Podcasts about redio

  • 23PODCASTS
  • 418EPISODES
  • 28mAVG DURATION
  • ?INFREQUENT EPISODES
  • Jun 2, 2025LATEST

POPULARITY

20172018201920202021202220232024


Best podcasts about redio

Latest podcast episodes about redio

Habari za UN
Shirika la kiraia lawezesha vijana wa kike kujiajiri badala ya kutumbukia kwenye umaskini

Habari za UN

Play Episode Listen Later Jun 2, 2025 3:36


Nchini Tanzania ugumu wa maisha na kukabiliwa na vishawishi, umewapa fikra mpya vijana wa kike mkoani Morogoro, mashariki mwa taifa hilo la Afrika Mashariki, ambao sasa wanajimudu kiuchumi,  kwa kuanzisha biashara na shughuli za ujasiriamali. Wanasongesha Malengo ya Maendeleo Endelevu, SDGs hususan namba 8 la ajira zenye staha, nan amba 1 la kutokomeza umaskini. Hamad Rashid wa Redio washirika Tanzania Kids Time FM amewatembelea vijana hao na kuandaa makala hii.

Habari za UN
19 FEBRUARI 2025

Habari za UN

Play Episode Listen Later Feb 19, 2025 9:55


Hii leo jaridani tunaangazia msaada wa kibinadamu nchini DRC, na simulizi y amkimbizi wa DRC aliyekimbilia nchini Uganda. Makala inatupeleka nchini Tanzania, namashinani nchini Kenya, kulikoni?Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa likifanya kikao cha dharura jijini New York, Marekani kujadili hali ya usalama inayozidi kuzorota kila uchao huko Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, Mratibu wa Umoja wa Mataifa wa Masuala ya kibinadamu nchini humo, Bruno Lermaquis amesema kupanuka kwa mzozo huo kumezidi kugharimu maisha na mustakabali wa raia.Sina mpango tena wa kurejea nyumbani Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, ni kauli yake Twagirayesu Gato, mwanafunzi huyu raia wa DRC aliyekimbia  nchini mwake mwaka jana na kuingia Uganda ambako sasa anapata hifadhi. Amesema hayo kwenye video ya shirika la Umoja wa MAtaifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR iliyochapishwa katika ukurasa wa YouTube wa shirika hilo.Makala inatupeleka nchini Tanzania ambako tunamsikiliza Brigedia Jenerali George Mwita Itang'are, Mkuu wa Kituo cha Mafunzo ya Ulinzi wa Amani cha Tanzania (TPTC) akitoa wito kwa Nchi Wanachama wa Umoja wa Mataifa kuendelea kuunga mkono ulinzi wa amani duniani kwa kuzikabili changamoto wanazokutana nazo walinda amani. Anold Kayanda anasimulia.Na mashinani ikiwa hivi majuzi Dunia iliadhimisha siku ya redio duniani fursa ni yake Irene munyua kutoka Kenya akieleza washirika wetu Radio Domus kuhusu umuhimu wa radio kwa jamii katika maisha ya kila siku.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!  

Habari za UN
13 FEBRUARI 2025

Habari za UN

Play Episode Listen Later Feb 13, 2025 11:05


Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini Tanzania kumulika siku ya redio duniani, maudhui yakiwa Radio na Tabianchi, na ni kwa vipi chombo kinachodaiwa kutwamishwa na maendeleo ya teknolojia kinaendelea kusaidia kuelimisha umma kuhusu madhara ya mabadiliko ya tabianchi, Teonas Aswile wa TBC Taifa nchini Tanzania anaeleza.Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC ambapo hali inazidi kuwa tete na leo Mkurugenzi Mtendaji wa shirkika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF, Catherine Russell, ameelezea wasiwasi mkubwa kuhusu kuongezeka kwa ghasia mashariki mwa mwa  nchi hiyo katika majimbo ya Kivu Kaskazini na Kivu Kusini, ambapo watoto na familia wanakabiliwa na ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu.Naibu mkuu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu masiala ya kibinadamu na misaada ya dharura OCHA nchini Sudan Edmore Tondhlana akizungumza na UN News amesema hali nchini Sudan inaendelea kuwa janga la kibinadamu wakati vita ikishika kasi na watu wakiendelea kufurushwa makwao. Amesema "Tunashuhudia hali ambapo Sudan ina mahitaji ya kibinadamu yaliyo miongoni mwa makubwa zaidi duniani. Takriban watu milioni 30 wanahitaji msaada wa kibinadamu. Hili ni ongezeko la takriban watu milioni tano zaidi ikilinganishwa na mwaka uliopita, pia, Sudan ina idadi kubwa zaidi ya watu waliopoteza makazi yao.Na leo ni siku ya Redio Duniani mwaka huu ikibeba maudhui Redio na mabadiliko ya tabianchi. Kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na utamaduni UNESCO lengo la maudhui haya ni kudhihirisha jukumu la redio katika kusambaza ujumbe na kuelimisha kuhusu changamoto za mabadiliko ya tabianchi, kutanabaisha kuhusu hatua endelevu na kuwapa sauti wanaharakati wa mabadiliko ya tabianchi.Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili leo fursa ni yake mtaalam wetu Onni Sigalla, Mhariri mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa      nchini Tanzania, BAKITA anafafanua maana za neno “MSUMBI”.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!  

VOA Express - Voice of America
Waandishi wa habari wanaelezea mtazamo wao iwapo redio bado ina mchango mkubwa kwa jamii katika maadhimisho ya Siku ya Redio Duniani. - Februari 13, 2025

VOA Express - Voice of America

Play Episode Listen Later Feb 13, 2025 29:59


VOA Express pia inafuatilia kwa karibu sana maswala yanayovuma katika mitandao ya kijamii kama sehemu moja muhimu ya upashanaji habari siku hizi.

katika siku habari jamii redio maadhimisho mtazamo
Habari za UN
12 FEBRUARI 2025

Habari za UN

Play Episode Listen Later Feb 12, 2025 9:58


Hii leo jaridani tunaangazia matokeo ya maandamani nchini Bangladesh, na machafuko nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC. Makala inatupeleka nchini Kenya na mashinani nchini Tanzania, kulikoni?Ripoti ya Umoja wa Mataifa iliyotolewa leo mjini Geneva Uswisi na ofisi ya haki za binadamu (OHCHR) imefichua kuwa viongozi wa juu wa serikali ya Bangladesh walihusika moja kwa moja katika ukandamizaji wa maandamano makubwa yaliyoitikisa nchi hiyo mwaka 2024 na kusababisha vifo vingi.Baada ya waasi wa M23 jimboni Kivu Kaskazini, Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC kupatia wakimbizi waliokuwa wamesaka hifadhi kambini mjini Goma, wawe wamerejea makwao ndani ya saa 72 kuanzia juzi jumatatu, mamia wameanza kutii amri hiyo licha ya hofu inayowakabili ya kule wanakotakiwa kurejea.Makala inatupeleka jijini Nairobi, Kenya ambako ambako Kevin Keitany wa redio washirika wetu Domus FM kwa kuzingatia kuwa kesho Februari 13 ni Siku ya Kimataifa ya Redio, ametutumia maoni ya vijana wawili wanaozungumzia namna redio imewasaidia kusambaza ujumbe wao kuhusu hatua dhidi ya mabadiliko ya tabianchi.Mashinani fursa ni yake Tupokigwe Simon, msichana      mwenye  umri wa miaka 16, ambaye ni mwanaharakati wa  Sayansi, Teknolojia, Uhandisi na hisabati , STEM, wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto, UNICEF, akieleza umuhimu wa  msichana katika sayansi na kuwahimiza wasichana wenzake kusoma  sayansi.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!  

Habari za UN
Redio imetusaidia kufikisha elimu kwa umma kuhusu hatua dhidi ya mabadiliko ya tabianchi

Habari za UN

Play Episode Listen Later Feb 12, 2025 3:12


Ikiwa kesho Februari 13 ni Siku ya Kimataifa ya Redio, makala inatupeleka jijini Nairobi, Kenya ambako ambako Kevin Keitany wa redio washirika wetu Domus FM kwa kuzingatia kuwa kesho Februari 13 ni Siku ya Kimataifa ya Redio, ametutumia maoni ya vijana wawili wanaozungumzia namna redio imewasaidia kusambaza ujumbe wao kuhusu hatua dhidi ya mabadiliko ya tabianchi.

Habari za UN
07 FEBRUARI 2025

Habari za UN

Play Episode Listen Later Feb 7, 2025 10:56


Hii leo jaridani tunaangazia hali ya haki za binadamu nchini Jamhuri ya kidemokasia ya Congo DRC, Na masuala ya afya nchini Jamhuri ya Congo, au Congo-Brazaville. Makala inatupeleka nchini Tanzania, na mashinani nchini Kenya, kulikoni?Kamishna Mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa, Volker Türk, leo akizungumza katika Kikao Maalum cha Baraza la Haki za Binadamu kinachofanyika jijini Geneva, Uswisi, ameonya kuwa ghasia zinazoendelea mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) zinaweza kuwa mbaya zaidi ikiwa hazitashughulikiwa.Wananchi wa Jamhuri ya Congo, au Congo-Brazaville, ni mashuhuda wa jinsi shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ulimwenguni, WHO limewasaidia kukabiliana na ugonjwa wa macho na ngozi unaosababishwa na nzi mweusi wanaozaliana kwenye mito na vijito, ugonjwa ambao uliathiri shughuli zao za kijamii na kiuchumi kutokana na muwasho wa kila mara na upofu.Katika makala Hamad Rashid wa Redio washirika KidsTime FM ya mkoani Morogoro Tanzania anaangazia kuhusu namna Tanzania inaendelea kufanikisha Lengo Namba 16 la Maendeleo Endelevu ya Umoja wa Mataifa linalotilia mkazo upatikanaji wa amani, haki na taasisi imara kwa kupunguza mrundikano wa mashauri au kesi mahakamani, kuwezesha upatikanaji wa haki kwa makundi maalumu katika jamii.Na mashinani fursa ni yake Ahmed kutoka kaunti ya Laikipia nchini Kenya, ambaye kupitia video iliyoandalia na Shirika la Umoja wa Mataifa la uhamiaji, IOM anaeleza jinsi ambavyo ukame wa mara kwa mara unavyoathiri mifugo ya.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!  

Habari za UN
Juhudi za mahakama Tanzania kutekeleza Lengo namba 16 ya SDG

Habari za UN

Play Episode Listen Later Feb 7, 2025 3:57


Leo katika makala Hamad Rashid wa Redio washirika KidsTime FM ya mkoani Morogoro Tanzania aanaangazia kuhusu namna Tanzania inaendelea kufanikisha Lengo Namba 16 la Maendeleo Endelevu ya Umoja wa Mataifa linatilia mkazo upatikanaji wa amani, haki na taasisi imara kwa kupunguza mrundikano wa mashauri au kesi mahakamani, kuwezesha upatikanaji wa haki kwa makundi maalumu katika jamii.

Habari za UN
Tanzania: FAO yawezesha ufugaji kuku bila kutumia dawa ili kuepusha UVIDA

Habari za UN

Play Episode Listen Later Nov 25, 2024 3:55


Nchini Tanzania wanufaika wa  mradi wa kudhibiti usugu wa vimelea vya magonjwa dhidi ya dawa, (AMR) au kwa lugha ya Kiswahili, (UVIDA) unaotekelezwa na shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo, (FAO) nchini Tanzania, kwa kushirikiana na Wizara ya Mifugo na Uvuvi wamezungumzia manufaa ya ufugaji wa kuku bila kutumia dawa. Unaweza kujiuliza wanafuga vipi kuku bila kutumia dawa. Na je ni kwa nini wanafanya hivi. Je hawatumii dawa kabisa au wanafanya nini?Katika makala hii, mwandishi wa habari wa Redio washirika wetu Tanzania Kids Time ya mkoani Morogoro,mashariki mwa taifa hilo la Afrika Mashariki, Hamad Rashid, amezungumza na wanufaika hao  ambao pia walipata nafasi ya kuonesha shamba darasa la ufugaji kuku bila ya kutumia dawa kupitia hafla iliyoratibiwa na FAO katika shule ya sekondari Kihonda, Manispaa ya Morogoro, ikienda sambamba na Wiki ya utoaji elimu kuhusu UVIDA  ambayo hufanyika duniani kote kila ifikapo tarehe 18 hadi 24 mwezi Novemba. Kwako Hamad.

Habari za UN
22 OKTOBA 2024

Habari za UN

Play Episode Listen Later Oct 22, 2024 9:57


Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini DRC kufuatilia kazi za kituo cha Taifa cha Redio na Televisheni, RTNC huko Beni jimboni Kivu Kaskazini za kakabiliana na habari potofu. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na mashinani.Ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa iliyotolewa leo mjini Cairo, Misri, imebainisha kwamba athari za vita zimerudisha nyuma maendeleo huko Gaza kwa takriban miaka 69. Ripoti hiyo iliyoratibiwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo UNDP na  Kamisheni ya Umoja wa Mataifa ya Kiuchumi na Kijamii kwa Asia Magharibi imeonya kwamba bila kuondoa vikwazo vya kiuchumi na kuwekeza katika maendeleo, uchumi wa Palestina unaweza kushindwa kurejesha viwango vya kabla ya vita na kusonga mbele kwa kutegemea misaada ya kibinadamu pekee.Kiongozi wa timu ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani (WHO) ya kupambana na mlipuko wa ugonjwa wa Marburg Dkt. Janet Diaz ameeleza kwamba uongozi thabiti wa serikali ya Rwanda umewezesha kufanya uamuzi wa haraka na kuchukua hatua kuanzisha mwitikio wa sekta mbalimbali dhidi ya mlipuko wa sasa wa ugonjwa huo wa Marburg nchini humo.Na uongozi wa Kikosi cha Muda cha Umoja wa Mataifa nchini Lebanon (UNIFIL) umeendelea kusisitiza kwamba pamoja na changamoto zilizopo, walinda amani wa UNIFIL wanaendelea kufanya kazi kwa karibu na jamii za kusini mwa Lebanon ili kuwezesha utoaji wa misaada ya kibinadamu kwa wenye uhitaji. Hivi karibuni kumekuwa na mashambulizi dhidi ya walinda amani hao wa Umoja wa Mataifa yanayotekelezwa na majeshi ya Israeli.Mashinani kupitia video ya Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu masuala ya Kibinadamu na misaada ya dharura OCHA tunamuangazia mmoja wa watu waliokimbia makazi yao akiwa katika shule ya Al Rimal, akielezea changamoto wanazokutana nazo katika kukabiliana na hali ngumu inayowakabili raia wa Gaza.Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu! 

Habari za UN
Kuanza tena kwa shughuli za Redio RTNC kutawawezesha kupigana dhidi ya taarifa potofu na za uongo - MONUSCO

Habari za UN

Play Episode Listen Later Oct 22, 2024 5:26


Umoja wa Mataifa unaendelea kuunga mkono serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC katika kukabili habari potofu na za uongo hususan huko mashariki mwa nchi ambako vikundi vilivyojihami vinaendelea kushambulia raia na kupambana na jeshi la serikali. Hivi karibuni Umoja wa Mataifa kupitia ujumbe wake wa kulinda amani nchini humo, MONUSCO, umeipatia kituo cha Taifa cha Redio na Televisheni, RTNC huko Beni jimboni Kivu Kaskazini jengo na vifaa vyenye thamani ya takriban dola elfu hamsini za Kimarekani. Hatua hiyo iliwezesha RTNC kuanza tena matangazo yake. Mwandishi wetu wa DRC, George Musubao alifika kituoni hapo kuzungumza na wahusika na wanufaika.

Habari za UN
11 SEPTEMBA 2024

Habari za UN

Play Episode Listen Later Sep 11, 2024 9:59


Hii leo jaridani tunaangazia ugonjwa wa homa ya nyani au mpox barani Afrika na kufufuliwa kwa kituo chao cha Redio na Televisheni ya Taifa, RTNC huko Beni nchini DRC. Makala tanakupeleka nchini Tanzania na mashinani nchini Kenya, kulikoni?Ugonjwa wa homa ya nyani au mpox ukisalia kuwa dharura ya afya ya umma duniani, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR linasaka zaidi ya dola milioni 21 zitakazotumika hadi mwishoni mwa mwaka huu kuongeza harakati dhidi ya ugonjwa huo miongoni mwa wakimbizi katika nchi zilizokumbwa na dharura ya ugonjwa huo, hususan Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC.Wakazi wa mji wa Beni, jimboni Kivu Kaskazini nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC wana furaha tele baada ya kufufuliwa kwa kituo chao cha Redio na Televisheni ya Taifa, RTNC. Kupitia msaada wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo, MONUSCO, wakazi hao sasa wanaweza kusikiliza na kutazama vipindi vyao wanavyovipenda, waandishi wa habari nao, hawafanyi tena kazi chini ya mti.Makala inatupeleka mkoani Kigoma kaskazini magharibi mwa Tanzania kusikia manufaa ya mradi wa Kilimo Tija Kigoma (KiTiKi) unaoendeshwa na shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) kwa ufadhili wa Watu wa Jamhuri ya Korea.Na mashinani kupitia video ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa chakula duniani kanda ya Afrika, tunamsikia Shane Prigge mkuu wa mnyororo wa usambazaji, WFP Kenya akieleza jinsi UNHAS ambalo ni shirika la ndege la Umoja wa Mataifa la huduma za kibinadamu linavyowezesha mashirika ya kibinadamu kufanya kazi zao.Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu! 

Habari za UN
MONUSCO yafanikisha kufufuliwa kwa kituo cha  Redio na TV cha taifa RTNC mjini Beni

Habari za UN

Play Episode Listen Later Sep 11, 2024 1:55


Wakazi wa mji wa Beni, jimboni Kivu Kaskazini nchini  Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC wana furaha tele baada ya kufufuliwa kwa kituo chao cha Redio na Televisheni ya Taifa, RTNC. Kupitia msaada wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo, MONUSCO, wakazi hao sasa wanaweza kusikiliza na kutazama vipindi vyao wanavyovipenda, waandishi wa habari nao, hawafanyi tena kazi chini ya mti. Kupitia video ya Monusco iliyochapishwa mtandao wa X, John Matemuli, mwandishi wa habari wa kituo hicho cha Redio na Televisheni Beni, kilichositisha matangazo kwa karibu miaka mitano, anafafanua jinsi mambo yalivyokuwa kabla ya kujengwa upya kwa kituo hicho.“Miaka mitano bila Radio na Televisheni ya kitaifa ya Kongo (RTNC) mjini Beni ilikuwa ya machafuko sana. Kulikuwa na wakati ambapo tulikuwa tukifanya kazi hata kutoka juu ya mti, unaweza kuamini! Tulihisi kwamba kulikuwa na hitaji, wananchi na hata baadhi ya viongozi walihisi vivyo hivyo.”Ezechiel Kambale, mkazi wa Beni naye pia anaeleza furaha yake.“Ulipita muda mrefu tangu redio hii kuwa hewani. Lakini sasa nashukuru kwamba wamerudi. Kuna tofauti kubwa ikilinganishwa na zamani, kwa sababu leo, hata kama niko mbali na mji, bado nayapata mawimbi ya redio kana kwamba nipo hapa mjini.”Tulimrudia John na kumuuliza kilichokuwa tofauti kuhusu kituo hicho hasa kabla ya msaada wa MONUSCO.“Kazi ilofanywa hapa imewaridhisha wananchi. Leo, tuna ofisi za usimamizi. Tuna studio za kisasa za televisheni. Tuna studio ya redio kwa ajili ya kutengeneza vipindi  vyetu. Tuna chumba cha habari kilicho na vifaa vya kutosha. Tulikumbana na matatizo ambayo yalihitaji msaada katika ngazi zote, lakini MONUSCO ilitupatia vifaa, ambavyo sasa vinaturuhusu kufanya kazi katika hali bora.”

Habari za UN
29 AGOSTI 2024

Habari za UN

Play Episode Listen Later Aug 29, 2024 11:01


Yaliyomo kwenye Jarida la Habari za UN hii leo ni pamoja na ziara ya Katibu Mkuu wa UN huko Timor-Leste; maadhimisho ya siku ya kimataifa ya kupinga majaribio ya nyuklia na kauli ya Mkurugenzi Mteule wa WHO kanda ya Afrika, Dkt. Faustine Ndugulile baada ya kuteuliwa. Mada kwa kina ni Morogoro Tanzania. Na pia kuna kujifunza lugha ya kiswahili. Karibu na mwenyeji wako ni Anold Kayanda.Nchini Tanzania katika mkoa wa Morogoro, ulioko mashariki mwa nchi hiyo, wakulima 50 kutoka skimu za umwagiliaji za Ifakara Dakawa mkoani humo na Mbarali mkoa wa Mbeya, kusini magharibi mwa Tanzania wamepatiwa ujuzi wa kutumia zana bora za kisasa za Kilimo cha mpunga ikiwemo zana za kusawazisha mashamba, kupanda mbegu na kuvuna. Lengo ni kuongeza thamani katika uzalishaji wa zao la mpunga. Mafunzo yaliyotolewa na Taasisis ya Utafiti wa Kilimo TARI kwa usimamizi wa shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo, FAO huku zana zikiwezeshwa na shirika la Korea Kusini la ushirikiano wa maendeleo, KOICA. Hamad Rashid wa Redio washirika Tanzania Kids Time FM mkoani Morogoro alifika kwenye skimu hiyo kuzungumza na wakulima walionufaika. Je wajua neno la kiingereza LINK tafsiri yake ni ipi kwa lugha ya Kiswahili? Onni Sigalla, Mhariri Mwandamizi Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania anafafanua.

WAPL Home Brewed
WAPL Home Brewed Redio REWIND - Episode 1.13.24

WAPL Home Brewed

Play Episode Listen Later Jan 19, 2024 55:11


Turn On & Tap In to an Original Music Mélange ♫ from Wisconsin & Midwest Americana with WAPL Home Brewed Radio!Saturday Mornings at 9am on 105.7 FM & Streaming at wapl.com+ Produced & Hosted by John Jordan♫This Week's Featured Home Brewed Artists♫Charlie Parr / DUSK / Brad Bordini / Sister Winchester / Scorched Waves / Michael Grabner / Rocky Bodsberg/Thomas / Tom Thiel Trio / Maxmilian / Strategic / Jackson Mankowski / Modern JoeyKUDOS to the Cool Venues That Book Original ♫usicAppleton Beer Factory / NYE with A-Town Unplugged at Appleton Music Factory / Stone Arch Brewpub / Gibson Community Music HallGET OUT & SIGN UP at Fox Valley Music Scene Fans for more LIVE ♫ Music happenings from around N.E. Wisconsin!CHEERS to Your Ears! ♫

Habari za UN
11 JULAI 2023

Habari za UN

Play Episode Listen Later Jul 11, 2023 0:10


Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina ambapo leo ninatupeleka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, kama ilivyo sehemu nyingi za Afrika Mashariki nako lugha ya kiswahili inatajwa kuwa chombo chenye nguvu sana kinachoingilia kati ujenzi wa amani na pia katika biashara hasa kwa wakaazi wa mji wa Goma katika jimbo la Kivu Kaskazini mashariki mwa nchi hiyo. Kiswahili ndio lugha ya kwanza nchini DRC yenye idadi kuwa ya wazungumzaji katika mikoa ya Mashariki na Magharibi mwa nchi ambako inatumiwa hata kwenye vyombo vya habari kama Redio na televisheni. Pia tunaangazi ripoti ya UNFPA ya idadi ya watu Duniani. Mashinani tunakupeleka nchini Haiti, kulikoni?Mwenyenji wako ni Leah Mushi, karibu!

Alfajiri - Voice of America
Kituo kimoja cha redio nchini Kenya cha Ghetto radio kimewavutia wasikilizaji wake wanaowafuatilia kwa kutangaza lugha ya mtaani ya “Sheng” - Julai 05, 2023

Alfajiri - Voice of America

Play Episode Listen Later Jul 5, 2023 29:59


Matangazo ya nusu saa kuhusu habari za mapema asubuhi pamoja na habari za michezo.

Habari za UN
Mradi wa ALiVE awamu ya pili kupima stadi za watoto nje ya masomo ya kawaida Zanzibar

Habari za UN

Play Episode Listen Later Jun 21, 2023 0:05


Baada ya kufanya tathmini ya upimaji Stadi za maisha na maadili kwa vijana wenye umri wa miaka 13  hadi 17 nchini Kenya, Uganda na Tanzania, mradi wa ALiVE katika awamu ya pili umepanga kuwafikia watoto wenye umri wa miaka  6  hadi 12 ambao bado wako shule ili kuwapima viwango vyao vya Stadi za maisha na maadili ikiwa ni katika jitihada za kuchechemua fikra tunduizi na kusongeza malengo ya Umoja wa Mataifa ya maendeleo endelevu, SDGs. Kama ambavyo mradi huu utatekelezwa katika maeneo mengine ya Afrika Mashariki, Visiwani Zanzibar nako uzinduzi umefanyika na hapa Hamad Rashid wa Redio washirika MVIWATA FM kutoka Morogoro, Tanzania amesafiri hadi Wilaya ya Mjini, Mkoa wa Mjini Magharibi visiwani humo Zanzibar na kutuandalia na kutuandalia Makala hii. 

Habari za UN
Taasisi 16 zakutana Morogoro Tanzania kusongesha SDG 4

Habari za UN

Play Episode Listen Later Jun 14, 2023 0:05


Taasisi 16 zikiwemo mashirika yasiyo ya kiserikali, asasi za kiraia na vyuo vikuu ambao kwa pamoja ni wanachama wa Mtandao wa Elimu Afrika Mashariki (RELI) wamekutana mjini Morogoro, Tanzania kujengewa uwezo wa namna ya kuimarisha juhudi za kuchochea mabadiliko ya elimu na kuhamasisha ujengaji fikra tunduizi kwa vijana ili kusongesha lengo namba 4 la Malengo ya Umoja wa Mataifa ya Maendeleo Endelevu SDGs. Mafunzo haya yameratibiwa na Shirika lisilo la kiserikali la GESCI (The Global e-Schools and Communities Initiative) kutoka nchini Kenya linalotekeleza mradi wa ADAPT Kenya na Tanzania, Mwandishi wa Habari Hamad Rashid wa Redio washirika wetu MVIWATA FM ya Morogoro Tanzania amefuatilia mafunzo hayo ya siku tatu na kutuandalia makala ifuatayo.

Habari za UN
Mradi wa Binti Shupavu wasongesha SDG4 nchini Tanzania

Habari za UN

Play Episode Listen Later May 22, 2023


Nchini Tanzania Shirika la lisilo la kiserikali la Girls Livelihood and Mentorship Initiative (GLAMI) kupitia Mradi wake wa Binti Shupavu, unaowajengea Stadi za Maisha ikiwemo uwezo wa kujitambua, mabinti walioko Shule, unaendelea na juhudi za kufanikisha Lengo la Nne la maendeleo endelevu SDG's linalohusu Elimu, ambapo Jumla ya wasichana 824 wananufaika kutoka katika Shule Tisa zilizopo Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro Vijijini, ambapo Mwezi huu wa Tano limekamilisha Programu ya kufanya vikao na wazazi katika Shule hizo ili kuwajengea uwezo wa malezi ya watoto wao. Hamad Rashid wa Redio washirika MVIWATA FM kutoka Morogoro, mashariki mwa Tanzania amehudhuria baadhi ya vikao vya wazazi na GLAMI kisha kutuandalia makala ifuatayo. 

Habari za UN
Kupitia FISH4ACP, FAO Tanzania yachukua hatua kukwamua wavuvi wanawake na wanaume

Habari za UN

Play Episode Listen Later Apr 14, 2023 0:02


Nchini Tanzania, shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo, FAO kupitia  mradi  wake FISH4ACP  limepokea matokeo ya Utafiti kuhusu Usawa wa Kinjisia katika Masuala ya Uvuvi, moja ya hoja ambayo ikitekelezwa vema itasaidia kufanikisha malengo ya maendeleo endelevu, SDGs hasa la kutokomeza njaa na kuondokana na umaskini.Uzinduzi wa matokeo hayo umefanyika wakati wa kikao cha siku mbili  hapa mkoani Kigoma na unatoka na Utafiti kuhusu Usawa wa kijinsia katika mnyororo wa thamani wa mazao ya Uvuvi Ziwa Tanganyika ukishirikisha wadau mbalimbali  wakiwemo wavuvi, wachakataji, wasafarishaji,  Jeshi la Polisi, serikali na wadau wa maendeleo.Devotha Songorwa wa Redio washirika Kids Time FM nchini Tanzania ndio shuhuda wetu wa uzinduzi huo uliofanyika katika  Mkoa wa Kigoma, Magharibi mwa Taifa hilo la Afrika Mashariki amezungumza na Afisa Mtaalamu Mnyororo wa Thamani wa Uvuvi na Ufugaji  Viumbe Maji, kutoka FAO nchini Tanzania anayesimamia mikoa ya Katavi, Rukwa na Kigoma nchini Tanzania, Hashim Muumin,  ambaye amempatia muhtasari wa matokeo ya utafiti huo kutokana na mradi huo wa miaka mitano  unaotekelezwa katika nchi 12 za Afrika  ikiwemo  Tanzania .“Imeonekana uvuvi ni suala la kiume zaidi kuliko wanawake lakini kwa utafiti tulioufanya tuliona asilimia 78 ya wachakataji ni wanawake na  asilimia  99 ya wavuvi ni wanaume na kuna masuala ambayo yanawakwaza kina wanawake na wanaume wavuvi katika kujikwamua kiuchumi,” amesema Afisa huyo.Ameeleza kuwa  utafiti huo utasaidia kubaini changamoto zinazokabili masuala ya Jinsia na fursa zake  katka Ziwa Tanganyika ili kutoa mwamko kwa wanawake na watu wenye ulemavu kujihusisha na Uvuvi kuinua kipato chao.“Shirika la FAO limeanzisha dawati la jinsia katika Wizara ya Mifugo na Uvuvi ambalo linafanya kazi na sisi kama mradi wa FISH4ACP tunafanya kazi kwa karibu sana kuhakikisha sera, mikakati na sheria za Serikali zinatekelezwa,” amebainisha Hashim.

Habari za UN
14 APRILI 2023

Habari za UN

Play Episode Listen Later Apr 14, 2023 0:11


Hii leo jaridani tunaangazia wasichana waliotekwa nyara katika shule ya bweni huko Chibok Nigeria ambapo mpaka sasa 96 bado wapo utumwani, na matokeo ya mradi wa FISH4ACP nchini Tanzania. Makala tunakupeleka nchini Rwanda na Mashinani nchini Jamhuri ya Congo, Brazaville, kulikoni?Ikiwa ni miaka tisa imepita tangu wasichana 276 kutekwa nyara wakiwa katika shule ya bweni huko Chibok Nigeria ambapo mpaka sasa 96 bado wapo utumwani, Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF limetaka wadau kusaidia katika kuwekeza zaidi katika usalama wa wanafunzi mashuleni kwani bado vitendo vya utekaji vinaendelea nchini humo.Nchini Tanzania, shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo, FAO kupitia  mradi  wake FISH4ACP  limepokea matokeo ya Utafiti kuhusu Usawa wa Kinjisia katika Masuala ya Uvuvi, moja ya hoja ambayo ikitekelezwa vema itasaidia kufanikisha malengo ya maendeleo endelevu, SDGs hasa la kutokomeza njaa na kuondokana na umaskini. Devotha Songorwa wa Redio washirika Kids Time FM nchini Tanzania ndio shuhuda wetu wa uzinduzi huo uliofanyika katika  Mkoa wa Kigoma, Magharibi mwa Taifa hilo la Afrika Mashariki.Katika tunasalia hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa kusikiliza simulizi ya manusura wa mauaji ya kimbari dhidi ya watutsi nchini Rwanda mwaka 1994, ikiwa leo Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa lina kumbukizi maalum ya mauaji hayo.Na katika mashini tutaelekea katika mji mkuu wa Jamhuri ya Congo, Brazaville kusikia ushauri kutoka kwa mwanamke ambaye amekuwa akiishi na Virusi vya Ukimwi, VVU kwa miaka 24.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, Karibu!

Habari za UN
Redio Ngoma ya Amani inachangia utunzaji wa amani hapa mashariki mwa DRC - Wasikilizaji

Habari za UN

Play Episode Listen Later Feb 13, 2023 0:04


Katika Siku ya Redio Duniani mwaka huu wa 2023, UNESCO inaangazia redio huru kama nguzo ya kujenga amani na kuzuia migogoro. Redio inatazamwa kama chombo muhimu na sehemu muhimu ya kutunza amani. Redio hushughulikia visababishi na vichochezi vya migogoro, kabla hazijaweza kulipuka na kuwa vurugu. Inatoa mbinu mbadala ya kuzuia migogoro, au migongano ya maslahi, kuondoa kutoelewana, na kutambua masuala ya kutoaminiana. Hii inaweza kusaidia kukabiliana na chuki, hamu ya kulipiza kisasi, au nia ya kutumia silaha. Na sasa hii leo dunia ikiadhimisha siku hii ya Redio Duniani, mwandishi wetu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) Byobe Malenga anaangazia Redio Ngoma ya Amani, kituo cha redio cha mjini Fizi jimboni Kivu Kusini kinachohamasisha amani hususani katika maeneo ya mashariki mwa DRC. 

unesco drc hii hapa ngoma jamhuri mashariki redio kidemokrasia wasikilizaji
Habari za UN
Radio na ujenzi wa amani

Habari za UN

Play Episode Listen Later Feb 13, 2023 0:01


Hii leo ni siku ya redio duniani ambapo Umoja wa Mataifa unamulika nafasi ya chombo hicho kilichobuniwa takribani karne moja iliyopita katika kukuza na kujenga amani  wakati huu ambapo pia ni miaka 75 tangu kuanzishwa kwa operesheni za ulinzi wa amani za Umoja wa Mataifa.Ujumbe wa mwaka huu ni radio na amani ambapo Mkuu wa mawasiliano ya kimkakati kwenye Idara ya Umoja wa Mataifa ya ulinzi wa amani Francesca Mold  amesema maadhimisho ya sasa yamekuja wakati muafaka zaidi kwani Umoja wa Mataifa umeanza kampeni yam waka mmoja kuelekea kilele miaka 75 tangu kuanza kwa operesheni za ulinzi wa amani. Amesema operesheni za ulinzi wa amani zinategemea mitandao ya redio ambayo ni muhimu sana katika kufikia jamii mbalimbali hasa kwenye maeneo ambako hakuna mtandao wa intaneti na watu wako kwenye mbio mbio kila wakati kutokana na mapigano. Ametoa shukrani kwa wafanyakazi wa redio zilizo chini ya operesheni za ulinzi wa amani za Umoja wa Mataifa kama vile Radio Okapi iliyoko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Redio Guira huko Jamhuri ya Afrika ya Kati. Halikadhalika redio huru ambazo amesema zinatumia vipindi kama vile mijadala jumuishi kujibu hoja za wenyeji kwa kusambaza taarifa sahihi na kuhakikisha taarifa potofu na zisizo sahihi hazipati nafasi. Ametoa shukrani pia kwa msikilizaji akisema kuwa kupitia ushiriki wa msikilizaji, “tunakuwa thabiti zaidi na tunaungana ili kuleta amani.” Siku ya Redio duniani huadhimishwa kila mwaka tarehe 13 mwezi Februari kukumbuka kuanzishwa kwa Redio ya Umoja wa Mataifa mwaka 1946. 

Habari za UN
27 JANUARI 2023

Habari za UN

Play Episode Listen Later Jan 27, 2023 0:11


Hii leo jaridani tuakuletea ujumbe wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres kuhusu makumbusho ya Holocaust, pia tunamulika kazi ya walinda amani nchini DR Congo. Makala tunakwenda nchini Tanzania na mashinani tunasalia hapa makao makuu wa Umoja wa Mataifa.Ikiwa leo ni siku ya kimataifa ya kumbukizi ya waathitrika wa mauaji ya maangamizi makubwa au Holocaust dhidi ya wayahudi, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema mauaji hayo yalikuwa ni malimbikizo ya miongo ya chuki dhidi ya Wayahudi ndio maana sasa ni wakati wa kuhakikisha chuki za aina yoyote ile zinakomeshwa duniani.Kufuatia mashambulizi yanayofanywa na makundi mbalimbali ya waasi kwa raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC hususani mashariki mwa nchi hiyo ya pili kwa ukubwa wa eneo barani Afrika, walinda amani wa Umoja wa Mataifa wa kikosi cha 9 kutoka Tanzania, TANZBATT 9 kinachohudumu katika kikosi cha Umoja wa Mataifa cha kujibu mashambulizi cha FIB-MONUSCO, wamefanya doria katika barabara ya Mbau-Kamango nje ya mji wa Beni jimboni Kivu Kaskazini.Makala tunakwenda nchini Tanzania kusikia ni kwa vipi Mahakama inachagiza moja ya malengo ya maendeleo endelevu, SDGs na shuhuda wetu ni Hamad Rashid wa Redio washirika MVIWATA FM mkoani Morogoro, Mashariki mwa Tanzania.Katika mashinani leo ikiwa ni siku ya kimataifa ya kukumbuka waathirika na waliokufa kutokana na mauaji ya maangamizi dhidi ya wayahudi yaliyofanywa na manazi nakuletea ujumbe wa nini kifanyike kuepusha hali hiyo na ujumbe unatolewa na Dani Dayan, Mwenyekiti wa jumba la makumbusho ya mauaji ya maangamizi ya wayahudi huko Israel, liitwalo Yad Vashem. Ujumbe huu ameutoa wakati wa uzinduzi wa maonesho ya kitabu chenye majina ya wayahudi waliouawa na manaziMwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!

Habari za UN
Elimu ya usuluhishi na haki kusaidia kufanikisha SDGs Morogoro, Tanzania

Habari za UN

Play Episode Listen Later Jan 27, 2023 0:04


Lengo namba 16 la malengo ya maendeleo endelevu SDGs yaliyopitishwa na nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa mwaka 2015 linasisitiza amani, haki na taasisi thabiti. Uvunjivu wa amani utokanao na migogoro kwenye jamii ni moja ya maeneo yanayomuikwa ili kuhakikisha amani inakuweko na hivyo kuwezesha kufikia SDGs mwaka 2030.Nchini Tanzania, wiki ya sheria imefungua pazia na Mahakama Kuu inatimiza wajibu wake kusaidia nchi kufanikisha SDGs. Mathalani mkoani Morogoro, Mashariki mwa taifa hilo, Mahakama Kuu imesema sasa itasongesha zaidi elimu ya usuluhishi na haki kwa lengo la sio tu kujenga amani bali pia kuchochea uchumi. Je nini kinafanyika? Hamad Rashid wa Redio washirika MVIWATA FM alikuwa shuhuda wetu na ameandaa makala hii, 

Habari za UN
26 OKTOBA 2022

Habari za UN

Play Episode Listen Later Oct 26, 2022 0:11


Hii leo kwenye Jarida la Umoja wa Mataifa tunamulika masuala ya kibinadamu, ugaidi, tabianchi na mazingira na ufugaji wa samaki kibiashara.Kamishna Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi duniani, UNHCR, Filippo Grandi amehitimisha ziara yake ya siku mbili nchini Somalia na kutoa wito kwa viongozi wa kimataifa kuongeza kasi ya usaidizi wa kibinadamu ili kuepusha janga la kibinadamu linalozidi kushika kasi kwenye taifa hilo lililokumbwa na ukame.Kesho kutwa Ijumaa huko nchini India, Kamati ya kukabili ugaidi ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa itakutana nchini India kutathmini vitisho vipya duniani vitokanavyo na teknolojia mpya. Mkutano huo wa siku mbili ni wa kwanza kufanyika nje ya makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani tangu mwaka 2015.Makala leo tunakwenda Tanzania ambako huko John Kabambala wa Redio washirika Kids Time FM ya mkoani Morogoro anamulika uzinduzi wa mpango wa pamoja wa mashirika yasiyo ya kiserikali wa kutafiti athari za mabadiliko ya tabianchi kwa watoto.Mashinani nampisha Levedy Céleste Lossangoye msichana kutoka Gabon ambaye ni mhitimu wa shahada ya kwanza ya uhandisi wa kilimo na sasa anapata mafunzo ya ufugaji wa samaki kibiashara kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na kilimo, FAO akilenga kuimarisha biashara ya baba yake ya ufugaji samaki.Karibu na mwenyeji wako leo ni Assumpta Massoi

Habari za UN
Bonga bongo kufanyika India kutathmini teknolojia na ugaidi

Habari za UN

Play Episode Listen Later Oct 26, 2022 0:02


Kesho kutwa Ijumaa huko nchini India, Kamati ya kukabili ugaidi ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa itakutana nchini India kutathmini vitisho vipya duniani vitokanavyo na teknolojia mpya. Mkutano huo wa siku mbili ni wa kwanza kufanyika nje ya makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani tangu mwaka 2015. Happiness Pallangyo wa Redio washirika Uhai FM kutoka Tabora Tanzania anafafanua zaidi.Mjadala utajikita kwenye maeneo matatu makuu ambayo ni mosi; Intaneti na mitandao ya kijamii; Pili,  Ufadhili wa mitandao ya kigaidi duniani na tatu; kuenea kwa matumizi ya mifumo ya angani isiyo na rubani kama vile droni.Umoja wa Mataifa unasema teknolojia hizo mpya zinakua kwa kasi kubwa na zinatumika mara kwa mara katika nchi mbalimbali duniani ikiwemo kwenye usalama wa taifa na kukabili ugaidi.Hata hivyo teknolojia hizo zinatumiwa vibaya na vikundi vya kigaidi kwa manufaa yao binafsi yasio na nia njema.Mkutano pia utakuwa ni jukwaa la kubadilishana mawazo ya jinsi teknolojia inaweza kusaidia kukabili kusambaa kwa maudhui ya kigaidi mtandaoni na kukabili pia simulizi za kigaidi.Hofu nyingine iliyoko na itakayomulikwa ni matumizi kwa nia mbaya ya uchapishaji wa chapa tatu au 3D, maroboti, akili bandia na mifumo ya angani isiyo na usimamizi.Kwa sasa India ndio inashikilia kiti cha Uenyekiti wa Kamati hiyo hadi mwishoni mwa mwaka huu ambapo akizungumza na waandishi wa habari jijini New York, Marekani, Mwakilishi wa Kudumu wa India Kwenye Umoja wa Mataifa Balozi Ruchira Kamboj ambaye ndiye Mwenyekiti amesema,(Sauti ya Ruchira Kamboj)“Ugaidi katika aina zote zile, katika muonekano wowote ule ni moja ya vitisho vikubwa zaidi vya amani na usalama duniani. Kitendo chochote cha kigaidi hakiwezi kuhalalishwa kwa misingi ya nia yoyote ile, wakati uliofanyika, pahali ilipofanyika na ni nani aliyetekeleza. Kamati imejizatiti kupambana na janga hili katika ngazi ya kimataifa.”Kutokana na ugumu wa suala zima, na kasi ya mapinduzi yake, matarajio ni kwamba wajumbe watakuwa na nyaraka ya mwisho ambayo itatoa mwelekeo wa jinsi magaidi wanatumia teknolojia, kwa lengo la kufunga simulizi zao na matumizi ya teknolojia.Kamati ya kukabili ugaidi ya Baraza la Usalama la UN iliundwa kwa kauli moja tarehe 28 mwezi Septemba mwaka 2001, kufuatia shambulio la kigaidi dhidi ya Marekani tarehe 11 Septemba 2001 na wanachama ni wajumbe wote 15 wa Baraza la Usalama.

Habari za UN
Juhudi za UNICEF Uganda zafanikisha watoto kupata chanjo

Habari za UN

Play Episode Listen Later Oct 17, 2022 0:03


Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF kwa ushirikiano na serikali ya Japan , wanaisaidia serikali ya Uganda kuimarisha uwezo wa mfumo wa uhifadhi wa chanjo baada ya mfumo wa afya kuathirika vibaya na janga la COVID-19, lengo likiwa kuhakikisha kila mtoto na kila mtu hasa katika jamii zisizojiweza anapata chanjo za kuokoa maisha. Taarifa zaidi inasomwa studio na Happiness Palangyo wa Redio washirika Uhai FM  (TAARIFA YA HAPPINESS PALANGYO)  Eneo la Lira Kaskazini mwa Uganda ni moja ya maeneo yaliyoathirika kwa kiasi kikubwa na janga la COVID-19 ambalo limeuacha hoi mfumo mzima wa afya ikiwemo huduma za uhifadhi na utoaji chanjo.  Lakini sasa kupitia uwekezaji mkubwa uliofanywa na shirika la UNICEF kwa ufadhili wa serikali ya Japan umerejesha matumaini ya wakazi na hususan watoto kupata chanjo wanazostahili kwani shirika hilo limenunua na kuweka majokofu maalum 115 ya kuhifadhi chanjo ya COVID-19 na kupiga jeki chanjo zingine za kawaida ambazo ni za kuokoa maisha kwa watoto. Dkt. Ochen Buchan Patrick ni afisa wa huduma za afya wilayani Lira anasema  “Huu ni uwekezaji mkubwa ambao utatusaidia sana kutoa huduma zote muhimu kwa saa 24 bila kuingiliwa na ukarabati wa mfumo wa baridi . Mfumo huu mpya sasa unafanya kazi vizuri kwa sababu unatumia  nishati ya sola na ninafurahi kwamba sasa hatuhangaiki kugawanyaganywa gesi na kisha Kwenda kukusanya mitungi. Hivyo gharama za uendeshaji zimepungua kwa kiasi kikubwa , lakini pia mfumo wetu wa baridi wa uhifadhi umeimarika sana.”  Kabla ya mfumo huu mpya wa kuhifadhi chanjo,ilikuwa changamoto kubwa kuwafikia walengwa na chanjo muhimu kama asemavyo Mirriam Adongo afisa wa program ya chanjo katika kituo cha afya cha Ogur  “Tulikuwa tunakwenda hadi Lira mjini kupeleka chanjo. Tulikuwa tunaendesha pikipiki hata wakati wa mvua , na chngamoto ya hali mbaya ya hewa, barabara mbaya vyote vilikuwa vinatusibu, lakini sasa kwa mfumo kuletewa hapa imefanya kuwa rahisi kwetu hata kutoka nje kwa sababu tunaweza kupata chanjo kwa urahisi na pili unatumia sola, kabla ya hapo tulipokuwa na mtambo unaotumia umeme , umeme ukikatika tu ilitulazimu kukimbiza chanjo zote hadi kwenye kituo cha wilaya cha kuhifadhi chanjo mjini ambayo ilikuwa kazi kubwa”  Uongozi wa huduma za afya wa Lira unasema sasa huduma zimeimarika na la msingi lililosalia ni kuhakikisha vifaa hivyo  vinatunzwa vyema na kudumu kwa mufda mrefu ili kuendelea kuihamasisha jamii na kuwapa chanjo muhimu.  Nalo shirika la UNICEF limesema furaha yake ni kuona lengo lililokusudiwa linatima kwani kwao kuwekeza katika vifaa hivyo vya mfumo wa bardidi wa kuhifadhi chanjo ilikuwa muhimu sana kama ilivyo kuwekeza kwenye upatikanaji wa chanjo zenyewe na sasa hata vituo vya afya vya vijijini kabisa vinaweza kuhifadhi chanjo zake, shukran kubwa kwa serikali ya Japan. 

Habari za UN
Kuhakikisha afya ya mtoto, Tanzania yatekeleza programu ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto

Habari za UN

Play Episode Listen Later Oct 12, 2022 0:03


Mashiriki 77 yasiyo ya kiserikali mkoani Morogoro, Tanzania yameanza kunufaika na mradi jumuishi wa kitaifa unaofahamika kwa kifupi MMMAM yaani Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto. Programu ya MMMAM inasimamiwa na Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na wadau kama  Shirika lisilo la kiserikali la Community Development Organization (CDO). Kutoka Morogoro, Tanzania, Mwandishi Hamad Rashid wa Redio washirika MVIWATA FM ya Morogoro Tanzania ametuandalia makala hii kuhusu mradi huo.   

Habari za UN
Waandishi wa Habari Tanzania wajengewa uwezo kuhusu umiliki wa ardhi kwa wanawake

Habari za UN

Play Episode Listen Later Oct 3, 2022 0:04


Mashirika mbalimbali ya kiraia nchini Tanzania yamezidi kuhamasika kuelimisha Jamii juu ya Haki ya Ardhi kwa wananchi, wanawake nikundi ambalo bado wameendelea kushindwa kumiliki ardhi hivyo inahitajika sauti ya pamoja katika utetezi wa Haki ya kumiliki Ardhi hususan katika mazingira magumu ya umasikini, mila na desturi kandamizi katika baadhi ya jamii. Hamad Rashid wa Redio washirika MVIWATA FM ya Morogoro mashariki mwa Tanzania ni miongoni mwa waandishi wa habari waliopatiwa mafunzo na shirika la Landesa Tanzania ili waweze kuelimisha jamii umuhimu na haki ya wanawake kumiliki ardhi na umuhimu wa kulinda Haki ya Ardhi kwa wananchi kwenye maeneo ya uwekezaji wa Ardhi. Tuungane naye katika Makala hii aliyotuandalia.

Habari za UN
Wanafunzi wapatiwa elimu ya namna ya kuishi na watu wenye ualbino

Habari za UN

Play Episode Listen Later Sep 30, 2022 0:03


Mtoto umleavyo ndio akuavyo ni methali unaofundisha jamii kuhakikisha iwapo inataka watoto wawe na tabia fulani basi ni vyema waanze kuwafundisha wangali wadogo. Na ndicho kinachofanywa nchini Tanzania na Chama cha watu wenye ualbino TAS mkoa wa Morogoro, mashariki mwa taifa hilo.  Chama hicho kinaendelesha programu ya kutoa elimu kwa wanafunzi na kimetembelea shule ya msingi kilakala iliyopo Manispaa ya Morogoro na kutoa elimu kwa wanafunzi wa darasa la sita na la saba juu ualbino na namna ya kuishi nao katika Jamii. Miongoni mwa kilichowasukumua kutoa elimu kwa wanafunzi hao ni kuwa wanatumaini pindi wanfunzi watakapopata elimu hiyo wataenda kuwaelimisha na wengine na hii inaweza kuleta uelewa zaidi kwa Jamii hasa kwa watoto wenyewe kwa wenyewe wakikutana. Tuungane na Sure Ndereka wa Redio washirika Mviwata fm aliyeshuhudia wanafunzi hao wakipatiwa mafunzo na kutuandalia makala hii

Habari za UN
Wanafunzi wapatiwa elimu ya namna ya kuishi na watu wenye ualbino

Habari za UN

Play Episode Listen Later Sep 30, 2022 0:03


Mtoto umleavyo ndio akuavyo ni methali unaofundisha jamii kuhakikisha iwapo inataka watoto wawe na tabia fulani basi ni vyema waanze kuwafundisha wangali wadogo. Na ndicho kinachofanywa nchini Tanzania na Chama cha watu wenye ualbino TAS mkoa wa Morogoro, mashariki mwa taifa hilo.  Chama hicho kinaendelesha programu ya kutoa elimu kwa wanafunzi na kimetembelea shule ya msingi kilakala iliyopo Manispaa ya Morogoro na kutoa elimu kwa wanafunzi wa darasa la sita na la saba juu ualbino na namna ya kuishi nao katika Jamii. Miongoni mwa kilichowasukumua kutoa elimu kwa wanafunzi hao ni kuwa wanatumaini pindi wanfunzi watakapopata elimu hiyo wataenda kuwaelimisha na wengine na hii inaweza kuleta uelewa zaidi kwa Jamii hasa kwa watoto wenyewe kwa wenyewe wakikutana. Tuungane na Sure Ndereka wa Redio washirika Mviwata fm aliyeshuhudia wanafunzi hao wakipatiwa mafunzo na kutuandalia makala hii

Habari za UN
Ufadhili wa UNCDF umetukwamua sana Kibondo Big Power Group

Habari za UN

Play Episode Listen Later Sep 12, 2022 3:52


  Kibondo Big Power Group (KBPG) ni ushirika wa kilimo mkoani Kigoma, kaskazini magharibi mwa Tanzania. Shirika la mitaji la Umoja wa Mataifa, UNCDF lilisaidia KBPG kwa msaada wa kifedha ambao ulitumika kupanua shughuli zake kwa kufanya shughuli zifuatazo: kuchimba kisima cha maji mita 100, ununuzi wa pampu ya maji ya jua na ujenzi wa ghala na nyumba za kukausha jua za mihogo na chanja na mtaji wa kufanyia kazi. Hamad Rashid wa redio washirika  Hamad Rashid wa redio washirika wa Redio washirika wetu MVIWATA FM ya mkoani Morogoro, Tanzania anasimulia zaidi.

Habari za UN
Tukomeshe ubaguzi kwa watu wenye asili ya Afrika :Guterres

Habari za UN

Play Episode Listen Later Aug 31, 2022 1:47


Katika kuadhimisha siku ya kimataifa ya watu wenye asili ya Afrika Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema pamoja na utajiri wa urithi wa utamanduni na mchango mkubwa unaotolewa na watu wenye asili ya Afrika katika jamii lakini bado wanakabiliwa na ubaguzi ulio ota mizizi. Tupate taarifa zaidi kutoka kwa Evarist Mapesa wa Redio washirika wetu SAUT FM   Huu ni mwaka wa pili tangu kuanza kwa maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya watu wenye asili ya Afrika ambapo katibu Mkuu Guterres amesema mwezi Desemba mwaka huu kutafanyika kikao cha kwanza cha Jukwaa la Kudumu la Watu Wenye Asili ya Kiafrika na kuhimiza watu wote kujiandaa kushiriki na kusukuma mbele kazi ya Jukwaa. Mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa ameeleza kuwa “ Duniani kote, mamilioni ya watu wenye asili ya Kiafrika bado wanashuhudia ubaguzi wa rangi uliokita mizizi na wa kimfumo. Ndiyo maana Umoja wa Mataifa unaendelea kutoa wito wa kuheshimiwa kikamilifu kwa haki zao za kibinadamu na uhuru wao wa kimsingi, kwa ajili ya kurekebisha mambo hayo yanapokiukwa, na kuomba msamaha rasmi na kulipwa kwa makosa makubwa ya utumwa na ukoloni.” Ameeleza pia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa limeomba kuwepo na kikosi kazi kitakacho simamia utekelezwaji kwa Ufanisi wa Azimio la Durban na Mpango wa Utekelezaji , kikosi kazi hicho kitaandaa rasimu ya tamko la Umoja wa Mataifa kuhusu kukuza na kuheshimu kikamilifu haki za binadamu za watu wenye asili ya Afrika.  Amesisitiza kuwa jukwaa litachangia kazi hii muhimu sana na kwamba “ni muhimu kwa pamoja tuendelee kuongea  kwa sauti kubwa na bila kukosa dhidi ya dhana yoyote ya ubaguzi wa rangi na kwamba tufanye kazi bila kuchoka ili kukomboa jamii zote kutoka kwa balaa ya ubaguzi wa rangi.”

Habari za UN
Mwani haribifu wageuzwa tofali Mexico

Habari za UN

Play Episode Listen Later Aug 19, 2022 2:12


Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa maendeleo duniani, UNDP nchini Mexico linafadhili miradi ya maabara za wabunifu wanaopatia majawabu changamoto za kijamii zitokanazo na  matatizo yanayowazunguka. Miongoni mwa miradi hiyo ni ule wa kusafisha fukwe za bahari na uchafu unaokusanywa ukiwemo mwani aina ya Sargusssum, kutumika kutengeneza nyumba. Tupate undani wa taarifa hii iliandaliwa na UNDP na kusomwa studio na Evarist Mapesa wa Redio washirika SAUT FM. Maji yakipiga fukwe ya baharí ya Riviera Maya, maji hayo ya bahari yanakuja na lundo la mwani na mfanyabiashara Omar Sánchez aliona fursa ya kufanya usafi na mwaka 2015 aliingia mkataba na hoteli zilizopo ufukweni kwa ajili ya kusafisha, mkataba ambao uliwanufaisha takriban familia 300 zilizopata ajira ya kusafisha mwani huo wa Sargassum.  Sánchez anasema “Tatizo la mwani wa sargassum ni kubwa. Kwa uzoefu wangu, nimeliona likikua na kukua na kukua kila mwaka.” Mfanyabiashara huyo alikuwa akikusanya na kutupa mwani huo lakini baada ya kujiunga na maabara ya UNDP inayolenga kuongeza kasi ya suluhisho zinazobuniwa na wanajamii ndipo alipopata wazo la kutotupa mwani wa Sargassum bali kuuchakata na kutengeneza matofali ya kujengea nyumba na kuyapa jina la Sargablock. Sánchez nasema historia yake ndio ilimsukuma kupata wazo la matofali hayo wakati akiwaza kutafuta mbinu bora za kuisaidia jamii “ jambo la kwanza nililofanya ni kujiweka katika viatu vya wengine. Mama yangu alikufa na hakuwahi kuwa na nyumba yake mwenyewe. Kwa hivyo, nina nini kwa 'Casa Angelita'? Kwanza, nikafikieia wengine na kuanza na wazo la nyumba. Kutokuwa na nyumba ni kejeli ya maisha: Mimi nimekuwa bila makao na sasa nimepata fursa hii ya kusaidia watu wengine.” Kampuni yake kwa siku inauwezo wa kutengeneza matofali 1,000 na maono haya ya Sanchez yanamuwezesha kutoa nyenzo ya ujenzi wa gharama nafuu, kujenga nyumba za bei nafuu kwa wakazi wa eneo la Riviera Maya na kutimiza kiu ya familia nyingi ya kuishi katika nyumba zao wenyewe kwa staha.    

Habari za UN
Wanaume Morogoro nchini Tanzania wasaidia kufanikisha unyonyeshaji wa mtoto maziwa ya mama

Habari za UN

Play Episode Listen Later Aug 8, 2022 1:56


Wiki ya unyonyeshaji wa maziwa ya mama kwa watoto ambayo ilianza tarehe mosi ya mwezi huu wa Agosti na kuadhimishwa duniani kote kwa jamii kuelimishwa kuhusu umuhimu wa mama kumnyonyesha mtoto imehitimishwa jana tarehe 7. Huko mkoani Morogoro nchini Tanzania, kwa wiki nzima mashirika mbalimbali kwa kushirikiana na serikali yamekuwa yakizungumza na wanajamii ili kufahamu uelewa wao kuhusu suala hili la unyonyeshaji na pia kuwapa elimu panapohitajika. Hamad Rashid wa Redio washirika wetu MVIWATA FM ya Mkoani Morogoro, amehudhuria sherehe za ufungaji wa maadhmisho hayo yaliyofanyika katika viwanja vya Kata ya Mkambalani Kijiji cha Mkambalani Manispaa ya Morogoro na hii ni taarifa yake.

Habari za UN
Wavuvi wanawake Kigoma wapata mtandao wao, shukrani kwa FAO

Habari za UN

Play Episode Listen Later Jul 29, 2022 4:19


Katika kutekeleza lengo namba 8 la malengo ya maendeleo endelevu, SDGs kuhusu ajira za staha na ukuaji kiuchumi sambamba na namba 5 la usawa wa kijinsia, shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo duniani FAO nchini Tanzania,  limezindua tawi la tatu la Mtandao wa Wanawake Wanaojihusisha na Shughuli za Uvuvi TAWFA kupitia mradi wake wa kukuza mnyororo wa thamani wa mazao ya uvuvi katika ziwa Tanganyika. Devotha Songorwa wa Radio Washirika KIDS Time  FM ya Morogoro nchini Tanzania ameshuhudia uzinduzi na kuandaa taarifa hii. Sherehe za uzinduzi huo zimefanyika mkoani Kigoma nchini humo ambapo wanawake wavuvi, viongozi wa serikali na wafanyakazi wa FAO walifungua rasmi tawi hili ikiwa ni la tatu nchini humo baada ya mwengine mawili yaliyozinduliwa huko kanda ya Ziwa Victoria na Ukanda wa Bahari ya Hindi. Uzinduzi huo unafanyika kupitia mradi wa FISH4ACP unaotekelezwa katika mikoa ya Kigoma, Rukwa na Katavi ambapo Mratibu wa Sekta ya Uvuvi Kitaifa kutoka FAO, Oliva Mkumbo akizungumza na Devotha Songorwa wa Redio washirika wa Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa alimueleza lengo ni kuwawezesha wanawake kiuchumi kupitia uvuvi ili kuinua kipato cha familia na kuondokana na umasikini. “Lengo la kuanzisha jukwaa la wanawake ni kuwawezesha kina mama ili mchango wao utambulike na kuleta athari chanya katika jamii. Tunataka kila mwanamke anayejihusisha na mnyororo wa thamani katika uvuvi anakuwa na sehemu ya kutoa mawazo yake na kubadilishana uzoefu ili kwa pamoja wachangie uboreshaji wa uvuvi,” Anasema Oliva. UN News Oliva Mkumbo Mratibu wa Sekta ya Uvuvi Kitaifa kutoka FAO Mratibu huyo wa FAO amesema hili halitakuwa tawi la mwisho nchini humo. “Jukwaa rasmi kitaifa lilifunguliwa 2017 ili kuwafikia wanawake wengi wakaanzisha Zone Chapters, Chapter ya Kanda ya Ziwa Victoria 2019, baadaye ikaja ya Uvuvi baharini, Kanda ya Ziwa Tanganyika na baadaye huko tutakuwa na linguine linalohusika na wavuvi kutoka katika maziwa madogo madogo,” Ameeleza Mratibu huyo. Beatrice Mmbaga ni Mwenyekiti wa Taifa wa Mtandao wa Wanawake Wanaojihusisha na Shughuli za Uvuvi Tanzania (TAWFA) anasema jukwaa hili ni sehemu ya kutatua changamoto zinazowakabili kina mama walio katika sekta ya uvuvi. “Nia ya kuanzisha chombo hiki ni kumfikia mama popote alipo anayejishusisha na samaki na mazao yake Tanzania nzima ndipo sasa tunashuka ngazi za chini katika Mikoa yetu, Kanda na Wilaya ili tuwe na sauti moja kwa sababu kina mama ndiyo asilimia kubwa wanajihusisha na samaki baada ya mavuvi hasa kwenye kuchakata na masoko lakini wana changamoto nyingi sana,” amebainisha Mwenyekiti huyo. UN News Wanawake wajasiriamali katika sekta ya Uvuvi Tanzania Kwa upande Mkurugenzi Msaidizi anayesimamia masuala ya Udhibiti Ubora na Mazao ya Uvuvi kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi Steven Lukanga amebainisha kwamba wanawake bado wanahitajika kupatiwa elimu ya uvuvi salama na kukidhi mahitaji ya walaji. “Kikubwa ni kuwajengea uwezo wanawake kutambua viwango vinavyopaswa kuzalisha yale mazao yanayowaendea walaji kwa kuzingatia viwango vilivyopo chini ya Shirika la Viwango Tanzania (TBS) kwahiyo sisi kama wizara tunashirikiana nao kuhakikisha wachakataji wanawake wanakidhi viwango vinavyotakiwa,”Amesema Lukinga.  

Habari za UN
Stadi za maisha ni muhimu hususani kwa vijana ili kufikia malengo ya maendeleo endelevu

Habari za UN

Play Episode Listen Later Jul 20, 2022 4:08


Nchini Tanzania Jumla ya Kaya 13,600 na vijana 2,700 wanatarajiwa kunufaika na tathmini ya upimaji stadi za maisha kwa kuangalia viwango vyao vya kujitambua, ushirikiano walionao kwao na kwa jamii, jinsi wanavyotatu matatizo pamoja na heshima binafsi jinsi wanavyojiheshimu wao, jamii na mali za wengine. Sifa zote hizo ni muhimu katika kusaidia wanajamii wa rika mbalimbali wanashiriki katika kufanikisha Malengo ya Umoja wa Mataifa ya Maendeleo Endelevu, SDGs.  Taasisi ya Milele Zanzibar Foundation inatekeleza mradi huo ikilishirikisha Shirika la Uwezo Tanzania kusimamia upande wa Tanzania Bara ambapo mradi utafika katika katika Halmashauri za Wilaya 34, Hamad Rashidi ni mwanahabari kutoka Redio washirika wetu Tanzania Kidstime ya mkoani Morogoro amehudhuria mafunzo yaliyofanyika Mkoa wa Morogoro wakipewa wakufunzi watakaoenda kufundisha wapimaji wa tathmini ya stadi za maisha kwa vijana na kutuandalia makala ifuatayo. 

Habari za UN
Kongamano lafanyika Dodoma kujadili sekta ya kilimo, uvuvi na mifugo Tanzania

Habari za UN

Play Episode Listen Later Jun 13, 2022 4:18


Mabadiliko ya tabianchi ni moja ya majanga yanayokumba dunia hivi sasa na kuathiri sekta mbalimbali ikiwemo kilimo, ufugaji na uvuvi. Nchini Tanzania kwa kutambua athari hizo hasi, kumefanyika kongamano la nane la mwaka 2022 la  sera kwa wadau wa sekta hizo, kongamano lilofanyika katika mji mkuu wa taifa hilo, Dodoma.  Washiriki takribani 600 wametoka mikoa na pande mbalimbali ikiwemo shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo, FAO Tanzania, serikali na sekta binafsi.  Mathalani wadau kutoka sekta binafsi wametoa wito kwa serikali kuwashirikisha katika mapitio ya sera mpya ya kilimo,  mifugo na uvuvi  ili waweze kutoa mawazo yao yatakayosaidia kukabiliana na changamoto  zinazokabili sekta hizo zinazotokana  na mabadiliko ya tabianchi.  Lakini kwa kina tuungane na Devotha Songorwa wa Redio washirika KidsTime FM nchini Tanzania ambaye alikuwa shuhuda wetu kwenye kongamano hilo. 

Habari za UN
Tanzania yazindua programu ya malezi, ustawi na makuzi ya watoto katika mikoa 10

Habari za UN

Play Episode Listen Later Jun 10, 2022 3:37


Lishe duni ni moja ya changamoto mtambuka hususani katika ustawi na makuzi ya watoto. Kwa kulizingatia hilo na kwa kutambua kuwa kila nchi inapaswa kushiriki katika kuyasongesha malengo ya Umoja wa Mataifa ya Maendeleo Endekevu, SDGs, Tanzania imezindua programu jumuishi ya malezi, makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto kwa lengo la kumaliza changamoto ya lishe duni na changamoto nyingine dhidi ya watoto hususani walio chini ya umri wa miaka nane. Pamoja na mambo mengine, lishe duni inachangia kwa kiasi kikubwa kukwamisha lengo namba 3 kwa kuwakosesha watoto afya bora, na lengo namba 4 kwa kuwa kikwazo katika ujifunzaji wao. Hamad Rashid mwandishi kutoka Redio washirika wetu Tanzania kidstime, amehudhuria uzinduzi huo uliofanyika katika ukumbi wa mikutano Ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Morogoro na kuandaa makala ifuatao.

Habari za UN
FAO na SIDO Tanzania yapatia mama lishe mafunzo ya usalama wa chakula

Habari za UN

Play Episode Listen Later Jun 6, 2022 4:05


Tarehe 7 mwezi Juni kila mwaka ni siku ya usalama wa chakula duniani, ambapo Umoja wa Mataifa kupitia shirika lake la chakula na kilimo FAO, unaangalia ni kwa jinsi gani chakula kinaweza kuwa ni bora kwa mlaji bila kuathiri afya yake kuanzia shambani hadi mezani. Nchini Tanzania, FAO  imeshirikiana na shirika la viwanda vidogo nchini humo, SIDO na kupatia mafunzo mama na baba lishe katika majiji mawili ya mkoa wa Dodoma na DAr es salaam. Kulikoni? Majibu ya swali hilo ndio msingi wa makala yetu ya leo ambapo Devotha Songorwa wa Redio washirika Kids Time FM mkoani Dodoma amezungumza na mkufunzi kutoka SIDO anayeanza kwa kujitambulisha.

Habari za UN
Stadi za maisha ni muhimu hususan kwa vijana ili kufikia malengo ya maendeleo endelevu

Habari za UN

Play Episode Listen Later Jun 1, 2022 4:07


Nchini Tanzania Jumla ya Kaya 13,600 na vijana 2,700 wanatarajiwa kunufaika na tathmini ya upimaji stadi za maisha kwa kuangalia viwango vyao vya kujitambua, ushirikiano walionao kwao na kwa jamii, jinsi wanavyotatua matatizo pamoja na heshima binafsi jinsi wanavyojiheshimu wao, jamii na mali za wengine. Sifa zote hizo ni muhimu katika kusaidia wanajamii wa rika mbalimbali wanashiriki katika kufanikisha Malengo ya Umoja wa Mataifa ya Maendeleo Endelevu, SDGs.  Taasisi ya Milele Zanzibar Foundation inatekeleza mradi huo ikilishirikisha Shirika la Uwezo Tanzania kusimamia upande wa Tanzania Bara ambapo mradi utafika katika Halmashauri za Wilaya 34, Hamad Rashidi ni mwanahabari kutoka Redio washirika wetu Tanzania Kidstime ya mkoani Morogoro amehudhuria mafunzo yaliyofanyika Mkoa wa Morogoro wakipewa wakufunzi watakaoenda kufundisha wapimaji wa tathmini ya stadi za maisha kwa vijana na kutuandalia makala ifuatayo. 

Habari za UN
Serikali ya Tanzania itakomboa watu wenye ulemavu kwa kuboresha mfumo wa ajira serikalini -  Shega Mboya

Habari za UN

Play Episode Listen Later Apr 29, 2022 2:40


Serikali nchini Tanzania imeshauriwa kuboresha Sekretarieti ya mfumo wa uombaji ajira kwa njia ya mtandao maarufu kama Ajira Portal ili uweze kuwatambua watu wenye ulemavu na hivyo kumiza matakwa ya sera ya ajira ambayo ina kipengele mahususi kinacholenga kuwajumuisha watu wenye ulemavu.  Ushauri huo umetolewa na Shega Mboya wa Morogoro, Tanzania ambaye pamoja na kuwa na elimu ya juu ya digrii mbili, hajaweza kupata ajira ingawa anaamini pamoja na vigezo vingine ambavyo anaamini anavyo, laiti mfumo wa kidijitali ungeweza kutambua watu wenye ulemavu, ingekuwa rahisi kwake na kwa wengine. Hamad Rashid ni Mwandishi wa Habari wa Redio washirika Tanzania Kids time fm kutoka Morogoro amezungumza na msichana huyo na ameandaa makala ifuatayo.

Habari za UN
Tunaishukuru UNHCR imetusaidia kubadilisha maisha – Watu wa asili ya Warao ukimbizini Brazil 

Habari za UN

Play Episode Listen Later Apr 21, 2022 2:49


Kuelekea kuanza kwa Kikao cha 21 cha Jukwaa la kudumu la Umoja wa Mataifa la watu wa asili ambalo litaanza Jumatatu wiki ijayo kwa kuwakutanisha katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa jamii za watu wa asili, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR limeutumia mfano wa watu asili wa wa jamii ya Warao wa Venezuela walioko ukimbizini Brazil, kuonesha kuwa watu wa asili ni miongoni mwa makundi yanayoathiriwa zaidi na mizozo inapotokea katika jamii. Evarist Mapesa wa Redio washirika SAUT FM ya Mwanza Tanzania anaisoma taarifa hii.   Brazil ni mwenyeji wa zaidi ya wakimbizi na wahamiaji 300,000 kutoka Venezuela, ambao wamekimbia uhaba mkubwa wa chakula na dawa na kuongezeka kwa mfumuko wa bei na ukosefu wa usalama nchini mwao Venezuela.  Takriban watu 7,000 kati ya wakimbizi hao 300,000 walioko Brazil ni Warao, watu wa asili ambao wengi wao walifika Brazil wakiwa maskini na wenye utapiamlo.  Raia hawa wa Venezuela wanakabiliwa na vikwazo vikali linapokuja suala la kukidhi mahitaji yao ya kimsingi na kuzoea maisha ya Brazili.  Katika nchi ya Brazil ambayo inayozungumza Kireno, mara nyingi wanakabiliana na kizuizi cha lugha mbili, kwani wengi, hasa Warao wenye umri mkubwa, wanazungumza tu lugha yao ya asili na hata lugha ya kihispania inayozugumzwa katika nchi yao Venezuela, hawaielewi vizuri.    Mmoja wa watu hawa wa asili wa jamii ya watu wa Warao ni Marcelino Moraleda, kiongozi wa Jamii na muhudumu wa afya. Ujuzi na uelewa wa Marcelino unahitajika sana kwa wakimbizi wenzake.  “Kazi yangu ni kuwachukua Warao wenzangu na kufuatilia hali yao ya lishe. Lengo ni kupunguza hatari zozote za kiafya za Warao kukaa kwenye makazi hayo.” Marcelino ameiambia UNHCR.   Marcelino anasimulia kuwa kabla ya kuhamia hapa katika makazi maalum ya wahamiaji hawa katika eneo la Manaus na kupata usaidizi kutoka kwa Umoja wa Mataifa, walikuwa na hali mbaya hata ya kukosa mlo lakini sasa hali imebadilika, anasema, "hatushughulikii tena matatizo ya utapiamlo. Ninajitahidi kuboresha afya ya Warao mwenzangu. Tuna msemo katika Warao: "Nobarana ja takitane". Yaani Ili kuepuka kuugua."  UNHCR inaenda mbali zaidi kiasi imekuwa ikifanya kazi na wadau na vyuo vikuu katika mkakati wa kuwasaidia wakimbizi na wahamiaji wanaoishi nchini humo kuthibitisha viwango vyao vya elimu na vyeti vingine vya kitaaluma.    Kiujumla, Marcelino kwa niaba ya wenzake anaishukuru UNHCR akisema, "Wafanyakazi wa UNHCR hutufanya tujisikie salama, pamoja na mashirika mengine ambayo yanatuunga mkono kila wakati, yanatuunga mkono kila wakati."   

Habari za UN
Tanzania imepata funzo katika janga la Covid-19, inaboresha miundombinu ya elimu

Habari za UN

Play Episode Listen Later Apr 19, 2022 4:26


Baadhi ya wanafunzi wa Shule za Sekondari nchini Tanzania wameeleza kunufaika na mkopo wa riba nafuu Trilioni 1.3 ambao Tanzania iliupata mwaka jana 2021 kutoka Shirika la Fedha Dunia IMF kwa kuelekeza sehemu ya fedha katika uboreshaji wa mpango wa maendeleo kwa ustawi wa taifa na mapambano dhidi ya Uviko 19, ikijenga vyumba vya madarasa 12,000 vilivyogharimu shilingi Bilioni 240 kwa lengo la kupunguza msongamano shuleni sambamba na miundombinu ya madarasa na samani za ndani kuzingatia afua za kujikinga na ugonjwa wa Covid 19 au kama wanavyoita katika nchi hiyo, Uviko 19. Katika kuonesha taswira halisi, Hamad Rashid ni mwandishi wa Habari wa Redio washirika Tanzania kids time Fm ya mkoani wa Morogoro, amefanya ziara ya kutembelea mradi uliokamilika wa vyumba vya madarasa ya Uviko 19 katika Shule za Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro, Manispaa ambayo imejenga jumla ya vyumba vya madarasa 86. 

Habari za UN
Tutawaelekeza maafisa ugani wasaidie wakulima Uyui, Tabora - Kosare Makori

Habari za UN

Play Episode Listen Later Apr 12, 2022 3:33


Kutokana na athari za mabadiliko ya tabianchi kuleta ukame katika maeneo mbalimbali ya dunia, kusababisha kupungua kwa mvua za masika, baadhi ya wakulima wa  wilaya ya Uyui mkoani Tabora, nchini Tanzania wanasema hawajasazwa katika kukumbana na athari za mabadiliko hayo kwani hata mvua za masika walizokuwa wanazitegemea kukuzia mazao yao, zimekuwa za kusuasua. Kwa sababu hiyo wameamua kujikita katika kilimo cha muda mfupi katika bustani ndogondogo ili waweaze kujikumu kimaisha  lakini bado wanakumbana na changamoto nyingine ikiwemo kukosa mbegu na pembejeo, na kulazimika kutumia sumu nyingi ambazo ni hatari kwa mazingira na afya.  Hamad Rashid wa Redio washirika Tanzania kidstime fm kutoka Mkoa wa Morogoro amesafiri hadi Magharibi mwa Tanzania Kata ya Ibelamilundi Wilaya ya Uyui Mkoa wa Tabora na kuzungumza na wakulima.

tanzania kwa tabora redio magharibi
Habari za UN
Tutawaelekeza maafisa ugani wetu wawasaidie wakulima Uyui, Tabora - Kosare Makori

Habari za UN

Play Episode Listen Later Apr 12, 2022 3:37


  Kutokana na athari za mabadiliko ya tabianchi kusababisha ukame katika maeneo mbalimbali ya dunia, kusababisha kupungua kwa mvua za masika, baadhi ya wakulima wa  wilaya ya Uyui mkoani Tabora, nchini Tanzania wanasema hawajasazwa katika kukumbana na athari za mabadiliko hayo kwani hata mvua za masika walizokuwa wanazitegemea kukuzia mazao yao, zimekuwa za kusuasua. Kwa sababu hiyo wameamua kujikita katika kilimo cha muda mfupi katika bustani ndogondogo ili waweze kujikumu kimaisha  lakini bado wanakumbana na changamoto nyingine ikiwemo kukosa mbegu na pembejeo, na kulazimika kutumia sumu nyingi ambazo ni hatari kwa mazingira na afya.  Hamad Rashid wa Redio washirika Tanzania kidstime fm kutoka Mkoa wa Morogoro amesafiri hadi Magharibi mwa Tanzania Kata ya Ibelamilundi Wilaya ya Uyui Mkoa wa Tabora na kuzungumza na wakulima.

tanzania kwa tabora redio magharibi
Habari za UN
Mfumo dume katika sekta ya ardhi na kilimo bado ni kikwazo kwa lengo namba 5 la SDGs 

Habari za UN

Play Episode Listen Later Mar 22, 2022 3:58


Pamoja na uwepo wa lengo namba tano la Umoja wa Mataifa linalosisitiza kupatikana haki sawa kwa jinsia zote, hali bado ni tofauti hasa katika sekta ya ardhi na kilimo. Mfano halisi ukiwa katika maeneo mengi barani Afrika amba wanawake wanaendelea kuwa waathirika wa mfumo dume kandamizi unaowafanya kukosa haki ya kumiliki ardhi.    Mtandao unaojulikana kama, Vuguvugu la Wakulima Wadogo Kusini na Mashariki mwa Afrika, La Via Campesina umewakutanisha wanawake wakulima wadogo kutoka mataifa 10 ya Afrika katika mjadala wa kubadilishana ujuzi na uzoefu kwa wakulima wadogo walio kwenye tabaka la chini, wakijadili masuala mbalimbali ikiwemo umiliki wa ardhi, mjadala uliofanyika nchini Tanzania mkoa wa Morogoro katika makao makuu ya Mtandao wa Vikundi vidogo vya Wakulima Tanzania MVIWATA. Hamad Rashid wa Redio washirika Tanzania Kids Time amehudhuria mjadala huo na kuandaa makala ifuatayo. 

Habari za UN
Radio Sauti ya Injili Goma yatumia Kiswahili kusongesha amani DRC

Habari za UN

Play Episode Listen Later Mar 15, 2022 3:45


katika kukuza lugha ya Kiswahili duniani Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania BAKITA limeandaa kongamano la wiki moja la Idhaa za Kiswahili duniani na kuwakutanisha wadau kutoka nchi mbalimbali zinazozungumza lugha ya Kiswahili jijini Arusha nchini humo. Stella Vuzo wa Kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa UNIC Dar es Salaam, Tanzania anashiriki Kongamano hilo na amefanya mahojiano na Mkurugenzi wa Redio sauti ya Injili iliyoko Goma jimboni Kivu Kaskazini nchini Jamhuri ya Kidemokrasia Kongo -DRC Mchungaji Ezra Kasereka Makoma anayeanza kwa kueleza namna redio yao inavyofundisha lugha ya Kiswahili wananchi wa DRC na nchi jirani ya Rwanda.