka ((AUKMIN)) mjini London ambako amekubali kuimarisha zaidi ushirikiano kwa ulinzi, biashara na sera yakigeni.

australia habari uingereza disemba
Habari RFI-Ki
Baraza la usalama limejadili mapendekezo ya Uingereza kuhusu mzozo wa Sudan

Habari RFI-Ki

Play Episode Listen Later Nov 14, 2024 9:54


Mapendekezo ya taifa la Uingereza  yanataka  vita kusitishwa nchini Sudan na kuruhusiwa  misaada ya kibinadamu kuwafikia waathiriwa.

Habari RFI-Ki
Baraza la usalama limejadili mapendekezo ya Uingereza kuhusu mzozo wa Sudan

Habari RFI-Ki

Play Episode Listen Later Nov 14, 2024 9:54


Mapendekezo ya taifa la Uingereza  yanataka  vita kusitishwa nchini Sudan na kuruhusiwa  misaada ya kibinadamu kuwafikia waathiriwa.

Habari za UN
Kiswahili imevuka mipaka, jiunge na wanafunzi katika vyuo mbalimbali kote ulimwenguni ujifunze Kiswahili - Nick

Habari za UN

Play Episode Listen Later Nov 11, 2024 3:07


Kongamano la kimataifa ka Kiswahilii limekunja jamvi mwishoni mwa wiki huko Havana Cuba, ambako shuhuda wetu Flora Nducha amezungumza na watu mbalimbali akiwemo mchechemuzi wa Kiswahili hususan kwenye mitandao ya kijamii Nick Reynold ali maarufu Bongo Zozo, ambaye ni raia wa Uingereza. Ungana nao katika makala hii.

Habari za UN
11 NOVEMBA 2024

Habari za UN

Play Episode Listen Later Nov 11, 2024 9:59


Hii leo jaridani tunaangaziamkutano wa 29 wa nchi wanachama wa Mkataba wa Mabadiliko ya Tabianchi, COP29, na mradi wa lishe bora kwa watotot Afar nchini Ethiopia. Makala inatupeleka Havana Cuba na mashinani tunasalia huko huko Havana Cuba, kulikoni?Kufuatia mwaka mwingine wa viwango vya juu vya joto kali na matukio ya kupitiliza ya hali ya hewa, Mkuu wa Sekretarieti ya Mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu Tabianchi Simon Stiell amewaeleza washiriki wa mkutano wa 29 wa nchi wanachama wa Mkataba wa Mabadiliko ya Tabianchi, COP29, kwamba malengo mapya ya ufadhili kwa tabianchi ni muhimu kwa ajili ya ustawi wa mataifa, yakiwemo yale tajiri na yenye uthabiti.Mradi wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF wa kuchagiza kaya kulima bustani za mboga za majani pamoja na ufugaji wa kuku huko jimbo la Afar, kaskazini mashariki mwa Ethiopia umesaidia familia za vijijini kukabiliana na utapiamlo miongoni mwa watoto.Makala inatupeleka Havana Cuba ambako kongamano la kimataifa ka Kiswahilii limekunja jamvi mwishoni mwa wiki na shuhuda wetu huo Flora Nducha amezungumza na watu mbalimbali akiwemo mchechemuzi wa Kiswahili hususan kwenye mitandaao ya kijamii Nick Reynold ali maarufu Bongo Zozo, ambaye ni raia wa Uingereza.Na mashinani fursa ni yake Profesa msaidizi Xiaoxi Zhang raia wa China ambaye ni mshirika wa kimataifa au (Global Fellow) na mhadhiri wa masuala ya fasihi linganishi katika chuo kikuu cha Habib kilichopo Sindhi Karachi nchini Pakistan mmoja wa waliohudhuria kongamano la Kiswahili lililomalizika mwishoni mwa wiki akitoa ujumbe kuhusu changamoto ya kujifunza  Kiswhili.Mwenyeji wako ni Bosco Cosmas, karibu! 

Alfajiri - Voice of America
Zaidi ya wahamjiaji 900 waingia Uingereza kwa siku moja wakitokea Ufaransa kwa njia ya bahari. - Oktoba 07, 2024

Alfajiri - Voice of America

Play Episode Listen Later Oct 7, 2024 30:00


Matangazo ya nusu saa kuhusu habari za mapema asubuhi pamoja na habari za michezo.

SBS Swahili - SBS Swahili
Taarifa ya Habari 13 Agosti 2024

SBS Swahili - SBS Swahili

Play Episode Listen Later Aug 13, 2024 15:46


Viongozi wa Marekani na Uingereza wanaweza jiondoa katika makubaliano ya manowari yaliyofanywa na Australia chini ya mpangilio wa AUKUS, kwa kutoa onyo la mwaka mmoja tu kulingana na hati mpya ya ushirikiano huo.

Jioni - Voice of America
Waziri Mkuu wa Uingereza Keir Starmer anaapa kuweka vikwazo vya uhalifu kuhusu ghasia za mrengo wa kulia zilizozuka nchini mwake. - Agosti 05, 2024

Jioni - Voice of America

Play Episode Listen Later Aug 5, 2024 29:59


Matangazo ya saa nzima kuhusu habari za kutwa, ikiwa ni pamoja ripoti kutoka kwa waandishi wetu sehemu mbali mbali duniani na kote Afrika Mashariki na Kati, na vile vile vipindi na makala maalum kuhusu afya, wanawake, jamii na maendeleo.

keir starmer agosti afrika mashariki uingereza waziri mkuu uhalifu
Jioni - Voice of America
Waziri Mkuu wa Uingereza Keir Starmer anasema serikali yake haitatekeleza sera za mtangulizi wake kuwahamisha waomba hifadhi kwenda Rwanda - Julai 06, 2024

Jioni - Voice of America

Play Episode Listen Later Jul 6, 2024 29:59


Matangazo ya saa nzima kuhusu habari za kutwa, ikiwa ni pamoja ripoti kutoka kwa waandishi wetu sehemu mbali mbali duniani na kote Afrika Mashariki na Kati, na vile vile vipindi na makala maalum kuhusu afya, wanawake, jamii na maendeleo.

Kwa Undani - Voice of America
Marekani yaadhimisha miaka 248 tangu kupata uhuru kutoka kwa Uingereza - Julai 04, 2024

Kwa Undani - Voice of America

Play Episode Listen Later Jul 4, 2024 29:59


Kwa Undani ni matangazo ya dakika 25 yanayochambua habari kwa undani zaidi na kumpa msikilizaji maelezo ya kina kuliko ilivyo kawaida kuhusu tukio au swala lililojitokeza katika habari.

Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii
Marekani yataka Kenya kujiunga na NATO, mapigano mashariki yaendelea DRC

Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii

Play Episode Listen Later May 25, 2024 20:13


Makala imeangazia ziara ya rais wa Kenya William Ruto nchini Marekani, Uingereza na mpango wa kuwapeleka waomba hifadhi Rwanda, Jeshi la Congo FARDC laimarisha mapambano kwenye eneo la mashariki mwa nchi hiyo, uchaguzi kule Afrika kusini, siasa za Chad baada ya kuapishwa kwa Mahamat Idriss Debi, siasa za Afrika Magharibi, hati ya kukamatwa kwa waziri mkuu wa Israeli B-Netanyahu, na viongozi wa Hamas pia mengineyo

Sepetuko
Safari ya Haki: Balozi wa Uingereza Azuru Kenya Kutafuta Ukweli kwa Agnes Wanjiru

Sepetuko

Play Episode Listen Later May 24, 2024 4:23


Ziara ya Balozi wa Uingereza Nchini Kenya kwa familia ya Mkenya Agnes Wanjiru aliyetuhumiwa kuuliwa na mwanajeshi wa Uingereza kwenye kambi ya Jeshi ya Uingereza iliyoko Nanyuki uwe mwanzo wa kupatikana kwa haki kwa Wanjiru na waathiriwa wengine wa hujuma mikononi mwa wanajeshi wa Uingereza waliomo nchini.

Jukwaa la Michezo
CAF: Nani ataibuka na taji la Klabu bingwa barani Afrika 2024?

Jukwaa la Michezo

Play Episode Listen Later May 18, 2024 24:42


Tuliyokuandalia ni pamoja na uchambuzi wa fainali ya Klabu Bingwa Afrika mwaka 2024, Zanzibar kuandaa fainali za mashindano ya shule za upili barani Afrika, Mkusanyiko wa michezo kwenye ukanda wa Afrika Mashariki, Maniema yarejea kwenye mashindano ya vilabu barani Afrika, uchambuzi wa mbio za kuwania taji la Uingereza kati ya Man City na Arsenal, Ngolo Kante arejea kikosini mwa Ufaransa, Brazil yateuliwa kuandaa Kombe la Dunia la kina dada la mwaka 2027.

Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii
Mazishi ya wakimbizi wa ndani 35 DRC, Uganda na Kenya zaimarisha mapatano yao

Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii

Play Episode Listen Later May 18, 2024 20:09


Baadhi ya mambo tunayoangazia ni mazishi ya watu 35 waliouawa baada ya bomu kulipuka katika kambi ya wakimbizi wa ndani eneo la Mugunga nje kidogo ya jiji la Goma, suala la Uingereza kuwahamisha wahamiaji huko Rwanda, ziara ya rais wa Uganda Yoweri Museveni nchini Kenya, siasa za Sudan na eneo la Afrika Magharibi, pia huko Ulaya na Marekani

Kwa Undani - Voice of America
Siasa za Uingereza: Chama cha Conservative kinaendelea kupoteza uungwaji mkono - Mei 09, 2024

Kwa Undani - Voice of America

Play Episode Listen Later May 9, 2024 30:00


Kwa Undani ni matangazo ya dakika 25 yanayochambua habari kwa undani zaidi na kumpa msikilizaji maelezo ya kina kuliko ilivyo kawaida kuhusu tukio au swala lililojitokeza katika habari.

Alfajiri - Voice of America
Uingereza yatuma mtafuta hifadhi wake wa kwanza nchini Rwanda - Mei 01, 2024

Alfajiri - Voice of America

Play Episode Listen Later May 1, 2024 29:59


Uingereza yatuma mtafuta hifadhi wake wa kwanza nchini Rwanda .

Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii
Tanzania yaadhimisha miaka 60 ya Muungano wa Jamhuri ya Tanganyika ,mafuriko yaripotiwa Kenya

Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii

Play Episode Listen Later Apr 27, 2024 19:51


Makala haya yanaangazia yaliyojiri nchini Kenya na Tanzania kufuatia mafuriko makubwa yaliyosababisha vifo vya watu zaidi ya 70 ,mgomo wa madaktari nchini Kenya, Tanzania kuadhimisha miaka 60 tangu kuundwa kwa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, safari za wahamiaji walioko nchini Uingereza kuelekea nchini RwandaTutaangazia pia uchaguzi wa wabunge nchini Togo,usalama wa Burkina Faso , na Ulimweguni  tutazidi kuangazia Mzozo unaondelea baina ya Israel na Hamas .

Jioni - Voice of America
Uingereza kutoa pauni 3,000 kwa wahamiaji watakaojitolea kupelekwa Rwanda kwa hiari. - Machi 27, 2024

Jioni - Voice of America

Play Episode Listen Later Mar 27, 2024 29:59


Matangazo ya saa nzima kuhusu habari za kutwa, ikiwa ni pamoja ripoti kutoka kwa waandishi wetu sehemu mbali mbali duniani na kote Afrika Mashariki na Kati, na vile vile vipindi na makala maalum kuhusu afya, wanawake, jamii na maendeleo.

SBS Swahili - SBS Swahili
Taarifa ya Habari 22 Machi 2024

SBS Swahili - SBS Swahili

Play Episode Listen Later Mar 22, 2024 15:58


Waziri wa Ulinzi Richard Marles amesema uchumi utafaidi kupitia makubaliano yakupiga jeki uzalishaji wa manowari yanayo tumia nishati ya nyuklia ya Uingereza kama sehemu ya mkataba wa AUKUS.

SBS Swahili - SBS Swahili
Makubaliano ya Uingereza na Rwanda kuhusu waomba hifadhi mashakani

SBS Swahili - SBS Swahili

Play Episode Listen Later Dec 8, 2023 7:25


Waziri mkuu wa Uingereza Rishi Sunak amewataka wabunge wa chama chake cha Conservative siku ya Alhamisi kuunga mkono mpango wake wa kuwapeleka Rwanda waomba hifadhi.

conservatives rwanda waziri uingereza alhamisi
SBS Swahili - SBS Swahili
Mahakama yasema mipango ya serikali ya Uingereza kwa waomba hifadhi ni kinyume cha sheria

SBS Swahili - SBS Swahili

Play Episode Listen Later Jul 4, 2023 4:28


Mpango wa serikali ya Uingereza waku wapeleka waomba hifadhi Rwanda, ume patwa kuwa ni kinyume ya sheria na mahakama moja mjini London.

Habari za UN
Ukame: Dola bilioni 7 zinahitaji kusaidia pembe ya Afrika

Habari za UN

Play Episode Listen Later May 24, 2023 0:02


Hii leo jijini New York Marekani, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres kwakushirikiana na nchi saba wanachama wa UN wanaendesha tukio la uchangishaji fedha lengo likiwa ni kukusanya dola bilioni 7 kwa ajili ya usaidizi wa kibinadamu kwa nchi zilizopo pembe ya Afrika. Kwa miongo kadhaa pembe ya Afrika imekuwa ikikabiliwa na ukame mkali hali iliyofanya takriban watu milioni 43.3 kuhitaji usaidizi wa kuokoa maisha na kustahimili changamoto zinazo wakabali hususan katika nchi za Kenya, Somalia na Ethiopia.Ukame umeleta njaa, kutokuwa na uhakika wa upatikanaji wa chakula na shida ya maji ambayo inachangia katika kuleta magonjwa.Hivi karibuni mvua zimeanza kunyesha, wananchi wamekuwa wakitarajia zitasaidia kupunguza changamoto zao lakini kama waswahili wasemavyo ‘ngombe wa masikini hazai' ndicho kilichotokea kwa nchi hizo kwani mvua kubwa zimeleta mafuriko na kwa mujibu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu misaada ya dharura, OCHA zaidi ya watu 900,000 wameathiriwa na mvua hizo.Mmoja wa watu hao ni Abdirahaman Ali Sheikh kutoka nchini Somalia, “Angalia hali ilivyo sasa, maji yametapakaa kwenye nyumba yangu yote na watoto wangu.”Bi. Qiyaas Axmed Farax amelazimika kuyakimbia makazi yake sababu ya mafuriko na sasa anahitaji msaada wa kibinadamu.“Tunahitaji chakula, malazi na maji, hatuna kitu, nguo zetu, vyakula na vingine vyote vimesombwa na maji. Watoto wangu walikuwa hatarini lakini namshukuru Mungu kwasasa tupo salama.”Mkutano huu wa ngazi za juu unaofanyika hapa jijini New York Marekani unatarajia kusaidia zaidi ya watu milioni 32 ikiwemo hawa waliathirika na mafuriko.Nchi saba zinazoshirikiana na Katibu Mkuu Guterres katika kendesha tukio hilo la ahadi ni Marekani, Uingereza, Qatar, Italia pamoja na nchi ambazo zinauhitaji wa haraka wa misaada hiyo ambazo ni Ethiopia, Somalia na Kenya.

Habari za UN
02 MEI 2023

Habari za UN

Play Episode Listen Later May 2, 2023 0:12


Jaridani leo tunakuletea mada kwa kina na leo tunamulika juhudi za kumkwamua mjasiriamali hasa nchini Kenya. Pia tunakuletea habari kwa ufupi zikiwemo ziara za Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Qatar, haki za binadamu na misaada kutoka mashirika nchini Sudan. Katika mashinani na kuelekea siku ya kimataifa ya uhuru wa vyombo vya habari hapo kesho, tunakuletea ujumbe wa Mwandishi wa Habari kutoka Uingereza kuhusu changamoto zinazowakumba waandishi wa habari.Mratibu Mkuu wa Umoja Mataifa kuhusu misaada ya dharura, Martin Griffiths ambaye yuko Kenya kusaka suluhu ya kufikisha misaada ya kiutu nchini Sudan, amemshukuru Rais William Ruto kwa uongozi na usaidizi wake kuona hatua za dharura za kiutu zinachukuliwa ili misaada ifikie nchini Sudan. Ametoa kauli hiyo baada ya Rais Ruto kuongoza mkutano uliohudhuriwa na viongozi waandamizi wa Umoja wa Mataifa wakiwemo Naibu Katibu Mkuu wa UN Amina Mohammed, Mkuu wa UNHCR Filippo Grandi na Bwana Griffiths.Hayo yakiendelea, msemaji wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya uratibu wa misaada ya dharura, OCHA Jens Laerke amezungumza na waandishi wa habari huko Geneva Uswisi hii leo na kusema mashirika ya Umoja wa Mataifa ya usaidizi wa kiutu yanakabiliwa na pengo la dola bilioni 1.5 la kufanikisha operesheni zake Sudan wakati huu mahitaji yanaongezeka kutokana na mapigano yanayoendelea, maelfu ya watu wakifurushwa makwao.Naye msemaji wa shirila la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi duniani, UNHCR mjini Geneva, Uswisi Olga Sarrado Mur amewaambia waandishi wa habari hii leo kwamba shirika hilo litazindua Mpango wa mashirika ya Umoja wa Mataifa wa kuchukua hatua za usaidizi Sudan, wakati huu ambapo takwimu za serikali, wadau na UNHCR zinaonesha zaidi ya watu 800, 000 wamekimbia Sudan na kuelekea Chad, Ethiopia, Sudan Kusini, na kwingineko, ambapo 600,000 ni wasudan na 200,000 ni wasudan kusini na wengineo waliokuwa wanapatiwa hifadhi Sudan.Na katika mashinani na kuelekea siku ya kimataifa ya uhuru wa vyombo vya habari hapo kesho, tunakuletea ujumbe wa Mwandishi wa Habari kutoka Uingereza kuhusu changamoto zinazowakumba waandishi wa habari.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!

Salama Na
SE7EP32 - SALAMA NA MRISHO NGASSA | MACHACHARI…

Salama Na

Play Episode Listen Later Jan 19, 2023 80:32


Mrisho Halfani Ngassa alikua top top top footballer na kwa bahati nzuri nishawahi kumshuhudia akiwa kazini kwake, tena ukimkuta kaamka vizuri basi uhakika wa burudani ni UHAKIKA . Na kipindi ambacho alikua kwenye peak yake pia kulikua na vitasa imara na magolkipa wazuri tu lakini nna uhakika kila mmoja kati yao ana la kusema kuhusu winga na forward hii machachari ambayo nchi yetu ishawahi kuona. Hakuna kitasa ambacho hakijawahi kukataa kufungua mlango muda ambao Mrisho Ngassa alikua anakuja kupiga hodi. Uzuri wake alianza kucheza mapema sana na kwasababu alikua machachari basi hata utulivu kidogo wakati anakua ulikua sio mzuri sana maana alikua na haraka. Ananiambia kwenye session hii vile ambavyo ali sign Yanga pasi na kumskiliza kocha wake kutoka Mwanza ambaye alikua anaamini kama dogo bado hajaiva, Pengine miaka miwili au mitatu ya kuendelea kujijenga ingemfanya awe bora zaidi na zaidi lakini kwenye kichwa na fikra za kijana huyu ambaye alikua na uchu wa mafanikio na kutaka kufika mjini maongezi hayo ya kusubiri yalikua ni kama kumuona sisimizi kwenye sukari alafu unamuambia asile leo badala yake ataila asubuhi, isingewezekana. Hivyo kocha akaona basi si mbaya, aende akayaone na kujifunza akiwa kazini. Yanga ndo Yanga, kwa wachezaji wote wanao chipukia au ambao ndo wanatafuta maisha kuichezea klabu kama ya wananchi ni heshima kubwa sana na zaidi kama wao ndo wametaka iwe hivyo. Kwa kijana mdogo ambaye alikua na spidi na uchu mkubwa wa kuzitia nyavuni basi klabuni pale ndo ilikua steji muafaka ya kuonyesha kipaji chake. Mrisho anakumbuka aina ya ‘vifaa' ambavyo vilikua vinapatikana mitaa ya Jangwani. Majina makubwa na kazi ilotukuka ambayo walikua wakiifanya ilikua inajielezea. Kwa kijana kutoka mkoani kuweza kupata namba haikua kazi rahisi, ila pia haikua kazi ngumu maana ulichokisia ndo ambacho unakiona, kuanzia mazoezini mpaka anapopatiwa nafasi wakati wa mechi. Kwenye episode hii tunazungumzia aina ya mitihani na maamuzi ambayo ilikua inabidi yafanyike. Kwenye wasifu wake Mrisho amewahi kucheza kwenye team zote tatu kubwa hapa nyumbani kwetu. Kashawahi kuwa muajiriwa wa Yanga, Azam na Simba ambapo alienda kwa mkopo kutoka Azam FC, lakini pia ashawahi kupatiwa majaribio katika team kadhaa nje ya nchi yetu na wakubwa wanasema kama Ndugu yetu angekua katuliza akili na angefahamu aina ya nafasi ambayo alikua nayo kipindi kile basi yeye ndo angekua mtanzania wa kwanza kucheza kwenye ligi pendwa ya Uingereza. Trials kwenye klabu kama Westham alipata na ofa kwenye vilabu kadhaa kutoka hapa hapa barani Afrika nazo zilikua hazikati. Sasa, nini haswa kilitokea? Wapi hasa alienda mrama? Ni kweli alikosea? Au malengo yake si malengo yetu? Au tulipokua tunamuona sisi yeye alikua hapaoni huko? Vikwazo vilikua nini? Mambo yepi hasa ndo ambayo yanaweza yakawa ndo chachu ya hayo yote kutotokea? Kama Mrisho angekua anawez kufunguka zaidi nami kwenye episode hii naamini tungeweza kupata funzo lilonyooka kwa wenetu na ukichukulia sasa mambo ndo yameanza kufunguka. Naamini angekua mwalimu mzuri kwa wake wote ambao wangetaka kusoma somo ambalo lina uhitaji mkubwa. Yangu matumaini utaweza kuelewa na kupata chochote kitu kutoka kwenye maongezi haya. Tafadhali enjoy. Love, Salama. --- Support this podcast: https://anchor.fm/yahstonetown/support

Habari za UN
Mradi uliofadhiliwa na TAKEDA, wawezesha Rwanda kuimarisha huduma kwenye hospitali na vituo vya afya: UNICEF

Habari za UN

Play Episode Listen Later Jan 10, 2023 0:07


Nchini Rwanda, Umoja wa Mataifa unashirikiana na serikali kuimairisha huduma za uzazi ili hatimaye kuhakikisha kila uzazi unakuwa salama si tu kwa mama bali pia mtoto anayezaliwa. Kupitia mradi uliofadhiliwa na TAKEDA, kampuni hii ya utafiti na dawa duniani, Rwanda imeweza kuimarisha huduma kwenye hospitali na vituo vya afya.Mradi huo wa ubia ulianza mwaka 2017. Wakati huo, Rwanda ndio ilikuwa imekamilisha malengo ya milenia, ikimaanisha baadhi ya malengo yalitimizwa, lakini kulikuwa na kusuasua katika baadhi ya maeneo mengine.Mathalani hadi leo vifo vya watoto wachanga ni 20 katika kila watoto 1,000 wanaozaliwa hai na theluthi moja ya watoto nchini Rwanda wamedumaa. Sasa jawabu ni mradi wa kusaidia watoto kabla tu na baada ya kuzaliwa, au RPIP. Mradi huu ni ubia baina ya Wizara ya Afya ya Rwanda, Chama cha madaktari wa watoto Rwanda, na Chuo cha madaktari watoto na afya ya watoto nchini Uingereza. Vituo 85 na hospitali 19 zimefikiwa na mradi huu ambapo ufuatiliaji unaanza kwa mjamzito hadi mtoto mchanga anapozaliwa. Hospitali ya Muhima kwenye mji mkuu Kigali ni miongoni mwa wanufaika na kwenye mada hii kwa kina Selina Jerobon anakusimulia kilichofaniyka kupitia mazungumzo kati ya Afisa kutoka UNICEF na wahudumu wa afya kutoka hospitali ya hiyo ya Muhima.

Salama Na
SE7EP30 - SALAMA NA BRENDA | MY DEAR…

Salama Na

Play Episode Listen Later Jan 5, 2023 66:17


Ushawahi kumuangalia mtu kwa mbali na kujiuliza maswali mengi juu yake? Maswali kama siku yake ikoje, amewezaje? Kama ana familia? Ki kawaida huwa anaamka saa ngapi? Amesoma wapi? Siku yake anaipangaje? Ana watoto? Mtoto? Huwa anawaandaa kwenda shule? Muda je wa kukaa nao? Elimu yake ameipatia wapi? Kwenye familia aliyotoka je? Wazazi wake wapo? Na je wanajivunia yeye kwa kiasi gani? Sasa ili kupata majibu ya maswali hayo yote ilibidi tumtafute Bi Brenda Msangi-Kinemo ambaye ndo nilikua namzungumzia hapo juu. Kama wewe utakua mtu wa kujua ambayo yanaendelea nchini, na pia kama ni mkazi wa Dar es Salaam basi lazima utakua unajua kuhusu hospitali ya CCBRT ambayo kwa kiasi kikubwa imesaidia na inaendelea kutoa huduma za macho, mifupa na magonjwa mengine kwa watu wengi kwenye nchi yetu. Sasa Bi Brenda yeye ndo Mkurugenzi pale. Na amekua kwenye cheo hicho kwa zaidi ya miaka minne sasa na hiyo ukiachilia mbali miaka ambayo alikua akifanya kazi pale wakati bado hakua Mkurugenzi. Yeye ni mtaalamu wa masuala ya afya, hicho ndo ambacho aliendea skuli huko nchini Uingereza na kwa mujibu wa baadhi ya majarida ambayo nimesoma maisha yake kama yalikua yanataka kubaki huko baada ya kuhutimu ila aliporudi nyumbani na kupata nafasi pale hospitali mambo mengi yalibadilika. Kwenye kipindi hiki anatusimulia jinsi ambavyo hayo yalitokea. Na aina ya maamuzi ambayo ilibidi ayachukue ili mambo yatuwame. Kwa wasichana wengi hasa wale ambao wanakua na kuanza kujitafuta Brenda ni role model wao sana na ni nafasi ambayo kwake yeye ilikuja baada ya kuwa anaandika kwenye ukurasa wake wa Instagram kuhusu kupambana na kuweza kuvaa kofia zaidi ya moja kwenye maisha ukiwa kama mwanamke. Humu pia ananiambia jinsi ambavyo hizo nondo za ku inspire zilivyoanza, ananiambia jinsi ambavyo alikua akisoma na kufanya kazi na wakati mwengine jinsi ambavyo majukumu yalikua yakimzidi mpaka anakaribia kukata tamaa ila msukumo ambao alikua akiupata kutoka ndani yake ndo ambao ulimfikisha alipo. Aliamini kwamba kuna wanawake na wasichana wengi ambao wanapitia kwenye mitihani ambayo yeye alikua nayo na kama yeye aliweza kushinda basi aliona atumie sauti yake na busara zake kuwaambia wengine kama hakuna kinacho shindikana kama nia inakuwepo. Binafsi nilijichotea mengi sana kutoka kwenye kisima chake cha busara na uthubutu na bado darasa naendelea kulipata kwasababu nafuatilia yale anayo yafanya na ambayo anayaandika ili kusaidia wengine wasijione wako peke yao. Mungu amueke na aendelee kumsimamia kwenye kazi zake na maono yake ambayo yanasaidia watu wengi wengine kuanzia ofisini kwake mpaka kanisani na nyumbani. Yangu matumaini nawe uta enjoy na kupata faida kwenye episode hii kama ilivyo nia yetu. Love, Salama. --- Support this podcast: https://anchor.fm/yahstonetown/support

Habari za UN
09 DESEMBA 2022

Habari za UN

Play Episode Listen Later Dec 9, 2022 0:12


Hii leo jaridani tunaangazia afya na waathirika wa ukame nchini Ethiopia. Makala tunakupeleka nchini Kenya na mashinani nchini Sudan Kusini.Utafiti mpya wa kisayansi uliofanyika kwa muda wa miaka sita umebaini kuna viwango vya juu vya usugu wa dawa dhidi ya vimelea au bakteria vinavyosababisha maambukizi kwenye mfumo wa damu yanayoweza kuhatarisha halikadhalika ongezeko la usugu w atiba dhidi ya vimelea vinavyosababisha magonjwa yaliyozoeleka kwenye jamii. Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ulimwenguni WHO limesema hayo katika taarifa iliyotolewa leo jijini Geneva Uswisi. Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza, James Cleverly akiambatana na Mwakilishi wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF Ethiopia, Gianfranco Rotigliano wametembelea eneo la Afar, nchini Ethiopia kujionea athari za ukame kwa watoto na familia na kutathimini hatua za dharura zizazochukuliwa na UNICEF ambapo Uingereza ni mdau muhimu kama mwanachama wa Umoja wa Mataifa na muhisani. .  Makala leo tunakwenda nchini Kenya kumulika jinsi mradi wa maji uliofanikishwa na Umoja wa Mataifa umeleta ahueni kwa watoto na familia zao.Na mashinani wakati siku 16 za uhamasishaji kupinga ukatili wa kijinsia tutabisha hodi Gurei Juba nchini Sudan Kusini, kulikoni?Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi.

Habari za UN
Jamii katika maeneo ya kusini na kaskazini mashariki mwa Ethiopia bado wanateseka na ukame mbaya zaidi: UNICEF Ethiopia

Habari za UN

Play Episode Listen Later Dec 9, 2022 0:02


Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza, James Cleverly akiambatana na Mwakilishi wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF Ethiopia, Gianfranco Rotigliano wametembelea eneo la Afar, nchini Ethiopia kujionea athari za ukame kwa watoto na familia na kutathimini hatua za dharura zizazochukuliwa na UNICEF ambapo Uingereza ni mdau muhimu kama mwanachama wa Umoja wa Mataifa na muhisani. Jamii katika maeneo ya kusini na kaskazini mashariki mwa Ethiopia bado wanateseka na ukame mbaya zaidi kuwahi kutokea katika kipindi cha miaka arobaini na kuwasukuma watoto zaidi na familia zao ukingoni mwa maisha yao. Kwa ujumla, zaidi ya watu milioni 24.1 wakiwemo watoto milioni 12.6 wanakadiriwa kuathiriwa na ukame huu. Kutokana na changamoto za ukame, mafuriko, na migogoro, kumekuwa na ongezeko la mahitaji ya kibinadamu na kuzorota kwa mafanikio ya maendeleo. Mathalani, katika eneo moja tu la Afar, inakadiriwa kuwa watu milioni 1.7 wanahitaji msaada wa kibinadamu.  Baadhi ya wanaotoa usaidizi mbalimbali ni ili kuunga mkono misaada ya kibinadamu ni Shirika la misaada la Uingereza, UK Aid, linalofadhiliwa na Ofisi ya Mambo ya Nje, Jumuiya ya Madola na Maendeleo (FCDO) ya serikali ya Uingereza. Waziri wa Mambo ya nje wa Uingereza James Cleverly anasema, "jambo muhimu zaidi ambalo tunaweza kufanya ni kuunga mkono mchakato wa amani ambao unafanyika kwa sasa. Amani ni jiwe la msingi ambalo kila kitu tunachofanya kinajengwa juu yake. Lakini pia tunachohitaji kufanya ni kuhakikisha kuwa tunaendelea kuunga mkono kazi ambayo inafanywa na wadau wetu mashinani ikiwa ni pamoja na UNICEF.” Akishukuru hatua kama hizo zinazochukuliwa wahisani kama Uingereza kupitia UKAid, Mwakilishi wa UNICEF nchini Ethiopia, Gianfranco Rotigliano, anasema, "Ushirikiano na UK Aid/FCDO ni jambo la msingi. Imekuwa miaka mingi ambapo tunashirikiana na UK Aid/FCDO katika dharura na katika maendeleo. Kwa Ethiopia, tumepata mchango mkubwa kwa ajili ya dharura na maendeleo, kwa lishe, kwa elimu, na katika maeneo yaliyoathiriwa na migogoro na ukame kama hapa Afar tulipo sasa. 

Alfajiri - Voice of America
Biden asema chaguo la Sunak kama Waziri Mkuu mpya wa Uingereza ni 'la msingi' - Oktoba 25, 2022

Alfajiri - Voice of America

Play Episode Listen Later Oct 25, 2022 30:00


Rais wa Marekani Joe Biden Jumatatu alitaja chaguo la Rishi Sunak, waziri wa zamani wa fedha, kama waziri mkuu wa kwanza wa Uingereza asiye mzungu, kuwa "la msingi" huku White House ikisema Biden angewasiliana na kiongozi huyo mpya na kumpongeza.

Habari za UN
Misingi ya kuanzisha UN miaka 77 iliyopita inakumbwa na mtikisiko, tuchukue hatua- Katibu Mkuu UN

Habari za UN

Play Episode Listen Later Oct 24, 2022 0:02


Ikiwa leo ni maadhimisho ya siku ya Umoja wa Mataifa, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema ni wakati muhimu wa kurejesha tena matumaini na imani katika kile ambacho ubinadamu unaweza kufanikiwa pindi jamii yote ya kimataifa itakapofanya kazi kama kitu kimoja na kwa mshikamano wa kimataifa. Thelma Mwadzaya na taarifa kamili.Siku ya Umoja wa Mataifa huadhimishwa tarehe 24 ya mwezi Oktoba kila mwaka kukumbuka tarehe kama hiyo mwaka 1945 wakati Chata ya kuanzisha Umoja huo ilipoanza kutumika baada ya kutiwa saini na kuridhiwa na nchi waanzilishi 51 zikiwemo tano zenye ujumbe wa kudumu katika Baraza la Usalama ambazo ni China, Ufaransa, Uingereza, Urusi na Marekani.,Katibu Mkuu Guterres katika ujumbe wake wa siku hii anasema Umoja wa Mataifa ni tunda la matumaini. Matumaini na azma baada ya Vita Kuu ya Pili ya Dunia ya kwamba kusonga kutoka mizozo na kuelekea katika ushirikiano wa kimataifa.Guterres amesema “leo hii shirika letu linakumbwa na majaribu kuliko wakati wowote ule. Lakini Umoja wa Mataifa uliundwa kwa ajili ya nyakati kama hizi. Sasa kuliko wakati wowote ule tunahitaji kurejesha tena uhai wa misingi ya Chata ya Umoja wa Mataifa katika pembe zote za dunia.”Misingi mikuu saba ya Umoja wa Mataifa  ambao sasa una wanachama 193 ni pamoja na kila nchi mwanachama ni sawa na mwingine na migogoro yote inapaswa kutatuliwa kwa njia ya amani.Katibu Mkuu anasema hilo lifanyike kwa kupatia fursa amani na kwa kumaliza migogoro ambayo inavuruga maisha, mustakabali na maendeleo ya dunia.Halikadhalika kwa kufanya kazi kutokomeza lindi la  umaskini, kupunguza ukosefu wa usawa na kunusuru malengo ya maendeleo endelevu, SDGs.Ametaja pia kulinda sayari dunia, ikiwemo kuondokana na uraibu wa matumizi ya nishati kisukuku na kuanza kutekeleza mapinduzi ya nishati jadidifu isiyoharibu mazingira.Hatimaye kuweka mizania ya fursa na uhuru kwa wanawake na wasichana na kuhakiksha haki zao kibinadamu zinazingatiwa.Wakati Chata ya Umoja wa Mataifa ina misingi saba, kwa upande wa malengo  yake ni manne ambayo ni kulinda amani na Usalama duniani, kuimarisha uhusiano wa kirafiki baina ya nchi, kufanikisha ushirikiano wa kimataifa katika kutatua matatizo ya kiuchumi, kijamii, kitamaduni au kiutu na kuwa kitovu cha kuweka utangamano wa vitendo vya nchi katika kufanikisha malengo hayo. 

SBS Swahili - SBS Swahili
Je! Tanganyika ilikuwa bora chini ya ulinzi wa Uingereza kuliko ukoloni wa Ujerumani?

SBS Swahili - SBS Swahili

Play Episode Listen Later Sep 29, 2022 9:19


Kifo cha Malkia Elizabeth II kili ibua hisia mseto kote duniani, haswa Tanzania ambako watu wa vizazi tofauti walipokea taarifa ya kifo chake katika hali tofauti.

SBS Swahili - SBS Swahili
Jukumu la Ufalme wa Uingereza ni nini nchini Australia?

SBS Swahili - SBS Swahili

Play Episode Listen Later Sep 13, 2022 9:32


Australia inadumisha uhusiano rasmi nawa hisia na ufalme wa Uingereza, kama urithi wa ukoloni wa Uingereza.

australia nini uingereza
Habari za UN
12 SEPTEMBA 2022

Habari za UN

Play Episode Listen Later Sep 12, 2022 11:48


Hii leo jaridani Flora Nducha anaanza kwa taarifa ya kwamba utumwa wa kisasa una aina mbalimbali ikiwemo kwenye ajira na pia kwenye ndoa. Kisha anakupeleka kaunti ya Tukrana nchini Kenya ambako UNICEF imenusuru wanawake na mwendo mrefu wa kusaka maji kwa kuwajengea mabwawa ya mchanga. Makala anakukutanisha na Hamad Rashid wa redio washirika MVIWATA FM mkoani Morogoro akikuletea mradi wa UNCDF ambao umekwamua maisha ya wakazi wa Kibondo mkoani Kigoma Tanzania kupitia ushirika wa kilimo uitwao Kibondo Big Power Group. Mashinani ni kauli ya Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania kwenye Umoja wa Mataifa Balozi Profesa Kennedy Gastorn kuhusu kifo cha Malkia wa Uingereza na ushirikiano wa kimataifa. Karibu!

Alfajiri - Voice of America
Viongozi wa dunia waendelea kutoa rambirambi zao kufuatia kifo cha Malkia Elizabeth II - Septemba 09, 2022

Alfajiri - Voice of America

Play Episode Listen Later Sep 9, 2022 29:56


Rais wa Marekani Joe Biden alikuwa kati ya viongozi wa kwanza wa kimataifa kutuma risala za rambirambi kwa serikali na watu wa Uingereza kufuatia kifo cha Malkia wao, Elizabeth II kilichotokea Alhamisi akiwa na umri wa miaka 96

dunia elizabeth ii rais kifo uingereza septemba alhamisi
SBS Swahili - SBS Swahili
Liverpool yatoa kichapo chakihistoria

SBS Swahili - SBS Swahili

Play Episode Listen Later Aug 31, 2022 11:39


Ligi kuu ya soka ya Uingereza huvutia mamilioni yamashabiki kote duniani.

liverpool ligi uingereza
Salama Na
SE7EP08 - SALAMA NA SAMATTA | HEADMASTER

Salama Na

Play Episode Listen Later Aug 4, 2022 60:51


Kila kijana wa ki Tanzania ambae anaupenda na kuuthamini mpira wa miguu na ambaye angependa ndo iwe kazi ya maisha yake basi Mbwana Ally Samatta ndiye role model wake, hakuna doubt kwamba watakua na mapenzi na Cristiano Ronaldo au Leo Messi au Kylian Mbappe au Marcus Rashford ila yule ambaye amewaaminisha kwamba INAWEZEKANA ukacheza POPOTE hapa duniani na hasa kwenye ligi yetu pendwa ya Uingereza ni Samatta. Rafiki tu kutoka Mbagala rangi tatu ambaye kashacheza saaana ndondo na makombe ya mbuzi wakati anakua na mwisho wa siku akaenda kucheza kwa wazungu na bado anaendelea kutafuta rizki yake huko, hata kama sio ligi ile ambayo hata yeye mwenyewe angependa awepo ila BADO ni MWAMBA wetu. Samatta huyu huyu ndo ambaye alijitwika mpira kichwani na kuitika nyavuni mbele ya beki ambae anaaminika kuwa BORA kwa misimu hii miwili mitatu ndani ya Virgil van Dijk. Hata wakati naandika hii bado mwili unanisisimka kwa wazo tu kwamba nililishuhudia lile, pata picha kwa mtoto ambaye ana ndoto hizo. Lile goli lilimfanyia NINI kwenye ndoto zake. KRC Genk walipoteza mchezo ule wa ugenini wa kombe la mabingwa wa Ulaya kwa magoli 2-1 ila kwenye mitaa yote ya mikoa ya Tanzania ile mechi ilikua ya USHINDI. Mbwana ametokea kwenye familia ya kawaida sana sana, wazazi wake wote kama kumbukumbu yangu itakua 100 basi walikua polisi, najua kwa hakika Baba yake alikua Polisi kwa asilimia 100. Kwa marehemu Bi Mkubwa wake ndo sina hakika sana ila kwa hakika jibu limo kwenye haya maongezi yetu. Anakumbuka jinsi ambavyo Mzee wake alikua anasisitiza kwenye suala la elimu na heshima, kama mtoto wa mwisho kwenye familia hiyo, Mbwana aliupenda sana mpira, zile za kujiiba na kwenda kucheza mechi za mbali alishafanya sana na matunda ndo haya ya leo. Nadhani ilifika kipindi Mzee mwenyewe aliona basi sawa, twende huko utakako. Familia yao yote ni wapenzi wa mpira na Kaka yake Mouhamed bado anacheza hapa hapa Tanzania. Sasa akiwa kama kioo kikubwa sana kwenye jamii hii Samatta anazungumzia presha ambayo hupewa hasa pale anapoitwa kwenye timu ya Taifa, jinsi maneno mengi ya kashfa yanaporushwa kwake kutoka kwa wananchi na anakumbuka pia wakati bado anacheza T.P Mazembe kuna kipindi kocha aliacha kumuita yeye na Rafiki yake Thomas Ulimwenguna ilisemekana kama pengine hakuna na interest na team au hakua anatoa 100. Pengine kipindi hicho aliumia zaidi maana hiyo haikua jambo zuri kwake. Mbwana anazungumza na mimi kuhusu urafiki wake na Ulimwengu na maisha ambayo walikua wanaishi pamoja wakati wako DRC, anakumbuka jinsi walivyokua wanapanga kufanikiwa pamoja na mipango yao endelevu kwenye career yao. Ulimwengu nae ana siku yake kwenye kiti chetu In Shaa Allah maana nae ana mengi ya kutuelezea. Majeraha ya mara kwa mara bila ya shaka yalisababisha kwa kiasi kikubwa ndoto zake za kucheza Ulaya kutochukua hatua ya juu kama ambavyo angependa, ila mimi naamini hayo yote maisha tu, kila kitu kilikua tayari kimesha andikwa. Samatta ni Baba ambaye watoto wake wanasoma hapa hapa nyumbani, nilimuuliza kama watoto wake wanajua yeye ni nani na akanipa story ndogo ya yeye kung'amua kama wanafahamu fika Baba yao ni nani. Mwenzangu humu kuna mengi sana ambayo yatakufaa na kwa nafasi ya kipekee ningependa kumshukuru Captain wa Taifa kwa kuchukua time kwenye ratiba yake ambayo ilikua imebana kweli kweli ili tu aje kutubarikia meza yetu kwa uwepo wake. Yangu matumaini uta enjoy sana. Love, Salama. --- Support this podcast: https://anchor.fm/yahstonetown/support

Habari za UN
19 JULAI 2022

Habari za UN

Play Episode Listen Later Jul 19, 2022 12:05


Hii leo jaridani tuna mada kwa kina mahsusi ikimulika raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC aitwaye Esperance Tabisha aliyenufaika na mpango wa Umoja wa Mataifa wa kuhamishia wakimbizi nchi ya tatu kupitia mkataba wa kimataifa wa wakmbizi, GCR. Katoka DRC kaingia kambini Kakuma nchini Kenya na kisha Canada na sasa ni mbunifu wa mitindo akitumia mtandao wa kijamii kupata wateja wake. Janga la COVID-19 lilikuwa chungu na tamu hapo hapo kwa vipi? Thelma anasimulia. Usisahau kuna habari kwa ufupi ikiletwa na Leah Mushi akianza na wakimbizi wa DRC wanaorejea nyumbani kwa hiari kutoka Angola, kisha hatua ya UN kupatia fedha Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR ili kukidhi mahitaij ya chakula na mwisho ni watoto kwenye mizozo ikimluika ripoti ya Katibu Mkuu. Mashinani ni nchini Rwanda ambako shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF linashirikiana Chama cha Madaktari wa Watoto wa nchini Rwanda na Chuo cha Madaktari wa Watoto, Royal College of Pediatrics cha Uingereza ili kuboresha upatikanaji wa huduma bora za afya kwa akina mama na watoto ndani ya siku 1,000 za kwanza za maisha kwa kuimarisha uwezo wa watoa huduma za afya na kwa kuvipa vituo vya afya vifaa muhimu vya matibabu. Noella Uwera ni Muuguzi anayehusika na watoto wachanga katika Hospitali ya Kacyiru katika mji mkuu wa Rwanda, Kigali. 

Habari za UN
27 Aprili 2022

Habari za UN

Play Episode Listen Later Apr 27, 2022 13:57


Jaridani Aprili 27, 2022 na Leah Mushi kwanza ni habari kwa ufupi- Takriban dola bilioni 1.4 zimeahidiwa na wafadhili kwa ajili ya kusaidia nchi zilizoko katika pembe ya Afrika zinazokabiliwa na ukame mkali kuwahi kutokea katika kipindi cha miaka 40. Ahadi hizo zimetolewa jijini Geneva, Uswisi katika mkutano wa ngazi za juu ulioandaliwa na Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Misaada ya dharura -OCHA na Shirika la Muungano wa Ulaya la Ulinzi la Kiraia na Operesheni za Misaada ya Kibinadamu -ECHO, na kuhudhuriwa na wawakilishi wa serikali wa nchi zilizoathiriwa na ukame za Somalia, Kenya na Ethiopia. Ahadi hizo za fedha zitasaidia mashirika ya kibinadamu kutoa chakula cha dharura, lishe, fedha taslimu na usaidizi wa kiafya, pamoja na malisho na dawa ili kuweka mifugo hai. Tayari watu milioni 1 wameyakimbia makazi yao kutokana na ukosefu wa maji au malisho, na mifugo isiyopungua milioni 3 imekufa.   =====================================  Leo Aprili  27, Uingereza imetarifu Shirika la afya la Umoja wa Mataifa, WHO kuhusu kundi la wagonjwa wenye maambukizi ya Salmonella Typhimurium. Uchunguzi ulihusisha mlipuko huo na chokoleti inayotengenezwa nchini Ubelgiji, ambayo imesambazwa kwa angalau nchi 113. Tahadhari ya kimataifa ilitolewa na INFOSAN tarehe 10 Aprili, na kuanzisha mkakati wa kimataifa wa kurejeshwa kwa bidhaa. Kufikia sasa, jumla ya wagonjwa 151 wanaohusishwa na genetiki zinazoshukiwa kuhusishwa na ulaji wa bidhaa za chokoleti husika wameripotiwa  kutoka nchi 11. Hatari ya kuenea katika kanda ya Ulaya ya WHO na kimataifa inatathminiwa kuwa ya wastani hadi taarifa zipatikane juu ya urejeshaji kamili wa bidhaa hizo.    ============================= Na Binti mfalme Basma bint Ali wa Jordan leo ameteuliwa kuwa balozi mwema wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na kilimo, FAO kwa Mashariki ya Karibu na Kaskazini mwa Afrika.  Katika jukumu lake jipya Binti mfalme atasaidia FAO kuongeza ufahamu kuhusu umuhimu wa kubadilisha mifumo ya kilimo cha chakula duniani, ili kuondokana na changamoto za kuendelea na kukua kwa njaa.  Mkurugenzi Mkuu wa FAO QU Dongyu amesema kuwa Binti Mfalme amekuwa muungaji mkono wa muda mrefu wa FAO na mtetezi na mjuzi wa uhifadhi wa bayoanuai duniani kote na kusema, "Ufalme wake umeongeza ufahamu kwa watu wa Jordan na watu wote wa Mashariki ya Karibu. na Afrika Kaskazini  kuhusu umuhimu wa kuhifadhi mimea asilia na mifumo ikolojia na kukuza utafiti wa bayoanuai na ujifunzaji wa mazingira, ambayo ni msingi wa kuhakikisha mifumo endelevu ya chakula cha kilimo na kuboresha uhakika wa chakula.  Katika mada kwa kina  tutapata ujumbe kutoka kwa washiriki kutoka Burundi kwenye mkutano wa jukwaa la kudumu la watu wa asili ulioanza wiki hii. Na katika mashinani ni ujumbe wa rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kuhusu ufunguzi wa jukwaa la kudumu la watu wa asili.

Habari za UN
Wakimbizi kuhamishwa kutoka Uingereza hadi Rwanda, UNHCR yatoa tamko

Habari za UN

Play Episode Listen Later Apr 14, 2022 1:21


Kufuatia uwepo wa taarifa za kuwa Uingereza imeingia makubaliano na Rwanda ya kuwahamisha wasaka hifadhi nchini Uingereza na kuwapeleka Rwanda, Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR limesema linaelewa kuwa serikali ya Uingereza inatangaza ushirikiano wa uhamiaji na maendeleo ya kiuchumi na nchi ya Rwanda lakini linahitaji kuyaona makubaliano hayo kwanza kabla ya kutoa maoni.

Habari za UN
14 Aprili 2022

Habari za UN

Play Episode Listen Later Apr 14, 2022 11:34


Jaridani Aprili 14, 2022 na Leah Mushi -Watu milioni 7 wameambukizwa chagas, upimaji na tib ani muhimu:WHO/UNITAID -Tunazifuatilia taarifa kuwa Uingereza inataka kuwahamishia nchini Rwanda wasaka hifadhi -Programu za mlo shuleni ni daraja la kufikia ndoto za elimu kwa watoto masikini :WFP Kwenye makala, tumsikilize muuguzi Rebecca Deng ambaye ni mkimbizi wa Sudani Kusini aliyeko katika kambi ya wakimbizi ya Kakuma nchini Kenya na kupitia programu ya Uzazi Salama inayoendeshwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la kuwahudumia wakimbizi UNHCR kwakushirikiana na Shirika la Msalaba Mwekundu nchini Kenya amekuwa akitoa elimu kwa jamii juu ya afya ya uzazi. Mashinani tunakutana na afisa wa lishe wa UNICEF akiwa Oromia, Ethiopia.

Habari za UN
Uingereza yaaswa na OHCHR kufukiria upya mswada kuhusu uhamiaji

Habari za UN

Play Episode Listen Later Mar 17, 2022 2:33


Umoja wa Mataifa umeisihi serikali ya Uingereza na watunga sheria kufikiria upya juu ya mswada wa  sheria mpya ya Utaifa na mipaka ya nchi hiyo kwakuwa ikipitishwa kama iliyo itakuwa na athari kubwa kwa wahamiaji na wakimbizi. Flora Nducha ana taarifa zaidi . (TAARIFA YA FLORA NDUCHA) Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Haki za Kibinadamu Michelle Bachelet ametoa wito huo na kueleza kuwa mswada huo wa sheria mbali na kudhoofisha ulinzi wa haki za binadamu pia unaenda kinyume na sheria za kimataifa za haki za binadamu. Miongoni mwa vifungu vilivyopo kwenye mswaada huo vinavyoonekana kutofaa ni pamoja na vile vinavyo pendekeza kuwashughulikia wanaotafuta hifadhi kwa njia tofauti kulingana na jinsi walivyofika nchini Uingereza, walipoomba hifadhi, njia waliyotumia katika kusafiri, na uhusiano wao na zile zinazoitwa nchi za tatu salama.  Pia mswada huo unapendekeza kuharamisha uingiaji nchini humo bila mpangilio pamoja na kurahisisha uhamiaji usio wa kawaida na kuipa mamlaka nguvu ya kuwavua uraia ambao tajari ni raia wa Uingereza bila taarifa.  Bachelet amesema ndani ya vifungu hivyo pia kuna pendekezo la kuanzishwa kwa vituo vya kuwashughulikia watu wanaoomba hifadhi katika pwani ya nchi hiyo na kwamba baraza la mawaziri limeukataa mswada huo waziwazi na kutaka ufanyiwe marekebisho makubwa.  "Kukataa kwa mawaziri kwa vifungu muhimu vya mswada huo kunapaswa kutuma ishara ya kulazimisha serikali ya Uingereza kwamba inahitaji kufanya marekebisho muhimu. Ninaiomba serikali na wabunge kufanyia kazi ishara hii na kuleta sheria inayopendekezwa kulingana na sheria za kimataifa za haki za binadamu na mkataba wa wakimbizi wa 1951,” amesema Bachelet. Akizungumzia athari za vifungu vya mswada huo Bachelet ametolea mfano kile cha kuwavua watu uraia akisema“ Mswada huo kama ulivyotungwa hapo awali ungeruhusu raia wa Uingereza kunyimwa uraia wao wa Uingereza bila taarifa na kwa njia ya kiholela na hivyo kuhatarisha kuongezeka kwa watu wasiokuwa na utaifa.” Bachelet amesema mswada huo usiporekebishwa “ sheria itakayopatikana itawaadhibu watu wanaoingia Uingereza kwa njia zisizo za kawaida kana kwamba ni wahalifu, kinyume na sheria na viwango vya kimataifa, na kuwatenganisha waomba hifadhi wanaofika Uingereza katika mafungu mawili na kukiuka haki ya kila mtu, zaidi ya hayo, vituo vya wakimbizi vilivyopendekezwa vya pwani vinaweza kuwaweka wanaotafuta hifadhi katika hatari, kutengwa na kunyimwa uhuru vitu ambavyo ni ukiukwaji wa haki zao za kibinadamu na utu.”.  

Habari za UN
17 MACHI 2022

Habari za UN

Play Episode Listen Later Mar 17, 2022 13:49


Miongoni mwa yaliyomo leo katika jarida letu la Habari linaloletwa kwako na Leah Mushi - Mswada mpya unaopendekewa Uingereza kuhusu uhamiaji hauna tija kwa wakimbizi, waomba hifadhi na wahamiaji yaonya ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa na kutoa raia kwa serikali ya nchi hiyo kuufikiria upya -Huko Gambia mradi wa mfuko wa Umoja wa Mataifa la ufadhili kwa kilimo IFAD waleta nuru kwa wakulima wa mpunga ambao pia wanafanya biashara -Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, kikosi cha 8 cha Tanzania TANZBATT 8 kilichomaliza muda wake chini ya mpango wa Umoja wa Mataifa nchini humo MONUSCO kinajivunia mafanikio makubwa yenye tija kwa wananchi. -Makala yetu leo inatupeleka Uganda wilayani Hoima kuangazia changamoto na athari za mafuriko kwa wanawake wa kikundi cha Kaiso Women Group (KWG) -Na mashinani tunabisha hodi Lviv Ukraine kwake Nataliya Ambarova mfanyakazi wa kujitolea anasimulia jinsi machungu wanayopitia wakimbizi wa ndani nchini Ukraine 

SBS Swahili - SBS Swahili
Giza la zingira Manchester United

SBS Swahili - SBS Swahili

Play Episode Listen Later Mar 10, 2022 9:14


Mechi chache zinasalia kwa ligi kuu ya Uingereza kuisha, ila tumbo joto linaendelea kusambaa katika timu zinazo wania nafasi zakushiriki katika mechi za klabu bingwa msimu ujao.