Podcasts about wizara

  • 18PODCASTS
  • 72EPISODES
  • 13mAVG DURATION
  • 1EPISODE EVERY OTHER WEEK
  • Feb 27, 2026LATEST

POPULARITY

20192020202120222023202420252026


Best podcasts about wizara

Latest podcast episodes about wizara

SBS Swahili - SBS Swahili
Yaliyo jiri Afrika: Tahadhari yatolewa kwa mlipuko wa virusi vinavyo sababisha UVIKO-19 Tanzania

SBS Swahili - SBS Swahili

Play Episode Listen Later Feb 27, 2026 8:05


Wizara ya afya Tanzania imesema kuwa maambukizi ya wagonjwa wa mafua makali ya Influenza na Uviko-19 yameongezeka na kuwataka wananchi kuchukua hatua stahiki za kujikinga na maambukizi hayo.

Habari za UN
10 FEBRUARI 2026

Habari za UN

Play Episode Listen Later Feb 10, 2026 13:04


Hii leo jaridani Anold Kayanda wa Idhaa hii amezungumza na Wakili Amon Mpanju, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum kutoka Tanzania aliyehudhuria Mkutano wa Kamisheni ya Maendeleo ya Kijamii (CSocD64).Mashirika ya kibinadamu ya Umoja wa Mataifa leo yametoa onyo kali kuhusu hali mbaya ya kibinadamu inayowakumba watoto nchini Sudan. Mashirika hayo lile la kuhudumia watoto UNICEF, la afya WHO na Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Binadamu wamenasema ghasia zisizoisha, njaa na magonjwa vinawasababisha watoto kupoteza Maisha na kudhoofika, huku mashambulizi dhidi ya vituo vya afya na vikwazo vya upatikanaji wa misaada vikizorotesha juhudi za kuwaokoa. Akizungumza na waandishi wa habari mjini Geneva, msemaji wa UNICEF, Ricardo Pires, amesema “Katika baadhi ya maeneo ya jimbo la Darfur Kaskazini, zaidi ya nusu ya watoto wote wanakabiliwa na utapiamlo mkali, si makadirio, si mfano, imethibitishwa.”.Kikosi cha 12 cha Ulinzi wa Amani kutoka Tanzania TANZBAT 12 kinachohusumu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Condo DRC chini ya mpango wa Umoja wa Mataifa nchini humo MONUSCO kimeendelea kudumisha uhusiano wa kijamii na wakazi wa mji wa Beni Mashariki mwa DRC, kwa kutoa msaada wa vifaa vya elimu kwa wanafunzi katika shule ya msingi Ngite iliyopo eneo la Mavivi. Mkuu wa shule hiyo Neema Nyamwaka amewashukuru walinada amani hao kutoka Tanzania kwa kujali sekta ya elimu.Leo ni siku ya mikunde duniani Shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo FAO likisistiza umuhimu kwa chakula hicho kwa lishe na mazingira. Huko Kigoma Tanzania FAO kupitia mpango wa Pamoja wa KJP imekuwa ikitoa mafunzo kwa wakulima kuhusu umuhimu wa mazao ya jamii ya mikunde huyu ni mmoja wa wanufaika wa mafunzo hayo.Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili, leo mchambuzi wetu ni Dkt. Josephat Gitonga, ambaye ni Mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi nchini Kenya, kwenye kitivo cha Tafsiri na Ukalimani anafafanua maana ya methali “Atokeapo mtoto wa fuko mshike japo wawinda fuko.”Mwenyeji wako ni Rashid Malekela, karibu!

kenya ethiopia tanzania sudan unicef nairobi drc fao maisha umoja hii haki kiswahili katika monusco pamoja jamii wanawake dkt jamhuri mataifa maendeleo mkuu mkutano shirika kidemokrasia wizara mashirika tigrai chuo kikuu
Habari za UN
28 JANUARI 2026

Habari za UN

Play Episode Listen Later Jan 28, 2026 10:45


Hii leo jaridani tunaangazia….mafunzo ya usalama katika Ziwa Victoria, na harakati za Shirika la kiraia la kusongesha elimu kwa watoto wa kike, CAMFED za kuwawezesha wanafunzi wa kike nchini Tanzania.Ikiwa leo ni siku ya kimataifa ya kukumbuka waathirika pamoja na manusura wa mauaji ya kimbari ya holokosti hususan yale yaliyofanywa na manazi wa kijerumani, hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa katika ukumbi wa Baraza Kuu kumefanyika kumbukizi ikileta pamoja manusura waliotoa shuhuda za waliyopitia wakikimbia maeneo kadhaa ikiwemo Austria baada ya kutwaliwa na wajerumani.Ziwa Viktoria barani Afrika, licha ya kuwa mhimili muhimu wa maisha kwa zaidi ya watu milioni 40 nchini Kenya, Uganda na Tanzania, bado linakabiliwa na vitisho vihusianavyo na biashara haramu za magendo, usafirishaji haramu binadamu na uvuvi haramu. Ili kupatia suluhu changamoto hiyo Ofisi ya Masuala ya Kimataifa ya kupambana na dawa za kulevya na utekelezaji wa sheria (INL) ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani na Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji, (IOM), na walinzi wa pwani wa Kenya wamechukua hatua.Nchini Tanzania shirika la kiraia la kuendeleza elimu kwa watoto wa kike, CAMFED limeendelea kufanikisha Malengo ya Maendeleo Endelevu, SDGs kwa kuwezesha wanafunzi wa kike kuimarika sio tu kimasomo darasani bali pia stadi za maisha na hatimaye wawajengee uwezo wenzao.Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!

kenya austria uganda tanzania afrika sdgs mambo inl iom umoja ili hii vijana nje mataifa camfed marekani shirika kimataifa ikiwa wizara
Habari za UN
IOM, Marekani na wadau washirikiana kukabili uhalifu Ziwa Viktoria

Habari za UN

Play Episode Listen Later Jan 28, 2026 3:38


Ziwa Viktoria barani Afrika, licha ya kuwa mhimili muhimu wa maisha kwa zaidi ya watu milioni 40 nchini Kenya, Uganda na Tanzania, bado linakabiliwa na vitisho vihusianavyo na biashara haramu za magendo, usafirishaji haramu binadamu na uvuvi haramu. Ili kupatia suluhu changamoto hiyo Ofisi ya Masuala ya Kimataifa ya kupambana na dawa za kulevya na utekelezaji wa sheria (INL) ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani na Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji, (IOM), na walinzi wa pwani wa Kenya wamechukua hatua. Je ni hatua zipi? Sheilah Jepngetich na taarifa zaidi.

kenya uganda tanzania afrika mambo viktoria inl iom umoja ili sheria nje mataifa marekani shirika kimataifa wizara uhalifu
Habari za UN
Kenya: WHO yasaidia huduma za afya katika Kaunti ya Tana River

Habari za UN

Play Episode Listen Later Jan 5, 2026 2:43


Huko nchini Kenya katika kaunti ya Tana River, hali mbaya ya hewa na migogoro imesababisha takriban watu 140,000 kuyahama makazi yao. Upatikanaji wa huduma za afya nao umekuwa mgumu na kuongeza magumu hususani kwa wanawake na watoto. Katika kukabiliana na hali hiyo Wizara ya Afya nchini humo inashirikiana na shirika la Umoja wa Mataifa la Afya duniani WHO katika kutoa huduma za afya kipaumbele kikielekezwa kwenye masuala ya uzazi salama. Rashidi Malekela na taaria zaidi

kenya umoja katika afya mataifa huko kaunti wizara
Habari za UN
05 JANUARI 2025

Habari za UN

Play Episode Listen Later Jan 5, 2026 11:19


Hii leo jaridani tunaangazia hali nchini Venezuela operesheni ya kijeshi ya Marekani, afya ya uzazi Tana River nchini Kenya, na wanawake wakimbizi wa DR Congo wanaopitia ukatili wa kijinsia wakikimbia machafuko. Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limekutana leo katika kikao cha dharura baada ya operesheni ya kijeshi ya Marekani nchini Venezuela tarehe 3 Januari mwaka huu, hatua iliyozua hofu ya kuongezeka kwa hali ya kutokuwa na utulivu nchini humo na katika eneo zima.Huko nchini Kenya katika kaunti ya Tana River, hali mbaya ya hewa na migogoro imesababisha takriban watu 140,000 kuyahama makazi yao. Upatikanaji wa huduma za afya nao umekuwa mgumu na kuongeza magumu hususani kwa wanawake na watoto. Katika kukabiliana na hali hiyo Wizara ya Afya nchini humo inashirikiana na shirika la Umoja wa Mataifa la Afya duniani WHO katika kutoa huduma za afya kipaumbele kikielekezwa kwenye masuala ya uzazi salama.Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu na Afya ya Uzazi (UNFPA), nchini Burundi, linaongeza juhudi zake kukabiliana na mahitaji yanayoongezeka ya wakimbizi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, (DRC) wanaokimbia mapigano yanayoendelea mashariki taifa hilo la Maziwa Makuu ili kulinda afya, usalama na utu wao na wa jamii zinazowapokea.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!

venezuela kenya congo burundi drc umoja hii katika afya watu baraza jamhuri mataifa marekani huko shirika kidemokrasia wizara
Siha Njema
Juhudi za wazee kukomesha ukeketaji wa wasichana kaskazini mwa Kenya

Siha Njema

Play Episode Listen Later Dec 23, 2025 10:04


Ukeketaji wa wasichana bado ni changamoto kubwa katika baadhi ya maeneo ya kaskazini mwa Kenya, licha ya marufuku ya kitaifa na juhudi za uhamasishaji zinazoendelea. Takwimu za Kitaifa KNBS na  zile Wizara ya Afya zinaonyesha kuwa asilimia 83 ya wanawake na wasichana wa Marsabit na 66 wa Isiolo tayari wamekeketwa—ikiziweka kaunti hizi miongoni mwa maeneo yenye viwango vya juu zaidi nchini.Sasa wazee maeneo hayo wameanza mchakato kukabiliana na ukeketaji huo

Habari za UN
Hali si hali huko El Fasher nchini Sudan, watoto 'walipa gharama' zaidi

Habari za UN

Play Episode Listen Later Oct 29, 2025 2:43


Ghasia zinazoendelea kwa kasi zinawakwamisha zaidi watoto katikati ya mashambulizi ya mabomu yasiyokoma, mapigano makali, na uhaba mkubwa wa chakula, maji salama na dawa kwa zaidi ya siku 500 sasa.“Hakuna mtoto aliye salama,” anasema Catherine Russell, Mkurugenzi Mtendaji wa Shrika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto, UNICEF kupitia taarifa iliyotolewa na makao makuu ya shirika hilo jijini New York, Marekani leo.Taarifa hiyo pia inamnukuu Catherine Russell akisema, “ingawa athari kamili bado haijulikani kutokana na kukatika kwa mawasiliano kote nchini Sudan, inakadiriwa kuwa watoto wapatao 130,000 huko Al Fasher wako katika hatari kubwa ya kukiukwa haki zao, huku kukiripotiwa visa vya utekaji nyara, mauaji na ukataji viungo vya mwili, pamoja na ukatili wa kingono.”Pia kuna taarifa za wafanyakazi wa mashirika ya kibinadamu kukamatwa au kuuawa.UNICEF inatoa wito wa kusitishwa mara moja kwa mapigano, kuhakikisha upatikanaji salama na usiokatizwa wa misaada ya kibinadamu, ulinzi wa raia hasa watoto, na kupatiwa uhakika wa njia salama kwa familia zinazotafuta hifadhi, kwa mujibu wa sheria za kimataifa za kibinadamu. Wale wanaohusika na ukiukaji lazima wawajibishwe.Wakati huohuo, Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) limethibitisha kwamba Wizara ya Mambo ya Nje ya Sudan imewataarifu kuwa viongozi  wawili wa juu wa WFP nchini  wametangazwa kuwa watu wasiotakiwa nchini Sudan na hivyo wameamriwa kuondoka nchini humo ndani ya saa 72, bila maelezo yoyote.WFP inaeleza kwamba uamuzi huu wa kuwafukuza Mkurugenzi wa WFP nchini Sudan na Mratibu wa Dharura wa WFP nchini humo unakuja katika kipindi muhimu kwani mahitaji ya kibinadamu nchini Sudan hayajawahi kuwa makubwa zaidi kama kipindi hiki, huku zaidi ya watu milioni 24 wakikabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula na jamii zikikumbwa na baa la njaa.Wakati ambapo WFP na washirika wake wanapaswa kupanua wigo wa msaada, uamuzi huu unalazimisha shirika kubadilisha uongozi bila mpango, jambo linalohatarisha shughuli zinazowaunga mkono mamilioni ya Wasudani walio hatarini kukumbwa na njaa kali, utapiamlo, na hata kifo kutokana na njaa.WFP na maafisa wa ngazi ya juu wa Umoja wa Mataifa wanaendelea kuzungumza na mamlaka za Sudan kupinga hatua hii na kutaka ufafanuzi wa uamuzi huo.Tags: Sudan, El Fasher, WFP, UNICEF

Habari za UN
23 OKTOBA 2025

Habari za UN

Play Episode Listen Later Oct 23, 2025 15:53


Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayoangazia siku ya Umoja wa Mataifa na tutasikia kutoka mashinani wananchi na asasi za kiraia zina yapi ya kusema kuhusu shirika hili kubwa na la kipekee linalounganisha nchi wanachama 193 duniani.Mashirika manne ya Umoja wa Mataifa lile la uhamiaji IOM, la kuhudumia wakimbizi UNHCR, la Kuhudumia watoto UNICEF na la mpango wa chakula duniani WFP leo yametoa wito wa dharura kwa dunia kuchukua hatua mara moja kukabiliana na janga la kibinadamu linaloongezeka nchini Sudan. Zaidi ya watu milioni 30 wanahitaji msaada, nchini humo wakiwemo watoto milioni 15 na wakimbizi karibu milioni moja.Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) jana Oktoba 22 ilisema Israeli lazima itimize majukumu yake kama “anayekalia kimabavu” kwa kuhakikisha kuwa msaada unaweza kupita bila vizuizi na kwa kuheshimu haki za Umoja wa Mataifa na mashirika mengine ya kibinadamu yanayofanya kazi katika Ardhi ya Palestina Iliyokaliwa kwa Mabavu. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres ameelezea maoni hayo ya ICJ kuwa “muhimu sana,” akiongeza kuwa yametolewa wakati ambapo Umoja wa Mataifa unafanya kila juhudi kuongeza kasi ya misaada kuingia Gaza baada ya kusitishwa kwa mapigano.Nchini Kenya, wahudumu wa afya waliokuwa wakisubiri hadi siku 15 kupata malipo sasa wanapokea pesa ndani ya saa 72 pekee, shukrani kwa mfumo mpya wa malipo ya kidijitali uliotolewa na Shirika la Sfya la Umoja wa Mataifa WHO na Wizara ya Afya ya nchi hiyo. Mfumo huu unapeleka fedha moja kwa moja kwenye pochi za simu za wafanyakazi, ukipunguza ucheleweshaji, gharama na kuongeza motisha. Wafanyakazi zaidi ya 120,000 sasa wanafaidika, kuboresha ufanisi wa kampeni za chanjo na juhudi za kudhibiti polio.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!

Habari za UN
MINUSCA washiriki kutoa elimu ya usalama barabarani CAR

Habari za UN

Play Episode Listen Later Sep 5, 2025 2:41


Kila mwaka,Wizara ya Uchukuzi na Usafirishaji wa Anga nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati CAR,  kwa msaada wa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo MINUSCA,huandaa kampeni za usalama barabarani. Na hivi karibuni katika mji mkuu wa nchi hiyo,Bangui, MINUSCA kwa kushirikiana na Vikosi vya Usalama vya Ndani ISF wameungana kupambana na ajali za barabarani zinazoongezeka kila uchao,doria ya pamoja imefanyika kutoa elimu kwa watumiaji wa barabara. Sabrina Saidi anatujuza zaidi....​(TAARIFA YA SABRINA SAIDI)Natts ....ongeza hii; katikaa mitaa ya Banguimji mji mkuu wa CAR pisha nikupishe ni nyingi. Kufuatia ongezeko la ajali za barabarani,zinazopoteza maisha ya watu kila uchao, kikosi cha polisi cha Ujumbe wa Umoja wa Mataifa MINUSCA kimeendesha doria ya pamoja ya usalama kwa kushirikiana na Vikosi vya Usalama vya nchi hii (ISF) katika mji mkuu BanguiOperesheni hii iliyofanyika tarehe 4 mwezi Septemba,mwaka huu imelenga kutoa elimu kwa waendesha pikipiki za abiria maarufu kama "moto taxi" nchini CAR na watumiaji wengine wa barabara kuhusu umuhimu wa kufuata sheria za barabarani.Kwa mujibu wa MINUSCA Hatua hii ina lengo la kuimarisha usalama na kujenga uhusiano mwema kati ya vikosi vya usalama na raia.​Akizungumza kuhusu umuhimu wa hatua hii, Kamanda wa Mkoa wa Plateaux(PLATIU) na Bas-Oubangui(BA OBANGI), Douflé Avi Chico( DOFLE AVII CHIKO BERNAA) Bernard, amesema,CUT- Sauti ya Douflé Avi Chico Bernard“Kwa kushirikiana na MINUSCA, kupitia brigedi yao ya magari, tunafanya kazi ya kuongeza uelewa kwa watumiaji wa barabara, waendesha pikipiki au teksi, ili kupunguza ajali nyingi ambazo kwa bahati mbaya zinagharimu maisha ya watu. Tutaendelea na kampeni hizi kubwa ili kurekebisha hali hii.”​Kwa upande wa watumiaji wa barabara, dereva wa pikipiki za abiria, Jean Terence Bokassa (JANI TEREE BOKASA), ameomba serikali iimarishe udhibiti wa sekta hiyo.CUT- Sauti ya Jean Terence Bokassa“Tunaomba serikali ihakikishe usalama wa waendesha pikipiki za abiria kwa sababu sisi ni watu kama wengine. Tunatoka nje kutafuta riziki, lakini maisha yetu yako hatarini. Tungependa serikali itusaidie kwa kuwafundisha ndugu zetu ambao hawana leseni ya udereva kanuni za barabarani ili kuhakikisha usalama wao.”Nattss.. Sauti za magari honi nk.​Doria hii ya pamoja inaonesha ushirikiano mzuri kati ya Polisi wa Umoja wa Mataifa na ISF, wote wakiwa wamejitolea kulinda raia na kupunguza ajali za barabarani na MINUSCA inasema wananchi wakipata uelewa wa kutosha basio sio tu barabara zitakuwa salama bali pia idadi ya vifo vitokanavyo na ajali za barabarani vitapungua.

car afrika anga umoja polisi isf kila kwa bangui sauti elimu jamhuri mataifa kamanda ujumbe septemba wizara
Habari za UN
Pamoja na mafanikio makubwa bado kuna changamoto kumjumuisha kikamili mwanamke mwenye ulemavu Zanzibar: Ms. Abeida Abdallah

Habari za UN

Play Episode Listen Later Jul 7, 2025 3:33


Kisiwa cha Zanzibar nchini Tanzania Mashariki mwa Afrika kimepiga hatua kubwa katika suala la ujumuishaji wa watu wenye ulemavu katika sekta mbalimbali kwa kuzingatia mikataba ya Umoja wa Mataifa ya watu wenye ulemavu na pia usawa wa kijinsia kuhakikisha hakuna anayeachwa nyuma. Lakini licha ya mafanikio waliyoyapata katika masuala kama elimu na haki za watu wenye ulemavu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Bi. Abeida Rashid Abdallah akizungumza na Flora Nducha wa Idhaa hii kandoni mwa kikao cha mwaka huu cha 69 cha kamisheni ya hali ya wanawake duniani CSW69 amesema bado kuna kibarua kikubwa cha kufanya kuhakikisha kila mtu  hususan mwanamke mwenye ulemavu anajumuishwa. Kwa undani zaidi ungana nao katika makala hii.

bi afrika zanzibar abdallah kuna umoja kwa makala watoto pamoja jamii lakini wanawake mataifa mwanamke maendeleo wizara
Habari za UN
07 JULY 2025

Habari za UN

Play Episode Listen Later Jul 7, 2025 10:00


Hii leo jaridani tunaangazia mafuriko katika Jimbo la Texas, Marekani, na shairi linaloenzi siku ya Kiswahili Duniani. Makala inamulika haki za watu wenye ulemavu hususani wanawake, na mashinani tunakwenda Osaka nchini Japani kunakofanyika maonesho au EXPO2025, kulikoni?Umoja wa Mataifa umeonesha mshikamano mkubwa na watu wa Jimbo la Texas, Marekani serikali kufuatia mafuriko makubwa yaliyotokea Ijumaa na kusababisha vifo hasa vya watoto na uharibifu mwingine mkubwa.Kuelekea siku ya Kiswahili duniani hapo Julai 7 mwaka huu ikibeba maudhui “Kiswahili: zama zilizopita, sasa na zijazo” kwa lengo la kutathimini ukuaji na mabadiliko katika ligha hiyo adhimu leo tunakupeka Nairobi Kenya kwenye mpango wa kujitolea wa Umoja wa Mataifa UNV apmbapo mmoja wa wafanyakazi wa mpango huo mghani wa mashairi Jescah Muyia ameamua kuienzi lugha hiyo kwa shairi murua.Makala inaturejesha Zanzibar Tanzania katika sehemu ya mwisho ya mahojiano baina Flora Nducha wa Idhaa hii na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Bi. Abeida Rashid Abdallah kuhusu ujumuishwaji wa watu wenye ulemavu ungana nao.Na katika mashinani, kuanzia Aprili 13 hadi Oktoba 2025 huko Osaka nchini Japani kunafanyika maonesho au EXPO2025 ikileta nchi na mashirika ya Umoja wa Mataifa maudhui yakiwa Kuumba Jamii za siku zijazo kwa maisha yetu. Banda la Umoja wa Mataifa limedadavua maudhui hayo na kuwa kujikita kwenye Kuungana kwa Mustakabali Bora washiriki wakionesha masuala tofauti tofauti ikiwemo onesho la picha likisimamiwa na mpiga picha kutoka Ufaransa. Mhusika anafafanua.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!

texas japan bi osaka banda jimbo umoja nairobi kenya hii makala kiswahili watoto julai jamii wanawake japani mataifa aprili maendeleo oktoba marekani ufaransa wizara
Habari za UN
29 APRILI 2025

Habari za UN

Play Episode Listen Later Apr 29, 2025 11:44


Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka katika mkoa wa Mwanza kaskazini magharibi mwa Tanzania ambapo vijana wameshika hatamu kuboresha mustakabali wao. Pia tunakuletea muhtasari wa habari  na mashinani tunasalia hapa makao makuu.Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa Kudumisha Amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, MONUSCO, umeikaribisha kusainiwa kwa “Azimio la Kanuni” tarehe 25 Aprili 2025 mjini Washington, D.C chini ya usimamizi wa Wizara ya mambo ya nje ya Marekani, kati ya serikali za DRC na Rwanda kwa lengo la kulinda rai ana kutekeleza azimio la Baraza la Usalama namba 2773 (2025).Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Shirika la Umoja wa Mataifa la msaada kwa wakimbizi wa Kipalestina UNRWA, Juliette Touma, akizungumza na waandishi wa habri mjini Geneva kwa njia ya video kutoka mji mkuu wa Jordan, Amman, wakati  kuzingirwa kwa Ukanda wa Gaza kukikaribia kuingia mwezi wa pili amesema “Mzingiro wa Gaza ni muuaji wa kimya muuaji wa watoto, wazee, na watu walioko katika mazingira magumu zaidi. Mzingiro huu unamaanisha kwamba familia nzima, watu saba au wanane wanalazimika kushirikiana kopo moja la maharagwe au njegere”.Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo, FAO limezitaka nchi za Kaskazini Magharibi mwa Afrika kuongeza ufuatiliaji na kuchukua hatua za mapema kudhibiti makundi ya nzige wa jangwani. Hii ni baada ya nzige wakubwa na makundi madogo kutoka ukanda wa Sahel kuhamia maeneo ya kusini mwa Sahara, hasa katikati ya Algeria, magharibi mwa Libya, na kusini mwa Tunisia tangu Februari hadi Machi mwaka huu.Na katika mashinani fursa ni yake Maruping Onkemetse Mkurugenzi na Mwanzilishi wa Kituo cha Msaada wa Familia, shirika linaloongozwa na wanawake wa asili  katika Wilaya ya Gantsi, kijiji cha Chobokwane nchini Botswana anayeshiriki mkutano unaoendelea hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa wa Jukwaa la Watu wa Asili akizungumzia alichojifunza hadi sasa.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!  

washington gaza familia rwanda tanzania afrika sahara libya tunisia botswana algeria sahel sdgs drc fao amman umoja machi congo drc hii asili mwanza watu monusco baraza vijana jamhuri mataifa aprili marekani shirika juliette touma ujumbe kidemokrasia azimio wizara jukwaa mkurugenzi
Habari za UN
08 APRILI 2025

Habari za UN

Play Episode Listen Later Apr 8, 2025 11:50


Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayomulika shughuli za shirika lisilo la kiserikali la KINNAPA Development Programme la huko nchini Tanzania katika kutekeleza Malengo ya Maendeleo Endelevu likijikita zaidi katika usawa wa kijinsia. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na mashinani:Uganda, ambayo tayari ni mwenyeji wa wakimbizi wengi zaidi barani Afrika, inakabiliwa na shinikizo kubwa baada ya wakimbizi zaidi ya 41,000 kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC kuingia nchini humo tangu Januari mwaka huu, wakikimbia machafuko mapya mashariki mwa nchi yao limesema leo Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR. UNHCR imesema watu walioko katika mazingira hatarishi wanatambuliwa kwa msaada maalum, huku familia zilizotengana zikisaidiwa kuunganishwa tena.Siku kumi baada ya matetemeko ya ardhi ya kutisha yaliyoitikisa Myanmar tarehe 28 Machi, idadi ya vifo inaendelea kuongezeka. Titon Mitra, Mwakilishi wa Kikanda wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo UNDP nchini humo, akiripoti leo akiwa katika jiji liloharibiwa sana la Mandalay, kwa njia ya video ameripoti kwa waandishi wa habari jijini Geneva, Uswisi akisema, “idadi ya vifo ya hivi karibuni imepita watu 3,500 na “inaweza kuendelea kuongezeka.”Kenya, Uganda na Rwanda zitanufaika na mpango wa mlo shuleni baada ya leo Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) kutangaza kuwa linaendeleza ushirikiano wake na Taasisi ya Novo Nordisk, kupitia ushirikiano wa kihistoria kati ya sekta binafsi na ya umma unaojumuisha Wizara ya Mambo ya Nje ya Denmark na Taasisi ya Grundfos, ili kupanua mpango wa mlo shuleni kutokana na chakula kinachozalishwa ndani ya nchi husika. Ushirikiano huu utajenga mfumo wa msaada unaohakikisha uendelevu wa muda mrefu wa mpango huu.Na mashinani mashinani jana tarehe 7 Aprili hapa Umoja wa Mataifa kumefanyika kumbukizi ya miaka 31 ya mauaji ya kimbari nchini Rwanda ambapo mmoja wa wazungumzaji alikuwa Germaine Tuyisenge Müller, manusura wa mauaji hayo na wakati huo alikuwa na umri wa miaka 9 wakiishi mji mkuu Kigali.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!

VOA Express - Voice of America
Wizara ya elimu Kenya imeondoa somo la Hesabu na sayansi kwa wanafunzi wa shule za sekondari kwamba sio lazima kucukua masomo hayo. - Machi 14, 2025

VOA Express - Voice of America

Play Episode Listen Later Mar 14, 2025 29:59


VOA Express pia inafuatilia kwa karibu sana maswala yanayovuma katika mitandao ya kijamii kama sehemu moja muhimu ya upashanaji habari siku hizi.

kenya machi somo hayo shule elimu wizara
Habari za UN
26 FEBRUARI 2025

Habari za UN

Play Episode Listen Later Feb 26, 2025 11:13


Hii leo jaridani tunaangazia hali ya kibinadamu nchini Somalia na huduma zaa faya kwa wakimbizi wajawazito nchini Chad. Makala inatupeleka nchini Kenya na mashinani nchini Uganda, kulikoni?Watu milioni 4.4 nchini Somalia wako hatarini kukumbwa na njaa ifikapo mwezi Aprili mwaka huu wa 2025, kutokana na ukame mkali, mizozo na ongezeko kubwa la bei za vyakula.Nchini Chad, taifa lililoko kaskazini-kati mwa Afrika mkunga mmoja amehamia kwa muda katika kambi ya wakimbizi ili kuhakikisha wajawazito wanapata huduma bora kabla na baada ya kujifungua kama njia mojawapo ya kuepusha vifo vya wajawazito na watoto wachanga.Makala inatupeleka nchini Kenya kumulika mradi wa shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo FAO, wa kulinda lishe ya wasiojiweza unavyoleta mabadiliko katika  jamii kuanzia kaunti ya Turkana hadi kwenye kambi ya wakimbizi ya Kakuma.Katika mashinani fursa ni yake Dkt Annett Alenyo Ngabirano kutoka Uganda akisema juhudi za Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani WHO na Wizara ya Afya ya Uganda zimeweza kudhibiti mlipuko wa ugonjwa wa Ebola nchini humo, WHO ikitoa msaada wa vifaa vya matumizi, dawa ya hospitali, msaada wa kiufundi na kuratibu wadau katika idara hiyo.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!  

Habari za UN
Gaza: Awamu ya tatu ya chanjo dhidi ya polio inaendelea

Habari za UN

Play Episode Listen Later Feb 24, 2025 3:02


Katika makala hii Anold Kayanda wa Idhaa hii anaangazia chanjo inayoendelea katika Ukanda wa Gaza dhidi ya polio chini ya usimamizi wa Wizara ya Afya ya Palestina kwa kusaidiwa na Mashirika ya Umoja wa Mataifa. Uchanjaji huu wa sasa kwa njia ya matone dhidi ya polio ni wa dharura kutokana na kugunduliwa kwa virusi vya polio katika sampuli za maji taka huko Gaza hivi karibuni, ikionesha kuwa virusi hivyo vinaendelea kuzunguka katika mazingira na hivyo kuwaweka watoto katika hatari. 

Habari za UN
24 FEBRUARI 2025

Habari za UN

Play Episode Listen Later Feb 24, 2025 9:59


Hii leo jaridani tunaangazia miaka mitatu ya vita nchini Ukraine, machafuko nchini DRC na elimu Sudan Kusini. Makala inatupeleka katika ukanda wa Gaza kumulika harakati za chanjo ya polio, na mashinani nchini Kenya kusikia ujumbe kuhusu umuhimu wa lugha mama.Mkutano wa 58 wa Baraza la Umoja wa Mataifa la Haki za Binadamu umeanza leo jijini Geneva, Uswisi ambapo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amezungumzia kiza kilichotanda duniani hivi sasa kutokana na mapigano  yanayoendelea sehemu mbalimbali kuanzia Ukraine, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC  hadi Ukanda wa Gaza, yakiambatana na ukiukwaji mkubwa wa haki, akitaka kila juhudi zichukuliwe kusaka amani ya kudumu.Huko Gaza Kaskazini, kwenye eneo la wapalestina linalokaliwa na Israeli, wanafamilia zilizofurushwa makwao kutokana na vita kati ya Israeli na wanamgambo wa Hamas wanavumilia msimu wa baridi kali katika makazi ya muda ya mahema yanayopigwa na upepo na mvua usiku na mchana, limesema shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Watoto UNICEF. Nyumba zao zimeharibika na kuacha watoto kuishi katika mazingira mabaya.Katika makala Anold Kayanda wa Idhaa hii anaangazia chanjo inayoendelea katika Ukanda wa Gaza dhidi ya polio chini ya usimamizi wa Wizara ya Afya ya Palestina kwa kusaidiwa na Mashirika ya Umoja wa Mataifa.Na mashinani ikiwa hivi majuzi Dunia iliadhimisha siku ya kimataifa ya lugha mama, tunakwenda Kajiado nchini Kenya kusikia ujumbe kuhusu umuhimu wa lugha mamaMwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!  

ukraine kenya gaza israelis hamas congo palestina dunia drc umoja hii haki makala katika afya baraza jamhuri mataifa nyumba mkutano kidemokrasia wizara mashirika sudan kusini
Habari za UN
18 FEBRUARI 2025

Habari za UN

Play Episode Listen Later Feb 18, 2025 10:34


Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina leo inayotupeleka DRC katika mji wa Goma uliokuwa mji mkuu wa jimbo la Kivu Kaskazini ambao sasa uko mikoni mwa waasi wa kundi la M23. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na ujumbe kutoka mashinani.Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Binadamu, OHCHR imesema hali huko Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC inazorota kwa kasi kubwa, na kusababisha ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu, ukatili kama vile watu kuuawa kiholela, wakiwemo watoto, wakati huu ambapo waasi wa M23 yaripotiwa wametwaa mji wa Bukavu, jimboni Kivu Kusini.Wakati hayo ya kiendelea ndani ya DRC, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limeripoti kuwa katika siku chache zilizopita, wakongo kati ya 10,000 na 15,000 wamevuka mpaka wa DRC na kuingia Burundi wakikimbia mapigano.Na shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula duniani, WFP limekaribisha mchango wa dola milioni 5 kutoka Wizara ya Mambo ya Nje ya Korea Kusini. kwa ajili ya kujengea mnepo na kuimarisha upatikanaji wa chakula kwa familia za maeneo kame nchini Kenya.Na mashinani kupitia video ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi, UNHCR, fursa ni yake Faraja Kashindi Malumalu kutoka Tanzania ambaye ni mkimbizi katika kambi la Nyarugusi na mfanyakazi wa kituo hicho cha matibabu  ambaye anaonesha furaha kutokana na ujenzi wa kituo kipya cha wagonjwa wa ukimwi ambao umesaidia kuhifadhi faragha(privacy) ya wagonjwa.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!

kenya korea congo tanzania burundi mambo drc unhcr goma m23 wfp umoja hii haki bukavu wakati ohchr nje jamhuri mataifa shirika mashariki kidemokrasia wizara
Habari za UN
Tanzania: FAO yawezesha ufugaji kuku bila kutumia dawa ili kuepusha UVIDA

Habari za UN

Play Episode Listen Later Nov 25, 2024 3:55


Nchini Tanzania wanufaika wa  mradi wa kudhibiti usugu wa vimelea vya magonjwa dhidi ya dawa, (AMR) au kwa lugha ya Kiswahili, (UVIDA) unaotekelezwa na shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo, (FAO) nchini Tanzania, kwa kushirikiana na Wizara ya Mifugo na Uvuvi wamezungumzia manufaa ya ufugaji wa kuku bila kutumia dawa. Unaweza kujiuliza wanafuga vipi kuku bila kutumia dawa. Na je ni kwa nini wanafanya hivi. Je hawatumii dawa kabisa au wanafanya nini?Katika makala hii, mwandishi wa habari wa Redio washirika wetu Tanzania Kids Time ya mkoani Morogoro,mashariki mwa taifa hilo la Afrika Mashariki, Hamad Rashid, amezungumza na wanufaika hao  ambao pia walipata nafasi ya kuonesha shamba darasa la ufugaji kuku bila ya kutumia dawa kupitia hafla iliyoratibiwa na FAO katika shule ya sekondari Kihonda, Manispaa ya Morogoro, ikienda sambamba na Wiki ya utoaji elimu kuhusu UVIDA  ambayo hufanyika duniani kote kila ifikapo tarehe 18 hadi 24 mwezi Novemba. Kwako Hamad.

tanzania wiki fao bila amr kuku dawa umoja kiswahili katika mataifa unaweza novemba afrika mashariki redio wizara ufugaji
Alfajiri - Voice of America
Wizara ya afya nchini DRC yaanzisha kampeni ya kutoa chanjo dhidi ya mpox katika majimbo mbalimbali ya nchi hiyo - Oktoba 01, 2024

Alfajiri - Voice of America

Play Episode Listen Later Oct 1, 2024 29:59


Matangazo ya nusu saa kuhusu habari za mapema asubuhi pamoja na habari za michezo.

mpox katika afya hiyo nchi oktoba wizara kampeni
Habari za UN
WHO na Zanzibar zashirikiana kutokomeza ugonjwa wa matende

Habari za UN

Play Episode Listen Later Sep 4, 2024 1:52


Huko Zanzibar Tanzania, shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani, WHO kanda ya AFrika, linashirikiana na serikali kukabili ugonjwa wa matende ambao ni miongoni mwa magonjwa ya kitropiki yaliyopuuzwa au NTDs. Bosco Cosmas na maelezo zaidi.(Taarifa ya Bosco Cosmas)Video ya WHO kanda ya Afrika inatupeleka Zanzibar, Tanzania nyumbani kwa  Hamis Njani akitembea kwa shida, miguu imevimba. Alipata ugonjwa wa matende akiwa na umri wa miaka 18 lakini sasa WHO imempatia matumaini.(Sauti ya Hamis Njani)“Inaweza kukupata homa siku mbili kwa wiki, kwa hiyo nikashindwa kwenda shuleni.  Wakati mwingine nashindwa kuhudhuria shule kwa miezi hata mitatu. Ninapokwenda kule hospitali, ninapata huduma na mafunzo ya jinsi ya kuishi na haya maradhi kama vile kusafisha, kutumia dawa na mengine yote.”Ugonjwa huu huenezwa na mbu. Husababisha miguu au korodani kujaa maji  .Tangu mwaka 2010 Zanzibar imeendesha kampeni 20 za mgao wa dawa na WHO imetoa dawa kutibu watu milioni 1.5 kila mwaka. Asha Makame ni Mgawaji wa dawa kwenye jamii.(Sauti ya Asha Makame)“Mwanzo ulikuwa mgumu kwa sababu watu walikuwa hawaelewi.  Kwa sasa hivi mwitikio ni mzuri kwa sababu kile kitu watu wamekitumia na wanajua faida yake.WHO imefundisha pia madaktari katika kila hospitali ya wilaya kufanya upasuaji wa kisasa wa mabusha kwa wagonjwa 500.  Dkt. Shali Ahmed ni Meneja Mradi wa NTDs, Wizara ya Afya, Zanzibar.(Sauti ya Dkt. Shali Ahmed - Meneja wa mradi)“Ninaamini kufikia mwaka 2030, hata kabla ya hapo tutakuwa tumekomesha ugonjwa wa matende. Kwa hiyo tunawashukuru sana WHO kwa ushirikiano tunaoupata kwa kupata dawa, mara nyingi tunapata dawa kwa wakati na za kutosha kwa ajili ya nchi nzima.”

Habari za UN
Polio yathibitishwa Gaza, WHO yasema ni mtoto mwenye umri wa miezi 10

Habari za UN

Play Episode Listen Later Aug 23, 2024 2:02


Vuta nikuvute ikiendelea Gaza kuhusu ufikishaji, usambazaji na utoaji wa chanjo dhidi ya polio wakati huu ambapo makombora yanaendelea kurindima kutoka jeshi la Israeli, hii leo shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ulimwenguni WHO, limethibitisha kubainika kwa mgonjwa mmoja wa polio, ikiwa ni miaka 25 tangu ugonjwa huo utokomezwe eneo hilo. Assumpta Massoi na maelezo zaidi.(Taarifa ya Assumpta Massoi)Ni kwamba tarehe 20 mwezi uliopita wa Julai, mtoto huyo mwenye umri wa miezi 10 alilazwa katika hospitali ya Al-Aqsa akiwa ana homa kali, anatapika, anahara huku akiwa hana nguvu mwilini, limesema shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi wa kipalestina, UNRWA katika ripoti yake ya 130 kutolewa tangu vita ianze huko Gaza, ikimulika Gaza, Ukingo wa Magharibi na Yerusalem Mashariki.Tarehe 22 Wizara ya Afya kwenye eneo linalokaliwa la Palestina likathibitisha ugonjwa wa polio virusi namba 2 kwa mtoto huyo ambaye hakuwa amepatiwa chanjo kutoka Deir al-Balah huko Gaza. Siku tatu baadaye yaani tarehe 25 Julai mtoto huyo akapooza sehemu ya chini ya mguu wake. Hivi sasa anaendelea na matibabu na hali yake ni nzuri.Uchunguzi uliofanywa na Kituo cha Marekani cha Kudhibiti na Kuzuia magonjwa, CDC ukaunganisha virusi hivyo na aina ya ile iliyobainika kwenye mazingira huko Gaza mwezi Juni mwaka huu.Sasa WHO imethibitisha kuwa ni polio ambapo Mkurugenzi Mkuu wa UNRWA Philippe Lazzarini kupitia mtandao wa X amesema “inasikitisha sana kwamba mtoto huyo amepooza kutokana na Polio. Polio haitotofautisha kati ya watoto wa Palestina na Israeli. Kuchelewecha sitisho la mapigano kwa misingi ya kiutu kutaongeza hatari ya ugonjwa huo kusambaa zaidi kwa watoto.”Awamu mbili za utoaji chanjo zimepangwa kuanza wiki zijazo na UNRWA imesema wataalamu wake wa afya na kupitia kliniki zake tembezi watasaidia usambazaji kwa ushirikiano na WHO na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF.

Radio Maria Tanzania
Fahamu Maendeleo ya awali ya Mtoto.

Radio Maria Tanzania

Play Episode Listen Later Aug 2, 2024 52:21


Karibu uungane nami Martin Joseph, katika kipindi cha Elimu Jamii leo tupo  naye Bi. Miriam Luka Afisa Ustawi wa Jamii Mkuu kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsi, Wanawake na Makundi maalum akijikita katika mada isemayo Malezi, Makuzi na Maendeleo ya awali ya Mtoto. L'articolo Fahamu Maendeleo ya awali ya Mtoto. proviene da Radio Maria.

bi radio maria karibu jamii jinsi wanawake fahamu maendeleo wizara
Radio Maria Tanzania
Je, wafahamu mbinu zinazotumika kuimarisha Ndoa?

Radio Maria Tanzania

Play Episode Listen Later Jul 19, 2024 54:23


Karibu uungane nami Martin Joseph katika kipindi cha Elimu Jamii, ukiwa nami  Averino Chaula Afisa ustawi wa jamii Mwandamizi kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wanawake na Makundi maalum nikizungumzia juu ya kuimarisha Ndoa. L'articolo Je, wafahamu mbinu zinazotumika kuimarisha Ndoa? proviene da Radio Maria.

radio maria karibu ndoa maendeleo wizara
Jioni - Voice of America
Madktari na maafisa wa wizara ya afya washauriana kuhusu hatua za kusitishwa kwa mgomo wa kitaifa unaoendelea. - Machi 18, 2024

Jioni - Voice of America

Play Episode Listen Later Mar 18, 2024 29:59


Matangazo ya saa nzima kuhusu habari za kutwa, ikiwa ni pamoja ripoti kutoka kwa waandishi wetu sehemu mbali mbali duniani na kote Afrika Mashariki na Kati, na vile vile vipindi na makala maalum kuhusu afya, wanawake, jamii na maendeleo.

machi afya hatua afrika mashariki wizara
Alfajiri - Voice of America
Marekani yasema yawekea vikwazo mtandao mpana wa taasisi, makampuni na watu binafsi, inaosema unafadhili wanamgambo wa al-Shabaab - Machi 12, 2024

Alfajiri - Voice of America

Play Episode Listen Later Mar 12, 2024 30:00


Afisi ya Wizara ya Fedha ya  Marekani inayohusika na Udhibiti wa Mali za Kigeni (OFAC), Jumatatu imeyawekea vikwazo mashirika 16 na watu binafsi, ambao inasema wanahusika katika mtandao mpana wa biashara unaozunguka Pembe ya Afrika, Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) na Cyprus.

Jioni - Voice of America
Wizara ya fedha Marekani imewawekea vikwazo watu 16 na taasisi katika pembe ya Afrika na Mashariki ya Kati - Machi 12, 2024

Jioni - Voice of America

Play Episode Listen Later Mar 12, 2024 29:59


Matangazo ya saa nzima kuhusu habari za kutwa, ikiwa ni pamoja ripoti kutoka kwa waandishi wetu sehemu mbali mbali duniani na kote Afrika Mashariki na Kati, na vile vile vipindi na makala maalum kuhusu afya, wanawake, jamii na maendeleo.

afrika machi katika watu pembe marekani afrika mashariki mashariki fedha wizara
Siha Njema
Ushirikiano kati ya shirika la Village Reach na wizara ya afya nchini Kenya na nchi za ukanda wa Afrika

Siha Njema

Play Episode Listen Later Feb 6, 2024 10:07


Village Reach ambayo kwa tafsiri rahisi ni kufikia maeneo ya vijijini, imefungua ofisi za kikanda jijini Nairobi kujaribu kusaidia serikali kusimamia namba ya dharura,usafirishaji wa sampuli za Polio na kuboresha utendakazi wa wahudumu wa afya wanaofanya kazi katika jamii tofauti Baada ya kupata mafanikio makubwa katika nchi za Msumbiji, Malawi ,Village Reach inapanga kutumia mafunzo hayo kusaidia kuboresha huduma za afya katika mataifa ya Afrika.Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ,Village reach imeimarisha huduma za utoaji chanjo ,usafirishaji wa chanjo kutumia ndege zisizo na rubani katika maeneo yasiyo na miundo mbinu ikiwemo mkoa wa Equateur.Aidha shirika hilo linatoa huduma kwa ushirikiano na serikali katika mataifa mengine yenye mzozo kama vile Niger na Sudan Kusini.Afisa mkuu mtendaji Emily Bancroft amesisitiza mifumo ya afya inastahili kuwa thabiti ili kuwa na uwezo wa kustahimili majanga na hali za dharura kama ilivyoshuhudiwa wakati wa Uviko 19

Jioni - Voice of America
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani, Antony Blinken atatembelea nchi za Afrika wiki ijayo wizara ya mambo ya nje imetangaza Alhamis - Januari 18, 2024

Jioni - Voice of America

Play Episode Listen Later Jan 18, 2024 29:59


Matangazo ya saa nzima kuhusu habari za kutwa, ikiwa ni pamoja ripoti kutoka kwa waandishi wetu sehemu mbali mbali duniani na kote Afrika Mashariki na Kati, na vile vile vipindi na makala maalum kuhusu afya, wanawake, jamii na maendeleo.

afrika wiki antony blinken mambo waziri nchi marekani afrika mashariki wizara alhamis
Alfajiri - Voice of America
Wizara ya ulinzi Marekani imekiri kwamba Waziri wa ulinzi Lloyd Austin alitibiwa saratani ya tezi dume na kulazwa hospitali. - Januari 10, 2024

Alfajiri - Voice of America

Play Episode Listen Later Jan 10, 2024 30:00


Matangazo ya nusu saa kuhusu habari za mapema asubuhi pamoja na habari za michezo.

dume waziri marekani wizara
Habari RFI-Ki
Uganda : Raia wabugia pombe kupita kiasi

Habari RFI-Ki

Play Episode Listen Later Nov 1, 2023 9:55


Kweny makala haya tunajadili hatua ya Wizara ya afya nchini Uganda kusema raia wake zaidi ya milioni 1.2 wamezama kwenye unywaji wa pombe kupita kiasi, hili likitia serikali wasiwasi. Serikali zetu zinaweza kufanya nini kudhibiti unywaji wa pombe kupita kiasi ?Haya hapa baadhi ya maoni yako.

kenya uganda haya raia serikali wizara
Habari RFI-Ki
Uganda : Raia wabugia pombe kupita kiasi

Habari RFI-Ki

Play Episode Listen Later Nov 1, 2023 9:55


Kweny makala haya tunajadili hatua ya Wizara ya afya nchini Uganda kusema raia wake zaidi ya milioni 1.2 wamezama kwenye unywaji wa pombe kupita kiasi, hili likitia serikali wasiwasi. Serikali zetu zinaweza kufanya nini kudhibiti unywaji wa pombe kupita kiasi ?Haya hapa baadhi ya maoni yako.

kenya uganda haya raia serikali wizara
Kwa Undani - Voice of America
Marekani yatoa tahadhari ya biashara na Uganda - Oktoba 24, 2023

Kwa Undani - Voice of America

Play Episode Listen Later Oct 24, 2023 29:59


Wizara za Marekani za mambo ya nje, kazi, afya na huduma za kibinadamu, biashara, na shirika la maendeleo la kimataifa la Marekani, Jumatatu zimetoa tahadhari ya kibiashara dhidi ya Uganda.

uganda biashara oktoba marekani wizara
Jioni - Voice of America
Mkuu wa itifaki katika wizara ya afya Kivu Kusini, mashariki mwa DRC anaeleza idadi ya watu wanaoathiriwa na afya ya akili nchini humo - Oktoba 10, 2023

Jioni - Voice of America

Play Episode Listen Later Oct 10, 2023 29:59


Matangazo ya saa nzima kuhusu habari za kutwa, ikiwa ni pamoja ripoti kutoka kwa waandishi wetu sehemu mbali mbali duniani na kote Afrika Mashariki na Kati, na vile vile vipindi na makala maalum kuhusu afya, wanawake, jamii na maendeleo.

humo akili kivu katika afya watu oktoba mkuu afrika mashariki mashariki wizara
Kwa Undani - Voice of America
Mkutano wa kilele wa YALI kuhusu sera ya Marekani na Afrika wafanyika mjini Washington DC. - Agosti 01, 2023

Kwa Undani - Voice of America

Play Episode Listen Later Aug 1, 2023 29:59


Wizara ya mambo ya nje ya Marekani imeandaa Mkutano wa Mandela Washington Fellowship kuanzia Julai 31 hadi Agosti 2 katika Hoteli ya Omni Shoreham Washington, D.C. Mkutano huu unakutanisha viongozi vijana takriban 700 kutoka bara la Afrika

washington dc afrika sera yali hoteli agosti julai mandela washington fellowship marekani mkutano wizara
Habari za UN
Je unafahamu kuwa kuna fursa ya ufadhili katika nishati safi na salama Tanzania?

Habari za UN

Play Episode Listen Later Jul 31, 2023 0:05


Kwa mujibu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la mfuko wa maendeleo ya mitaji UNCDF wakizingatia Utafiti wa Bajeti ya Kaya Tanzania Bara (2017/18), upatikanaji wa nishati safi na teknolojia ya kupikia ni asilimia 17.1 tu ya wakazi wa mijini na asilimia 2 ya wakazi wa vijijini. Kuongezeka kwa mahitaji ya nishati ya kuni kunatokana na ukuaji wa haraka wa miji, bei ya juu, na upatikanaji mdogo wa nishati mbadala. Ili kuondokana na changamoto hizi, Programu ya CookFund ambayo inatekelezwa chini ya UNCDF kwa kushirikiana na Wizara ya Nishati nchini Tanzania, ina nia kuongeza idadi ya watu kwa kutumia suluhu endelevu za nishati safi ya kupikia katika maeneo ya mijini. Tayari awamu ya kwanza ya ufadhili imeenda kwa makampuni 16 kama anavyosimulia Anold Kayanda katika makala hii. 

Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii
Wizara ya mambo ya ndani yasitisha shughuli za CNL Burundi, msako makazi ya Katumbi DRC

Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii

Play Episode Listen Later Jun 10, 2023 20:14


Hatua ya rais wa Rwanda Paul Kagame kufanya mabadiliko katika vyombo vya usalama na jeshi nchini mwake, viongozi wa COMESA wakutana jijini Lusaka nchini Zambia, msako mkali ulifanyika katika makazi ya Moise Katumbi na mshauri wake nchini DRC, tumeangazia yaliyojiri nchini Kenya, Uganda, na hali ya mapigano kule Sudan Khartoum, na pia Afrika magharibi na kwengineko duniani! Ungana na mwandishi wetu Ruben Lukumbuka kusikiliza mengi zaidi

Alfajiri - Voice of America
Wizara ya mambo ya nje ya Iran imetangaza itafungua tena ofisi zake za kibalozi nchini Saudi Arabia wiki hii - Juni 06, 2023

Alfajiri - Voice of America

Play Episode Listen Later Jun 6, 2023 29:59


Matangazo ya nusu saa kuhusu habari za mapema asubuhi pamoja na habari za michezo.

Habari za UN
Wananchi wa Sudan Kusini washerehekea tamasha la utamaduni la amani

Habari za UN

Play Episode Listen Later Apr 19, 2023 0:04


Mwanzoni mwa mwezi huu wa April dunia iliadhimisha Siku ya Kimataifa ya michezo kwa maendeo na amani, nchini Sudan Kusini kwa siku mbili mfululizo maelfu ya wananchi walikusanyika kusherehekea tamasha la utamaduni la amani lililoandaliwa na Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini UNMISS kwa kushirikiana na Wizara ya Utamaduni ya jimbo la Kaskazini la Bahr El Ghazal.Maelfu ya wananchi walikusanyika kwa ajili ya sherehe hizo katika mji wa Aweil, wakitazama na kushiriki kuimba na kucheza nyimbo na ngoma za kitamaduni. Leah Mushi anasimulia hali ilivyokuwa

umoja makala siku tamasha mataifa kimataifa ujumbe wananchi michezo wizara sudan kusini aweil
Habari za UN
Kupitia FISH4ACP, FAO Tanzania yachukua hatua kukwamua wavuvi wanawake na wanaume

Habari za UN

Play Episode Listen Later Apr 14, 2023 0:02


Nchini Tanzania, shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo, FAO kupitia  mradi  wake FISH4ACP  limepokea matokeo ya Utafiti kuhusu Usawa wa Kinjisia katika Masuala ya Uvuvi, moja ya hoja ambayo ikitekelezwa vema itasaidia kufanikisha malengo ya maendeleo endelevu, SDGs hasa la kutokomeza njaa na kuondokana na umaskini.Uzinduzi wa matokeo hayo umefanyika wakati wa kikao cha siku mbili  hapa mkoani Kigoma na unatoka na Utafiti kuhusu Usawa wa kijinsia katika mnyororo wa thamani wa mazao ya Uvuvi Ziwa Tanganyika ukishirikisha wadau mbalimbali  wakiwemo wavuvi, wachakataji, wasafarishaji,  Jeshi la Polisi, serikali na wadau wa maendeleo.Devotha Songorwa wa Redio washirika Kids Time FM nchini Tanzania ndio shuhuda wetu wa uzinduzi huo uliofanyika katika  Mkoa wa Kigoma, Magharibi mwa Taifa hilo la Afrika Mashariki amezungumza na Afisa Mtaalamu Mnyororo wa Thamani wa Uvuvi na Ufugaji  Viumbe Maji, kutoka FAO nchini Tanzania anayesimamia mikoa ya Katavi, Rukwa na Kigoma nchini Tanzania, Hashim Muumin,  ambaye amempatia muhtasari wa matokeo ya utafiti huo kutokana na mradi huo wa miaka mitano  unaotekelezwa katika nchi 12 za Afrika  ikiwemo  Tanzania .“Imeonekana uvuvi ni suala la kiume zaidi kuliko wanawake lakini kwa utafiti tulioufanya tuliona asilimia 78 ya wachakataji ni wanawake na  asilimia  99 ya wavuvi ni wanaume na kuna masuala ambayo yanawakwaza kina wanawake na wanaume wavuvi katika kujikwamua kiuchumi,” amesema Afisa huyo.Ameeleza kuwa  utafiti huo utasaidia kubaini changamoto zinazokabili masuala ya Jinsia na fursa zake  katka Ziwa Tanganyika ili kutoa mwamko kwa wanawake na watu wenye ulemavu kujihusisha na Uvuvi kuinua kipato chao.“Shirika la FAO limeanzisha dawati la jinsia katika Wizara ya Mifugo na Uvuvi ambalo linafanya kazi na sisi kama mradi wa FISH4ACP tunafanya kazi kwa karibu sana kuhakikisha sera, mikakati na sheria za Serikali zinatekelezwa,” amebainisha Hashim.

tanzania afrika sdgs fao hashim umoja polisi taifa wanawake jeshi hatua mataifa serikali afrika mashariki shirika redio magharibi wizara
Siha Njema
Mapambano ya kumaliza kifua kifuu nchini Kenya kuelekea mwaka 2035

Siha Njema

Play Episode Listen Later Mar 21, 2023 10:12


Kwa mujibu wa mpango kazi wa shirika la afya duniani,WHO,mataifa yanastahili kupunguza vifo vinavyosababishwa na TB kwa asilimia 90 na maambukizo mapya kwa asilimia 80. Kila mwake tarehe 24 mwezi Machi ,dunia huungana kuadhimisha siku ya TB , kaulimbiu ya siku ya kifua kikuu duniani mwaka huu. ikiwa  Ndiyo tunaweza kuwekeza zaidi kumaliza Kifua Kikuu nchini Kenya kufikia 2035 ikiwa tutashirikiana. Kukomesha Kifua Kikuu nchini Kenya si jukumu la Wizara ya Afya kupitia mpango wa kitaifa wa Kifua Kikuu pekee bali ni jukumu letu sote.Aidha katika makala haya ,utaskia utambulisho kuhusu usafi wa kinywa naye daktari David Amenya.

Habari za UN
Waandishi wa habari wana fursa kubwa ya ushawishi chanya kwa jamii: Fatma Hamad – Zanzibar

Habari za UN

Play Episode Listen Later Mar 20, 2023 0:03


Tangu shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni lilipoitangaza lugha ya Kiswahili kuwa miongoni mwa lugha za kimataifa, taasisi mbalimbali zimeendelea kuhamasisha makundi mbalimbali kuitumia lugha hiyo katika masuala mbalimbali ya kijamii kama vile elimu kuhusu mabadiliko ya tabianchi, uchumi, ukatili wa kijinsia na kadhalika. Miongoni mwa makundi muhimu kufanikisha hayo ni waandishi wa habari ambao wana fursa kubwa ya ushawishi kwa jamii kama asemavyo Fatma Hamad,Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Michezo, Vijana na Utamaduni katika serikali ya mapinduzi, Zanzibar alipozungumza baada ya kukamilika kwa Kongamano la Idhaa za Kiswahili lililofanyika kwa siku mbili visiwani humo. Fatma Hamad anaanza kumweleza mwenzetu Anold Kayanda aliyehudhuria Kongamano hilo tathmini ya Kongamano lilivyokuwa.  

tanzania zanzibar fatma hamad umoja wana kiswahili habari jamii vijana elimu mataifa miongoni michezo wizara
Habari za UN
20 MACHI 2023

Habari za UN

Play Episode Listen Later Mar 20, 2023 0:12


Hii leo katika jarida tunamulika upatikanaji wa huduma za maji na za usafi, siku ya furaha, kongamano la kiswahili Zanzibar, Tanzania na changamoto za maji yatokanyo ziwa Kivu mwenyeji wako ni Assumpta Massoi.Wakati viongozi wa dunia wakijiandaa kuhudhuria mkutano wa kihistoria wa maji wa Umoja wa Mataifa, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF llimetoa wito wa uwekezaji wa haraka katika huduma za maji, usafi na usafi wa mazingira (WASH) zilizo na mnepo ili kuwalinda watoto. Leo ni siku ya furaha duniani ambapo Umoja wa Mataifa unasema ni siku ya kutabua umuhimu wa furaha kwa watu wote ulimwenguni kwani ni msingi wa lengo la ubinadamu na pia huchagiza ukuaji wa kiuchumiAnold Kayanda wa Idhaa hii  ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa amezungumza na Fatma Hamad, Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Michezo, Vijana na Michezo katika serikali ya mapinduzi Zanzibar kuhusu Kongamano la Idhaa za Kiswahili lililofanyika visiwani humo.  Mashinani: Paschal, mtoto mwenye umri wa miaka 15 ambaye kila siku kabla ya kwenda shule anadamkia Ziwa Kivu jimboni Kivu Kaskazini nchini DR Congo kuokota taka ili kuhakikisha wanaoteka maji hawapati magonjwa.

Habari za UN
16 MACHI 2023

Habari za UN

Play Episode Listen Later Mar 16, 2023 0:13


Hii leo jaridani tunanasalia hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa kusikiliza mahojiano yetu na viongozi waandamizi wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto huko Zanzibar Tanzania wanaoshiriki mkutano wa 67 wa hali ya wanawake duniani, CSW67 maudhui yakiwa matumizi ya dijitajitali katika zama za sasa za teknolojia kwa lengo la kusaidia wanawake na wasichana na hatimaye jamii. Pia tunakuletea habari kwa ufupi zikiwemo hali nchini Malawi baada ya kimbunga Freddy kuzuka nchini humo, Wakimbizi Ethiopia WHO na teknolojia UNCTAD. Katika kjifunza Klugha ya Kiswahili Dkt. Mwanahija Ali Juma anafafanua matumizi ya maneno Yeyote na Yoyote, baki nasi!Nchini Malawi, Umoja wa Mataifa umeendelea kuchukua hatua za usaidizi baada ya Rais wa nchi hiyo Lazarus Chikwera kutangaza hali  ya hatari kwenye mkoa wa kusini kufuatia mvua kubwa zilizosababishwa na kimbunga Freddy na katika wiki hii pekee zaidi ya watu 170 wamekufa na 178 wameokolewa.Nchini Ethiopia, shirika la Umoja wa Mataifa la afya ulimwenguni WHO linaimarisha harakati zake za kuhakikisha wakimbizi wanaokimbia ghasia Somalia na kuingia ukanda wa Dollo ulioko mkoa wa Somali nchini Ethiopia wanapata huduma za afya pamoja na wenyeji wao, wakati huu ambapo idadi yao inaongezeka kila uchao kwani tangu mwezi Februari mwaka huu idadi ya wakimbizi walioingia imefikia takribani laki moja.Na Kamati ya Umoja wa Mataifa ya Maendeleo ya Biashara duniani, UNCTAD imesema teknolojia rafiki kwa mazingira ambazo zinatumika kuzalisha bidhaa na huduma zinazidi kushamiri kila uchao na kuongeza fursa za kiuchumi, lakini nchi zinazoendelea ziko hatarini kutonufaika nazo iwapo serikali na jamii ya kimataifa hazitachukua hatua madhubuti.Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili na tunasalia visiwani Zanzibar nchini Tanzania ambako mchambuzi wetu Dkt. Mwanahija Ali Juma, Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili la Zanzibar, BAKIZA anafafanua matumizi ya maneno Yeyote na Yoyote..Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!

Habari za UN
03 MACHI 2023

Habari za UN

Play Episode Listen Later Mar 3, 2023 0:15


Jaridani leo  tunaangazia afya na hali ya kiuchumi katika nchi zenye maendeleo duni- LDC5.  Makala tutaelekea nchini Tanzania na mashinani nchini Sudan, kulikoni?Ikiwa leo ni siku ya kusikia duniani , shirika la afya la Umoja wa Mataifa WHO limesema maelfu ya watu duniani wanakabiliwa na changamoto ya kupoteza uwezo wa kusikia katika kiwango cha kuhitaji vipimo na matibabu.Kuanzia siku ya jumapili tarehe 5 mpaka 9 ya mwezi huu wa Machi, huko Doha nchini Qatar viongozi kutoka kila pembe ya dunia watakutana katika mkutano wa tano wa Umoja wa Mataifa wa nchi zenye maendeleo duni- LDC5 ili kukubaliana na kuangalia namna ya kuzisaidia nchi hizo ziweze kustawi wakati huu ambapo dunia inakabiliwa na changamoto lukuki.Katika makala tunakwenda nchini Tanzania kumulika ni kwa vipi mradi wa Jumuiya za Hifadhi za Wanyamapori, WMAs, unaotekelezwa kwa pamoja kati ya Wizara ya Maliasili na Utalii nchini humo na shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa maendeleo duniani, UNDP wa kuzuia ujangili na uhifadhi wa wanyamapori umesaidia jamii kunufaika sio tu na uwepo wa wanyamapori kwenye maeneo yao lakini pia kuishi kwa utangamano na wanyama kwa kuzingatia kuwa leo ni siku ya wanyamapori duniani na ujumbe ni ushirikishaji jamii katika hifadhi ya wanyamapori.Na katika mashinani na tutaelekea nchini Sudan kusikia njia mbadala za kuhakikisha usalama wa chakula na kuondokana na umaskini kwa jamii ambazo zilikuwa zinategemea upatikanaji wa ardhi, maji na malisho ya mifugo wengi.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!

Habari za UN
Matunda ya ubia katika kuhifadhi wanyamapori wazaa matunda pori la Waga Tanzania

Habari za UN

Play Episode Listen Later Mar 3, 2023 0:05


Nchini Tanzania kumulika ni kwa vipi mradi wa Jumuiya za Hifadhi za WAnyamapori, WMAs, unaotekelezwa kwa pamoja kati ya Wizara ya Maliasili na Utalii nchini humo na shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa maendeleo duniani, UNDP wa kuzuia ujangili na uhifadhi wa wanyamapori umesaidia jamii kunufaika sio tu na uwepo wa wanyamapori kwenye maeneo yao lakini pia kuishi kwa utangamano na wanyama kwa kuzingatia kuwa leo ni siku ya wanyamapori duniani na ujumbe ni ushirikishaji jamii katika hifadhi ya wanyamapori.Mwenyeji wetu ni Sawiche Wamunza, Mkuu wa Mawasiliano UNDP Tanzania akizungumza na Mwenyekiti na Katibu wa Jumuiya ya eneo la hifadhi ya wanyamapori ya Waga inayojumuisha vijiji vilivyoko mkoa wa Iringa na Mbeya. 

tanzania undp umoja makala katika pori waga mataifa wmas mkuu mbeya wizara
Habari za UN
Mikunde imetusaidia kutuimarisha kiafya na kielimu- Wanafunzi Njombe Tanzania

Habari za UN

Play Episode Listen Later Feb 10, 2023 0:04


Nchini Tanzania tayari wanafunzi wa shule za msingi wameanza kunufaika na maadhimisho ya siku ya mikunde duniani kwa kutambua kuwa Umoja wa Mataifa unasisitiza matumizi ya mimea ya jamii ya mikunde katika sio tu kuhimili mabadiliko ya tabianchi kwa kustahimili ukame, bila pia nafasi yake katika kuimarisha lishe kwa walaji. Mathalani mkoa wa Njombe ulio kusini mwa taifa hilo umekuwa unaongoza kwa udumavu wa watoto kwa mujibu wa takwimu za kitaifa za mwaka 2018, lakini takwimu za mwaka jana wa 2022 kutoka Wizara ya Afya zimebainisha kupungua kwa kiwango cha udumavu miongoni mwa watoto kutoka asilimia 53.6 mwaka 2018 hadi asilimia 50 mwaka 2022. Siri ni pamoja na mradi wa bustani za kilimo cha mboga na mikunde shuleni. Sasa John Kabambala wa redio washirika wetu KIDS Time FM amezungumza na wanafunzi wa shule ya msingi Itipingi katika halmashauri ya wilaya ya Njombe, wanufaika wa mradi wa kilimo cha bustani na mlo shuleni unaopatia kipaumbele kilimo na mlo wa mazao aina ya mikunde, mradi unaofadhiliwa na shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo FAO nchini humo, Kwako John. 

Habari za UN
Kilimo cha bustani shuleni huko Njombe Tanzania chainua kiwango cha lishe

Habari za UN

Play Episode Listen Later Feb 8, 2023 0:02


Kuelekea siku ya mikunde duniani, nchini Tanzania harakati za shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo duniani, FAO za kuboresha lishe ya watoto kuanzia shuleni, zimeanza kuzaa matunda hasa mkoani Njombe kusini mwa taifa hilo la Afrika Mashariki kwa kuzingatia kuwa mkoa huo ulikuwa unaongoza mwaka 2018 kwa kuwa na watoto wengi zaidi wadumavu. Hata hivyo takwimu mpya za Wizara ya Afya nchini Tanzania zimeonesha kiwango kupungua. Je ni hatua gani ambazo FAO imechukua na wanufaika wanasema nini? Ungana basi na John Kabambala, kutoka redio washirika Kids Time FM, nchini Tanzania ambaye amefunga safari hadi mkoani Njombe.  

tanzania fao hata umoja makala afya mataifa bustani huko afrika mashariki ungana wizara
Habari za UN
Mradi uliofadhiliwa na TAKEDA, wawezesha Rwanda kuimarisha huduma kwenye hospitali na vituo vya afya: UNICEF

Habari za UN

Play Episode Listen Later Jan 10, 2023 0:07


Nchini Rwanda, Umoja wa Mataifa unashirikiana na serikali kuimairisha huduma za uzazi ili hatimaye kuhakikisha kila uzazi unakuwa salama si tu kwa mama bali pia mtoto anayezaliwa. Kupitia mradi uliofadhiliwa na TAKEDA, kampuni hii ya utafiti na dawa duniani, Rwanda imeweza kuimarisha huduma kwenye hospitali na vituo vya afya.Mradi huo wa ubia ulianza mwaka 2017. Wakati huo, Rwanda ndio ilikuwa imekamilisha malengo ya milenia, ikimaanisha baadhi ya malengo yalitimizwa, lakini kulikuwa na kusuasua katika baadhi ya maeneo mengine.Mathalani hadi leo vifo vya watoto wachanga ni 20 katika kila watoto 1,000 wanaozaliwa hai na theluthi moja ya watoto nchini Rwanda wamedumaa. Sasa jawabu ni mradi wa kusaidia watoto kabla tu na baada ya kuzaliwa, au RPIP. Mradi huu ni ubia baina ya Wizara ya Afya ya Rwanda, Chama cha madaktari wa watoto Rwanda, na Chuo cha madaktari watoto na afya ya watoto nchini Uingereza. Vituo 85 na hospitali 19 zimefikiwa na mradi huu ambapo ufuatiliaji unaanza kwa mjamzito hadi mtoto mchanga anapozaliwa. Hospitali ya Muhima kwenye mji mkuu Kigali ni miongoni mwa wanufaika na kwenye mada hii kwa kina Selina Jerobon anakusimulia kilichofaniyka kupitia mazungumzo kati ya Afisa kutoka UNICEF na wahudumu wa afya kutoka hospitali ya hiyo ya Muhima.

Habari za UN
UNICEF yawezesha wanafunzi waliokuwa karantini Uganda kufanya mitihani

Habari za UN

Play Episode Listen Later Nov 30, 2022 0:02


Nchini Uganda shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF limewezesha wanafunzi wa shule moja ya msingi nchini humo kufanya mtihani wa kuhitimu shule ya msingi baada ya shule hiyo kulazimika kufungwa na wanafunzi kuwekwa karantini kufuatia mwanafunzi mmoja kupata maambukizi ya Ebola, mlipuko uliotangazwa mwezi SEptemba mwaka huu.Tarehe 20 mwezi Septemba mwaka huu wa 2022, Wizara  ya Afya nchini Uganda ilitangaza mlipuko wa Ebola, mlipuko ambao ulihatarisha kuvuruga mitihani ya kuhitimu elimu ya msingi kwa wanafunzi wa darasa la saba. Shule ya msingi ya Green Valley kwenye mji mkuu Kampala ilikuwa hatarini zaidi kwa sababu mwanafunzi mmoja aliambukizwa Ebola hivyo  madarasa matatu yalifungwa na shule ikafungwa ili ifanyiwe usafi. Mpaka Katula ni Mkurugenzi wa Shule ya msingi Ya Green Valley. “Uhai wa walimu wangu, wanafunzi wangu na wangu mwenyewe ulikuwa hatarini, ningaliweza kuachia shule, kwa hiyo kufunga shule lilikuwa ni jambo dogo.” Shule hiyo ilifungwa wiki tatu kabla ya kufanyika kwa mtihani ambapo Ian Mugisha mmliki wa shule ya msingi Green Valley anafafanua kwamba.. “Hii mitihani hufanyika katika siku maalum iliyopangwa. Usipofanya siku hizo, hutaweza kufanya tena, lazima usubiri mwaka unaofuatia. Kwa maajabu Wizara ya Afya, Wizara ya Elimu na Bodi ya Taifa ya mitihani Uganda, walishirikiana kuona wanafunzi wanafanya mitihani na UNICEF ikasaidia.” Jane, jina lake hili si rasmi ni mmoja wa wanafunzi 30 waliokuwa karantini na anasema, « UNICEF imenisaidia vifaa vya kufanyia mtihani, mlo wa mchana na usafiri kutoka nyumbani hadi hapa. Nilifanya mitihani ya kuhitimu darasa la Saba nikiwa karantini na nina imani nimefanya vizuri.” Na Bwana Katula anarejea na shukrani akisema, “sijui hii shule ingalifanya bila UNICEF kuingilia kati. Lakini kile ninachoweza kusema, asante UNICEF.” 

uganda unicef ebola kampala green valley bodi umoja hii kwa afya taifa lakini shule elimu mataifa septemba wizara mkurugenzi
Alfajiri - Voice of America
Malawi yasema itatoa chanjo ya kwanza ya malaria barani Afrika - Oktoba 11, 2022

Alfajiri - Voice of America

Play Episode Listen Later Oct 11, 2022 29:59


Wizara ya afya ya Malawi inasema hivi karibuni itatoa chanjo ya kwanza ya malaria barani Afrika kwa watoto walio chini ya umri wa miaka mitano.

Alfajiri - Voice of America
Rwanda yatangaza hatua madhubuti za kuzuia kuenea kwa viruzi vya Ebola villivyoripotiwa Uganda. - Septemba 28, 2022

Alfajiri - Voice of America

Play Episode Listen Later Sep 28, 2022 29:59


Wizara ya afya imesema kwamba hatua madhubiti zimechukuliwa ili kuhakikisha kwamba kuna uangalizi wa kutosha kwenye mipaka.

uganda rwanda ebola hatua septemba wizara
VOA Express - Voice of America
Madaktari Kenya wapokea vyema pendekezo la matibabu ya chemotherapy bila kikomo kwa watoto - Septemba 21, 2022

VOA Express - Voice of America

Play Episode Listen Later Sep 21, 2022 29:59


Watoto walio na saratani nchini Kenya hivi karibuni huenda wakapata vipindi vya chemotherapy bila kikomo ikiwa mapendekezo mapya ya Wizara ya Afya nchini humo yatapitishwa.

RadioRahma
Changamoto za mimba za utotoni kwa wasichana wenye matatizo ya akili

RadioRahma

Play Episode Listen Later Sep 15, 2022 8:14


Wizara ya afya nchini Kenya ilirekodi visa 45,724 vya mimba za utotoni mnamo Januari na Februari mwaka 2022.Visa hivyo ni vya wasichana wenye umri wa kati ya miaka 10 na 19 wakiwemo watoto wenye ulemavu wa akili.Watoto hao wenye ulemavu wengi ubakwa na kupachikwa mimba na kuachwa wakiangaika pasi usaidizi. Mwandishil:Rose Tawa

Alfajiri - Voice of America
Mikusanyiko ya kidini yalaumiwa kueneza ugonjwa wa Surua Zimbabwe. - Agosti 15, 2022

Alfajiri - Voice of America

Play Episode Listen Later Aug 15, 2022 29:59


Wizara ya afya imesema kwamba takriban watu 80 tayari wamekufa tangu ugonjwa huo ulipozuka wakati ikisemekana kwamba unaenea kwa haraka zaidi kutokana na mikusanyiko mikubwa ya kidini. Baadhi ya madhehebu wamewakataza wafuasi wao kupata chanjo za aina yoyote zile.

zimbabwe agosti baadhi ugonjwa wizara
Habari za UN
Wavuvi wanawake Kigoma wapata mtandao wao, shukrani kwa FAO

Habari za UN

Play Episode Listen Later Jul 29, 2022 4:19


Katika kutekeleza lengo namba 8 la malengo ya maendeleo endelevu, SDGs kuhusu ajira za staha na ukuaji kiuchumi sambamba na namba 5 la usawa wa kijinsia, shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo duniani FAO nchini Tanzania,  limezindua tawi la tatu la Mtandao wa Wanawake Wanaojihusisha na Shughuli za Uvuvi TAWFA kupitia mradi wake wa kukuza mnyororo wa thamani wa mazao ya uvuvi katika ziwa Tanganyika. Devotha Songorwa wa Radio Washirika KIDS Time  FM ya Morogoro nchini Tanzania ameshuhudia uzinduzi na kuandaa taarifa hii. Sherehe za uzinduzi huo zimefanyika mkoani Kigoma nchini humo ambapo wanawake wavuvi, viongozi wa serikali na wafanyakazi wa FAO walifungua rasmi tawi hili ikiwa ni la tatu nchini humo baada ya mwengine mawili yaliyozinduliwa huko kanda ya Ziwa Victoria na Ukanda wa Bahari ya Hindi. Uzinduzi huo unafanyika kupitia mradi wa FISH4ACP unaotekelezwa katika mikoa ya Kigoma, Rukwa na Katavi ambapo Mratibu wa Sekta ya Uvuvi Kitaifa kutoka FAO, Oliva Mkumbo akizungumza na Devotha Songorwa wa Redio washirika wa Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa alimueleza lengo ni kuwawezesha wanawake kiuchumi kupitia uvuvi ili kuinua kipato cha familia na kuondokana na umasikini. “Lengo la kuanzisha jukwaa la wanawake ni kuwawezesha kina mama ili mchango wao utambulike na kuleta athari chanya katika jamii. Tunataka kila mwanamke anayejihusisha na mnyororo wa thamani katika uvuvi anakuwa na sehemu ya kutoa mawazo yake na kubadilishana uzoefu ili kwa pamoja wachangie uboreshaji wa uvuvi,” Anasema Oliva. UN News Oliva Mkumbo Mratibu wa Sekta ya Uvuvi Kitaifa kutoka FAO Mratibu huyo wa FAO amesema hili halitakuwa tawi la mwisho nchini humo. “Jukwaa rasmi kitaifa lilifunguliwa 2017 ili kuwafikia wanawake wengi wakaanzisha Zone Chapters, Chapter ya Kanda ya Ziwa Victoria 2019, baadaye ikaja ya Uvuvi baharini, Kanda ya Ziwa Tanganyika na baadaye huko tutakuwa na linguine linalohusika na wavuvi kutoka katika maziwa madogo madogo,” Ameeleza Mratibu huyo. Beatrice Mmbaga ni Mwenyekiti wa Taifa wa Mtandao wa Wanawake Wanaojihusisha na Shughuli za Uvuvi Tanzania (TAWFA) anasema jukwaa hili ni sehemu ya kutatua changamoto zinazowakabili kina mama walio katika sekta ya uvuvi. “Nia ya kuanzisha chombo hiki ni kumfikia mama popote alipo anayejishusisha na samaki na mazao yake Tanzania nzima ndipo sasa tunashuka ngazi za chini katika Mikoa yetu, Kanda na Wilaya ili tuwe na sauti moja kwa sababu kina mama ndiyo asilimia kubwa wanajihusisha na samaki baada ya mavuvi hasa kwenye kuchakata na masoko lakini wana changamoto nyingi sana,” amebainisha Mwenyekiti huyo. UN News Wanawake wajasiriamali katika sekta ya Uvuvi Tanzania Kwa upande Mkurugenzi Msaidizi anayesimamia masuala ya Udhibiti Ubora na Mazao ya Uvuvi kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi Steven Lukanga amebainisha kwamba wanawake bado wanahitajika kupatiwa elimu ya uvuvi salama na kukidhi mahitaji ya walaji. “Kikubwa ni kuwajengea uwezo wanawake kutambua viwango vinavyopaswa kuzalisha yale mazao yanayowaendea walaji kwa kuzingatia viwango vilivyopo chini ya Shirika la Viwango Tanzania (TBS) kwahiyo sisi kama wizara tunashirikiana nao kuhakikisha wachakataji wanawake wanakidhi viwango vinavyotakiwa,”Amesema Lukinga.  

tanzania hindi sdgs fao umoja kanda kiswahili tanganyika bahari katika sekta taifa wanawake mataifa shirika lengo sherehe redio wizara jukwaa
Habari za UN
28 JULAI 2022

Habari za UN

Play Episode Listen Later Jul 28, 2022 14:02


Leo ni siku ya homa ya ini duniani! Hivyo tunakuletea jarida maalum linaloangazia kwa undani aina, maambukizi na vipi mtu anaweza kujikinga asipate homa ya ini ambayo shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ulimwenguni WHO linasema zaidi ya wakazi milioni 91 barani Afrika wanaishi nao hususan aina B au C ambayo ni mbaya zaidi. WHO inasema iwapo homa ya ini haitagunduliwa mapema unaweza kupata saratani au kansa ya ini. Je kuna aina ngapi ya homa ya ini? Homa Kali ya ini ni ipi ambayo imegunduliwa sasa? Njia za maambukiz ini zipi? Na nini ufanye uweze kujikinga? Leah Mushi wa Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa, na Evarist Mapesa wa Radio washirika SAUT FM ya Mwanza Tanzania wanakuletea kwa kina. Shukrani ikiwa ni kwa kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa, UNIC Dar es Salaam nchini Tanzania kwa kuratibu mahojiano na maafisa kutoka Wizara ya Afya Tanzania na shirika la Umoja wa Mataifa la afya ulimwenguni, WHO nchini Tanzania. Karibu na mwenyeji wako ni Assumpta Massoi.

Changu Chako, Chako Changu
Makala kuhusu Tamasha la MOCA lililofanyika huko Kigali Rwanda

Changu Chako, Chako Changu

Play Episode Listen Later Jul 7, 2022 19:50


Karibu kuwa nami Jumapili hii katika Makala Changu Chako Chako Changu, makala maalum kuhusu Tamasha lijulikanalo kama MOCA, Movement Of Creative Africas, yaani jukwaa la Viwanda vya Utamaduni na Ubunifu vya Kiafrika (ICC) na diaspora. Jumapili hii siko pekeangu nitakuwa naye mtangazaji mwenzangu ambae tumeambatana pamoja mpaka Kigali nchini Rwanda Florence Kihuwa. Tamasha la 7 linafanyika kuanzia Juni 30 hadi Julai 3, 2022 mjini Kigali, nchini Rwanda, kwa ushirikiano na Wizara ya Utamaduni, na jiji la Kigal…, toleo ambalo halijawahi kushuhudiwa kuhusu mada “Ubunifu na Sanaa kwa ajili ya mabadiliko!”. Fursa ya kuelewa jinsi ubunifu na sanaa inavyochangia katika maendeleo ya Afrika. Mengi zaidi kuhusu MOCA FESTIVAL nimezungumza na Muasisi wa Tamasha hilo Alain Bijek raia wa Cameroon.

Mazingira Leo, Dunia Yako Kesho
Hali ya mipango miji nchini Kenya na Tanzania

Mazingira Leo, Dunia Yako Kesho

Play Episode Listen Later May 30, 2022 10:01


Shirika la Umoja wa Mataifa la makazi UN-HABITAT inasema idadi ya watu wanaoishi mijini itaongezeka na kufikia zaidi ya Bilioni 5 kufikia mwaka 2030. Je, miji ya Kenya na Tanzania imejipanga vipi kuhakikisha kuwa miji yao inapangwa ?  Wiki hii tunazungumza na watalaam, Dokta  Robert Sangori kutoka Wizara ya ardhi na makaazi  nchini Kenya na Immacuate Senje Mkurugenzi Msaidizi anayehusika na upangaji na usanifu miji katika  Wizara ya ardhi nyumba na maendeleo ya makaazi nchini Tanzania.

kenya tanzania wiki umoja un habitat mataifa miji shirika wizara
Jioni - Voice of America
Bunge la Kenya lakataa mapendekezo ya wizara ya fedha ya kuongeza kodi kwa bidhaa muhimu - Mei 25, 2022

Jioni - Voice of America

Play Episode Listen Later May 25, 2022 29:59


Kamati ya bunge la Kenya ya masuala ya fedha imekataa mapendekezo ya wizara ya fedha yaliyomo kwenye makadirio ya matumizi ya fedha za serikali yaliyotaka kodi iongezwe kwa bidhaa mbalimbali muhimu.

kenya kodi bunge fedha wizara
Alfajiri - Voice of America
Wizara ya ulinzi ya Russia ilisema Alhamis mamia ya wanajeshi wa Ukraine wamejisalimisha katika kiwanda cha chuma cha Azovstal - Mei 20, 2022

Alfajiri - Voice of America

Play Episode Listen Later May 20, 2022 30:00


Wizara ya ulinzi ya Russia ilisema wanajeshi wa Ukraine wamejisalimisha katika kiwanda cha chuma cha Azovstal kilichozingirwa huko Mariupol na kufanya jumla ya wanajeshi 1,730 waliojisalimisha wiki hii. Pia kamati ya kimataifa ya msalaba mwekundu (ICRC) ilisema katika taarifa yake

Alfajiri - Voice of America
Kenya : wafanyakazi wa nyumbani Mashariki ya kati wapewa mafunzo kuhusu haki zao - Mei 05, 2022

Alfajiri - Voice of America

Play Episode Listen Later May 5, 2022 30:00


Wizara ya kazi ya Kenya imeamua kutoa mafunzo kwa wafanyakazi hao baada ya ripoti za unyanyasaji, ubakaji na vipigo dhidi yao. Wafanyakazi 23 walifariki tangu mwezi Novemba mwaka jana, vifo vingi vikiwa vilitokea Saudi Arabia.

kenya saudi arabia haki nyumbani novemba mashariki wizara
MAELEZO PODCASTS
Ufahamu zaidi Mradi wa Kuendeleza Utalii Kusini mwa Tanzania - REGROW

MAELEZO PODCASTS

Play Episode Listen Later Feb 28, 2022 12:29


Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii inatekeleza mradi wa kukuza utalii kusini mwa Tanzania (REGROW). Mradi wa REGROW ni mkopo kutoka Benki ya Dunia na lengo kuu la mradi huu ni kuboresha maeneo yenye vivutio vya utalii katika ukanda wa kusini mwa Tanzania.Hii ni pamoja na kuboresha usimamizi wa maliasili na kuimarisha fursa za kiuchumi kwa wananchi wanaozunguka hifadhi ili kuongeza mchango wa sekta ya utalii katika maendeleo ya kiuchumi nchini . Serikali inadhamiria mradi huu uwe wa mfano katika kuleta maendeleo kwa kufungua fursa za kiuchumi kwa jamii na taifa kwa ujumla.

tanzania dunia zaidi hii regrow jamhuri serikali wizara
Habari za UN
UNICEF yawatumia viongozi wa dingi kuhamasisha kampeni ya chanjo ya COVID-19 Garissa

Habari za UN

Play Episode Listen Later Dec 30, 2021 2:12


Janga la ugonjwa wa Corona au COVID-19 likiendelea kutikisa dunia huku taarifa potofu kuhusu chanjo zikiendelea kusambaa, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF nchini Kenya limechukua hatua ya kushirikiana na viongozi wa dini ikiwemo wale wa madhehebu ya kiislamu ili kusaidia kuelimisha waumini wao juu ya chanjo na faida zake katika kuepusha kusambaa zaidi kwa virusi vinavyosababisha ugonjwa huo. Taarifa ya John Kibego inafafanua zaidi.(Taarifa ya John Kibego)Nats.. Tuko katika kaunti ya Garissa nchini Kenya waumini wa madhehebu ya kiislamu wakiingia msikitini tayari kwa ibada wakati huu ambapo gonjwa la Corona bado linaendelea kuleta shaka na shuku. Kama mbinu ya kudhibiti kuenea kwa COVID-19 nchini Kenya, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF imeshapeleka dozi milioni 21 za chanjo dhidi ya Corona na linasaidiana na Wizara ya afya kuhakikisha watu wanachanjwa. Hata hivyo kuna changamoto ya taarifa potofu kuhusu chanjo na ndipo UNICEF ikashirikisha viongozi wa dini akiwemo Sheikh Omar Dagane, Imán wa msikiti hapa Garissa.(Sauti ya Sheikh Omar Dagane)- Jongo“Kama Imam wa jamii hii niña wajibu wa kushauri jamii kuhusu suala lolote la maslahi yao. Leo nimewaeleza waumini umuhimu wa kujikinga na COVID-19 kwa kupata chanjo. kupata chanjo ili kujikinga na COVID-19. Nimenukuu moja ya kauli za Mtume Muhamad SAW alipoulizwa na mfuasi wake iwapo amfunge kamba ngamia wake ambapo jibu lilikuwa Muamini Mungu lakini funga ngamia wako. Na vivyo hivyo tunapaswa kumuamini Mungu lakini tupate chanjo, vaa barakoa, nawa mikono, ili kujikinga.” Baada ya mahubiri mmoja wa washiriki Isak Abidi akafunguka akisema, “Nimesikiliza mahubiri ya Imam na ujumbe wa afisa wa afya na sasa nimeamua kuwa nakwenda kupata chanjo.” Abdullahi Abagira ni afisa wa UNICEF kaunti ya Garissa na anasema COVID-19 imekuwa na madhara ya aina mbalimbali hususan kwa watoto na hivyo UNICEF imesaidia kwa kusambaza siyo tu chanjo bali pia kufanikisha uwepo wa wahudumu wa afya wa kutoa huduma hizo.  

Jukwaa la Michezo
Hatima ya mchezo wa soka nchini Kenya baada ya kuvunjwa kwa Shirikisho

Jukwaa la Michezo

Play Episode Listen Later Nov 21, 2021 23:53


Nchini Kenya, Wizara ya Michezo imevunja Shirikisho la soka nchini humo na rais wa Shirikisho hilo Nick Mwendwa kukamatwa kwa madai ya ufisadi. Tunachambua hili na mengine mengi yanayotokea viwanjani barani Afrika na kwingineko duniani.

kenya afrika soka baada michezo mchezo wizara
Siha Njema
Ugonjwa wa fistula waendelea kuwaathiri kina mama waliobakwa nchini DRC

Siha Njema

Play Episode Listen Later Nov 2, 2021 8:39


Wizara ya afya nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo pamoja na baadhi ya mashirika yasiyokuwa ya kiserikali wameendelea kuwahimiza wamama waliobakwa katika eneo lenye mizozo ya kivita huko mashariki ya nchi hiyo na baadaye kukumbwa na ugonjwa wa Fistula, kujitokeza katika kushiriki kampeini ya tiba bure. Miongoni mwa mashirika hayo ni pamoja na FISPRO lenye makao yake jijini Kinshasa na pia mjini Butembo, ambako inaarifiwa wamama hao bado wamekuwa wakijificha.  

mama congo kina kinshasa fistula jamhuri butembo ugonjwa miongoni wizara
Uchumi na Biashara
Uchumi na Biashara Podcast; COVI-19, pigo kwa sekta ya hoteli

Uchumi na Biashara

Play Episode Listen Later Oct 7, 2021 8:53


Athari za virusi vya korona zinazidi kushuhudiwa katika sekta mbalimbali hasa zinazotegemewa na Wakenya, huku baadhi ya sekta hizo zikikadiria hasara kubwa au mapato ya chini ikilinganishwa na hapo awali. Mwanahabari wetu wa Kunti ya Taita Taveta, Rajab Kafuta amezuru baadhi ya hoteli za kitalii katika Mbuga ya Wanyamapori ya Tsavo, na kufanya mahojiano na Willie Mwadilo ambaye ni Meneja wa Hoteli za Taita Hills. Mwadilo ameweka wazi jinsi hali ilivyokuwa kabla ya taifa hili kukumbwa na korona na hali ilivyo kwa sasa ikizingatiwa maagizo yaliyowekwa na Wizara ya Afya kudhibiti virusi hivyo. Kuu linalojitokeza katika mahojiano haya ni kwamba sekta hiyo ingali inakadiria hasara ya mamilioni ya fedha na kuna haja ya masharti kulegezwa ili kuikwamua.

tsavo sekta kunti kuu afya hoteli biashara wizara
Habari za UN
Wakimbizi 51 waki Afghan wawasili nchini Uganda

Habari za UN

Play Episode Listen Later Aug 25, 2021


Serikali ya Uganda imethibitisha kupokea awamu ya kwanza ya wakimbizi kutoka Afghanistan asubuhi leo. Hiii ni ya kutimiza ahadi yake iliofuatia ombi la Marekani la kuhufadhi wakimbizi Zaidi ya 2,000 kutoka Afghanistan kwa muda. Hii hapa maelezo Zaidi katika ripoti ilioandaliwa na mwandishi wetu wa Uganda. (Taarifa ya John Kibego) Taarifa iliotolewa na wizara ya mambo ya kigeni ya Uganda inasema kuwa raia 51 wa Afghanistani wamewasili kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Enteebbe asubuhi ya leo kwa za Afrika Mashariki. Wakimbizi hao wakiwemo wanwake, watoto na wanaume ni sehemu ya wakimbizi Zaidi ya 2,000 wanaotarajiwa kuwasili huku Uganda kutoka Afghanistan kutokana na kuzorota kwa hali ya usalama nchini mwao. Wizara ya mambo ya nje ya Uganda imeongeza kuwa Waganda waliotarajiwa kuja kwneye ndege hiyohiyo hawakuweza  kuipanda kutokana na changamoto za usalama mjini Kabul. Wanatarajiwa kusfirishwa pamoja na wakimbizi wengine katika awamu zijazo. Maafisa wa serikali kutoka ofisi yawaziri mkuu wameonekana wakishirikiana na maafisa wa mashirika ya kibinadamu ya Umoja wa Mataifa kuwapatiachakula na huduma zingine za kujisafi wakimbizi hao kwneye migahawa mjini Entebbe. Taafia kuhusu makaazi ya wakimbizi ambapo Wafghanistan hao watapelekwa baado zinasubiriwa.  

afghanistan uganda afghan kabul zaidi umoja entebbe hiii hii mataifa serikali marekani afrika mashariki wizara
Msasaonline
KENYA: MUDA WA WANANCHI KUTOTOKA NDANI WAONGEZWA KWA SIKU 30.

Msasaonline

Play Episode Listen Later Aug 27, 2020 1:37


Katika jitihada za kudhibiti maambukizi ya Covid-19, Rais Uhuru Kenyatta ameongeza muda wa wananchi kutotoka ndani kuanzia saa 3 usiku hadi saa 10 alfajiri kwa siku 30. Akihutubia Taifa kutoka Ikulu, amesema baa zitaendelea kufungwa kwa siku 30 huku akiagiza Wizara ya Afya kukutana na wamiliki ili kupata muongozo sahihi wa kuzifungua. Aidha, Rais Kenyatta ameongeza idadi ya watu wanaoweza kuhudhuria misiba na harusi kutoka 15 iliyokuwepo awali hadi 100.Migahawa itafungwa saa 2 usiku baada ya saa 1 usiku kuanzia kesho. Pia, Rais amezitaka Wizara za michezo na Afya kuandaa miongozo ya pamoja ili kurejesha shughuli za michezo nchini humo. Kama utakumbuka siku mbili zilizopita ndani ya Taifa hilo kulikuwa na taarifa za madarasa ya shule binafsi kwasasa yanatumiwa kufugia kuku kutokana na shule kufungwa mpaka mwezi Januari, 2021. Kenya imerekodi visa 33,016 na vifo 564 huku idadi ya wagonjwa waliopona ikiwa 19,296.

Msasaonline
CHINA YAIAMURU MAREKANI KUFUNGA OFISI YAKE YA KIDIPLOMASIA CHENGDU.

Msasaonline

Play Episode Listen Later Jul 26, 2020 1:35


Wizara ya mambo ya nje ya China,imeiamuru Marekani kufunga jengo lake la kidiplomasia lililopo Chengdu China, Uamuzi umekuja baada ya Marekani kufunga ofisi ya kidiplomasia ya China iliyopo Texas, Marekani. Kufungiana ofisi za kidiplomasia linaonekana kuwa suala linalozidi kuleta utengano kwa Mataifa hayo ambayo awali yalianza kwa kuwekeana vikwazo katika upatikanaji wa VISA,na kuongeza sheria kwa wanaosafiri kidiplomasia. Awali, Marekani ililaumu ofisi za China wanasaidia wizi wa kijeshi unaoiba tafiti za wamarekani.pia, walilaumu watu wa ofisi hizo kutumia majina yasiyo halisi katika kufanikisha suala la kuiba taarifa za kiintelijensia. Maafisa wa China wanasema utawala wa Rais Trump unaonyesha chuki ya wazi kwa wachina na wamelaumu Pompeo kwa kuendeleza itikadi ya vita baridi. Vile vile China imemkosoa waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani Mike Pompeo, akimtuhumu kusambaza uongo wa kisiasa kuhusu China. Pompeo aliishutumu China kwa kuendesha kambi ya watu wengi katika jimbo la magharibi la Xinjiang, na wizi wa taarifa za kitaaluma na siri za kibiashara. Wang aliwashutumu wanasiasa wa sasa wa Marekani kwa kuchochea makusudi kile alichokiita "Mabishano ya kiitikadi" kati ya nchi hizo mbili, ili kubadili mkondo wa mtazamo wa raia wa Marekani.

texas china visa wang vile xinjiang pompeo chengdu yake mataifa chengdu china marekani wizara
Msasaonline
CHINA: YATANGAZA HATUA MPYA DHIDI YA VYOMBO VYA HABARI VYA MAREKANI.

Msasaonline

Play Episode Listen Later Jul 3, 2020 1:25


Serikali ya China imeyataka mashirika manne ya habari ya Marekani kutoa maelezo ya kina kuhusu opereseheni zao nchini China ikiwa ni hatua ya kulipiza kisasi katika ugomvi wao wa vyombo vya habari na utawala wa Trump. Mashirika hayo ya Associated Press United Press International, CBS News na National Public Radio yanahitajika kufichua taarifa kuhusu wafanyakazi wao, taarifa za kifedha, opereseheni zao pamoja na mali isiyohamishika nchini China katika siku 7 zijazo. Msemaji wa Wizara ya mambo ya kigeni ya China, Zhao Lijian amesema maelezo hayo ni muhimu ili kukabiliana na hatua ya Marekani ya kuvikandamiza vyombo vya habari vya nchini China, Marekani. Mwezi uliopita Marekani iliamuru kuwa mashirika manne ya habari ya serikali ya China, China Central Television, China News Service, Peoples Daily na Global Times kujisajili kama ujumbe wa kigeni, hivyo kukabiliwa na masharti sawa na ofisi za kibalozi nchini Marekani. Nchi hizo mbili zimezozana kuhusu Opereseheni za vyombo vya habari kwa miezi kadhaa, wakati kukiwa pia na mvutano wa mambo ya kibiashara, mlipuko wa virusi vya Corona na uhuru wa Hong Kong.

donald trump china corona hong kong cbs news national public radio global times habari nchi hatua mwezi serikali marekani china central television zhao lijian wizara mashirika