POPULARITY
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayomulika miaka miwili tangu kuzuka kwa vita kati ya Israel na wanamgambo wa kipalestina wa Hamas, vita ambavyo vimeacha maelfu ya watu wakiwa wamepoteza maisha na mamilioni wakikosa makazi, chakula na huduma za msingi.Leo ikiwa ni miaka miwili kamili tangu kufanyika mashambulizi ya Hamas Oktoba 7 mwaka 2023 Kusini mwa Israel na kuzusha vita vinavyoendelea sasa Gaza, mashirika ya kibinadamu ya Umoja wa Mataifa yametoa wito kutisishwa mapigano na mateka wote kuachiliwa. Mratibu mkuu wa misaada wa Umoja wa Mataifa Tom Fletcher amesema maumivu yanayosababishwa na mzozo huo hayaelezeki,”huku Kamishina Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la msaada kwa wakimbizi wa Kipalestina UNRWA Philippe Lazzarini akielezea vita inayoendelea Gaza kama jinamizi kwa watu wa Gaza.Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) limeelezea wasiwasi wake mkubwa kuhusu ongezeko kubwa la idadi ya watu waliolazimika kuyahama makazi yao kaskazini mwa Msumbiji. Hali hiyo inatokana na kuongezeka kwa machafuko ya mzozo unaoingia mwaka wa nane, hali iliyowalazimu karibu idadi ya watu 22,000 kukimbia makazi yao katika kipindi cha wiki moja tu mwishoni mwa mwezi Septemba. Tangu mzozo huo uanze mwaka 2017, zaidi ya watu milioni 1.3 wamelazimika kuyahama makazi yao.leo ni Siku ya Pamba Duniani na katika kuadhimisha siku hii mbunifu maarufu wa mitindo kutoka Niger, Alphadi, ameendesha darasa la kitaalamu kwa wanafunzi katika Chuo cha Mitindo cha Roma kusherehekea pamba na mitindo ya Kiafrika, kama sehemu ya matukio yaliyopangwa na Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) kusherehekea siku hii ambayo huadhimishwa kila mwaka Oktoba 7. Alphadi amesema “Kwangu mimi, hii ni njia ya kuonesha yote ambayo Afrika inaweza kufanya. Na naamini, kwangu mimi, hii ni njia inayofaa ya kuadhimisha bara letu, na pia kuthamini kazi na kuonesha nguvu ya Afrika. Pamba ya Kiafrika ni bidhaa ubora, na inaweza kutumika na watu wa Sahel, pamoja na Wazungu wa Ulaya, Wamarekani ulimwengu wote.”Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili hii leo, Mtaalam wetu Onni Sigalla, Mhariri mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania, BAKITA. Anafafanua maana za neno "TITIMA"Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayomulika ujumbe wa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki EAC, Veronica Nduva ambaye alizungumza na Flora Nducha kandoni mwa UNGA80. Pia tunakuletea muhtasari wa habari kama zifuatazo.Ikiwa ni zaidi ya miaka minane tangu zaidi ya wakimbizi 750,000 waislamu wa kabila la warohingya wakimbie Myanmar kuelekea kwenye kambi kubwa nchini Bangladesh, mgogoro huo bado haujapatiwa suluhisho na leo hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa viongozi wamekutana kusaka suluhu ya kudumu kwa warohingya na makabila mengine madogo nchini Myanmar. Katibu Mkuu Antonio Guterres kupitia Afisa Mtawala Mkuu wa UN Courtenay Rattray amesema, “mgogoro huu, ambao umezidi kuongezeka tangu mapinduzi ya kijeshi Myanmar ya mwaka 2021, unasigina haki za binadamu, utu na usalama wa mamilioni ya watu na unatishia uthabiti wa kikanda. Haitoshi tu kutathmini hali ilivyo. Tunapaswa pia kuendeleza mshikamano na kubuni suluhisho.”Amani nchini DRC imesalia bado ahadi, ni kauli ya Bintou Keita, Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC aliyotoa wakati akihutubia Baraza la Usalama lililokutana leo kujadili hali Mashariki mwa DRC. Anasema hali inazidi kuwa tete. “Ghasia zinaendelea kushamiri jimboni Kivu Kaskazini hususan eneo la Rutshuru tangu waasi wa M23 watwae eneo hilo. Kuanzia mwezi Juni na kuendelea ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani, MONUSCO umepokea maombi lukuki ya watu wakitaka ulinzi kwenye maeneo yanayodhibitiwa na M23.”.Na mashirika ya Umoja wa Mataifa leo yamesisitiza wito wa kupatikana kwa sitisho la mapigano huko Gaza, eneo la Palestina linalokaliwa kimabavu na Israel, ili kupunguza machungu wakati huu ambapo Mpango wa Marekani wa Vipengele 20 unaibua matumaini ya kukomeshwa kwa mapigano. Ricardo Pires, msemaji wa shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia watoto, UNICEF amesema, “ni muhimu tupate sitisho la mapigano na misaada iweze sio tu kuingia na kuepusha baa la njaa, bali pia kuelekezwa maeneo ya kusini. Lakini vile vile kuhakikisha watoto na familia zao wanapata malazi bora wakati huu majira ya baridi kali yanakaribia. La sivyo italeta zahma ya afya kwa watoto na familia zao.”.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
Matangazo ya nusu saa kuhusu habari za mapema asubuhi pamoja na habari za michezo.
Matangazo ya saa nzima kuhusu habari za kutwa, ikiwa ni pamoja ripoti kutoka kwa waandishi wetu sehemu mbali mbali duniani na kote Afrika Mashariki na Kati, na vile vile vipindi na makala maalum kuhusu afya, wanawake, jamii na maendeleo.
Hii leo jaridani tunaangazia leo Mjadala Mkuu wa ngazi ya juu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa UNGA80 tukimulika hotuba za viongozi na mikutano mingine ya pepmbezoni kuhusu malengo ya maendeleo enedelevu, SDGs.Viongozi wa mataifa ya nchi wanachama 16 waliopanda kwenye mimbari ya ukumbi wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa hii leo Jumatatu ya tarehe 29 Septemba 2025 ambayo ndio ukomo wa Mjadala Mkuu wa mkutano wa 80 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, (UNGA80) wamepaza sauti zao kuhusu masuala mbalimbali yanayokumba dunia hivi sasa ikiwemo vita Gaza, na hali ya kiuchumi Afrika.Leo Mjadala Mkuu wa ngazi ya juu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa UNGA80 hotuba za viongozi ukifunga pazia, Afrika imeweka bayana kauli moja ya mshikamano, kwamba lazima iwe na viti na sauti kwenye Baraza la Usalama na kuahidi kufanya kila liwezekanalo kuhakikisha dhamira hiyo inatimia. Mchakato ulishaanza na unaendelea kuelekea lengo hilo kama ambavyo Balozi Ekitela Lokaale mwakilishi wa kudumu wa Kenya kwenye Umoja wa Mataifa alivyomfahamisha.Tukisalia hapa katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa, kandoni mwa Mjadala Mkuu wa Mkutano wa 80 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, UNGA80, inafanyika mikutano mingine ya pembezoni kujadili masula mengine ya kusongesha maendeleo ya ulimwengu. Wiki iliyopita tulizungumza na Dkt. Ntuli Kapologwe Mkurugenzi Mkuu wa Jumuiya ya Afya ya Mashariki, Kati na Kusini mwa Afrika, ECSA wakati alipokuwa akisubiri kushiriki mkutano wa nchi wanachama wa jumuiya hiyo kujadili jinsi ya kusongesha diplomasia ya kisayansi ili kuhakikisha bara la Afrika haliachwi nyuma kwenye kukabiliana na changamoto za kiafya.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
Viongozi wa mataifa ya nchi wanachama 16 waliopanda kwenye mimbari ya ukumbi wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa hii leo Jumatatu ya tarehe 29 Septemba 2025 ambayo ndio ukomo wa Mjadala Mkuu wa mkutano wa 80 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, (UNGA80) wamepaza sauti zao kuhusu masuala mbalimbali yanayokumba dunia hivi sasa ikiwemo vita Gaza, na hali ya kiuchumi Afrika.
Matangazo ya nusu saa kuhusu habari za mapema asubuhi pamoja na habari za michezo.
Matangazo ya saa nzima kuhusu habari za kutwa, ikiwa ni pamoja ripoti kutoka kwa waandishi wetu sehemu mbali mbali duniani na kote Afrika Mashariki na Kati, na vile vile vipindi na makala maalum kuhusu afya, wanawake, jamii na maendeleo.
Matangazo ya saa nzima kuhusu habari za kutwa, ikiwa ni pamoja ripoti kutoka kwa waandishi wetu sehemu mbali mbali duniani na kote Afrika Mashariki na Kati, na vile vile vipindi na makala maalum kuhusu afya, wanawake, jamii na maendeleo.
Matangazo ya saa nzima kuhusu habari za kutwa, ikiwa ni pamoja ripoti kutoka kwa waandishi wetu sehemu mbali mbali duniani na kote Afrika Mashariki na Kati, na vile vile vipindi na makala maalum kuhusu afya, wanawake, jamii na maendeleo.
Hii leo ni hotuba ya Israeli kwenye mjadala mkuu wa baraza kuu, nini kilitokea? Kijana daktari mwanaharakati kutoka Ghana aishiye Uingereza akiwa UNGA80 na matumaini mapya ya kinga dhidi ya maambukizi ya VVU.Mjadala Mkuu wa Mkutano wa 80 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa ukiwa umeingia katika siku yake ya nne hapa kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani leo Ijumaa, Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu amekuwa wa kwanza kuzungumza akitumia muda wake mwingi kushambulia wanamgambowa kipalestina, Hamas na kutetea kila uamuzi wa Israel. Anold Kayanda ameifuatilia hotuba hiyo kwa kina. Karibu Anold utupe japo kwa muhtasari.Tukisalia hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa, moja ya mikutano ya ngazi ya juu iliyofanyika kando ya mjadala mkuu wa Baraza Kuu, ni ule wa kuadhimisha miaka 30 tangu kuanzishwa kwa program ya Umoja wa Mataifa kuhusu vijana, mkutano ukileta vijana kutoka kona mbali mbali za dunia. Miongoni mwao ni daktari wa tiba na mwanaharakati wa kijamii wa vijana kutoka Uingereza mwenye asili ya Ghana, Dkt. Khadija Owusu. Amezungumza na Flora Nducha anayetujulisha zaidi katika taarifa hiiKatika hatua kubwa ya kihistoria kwenye mapambano dhidi ya Virusi Vya UKIMWI (VVU) dawa mpya ya kudungwa inayoitwa Lenacapavir inatarajiwa kupatikana kwa gharama nafuu katika nchi 120 zenye kipato cha chini na kati kuanzia mwaka 2027. Dawa hiyo itauzwa kwa kiasi cha dola 40 pekee ikiwa ni gharama ya vidonge vya kila siku vya kujikinga na VVU ambavyo mhusika atatumia kwa mwaka mzima. Sabrina Saidi ana taarifa zaidi.
Waziri wa Mambo ya Nje Penny Wong amesema Australia ina simama kidete juu ya tamaduni nyingi, baada ya Rais wa Marekani Donald Trump kukosoa uhamiaji katika hotuba yake kwa kikao cha mkutano wa Umoja wa Mataifa.
Matangazo ya nusu saa kuhusu habari za mapema asubuhi pamoja na habari za michezo.
Matangazo ya saa nzima kuhusu habari za kutwa, ikiwa ni pamoja ripoti kutoka kwa waandishi wetu sehemu mbali mbali duniani na kote Afrika Mashariki na Kati, na vile vile vipindi na makala maalum kuhusu afya, wanawake, jamii na maendeleo.
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina maalum inayomulika mkutano wa ngazi ya juu kuhusu magonjwa yasiyo ya kuambukiza NDCs unaoendelea kandoni mwa UNGA80, na tumezungumza na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa WHO Kanda ya Afrika Dkt. Mohamed Yakub Janabi.Wakati viongozi wa nchi na serikali wanahutubia wakiwa ndani ya jengo la Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa jijini New York, Kiongozi wa Palestina, Mahmoud Abbas ujumbe wake kwa UNGA80 ameutoa kwa njia ya video iliyorekodiwa kutokana na kutopata kibali cha kuingia Marekani. Katika hotuba hiyo amesisitiza kuwa, Ukanda wa Gaza utaendelea kuwa sehemu ya Taifa la Palestina na tuko tayari kuwajibika kikamilifu kwenye uongozi na usalama wa eneo hilo. Hamas hawatokuwa na jukumu lolote kwennye utawala.”.Mapema kabla ya Palestina, Rais wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud, alihutubia wajumbe akitaka nchi wanachama kujitolea upya kwa misingi ya usawa, mshikamano na ushirikiano wa kimataifa. Amesema hilo ni muhimu kwa kuwa “wakati ambapo hapo awali tulijitahidi kujiuliza ‘Nini ni sahihi' chini ya sheria ya kimataifa, leo tunashuhudia kwa wazi kuibuka kwa matumizi ya NGUVU ya kitaifa katika kusuluhisha migogoro. Hii ni njia ya giza na ya hatari sana inayotishia utawala wa sheria wa kimataifa tuliokubaliana kwa pamoja kama nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa.”Kando ya hotuba za viongozi, kunafanyika maadhimisho ya miaka 30 tangu kupitishwa kwa Programu ya Dunia kwa ajili ya vijana. Je vijana kutoka Malawi wana ujumbe gani? Mwakilishi wao kwenye mkutano huu Rachel Mganga Wanangwa anasema, “Ujumbe kutoka vijana wa Malawi ni wekezeni kwetu, tusaidieni, shirikianeni nasi, na wanashiriki kwenye meza za mazungumzo ili kuhakikisha kuwa sauti zao zinawakilishiwa.”.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
Matangazo ya nusu saa kuhusu habari za mapema asubuhi pamoja na habari za michezo.
Matangazo ya saa nzima kuhusu habari za kutwa, ikiwa ni pamoja ripoti kutoka kwa waandishi wetu sehemu mbali mbali duniani na kote Afrika Mashariki na Kati, na vile vile vipindi na makala maalum kuhusu afya, wanawake, jamii na maendeleo.
Hii leo jaridani tunaangazia hotuba ya Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy katika siku ya pili ya mjadala mkuu wa UNG80, na ujumbe wa washiriki wa mkutano huu kutoka Nigeria na Tanzania.Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy amesema taasisi za kimataifa zimekuwa dhaifu wanachoweza kufanya ni kutoa matamko makali pekee na kwamba kwa sasa duniani sheria pekee za Kimataifa haziwezi kusaidia nchi kujilinda bila ya kuwa na silaha pamoja na marafiki wenye nguvu wa kukusaidia.Katika siku ya pili ya Mjadala Mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, UNGA, kando ya hotuba, viongozi wa nchi 9 wanachama wa Jumuiya ya Afya ya Mashariki, Kati na Kusini mwa Afrika, ECSA watakuwa na mkutano wa kusongesha diplomasia ya kisayansi ili kuhakikisha bara la Afrika haliachwi nyuma kwenye kukabiliana na changamoto za kiafya, baada ya kujifunza kutokana na COVID-19 au UVIKO19.Tukisalia hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa Mjadala Mkuu wa UNGA80 mbali ya kusikiza hotuba za viongozi unaambatana na mamia ya matukio na mikutano ya kando. Leo, sauti kutoka pande zote za dunia zinaitaka haki ya kijamii katika moja ya mikutano ya kando na miongoni mwa sauti hizo ni ya mwanaharakati na mhamasishaji wa masuaa ya wasichana kutoka Nigeria ambaye anasema wasichana vigori hawapaswi kusahaulika.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
Matangazo ya nusu saa kuhusu habari za mapema asubuhi pamoja na habari za michezo.
Matangazo ya saa nzima kuhusu habari za kutwa, ikiwa ni pamoja ripoti kutoka kwa waandishi wetu sehemu mbali mbali duniani na kote Afrika Mashariki na Kati, na vile vile vipindi na makala maalum kuhusu afya, wanawake, jamii na maendeleo.
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina maalum na mada yetu inamulika maoni kuhusu miaka 80 ya Umoja wa Mataifa. Pia tunakuetea muhtasari wa habari unaofuatilia ujumbe wa viongozi katika mjadala mkuu wa UNG80.viongozi wa dunia wamekutana leo hapa kwenye Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani ikiwa ni siku ya kwanza ya Mjadala Mkuu wa 80 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, ukiambatana na vikao vya kando vya ngazi ya juu. Katika hotuba yake ya UNGA 80 Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametoa wito kwa dunia kufanya maamuzi “ni aina gani ya dunia tunataka kujenga pamoja.”Kuanza kwa UNGA maana yake idadi kubwa ya wageni, Msaidizi wa Katibu Mkuu wa UN anayeshughulikia habari na teknolojia, Bernardo Mariano, amesema wamejipanga kutoa huduma ya internet (Wi Fi) kwa watu 40,000 huku wakihakikisha hotuba za viongozi zinapeperushwa bila hitilafu za kiufundi wala kuvurugwa na mashambulizi ya mtandaoni.Na Hapo kesho Jumatano viongozi wa jumuiya ya Afya ya nchi za Afrika Mashariki, Kati na Kusini, ESCA watakutana kumulika Diplomasia ya kisayansi na afya ili kusongesha Mkataba wa Zama Zijazo. Mkurugenzi Mkuu wa ECSA Dkt. Ntuli Kapologwe ameeleza kulikoni?.Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!
Waziri Mkuu amesema ombi la utaifa wa Palestina ni fursa ya amani, katika hotuba yake kuhusu soluhu ya nchi mbili, alipo hudhuria kikao cha Umoja wa Mataifa hii leo Jumanne 23 Septemba 2025.
Matangazo ya nusu saa kuhusu habari za mapema asubuhi pamoja na habari za michezo.
Matangazo ya saa nzima kuhusu habari za kutwa, ikiwa ni pamoja ripoti kutoka kwa waandishi wetu sehemu mbali mbali duniani na kote Afrika Mashariki na Kati, na vile vile vipindi na makala maalum kuhusu afya, wanawake, jamii na maendeleo.
Hii leo jaridani tunaangazia ujumbe wa washirirki ya mkutano wa 80 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, hasa maadhimisho ya miaka 80 ya umoja huo. Pia tunamulika mashauriano ya faragha yenye lengo la kusaka majawabu ya madhara ya mabadiliko ya tabianchi.Umoja wa Mataifa hii leo umeadhimisha miaka 80 tangu kusainiwa kwa Mkataba wake tarehe 26 Juni 1945, tukio lililotoa matumaini mapya kwa dunia iliyokuwa imechoka kutokana na vita viwili vya dunia, mauaji ya halaiki na ukoloni. Katika maadhimisho hayo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amesema kumbukizi ya kuanzishwa kwa UN ni fursa ya kukumbuka ujasiri wa waanzilishi wa taasisi hiyo na kuimarisha mshikamano wa kimataifa katika kukabili changamoto zinazokabili dunia hivi sasa.Tukisalia na maadhimisho ya miaka 80 ya Umoja wa Mataifa , moja ya mchango mkubwa unaotoa kwa dunia tangu ulipoanzishwa mwaka 1945 ni kusaidia mamilioni ya watu wanaolazimika kufungasha virago kukimbia makwao na kuwa wakimbizi kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo vita. Uganda ni moja ya nchi zinazohifadhi maelfu ya wakimbizi wengi kutoka Sudan, Sudan Kusini na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC wakisaidiwa chini ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR na mengine. John Kibego kutoka Radio washirika Kazi-Njema FM iliyoko mjini Hoima Uganda amepata fursa ya kuzungumza na mmoja wa wakimbizi hao akielezea mchango mkubwa wa Umoja wa Mataifa kwake.Kando ya maadhimisho ya siku ya miaka 80 ya Umoja wa Mataifa, hapa makao makuu kumefanyika mashauriano ya faragha yenye lengo la kusaka majawabu ya madhara ya mabadiliko ya tabianchi. Mashauriano ya leo ni sehemu ya mashauriano 10 yatakayofanyika kuelekea mkutano wa tabianchi wa wakuu wa nchi na serikali utakaofanyika keshokutwa Jumatano hapa Umoja wa Mataifa. Assumpta Massoi amezungumza na mmoja wa watoa mada kwenye mashauriano hayo ambayo matokeo yake yatawasilishwa kwenye mkutano wa viongozi.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
Matangazo ya nusu saa kuhusu habari za mapema asubuhi pamoja na habari za michezo.
Matangazo ya saa nzima kuhusu habari za kutwa, ikiwa ni pamoja ripoti kutoka kwa waandishi wetu sehemu mbali mbali duniani na kote Afrika Mashariki na Kati, na vile vile vipindi na makala maalum kuhusu afya, wanawake, jamii na maendeleo.
Kuelekea maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Amani, hapo Jumapili tarehe 21 mwezi Septemba 2025, Umoja wa Mataifa nchini Tanzania kwa kushirikiana na baadhi ya wadau nchini humo, umeendesha warsha ya siku moja ya kutoa elimu kwa wanafunzi wa shule ya msingi Hazina jijini Dar es Salaam kuhusu ya umuhimu wa kuishi kwa amani na kuchukua hatua sasa katika kuidumisha. Warsha hiyo imeongozwa na kauli mbiu “Chukua hatua Sasa, kwa ajili ya Dunia yenye Amani.” Katika warsha hiyo, baadhi ya wanafunzi wameeleza walichojifunza na namna elimu hiyo inavyoweza kuwanufaisha katika maisha yao ya kila siku. Shuhuda wetu katika mafunzo ni Sabrina Saidi anatupasha ilivyokuwa
Hii leo jaridani tunaangazia wakimbizi wa ndani wa Palestina Gaza, na ujumbe wa mwakilishi wa kudumu wa Kenya kwenye Umoja wa Mataifa Balozi Ekitela Lokaale kuhusu mchango wa Afrika katika kazi za Umoja wa Mataifa. Pia tunakwenda Tanzania kumulika amani.Baada ya amri iliyotolewa na jeshi la Israel la kuwataka Wapalestina walioko katika eneo la mji wa Gaza huko Ukanda wa Gaza eneo la Palestina linalokaliwa kimabavu na Israel kuondoka eneo hilo kwani linataka kufanya mashambulizi, hali imekuwa mbaya kwa wananchi hususan wazee ambao sasa wanafunga safari kilometa nyingi kuondoka eneo hilo.Ilikuwa miezi, wiki na sasa imesalia siku tatu tu kabla ya mjada mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa UNGA80 kun'goa nanga hapa kwenye Makao Makuu jijini New York Marekani ambapo viongozi wa Dunia na wakilishi mbalimbali watashiriki kwenye mkutano wa 80 wa Baraza Kuu. Mada mbalimbali zitajadiliwa ikiwemo maadhimisho ya miaka 80 ya Umoja wa Mataifa.Kuelekea maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Amani, hapo Jumapili tarehe 21 mwezi Septemba 2025, Umoja wa Mataifa nchini Tanzania kwa kushirikiana na baadhi ya wadau nchini humo, umeendesha warsha ya siku moja ya kutoa elimu kwa wanafunzi wa shule ya msingi Hazina jijini Dar es Salaam kuhusu ya umuhimu wa kuishi kwa amani na kuchukua hatua sasa katika kuidumisha. Warsha hiyo imeongozwa na kauli mbiu “Chukua hatua Sasa, kwa ajili ya Dunia yenye Amani.”Mwenyeji wako ni Assumpta, karibu!
Kampuni ya pili kwa ukubwa ya madini imetangaza inapunguza ajira. Anglo American Australia imesema ita angaza kupunguza idadi ya wafanyakazi Queensland, na takriban wafanyakazi 200 wata athirika.
Matangazo ya nusu saa kuhusu habari za mapema asubuhi pamoja na habari za michezo.
Jaridani leo jaridani tunakuletea mada kwa kina kuhusu masuala ya wanawake, tathmini ya miaka 30 ya harakati za kusongesha haki za wanawake na utamsikia maoni ya Balozi Gertrude Mongella kutoka Tanzania. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na uchambuzi wa methali.Mjadala Mkuu wa mkutano wa 80 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa ukianza Jumatatu ijayo, Rais wa Mkutano huo Annalena Baerbock amewaambia waandishi wa habari jijini New York, Marekani kuwa “jukumu letu ni Umoja wa Mataifa uwe thabiti kwa miaka 80 ijayo. Michakato ya kuhakikisha hilo ndio itakuwa jukumu letu mwaka huu, ikiwemo kusongesha ajenda ya marekebisho ya Umoja wa Mataifa. Kwa hiyo tukitaka Umoja wa Mataifa thabiti, basi tunahitaji ahadi kutoka serikali zote duniani.Ripoti ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa inayotolewa kila mwaka kabla ya kuanza kwa Mjadala Mkuu wa Baraza Kuu inasema Umoja wa Mataifa umeendelea kusimama imara, ukifanya kazi ya kuendeleza amani, kuchochea maendeleo endelevu, na kupunguza mateso ya kibinadamu licha ya majaribu makubwa. Katika ripoti hiyo Antonio Guterres amesisitiza uimara wa watumishi wa Umoja wa Mataifa, ambao wamejitolea kuleta matumaini na msaada kwa wale wanaohitaji licha ya kufanya kazi katika mazingira magumu.ripoti ya Hali ya Rasilimali za Maji Duniani iliyotolewa leo inasema ni takriban theluthi moja tu ya mabonde ya mito duniani yaliyokuwa na hali ya “kawaida” mwaka 2024 ilhali mengine yote yalikuwa na kiwango cha juu zaidi cha maji au chini ya kiwango cha kawaida — ikiwa ni mwaka wa sita mfululizo wa kutokuwepo kwa uwiano wa wazi. Ikitolewa na shirika la Umoja wa Mataifa la Hali ya Hewa, WMO, ripoti inasema mwaka 2024 uliokuwa mwaka wa joto zaidi kuwahi kurekodiwa ulianza na tukio la El Niño ambalo liliathiri vibaya mabonde makubwa ya mito na kusababisha ukame katika maeneo kadhaa ikiwemo kusini mwa Afrika.Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili, leo mchambuzi wetu ni Dkt. Josephat Gitonga, ambaye ni Mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi nchini Kenya, kwenye kitivo cha Tafsiri na Ukalimani anafafanua maana ya methali "MZOEA PUNDA HAPENDI FARASI"Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!
Matangazo ya nusu saa kuhusu habari za mapema asubuhi pamoja na habari za michezo.
Tarehe kama ya leo, 18 Septemba mwaka 2021 dunia ilishitushwa na kuhuzunishwa na tangazo lililotolewa la uongozi wa Taliban nchini Afghanistan la kukataza wasichana barubaru kuendelea na masomo na kwamba darasa la sita ndio mwisho wa elimu yao. Sasa ni miaka minne na katazo hilo bado limesimama kitu ambacho Umoja wa Mataifa umeeleza kuwa ni “moja ya dhulma kubwa za wakati wetu.” Leah Mushi na taarifa zaidi.
Jaridani leo jaridani tunaangazia haki ya elimu kwa wasichana na wanawake nchini Afghanistan, na kuzorota kwa huduma za afya katika ukanda wa Gaza. Pia tunakwenda nchini Zambia kumulika mradi wa wakulima wadogo.Tarehe kama ya leo, 18 Septemba mwaka 2021 dunia ilishitushwa na kuhuzunishwa na tangazo lililotolewa la uongozi wa Taliban nchini Afghanistan la kukataza wasichana barubaru kuendelea na masomo na kwamba darasa la sita ndio mwisho wa elimu yao. Sasa ni miaka minne na katazo hilo bado limesimama kitu ambacho Umoja wa Mataifa umeeleza kuwa ni “moja ya dhulma kubwa za wakati wetu.”Wakati Israeli ikiwa imetoa amri mpya ya watu kuhama kutoka jiji la Gaza katika eneo inalokalia kimabavu la Palestina, na kuelekea eneo ililotenga na kuliita ukanda wa kibinadamu kusini mwa Ukanda wa Gaza, shirika la Umoja wa Mataifa la Afya duniani, WHO limesikitishwa na agizo hilo jipya ikisema eneo halina ukubwa wala huduma za kutosha kusaidia wale walioko tayari huko, sembuse wale watakaowasili. Huduma za afya ni tete.Kupitia mradi wa SCRALA uliowezeshwa na shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa maendeleo, UNDP, wakulima wadogo nchini Zambia sasa wanaweza kulima mwaka mzima kwa kutumia miundombinu inayostahimili mabadiliko ya tabianchi kama vile mifumo ya umwagiliaji na vituo vya ukusanyaji mazao, jambo linalochangia kuongezeka kwa tija na upatikanaji wa masoko.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
Matangazo ya nusu saa kuhusu habari za mapema asubuhi pamoja na habari za michezo.
Jaridani leo jaridani tunakuletea mad akwa kina inayoangazia mjadala Mkuu wa mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na ufafanuzi wa neno la wiki.Tume ya Uchunguzi ya Umoja wa Mataifa imesema Israel imetekeleza mauaji ya kimbari Gaza. Ripoti ya tume hiyo hiyo iliyotolewa leo mjini Geneva pia inamtaja Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu na maafisa wengine wakuu wa Israel kwa kuchochea vitendo hivyo. Israel imepinga vikali, na kuuita ripoti hiyo kuwa ni “kashfa.” Taarifa hii imetolewa huku mashambulizi makali ya anga yakiendelea usiku kucha mjini Gaza bila dalili za kukoma.Hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa, shirika hilo limekamilisha makadirio mapya ya bajeti ya mwaka 2026, yakionesha kupunguzwa kwa zaidi ya dola milioni 500. Hatua hiyo ni sehemu ya mpango wa mageuzi ya UN80, unaolenga kuongeza ufanisi wakati Umoja wa Mataifa ukiadhimisha miaka 80. Bajeti mpya inapendekeza kupunguzwa kwa rasilimali kwa zaidi ya asilimia 15 na nafasi za kazi kwa karibu asilimia 19 ikilinganishwa na mwaka 2025.Huko Nairobi, Kenya leo imezindua maabara ya kisasa ya polio iliyoidhinishwa na Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa Duniani WHO katika Taasisi ya Utafiti wa Tiba ya Kenya, KEMRI. Kituo hicho, kilichofadhiliwa na WHO na wakfu wa Gates, kimeelezwa kuwa nyenzo muhimu katika kugundua mapema na kukabiliana na virusi vya polio pamoja na magonjwa mengine yenye uwezekano wa kusambaa, si tu nchini Kenya bali pia katika kanda nzima ya Afrika.Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili hii leo, mtaalam wetu Onni Sigalla, Mhariri mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania, BAKITA, anafafanua maana za neno "MJOLI"Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
Naibu Waziri Mkuu Richard Marles amekana madai kuwa uwekezaji wa $12 bilioni iliyo tangazwa juzi ime undwa ili kutuliza maombi ya Marekani kwa Australia kuongeza matumizi yake katika ulinzi.
Jaridani leo jaridani tunaangazia hali ya kibinadamu katika ukanda wa Gaza, haki za binadamu nchini Sudan Kusini na ujumbe wa Katibu Mkuu kuhusu siku ya demokrasia duniani.Kamishina Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia wakimbizi wa Kipalestina UNRWA, Philippe Lazzarini, ametoa onyo kali kuwa “hakuna sehemu yoyote iliyo salama Gaza, na hakuna mtu aliye salama”akisema zahma na madhila yametanda kila kona ya eneo hilo linalokaliwa kimabavu na Israel.Leo ni siku ya demokrasia duniani ambapo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres, ameeleza bayana kuwa demokrasia iko hatarini duniani.Nchini Sudan Kusini ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo UNMISS unaendelea kuimarisha mfumo wa mahakama ili kuhakikisha haki inapatikana kwa wote hata maeneo yote ya nchi hiyo.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
Benki ya ANZ imekiri kujihusisha na mwenendo usiofaa, katika huduma iliyotoa kwa serikali ya Australia, kulingana na Tume ya Uwekezaji na usalama ya Australia (ASIC).
Leo hapa katika makao Makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York Marekani hafla maalum imefanyika kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Amani ambayo kwa kawaida huwa kila mwaka tarehe 21 Septemba. Katibu Mkuu António Guterres katika hafla hiyo ameisihi dunia ambayo imeghubikwa na vita na machafuko kila kona kuwa wakati ni sasa kuchukua hatua na kutimiza ndoto ya amani iliyoanza mwaka 1945 baada ya vita vya pili vya dunia. Flora Nducha amefuatilia hafla hiyo na kutuandalia taarifa hii. Karibu Flora(TAARIFA YA FLORA NDUCHA)Natts --bellLeo, mlio mzito wa Kengele ya Amani umesikika kwenye Makao Makuu ya Umoja wakati wa hafla hiyo iliyoambatana na na burudani ya muziki wa allaNatts........Kisha Katibu Mkuu Guterres akawageukia washiriki na kusema “miaka ni themanini iliyopita Umoja wa Mataifa kuzaliwakutoka kwenye majivu ya vita ili kusaka amani”, akatoa ujumbe ulio wazi,sasa jukumu la amani duniani ni la dharura kuliko wakati mwingine wowote.Wakati migogoro ikienea na mamilioni ya raia wakiendelea kunaswa kwenye mzunguko wa ghasia, Katibu Mkuu ametahadharisha kwa onyo kali “Amani imo hatarini.”Amesema haki za binadamu na sheria za kimataifa zinakanyagwa, na kuacha nyuma kile alichokiita “mandhari yanayodhalilisha ubinadamu wetu wa pamoja.”Ameongeza kuwa kauli mbiu ya mwaka huu ya siku ya Amani “Tuchukue Hatua Sasa kwa Dunia yenye Amanisi maneno ya kupita tu, bali ni wito wa dhati wa kuchukua hatua. Guterres amewakumbusha wanachama wa Umoja wa Mataifa na raia kila mahali kwamba amani haiji kwa bahati. Inajengwa hatua kwa hatua, kwa maelewano, ujasiri, na vitendo.“Ni lazima tuchukue hatua kunyamazisha bunduki na kukuza diplomasia. Ni lazima tuchukue hatua kuwalinda raia na kutetea Mkataba wa Umoja wa Mataifa. Ni lazima tuchukue hatua kushughulikia chanzo cha migogoro kuanzia ukosefu wa usawa na kutengwa, hadi kauli za chuki, na janga la tabianchi.”Katibu Mkuu amesisitiza kwamba amani bado iko ndani ya uwezo wa binadamu lakini ni iwapo tu tutaichagua. Ameiitaja kama nguvu kubwa zaidi kwa mustakabali bora, na kuwataka watu wote kuwaunga mkono wale wanaojenga amani, hususan wanawake na vijana walioko mstari wa mbele wa matumaini.Natts kengele.....muzukiKengele ya Amani ilipopigwa iliyotengenezwa miongo kadhaa iliyopita kutokana na sarafu na medali zilizotolewa na watu wa kawaida kote duniani Guterres amewakumbusha hwashiriki wa hafla hiyo ishara yake “Hata katika dunia iliyogawanyika, bado tunaweza kuungana na kuiacha amani ishike hatamu.”Amehitimisha kwa kusema Katika Siku ya Kimataifa ya Amani, mlio wa kengele unatoa si tu wito wa kimya cha tafakuri, bali pia wito wa kuchukua hatua kwa viongozi, kwa raia, na kwa vizazi vijavyo.Natts muziki..
Karibu usikilize jarida la habari za Umoja wa Mataifa hii leo tunaangazia masuala ya amani pamoja na ushirikiano wa nchi zinazoendelea na zile zilizoendelea duniani. Pia utasikia habari kutoka mashinani nchini Kenya kuhusu mradi wa UNICEF kwenye kilimo uliowainua kiuchumi vijana. Mtangazaji wako ni Leah Mushi.
Waziri Mkuu amesifu msaada wa wanachama wa kongamano la Visiwa vya Pasifiki, Australia inapo saka uenyeji wa kongamano la mazingira la Umoja wa Mataifa la, COP-31.
Katika Jarida la Habari za Umoja wa Mataifa leo Flora Nducha anakuletea-Utapiamlo kwa watoto katika Ukanda wa Gaza eneo la Palestina linalokaliwa kimabavu na Israel umefikia kiwango cha kutisha, huku takwimu mpya zikionesha ongezeko kubwa mwezi Agosti kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa-Umoja wa Mataifa umeanzisha mradi mpya wa miaka mitatu wenye lengo la kusaidia nchi za Afrika Mashariki kukabiliana na matumizi ya kigaidi ya vilipuzi. Kupitia mradi huu, Kenya, Somalia na Uganda zitasaidiwa-Hali nchini Haiti inaendelea kuzorota, sehemu kubwa ya nchi inadhibitiwa na magenge yenye silaha, nusu ya idadi ya watu wanakabiliwa na upungufu wa chakula, na idadi ya watu waliofurushwa imefikia kiwango ambacho hakijawahi kushuhudiwa amesema Tom Fletshe mkuu wa OCHA-Mada kwa kina inatupeleka Uganda watumiaji wa Ziwa Albert wafunguka kuhusu changamoto za uvuvi haramu na faida za ziwa hilo-Na katika jifunze KIswahili leo mtaalam wetu Dkt Mwanahija Ali Juma, Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili, Zanzibar nchini Tanzania, BAKIZA anafafanua maana ya neno "UKWASI!
Leo jaridani Assumpta Massoi anamulika kauli ya OHCHR kufuatia maandamano yanayoendelea Nepal; Utipwatipwa 'wapiku' utapiamlo na harakati za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi huko Karamoja nchini Uganda,Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Haki za Binadamu ameonesha wasiwasi mkubwa kufuatia ghasia zinazoendelea na kushika kasi nchini Nepal, huko barani Asia, ambako maandamano dhidi ya ufisadi na marufuku ya mitandao ya kijamii yamesababisha vifo vya watu wengi pamoja na majeruhi. Flora Nducha amefuatilia taarifa hiyo na anatupasha zaidi.Kwa mara ya kwanza idadi ya watoto na vijana wa umri wa kwenda shule wenye unene wa kupindukiaau utipwatipwa imezidi idadi ya watoto wenye utapiamlo duniani ikiathiri watoto milioni 188 sawa na mtoto 1 kati ya kila watoto 10 imesema leo ripoti iliyotolewa leo na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF. Tuungane na Leah Mushi kusikia zaidi kuhusu ripoti hiyo, karibu LeahKaramoja, eneo la kaskazini mashariki mwa Uganda, linakabiliwa na changamoto kubwa za tabianchi kama vile ukame wa mara kwa mara na milipuko ya magonjwa ya mimea na mifugo, hali inayotishia uhakika wa chakula. Kupitia mradi wa PROACT, mashirika ya Umoja wa Mataifa lile la Chakula na Kilimo Duniani (FAO), na Mpango wa chakula Duniani (WFP) pamoja na Ofisi ya Waziri Mkuu wa Uganda kwa ufadhili wa Muungano wa Ulaya, EU, wameshirikiana katika kuimarisha mifumo ya kushughulikia mabadiliko ya kiikolojia na kijamii. Anold Kayanda na maelezo zaidi.
-Katika Jarida la Habari la Umoja wa Mataifa hii leo Flora Nducha anakuletea UNGA79yafikia tamati hii leo na kupisha UNGA80 chini ya uongozi wa Rais mpya Annalena Baerbock-Ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa iliyozinduliwa leo imesema matumizi ya kijeshi duniani yalifikia dola trilioni 2.7 mwaka 2024, yakiwa yameongezeka kwa zaidi ya asilimia 9 kutoka mwaka 2023-Mratibu wa Misaada ya Dharura wa Umoja wa Mataifa Tom Fletcher ametangaza leo dola milioni 1 za kimarekani kutoka Mfuko wa Dharura wa Umoja wa Mataifa CERF ili kudhibiti mlipuko wa kipindupindu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC. -Mada kwa kina inatupeka Pemba Kaskazini kisiwani Zanzibar nchini Tanzania kuangazia mradi wa FAo wa ZJP unavobadili maisha ya wakulima wa ndiziNa katika jifunze Kiswahili utamsikia mlumbi Jorum Nkumbi kutoka Tanzania akifafanua maana ya neno LISANI
Dau Akouny, mmoja wa wavulana wawili walio uawa katika shambulizi la kisu mjini Melbourne wikiendi iliyopita, amekumbukwa na familia yake kama "mtoto mzuri" na alikuwa "sehemu ya mustakabali wa kesho wa jumuiya."
Huko Bunia, jimboni Ituri Mashariki Mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, Mkuu wa Operesheni za Ulinzi wa Amani za Umoja wa Mataifa, Jean-Pierre Lacroix, amepongeza juhudi za pamoja za walinda amani wa Mpango wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo MONUSCO na jeshi la serikali ya Congo, FARDC, katika juhudi za kulinda raia na kupunguza ghasia za makundi yenye silaha.Akizungumza wakati wa ziara yake iliyoanza Septemba 6, Mashariki mwa DRC katika jimbo la Ituri Lacroix amesema ushirikiano na kuaminiana kati ya mamlaka za jimbo la Ituri na vikosi vya Umoja wa Mataifa ni msingi muhimu wa kurejesha amani.Anasema “Nipo katika eneo liitwalo Fataki, katika jimbo la Ituri, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, na hapa kuna kambi ya MONUSCO yenye kikosi cha Nepal, pamoja na kambi ya wakimbizi wa ndani. Maelfu ya watu wanalindwa hapa na wenzetu wa MONUSCO, na wanapatiwa msaada wa kibinadamu pamoja na ulinzi.”Gavana wa Ituri, Jenerali Johnny Luboya, alikaribisha msaada wa MONUSCO katika operesheni za kijeshi na mazungumzo ya amani, yakiwemo dhidi ya kundi la CRP katika eneo la Djugu Ituri ambako mamia ya maelfu ya wakimbizi wa ndani sasa wananufaika na ulinzi wa pamoja wa FARDC na walinda amani wa Umoja wa Mataifa. Lacroix amesema “Katika jimbo la Ituri pekee kuna makambi kadhaa ya wakimbizi wa ndani, ambayo yanalindwa na MONUSCO, ambapo makumi ya maelfu kwa hakika mamia ya maelfu ya watu wanalindwa na wenzetu wa MONUSCO na wanapatiwa msaada.”Mkuu huyo wa operesheni za ulinzi wa amani ameohitimisha kwa kusema ziara hii ni muhimu sana kwani “Nipo hapa kuonyesha kile ambacho MONUSCO hufanya kila siku, tofauti ambayo MONUSCO inaleta katika kuwalinda raia hawa, tofauti kati ya kuwa salama au kuwa katika hatari kubwa, na nilitaka pia kutoa shukrani zangu kwa wenzetu wa MONUSCO. Aidha, nilitaka kuwasikiliza wananchi, hawa wakimbizi wa ndani, pamoja na jamii, na kuona namna ambavyo tunaweza kushirikiana nao zaidi ili kuboresha hali na kupiga hatua katika kukabiliana na ghasia ambazo bado zinaendelea katika eneo hilo.”Baada ya zira yake jimboni Itari Lacrix ameelekea katika mji Mkuu Kinshasa ambako amekutana na na kuzungumza na maafisa wa serikali.
Heko MONUSCO na FARDC kwa kulinda raia na kupunguza ghasia za makundi yenye silaha: LacroixSiku ya kimataifa ya kujua kusoma na kuandika.WHO yatoa orodha ya dawa muhimu duniani.
Ikiwa leo tarehe 8 Septemba ni siku ya Kimataifa ya kujua kusoma na kuandika ambapo Umoja wa Mataifa ulianzisha siku hii ili kuwakumbusha watunga sera, walimu, wadau wa elimu, na jamii juu ya umuhimu wa ujuzi wa kusoma na kuandika katika kujenga jamii yenye elimu, haki, amani na endelevu, Sabrina Saidi wa Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa anaiangazia kauli mbiu ya mwaka huu "Kukuza ujuzi wa kusoma na kuandika katika zama za kidijitali" akiwashirikisha baadhi ya wadau wa elimu nchini Tanzania.Amezungumza na baadhi ya wadau kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino, SAUT kilichoko jijini Mwanza, kaskazini-magharibi mwa Tanzania.Dismas Nziku ni mwalimu wa masomo ya Biashara na Ujasiriamali anazungumza kuhusu ni kwa jinsi gani ufundishaji wa zama hizi za kidijitali unavyochochea na kukuza ujuzi wa kusoma na kuandika. "Kwenye dunia ya sasa ujuzi wa kusoma na kuandika kidijitali ni msingi mkubwa kwa mwanafunzi, na miongoni mwa juzi hizi muhimu ni kama vile kujua kutumia vifaa vya kidijitali kama kompyuta, simu janja kwa ajili ya kujisomea na kutafuta maarifa, lakini pia kama mwalimu ninawafundisha wanafunzi kwa njia ya vitendo,kuandaa maswali ya utafiti kwa kutumia internet,kufanya kazi na kufanya kazi ya kikundi mitandaoni."Kuhusu umuhimu wa siku hii kwake na inachangia vipi katika kukuza uelewa wa umuhimu wa kusoma na kuandika shuleni na katika jamii Mwalimu Nziku amesema, "Siku ya Kimataifa ya kujua kusoma na kuandika ni kumbusho muhimu kwamba elimu ni haki ya msingi, na ni msingi wa maendeleo kwa kila mmoja kujua kusoma na kuandika hasa hasa kidijitali, inanipa hamasa kama mwalimu kuendelea kuwajengea wanafunzi ujuzi wa kusoma na kuandika si kwa ajili ya mitihani tu, bali kwa maisha yao ya kila siku."Didas Karoli ni mwanafunzi katika chuo hicho cha SAUT akisoma shahada ya kwanza ya Mawasiliano kwa Umma, ameeleza kuhusu siku hii na jinsi maendeleo ya kidijitali yanavyochagiza katika kujifunza kwake akisema "Zana za kidijitali zimebadilisha sana upeo wangu katika suala la kujifunza,kutokana na zamani nilikuwa nategemea vitabu lakini hivi sasa natumia tu smartphone au kompyuta na kutengeneza notisi zangu mwenyewe za kujifunzia.Siku ya hii ya kujua kusoma na kuandika ni siku ambayo ni muhimu inafanya watu waweze kujua umuhimu wa kusoma na kuandika."