Podcasts about ikiwa

  • 20PODCASTS
  • 181EPISODES
  • 7mAVG DURATION
  • 5WEEKLY NEW EPISODES
  • May 5, 2025LATEST

POPULARITY

20172018201920202021202220232024


Best podcasts about ikiwa

Latest podcast episodes about ikiwa

Habari za UN
Mkunga nchini Tanzania atoa wito wa uwekezaji kwenye fani hiyo

Habari za UN

Play Episode Listen Later May 5, 2025 2:07


Ikiwa leo ni siku ya kimataifa ya wakunga, tunakwenda nchini Tanzania kummulika mkunga ambaye alinusuru maisha ya wajawazito wawili wakati wa mafuriko makubwa ya Novemba 2023 wilayani Hanang, mkoani Manyara, kaskazini mwa taifa hilo la Afrika Mashariki, ikiwa ni ushuhuda wa majukumu mazito yanayokumba wakunga. Anold Kayanda na maelezo zaidi.

Habari za UN
05 MEI 2025

Habari za UN

Play Episode Listen Later May 5, 2025 10:52


Hii leo jaridani tunaangazia Siku ya kimataifa ya wakunga na kazi zao muhumi, na mafunzo ya jerahani kwa wakimbizi wa ndani nchini DRC. Makala tunasalia hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa na mashinani tunakwenda Gaza.Ikiwa leo ni siku ya kimataifa ya wakunga, tunakwenda nchini Tanzania kummulika mkunga ambaye alinusuru maisha ya wajawazito wawili wakati wa mafuriko makubwa ya Novemba 2023 wilayani Hanang, mkoani Manyara, kaskazini mwa taifa hilo la Afrika Mashariki, ikiwa ni ushuhuda wa majukumu mazito yanayokumba wakunga.Wanawake 125 katika kambi ya wakimbizi wa ndani ya Kigonze, karibu na Bunia, mji mkuu wa jimbo la Ituri, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) ambako ghasia huripokiwa mara kwa mara, sasa wana matumaini mapya ya kujikwamua kiuchumi baada ya kujiunga na mradi wa mafunzo ya kushona nguo unaofadhiliwa na Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa Kulinda Amani nchini humo (MONUSCO).Makala Assumpta Massoi anamulika uzinduzi wa mtandao wa Mashirika ya Manusura wa Ugaidi duniani,  VoTAN      uliofanyika wiki iliyopita hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa.Na mashinani kupitia video iliyoandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji (IOM), fursa ni yake Rawhiyeh, mkimbizi kutoka Gaza eneo la Palestina linalokaliwa na Israel ambaye anasimulia kwa uchungu madhila yanayowakumba yeye na familia yake baada ya kupoteza makazi yao kutokana na mashambulizi ya mabomu.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!

Habari za UN
Chanjo imepunguza vifo na maambukizi ya malaria Kenya

Habari za UN

Play Episode Listen Later Apr 25, 2025 3:27


Ikiwa leo ni siku ya malaria duniani mwaka huu ikibeba maudhui ““Malaria inatokomezwa na sisi: wekeza upya, fikiria upya, chochea upya” shirika la afya la Umoja wa Mataifa  Duniani WHO limetoa wito wa kuongeza juhudi mara dufu na kutumia kila mbinu kutokomeza ugonjwa huo hatari unaoathiri mamilioni ya watu kila mwaka na kusababisha maelfu kwa maefu ya vifo. Moja ya mbinu hizo ni chanjo ambayo nchini Kenya imeanza kuzaa matunda kama anavyofafanua mwandishi wetu wa Nairobi Thelma Mwadzaya katika makala hii.

Habari za UN
Ujumbe wa Ernest Makulilo kuhusu siku ya Kimataifa ya Kitabu na Haki Miliki

Habari za UN

Play Episode Listen Later Apr 23, 2025 3:31


Ikiwa leo ni Siku ya Kimataifa ya Kitabu na Haki Miliki ambapo kila mwaka tarehe kama ya leo siku hii huadhimishwa ili kutambua nguvu ya vitabu kama daraja kati ya vizazi na vizazi na tamaduni mbalimbali. Katika makala hii Anold Kayanda wa Idhaa hii amezungumza na mwandishi maarufu wa vitabu vya elimu, Uchumi na uhamiaji, Ernest Makulilo mkazi wa Marekani katika jimbo la Missouri, kuhusu siku ya leo iliyoanzishwa na shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni UNESCO mnamo mwaka 1995.

Habari za UN
22 APRILI 2025

Habari za UN

Play Episode Listen Later Apr 22, 2025 9:56


Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina ambayo inatupeleka Msasani nchini Tanzania kusikia namna vijana na serikali wanavyolinda Mama Dunia. Pia tunakuletea muhtasari wa habari ujumbe wa Katibu Mkuu, watoto kulinda mazingira DRC, na kifo cha Papa Francis.Ikiwa leo ni siku ya kimataifa ya Mama Dunia, ikilenga kuchagiza hatua ya kuhifadhi sayari dunia, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametumia neno ‘homa' kuwa inakumba dunia hivi sasa kutokana na viwango vya joto vinavyoongezeka kila mwaka. Hata hivyo amesema majawabu ya kutibu homa hiyo yapo ikiwemo kutumia nishati rejelezi ambayo ni rahisi, ina afya na salama kuliko nishati kisukuku.Huko nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, kando ya mapigano yanayotikisa eneo la mashariki mwa nchi, watoto wamechukua hatua kulinda sayari dunia kwa kuhifadhi misitu kwenye taifa hilo ambako ukataji miti kiholela umefurutu ada.Kufuatia kifo cha Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Francis hapo jana Jumatatu, ambaye maziko yake yamepangwa kufanyika Jumamosi wiki hii, mashirika ya Umoja wa Mataifa yameendelea kukumbuka mchango wake wa kutetea walio taabuni. Mathalani shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia wakimbizi, UNHCR limekumbuka wito wake wa kutaka kila mtu kukaribisha, kusindikiza na kujumuisha wale wote wanaobisha hodi kwenye milango yao.Na mashinani  kupitia video iliyoandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo, FAO fursa ni yake Meena Poudel kutoka nchini Nepal, Kusini mwa Asia ambaye ni Katibu wa kikundi cha wanawake watumiaji wa msitu ambacho kinabadilisha takataka za misitu kuwa mbolea rafiki kwa mazingira huku pia wakijipatia kipato."Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!  

Habari za UN
04 APRILI 2025

Habari za UN

Play Episode Listen Later Apr 4, 2025 9:59


Hii leo jaridani tunaangazia Siku ya kimataifa ya kuelimisha umma kuhusu mabomu ya kutegwa ardhini. Makala inamulika harakati za kusongesha malengo ya maendeleo endelevu ikitupeleka nchini Kenya na mashinani tunasalia huko huko nchini Kenya, kulikoni?Ikiwa leo ni Siku ya kimataifa ya kuelimisha umma kuhusu mabomu ya kutegwa ardhini na Msaada wa Hatua Dhidi ya Mabomu hayo, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa akisisitiza nchi kuheshimu mikataba ya kimataifa dhidi ya vilipuzi na silaha nyingine, Umoja wa Mataifa leo umethibitisha tena dhamira yake ya kusaidia Somalia katika mapambano dhidi ya hatari za vilipuzi kwa ajili ya mustakabali salama kwa Wasomali wote.Mwaka huu wa 2025, Siku ya Kimataifa ya Uhamasishaji Kuhusu Mabomu ya Ardhi na Usaidizi kwa Hatua Dhidi ya Mabomu inaadhimishwa chini ya kaulimbiu “Mustakabali Salama Unaanzia Hapa.” Umoja wa Mataifa inasisitiza umuhimu wa kufadhili miradi midogo yenye athari za haraka kusaidia watu wenye ulemavu wa viungo waliathirika katika mizozo. Juhudi hizi zinaimarisha ulinzi wa raia na kupanua teknolojia na uvumbuzi katika nchi zinazoendelea.Makala ambayo inamulika majadiliano ya siku mbili yanayofanyika kila mwaka ya será kuhusu maendeleo endelevu. Majadiliano hayo yanayokunja jamvi leo jijini Nairobi Kenya yameandaliwa na Club De Madrid na mwaka huu yamejikita na ufadhili wa maendeleo, Stella Vuzo kutoka kitengo cha habari cha Umoja wa Mataifa UNIS Nairobi amepata fursa ya kuzungumza na baadhi ya vijana wanaoshiriki mkutano huo wa club de Madrid.Na mashinani leo utamsikia mhadhiri kutoka chuo kikuu cha Bayero jimboni Kano nchini Nigeria anayeshiriki mkutano wa majadiliano ya ufadhili wa maendeleo endelevu unaofanyika Nairobi Kenya.Mwenyeji wako ni Assumpta, karibu!

Habari za UN
Umoja wa Mataifa kuendelea kuisaidia Somalia kuonda mabomu ya kutegwa ardhini

Habari za UN

Play Episode Listen Later Apr 4, 2025 1:52


Ikiwa leo ni Siku ya kimataifa ya kuelimisha umma kuhusu mabomu ya kutegwa ardhini na Msaada wa Hatua Dhidi ya Mabomu hayo, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa akisisitiza mataifa duniani kote kuheshimu mikataba ya kimataifa dhidi ya vilipuzi na silaha nyingine, Umoja wa Mataifa leo umethibitisha tena dhamira yake ya kusaidia Somalia katika mapambano dhidi ya hatari za vilipuzi kwa ajili ya mustakabali salama kwa Wasomali wote. Anold Kayanda na taarifa zaidi.

Habari za UN
Uteguaji mabomu ya ardhini ni suala la amani na kiutu - UNMAS

Habari za UN

Play Episode Listen Later Apr 4, 2025 2:00


Ikiwa leo ni siku ya kimataifa ya kuelimisha umma kuhusu mabomu ya kutegwa ardhini, kauli mbiu ikiwa Mustakabali salama unaanzia hapa, Umoja wa Mataifa unasisitiza umuhimu wa kufadhili miradi midogo yenye matokeo chanya na ya haraka ili kusaidia sio tu watu wanaopata ulemavu wa viungo kutokana na madhara ya mabomu hayo bali pia kuwezesha watu kurejea kwenye maisha yao ya kawaida Sharon Jebichii anamulika Lebanon na Libya.

Jioni - Voice of America
Papa Francis anaendelea na matibabu ikiwa ni siku ya 17 toka alazwe - Machi 02, 2025

Jioni - Voice of America

Play Episode Listen Later Mar 2, 2025 29:59


Matangazo ya saa nzima kuhusu habari za kutwa, ikiwa ni pamoja ripoti kutoka kwa waandishi wetu sehemu mbali mbali duniani na kote Afrika Mashariki na Kati, na vile vile vipindi na makala maalum kuhusu afya, wanawake, jamii na maendeleo.

Habari za UN
27 FEBRUARI 2025

Habari za UN

Play Episode Listen Later Feb 27, 2025 11:04


Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayokupeleka nchini DRC ambako leo tunamulika mmoja wa raia aliyerejea makazi yake huko Sake, nje kidogo ya mji wa Goma, jimboni Kivu Kaskazini baada ya waasi wa M23 kutangaza kuwa wakimbizi wote wa ndani lazima warejee vijijini kwao. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na uchambuzi wa methali.Ikiwa ni mwezi mmoja sasa tangu waasi wa M23 watwae mji wa Goma jimboni Kivu Kaskazini mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC na kuendelea kutwaa miji mingine huku mamia ya maelfu ya watu wakifurushwa makwao, hii leo mashirika ya Kibinadamu nchini humo yametoa ombi la dola bilioni 2.54 ili kusaidia watu milioni 11 walioathiriwa vibaya na mzozo unaoendelea.Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la Afya duniani, WHO Dkt. Tedros Ghebreysus ametangaza kuwa ugonjwa wa mpox bado ni tishio la afya ya umma duniani na hivyo nchi lazima ziendelee kuwa makini katika ufuatiliaji, uchunguzi, kinga na matibabu.Na kuelekea Mkutano wa viongozi kuhusu Mifumo ya uzalishaji chakula mwezi Julai mwaka huu huko Addis Ababa, Ethiopia, Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Amina J. Mohammed amezungumza hivi karibuni akiwa Nairobi, Kenya kwenye kikao cha maandalizi ambako alitembelea jiko la Giga, mpango wa Chakula kwa ajili ya Elimu, unaoendeshwa na Wawira Njiru, mshindi wa tuzo ya Mtu Maarufu Kenya mwaka 2021.Katika kujifunza lugha ya Kiswahili leo mchambuzi wetu Dkt. Josephat Gitonga, kutoka Kenya ambaye ni mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi kwenye kitivo cha tafsiri na ukalimani anatufafanulia maana ya methali “FAHARI ISIYO PARI HAINA HERI.”.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!  

Habari RFI-Ki
Mada Huru: Maoni kuhusu habari kuu wiki hii na matukio katika maeneo mbalimbali

Habari RFI-Ki

Play Episode Listen Later Feb 21, 2025 9:57


Ikiwa ni siku ya Ijumaa, ni wakati wa mada huru, yaani tunampatia mskilizaji nafasi kuchangia habari kuu ambazo tumekuwa nazo wiki hii hapa RFI Kiswahili au kutueleza jambo ambalo limetokea nchini mwake juma hili. Leo pia msikilizaji ni siku ya lugha mama, ningependa sana nikusalimie kwa lugha yako mama lakini ningependa kusikia kutoka kwako kwanza. Jambo! 

Habari RFI-Ki
Mada Huru: Maoni kuhusu habari kuu wiki hii na matukio katika maeneo mbalimbali

Habari RFI-Ki

Play Episode Listen Later Feb 21, 2025 9:57


Ikiwa ni siku ya Ijumaa, ni wakati wa mada huru, yaani tunampatia mskilizaji nafasi kuchangia habari kuu ambazo tumekuwa nazo wiki hii hapa RFI Kiswahili au kutueleza jambo ambalo limetokea nchini mwake juma hili. Leo pia msikilizaji ni siku ya lugha mama, ningependa sana nikusalimie kwa lugha yako mama lakini ningependa kusikia kutoka kwako kwanza. Jambo! 

Habari za UN
Redio imetusaidia kufikisha elimu kwa umma kuhusu hatua dhidi ya mabadiliko ya tabianchi

Habari za UN

Play Episode Listen Later Feb 12, 2025 3:12


Ikiwa kesho Februari 13 ni Siku ya Kimataifa ya Redio, makala inatupeleka jijini Nairobi, Kenya ambako ambako Kevin Keitany wa redio washirika wetu Domus FM kwa kuzingatia kuwa kesho Februari 13 ni Siku ya Kimataifa ya Redio, ametutumia maoni ya vijana wawili wanaozungumzia namna redio imewasaidia kusambaza ujumbe wao kuhusu hatua dhidi ya mabadiliko ya tabianchi.

Mwalimu Huruma Gadi
S0604. Mungu ni Mwaminifu

Mwalimu Huruma Gadi

Play Episode Listen Later Feb 10, 2025 104:55


Shalom!Ikiwa unatafuta ukweli kuhusu uaminifu wa Mungu katika maisha yako, ikiwa unatafuta jibu la siri ya kuwa na udhihirisho katika kila ombi unaloliomba mbele za Mungu. Somo la "UAMINIFU WA MUNGU - IV" ni la kwako.

Habari za UN
Tutafute majadiliano badala ya kugawanyika - Guterres

Habari za UN

Play Episode Listen Later Feb 3, 2025 1:50


Ikiwa kesho Februari 4 ni Siku ya Kimataifa ya Udugu wa Kibinadamu, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres,kupitia ujumbe mahususi kwa ajili ya siku hii ametoa wito wa kuimarisha umoja, usawa, na kuheshimiana katika kipindi hiki cha ongezeko la ubaguzi na kutovumiliana duniani. Anold Kayanda na maelezo zaidi.

Habari za UN
Maandamano huko Goma DRC, wakimbizi waomba UN iwafikishie misaada

Habari za UN

Play Episode Listen Later Feb 3, 2025 3:44


Ikiwa ni wiki moja sasa tangu waasi wa M23 watangaze kutwaa Goma, jimboni Kivu Kaskazini, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, na kisha serikali kutangaza Beni kuwa mji mkuu wa sasa wa jimbo hilo, hii leo Jumatatu Februari 3, maandamano makubwa ya amani yamefanyika mjini Beni, yakiongozwa na mashirika ya kiraia na wananchi. Taarifa zaidi na Assumpta Massoi

Habari za UN
03 FEBRUARI 2025

Habari za UN

Play Episode Listen Later Feb 3, 2025 9:59


Hii leo jaridani tunaangazia machafuko nchini Jamhuri ya Kidemocrasia ya Congo DRC, na ujumbe wa Katibu Mkuu wa UN kuhusu Siku ya Kimataifa ya Udugu wa Kibinadamu. Makala inatupeleka nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati CAR na mashinani tunarejea DRC, kulikoni?Ikiwa ni wiki moja sasa tangu waasi wa M23 watangaze kutwaa Goma, jimboni Kivu Kaskazini, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, na kisha serikali kutangaza Beni kuwa mji mkuu wa sasa wa jimbo hilo, hii leo Jumatatu Februari 3, maandamano makubwa ya amani yamefanyika mjini Beni, yakiongozwa na mashirika ya kiraia na wananchi.Ikiwa kesho Februari 4 ni Siku ya Kimataifa ya Udugu wa Kibinadamu, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres,kupitia ujumbe mahususi kwa ajili ya siku hii ametoa wito wa kuimarisha umoja, usawa, na kuheshimiana katika kipindi hiki cha ongezeko la ubaguzi na kutovumiliana duniani.Makala inatupeleka Jamhuri ya Afrika ya Kati CAR, kwenye kambi ya wakimbizi ya Korsi inayohifadhi zaidi ya wakimbizi 18,000 kutoka Sudan wengi wakiwa ni wanawake na watoto na shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu na afya ya uzazi UNFPA linawasaidia.Na katika mashinani  Lodja Salizre, Mkimbizi wa ndani katika kambi ya Loda jimboni Ituri kaskazini magharibi mwa Jamhuri ya Kidemocrasia ya Congo DRC akileleza ni kwa jinsi gani vita inayoendelea vimeameathiri yeye na familia yake na jinsi ambavyo uwepo wa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo inavyosaidia maisha ya kila siku ya wakazi wake.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!  

Alfajiri - Voice of America
Mali yachukua tani tatu za dhahabu kutoka kwa kampuni ya Barrick Gold ikiwa sehemu ya mzozo wa kifedha kati yao. - Januari 28, 2025

Alfajiri - Voice of America

Play Episode Listen Later Jan 28, 2025 30:00


Matangazo ya nusu saa kuhusu habari za mapema asubuhi pamoja na habari za michezo.

Habari za UN
Guterres: Siku ya Kimataifa ya Wahamiaji tujikumbushe changamoto wanazokumbana nazo

Habari za UN

Play Episode Listen Later Dec 18, 2024 1:42


Ikiwa leo ni siku ya kimataifa ya Uhamiaji, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres kupitia ujumbe wake mahususi kwa ajili ya Siku ya Kimataifa ya Wahamiaji ametoa wito kwa ulimwengu kuitumia siku hii kujikumbusha kwamba pamoja na kwamba tunasherehekea michango ambayo mamilioni ya wahamiaji hutoa kwa jamii leo pia ni siku ya kujikumbusha changamoto ambazo wahamiaji wanaweza kukumbana nazo. Selina Jerobon na maelezo zaidi.

Habari za UN
Mjumbe wa UN aendelea na ziara ya kukutana na wadau nchini Syria

Habari za UN

Play Episode Listen Later Dec 16, 2024 1:31


Mjumbe Maalum wa Umoja wa Mataifa kwa Syria Geir O. Pedersen bado yuko nchini Syria alikowasili jana Jumapili  ikiwa ni wiki moja baada ya wapiganaji wa Hayʼat Tahrir al-Sham (HTS) walioko kwenye orodha ya vikundi vya kigaidi kutwaa mji mkuu Damascus na kusababisha Rais Bashar Al-Assad kukimbia nchi. Ikiwa ni sehemu ya juhudi za Umoja wa Mataifa kuhakikisha mabadiliko ya utawala nchini Syria yanafanyika kwa amani na kuisaidia Syria kutokuingia kwenye mgogoro zaidi, Bwana Pederson aliyewasili jana Damascus  hadi sasa ameshakutana na Kamanda wa Utawala Mpya Ahmed al-Sharaa na Waziri Mkuu wa Serikali ya Muda Mohammed al-Bashir.Taarifa iliyotolewa leo na Ofisi yake inasema Pederson ameeleza muhtasari wa matokeo ya Mkutano wa Kimataifa wa Aqaba kuhusu Syria uliofanyika tarehe 14 ya mwezi huu wa Desemba akisisitiza haja ya kuwepo kwa mpito wa kisiasa unaoaminika na unaoongozwa na kumilikiwa na Wasyria wenyewe kama kanuni za azimio 2254 la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa (2015) zilivyopendekeza. Aidha Mjumbe huyo maalum amesisitiza azma ya Umoja wa Mataifa ya kutoa usaidizi wa kina kwa watu wa Syria.Taarifa imedokeza kuwa Bwana Pedersen ana shughuli nyingi zilizopangwa siku zijazo katika harakati za kusaka suluhu ya amani nchini Syria.

Mazingira Leo, Dunia Yako Kesho
Wataalam wa mazingira: Kuchakata plastiki sio suluhu ikiwa nchi zinazalisha zaidi

Mazingira Leo, Dunia Yako Kesho

Play Episode Listen Later Dec 10, 2024 10:00


Mkutano wa kukabiliana na uchafuzi wa plastiki ulikamilika mwanzoni mwa Disemba 2024 bila mwafaka kufikiwa, wataalam wa mazingira wakisema pendekezo la kuchakata plastiki wakati nchi nyingine zikiendelea kuzalisha sio suluhu la tatizo hilo. Kwenye makala hii leo tunaangazia athari za plastiki kwa afya na mazingira, suluhu zinazopendekezwa lakini pia kupata ufafanuzi zaidi kilichokwamisha kupatikana kwa mkataba wa kumaliza tatizo linalosababishwa na uchafuzi wa plastiki.

Habari za UN
14 NOVEMBA 2024

Habari za UN

Play Episode Listen Later Nov 14, 2024 9:59


Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka Baku kwa mkutan wa COP29, amabyo washiriki wanasaka mbinu za kujumuisha makundi yote katika harakati za kukabili na kuhimili madhara ya mabadiliko ya tabianchi yanayochochewa na ongezeko la hewa chafuzi. Idhaa ya Kiswahili imezungumza na Naomi mmjoja wao kutoka Tanzania. Pata pia muhtasari wa habari na ujifunze Kiswahili.Ikiwa leo ni siku ya kimataifa ya kuelimisha umma kuhusu ugonjwa wa kisukari, shirika la afya la Umoja wa Mataifa duniani WHO leo limesema idadi ya watu wazima wanaoishi na Kkisukari duniani ni zaidi ya milioni 8000 ikiwa ni ongezeko la zaidi ya mara 4 tangu mwaka 1990.Baku Azerbaijan ambako mkutano wa 29 wa nchi wanachama wa mkataba wa Umoja wa Mataifa wa mabadiliko ya tabianchi, COP29 leo umejikita na na lengo la kutozalisha kabisa hewa ya ukaa ambapo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antinio Guterres ameainisha jukumu muhimu ambalo miji, mikoa, biashara na taasisi za kifedha lazima zitekeleze katika kuendesha juhudi za dunia nzima kufikia lengo la kutozalisha kabisa hewa ya ukaa katikati ya karne hii.Nchini Sudan shirika la Umojja wa Mataifa la kuratibu misaada ya kibinadamu na masuala ya dharida OCHA limesema ghasia za kutumia silaha na mashambulizi katika Jimbo la Aj Jazirah zinadhihirisha ukatili wa karibu miezi 19 ya vita nchini Sudan,huku kukiwa na ripoti za ubakaji, mauaji ya halaiki na uporaji mkubwa. Katika chini ya wiki mbili, OCHA inasema uhasama huko Aj Jazirah umefurusha zaidi ya watu 135,000 kutoka makwao, wengi wao walikimbilia majimbo jirani ya Gedaref na Kassala.Katika kujifunza lugha ya Kiswahili hii leo mchambuzi wetu mlumbi wa Kiswahili Joramu Nkumbi kutoka nchini Tanzania, anafafanua maana ya maneno “MADHALI, WAMA, FALAU NA HOBE”Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu! 

Habari za UN
UNICEF yatoa mafunzo ya kutengeneza sodo kwa kijana mkimbizi wa dani nchini Sudan

Habari za UN

Play Episode Listen Later Oct 14, 2024 2:20


Sodo au taulo za kike, vile vile pedi,  ni muhimu kwa wanawake na  wasichana, lakini wengi hawawezi kuzipata wakati wa vita na ukimbizi. Leo tunakutana na Samer, mvulana huyu ambaye akiwa na umri wa miaka 16 tu, kwa msaada wa klabu ya  usafi ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Watoto UNICEF, anatengeneza na kusambaza sodo kwa wanawake na wasichana katika maeneo ya wakimbizi wa ndani jimboni Atbara, nchini Sudan. Msaada wa kifedha kutoka  Mfuko wa dharura wa Umoja wa Mataifa CERF, vilabu vya usafi vya UNICEF, na Shirika la Marekani la misaada ya maendeleo USAID,  vijana wakimbizi wa ndani wanawezeshwa kupata suluhisho kwa changamoto za usafi wanazokutana nazo, wakati wa vita na ukimbizi. Mmoja wa vijana hawa wakimbizi ni Samer mvulana mwenye umri wa miaka 16, ambaye amefundishwa kutengeneza sodo na sasa, anazisambaza bure kwa wanawake na wasichana wakimbizi wa ndani katika jimbo la Atbara, nchini Sudan.Nikataka kujua jinsi Samer anatengeneza sodo hizo…"Nashona kati ya vipande kumi na tano hadi ishirini kwa siku. Kwanza, nakata sponji au sifongo, kisha naweka ndani ya kitambaa. Naishona na kuongeza kifungo ili kuifunga vizuri."Kwa nini Samer, katika umri wa miaka 16, anatengeneza sodo"Hiki ndicho wasichana na akina mama wanachohitaji zaidi wakati wa ukimbizi, lakini hakipatikani. Ikiwa hawatumii sodo, huenda wasiweze kusafiri au kutembea kwa uhuru. Kwa hiyo, nazitengeneza na kuwapatia bure kwa ajili yao kutumia. Kwa sababu ya vita, watu hawana pesa za kununua pedi, kwa hiyo nazitengeneza na kuzisambaza. Sodo hizi zinaweza kufuliwa na kutumika tena. Pedi nyingi ni   hutumiwa mara moja tu, na watu wanalazimika kununua mpya kila wakati."Je nini kilimpa Samer hamasa ya kutengeneza sodo, na anajisikia vipi anapoifanya kazi hii?"Nilipojiunga na warsha ya UNICEF, nilianza kusaidia familia yangu kwa kuwatengenezea sodo. Napokea vifaa kutoka  kiwanda cha UNICEF. Nilipoanza kutengeneza sodo, nilihisi furaha kujua kuwa kuna watu wanaozihitaji. Baadhi yao, hawana pesa na wanakabiliwa na changamoto. Sijihisi aibu kwa kile ninachofanya, kwa sababu kutimiza mahitaji ya watu ni muhimu zaidi kuliko kitu kingine chochote."

Habari za UN
Guterres: Ni wakati muafaka sisi kuwasikiliza wasichana

Habari za UN

Play Episode Listen Later Oct 11, 2024 1:45


Ikiwa le oni Siku ya Kimataifa ya Mtoto wa Kike, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres ametoa wito wa kuwapa sikio watoto wa kike akianza ujumbe wake mahususi kwa ajili ya siku hii akisema uwezo wa wasichana zaidi ya bilioni 1.1 duniani hauna kikomo lakini tunapokaribia tarehe mwaka 2030, wa mwisho kwa Malengo ya Maendeleo Endelevu, ulimwengu unaendelea kuwaangusha wasichana.“Wasichana wanachangia zaidi ya asilimia 70 ya maambukizi mapya ya Virusi Vya Ukimwi, VVU” anasema Guterres na kwamba wana uwezekano mara mbili zaidi wa wavulana kukosa elimu au mafunzo. Na ndoa za utotoni bado zimeenea, huku takriban msichana mmoja kati ya watano duniani akiolewa kabla ya kufikia umri wa miaka 18. Kotekote duniani, mafanikio yaliyopatikana kwa bidii ya usawa wa kijinsia yanafutwa na vita dhidi ya haki za kimsingi za wanawake na wasichana, na kuhatarisha maisha yao. kuzuia uchaguzi wao, na kuweka kikwazo cha mustakabali wa wasichana.Kwa kutumia kaulimbiu ya mwaka huu ya Siku ya Kimataifa ya Mtoto wa Kike ambayo ni ‘Dira ya Msichana' kwa Zama Zijazo, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anasema, wasichana tayari wana dira ya ulimwengu ambamo wanaweza kustawi. Wanafanya kazi kugeuza maono hayo kuwa vitendo, na kutaka sauti zao zisikike. Ni wakati muafaka sisi kusikiliza. Ni lazima tuwape wasichana nafasi kwenye meza, kupitia elimu, na kwa kuwapa rasilimali wanazohitaji na fursa za kushiriki na kuongoza.Ujasiri, matumaini na uamuzi wa wasichana ni nguvu ya kuzingatia. Ni wakati wa ulimwengu kuchukua hatua na kusaidia kubadilisha maono na matarajio yao kuwa ukweli.

Habari za UN
11 OKTOBA 2024

Habari za UN

Play Episode Listen Later Oct 11, 2024 9:58


Hii leo jaridani tunaangazia siku ya Kimataifa ya Mtoto wa Kike na juhudi za Umoja wa Mataifa za kutokomeza ukatili wa kijinsia ikiwa ni pamoja na unaofanyika mtandaoni. Makala tunakupeleka katika ukanda wa Gaza, na mashinani nchini Tanzania, kulikoni?Ikiwa leo ni Siku ya Kimataifa ya Mtoto wa Kike, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres ametoa wito wa kuwapa sikio watoto wa kike akisema uwezo wa wasichana zaidi ya bilioni 1.1 duniani hauna kikomo lakini tunapokaribia mwaka 2030, wa mwisho kwa Malengo ya Maendeleo Endelevu, ulimwengu unaendelea kuwaangusha wasichana.Nchini Ethiopia hususan katika jimbo la Somali, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF limechukua hatua kusaidia manusura wa ukatili wa kijinsia kuweza kujenga upya maisha yao wakati huu ambapo takwimu za shirika hilo zinaonesha kuwa zaidi ya wanawake na wasichana milioni 370 duniani kote wamekumbwa na ukatili wa kingono wakati wa utoto wao, yaani kabla ya kutimiza umri wa miaka 15.Makala tunakupeleka Gaza ambapo mwaka mmoja wa vita nchini Gaza iliyochochewa na mashambulizi ya Hamas dhidi ya Israeli Oktoba 7, 2023 na kisha Israeli kujibu mashambulizi yanayoendelea hadi leo, umekuwa ukimulika zaidi madhara ya vifo na majeruhi. Lakini sasa shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo FAO limekusogezea madhara ya vita katika kilimo na ufugaji.Katika mashinani leo ikiwa ni Siku ya kimataifa ya Mtoto wa Kike tunaelekea nchini Tanzania kupitia video iliyoandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF nchini humo, kujifunza kutoka mtoto mmoja wa kike kuhusu haki za watoto.Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu! 

Kwa Undani - Voice of America
Raia wa Msumbiji milioni 17 wamejiandikisha kupiga kura Jumatano huku nchi ikiwa na changamoto za ukosefu wa usalama na chakula. - Oktoba 08, 2024

Kwa Undani - Voice of America

Play Episode Listen Later Oct 8, 2024 29:54


Kwa Undani ni matangazo ya dakika 25 yanayochambua habari kwa undani zaidi na kumpa msikilizaji maelezo ya kina kuliko ilivyo kawaida kuhusu tukio au swala lililojitokeza katika habari.

Habari za UN
02 OCTOBA 2024

Habari za UN

Play Episode Listen Later Oct 2, 2024 9:59


Hii leo jaridani tunaangazia ujumbe wa Katibu Mokuu katika Siku ya Kimataifa ya Kutokuwa na Ghasia, na waandishi wa habari katika harakati za kusongesha malengo ya maendeleo endelevu. Makala inatupeleka Tanzania kuangazia taasisi ya watoto Afrika Initiative, na mashinani inatupeleka Amhara, Ethiopia, kulikoni?Ikiwa leo ni Siku ya Kimataifa ya Kutokuwa na Ghasia, Katibu Mkuu wa Umoja Mataifa amezitaka nchi kubadilisha kuwa uhalisia ahadi za kuleta amani duniani walizojiwekea katika Mkutano wa Zama zijazo uliokamilika hivi majuzi hapa katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani.Umoja wa Mataifa kila uchao unapigia chepuo wadau mbali mbali wakiwemo waandishi wa habari kusongesha Malengo ya Maendeleo Endelevu, SDGs ili sio tu yaweze kufahamika bali pia wale wanaowajibika kuyatekeleza wafanye hivyo ili hatimaye maisha ya wananchi yawe bora na si bora maisha.Makala inatupeleka Tanzania kuangazia taasisi ya watoto Afrika Initiative, iliyoanzishwa ili kuwasaidia watoto hususani vijana balehe. Je, inawasaidia vipi? Flora Nducha wa Idhaa hii amezungumza na mwanzilishi na mkurugenzi mtendajiwa taasisi hiyo Vivian Joseph ambaye anaanza kwa kufafanua kuhusu taasisi hiyo ya Watoto Afrika Initiative.Katikashinani fursa ni yake Teyban Mohammed kutoka Amhara, Ethiopia, mama aliyenufaika kwa vocha za milo mbalimbali yenye lishe bora kutoka kwa WFP, akieleza manufaa ya mradi huu kwa watoto pamoja na kina mama wajawazito na wanaonyonyesha?Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu! 

Habari za UN
Guterres: Ili kutokuwa na ghasia duniani nchi zibadilishe ahadi kuwa uhalisia

Habari za UN

Play Episode Listen Later Oct 2, 2024 2:12


Ikiwa leo ni Siku ya Kimataifa ya Kutotumia vurugu, Katibu Mkuu wa Umoja Mataifa António Guterres amezitaka nchi kubadilisha kuwa ukweli ahadi za kuleta amani duniani walizojiwekea katika Mkutano wa Zama zijazo uliokamilika hivi majuzi hapa katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani.Ni kupitia kwenye ujumbe wake mahususi kwa ajili ya kuadhimisha Siku hii ya kimataifa ya kutotumia vurugu ambayo huadhimishwa kila tarehe pili ya mwezi Oktoba tarehe ya kuzaliwa Mahatma Gandhi, kiongozi wa vuguvugu la uhuru wa India na mwanzilishi wa falsafa na mkakati wa kutotumia vurugu kama njia ya kufanikisha mabadiliko katika jamii, Bwana Guterres amekumbushia namna ambavyo siku chache zilizopita katika Mkutano wa Zama Zijazo nchi zilikuja pamoja ili kuweka msingi wa umoja mpya wa ushirikiano wa kimataifa, ulio na nyenzo za kusaidia amani katika ulimwengu unaobadilika.Kiongozi huyo wa Umoja wa Mataifa anataja kwamba moja ya ahadi walizojiwekea viongozi wa ulimwengu ni kuangalia upya sababu za msingi za migogoro kuanzia kwa ukosefu wa usawa hadi umaskini na mgawanyiko na kwa hivyo sasa “tunahitaji nchi kubadilisha ahadi hizo kuwa uhalisia.” Akasisitiza.Bwana Guterres anaeleza kwamba siku hii ya kimataifa ya kutotumia vurugu inathibitisha tena maadili ambayo Mahatma Gandhi alijitolea maisha yake yaani usawa, heshima, amani na haki.Gandhi aliamini kutotumia vurugu ndio nguvu kuu zaidi inayopatikana kwa wanadamu yenye nguvu zaidi kuliko silaha yoyote. Na hivyo Guterres akazitaka nchi kwa pamoja, zijenge taasisi za kuunga mkono dira hiyo adhimu.

Jioni - Voice of America
Rais Azali wa Comoros ameongoza mkutano wa Baraza la Mawaziri ikiwa ni mara ya kwanza kuonekana hadharani tangu kushambuliwa na kujeruhiwa. - Septemba 19, 2024

Jioni - Voice of America

Play Episode Listen Later Sep 19, 2024 29:59


Matangazo ya saa nzima kuhusu habari za kutwa, ikiwa ni pamoja ripoti kutoka kwa waandishi wetu sehemu mbali mbali duniani na kote Afrika Mashariki na Kati, na vile vile vipindi na makala maalum kuhusu afya, wanawake, jamii na maendeleo.

Habari za UN
Guterres: Vita huharibu miili, akili na fikra za vijana na watoto

Habari za UN

Play Episode Listen Later Sep 9, 2024 1:47


Ikiwa leo ni siku ya kimataifa ya kulinda elimu isishambuliwe wakati wa mizozo kutokana na umuhimu wake kwa watoto na jamii, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amesema miaka ya karibuni imeshuhudia ongezeko kubwa la mashambulizi dhidi ya wanafunzi, walimu na shule duniani kote. Hivyo ndivyo alivyoanza ujumbe wake wa siku hii. Katibu Mkuu anasema kuanzia Gaza hadi Sudan, Myanmar, Ukraine, Colombia hadi Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC na kwingineko, vita inasababisha ukatili kwa binadamu, lakini kwa watoto na vijana waliokutwa katikati ya jinamizi la vita, gharama haiwezi kukokotolewa.Anasema ndio maana siku hii inatukumbusha jinsi vita inaharibu miili, akili na fikra za watoto na vijana. Kuanzia majeraha hadi vifo, kutekwa nyara, kulazimika kukimbia, ukatili wa kingono, kutumikishwa vijana na kupoteza fursa. Hatari ni kubwa sana.Anakumbusha kuwa elimu sio tu haki ya msingi ya binadamu, bali ni muhimu kwa ajili ya kutimiza haki nyingine zote za binadamu.Ni kwa mantiki hiyo anataka nchi ziwekeze kwenye elimu na zifanye juhudi zote kuhakikisha wakati wa mizozo elimu na maeneo ya kujifunza yanalindwa, zilinde wanafunzi na walimu na ziwawajibishe wale wote wanaoshambulia shule.Ametumia pia ujumbe huo kuzitaka nchi ziridhie na zitekeleze Azimio la Shule Salama, ziunge mkono Ubia wa Kimataifa wa Kuepusha Mashambulizi dhidi ya Shule na zishikamane na juhudi zote za kuhakikisha watoto na vijana wanaendelea kujifunza iwe wakati wa majanga au wakati majanga yanapokoma.Ametamatisha akisema hebu na tulishe elimu isishambuliwe, tulinde haki ya msingi ya elimu ambayo ni haki ya kila mtoto, kila mtu kokote kule.

Habari za UN
09 SEPTEMBA 2024

Habari za UN

Play Episode Listen Later Sep 9, 2024 9:58


Hii leo jaridani tunaangazia suala la elimu katika maeneo ya migogoro, na msaada wa kibinadamu huko Upper Nile nchini Sudan Kusini. Makala tunakupeleka nchini Nigeria na mashinani nchini Afghanistan, kulikoni??Ikiwa leo ni siku ya kimataifa ya kulinda elimu isishambuliwe wakati wa mizozo kutokana na umuhimu wake kwa watoto na jamii, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amesema miaka ya karibuni imeshuhudia ongezeko kubwa la mashambulizi dhidi ya wanafunzi, walimu na shule duniani kote. Hivyo ndivyo alivyoanza ujumbe wake wa siku hii.Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Sudan Kusini (UNMISS) umewaeleza wananchi wa Kaunti ya Nasir au Keich Kon iliyoko jimboni Upper Nile nchini Sudan Kusini kuwa ili waweze kurejeshewa huduma za misaada ya kibinadamu ni vyema wakafikia makubaliano ya kusitisha mapigano.Makala inatupeleka Maiduguri nchini Nigeria kusikia namna mfuko wa kimatifa wa elimu haiwezi kusubiri yaani Education Cannot Wait (ECW) kwa kushirikiana na shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia watoto (UNICEF) na wadau wengine wanarejesha matumaini kwa waliokosa elimu rasmi hasa kutokana na hali mbayá ya usalama katika maeneo yao.Na katika mashinani, fursa ni yake Faeza, mfanyakazi wa kiwanda cha kutengeneza biskuti nchini Afghanistan, mradi unaowezeshwa na shirika la WFP akitueleza manufaa ya mradi huo kwa jamii iliyoathirika na vita hasa wanawake na watoto.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu! 

Habari za UN
ECW yarejesha matumaini kwa msichana Fatima wa Nigeria

Habari za UN

Play Episode Listen Later Sep 9, 2024 3:12


Alipokuwa na umri wa miaka 10 mnamo mwaka 2015, Fatima na familia yake walilazimika kutoroka nyumbani kwao Konduga, ili kuepuka mashambulizi kutoka kwa makundi yenye silaha. Konduga iko kilomita 25 kusini mashariki mwa mji wa Maiduguri, kaskazini mashariki mwa Nigeria.Familia ya Fatima haikuwa na namna ya kumuandikisha katika shule yoyote rasmi. Alitumia muda wake mwingi kuuza chakula.Shukrani kwa usaidizi wa mfuko wa kimatifa wa elimu haiwezi kusubiri yaani Education Cannot Wait (ECW) na wadau wake wa kimkakati, Fatima sasa amesajiliwa katika mpango mesto unaolenga kuwapa elimu wasichana walio nje ya shule.Msichana huyu ni mmoja wa walengwa 250 wa programu ya miezi mitano ya kusoma, kuandika na kuhesabu, ambayo imemwezesha kusoma kwa lugha ya Kihausa na hata kuandika jina lake kama anavyoeleza."Niliingia katika shule ya ufundi baada ya kusikia kuihusu wakati nilipokuwa nimeenda kuuza chakua. Mara moja nilihifadhi kile nilichoenda kuuza kisha nikajiandikisha jina langu. Wale ambao tulikuwa hatuendi shule tulitambuliwa na kuchaguliwa. Tulifundishwa jinsi ya kusoma na kuandika. Kabla hapo nilikuwa siwezi hata kuandika jina langu.”Sehemu ya pili ya programu hii mseto ilihusisha kipengele cha ufundi ambapo wasichana wanaoishi katika mazingira hatarishi hupata mafunzo ya ufundi kwa muda wa miezi mitatu. Mpango unaotekelezwa na shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto, UNICEF, Norwegian Refugee Council (NRC) na Save the Children."Pia, sasa ninajua namba, na ninaweza kupima watu  ninaposhona." Anasema Fatima ambaye katika kipengengele cha ufundi yeye amechagua ushoni wa nguo.Mpango huu tayari umewanufaisha wasichana balehe 600 tangu kuanzishwa kwake, na kuwapa vifaa vya kuanzia na ujuzi wa kujitegemea. Fatima naye ana matumaini.“Nataka kujifunza stadi hii ili niwahishimishe wazazi wangu na wawe na furaha. Nikimaliza kujifunza nataka kuwa mtu wa kuwashonea ndugu zangu nguo.”Kama ambavyo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres anatoa wito kwa nchi zote kuwekeza katika elimu na kufanya juhudi za kila namna kulinda elimu na maeneo ya kusomea, kulinda wanafunzi na walimu,  Mkurugenzi Mtendaji wa Education Cannot Wait (ECW) Yasmine Sherif, anaeleza namna ambavyo mfuko wa kimatifa wa elimu haiwezi kusubiri umejizatiti kuendelea kuiunga mkono elimu kote duniani wakati huo akitoa wito kwa kila anayeweza kuwaongezea nguvu afanye hivyo."Kuna ustahimilivu na watoto hawa wamepitia kiwewe na mambo mengi. Ni lazima tuwepo kwa ajili yao, na tunaweza kuona matokeo. Tunatazamia kuufanya tena mpango huu mwaka katika mwaka huu, tunatarajia kufanya hivyo kwa takribani dola milioni 15, kama sio zaidi. Ikiwa nyinyi nyote mtakuja na kutusaidia kuongeza."

Habari za UN
Uhalifu kote duniani unaleta madhila yaleyale kwa wanadamu – Maonesho ya picha za ICC

Habari za UN

Play Episode Listen Later Aug 23, 2024 3:55


Ikiwa leo ni siku ya mwisho ya maonesho ya picha yaliyoandaliwa na Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York Marekani, Anold Kayanda anatupitisha katika picha hizo zinazoonesha athari mbalimbali kwa wanadamu kutokana na uhalifu unaotekelezwa katika maeneo mbalimbali duniani.Maonyesho haya yanachunguza uhusiano wa pamoja unaooneshwa katika simulizi za watu kutoka hali zote ambapo ICC imeanzisha uchunguzi. Maonesho haya pia yanaangazia baadhi ya wapokeaji wa kwanza wa maagizo ya malipo ya ICC.Ingawa simulizi hizi zinatoka katika mabara manne, zina ufanano mwingi. Watu wanapoteza nyumba, ardhi na familia zao. Pia zinaonesha jinsi jamii ni muhimu katika kujenga upya maisha. Kwako Anold

Alfajiri - Voice of America
Russia inaweza kuteka miji ya Ukraine ikiwa Marekani itachelewa kutoa msaada wa kijeshi kwa Ukraine-mchambuzi - Februari 20, 2024

Alfajiri - Voice of America

Play Episode Listen Later Feb 20, 2024 30:00


SBS Swahili - SBS Swahili
Australia ya elezewa: Wazazi wanaweza msaidiaje mtoto kupona kiwewe?

SBS Swahili - SBS Swahili

Play Episode Listen Later Nov 28, 2023 12:09


Ikiwa mtoto wako amepata kiwewe ng'ambo au nchini Australia, ikiwa ilifanyika hivi karibuni au katika siku za nyuma, pakiwa msaada unao faa, mtoto anaweza pona.

australia wazazi ikiwa
Habari za UN
Nicholas Haysom: Hatua inahitajika sasa kwa ajili ya uchaguzi kwa wakati na wa huru na haki nchini Sudan Kusini

Habari za UN

Play Episode Listen Later Aug 2, 2023 0:02


Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ambaye pia ni Mkuu wa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini (UNMISS), Nicholas Haysom ametahadharisha kwamba muda unazidi kuyoyoma kuelekea Sudan Kusini kufanya uchaguzi mkuu unaotarajiwa mwezi Desemba mwaka ujao wa 2024 lakini bado masuala muhimu ya kuufanya uchaguzi huo uende kama ulivyopangwa bila kuchelewa hayajakamilika."Ikiwa imesalia miezi 17 tu kwenye ratiba ya kuelekea uchaguzi wa mwaka 2024, narudia kile nilichokisema katika mkutano wa awali na waandishi wa habari, kwamba mwaka 2023 ni mwaka wa 'kutengeneza au kuvunja'," amesema Bwana Haysom mapema leo Agosti pili alipozungumza na vyombo vya Habari mjini Juba ambao ni mji mkuu wa nchi hiyo changa zaidi duniani.    Ghasia miongoni mwa jamii za Sudan Kusini zinaendelea kuongezeka pamoja na shinikizo la kuongezeka kwa ufinyu wa rasilimali huku maelfu ya watu wakiendelea kuingia nchini humo wakikimbia mapigano katika nchi jirani ya Sudan.  Kwa mujibu wa Bwana Haysom, miongoni mwa hatua muhimu ambazo inabidi zichukuliwe ni pamoja na hitaji la kuunda upya vyombo vitatu muhimu, ambavyo ni, Tume ya Kitaifa ya Marekebisho ya Katiba, Tume ya Kitaifa ya Uchaguzi, na Baraza la Vyama vya Kisiasa; kukamilisha mipango ya mpito ya usalama; kuendeleza mchakato wa kudumu wa kutengeneza katiba; na kuunda nafasi za kiraia na kisiasa ambapo kila raia ana uhuru wa kujadili na kujihusisha na uchaguzi wa kisiasa na kikatiba bila woga.  "Kufanya uchaguzi tu hakutoshi - uaminifu, uwazi na ushirikishwaji wa mchakato ndio unaoleta uhalali. Hii ni pamoja na kwamba vyama vya siasa lazima viweze kujiandikisha na kufanya kampeni kwa uhuru; asasi ya kiraia kwa ajili ya elimu ya uraia na kuwa waangalizi wa mchakato. Inajumuisha vyombo vya habari vinavyoweza kuripoti kuhusu mchakato huo na kutoa nafasi kwa sauti na maoni mbalimbali kwa wapiga kura kufanya uamuzi sahihi,” amesema Mwakilishi huyo wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini.  Aidha Bwana Haysom amesisitiza kuwa UNMISS itaendelea kuiunga mkono Sudan Kusini katika michakato ya uchaguzi na uundaji wa katiba kwa kushirikiana na wadau wa kikanda kama vile Muungano wa Afrika (AU) na mamlaka ya pamoja ya kitaifa kwa ajili ya maendeleo kwenye eneo la Pembe ya Afrika (IGAD).  

Habari za UN
01 AGOSTI 2023

Habari za UN

Play Episode Listen Later Aug 1, 2023 0:12


Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina ambapo mradi wa serikali ya DRC na UN Women wajengea uwezo wajasiriamali Goma. Pia tunakuletea habari kwa ufupi kutoka IFAD, FAO, WHO na UNICEF ikiwa ni pamoja na Tamko la Haki za binadamu. Mashinani tunakupeleka nchini Sudan, kulikoni? Ikiwa leo ni mwanzo wa Wiki ya Kimataifa ya Unyonyeshaji Maziwa ya Mama kwa mtoto, kaulimbiu ikiwa, "Tufanye unyonyeshaji kazini, ufanye kazi" Mashirika ya Umoja wa Mataifa la kuhudumia Watoto (UNICEF) na la Afya Ulimwenginu (WHO) wanasisitiza haja ya usaidizi mkubwa wa unyonyeshaji katika sehemu zote za kazi ili kuendeleza na kuboresha maendeleo katika viwango vya unyonyeshaji duniani kote huku ushauri wao ukijumuisha likizo ya uzazi yenye malipo ikiwezekana kwa muda wa miezi sita au zaidi baada ya kujifungua.Wakuu wa mashirika matatu ya Umoja wa Mataifa, lile la Chakula na Kilimo (FAO), Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo (IFAD) na la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) wameonya leo walipokuwa wakihitimisha ziara ya siku tatu nchini Sudan Kusini kuwa madhara ya kutochukua hatua katika kushughulikia majanga tata ya chakula, tabianchi na ukosefu wa usalama nchini humo yatajitokeza katika kupoteza maisha, ustawi na mustakabali wa mamilioni ya watu katika taifa hilo changa duniani.Na tukiendelea na ufafanuzi wa tamko la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa ambalo mwaka huu linatimiza miaka 75, Mwanasheria wa Haki za Binadamu nchini Tanzania, Wakili Jebra Kambole anafafanua ibara ya 6 ya tamko hilo.Na mashinani tutamsikia Mkuu wa Operesheni wa Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya kibinadamu pamoja na kuratibu masuala ya dharura OCHA aliyetembelea kambi za wakimbizi wa ndani nchini Sudan.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!

Habari za UN
Kutoka Dodoma Tanzania Bara hadi Paje, Zanzibar kukabiliana na  umaskini

Habari za UN

Play Episode Listen Later Jul 28, 2023 0:03


Moja ya malengo ya Umoja wa Mataifa kuhusu maendeleo endelevu, SDGs ni kutokomeza umaskini ifikapo mwaka 2030. Ikiwa imesalia miaka 7 kabla ya kufikia ukomo, nchi, jamii na kila mtu mmoja mmoja anachukua hatua kutokomeza umaskini hasa kuanzia ngazi ya familia. Umaskini unasababisha watu washindwe sio tu kupata mlo bali pia kupeleka watoto wao shuleni kupata elimu bora. Nchini Tanzania,  hususan visiwani Zanzibar katika mkoa wa Kusini Unguja Assumpta Massoi katika pita ya hapa na pale alikutana na mwananchi mmoja ambaye ameamua kuvuka baharí ya Hindi kutoka Bara  hadi visiwani kukabiliana na umaskini. Ungana naye basi Assumpta Massoi katika makala hii. 

Habari za UN
25 JULAI 2023

Habari za UN

Play Episode Listen Later Jul 25, 2023 0:11


Hii leo jaridani mada kwa kina ambapo wakimbizi kutoka nchini Rwanda na Burundi wanaopata hifadhi katika nchi Jirani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, wamepata matumaini mapya ya maisha baada ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR na shirika lisilo la kiserikali ya AIDES kuwawezesha kuanzisha mradi wa kazi za Sanaa ambao unawasidia kujikimu kimaisha pamoja na familia zao. Ashinani tutaelekea Bahari ya Shamu au Red Sea, kulikoni? Hatimaye operesheni kubwa imeanza leo huko Yemen ya kupakua mapipa ya mafuta ghafi kutoka meli ya FSO Safer iliyoanza kuoza kwenda meli ya  Nautica au Yemen katika pwani  ya bahari ya Shamu.Ikiwa leo ni siku ya kimataifa ya kuzuia watu kuzama majini, shirika la Umoja wa MAtaifa la chakula na kilimo, FAO limesema linatumia siku hii kushirikiana na shirika la Umoja wa Mataifa la afya ulimwenguni WHO kuelimisha umma juu ya kuzama majini hasa katika sekta ya uvuvi.Nchini Sudan Kusini, shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu na Afya ya Uzazi, UNFPA linaendesha semina kuhusu ukatili wa kijinsia na kingono ili kusaidia manusura ambao wanakabiliwa na vitendo hivyo wakati wakirejea nyumbani kutokana na mapigano yanayoendelea nchini Sudan.Mashinani tutamsikia Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo, UNEP hatua iliyoanza asubuhi ya leo kwa saa za Yemen ya kuhamisha mafuta yaliyokuwa yanahatarisha usalama kwenye Bahari ya Shamu au Red Sea.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!

Habari za UN
27 JUNI 2023

Habari za UN

Play Episode Listen Later Jun 27, 2023 0:15


Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina ambayo leo inaturejesha hapa Makao makuu ya umoja wa Mataifa kusiki maandalizi ya maadhimisho ya pili ya siku ya Lugha ya Kiswahili duniani. Pia tunakuletea habari kwa ufupi zikiwemo ripoti ya Katibu Mkuu kuhusu watoto katika migogoro ya silaha, msaada kwa wakimbizi nchini Sudan na maadili ya akili bandia. Katika mashinani tunakupeleka nchini Mali, kulikoni?Ikiwa leo ni Siku ya Biashara Ndogondogo na za Kati, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amewapigia chepuo wanawake na wajasiriamali wadogo kwamba wanahitaji kusaidiwa ili kukabiliana na changamoto nyingi ambazo mara nyingi huzuia ukuaji wa biashara zao, na kuwakwamisha wengi wao katika ujasiriamali usio rasmi.Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR, limeeleza kuwa linazidi kutishwa na kuongezeka kwa mahitaji ya kibinadamu miongoni mwa walioathirika na vita nchini Sudan. Kamishna Mkuu Msaidizi wa Operesheni za UNHCR, Raouf Mazou hii leo mjini Geniva Uswisi amesema wafanyakazi wa UNHCR wanafanya juhudi za kusaidia wananchi lakini ukosefu wa usalama unazuia kufika katika baadhi ya maeneo ili kuwasaidia wenye uhitaji.   Na shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) na Kamisheni ya Ulaya wametia saini makubaliano ya kuharakisha utekelezaji wa kimataifa wa Pendekezo la UNESCO kuhusu maadili ya akili bandia. Bajeti ya Euro milioni 4 itatolewa kusaidia nchi zenye maendeleo duni zaidi duniani ili zifanikishe uundaji wa sheria zao za kitaifa. Takriban nchi 30 tayari zimeanza kutumia Pendekezo hili kutunga sheria za kitaifa zinazohakikisha kwamba matumizi ya akili bandia yanaheshimu uhuru wa kimsingi na haki za binadamu na kuwanufaisha wanadamu wote.Mashinani tutakupeleka nchini Mali ambapo tutaskikiliza jinsi vita inavyoathiri watoto.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!

Habari za UN
HABARI ZA UN 20 JUNI 2023

Habari za UN

Play Episode Listen Later Jun 20, 2023 0:10


Ikiwa leo ni Siku ya Wakimbizi Duniani tutawasikia wakimbizi wa ndani DRC wanavyozungumzia harakati za Umoja wa Mataifa katika kutekeleza Kauli mbiu ya mwaka huu:"Matumaini Mbali na Nyumbani.".Pia utasikia habari kwa ufupi zikiangazia ujumbe wa katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres kwa siku hii ya wakimbizi duniani akihimiza mshikamano na ushirikiano na wakimbizi. Naye kamishna wa wakimbizi Filippo Grandi ameadhimisha siku hii akiwa katika kambi ya wakimbizi ya Kakuma iliyoko nchini kenya ambapo ametoa wito kwa wadau kuunga mkono wakimbizi lakini pia kuzisaidia nchi zinazopokea na kuwahifadhi wakimbizi kama Kenya. 

Habari za UN
Ukatili wa kingono katika mizozo ni jinamizi lililokita mizizi katika pengo la usawa: UN

Habari za UN

Play Episode Listen Later Jun 19, 2023 0:03


Ikiwa leo ni siku ya kimataifa ya kutokomeza ukatili wa kingono katika mizozo ya vita Umoja wa Mataifa umesenma jinamizi hilo ni janga lililokita mizizi katika kukosekana kwa usawa na kanuni na tamaduni kali za masuala ya kijinsia. Tupate maelezo Zaidi kutoka kwa Flora Nducha(TAARIFA YA FLORA NDICHA)Katika taarifa ya pamoja iliyotolewa leo mjini Brussells na New York na mwakilishi wa pamoja wa Umoja wa Mataifa kuhusu ukatili wa kingono katika mizozo Pramila Patten na mwakilishi wa Muungano wa Ulaya kwa ajili ya mambo yan je na sera za usalama Josep Borrell wametoa wito wa hatua madhubuti zaidi za kuzuia na kukomesha unyanyasaji wa kingono, na kuendeleza usawa wa kijinsia kama kipaumbele cha kisiasa. Wamesema “Tunasikitishwa na kuongezeka kwa matumizi ya unyanyasaji wa kingono kama mbinu ya kikatili ya vita, mateso, ugaidi na ukandamizaji wa kisiasa, na tishio kwa usalama wa pamoja. Hatari ya kuwa mlengwa wa unyanyasaji wa kingono leo inazidishwa na ukweli kwamba uhalifu huu unaweza pia kuwezeshwa na kukuzwa mtandaoni, kwa kutumia chaneli za kidijitali.”Badala ya kutumika vibaya wamekumbusha kuwa “Wakati huo huo, majukwaa ya kidijitali yanaweza kuwa na jukumu muhimu na kuwa chombo chenye nguvu cha kuboresha usawa wa kijinsia na kuwawezesha wanawake na wasichana, na kuchangia katika kujenga uwezo wao wa kustahimili nyakati za shida. Wanaweza pia kusaidia katika kuzuia unyanyasaji wa kingono na kijinsia, na hatua zinazohitajika, kupitia tahadhari za  mapema na kuunganisha waathiriwa na njia za kuwatambulisha kwenye huduma, na kuwezesha kuripoti..”Viongozi hao wameonya kwamba badala ya kuwa msaada kwa waathirika leo hii “Mitandao hiyo inatumika vibaya kusambala kauli za chuki na kuchochea ukatili wa kijinsia na ubaguzi, kwani kauli za chuki za kijinsia zinaendelea kuongezeka kutumika kuwanyamazisha watetezi wa haki za binadamu, na wanaharakati wa kisiasa kwa kuchagiza utekelezaji wa ukatili wa kingono. Katika mazingira yaliyoathiriwa na migogoro, majukwaa ya kidijitali yanatumiwa kusafirisha kiharamu wanawake na wasichana kwa madhumuni ya unyanyasaji wa kingono. Walanguzi wa ngono wanatumia mtandao kama zana ya kuajiri wanawake na haswa Watoto na kutangaza huduma za kinyonyaji.”Wameongeza kuwa na katika mazingira mabaya zaidi wanawake na wasichana wanauzwa mtandaoni kama ilivypoainishwa kwenye maenmeo yanayodhibitiwa na kundi la kigaidi la ISILZaidi ya hayo wamesema “ upotoshaji wa habari kwa makusudi na udhibiti kupitia kampeni za kutoa taarifa potofu unaathiri uwezo wa mataifa kulinda raia na kushughulikia unyanyasaji wa kingono. Matumizi ya intaneti kama silaha katika maeneo yenye migogoro pia huzuia waathiriwa wa unyanyasaji wa kingono unaohusiana na migogoro kupata taarifa kuhusu huduma za kuokoa maisha na kupata usaidizi wa mtandaoni kama vile usaidizi wa kisaikolojia.”Kwa mantiki hiyo wametoa wito wa kuwa na “Majukwaa salama ya kidijitali yanayotii sheria za kimataifa, ili waathirika wa unyanyasaji wa kingono unaohusiana na migogoro na wale wanaowaunga mkono watumie mifumo hii kupambana na ukwepaji wa sheria na kudai uwajibikaji ulioboreshwa. Ni muhimu kukuza mazingira ya ulinzi mtandaoni na nje ya mtandao, ambayo yanazuia unyanyasaji wa kijinsia na vile vile kuwezesha kuripoti kwa usalama na makuchukuliwa hatua zinazofaa.”Pia wameitaka Jumuiya ipambane kwa Pamoja dhidi ya tishio linaloongezeka kila mara linaloletwa na teknolojia ya kidijitali na kuziba pengo la mgawanyiko wa kidijitali wa kijinsia ili kuruhusu waathiriwa kupata rasilimali na kupambana na ukwepaji wa sheria kwa kuzingatia kujenga usawa wa kijinsia kwa kuzuia na kupambana na unyanyasaji wa kingono katika migogoro.Wamehitimisha ujumbe wao kwa kusema kuwa “Kwa kushughulikia mgawanyiko wa kidijitali wa kijinsia, tunaweza kuunda ulimwengu ambapo wanawake na watoto wanaweza kuishi bila woga na vurugu.”Siku ya kimataifa ya kutokomeza ukatili wa kingono katika mizozo…

Habari za UN
12 JUNI 2023

Habari za UN

Play Episode Listen Later Jun 12, 2023 0:10


Hii leo jaridani tunaangazia ajira kwa watoto na wakimbizi nchini Jordan. Makala tunakupeleka nchini CAR na mashinani nchini Kenya, kulikoni?Ikiwa leo ni Siku ya Kimataifa dhidi ya Ajira au Utumikishaji wa Watoto ambayo inakusudia kutumika kama kichocheo cha kuongeza harakati za kimataifa dhidi ya ajira au utumikishwaji kwa watoto na ikisisitiza uhusiano kati ya haki za kijamii na ajira kwa watoto, kama ilivyo kwa nchi nyingine wanachama wa Umoja wa Mataifa, Tanzania nayo imeungana na mataifa mengine kuadhimisha siku hii ambapo maadhimisho hayo yamefanyika Kitaifa katika kijiji cha Gua.Katika kambi ya wakimbizi ya Za'atari iliyoko nchini Jordan, roho ya ubunifu ya mtu mmoja na dhamira yake isiyoyumba imebadilisha vitu mbalimbali vinavyotupwa na kuonekana havifai tena kuwa nyenzo muhimu za urembo.Katika makala leo Afisa Habari wa Kikosi cha 6 cha walinda amani wa Umoja wa Mataifa kutoka Tanzania, TANBAT 6 wanaohudumu nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, anatupeleka katika ziara ya walinda amani hao kukagua miradi ambayo wameianzisha kwa ajili ya wananchi.Na mashinani tutakupeleka kijinini Kareman katika kaunti ya Turkana nchini Kenya kushuhudia jinsi ambavyo wenyeji wanajitolea kuhakikisha wanawake na watoto wanaweza kufikia huduma za afya licha ya ukame ambao umezikumba jamii za kaunti hiyo kwa muda mrefu.Mwenyeji wako ni Flora Nducha, Karibu!

Habari za UN
Watoto Tanzania wapaza sauti yao katika maadhimisho dhidi ya utumikishaji watoto

Habari za UN

Play Episode Listen Later Jun 12, 2023 0:01


Ikiwa leo ni Siku ya Kimataifa dhidi ya Ajira au Utumikishaji wa Watoto ambayo inakusudia kutumika kama kichocheo cha kuongeza harakati za kimataifa dhidi ya ajira au utumikishwaji kwa watoto na ikisisitiza uhusiano kati ya haki za kijamii na ajira kwa watoto, kama ilivyo kwa nchi nyingine wanachama wa Umoja wa Mataifa, Tanzania nayo imeungana na mataifa mengine kuadhimisha siku hii ambapo maadhimisho hayo yamefanyika Kitaifa katika kijiji cha Gua, Kata ya Gua katika Halmashauri ya Wilaya ya Songwe Mkoani Songwe. Kupitia siku hii muhimu kwa Watoto ulimwenguni kote, baadhi ya watoto kutoka Shule ya Msingi Gua wametoa maoni yao kuhusu umuhimu wa maadhimisho haya, miongoni mwao ni, Grace yeye ni muelimishaji jamii kuhusu utumikishwaji wa mtoto kwenye mashamba ya tumbaku, hapa anazungumzia hali ya utumikishwaji ilivyo kwa sasa, Kwa upande wake Innocent David Pesa amewashauri wazazi na walezi juu ya athari za utumikishwaji wa mtoto, Maadhimisho ya mwaka huu yanaenda Sambamba na kauli mbiu isemayo “Haki za Jamii kwa Wote, Tokomeza utumikishwaji wa Mtoto” 

Habari za UN
Hatua zichukuliwe kutokomeza taka za plastiki: UN

Habari za UN

Play Episode Listen Later Jun 5, 2023 0:03


Ikiwa leo ni siku ya mazingira duniani Umoja wa Mataifa imetoa wito kwa kila mtu kusaidia vita ya kutokomeza plastiki kwa faida ya mustakbali wa mazingira ya dunia na viumbe vyake.Maudhui ya siku ya mazingira mwaka huu ni “tokomeza taka za plastiki” utajiuliza   kwa nini? Jibu analo Inger Anderson mkurugenzi mtendaji wa shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa mazingira duniani UNEP kupitia ujumbe wake wa siku hii anasema ni, “Kwa sababu taka za plastiki Kwa sababu zinasonga mifumo yetu ya ikolojia, zinapasha joto hali ya hewa yetu na kuna uwezekano mkubwa wa kuharibu afya zetu. Urejelezaji sio mazingaombwe. Mifumo yetu haiwezi kuhimili. Mabadiliko lazima yafanyike katika mzunguko mzima wa maisha wa plastiki. Ni lazima kukataa vitu visivyo vya lazima vya matumizi ya mara moja. Tupange upya bidhaa na vifungashio ili kutumia plastiki kidogo, tutumie tena, turejeleze, tuelekeze upya na tubadilishe mifumo yetu.”Amesema kwa njia hiyo ndio Dunia itaweza kuengua plastiki katika mifumo ya ikolojia na uchumi na hilo amsisitiza ni jukumu la kila mtu,  “ Kila mtu lazima atimize wajibu wake. Serikali zinaweza kutoa matokeo madhubuti kwenye mpango huo wa kukomesha uchafuzi wa plastiki kwa majadiliano. Biashara zinaweza kuchukua mtazamo mpya, sekta ya fedha inaweza kuweka mtaji wake katika kusongesha mabadiliko, na wananchi wanaweza kutumia sauti, kura na pochi zao kuleta mabadiliko.Naye Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres akiunga mkono wito huo amesema, “Kila mwaka, zaidi ya tani milioni 400 za plastiki huzalishwa duniani kote - theluthi moja ambayo hutumiwa mara moja tu. Kila siku, zaidi ya lori 2000 za takataka zilizojaa plastiki hutupwa katika bahari, mito na maziwa yetu. Matokeo yake ni janga. Chembechembe za plastiki huishia kwenye chakula tunachokula, maji tunayokunywa, na hewa tunayopumua.”Ameongeza kuwa plastiki imetengenezwa kutokana na nishati ya kisukuku na kadiri tunavyozalisha plastiki zaidi, ndivyo mafuta ya kisukuku tunavyoyachoma, na ndivyo tunavyofanya mgogoro wa mabadiliko ya tabianchi kuwa mbaya zaidi.Hata hivyo amesema kuna suluhu “Mwaka jana, jumuiya ya kimataifa ilianza kujadili makubaliano ya kisheria ya kukomesha uchafuzi wa taka za plastiki. Hii ni hatua ya kwanza ya matumainii, lakini tunahitaji kila hatua kutekelezwa.”Ameongeza kuwa ripoti mpya ya UNEP inaonyesha, “tunaweza kupunguza uchafuzi wa taka za plastiki kwa asilimia 80 ifikapo mwaka 2040 ikiwa tutachukua hatua sasa kurejeleza, kuchakata tena, kuelekeza upya, na kutenganisha plastiki.”Kwa mantiki hiyo amesisitiza “Ni lazima tufanye kazi kama kitu kimoja, serikali, kampuni na watumiaji kwa pamoja  ili kuondokana na uraibu wetu wa matumizi ya plastiki, kuchagiza kutokuwa na taka za plastiki na kujenga uchumi wa kweli. Kwa pamoja, tutengeneze maisha safi, yenye afya na endelevu zaidi kwa wote.”Siku ya mazingira duniani huadhimishwa kila mwaka Juni 5.

Habari za UN
05 JUNI 2023

Habari za UN

Play Episode Listen Later Jun 5, 2023 0:13


Jaridani hii leo tunaangazia siku ya mazingira duniani na ukiukwaji haki dhidi ya watoto walio katika migogoro inayotumia silaha. Makala tunakuletea uchambuzi wa Ibara ya Tatu ya Tamko la Umoja wa Mataifa la Haki za binadamu, na mashinani tunakupeleka nchini Kenya kusikia ujumbe kutoka kwa mwanaharakati wa mazingira kuhusu taka za plastiki.Ikiwa leo ni siku ya mazingira duniani Umoja wa Mataifa imetoa wito kwa kila mtu kusaidia vita ya kutokomeza plastiki kwa faida ya mustakbali wa mazingira ya dunia na viumbe vyake.    Zaidi ya matukio laki tatu ya ukiukwaji haki dhidi ya watoto walio katika migogoro inayotumia silaha yamethibitishwa na Umoja wa Mataifa kati ya mwaka 2005 na 2022, hicho kikiwa ni kielelezo tosha cha athari mbaya za vita na migogoro kwa Watoto, imeeleza taarifa ya shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto, UNICEF iliyotolewa.Makala, katika kuadhimisha miaka 75 ya Tamko la Umoja wa Mataifa la Haki za binadamu tunaendelea na uchambuzi wa wa Ibara kwa Ibara na leo tunamulika Ibara ya Tatu ya Tamko hilo inayosema Kila mtu ana haki ya kuishi, haki ya kuwa huru na kulindwa . Na mchambuzi wetu ni Getrude Dyabene Afisa Mwandamizi wa Dawati la Jinsia kutoka Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu nchini Tanzania, LHRC akihojiwa na Assumpta Massoi wa Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa, jijini New York, Marekani..Na katika mashinani Nasenya Kutoka Kenya, ambaye ni Muigizaji na pia Balozi Mwema wa Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa mazingira duniani UNEP anasema anaamini kwamba tunaweza kukomesha uchafuzi wa mazingira unaosababishwa na taka za plastiki.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, Karibu!

Habari za UN
31 MEI 2023

Habari za UN

Play Episode Listen Later May 31, 2023 0:11


Hii leo katika jarida Anold Kayanda anamulika kwa kiasi kikubwa siku ya kutokomeza matumizi ya tumbaku duniani halikadhalika hatua ya kupunguza mgao wa chakula kwa wakimbizi walioko nchini Tanzania.Ikiwa leo ni siku ya kupinga matumizi ya tumbaku duniani shirika la Umoja wa Mataifa  la afya duniani WHO, limezitaka nchi kuacha kutoa ruzuku kwa kilimo cha tumbaku na badala yake kuunga mkono na kusaidia kilimo cha mazao endelevu yatakayoweza kulisha mamilioni ya watu wenye uhitaji wa chakula.Zaidi ya wakimbizi 200,000 walioko nchini Tanzania wataanza kupokea nusu mgao wa chakula wanachopatiwa kutokana na ukata unaokabili shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula duniani, WFP. Asilimia 70 ya wakimbizi hao wanatoka Burundi ilhali asilimia 30 wanatoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC.Makala: Harakati za mkulima Sprina Robi Chacha, wa nchini Kenya za kuondokana na kilimo cha tumbaku na sasa analima maharage. Ameshinda tuzo ya shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ulimwenguni, WHO.Mashinani: Harakati huko Cabo Verde za kukabiliana na uvutaji wa sigara

Habari za UN
WHO: Watu milioni 8 hupoteza maisha kila mwaka kutokana na tumbaku:

Habari za UN

Play Episode Listen Later May 31, 2023 0:02


Ikiwa leo ni siku ya kupinga matumizi ya tumbaku duniani shirika la Umoja wa Mataifa  la afya duniani WHO, limezitaka nchi kuacha kutoa ruzuku kwa kilimo cha tumbaku na badala yake kuunga mkono na kusaidia kilimo cha mazao endelevu yatakayoweza kulisha mamilioni ya watu wenye uhitaji wa chakula. Kupitia ujumbe wake wa siku hii mkurugenzi mkuu wa WHO Dkt. Tedros Ghebreyesus amesema “Tumbaku inawajibika kwa vifo milioni 8 kila mwaka  lakini bado serikali duniani kote zitatumia mamilioni ya dola kuunga mkono mashamba ya tumbaku. Watu duniani kote wanakabiliwa na njaa wakati ekari milioni 300 za dunia yetu zinatumika kulima tumbaku.”Akaenda mbali zaidi na kusistiza kwamba “Ni wakati wa kubadili mwelekeo wa juhudi zetu na kujikita na kilimo ambacho kinastawisha siha yetu na mazingira yetu.”Hivi sasa kwa mujibu wa WHO zaidi ya watu milioni 300 duniani kote wanakabiliwa na changamoto kubwa ya kutokuwa na uhakika wa chakula wakati ambapo Zaidi ya ekari milioni 300 katika nchi zaidi ya 120 duniani zinatumika kulima tumbaku hata kwenye nchi ambazo watu wana njaa kali.WHOWHO imesema tumbaku inagharimu maisha wa watu milioni 8 kila mwaka.Dkt. Tedros amesema WHO inafanyakazi kwa karibu na mashirika mengi ya Umoja wa Mataifa likiwemo la chakula na kilimo FAO na la mpango wa chakula duniani WFP kuwasaidia wakulima kuhamia kwenye kilimo mbadala wa tumbaku kwani “kwa kuchagua kulima chakula badala ya tumbaku tutatoa kipaumbele kwa afya, kulinda mfumo wa maisha na kuimarisha uhakika wa chakula kwa wote.”Lengo la maadhimisho ya mwaka huu ni kuujulisha umma hatari za matumizi ya tumbaku, mwenendo wa biashara wa makampuni ya tumbaku, nini kinachofanywa na WHO kupambana na janga la tumbaku na nini watu duniani kote wanaweza kufanya ili kudai haki yao ya afya,  maisha yenye afya na kuvilinda vizazi vijavyo.Siku ya kupinga matumizi ya tumbaku duniani huadhimishwa kila mwaka Mei 31 na mwaka huu imebeka maudhui “Lima chakula sio tumbaku.”  

Habari za UN
UNAIDS: Ili kutokomeza ukimwi ifikapo 2030 kila mtu lazima ajumuishwe hata watumia mihadarati

Habari za UN

Play Episode Listen Later May 8, 2023 0:04


Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na vita dhidi ya ukimwi UNAIDS limesema ili kuhakikisha ukimwi unatokomezwa ifikapo mwaka 2030 basi kila mtu anapaswa kujumuishwa katika vita hivyo ikiwemo wafungwa na wanaotumia mihadarati, kwani Mifumo mingi ya magereza inajitahidi kukabiliana na msongamano, rasilimali duni, ufikiaji mdogo wa huduma za afya na huduma zingine za msingi, vurugu na matumizi ya dawa za kulevya.Nchini Moldova, gereza namba 16 la Pruncul moja ya magereza ambako UNAIDS inashirikiana na serikali na mamlaka za afya kuhakikisha wafungwa na hasa wanaotumia mihadarati wanapata huduma za kudhibiti virusi vya ukimwi au VVU na kukabiliana na athari za matumizi ya mihadarati.Shirika hilo linasema mwaka 2021, idadi ya wafungwa magerezani duniani kote iliongezeka kwa asilimia 24 ikilinganishwa na mwaka wa 2020 hadi kufikia zaidi ya watu milioni 10.Kwa mujibu wa takwimu za ofisi ya Umoja wa Mataifa ya dawa za kulevya na uhalifu UNODC katika baadhi ya nchi hadi asilimia 50 ya watu walio gerezani hutumia au hujidunga dawa za kulevya ambayo ni moja ya sababu kubwa ya maambukizi ya magonjwa yatokanayo na damu kama vile VVU na hepatitis C.Moldova ni miongoni mwa nchi zilizathirika na matatizo haya kwani tangu mwaka2000, ni magereza machache tu nchini humo yaliyokuwa yakitoa huduma za kupunguza madhara. Lakini sasa kwa msaada wa UNAIDS magereza yote 17 yana huduma na mfungwa yeyote mpya katika jela za nchi hiyo anawajibika kumuona daktari wa magonjwa ya akili, na daktari wa kawaida kwa vipimo na ikihitajika basi anajumuishwa katika mpango wa matibabu.Mfungwa Alexander Godin ni miongoni mwa waathirika anapitia katika milango kadhaa iliyofungwa katika gereza namba hili huku akisindikizwa na mlinzi hadi kwenye duka la dawa gerezani hapo. Hii ni sehemu ya utaratibu wake wa kila siku. Anakuja kuchukua dawa yake ya maji ya methadone baada ya kuacha uraibu wa dawa za kulevya, "Nimekuwa kwenye matibabu mbadala ya methadone kwa miaka 10. Familia yangu ilifanya uamuzi huu. Kabla ya hapo, nilitumia dawa za kulevya, afuni. Kwa hili, pesa zilihitajika, na hapo ndipo shida zilianza katika familia. Familia ilipendekeza niende kujiorodhesha kwenye zahanati inayotoa matibabu na tangu hapo nimekuwa kwenye mpango huo.” Methadone ni tiba inayosaidia watu kukabiliana na dalili za athari za mihadarati, msongo wa mawazo, kupunguza utegemezi wa heroini na kuzuia maambukizi ya VVU kutoka kwenye sindano zenye maambukizi.Maria Potrimba, mkuu, idara ya magonjwa ya kuambukiza, Gereza hapa anasema "Ikiwa mgonjwa yuko kwenye matibabu haya mbadala, anafahamu zaidi kuhusu athari na anazingatia zaidi matibabu yake."Maambukizi ya VVU ni asilimia 11 kati ya watu wanaojidunga dawa za kulevya nchini Moldova ambao ni zaidi ya asilimia 0.36 ya watu wote. Na ni moja ya makundi yaliyoathirika zaidi nchini humo.Svetlana Plamadeala, ni mkurugenzi wa UNAIDS nchini Moldova amasema, "Nchini Moldova mzigo wa VVU ni mkubwa zaidi miongoni mwa makundi muhimu na pia huathiri wafungwa. Ofisi UNAIDS nchini humu iliunga mkono serikali kufanya majaribio ya programu za kupunguza madhara na matibabu ya mbadala wa afyuni magerezani tangu mapema mwaka wa 2000. Leo tunasherehekea ukweli kwamba tumepanua wigo wa huduma hizo kutoka kwenye mradi wa majaribio hadi kwenye mfumo mzima wa magereza au kila gereza lina huduma hizo. Ni katika kutoa kipaumbele kwa watu na pia ni kuhusu mtazamo wa afya ya umma.”UNAIDS, na washirika wengine wa Umoja wa Mataifa kwa muda mrefu wamekuwa wakiunga mkono kupanua huduma hizi kwenye magereza yote.Kwa sasa, kulingana na Harm Reduction International, ni nchi 59 pekee duniani ndio zinazotoa huduma hizo katika magereza yake.

Habari za UN
05 MEI 2023

Habari za UN

Play Episode Listen Later May 5, 2023 0:12


Jaridani leo tunaangazia siku ya urithi duniani hasa barani Afrika na wakimbizi wa Sudan. Makala tunakupeleka nchini Sudan Kusini na mashinani nchini Tanzania, kulikoni?Ikiwa leo ni siku ya uruthi wa dunia wa Afrika, shirika la elimu, sayansi na utamaduni la Umoja wa Mataifa UNESCO linasema urithi huo ambao thamani yake ya kipekee inaadhimisha leo, bado haujatambuliwa kulingana na umuhimu wake wa kihistoria, wa kibinadamu na wa asili. Maelfu ya watu wamevuka na kuingia Sudan Kusini wakikimbia mzozo unaoendelea nchini Sudan. Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) liko linawasaidia wanaowasili lakini mzigo huu wa ziada unaweka shinikizo katika shughuli za shirika hilo ambazo tayari ziko katika hali mbaya ya ufadhili.Makala tutakupeleka nchini Sudan Kusini ambapo katika Chuo Kikuu cha Juba nchini Sudan Kusini, kulifanyika mashindano ya sanaa yakihusisha wanafunzi 20 kutoka chuo hicho. Maudhui yalikuwa ni Amani Yaanza Nami yakienda sambamba na miaka 75 ya operesheni za ulinzi wa amani kwenye Umoja wa Mataifa.Na katika mashinani na tutakupeleka Kasulu mkoani Kigoma nchini Tanzania kusikia ujumbe wa mwanafunzi wa shule kuhusu haki ya maji safi na salama.Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!