POPULARITY
Leo ikiwa ni siku ya kimataifa ya kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake, Je wajua kwamba wanawake na wasichana 140 walifariki dunia kila siku duniani kote mwaka 2023 wakiwa mikononi mwa wapenzi wao au ndugu wa karibu, ikimaanisha kuwa mwanmake mmoja anauawa katika kila dakika 10. Na zaidi ya yote bara la Afrika linaongoza? Maudhui ya siku hii yanasema “Hakuna kisingizio” cha ukatili dhidi ya wanawake lama alioushuhudia Ester manusura kutoka Uganda, ambaye kwa miaka mingi amekuwa akifanyiwa ukatili na mpenzi wake anaema “Nilikuwa na umri wa miaka 15 aliponioa naye alikuwa na miaka 28wakati mwingine alikuwa akinivua nguo zote na kunilazimisha kukaa kwenye varandana nilikuwa nikichelewa kurudi ananitandika nje nyumba kila mtu kushuhudia Nilikuwa katika hali mbaya ya uchungu Mkubwa na kuvuja damu.”maadhimisho ya mwaka huu yanaambatana na ripoti iliyotolewa leo jijini New York, Marekani na mashirika ya Umoja wa Mataifa likiwemo lile la masuala ya wanawake, UN Women na Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kudhibiti Dawa za kulevya na Uhalifu, (UNODC), inaangazia mwanga wa janga la mauaji ya wanawake na kutoa wito kwa hatua za dharura ili kukabili janga hilo.Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres katika ujumbe wake wa siku hii inayoadhimishwa tarehe 25 mwezi Novemba kila mwaka, ikiashiria pia kuanza kwa siku 16 za kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake, zikiwa na kilele chake tarehe 10 mwezi Desemba, siku ya Haki za Binadamu duniani amesema “Janga la ukatili dhidi ya wanawake na wasichana linaaibisha ubindamu, dunia lazima iitikie wito huu. Tunahitaji hatua za dharura kwa ajili ya haki na uwajibikaji, na kusaidia uchechemuzi.”Mkurugenzi mtendaji wa UN Women Sima Bahous amesisitiza kuwa “Ukatili dhidi ya wanawake na wasichana si kwamba hauepukiki, unaweza kuzuilika. Tunahitaji sheria thabiti, ukusanyaji bora wa takwimu, uwajibikaji zaidi wa serikali, utamaduni wa kutovumilia, na kuongezeka kwa ufadhili kwa mashirika ya kupigania haki za wanawake na taasisi. Tunapokaribia kuadhimisha miaka 30 ya Azimio la Beijing na Jukwaa la Utekelezaji mwaka 2025, ni wakati wa viongozi wa dunia kuungana na kuchukua hatua kwa haraka, kujitolea na kuelekeza rasilimali zinazohitajika kumaliza mgogoro huu mara moja na kwa wote”Mauaji ya wanawake yanavuka mipaka, hali ya kiuchumi na kijamii, utamaduni. Hata hivyo kiwango au ukubwa wake unatofautiana.Kwa mujibu wa ripoti hiyo, bara la Afrika lilivunja rekodi ya kuwa na viwango vya juu vya wanawake kuuawa na wapenzi wao au mwanafamilia. Wanawake 21,700 waliuawa Afrika mwaka huo wa 2023, ikifuatiwa na bara la Amerika na kisha Oshenia.Mashirika ya UN Women na…
Zaidi ya watu 20,000 wamekimbia makazi yao katika mji mkuu wa Haiti Port-au-Prince katika muda wa siku nne tu, ikiwa ni pamoja na watu wengine zaidi ya 17,000 wanaohifadhiwa katika makazi 15 ya wakimbizi wa ndani, kutokana na kuongezeka kwa ghasia za magenge ya uhalifu ambazo ziumevuruga kabisa minyororo muhimu ya usambazaji wa misaada na kulitenga jiji la Port-au-Prince (POTOPRINSI) limesema shirika la Umoja wa Mataifa la uhamiaji IOM. Kupitia taarifa iliyotolewa leo na IOM nmini Port-au-Prince asilimia kubwa ya watu hawa waliofurushwa makwao wametawanywa zaidi ya mara moja wakilazimika kukimbia na kuacha kila kitu walichokuwa nacho na shirikika hilo linasema kiwango hiki cha watu kutawanywa hakijashuhudiwa Haiti tangu Agost 2023.Shirika hilo linasema kufungwa kwa usafiri wa anga kufuatia shambulizi lililolenga ndege tatu za kibiashara mjini Port-au-Prince, kuzuia ufikiaji wa bandari kuu ya nchi hiyo, na barabara zisizo salama zinazodhibitiwa na makundi yenye silaha kumeliacha eneo la Katikati ya mji mkuu taabani na kutengwa bila msaada na hivyo kuzidisha mateso kwa watu ambao tayari wako hatarini.Mkuu wa IOM nchini Haiti Grégoire Goodstein ameonya kwamba "Kutengwa kwa Port-au-Prince kunaongeza janga la ibinadamu. Uwezo wetu wa kutoa misaada umewekwa njiapanda na bila msaada wa haraka wa kimataifa, mateso yataongezeka sana kwa raia wa Haiti huku kukiwa na asilimia 20 pekee ya mji wa Port-au-Prince inayofikika, wakati wafanyakazi wa misaada ya kibinadamu wanakabiliwa na changamoto kubwa katika kufikia watu walioathirika.”Kulingana na Ofisi ya Haki za Kibinadamu ya Umoja wa Mataifa OHCHR, vikundi vya uhalifu katika mji mkuu wa Hati vinaendelea kupanuka wigo vikichukua udhibiti wa vitongoji vya ziada na kutenganisha zaidi jamii.Hadi sasa ofisi hiyo inasema ghasia zinazohusiana na magenge zimesababisha karibu vifo 4,000 mwaka 2024, unyanyasaji wa kijinsia, ikiwa ni pamoja na unyanyasaji wa kingono unaotumiwa kama silaha ya ugaidi, umefikia viwango vya kutisha.Pia imesema wanawake na watoto wameathiriwa kupita kiasi, huku asilimia 94 ya wanawake na wasichana waliokimbia makazi yao wakiwa katika hatari kubwa ya kudhulumiwa kingono.Licha ya changamoto hizi, IOM na washirika wake wameahidi kuendelea kutoa msaada wa kuokoa maisha.IOM pia inatoa wito wa kuongeza haraka ufadhili kwa shughuli za kibinadamu Haiti kwani hadi kufikia mwezi huu wa Novemba, ombi la dola milioni 674 la Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Haiti limefadhiliwa kwa asilimia 42 pekee, na kuwaacha mamilioni ya watu bila msaada wanaohitaji.
Katika makala haya tunajadili kinachoendelea katika mataifa mengi ya Afrika kuendelea kushuhudia ukosefu wa ajira miongoni mwa vijana, hii likichangia kwa kiasi kikubwa uhalifu. Je Wewe unafanya nini ili kupata riziki ya kila siku ?Ndilo swali tumekuulizaHaya hapa baadhi ya maoni yako.
Katika makala haya tunajadili kinachoendelea katika mataifa mengi ya Afrika kuendelea kushuhudia ukosefu wa ajira miongoni mwa vijana, hii likichangia kwa kiasi kikubwa uhalifu. Je Wewe unafanya nini ili kupata riziki ya kila siku ?Ndilo swali tumekuulizaHaya hapa baadhi ya maoni yako.
Ikiwa leo ni siku ya mwisho ya maonesho ya picha yaliyoandaliwa na Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York Marekani, Anold Kayanda anatupitisha katika picha hizo zinazoonesha athari mbalimbali kwa wanadamu kutokana na uhalifu unaotekelezwa katika maeneo mbalimbali duniani.Maonyesho haya yanachunguza uhusiano wa pamoja unaooneshwa katika simulizi za watu kutoka hali zote ambapo ICC imeanzisha uchunguzi. Maonesho haya pia yanaangazia baadhi ya wapokeaji wa kwanza wa maagizo ya malipo ya ICC.Ingawa simulizi hizi zinatoka katika mabara manne, zina ufanano mwingi. Watu wanapoteza nyumba, ardhi na familia zao. Pia zinaonesha jinsi jamii ni muhimu katika kujenga upya maisha. Kwako Anold
Matangazo ya saa nzima kuhusu habari za kutwa, ikiwa ni pamoja ripoti kutoka kwa waandishi wetu sehemu mbali mbali duniani na kote Afrika Mashariki na Kati, na vile vile vipindi na makala maalum kuhusu afya, wanawake, jamii na maendeleo.
Matangazo ya nusu saa kuhusu habari za mapema asubuhi pamoja na habari za michezo.
Kwenye Makala haya Ali Bilali akiwa pamoja na wachambuzi wa siasa Mali Ali kutoka Paris Ufaransa na Abdulkarim Atiki wanaangazi kuhusu tuhuma za Burundi kwa Rwanda kuhusika na vitendo vya uhalifu hususan uvurumishaji guruneti katika mji wa Bujumbura, tukio la hivi karibuni liligharimu maisha ya watu kadhaa na kuwajeruhi wengine.
Matangazo ya nusu saa kuhusu habari za mapema asubuhi pamoja na habari za michezo.
Mahakama ya Kenya siku ya Jumatatu ilisitisha kwa muda mpango wa serikali wa kutuma polisi nchini Haiti kwenye operesheni inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa inayolenga kurejesha utulivu katika taifa hilo linalokabiliwa na changamoto kubwa ya magenge.
Matangazo ya nusu saa kuhusu habari za mapema asubuhi pamoja na habari za michezo.
Kwa Undani ni matangazo ya dakika 25 yanayochambua habari kwa undani zaidi na kumpa msikilizaji maelezo ya kina kuliko ilivyo kawaida kuhusu tukio au swala lililojitokeza katika habari.
Kwa Undani ni matangazo ya dakika 25 yanayochambua habari kwa undani zaidi na kumpa msikilizaji maelezo ya kina kuliko ilivyo kawaida kuhusu tukio au swala lililojitokeza katika habari.
Uhalifu wa utambulisho ni tisho kubwa nchini Australia, ambako kuna ongezeko ya idadi ya watu wanao endelea kuwa waathiriwa wa uhalifu wa utambulisho kila mwaka.
Makala haya yanazungumzia kuhusu mbinu ya Rangi ambayo wanabodaboda kaunti ya Mombasa wanatumia kutofautisha sehemu wanazohudumu kama njia moja ya kukabiliana na visa vya uhalifu. Makala yametayarishwa na Ruth Keah.
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina tukimulika ukuaji wa lugha ya Kiswahili nchini Rwanda. Na habari kwa ufupi kutoka nchini Thailand, Ukraine na DR Congo. Katika kujifunza lugha ya Kiswahili Dkt. Josephat Gitonga atafafanua maana ya methali “Usishindane na kari, kari ni mja wa Mungu”. Katika mkutano wa kimataifa kuhusu Ukimwi unaoendelea huko Thailand, washiriki wamepitisha makubaliano ya kutambua nafasi kubwa ya jamii katika kukabili janga la UKIMWI wakisema hatua zinazoongozwa na jamii ziwe rasmi au si rasmi ni lazima zipewe kipaumbele kwenye ufadhili.Mkuu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu misaada ya dharura, OCHA, Martin Griffiths ametamatisha ziara yake ya siku nne nchini Ukraine na kutaja mambo makuu matatu muhimu ya kupatiwa kipaumbele kuwa ni mosi; kurejesha umeme kwenye makazi, pili kutegua mabomu yaliyoko kwenye makazi ya watu na tatu, ni kuchechemua shughuli za kiuchumi ili maisha yaweze kuendelea na kwamba Umoja wa Mataifa uko tayari kusaidia. John Bosco Ntaganda, kiongozi wa zamani wa waasi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo aliyehukumiwa kifungo cha miaka 30 jela na Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu, ICC mwezi Novemba mwaka 2019 baada ya kupatikana na hatia ya makosa 18 ya uhalifu wa kivita na uhalifu wa kibinadamu huko Ituri jimboni, DRC amewasili nchini Ubelgiji tayari kuanza kutekeleza adhabu yake kwenye gereza la Leuze-en-Hainaut nchini humoNa katika kujifunza Kiswahili Dkt. Josephat Gitonga atafafanua maana ya methali “USISHINDANE NA KARI, KARI NI MJA WA MUNGU”.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, Karibu!
Hii leo katika Habari za UN Assumpta Massoi anamulika masuala ya haki, wakimbizi, maendeleo na afya.Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Haki za Kibinadamu Volker Türk ameipongeza serikali ya Kenya kwa kile alichoeleza ni hatua muhimu ya kuelekea uwajibikaji kwa ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu nchini Kenya, kufuatia uamuzi wake wa wa kutumia Sheria ya Uhalifu wa Kimataifa kuwafungulia mashitaka maafisa wakuu wa polisi kwa mauaji, ubakaji na utesaji kama uhalifu dhidi ya ubinadamu kufuatia vurugu zilizotokea wakati wa uchaguzi Mkuu wa nchi hiyo mwaka 2017.Kamishna Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR, Filippo Grandi ambaye amezuru Kenya ameshuhudia ni kwa kiasi gani miradi inayoIenga wakimbizi na wenyeji inasaidia sio tu kuinua vipato vya pande zote bali pia kujenga utangamano, maelewano na amani kwenye makazi ya wakimbizi.Makala hii leo tunaangalia namna wakulima wa viazi lishe huko Mkoani Simiyu Kaskazini mwa Tanzania walivyonufaika na mradi uliofadhiliwa na shirika la Umoja wa Mataifa la maendeleo ya mitaji UNCDF na kupata ufumbuzi wa changamoto kubwa ya kukosa soko la mazao yao.Mashinani: Falassa Sissoko, mtoa chanjo dhidi ya COVID-19 katika mji wa Logo Sabouciré jimboni Kayes nchini Mali. Anasafiri akiwa na kasha lenye chanjo dhidi ya COVID-19.Karibu!
Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Haki za Kibinadamu Volker Türk ameipongeza serikali ya Kenya kwa kile alichoeleza ni hatua muhimu ya kuelekea uwajibikaji kwa ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu nchini Kenya, kufuatia uamuzi wake wa wa kutumia Sheria ya Uhalifu wa Kimataifa kuwafungulia mashitaka maafisa wakuu wa polisi kwa mauaji, ubakaji na utesaji kama uhalifu dhidi ya ubinadamu kufuatia vurugu zilizotokea wakati wa uchaguzi Mkuu wa nchi hiyo mwaka 2017. Leah Mushi anataarifa zaidi.Taarifa iliyotolewa hii leo huko Geneva, Uswisi na ofisi ya Umoja wa Mataifa ya haki za binadamu imemnukuu Kamishna Mkuu wa Umoja wa Matifa wa Haki za binadamu Volter Turk akipongeza Kenya na kusema hii ni mara ya kwanza kwa Kenya kutumia Sheria ya Kimataifa ya Uhalifu kushtaki uhalifu dhidi ya ubinadamu katika mahakama zake za ndani.Kwa mujibu wa taarifa hiyo, wakati wa uchaguzi mkuu wa Kenya mwaka 2017, Tume ya Taifa ya Haki za Kibinadamu ilirekodi vifo 94 na matukio 201 yakihusiana na unyanyasaji wa kingono na zaidi ya majeruhi 300 wengi wao wakieleza kufanyiwa vitendo hivyo na vikosi vya usalama.Bwana Turk amesema “Uamuzi uliochukuliwa leo na Kenya ni wa msingi, ni hatua nzuri kuelekea haki na uwajibikaji kwa waathirika na familia za waathirika, wa ghasia za uchaguzi, na inaweza kuimarisha na kuzuia ukiukaji wa haki za binadamu kwa siku zijazo.”Amebainisha kuwa uamuzi huo wa Kenya unatokana na maendeleo ya hivi karibuni ya taasisi za Kenya zinazoungwa mkono na Ofisi yake ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Kibinadamu katika kuimarisha uwajibikaji kwa ukiukaji wa haki za binadamu.Kamishna Mkuu Türk amesema ofisi yake itaendelea kujitolea kuendelea kuunga mkono juhudi za Serikali ya Kenya kuendeleza uwajibikaji kwa ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu, ikiwa ni pamoja na kushughulikia mauaji ya kiholela na kulazimisha watu kutoweka.
Nchini Haiti, ambako karibu nusu ya idadi ya watu tayari hawana uhakika wa chakula, njaa inatazamiwa kuongezeka huku kukiwa na ongezeko la mfumuko wa bei, gharama kubwa za chakula na mafuta na kuzorota kwa usalama, linaonya Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani, WFP ingawa linaendelea kutoa msaada kwa Wahaiti walio katika mazingira hatarishi. Anold Kayanda ameaingazia hali hiyo na hii ni taarifa yake. Kupitia video zilizochukuliwa kutoka angani zikionesha Port-au-Prince, mji mkuu wa Haiti ulivyo tulia ufukweni mwa bahari, ni vigumu kwa mtu kujua kuwa hali si shwari hadi unaposhuka chini mitaani. (Nats) Ni maandamano. Wengine wamebeba mabango, wengine bendera na wengine matawi ya miti. Wanadai amani na usalama dhidi ya vurugu za magenge ya uhalifu. Polisi wameweka vizuizi vya ukaguzi lakini katika baadhi ya maeneo yanayosemwa kuwa ngome za magenge, unaweza kusikia milio ya risasi mchana kweupe. Kwingine watu wanaonekana wamekusanyika kwenye vituo vya mafuta na midumu. Uhaba wa mafuta unaosababishwa na magenge ya wahalifu kukata njia kuu za kufikia Port au Prince sasa unachangiwa na kupanda kwa bei ya mafuta duniani kote kutokana na mgogoro wa Ukraine. Vituo vingine hata vimefungwa kwa kukosa mafuta. Licha ya vikwazo, WFP nchini Haiti imekuwa ikiisaidia Serikali kwa misaada ya kibinadamu na maendeleo ili kukabiliana na chanzo cha njaa na inapanga kuwasaidia watu milioni 1.7 mwaka huu wa 2022. WFP inaimarisha mnepo wa Wahaiti na kuimarisha ulinzi wa kijamii na mifumo ya chakula. Jean-Martin Bauer ni Mkurugenzi wa WFP nchini Haiti anasema, (Sauti ya Jean-Martin Bauer) "Kwanza kabisa magenge na athari zao katika biashara ya masoko na maisha vimesababisha ongezeko la uhaba wa chakula. Bei za juu za vyakula za kimataifa pia zinachangia janga la chakula hapa nchini. Ili kutatua, WFP imezindua huduma ya baharini, tuna feri inayochukua misaada kutoka hapa hadi katika maeneo mengine ya nchi. Pia tuna huduma ya anga, helikopta inayosafirisha misaada kutoka hapa hadi sehemu zote za Haiti.” Ingawa WFP inajitahidi kuokoa maisha, kwa muda wa miezi sita ijayo, inakabiliwa na upungufu wa ufadhili wa dola za Marekani milioni 39 kwa ajili ya kutimiza shughuli zake nchini Haiti.
Mwandishi wetu wa Kenya, Jason Nyakundi anafanya mahojiano na Wango Michael kutoka shirika la Reformers Sports and Community Services kwenye mtaa wa Kayole mjini Nairobi. Shirila la Reformers sports and community Services huwasaidia vijana kuacha uhalifu na kufanya mambo ya kujitegemea maishani.
Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa imeonya kwamba mashambulizi yanayofanywa na kundi la wapiganaji la ADF Mashariki wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, yanaweza kuwa ni uhalifu wa vita na uhalifu dhidi ya ubinadamu. Assumpta Massoi na taarifa zaidi Kwa mujibu wa ripoti ya ofisi hiyo ya haki za binadamu iliyotolewa leo mjini Geneva Uswis mashambulizi ya kundi hilo dhidi ya raia yameshika kasi katika miezi 18 iliyopita na kupanua wigo wake hata katika maeneo ambayo hapo awali hawakuwepo.
New Zealand's Prime Minister has described multiple shootings in Christchurch as causing "one of New Zealand's darkest days." - Waziri Mkuu wa New Zealand amesema mashambulizi kwa bunduki mjini Christchurch, kuwa yame sababisha moja ya siku mbaya zaidi nchini New Zealand.
Two of National Australia Bank's (NAB) most senior figures, CEO Andrew Thorburn and Chairman Ken Henry, have announced their departures from the bank. - Viongozi wawili maarufu wa benki ya National Australia Bank (NAB), mkurugenzi mtendaji mkuu Andrew Thorburn na mwenyekiti Ken Henry, wametangaza wanajiuzulu kutoka uongozi wa benki hiyo.
Gunmen have blasted their way into a luxury hotel and office complex in Nairobi, Kenya. - Magaidi wame vamia hoteli yaki fahari, pamoja na jengo lenye maofisi mjini Nairobi, Kenya.
Mission Europe - Mission Berlin | Kujifunza Kijerumani | Deutsche Welle
Anna anaelekea Kantstraße lakini anachelewa kwa kuwa inambidi kuulizia njia. Anapoteza muda zaidi wakati watu wenye pikipiki wanapofika na kumfyatulia risasi. Kazi ya Anna inakabiliwa na vikwazo. Anapowataka watoto waliyovaa vitau vyenye magurudumu kumwelekeza njia, wenye pikipiki wanampiga risasi. Mchezo unapoanzishwa tena, hatimaye Anna anawasili Kantstraße. Lakini je atapata anachotafuta?
Mission Europe - Mission Berlin | Kujifunza Kijerumani | Deutsche Welle
Muda unayoyoma na Anna anamuaga Paul kabla ya kurejea tarehe 9 Novemba mwaka 2006. Atakapowasili atakuwa amebakiwa na dakika tano pekee. Je zitatosha? Huku zikiwa zimesalia dakika chache Anna akamilishe jukumu lake, mchezaji anamshauri kutumia fursa ya zogo lililopo kuondoka pole pole. Lakini hataki kuondoka bila kumuaga Paul sawasawa. Anna anachunguza mchezo na kugundua anahitaji ufunguo uliochakaa kutekeleza jukumu lake. Anaitaji pia muziki. Je atarejea kwa wakati ufaao kutekeleza wajibu wake? Amesalia na dakika 5 pekee ili akamilishe vizuri jukumu lake.
Mission Europe - Mission Berlin | Kujifunza Kijerumani | Deutsche Welle
Anna analipata kasha la chuma lililofichwa katika mwaka 1961 lakini hawezi kulifungua kwa kuwa limechakaa. Anapofanikiwa kulifungua anapata ufunguo wa zamani. Je huo ndio ufunguo wa ufumbuzi wa siri? Muda unayoyoma na Anna ni lazima afungue kasha la chuma. Lakini mchezaji anamtahadharisha kutolifungua mbele ya watu. Analifungua kasha hilo na kupata ufunguo wa zamani uliochakaa. Sasa anatakiwa kurudi mwaka 2006 ili akabiliane na mwanamke mwenye mavazi mekundu. Lakini ana muda wa kutosha?
Mission Europe - Mission Berlin | Kujifunza Kijerumani | Deutsche Welle
Anna anadandia skuta ili afike barabara ya Bernauer. Mhisani wake ni Emre Ogur anayemtakia ufanisi mjini Berlin. Lakini atahitaji nini zaidi kumkimbia mwanamke mwenye mavazi mekundu ili apate kasha la chuma lililofichwa? Mchezaji anamwambia Anna kutafuta usafiri wa kwenda barabara ya Bernauer kwa kuwa muda unamtupa mkono. Anadandia skuta inayoendeshwa na kijana mmoja, ambaye siku za usoni ni Inspekta Emre Ogur. Lakini Anna anapokutana na Heidrun Drei na Paul, mwanamke mwenye mavazi mekundu anawasili.Paul na Robert, mume wake Heidrun Drei, wanamrushia vipande vya ukuta. Wakati huo huo Anna anakimbia kwenda kuopoa kasha la chuma. Lakini je litakuwepo bado baada ya miaka yote hiyo?
Mission Europe - Mission Berlin | Kujifunza Kijerumani | Deutsche Welle
Anna anapelekwa mwaka 1989 na anafika katika jiji ambalo lina kizaazaa cha kuanguka Ukuta. Anahitajika kupitia umati mkubwa wa watu ili apate kasha la chuma lililofichwa. Je atafanikiwa? Anna anapotaka kuondoka kuelekea mwaka 1989, waendesha pikipiki wanajitokeza. Mwanamke mwenye mavazi mekundu analiamuru kundi lake kumsaka Anna. Anamtaka Anna akiwa hai. Anna anaingia kwenye mtambo wa wakati na anarudi mjini Berlin mwaka 1989 wakati jiji hilo limezama kwenye shamrashamra za kuanguka ukuta. Lakini yuko katika lango la Brandenburg ambapo kila mtu anasherehekea. Anna anapaswa kwenda katika barabara ya Bernauer. Kwa dakika 30 zilizobaki, je anaweza kuharakisha kuuvuka umati wa mamilioni ya watu katika jiji hilo ambalo hapo awali lilikuwa limegawanyika?
Mission Europe - Mission Berlin | Kujifunza Kijerumani | Deutsche Welle
Anna anarejea mwaka 2006 na anagundua, mchungaji Kavalier ametekwa nyara. Kwa kuwa hana uwezo wa kujua aliko mchungaji, Anna anaelekea tisa Novemba, 1989, usiku ambao Ukuta wa Berlin ulianguka. Mwaka 2006, Paul anamwambia Anna kuwa mchungaji ametoweka. Mwanamke mwenye mavazi mekundu amemteka nyara. Paul bila shaka anajua mambo mengi kumuhusu Mchungaji Kavalier na mtambo wa wakati, lakini hana muda wa kuzungumzia hayo. Anna anakubali kuelekea usiku wa tarehe 9 Novemba mwaka 1989 wakati wakazi wa Berlin walipokuwa wakisherehekea kuanguka kwa Ukuta. Anataka kuliopoa kasha kutoka katikati ya kundi la watu.
Mission Europe - Mission Berlin | Kujifunza Kijerumani | Deutsche Welle
Anna bado hajapata ufumbuzi wa kitendawili chake. Tukio gani la kihistoria RATAVA inataka kuzuia? Mchezaji anamwambia kurejea mwaka 2006 na kisha kurudi tena mwaka 1989. Je harakati hizo zina hatari kiasi gani? Kabla ya Anna kurejea mwaka 2006, anataka kuagana vizuri na Paul. Ana muda wa dakika 35 kukamilisha jukumu lake na inambidi kuchunguza ajue tukio ambalo kundi la RATAVA linataka kusimamisha. Anna na mchezaji wanagundua kuwa kundi la RATAVA halizingatii ujenzi wa ukuta bali kuanguka kwake. Mchezaji anamwambia kwanza arudi mwaka 2006 kisha aende mwaka 1989 wakati ukuta ulipoanguka.
Mission Europe - Mission Berlin | Kujifunza Kijerumani | Deutsche Welle
Zimesalia dakika 40 na Paul na Anna wanamkimbia mwanamke mwenye mavazi mekundu wanafika Berlin Magharibi. Lakini ni upande usioafiki. Mambo yanazidi kutatizika wakati Paul anapomwambia Anna kwamba anampenda. Anna anatakiwa kuwa Berlin Mashariki ili afanikiwe kutekeleza jukumu lake. Lakini amekwama upande wa magharibi. Kisha kuna tatizo jingine: Katika hali ngumu kama hiyo, Paul anamwambia Anna kuwa anampenda. Anamtaka Anna kuacha kutekeleza jukumu lake. Hata hivyo mchezaji anamwambia Anna kurudi mwaka 2006 ili aanzishe mpango mwingine. Dakika 35 zitatosha kupata suluhisho?
Mission Europe - Mission Berlin | Kujifunza Kijerumani | Deutsche Welle
Anna anagundua kuwa mwanamke mwenye mavazi mekundu ndiye mkuu wa RATAVA. Dakika 45 zimebaki za kuinusuru Ujerumani na kidokezo alicho nacho Anna ni kasha lililofichwa. Je atalipata na kuweza kukamilisha jukumu lake? Heidrun Drei, Paul na Anna wanaelekea barabara ya Bernauer na njiani wanakutana na Robert, mume wake Heidrun Drei. Anawaarifu kuwa wanajeshi wametapakaa kila mahali: Zaidi ya hayo, wenye pikipiki nao wamejitokeza. Anna na wenzake wanajificha kwenye uwa wa mkahawa wa zamani. Mwanamke mwenye mavazi mekundu anajitokeza na Paul anamwambia Anna kuwa mwanamke huyo ndiye kiongozi wa RATAVA. Mchezaji anamwambia Anna kumfuata kiongozi huyo. Anna na Paul wanakwenda kwenye selo ambako wanamshuhudia mwanamke huyo akificha kasha. Wanachukua kasha lile na kulificha katika sehemu nyingine na kisha kukimbia. Mchezaji anasema atafikiria njia ya kulipata tena. Lakini kwa dakika 40 zilizobaki, atakuwa na muda wa kutosha?
Mission Europe - Mission Berlin | Kujifunza Kijerumani | Deutsche Welle
Huku zimesalia dakika 50, mchezaji anasema wakati umefika wa kumwamini keshia. Taarifa ya redio inasema wanajeshi wa Ujerumani Mashariki wanajenga uzuio wa seng'enge. Je hilo ndilo tukio la kihistoria la RATAVA? Anna hajatambua kuwa keshia ni Heidrun Drei na mchezaji anamwambia amwamini keshia huyo anayetaka kumsaidia hata kama kaka yake ana shaka. Hata hivyo ndugu hao wawili wanakubaliana kumsaidia Anna kulikwepa genge la waendesha pikipiki. Wote watatu wanakwenda kuwachungulia wanajeshi wa Ujerumani Mashariki ambao wanaanza kujenga uzio wa seng'enge. Mchezaji anamwambia Anna kuwa huo ni ujenzi wa Ukuta wa Berlin. Zimebaki dakika 45 kuinusuru Ujerumani.
Mission Europe - Mission Berlin | Kujifunza Kijerumani | Deutsche Welle
Anna anaporudi nyuma hadi mwaka 1961, waendesha pikipiki wenye silaha bado wanamwandama. Mwanamke fulani asiyemjua anamwokoa. Kwa nini akafanya hivyo? Je Anna anaweza kumwamini? Genge la waendesha pikipiki linamwandama Anna. Anajificha kwenye duka la kuuza vyakula na wakati huo huo msimamizi wa duka anamwambia kwamba wakati wa kufunga duka umefika. Msaidizi wake anasema kuwa Anna ni rafiki yake. Keshia huyo anamchukua Anna hadi nyumbani kwake na anamwambia kwamba walisoma pamoja. Nyumbani kwake, keshia anamjulisha Anna kwa Paul Winkler, ambaye ni kaka yake.
Mission Europe - Mission Berlin | Kujifunza Kijerumani | Deutsche Welle
Anna anagundua mtambo wa wakati na anaambiwa kuwa genge la magaidi linataka kufuta tukio la kihistoria. Lakini tukio lipi? Mchezaji anamrejesha hadi mwaka 1961. Anasalia na dakika 60. Je amwamini mchungaji? Mchungaji anajua maana ya msemo "In der Teilung liegt die Lösung" na anaelewa hatari ya genge la RATAVA. Mchezaji anasema Anna anapaswa kurudi hadi mwaka 1961 ili kufumbua fumbo hilo. Mchezaji anaahidi atamrejesha Anna alikotoka pindi akifika mwaka huko. Mchungaji anampa msemo "Die Liebe versetzt Berge",…"Mapenzi husogeza milima"… ambao unamsaidia kurejea nyuma. Anaanzia tarehe 13 Agosti lakini akiwa na dakika sitini kutekeleza jukumu lake. Je muda huu unatosha?
Mission Europe - Mission Berlin | Kujifunza Kijerumani | Deutsche Welle
Katika Berlin iliyogawanyika, Anna anapaswa kutoka Mashariki kwenda Magharibi. Hilo silo tatizo la pekee. Ana muda wa dakika 55 kuchunguza lengo la RATAVA. Je ni ujenzi au kubomolewa ukuta? Mwaka 1961, Anna anajaribu kufika Kantstraße. Lakini Kantstraße iko Berlin Magharibi na yeye yuko Berlin Mashariki. Anna hawezi kwenda Magharibi kwa sababu serikali ya Ujerumani Mashariki imeanza kujenga ukuta. Baada ya kuanzishwa upya kwa mchezo, mchezaji na Anna wanagundua kuwa huenda malengo ni mawili: ujenzi au kubomolewa Ukuta wa Berlin. Wanabakiwa na dakika 55 kuchunguza kujua lengo la RATAVA.
Mission Europe - Mission Berlin | Kujifunza Kijerumani | Deutsche Welle
Kanisa linakuwa mahali pa kupata mwongozo. Mchungaji anamweleza Anna kuhusu sauti na kwamba sautii hiyo ni ufunguo wa mtambo wa wakati. Lakini anazungumzia kifaa gani? Mchezo unapoanzishwa tena, Anna na mwanamke mwenye mavazi mekundu wanagombana lakini mwanamke huyo anakimbia pindi mchungaji anapowasili. Anamwarifu Anna kwamba Inspekta Ogur amejeruhiwa na anajiuguza hospitalini. Mchungaji anaicheza tena sauti hiyo tena na kumwambia kwamba sauti za muziki D A C H F E G ndizo ufunguo wa mtambo huo. Ugunduzi huo unampa Anna na mchezaji dakika kumi za nyongeza. Lakini muda huo utatosha?
Mission Europe - Mission Berlin | Kujifunza Kijerumani | Deutsche Welle
Anna amebakiwa na dakika 65. Anatambua kuwa kikasha cha muziki ndicho sehemu inayokosekana kwenye kinanda cha kanisa. Mwanamke mwenye mavazi mekundu anajitokeza na kudai apewe ufunguo. Ufunguo gani? Anna anasikia wimbo anaoufahamu. Kinanda cha kanisa kinatoa mirindimo sawa na ile ya kwenye kikasha cha muziki. Wakati Anna anapokikaribia kinanda anamsikia mtunza kanisa akimweleza mgeni kuwa kinanda hicho kimerekebishwa ila kinakosa kipande kimoja…ein Element.. tangu ukuta ulipojengwa. Anna anatambua kuwa kikasha ndicho kiungo kinachokosekana na anakibandika kwenye kinanda. Kinanda kinapoanza kupiga, mlango unafunguliwa na anajikuta akiwa amekabiliana na mwanamke mwenye mavazi mekundu. Anatokwa na uhai mwingine na anasaliwa na dakika 60 pekee.
Mission Europe - Mission Berlin | Kujifunza Kijerumani | Deutsche Welle
Anna anamweleza Paul kuhusu msemo usioleweka, "In der Teilung liegt die Lösung. Folge der Musik!" Paul anatambua hatari iliyopo. Anamshauri Anna kumwendea Mchungaji Markus Kavalier. Je pendekezo lake ni sawa? Paul anatambua kuwa sauti iliyopo kwenye kikasha cha muziki haipigi mpaka mwisho wake. Kipande fulani kinakosekana. Anna anamwambia kuhusu ujumbe usioeleweka, "In der Teilun liegt die Lösung; folge der Musik!" Paul anampa "die Spieldose" na anamshauri kwenda kumwona Mchungaji Markus Kavalier katika kanisa la Gethsamane. Mchezaji anamwambia Anna kuwa mahali hapo palikuwa eneo la mikutano ya wapinzani wa utawala wa zamani wa Kikomunisti.
Mission Europe - Mission Berlin | Kujifunza Kijerumani | Deutsche Welle
Mchezaji anazijumuisha tarehe 13 Agosti, 1961, siku ya kujengwa ukuta wa Berlin na tarehe 9 Novemba, 1989 wakati ukuta ulipoanguka. Mafanikio ya Anna kwenye jukumu lake yanategemea tarehe hizo. Anna afanye nini? Paul na Anna wanajificha katika duka kubwa la KaDeWe ambako Anna anacheza mchezo wake. Mchezaji anamwambia Anna kuwa ukuta wa Berlin ulijengwa tarehe 13 Agosti, 1961 na ukaanguka tarehe 9 Novemba, 1989. Anna atagundua kuwa ufumbuzi wa fumbo lote hilo ni kugawanywa kwa Berlin.
Mission Europe - Mission Berlin | Kujifunza Kijerumani | Deutsche Welle
Anna anakimbia kutoka ukumbi wa maonyesho lakini mwanamke mwenye mavazi mekundu anamuwahi katika duka la Paul. Anna anafanikiwa tena kukimbia na kidokezo kimoja cha fumbo hilo na vipi apate kidokezo kingine? Ogur amemdokeza Anna kuhusu kundi la majambazi la RATAVA . Kwenye duka la saa, Paul Winkler anamwonyesha kwamba amekitengeneza kikasha chake cha muziki. Kinapiga wimbo uitwao "Nostagie" wa Friedrich August Dachfeg. "Ni wimbo wetu", Paul anamwambia Anna lakini Anna haelewi. Ghafla mwanamke mwenye mavazi mekundu anajitokeza na kufyatua risasi. Heidrun Drei anawasili na kupambana na mwanamke huyo ili kuwapa Paul na Anna fursa ya kukimbia. Anna amebakiwa na tarehe mbili: Agosti 13, 1961 na Novemba 9. Lakini mwaka gani?
Mission Europe - Mission Berlin | Kujifunza Kijerumani | Deutsche Welle
Ogur anamwarifu Anna kuhusu mpango muovu wa genge la RATAVA linalotaka kubadilisha historia. Kabla ya kupoteza fahamu, Inspekta Ogur anampa Anna tarehe. Novemba 9. Lakini mwaka gani? Ogur, anayeshuku kuwa Anna amejificha mahali fulani kwenye ukumbi, anamwagiza Anna kutoroka. Mwanamke mwenye mavazi mekundu anampiga Anna risasi na kumtoa uhai mara nyingine. Mchezo unaanzishwa tena na Ogur anamwambia Anna kuwa RATAVA ni kundi la majambazi wanaotaka kubadilisha historia. Ingawa Ogur amejeruhiwa, anampa kidokezo cha tarehe, Novemba 9. Lakini mwaka gani?
Mission Europe - Mission Berlin | Kujifunza Kijerumani | Deutsche Welle
Anna analikwepa genge la waendesha pikipiki na kuingia kwenye ukumbi wa maonyesho. Huko anakutana tena na Heidrun, na Ogur anamwambia kuwa RATAVA wanamwandama. Lakini wanamtakia nini? Mchezaji anamwambia Anna kurejea dukani kwa Paul Winkler kuchukua kikasha chake cha muziki. Njiani inambidi kulikwepa genge la waendesha pikipiki kwa kuingia kwenye ukumbi wa maonyesho. Huko anakutana tena na Heidrun Drei. Inspeka Ogur anawasili kumhoji Heidrun Drei kuhusu aliko Anna. Ogur anakisia kuwa Anna kajificha kwenye ukumbi huo na anamtahadharisha kwamba genge la RATAVA linamwandama. Wakati huo mwanamke aliyevalia mavazi mekundu anawasili.
Mission Europe - Mission Berlin | Kujifunza Kijerumani | Deutsche Welle
Anna anakutana na mtu mwingine anayeonekana kama anayefahamiana naye. Mara hii ni mwanamke anayesema walikuwa marafiki mwaka 1961. Anna anazidi kutatizika kwa habari kwamba kuna mwanamke anamwandama. Watu ambao Anna hawafahamu wanajitokeza kila pembe. Mara hii ni mwanamke. Anasema yeye na Anna waliishi chumba kimoja mwaka 1961 na kwamba anataka kumsaidia Anna kutekeleza jukumu lake la hatari. Heidrun Drei anamtahadharisha Anna kujichunga na mwanamke aliyevaa mavazi mekundu ambaye anamwandama. Lakini Heidrun Drei hayo yote ameyajulia wapi?
Mission Europe - Mission Berlin | Kujifunza Kijerumani | Deutsche Welle
Anna anakipeleka kikasha chake cha muziki kwa mtengeza-saa ili kitengenezwe. Paul Winkler anaikubali kazi hiyo na kumwambia Anna kuwa anamjua tangu kitambo. Inawezekana vipi? Anna ndio kwanza amewasili. Kikasha cha muziki kinapofunguliwa, kinaonekana kimeharibika zaidi. Paul Winkler anapata kipande cha karatasi kilichoandikwa tarakimu hizi 19610813. Zina maana gani? Na je Paul Winkler anazungumzia nini? Anna anamuomba amtengeneze saa, naye anasema wanajuana tangu kitambo. Katika hali hii ya butwaa, Anna anajitahidi kuokoa muda na ana dakika 90. Amefuata muziki kama maandishi yalivyopendekeza lakini nini maana ya "mgawanyiko ndio suluhisho"?
Mission Europe - Mission Berlin | Kujifunza Kijerumani | Deutsche Welle
Jukumu la Anna ni kuinusuru Ujerumani isifikwe na janga. Ni lazima aihifadhi siri, atengue kitendawili, na kuwachunguza wanaume wenye pikipiki. Anahitaji dakika 130. Dalili ya kwanza i wapi? Anna anaamka katika chumba namba 14 … Zimmer vierzehn, kwenye mkahawa mmoja nchini Ujerumani. Wakati huo huo Kamanda wa Polisi anaelekea chumbani kwa Anna. Kamanda Ogur anajitambulisha na anagusia mauaji ya mgeni kwenye chumba nambari 40. Zimmer vierzig. Kwenye kioo cha bafu anatambua maandishi "In der Teilung liegt die Lösung. Folge der Musik". Anna anaanza kujibu maswali ya kamanda. Lakini maandishi hayo yana maana gani?
Mission Europe - Mission Berlin | Kujifunza Kijerumani | Deutsche Welle
Anna anaanza kujibu maswali ya Ogur lakini anakatizwa na sauti ya pikipiki pamoja na milio ya risasi. Anakimbilia kwenye makumbusho anakopata anwani juu ya kasha lake la muziki. Je anwani hii itamfaa? Anna anajificha kwenye jumba la makumbusho. Anajificha ndani ya choo cha wanaume kwa kuwa ana wasiwasi huenda polisi au wenye pikipiki walio na silaha wangali wanamwandama. Hapo anagundua anwani ya Leo Winkler katika barabara ya Kantstraße iliyoandikwa kwenye kasha lake la muziki. Je huyo bwana yu hai na je anaweza kumsaidia Anna?