Fahamu masuala kadha wa kadha kuhusu uchumi kama vile, namna ya kupambana na umaskini, mfumuko wa bei, kushamiri kwa matumizi ya dola na athari za kuyumba kwa uchumi wa dunia kwa nchi za Afrika. Mada hizi zinafanyiwa utafiti wa kina na zinazungumzwa kwa
Msikilizaji wiki iliyopita katika makala ya Gurudumu la Uchumi, tulianza na sehemu ya kwanza ya mada kuhusu namna teknolojia inavyoweza kuhusihwa kwenye biashara kutatua changamoto zinazolikabili bara la Afrika, ikiwemo biashara ya kidijitali kuchochea utangamano, kuongeza ufanisi na kuleta maendeleo.Leo nakuletea sehemu ya pili ya mazungumzo yangu na Ali Mkimo, mchambuzi na mtaalamu wa masuala ya uchumi na biashara akiwa Tanzania.
Leo Katika makala ya gurudumu la uchumi tunakuletea sehemu ya kwanza ya mada kuhusu namna teknolojia inavyoweza kuhusihwa kwenye biashara kutatua changamoto zinazolikabili bara la Afrika, ikiwemo biashara ya kidijitali kuchochea utangamano, kuongeza ufanisi na kuleta maendeleo.Leo nakuletea sehemu ya kwanza ya mazungumzo yangu na Ali Mkimo, mchambuzi na mtaalamu wa masuala ya uchumi na biashara akiwa Tanzania.
Katika Makala ya Gurudumu la uchumi juma hili, tunatuama nchini Kenya, na tunaiangazia jamii ya Wanandi, ambapo kama ilivyo kwa mataifa mengi ya kiafrika, wanawake hawapewi nafasi ya kumiliki mali kama ardhi, mifugo – hasa ng'ombe wa maziwa – hali ambayo imesababisha uduni wa maendeleo ya kiuchumi miongoni mwao.Kufahamu kwa undani, ungana na Emmanuel Makundi na Victor Moturi, ambaye alizuru eneo la Nandi na kuandaa makala haya.
Msikilizaji wakati dunia ilipoazimisha siku ya kimataifa ya wafanyakazi, viongozi barani Afrika na hasa kwenye ukanda wa Afrika Mashariki walitangaza nyongeza ya mshahara huku wengine wakitoa ahueni ya ushuru wa mapato. Kwenye makala ya Gurudumu la uchumi juma hili, tunaangazia kodi ya lipa kadiri unavyopata (PAYE) kwa wafanyakazi na waajiri. Kuzungumzia hili msikilizaji kwenye line ya simu nimemualika Ali Mkimo, mtaalamu na mchambuzi wa masuala ya uchumi na biashara akiwa Tanzania.
Mizozo ya kibiashara kati ya nchi wanachama wa jumuiya za kikanda kama zile zilizoko SADC na EAC, ina athari endelevu kwa uchumi, biashara na jamii kiujumla.Mfano hivi karibuni Tanzania iliingia katika mvutano na nchi za Malawi na Afrika Kusini, zote zikiwa ni wanachama wa SADC, aidha wakati fulani Tanzania, Kenya na Uganda zilishawahi kuvutana.Ali Mkimo mchambuzi wa masuala ya uchumi na biashara anadadavua hili kwa kina kwenye makala ya wiki hii.
Katika juhudi za kuimarisha ubunifu na ushindani wa kilimo biashara barani Afrika, Kenya kwa kushirikiana na Ufaransa zimeanzisha mpango wa mafunzo ya matumizi ya teknolojia kwa wakulima wanawake, yakiangazia Akili Mnemba (AI) kuongeza thamani ya mazao, mpango umefikia zaidi ya vikundi na mashirika 1200 ya wanawake wakulima na kuwawezesha kutumia teknolojia za kisasa kuongeza ubora, usindikaji na masoko.
Msikilizaji kwa majuma kadhaa sasa, kumekuwa na mjadala duniani kote kufuatia uamuzi wa rais wa Marekani, Donald Trump, kutangaza ushuru wa bidhaa zinazoingia kwenye taifa hilo, mataifa ya Afrika yakiwa miongoni mwa waathirika, baadhi wakiwekewa ushuru wa hadi asilimia 50. Hata hivyo juma lililopita, rais Trump alitangaza kusitisha kwa muda wa siku 90 utekelezwaji wa ushuru kwa baadhi ya mataifa isipokuwa Uchina, ambayo imewekewa ushuru wa zaidi ya asilimia 125.Katika sehemu hii ya pili ya makala ya wiki hii, tumezungumza na Ali Mkimo, mtaalamu na mchambuzi wa masuala ya uchumi na biashara.
Msikilizaji takwimu zinaonesha kuwa, ifikapo mwaka 2050, idadi ya watu barani Afrika itaongezeka kufikia bilioni 2.5, ambapo zaidi ya nusu ya watu hawa watakuwa ni vijana walio na umri wa chini ya 25. Hata hivyo Ujasiriamali wa vijana unaonekana kama suluhisho linalowezekana kwa changamoto hii. Msikilizaji juma hili nimebahatika kuwa na mgeni studioni nae si mwingine bali ni Kenneth Ochien'g, ambaye yeyé anajihusisha na uchakataji upya wa taka za plastiki kwa matumizi mengine.
Msikilizaji takwimu zinaonesha kuwa, ifikapo mwaka 2050, idadi ya watu barani Afrika itaongezeka kufikia bilioni 2.5, ambapo zaidi ya nusu ya watu hawa watakuwa ni vijana walio na umri wa chini ya 25. Hata hivyo Ujasiriamali wa vijana unaonekana kama suluhisho linalowezekana kwa changamoto hii. Msikilizaji juma hili nimebahatika kuwa na mgeni studioni nae si mwingine bali ni Kenneth Ochien'g, ambaye yeyé anajihusisha na uchakataji upya wa taka za plastiki kwa matumizi mengine.
Msikilizaji juma moja lililopita, mtandao wa wafanyabishara na makampuni ya Ufaransa hapa nchini Kenya, walikutana na wenzao wa Kenya kuangalia namna bora zaidi ya kushirikiana hasa katika masuala ya teknolojia. Kwa mujibu wa takwimu zilizoko hali ya biashara za mtandaoni kikanda inaendelea kuimarika, huku matarajio ya matumizi ya akili mnemba yakionekana kuleta mageuzi makubwa katika sekta hiyo. Victor Moturi alizungumza na Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia wa Kenya, William Kabogo.
Wiki hii katika makala ya Gurudumu la Uchumi, tunajadili changamoto za upatikanaji wa nishati ya uhakika barani Afrika, ambapo pamoja na baadhi ya mataifa kuwa na rasilimali za kutosha kuzalisha nishati ya ziada, suala la miundombinu limeendelea kusalia kikwazo, ambapo baadhi ya mataifa yanalazimika kununua nishati toka mataifa jirani.Ali Mkimo, mchambuzi na mtaalamu wa masuala ya Uchumi atakuwa nasi kudadavua hili kwa kina.
Katika makala ya Gurudumu la Uchumi juma tunajadili athari za kibiashara kimataifa kutokana na hatua ya hivi karibuni ya Marekani kutangaza vikwazo vya kikodi kwa mataifa ya Canada, Mexico, India na Uchina ambao ni washirika wake wakubwa kibiashara.Kujadili hili, kwenye line ya simu tunaungana na Profesa Wetengere Kitojo, mchambuzi wa masuala ya uchumi na biashara akiwa Tanzania.
Msikilizaji juma lililopita tulianza kwa kujadili yaliyotokana na mkutano wa wakuu wa nchi za Afrika, na suala kuu lilikuwa ni je, nchi za Afrika zitafanikiwa kushinikiza mabadiliko katika taasisi za kifedha za kimataifa na kuondokana na mikopo na madeni yasiyostahimilika ?Leo katika makala ya Gurudumu la Uchumi, nakuletea sehemu ya pili ya mjadala huu, nimemualika Ali Mkimo, mtaalamu namchambuzi wa masuala ya uchumi na biashara akiwa nchini Tanzania.
Msikilizaji mwishoni mwa wiki iliyopita, viongozi wa Afrika waliokutana mjini Addis Ababa, Ethiopia, walikubaliana kuongeza kasi ya kudai mabadiliko kwa mifmo ya kifedha ya kimataifa, ili kuziwesha kuwa na nafasi katika maamuzi. Afrika inalalamika kutokuwepo usawa, na hivyo kuyaweka mataifa ya Afrika katika hali ya kutegemea mikopo yenye masharti magumu.Makala ya Gurudumu la uchumi juma hili, tunajadili ikiwa azma hii ya viongozi wa Afrika itafanikiwa.
Hujambo msikilizaji wa RFI Kiswahili popote pale unapotegea sikio matangazo yetu, makala ni Gurudumu la Uchumi na leo hii tunazungumzia kuhusu athari za kiuchumi kutokana na mizozo kwenye nchi za Afrika.Tutazungumza na Hamduni Marcel, mchambuzi wa siasa za kimataifa akiwa Tanzania na Ali Mkimo, mchambuzi wa masuala ya uchumi akiwa Tanzania.
Juma hili katika makala ya Gurudumu la Uchumi, tunajadili kuhusu athari za hatua ya Marekani kusitisha kwa muda utoaji wa misaada ya nje. Uamuzi huu tayari umeonekana kutishia baadhi ya sekta zilizokuwa zinasaidiwa kupitia USAID kama vile Afya na Elimu.Tumezungumza na Ali Mkimo, mchambuzi wa masuala ya uchumi na biashara akiwa Tanzania.
Juma hili viongozi wa nchi za Afrika walikutana Tanzania, kujadili namna bora ya kuhakikisha raia wake wanaunganishwa na nishati ya uhakika, endelevu na nafuu ifikapo mwaka 2030.Takwimu zinaonesha raia zaidi ya milioni 600 hawana umeme, bilioni 1 hawatumii nishati safi na salama.Makala ya Gurudumu la Uchumi juma hili imezungumza na Walter Nguma, mchambuzi wa masuala ya uchumi akiwa Tanzania, kuangazia changamoto zinazokwamisha upatikanaji wa nishati, fursa zilizopo.
Msikilizaji ripoti mpya ya shirika la kupambana na umasikini Oxfam, inaonesha kuwa utajiri wa mabilionea uliongezeka mara tatu zaidi katika mwaka uliopita, ikiwa ni zaidi ya ilivyokuwa mwaka 2023.Katika makala ya Gurudumu la Uchumi, tumezungumza Ali Mkimo, mchambuzi wa masuala ya uchumi na biashara, kuangazia kwa kina ripoti hii na athari ya kuendelea kushuhudiwa kwa pengo la matajiri na masikini.
Teknolojia bunifu ya biashara ndogo ndogo imekuwa ikijulikana kuwa ya watu waliojiweza katika jamiii kutokana na gharama yake ,hali ambayo inawafungia nje watu hasa vijana kutoka maeneo duni na vijijini hivyo kukosa kuimarika kibiashara na kiuchumi kupitia teknolojia hizo .Lakini hata hivyo vijana pamoja na mashirika mbalimbali mtaa wakibera jijini Nairobi Kenya wapata fursa ya mafunzo na kuimarika kibiashara
Hivi leo ni sehemu ya pili ya makala ya Gurudumu la Uchumi, hasa tunapouanza mwaka 2025 tunaenda kujadili kuhusu nidhamu ya kuweka akiba ya fedha, ufanye nini kuongeza kipato, unatumiaje fedha ulizonazo kuwekeza ? Haya ni baadhi ya mambo ambayo tutaenda kuyatazama kwenye makala ya juma hili. Tutakuwa na Ali Mkimo, mchambuzi na mtaalamu wa masuala ya uchumi na biashara akiwa Tanzania.
Heri ya mwaka mpya 2025 msikilizaji wa RFI Kiswahili popote pale unapotegea sikio matangazo yetu na hasa makala ya Gurudumu la Uchumi, ni imani yetu kuwa nyote mbuheri wa afya. Makala ya Gurudumu la Uchumi, tutajadili kuhusu nidhamu ya kuweka akiba ya fedha. Kuzungumzia hili msikilizaji kwenye line ya simu nimemualika Ali Mkimo, mchambuzi na mtaalamu wa masuala ya uchumi na biashara akiwa Tanzania.
Katika makala ya hivi leo, tunajadili kuhusu umuhimu wa kuwa na nidhamu ya fedha, kwanini ipo haja ya kuwa na nidhamu ya matumizi binafsi, vipi unaweza kujipanga kwa mwaka ujao? Haya ni miongoni mwa maswali ambayo mtaalamu wetu wa uchumi na biashara Ali Mkimo anaenda kuyajibu.
Makala haya yanazungumzia hatua za wanawake na wasichana katika eneo la Opapo, Kaunti ya Migori nchini Kenya, kwa msaada wa mashirika yasiyo ya kiserikali na serikali ya kaunti, wameanzisha kiwanda cha kuchakata samaki, kuboresha biashara ya samaki, na kuongeza thamani kwa kutengeneza bidhaa kama soseji na baga,hivyo kuinua uchumi
Msikiliza mataifa 54 ya Afrika yametia saini mkataba wa biashara huria barani Afrika, mataifa 48 yakitia saini itifaki kuanza kuutekeleza. Huu ni moja ya mikataba mikubwa ya kibiashara duniani, ukitarajiwa kuwaondoa raia milioni 30 kutoka kwenye umasikini na kuongeza mapato ya bara hil hadi kufikia dola bilioni 450 ifikapo mwaka 2030.Kuangazia kwa kina mkataba huu pamoja na hali ya madeni ya nchi za Afrika, tumezungumza na Ali Mkimo, mtaalamu na mchambuzi wa masuala ya uchumi akiwa Tanzania.
Msikilizaji kwa muda sasa, eneo la pwani ya Kenya limekuwa likikabiliwa na kiwango kikubwa cha matumizi ya dawa za kulevya miongoni mwa vijana, Hali hii ikichangia vitendo vya utovu wa nidhamu, kuongezeka kwa magonjwa ya zinaa na ndoa za mapema. Hata hivyo, kutokana na juhudi za mashirika mbalimbali ya kijamii na yasiyo ya kiserikali, vijana wengi walioacha kutumia dawa za kulevya sasa wanajihusisha na miradi ya kibiashara ili kujikimu.Makala ua Gurudumu la Uchumi juma hili, inawaangazia vijana wa eneo la Pwani ambao wameamua kuachana na matumizi ya dawa za kulevya.
Msikilizaji kwa muda sasa mataifa ya Afrika yameendelea kupitia changamoto za kifedha, kuanzia katika kukusanya mapato na matumizi kwa ajili ya maendeleo yake, hali ambayo imesababisha nchi nyingi kujikuta pabaya kutokana na kulazimika kukopa fedha toka kwa taasisi za kimataifa au nchi zilizoendelea huku ziklipa riba kubwa katika urejeshaji.Lakini je, kuongza kodi ndio suluhu? Mchambuzi wa masuala ya uchumi kutoka Tanzania, Ali Mkimo anafafanua.
Mataifa ya Afrika yameendelea kupitia changamoto za kifedha, katika kukusanya mapato kwa ajili ya maendeleo, hali ambayo imesababisha nchi nyingi kujikuta pabaya kutokana na kulazimika kukopa fedha toka kwa taasisi za kimataifa au nchi zilizoendelea huku ziklipa riba kubwa katika ureje shaji.Lakini je, kuongeza wigo wa kodi kwa mataifa yanayoendelea ndio njia pekee kuwezesha mataifa haya kujikwamua kiuchumi? Tumezungumza na Ali Mkimo, mchambuzi na mtaalamu wa masuala ya uchumi akiwa Tananzania
Msikilizaji dunia inashuhudia ongezeko kubwa la idadi ya watu katika miongo 6 iliyopita, ambapo mwaka 1960 idadi ilikuwa bilioni 3 lakini katika miongo miwili tu hadi mwaka 1982 ilikuwa imevuka watu bilioni 5 na November mwaka 2022 kulikuwa na watu bilioni 8 duniani.Makala ya Gurudumu la Uchumi juma hili, tunajadili Athari za Kiuchumi kutokana na ongezeko la watu barani Afrika: Changamoto na fursa.Tumezungumza na Walter Nguma, mchambuzi wa masuala ya uchumi akiwa Tanzania
Tatizo la fedha haramu barani Afrika linaligharibu bara hili kiasi cha dola za Marekani bilioni 50 na bilioni 80 kila mwaka, Asilimia 44 ya utajiri wa kifedha wa Afrika inadhaniwa kuwa nje ya nchi. Kwa mujibu wa Ripoti ya Maendeleo ya Uwazi wa Ushuru barani Afrika ya 2023, nchi za Afrika zimeokoa dola bilioni 2 kwa mwaka kutokana na watu kuweka wazi mapato yao, ubora wa kubadilishana taarifa na uchunguzi wa nje ya nchi.Tumezungumza na Ali Mkimo, mtaalamu na mchambuzi wa masuala ya uchumi na biashara akiwa Tanzania.
Msikilizaji kwa mujibu wa benki ya dunia, ni asilimia 49 tu ya watu wazima wanamiliki akaunti benki, takwimu za hivi karibuni zikionesha ongezeko la asilimia 55 mwaka 2021 kutoka asilimia 43 mwaka 2017, hata hivyo kiwango hiki kikiwa kidogo ukilinganisha na wastani wa kidunia wa asilimia 76. Makala ya Gurudumu la Uchumi, juma hili tunajadili kuhusu huduma jumuishi za mifumo ya kifedha barani Afrika. Machambuzi wa masuala ya uchumi ALI MKIMO anajibu maswali kadhaa kuhusu sekta hii.
Msikilizaji juma lililopita Rwanda ilikuwa mwenyeji wa kongamano la mfumo wa chakula barani Afrika, ambapo wadau zaidi ya elfu 4 kutoka kila pembe ya mataifa ya Afrika walishiriki.Mkutano uliangazia kuhusu mifumo ya chakula, mbinu bora na teknolojia ambazo zinaweza kubadilisha mifumo ya kilimo na chakula barani Afrika na wakati huohuo kutengeneza nafasi za kazi na fursa kwa wanawake.Msikilizaji wiki hii nimeshirikiana na mwanahabari wetu wa Kigali, Christopher Karenzi;
Uchina wiki hii imekuwa mwenyeji wa mkutano kati yake na viongozi wa Afrika, kwa mujibu wa takwimu zilizoko, China ni taifa la pili duniani kufanya biashara nyingi zaidi na bara la Afrika, biashara inayokadiriwa kufikia dola za Marekani bilioni 167 kwa mwaka. Kuangazia mkutano huu na wasiwasi ulioko kuhusu uwekezaji wa China barani Afrika, tumezungumza na Ali Mkimo, mchambuzi wa masuala ya uchumi na biashara akiwa Tanzania.
Kwa wastani, wanawake hufanya angalau mara mbili na nusu zaidi ya kazi za nyumbani zisizo na malipo kuliko wanaume. Zaidi ya hayo, wanawake hutumia saa 4 na dakika 30 kwa siku kwa kazi ya matunzo bila malipo, ikilinganishwa na saa 1 dakika 20 kwa wanaume katika nchi zinazoendelea.Makala ya Gurudumu la uchumi wiki hii tunajikita kule mashariki mwa nchi ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, ambako baadhi ya wanawake kwenye mji wa Goma, sasa wanalazimika kuponda mawe kujikimu na familia zao.
Msikilizaji asilimia 70 ya watu katika mataifa ya Afrika yaliyoko Kusini mwa Jangwa la Sahara wana umri wa chini ya miaka 30, hata hivyo ni hatari ikiwa mataifa yatashindwa kuhakikisha vijana wana nafasi nzuri za maisha, kwakuwa Vijana wana haki sio tu ya afya bora, lishe bora na elimu, lakini fursa za uhuru na kazi nzuri.Kuzungumzia mada hii hivi leo, kwa njia ya simu nimemualika Ali Mkimo, mtaalamu na mchambuzi wa masuala ya uchumi na biashara akiwa nchini Tanzania.
Msikilizaji kwa mujibu wa Jukwaa la dunia la uchumi, World Economic Forum, ujio wa teknolojia mpya kama akili mnemba (Artuificial inteligency), ikiwa zitatumika vizuri, zitasaidia kujenga uchumi wenye ushindani, unaostahimili changamoto na endelevu.Katika makala ya gurudumu la uchumi juma hili, tunajadili Kuibuka au ugunduzi wa teknolojia na ushawishi wake katika kukuza uchumi.
Msikilizaji juma hili katika makala ya Gurudumu la uchumi nakuletea mseto wa taarifa za uchumi na biashara toka kwenye kanda ya Afrika Mashariki, katika Makala ya leo mwenzangu victor Abuso, alizungumza na Christian Yoka, mkurugenzi wa shirika la maendeleo la Ufaransa, AFD kanda ya Afrika, lakini pia mwandishi wetu wa Lubumbashi, Denise Mayoo, alizuru mji wa Kalemie nchini DRC ulioathirika pakubwa na mafuriko, ambako shughuli za biashara na uchimi zimeathiriwa pakubwa.
Msikilizaji katika miaka ya hivi karibuni, mataifa ya Ulaya, Amerika, Asia na sasa Uarabuni, yameongeza kasi ya uwekezaji, utoaji wa mikopo na misaada kwa nchi za Afrika, mataifa haya yamewekeza mabilioni ya dola za marekani kwa bara hilo kwa kubadilishana na rasilimali zake, hatua ambayo mbali na kuonekana kama ni urafiki lakini inaibua maswali kuhusu nia hasa ya nchi hizo kwa bara la Afrika. Ni juma hili tu, Korea Kusini kwa mara ya kwanza imefanya kongamano na viongozi wa Afrika, ambapo imetangaza msaada wad ola za marekani bilioni 10 kwa ajili ya maendeleo ya kiuchumi na biashara kati yake na nchi hizo. Makala ya Gurudumu la uchumi juma hili, tunaangazia kasi hii mpya ya nchi za magharibi kwa bara la Afrika, tukijiuliza maswali kadhaa, je nia yao ni safi? Na vipi Afrika inaweza kutumia fursa hii kujikwamua kiuchumi?
Msikilizaji kwa wiki kadhaa sasa nchini Kenya, kumekuwa na mjadala mkali baada ya kutolewa kwa mapendekezo ya serikali kuhusu muswada wa fedha wa mwaka 2024 unaolenga kuongeza kodi katika baadhi ya sekta na bidhaa nchini humo.Wazalishaji na wawekezaji wakitarajiwa kuwa waathiriwa wakbwa ikiwa muswada huu utapitishwa kama ulivyo, ambapo baadhi ya vinavyolalamikiwa na wazalishaji ni nyongeza ya ushuru wa thamani katika malighafi kutoka nje pamoja na tozo za mazingira maarufu kama Eco Levy. Sekta ya uzalishaji wa viwanda inatarajiwa kuchangia asililia 20 katika pato ghafi la taifa hadi kufikia mwaka 2030. Makala ya Gurudumu la uchumi juma hili, imezungumza na mwenyekiti wa shirikisho la wazalishaji nchini Kenya, Antony Mwangi, kuangazia changamoto na faida za muswada huu. Jina langu ni Emmanuel Makundi, karibu. Msikilizaji nilianza kwa kumuuliza Antony, wao wanautazamaje muswada huu? Insert /// Msikilizaji kama umeungana nasi Makala ni Gurudumu la uchumi na leo tunaujadili muswada wa fedha nchini Kenya unaoelnga kuongeza ushuru wa bidhaa na wazalishaji, na tunazungumza na Antony Mwangi, mwenyekiti wa shirikisho la wazalishaji nchini Kenya. Insert /// Kufikia hapa ndio tunatia nanga ya Makala ya Gurudumu la uchumi kwa juma hili, shukrani kwa Antony Mwangi, mwenyekiti wa shirikishi la wazalishaji nchini Kenya, usikose kuungana nami katika makala nyingine wiki ijayo, ulikuwa nami Emmanuel Makundi, kwaheri.
Msikilizaji wakati wa kongamano la kimataifa la wakurugenzi wakuu wa kampuni mbalimbali duniani waliokutana nchini Rwanda, maswali kadhaa yaliibuliwa, kubwa lilikuwa ni je bara la Afrika linapaswa kuwa katika meza ya maamuzi au kwenye orodha, na ikiwa huu ni muda muafaka wa kutoa mustakabali wake. Ni maswali magumu ambayo hata hivyo viongozi wa Afrika walioshiriki, wanakubaliana kuwa bara hili lina rasilimali zakutosha kubadili uelekeo wake na maendeleo kwa raia, lakini pia halipaswi kuwa linaomba kwa viongozi wa magharibi kuwa katika meza ya majadiliano kuhusu mustakabali wa uchumi na maendeleo ya dunia. Suala la mabadiliko ya tabia nchi na utekelezaji wa mkataba wa biashara huria wa bara hili, maarufu kama AfCFTA, liliibuka, ambapo licha ya utiwaji saini itifaki yake, bado kuna vikwazo vya kufanya biashara baina ya nchi za Afrika.
Hujambo msikilizaji wa rfikiswahili popote pale unapotegea sikio matangazo yetu nikukaribishe katika makala ya Gurudumu la Uchumi, na hivi leo tunaangazia ukanda wa Afrika Mashariki, eneo lililojaa nguvu kazi ya vijana pamoja na ari ya ujasiriamali, lakini bado linakabiliwa na tatizo la ukosefu wa ajira. Takwimu za hivi karibuni za benki ya dunia zinaonesha uhalisia wa tatizo, takwimu zikitofautiana baina ya nchi na nchi, lakini kiujumla ni kuanzia kati ya asilimia 4 hadi 19 ya vijana hawana ajira, huku wanawake walioko vijijini wakiwa waathirika wakubwa. Katika makala haya hivi leo, tutaangazia kwa kina namna gani bora ya kukabiliana na tatizo la ajira na kuongeza wajasiriamali wengi zaidi kwenye ukanda. Kwenye line ya simu nimewaalika, Ali Mkimo, yeye ni mchambuzi wa masuala ya Uchumi pamoja na Emmanuel Cosmas, kijana mbunifu wa masuala teknolojia na nibalozi wa UNICEF, wote hawa wakiwa nchini Tanzania.
Makala ya Gurudumu la Uchumi juma hili, inaangazia mchango na changamoto ya biashara ndogondogo na zile za kati kwenye nchi za Afrika Mashariki.Matayarishaji amezungumza na wafanyabiashara wadogowadogo na kati nchini Kenya, lakini mchambuzi wa masuala ya uchumi Ally Mkimo.
Msikilizaji katika miaka ya hivi karibuni, wito umeendelea kutolewa na mataifa ya Afrika kuhusu kuwepo usawa na haki katika mfumo wa kifedha duniani, ambao Kihistoria, nchi za Kiafrika zimekuwa katika hali mbaya linapokuja suala la kupata ufadhili, rasilimali, na makubaliano yenye usawa ya kibiashara.Kuzungumzia hili, nimemualika kwa njia ya simu kutoka Tanzania, Walter Nguma, mtaalamu na mchambuzi wa masuala ya uchumi na biashara.
Kulingana na Benki ya Maendeleo ya Afrika, uchumi wa bluu barani Afrika una uwezo wa kuchangia pakubwa katika ukuaji wa uchumi na maendeleo ya bara hilo.Uchumi wa bluu unatajwa kuchangia dola za Marekani trilioni 1 kila mwaka, Sekta ya uvuvi ikiwa kitovu kikuu na kuajiri zaidi ya watu milioni 12.Profesa Omary Mbura, mtaalamu na mhadhiri wa masuala ya uchumi kutoka chuo kikuu cha Dar es Salaam, anaangazia sekta hii.
Shughuli za sekta binafsi na uwekezaji ni vyanzo vikuu ya ukuaji wa uchumi, uzalishaji wa ajira na maendeleo endelevu.Kwa wastani, sekta binafsi inachangia zaidi ya Asilimia 80 ya mapato ya serikali kwa watu wa kipato cha chini na cha kati, kupitia kodi ya kampuni, kodi ya rasilimali na mapato ya kodi kwa wafanyakazi.Sekta hii inazalisha zaidi ya asilimia 90 ya ajira katika nchi zinazoendelea kiuchumi.
Makala ya Gurudumu la Uchumi, juma hili inaangazia kilimo cha matunda nchini Kenya, na namna wakulima wa nchi hiyo, wameendelea kukumbatia mbinu mpya za kilimo, uvunaji na usindikaji.
Uhamiaji unaweza kuwa nguzo muhimu kwa maendeleo ya uchumi wa Afrika ikiwa mtu anaweza kutoa mwelekeo bora wa fedha zinazotumwa na wageni kuelekea uwekezaji na ufadhili wa maendeleo katika nchi za Afrika.Diasporas wanachangia kwa kiasi kikubwa maendeleo ya kiuchumi na kijamii ya nchi zetu ambazo kimsingi ni nchi za asili lakini pia nchi mwenyeji. Wanafanya hivyo kwa kuhamisha pesa, ujuzi, teknolojia, mifano ya utawala, maadili, na mawazo. Serikali ya Senegal inafahamu mabadiliko yanayohitajika tunapojitahidi kutekeleza Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) na Mkataba wa Kimataifa wa Uhamiaji Salama, Ulio na Utaratibu na wa Kawaida nchini Senegali.
Makala ya Gurudumu la uchumi juma hili, tunaangazia namna maboreshi ya huduma ya Inteneti nchini Kenya imechochea maendeleo, biashara na ustawi wa watu.
Msikilizaji, hatimaye nchi ya Tanzania imeondoa zuio ililoweka juma hili kwa ndege za shirika la Kenya KQ, uamuzi iliyokuwa imeuchukua baada ya Nairobi kukataa kutoa kibali kwa ndege za mizigo za shirika la Tanzania kushusha na kupakia kutokea Kenya.Uamuzi huo msikilizaji ulisababisha mawaziri wa pande zote kukutana na Jumanne ya wiki hii wakakubaliana kumaliza tofauti zilizojitokeza na sasa safarai za ndege za Kenya na zile za Tanzania zitaruhusiwa.
Makala ya Gurudumu la uchumi juma hili inaangazia mustakabali wa jumuiya ya Afrika Mashariki kiuchumi kwa mwaka 2024, hasa baada ya athari za uviko 19 za tangu mwaka 2020 na sasa mdororo wa uchumi wa dunia, ambao umesababisha mataifa masikini, ikiwemo ya ukanda kushuhudia kupanda kwa gharama ya maisha.Nimezungumza na Johnson Denge, mchambuzi wa masuala ya uchumi akiwa nchini Kenya.
Makala ya Gurudumu la Uchumi juma hili, inaangazia namna wafanyabiashara wamejipanga katika mwaka 2024, kuhakikisha biashara zao zinashamiri licha ya changamoto za kiuchumi zinazoikabili dunia kwa sasa. Mwandishi wetuj Victor Moturi, kwa niaba ya mtayarishaji wa makala haya, Emmanuel Makundi, amezungumza na wafanyabiashara nchini Kenya, ambao mwaka uliopita, walilalama kupata changamoto za kifedha na hata upandaji wa bidhaa na kukosekana kwa dola.
Makala ya Gurudumu la uchumi juma hili inaangazia mustakabali wa jumuiya ya Afrika Mashariki kiuchumi kwa mwaka 2024, hasa baada ya athari za uviko 19 za tangu mwaka 2020 na sasa mdororo wa uchumi wa dunia, ambao umesababisha mataifa masikini, ikiwemo ya ukanda kushuhudia kupanda kwa gharama ya maisha.Nimezungumza na Johnson Denge, mchambuzi wa masuala ya uchumi akiwa nchini Kenya.