Msasaonline inaamini kila binadamu ana haki ya kuhabarika kuburudika, na kuelimika hivyo basi kazi yetu kuhakikisha tunakuletea habari sahihi, na kupunguza msongo wa mawazo kwa burudani nzuri na kubadirisha maisha yako kwa kuleta episode zenye mafunzo zaidi. Kwa undani zaidi tembelea web site yetu www.msasaonline.co karibu jisikie huru kuungana nasi.
Mziki mzuri na maelezo ya wasani mbalimbali yana patikana hapahapa jamsingi subscribe ili uwe wa kwanza kupata vibes connection
"COUNTRY BOY" AZUNGUMZIA UMUHIMU WA MSANII KUWA TRENDING YOUTUBE NA VIEWS WENGI KWENYE MUZIKI WAKE.
Karibu kwa mara nyingine tena kusikiliza show yako matata una weza ku subscribe ili kuwa wakwanza kupata burudani .
Karibu sana endelea kupata burudani ya connection vibes ya Msasaonline. Ukibonyeza www.msasaonline.co utafurahia show
Connection vibes ni bonge la kipindi ambacho ni collection ya story zote za burudani ambacho hupatikana www.msasaonline.com
KARIBU KWA MARA NYINGINE TENA KWENYE MWENDELEZO WA EPISODE ZA CONNECTION VIBES KIUNDANI ZAIDI BONYEZA www.msasaonline.co ili uweze kuala unapatamwendelezo subscribe
KARIBU SANA UBURUDIKE NA CONNECTION VIBES YA MSASAONLINE KWA TAARIFA NA BURUDANI TEMBELEA WWW.MSASAONLINE.CO
Haijalishi uko wapi, unaishi wapi, wewe ni nani na unafanya nini. Ila ukweli ni kuwa kila mmoja wetu ana masaa 24 kwa siku. Na katika masaa hayo hayo tunatumia kwa kupumzika na kufanya mambo mbalimbali katika maisha. Moja kati ya maswali mwanadamu amekua akijiuliza mara kwa mara, ni kutaka kufahamu dhumuni la maisha yake hapa duniani. Tumekua tukijiuliza mimi ni nani? kwanini nipo hapa duniani?.Na katika kutafakari huko ndipo wengi wetu tunafikiria kuhusu kazi au wito wetu. Kwani kuna utofauti mkubwa uliopo kati ya KAZI na WITO. 1. KAZI. Neno "KAZI" linawakilisha aina ya huduma unayoitoa kwa mabadilishano. Kwa kufanya kazi unakua unatoa muda wako, juhudi, ujuzi, umakini, maarifa na ufahamu wako kwaajili ya kujipatia kipato. Na kitendo hiki ndo kinajulikana kama AJIRA, BIASHARA, POSHO. Unaweza kuwa na sababu nyingi za kwanini kila siku unaenda kufanya kazi. Lakini kama haupo huru kifedha , kujiingizia kipato ndio azimio kuu la kazi. 2. WITO. Neno "WITO" linawakilisha maslahi ya mtu binafsi, kile anachopenda, kinachomvutia na kumsukuma mtu. Wito sio kitu unachohitaji kukifanya, hiki ni kitu chenye msukumo mkubwa ndani yako. Lakini licha ya hivyo wito unaweza kukuingizia kipato au ikawa kazi pia wakati huohuo. Wito unaweza kuja Kupitia njia mbalimbali mfano Sanaa, Usafi, au shughuli zozote za kibunifu (mfano Uandishi au uchoraji). Lakini licha ya hivyo WITO wa kweli na wenye nguvu ni ule wa kiutumishi. Na kupitia wito huu ndipo utakutana na huduma kadhaa za kujitolea mfano kufundisha, kufanya kazi kwa pamoja, kutoa misaada mbalimbali. Hapo ndio utajua utofauti wa KAZI na WITO. KAZI : ni kwaajili ya kipato. WITO : ni kwaajili ya utoshelezi. Lakini inaweza kutokea unaipenda sana kazi yako mpaka upo tayari kufanya hata bure, basi hapo hubalika na kuwa WITO na sio KAZI. na ikiwa wito itaanza kuzalisha faida.
Neno mafanikio kila mtu huwa ana maana yake kwa wakati wake na kwa eneo lake katika maisha. Nikiwa na maana kuwa kila mtu ana tafsiri yake kuhusu mafanikio kutokana na muda na wakati alionao na anaoendelea kuishi hapa duniani. Mfano : kuna mafanikio ya kiafya, kiuchumi, kiuchumi, kimahusiano. Sasa katika makala yetu leo hii tutazungumzia zaidi juu ya Mafanikio ya kiuchumi na kifedha. Hizi ni Siri muhimu ambazo ni nguzo kuu za kukusaidia kufikia Mada makubwa kiuchumi na kifedha. 1. IMANI NA IBADA. Siku zote hakuna njia ya kufanikiwa kirahisi bila ya kuwa na imani na kufanya ibada, na ndio maana kuna watu wanashinda kwenye nyumba za ibada wakimuomba Mungu huku wengine wakikesha kwa waganga kutokana na imani yao ili kupata utajiri na mali. Lakini nikwambie tu MFANIKIO ya kweli na yenye furaha ni yale utakayoyapata kutokana na kumuamini mwenyezi Mungu pekee. Jifunze kufanya ibada kila mara na utambue kuwa binadamu sio kazi ya mikono yake pekee bali ni kazi inayotokana na Mungu pekee na kila binadamu ana fungu lake jema mbele ya mwenyezi Mungu aliye muumba. 2. KUFANYA KAZI KWA BIDII. Suala zima la kufanikiwa katika maisha linahitaji kujitoa kila mara na kufanya kazi kwa bidii hasa. Kwani kufanya kazi kwa bidii huendana na ufanisi na ujuzi wako ulionao. Acha kuwa mtu wa kulalamika sana na kukata tamaa mapema, bali anza sasa kujituma utaona mafanikio mapema sana. 3. KUWA MSOMAJI ZAIDI. Kusoma mambo mbalimbali yanayohusu maisha au kile kitu ulichowekeza katika maisha yako kukifanya, hiyo ni sehemu tosha inayoweza kukubadilisha fikra zako na kukufanya kuwa bora na kuwa mtaalamu au mfanisi mkubwa katika utafutaji wa mafanikio yako. Kusoma sio mpaka urudi darasani, ila nina maana kuwa UJIFUNZE kusoma hata mambo hata yale ya kawaida yanayohusu maisha na mafanikio binafsi. Anza kusoma vitabu mbalimbali vinavyohusu maendeleo ya mtu binafsi, utajiri, kuwekeza, afya, usafi, ufanisi wa kazi au masoko. Mfano vitabu kama Rich Dad poor Dad, Maximum Achievement, The power of positive thinking au Self Billionaire. 4. MAHUSIANO MZURI NA WATU. Kuwa na mahusiano na watu wako wa karibu ni jambo jema linaloweza kukuweka katika mazingira mazuri zaidi ya mafanikio makubwa na ukawa mtu wa tofauti na wengine katika nyanja za maisha. Kama usipokua na mahusiano mazuri na watu basi swala la kukosa furaha na amani kwako itakua ni la kawaida sana. 5. KUWA NA NIDHAMU YA MUDA. Muda ndio msingi mzuri na wa kipekee wa kukusaidia kufikia malengo yako uliyojiwekea. Huwezi kufikia mafanikio makubwa kama bado hauna nidhamu kwenye swala la muda. Jifunze kwenda na muda ili uongeze ubora katika kazi yako, heshima yako na nidhamu yako binafsi. 6. NIDHAMU YA MATUMIZI YA FEDHA. Ukishindwa kutumia fedha zako vizuri na kujiwekea akiba basi hesabu kuwa wewe utakuwa unafanya jambo ambalo halina mwisho wake. Kutokua na nidhamu ya fedha ni kama vile unataka kuanzisha safari bila kujua mwisho wake ni nini. 7. KUJIAMINI NA KUJIKUBALI BINAFSI. Kujiamini ni hali pekee ndani ya mtu ya kuwa jasiri bila uongo katika jambo lolote lile analolikabili mbele yake. Ukijiamini na kujikubali wewe mwenyewe itakua ni rahisi na wengine kukuamini.
Nidhamu ni utii, kusikia, na kusikiliza. Nidhamu ni kufuata sheria, kanuni na taratibu kutoka kwa wanaokuongoza. Nidhamu ni kuwa mahala sahihi, wakati sahihi na kufanya jambo lililokuhitaji kuwa mahala pale kwa wakati ule. Nidhamu sio shikamoo, nidhamu sio upole na nidhamu sio Mavazi yenye staha pekee. Nidhamu ni zaidi ya mwonekano nadhifu na mavazi adili. Nidhamu ni mwenendo chanya, tabia nzuri, fikra chanya na kauli jengefu. Taaluma ni maarifa, ujuzi na mjongeo fulani wa fikra unaokuwa umepangiliwa utolewe kwa wanaojifunza ili wawe wataalamu ktk ugha fulani. Taaluma ni mafunzo yatolewayo kwa kufundisha wanafunzi ili wawe wataalamu wa kada fulani ktk jamii au Taifa. Mfano, Taaluma ya Umeme ni matokeo ya kufundishwa na kujisomea ktk mazingira rasmi na kufuata taratibu rasmi ili kuweza kuhitimu masomo ya UHANDISI wa UMEME na kujiajiri au kuajiriwa kama mtaalamu wa UMEME. NIDHAMU NI TAALUMA. Hakika, awae mwanajeshi huwa na nidhamu.Awae nurse au Daktari huwa na nidhamu na Awae padre huwa na nidhamu. Nidhamu hupaswa kuwa nayo kabla, wakati na baada ya kuhitimu elimu ya Taaluma fulani. Nidhamu sio jambo la Mda ingawaje Wanadamu tumeumbiwa kujisahau au hisia(mood). Hii huleteleza hasira, chuki na wakati mwingine kukengeuka na kujikuta Daima tunafanya au Tunasaka taaluma tukiwa watovu wa nidhamu mbele ya watoaji wataaluma tuliopaswa kuwaheshimu na kuwaonesha nidhamu kila mawio na machweo ya elimu tuitafutayo. Taaluma ni nidhamu. Ili mtoto afanye vyema ktk Taaluma yake, yaani ufaulu maridhawa Itampasa kuwa msikivu(nidhamu), mtulivu(nidhamu), mfuata maelekezo(nidhamu), mhudhuriaji shuleni(nidhamu), msomaji na mfanyaji wa mitihani(nidhamu) huku akiambatanisha na tabia, mienendo na maadili mema(nidhamu).
Kocha wa timu ya taifa ya Ufaransa, Didier Deschamps amesema kiungo wa kati wa klabu ya Manchester United, Paul Pogba amepatikana na maambukizi ya Virusi vya Corona. Kutokana na taarifa hiyo Pogba mwenye umri wa miaka 27 atalazimika kujitenga na wachezaji wenzake ambao wapo kwenye maandalizi ya michuano ya ligi ya Taifa la Ufaransa. Kwahiyo mfaransa huyo atakosa mechi ya kitaifa ya Ufaransa itakayochezwa siku ya Jumamosi tarehe 5 Septemba, 2020 na siku 3 baadae atakosa kwenye mechi dhidi ya Crotia. Hata hivyo Pogba huenda akachaguliwa katika uteuzi wa timu ya ufunguzi Manchester United dhidi ya Crystal Palace kwenye ligi kuu ya Uingereza ndani ya uwanja wao wa Old Trafford. Vile vile baada ya kuenea kwa taarifa ya kuambukizwa Corona, klabu ya ya Manchester United na Wachezaji wenzake wamemtakia heri ya kupona haraka kabla ya kuanza kwa msimu. Ila nafasi ya Paul Pogba katika kikosi cha Ufaransa itachukuliwa na kiungo wa kati wa Rennes Eduardo Camavinga mwenye asili ya Angola, anaecheza Klabu ya Stade Rennais FC.
MAMLAKA ya Mwasiliano Tanzania (TCRA) imeagiza Clouds TV na Redio kusitisha matangazo yao kwa muda wa siku saba kuanzia kesho Ijumaa 28 Agosti hadi 3 Septemba 2020 kwa kosa la kukiuka kanuni za utangazaji na kanuni ndogo za utangazaji za uchaguzi. Pia, mamlaka hiyo imevitaka Clouds TV na Redio kuomba radhi siku nzima ya leo Alhamisi tarehe 27 Agosti 2020 kwa kosa hilo. Akizungumza na waandishi wa habari makamo makuu ya mamlaka hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, James Kilaba amesema, adhabu hiyo inatokana na kukiuka kanuni mbalimbali za utangazaji na kanuni ndogo za wakati wa uchahuzi za mwaka 2015. Kilaba amesema, Clouds TV na Redio walikiuka kanuni za utangazaji kwa kutangaza wagombea kupita bila kupingwa wakati wenye uwezo wa kutangaza ni Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC). "Mnamo tarehe 26 Agosti 2020 kati ya saa 1 hadi 4 asubuhi kupitia vipindi Clouds 360 na Powerbreakfast Clouds Redio. Walirusha takwimu za wagombea ubunge waliopita bila kupingwa lakini wakijua taarifa hiyo haijathibitishwa na NEC na kukosa pia midhania," amesema Kilaba. Kutokana na ukiukwaji huo, Kilaba amesema, “kuanzia muda wa agizo hili saa 8 mchana leo mpaka mwisho wa siku hii ya leo, Clouds TV wanatakiwa kuahirisha matangazo yote na kutumia muda wote uliobaki kuomba radhi kwa Watanzania wote kwa kukiuka kanuni ya utangazaji kupitia kipindi chao cha Clouds 360." “TCRA imesitisha utoaji wa huduma za utangazaji kwa Clouds TV kuanzia kesho 28 Agosti 2020 hadi 3 Septemba 2020. Yaani hakuna kwenda hewani. Iwapo Clouds TV itashindwa au itakaa au itakaidi uamuzi huu, hatutakuwa na jinsi nyingine, tutachukua hatua zingine za kisheria na kithidhibiti,” amesema Kilaba amesema, maagizo hayo kwa Clouds Tv yanafanyika pia kwa Clouds Redio kwa muda huo huo. “Iwapo Clouds Redio itashindwa, itakaa au kukaidi, basi TCRA itachukua hatua za kisheria kati yao,” amesema Kilaba Mkurugenzi huyo amesema, “kwa kipindi chote cha uchaguzi, tuzingatie sheria na hii ni kwa vyombo vyote vya habari na pia zile za online.” Pia, Kilaba ametumia fursa hiyo kutoa wito kwa watumiaji wa mitandao ya kijamii hususan makundi, “wananchama wa vyama vyote vya siasa kuzingatia matakwa ya kisheria kuhusu masuala ya uchaguzi tunapohusisha mitandao ya mawasiliano."
Katika jitihada za kudhibiti maambukizi ya Covid-19, Rais Uhuru Kenyatta ameongeza muda wa wananchi kutotoka ndani kuanzia saa 3 usiku hadi saa 10 alfajiri kwa siku 30. Akihutubia Taifa kutoka Ikulu, amesema baa zitaendelea kufungwa kwa siku 30 huku akiagiza Wizara ya Afya kukutana na wamiliki ili kupata muongozo sahihi wa kuzifungua. Aidha, Rais Kenyatta ameongeza idadi ya watu wanaoweza kuhudhuria misiba na harusi kutoka 15 iliyokuwepo awali hadi 100.Migahawa itafungwa saa 2 usiku baada ya saa 1 usiku kuanzia kesho. Pia, Rais amezitaka Wizara za michezo na Afya kuandaa miongozo ya pamoja ili kurejesha shughuli za michezo nchini humo. Kama utakumbuka siku mbili zilizopita ndani ya Taifa hilo kulikuwa na taarifa za madarasa ya shule binafsi kwasasa yanatumiwa kufugia kuku kutokana na shule kufungwa mpaka mwezi Januari, 2021. Kenya imerekodi visa 33,016 na vifo 564 huku idadi ya wagonjwa waliopona ikiwa 19,296.
Mahakama imemhukumu kifungo cha maisha jela bila uwezekano wa msamaha Brenton Tarrant(29) aliyeua watu 51 kwenye misikiti miwili nchini humo.mtoto mwenye umri wa miaka 3 alikuwa miongoni mwa waliouawa. Machi mwaka jana, waumini waliokuwa wanasali katika msikiti wa Al Noor na Linwood walishambuliwa na Tarrant ambae alirusha tukio hilo mubashara Kupitia mtandao wa facebook. New Zealand haina adhabu ya kifo na Jaji Cameron Mander amesema hukumu hiyo hutolewa kwa wauaji wabaya zaidi,akiongezea kuwa kitendo kilichofanywa na mtuhumiwa hakikuwa na ubinadamu. Hii ni kwa mara ya kwanza kwa hukumu ya aina hiyo kutokewa katika historia ya New Zealand.Mtuhumiwa ambae ni raia wa Australia alikiri kufanya mauaji hayo na kujaribu kuuwa wengine 40.
Mchezaji wa muda mrefu ndani ya klabu ya Valencia, Dani Pajero amejikuta akitokwa na machozi baada ya kupigwa chini na klabu yake ya Valencia, na sasa ataichezea klabu ya Villarreal ambao ni wapinzani wa Valencia. Kiungo huyo wa kati wa Uhispania amecheza Valencia mechi 383 tangu mwaka 2008 alipojiunga na klabu hiyo akitokea Getafe, na mwaka 2011 alikaririwa akisema kuwa ndoto yake ni kuja kustaafu klabuni Hapo, lakini kwa bahati mbaya ameshawekwa pembeni. Itakumbukwa Pajero alifanikiwa kuiongoza Valencia Kwenye ubingwa wao wa kwanza tangu 2008, wakati aliposhinda kikombe cha Copa Del Ray msimu wa 2018 / 2019. Vilevile nchini Hispania klabu ya Atletico Madrid imeondolewa kwenye mashindano ya klabu bingwa Ulaya baada ya kufungwa magoli 2 - 1 dhidi ya RB Leipzig kwenye hatua ya robo fainali na kuifanya klabu hiyo ya Ujerumani kuandika historia ya kuingia nusu fainali kwa mara ya kwanza tangu ilipoanzishwa mwaka 2009. Kocha wa RB Leipzig, Julian Nagelsman nae ameingia kwenye historia ya kuwa kocha wa kwanza mdogo (miaka 33) aliewahi kufika kwenye nusu fainali ya ligi ya mabingwa barani Ulaya.
Sampuli ya vipapatio / mabawa ya kuku yaliyogandishwa, zimegundulika kuwa na virusi vya Corona mjini Shenzhen. Nyama hizo ziliagizwa kutoka nchini Brazil. Baada ya ugunduzi huo, mamlaka za afya ziliwatafuta na kuwapima watu waliokuwa karibu na bidhaa hiyo ambapo majibu yamesema kuwa hawana maambukizi. Aidha eneo ambalo vipande vyenye virusi viliwekwa limepuliziwa dawa na mamlaka inatafuta bidhaa zingine za kampuni hiyo ambayo bado haijawekwa wazi. Hata hivyo shirika la Afya Duniani (WHO) na kituo cha kudhibiti na kuzuia magonjwa Marekani (CDC) zimewahi kusema uwezekano wa kupata Corona ni mdogo kupitia chakula. Taarifa hiyo ya kupatikana kwa Covid-19 kwenye mabawa ya kuku, imekuja huku siku moja tu nyuma yake nchini Ecuador kulipatiana virusi vya Corona kwenye samaki wadogo wa baharini aina ya uduvi wakiwa kwenye moja kati ya migahawa nchini humo kwaajili ya kuuzwa kwa wateja. Mpaka sasa taifa la China limeripoti kuwa na visa 84,786, huku Brazil ikiwa na nchi ya pili kuwa na maambukizi makubwa ya Covid-19, kwa kuwa na visa Milioni 3.1 na taifa la Marekani likiwa linaongoza kwa kuwa na visa Milioni 5.26
Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Linah Sanga (Linah) ameamua kuuvunja ukimya baada ya kusambaa taarifa za kuwepo na mahusiano ya kimapenzi kati yake na mchezaji wa Simba, Benard Morrison. Ule msemo wa "uongo ukiachwa ukasambaa kwa ukubwa zaidi, huwa unageuka ukweli" umejaribu kupingwa vikali na mrembo huyo na kusema kuwa, Yeye na Benard Morrison Ni washkaj tu na wala hakuna mapenzi yoyote yanayoendelea kati yao kama watu wanavyodhani. Linah akaongezea kwa kusema, "yeye ni shabiki yake na mimi ni shabiki yake, tulikutana kwenye mazingira fulani ambayo hata mimi sikutegemea kama ningekuwa hapo, kwani alivyoniona alisema ni mwanamuziki anaefatilia kazi zangu tangu muda mrefu sana, na hata alivyoniita nikaingia hiyo sehemu aliyekuwepo alikua anacheza game na washkaj zake,basi tukapiga picha. Mpenzi wa msasa online kama utakua unakumbuka Msanii Linah mara kadhaa ameshaingia kwenye taarifa za ku'date na watu maarufu, kwa mfano alishawahi kupiga picha za ukaribu na mchekeshaji Idriss Sultan ambapo baadae ikajulikana ilikua ni kutengeneza kiki ya ujio wa wimbo wake wa raha jipe mwenyewe. Benard Morrison hivi karibuni aliingia vichwa vya habari vya nchini Tanzania, baada ya kushinda shauri lake dhidi ya klabu ya Yanga aliyokua anaichezea hapo awali.
Rais wa Iran Hassan Rouhani ametishia kuwepo na madhara iwapo baraza la usalama la umoja wa Mataifa litarefusha marufuku ya silaha dhidi ya Iran kwa shinikizo la Marekani. Rouhani amesema kupitia televisheni ya taifa, kwamba azimio nambari 2231 la umoja wa Mataifa, ambalo ni sehemu ya makubaliano ya nyuklia yaliyofikiwa mjini Vienna mwaka 2015 linahitaji marufuku hiyo iondolewe ifikapo mwezi Oktoba. "Hivi sasa wamarekani wamependekeza azimio dhidi ya sehemu ya azimio nambari 2231 ili kulikiuka. Tuna matumaini makubwa kwamba Marekani itashindwa. Tuna matumaini makubwa tena, kwamba Marekani itagundua kushindwa kwake na kushuhudia kutengwa kwake, amesema Rouhani. Marekani ilijitoa kwenye makubaliano hayo mei 2018,na baadae utawala wa Trump ukaiwekea Iran vikwazo zaidi. Makubaliano hayo yamekabiliwa na kitisho cha kuvunjika, kwa sababu Mataifa yaliyosalia China, Ufaransa, Uingereza, Urusi na Ujerumani, hayawezi kutekeleza sehemu ya kiuchumi ya makubaliano kukiwa na vikwazo vya Marekani,hali iliyoisukuma Terhan pia kuanza kuyakiuka.
Usaliti ni jambo baya sana katika mahusiano, usaliti si ujanja japo wengi wanaowaza kusaliti huwa wanajiona wajanja.wanajiona wamefanikiwa pale ambapo wanasaliti wenza wao kutogundua kama wanasalitiwa. Siku zote anaekusaliti huwa anajiona mjanja sana, kwamba yeye anasaliti mwenza wake hasaliti. Kwa asilimia kubwa wanaume hujiona kama usaliti ni halali yao, wanataka wao wasaliti lakini wapenzi nb wao wasithubutu kuwasaliti. Kwanini hawataki wenza wao wasaliti? eti wanaumia, hakuna kitu kinacho mchukiza mwanaume kama kusalitiwa. kusaliti asaliti yeye akisaliti mwenzake ni kosa la jinai anaona amedhalilishwa Anajisikia fedheha kwamba Mpenzi wake amemuonaje? amemchukuliaje?hajakamilika idara gani? Anawaza sana na kujiuliza jamii nzima inayojua kitendo hicho inamtazamaje?. Hapo ndio unakuta mwanaume anaamua kuchukua uamuzi mgumu ikiwemo hata kuhatarisha maisha ya mwenza wake. Zifuatazo ni dalili za usaliti. 1. KUTOPENDA KUFATILIWA KIUNDANI. Mara nyingi anaekusaliti hapendi kuchimbwa mambo kwa undani, anahofu anaweza kuchanganya madawa, hapendi mazungumzo mafupi ya moja kwa moja. Hapendi kuulizwa maswali mengi, ukimuuliza anayakwepa na kutaka kukupeleka kwenye mazungumzo anayoyataka yeye. Ukimuuliza Kuhusu mipango yenu, ukimuuliza Kuhusu mustakabali wa mahusiano yenu hawezi kukujibu moja kwa moja baada huku ondoa kwenye mstari na kukufanya usiwe na hamu ya kumuuliza. 2. HAPENDI UJUE RATIBA ZAKE. Mara nyingi mtu ambaye ana mambo yake hapendi ujue ratiba zake, anataka usimzoee ,iwe anafanya maamuzi yake kulingana na yeye mwenyewe anavyotaka, ikitokea unaijua ratiba yake atakuwa ni mtu wa kutoa udhuru kila wakati. Leo atakwambia kuna mgonjwa anakwenda kumuona, kesho atakwambia kuna kikao cha wafanyakazi wenzake, siku nyingine atakwambia gari imepata pancha analazimika kusubiri mafundi hadi wafike ndio aweze kuanza safari. 3. SIMU YAKE NI KITUO CHA POLISI. Anayesaliti mara nyingi hapendi kuacha simu yake kiholela, simu inakaa mfuko kwake hata kama hakuna ulazima wa kufanya hivyo mpo nyumbani kwenye kikao cha mazungumzo ya kifamilia yeye simu yake ipo mfukoni. Imetolewa mlio hataki usikie ikiita, au ujumbe ukiingia ,au picha na mambo mengine ya kimapenzi. Anayejiamini na yupo kwenye uhusiano imara hana sababu ya kuficha ficha simu yake au kuweka paswedi kila mahali simu yake anaiweka hadharani. Mwingine anakusetia simu yake ukimpigia kila wakati inaonekana inatumika wakati huo anakusaliti. 4. ANACHATI SANA. Wanaosaliti wengi wao hupenda kutumia meseji katika mawasiliano yao, yaani anawazoesha michepuko yake wote kusaliti hapendi kupokea simu zaidi anapenda kuchati hivyo ni rahisi kuchati na wapenzi wengine bila wewe kujua na kufuta meseji zote ili hata ukishika simu kwa bahati mbaya usizione na usigundue kitu. Mwisho hakutambulishi kwa watu wake wa karibu, ukiona mpenzi wako hajawahi kukutambulisha kwa rafiki zake, ndugu zake na watu wengine wa karibu ujue hapo hamna muelekeo wa mapenzi yenu tafuta njia mapema ya kujiundoa kabla ya kupotezewa muda wako. Kwa haya machache natumaini utakuwa umeshafahamu Mpenzi wako uliyenae kwa sasa ana malengo gani? na je anakusaliti ama ni mwaminifu ili uweze kuchukua hatua mapema kabla mambo hayajaharibika.
1. Uhuru wa kifedha. Uhuru wa kifedha ni zaidi ya kuwa na fedha, uhuru wa kifedha ni kuwa mtu ambaye unatakiwa kuwa maishani na kuweza kufanya au kupata kile unachokihitaji maishani. Hata hivyo pesa ni muhimu sana kwenye suala la uhuru wa kifedha,ingawa pesa hizi zinatakiwa ziambatane na fikra sahihi. Kwa njia ya kujiwekea akiba utaweza kujijengea msingi mzuri wa kifedha ambao ukiambatanishwa na fikra sahihi utakuletea uhuru wa kifedha. 2. Matumizi mazuri ya pesa. Kama nilivyoeleza hapo mwanzo kuwa kuweka akiba sio kuwa na pesa nyingi bali ni maamuzi na mipango stahiki pekee. Hivyo kuweka akiba kutakufaidisha kwa kukuwezesha kutumia pesa vyema.ikiwa unapata elfu 10 kwa siku,itakubidi uitumie vizuri ili uweze kutenga pesa ya akiba. Kama huweki akiba huna haja ya kutumia pesa vyema kwani hakuna sehemu ya akiba inayotakiwa kutengwa. 3. Kujiandaa kwa dharura Watu wengi huingia kwenye madeni au kupata uhitaji mkubwa wa pesa mara wapatwapo na dharura. Hivyo kwa kuweka akiba utapata faida ya kukuepushia mahangaiko wakati wa dharura kama vile magonjwa, misiba majanga n.k 4. Kuweza kufanya manunuzi au miradi ya gharama kubwa Kuna manunuzi au miradi inahitaji pesa nyingi ili kuitekeleza. Maswala kama vile ujenzi wa nyumba, ununuzi wa viwanja kununua gari n.k, ni baadhi ya mambo yanayohitaji fedha nyingi. Hivyo,kwa kuwa na akiba utaweza kutekeleza mambo haya kwa urahisi kuliko ungeyafanya bila akiba. 5. Kuweza kumudu wanaokutegemea Ikiwa kuna watu wanaokutegemea kama vile wazazi, ndugu au watoto ni vyema kuweka akiba ili uwe na fedha ya kukidhi mahitaji yao mara wapatwapo na uhitaji. Kutokuweka akiba kutakufanya uhangaike huku na huko ili kutafuta pesa ya kukidhi mahitaji ya wategemezi wako kama vile chakula, matibabu au hata ada za shule. 6. Utulivu wa akili Unapokuwa huna akiba yoyote huwezi kuwa na utulivu wa akili, Kila wakati unahofu na wasiwasi juu ya maisha yako, unajiuliza likitokea tatizo itakuwaje? au hitaji fulani linalokuja hivi karibuni itakuwaje?n.k Unapokuwa na fungu fulani la akiba huna haja ya kuwa na wasiwasi kwa unajua hata ukikosa pesa akiba yako itakusaidia. 7. Hukuwezesha kuandaa kesho vyema Maandalizi ya kesho yanafanywa leo.kuweka akiba maana yake unajiandaa na mahitaji ya kifedha ya baadaye yaani kesho.mtu asiye kuwa na akiba mara nyingi hafikirii Kuhusu kesho wala hamna malengo kwa ajili ya baadaye yake. Ili kujenga baadae au kesho njema,ni muhimu pia kuimarisha msingi wako wa kiuchumi kwa njia ya kuweka akiba. 8. Hukuwezesha kuwahi fursa Ni mara ngapi umekuwa ukisema au ukisikia kauli kama vile" ningekuwa na pesa ningenunua hiki kitu",au "ningekuwa na pesa ningejiunga kwenye hii huduma" au "ningekuwa na pesa ningejiunga kwenye huu mradi".n.k Hili kinadhihirisha watu hukosa fursa mbalimbali kutokana na kukosa akiba ya pesa,unapokuwa na akiba ya pesa ni rahisi kuwahi fursa mpya au bidhaa zenye manufaa mara zinapopatikana. Hitimisho Fedha ni jambo linalohitaji nidhamu na busara ya hali ya juu, vivyo hivyo kuweka akiba ni swala linalohitaji kufanya maamuzi sahihi ili uweze kulitekeleza.
Mwinyi zahera ametambulishwa rasmi kuwa kocha Mkuu wa klabu ya Gwambina FC ambayo imepanda daraja msimu wa 2019/20 na itashiriki ligi kuu Bara msimu wa 2020/21. Zahera aliwahi kuifundisha yanga ndani ya ligi msimu wa 2018/19 na alianza nayo msimu wa 2019/20 kabla ya kufungashiwa virago kwa kile kilichoelezwa kuwa aliboronga kwenye michuano ya kimataifa. Kocha huyo amesaini dili la miaka 5 na inaelezwa kuwa ataanza kusajili nyota wake ambao alifanya nao kazi ndani ya Yanga. Wanaotajwa kuibukia Gwambina ni pamoja na Mrisho Ngassa na Kelvin Yondani ambao kwa sasa ni wachezaji huru. Vilevile Waziri wa michezo Tanzania, Dkt Harison Mwakyembe ametangaza uamuzi wa serikali kuendelea kuruhusu idadi ya wachezaji 10 wa kigeni huku idadi ya wachezaji wanaotakiwa kucheza itaratibiwa chini ya baraza la Michezo la Taifa BMT. Amesema bado wizara kwa kushirikiana na BMT na wadau wa soka watakaa kikao kujadili aina ama viwango vya wachezaji wanaopaswa kusajiliwa na kuingia nchini. Amefafanua, "Angalau nchi zilizopo katika nafasi 50 kwa FIFA ndiyo tusajili huko hata kwa daraja la kwanza, ingawa bado hii si sheria ni maoni tuu,ni vyema pia aina ya wachezaji watakaosajiliwa kutoka nje wawe na weledi na uwezo mkubwa.
Mamlaka ya Somalia inasema watu 10 wamefariki wakati wa majibizano ya risasi nje ya gereza la Mogadishu. Msemaji wa wizara ya habari alisema mahabusu 6 ambao walikuwa wanamgambo wa kundi la kigaidi Al-Shabab waliuliwa na askari wanne pia waliuawa. Chanzo cha majibizano ya risasi ni jaribio la mahabusu mmoja kutaka kutoroka. Kuna taarifa zinazosema mahabusu mmoja aliweza kupora bunduki kutoka kwa msimamizi wa gereza na baadae mahabusu na wafungwa wengine walivunja chumba cha kuhifadhia bunduki. Kikosi maalumu cha polisi kililelekwa kukabiliana na ghasia hizo ambazo zilikuwa zinalenga kuvunja gereza. Gereza hilo lina wafungwa ambao ni wanamgambo maarufu wa Al-Shabab ambao wanatumikia kifungo cha maisha au kunyongwa.
Mfanyabiashara,Tariq Machibya (29) maarufu kama Mr kuku, amefikishwa mahakama ya kisutu, akikabiliwa na mashtaka 7 likiwemo la kufanya biashara haramu ya upatu kwa kukusanya fedha za umma zaidi ya Tsh. bilioni 17. Machibya amesomewa mashitaka yake tarehe 10.08.2020 na wakili mwandamizi wa Jamhuri, Simon Wankyo mbele ya hakimu Mfawidhi wa mahakama hiyo, Godfrey Isaya. Mbali na shtaka la kusimamia biashara haramu ya upatu,Mr kuku anakabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi pia ana mashtaka ya kupokea maingizo ya fedha kutoka kwa umma bila leseni na kutakatisha fedha. Anatuhumiwa kupokea maingizo ya fedha kutoka kwa umma aliwadanganya kuwa watafanya ujasiriamali wa ufugaji wa kuku na watapata faida ya asilimia 70 kwa waliowekeza kwa miezi 8 na asilimia 90 kwa waliowekeza kwa miezi 6, kiasi kinachoelezwa kuwa kikubwa kuliko mtaji uliokusanywa. Pia kati ya Aprili 26,2019,na Januari 26, 2020 jijini Dar anadaiwa kujihusisha na miamala ya Tsh. Bilioni 6.4 kutoka katika akaunti inayoitwa Mr. kuku pharmacy katika benki ya CRDB huku akijua fedha hizo ni zao tangulizi la biashara haramu ya Upatu. Aidha anadaiwa kupokea fedha kiasi cha Tsh.Bilioni 17 ya maingizo ya umma bila kuwa na leseni. upande wa Mashtaka umesema upelelezi haujakamilika na kesi imeahirishwa hadi Agosti 24,2020 huku mtuhumiwa akirudi rumande kutokana na makosa hayo kutokuwa na dhamana.
Rais wa Afghanistan Ashraf Ghani amesema atatoa amri ya kuachiwa huru kwa wafungwa 400 wa kundi la wanamgambo wa Taliban baada ya baraza la jadi la viongozi wa kikabila kuunga mkono hatua hiyo kama njia ya kufufua mazungumzo ya amani. Akizungumza wakati wa hotuba yake ya kufunga mkutano wa baraza hilo linalojulikana kama 'loya jirga' amesema atatia saini amri hiyo kama ilivyotakiwa na kundi la Taliban na baada ya viongozi hao wa kikabila kufikia mwafaka. Uamuzi huo utaondoa kikwazo cha mwisho kilichotatiza kusonga mbele kwa mazungumzo ya kusaka amani kati ya serikali mjini Kabul na kundi la Taliban. Ghani alilazimika kuitisha kikao cha baraza hilo baada ya kushindwa kutoa idhini ya kuachiwa wafungwa hao 400 ambao wengi wanatuhumiwa kwa makosa makubwa ya jinai ikiwemo kupanga mashambulizi yaliyowaua maelfu ya raia Afghanistan na wageni. Vilevile Serikali ya Afghanistan na kundi la wanamgambo la Taliban wanakaribia kuafikiana kuhusu mazungumzo ya amani baada ya wawakilishi wa makabila kuidhinisha kuachwa huru wafungwa 400 waliokitovu cha mvutano kati ya pande mbili. Azimio hilo limefikia mwishoni mwa mkutano wa siku tatu unaofahamika kama 'loya jirga' unaowakutanisha viongozi wa kikabila na wawakilishi wa makundi mengine, mkutano ambao wakati mwingine huitishwa ili kutafuta majibu ya masuala tata. Mjumbe mmoja wa mkutano huo amesema kwa lengo la kuondoa vizingiti vya kuanza kwa mazungumzo ya amani na kukomesha umwagaji damu, baraza hilo limeridhia kuachiwa huru kwa wafungwa 400 kama kundi la Taliban lilivyotaka. Orodha ya wafungwa hao inajumuisha wale wanaotuhumiwa kwa makosa makubwa ya jinai ikiwemo kushiriki kwenye mashambulizi yaliyowaua maelfu ya raia wa Afghanistan na wageni.
Tarehe 09, Agosti, Malawi imetangaza kuyafunga makanisa yote na kumbi za starehe katika awamu mpya ya vizuizi vya kudhibiti ongezeko linalotia wasiwasi la Virusi vya Corona. Vizuizi vipya vilivyotangazwa Kupitia gazeti la serikali vinajumuisha pia amri ya kuvaa barakoa na marufuku kwa Mikusanyiko inayozidi watu 10 isipokuwa kwa shughuli za mazishi zitakazo ruhusu jumla ya watu 50. Mwanasheria Mkuu wa serikali Chikosa Silungwe, amesema kikosi maalumu cha maafisa wa jeshi kimeundwa kuhakikisha Masharti hayo mapya yanatekelezwa. Malawi haijatekeleza marufuku kamili ya shughuli za umma baada ya mahakama kuzuia mwezi Aprili nia ya serikali ya kuifunga nchi nzima kwasababu ilishindwa kutangaza msaada utakaotolewa kwa watu wasiojiweza. Tangu taifa hilo la Kusini mwa Afrika lililotangaza kisa cha kwanza cha Covid-19 mnamo Aprili 2, idadi ya maambukizi imepanda maradufu katika kipindi cha wiki nne zilizopita na kufikia visa 4,624 ikiwemo vifo 143.
Washindi wa soka la FA Arsenal wana mlenga beki wa kati wa Brazil Diego Carlos huku Mikel Arteta akipanga marekebisho makubwa msimu ujao.(Telegraph - Subscription required). Arsenal itatoa ofa kwa mshambuliaji wa Gabon Pierre -Emerick Aubameyang,31,wiki hii ya pauni milioni 250,000 kwa wiki katika makubaliano ya miaka mitatu kuendelea kusalia kwenye klabu hiyo.(mirror) Hata hivyo, Aubameyang anataka Arsenal kutia saini makubaliano ya hali ya juu kabla ya kukubali mkataba mpya baada ya kuhakikishia klabu hiyo taji ya 14 la kombe la FA. (Le10 sport,via Metro). Aston Villa inamlenga mshambuliaji wa Liverpool,25,raia wa Ubelgiji Divock Origi.(Sun). Maelezo ya picha Troy Deeney alifunga bao lake la 10 katika ligi ya premier msimu huu katika mechi dhidi ya Arsenal Kocha wa Tottenham Jose Mourinho amepewa fursa ya kumsajili mshambuliaji wa Watford Troy Deeney,32, kuchukua nafasi ya Harry Kane kwa muda.(Mail) Liverpool imeitangulia Paris St-Germain katika kinyang'anyiro cha kutaka kumsajili Thiago Alcantara wa Bayern Munich na sasa hivi ina uwezekano mkubwa wa kumsajili kiungo wa kati wa Uhispania.(Mundo Deportivo,via talkSPORT) Mtendaji mkuu wa Manchester United Ed Woodward amefanya mazungumzo na wawakilishi wa mchezaji wa Lille Gabriel Magalhaes juu ya uhamisho wa mlinzi huyo wa Vrazil,22.(RMC sport, via Express) Wakati huohuo United ina matumaini ya kumtumia mlinzi Chris Smalling,30, katika makubaliano ya mabadilishano na mlinzi wa Inter Milan,25, raia wa Slovakia Milan Skriniar - lakini Roma inaendelea na mchakato wake wa kumtafuta mwingereza baada ya kuiridhisha timu hiyo alipokuwa kwa mkopo.(Star) Mabingwa wa Italia AC Milan na Napoli inafanya mazungumzo na mlinzi wa Uingereza wa timu ya Norwich city,Ben Godfrey,22, baada ya Canaries kushushwa daraja kwenye ligi ya premier. (Calciomercato,via Mail)
Mkuu wa zamani wa kanisa katoliki, Papa Benedict XVl,ameripotiwa kuumwa sana baada ya kumtembelea kaka yake aliyekuwa mgonjwa nchini Ujerumani na sasa hali yake ni dhaifu sana. Gazeti la Pasaauer Neue presse la nchini Ujerumani limeripoti kwamba Papa Benedict Mwenye umri wa miaka 93 anasumbuliwa na Ugonjwa unaotokana na kirusi kinachosababisha pelepele usoni na maumivu makali, kwa muujibu wa mwandishi wa tawasifu ya Papa huyo , Peter Seewald. Kwa muujibu wa Seewald,"Papa kwa sasa ana hali dhaifu sana" limeandika gazeti hilo ."Akili na uwezo wake wa kufikiri bado viko makini lakini sauti yake inasikika kwa shida sana. Seewald alimtembelea Papa Benedict mjini Rome siku ya Jumamosi Agosti 01 kumkabidhi tawasifu yake. "Kwenye mkutano huo licha ya kuumwa kwake, Papa alikuwa na matumaini na kusema kwamba endapo hali yake itaimarika, atachukua kalamu tena aandike," limeandika gazeti hilo. Papa Benedict alimtembelea kaka yake aliyekuwa mgonjwa aitwaye Georg nchini Ujerumani mwezi Juni,ikiwa ziara yake ya kwanza nje ya Italia tangu alipojiuzulu ghafla upapa mwaka 2013. Georg Ratzinger alifariki dunia wiki mbili tu baada ya hapo akiwa na umri wa miaka 96. Papa huyo wa zamani, ambaye jina lake halisi ni Joseph Ratzinger,sasa anaishi kwenye nyumba ndogo ya watawa mjini Vatican. Tangu awe Papa wa kwanza kujiuzulu kwa takribani miaka 600 iliyopita,amekuwa haonekani sana hadharani kutokana na hali yake ya kiafya. Akiwa mwanamapokea ya kanisa katoliki, nafasi yake ilichukuliwa na mwanamgeuzi Papa Francis.
Katika harakati zako za kutafuta mpenzi, unaweza kukutana na mwanamke ambaye kwasababu moja ama nyingine anakuondolea uwezo wako wa kufikiri, kutumia mantiki na pia kutumia akili yako ya kuzaliwa.si lazima awe amekufanyia kitu, lakini inaweza kuwa ni ulevi wako tu unasababisha ufanye mambo yasiyo ya kawaida.pengine ndio maana baadhi ya wasanii huzungumzia suala la "kudata" kutokana na mapenzi. Ni jambo jema kudhani kuwa wewe na mpenzi wako mnapendana kwa dhati na kwamba kila mmoja amefika kwa mwenzake, lakini kama moja wapo ya mambo haya yaliyoelezwa hapa chini litajitokeza basi fahamu kuwa yamkini unependa kuliko kawaida, yaani ni kama umenyweshwa sumu ya penzi.kumbuka kupenda ni kuzuri, lakini kupenda kupindukia kunaweza kukutumbukia nyongo kwani katika kila jambo kunahitajika kiasi. Yafuatayo ndio mambo ambayo ni sumu katika mahusiano ya kimapenzi Kumuingilia mpenzi wako katika mambo yake Unaweza kujikuta ukisumwa kumwambia mpenzi wako awe anavaa nini kwa wakati gani, akutane na nani kwa wakati gani au ale nini.ukiona fahamu kuwa hayo si mapenzi, bali umepitiliza na pengine mwisho wa uhusiano wenu unanukia. Hata ukiachilia mbali suala zima la usawa wa kijinsia, hakuna mwanamke angependa apangiwe kila kitu kuhusiana na maisha yake, kama ilivyo dokezwa hapo juu kila mtu ana maisha yake na kilichowaunganisha ni mapenzi tu.kama unataka kumpangia kila kitu ni wazi utaishia kuishi pekee yako. Kutompa nafasi mpenzi wako Kama huishi na mpenzi wako ni jambo la kawaida kuwa na hamu ya kumuona mara kwa mara, lakini kumbuka kuwa mpenzi wako naye ana maisha yake na anahitaji nafasi ya kuwa pekee yake kwaajili ya mambo yake binafsi. Hisia za kutaka kuwa na mpenzi wako muda wote zinaweza kudhaniwa kuwa ni za mapenzi ya dhati, ila kwa hakika hiyo siyo ishara njema ya mapenzi ya kudumu. hebu jiulize kama unaweza kuendeleza hali hiyo maisha yako yote. Ni wazi kuwa utachoka, kwahiyo mpe mpenzi wako fursa ya kupumua.namna hii mpenzi wako atajenga hamu ya kukutana nawe lakini ukiwa naye muda wote hamu itaisha. Wivu kupindukia Ni jambo jema kwa mwanamume kumtakia heri mpenzi wake na kufanya kila awezalo kuhakikisha kuwa hapati madhara, lakini iwapo utakuwa mtu wa wasiwasi na mashaka pale unapomuona mpenzi wako akizungumza na mwanaume mwingine,au anapotoka na marafiki zake wa kike,au anapovaa nguo inayomfanya atamanishe, basi fahamu kuwa unakunywa sumu ya mapenzi. Katika uhusiano wa kimapenzi, kuaminiana ni jambo muhimu sana.kama kweli unataka Mpenzi yako akupende kwa dhati,mwonyeshe kuwa unamwamini na unaheshimu maamuzi yake ikiwa ni pamoja na maamuzi ya kutoka na marafiki zake wa kike na kuwa na marafiki wa kawaida wa kiume. Ondoa hofu na acha kabisa kumpeleleza, maana wapo wanaume ambao hutumia muda mwingi kuwapeleleza wapenzi wao ikiwa ni pamoja na kuwategeshea kamera na rekoda za simu. Kama ukizingatia mambo haya machache katika mahusiano yako ya kimapenzi na kama kweli mnapendana na mnamalengo ya kufika mbali na mahusiano yenu basi zingatia haya na utayafurahia mahusiano yenu na yatakuwa mfano wa kuigwa na watu wengine.
Mahakama ya Somalia imemuhukumu mwandishi wa habari maarufu nchini humo, Abdiaziz Ahmed Gurbiye kifungo cha miezi 6. Abdiaziz ambae ni mhariri mkuu na naibu mkurugenzi wa shirika binafsi la Goobjoog, mjini Mogadishu, alishtakiwa kwa kuikosoa Serikali ya Somalia katika kukabiliana na mlipuko wa Corona. Mahakama ya mjini Banadir ilimtaka kutoa faini ya shilingi milioni 5 za Somalia (208.3 USD) kwa kuchapisha taarifa za kizushi na kuitusi Serikali na mahakama, muda mfupi baada ya kuhamishiwa katika Gereza la Mogadishu. Wakili wake anasema Mahakama ilitumia sheria iliyopitwa wakati wa kutoa hukumu hiyo. Kesi ya Gurbiye imekua ikiendelea kwa miezi kadhaa, ilikua ni miongoni mwa kesi kubwa dhidi ya waandishi nchini Somalia katika miaka ya hivi karibuni.
Rais wa Rwanda Paul Kagame ametangaza siku 3 za maombolezo kuanzia July 27 - 29, 2020 kufuatia kifo cha aliekuwa Rais wa Tanzania, Benjamin William Mkapa. Kagame ambae pia ni mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika mashariki (EAC) amemzungumzia Hayati Benjamin kama kiongozi ambae mchango wake ulienda nje ya mipaka ya Tanzania. Vilevile Serikali ya Burundi imetangaza siku 3 za maombolezo kutokana na kifo cha Benjamin William Mkapa. Waziri mkuu wa Burundi, Alain Guillaume Bunyoni atakaeiwakilisha nchi yake katika msiba huo, ameshawasili jana nchini Tanzania na kupokelewa na mkuu wa mkoa wa Kigoma, CP Thobias Andengenye katika mpaka wa Manyovu. Rwanda na Burundi zinaungana na Watanzania kuomboleza kifo hicho na bendera za nchi hizo pamoja na ile ya Jumuiya ya Afrika mashariki (EAC) zitapepea nusu mlingoti.
Viongozi wa Mataifa ya Afrika magharibi wamemaliza siku nzima wa mkutano wa kilele hapo tarehe 24, Julai bila ya kufukia makubaliano juu ya mgogoro wa kisiasa unaotokota nchini Mali. Viongozi watano wa Mataifa ya Afrika magharibi wamekutana na Rais wa Mali Ibrahim Boubacar Keita, pamoja na viongozi wa vuguvugu la maandamo wanaomtaka ajiuzulu. Hata hivyo, upatanishi ilishindikana,na Rais wa Niger Mahamadou Issoufou pamoja na wenzake wa Senegal,Ivory Coast, Ghana, Nigeria wamesema jumuiya ya uchumi wa Mataifa ya Afrika magharibi, ECOWAS itaitisha mkutano mwingine wa kilele Jumatatu. Vuguvugu la Juni 5 lililopewa jina la siku yalipoanza maandamo hayo,linamtaka Keita aondoke madarakani kwa kushindwa kushughulikia uliyoporomoka nchini humo ufisadi pamoja na uasi wa miaka minne wa makundi ya kijihadi.
Wizara ya mambo ya nje ya China,imeiamuru Marekani kufunga jengo lake la kidiplomasia lililopo Chengdu China, Uamuzi umekuja baada ya Marekani kufunga ofisi ya kidiplomasia ya China iliyopo Texas, Marekani. Kufungiana ofisi za kidiplomasia linaonekana kuwa suala linalozidi kuleta utengano kwa Mataifa hayo ambayo awali yalianza kwa kuwekeana vikwazo katika upatikanaji wa VISA,na kuongeza sheria kwa wanaosafiri kidiplomasia. Awali, Marekani ililaumu ofisi za China wanasaidia wizi wa kijeshi unaoiba tafiti za wamarekani.pia, walilaumu watu wa ofisi hizo kutumia majina yasiyo halisi katika kufanikisha suala la kuiba taarifa za kiintelijensia. Maafisa wa China wanasema utawala wa Rais Trump unaonyesha chuki ya wazi kwa wachina na wamelaumu Pompeo kwa kuendeleza itikadi ya vita baridi. Vile vile China imemkosoa waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani Mike Pompeo, akimtuhumu kusambaza uongo wa kisiasa kuhusu China. Pompeo aliishutumu China kwa kuendesha kambi ya watu wengi katika jimbo la magharibi la Xinjiang, na wizi wa taarifa za kitaaluma na siri za kibiashara. Wang aliwashutumu wanasiasa wa sasa wa Marekani kwa kuchochea makusudi kile alichokiita "Mabishano ya kiitikadi" kati ya nchi hizo mbili, ili kubadili mkondo wa mtazamo wa raia wa Marekani.
Idadi ya watu wanaotafuta hifadhi nchini Ujerumani kutokutoka na vita ama mateso katika nchi zao iliongezeka kupita milioni 1.8 mwishoni mwa mwaka jana kulingana na takwimu rasmi zilizotolewa tarehe 23, Julai. Idara ya takwimu ya serikali kuu (Destatis) imesema kuwa nb idadi hiyo iliongezeka kwa kiwango cha chini cha kila mwaka kutoka asilimia 3 mnamo mwaka 2012, idadi hiyo ilijumuisha raia wa kigeni ambao walikuja nchini Ujerumani kwasababu za kisheria, kisiasa ama kibinadamu. Mnamo Desemba 31, takribani watu 266000 miongoni mwa waomba hifadhi hao walikuwa bado wanasubiri uamuzi wa mwisho wa maombi yao ya kutafuta hifadhi, idara hiyo ya (Destatis) imeripoti kuwa kiwango hicho ni asilimia 13 chini ya kile kilichoshuhudiwa wakati sawa na huo wa mwaka jana. Hii inahusishwa na ufanisi uliopatikana katika kazi iliyoko pamoja na kupunguzwa kwa ujumla wa kiwango cha maombi ya kutafuta hifadhi.
Miili ya watu 7 imegunduliwa katika kaburi moja katika mji uliokuwa umetekwa na waasi Libya. Miili ya watu 7 ambao wanakisiwa kuwa raia imegunduliwa katika mji wa Terhune, mji ambao ulikuwa umetekwa na waasi nchini Libya. Mji huo ulikombolewa mnamo June 5 baada ya makubaliano makali kati ya jeshi la serikali inayotambulika na jumuiya ya kimataifa na wapiganaji wa jenerali Khalifa Haftar. Kiongozi wa jopo lililoandaliwa kwa ajili ya kufanya uchunguzi kuhusu mauaji katika maeneo yaliyokuwa yametekwa na waasi Libya Kemal es Seyewi amefahamisha kuwa katika hatua iliyopigwa hadi kufikia sasa ni miili ya watu 7 ndio iliyogunduliwa katika kaburi la pamoja. Miili hiyo imepelekwa katika hospitali moja uhifadhiwe na kuzikwa kwa heshima. Kulingana na taarifa zilizotolewa na serikali hiyo inayotambulika na jumuiya ya kimataifa, Terhune kuna zaidi ya makaburi 11 ya pamoja. Wapiganaji wa Haftar waliondoka katika eneo hilo baada ya kuzidiwa na mashambulizi yaliyoendeshwa kwa ushirikiano wa jeshi la Uturuki.
Jaji mkuu wa Iran Ebrahim Rais amefifisha matumaini kwamba adhabu ya kifo iliyotolewa kwa waandamanaji watatu vijana wa kiiran itafutwa kufuatia malalamiko ya mitandaoni. Jaji mkuu huyo amesema maandamano yanakubalika lakini machafuko na fujo vinavyohatarisha usalama wa taifa ni mstari mwekundu. Ameongeza katika matamshi yaliyochapishwa na shirika la habari Isna, kwamba katika matukio kama hayo mahakama haiwezi kushawishiwa na kampeni na propaganda. Chini ya hashtag ya kupinga hukumu hiyo ya No ToExecution, mamillioni ya raia wa Iran wametumia Mitandao ya kijamii kupinga hukumu baada ya mahakama ya juu kuthibitisha adhabu ya kifo iliyotolewa dhidi ya Amirhossein M, Mohammad R, na Saeed T. Msemaji wa wizara ya sheria ya Iran Gholam Hussein Ismail amesema wanaume hao waliongoza magenge ya vurugu na walijirekodi video wakichoma moto majengo kadha na miundombinu ya usafiri wakati wa maandamano ya Novemba, mwaka 2019. Novemba mwaka jana,Iran ilitikiswa na maandamano ya siku kadhaa yaliyochochewa na kupanda kwa bei ya mafuta. Hata hivyo, maandamano hayo yalizimwa na vikosi vya usalama.
Shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch,limedai kuwa kuna Utamaduni wa udhalilishaji wa kimwili wa kimaneno unaowalenga wanariadha vijana nchini Japan,Ikiwa imesalia mwaka mmoja kuelekea mashindano ya michezo ya olimpiki ya dunia yanayopangwa kufanyika mjini Tokyo. Shirika hilo limesema lilifanya mahojiano zaidi ya 50 na wanariadha watoto wa sasa na wa zamani kwa ngazi tofauti za mashindano, utafiti wa mtandaoni na mashirika ya michezo. Waligundua kuwa watoto nchini Japan,bado wanapitia udhalilishaji michezoni na limeainisha maswala ya kitaasisi ambayo yanayofanya uitikiaji wa taifa hilo kwa matukio kama hayo kukosa ufanisi. Shirika la michezo la Japan limesema linafahamu Kuhusu ripoti hiyo na kuongezea kuwa limechukua hatua kuondoa udhalilishaji kwenye michezo, ikiwa ni pamoja na kuunda Mtaala wa mafunzo au kutengeneza miongozo kwa mashule.
1. Inachangia kufahamika zaidi kwa biashara yako. Mitandao ya kijamii ni moja ya njia za kutangaza biashara yako kwa gharama nafuu zaidi na inauhakika wa kuwafikia wateja wengi zaidi, kwani asilimia kubwa ya watu wengi sasa hivi wanatumia muda mwingi sana katika mitandao ya kijamii hivyo kutangaza biashara yako kutakuongezea idadi ya wateja na watu wenye ufahamu wa kutosha kuhusu biashara yako kwa ujumla. 2. Inapanua wigo wa kupata wateja wapya tofauti na wale wanaokuzunguka. Kutumia mitandao ya kijamii kwa ajili ya kutangaza biashara yako kuna kuongezea wigo wa wateja wapya ambao ni vigumu kufahamu kuhusu biashara yako kwani wako mbali na eneo la biashara husika lakini Mitandaoni ya kijamii inakupatia nafasi ya watu wote watakao Kutana na tangazo la biashara yako kuifahamu na kushawishika kutumia bidhaa zako na hivyo kugeuka wateja wa biashara yako. 3. Inajenga uhusiano wa karibu na wateja wako. Kupitia ukaribu unaojengeka baina ya biashara yako na wateja wako hii inasaidia kuweka ukaribu wa kusikiliza maoni, shida na kutafuta ufumbuzi kiurahisi wa kero za wateja wako kwani kwa urahisi kabisa wanaweza kuwasilisha maoni yao kupitia akaunti za biashara yako za mitandao ya kijamii. 4. Inaongeza imani na uaminifu wa watu kwenye biashara yako. Moja ya malengo ya kila biashara ni kutengeneza wateja waaminifu na wakudumu wa bidhaa za biashara hiyo, hivyo Mitandaoni ya kijamii kupitia ukaribu unaojengeka baina ya biashara na wateja wake na urahisi wa taarifa za biashara yako kumfikia mteja inapeleka kutengeneza wateja waaminifu na wakudumu wa biashara yako. 5. Inasaidia kupunguza gharama za uendeshaji wa biashara yako. Biashara nyingi hutumia fedha nyingi kwaajili ya kujitangaza na hili huonekana pale ambapo njia zinazotumika kutangaza biashara husika zinakuwa ni ghali sana na hivyo kuongeza gharama za uendeshaji wa biashara husika. Kupitia matumizi ya mitandao ya kijamii kama njia ya kujitangaza inapunguza gharama hizo na kujitangaza na kupelekea kupunguza gharama za uendeshaji wa biashara na kuipatia nafasi nzuri ya kifedha zaidi. 6. Inaongeza ufahamu wa kutosha dhidi ya soko husika na wateja wako. Kupitia ukaribu unaojengeka wateja wako katika mitandao ya kijamii na kujibu comments za wateja wako katika mitandao ya kijamii hii inapelekea biashara husika kupata taarifa za kutosha za soko husika na kuipa nafasi biashara kuwa na taarifa za kutosha za wateja wake na hii inasaidia biashara Kufanya maamuzi na kuweka mikakati inayohitajika kwa wakati husika na soko husika. Hizo ni baadhi ya faida za kuitumia mitandao ya kijamii kuitangaza biashara yako na kama bado haujaanza kutumia mitandao ya kijamii ni vyema ukaanza sasa kwani unapitwa na mengi ambayo biashara yako ingenufaika kwa kutumia mitandao ya kijamii. Asilimia 90 ya wataalamu wa masoko wanakiri kuwa Mitandaoni ya kijamii ina nguvu sana katika kutangaza biashara na imekuwa ikionyesha matokeo chanya katika biashara zao.baadhi ya mitandao ya kijamii inayotumika sana katika matangazo ya biashara ni kama Facebook, Instagram, Twitter, Blogs, YouTube, LinkedIn,nk.
Naomba pasipo kupoteza wakati nikukaribishe katika somo letu la leo,na siku ya leo tutazungumza kuhusiana na mbinu moja itakayo kusaidia katika ukuaji wa biashara. Moja kati ya changamoto kubwa kubwa ya ufanyaji wa biashara ni kule kufanya kazi kwa mazoea, nasema hivi kwasababu wafanyabishara wengi husikika wakisema ya kwamba mteja ni mfalme, lakini katika hili kumekuwa na ukakasi ni wateja wachache sana ambao huona ufalme huo. Hii ni kwasababu wafanyabishara wachache sana ambao wamekuwa wakijua ni nini maana ya mteja. Wafanyabishara wengi wamekuwa wakimchukulia mteja pale anapokuja kwenye biashara ambayo anafanya tu.kufanya hivi kutakufanyanya kuiona ramani ya biashara haina usawa kwani biashara utazidi kuiona ni ngumu siku zote. Hivyo ili uweze kumfanya mteja wako awe mfalme unatakiwa kufanya mambo yafuatayo; 1. Acha mara moja kumsubiri mteja wako aje kukufuata mfanyabiashara mahali ulipo, bali anza utaratibu wa kumfuata mteja wako mahali alipo, Kufanya hivyo kutamfanya mteja wako ajisikie huru na pia ajihisi kuwa yeye ni mfalme kweli na kufanya hivi kutamjengea utaratibu mpya na pia kujiona yeye si kama tu mteja bali ni sehemu ya biashara yako. 2. Tengeneza utaratibu mpya wa kuwa na mawasiliano ya karibu na mteja wako,si umekuwa ukisema ya kwamba mteja ni mfalme, kama ndivyo hivyo basi hakikisha ya kwamba unakuwa na mawasiliano na wateja, Mawasiliano hayo basi naomba yawe ni kwaajili ya biashara tuu na si vinginevyo na kama ukiyatumia mawasilaino hayo vibaya basi jiandae kuwapoteza wateja wako wote, Mawasiliano hayo yanatumika kuwajuza wateja wako kuhusu ujio wa bidhaa mpya na mambo mengine muhimu kuhusu biashara tu. 3. Jifunze mbinu mpya ya kuweza kufanya mazungumzo na wateja, hivi hujawahi enda katika biashara ya mtu mwingine mpaka ukajuta kwanini ulienda mahali hapo, bila shaka kama hali hii imewahi kukutokea basi ni vyema katika biashara yako uweze kujenga utaratibu mpya ambao utakufanya wateja wako wajisikie huru kila wakija kwako. 4. Uchawi mkubwa ambao unafanyika katika biashara ni kutoa ofa kwa wateja wako. Hii siri ambayo nakuibia wewe siku ya leo, haijalishi ni biashara gani ambayo unaifanya ila ili uweze kukua katika biashara hiyo ni vyema ukajiwekea utaratibu wa kutoa ofa kama yafanyavyo makampuni ya simu Kufanya hivyo kutawafanya wateja wengi waje kwako. Asante sana kwa kusoma makala haya, mpaka kufikia hapo sina la ziada nikutakie kazi njema na siku njema.
Wakati taifa la Tanzania likiwa kwenye maandalizi ya uchaguzi mkuu mwezi Oktoba mwaka huu 2020, huku ikishuhudiwa muamko mkubwa wa wasanii na watu maarufu wakijitokeza kuchukua fomu kwaajili ya kuhitaji ridhaa ya kugombea nafasi mbalimbali. Nchini Marekani msanii Kanye West amejitoa kwenye mbio hizo za kugombea nafasi ya Urais. Rapa Kanye West alitangaza azma yake ya kugombea nafasi ya Urais kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka huu ndani ya Marekani, huku akiwa anajaribu kushindana na Donald Trump ambae alikua ni rafiki yake kwenye harakati za kumsaidia kumfanyia kampeni wakati anataka kuingia White House. Taarifa za Kanye West kujiondoa kwenye mbio hizo zimetolewa na watu wa karibu sana ambao walikuwa kwenye kamati yake ya kampeni. Taarifa zinasema timu ya Kanye West tayari ilikuwa imeshaingia kwenye majimbo ya Florida na Carolina Kwaajili ya kuanza kuwaandaa baadhi ya wanahabari ili kujitengenezea mazingira mazuri kwenye kampeni yao, jambo ambalo lilihitaji mawakili wengi kushiriki na kuliunga mkono. Kwenye taarifa hiyo, wanasema watu wengi walijitokeza kumuunga mkono rapa Kanye West na kusaini, namba ilikua kubwa mpaka ikatuzidi huku watu wengi waliamua sio tu kusimamia mikataba yao lakini walijitolea pia. Lakini baadae kidogo baada ya chanzo hicho kuulizwa kuhusu maendeleo ya timu ya kampeni ya Kanye, Jibu lilikua ni "Amejitoa" Pindi alipoulizwa zaidi kuhusu mwisho wa mbio za kugombea urais za Kanye West akajibu "Nitawafahamisha ninachojua mara moja"
Uingereza imepiga marufuku Kampuni ya Huawei kuweka mitambo ya 5G huku kampuni kama BT (BTGOF) na Vodafone (VOD) zikipewa muda mpaka 2027 kuondoa mitambo ya kampuni hiyo kwenye mitandao yao. Waziri wa masuala ya kidigitali na Utamaduni, Oliver Dowden amesema kutokana na hali ya sintofahamu inayozunguka Kampuni hiyo ya china, Uingereza imekosa imani na mitambo ya 5G ya Huawei. Marufuku iliyotolewa na Uingereza ni ushindi mkubwa kwa Marekani ambayo imekua ikishinikiza Mataifa kupiga marufuku Kampuni hiyo kwa madai kuwa ni tishio kwa usalama wa taifa. Uamuzi wa Uingereza umetejwa kuwa ni pigo kubwa sana kwa kampuni ya Huawei kwani soko muhimu kwa kampuni hiyo na 24% ya mauzo ya mwaka jana yalitokea huko. Vilevile Kampuni hiyo ya kichina ambayo imeanza kuzalisha bidhaa za mawasiliano tangu mwaka 1997 bado inaendelea kufanya vizuri sokoni kwa kuleta bidhaa mpya za simu na tablets.
Hayo yameelezwa na mwanamuziki Diamond Platinumz Wakati lebo ya WCB ikizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam Kuhusu usiku wa Zuchu utakaokuwa Julai 18 mwaka huu mlimani city jijini Dar es salaam. "Sijui kama nilitakiwa kusema hili au la, lakini bosi wangu Sallam atakuwa balozi wa Universal Music Group east Afrika (Afrika mashariki),na tunaamini kupitia yeye ataboresha zaidi", ametangaza Diamond. Mwanamuziki huyo amesema hayo wakati akijibu swali la mwandishi wa habari aliyetaka kufahamu uzoefu alioupata kwa kufanya kazi na kampuni hiyo kwa miaka minne, na nini kinasababisha wasanii wengine kuilalamikia Kampuni hiyo. Akijibu amesema kuwa amejifunza mengi na kwa kiasi fulani amefanikiwa japo baadhi ya mambo hayakwenda kama alivyotarajia. Ameongezea kuwa uzoefu alioupata utamsaidia endapo ataingia mkataba tena na kampuni hiyo au kama msanii yeyote kutoka WCB ataingia mkataba,kwa sasa ataweza kuwashauri. Aidha amewashauri wasanii wenzake kwanza wajijengee mizizi ndani ya nchi kabla ya kufanya kazi na kampuni za nje kwani hizo hazina kujuana na pia wawe makini katika mikataba wanayoingia ili wasije wakaishia kupata hasara.
Ule msemo wa wapendanao wakigombana chukua jembe ukalime, umeonekana kudhihirika baada ya Princess Love ambae ni mke wa msanii Ray J, kuamua kurudi mahakamani kusitisha kesi yake ya kudai talaka kutoka kwa mumewe. Princess Love alifungua file la kudai talaka mwanzoni mwa May, 2020 Baada ya kuwa Kwenye mahusiano ya ndoa na Ray J kwa kipindi cha miaka 4, huku wakifanikiwa kupata watoto wawili (Melody love & Epik Ray). Wawili hao wamekuwa hawaishi pamoja kwa muda wa mwaka mmoja sasa, huku sababu kubwa iliyopelekea kuachana ni kutokana na Ray J kusemekana kumuacha Princess Las Vegas wakati alipokuwa na ujauzito wa miezi 8 wa mtoto wao wa pili, Lakini ingawaje mpaka sasa bado haijafahamika sababu kubwa iliyopelekea Princess kusitisha kudai talaka. Kutokana na kurudi tena kwa mahusiano hayo, watu wa karibu wanadai kuwa hivi sasa wawili hao wamefanya hivyo ili kulea watoto wao ambao bado ni wadogo na wanahitaji malezi toka kwa wazazi. Kwenye moja ya mahojiano aliyofanya, Ray J amesema " Nina furaha sana kurudi tena kuishi pamoja na watoto wangu, tena ukizingatia wiki ijayo ni sherehe ya kuzaliwa ya mmoja kati ya watoto wangu, kwa kipindi chote cha Lockdown Nimekua nikijifungia studio tu. Ray J akaongezea kwa kusema, "mke wangu ni mama bora sana kwa watoto wake kwani naamini kila analofanya huwa na sababu.
.Habari rafiki mpendwa, natumaini unaendelea vizuri na mapambano ya maisha.Nikutie tu moyo endelea na harakati hizo naamini ipo siku utayaona matunda ya unachokifanya.Kama kawaida leo nakuletea makala nyingine hii ni juu ya sifa za mjasiriamali. Kuna watu wengi sana wanajiita wajasiriamali lakini kiuhalisia si wajasiriamali.Hii imenifanya nifikirie juu ya hili. Zifuatazo ni sifa za mjasiriamali na kama huna sifa kati ya hizi basi hujawa mjasiriamali wa ukweli bali utakuwa unabip tu. sifa zenyewe ni kama zifuatazo, 1. AWE NA MALENGO Hii ni sifa kubwa ambayo mjasiriamali anatakiwa kuwa nayo, kwanza lazima uwe na malengo uliyojiwekea kwamba unataka kufikia wapi katika biashara yako.kama ni kuwa na pesa nyingi sema unataka kiasi gani kabla ya mwaka kuisha.kwa mfano; nataka kabla ya mwaka 2016 kuisha niwe nimetengeneza Milioni 20.Hii itakufanya ufanye kazi kwa bidii ili ufikie malengo hayo. 2. AWE NI MTU ASIYE KATA TAMAA. Mjasiriamali yoyote duniani ni mtu ambaye si rahisi sana kukata tamaa katika kazi zake, watu wengi sana wamekuwa na malengo makubwa lakini wanashindwa kuyafikia kwasababu wanakata tamaa mapema sana,hii huwafanya warudi nyuma.Mfano mtu aliyeajiriwa anakuwa na malengo ya kujiajiri, anaanzisha biashara asipopata faida kama alivyotarajia hukata tamaa na kutamani tena kuajiriwa na hatimaye kutafuta ajira tena.Nikutie moyo tu hakuna kitu kinachokuja kwa urahisi kama unavyofikiria,kaza buti songa mbele changamoto ni chachu ya mafanikio. 3. AWE NI MTU WA KUJIAMINI. Siku zote anayejiamini ndio hupata mafanikio kwa urahisi, watu wengi wamekuwa wakishindwa katika biashara zao kwa kushindwa kujiamini.Kumbuka hiyo ni biashara yako acha kuangalia watu wanasema nini wewe endelea tu na harakati zako ipo siku hao wanaokubeza watakusifia kwa unachokifanya. 4. KUJALI MUDA WAKO. Muda ni kitu kidogo sana lakini muhimu kuliko kitu chochote, mbaya zaidi dakika moja au hata sekunde moja kupita hatokutana nayo tena katika mzunguko wa maisha yako yote.Kwahiyo kama umekuwa na malengo ya kufanya kitu fulani basi fanya haraka iwezekanavyo, ukizidi kuchelewa unaendelea kuweka matatizo na vikwazo katika kazi yako au hata biashara yako kuna msemo unasema"muda ni mali" au "time is money". Misemo hii imefananisha muda ni pesa, kwasababu pesa ni kitu muhimu lakini utapata pesa kwa kutumia muda vizuri.Acha kuahirisha mambo mara kwa mara fanya maamuzi sasa, kesho kamwe haitafika. 5. AWE NA KAULI NZURI, TABASAMU NA NADHIFU. Hii ni nguzo muhimu sana kwa mjasiriamali, unapokuwa na kauli nzuri na mwenye tabasamu na nadhifu, unapokuwa unatoa huduma utawavutia wateja wengi zaidi na kama utakuwa na kauli mbaya na mchafu wateja watakimbia na mwisho wa siku unaanza kufikiria umelogwa kumbe wewe ndiye mchawi namba moja wa biashara yako. Zingatia hilo na utaona utakavyopata wateja kuliko kawaida.
Zifuatazo ndizo hatua tano jinsi ya kuwa mfanyabiashara mwenye mafanikio. 1. Ainisha aina za biashara ambazo unataka kuzifanya. katika hili ni kwamba kama unataka kuwa mfanyabiashara mwenye mafanikio, unatakiwa kuainisha aina mbalimbali za biashara ambazo unataka kuzifanya huwenda zikawa ni zaidi ya biashara hata sita.Ukisha pata biashara hizo jaribu kuwashirikisha hata baadhi ya ndugu na jamaa ili wakupe mtazamo wao ni biashara ipi inafaa. 2. Chagua biashara moja ambayo unaona inafaa. Hatua ya pili baada ya kuwashirikisha ndugu na jamaa, unachotakiwa kufanya ni kwamba kaa chini pamoja na halmashauri yako ya kichwa ili kuweza kupambanua ni biashara ipi ambayo inafaa, baada ya kupata majibu tafakari kisha chagua mwenyewe biashara moja ambayo itakuwa na faida kwako hapo mbeleni. 3. Fanya utafiti juu ya washindani wako. Baada ya kupata wazo moja la biashara hatua ya tatu ni kwamba unatakiwa kufanya utafiti wa juu ya washindani wako ambao tayari umewakuta wakifanya biashara.Na katika kufanya utafiti wako unatakiwa kujua ni mbinu zipi ambazo wao huzitumia katika kupata wateja, baada ya kujua hii itakusaidia kujua mbinu mpya ambayo itakufanya uweze kuwavuta baadhi ya wateja ili waje kwako. 4. Tengeneza mpango wa biashara hiyo. Baada ya kujua mbinu za kuwatambua na kuwashinda washindani wako, jambo la nne ni kuhakikisha unaandaa mpango biashara ambao ndiyo utaongoza biashara yako.katika mpango wa biashara ndio ambao utakusaidia kwa kiwango kikubwa kujua biashara yako jinsi ambavyo utakavyokuwa.Nakusihi tuu endelea kufuatana nami afisa mipango kila wakati nitakueleza siku nyingine jinsi ya kuandaa mpango wa biashara. 5. Tafuta mtu atakaye kuongoza na kusimamia katika biashara yako. Mwisho kabisa ili uweze kufanikiwa katika biashara yako unahitaji kuwa na mtu wa kuongoza katika biashara yako, mtu huyo anatakiwa kuwa mzoefu katika biashara ambayo unatakiwa kufanya.Uzoefu w mtu huyo litakuwa darasa tosha kwako na kukuelekeza ni nini ufanye na nini usifanye. Lakini nikuibie siri moja, hatuna siri kubwa katika mafanikio makubwa ya kibiashara kama kuwa mbunifu, ubunifu ndio siri na silaha makini ya utendaji wako wa kibiashara yenye mafanikio.
Mwanamuziki wa bongo na mfanyabiashara Shilole ameibuka tena baada ya siku chache kuposti picha zikimuonyesha ameumizwa na mume wake baada ya kupigwa na mumewe leo ameibuka na kuwashukuru watanzania kwa ushirikiano Kipindi cha matatizo yake. Kupitia ukurasa wake wa instagram Shilole aliandika hivi Salaam ndugu zangu, Nimeona upendo, nimeona heshima na kukubalika kwa kiwango cha pekee katika wakati huu wa changamoto niliyokutana nayo. Nashukuru sana kwa upendo wenu, nashukuru sana wote walionijulia hali na kuniombea dua. Kuhusu maendeleo yangu mimi niko sawa naendelea kupambana.Changamoto ni sehemu ya maisha haziwezi kunifanya nianguke, lakini yote hayo si kwa nguvu zangu ni Mungu pamoja na watanzania wenzangu mnaonitakia mema. Maisha yanaendelea tuendelee kuijenga jamii yetu, jamii inayokataa unyanyasaji wa kijinsia. Kutokana na yaliyomkuta Shilole naamini kabisa bado katika jamii zetu mambo haya yapo na yanawakuta wanawake wengi hasa sehemu za vijijini kutokana na kwamba bado kuna mambo ya unyanyasaji wa kijinsia. Taarifa ya Shilole natumaini itakuwa imewagusa wengi ambao wanakutana na changamoto kama hizi na waweza kuamka na kuzipinga kwa kutoa taarifa sehemu husika ili wanaofanya vitendo hivi vya unyanyasaji wa kijinsia vifike kikomo na tuishi kwa amani katika jamii zetu.
Luteni Jenerali Madeline Swegle amekuwa mwanamke wa kwanza Mmarekani mweusi kuendesha ndege ya kivita inayotumiwa na kikosi cha wanamaji cha Marekani. Ameandika historia kwa kupaa angani kama rubani wa ndege ya kivita ya Marekani inayotumiwa na wanamaji na atatunukiwa cheo cha "wings of Gold" au (mbawa za dhahabu), baadae mwezi huu wa Julai kwa mujibu wa ujumbe wa twitter uliotumwa alhamisi wiki hii na mkuu wa mafunzo ya ndege za kijeshi za majini. Mkuu wa mafunzo ya kijeshi alimsifu Bi Swegle akitumia herufi"BZ" au "Bravo Zulu",neno linalotumiwa na wanajeshi wanamaji linalomaanisha"umefanya vyema". BZ kwa Lt.j.g Madeline Swegle kwa kumaliza Mtaala wa mafunzo ya kimkakati ya kijeshi ya mashambulio ya anga, aliandika mkuu wa mafunzo ya kijeshi ya ndege za kivita za majini.Swegle ni mmarekani mweusi wa kwanza mwanamke anaetambuliwa kuwa rubani wa TACAIR na atapokea mbawa za dhahabu baadae mwezi huu. HOOYAH!", Uliandikwa ujumbe wa mkuu huyo wa mafunzo. Kwa mujibu wa jeshi la majini la Marekani, ambalo limetoa taarifa chache sana kuhusu rubani huyu mpya Swegle kwasasa yuko katika kituo cha mafunzo cha Redhawks squadron (VT) 21 katika kituo cha ndege za vita vya majini-Naval Air station cha kingsville kilichopo Texas.
Diamond na Alikiba pamoja na wasani wengine kutumbwiza pamoja na kwenye jukwa moja hukwo DODOMA
BEKA na mzazi mwenzake kuna wakati ilisemekana wa meachana ila kwa awamuhii imeonekana Beka kumshurikisha kwenye mziki wake mpya kitu ambacho mashabiki hawaelelewi kua wa meridians au vipi?
Inaonekana hii couple ya ZARI na Daimondi kurudiana na siku hizi kama vile kuna kujaliana hadi kununuliana gari na zari kutumia nafasi hiyo kupata attentions toka kwa mashabiki zake.