POPULARITY
Hii leo jaridani tunaangazia machafuko ya muda mrefu nchini Myanmar, hali ya kibinadamu nchini Sudan kufuatia ripoti za vifo vya raia na wimbi la wakimbizi wa ndani, na masuala ya afya nchini Kenya.Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres, ametoa wito kwa dunia na mataifa wanachama wa Jumuiya ya Nchi za Kusini-Mashariki mwa Asia, ASEAN kuchukua hatua za haraka kumaliza machafuko ya muda mrefu nchini Myanmar, akisisitiza kuwa mgogoro huo si tishio kwa watu wa Myanmar pekee bali pia kwa amani na usalama wa kanda nzima ya Asia ya Kusini Mashariki.Ofisi ya Uratibu wa Misaada ya Kibinadamu ya Umoja wa Mataifa (OCHA) imeelezea wasiwasi mkubwa kufuatia ripoti za vifo vya raia na wimbi la wakimbizi wa ndani, kufuatia kuendelea kwa mapigano makali katika mji wa El Fasher, huko Darfur Kaskazini nchini Sudan. Tupate tarifa zaidi kutoka kwa Leah Mushi.Katika kaunti ya Mombasa nchini Kenya, Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) kwa kushirikiana na wa Mastercard Foundation na Serikali ya Kaunti ya Mombasa, imechukua hatua za kukabiliana na mlipuko wa MPOX kwa kutoa huduma muhimu za afya na WASH kwa wagonjwa na waliopona, ikiwa ni pamoja na vifaa vya kujikinga (PPEs), vituo vya kusafisha mikono na ujumbe wa mabadiliko ya tabia za kijamii.Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!
Katika kaunti ya Mombasa nchini Kenya, Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) kwa kushirikiana na wa Mastercard Foundation na Serikali ya Kaunti ya Mombasa, imechukua hatua za kukabiliana na mlipuko wa MPOX kwa kutoa huduma muhimu za afya na WASH kwa wagonjwa na waliopona, ikiwa ni pamoja na vifaa vya kujikinga (PPEs), vituo vya kusafisha mikono na ujumbe wa mabadiliko ya tabia za kijamii. Sheilah Jepngetich na taarifa zaidi
Mashirika matatu ya Umoja wa Mataifa na serikali ya Kenya wanatekeleza mradi unaowashirikisha wananchi wa Kauti ya Samburu katika kuhakika kuna upatikanaji wa chakula kwani eneo hilo linahali ya ukame ikiwa ni hatua mojawapo ya kutafsiri na kutekeleza malengo ya maendeleo endelevu ya Umoja wa Mataifa SDGs huko mashinani. Tuungane na Sheilah Jepngetich anayetuletea tarifa hii iliyoandaliwa na UNICEF Kenya.
Kaunti ya Kirinyaga, iliyoko katikati mwa nchi ya Kenya kaskazini mwa mji mkuu wa nchi hiyo, Nairobi, inashuhudia mageuzi mapya katika sekta ya kilimo kupitia mradi wa kuwahusisha vijana katika kilimo na lishe unaojulikana kama EKYAN. Mradi huu unatekelezwa kwa ushirikiano kati ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto UNICEF, na wadau nchini humo. Karibu Sabrina Saidi utupe taarifa zaidi.....(TAARIFA YA SABRINA SAIDI)Mradi wa EKYAN ni mfano wa ujasiriamali wa kilimo unaoongozwa na vijana, ukiwa na lengo la kutengeneza fursa za ajira, kuwanufaisha na kubadilisha maisha ya vijana walioko vijijini, kupitia mbinu bora za kilimo na lishe, ukitekelezwa kwa ushirikiano kati ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto UNICEF, serikali ya kaunti ya Kirinyaga na shirika linalotoa mafunzo, elimu ya biashara ndogo ndogo na uwezeshaji barani Afrika KUZA Biashara.Felista Nyakio Mutungi kijana mkulima wa kaunti ya Kirinyaga, ni mmoja wa wanufaika wa mafunzo kupitia mradi huo. Na hapa anasema....CUT 2- Sauti ya Felista Nyakio Mutungi“Kabla ya kuanza kilimo, nilikuwa nauza barabarani viazi vya kukaanga au chipsi, na mihogo, pamoja na nafaka. Haikuwa vizuri sana, lakini ndiyo nafasi pekee niliyokuwa nayo wakati huo. Kupitia serikali ya kaunti ya Kirinyaga, tulisajiliwa kama vijana wanaopenda kilimo na tukapata mafunzo kupitia KUZA na UNICEF. Sasa mimi ni mkulima na mjasiriamali.”Felista anasema awali alikuwa akilima robo ekari ya mpunga na kuvuna magunia manne hadi matano pekee. Lakini baada ya mradi wa EKYAN, kwa robo ekari hiyo hiyo sasa anapata hadi magunia saba. Aidha, shamba lake limepanuka hadi ekari nne katika eneo la 'mradi wa umwagiliaji wa Bura.Felista hakutaka kuwa mchoyo wa manufaa aliyopata, hivyo ameamua kueneza ujuzi wa kilimo cha kibiashara kwa kuwafundisha baadhi ya wakulima wengine mbinu na maarifa ya kilimo hiki.CUT- Sauti ya Felista Nyakio Mutungi“Sasa si tu kwamba nalima, bali pia nawafundisha wakulima wengine kuongeza thamani katika mazao yao. Wanapata ujuzi wa kufanya biashara kupitia kilimo. Na kwa kweli tunawashukuru wahisani na UNICEF kwa kutuwezesha. Bila mpango huu, nisingekuwa hapa nilipo leo.”Kwa upande wake mtaalamu wa ubunifu wa UNICEF nchini Kenya Lilian Njoro, anaeleza kwa nini mradi huo ni muhimu kwa vijana.CUT- Sauti ya Lilian Njoro."Ni asilimia 10 pekee ya vijana wanaojihusisha na sekta ya kilimo. Kwa hivyo, kupitia mradi wa EKYAN, tulitaka kuona jinsi ya kuwahusisha vijana wengi zaidi katika kilimo na kuwavutia ili waweze kuanza kupata maisha yenye utulivu na ajira bora kupitia sekta hii.”Njoro anasisitiza kuwa teknolojia mpya zinafungua njia kwa kilimo cha kisasa tofauti na enzi za wazazi na mababu zao.Namna kilimo kinavyofanyika nyakati hizi ni tofauti na zamani,hii ni kwa sababu ya uwepo wa teknolojia bunifu, majukwaa ya kidijitali, na fursa nyingi.Kwa sasa, mradi wa EKYAN umeendelea kuwajengea vijana ujuzi, kuwapatia nafasi ya ajira, na kubadilisha mtazamo wao kuhusu kilimo, kutoka shughuli ya kizamani hadi kuwa biashara yenye faida.Link: https://youtu.be/hv17nk-2l5kTAGS:UNICEF Kenya/Kilimo/Biashara na ujasiriamali
Jaridani hii leo tunaangazia hakiza binadamu nchini Uganda, na mahakama ya kuhamama kwa ajili ya amani Sudan Kusini. Makala tunaangazia vijana na mpango wa wa kuwa wazazi siku zijazo, na mashinani tunakwenda nchini Kenya kumulika vijana wakulima.Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Binadamu, (OHCHR), imesema kitendo cha kiongozi wa upinzani nchini Uganda Kizza Besigye pamoja na mshirika wake Obeid Lutale kunyimwa dhamana mara kwa mara katika kesi inayowakabili ni jambo linalotia hofu kubwa. Assumpta Massoi na maelezo zaidi.Mahakama ya kuhamahama iliyopelekwa katika eneo la utawala la Greater Pibor, Kaunti ya Pibor jimboni Jonglei Mashariki mwa Sudan Kusini imeleta haki na amani kwa kiasi kikubwa katika eneo hilo.Makala wakati hapo jana dunia iliadhimisha siku ya kimataifa ya vijana duniani, shirika la Umoja wa Mataifa la afya ya uzazi na idadi ya watu UNFPA liliwahoji vijana iwapo wangependa kuwa na watoto hapo baadaye.Na katika mashinani fursa ni yake Emily, mwanachama wa kikundi cha vijana wakulima nchini Kenya wanaolima mbogamboga kupitia mradi uliofanikishwa na shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula WFP wa kilimo cha bustani.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
Mahakama ya kuhamahama iliyopelekwa katika eneo la utawala la Greater Pibor, Kaunti ya Pibor jimboni Jonglei Mashariki mwa Sudan Kusini imeleta haki na amani kwa kiasi kikubwa katika eneo hilo. Anold Kayanda anatupasha kwa kina
Jaridani leo tunaangazia waandishi wa habari waliouawa katika ukanda wa Gaza, na wakimbizi wa Burundi huko Tanzania. Makala inamulika maendeleo na ustawi kwa wakimbizi Kakuma nchini Kenya na mashinani inatupeleka katika kaunti ya Tana River nchini humo, kulikoni?Kufuatia kuuawa kwa waandishi sita wa habari huko Gaza, viongozi wa mashirika mbalimbali ya Umoja wa Mataifa wamekosoa vikali shambulio hilo lililotekelezwa na majeshi ya Israel usiku wa kuamkia leo.Moja ya changamoto kubwa wanazokutana nazo wakimbizi pale wanapokaa nchi waliyopatiwa uhifadhi kwa muda mrefu ni kukosa nyaraka muhimu za utambulisho. Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya wakimbizi UNHCR limekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha wanapata suluhu ya changamoto hii. Makala inamulika mnufaika wa Jamii Biashara ambalo ni jukwaa la mtandaoni la masoko lililobuniwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kazi duniani, (ILO) na Chama cha Wafanyabiashara na Viwanda Kenya, (KNCCI). Jukwaa hili limefungua fursa kwa wakimbizi wanaoshughulika na biashara ndogo ndogo ili kujikimu maisha katika kambi ya wakimbizi ya Kakuma nchini Kenya. Assumpta Massoi ndiye mwenyeji wako kupitia video ya ILO.Na katika mashinani fursa ni yake Mariam Kazungu kutoka Kaunti ya Tana River nchini Kenya, ambaye anasema Watoto wake wamenufaika kupitia mradi wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF wa utoaji wa chanjo dhidi ya homa ya tumbo na ugonjwa wa surua.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
Umoja wa Mataifa kwa kutambua nafasi ya urafiki katika kujenga amani, utulivu na kusongesha maendeleo kuanzia ngazi ya mtu mmoja mmoja hadi ngazi ya mataifa, mwaka 2011 kupitia Baraza lake Kuu, ulitenga Julai 30 kuwa siku ya urafiki duniani. Umoja wa Mataifa unasema katika wakati ambapo kelele za mgawanyiko zinazidi kuwa kubwa — zikiendeshwa na vita, migogoro, ukosefu wa usawa, na hofu — urafiki unaonekana kuwa wa kishujaa kutokana na unyenyekevu wake. Urafiki huanza na kitu cha utulivu zaidi: mazungumzo, wakati wa pamoja, utayari wa kuonana si kama wageni bali kama wasafiri wenza katika safari ya utu. Je huko Kenya, mkazi mmoja wa Kaunti ya Kajiado, urafiki kwake ni nini? Kelvin Keitany wa Redio washirika Radio Domus amefunga safari na kutuandalia makala hii.
Hii leo jaridani tunaangazia masuala ya malengo ya maendeleo endelevu, na mradi wa uvuvi unaosaidia kupunguza migogoro Ituri DRC. Makala tunakupeleka nchini Tanzania na mashinani nchini Kenya, kulikoni?Jukwaa la Kisiasa la Ngazi ya Juu la Maendeleo Endelevu, HLPF la mwaka huu wa 2025 limeanza leo hapa katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani ambapo wadau kutoka katika nyanja mbalimbali duniani wanakutana kujadili namna ya kuharakisha utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu, SDGs.Kutoka msituni kupigana upande wa waasi hadi kuingia ziwani na kuwa mtaalamu wa ufugaji wa samaki, ndio simulizi tunayopata kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, simulizi ya matumaini kwa mustakabali wa jamii iliyogubikwa na vita kila uchao.Katika makala tunakupeleka mkoani Mwanza, kaskazini-magharibi mwa Tanzania ambako kuelekea siku ya kimataifa ya vijana na stadi hapo kesho Julai 15, Sabrina Said anazungumza na mmoja wa vijana anayetumia majukwaa ya kidijitali kutoa elimu ya uelimishaji rika.Na kaika mashinani leo fursa ni yake Imam Ustaadhi Matano Bin Salim kutoka Kaunti ya Mombasa nchini Kenya, ambaye amewezesha shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF kufika kwenye kituo cha mafunzo ya dini kupatia watoto chanjo. Akisema typhoid ni homa ya tumbo, na measles ni ugonjwa wa surua.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
Hii leo jaridani tunaangazia masuala ya afya nchini Burundi, na elimu ya upatanishi kwa jamii Ituri nchini DRC. Makala tunakupeleka nchini Kenya kumulika kilimo kichopatia riziki jamii na mashinani tunasalia hapa makao makuu kusikia ujumbe kuhusu haki za wasichana.Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani (WHO) leo Julai 11 limetangaza kwamba limeidhinisha Burundi kuwa imefanikiwa kuoandoa ugonjwa wa macho unaofahamika kama trakoma au vikope kama tatizo la kiafya la umma, na kuifanya kuwa nchi ya nane katika Kanda ya Afrika ya WHO kufikia mafanikio haya muhimu.Huko Djugu, jimboni Ituri, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, wanawake wapatanishi waliopatiwa mafunzo na ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo, MONUSCO, wamewezesha kurejea kwa mazungumzo baina ya jamii za Ezekere na Mandro ambazo kwa miaka kadhaa zilikuwa zinazozana.Katika makala Sharon Jebichii anatupeleka Kaunti ya Tana River huko Kenya kumulika juhudi za Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo (UNDP) kwa kushirikiana na Mamlaka ya Kitaifa ya Kusimamia Ukame (NDMA) na Serikali za Kaunti katika kilimo, ambayo imeleta mabadiliko na matumaini kwa jamii za wakulima.Na kaika mashinani leo ikiwa siku ya idadi ya watu duniani, nampisha Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu na AFya ya Uzazi, Dkt. Natalia Kanem akizungumzia umuhimu wa takwimu katika kuboresha maisha ya wakazi wa dunia!Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
Katika maeneo kame ya Kenya, mvua moja ikikosa kunyesha, inaweza kuleta njaa, umaskini na kukosa matumaini. Lakini badala ya kukata tamaa, jamii za wakulima katika kaunti za Tana River sasa zinatoa simulizi kwa ujasiri na mabadiliko. Kupitia msaada kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP) kwa kushirikiana na Mamlaka ya Kitaifa ya Kusimamia Ukame (NDMA) na Serikali za Kaunti, wakulima wanatumia teknolojia rafiki kama umwagiliaji wa maji kwa nishati ya jua, kilimo cha kisasa na ushirika wa kijamii kuinua maisha yao. Sharon Jebichii na maelezo zaidi.
Hii leo jaridani tunaangazia haki za binadamu nchini Ukraine na upatikanaji wa elimu nchini Kenya. Makala tunakupeleka nchini Sudan Kusini, na amashinani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, kulikoni?Tume Huru ya Umoja wa Mataifa ya Uchunguzi kuhusu Ukraine imehitimisha kwamba vikosi vya kijeshi vya Urusi vimetenda uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya ubinadamu, hasa mauaji, kupitia mashambulizi ya ndege zisizo na rubani (drones) yaliyoelekezwa dhidi ya raia.Mradi wa "operesheni rejea shuleni" unaoendeshwa na shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia watoto UNICEF kwa ushirikiano na wizara ya elimu ya Kenya, shirika liliso la kiserikali la Hapag Lloyd na wadau wengine kwa kuzipa fedha familia zisizojiweza kuendesha shughuli za kiuchumi, umerejesha mautumaini ya elimu kwa mamia ya watoto katika Kaunti ya Kwale Pwani ya Kenya ambao waliacha shule sababu ya umasikini. Katika makala ikielekea siku ya walinda amani kesho Mei 29, tunamulika harakati za walinda amani wa Umoja wa Mataifa nchini SUdan Kusini za kulinda raia na mwenyeji wako katika makala hii iliyoandaliwa kupitia video ya ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa Kulinda amani Sudan Kusini, UNMISS ni Sharon Jebichii.Na katika mashinani huku machafuko yakiendelea mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, wafanyakazi wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR wako mashinani mjini Goma na maeneo mengine yaliyoathirika ili kutoa msaada muhimu, ikiwa ni pamoja na kufanikisha nia ya wakimbizi wanaorejea nchini mwao Rwanda. Raab na Ruusi ni baadhi yao.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
Mradi wa "operesheni rejea shuleni" unaoendeshwa na shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia watoto UNICEF kwa ushirikiano na wizara ya elimu ya Kenya, shirika liliso la kiserikali la Hapag Lloyd na wadau wengine kwa kuzipa fedha familia zisizojiweza kuendesha shughuli za kiuchumi, umerejesha mautumaini ya elimu kwa mamia ya watoto katika Kaunti ya Kwale Pwani ya Kenya ambao waliacha shule sababu ya umasikini. Flora Nducha na maelezo zaidi.
Kesho ikiwa ni siku ya nyuki duniani ikimulika umuhimu wa nyuki tunakupeleka nchini Kenya, katika kijiji cha Embulmbul, ambapo mradi wa ufugaji nyuki uliofanikishwa na Shirika la Marekani la Misaada ya maendeleo, USAID, kwa kushirikiana na Idara ya Misitu ya Kenya, KFS na wadau wengine, umeleta tija kwa wenyeji. Mmoja wa wanufaika hao ni mwanamazingira Christopher Mureithi ambaye ni kiongozi wa kikundi cha kufuga nyuki katika msitu wa Ololua ambao wamefanikiwa sio tu kuboresha uzalishaji wa asali, bali pia kuchangia katika uhifadhi wa bioanuwai na misitu. Katika makala hii iliyoandaliwa na Sharon Jebichii Bwana Mureithi anaanza kwa kueleza mafanikio yao.
Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF kwa kushirikiana na wadau wameleta neema kwa watoto wanaoishi na ulemavu katika Kaunti ya Kisumu Magharibi mwa Kenya baada ya kuwapa msaada wa vifaa ikiwemo viti mwendo na viungo bandia kupitia mradi wa ubunifu kwa ajili ya watoto wenye ulemavu, msaada uliobadili maisha yao. Flora Nducha amefuatilia tabasamu la mama ambaye mwanye amenufaika na kiungo bandia ungana naye kwa tarifa zaidi
Hii leo jaridani tunaangazia mvutano unaoendelea barani Asia kati ya majirani wawili India na Pakistani, na msaada wa mguu bandia uliowezesha mtototo nchini Kenya kwenda shule. Makala tunakupeleka nchini Tanzania na mashinani tunakwenda katika ukanda wa Gaza.Huko barani Asia majirani wawili India na Pakistani wameendelea kuoneshana mvutano kati yao kwenye eneo la Jammu na Kashmiri tangu tarehe 22 mwezi uliopita wa Aprili baada ya shambulizi huko Pahalgam. Katibu Mkuu ametoa wito kwa mara nyingine tena.Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF kwa kushirikiana na wadau wameleta neema kwa watoto wanaoishi na ulemavu katika Kaunti ya Kisumu Magharibi mwa Kenya baada ya kuwapa msaada wa vifaa ikiwemo viti mwendo na viungo bandia kupitia mradi wa ubunifu kwa ajili ya watoto wenye ulemavu, msaada uliobadili maisha yao.Makala katika wiki ya chanjo duniani, iliyotamatishwa tarehe 30 wiki iliyopita, mtaa wa Butiama, ulioko Mtoni Kijichi katika wilaya ya Temeke, jijini Dar es Salaam, nchini Tanzania ulishuhudia wazazi na walezi wakijitokeza kuwapatia watoto wao chanjo muhimu za kuwalinda dhidi ya maradhi hatari. Miongoni mwao ni Hija Halfani ambaye alimpeleka mtoto wake mwenye umri wa siku 42 kupata chanjo yake ya kwanza.”Na mashinani mashinani, kama sehemu ya juhudi za kutoa nafasi ya kujieleza kisanii na kuwaunga mkono Wapalestina kihisia (emotional support), UNRWA imeandaa maonesho ya sanaa katika Shule ya Al-Rimal, ambayo sasa ni makazi ya wakimbizi wa ndani katika ukanda wa Gaza, na watoto walipata fursa ya kuonesha kazi za sanaa zinazoakisi(reflect) madhila wanayopitia wakati wa vita kati ya Israeli na Hamas ambavyo bado vinaendelea. Malak Fayad, msichana mkimbizi kutoka Beit Hanoun ni mmoja wao akionesha sanaa yake.….Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
Matangazo ya saa nzima kuhusu habari za kutwa, ikiwa ni pamoja ripoti kutoka kwa waandishi wetu sehemu mbali mbali duniani na kote Afrika Mashariki na Kati, na vile vile vipindi na makala maalum kuhusu afya, wanawake, jamii na maendeleo.
Hii leo jaridani tuanaangazia masuala ya ufadhili wa huduma za afya, na kilimo cha cacao nchini Liberia. Makala inatupeleka nchini DRC na mashinani nchini Kenya, kulikoni?Baada ya Serikali ya Marekani kutoa tangazo jipya sasa kwamba itaendelea kufadhili huduma zinazolenga vita dhidi ya Virusi vya Ukimwi (VVU), shirika la Umoja wa Mataifa la kukabiliana na VVU na Ukimwi (UNAIDS) limeeleza kuupokea uamuzi huo kwa furaha na kuuita wa kuokoa maisha.Kilimo bora cha kakao huko Liberia kimemwondolea uchovu na kukosa kulala, mkazi wa kaunti ya Nimba, kaskazini mashariki mwa Liberia, baada ya mradi wa mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Maendeleo ya Kilimo, IFAD nchini humo kumwezesha sio tu kugeukia kilimo, bali pia kuajiri vijana wengine na hivyo kufanikisha lengo la Umoja wa Mataifa la kuondokana na umaskini.Makala inatupeleka kwenye msitu wa bonde la mto Congo nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC wa pili kwa ukubwa duniani unaofyonza kiasi kikubwa cha hewa ukaa, ambako mradi wa Umoja wa Mataifa wa kulinda bayoanuwai na kupambana na umasikini UNREDD unaleta nuru kwa jamii na mazingira.Na mashinani fursa ni yake fursa ni yake Esther Wangoi Mbugua, Mama mfugaji nyuki kutoka Kaunti ya Kajiado nchini Kenya ambaye alizungumza na washirika wetu Redio Domus akieleza kuwa ameweza kujipatia kipato na kumudu mahitaji ya familia yake kupitia mradi wa ufugajji nyuki.Mwenyeji wako niAnold Kayanda karibu!
Hii leo jaridani tunaangazia jitihada za kuudhibiti mlipuko wa ugonjwa wa Maburg nchini Rwanda, na juhudi za kuchunguza virusi vya VVU nchini Ghana. Makala tunakupeleka nchini Kenya na mashinani nchini DRC, kulikoni?Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani (WHO) limeipongeza serikali ya Rwanda kwa kufanikiwa kuudhibiti mlipuko wa ugonjwa wa Maburg. Hii leo Rwanda imetangaza mwisho wa mlipuko wa hivi karibuni wa ugonjwa huo baada ya kutokuwepo maambukizi mapya katika siku 42 na mgonjwa wa mwisho akiwa amepimwa mara mbili bila kukutwa na ugonjwa kama matakwa ya WHO yanavyotaka ili kutangaza kuisha kwa mlipuko wa magonjwa namna hii.Mwaka 2020 Ghana iliripoti kuwa na watu 350,000 wanaioshi na virusi vya Ukimwi na kati yao hao 31,000 walikuwa ni wajawazito. Jambo lililoshtua ni kwamba ni sehemu ndogo mno ya wajawazito hao ndio walipimwa kufahamu iwapo wana VVU au la. Jambo lililofanya serikali kwa kushirikiana na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF kuchukua hatua.Makala inatupeleka kwenye kambi ya wakimbizi ya Kakuma iliyokoko Kaunti ya Turkana Kaskazini Magharibi mwa Kenya kukukutanisha na mkimbizi kutoka Somalia anayetumia mpira wa kikapu anatumia mpira wa vikapu kuhamasisha jamii yake na kupinga mil ana desturi zisizofaa.Mashinani ikiwa leo ni Siku ya Kimataifa ya Mpira wa Kikapu, fursa ni yake Danny Batachoka, mwanariadha wa Paralimpiki kutoka Goma nchini Jamhuri ya kidemocrasia ya Congo, DRC ambaye kupitia video ya ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo MONUSCO, anasema ana ndoto ya kuwa mmoja wa wachezaji wakubwa wa mpira wa vikapu katika kitengo chake.” Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
Makala haya yanazungumzia hatua za wanawake na wasichana katika eneo la Opapo, Kaunti ya Migori nchini Kenya, kwa msaada wa mashirika yasiyo ya kiserikali na serikali ya kaunti, wameanzisha kiwanda cha kuchakata samaki, kuboresha biashara ya samaki, na kuongeza thamani kwa kutengeneza bidhaa kama soseji na baga,hivyo kuinua uchumi
Makala haya yanazungumzia hatua za wanawake na wasichana katika eneo la Opapo, Kaunti ya Migori nchini Kenya, kwa msaada wa mashirika yasiyo ya kiserikali na serikali ya kaunti, wameanzisha kiwanda cha kuchakata samaki, kuboresha biashara ya samaki, na kuongeza thamani kwa kutengeneza bidhaa kama soseji na baga,hivyo kuinua uchumi
Katika miji ya pwani ya Kenya, vita dhidi ya uraibu vimepata mwelekeo mpya wa kusisimua. Kupitia miradi ya kimazingira, vijana kutoka vituo vya kuwarekebisha tabia hawajizuia tu na mihadarati, bali wanabadili jamii zao pia kupitia miradi hiyo. Mwanahabari wetu Victor Moturi alitembelea Mtopanga, Kaunti ya Mombasa, ambako vijana wamepata matumaini kutokana na utunzaji wa mazingira huku wakipata riziki.
Hii leo jaridani tunaangazia mashauriano huko Busan kuhusu matumizi ya plastiki, na ripoti ya UNODC kuhusu UKIMWI na kudhibiti dawa za kulevya katika magereza. Makala inaturejesha Havana Cuba na mashinani inatupeleka nchini Kenya, kulikoni?Vuta nikuvute kwenye mashauriano huko Busan, Korea Kusini kuhusu mkataba wenye nguvu za kisheria dhidi ya uchafuzi utokanao na matumizi ya plastiki na kulinda mazingira ya baharini imefikia ukingoni kwa mkutano kuahirishwa na wawakilishi wa nchi zilizokuwa zinashiriki kuridhia rasimu mpya yenye ibara 32 itakayojadiliwa mwakani.Wakati jana Desemba Mosi Ulimwengu ukiadhimisha Siku ya Kimataifa ya UKIMWI kwa kuhamasisha haki za binadamu ili kufanikisha vita dhidi ya ugonjwa huu hatari, Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya ya Kudhibiti Dawa za Kulevya na Uhalifu (UNODC) inajivunia miaka 25 ya kujiunga na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kukabiliana na UKIMWI (UNAIDS) katika kushughulikia janga la Virusi Vya UKIMWI (VVU) miongoni mwa watu wanaotumia dawa za kulevya na miaka 20 ya kazi ya kupambana na UKIMWI magerezani.Makala leo inamulika jinsi bidhaa za kitamaduni zinavyotumika kukuza na kuendeleza mila na desturi za Kiswahili mkoani Tanga Kaskazini mwa Tanzania. Je ni bidhaa zipi hizo na zinatumika vipi? Tuungane na Flora Nducha aliyeyabaini hayo hivi karibuni alipokuwa Havana Cuba kwenye kongamano la kimataifa la Kiswahili.Na mashinani tunasikiliza manufaa ya ufadhili wa Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Maendeleo ya kilimo, IFAD kwa wakulima kutoka kwake Sharon Kirui kutoka Kaunti ya Nakuru nchini Kenya ambaye ni mnufaika wa vocha za kielektroniki za ununuzi kutoka kwa IFAD na ameweza kupanua biashara yake ya kilimo.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
Hii leo jaridani tunaangazia machafuko katika ukanda wa Gaza na masuala ya afya nchini Kenya. Makala inatupeleka nchini DRC kumsikia mkimbizi mjasiriamali na mnufaika wa pesa taslimu kutoka WFP, na mashinani tunakupeleka nchini Lebanonon kwa waathirika wa vita.Kadri siku zinavyozidi kusonga mbele, hali ya usalama na kibinadamu huko Ukanda wa Gaza inazidi kuzorota huku raia na hata wafanyakazi wa kutoa misaada wakisalia wamepigwa butwaa kwani mashambulizi kutoka Israeli yanaendelea kila uchao.Serikali ya Kaunti ya Lamu katika pwani ya kaskazini ya Kenya, kwa ushirikiano na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF), wanaendesha shughuli ya kuwafikia wanajamii ili kubadilishana taarifa kuhusu jinsi watu wanaweza kuwalinda watoto na familia zao dhidi ya mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu na kutoa huduma za maji, vifaa vya kujisafi na usafi kwa jamii zilizoathirika. Kutoka katika video iliyoandaliwa na UNICEF.Makala George Musubao, mwandishi wetu wa mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC anazungumza na mkimbizi Esther Josephine aliyeko kambi ya Bulengo nje kidogo ya mji wa Goma, jimboni Kivu Kaskazini ambaye amenufaika na msaada kutoka shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula duniani, WFP.Mashinani tutakuwa Lebanon, kumsikia mama aliyenusurika kifo na wanawe kutokana na makombora ya Israel.Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!
Serikali ya Kaunti ya Lamu katika pwani ya kaskazini ya Kenya, kwa ushirikiano na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF), wanaendesha shughuli ya kuwafikia wanajamii ili kubadilishana taarifa kuhusu jinsi watu wanaweza kuwalinda watoto na familia zao dhidi ya mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu na kutoa huduma za maji, vifaa vya kujisafi na usafi kwa jamii zilizoathirika. Kutoka katika video iliyoandaliwa na UNICEF.Wamekaa chini ya mti, wanawake kwa wanaume. Nyuma ni nyumba ya makuti na matumbawe, Lamu, Pwani ya Kenya. Muelimishaji wa masuala ya afya anawaeleza namna ya kuweka mazingira safi ili kupambana na kipindupindu. Mwanajuma Kahidi yamewahi kumkuta. Anaposema Cholera anamaanisha hiyo hiyo kipindupindu iliyokuwa imetishia Uhai wake na familia yake.“Nilipopata maambukizi ya Kipindupindu nilihisi siko sawa kwa sababu nilikosa nguvu na nikakosa raha na nikapoteza nuru ya macho ndio nikakimbilia hospitali. Huo ugonjwa ulipitia kwenye maji na chakula. Mimi na watoto wangu tulipatwa na kipindupindu. Mimi nilichukua siku tatu. Watoto wangu wote mmoja baada ya mwingine walichukua siku nane nane. Madaktari wanajibidiisha sana juu yetu. Baada ya siku kadhaa wanajitokeza na kutuuliza, je mnafanya juhudi tulizowaambia?”Leila Abrar ni Mshauri katika UNICEF anayehusika na mabadiliko ya tabia katika jamii anasema, "kiwango cha ufahamu ni cha juu zaidi kuliko tulipokuwa tunaanza uelimishaji. Na pia tunaambiwa kuwa kiwango cha unawaji mikono kimeongezeka. Mabadiliko ya kijamii na tabia kwa kweli yanahusu kushirikisha jamii, kuwezesha jamii.
Hii leo jaridani tunaangazia janga la nja linalokumba wananchi waathirika wa mizozo nchini Sudan, na simulizi za walinda amani wa UNIFIL nchini Lebanon. Makala tunakupeleka nchini Kenya na mashinani nchini Haiti, kulikoni?Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula duniani, (WFP) leo kwa mara nyingine tena limetahadharisha kwamba bila msaada wa kibinadamu nchini Sudan, mamia ya maelfu wanaweza kufa kwa njaa.Kikosi cha muda cha Umoja wa Mataifa nchini Lebanon, UNIFIL, ambapo, katikati ya mvutano unaoongezeka kati ya Lebanon na Israel, walinda amani walioko katika makao makuu ya UNIFIL huko Naqoura wamekuwa wakivumilia mazingira magumu. Ushuhuda wa hivi karibuni kutoka kwa walinda amani hao unaonesha ukubwa wa changamoto wanazokabiliana nazo, ikiwemo vitisho vilivyoongezeka kutoka kwa shughuli za kijeshi za Israel zilizo karibu na eneo hilo, vizuizi vya kusafiri, na changamoto za uendeshaji wa shughuli.Makala inatupeleka Nairobi Kenya kwa washindi waliotwaa tuzo ya “Mtu Bora wa Mwaka wa Umoja wa Mataifa 2024” ambao ni kampuni ya Craftskills Wind Energy International Limited wamiliki wa mradi wa nishati ya upepo ya Kipeto Energy iliyoko Kaunti ya Kajiado nchini Kenya.Katika mashinani mashinani leo tutakuwa Haiti ambapo nafasi ni yake Andre Rose, mama wa kijana Kerby, akieleza jinsi msaada wa kifedha unaotolewa na Shirika la UNICEF umekuwa mkombozi kwa familia yake iliyolazimika kukimbia makazi yao kutokana na ghasia za magenge ya uhalifu nchini Haiti.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
Kampuni ya Craftskills Wind Energy International Limited wamiliki wa mradi wa nishati ya umeme itokanayo na upepo ya Kipeto Energy iliyoko Kaunti ya Kajiado nchini Kenya wamejitwalia tuzo ya “Mtu Bora wa Mwaka wa Umoja wa Mataifa. 2024”Mkurugenzi mtendaji wa kampuni hiyo anasema ushindi huo ni kwa watu wa Kaunti ya Kajiado nchini Kenya ambao ni wanaufaika wakubwa wa mradi kwani sio tu umewaletea umeme, bali pia umewainua kiuchumi na kijamii kwa miradi mingine mbalimbali kama inabobainisha makala hii iliyoandaliwa na Flora Nducha..
Hii leo jaridani tunaangazia mkutano wa COP16 katika mji wa Santiago de Cali au Cali huko nchini Colombia na ufugaji nyuki Turakana nchini Kenya. Pia tunakupeleka nchini Somalia kufutilia programu wa WFP wa mlo shuleni na mashinani inatupeleka nchini Lebanon.Mkutano wa 16 wa nchi wanachama wa Mkataba wa Kimataifa wa bayonuai (COP16) umeng'oa nanga leo katika mji wa Santiago de Cali au Cali huko nchini Colombia ambapo mataifa 196 yatajadili jinsi ya kusitisha na kubadili mwelekeo wa kudorora kwa ulimwengu wa asili.Kila siku, mamilioni ya watoto kote ulimwenguni huenda shule wakiwa na njaa, wengi wao wakiteseka na utapiamlo sugu ambao huathiri ukuaji wa kiakili na utendaji wao katika masomo. Wanaobahatika huweza tu kumaliza masomo yao na kufanikiwa maishani kutokana na programu ya ‘mlo ya shuleni' inayoendeshwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa chakula Duniani (WFP). Mfano wa wanufaika hao ni El-Khidir Daloum, Mkurugenzi wa sasa wa WFP nchini Somalia.Makala inatupeleka Kaunti ya Turkana Kaskazini mwa Kenya moja ya maeneo kame ambako mradi wa ufugaji nyuki wa WFP umekuwa mkombozi kwa wakulima walioathirika na mabadiliko ya tabianchi.Mashinani fursa ni yake Waffiyah Diyah kutoka Lebanon ambaye ni muathirika wa vita vilivyolazimisha maelfu ya watu kufangasha viragoanaelezea hali ya familia yake baada ya kukimbia mashambulizi na kupoteza kila kitu, lakini sasa anapokea msaada kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji (IOM).Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
Kaunti ya Turkana Kaskazini mwa Kenya moja ya maeneo kame mradi wa ufugaji nyuki wa WFP umekuwa mkombozi kwa wakulima walioathirika na mabadiliko ya tabianchi.Katika kaunti hii vumbi linalotimuka katika eneo tambarare lisilo na miti linakufanya kujiuliza je Nini kizuri kinaweza kufanyika hapa kwenye ukame uliotamalaki? Lakini cha kustaajabisha ni kwamba kwa kuwezeshwa mengi yanawezekana ikiwemo njia bora za kuhakikisha uhakika wa chakula na hata kubadili maisha ya watu kama anavyosema mkulima wa nyuki Nadipo Lotelei mnufaika wa mradi wa mizinga ya nyuki kutoka shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP. “Hatua iliyochukuliwa na WFP kutupatia mizinga ya nyuki imekuja kama nyota ya jaha kwangu kwa sababu siwezi kutembea umbali mrefu kutokana na ajali niliyopata. Mradi huu umenisaidia sana mimi ili kuweza kusaidia watoto wangu na mke wangu. Mke wangu ameweza kuanzisha biashara ya duka kutokana na faida niliyopata ambayo sasa inatumika kama chnzo cha kipato cha mahitaji ya kaya yetu.”Nadipo ni miongoni mwa wafuga nyuki 1,900 katika kaunti ya Turkana ambao wamepewa mafunzo ya ufugaji nyuki na vifaa kupitia mradi wa WFP kwa ushirikiano na shirika binafsi la HIVE ambalo mwenyekiti mtendaji wake ni Christopher Nzuki. “Tunahusika katika ufungaji na usambazaji wa vifaa. Na wakati huohuo tunatoa mafunzo kwa wafugaji nyuki na kisha kuwapatia masoko. Tunachukua kila kitu wanachozalisha.”Ufugaji wa nyuki wa kisasa si kazi kubwa, na pia unatumia nafasi ndogo na maji kidogo. Nyuki huchavusha asilimia 80 ya miti ya maua ikiwemo mazao ya chakula. Huzalisha asali, nta, mafuta na sumu, bidhaa ambazo huuzwa kwa gharama kubwa sokoni. Kwa sasa WFP inasaidia karibu wafugaji wa nyuki 5,000 katika kaunti 9 nchini Kenya lakini lengo ni kuwafikia wengi zaidi na mradi huu kama anavyosema afisa wa WFP Timothy Koskei. “Dhamira yetu mwisho wa yote ni kuwafikia wastani wa wafuga nyuki 10,000 katika kaunti 9 na kuvuna takriban tani 600 za asali.” Kwa mujibu wa WFP nyuki wana uwezo mkubwa na wanaweza kutoa mavuno mengi ambayo ni neema kwa familia sisizojiweza katika maeneo haya kame. Mkurugenzi wa WFP nchini Kenya Lauren Landis anasema mradi umezaa matunda. “Hivi sasa tunasikia kutoka miongoni mwa wanaufaika ambao awali walikuwa wakipokea msaada wa chakula ,ambao sasa sio tu wanazalisha asali kwa ajili ya faida bali pia wanafikiria kuongeza ununuzi wa pembejeo zaidi kutoka kwa Hive. Hivyo tunachokishuhudia ni mchakato ulio wazi ambapo mtu anatoka kuwa mpokea msaada na kuwa mteja, kuwa mpokeaji wa faida na si mpokeaji wa msaada wa chakula.”Kwa mafanikio haya WFP inasema itaendelea kupanua wigo wa mradi huu ili kunufaisha familia nyingi zaidi.
Maelfu ya watoto katika Kaunti ya Kilifi Pwani ya Kenya kwa miaka mitatu iliyopita wamelazimika kuacha shule kutokana na umasikini na ukame na mafuriko yaliyochangiwa na mabadiliko ya tabianchi. Lakini sasa wizara ya elimu ya Kenya kwa kushirikiana na mradi wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF, wakfu wa Education Above all na wadau wengine juhudi zinafanyika kuwarejesha watoto shuleni. “Niliacha shule darasa la nne ilikuwa mwaka 2022, kwasababu shuleni walikuwa wananirejesha nyumbani nikalete ada. Sasa nikifika nyumbani wazazi wanasema hawana”Huyo ni David Tumaini kijana mwenye umri wa miaka hivi sasa 16 mmoja wa wanafunzi waliolazimiika kukatiza masomo miaka miwili iliyopita katika shule ya msingi ya Soyosoyo kutokana na umasikini. Kwa miezi kadhaa alihaha kusaka njia ya kuendelea na masomo."Nilikaa nyumbani kwa muda wa miezi mitano, wakati wenzangu wanakwenda shule na ni siku za masomo na wewe uko nyumbani. Hii inakufanya ujihisi kama wewe si mtu muhimu.”Hisia kama hizo na mustakbali wa watoto hao ndio kilicholisukuma shirika la UNICEF kuanzisha mradi wa “Elimisha mtoto” likishirikisha wizara ya elimu ya kenya na wadau wengine ili kuhakikisha watoto kama David wanarejea shuleni. Elizabeth Waitha ni afisa elimu wa UNICEF.“Tuliweza kubaini Kaunti 16 ambazo zilikuwa na watoto zaidi ya 10,000 ambao wanaendi shuleni, na hii ilikuwa ni kwa shule za msingi tu. Na tukaangalia ni jinsi gani ya kuhakikisha mazingira bora ya kusoma kwa watoto waliosajiliwa kwenye mradi. Na tumeweza kuwasaidia zaidi ya wanafunzi milioni kwa vifaa vya shule na pia kwa waalimu vifaa vya kuandikia kama chaki, kalamu na vingine.”Na ndipo David akasikia kuhusu mradi huo,“Nilipata taarifa kutoka kwa walimu ya kwamba kuna mradi ambao unawasaidia watoto walioacha shule ili warehjee shuleni kuendelea na masomo. Sasa nilipokuja shuleni nikaambiwa wewe tutakusajili katika huu mradi wa msaada , ndipo nikaweza kurejea masomoni, hadi sasa nipo shuleni kwa sababu ya msaada huu. Vitu ambavyo nilipewa ni pamoja na mkoba wa madaftari, vitabu, kalamu na vifutio.”Hii imemrejeshea David matumaini ya ndoto yake“Mimi nikimaliza kusoma nataka kuwa Daktari ili kusaidia wagonjwa. Na katika kusaidia wagonjwa mshahara nitakaolipwa ntajisaidia mwenyewe na pia kusaidia familia yangu”Kupitia mradi huu mbali ya vifaa umewezesha zaidi ya watoto 256,000 kurejea shuleni na bado wanaendelea na masomo.
Hii leo jaridani tunaangazia amani na usalama nchini DRC, na suala la elimu katika malengo ya maendeleo endelevu tukimulika wanafunzi Kilifi nchini Kenya. Makala tunasalia na mada hiyo hiyo ya elimu na mashiani inamulika sheria za kibnadamu.Wajumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa hii leo wameelezwa jinsi ushindani wa uchimbaji kupita kiasi na biashara ya maliasili huko Mashariki ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC unavyozidi kuchochea mapigano kwenye eneo hilo, madini kama vile dhahabu na Koltani.Maelfu ya watoto katika Kaunti ya Kilifi Pwani ya Kenya kwa miaka mitatu iliyopita wamelazimika kuacha shule kutokana na umasikini na ukame na mafuriko yaliyochangiwa na mabadiliko ya tabianchi. Lakini sasa wizara ya elimu ya Kenya kwa kushirikiana na mradi wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF, wakfu wa Education Above all na wadau wengine juhudi zinafanyika kuwarejesha watoto shuleni.Makala leo inatupeleka Paris Ufaransa katika makao makuu ya shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni UNESCO kuzungmzia juhudi za shirika hili katika kuhakikisha kwamba wanafunzi walio katika maeneo ya migogoro wanaendelea na masomo yao na wenzao waliohamishwa wanapata ufikiaji wa elimu juu katika nchi zilizowapokea.Katika mashinani fursa ni yake Mirjana Spoljaric Egger, Rais wa Kamati ya Kimataifa ya chama cha Msalaba Mwekundu ICRC akitoa wito wa kutafakari machungu yanayowakumba waathirika wa mizozo wakati wa mazungumzo yake na waandishi wa habari kandoni mwa mjadala mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa UNGA79.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Sudan Kusini (UNMISS) umewaeleza wananchi wa Kaunti ya Nasir au Keich Kon iliyoko jimboni Upper Nile nchini Sudan Kusini kuwa ili waweze kurejeshewa huduma za misaada ya kibinadamu ni vyema wakafikia makubaliano ya kusitisha mapigano. UNMISS pamoja na wadau wengine wa misaada ya kibinadamu walifikia uamuzi wa kusitisha huduma zao katika kaunti ya Nasir kutokana nae eneo hilo kutofikika na pia ukosefu wa usalama uliosababishwa na mapigano ya mara kwa mara baina ya wanajamii wa kuanti hiyo, na pia mapigano na kaunti za jirani.Hata hivyo mwanzoni mwa mwezi huu wa Septemba kilifanyika kikao kilichowaleta pamoja wadau na wananchi baada ya kupatikana uongozi mpya wa kaunti hiyo ambapo katika kikao hicho, wadau wa misaada ya kibinadamu ikiwemo Umoja wa Mataifa waliombwa kurejesha operesheni zao hususan UNMISS, Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula duniani (WFP) na wadau wa Sekta ya afya.Paul Ebikwo ni afisa wa masuala ya kiraia wa UNMISS na akawaeleza anaelewa wasiwasi wao.“Wasiwasi wenu ni wa halali, ni wa kweli, tunaelewa. Lakini mkiongeza mizozo ndani yake, mnafanya mambo kuwa mabaya zaidi, kwa hivyo hebu tufanye maamuzi ya kuachana, na kuweka kando migogoro na sote tufikirie jinsi ya kutatua maswala haya.”Bwana Ebikwo aliongeza kuwa suluhu zote za kuzuia ghasia lazima ziongozwe na wanajamii wenyewe huku akitoa wito kwa makundi ya vijana wanaotumia silaha kujiepusha na mapigano na kutafuta amani.Majadiliano yalihitimishwa kwa wote kukubaliana kuwa na dhamira ya pamoja ya kutafuta njia za kuleta jamii hususani vijana pamoja kwa ajili ya upatanisho na ujenzi wa amani ili kusaidia kurejesha utulivu na kuwezesha jamii katika kaunti ya Nasir kupata ahueni na maendeleo baada ya kuteseka kwa muda mrefu.
Hii leo jaridani tunaangazia suala la elimu katika maeneo ya migogoro, na msaada wa kibinadamu huko Upper Nile nchini Sudan Kusini. Makala tunakupeleka nchini Nigeria na mashinani nchini Afghanistan, kulikoni??Ikiwa leo ni siku ya kimataifa ya kulinda elimu isishambuliwe wakati wa mizozo kutokana na umuhimu wake kwa watoto na jamii, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amesema miaka ya karibuni imeshuhudia ongezeko kubwa la mashambulizi dhidi ya wanafunzi, walimu na shule duniani kote. Hivyo ndivyo alivyoanza ujumbe wake wa siku hii.Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Sudan Kusini (UNMISS) umewaeleza wananchi wa Kaunti ya Nasir au Keich Kon iliyoko jimboni Upper Nile nchini Sudan Kusini kuwa ili waweze kurejeshewa huduma za misaada ya kibinadamu ni vyema wakafikia makubaliano ya kusitisha mapigano.Makala inatupeleka Maiduguri nchini Nigeria kusikia namna mfuko wa kimatifa wa elimu haiwezi kusubiri yaani Education Cannot Wait (ECW) kwa kushirikiana na shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia watoto (UNICEF) na wadau wengine wanarejesha matumaini kwa waliokosa elimu rasmi hasa kutokana na hali mbayá ya usalama katika maeneo yao.Na katika mashinani, fursa ni yake Faeza, mfanyakazi wa kiwanda cha kutengeneza biskuti nchini Afghanistan, mradi unaowezeshwa na shirika la WFP akitueleza manufaa ya mradi huo kwa jamii iliyoathirika na vita hasa wanawake na watoto.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
Matangazo ya saa nzima kuhusu habari za kutwa, ikiwa ni pamoja ripoti kutoka kwa waandishi wetu sehemu mbali mbali duniani na kote Afrika Mashariki na Kati, na vile vile vipindi na makala maalum kuhusu afya, wanawake, jamii na maendeleo.
Gavana wa Kaunti ya Mandera Mohamed Adan Khalif, amesema asilimia 60 ya kaunti yake iko chini ya udhibiti wa Al Shabaab.
Wakati ukame mkali ukiendelea kuathiri Afrika hususan Ukanda wa jangwa la Sahara na kusababisha mamilioni ya watu kuyakimbia makazi yao kwenda kusaka misaada, baadhi ya wananchi waliosalia kwenye maeneo yao wanasema hali ni mbali lakini wamebaki kwa mustakabali wa watoto wao. Miaka 40 ya jua kali na ukame katika pembe ya Afrika, imekuwa na athari kubwa kwa wananchi wengi wasijue hali yao ya kesho itakuwaje kama mama huyo aitwaye Nurta Andow Nurinye mkazi wa Kaunti ya Garissa nchini Kenya. “Nina watoto watano, kabla ya ukame tulikuwa na mifugo, maziwa na nyama. Tangu ukame uje hakuna mvua, Wanyama wamekufa mbuzi, ngamia kila kitu kimekwenda. Maisha yamebadilika, hakuna chakula hakuna maziwa, hatuna kitu chochote, watoto wakirejea kutoka shuleni hakuna kitu chochote.” Lakini kwanini Bi.Nurta na familia yake hawaendi kusaka msaada zaidi kwenye kambi za wakimbizi wa ndani? “Tungeweza kuondoka na kwenda kusaka chakula sehemu nyingine lakini hatuwezi kwenda. Hapa watoto wapo shule, na hapa watoto wanaenda Madrasa na kwa sababu hiyo hatuwezi kufungasha virago na kwenda sehemu nyingine, ni lazima tubaki hapa.” Mashirika mbalimbali ya Umoja wa Mataifa ikiwemo lile la idadi ya watu duniani na afya ya uzazi UNFPA yanafanya kila juhudi kuhakikisha wanawafikia wananchi kama Nurta Nurinye ili kuwafikishia misaada ya kuokoa maisha.
Haii ya wasiwasi imeripitiwa baada ya wavamizi kushambulia vijiji viwili katika kaunti ya Lamu nchini Kenya katika kile mamlaka zinasema ni shambulizi la kigaidi.
Jaridani hii leo tunaangazia machafuko nchini Sudan na mchakato wa uchaguzi nchini Sudan Kusini. Makala tunakupeleka nchini Kenya na Mashinani yunasalia hapa makao makuu kusikia ujumbe kuhusu idadi ya watu duniani.Mzozo nchini Sudan ukiingia mwezi wa pili, hii leo Umoja wa Mataifa na wadau wake wamefanyia marekebisho ombi la usaidizi kwa nchi hiyo na sasa linafikia dola bilioni 3 kwa ajili ya kusaidia mamilioni ya watu nchini humo na mamia ya maelfu wengine waliokimbilia nchi jirani kusaka usalama. Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Sudan Kusini (UNMISS) umefanya warsha za majadiliano katika mji wa Torit na Magwi mashariki mwa mji mkuu Juba jimboni Equatorial Mashariki ili kujadili kuhusu utungaji katiba na michakato ya uchaguzi.Makala leo inatupeleka Kaunti ya Kilifi Pwani ya Kenya ambako shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF linashirikiana na serikali na wadau wengine kuzisaidia familia zisizojiweza na zilizo hatarini kupitia program ya lishe na elimu ya afya na malezi bora ijulikanayo kama NICHE.Katika mashinani tutasikia ujumbe kuhusu idadi ya watu duniani na jinsi ambavyo inatofoutiana kulingana na nchi.Mwenyeji wako ni Anold Kyanda, Karibu!
Kaunti ya Kilifi iliyoko Pwani ya Kenya ni moja ya maeneo ambako mradi wa majaribio wa elimu ya malezi na lishe kwa watoto unaendeshwa na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF ukifanyika kwa ushirikiano na serikali na wadau wengine,lengo kubwa likiwa ni kuzisaidia familia zisizojiweza na zilizo hatarini kupitia program ya lishe na elimu ya afya ziweze kutoa malezi bora kwa watoto wao huku zikikabiliana na ukatili katika familia hasa dhidi ya watoto.Mradi huu umeleta faraja kubwa kwa familia nyingi za kauti hiyo tuungane na Flora Nducha katika Makala hii kwa undani zaidi.
Maelfu ya watu wamevuka na kuingia Sudan Kusini wakikimbia mzozo unaoendelea nchini Sudan. Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) liko linawasaidia wanaowasili lakini mzigo huu wa ziada unaweka shinikizo katika shughuli za shirika hilo ambazo tayari ziko katika hali mbaya ya ufadhili.Video iliyoandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) inatupeleka katika Kaunti ya Renk iliyoko kaskazinimashariki mwa nchi ya Sudan Kusini inakopakana na Sudan. Hapa ni kila mtu anajaribu kukumbatia kile alichofanikiwa kutoroka nacho akikwepa mabaya ambayo yangemkumba ikiwa angesalia Sudan ambako tangu tarehe 15 mwezi jana Aprili kunafukuta mapigano makali. Wanaobahatika wanabebwa na magari ya Umoja wa Mataifa, wengine punda na wengine wametembea mwendo mrefu kufika hapa. Kwa mujibu wa WFP, zaidi ya watu 30,000 hadi sasa wamevuka mpaka kutoka Sudan na kuingia Sudan Kusini. Wengi wao ni waliorejea kwani walikimbia madhila hapa Sudan Kusini lakini nako ugenini Sudan kumechafuka, wamerejea. Naimat Khamis, ni mmoja wa waliorejea anasema, "Tulilazimika kuja hapa kwa sababu ya mapigano ya Khartoum…tulilazimika kukimbia haraka iwezekanavyo kwa sababu ya vita…ilikuwa safari ngumu…tunataka kubaki na jamaa zetu hapa kwa sababu tumeteseka sana.” Hassan Abdallaziz, kijana mwenye umri wa miaka 17 huyu yeye ni raia wa Sudan kwa hiyo kwa Sudan Kusini yuko ukimbizi anasema, “Hali ya nchi ilinilazimu kuja hapa. Hakuna kitu kizuri kilichobaki nchini, hakuna kazi, ni machafuko. Mtu yeyote anaweza kupora mali yako, ni kama msitu." WFP tayari inawasaidia waliowasili na wanaowasili ikiwa ni pamoja na kuwapa chakula, kuwapima watoto, wajawazito na wanaonyonyesha, lakini mzigo huu wa ziada unaongeza chumvi kwenye kidonda. Mary-Ellen McGroarty ni Mkurugenzi wa WFP nchini Sudan Kusini akiwa mjini Juba anasema, "Mgogoro huu umekuja katika wakati mbaya zaidi. Unajua nchini Sudan Kusini tunaingia katika msimu wa muambo na msimu wa mvua. Tayari tuna watu milioni 7.4 wanaohitaji msaada wa chakula. Hatuwezi kuwafikia wote kwa sababu ya changamoto za rasilimali. Tumelazimika kupunguza programu zetu kwa sababu ya vikwazo vikali vya ufadhili. Na sasa tena tunalazimika kuweka vipaumbele upya kati ya watu wenye njaa, hawa wapya wanaowasili, ambao wako hatarini sana.”
Nchini Kenya shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya wanawake, UN Women kwa ushirikiano na wadau wanajengea uwezo wajenzi wa amani mashinani hata kwenye maeneo yenye changamoto kama vile kambi ya wakimbizi ya Daadab kwenye kaunti ya Garissa nchini humo kwa lengo la kuepusha vijana kutumbukizwa kwenye vikundi vyenye msimamo mkali. UN Women inafanya hivyo kupitia warsha inazoendesha kwa ushirikiano na mashirika ya kiraia ya wanawake kama vile WomanKind Kenya ambapo katika moja ya warsha huko kambini Daadab, Nimo Dubat, mwenyekiti wa chama cha wanawake wachuuzi sokoni anaelezea umuhimu wa warsha hizo akisema, “kwa upande wa usalama, wanawake na vijana ndio wanaweza kufuatilia, sisi ndio vijana tumezaa na tunajua ambaye anaanza kuleta shida nyingi. Katika watoto wetu, mama ndiye mzazi, mama ndiye anajua ambaye anaanza tabia mbaya. Mama ndiye anajua nani ameingia kwenye mtaa mgeni, na nani Jirani yake amepokea mgeni, hata tumetengeneza kikundi cha wanawake wa nyumba 10. Hata kuna wasichana wajumbe wa nyumba 10. Sasa tunataka tupatiwe nguvu, tushikamane na polisi kwenye ulinzi. Mama ndiye anabeba mzigo wa shida yote. NasibaAbdi Farah mkazi wa Daadab na mnufaika wa warsha hiyo iliyojumuisha wanaume na vijana wa kike na wa kiume, hakuficha hisia zake akisema kupitia mafunzo waliyopata akisema kuwa "yule kijana ambaye sitamuona nitauliza kwa wenzake ameenda wapi? Ameenda mpakani? Basi nitaenda kwa mama na kumuuliza mtoto wake ameenda kufanya nini mpakani? Akisema sijamuona? Namueleza tafuta kijana wako na umlete.” Warsha hii ilipatia fursa pia viongozi wa eneo la Daadab kushirkiana na mashirika yenye mtazamo sawa kupitisha na kuridhia na kuanza kutekeleza Mpango wa Utekelezaji wa Kaunti ya Garissa wa kuzuia na kukabiliana na misimamo mikali.
Hii leo jarida linamulika ukatili dhidi ya wanawake na wasichana na pia mradi wa kupatia fedha jamii nchini Malawi. Makala tunakwenda nchini Kenya na Mashinani nchini Tanzania.Ripoti ya utafiti mpya iliyotolewa leo na shirika la Umoja wa Mataifa la masuala ya wanawake UN Women na ofisi ya Umoja wa Mataifa ya madawa na uhalifu UNODC inaonyesha kuwa wanawake na wasichana ndio walio katika hatari kubwa ya kuuawa majumbani, ikionyesha kuwa kwa wastani zaidi ya wanawake au wasichana watano waliuawa kila saa na wenzi wao au jamaa wa familia kwa mwaka 2021. Flora Nducha na taarifa zaidiNchini Malawi,shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto duniani, UNICEF kwa msaada kutoka kwa wadau wake wa maendeleo linatekeleza mradi wa kupatia fedha jamii au MSCTP kwa ajili ya kupunguza umaskini, kukabili utapiamlo halikadhalika kuondokana na utoro shuleni utokanao na wazazi kushindwa kulipa karo.Makala ambapo tunaelekea nchini Kenya katika Kaunti ya Garissa kuangazia hali mbaya ya ukame iliyosababishwa na mabadiliko ya tabianchi na hatua zinazochukuliwa na Umoja wa Mataifa kwa kushirikiana na serikali.Na leo mashinani na tunakwenda nchini Tanzania kusikia ni harakati za kunusuru wanawake dhidi ya ukatili kwa misingi ya umiliki wa ardhi.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
Umoja wa Mataifa na wadau wake wa masuala ya kibinadamu nchini Kenya wameomba dola milioni 472.6 kusaidia watu milioni 4.3 walioathiriwa na ukame, ili kuunga mkono mwitikio unaoongozwa na Serikali, huku janga hilo likitarajiwa kuwa mbaya zaidi. Hali katika baadhi ya maeneo ya nchi hiyo katika Pembe ya Afrika, ni mbaya. Naibu Rais wa Kenya Rigathi Gachagua anaeleza kuwa mzigo huu wa janga la mabadiliko ya tabianchi ni mkubwa kwa nchi yake na kwa hivyo ni muhimu jumuiya ya kimataifa ikasaidia lengo hilo la Umoja wa Mataifa kwani hali ya wananchi inazidi kuwa mbaya. Mfano mmoja ni katika Kaunti ya Garissa ambako video iliyoandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa Mazingira, UNEP, inaonesha hali ya wananchi kuwa maisha yako hatarini. Kutoka Kenya, Mwadishi wetu Thelma Mwadzaya anaeleza zaidi kupitia makala hii.
Hii leo jarida linaangazia ripoti iliyotolewa leo na UNICEF kuhusu ubaguzi wa rangi na ubaguzi dhidi ya watoto na pia habari kutoka Garissa, Kenya, makala ya maandamanano ya wanaharakati huko Sharm-el-Sheikh nchini Misri kwenye mkutano wa 27 wa nchi wanachama wa Mkataba wa mabadiliko ya tabianchi, COP27, kisha mashinani nchini Ethiopia.Ubaguzi wa rangi na ubaguzi mwingine dhidi ya watoto kwa misingi ya makabila, lugha na dini zao umeenea duniani kote na kuleta athari kwenye mfumo wa haki, usawa na hata uwezo wa kujua kusoma, hayo yapo kwenye ripoti iliyotolewa leo na Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Watoto UNICEF.Msaada wa kisima cha maji uliofanikishwa na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF katika shule ya Msingi ya Daley kwenye Kijiji cha Daley, Kaunti ya Garissa nchini Kenya, umesaidia sana jamii hasa katika suala la elimu katika eneo hilo la nchi ambalo limekosa mvua ya kutosha kwa misimu mitano mfululizo.Makala tunafuatilia maandamanano ya wanaharakati huko Sharm-el-Sheikh nchini Misri kwenye mkutano wa 27 wa nchi wanachama wa Mkataba wa mabadiliko ya tabianchi, COP27, maandamanayo yaliyofanyika tarehe 17 mwezi huu wa Novemba, kulikoni?Mashinani tunakwenda nchini Ethiopia kuona ni kwa vipi mtoto mmoja kwa kuwa ni wa kike analazimika kutumia muda wake kuteka maji badala ya kwenda shuleni.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
Msaada wa kisima cha maji uliofanikishwa na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF katika shule ya Msingi ya Daley kwenye Kijiji cha Daley, Kaunti ya Garissa nchini Kenya, umesaidia sana jamii hasa katika suala la elimu katika eneo hilo la nchi ambayo imekosa mvua ya kutosha kwa misimu mitano mfululizo.Ni wanafunzi wakiwa darasani, kwa uchangamfu wakijadiliana na mwalimu wao kuhusu umuhimu wa maji katika maisha ya kila siku. Nje ya darasa lao kunaonesha wazi hali ya ukame ilivyo ya kutisha. Ardhi imekauka na ni miti michache tu imebaki na ukijani. Kabla ya UNICEF kwa kushirikiana na jamii na serikali kuigilia kati, hali ya kukosekana kwa mvua imesumbua maisha ya wakazi wa hapa ikiwemo upatikanaji wa elimu kwa watoto wa jamii hii ya wafugaji kama asemavyo Mwalimu Mkuu Msaidizi, Wasula Samson Saiya anasema "Tuna takribani wasichana 146 na wavulana 200 jumla wanafunzi 346. Unagundua kwamba wengi wa wanafunzi wanachunga mifugo. Kwa hiyo, wakati wa ukame kama hivi unakuta pia wanahama na wanyama hao kule walikokwenda kulishia ili wawachunge. Kwa hivyo, tunajikuta tuna wanafunzi wachache darasani.” Ili kuitatua hali hiyo, UNICEF ilitoa msaada wa kifedha na kiufundi kuchimba kisima cha chini ya ardhi na kuweka mfumo wa kupaadisha maji kwa kutumia nguvu ya nishati ya jua na pia ujenzi wa upanuzi mpya wa bomba ili kuunganishwa na miundombinu iliyopo ya usambazaji wa maji. Takriban watu 6200 wakiwemo wanafunzi kutoka Shule ya Msingi ya Daley na Kituo cha Maendeleo ya Awali ya Watoto (ECDC) wanapata huduma ya maji salama. Aidha, zahanati moja ya afya ina huduma ya maji salama. Osman Aden Abdi, Naibu Mkurugenzi, Kitengo cha Ufuatiliaji na Tathmini, Idara ya Maji ya Kaunti ya Garissa anasema "Faida ni nyingi. Wakati tulipopata kisima, hali ya hatari katika suala la wanyama pori imepungua. Unyanyasaji wa kijinsia pia umepungua kwa sababu kioski hiki cha maji kiko mahali pa wazi sana. Tuna bahati sana kwa sababu umbali ni kama mita 50 tu hadi mahali pa maji. Inaokoa muda linapokuja suala la masomo ... unajua, katika maeneo yetu ni kukavu sana na joto sana. Kwa hivyo, tunawaruhusu wanafunzi kupata maji kila baada ya dakika 30...badala ya kurudi nyumbani. Kuna maeneo kadhaa ambako UNICEF, kwa usaidizi wa serikali ya kaunti imeweka mitambo ya nishati ya jua. Baada ya kisima hiki kilichimbwa na kuwekewa nishati ya jua, hakuhitajiki gharama zaidi, ili kwa muda mrefu jamii ziweze kujikimu zenyewe.” Kufikia Novemba 2022, katika Kaunti ya Garissa, UNICEF tayari imesaidia ukarabati wa mifumo 21 ya usambazaji wa maji na kufikia jumla ya watu 92,279 wanaopata maji salama.
Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF limesema watoto wengi na hususan wa kike katika jamii zilizoathirika na ukame nchini Kenya ikiwemo Turkana wako katika hatari hasa ya kuozwa mapema kwa sababu familia nyingi zinahaha kuweka mlo mezani na suluhu ya karibu wanayoiona ni kuoza binti zao mapema ili kujikimu. Sasa shirika hilo linashirikiana na mamlaka za huduma ya ulinzi kwa watoto katika maeneo yaliyoathirika ili kuwalinda dhidi ya ajira ndoa za utotoni. Mary Kabora na maelezo zaidi. Carol , hilo si jina lake halisi ila amepewa sababu ya kulinda usalama wake, ana umri wa miaka 11 na anaishi katika Kaunti ya Turkana anasema mjomba wake aliamua kumuoza baada ya hali ya maisha kuzidi kuwa mbaya kutokana na ukame , kwani sasa hawana mbuzi tena, wala hawana chochote na matatizo yamekuwa mengi nyumbani. Lakini Caro mwenye ndoto za kusoma alikataa katakata akisema, “nilisema siwezi kukubali hata kama ni njaa basi wacha niake tu mi siwezi kukubali hicho kitu.” Hii ni changamoto inayozikabili familia nyingi hapa Turkana, kisa ni ukame wa muda mrefu uliowafanya kupoteza uwezo wa kujikimu kimaisha, mazao yamekauka, mifugo imekufa, fedha hakuna na msaada ni changamoto. Kukosekana kwa fedha ya kulipia mtihani ndio kulimponza Carol na kisha, “Mama yangu niliporudishwa nyumbani kwenda kuleta hela ya kulipia mtihani alisema hana hela, hakunipa na hiyo likanifanya nikaacha shule. Na ndio ikafanya wanipe mzee anioe, mimi nikakataa nikasema huyo bwana siwezi kukubali.” Ameendelea kusema kuwa mwanaume huyo mzee alikuja kumchukua na pikipiki akaondoka naye na wakiwa njiani walisimama porini na mwanaume huyo akamnajisi. Mkurugenzi wa huduma ya ulinzi kwa watoto Turkana Julius Yator anasema “Kisa hicho kutoka Turkana South kiliripotiwa na jirani kwenye ofisi ya huduma kwa watoto ambayo ni ofisi yangu, na kuanzia hapo mchakato wa kukamata wahusika na kumuokoa mtoto ukaanza.” UNICEF inashirikiana na ofisi hiyo ili kuwalinda watoto walioathirika na ukame na walio hatarini kama Carol, na hadi sasa watoto 1,600 katika Kaunti hiyo wameshafikiwa na kuokolewa dhidi ya ajira na ndoa za utotoni. Mkuu wa UNICEF ofisi ya kanda ya Lodwar Laban Rotuno Kipsang anasema “kwa kawaida tunaporipoti kesi kama hizo binti huokolewa na anapewa malazi na ushauri nasaha. Ukanda wangu pia unafanya kazi kubwa ya kushirikisha jamii kupitia msaada wa UNICEF peke yetu na washirika wengine, na sasa hivi tuna kampeni inayosema baini na komesha , ili unapoona unazuia ni kama katika kesi hii mtu aliona na akaamua kuripoti na mtoto akaokolewa asiolewe.” Na Carol baada ya kuokolewa anasema anataka kurejea ndoto yake “Nataka kusaidiwa niendelee na shule.”
Kaunti ya Turkana nchini Kenya inakabiliwa na ukame wa muda mrefu. Ili kusaidia kuimarisha mifumo ya lishe, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF, nchini Kenya limeanzisha mfumo wa simu za mkononi uitwao RapidPro. Huduma hii huwezesha vituo vya afya kushirikishana ujumbe wa lishe na wafanyakazi wa kujitolea wa afya ya jamii, ambao huripoti taarifa na takwimu mbalimbali za kiafya kuhusu jamii zao.
Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Watoto UNICEF leo limemteua na kumtangaza mwanaharakati wa mazingira kutoka nchini Uganda Vanessa Nakate kuwa balozi mwema mpya wa shirika hilo. Vanessa Nakate, Balozi mwema wa UNICEF, akiwa ziarani Turkana nchini Kenya alitembelea hospitali ya rufaa ya Lodwar na hapo anazungumza na mtoto Eunice Asukuku ambaye alifikishwa hospitali kwa tatizo la utapiamlo mkali, kuvimba mwili na ukosefu wa damu. Chanzo cha matatizo ni uhaba wa chakula utokanao na ukame uliosababishwa na mabadiliko ya tabianchi. Uteuzi wa Vanessa, mwenye umri wa miaka 25 unafuatia ziara yake kwenye Pembeme ya Afrika ambako alishuhudia jinsi gani mabadiliko ya tabianchi yalivyochangia athari mbaya kwa maisha ya watoto nchini Kenya kutokana na ukame unaoendelea. Pia uteuzi huo ni kuthibitisha ushirikiano wake na shirika la UNICEF na kutambua utetezi wake bora wa kimataifa wa haki za kimazingira kwa vizazi vya sasa na vijavyo. Vanessa alisafiri wiki iliyopita na UNICEF hadi Kaunti ya Turkana Kaskazini Magharibi mwa Kenya ili kujionea athari za uhaba wa maji na chakula unaosababishwa na ukame mbaya zaidi kuwahi kushuhudiwa katika Pembe ya Afrika katika kipindi cha miaka 40. Katika safari yake ya kwanza na UNICEF, alikutana na jamii zilizo katika kitovu cha athari za mabadiliko ya tabianchi ikiwa ni pamoja na kinamama na watoto wanaopata matibabu ya kuokoa maisha kutokana na utapiamlo mkali na familia zinazonufaika na mifumo ya usambazaji wa maji inayotumia nishati ya jua kwa msaada wa UNICEF. Nitahakikisha sauti za watoto zinasikika Baada ya kuteuliwa kwake Bi. Nakate amesema "Kama balozi mwema wa UNICEF, itakuwa jukumu langu la kwanza kuwasilisha sauti za watoto na watu waliotengwa katika mazungumzo ambayo awali hawakujumuishwa. Jukumu hili na UNICEF litanipa fursa zaidi za kukutana na watoto na vijana katika maeneo yaliyoathiriwa zaidi na mabadiliko ya tabianchi na jukwaa lililopanuliwa la kutetea kwa niaba yao. Nchini Kenya, watu niliokutana nao waliniambia kuhusu athari za mabadiliko ya tabianchi na ukame katika maisha yao, huku misimu minne ya mvua iliyofeli mfululizo ikiwanyima watoto haki zao za msingi.” Ameongeza kuwa moja ya jamii alizokutana nazo imemweleza kuwa haijashuhudia mvua kwa zaidi ya miaka miwili. “Hii ni zaidi ya shida ya chakula na lishe, ni mwelekeo mwingine wa changamoto yetu ya mabadiliko ya tabianchi inayozidi kuwa mbaya.” Ombi la UNICEF la kuboresha na kusaidia maisha ya mamilioni ya watu walioathirika na ukame na kuwajengea mnepo kwa muda mrefu kwenye Pembe ya Afrika na kuzuia athari za ukame kwa miaka ijayo zinagonga mwamba kwani hadi sasa ombi hilo limefadhiliwa kwa asilimia 3% pekee. Akiwa Sopel, kaunti ya Turkana nchini Kenya, Vanessa Nakate alitembelea shule ya msingi na kuzungumza na wanafunzi kuhusu changamoto wanazozipata kutokana na janga la ukame kwenye eneo hilo la Afrika Mashariki. Safari ya uanaharakati ya Vanessa Nakate Vanessa alianza harakati zake Januari 2019 kwa maandamano na ndugu zake na binamu zake katika mitaa ya jiji la Kampala, nchini Uganda, maandamano yaliyochochewa na mwanaharakati mwingine nyota wa mabadiliko ya tabianchi na mazingira Greta Thunberg. Aliendelea kuandamana kila wiki, na kuwa sura inayojulikana katika harakati ya vijana kupiga mabadiliko ya tabianchi duniani kote. Mwaka 2020 alijulikana zaidi ulimwenguni wakati alipoondolewa kwenye picha ya habari aliyokuwemo pamoja na Thunberg na wanaharakati wengine weupe wa mabadiliko ya tabianchi. Kufuatia tukio hilo alochosema Vanessa ni kwamba chombo hicho cha habari "hakikufuta picha tu, bali kilifuta bara zima", kauli ambayo iligonga vichwa vya habari vya kimataifa. Vanessa amesema safari yake haikuwa rahisi “Kama mwanamke mwanaharakati mchanga wa Kiafrika, imenibidi kupigana ili kusikilizwa na vyombo vya habari na watoa maamuzi. Wakati nina bahati ya kuwa na jukwaa sasa, ninakusudia kuendelea kupigania wengine. Watoto walio katika kitovu cha athari za mabadiliko ya tabianchi, kama wale niliokutana nao Turkana, Kenya, ni watu ambao nitapigania katika jukumu langu jipya na UNICEF,” amesema Nakate. Tangu wakati huo Vanessa ametumia jukwaa lake kutetea haki ya masuala ya mabadiliko ya tabianchi kujumuisha kila jamii, haswa wale kutoka sehemu zilizoathiriwa zaidi. Alianzisha Rise Up Movement, jukwaa la kupaza sauti za wanaharakati wa mabadiliko ya tabianchi wa Afrika, pamoja na mradi wa kufunga paneli za sola katika shule za vijijini za Uganda. Amehutubia viongozi wa dunia katika mikutano ya mabadiliko ya tabianchi ya COP25 na COP26 na alionekana na hadithi yake kuchapishwa kwenye jarida la TIME.
Wakati Kenya ikijiandaa kwa uchaguzi mkuu tarehe 9 mwezi ujao wa Agosti, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF nchini humo linatoa wito kwa serikali itakayoingia madarakani ipatie kipaumbele hifadhi ya jamii ikiwemo kupatia fedha familia zilizo hatarini kama njia mojawapo ya kupunguza umaskini. UNICEF inatoa wito huo wakati huu ambapo mradi wake wa majaribio kupatia fedha famiilia maskini zenye watoto umeanza kuzaa matunda kama anavyoelezea Anold Kayanda katika taarifa hii. Huyo ni Monika Muema, mkazi wa Kaunti ya Kajiado nchini Kenya. Yeye ni bibi na mlezi wa wajukuu watano na binti yake ambaye ni kiziwi. Monika ni mnufaika wa mradi wa UNICEF wa kupatia fedha kaya maskini ambapo kila mwezi hupatiwa takribani dola 17 ili kuweza kulea wajukuu zake akiwemo Alice mwanafunzi wa darasa la 7. Monika anatumia fedha anazopata kusuka vikapu. Ukosefu wa fursa za ajira na changamoto itokanayo na COVID-19 ilifanya hali kuwa mbaya zaidi na watoto wakashindwa hata kwenda shule. Susan Momanyi, afisa wa UNICEF Kenya anasema, “hapa Kenya kaya milioni 1.4 zimeandikishwa kwenye mradi wa hifadhi ya jamii, na hivoy kuacha takribani watoto milioni 12 wanoahitaji huduma hiyo. Ndio maana UNICEF inatoa wito kwa serikali ijayo ya Kenya kuongeza bajeti kwenye hifadhi ya jamii kwa asilimia 1.7 ya pato lake la ndani, kiwango ambacho ni sawa na nchi zingine za kipato cha kati ili kila mtoto anufaike.” Sasa hata walimu wa Alice shuleni wanasema wameona tofauti tangu bibi yake aanze kunufaika na mradi wa kupatiwa fedha kwani mahudhurio ni bora halikadhalika sare za shule.
In 2019, 29-year-old Irene Gakwa made a big move: she flew from her home in Kenya to the United States to start a new life. Irene had always loved helping people, and she was going to turn that love into a career by studying nursing. Fortunately, Irene already had a support system in the states: her two brothers, Chris and Kennedy lived in Boise, Idaho, and she was going to join them. Everything was going according to plan, and Irene even fell in love. But her family alleges that her boyfriend was no Prince Charming. They say that he was controlling and worked to isolate Irene from her family.On February 24, 2022, Irene had a video call with her parents. She hasn't been seen since. Did she, as her boyfriend claims, decide to pack up and move once again, or has something much worse happened to Irene?If you have any information regarding the disappearance of Irene Gakwa, or if you've seen a grey or silver Subaru Crosstrek with Idaho license plates that may have been seen trespassing on private property or in rural parts of Campbell County between February 24 and March 20, please contact the Gillette Police Department at 307-682-5155.Iwapo una habari yoyote kuhusu kutoweka kwa Irene Gakwa, au ikiwa umeona Subaru Crosstrek ya kijivu au ya fedha yenye nambari za leseni za Idaho ambayo inaweza kuwa ilionekana ikiingilia mali ya kibinafsi au katika maeneo ya mashambani ya Kaunti ya Campbell kati ya Februari 24 na Machi 20. , tafadhali wasiliana na Idara ya Polisi ya Gillette kwa 307-682-5155.We are proud members of Spreaker Prime and The Darkcast Network.Find us everywhere: https://linktr.ee/attwgpodGet episodes early and ad-free on Patreon: https://patreon.com/attwgpodMerch store: https://www.teepublic.com/stores/attwgpodFor a full list of our sources, please visit our blog: https://andthentheyweregone.com/blogThis week's promo is brought to you by Partial list of sources:https://namus.nij.ojp.gov/case/MP90106https://whereisirene.com/index.phphttps://juryfile.com/2022/04/21/irene-gakwa/https://diasporamessenger.com/2022/05/online-love-ended-in-agony-for-missing-kenyan-woman-irene-gakwa-in-us/https://www.news-journal.com/fianc-of-missing-woman-arrested-for-allegedly-stealing-from-her/article_f5a7498c-ff3c-5e33-a7cd-9ac556a8cb5e.htmlhttps://county17.com/2022/05/11/person-of-interest-arrested-in-gillette-missing-woman-case/