POPULARITY
Hii leo jaridani tunaangazia ripoti ya FAO ya uhaba wa chakula, Mwanaharakati kijana kutoka Kenya katika mkutano wa pili wa WSSD Doha, na mradi wa Mifereji ya Maji wa Jiji la Kampala (Kampala Capital City Drainage Master Plan) inayosaidia kupunguza mafuriko Uganda.Ripoti mpya ya pamoja kutoka mashirika mawili ya Umoja wa Mataifa lile la Chakula na Kilimo Duniani (FAO) na la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) inaonya kwamba uhaba mkubwa wa chakula unazidi kuongezeka katika maeneo 16 yenye njaa duniani, hali inayoweza kusababisha mamilioni zaidi ya watu kukumbwa na njaa kali au hatari ya kufikia kiwango cha baa la njaa.Mkutano wa Pili wa Dunia wa Maendeleo ya Kijamii umefunga pazia mjini Doha, Qatar, mwishoni mwa wiki hii, ukiwaleta pamoja viongozi wa dunia, mashirika ya kiraia na vijana wakitoka na wito wa pamoja dhidi ya umasikini, ukosefu wa usawa na kutengwa kijamii. Kutoka Kenya, mwanaharakati kijana amesema mkutano huo umekuwa wa kuhamasisha akitoa wito wa hatua za haraka.Kituo cha utafiti wa kusaka Suluhu kuhusu mafuriko kinachoendeshwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo (UNDP) nchini Uganda kimetumia maarifa ya pamoja kukabiliana na changamoto za mafuriko katika eneo la Makerere Kavule, makazi yasiyo rasmi yaliyo pembezoni mwa mji wa Kampala, mji mkuu wa Uganda. Kituo hicho kimeunganisha juhudi za jamii, maarifa asilia, na teknolojia ya kisasa kubuni mfumo wa mifereji ya maji unaoendana na Mpango Mkuu wa Mifereji ya Maji wa Jiji la Kampala (Kampala Capital City Drainage Master Plan). Mfumo huu unalenga kupunguza mafuriko si tu katika jamii hiyo, bali pia katika eneo la katikati ya jiji.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
Ripoti mpya ya pamoja kutoka mashirika mawili ya Umoja wa Mataifa lile la Chakula na Kilimo Duniani (FAO) na la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) inaonya kwamba uhaba mkubwa wa chakula unazidi kuongezeka katika maeneo 16 yenye njaa duniani, hali inayoweza kusababisha mamilioni zaidi ya watu kukumbwa na njaa kali au hatari ya kufikia kiwango cha baa la njaa. Anold Kayanda na maelezo zaidi.
Maelfu ya kaya za Wenyeji kaskazini mwa Australia wanaishi na mfumo wa kulipa kabla wa umeme, ambapo kukatwa kunaweza kutokea wakati wowote. Ripoti mpya sasa imeonya kwamba bila ulinzi wa kutosha, mfumo huu unaweza kuwa hatari katika joto kali.
Dunia inapojiandaa kwa mkutano wa kimataifa wa Mazingira COP30 utakaofanyika Belém, Brazil, ripoti mpya imeibua mjadala mkali—si tu kuhusu uzalishaji wa hewa ukaa, bali pia kuhusu ukosefu wa usawa. Utafiti mpya wa shirika la Oxfam, unaonesha kuwa mataifa tajiri na watu wachache wenye utajiri mkubwa wanachangia kwa kiasi kikubwa katika mabadiliko ya tabianchi. Inaitwa “ukosefu wa haki wa hali ya hewa.” Mtaalam wetu leo kulichambua hili ni David Abudho, anayeshughulika na mabadiliko ya tabia nchi barani Afrika kutoka shirika la Oxfam.
Shirika la Umoja wa Mataifa ka Utabiri wa Hali ya Hewa Duniani WMO linaongeza kasi ya jitihada za kulinda maisha ya watu dhidi ya madhara ya mabadiliko ya tabianchi. Mkutano wake Maalum uliofunguliwa leo mjini Geneva Uswisi, unalenga kuharakisha mpango wa kimataifa wa Tahadhari za Mapema kwa Wote, sambamba na maadhimisho ya miaka 75 ya WMO. Flora Nducha amefuatilia na anafafanua zaidi (TAAFIFA YA FLORA NDUCHA)Asante Leah, kwa mujibu wa WMO idadi ya nchi zenye mifumo ya tahadhari za mapema kwa ajili ya majanga ya tabianchi imeongezeka maradufu katika kipindi cha miaka kumi iliyopita lakini bado mamilioni ya watu hawana ulinzi dhidi yah atua hiyo muhimu.Ndiyo maana shirika hilo limewakutanisha mawaziri na wataalamu kutoka nchi wanachama 193 kuharakisha mpango wa Tahadhari za Mapema kwa Wote, uliozinduliwa mwaka 2022 na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres unatekelezwa kwa vitendo.Katika mkutano huo Celeste Saulo Katibu Mkuu wa WMO amesema “Miaka 75 iliyopita, Shirika la WMO lilianzishwa kutokana na ukweli kwamba hali ya hewa, maji na tabianchi havina mipaka ya kitaifa. Ushirikiano wa kimataifa katika uchunguzi na utabiri ni wa lazima, kwa sababu hakuna nchi inayoweza kufanya hivyo peke yake.”Ripoti mpya ya WMO, iliyopewa jina Tahadhari za Mapema kwa Wote Mtazamo wa Dunia, inaonesha kuwa licha ya maendeleo makubwa katika ubadilishanaji wa takwimu na utabiri wa kidijitali, bado kuna mapengo makubwa, hasa katika nchi maskini na visiwa vidogo vinavyoendelea.Celeste amesisitiza kuwa“Tahadhari za Mapema kwa Wote sasa siyo mpango tena, bali ni nembo ya mshikamano wa dunia. Pamoja, tunaokoa maisha, tunaunda sera, na kuimarisha mnepo.”Takwimu za shirika hilo zinaonesha uzito wa changamoto. Katika miaka 50 iliyopita, WMO inasema majanga yanayohusiana na hali ya hewa na maji yamesababisha vifo vya zaidi ya watu milioni mbili huku asilimia 90 kati yao ni katika nchi zinazoendelea.Na ingawa mataifa 108 sasa yana mifumo ya tahadhari za majanga mchanganyiko, shirika hilo linasema viwango vya vifo bado ni mara sita zaidi katika maeneo yasiyo na mifumo hiyo.WMO inasema teknolojia mpya ikiwemo akili mnemba na matumizi ya takwimu za setilaiti kwa wakati halisi zinabadilisha uwezo wa utabiri, lakini pengo la kidijitali bado linawaacha wengi wakiwa hatarini.“Mafanikio ya Tahadhari za Mapema kwa Wote hayapimwi kwa ripoti au maazimio, anasema Celesto bali kwa maisha yanayookolewa na riziki zinazolindwa. Tunapoelekea mwaka 2027, hebu tuongeze juhudi kuhakikisha hakuna mtu anayeachwa bila ulinzi.”Mkutano huo Maalum wa WMO utaendelea wiki nzima mjini Geneva, huku Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres akitarajiwa kuhutubia siku ya Jumatano.Shirika la WMO wakati likiadhimisha miaka 75 ya kile linachoita Sayansi kwa Vitendo linataka kuhakikisha sayansi hiyo inawafikia wote, kabla ya majanga kutokea.
Ripoti ya 2025 ya tathmini ya kidunia juu ya kupunguza hatari za majanga inakadiria kuwa gharama kamili ya kukabili majanga ni karibu dola trilioni2.3, na licha ya uwekezaji huu, bajeti za kitaifa bado ni za kiwango cha chini mno.
Takribani watu milioni 887 duniani ambao ni maskini wanaishi kwenye maeneo yanayokumbwa moja kwa moja na madhara manne yasababishwayo na mabadiliko ya tabianchi ambayo ni joto kali, mafuriko, ukame na uchafuzi wa hewa, imesema ripoti mpya iliyotolewa leo na shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo, UNDP kwa kushirikiana na wadau. Ripoti inaonesha bayana kuwa hali hiyo inazidi kutwamisha watu hao kwenye hali tete zaidi. Assumpta Massoi amepitia ripoti hiyo na kuandaa taarifa hii.
Hii leo jaridani tunaangazia ripoti ya UNDP ya umaskini, mradi wa kusaidia jamii kupambana na athari za mabadiliko ya tabianchi nchini Zambia na juhudi za kuboresha hali ya lishe kwa watoto nchini Kenya.Takribani watu milioni 887 duniani ambao ni maskini wanaishi kwenye maeneo yanayokumbwa moja kwa moja na madhara manne yasababishwayo na mabadiliko ya tabianchi ambayo ni joto kali, mafuriko, ukame na uchafuzi wa hewa, imesema ripoti mpya iliyotolewa leo na shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo, UNDP kwa kushirikiana na wadau. Ripoti inaonesha bayana kuwa hali hiyo inazidi kutwamisha watu hao kwenye hali tete zaidi.Mradi wa kusaidia jamii kupambana na athari za mabadiliko ya tabianchi nchini Zambia mbali na kusaidia wananchi kwenye kilimo pia umewawezesha kiuchumi na kuwaondoa baadhi yao kwenye mstari wa umasikini. Mmoja wa walio utupa mkono umasikini ni Judith Mabeta aliyetoka kuishi nyumba ya udongo mpaka kuwa na nyumba ya kupangisha na sasa ni mama mwenye nyumba.Kupitia msaada wa fedha kutoka Ufaransa, juhudi za kuboresha hali ya lishe kwa watoto nchini Kenya, hasa kwa jamii zilizo katika mazingira hatarishi zinaendelea ambapo juhudi za hivi karibuni ni kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) kwa kushirikiana na Shirika la Msalaba Mwekundu la Kenya ambao kwa pamoja wameimarisha huduma hizo kwa manusura wa mafuriko Magharibi mwa taifa hilo la Afrika Mashariki. Huduma hizi ni sehemu muhimu ya kuhakikisha watoto na familia wanapata vyakula vyenye virutubishi kwa ustawi wa maisha yao.Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!
Hii leo jaridani tunaangazia kiwango cha gesi ya hewa ukaa, yaani carbon dioxide au CO₂, siku ya Kimataifa ya Wanawake wa Vijijini inayotupeleka nchini Kenya kumulika juhudi za wanawake za kumudu mahitaji ya familia zao, na uvuvi na uhalifu katika Ziwa Victoria.Ripoti mpya ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Hali ya Hewa Duniani, WMO, inasema kiwango cha gesi ya hewa ukaa, yaani carbon dioxide au CO₂, kimeongezeka kwa kiwango cha kuvunja rekodi mwaka 2024, na kufikia viwango vipya vya juu zaidi kuwahi kurekodiwa.Kuanzia Oktoba 15 mwaka 2008 dunia imekuwa ikiadhimisha siku ya Kimataifa ya Wanawake wa Vijijini kama fursa ya kutambua mchango mkubwa wa wanawake hawa katika maendeleo ya kijamii, kiuchumi, na kimazingira.Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji IOM kwa kushirikiana na Ofisi ya Marekani ya Masuala ya Kimataifa ya kupambana na Dawa za Kulevya na Utekelezaji wa Sheria (INL), na mamlaka kutoka Kenya, Tanzania na Uganda wanashirikiana kuimarisha uwezo na kukabiliana na uhalifu wa kimataifa unaotekelezwa katika ziwa victoria ambao ukiachwa unaweza kuleta athari kwa zaidi ya watu milioni 40 wanaotegemea ziwa hilo.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
Ripoti mpya ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Hali ya Hewa Duniani, WMO, inasema kiwango cha gesi ya hewa ukaa, yaani carbon dioxide au CO₂, kimeongezeka kwa kiwango cha kuvunja rekodi mwaka 2024, na kufikia viwango vipya vya juu zaidi kuwahi kurekodiwa. Flora Nducha ameisoma ripoti hiyo na anatupa tathimini
Hii leo jaridani tnakuletea mada kwa kina inayoangazia siku ya Mwalimu Nyerere na tunakupeleka nchini Tanzania ambako kunaendelea juhudi za kuimarisha matumimizi ya lugha ya Kiswahili na utangamano katika Jumuiya ya Afrika Mashairki, manufaa ya kiuchumi na kijami na kuenzi mchango wa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.Umoja wa Mataifa leo umeonya kwamba Gaza itahitaji karibu dola bilioni 70 kwa ajili ya ujenzi upya baada ya miaka miwili ya mzozo, huku dola bilioni 20 zikitakiwa katika miaka mitatu ijayo. Makadirio haya yanatokana na, tathmini ya pamoja kati ya Umoja wa Mataifa, Muungano wa Ulaya, na Benki ya Dunia. Mwakilishi Maalum wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo UNDP kwa ajili ya programu za msaada kwa Wapalestina Jaco Cilliers,amesema “Viwango vya uharibifu sasa vimefikia karibu asilimia 84, na katika baadhi ya sehemu za Jiji la Gaza, ni hadi asilimia 92.”Umoja wa Mataifa umeongeza hatua zake za dharura huko Gaza kwa kutoa dola milioni 11 kutoka Mfuko wake wa Dharura (CERF) kukidhi mahitaji ya haraka kabla ya kuanza kwa msimu wa baridi. Mgao huu, uliozinduliwa na Mratibu wa Misaada ya Dharura Tom Fletcher, utaunga mkono utoaji wa chakula, maji, huduma za afya na makazi kwa raia walioathiriwa na mzozo wa miaka miwili. Hatua hii inafuatia mgao wa dola milioni 9 wiki iliyopita kwa ajili ya kuhakikisha upatikanaji wa mafuta kwa hospitali na huduma muhimu, na kufanya jumla ya msaada wa hivi karibuni kufikia dola milioni 20.Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa Duniani WHO limeonya kuhusu ongezeko la magonjwa ya neva duniani, ambayo sasa yanachangia zaidi ya vifo milioni 11 kila mwaka. Ripoti mpya ya WHO iliyotolewa leo mjini Geneva inaonesha kuwa zaidi ya watu bilioni 3 sawa na zaidi ya asilimia 40 ya watu duniani wanaishi na magonjwa yanayoathiri ubongo, ikiwemo kiharusi, ugonjwa wa kusahau, kifafa, na maumivu ya kichwa ya muda mrefu. Kwa mujibu wa ripoti nchi maskini ndizo zinazoathirika zaidi, zikiwa na upungufu mara 80 wa idadi ya wataalamu wa magonjwa ya neva ikilinganishwa na nchi tajiri. WHO inazitaka serikali kutoa kipaumbele kwa afya ya ubongo, kuongeza fedha na kuboresha upatikanaji wa huduma za tiba."Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili na hii leo Dkt. Mwanahija Ali Juma, Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili, Zanzibar nchini Tanzania, BAKIZA anafafanua maana ya neno "MKWECHE!Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
Jaridani leo jaridani tunakuletea mada kwa kina kuhusu masuala ya wanawake, tathmini ya miaka 30 ya harakati za kusongesha haki za wanawake na utamsikia maoni ya Balozi Gertrude Mongella kutoka Tanzania. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na uchambuzi wa methali.Mjadala Mkuu wa mkutano wa 80 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa ukianza Jumatatu ijayo, Rais wa Mkutano huo Annalena Baerbock amewaambia waandishi wa habari jijini New York, Marekani kuwa “jukumu letu ni Umoja wa Mataifa uwe thabiti kwa miaka 80 ijayo. Michakato ya kuhakikisha hilo ndio itakuwa jukumu letu mwaka huu, ikiwemo kusongesha ajenda ya marekebisho ya Umoja wa Mataifa. Kwa hiyo tukitaka Umoja wa Mataifa thabiti, basi tunahitaji ahadi kutoka serikali zote duniani.Ripoti ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa inayotolewa kila mwaka kabla ya kuanza kwa Mjadala Mkuu wa Baraza Kuu inasema Umoja wa Mataifa umeendelea kusimama imara, ukifanya kazi ya kuendeleza amani, kuchochea maendeleo endelevu, na kupunguza mateso ya kibinadamu licha ya majaribu makubwa. Katika ripoti hiyo Antonio Guterres amesisitiza uimara wa watumishi wa Umoja wa Mataifa, ambao wamejitolea kuleta matumaini na msaada kwa wale wanaohitaji licha ya kufanya kazi katika mazingira magumu.ripoti ya Hali ya Rasilimali za Maji Duniani iliyotolewa leo inasema ni takriban theluthi moja tu ya mabonde ya mito duniani yaliyokuwa na hali ya “kawaida” mwaka 2024 ilhali mengine yote yalikuwa na kiwango cha juu zaidi cha maji au chini ya kiwango cha kawaida — ikiwa ni mwaka wa sita mfululizo wa kutokuwepo kwa uwiano wa wazi. Ikitolewa na shirika la Umoja wa Mataifa la Hali ya Hewa, WMO, ripoti inasema mwaka 2024 uliokuwa mwaka wa joto zaidi kuwahi kurekodiwa ulianza na tukio la El Niño ambalo liliathiri vibaya mabonde makubwa ya mito na kusababisha ukame katika maeneo kadhaa ikiwemo kusini mwa Afrika.Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili, leo mchambuzi wetu ni Dkt. Josephat Gitonga, ambaye ni Mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi nchini Kenya, kwenye kitivo cha Tafsiri na Ukalimani anafafanua maana ya methali "MZOEA PUNDA HAPENDI FARASI"Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!
Jaridani leo jaridani tunakuletea mad akwa kina inayoangazia mjadala Mkuu wa mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na ufafanuzi wa neno la wiki.Tume ya Uchunguzi ya Umoja wa Mataifa imesema Israel imetekeleza mauaji ya kimbari Gaza. Ripoti ya tume hiyo hiyo iliyotolewa leo mjini Geneva pia inamtaja Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu na maafisa wengine wakuu wa Israel kwa kuchochea vitendo hivyo. Israel imepinga vikali, na kuuita ripoti hiyo kuwa ni “kashfa.” Taarifa hii imetolewa huku mashambulizi makali ya anga yakiendelea usiku kucha mjini Gaza bila dalili za kukoma.Hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa, shirika hilo limekamilisha makadirio mapya ya bajeti ya mwaka 2026, yakionesha kupunguzwa kwa zaidi ya dola milioni 500. Hatua hiyo ni sehemu ya mpango wa mageuzi ya UN80, unaolenga kuongeza ufanisi wakati Umoja wa Mataifa ukiadhimisha miaka 80. Bajeti mpya inapendekeza kupunguzwa kwa rasilimali kwa zaidi ya asilimia 15 na nafasi za kazi kwa karibu asilimia 19 ikilinganishwa na mwaka 2025.Huko Nairobi, Kenya leo imezindua maabara ya kisasa ya polio iliyoidhinishwa na Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa Duniani WHO katika Taasisi ya Utafiti wa Tiba ya Kenya, KEMRI. Kituo hicho, kilichofadhiliwa na WHO na wakfu wa Gates, kimeelezwa kuwa nyenzo muhimu katika kugundua mapema na kukabiliana na virusi vya polio pamoja na magonjwa mengine yenye uwezekano wa kusambaa, si tu nchini Kenya bali pia katika kanda nzima ya Afrika.Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili hii leo, mtaalam wetu Onni Sigalla, Mhariri mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania, BAKITA, anafafanua maana za neno "MJOLI"Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
Ripoti mpya ya shirika la kimataifa ya Oxfam inasema kuwa nchi tajiri zimetoa tu asilimia 4 pekee ya fedha zinazohitajika Afrika Mashariki kushughulikia mabadiliko ya hali ya hewa. Nchi za Afrika Mashariki ni miongoni mwa nchi zilizoathirika zaidi na mzozo wa hali ya hewa, licha ya kuchangia asilimia 0.09 ya uzalishaji wa hewa ukaa duniani.
Katika Jarida la Habari la Umoja wa Mataifa hii leo Flora Nducha anakulatea-Ripoti mpya kwa jina Maendeleo katika Maji ya Kunywa na Kujisafi Majumbani iliyozinduliwa leo na mashirika ya Umoja wa Mataifa imeonesha kwamba, licha ya hatua kupigwa, mtu 1 kati ya 4 duniani bado hana upatikanaji wa maji salama ya kunywa. -Ofisi ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa, OHCHR imetoa wito kwa mamlaka za Misri kukomesha mfumo wa “mzunguko” unaofanya wakosoaji wa Serikali kuzuiliwa kiholela na kwa muda mrefu, hata baada ya kumaliza vifungo vyao. - Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi,UNHCR leo limepongeza Serikali ya Kifalme ya Thailand kwa kupitisha azimio litakalowapa wakimbizi wa muda mrefu kutoka Myanmar haki ya kufanya kazi nchini Thailand.-Katika mada kwa kina tunamulika uzinduzi wa shule ya kwanza ya Akili Mnemba iliyoanzishwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la masuala ya wanawake UN Women huko ukanda wa Asia na Pasifiki-Na mashinani utamsikia Ibrahim Al-Najjar mkimbizi huko Ukanda wa Gaza, eneo la Palestina linalokaliwa kimabavu na Israeli akielezea hali tete ya ajira hivi sasa tangu vita ianze Oktoba 7, 2023.
Tarehe 18 Agosti mwaka 2025 siku ya Jumatano, wajumbe 15 wa Baraza la Usalama walikutana kujadili Ripoti ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu kikundi cha kigaidi cha ISIL/Da'esh.Walikabidhiwa ripoti hiyo ya 21 ikimulika vitisho vinavyotokana na kikundi hicho ambacho kirefu chake ni Islamic State in Iraq and the Levant au pia Da'esh. Ripoti ikigusia tishio la kikundi hicho katika maeneo mbalimbali duniani, lakini makala hii initajikita zaidi barani Afrika!
Jaridani leo tunaangazia mkutano wa tisa wa maendeleo ya Afrika TICAD IX nchini Japan, na hali ya kibinadamu Gaza na majeraha kwa wenyeji. Makala tunaangazia ukatili wa kingono na mashinani tunakwenda Sudan kumulika jinsi wanavyokabiliwa na unyanyasaji huo wa kingono.Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amesema Afrika inahitaji mageuzi makubwa ya Baraza la Usalama na mfumo wa kimataifa wa fedha ili kufanikisha maendeleo yake na nafasi yake duniani. Akihutubia mkutano wa tisa wa maendeleo ya Afrika TICAD IX nchini Japan, Guterres ameweka vipaumbele vitano.Maelfu ya Wapalestina katika Ukanda wa Gaza ambao wamepoteza viungo vyao vya mwili na wanakabiliwa na hali mbaya ya maisha na matatizo makubwa ya kiafya kutokana na ukosefu wa huduma bora za matibabu na viungo bandia wanazohitaji sana.Tunakuletea makala yenye kugusa maisha ya maelfu ya watu kote duniani, ukatili wa kingono katika maeneo yenye mizozo. Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa tarehe 19 Agosti limekutana jijini New York Marekani kujadili hali hii inayozidi kuongezeka, na kushuhudia jinsi waathirika wanavyobaki bila msaada wa kutosha kutokana na ukosefu wa rasilimali. Ripoti ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa iliyowasilishwa na Mwakilishi wake imeonesha ongezeko kubwa la kesi za ukatili wa kingono, jambo linaloibua maswali makubwa kuhusu uwajibikaji na huduma kwa manusura.Na katika mashinani Mwanzilishi na mratibu wa Kundi la Utetezi la Darfur, Ikhlass Ahmed amelielezea Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa jijini New York kwa njia ya video jinsi wanavyokabiliwa na kuenea kwa kasi kwa unyanyasaji wa kingono.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
Msikilizaji wa Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa leo tunakuletea makala yenye kugusa maisha ya maelfu ya watu kote duniani, ukatili wa kingono katika maeneo yenye mizozo. Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa tarehe 19 Agosti limekutana jijini New York Marekani kujadili hali hii inayozidi kuongezeka, na kushuhudia jinsi waathirika wanavyobaki bila msaada wa kutosha kutokana na ukosefu wa rasilimali.Ripoti ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa iliyowasilishwa na Mwakilishi wake imeonesha ongezeko kubwa la kesi za ukatili wa kingono, jambo linaloibua maswali makubwa kuhusu uwajibikaji na huduma kwa manusura. Leah Mushi ametuandalia makala ifuatayo ikieleza hayo kwa kina.
Ripoti ya malengo ya maendeleo endelevu mwaka 2025, ikiwa ni miaka kumi tangu mataifa kuanza kufanyia kazi malengo hayo. Katika ripoti hiyo, UN inasema dunia bado iko nyuma katika kuhakikisha malengo hayo 17 yanaafikiwa kikamilifu kufikia mwaka wa 2030.
Harakati za kila uchao kwa raia wa Gaza huko eneo la Palestina linalokaliwa kimabavu na Israeli za kukimbilia chakula huku mashambulizi yakiendelea zimeendelea kusababisha vifo na majeruhi ambapo majeruhi wa hivi karibuni aliyetajwa ni Sahar, mtoto mwenye umri wa miaka 14 aliyepata ulemavu akikimbilia kupokea msaada wa chakula. Ripoti ya Selina Jerobon inayotokana na video iliyochapishwa mtandao wa X na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi wa kipaletina, UNRWA, inafafanua zaidi.
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayomulika utapiamlo kwa watoto na madhila yasiyo fikirika kwa wananchi wa kawaida huko Mashariki ya Kati, Ukanda wa Gaza eneo la Palestina linalokaliwa kimabavu na Israeli. Pata pia muhtasari wa habari na jifunze Kiswahili.Ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa imeweka bayana jinsi mitandao ya kihalifu duniani inavyoingiza kwenye masoko dawa za binadamu zenye viwango vya juu vya kemikali za sumu ambazo zimesababisha vifo na kuathiri afya ya wagonjwa wengi hasa watoto kwenye nchi za kipato cha chini.Tunasalia na afya ambapo hii leo WHO imethibitisha kwamba Timor-Leste imetokomeza ugonjwa wa malaria, hatua ya kipekee kwa nchi ambayo ilipatia kipaumbele malaria na kuanzisha juhudi za kitaifa na zilizoratibiwa mara tu baada ya kupata uhuru wake mwaka 2002. Mkuu wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Binadamu Volker Türk, amesema maoni ya ushauri yaliyotolewa na Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) kuhusu wajibu wa Mataifa kuhusiana na mabadiliko ya tabianchi ni ushindi mkubwa kwa wote wanaopigania kulinda hali salama ya tabianchi na sayari kwa ajili ya binadamu wote. Halikadhalika ni uthibitisho usio na shaka kuhusu madhara mapana ya mabadiliko ya tabianchi na wajibu mkubwa wa Mataifa, chini ya sheria za haki za binadamu na zaidi ya hapo, kuchukua hatua za haraka ili kuzuia uharibifu.Na katika kujifunza Kiswahili, leo mchambuzi wetu ni Dkt. Josephat Gitonga, kutoka Kenya ambaye ni mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi kwenye kitivo cha tafsiri na ukalimani anatufafanulia maana ya methali "UKIONA KIVULI CHA MTU MFUPI KIMEANZA KUREFUKA JUA KUMEKUCHA AU NI MACHWEO."Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
Ripoti ya siri ya watalaam wa Umoja wa Mataifa imeishtumu Rwanda kwa kutoa maagizo na kudhibiti shughuli za waasi wa M23.
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayokupeleka nchini Uganda katika Mbuga ya Wanyama inayofahamika kwa jina Murchison Falls National Park kuangazia namna washiriki wa Kongamano la kimataifa la lugha ya Kiswahili lililofanyika mapema mwaka huu jijini Kampala walivyofurahia mazigira asili nchini Uganda na namna yanavyounufaisha ulimwengu.Mkutano wa 4 wa ufadhili kwa maendeleo umemalizika leo huko Sevilla, Hispania ambapo mashirika ya kiraia yametaka utekelezaji kwa vitendo kwa yale yaliyomo katika nyaraka iliyopitishwa iliyopatiwa jina Makubaliano ya Sevilla.Mmoja wa wawakilishi wa mashirika ya kiraia, Paula Sevilla amesema kinachohitajika ni uongozi kutoka nchi tajiri ambako ndiko zilizko kampuni kubwa zinazokwepa kodi.Ripoti mpya iliyotolewa leo na shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo, FAO kuhusu vijana na mifumo ya uzalishaij chakula na kilimo inaonesha kuwa karibu asilimia 85 ya vijana duniani wanaishi katika nchi za kipato cha chini na cha kati, ambako mifumo hiyo ni muhimu kwa ajira na maisha yao. Ripoti inasema kuwajumuisha vyema vijana katika mifumo hiyo kunaweza kuleta mchango wa hadi trilioni moja ya dola kwa uchumi wa dunia..Na mwezi uliopita wa Juni umeshuhudia ongezeko kubwa la familia za raia wa Afghanistan zikirejeshwa nyumbani kutoka Iran, tofauti na awali ambapo waliokuwa wakirejeshwa walikuwa ni wanaume peke yao.Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili leo mchabuzi wetu Onni Sigalla, Mhariri Mwandamizi kutoka Baraza la Kiswahili la Taifa, BAKITA nchini Tanzania, anachambua neno KUTOHOA.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
Hii leo Jarida linamulika ripoti ya nishati jadidifu duniani, Afrika ikiwa bado inasuasua; Harakati za mabaharia wanawake Somalia, Mpango wa Umoja wa Mataifa wa UN80 na baba na malezi ya mtoto nchini Tanzania.Ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa inayofuatilia maendeleo kuelekea kutimiza Lengo la Umoja wa Mataifa la Maendeleo Endelevu namba 7 (SDG 7) linaloangazia nafasi muhimu ya nishati mbadala imetoa wito wa ufadhili zaidi kwani ingawa asilimia 92 ya watu duniani sasa wanapata umeme, lakini watu milioni 666 wengi wao wakiwa Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara bado hawapati umeme. Anold Kayanda na maelezo zaidi.Nchini Somalia, suala la usawa wa kijinsia katika sekta ya baharini limepatiwa kipaumbele kwenye mjadala kuhusu wanawake katika tasnia hiyo, mjadala uliofanyika kwenye mji mkuu Mogadishu ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya kimataifa ya mabaharia inayoadhimishwa tarehe 25 mwezi Juni kila mwaka ikibeba maudhui Meli yangu isiyo na unyanyasaji. Sharon Jebichii anatupasha zaidi.Je wafahamu kuhusu UN80? Flora Nducha anadadavua kwenye makala.Mashinani: Aloyce Siame, baba wa mtoto mwenye umri wa miaka 12 kutoka Tanzania ambaye kupitia Mpango wa Vijana uitwayo “Furaha”, unaoungwa mkono na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF na wadau wake sasa ni mmoja wa wanaume wanaojitokeza kwa malezi ya watoto na familia zao.
Ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa inayofuatilia maendeleo kuelekea kutimiza Lengo la Umoja wa Mataifa la Maendeleo Endelevu namba 7 (SDG 7) linaloangazia nafasi muhimu ya nishati mbadala imetoa wito wa ufadhili zaidi kwani ingawa asilimia 92 ya watu duniani sasa wanapata umeme, lakini watu milioni 666 wengi wao wakiwa Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara bado hawapati umeme. Anold Kayanda na maelezo zaidi.
Hii leo jaridani tunaangazia baa la njaa katika nchi 13 duniania amabzo hakuna uhakika wa chakula, na hali ya kibinadamu kwa wakimbizi wa DRC. Makala tunasalia hapa makao makuu na mashinani tunakwenda nchini Nepal, kulikoni?Ripoti mpya ya pamoja ya Umoja wa Mataifa iliyotolewa leo jijini Roma, Italia inatahadharisha kuwa watu katika nchi 5 kati ya nchi 13 zenye njaa duniani wako kwenye hatari kubwa ya kukumbwa na njaa kali, vifo na maafa ikiwa msaada wa kibinadamu hautatolewa haraka na juhudi za kimataifa hazitaelekezwa kukomesha migogoro, kupunguza ufurushwaji na kuongeza msaada wa haraka kwa kiwango kikubwa.Huko jimboni Kivu Kaskazini, Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, juhudi za kidiplomasia zinaendelea kumaliza mapigano, huko nalo shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo, UNDP likitoa wito wa msaada kwa watu waliofurushwa makwao kutokana na mashambulizi ya waasi wa M23, msaada ambao utawasaidia kujenga upya maisha yao na njia zao za kujipatia riziki. Katika makala leo Flora Nducha wa Idhaa hii amemuuliza Amon Anastaz Mpanju, Naibu Katibu Mkuu wizara ya Maendeleo ya jamii, jinsia, wanawake na makundi maalum nchini Tanzania aliyeshiriki mkutano wa 18 wa mkataba wa watu wenye ulemavu COSP18 uliokunja jamvi mwishoni mwa wiki nini kikubwa alichotoka nacho kwenye mkutano huo.Na katika mashinani leo ikiwa ni siku ya Kimataifa ya utumaji fedha kwa familia kutoka ughaibuni, fursa ni yake Bibha kutoka Chinnamastrial nchini Nepal, mnufaika wa utumaji fedha kutoka wanafamilia walioko ughaibuni akielezea jinsi ambavyo fedha hizo zinavyosaidia jamii zake kuondokana na umaskini.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
Ripoti mpya ya pamoja ya Umoja wa Mataifa inaonya kuwa watu katika nchi 5 kati ya nchi 13 zenye njaa kali duniani wako kwenye hatari kubwa ya kukumbwa na njaa kali, vifo na maafa ikiwa msaada wa kibinadamu hautatolewa haraka na juhudi za kimataifa hazitaelekezwa kukomesha migogoro, kupunguza ufurushwaji na kuongeza msaada wa haraka kwa kiwango kikubwa. Anold Kayanda na taarifa zaidi.
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina na leo ikiwa ni siku ya kimataifa ya kupinga utumikishaji wa watoto ambapo shirika la Umoja wa Mataifa la Kazi duniani, ILO, linasema maudhui ni Maendeleo yako dhahiri, lakini bado kuna mengi ya kufanya: Hebu tuongeze kasi. Tunakupeleka nchini Tanzania kumulika harakati za kuwaepusha watoto kutumikishwa.Watu waliolazimika kukimbia makazi yao kutokana na vita, ukatili na mateso duniani kote imefikia kiwango cha juu kisichovumilika, hasa wakati huu ambapo ufadhili wa misaada ya kibinadamu unapungua kwa kasi. Kwa mujibu wa Ripoti ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia wakimbizi UNHCR iliyotolewa leo kuhusu mwelekeo wa Ulimwengu, kufikia mwisho wa Aprili mwaka huu, kulikuwa na watu milioni 122.1 waliolazimika kuhama kwa nguvu, ikilinganishwa na watu milioni 120 mwaka uliopita katika kipindi kama hicho.Ikiwa leo ni Siku ya Kimataifa ya kupinga ajira kwa watoto, utafiti uliofanywa na mashirika ya Umoja wa Mataifa lile la kazi duniani, ILO na la kuhudumia Watoto UNICEF unaonesha licha ya hatua zilizopigwa, ajira kwa watoto bado inaathiri watoto milioni 138 duniani kote, kati yao milioni 54 wakifanya kazi hatarishi ambazo zinaweza kuhatarisha afya yao, usalama wao au maendeleo yao kwa ujumla.Nchini Sudan Kusini watu wako katika hatari ya njaa katika miezi ijayo, kutokana na kuongezeka kwa mapigano katika jimbo la Upper Nile. Utafiti mpya kutoka katika Mfumo wa Uainishaji wa Viwango vya Uhakika wa Chakula (IPC) unaonesha kudorora kwa hali ya chakula na lishe katika maeneo ya Sudan Kusini yaliyoathiriwa na mapigano katika miezi ya karibuni.Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili hii leo mchambuzi wetu mlumbi wa Kiswahili Joramu Nkumbi kutoka nchini Tanzania, anafafanua maana ya maneno "MBEUZI, MNYWANYWA NA MACHAGU.”Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!
Ripoti ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani (WHO) ya takwimu za afya duniani iliyochapishwa jana Mei 15 ikionesha athari kubwa zaidi za kiafya zilizosababishwa na janga la COVID-19 kuhusu vifo, muda wa kuishi na hali ya afya na ustawi kwa ujumla, imeweka wazi kuwa katika kipindi cha miaka miwili pekee, kati ya mwaka 2019 na 2021, matarajio ya kuishi yalipungua kwa mwaka mmoja na miezi nane ikiwa ni maporomoko makubwa zaidi katika historia ya hivi karibuni hali iliyobatilisha mafanikio ya afya yaliyopatikana kwa muongo mmoja.
Hii leo jaridani tunaangazia uhakika wa chakula, na takwimu za afya za janga la COVID-19 kusababisha vifo, muda wa kuishi na hali ya afya na ustawi kwa ujumla. Makala tunakwenda nchini Tanzania na mashinani nchini DRC, kulikoni?Ukosefu wa uhakika wa kupata chakula na utapiamlo kwa watoto uliongezeka kwa mwaka wa sita mfululizo mwaka 2024, na kuwatumbukiza mamilioni ya watu karibu na baa la njaa, huku wengine wakiepuka kutokana na misaada ya kimkakati. Imesema Ripoti ya Kimataifa kuhusu Janga la Chakula (GRFC) iliyotolewa leo huko Roma, Italia na shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo, FAO.Ripoti ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani (WHO) ya takwimu za afya duniani iliyochapishwa jana Mei 15 ikionesha athari kubwa zaidi za kiafya zilizosababishwa na janga la COVID-19 kuhusu vifo, muda wa kuishi na hali ya afya na ustawi kwa ujumla, imeweka wazi kuwa katika kipindi cha miaka miwili pekee, kati ya mwaka 2019 na 2021, matarajio ya kuishi yalipungua kwa mwaka mmoja na miezi nane ikiwa ni maporomoko makubwa zaidi katika historia ya hivi karibuni hali iliyobatilisha mafanikio ya afya yaliyopatikana kwa muongo mmoja.Katika makala Leah Mushi anatupeleka nchini Tanzania kusikia namna wanawake wenye ulemavu walivyoweza kujikwamua kutoka kwenye changamoto mbalimbali ikiwemo za kiuchumi na kuchangamkia fursa za uongozi.Na katika fursa ni yake Bernadette Kambonesa, mkimbizi wa ndani kutoka kijiji cha Bogoro, jimboni Ituri nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC akizungumzia manufaa yatokanayo na uwepo wa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa Kulinda Amani nchini humo (MONUSCO).Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
Ripoti mpya kuhusu “Hali ya Hewa Afrika 2024” iliyotolewa leo na Shirika la Umoja wa Mataifa la Utabiri wa Hali ya Hewa Duniani WMO imeonya kwamba muongo wa joto zaidi kuwahi kushuhudiwa Afrika umeleta madhara makubwa kwa bara hilo. Evarist Mapesa na taarifa zaidi
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa ambayo Flora Nducha wa Idhaa hii ya Kiswahili alipata fursa ya kuzungumza na kiongozi wa kijamii kutoka Jamii ya wafugaji ya Wamaasai mkoani Morogoro nchini Mashariki mwa Tanzania Adam Kulet Ole Mwarabu.Wiki kumi baada ya kuanza kwa mzingiro kamili wa Israel dhidi ya wakazi wa Gaza, zaidi ya robo tatu ya kaya katika eneo la Palestina kuna uhaba mkubwa wa huduma ya maji, huku hali ya usafi ikizidi kuwa mbaya, yameonya leo mashirika ya misaada ya Umoja wa Mataifa huku wasiwasi ukiongezeka kuhusu athari za "uhaba huo wa maji kwa kuzingatia kuwa msimu wa joto unakaribia.”Ripoti kutoka Sudan zikidai kwamba juzi jumatano kulikuwa na jaribio la mashambulizi mapya ya ndege zisizo na rubani dhidi ya kitovu muhimu cha misaada nchini humo juzi, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres kupitia tamko alilolitoa jana jioni kwa saa za New York, Marekani, ameongeza nguvu yake katika kutoa wito unaozidi kuwa wa muhimu kuhamasisha kuanzishwa kwa mazungumzo ya amani ya kweli.Kufuatia kuendelea kwa mvutano wa majirani, India na Pakistani, Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, Philemon Yang, ametoa wito wa kuzitaka nchi hizo mbili kuchukua tahadhari na kuepuka hatua zinazoweza kuongeza mzozo. Balozi Yang anasisitiza mazungumzo ya amani na kufuata sheria za kimataifa ndiyo njia pekee ya kusuluhisha migogoro.”Na katika jifunze Kiswahili leo Dkt. Mwanahija Ali Juma, Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili Zanzibar nchini Tanzania, BAKIZA anafafanua maana ya neno "DALALI”Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayoturejesha hapa makao makuu ambako Idhaa hii Dokta Willis Ochieng kutoka Kenya aliyehudhuria ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika lisilo la kiserikali linalojihusisha na masuala ya kilimo na maendeleo. Pia tunakuletea muhtasari wa habari, na mashinani tunakwenda Ghana.Ukuaji wa maendeleo ya binadamu – yanayopimwa kwa uhuru na ustawi wa watu – umeendelea kuwa wa kasi ndogo tangu mshtuko mkubwa wa janga la COVID-19 lakini kuna matumaini makubwa kwamba Akili Mnemba au AI, ikiwa itatumika kwa njia sahihi, inaweza kuwa chombo chenye nguvu cha kuboresha maisha ya mamilioni ya watu. Hii ni kwa mujibu wa Ripoti ya kila mwaka ya Maendeleo ya Binadamu iliyotolewa leo na Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo duniani, UNDP.Kulengwa kwa hospitali ya Médecins Sans Frontières nchini Sudan Kusini kunaweza kuwa uhalifu wa kivita imeeleza leo Kamisheni ya Umoja wa Mataifa kuhusu Haki za Binadamu Sudan Kusini kufuatia mashambulizi ya angani yaliyotekelezwa dhidi ya hospitali ya Médecins Sans Frontières (MSF) huko Old Fangak, Jimbo la Jonglei mapema majuzi asubuhi ya Jumamosi na kusababisha vifo vya takribani raia saba na kujeruhi wengine. Shambulio hilo lilifanyika baada ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Sudan Kusini (SSPDF) kutoa onyo la kufanya shambulizi iwapo dai lao la kuachiliwa meli zao zilizotekwa halitatekelezwa.Ripoti mpya ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani, WHO, iliyotolewa leo imeonesha jinsi mahali mtu anakozaliwa kulivyo na mchango katika maisha yake. Ripoti inasema, “mahali mtu anakozaliwa huweza kuamua kama ataishi zaidi ya miongo mitatu kuliko mtu mwingine aliyezaliwa katika nchi yenye hali duni za makazi, elimu na fursa za ajira.”Na mashinani leo nampa fursa Dorcas Awortwe, Naibu Mkurugenzi wa Tume ya Maendeleo ya Kanda ya Kati kutoka Ghana, aliyeshiriki kwenye mkutano wa jukwaa la watu wa asili hapa Makao Makuu wiki iliyopita anazungumzia changamoto zinazowakabili watu wa asili katika jamii yake na ombi lake kwa Umoja wa Mataifa.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
Maambukizi ya ugonjwa wa mpox kutokana na aina ya virusi vya monkeypox clade Ib /ˈmʌŋ.ki.pɑks kleɪd one bee/ (MPXV) yanaendelea kuripotiwa hasa barani Afrika, ambapo mataifa kumi na moja yameripoti maambukizi ya ndani ya jamii katika kipindi cha wiki sita zilizopita. Hiyo kwa mujibu wa ripoti 51 ya Shrika la Umoja wa Mataifa la Afya Ulimwenguni, WHO kuhusu hali ya mlipuko wa mpox katika nchi mbalimbali duniani. Anold Kayanda amefuatilia ripoti hiyo na anatufafanulia kwa ufupi.
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina ambayo tunasalia hapa makao makuu katika mkutano wa CSW69 uliokunja chamvi Ijumaa wiki jana, tunamsikia aliyekuwa Katibu Mkuu wa Mkutano wa 4 wa Umoja wa Mataifa wa Wanawake, Mkutano wa Beijing Bi. Gertrude Mongella.Hapa New York, Umoja wa Mataifa leo umetoa wito wa kuachiliwa kwa wafanyakazi wake wanaoshikiliwa kote ulimwenguni ambao wamejikuta matatani wakati wakiwahudumia watu walio katika hatari, huku wakihatarisha usalama wao binafsi kwa kukabiliwa na vitisho vya kutekwa nyara, vurugu, unyanyasaji, na kifungo katika maeneo yenye migogoro na majanga.Ripoti mpya iliyotolewa leo na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF kuhusu vifo vya watoto imeonya kwamba miongo ya maendeleo katika kupunguza vifo vya watoto na watoto wachanga wakati wa kuzaliwa yako hatarini kutokana na kupunguzwa kwa ufadhili. Idadi ya vifo vya watoto wa chini ya umri wa miaka mitano ilipungua hadi watoto milioni 4.8 mwaka 2023, huku vifo vya wakati wa kuzaliwa vikiendelea kubaki takriban milioni 1.9.Leo ni Siku ya Kimataifa ya Kumbukumbu ya Waathirika wa Utumwa na Biashara ya Watumwa ya Bahari ya Atlantiki, ikiwakumbuka mamilioni ya Waafrika walioteswa, kunyanyaswa, na kunyimwa utu wao. Katika ujumbe wake wa siku hii Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema “Kwa zaidi ya karne nne, mamilioni ya Waafrika walitekwa kwa nguvu, kusafirishwa kwa meli hadi mataifa ya kigeni, na kufanyishwa kazi katika hali mbaya za kikatili.”Na katika mashinani kupitia video ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani WFP, Lea mkimbizi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC ambaye sasa amekimbilia Burundi na familia anasilimua hali ilivyokuwa wakati wa kukimbia.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
Hii leo jaridani katika mada kwa kina tunajikita katika mkutano CSW69 ambao umebakiza siku moja tu, kesho Machi 21 unakunja jamvi, na tunamsikia Dkt. Dorothy Gwajima, Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia Tanzania, Waziri Riziki Pembe kutoka Zanzibar na Profesa Smile Dzisi, Mkugenzi wa Shirika la “I believe Global” kutoka Ghana.Kamishna Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi, UNHCR Filippo Grandi amesema kukata ufadhili kwa mashirika yanayotoa huduma za kibinadamu kunasababisha janga la uwajibikaji. Kupitia taarifa iliyotolewa leo Geneva, Uswisi na UNHCR, Bwana Grandi amesema kukata ufadhili kunaweka hatarini maisha ya mamilioni ya watu na madhara yake kwa watu wanaokimbia majanga, yatakuwa makubwa zaidi na yataonekana wazi ikiwemo wanawake na watoto wa kike kukosa huduma zitokanazo na kubakwa.Leo ni siku ya furaha duniani maudhui yakimulika umuhimu wa watu kusaidiana na kujaliana katika masuala mbalimbali ikiwemo chakula. Ripoti mpya ya wadau wa UN iliyozinduliwa leo imeonesha kuwa nchi yenye furaha zaidi duniani ni Finland na ya mwisho kabisa ni Afghanistani. Katika 10 bora zenye furaha hakuna hata moja ya Afrika, ilihali kwenye 10 za mwisho nchi za Afrika ni 7 ambazo ni Lesotho, Comoro, Botswana, Zimbabwe, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, Malawi na Sierra Leone.Mkutano wa 69 wa Kamisheni ya Hali ya Wanawake duniani, CSW69 ukikaribia ukingoni hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa tumemuuliza mshiriki Wakili Rosemary Mwaipopo kutoka Tanzania mkutano umekidhi kiu yake ya kusongesha usawa wa kijinsia?Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili hii leo mchambuzi wetu mlumbi wa Kiswahili Joramu Nkumbi kutoka nchini Tanzania, anafafanua maana ya maneno “Ashiraf, Janabi, gayagaya, kiti cha marimba na kiti cha msaji”Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
Ripoti mpya ya Chuo cha Monash imeonesha matukio ya unyanyasaji dhidi yawa Islamu wa Australia, yali ongezeka zaidi ya mara mbili kati ya Januari 2023 na Novemba 2024.
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina ambapo Umoja wa Mataifa kupitia miradi mbalimbali ikiwemo mradi wa Pamoja wa Kigoma, KJP nchini Tanzania, unaolenga kuhakikisha wanawake na wasichana wanajumuishwa kwenye mipango ya kuhimili na kukabili mabadiliko ya tabianchi, kwa kuwajengea uwezo.Kuelekea Siku ya Kimataifa ya Wanawake Machi 8, tathmini mpya ya Umoja wa Mataifa iliyowekwa wazi leo ikiangazia haki za wanawake miaka 30 baada ya Azimio la Beijing inaonesha uwepo wa maendeleo katika usawa wa kijinsia, kama vile sheria dhidi ya ubaguzi na sera jumuishi za kijinsia. Hata hivyo, ripoti hiyo inaeleza uwepo bado wa ubaguzi wa kijinsia uliojikita katika jamii, ukiendelea kuwazuia wanawake na wasichana kupata fursa.Ripoti nyingine ya Umoja wa Mataifa iliyochapishwa leo ikiangazia Sudan imefichua vitendo vya watu kukamatwa kiholela, mateso, na unyanyasaji huko Khartoum vinavyotekelezwa na Vikosi vya wanamgambo wa Rapid Support Forces (RSF) na pia Jeshi la Serikali ya Sudan (SAF). Ripoti hiyo imearifu pia kuwa makumi ya maelfu ya watu wamewekwa katika mazingira duni tangu Aprili 2023.Kutokana na kupungua kwa ufadhili wa misaada ya kibinadamu duniani, Umoja wa Mataifa leo jijini Geneva, Uswisi kutenga dola milioni 110 ili kusaidia majanga yaliyopuuzwa katika nchi 10 barani Afrika, Asia, na Amerika Kusini, zikiwemo Niger, Somalia, Jamhuri ya Afrika ya Kati na Zambia.Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili, mchambuzi wetu Dkt. Josephat Gitonga, kutoka Kenya ambaye ni mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi kwenye kitivo cha tafsiri na ukalimani anatufafanulia maana ya methali “MCHAWI AKIFICHUA MIRIMO YA WACHAWI HU UAWA”.Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!
Karibu jaridani hii leo na mwenyeji wako ni Flora Nducha akikuletea habari kuhusu haki za binadamu, elimu ya STEM kwa wasichana wakimbizi nchini Kenya; Harakati za kuhamishia wakimbizi wa DRC nchini Burundi kuelekea maeneo salama; mafunzo ya ujasiriamali wa ushoni kwa wanawake na wasichana.Kwenye mkutano wa 58 wa Baraza la Umoja wa Mataifa la Haki za Binadamu unaoendelea mjini Geneva Uswisi, Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Haki za Binadamu Volker Türk , amezungumzia hali ya kuzorota na kutoeleweka inayohusu haki za binadamu duniani, akionya kwamba ushawishi wa viongozi wa kiimla, matajiri wakubwa, na viongozi wa kimabavu unatishia kuvuruga maendeleo ya miongo kadhaa. Ripoti yake Anold Kayanda.Nchini Kenya, shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) na wadau wengine wanafanikisha mpango wa kuhamasisha wasichana kuingia katika masomo ya STEM yaani Sayansi, Teknolojia, Uhandisi na Hisabati.Ripoti yake Sharon Jebiichi.Makala Assumpta Massoi anakupeleka mpakani mwa Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC kusikia harakati za kuhamishia wakimbizi eneo salama zaidi.Mashinani anasalia nchini Jamhuri ya kidemkrasia ya Congo DRC kusikia jinsi ambavyo mafunzo ya ujasiriamali wa ushoni yanavyowawezesha wanawake na wasichana kujimudu kimaisha. Karibu
Matangazo ya nusu saa kuhusu habari za mapema asubuhi pamoja na habari za michezo.
Ripoti ya Umoja wa Mataifa iliyotolewa leo mjini Geneva Uswisi na ofisi ya haki za binadamu (OHCHR) imefichua kuwa viongozi wa juu wa serikali ya Bangladesh walihusika moja kwa moja katika ukandamizaji wa maandamano makubwa yaliyoitikisa nchi hiyo mwaka 2024 na kusababisha vifo vingi. Flora Nducha na taarifa zaidi
Hii leo jaridani tunaangazia matokeo ya maandamani nchini Bangladesh, na machafuko nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC. Makala inatupeleka nchini Kenya na mashinani nchini Tanzania, kulikoni?Ripoti ya Umoja wa Mataifa iliyotolewa leo mjini Geneva Uswisi na ofisi ya haki za binadamu (OHCHR) imefichua kuwa viongozi wa juu wa serikali ya Bangladesh walihusika moja kwa moja katika ukandamizaji wa maandamano makubwa yaliyoitikisa nchi hiyo mwaka 2024 na kusababisha vifo vingi.Baada ya waasi wa M23 jimboni Kivu Kaskazini, Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC kupatia wakimbizi waliokuwa wamesaka hifadhi kambini mjini Goma, wawe wamerejea makwao ndani ya saa 72 kuanzia juzi jumatatu, mamia wameanza kutii amri hiyo licha ya hofu inayowakabili ya kule wanakotakiwa kurejea.Makala inatupeleka jijini Nairobi, Kenya ambako ambako Kevin Keitany wa redio washirika wetu Domus FM kwa kuzingatia kuwa kesho Februari 13 ni Siku ya Kimataifa ya Redio, ametutumia maoni ya vijana wawili wanaozungumzia namna redio imewasaidia kusambaza ujumbe wao kuhusu hatua dhidi ya mabadiliko ya tabianchi.Mashinani fursa ni yake Tupokigwe Simon, msichana mwenye umri wa miaka 16, ambaye ni mwanaharakati wa Sayansi, Teknolojia, Uhandisi na hisabati , STEM, wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto, UNICEF, akieleza umuhimu wa msichana katika sayansi na kuwahimiza wasichana wenzake kusoma sayansi.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
Hali ya usalama kwenye mji mkuu wa jimbo la Kivu Kaskazini, Goma, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, ikiendelea kuwa tete, ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani, nchini humo, MONUSCO pamoja na SAMIDRC ambao ni ujumbe wa kulinda amani kutoka Jumuiya ya Maendeleo ya nchi za Kusini mwa Afrika, SADC wanadhibiti uwanja wa ndege wa Goma. Ripoti ya Selina Jerobon inafafanua zaidi.
Hii leo jaridani tunaangazia ripoti mpya kuhusu hali ya usalama na afya ya watoto kote duniani, na amnai na usalama nchini Syria. Makala inatupeleka nchini Uganda na mashinani nchini DRC, kulikoni?Ripoti mpya ya kila mwaka kuhusu mustakabali wa watoto ambayo imetolewa leo na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF, imeonya kwamba dunia inaingia katika zama mpya za majanga kwa watoto.Wasyria wana matarajio makubwa kwa nchi yao, na hamu kubwa ya watu kutoka katika kila nyanja ya jamii kuja pamoja na kuunda katiba mpya, ambayo lazima ianze na mazungumzo ya kitaifa yaliyo jumuishi. Hayo ni kwa mujibu wa Najat Rochdi, Naibu Mjumbe Maalum wa Umoja wa Mataifa kwa Syria, ambaye amekuwa Damascus kukutana na wajumbe kadhaa wa mamlaka ya mpito ili kuhakikisha Wasyria wote wana uwezo wa kushiriki katika mustakbali wa nchi hiyo.Makala inatupeleka nchini Uganda ambako shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) kwa muda sasa limekuwa likifanya jukumu muhimu katika kuwezesha usajili wa watoto.Na mashinani fursa ni yake Antoinette Nzale, mkimbizi wa ndani katika kijiji cha Fataki iliyoko Ituri mashariki mwa Jamhuri ya Kidemkrasia ya Congo, DRC akishuhudia jinsi ambavyo juhudi za pamoja za Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo MONUSCO na wanajeshi wa serikali FARDC zinavyowawezesha wakimbizi wa ndani kuanza kurejea katika mazingira yao ya awali taratibu.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
Ripoti mpya ya kila mwaka kuhusu mustakabali wa watoto ambayo imetolewa leo na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF, imeonya kwamba dunia inaingia katika zama mpya za majanga kwa watoto . Taarifa ya Flora Nducha inafafanua zaidi
Hii leo jaridani tunakuletea mad akwa kina inayotupeleka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC kumulika harakati za kusaidia manusura wa ukatili wa kingono na kijinsia kwenye mizozo. Pia tunakuletea muhtasari wa había za Sudan, Uganda na Tanzania, Mashinani tunarejea Sudan.Ripoti ya Kamati ya Tathmini ya Viwango vya Njaa (IPC) iliyotolewa leo inaeleza kwamba imegundua kuwa kuna maeneo matano zaidi nchini Sudan ambayo yanakabiliwa na baa la njaa kati ya mwezi huu wa Desemba na Mei mwaka ujao wa 2025. Ripoti hiyo imeyataja maeneo hayo kuwa ni ya Darfur Kaskazini yaani Um Kadadah, Melit, El Fasher, Twawisha, na Al Lait.Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) limekaribisha mchango wa EURO milioni 1 kutoka serikali ya Ujerumani ili kusaidia shughuli za lishe na ustawi kwa zaidi ya wakimbizi na wasaka hifadhi 254,000 nchini Uganda ambayo inawahifadhi wakimbizi milioni 1.7.Na Kikosi cha 7 cha Walinda amani wa Umoja wa Mataifa kutoka Tanzania, TANBAT 7 kilichokuwa kinahudumu katika Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa Kuleta Utulivu nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR (MINUSCA) kimerejea nyumbani Tanzania kikijivunia kuwa kikosi cha kwanza cha nchi hiyo kupokea barua ya pongezi kutoka Umoja wa Mataifa.Mashinani fursa ni yake Najwa Mohamed, mama mjamzito kutoka Jabal Moya nchini Sudan ambaye amepoteza makazi yake kufuatia vurugu zinazoendelea nchini humo na kulieleza Shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu na afya ya uzazi, UNFPA kwamba hali ni ngumu hasa kwa wanawake wajawazito.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
Mwaka 2020 Ghana iliripoti kuwa na watu 350,000 wanaioshi na virusi vya Ukimwi na kati yao hao 31,000 walikuwa ni wajawazito. Jambo lililoshtua ni kwamba ni sehemu ndogo mno ya wajawazito hao ndio walipimwa kufahamu iwapo wana VVU au la. Jambo lililofanya serikali kwa kushirikiana na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF kuchukua hatua. Ripoti ya Assumpta Massoi inafafanua zaidi.
Hii leo jaridani tunaangazia uzinduzi wa ombi la ufadhili wa mahitaji ya Kibinadamu (GHO), na umuhimu wa lugha mama katika kukuza haki za binadamu. Makala tunasalia hapa makao makuu ya umoja wa mataifa na mashinani tunakupeleka nchini Senegal, kulikoni?Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu (OCHA) ikizindua Ripoti ya Kimataifa ya mahitaji ya Kibinadamu (GHO) kwa mwaka ujao wa 2025 imetangaza ombi la ufadhili kwani takriban watu milioni 305 duniani kote watahitaji msaada wa kibinadamu katika mwaka ujao.Haki si haki iwapo inatolewa kwa lugha ambayo haileweki kwa wahusika, wamejulishwa washiriki wa mkutano wa pili wa wanazuoni unaofanyika hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa New York, Marekani na pia mtandaoni ukimulika Madaraka, Haki na Binadamu: Utawala wa Sheria na mabadiliko Afrika.Makala tunasalia hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa ambapo mkutano wa mwaka 2024 wa Taaluma kuhusu Afrika leo katika leo umeingia siku ya pili hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani. Mkutano huo ulioandaliwa na Ofisi ya mshauri maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu Afrika UNOSAA ni wa siku tatu na umebeba maudhui "Nguvu, Haki, na watu” kwa ajili ya mabadiliko ya Afrika.Na mashinani fursa ni yake Antar sarr, Kijana mkulima wa mbogamboga kutoka Senegal ambaye ni mmoja wa wanufaika wa mradi wa Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Maendeleo ya kilimo, IFAD unaowawezesha vijana nchini humo kwa kilimo na biashara ndogondogo ili kuondokana na fikra za kwenda Ulaya kusaka Maisha bora na ajira, akisema mradi huo imempatia matumaini.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu (OCHA) ikizindua Ripoti ya Kimataifa ya mahitaji ya Kibinadamu (GHO) kwa mwaka ujao wa 2025 imetangaza ombi la ufadhili kwani takriban watu milioni 305 duniani kote watahitaji msaada wa kibinadamu katika mwaka ujao. Selina Jerobon na maelezo zaidi.
Leo ni siku ya watoto duniani maudhui mwaka huu yakiwa "Kila mtoto, kila haki"na katika kuhakikisha sauti zao zinasikika kuhusu mustakbali wa utakao, shirika la Umoja wa Maataifa la kuhudumia watoto duniani UNICEF limewapa fursa ya kuandika barua kwenda kwa watu wazima kote duniani ili kutoa madukuduku yao na kutanabaisha wanachokitaka kwa ajili ya mustakbali wao. Hao ni baadhi tu ya makumi ya watoto walioandika barua , hawa ni kutoka Gaza, Tanzania na Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo DRC ambao walishika kalamu na karatasi kufikisha ujumbe wao kwa watu wazima wa dunia ya sasa iliyoghubikwa na changamoto lukuki zinazoweka rehani mustakbali wao.Kwa mujibu wa ripoti mpya ya UNICEF ya “Hali ya watoto duniani mwaka 2024: Mustakabali wa Utoto katika Ulimwengu Unaobadilika,” iliyotolewa leo sanjari na maadhimisho ya siku hii kuna masuala matatu makubwa ya kimataifa yatakatoathiri maisha ya watoto ifikapo 2050 na kuendelea. Mosi ni mabadiliko katika idadi ya watu, pili janga la mabadiliko ya tabianchi na migogoro na tatu teknolojiaUNICEF inasema yote haya ni changamoto na fursa ambazo watoto wanaweza kukabiliana nazo katika zama zijazo.Rafif mtoto mkimbizi wa ndani ameandika barua kutoka Palestina ambako vita imetamalaki, anasema“Ninatoka mjini Gaza na sasa nimefurushwa hadi Kusini mwa Gaza. kama watoto Ni haki yetu kuishi kwa usalama na kujenga mustakbali bora”Kutoka mashariki ya Kati hadi Afrika Mashariki kwa Steven akimulika afya“Na nianaandika kwenu kutoka Tanzania. Kwenye jamii yangu watoto wanaugua kila wakati , kwa nini? Huu ndio mustakbali wangu je unasikiliza?”Nako Congo DRC mitihani ni mingi, Andrea anasema“Nataka kushuhudia dunia ambayo kila mtoto anapendwa, dunia ambayo amani inashamiri ni raha na faraja. Napenda kuona hasira zinageuka na kuwa mazungumzo”Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres akiunga mkono suti hizo za watoto katika ujumbe wake amesema Katika Siku ya Watoto Duniani tunasherehekea washiriki wachanga zaidi wa familia yetu ya kibinadamu. Lakini leo pia ni wakati wa kutambua changamoto kubwa zinazowakabili watoto katika ulimwengu wetu uliogawanyika sana, wenye misukosuko na mara nyingi ulioshamiri ukatili.”Ripoti ya UNICEF imetoa wito wa kuwekeza katika elimu, miji endelevu na yenye mnepo kwa watoto, miundombinu inayohimili mabadiliko ya tabianchi, teknolojia, huduma muhimu na mifumo ya msaada wa kijamii na pia teknolojia iliyo salama kwa watoto ili kupambana na mzigo wa changamoto zinazowakabili.