Yesaya Software Podcast

Follow Yesaya Software Podcast
Share on
Copy link to clipboard

Ebwana mambo vipi, jina langu ni Yesaya, kila wiki ninakuletea mfululizo wa vipindi kwa njia ya sauti yaani Podcast. Dhumuni langu ni kukuhabarisha, kukuelimisha na kukuletea mijadala mbalimbali kuhusu Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) na mimi nitajikita zaidi kwenye upande wa mifumo ya kompyuta.

Yesaya R. Athuman


    • Jan 30, 2023 LATEST EPISODE
    • infrequent NEW EPISODES
    • 17m AVG DURATION
    • 53 EPISODES


    Search for episodes from Yesaya Software Podcast with a specific topic:

    Latest episodes from Yesaya Software Podcast

    Andika Ujumbe wa Msaaada Utakaojibiwa na Mtu Mwenye Followers Wengi

    Play Episode Listen Later Jan 30, 2023 6:08


    Kwenye episode hii nimeeleza kwa kina namna ya kuandika ujumbe wa kuomba msaada kwa mtu mwenye followers wengi. Yawezekana ni programmer au mtu mwenye uzoefu kwenye eneo fulani.

    Niliyojifunza kwenye #DevFestNairobi na Fursa zilizopo kwa Developers

    Play Episode Listen Later Nov 16, 2022 23:35


    Nimeandaa mjumuisho wa mambo niliyojifunza kwenye #DevFestNairobi na hamasa niliyopata na hivyo nimeona vyema niweze kukushirikisha wenzetu walipo ili nasi tupate kupiga hatua zaidi.Ndugu yangu, sikuwahi kujua event ya developers kuwa na wahudhuliaji zaidi ya 3000, vyombo kuletwa na kontena la 40 futi. Yaani nina mengi kukubadilisha mtazamo lakini nikaelewa ndio maana makampuni makubwa ya TEHAMA duniani yana ofisi Kenya.DevFestDar RSVP: http://zipa.me/devfestdar Be a Speaker: https://sessionize.com/devfest-dar-es-salaam

    Mambo Matatu (3) Muhimu kwa Wanafunzi wa Mwaka wa Kwanza Chuo

    Play Episode Listen Later Oct 14, 2022 8:51


    Tunapoelekea kufungua vyuo, nimeona ni vyema kuwapa abc wanafunzi wa mwaka wa kwanza hasa katika kozi za TEHAMA.Nimeweka mambo matatu (3) muhimu ya kuzingatia, unaweza niachia maoni yako kule Twitter @yesayasoftware.Video version unaweza kuipata hapa: https://youtu.be/n0mmLeqDlmc

    Nitumie Browser Gani?

    Play Episode Listen Later Apr 16, 2022 20:03


    Browser ni software application for retrieving, presenting and traversing information resources on the World Wide Web. Lakini pia inawezesha kucapture au kuinput taarifa ambayo inaweza kurudishwa kwa mfumo unaowasilisha, kisha kuhifadhiwa au kuchakatwa inapohitajika.

    Usijisikie Vibaya Kugoogle

    Play Episode Listen Later Mar 26, 2022 16:15


    Hey, Mambo vipi,Leo tutazungumza kuhusu kugoogle au kutafuta majibu ya changamoto unapokuwa kwenye ujenzi wa mfumo. Je, unajisikia vibaya unapogoogle mambo kwenye mtandao kama programmer unanielewa nikisema Stack Overflow. Lakini je, kugoogle kunakufanya wewe kuwa programmer mbaya?Nitakueleza kwa uzoefu wangu pamoja na programmers mashuhuri kabisa ninaowafahamu ambao pia wameshare uzoefu wao katika hili. Nitakueleza pia kuna time unagoogle na hutapata kitu lakini kuna mtu unamjua ana uzoefu na sala unalohaingaika nalo, nakumbuka usemi wa waswahili, KUULIZA sio Ujinga.  Hii ni Yesaya Software Podcast episode namba 34.

    Namna ya kutunza na kulinda taarifa za kadi mtandaoni

    Play Episode Listen Later Nov 9, 2021 16:59


    Hey, Mambo vipi,Leo tutazungumza kuhusu usalama wa taarifa za kibenki katika kufanya manunuzi online. Technolojia inabadilika kila leo, vilevile maarifa ya kulaghai watumia wa mitandao yazidi kuto tabirika.Mbinu mpya za udukuzi zinaibuka hivyo ni muhimu kutunza vizuri taarifa zako na kuwa makini na watu unaofanya nao biashara kwenye mtandao.Hii ni Yesaya Software Podcast episode namba 33.

    Uzoefu wangu katika kufanya manunuzi online II

    Play Episode Listen Later Nov 1, 2021 17:12


    Hey, Mambo vipi,Leo tutazungumza uzoefu wangu katika kufanya manunuzi online sehemu ya pili. Kwenye toleo lilipita nilikueleza maandalizi niliyofanya kabla sijaagizo mzigo. Nilikueleza niliapanga kuagiza mzigo kupitia Amazon na eBay kutokana na maoni mbalimbali niliyopata. Pia njia ya kusafirisha mzigo kupitia MyUs.com na namna nilivyofunga sanduku la posta kiganjani kupitia SmartPosta.Leo tutaendelea nitakupa experience yangu ya manunuzi online kupitia Amazon na eBay kisha kusafirisha mzigo kuja bongo.Hii ni Yesaya Software Podcast episode no 32.

    Ep 31: Uzoefu wangu katika kufanya manunuzi online

    Play Episode Listen Later Oct 18, 2021 14:18


    Hey, Mambo vipi,Leo tutazungumza uzoefu wangu katika kufanya manunuzi online. Mid this year niliamua kufanya refresh ya tools ninatumia hapa Yesaya Software (camera, light and mixer) na nilitamani kufanya manunuzi online based on specific models ambazo nilipata recommendations kwa watu wengi online.Ninaweza kusema ni kipindi cha excitement, pressure, maumivu na disappointment.Nitakusimulia uzoefu niliopata na maamuzi niliyofikia endapo nitafikiria kuagiza tena mzigo online. Uzoefu wangu na experience hii ni kwa e-commerce websites mbili kubwa ya Amazon na eBay.Hii ni Yesaya Software Podcast episode no 31.

    Ep 30: Mambo ninayofanya Bundle nikiwa sina Internet

    Play Episode Listen Later Oct 10, 2021 9:53


    Hey, Mambo vipi,Leo nitakushikisha mambo ninayofanya nikiwa sina access ya Internet - yaani bundle limekata. Kwa kawaida nikiwa na internet na niko nyumbani kama siko na watoto basi muda mingi niko kwenye computer. Sometimes sina mood ya kazi basi hapo ndio ninapoteza muda kwenye magroup na Twitter huko. Ila bundle limekata, ninafanya nini?Nitafurahi kusikia pia kutoka kwako, kuna rafiki yangu mmoja amenijubu, baada ya kummuliza anafanya nini bundle likikata, ameniambia ananunua bundle. 

    Nimekupa Summary ya Video 8 Nilizoupload

    Play Episode Listen Later Sep 19, 2021 15:06


    Hey, Mambo vipi,Leo nitakupatia update ya kazi niliyofanya this weekend. Nimekamilisha kurekodi na kupublish video 8 kuhusu Laravel Community Website. Na kubwa tunatengeza website hii pamoja, hakikisha unachek kule GitHub kuweza kushiriki ujenzi na pia kule YouTube kwa video tutorials kuhusu development ya hii website.Lakini kabla hatujasonga mbele ninapenda kuchukua fursa hii kukushukuru sana kwa kuweza nifanikisha kufikia download elfu 5 kwenye Yesaya Software Podcast. It means a lot kwangu na wewe ni modaux mkubwa kwenye hili. Asante.Hii ni Yesaya Software Podcast episode no 29.

    Mambo ya Kuzingatia kwenye Kuamua kutengeneza Multi/Cross Platform

    Play Episode Listen Later Sep 16, 2021 7:42


    Leo tunakwenda kujadili kidogo kuhusu path niliyochukua kutengeneza cross platform apps, hapa ninamaanisha Android and iOS App.  Kutokea awali nimekuwa mzito sana kudevelop apps ambazo sio native yaani sio specific kwa Android na iOS.Nina imani toleo hili litakuwa msaada pia kwa wadau mbalimbali wa TEHAMA kujua technolojia zinazohusika kutengeneza Mobile Apps.So balbu imewaka na unapata this next great idea for a mobile app ambayo unataka kuitengeneza. Itabadilisha maisha yake, utakupatia pesa sasa what's the next step you need to take?Jambo la muhimu unalopaswa kuamua mapema kabisa kabla hujaanza kutengeneza application yako. Na hapa ninazungumza from developer point of view.Okay kuna React Native, kuna … Flutter yes yes kuna KMM yaani Kotlin Multi Platform Mobile. Which one ninapaswa itumia? Je, nitaamua kutokana na technolojia ninayoifahamu au nitaassess features muhimu kwa app yangu kisha niwe guidance Framework ili itakuwa sahihi kwa use case yangu.Hilo ninaachia wewe sasa, huu ndio uamuzi wangu kuhusu hili kwa nini nimechagua KMM over other technology. But seriously hii inadepend ya use case yako na how quickly you want to address the problem. Anyways tuangalie kuna nini kwenye KMM, pia nitasubiri maoni yako.

    Ukweli na Elimu kuhusu YouTube Monetisation

    Play Episode Listen Later Aug 14, 2021 37:12


    Ukweli na Elimu kuhusu YouTube Monetisation

    Uhusiano wa Mentor na Mentee

    Play Episode Listen Later Aug 13, 2021 14:21


    Leo kwenye Twitter Spaces na Yesaya Software tumejadili kuhusu uhusiano wa Mentor na Mentee. Tulijadili mambo mengi ikiwa na kuangalia sababu za kwa nini utahiji mentor.Increased knowledgeConstructive criticismPersonal growthWords of encouragementFirm boundariesUnbiased opinionsTrusted allyGoal-settingNew perspectiveNetworking connections

    Kuwa mwangalifu na matumizi ya pesa kwenye mtandao

    Play Episode Listen Later Aug 12, 2021 7:41


    Historia kidogoZaidi huduma nyingi kwenye mtandao ilikuwa unalipia mara moja tuuHii ilikuwa ngumu lakini ukiweza lipia unakuwa umemaliza hiyo kitu   kwa miaka michacheSasa huduma zimebadilika utasikia manen mengi Software as a Service Hardware as a Service Na hizo subscriptionLengo ni kupunguza gharama za mwanzo na kufanya gharama kuwa  nafuu lakini utalipa kila mwezi which posses a riskUtajikuta sasa kila mwisho wa mwezi una lundo la mambo ya kulipia,   bado hujalipa bill za maji na umeme.Kama hutokuwa mwangalifu unaweza kujikuta umekatwa pesa kwa  subscription zisizo za msingi.

    Freelancer kwa miaka 5 nitakusimulia changamoto na fursa

    Play Episode Listen Later Aug 11, 2021 48:34


    Freelancer kwa miaka mitano nitakusimulia  changamoto na fursa. Hii ilikuwa sehemu ya mazungumzo yangu na wadau mbalimbali kwenye Twitter Spaces. Nilipata fursa kusikia uzoefu kutoka kwa Baraka, Justin, Kalebu na Alpha.Unaweza kusikiliza sasa na nina imani kuna jambo utajifunza.

    Content ya kuweka kwenye mtandao na kupata traffic kubwa

    Play Episode Listen Later Aug 10, 2021 7:34


    Kwenye toleo hili ni sehemu ya majadiliano kwenye Twitter Spaces na nilijadili na wadau niweke content ya aina gani kwenye mtandao ili niweze kupata traffic.Pia tulizungumza mambo ya kuzingatia kwenye kufanya option ya Voice chat (Twitter Spaces na Clubhouse), Livestream na Podcast. Ungana nasi sasa kusikiliza toleo hili na usiache kuingia pale Twtter @yesayasoftware

    Usalama wangu kwenye Mtandao na Ally

    Play Episode Listen Later Jun 27, 2021 26:01


    Hey Mambo vipi, jina langu ni Yesaya na hii ni Yesaya Software Podcast. Leo ninazungumza na Ally Ndimbo mtalaam wa usalama kwenye mtandao, tumezungumza mengi ikiwa ni pamoja na historia ya usalama kwenye mtandao na sheria zinazotulinda hapa nyumbani Tanzania.

    Mchango kwenye Open Source Community na Kalebu

    Play Episode Listen Later Jun 6, 2021 25:24


    Asante sana kusikiliza Yesaya Software Podcast na Leo ninazungumza na Kaleb Gwalugano. Kaleb ni Software Developer na nilifanya mazungumzo nae kuhusu mchango wake kwenye Open Source community. Je, unadhani1. Kuna wajibu kutoa mchango wako kutengeneza na kusaidia Open Source project?2. Na vipi unaweza kabiliana na mani hasi wakati ukiwa unajaribu kusaidia Open Source project.Basi waambie wengine unaweza kusikiliza Yesaya Software Podcast kupitia Google au Apple Podcast vilevile kwenye Spotify au Amazon Music. Pia kuna Youtube channel ya Yesaya Software ambayo ninawek a video kuhusu programming na zipo tutorial kadhaa unazoweza ziangalia.

    Marvin amenipatia uzoefu wake kuhusu Developers’ Community nchini Kenya

    Play Episode Listen Later May 29, 2021 32:29


    Asante sana kusikiliza Yesaya Software Podcast na leo ninazungumza na Marvin Collins kutoka nchini Kenya. Marvin ni Software Developer, sasa kuna mambo machache nilipenda kujadiliana na kubadilishana mawazo kuhusu Developers' Community nchini Kenya.1. Namna startup za kenya zinafanya kazi2. Ni vipi covid -19 imeathiri meetup za Developers3. Kuna urahisi au ugumu kuanzisha tech startup nchini KenyaBasi waambie wengine unaweza kusikiliza Yesaya Software Podcast kupitia Google au Apple Podcast vilevile kwenye Spotify au Amazon Music. Pia kuna Youtube channel ya Yesaya Software ambayo ninaweza video kuhusu programming na zipo tutorial kadhaa unazoweza ziangalia.

    Jetpack Compose na Muelekeo wa Kutengeneza App za Android

    Play Episode Listen Later May 22, 2021 27:02


    Mambo vipi, kwenye toleo hili nimezungumza na Stephen Chacha, Stephen ni Android na Machine Learning Developer kutoka nchini Kenya. Nilifanya majadiliano nae kuhusu Jetpack Compose kama UI toolkit kwenye Android.Tumejadili mambo kadhaa kwa kuanza na Jetpack Compose ni nini, urahisi unaoletwa na Jetpack Compose katika kutengeneza app yako, na je inafanya kazi na Java na ninaweza itumia sasa kwenye production apps?

    Lambert Katueleza Umuhimu wa Kanzi Data (Database)

    Play Episode Listen Later May 15, 2021 35:02


    Mambo vipi, kwenye toleo hili nimezungumza na Lambert Almasi, Lambert ni mtalaam wa kanzi data yaani database. Ninafahamu msingi wa mfumo wowote uko kwenye kanzi data. Mazungumzo yangu ya Lumbert yalijikita katika kuchanganua kwa kina umuhimu wa kanzi data na shughuli ambayo msimamizi wa kanzi data au Database Administrator anapaswa kufanya.Kwenye mazungumzo yetu. nilitambua dhamani kubwa waliyonayo hawa wasimamizi wa kanzi data ikanilazimu kudadisi zaidi kwa Lambert kuhusu faragha au privacy ya taarifa kwenye kanzi data, nina imani ujifunza sana.

    databases lambert mambo kwenye database administrator umuhimu kanzi
    Sikiliza Hamasa kutoka kwa Neema kuhusu Python

    Play Episode Listen Later May 8, 2021 19:53


    Mambo vipi, kwenye toleo hili nimezungumza na Neema Rajabu, Neema ni mhadhili msaidizi yaani assistant lecturer na mbobezi kwenye eneo la Software Engineering. Nilitamani kupata hamasa kutoka kwake kuhusu Python Programming Language. Kuna nini huko, ina wepesi gani na pengine kupata historia yake kidogo.Tuliangazia kwa mapana kuhusu language hii pia frameworks na community support ya Python ikoje?  

    Wazo la Kidigitali kuwa Bidhaa na Clemence

    Play Episode Listen Later May 1, 2021 24:44


    Mambo vipi, kwenye toleo hili nimezungumza na Clemence Mutalemwa, Clemence ameunda mfumo wa OCApp, ni mfumo unaowawezesha wanafunzi wa vyuo mbalimbali kufanya clearance baada ya kumaliza masomo yao. Nijadiliana nae kimsingi namna ambayo wazo la kidigitali linazaliwa, hatua katika kutekeleza wazo hilo na hatimae kupata bidhaa ya kidigitali. Mazungumzo yetu yalijikita katika mfumo wa OCApp kama case study, ambatana nasi sasa kuna jambo utajifunza. 

    Yesaya Software Update April 25, 2021

    Play Episode Listen Later Apr 25, 2021 0:52


    Hey mambo vipi,Asante sana kwa time yako na kuendelea kusikiliza Yesaya Software Podcast. Nilikuwa kimya lakini nimerudi na mipango mingi kwa ajili yako.Kila jumamosi kutakuwa na episode mpya na tayari nimekwisha kurekodi episode za kutosha kuhakikisha hukosi toleo jipya kila ifikapo jumamosi.Nimeweka pia video kadhaa kule YouTube kuhusu Jetpack Compose, ninafurahi sana na progress yake.Ninadhani kuna mambo mengi ninaweza kukujulisha katikati ya wiki na hivyo nitakuwa naweka mara kwa mara Bonus Episode nikikupa update kuhusu Yesaya Software.Fanya hima sasa pita kule YouTube @yesayasoftware na subscribe sasa.

    Jetpack Compose toolkit mpya kwenye Android

    Play Episode Listen Later Apr 25, 2021 1:21


    Jetpack Compose ni toolkit ya kisasa kutengeneza native Android UI. Imejikita katika declarative programming model, ambayo inakupa wepesi kwa kusema tuu unataka UI yako ionekanaje, na Compose itafanya mengi kwa ajili yako wakati app inabadili state, na UI yako itajiupdate automatically.Kwa kuwa imetengenezwa na Kotlin, basi inafanya kazi vizuri kabin na Java Programming Language na kutoa direct access kwa APIs zote za Android na Jetpack. Pia iko compatible na existing UI toolkit, so hapa unaweza mix and match classic (zile za XML) and new views na imetengenezwa kwa Material Theme pia animation kama zote vile tokea awali tuu.For the best experience developing with Jetpack Compose, nakushauri pakua sasa the latest canary version of Android Studio Preview. Kwa sasa Jetpack Compose iko kwenye Beta Version iliyotoka Mwezi wa Pili tarehe 24, na sasa ipo Beta 5 wakati narecord chapisho hili.Sasa kaa tayari tuanze pita code kwa Kotlin na Jetpack Compose, tupia like na subscribe sasa.

    Adam ametupa Somo na Safari ya Kuilea bidhaa ya Kidigitali

    Play Episode Listen Later Apr 24, 2021 30:28


    Mambo vipi, kwenye toleo hili nimezungumza na Adam Duma, Mjasiliamali wa kidigitali na kilimo, yeye pamoja na wenzake wameanzia mfumo mahiri wa Smartclass. Nilipenda kufahamu namna walivyoweza kuanzisha wazo lao hili, kulisimamia na pia changamoto wanazopitia?  

    Maandalizi na Uandishi wa CV kwa Developers na Umuhimu wake

    Play Episode Listen Later Nov 28, 2020 27:43


    Mambo vipi, kwenye toleo hili nimezungumza na Justin Chanda, Senior Software Developer huyu amefanya kazi na kwenye makampuni makubwa hapa Tanzania. Nilipenda kufahamu anapenya penyaje kwenye hizi interview, lakini kubwa anaandika nini kwenye CV yake? Umuhimu wa CV kwa Developer ukoje, na je ni CV moja kwa kazi zote utakazo ziona au kila kazi ya CV yake?  Justin amenieleza CV ni muhimu katika kupata kaziMambo gani ya kufanya kabla ya Kuandika CVMambo gani ni muhimu kuweka kwenye CV ya Developer?CV inaweza kusaidia kupata kazi hata kama sina experience?CV inatumika vipi kwenye interview/usaili

    wake developers cv tanzania mambo job applications senior software developer umuhimu
    Simeon amechambua mambo mapya ndani PHP 8

    Play Episode Listen Later Nov 21, 2020 28:52


    Mambo vipi, kwenye toleo hili nimezungumza na Simeon Mugisha Rwegayura mütalaam maridadi na mzoefu huyu kwenye mambo ya programming. Kama unavyofahamu November 26, 2020 toleo jipya ya PHP litatoka na hapa ninamaanisha PHP 8. Nilizungumza na Simeon kutusu nini tunatarajia katika toleo hili, linakuja na mambo gani mambo.Mazungumzo yangu na Simeon yalijikita kwenye feature mpya zilizopo kwenye PHP 8, kama1. Union Types2. Attributes3. FFI4. Just In Time CompilationNa mengine mengi. Check reference toka Spatie

    Nimeongea na Mke wangu kuhusu Maisha ya Mahusiano kwa Programmers

    Play Episode Listen Later Nov 14, 2020 23:14


    Mambo vipi, kwenye toleo hili nimezungumza na Dorah P. Ndazi ana title mbalimbali muhimu kabisa lakini kubwa kabisa ni mke wangu dada huyu na nilipenda kupata mawazo yake kuhusu kuishi na Programmer, changamoto anazopitia na ushauri wake. Niligusigusia tuu kuhusu kulea watoto, kusheherekea mambo mbalimbali kama birthday na vile uko na code inasumbua lakini unafanyaje kutoa muda kuwa na familia.Pia inakuwaje kufanyia kazi project isiyo na pesa wakati unadedicate muda wako kama mke anakabilianaje na hilo, unaonekana unafanya kazi na hakuna income yoyote, ni vipi unabaki kwenye lengo katika hali hii.Unafahamu nilimpataje?Nilikuwa na wakati mzuri sana kuzungumza na mke wangu kuhusu maisha ya mahusiano na programmer. Episode hii imenipa fursa binafsi kufahamu mambo anayoniwazia mke wangu na changamoto ninazompa kwa kazi yangu.  Hii itanisaidia katika kuyapa kipaumbele maeneo ambayo hayatasababisha nimkoseshe furaha na nizidi kuipatia familia yangu muda unaostaili na pia nijipange vizuri katika kazi zangu.It was a true conversation between us, na ninafuraha tumeweza zungumza.

    Maandalizi ya Devfest November 07 -08, 2020 na Faida ya Kushiriki Event hii ya Developers

    Play Episode Listen Later Oct 24, 2020 31:07


    Mambo vipi, kwenye toleo hili nimezungumza na waandaji na washiriki wa Sherehe ya Developers hapa Tanzania yaani Devfest. Devfest ni sherehe za kila mwaka kwa developers, tumekuwa tukienda pale Buni pamoja na yote kuhusu TEHAMA tumekuwa tukila na kujumuika kwa pamoja. Sasa sherehe hizi zimenasimamiwa na community ya Google Developers Group (GDG), kupata update kutoka kwao wafuate pale Twitter @GDGDarEsSalaam.Kwenye mazungumzo haya nilimwalika Georgia, yeye ni mmoja wa waandaji wa sherehe hizi, yupo pia Veronica ambaye mwaka jana alikuwa sehemu ya walioshiriki kuendesha sherehe hizo. Ninao pia wazungumzaji (speakers) kwenye event ya mwaka jana (David Tan pamoja na Fred German). Event hii kwa mwaka jana ilipata wageni kutoka nje ya nchi, nilimwalika Frank Tamre kutoka Kenya azungumze nasi. Hebu angalia link Pale Twitter na kwenye maelezo ya Podcast hii,ujiandikishe kushiriki event ya mwaka huu.Link: https://www.meetup.com/GDG-Dar-es-Salaam/events/273674254/

    Nimefanya Uchambuzi wa Episode Tisa (9) Zilizopita

    Play Episode Listen Later Oct 17, 2020 20:25


    Mambo vipi, kwenye toleo hili nimezungumza na … anyways leo mwenyewe na sina mgeni hapa nimeona ni vyema kukafanya mapitio ya matoleo tisa (9) yaliyopita na episode ya 10 imekuwa ni ya kipee kabisa kama milestone muhimu ya kujitafakari na kupata feedback kutoka kwako.Nimefanya uchambuzi wa matoleo tisa (9) yaliyopita, nimekukumbusha machache wasemaji wetu walivyochangia. Ilikuwa wakati mzuri sana na nimejifunza mengi sana kupitia wao. Nawashukuru sana sana.Episode 01 - GeorgiaEpisode 02 - SamEpisode 03 -  JonathanEpisode 04 - NaaminiEpisode 05 - BillyEpisode 06 - EphraimEpisode 07 - Dr. NeemaEpisode 08 - MohamedEpisode 09 - AnthonyKipee kabisa napenda niwashukuru wasikilizaji kwa kusikiliza Yesaya Software Podcast, nifuraha kubwa sana jumuika pamoja nanyi na ninapata hamasa na moyo kuendelea kwa ujumbe na comment mnazo nitumia. Nawashukuruni sana.Kwenye toleo hili nimegusia tuu pasi na umuhimu ujio wa Yesaya Software Website, Chatbot pamoja na Mobile app, Na kwa maana ya kuchangia huduma hii nitaanzisha e-commerce page ambapo nitaweka vitu kama t-shirts, kofia na stiker mbalimbali kuhusu Programming and Developers tool ili kuweza changia huduma nayo fanya.

    Anthony ametupa chachu na hamasa kwenye Data Science, Machine Learning and AI kwa nchi zinazoendelea

    Play Episode Listen Later Oct 10, 2020 33:05


    Mambo vipi, kwenye toleo hili nimezungumza na Anthony Faustine, yeye ni ni Data Scientist na Mtafiti kwenye masuala Machine Learning. Anafanya kazi kwenye kampuni mojawapo huko Ireland akaimplement Data Analytics na Artificial Intelligence Solutions kwenye maeneo mbalimbali. Pia Anthony amejikita kwenye kutumia machine learning, deep learning, data science, na signal processing kutengeneza computational models, methods, and tools ili kusaidia watunga sera kubuni suluhisho na sera bora zaidi kwa maendeleo endelevu.

    Mohamed ametueleza alifikaje Google na namna Maisha yalivyo huko

    Play Episode Listen Later Oct 3, 2020 30:37


    Mambo vipi, kwenye toleo hili nimezungumza na Mohamed Mnete, yeye ni Software Engineer kule Google. Nilifanya mahojiano naye akiwa huko Texas Marekani.Tunasikia mengi lakini kwa kuwa yupo ndugu yetu huko Google nilipenda yafahamu maisha ya huko Google yakoje, wanafanyaje kazi na kubwa kabisa huyu Mtanzania aliweza pata fursa hii adhimu kabisa.Pia nikagusiagusia kama upo uwezekano wengine kujiunga huko kama kuna links and website za kutumia kufanya maombi.

    Daktari Neema na Siri ya Kupata PhD katika Umri Mdogo

    Play Episode Listen Later Sep 26, 2020 31:10


    Mambo vipi, kwenye toleo hili nimezungumza na Daktari Neema Mduma, mhadhiri kutoka Taasisi ya Sayansi na Teknolojia Nelson Mandela, Arusha. Nilipenda kufahamu aliwezaje fikia ngazi ya PhD katika umri mdogo, safari yake ilikuwaje kufika huko, nilipenda kufahamu kuhusu utafiti wake sababu, matokeo na mapendekezo yake.Nilianza kwa kumuuliza Daktari Neema historia ya elimu yake, mawazo yangu yalikuwa amesoma nje ya nchi na ndio sababu amemaliza PhD katika umri mdogo. Daktari ameniambia kila mtu amempa nchi yake anayodhani amesoma huko, hebu sikiliza toleo hili ujue ukweli halisi. Ila kimsingi Daktari anasema, hakuna linaloshindikana kama umeweka lengo ni lazima ulikamilishe ndio nguzo iliyomfikisha hapo alipo.Niliendelea na mahojiano yangu na Daktari kwa kutaka kufahamu kuhusu utafiti wake, nilipenda kujua sababu, matokeo na mapendekezo yake. Utafiti wake ulilenga kutatua tatizo la wanafunzi kuacha shule yaani “Student Dropout”.Daktari anasema ametumia Teknolojia ya Akili Bandia (Artificial Intelligence) ili kuweza kutatua tatizo kabla halijatokea tofauti na kuwasaidia wanafunzi wakati tayari ameacha shule. Ameniambia matokeo yake na muhimu hapa ameangalia characters za wanafunzi , au viashiria vya mwanafunzi kutaka kuacha shule. Ametoa mapendekezo yake ambayo ninadhani ukisikiliza utapata vingi zaidi.Ukiachilia kazi na mafanikio yake kwa kupata PhD, Daktari ameshirki makongamano mengi ndani na nje nchi kwenye eneo la Machine Learning. Pia mimi nimegundua Daktari Neema ni mwandishi mzuri kweli, amepublish papers kadhaa unaweza kupita pale kwenye Website ya chuo cha Nelson Mandela.Daktari ni mwanzilishi wa initiative ya #BakiShule, lengo ni kuwapa hamasa wanafunzi wa shule kufikia malengo yao.  #Baki shule inawakutanisha wanafunzi na role model kwenye elimu, na kuwapa uelewa kuhusu Machine Learning.Nimeongea mengi sana na Daktari Neema na kubwa amekuwa akishirikisha fursa mbalimbali hebu mfollow pale Twitter (@nakadori) ili uweze kupata fursa nyingi kutoka kwake.Nina imani mazungumzo haya yatakusaidia na kukupata hamasa na moyo pale ulipokwana, go out and make that happen, hakuna linaloshindikana kutoka kwa Daktari Neema Mduma. #RoleModelWaWengi

    Ephraim Katupa somo la Kubaki kwenye Malengo na Ujasiriamali

    Play Episode Listen Later Sep 19, 2020 21:40


    Mambo vipi, kwenye toleo hili nimezungumza na Ephraim Swila yeye mjasiriamali wa TEHAMA na mkurungezi wa kampuni ya Inets. Nilipenda kufahamu wamewezaje kudumu kwenye ujasiriamali, walianzia wapi na wako wapi sasa.Nilipata wasahaa mzuri zungumza na Ephraim, ni kiongozi wa mfano hakika na nina amini ukifuatilia mazungumzo yetu kuna jambo jema na zuri utajifunza.Ephraim amenijulisha walianza harakati za ujasiriamali toka wakiwa chuo na ukisikiliza mazungumzo yetu utaona namna mwanzo watu hujitokeza na mambo yakianza kuwa magumu waanza potea.Ephraim amenipa hamasa na kunifundisha uvumilivu katika kuweka na kukamilisha malengo. Ni dhahiri kuwa na timu nzuri ni jambo la muhimu, lakini kwenye mazungumzo yetu amegusia kuhusu common value. Hebu pata muda fuatilia mazungumzo haya kujua zaidi kuhusu hili.Amenieleza changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na Ujuzi (Skills), na amefanunua vizuri sana kwamba hii ndio hatari kubwa sana kwenye Ujasiriamali wa TEHAMA.Ephraim amenifumbua kuhusu ushirikiano wa developers huku akiweka bayana Mafanikio ya Ujasiriamali wa TEHAMA hutengea mashirikiano (partnership).Hakika, nina imani utajifunza mengi sana kwenye mahojiano haya, kubwa kabisa amegusia matamanio na ushauri wake kuona uwepo wa association au board ya sector ya Software hapa Tanzania. Hii itasaidia linda maslahi ya sector software, ameniambia mambo ya patent and business secret. Nisaidie kupaza sauti kuhakisha hili tunalifanyia kazi kwa umoja wetu.Vipi kuhusu funding, pia Ephraim ameniambia nini kiliwalinda na pia kama walishawahi kuwa accerated au lah.Subscribe Google au Apple Podcast @yesayasoftware

    Billy Ametupa Uzoefu wake Kuongoza Google Developer Student Club

    Play Episode Listen Later Sep 12, 2020 21:40


    Mambo vipi, kwenye toleo hili nimezungumza na Billy Patrick yeye amehudumu kama Google Developer Student Club Lead katika chuo cha Uhasibu Arusha (IAA). Nilipenda kufahamu mchakato mzima wa kuomba nafasi hiyo, ushirikiano aliopata kwa uongozi wa chuo na wanafunzi, na vipi kuhusu changamoto alizopitia.Billy amenieleza Google Developer Student Club ni nini, namna inavyofanya kazi pia namna ya kufanya applicaion. Walengwa wa Google Developer Student Club ni kina nani.Billy amenijulisha kwa mwaka 2019/2020 ni chuo cha Uhasibu Arusha pekee hapa Tanzania ndio kilikuwa na Google Developer Student Club. Hii inafanya Billy yeye kuwa Google Developer Student Club Lead wa kwanza kwa vyuo hapa Tanzania.Billy ameniambia, kwa mwaka 2020/2021 kuna vyuo vitano, nadhani haya ni maendeleo makubwa katika kujenga developers wa kiwango hapa Tanzania.Billy amenieleza alipata ushirikiano wakutosha kwenye chuo cha Uhasibu Arusha, big shout out kwa chuo cha Uhasibu Arusha kwa support kubwa hii maana waliweza toa hata Computer Lab kwa Google Developer Student Club.Billy ameniambia mengi ikiwa ni pamoja na majukumu sasa ya Google Developer Student Club Lead na pia changamoto walizopitia. Pia amenipa faida alizopata katika kipindi chake alichohudumu kama Lead, na nini atafanya sasa baada ya kumaliza muda wake.Ninahamasika vya kutoka na hamasa aliyotupa Billy, nimefurahishwa na namba ya vyuo vingine kuongezeka kujiunga na Google Developer Student Club. Vilevile hamasa ametoa kwa vyuo vingine kuweza support jitahada kama hizi kuweza andaa developers kwa kuweza jifunza Technolojia mbalimbali. Fuatilia sasa uweze kusikiliza haya na mengine mengi kutoka kwa Billy.

    Safari ya Naamini kwenye Android Apps Development

    Play Episode Listen Later Sep 5, 2020 29:26


    Mambo vipi, kwenye toleo hili nimezungumza na Naamini Yonazi yeye ni Android Developer, pia ameshiriki kwenye makongamano ya Developer mbalimbali kama msemaji (ndani na nje ya nchi) vilevile ameandaa meetup kadhaa za Developers. Nilipenda fahamu safari yake na kufika alipo na je alipitia njia gani?Naamini amenieleza alikuwa na kampani nzuri akiwa chuo ambayo ilimsaidia kufanya mazoezi zaidi kwenye programminng. Pia jamii ya Developer (mfano @gdgdar) ni chachu ya yeye kupanua uelewa na mahusiano baina na Developers. Amenieleza kuhusu changamoto alizokabiliana nazo wakati akianza kazi, kubwa ikiwa na kutopata sauti ya kusikika hasa kwa developer wakike. Kutokuaminika kama wanaweza fanya code kama vijana wakiume. Amenieleza hali imekuwa ikiimarika na hivyo hata kwenye ajira kwa wadada kama uko vizuri fursa ni nyingi na unachotakiwa ni kuonyesha uwezo wako katika kazi. Kwa haya na mengine mengi unaweza fuatilia toleo hili nilipozungumza na Naamini Yonazi.

    Jonathan anatueleza kuhusu DevOps

    Play Episode Listen Later Aug 29, 2020 26:23


    Mambo vipi, kwenye toleo hili nimezungumza na Jonathan Kayumbo yeye ni DevOps and Infrastructure Engineer nchini Sweden, nilitaka kufahanu kuhusu DevOps, ina faida gani, vipi tunaweza itumia hapa Bongo na vipi kuhusu tools zinazohitajika.Jonathan amesoma Tanzania na kuweza kwenda kufanya kazi nchini Sweden, anafanya kazi kama DevOps and Infrastructure Engineer kwenye moja ya kampuni kubwa kule Sweden. Ametueleza namna alivyopambana kuendana na utendaji wa kazi na kuadopt best practices za Software Development.

    Sam aliwezaje Kujiunga na Kufanya Kazi Andela

    Play Episode Listen Later Aug 22, 2020 19:51


    Samwel Charles ni mtanzania na Software Engineer Andela/Cloudflare. Amesoma na kufanya kazi hapa nyumbani Tanzania, lakini aliona fursa kufanya kazi Andela na kwenye toleo hili atatueleza aliwezaje fanikisha hilo.Sam ameeleza hatua alizopitia kutokea mwanzo kabisa namna alivyoona fursa kutoka Andela, namna alivyojisikia baada kufika Andela na namna wanavyofanya kazi huko.

    Umuhimu wa Kujenga Jamii au Community ya Developers

    Play Episode Listen Later Aug 14, 2020 19:19


    Kwenye toleo hili nimezungumza na Georgia kuhusu umuhimu wa kujenga jamii au community ya Developers hapa nchini. Georgia ni mdau muhimu sana katika kuandaa meetup nyingi za Developers hapa Tanzania na pia anahusika na Google Developer Group (GDG) Dar, Women Tech Makers Dar es Salaam na Facebook Developers Cycle. 

    Tujadili Kotlin Pamoja Julai 27 - #KotlinEverywhere Dar es Salaam

    Play Episode Listen Later Jun 23, 2019 3:29


    Kotlin ndio lugha chagua kwa Google kwa kutengeneza mifumo katika program ya Android. Java huenda isiendee tumika na kupata usaidizi wa moja kwa moja toka Google hapo baadae.

    Kuwa Mtengeneza Mifumo Tanzania: Changamoto na Fursa

    Play Episode Listen Later May 26, 2019 13:02


    Kuwa Mtengeneza Mifumo Tanzania kunaambatana na changamoto na fursa mbalimbali. Katika toleo hili nitakurudisha enzi za zamani nakupata hadhithi za watengeneza mifumo wa zamani. Pia nitakusimulia niliaonza chuo changamoto nilizopitia na kupata kazi. Pia nimeainisha fursa zilizopo sasa kwa watengeza mifumo wa leo.

    Nitazungumza nini kwenye Mafunzo Mbeya?

    Play Episode Listen Later Mar 24, 2019 3:40


    Fuatilia toleo hili kujua ni nini nitazungumza kwenye mafunzo Mbeya juu ya Computer na namna tunayoweza itumia kama vijana na wanafunzi.

    Nimefanya nini Wiki Mbili?

    Play Episode Listen Later Feb 24, 2019 8:24


    Ebwana mambo vipi, leo nitakupa taarifa ya kazi nilizofanya kwa wiki mbili.

    Machine Learning imekuja, Usiachwe Nyuma

    Play Episode Listen Later Feb 4, 2019 4:36


    Ebwana mambo vipi jina langu ni Yesaya. Ninakukaribisha kwenye mfululizo wa vipindi kwa njia ya sauti yaani Podcast. Dhumuni langu ni kukuelimisha, kukuhabarisha na kukuletea mijadala mbalimbali kuhusu Teknolojia ya Habari na Mawasiliano - TEHAMA, na mimi nitajikita zaidi kwenye mifumo ya kompyuta. Leo tutaangalia kwa nini hupaswi acha nyuma na hili joto la Machine Learning na kwa wepesi tuu ni vipi Machine Learning inafanya kazi. Kumbuka wiki iliyopita nllikupa chachu tuu ya Machine Learning na kama bado hujasikia toleo lililopita nakusihi sasa usikilize ili twende pamoja. Na kwa tarifa tue, katika mwaka 2018 Machine Learning ilionekana kama moja ya Teknolojia zilizo zungumzwa sana, bado hata mapema mwaka 2019 ni mojawapo na teknolojia zinazongumwa kwa wingi. Si miaka mingi sana tangu Machine Learning ipate umaarufu na hata kampuni kupata uvuvi juu ya matumizi yake. Lakini sasa makampuni mengi yanahaha uhitaji tumia Machine Learning katika kutoa huduma zao. Imekuwa kama ni hitaji la muhimu katika mifumo. Kama ilivyokuwa muhimu kwa kampuni iwe na website itakayo weza onekana vizuri kwenye simu. Ni karibuni tuu makampuni yatahitaji mifumo ambayo itaweza toa ripoti zilizofanyiwa analysis kwa Machine Learning ili kuweza saidia toa maamuzi yatayoweza kuleta tija kwa makampuni. Machine Learning inatusaidia fanya Kazi za kibinadamu bora, haraka na rahisi kuliko wakati mwingine wowote. Na tukitazama mbele katika miaka iajyo, Machine Learning itatusaidia kufanya mambo ambayo hatungeweza kuyafanya wenyewe. Tunashuruku kuwa, si Kazi ngumu tena kuweza faidika na matunda ya Machine Learning sasa. Vyombo (tools) zimekuwa vizuri na rahisi sasa, unachohitaji ni taarifa, wetengeneza mifumo (developers) na hiari kuanza tumia Machine Learning. Tutazame kwa uchoche tuu namna ambavyo Machine Learning inafanya Kazi, Machine Learning inatumia taarifa kujibu maswali. Na hapa nimefupisha tuu, ili kuweza elewa kwa urahisi namna ambavyo Machine Learning inafanya Kazi. Sasa ngoja kwa urahisi kabisa tuangalia Machine Learning inavyofanya kazi. Ni lazıma tuwe na taarifa ili tuweze ifundisha Kompyuta. Na hapa nitakupa mfano mtoto anashika moto kwa mara kwanza ataangua na atatunza taarifa ya picha ya mato na maumivu yake baadae akiona hali hiyo hato thubuti kushika tena. Kwa namna hii tunaipa taarifa kompyuta ambazo zina maswali na majibu (kama ukigusa hapa utaungua) kisha yenyewe itajifunza kupitia taarifa hizo na baadae jambo jipya likija basi itaweza kulinganisha tariffa zilizopo kuweza jibu hilo jambo. Mfano kwa upande wa kutambua magonjwa, kompyuta itatumia taarifa za vipimo za wagonjwa wengi waliohudumiwa kwa miaka kadhaa kutoka maeneo mbalimbali na taarifa hizii ni pamoja na matokeo ya vipimo vyao kama alikuwa na ugonjwa au lah. Sasa basi, badare ya kujifunza, mgonjwa mmoja akija kompyuta itaweza kulinganisha na taarifa hizi kwa kila jambo kama umri, jinsia, urefu, wapi wanatokea na kadhalika. Ikimaliza inaweza toka utabiri ni kwa asilimia ngapi mgonjwa huyu anaweza kuwa na ugonjwa husika au lah. Kumbuka, ili Machine Learning ifanya kazi kwa ubora zaidi ni lazima kuwepo na taarifa za kutosha ili kuweza kutabiri kwa ufasaha zaidi. Na hapa tumejadili mfano mmoja tuu na hapa nimeeleza kwa kutumia nia moja ya kujifunza ya Machine Learning yaani Supervised Learning. Kwa haya machache ninaamini kuna jambo ambalo umeweza jifunza hapa, na hii ni moja ya jitahada kuweka hamasa au sensitisation kwa developers wa ndani kuona namna ambayo tunaweza tengeneza mifumo ya kompyuta. Mpaka wakati mwingine, jina langu ni Yesaya.

    Tujadili Machine Learning

    Play Episode Listen Later Jan 27, 2019 4:12


    Episode 8 Ebwana mambo vipi jina langu ni Yesaya. Ninakukaribisha kwenye mfululizo wa vipindi kwa njia ya sauti yaani Podcast. Dhumuni langu ni kukuelimisha, kukuhabarisha na kukuletea mijadala mbalimbali kuhusu Teknolojia ya Habari na Mawasiliano - TEHAMA, na mimi nitajikita zaidi kwenye mifumo ya kompyuta. Leo nitakupa chachu kidogo tuu kuhusu Machine Learning, nimejaribu kufuta maana yake kwa Kiswahili sijapata neno lililo rasmi juu ya Machine Learning. Ni imani yangu tutaelewana tuu hakuna tatizo kabisa, ndio Machine Learning. Dunia ya leo imejazwa na taarifa nyingi, nyingi sana, na tunazipata kidigitali sasa, taarifa hizi zinaweza kuwa picha, muziki, maneno, video na kadhalika. Nikuambie tuu, hali hii haitegemewi kusimama muda mufupi ujao. Taasisi mbalimbali na makumpuni mengi sasa huendesha shughuli zake kwa njia ya mifumo ya kompyuta. Sasa basi Machine Learning imekuja kuleta suluhu ya kuchakata taarifa hizi kwa niaba yako na kukufahamisha nini unapaswa kufanya. Kimsingi, binadamu tumekuwa tukichakata taarifa toka enzi, na baadae kupitia mifumo mbalimbali iliyopewa maagizo kuchakata taarifa mfano kwa kuandika formula mbalimbali kama unavyofanya kwenye Microsoft Excel na mifumo mingine ya kufanana na huu. Lakini sasa taarifa zinazokusanywa zimekuwa nyingi kupita uwezo wa binadamu kuzichakata na kuweza kupata maana na tafsiri ya taarifa hizo. Sasa basi, Machine Learning ni uwezo wa mashine au kompyuta kujifunza kwa kutumia taarifa zilizokusanywa na kuweza kutoa maana na tafsiri (insights) kutoka kwenye taarifa hizo. Machine Learning iko kila mahali sasa, na wengi tumeona hilo hata kama hujaona basi umetumia tayari bila kujua, kwani mifumo mingi mikubwa sasa nyuma ya pazia wanatumia Machine Learning. Wakati kumtag mtu kupitia Facebook ni mfano dhahiri Machine Learning na huwezi tambua mapendezo ya video za kuangalia kupitia YouTube imewezeshwa na Machine Learning. Bila shaka, labda mfano mzuri kabisa hapa ni Google. Kila wakati unapotumia Google kutafuta jambo, jua unatumia mfumo ambao unatumia Machine Learning nyuma yake ili kuweza tambua jambo unalotafuta na kuweza landana na maslahi yako binafsi kutokana na mazoea yako kwenye mtandao. Kwa mfano, umekuwa ukitafuta video za Diamond Platnumz kupitia Google. Google wakazutunza taarifa za maulizo yako, ili baadae waweze kuchakata taarifa kupitia Machine Learning ili kukupa majibu yatayoendana na mazoea yako. Hivyo ukija wakati mwingine ukiandika Diamond utaletewa taarifa za mwanamziki Diamond Platnumz na sio Diamond, yaani madini almasi. Leo, Machine Learning inatumika maeneo mbalimbali, kwenye utambuzi wa picha (Image Recognition), Utambuzi wa Ulaghi mitandao (Fraud Detection), Mifumo ya mapendekezo (Recommendation System) hasa kwenye tovuti za mauzo kupitia mitandao (ecommerce website), pia utambuzi wa maneno na sauti. Uwezo wa Machine Learning umeonekana kwenye maeneo ya Afya kuwezo utambuzi magonjwa ya kisukari (diabetic retinopathy) na kansa ya ngozi (skin cancer). Bila shaka umejionea kwenye upande wa usafirishaji kupitia magari yanayojipaki (self-parking) na yanayojiendesha (self-driving). Tupo sehemu nzuri sasa, katika majuma kadhaa yajayo tutaendelea na mada hii ya Machine Learning. Nikiwa bado ninaendelea na majaribio tegemea kufahamu zaidi namna ambayo unaweza anza fahamu vifaa (tools) na kuweza andaa mufumo wako utaoweza kutumia Machine Learning. Kwa haya machache ninaamini kuna jambo ambalo umeweza jifunza hapa, na hii ni moja ya jitahada kuweka hamasa au sensitisation kwa developers wa ndani kuona namna ambayo tunaweza tengeneza mifumo ya kompyuta. Mpaka wakati mwingine, jina langu ni Yesaya.

    Kuweka Vipaumbele kwenye Kutengeneza Mifumo ya Kompyuta

    Play Episode Listen Later Jan 20, 2019 9:04


    Ebwana mambo vipi bina langu ni Yesaya. Ninakukaribisha kwenye mfululizo wa vipindi kwa njia ya sauti yaani Podcast. Dhumuni langu ni kukuelimisha, kukuhabarisha na kukuletea mijadala mbalimbali kuhusu Teknolojia ya Habari na Mawasiliano - TEHAMA, na mimi nitajikita zaidi kwenye mifumo ya computer. Leo tutazungumza namna ya kuweka vipaumbele kwenye kutengeneza mifumo ya kompyuta. Bila kuweka vipaumbele unaweza tengeneza mfumo usioisha au ambao watu hawata tumia. Hivi karibuni nimekutana na mambo mawili ambayo yamenisukuma andaa podcast toleo la leo. Kama utakuwa umenifollow kwenye mitandao ya kijamii basi unaweza kuwa umekutana na post nitazozungumza hapa. Miezi michache iliyopita nilipata bahati pita eneo la Buiko, hapa ninaweza sema ni mpakani kati ya mkoa wa Tanga na Kilimanjaro, nilikutana na jamaa mmoja ambaye ametengeza mashine ya kubebea mizigo hapa mini unaweza sema KIRIKUU. Yeye ni fundi hivyo kwa kumia uzoefu wake na ubunifu ametengeza mashine hii yenye uweza wa kubeba mzigo katika jamii yake kusaidia kusukuma gurudumu la maendeleo. Nilishudia imebeba mzigo mkubwa wa tofali na unaweza angalia kwenye akaunti yangu ya Instagram kuona uwezo wa mashine hiii. Hivi karibuni pia nimekutana na nukuu ya Artistotle, “Well begun is Halt Done”. Hapa nimeelewa kwamba ninaweza anza jambo kwa hatua fulani ya ukamilifu wake. Ndio, huhitaji weka kila kitu kiwe tayari mwanzo, unaweza anza katika mazingira magumu japo lengo ni kufika mbali ya hapo ulipoanza. Niambie unatafari vipi juu ya haya mambo, yawezekana kuna jambo ulipanga anza na wewe uliweka sababu za kukufanya usiendelee kamilisha jambo ulilopanga. Pengine ulisema sina hiki au kile ndio maana sijaweza kamilisha. Mfano mzuri huenda ukawa ulipanga anza kufanya programming lakini huna kompyuta nzuri, ukasema usibiri mpaka utakapo pata muda, au ukasema sasa nina majukumu mengi ukasema usubiri kidogo majukumu yapungue. Sasa basi, hapa nilitaka zungumza mambo ya kuzingatia wakati unaanza tengeneza mifumo ya kompyuta. Lakini pia ni vyema uwe tayari kujidhibiti juu ya vishawishi utakavyopata wakati umeanza kazi au hata ukiwa katika ya utekelezaji. Mara nyingi tunapajadili wazo ambalo tunataka lifanyia kazi liwe mfumo maono yake huwa mazuri na yakupendeza sana. Na mara nyingi ili uweze pata na heshima kwa mteja wako utaongea mambo mbalimbali ya kupamba wazo na namna utakavyolitekeleza, mambo ambayo yatayopelekea mteja apate hamu ya kupata mfumo mapema na kusababisha muda wa mradi kufanyika kwa muda mfupi zaidi. Nilisema mwanzoni utapaswa jizuia, kuna wakati ukiendelea na kazi teknolojia mpya inaweza kuja na kupelekea kazi kuiona itakuwa rahisi kama utatumia teknolojia hiyo. Vumilia maliza na moja uliokuwa unaijua baadae kwenye matoleo ya mbele utaboresha zaidi kutumia teknolojia hiyo mpya. Pia muonekano wa mfumo wako ni eneo la kutazama sana, kwa unaweza poteza muda mwingi kama hautafanya maandalizi mazuri. Na hapa nazungumza hatua ambayo mara nyingi huwa tunaipotezea kidogo. Hii ni hatua ya User Interface Design, tunaenda chukua template flani au tunaanza bahatisha wakati tunaendelea na kazi. Unaweka rangi ya njano mara unaona haijakaa vizuri unaweka blue na baadae mteja pia unasema weka nyekundu. Mpango hauyaweka haya yalipaswa fanyanyika mapema kabisa. Ni vizuri sasa tukazingatia mambo haya ili kutafanya mfumo usiishe na pia ukifanya mpaka hatua flani, shirikisha watumiaji wape waanze tumia utapata mchango mkubwa wa namna ya kuboresha mfumo wako. Nakumbuka WhatsApp ilipoanza tulikuwa hatutumi picha tukawa tunatuma ujumbe tuu, baadae picha tukaanza tumiana ila voice note ilikuwa bado hadi sasa tunaweza piga hata simu za maneno na video pia. Huu ndio ukuaji wa mfumo, kutoka hatua moja mpaka nyingine. Tazama kwa makini uone unaanza na llpi litafuata lipi, yaweke vizuri kwenye mpango kazi wako kisha fanyia utekelezaji kwa kuhakikisha unafikia malengo ulijiwekea. Kwa haya muchachee ninaamini kuna jambo ambalo umeweza jifunza hapa, na hii ni moja ya jitahada kuweka hamasa au sensitisation kuona namna ambayo tunaweza tengeneza mifumo ya kompyuta. Mpaka wakati mwingine, jina langu ni Yesaya.

    kilimanjaro bila kama sasa hii tanga hapa kwa yeye kwenye user interface design habari hivi lakini huu artistotle teknolojia
    Nianzie wapi Kutengeneza Mifumo ya Kompyuta

    Play Episode Listen Later Jan 6, 2019 5:58


    Ebwana mambo vipi, jina langu ni Yesaya. Ninakukabirisha kwenye mfululizo wa vipindi kwa njia ya sauti yaani Podcast. Dhumuni langu ni kukuelimisha, kukuhabarisha na kukuletea mijadala mbalimbali kuhusu Teknolojia ya Habari na Mawasiliano - TEHAMA, na mimi nitajikita zaidi kwenye mifumo ya Kompyuta. Leo tutazungumza wapi utaanzia tengeneza mifumo ya kompyuta, watu wengi wamekuwa wakiniuliza namna gani wanaweza anza tengeneza mifumo ya kompyuta au lugha gani nijifunze ipi ni bora kuliko nyingine. Na wengine hushangaa mambo ninayopost kwenye mitandao ya kijamii na kuuliza hivyo vinini unaweka, jibu linaweza kuwa rahisi kuwa ni Code. Lakini kwa mtu ambaye hayuko kwenye uwanja wa TEHAMA basi huwa natumia muda kidogo fafanua hili. Hapa huwa napenda anza na mfano wa kawaida kabisa, ili niweze zungumza na mtu kutoka Italia na tuelewane vizuri nitapenda jifunza lugha yake, vivyo hivyo kwa lugha nyingine. Sasa basi uzuri wa kompyuta inaweza tii maagizo yangu kwa mambo nitayotaka itumaa. Lakini nitawezaje ituma kompyuta? Kuna lugha kadhaa ambazo ninaweza kuzitumia kuwasiliana na kompyuta ili iweze nielewa nachotaka na kuweza tekeleza ombi langu. Zipo lugha maalumu kwa ajili ya kuwasiliana na kompyuta na si kiingereza wala kiswahili au kichina lah, hapa naongelea Java, Kotlin, Swift, C, C++, na kwa wale wakongwe kidogo basi unafahamu kuhusu Pascal, Fortran na Cobol na nyingine nyingi. Chochote unachoweza fanya kwenye kompyuta yako, simu au tablet kuna mtu alitumia muda wake kuiambia kompyuta kutekeza hayo inayofanya. Mfano mzuri kabisa, ni pale unapopata wazo ambalo unadhani unaweza liweka katika mfumo wa kompyuta. Tuseme wazo lako ni kuwa na mfumo ya mauzo na upate taarifa za mauzo na manunuzi unayofanya. Basi utatumia moja ya lugha za kompyuta kuanza andika maelekezo ambayo tunaita code. Maelezo hayo ni namna ambayo unataka kompyuta ifanye vile wewe unataka na kitaalaam tunaita requirements. Kazi hii inahitaji mpango mzuri sana na kuweza tafakari kwa kina namna ambavyo kompyuta itatekeleza maagizo utakayo ipa kwa hatua na utaratibu. Kuna wakati mambo huwa mengi hivyo kama mpango sio mzuri au kwa sababu nyingine unaweza sahau jambo na hivyo mfumo ukianza tumika unakumbuka umeacha jambo fulani. Na changamoto kubwa ni pale unapokea requirements kutoka kwa mteja wako lakini pale unapoendelea na kazi au unahisi umemaliza, mteja anakumbuka jambo au amefurahishwa na kuanza ongeza mambo mengine zaidi. Hivyo, ni vizuri kuwa na mpango ambao utakusaidia telekeza kazi yako. Sasa basi, ili kuweza anza tengeneza mifumo ya kompyuta, weka nia thabiti na jaribu anza tumia lugha moja na tekeleza mradi mmoja ili kuona unaendaje. Tafuta watu wanajua wakushauri na kukusaidia na pale unapota changamoto, pia Google, Google mpaka utapate unachotaka. Zipo course mbalimbali kwenye mtandao zitakazoweza kukusaidia anza tengeneza mifumo ya kompyuta, kama tovuti ya YouTube, Lynda.com, Udemy na nyingine nyingi. Kitu cha kumalizia hapa ni kuwa, utahitaji jitoa kwani utahitajika kuwa up to date kwa kusoma mambo mapya yanayotokea kila siku kwenye lugha uliyochagua. Na pia kuna wakati utakumbwa na changamoto ambayo solution yake huenda ni nukta tuu na kazi ikawa imekutesa kwa muda hata siku mbili au tatu. Ila usivunjike moja unaweza kufikia malengo yako. Na kwa taarifa tuu, katika mwaka 2018 ripoti kadhaa zimeripoti huko Marekani Software Developer (Watengeza Mifumo) ndio kazi bora zaidi. Katika miaka ya karibuni tumeshuhudia kuwepo kwa ajira za namba kubwa katika fani ya TEHAMA serikalini, yaani nafasi hadi 39 katika taasisi moja wote ni TEHAMA kuajiriwa kwa wakati mmoja na nyingine zinaendelea tangazwa. Bado fursa za uwekezaji kwenye TEHAMA, mashindano na makongamano mbalimbali yapo mtaani, kikubwa ni uwezo wako kukabiliana na kupigania fursa hizi, jipange kuwa bora sasa. Haya yote yanaoyesha kuwa kuna fursa nyingi na uhitaji unaongezeka siku hadi siku. Uwezo tunao katika kukabiliana na changamoto zinazotukabili, hivyo tusiwe nyuma mpaka tufanyiwe au tungoje watalaam kutoka mbali. Tunaweza na tupo tayari kwa wewe kuanza tengeneza mifumo ya Kompyuta sasa. Kwa haya machache nina imani kuwa jambo umejifunza hapa, na hii ni moja ya jitahida kuweka hamasa au sensitazation kwa developers wa ndani, kuona namna ambayo tunaweza anza tengeneza mifumo ya kompyuta. Mpaka wakati mwingine, jina langu ni Yesaya.

    Viashiria Kukusukuma Kutumia ChatBot - 2

    Play Episode Listen Later Dec 29, 2018 4:06


    Ebwana mambo vipi, jina lamgu ni Yesaya, ninakuletea mfululizo wa vipindi kwa njia ya sauti yaani Podcast. Dhumuni langu ni kukuelimisha, kukuhabarisha na kukuletea mijadala mbalimbali kuhusu Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) na mimi nitajikita zaidi kwenye mifumo ya kompyuta. Leo tutazungumza kuhusu viashiria vitakavyokusukuma kutumia ChatBot. Nimetoa mifano mbalimbali ya makampuni yanatumia ChatBot, kama CNN, Whole Food, Mwananchi Magazine, eShangazi, UBA Bank na KLM Royal Dutch Airlines. Ungana pamoja nami sasa unaweza pata tafsiri ya ChatBot kutoka katika mazungumzo haya.

    Viashiria Kukusukuma Kutumia ChatBot

    Play Episode Listen Later Dec 17, 2018 4:57


    Ebwana mambo vipi, jina lamgu ni Yesaya, ninakuletea mfululizo wa vipindi kwa njia ya sauti yaani Podcast. Dhumuni langu ni kukuelimisha, kukuhabarisha na kukuletea mijadala mbalimbali kuhusu Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) na mimi nitajikita zaidi kwenye mifumo ya kompyuta. Leo tutazungumza kuhusu viashiria vitakavyokusukuma kutumia ChatBot. Nimeeleza kwa mfano katika toleo hili juu ya namna ambayo unaweza onya uhitaji wa ChatBot. Kuna shughuli mbalimbali ambazo zimekuwa zikijirudia na huenda zikahitaji usaidizi wa haraka lakini kutokana na idadi kwa ya wateja ukashindwa wahudumia kwa wakati. Ungana pamoja nami sasa unaweza pata tafsiri ya ChatBot kutoka katika mazungumzo haya.

    Kwanini Nijiunge Andela?

    Play Episode Listen Later Dec 9, 2018 5:02


    Ebwana mambo vipi, jina lamgu ni Yesaya, ninakuletea mfululizo wa vipindi kwa njia ya sauti yaani Podcast. Dhumuni langu ni kukuelimisha, kukuhabarisha na kukuletea mijadala mbalimbali kuhusu Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) na mimi nitajikita zaidi kwenye mifumo ya kompyuta. Leo tutazungumza juu ya Mpango Wezeshi wa Andela kwa Watengeza Mifumo Barani Africa. Hapa nimeeleza kwa mtazamo wangu tuu Andela ni nini na vipi unaweza faidika kwa kujiunga na Andela. Kwa maelezo zaidi unaweza tembelea website yao andela.com.

    Claim Yesaya Software Podcast

    In order to claim this podcast we'll send an email to with a verification link. Simply click the link and you will be able to edit tags, request a refresh, and other features to take control of your podcast page!

    Claim Cancel